Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV Exclusive: Harmonize AZUNGUMZIA ATAKAVYOWASHA MOTO Wasafi Festival USIKU WA LEO MJINI Morogoro


MNYETI AWAFAGILIA DC WA KITETO NA SIMANJIRO

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti amewafagilia wakuu wa Wilaya za Kiteto mhandisi Tumaini Magessa na Simanjiro mhandisi Zephania Chaula kuwa ndiyo wakuu wa wilaya bora kwa sasa kwenye mkoa wake, wenye kuchapa kazi na kuhudumia wananchi. Mnyeti akizungumza mjini Babati alisema mkuu wa wilaya ya Kiteto mhandisi Tumaini Magessa na mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula, ndiyo wakuu wa wilaya bora kwa sasa mkoani Manyara.

Alisema anataja majina hayo mawili ya wakuu hao wa wilaya ili iwe changamoto kwa wakuu wengine wa wilaya za mkoa huo wenye wilaya tano, kutekeleza wajibu wao ipasavyo. Alisema wakuu wengine wa wilaya ambao hawajatajwa wasife moyo ila waongeze bidii na juhudi katika kuwatumikia wananchi na kutekeleza wajibu wao ipasavyo. Alisema anatangaza majina ya wakuu hao wa wilaya wanaongoza mkoani humo baada ya yeye kushauriana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Simon Lulu na Katibu Tawala wa mkoa huo Missaile Mussa, ndipo wakapatikana hao.

Alisema mkuu wa wilaya anapaswa kutoa maamuzi kwenye eneo lake la utawala na siyo kupiga simu kwa mkuu wa mkoa kila wakati kuomba msaada ili hali uwezo wa kutoa maamuzi anayo. Alisema wameangalia namna wanavyotoa maamuzi yao, utulivu wa wilaya, wanavyowasimamia watumishi wao wa ngazi ya chini na kudhibiti ufujaji wa fedha za miradi ya maendeleo.

“Changamoto zenu pambaneni nazo kwani hata mimi napambana na nafasi yangu siyo kila wakati napiga simu kwa mheshimiwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa kuomba msaada ila mkizidiwa itajulikana hapo kweli ni haki,” alisema Mnyeti. Alisema hata Rais John Magufuli alipotangaza kuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka anaongoza kwa wakuu wa mikoa yeye hakulalamika hivyo na wakuu wa wilaya wengine wasihofie hilo. 

“Najua mkuu wa wilaya ya Hanang Joseph Mkirikiti atasema ohoo yeye hana mwaka tangu afike Hanang’ lakini hata mimi, alipotangazwa wa Simiyu sikusema sina mwaka tangu nije Manyara,” alisema Mnyeti. Mkuu wa wilaya ya Kiteto, mhandisi Tumaini Magessa alisema baada ya kuwepo utulivu eneo la Emboley Murtangos sasa wanageukia hifadhi ya msitu wa mlima wa simu ili kulinda uhifadhi. 


Mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula alisema ataendelea kusimamia maendeleo kwenye eneo lake na kuhakikisha wanazidi kupiga hatua nyingine zaidi ya hapo walipo.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mhandisi Tumaini Magessa ambaye ametangazwa na Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti kuwa ndiyo anaongoza kwa uchapakazi.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, mhandisi Zephania Chaula akisalimiana na wananchi wa eneo lake, mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amesema anashika nafasi ya pili kwa kuchapa kazi. 

MIAKA 60 YA VCT KUADHIMISHWA JUMATATU

MAHAFALI CHUO CHA KUMBUKUMBU YA HUBERT KAIRUKI YAFANA JIJINI DAR

RAIS WA ZANZIBAR DKT SHEIN AHUDHURIA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA ZSTC ZANZIBAR

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia na kutowa nasaha zake kwa Uongozi wa ZSTC na wananchi waliohudhuria hafla ya kuadhimisha Miaka 50 ya Shirika hilo zilizofanyika jana usiku katika viwanja vya hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.2-12-2018.(Picha na Ikulu).

