Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

UNAIDS kuendelea kushirikiana na serikali kupambana na UKIMWI

0
0
Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng amesema kuwa kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya Ugonjwa huo.
Akizungumza jana Jijini Dodoma wakati wa kilele cha shughuli za vijana kuelekea maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, Dk Zekeng alisema kwamba kuna haja kubwa ya kuhakikisha kwamba taifa linapambana na maambukizi mapya kwa kuhakikisha kwamba kunatolewa huduma rafiki miongoni mwa vijana ambao ndio kundi kubwa linalohitaji msaada kwa sasa ni jukumu la kila mwanajamii na kuomba ushirikiano wadau wote katika mapambano hayo.
Alisema wakati taifa nusu yake ni vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 na huku takwimu zikionesha kwamba kundi hilo linaathirika sana ipo kila sababu ya kutengeneza mkakati na kuweka mazingira rafiki ili kuokoa kizazi hicho. Alisema kwa sasa vijana wanahitaji kusaidiwa kwa kuwaweka katika mazingira rafiki ya kuhitaji huduma zinazotolewa katika kampeni ya kukabiliana na maambukzi ya VVU.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akihutubia wananchi wa Dodoma wakiwemo vijana wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akitoa salamu za Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
 Balozi wa Vijana ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo akizungumza na hadhira ya vijana (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akitoa neno kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akikabidhi zawadi ya kombe ya mshindi wa kwanza kwa kapteni wa timu ya mpira ya vijana walio nje ya shule ya Panama, Bw. Dunia Salumu wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akikabidhi zawadi ya kombe ya mshindi wa kwanza kwa kapteni wa timu ya mpira wa pete ya Vijana Queens, Ngesa Selemani wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Baadhi ya wakazi wa Dodoma walioshiriki hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wasomi waaswa kuleta matokeo cha chanya kwa kufanya ubunifu

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa kila mwaka kuna  wahitimu wengi ambao wanaingia katika soko la ajira lakini hakuna matokeo ya kazi wanazozifanya. Hayo aliyasema  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji wakati wa mahafali ya 44 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Amesema ripoti ya Tanzania katika kuandaa rasimali watu iko chini ya asilimia 62 ya viwango vya Dunia ambapo Tanzania imefikia asilimia  53 kufikia huko kumetokana na watu kukosa ubunifu na ujuzi. Dkt. Kijaji amesema kuwa katika viwango na ujuzi na ubunifu kwa viwango vilivyowekwa ni asilimia 50 ambapo Tanzania  imefikia asilimia 40 hivyo wasomi lazima kuondoa hali hiyo.

Amesema kuwa mikopo Chechefu kupanda kwake kumetokana na wataalam wa fedha ambapo wamepandisha kutoka asilimia 5 hadi kufikia asilimia 10 na kuendelea. "Mikopo Chechefu kupanda hakujanywa na mashine bali ni sisi wenyewe ni kazi kwetu wa wataalam wa fedha kutafakari katika kusaidia maendeleo ya Taifa"amesema Dkt.Kijaji. 

Hata hivyo amekipongeza Chuo katika ujenzi wa Chuo katika makao makuu jijini  Dodoma na kutaka wajenge kwa kutumia wabia na sio serikali kutoa fedha. Nae Mkuu wa Chuo hicho Dkt Tadeo Sata amesema kuwa cho kina changamoto ya walimu pamoja na kuwa na eneo la dogo.  Amesema kuwa wanatarajia kujenga Chuo cha Biashara katika eneo la Nara jijini Dodoma katika kuwasogezea huduma wafanyakazi wa serikali. Aidha amesema kuwa Chuo kimeendelea kuwa na ushirikiano na wadau katika utaoaji wa elimu bora.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mpango Dkt. Ashatu Kijaji  akizungumza katika mahafali ya 44 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dkt. Tadeo Sata akitoa taarifa ya Chuo katika mahafali 44 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya wadau wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM wakiwa katika mahafali ya 44 yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
 Wahitimu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) katika mahafali ya 44 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa shahada ya uzamili wakiwa katika mahafali ya 44 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATIKA KATA SITA