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Afisa Masoko wa Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) Nassor Salum Nassor, wakati akitembelea maonesho ya Bidhaa za ZSTC wakati wa maadhimisho ya 50 zilizofanyika katika viwanja vya Hotel Verde Mtoni Zanzibar,kushoto Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,Mke waMakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, Makamu Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif na Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salumu Ali, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hotel Verde jana usiku.

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mama Fatma Karume, wakati akiwasili katika ukumbi wa hafla ya sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya ZSTC zilizofanyika katika viwanja vya Hoteli Verde Mtoni Zanzibar, jana usiku.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi na Mama Mwanamwema Shein, na Viongozi wengi wakiwa wamesimama wakati ukiimbwa wimbo wa Taifa na Kikundi cha Taifa cha Taraab Zanzibar, jana usiku katika hoteli ya Verde Mtoni
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguji Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na kulia Waziri wa BiashaRA NA Viwanda Zanzibar,Mhe Balozi Amina Salum Ali na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, wakifuatilia onesho la “ Documentary “ ya Miaka 50 ya ZSTC,hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hotel Verde Mtoni Zanzibar, jana usiku.
WADAU wa ZSTC wakifuatilia hafla hiyo ya Maadhimisho ya sherehe za Miaka 50 ya Shirika hilo tangu kuazishwa kwake Zanzibar 1968, zilizoadhimishwa katika viwanja vya Hoteli Verde Mtoni Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Mhe. Dk. Shein, akihutubia hafla hiyo, jana usiku. 

MILIONI KUMI ZA TIGO JIGIFTISHE ZAENDA KWA MUOSHA MAGARI TABATA DAR

$
0
0



Kitita cha shilingi milioni 10 cha mshindi wa kila wiki katika promosheni inayoendelea ya Tigo Jigiftishe, kimenyakuliwa na Iyaka Seifu Muinga, anayefanya kazi ya kuosha magari Tabata jijini Dar es Salaam.
Muinga anakuwa ni mshindi wa pili wa zawadi ya shilingi milioni 10 baada ya milioni kumi ya kwanza kuchukuliwa na David John Mmuni mkazi wa Changanyikeni jijini Dar es Salaam.

Akipokea zawadi yake katika eneo analofanyia  kazi kutoka kwa Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushangama, mshindi huyo alielezea furaha yake na ksema kuwa Tigo imemkomboa kwa kuwa amepata mtaj wa kufungua biashara.

‘Nimefurahi sana kuibuka na mtaji huu kutoka promosheni ya Jigiftishe. Nitatumia pesa hizi kufungua biashara, ila kusema kweli sina mpango wa kuacha kazi yangu ya sasa,” Iyaka alisema huku akishangiliwa na wafanyakazi wenzake waliomsindikiza jukwaani kupokea zawadi.

Akiongea  wakati akimkabidhi mshindi huyo zawadi yahe, Bushangama aliwataka wateja kuendelea kutumia huduma mbali mbali za Tigo ili kujishindia mamilioni ya shilingi yaliyotengwa kwa ajili ya kuwazawadia katika msimu huu wa sikukuu.
 
 Mmoja wa washindi wa zawadi ya kilaa siku ya shilingi milioni moja kwenye promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Asha Shaban (wa pil kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Bidhaa waa Tigo, Suleiman Bushangama (kushoto) pamoja na Jafary Othman – Mtaalam wa Huduma za Tigo (wa pili kushoto) katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi zawadi zao iliyofanyika eneo la Tabata jijini Dar es Salaam. Wa kwanza  kulia ni Balozi wa promosheni hiyo, mtangazaji Mina Ally.    
6J9A0772-min
Mmoja wa washindi wa zawadi kila siku ya shilingi milioni moja kwenye promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Anna Eliudi Makala  (wa pili kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Bidhaa wa Tigo, Suleiman Bushangama (kulia) pamoja na Jafary Othman – Mtaalam wa Huduma za Tigo (wa pili kulia) katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi zawadi iliyofanyika Tabata jijini Dar es Salaam. 
6J9A0782-min
Mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Iyaka Seifu Muinga (kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Bidhaa wa Tigo, Suleiman Bushangama (kulia) pamoja na Jafary Othman – Mtaalam wa Huduma za Tigo (wa pili kulia) katika hafla fupi ya kumkabidhi washindi zawadi eneo la Tabata jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Balozi wa promosheni hiyo, mtangazaji Mina Ally.