0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewasihi wapiga kura wote waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na wanaoishi kwenye kata Sita za Tanzania Bara, kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Jumapili  Desemba 2  mwaka huu ili kuwachagua viongozi wanaowataka wawaongoze kwa kipindi cha takribani miaka miwili ijayo.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage wakati akisoma risala ya uchaguzi mdogo wa Udiwani unaohusisha  kata za Miteja, Kivinje au Sigino , Somanga na Mitole  katika Halmashauri ya Kilwa, kata ya Muhinda katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe na Kata ya Nkoanekoli katika Halmashauri ya wilaya ya Meru.

“Wapiga Kura wapatao 31,818 wanatarajiwa kupiga Kura kuwachagua Madiwani katika Kata 6 za Tanzania Bara na uchaguzi huo utafanyika katika Vituo 91 vya Kupigia Kura ambako ndipo Wapiga kura walijiandikishia kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015. Aliwataka kwenda kupiga kura bila hofu, woga, wasiwasi au ushawishi kwani chini ya Kanuni ya 3.1 (b) ya Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, Serikali imepewa wajibu wa kuhakikisha kuwa kuna hali ya usalama, amani na utulivu katika kipindi chote cha Uchaguzi.

Mbali na wito huo, Jaji Kaijage aliwataka wananchi, vyama vya Siasa na wadau wote wa uchaguzi kushirikiana ili kuhakikisha kuwa viashiria vya kuvunjika kwa amani na utulivu vinaepukwa ili uchaguzi utakaofanyika uwe huru, wazi na wa haki. Jaji Kaijage alivisisitiza vyama vya siasa kufanya  mikutano ya kampeni inatakiwa kufikia mwisho leo Jumamosi  saa kumi na mbili kamili (12:00) jioni na baada ya muda huo, vyama, wagombea na mashabiki waache kufanya kampeni za aina yoyote, kama vile kutumia alama za vyama zinazoashiria kampeni, vipeperushi, bendera, mavazi na vitu vingine visivyokubalika katika siku ya Uchaguzi.

“Aidha, wananchi waheshimu Sheria za Nchi wakati wote wa upigaji, kuhesabu, kujumlisha kura na kutangaza matokeo. Pale panapokuwa na malalamiko yoyote ya ukiukwaji wa Sheria na Taratibu za Uchaguzi, malalamiko hayo yafikishwe kwenye mamlaka inayohusika kwa utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria.”, alisema Jaji Kaijage na kuongeza kuwa:

“Vivyo hivyo, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Wagombea au wafuasi wao na wananchi kwa ujumla wajiepushe na vitendo vinavyoweza kusababisha fujo au vurugu katika vituo vya Kupigia, Kuhesabia na Kujumlishia Kura.” Jaji Kaijage aliwataka wapiga kura kuondoka kwenye maeneo ya kituo cha kupigia kura mara baada ya kupiga kura na kujiepusha na mikusanyiko au mikutano katika maeneo ya vituo vya kupigia kura kwani vyama vya siasa vimeweka mawakala vituoni ambao watalinda maslahi ya vyama husika na wagombea wao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA RAIS KENYATTA WAFUNGUA KITUO CHA KUTOA HUDUMA KWA PAMOJA MPAKANI NAMANGA

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakipata maelezo ya kituo hicho cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na   Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakipungia wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano pembezoni mwa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi funguo Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea funguo kutoka kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakipanda mti mara baada ya mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakimwagia maji mti mara baada ya kuupanda wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakiwa wameshikana mkono wakati  wakimwagia maji mti mara baada ya kuupanda wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na   Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakielekea upande wa mpaka wa Tanzania mara baada ya ufunguzi wa kituo cha kutoa huduma kwa pamoja kwa upande wa Kenya.PICHA NA IKULU

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BABA ADAIWA KUWAUA WATOTO WAKE WATATU AKIWEMO WA MIEZI 10

0
0

Na Mwamvua Mwinyi
JESHI la polisi mkoani Pwani, limethibitisha kutokea kwa vifo vya watoto watatu akiwemo wa miezi kumi, waliouawa kwa kunyweshwa sumu na baba yao mzazi. Chanzo cha kutenda kitendo hicho cha kikatili kinadaiwa ni kutokana na ugomvi mkubwa kati ya wazazi wa watoto hao. Kamanda wa polisi mkoani humo ,Wankyo Nyigesa alieleza tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana huko maeneo ya Kibindu ,Chalinze .