LUGOLA ATAKA MAGEREZA KUANZA KUJENGA VIWANDA VYA SAMANI VYA KISASA NCHINI, ASEMA VILIVYOPO HAVIWEZI KUTUPELEKA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0

Na Felix Mwagara (MOHA), Arusha

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelitaka Jeshi la Magereza lianze maandalizi ya ujenzi wa viwanda vya samani vya kisasa kwa kuwa vilivyopo havina hadhi ya kwenda na kasi ya uchumi wa viwanda nchini.

Alisema Viwanda vya Samani cha Ukonga, jijini Dar es Salaam, cha Arusha pamoja na cha Uyui Mkoani Tabora, havina hadhi ya kuitwa viwanda vya kisasa kutokana na uzalishaji wake kuwa mdogo na pia ukubwa wa viwanda hivyo ni mdogo.

Akizungumza leo akiwa katika Kiwanda cha Samani cha Magereza kilichoungua moto mwezi uliopita eneo la Unga Limited, jijini humo, Lugola alisema kiwanda hicho kilichoungua hakuna haja ya kukijenga kingine katika eneo hilo kwa kuwa kiwanda hicho ni kidogo, hivyo maandalizi ya ujenzi wa kiwanda kipya cha kisasa uanze kuanzia sasa. Alielekeza kuwa, kwa kuwa eneo hilo ni dogo, linatakiwa liboreshwe kwa ajili ya kuhifadhiwa samani ambavyo zitakua zimetengenewa katika kiwanda cha kisasa kitakachojengwa jijini humo.

“Kamishna Jenerali wa Magereza, aanzeni maandalizi ya ujenzi wa kiwanda kingine ambacho kitakua cha kisasa, hili eneo ni dogo mno, na pia hata cha kule Ukonga Dar es Salaam, eneo lake ni dogo, tafadhali anzeni kufikiria kwa upana zaidi kuanza maandalizi ya kutengeneza viwanda hivyo vya kisasa,” alisema Lugola. Lugola aliongeza kuwa, Jeshi la Magereza lina maeneo mengi nchini ya kuweza kujenga viwanda hivyo ambavyo vitaenda kuongeza kasi ya uchumi wa viwanda nchini ambao aliutangaza Rais Dk. John Magufuli katika mipango ya maendeleo ya nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto), akimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza, (CGP), Phaustine Kasike alipokua anamuonyesha moja ya mashine iliyoungua na moto mwezi uliopita katika Kiwanda cha Samani cha Magereza jijini Arusha, wakati Waziri huyo alipokitembelea kiwanda hicho leo, kuangalia moto ulivyokiteketeza kiwanda hicho. Lugola aliwataka viongozi wa Magereza kuanza maandalizi ya ujenzi wa viwanda vya samani vya kisasa katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Tabora ikiwa ni hatua ya kwenda na kasi na uchumi wa viwanda nchini. Kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho, SP Victor Ngwale. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimpa maelekezo   Kamishna Jenerali wa Magereza, (CGP), Phaustine Kasike (kushoto), akiwa nje ya jengo la kiwanda cha Magereza cha samani ambacho kiliungua mwezi uliopita jijini Arusha. Lugola alikitembelea kiwanda hicho leo, kuangalia moto ulivyokiteketeza na kumtaka CGP kuanza maandalizi ya ujenzi wa viwanda vya samani vya kisasa katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Tabora ikiwa ni hatua ya kwenda na kasi ya uchumi wa viwanda nchini. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akimsikiliza Mkuu wa Kiwanda cha Samani cha Magereza, jijini Arusha, SP Victor Ngwale  (kulia), alipokua akimfafanulia jinsi kiwanda hicho kilipotekea kwa moto mwezi uliopita na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha. Lugola alikitembelea kiwanda hicho leo, kuangalia moto ulivyokiteketeza na kumtaka CGP kuanza maandalizi ya ujenzi wa viwanda vya samani vya kisasa katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Tabora ikiwa ni hatua ya kwenda na kasi ya uchumi wa viwanda nchini. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza, (CGP), Phaustine Kasike. 


OPERESHENI YA UVUVI HARAMU YAPAISHA MAPATO SERIKALI KUU, SAMAKI WAONGEZEKA

$
0
0

“Operesheni uvuvi haramu yapaisha mapato ya serikali kuu”

Operesheni za kudhibiti uvuvi haramu hapa nchini, zimeiwezesha serikali kuu kupata mrabaha wa Shilingi Bilioni 2.2 kuanzia Mwezi Desemba mwaka 2017 hadi Mwezi Novemba mwaka 2018, kutoka Shilingi Milioni 457.

Hayo yalibainishwa (01.12.2018) Jumamosi jijini Mwanza na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akiongoza kikao cha kufanya tathmini ya operesheni sangara kitaifa awamu ya tatu kwa mwaka 2018, kanda ya Ziwa Victoria, kikao kilichohudhuriwa na maafisa waliohusika katika operesheni hiyo, ambapo amesema kiasi hicho cha pesa kimeongezeka kutokana na mafanikio ya udhibiti wa mianya ya utoroshaji fedha.

“Mwaka 2017 mpaka tunafunga mwaka mwezi Desemba mrabaha wa serikali kuu kabla ya kufanya operesheni ulikuwa Shilingi Milioni 457, mwaka 2018 hadi Mwezi Novemba mrabaha wa serikali kuu ni Shilingi Bilioni 2.290, kutoka Shilingi Milioni 457 mpaka Shilingi Bilioni 2.290 unaweza kuona kwamba ni ongezeko la zaidi ya asilimia 200, hii maana yake kulikuwa na utoroshaji mkubwa wa fedha ambazo zingeingia katika mfumo mkuu wa serikali.” Alisema Mhe. Ulega.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akitoa maelezo ya tathmini ya kitaifa ya operesheni sangara awamu ya III, mwaka 2018 kanda ya Ziwa Victoria kwa washiriki wa operesheni hiyo (hawapo pichani).
Afisa Mfawidhi kanda ya Ziwa Victoria Bw. Didas Mtambalike akisoma tathmini ya kitaifa ya operesheni sangara awamu ya III, mwaka 2018 katika kanda hiyo, kwa washiriki wa kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega.

Baadhi ya washiriki wa operesheni sangara awamu ya III, mwaka 2018 wakifuatilia maelezo ya tathmini ya operesheni hiyo ilivyokuwa ikitolewa katika kikao hicho.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi washiriki wa operesheni sangara awamu ya III, Mwaka 2018 katika Kanda ya Ziwa Victoria



MTOLEA AELEZA SABABU ZA KUJIUNGA CCM,AWAONYA WANAOBEZA JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KULETA MAENDELEO

$
0
0
Na Khadija Seif,Globu ya jamii

ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam Abdallah Mtolea amewaambia wajumbe wa Baraza la Hamashauri ya Manispaa ya Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuwa amefanya uamuzi sahihi kujiunga na Chama hicho.

Mtolea ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Wananchi(CUF)alitangaza kujiuzulu ubunge na nafasi zote ndani ya CUF siku za hivi karibuni akiwa Bungeni Mjini Dodoma.

Hivyo kwa sasa amejiunga na CCM na leo wakati anazungunza kwenye baraza hilo la halmashauri ya manispaa ya Temeke ameeleza kwa kina sababu za kuondoka CUF.Akifafanua zaidi wakati akifungua kikao cha baraza hilo Mtolea amesema uamuzi sahihi kurudi CCM katika kuendeleza na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora katika kila sekta nchini.