Aliwataja watoto hao kuwa ni pamoja na Shaila Salehe miaka sita ,Nurdin Salehe (4)na Sabrat Salehe mwenye miezi kumi waliouawa kwa kunyweshwa sumu ambayo ni dawa ya kuulia magugu iitwayo Twiga Amine na baba yao mzazi Salehe Masokola (22),mkazi wa kijiji cha Kunwe ,Mvomero mkoa wa Morogoro . Wankyo alibainisha,baba wa watoto hao alikuwa na mgogoro na mkewe ambae ndiye mama wa watoto .

"Mtuhumiwa alipowafuata watoto kutoka kwa mama mkwe wake kwa madai kwamba anakwenda kucheza nao na angewarudisha baadae " alifafanua Wankyo. Alielezea,mtuhumiwa aliwapakia marehemu kwenye baiskeli kutoka Kunke hadi kitongoji cha Ditele ,Kibindu ambapo aliwanywesha dawa hiyo kwa kuwachanganyia na juisi hivyo kupelekea vifo vya watoto hao. Kamanda huyo alisema ,katika eneo la tukio kumeokotwa chupa mbili za juisi zilizotumika ,chupa ya dawa na matapishi ambavyo vilichukuliwa kwa uchunguzi zaidi.

"Mara baada ya tukio mtuhumiwa alikunywa sumu kwa lengo la kutaka kujiua lakini aliokolewa na watu kisha kukimbizwa katika hospital ya mission Bwagala wilaya ya Mvomero kwa matibabu" Wankyo aliweka bayana. Mpaka sasa hali yake sio nzuri kwani yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi akiwa chini ya uangalizi wa polisi .Katika hatua nyingine ,Wankyo alisema jeshi hilo limekamata viroba saba vya bangi vilivyokuwa vikisafirishwa kwenye gari yenye chesesi namba V75w - aina ya mitsubishi station wagon huko Mwatemo Kiwangwa ,Bagamoyo
Kamanda wa polisi wa mkoani Pwani,Wankyo Nyigesa akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani hapo .(picha na Mwamvua Mwinyi)

WAZIRI MHAGAMA AAGIZA UONGOZI WA NSSF KUWA NA UZALENDO KATIKA UTENDAJI

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Waziri Mhagama ameuagiza uongozi wa Shiriki la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kubadili mitazamo dhaifu ya kiutendaji na kuanza kufanya kazi kwa kuongozwa na uzalendo ili kuleta tija na kufikia malengo ya Shirika hilo.

Ametoa kauli hiyo mapema mwishoni mwa wiki hii (Novemba 29, 2018) alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi inayoratibiwa na shirika hilo ikiwemo ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu Dar es Salaam. Maeneo aliyotembelea ni pamoja na; miradi wa nyumba za bei nafuu za Dungu, Mtoni Kijichi, Tuangoma na Mzizima pamoja na nyumba za Dege Beach Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Kauli ya waziri imekuja mara baada ya kutoridhishwa na hali ya maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo na kuuagiza uongozi wa Shirika hilo kubadili mitazamo ili kuwa na malengo yanayotekelezeka na kwa wakati. “Kwa muda mrefu mmekuwa mkifanya kazi kwa kujitenga katika makundi, mnapaswa kubadili mitazamo hasi na kuwa na mitazamo chanya yenye utendajikazi katika hali ya umoja ili kuendelea kubadili NSSF ili iwe na uzalizaji wa tija”.alieleza Mhagama