Amebainisha kuwa wapinzani wapo kwa ajili ya kupinga juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano na kazi kubwa ni kubeza na kushawishi vijana kufanya ushabiki ambao hauna manufaa kwa maslahi ya nchi na Taifa kwa ujumla.Pia Mtolea amezungumzia wasanii ambapo amesema hawajakatazwa kufanya kampeni bali wasanii wa Mkoa husika wapatiwe vipaumbele katika kuonesha vipaji vyao.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Kata ya Temeke kupitia CCM Fadhili Faungo amesema kuwa Rais Dk.John Magufuli amekuwa anashirikiana bega kwa bega na vijana kwani anaamini vijana ndio nguvu kazi ya Taifa .Pia amesema lengo la kukutana kwa wajumbe wa Baraza hilo ni kuangalia miradi ya maendeleo ambayo itatekelezwa kupitia fedha ambazo zimetolewa na Serikali.

Wakati huo huo imeelezwa kuwa baadhi ya wajumbe wameshawasilisha mawazo yao katika matumizi ya kufungua biashara ambazo zitaleta chachu ya kuongeza pato la Taifa.
ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam Abdallah Mtolea akizungumza mbele ya Wajumbe wa Baraza la Hamashauri ya Manispaa ya Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuwa amefanya uamuzi sahihi kujiunga na Chama hicho.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA JIJI LA ARUSHA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Maji safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Isaack Kamwelwe pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi mkubwa wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira utakaosaidia jiji la Arusha katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Kimyaki Arumeru mkoani Arusha.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia maji yanayotoka katika moja ya visima virefu vilivyopo katika mradi huo mkubwa wa maji safi na usafi wa mazingira katika jiji la Arusha. Mradi huo utakapokamilika utaweza kuzalisha lita za ujazo milioni 200  kwa siku tofauti na sasa ambapo lita za ujazo ni 45 milioni wakati mahitaji ya jiji la Arusha ni lita za ujazo milioni 90.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru wakati wa mkutano na wananchi wa Arumeru jijini Arusha mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Arumeru. PICHA NA IKULU

KAIMU MTENDAJI MKUU AITAKA TEMESA TANGA KUONGEZA UZALISHAJI

$
0
0
ALFRED MGWENO (TEMESA TANGA) 

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Japhet Y. Maselle, amehitimisha ziara yake mkoani Tanga kwa kuwataka watendaji na viongozi wa Wakala mkoani humo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa ili kuinua mapato ya kituo hicho.

Akizungumza na wafanyakazi wa TEMESA Tanga pamoja na mafundi wa karakana mara baada ya kuwasili mkoani humo, mhandisi Maselle aliwasisitizia suala la ubunifu hasa katika upande wa karakana ambapo aliwataka kuiga mfano kutoka mkoa wa Singida ambao uzalishaji wake umeongezeka kwa kipindi cha hivi karibuni kutokana na kubuni njia mbalimbali ili kuongeza pato lake ikiwemo kuepuka kupeleka kazi ndogo ndogo za ufundi katika karakana teule. 

Vilevile alipata pia fursa ya kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utendaji kazi wao pamoja na kukagua baadhi ya mitambo iliyopo katika karakana hiyo. Changamoto kubwa iliyoonekana ilikuwa ni uchakavu wa mitambo ambapo Mhandisi Maselle alisema kuwa ni vyema sasa Wakala ukaanza utaratibu wa kununua mitambo mipya ili kuongeza ufanisi zaidi upande wa Ukodishaji mitambo. 
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akitoa maagizo wakati akikagua gari ya kubeba mitambo mbalimbali (low bed truck) katika karakana ya TEMESA mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake mkoani humo kukagua utendaji kazi na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wa wakala huo. Kushoto ni Kaimu Meneja Mhandisi Mhangaiko Ngoroma. 
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akikagua Propela ya kivuko cha MV. PANGANI II ambacho kinafanyiwa ukarabati mkubwa katika yadi ya Songoro, kivuko hicho kinatarajiwa kuungana na kivuko cha MV. TANGA kutoa huduma katika eneo la Pangani na Bweni katika eneo la mto Pangani mara baada ya kukamilika kwa matengenezo yake. Nyuma yake ni Mkuu wa Kivuko cha Pangani Bweni Mhandisi Abdulrahman Ameir. 
vuko cha MV. TANGA kinachotoa huduma katika mto Pangani, kati ya Pangani na Bweni wilayani Pangani mkoani Tanga kikielea majini wakati kikiendelea kutoa huduma ya kuvusha abiria na magari. 
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle wa pili kushoto akisisita umuhimu wa kuzingatia usalama wa vivuko kwa wafanyakazi wa kivuko hicho wakati wote wanapotoa huduma hiyo katika kivuko cha MV TANGA kinachotoa huduma katika mto Pangani, kati ya Pangani na Bweni wilayani Pangani mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua usalama wa vivuko. 

INTRODUCING :Fik Fameica Ft Rayvanny - Mwaga (Official Video)

WATUMISHI WA SERIKALI MAKADA WA CCM SHINYANGA WAANDAMANA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI

$
0
0
Watumishi wa serikali kutoka idara mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi -CCM, wameandamana kumpongeza Rais John Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya ya kizalendo na kutetea wakulima kwa kupambana na wanyonyaji ambao wamekuwa wakitajirikia jasho lao na wao kubaki maskini.

Maandamano hayo yamefanyika leo Jumapili Desemba 2,2018 kutoka katika Soko Kuu la mjini Shinyanga hadi kwenye ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kufikisha ujumbe wao kwa Rais Magufuli za kuunga juhudi za utendaji wake kazi. 

Akizungumza mara baada ya kumaliza maandamano hayo. Msemaji wa umoja huo wa watumishi wa Serikali ambao ni makada wa CCM Christopher Malengo,sambamba na kutoa tamko lao mbele ya katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwambwa, amesema wameguswa na kazi ya kizalendo ambayo anaifanya Rais Magufuli ya kupigania maslahi ya wanyonge wakiwamo wakulima.

 Amesema Rais Magufuli amekuwa akijikita katika misingi ya ujamaa,utu,uzalendo na haki kama alivyokuwa akifanya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye utawala wake, katika kuhakikisha anapigania maslahi ya wanyonge na kukomesha wanyonyaji ili wananchi wote waweze kupata haki sawa, vitendo ambavyo zinapaswa kupongezwa.
Watumshi wa Serikali katika idara mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini ambao ni Makada wa Chama Cha Mapinduzi CCM wakiwa kwenye maandamano ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake mzuri wa kizalendo hasa kupigania maslahi ya wakulima,huku wakiwa wamebeba mabango ya pongezi hizo. Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwambwa akipokea mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kumpongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake kazi hasa kupigania wanyonge ili kuwainua kiuchumi. Upokeaji wa mabango ukiendelea. 

Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara Kushiriki katika Mafunzo ya Uongozi

$
0
0
Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa hamsini na mbili wa Tanzania Bara wanatarajiwa kushiriki katika programu ya mafunzo ya uongozi kwa kipindi cha wiki moja kuanzia Jumatatu ya tarehe 3 Disemba, 2018 hadi Ijumaa ya tarehe 7 Disemba, 2018, mkoani Dodoma. 

Warsha hiyo ya mafunzo ambayo imeandaliwa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) itafunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) leo. 

Kwa mujibu wa Taasisi ya UONGOZI, programu hii ya mafunzo ya uongozi, ni ya kwanza ya aina yake iliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa. 

“Lengo la programu hii ni kuimarisha uwezo wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika kufanya maamuzi ya kimkakati, kuongoza watu na kusimamia rasilimali nyingine, pamoja na kujijengea sifa binafsi za uongozi,” alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Joseph Semboja. 