Waziri aliongezea kuwa Shiriki linapaswa kubadili hali za mazoea yaliyokuwa si mazuri ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano iliyojikita katika uwajibikaji wa kizalendo. “Lazima mbadili mitazamo ya uongozi  wa mazoea na kuanza kufanya kazi kwa umoja ili kuwa na matokeo chanya yanayokusudiwa ili kuwa na tija kwa jamii na Serikali kwa ujumla”.Alisisitiza Mhagama
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama akiuliza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw.William Erio wakati wa ziara yake katika mradi wa ujenzi wa nyumba za Denge Beach Kigamboni Jijini Dar es Salaam Novemba 29, 2018.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama akiangalia ramani ya ujenzi wa mradi wa Dege Beach Kigamboni uliojengwa na Shirika la Mifuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF Dar es salaam, wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi huo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama akiuliza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw.William Erio (mwe nye koti la kijivu) wakati wa ziara yake eneo la Dungu lenye nyumba 439 ambapo tayari nyumba 94 zimekamilika katika eneo hilo.
 Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF Bi Jayne Nyimbo akitoa maelezo ya ufafanuzi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama wakati wa ziara yake katika mradi wa nyumba za Dege Kigamboni Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

CHUO CHA MIPANGO KUANZISHA KIWANDA CHA KUCHAKATA NGOZI MKOANI DODOMA

0
0
Na Benny Mwaipaja. WFM, Dodoma
CHUO Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, kimeanza ujenzi wa Kiwanda cha Kuchakata Ngozi na Kuzalisha Bidhaa za Ngozi katika Kata ya Idifu, Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kitakacho gharimu zaidi ya shilingi milioni 500 kitakapo kamilika. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Hozen Mayaya wakati wa sherehe za mahafali ya 32 ya Chuo hicho Kampasi ya Dodoma, ambapo wahitimu 2,596 wametunukiwa vyeti na shahada mbalimbali.

"Kupitia mradi wa Eco Act, unaofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya, Chuo kimetekeleza falsafa ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, ya Ujenzi wa uchumi wa viwanda hiki ambacho kikikamilika kitakuwa na jumla ya wafanyakazi 70, kati ya hao 50 watakuwa wa kudumu na vibarua 20" alisisitiza Prof. Mayaya. Aidha, Prof Mayaya ameeleza kuwa Chuo hicho kinatekeleza mradi mwingine wa kuhimili mabadiliko ya Tabia nchi kwa kuzijengea uwezo Halmashauri za wilaya ya  Longido, Ngorongoro na Monduli mkoani Arusha ambao umepunguza changamoto za ufugaji katika jamii za wafugaji kwa kujenga mabwawa matatu ya kunyweshea mifugo.

"Mradi huu ni wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Taasisi za kimataifa za mazingira na Maendeleo (IIED), Mfuko wa Umoja wa Mataifa na Maendeleo (UNCDF LoCAL), mashirika yasiyo ya kiserikali ya Haki Kazi Catalyst (HKC) na Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), aliongeza Dkt. Mayaya. Kwa Upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Bi. Mugabe Mtani, amesema utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo ya wananchi umelenga kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano iliyojipambanua kuimarisha uchumi wa nchi na maendeleo ya wananchi kwa ujumla
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu akihutubia wahitimu na wageni mbalimbali waliohudhuria katika mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini  yaliyofanyika katika Kampasi ya Chuo hicho, Dodoma.
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, akitoa taarifa ya maendeleo ya Chuo kwa wahitimu na wageni mbalimbali waliohudhuria katika mahafali ya 32 ya Chuo hicho  yaliyofanyika katika Kampasi ya Chuo, Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akimtunuku Shahada ya Uzamili, mmoja wa wahitimu katika mahafali ya 32 ya chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yaliyofanyika katika Kampasi ya chuo hicho, Dodoma.
 Baadhi ya wahitimu wa kada mbalimbali katika chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wakiwa katika sherehe za  mahafali ya 32 ya chuo hicho  yaliyofanyika chuoni hapo Jijini Dodoma.
Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Uzamili katika Chuo cha Maendeleo Vijijini wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu,  wakati wa Mahafali ya 32  yaliyofanyika chuoni hapo Jijini Dodoma.   
(Picha na Saidina Msangi-Wizara ya Fedha na Mipango)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI YAWATOA WASIWASI WAFANYABIASHARA WA UGANDA