Prof. Semboja pia alisema, “Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa wana nafasi muhimu katika kuwezesha ukuaji na maendeleo ya nchi. Hivyo, tunatarajia kwamba kupitia programu hii, uwezo wao wa kuongoza utaimarika na kuwawezesha kuchangia katika jitihada za kuleta maendeleo endelevu nchini na hatimaye, barani mwetu.” 

Prof. Semboja aliongezea kwamba huu ni mwendelezo wa jitihada za Taasisi ya UONGOZI na Ofisi ya Rais, TAMISEMI zinazolenga kuwafikia viongozi wengi iwezekanavyo wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ili kupanua uelewa wa masuala ya uongozi na kuongeza tija ya shughuli wanazozifanya za kuwatumikia wananchi. Kati ya Mei 2017 na Oktoba 2018, mafunzo ya uongozi yalitolewa kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa na Wilaya, kwa awamu tano tofauti. 

Warsha hiyo ya mafunzo ya siku tano itajumuisha mada kuu zifuatazo; Uongozi Binafsi na Akili Hisia, Mwingiliano na Mahusiano baina ya Viongozi wa Kisiasa na Viongozi Watendaji, Mawasiliano ya Kimkakati, Itifaki, Masuala yanayohusu Ulinzi na Usalama, Usimamizi wa Fedha za Umma na Rasilimali Nyingine, Manunuzi katika Sekta ya Umma na Udhibiti wa Madawa ya Kulevya. 

DC KAWAWA AAGIZA MWEKA HAZINA NA WATUMISHI WATATU IDARA YA FEDHA HALMASHAURI YA CHALINZE KUKAMATWA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO

MKUU wa wilaya ya Bagamoyo ,Mkoani Pwani ,Zainabu Kawawa ameagiza 
watumishi wa idara ya fedha wanaoshughulika na ukusanyaji mapato katika halmashauri ya Chalinze, wakamatwe ili kupisha uchunguzi na watakapobainika kusababisha upotevu wa mapato hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Amefikia hatua hiyo, kufuatia hali ya ukusanyaji mapato katika halmashauri hiyo kuwa chini ya kiwango ,kutoka wastani wa sh. milioni 950 kwa mwezi na kushuka hadi milioni 550-659 .#

Zainabu alitoa agizo hilo ,wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo.Aliwataja wahusika hao kuwa ni pamoja na mweka hazina David Rubibira na wahasibu watatu ambao ni Waziri Ally,Jumanne Sanga na Maneno Kwambwa,ili kupisha uchunguzi .

Zainab alisikitishwa na ukusanyaji mapato kwa kudai kuna mianya ya ubadhirifu wa mapato kwani mapato yakikusanywa kwa umakini yanafikia sh. milioni 920 kwa mwezi kwa chanzo cha madini ya kokoto nje ya vyanzo vingine kwa maana ya sh. milioni 33 kwa siku.

Hata hivyo ,kutokana na makisio hayo Zainab aliondoa imani na mapato yanayokusanywa katika halmashauri hiyo ambayo ni wastani wa milioni 550 hadi 659 kwa mwezi.Katika kikao hicho alimtaka mkuu wa polisi Chalinze kuwaweka chini ya ulinzi na kuwachukua kwa ajili ya uchunguzi .

"Nimekuwa nikifuatilia ukusanyaji mapato kuna mianya mingi ya utoroshaji mapato, tusitafutane wala kujaribiana kwa kuvujisha mapato tumepoteza mapato sana kwenye makrasha kwa siku tuna uwezo wa kukusanya milioni 33 ,kwa mwezi tuna uwezo wa kukusanya zaidi ya milioni 900"

"Badala ya kufuatilia na kukagua mnakaa ofisini ,katika hili hatuwezi kuvumiliana hata kidogo,,"mkurugenzi nakuagiza watumishi wanaohusika na mapato wakae pembeni kwa hatua zaidi kuanzia leo .Zainab alisisitiza , vyombo vya usalama vifanye kazi katika kuchunguza suala hilo.

MUWAKILISHI WA JIMBO LA MAGOMENI AKABIDHI MIPIRA YA MAJI.

$
0
0
Na Mwashungi Tahir - Maelezo Zanzibar

MWAKILISHI wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi amewaomba wananchi wa magomeni wandaras kuwa na mashirikiano na viongozi wao ili wanapopeleka huduma muhimu za maendeleo kwa jamii zipate ufumbuzi.

Hayo ameyasema huko Magomeni Wandaras wakati alipokuwa akikabidhi wananchi mipira ya maji katika shehia hiyo ikiwa anatimiza ahadi yake ili wananchi wa shehia hiyo waweze kupata huduma ya maji safi na salama kwa ukaribu na kupunguza masafa marefu yaliyokuwa yakiwakabili.

Amesema iwapo viongozi wa jimbo wanajitokeza kwa kuleta huduma za maendeleo inapaswa kuthamini na kuyafanyia kazi kwa moyo mmoja ili na wao waweze kufarijika zaidi na kuongeza kutatua changamoto nyengine zitazojitokeza .

Amesema wakati mliponichagua niliahidi kutatua changamoto na kuleta mambo ya maendeleo katika jimbo kati ya ahadi hizo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote muhimu miongoni mwa hayo ni maji safi na salama hii ikiwa ilani ya Chama chetu cha Mapinduzi kuwajali wananchi wake katika pande zote.
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi akikabidhi Mipira ya maji kwa Mzee wa mtaa Azizi Mbarouk Omar ( Kushoto) huko Shehia ya Magomeni Wandaras Mjini Unguja.Picha na Mwashungi Tahir – Habari Maelezo.

Wahitimu Chuo cha Mipango Watakiwa Kutumia Ujuzi Wao kwa Manufaa ya Taifa

MNYETI AWAFAGILIA DC WA KITETO NA SIMANJIRO

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti amewafagilia wakuu wa Wilaya za Kiteto mhandisi Tumaini Magessa na Simanjiro mhandisi Zephania Chaula kuwa ndiyo wakuu wa wilaya bora kwa sasa kwenye mkoa wake, wenye kuchapa kazi na kuhudumia wananchi. 

Mnyeti akizungumza mjini Babati alisema mkuu wa wilaya ya Kiteto mhandisi Tumaini Magessa na mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula, ndiyo wakuu wa wilaya bora kwa sasa mkoani Manyara. 

Alisema anataja majina hayo mawili ya wakuu hao wa wilaya ili iwe changamoto kwa wakuu wengine wa wilaya za mkoa huo wenye wilaya tano, kutekeleza wajibu wao ipasavyo. Alisema wakuu wengine wa wilaya ambao hawajatajwa wasife moyo ila waongeze bidii na juhudi katika kuwatumikia wananchi na kutekeleza wajibu wao ipasavyo. 

Alisema anatangaza majina ya wakuu hao wa wilaya wanaongoza mkoani humo baada ya yeye kushauriana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Simon Lulu na Katibu Tawala wa mkoa huo Missaile Mussa, ndipo wakapatikana hao. Alisema mkuu wa wilaya anapaswa kutoa maamuzi kwenye eneo lake la utawala na siyo kupiga simu kwa mkuu wa mkoa kila wakati kuomba msaada ili hali uwezo wa kutoa maamuzi anayo. 
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mhandisi Tumaini Magessa ambaye ametangazwa na Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti kuwa ndiyo anaongoza kwa uchapakazi.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, mhandisi Zephania Chaula akisalimiana na wananchi wa eneo lake, mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amesema anashika nafasi ya pili kwa kuchapa kazi. 

MICHUZI TV: Aika:Nahreel ananipa Mzuka Jukwaani hadi napagawa.

MICHUZI TV: Queen Darleen: Kuvaa nusu uchi kumeniongezea Mashabiki...!

Viewing all 110031 articles
Browse latest View live




Latest Images