0
0
Serikali imewahakikishia wafanyabiashara wa mafuta kutoka uganda kuwa imejipanga kutatua  changamoto zote zilizopo kwenye usafirishaji ili kupunguza gharama za uchukuzi  kati ya Tanzania na nchi hiyo. Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, amesema hayo wakati wa kikao maalum kilichowakutanisha wafanyabiashara wa Mafuta wa Uganda na taasisi za Uchukuzi za Tanzania na kusema kuwa Serikali inatekeleza hayo kwa kuboresha miundombinu ili kuvutia wafanyabiashara wengi zaidi

“Niwahakikishie kuwa changamoto zote zilizoainishwa baada ya majumuisho ya ziara yenu ya siku 5 nchini tutazifanyia kazi", amesema Naibu Waziri  Nditiye. Aidha, Naibu Waziri Nditiye ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ikiwemo upanuzi wa bandari,ukarabati wa reli na ukarabati wa meli ili mizigo inayokwenda Uganda kupitia bandari ya Dar es Salaam ifike kwa wakati.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya Meli, Eric Hamis amesema mpaka sasa tayari wamesafirisha zaidi ya tani elfu kumi na tano za Uganda kwa kutumia meli ya MV Umoja na kusema kuwa wamejipanga kusafirisha mzigo mkubwa zaidi kabla ya mwaka wa fedha kuisha. Sisi kama Kampuni ya meli tuliifanyia ukarabati meli ya MV Umoja na imekuwa ikisafirisha mzigo wa Uganda na niwahakikishie kuwa kupitia ziara hii na jitihada nyingine tunazozifanya tutapata wafanyabishara wengine ambao watasafirisha mizigo yao kwa kutumia meli hii” amesema Hamis.

Kwa upande wake Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi ya Uganda,  Gerald Akini,  amemwahidi Naibu Waziri Mhandisi Nditiye kuwa yale ya kisera yanayohusu Uganda atayafikisha katika ngazi husika ili yafanyiwe kazi ili kuimarisha ushirikiano uliopo kibiashara. Bw Gerald ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa utayari wake wa kuwapokea wafanyabiashara na kuweka mazingira mazuri ili watumie bandari ya Dar es Salaam.

Aidha, ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu ikiwemo kupunguza vituo vya mizani,ujenzi wa reli ya kisasa,uboreshaji wa bandari na kuahidi kuendeleza ushirikiano kwa kushawishi wafanyabiashara wengi zaidi kutumia bandari ya Dar es salaam. Wafanyabiashara wa mafuta kutoka nchini Uganda wamefanya ziara ya siku 5 nchini ambapo wametembelea bandari ya Dar es salaam, Tanga,Mwanza pamoja na kukagua miundombinu ya reli na meli za kampuni ya meli na kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Tanzania kuimarisha biashara baina ya nchi hizo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara wa mafuta wa Uganda mara baada ya kukutani nao jijini Mwanza.


WAZIRI MKUU AZINDUA MKAKATI WA KUDHIBITI UKIMWI

0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2018/19 - 2022/23 ambao unatarajia kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 85 ifikapo mwaka 2023. Matokeo mengine yanayotarajiwa kufikiwa kutokana na mkakati huo ni kupungua kwa maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa watoto kwa chini ya asilimia 5 ifikapo mwaka 2023 na chini ya asilimia 2 ifikapo mwaka 2030.

Waziri Mkuu amezindua mkakati huo leo (Jumamosi, Desemba 1, 2018) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Kitaifa jijini Dodoma na kusema kuwa matayarisho yake yamezingatia matokeo ya mapitio ya Mkakati wa Tatu wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2013/14 – 2017/18. Amesema mbali na matokeo hayo pia mkakati huo utawezesha kupungua kwa vifo vinavyohusiana na ukimwi  kwa asilimia  50 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 70 ifikapo mwaka  2023 na kupunguza unyanyapaa na ubaguzi ifikapo 2023 na kuelekea kutokomeza kabisa ifikapo mwaka 2030. 

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema mkakati huo umewianisha na kupanga programu mbalimbali zinazosaidia mwitikio wa Taifa zikiwemo afua zinazotekelezwa kupitia mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa uKIMWI (PEPFAR). “Pia Mfuko wa Dunia wa kudhibiti UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Globa Fund) na jitihada nyingine za makubaliano ya ushirikiano baina ya nchi mbalimbali na ili kupata matokeo mazuri tunapaswa kuimarisha mawasiliano na uratibu miongoni mwa wadau wote sambamba na kufuata na kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi Tanzania (2018/19 – 2022/23) katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa, kwenye Kiwanja cha Jamhuri jijini Dodoma, Desemba 1, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.  Faustine Ndugulile na Kushoto, Mkurugenzi Mtendaji  wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Kitabu  cha  Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi Tanzania (2018/19 – 2022/23)  baada ya kuzindua Mkakati huo katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa, kwenye Kiwanja cha Jamhuri jijini Dodoma, Desemba 1, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.  Faustine Ndugulile.
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akimkabidhi Kitabu cha Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi Tanzania (2018/19 – 2022/23) Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Nchini, Alvaro Rodriguez baada ya kuzindua Mkakati huo katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa, kwenye Kiwanja cha Jamhuri jijini Dodoma, Desemba 1, 2018. Watatu kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na Kushoto, Mkurugenzi Mtendaji  wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kwenye Kiwanja cha Jamhuri jijini Dodoma, Desemba 1, 2018.
  Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakipita kwa maandamano mbele ya Mgeni Rasmi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Kilele  cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa, kwenye Kiwanja cha Jamhuri jijini Dodoma, Desemba 1, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

JAMII YAASWA KUACHA FIKIRA POTOFU JUU YA UGONJWA WA KIFAFA

0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Imani potofu ndiyo inayopelekea kuongezeka wa Ugonjwa wa Kifafa katika maeneo mbali mbali ya nchi ya Tanzania hasa Wilaya ya Mahenge, Morogoro.
 

Hayo ameyasema Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja wakati akiwasilisha ufatifi wake  katika muhadhara uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ili kuweza kutoa mapendekezo yake njia za kuweza kusaidia jamii.

Profesa Matuja amesema Jamii inahitaji kuondokana na imani potofu maana watu wengi wamekuwa wakijua kuwa ugonjwa unasambabishwa na ushirikina.Ameongeza kuwa jamii ni bora kujitokeza kupima mara kwa mara ili kuweza kupatiwa tiba mahususi ili kuweza kuondokana na tatizo hilo.

"Nimefanya utafiti katika wilaya ya Mahenge, Morogoro ila tulichogundua mwanzo ni jamii haikuwa na ueleza zaidi kuhusiana na ugonjwa wa kifafa na hivyo kupelekea watu wengi sana kuugua ugonjwa huo, lakini wengi wao wanafikiria imani potofu hasa haya mambo ya ushirikina," ameongeza Prof Matuja.

Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja akiwasilisha utafiti wake juu ya Ugojwa wa Kifafa katika muhadhara wa Kiprofesa uliofanyika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Profesa Matuja alifanya utafiti wa Ugonjwa wa Kifafa kwa muda wa miaka minne katika Wilaya ya Mahenge, Morogoro. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Mwenyekiti wa Muhadhara huo, Prof. Gadi Kilonzo akifungua majadiliano ya kuulizana maswali juu somo la ugonjwa wa kifafa alilolitoa Profesa William Matuja (kushoto). 
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja akiwasilisha utafiti wake juu ya Ugojwa wa Kifafa katika muhadhara uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Profesa Matuja alifanya utafiti wa Ugonjwa wa Kifafa kwa miaka minne katika Wilaya ya Mahenge, Morogoro. 
Wageni waalikwa wakifuatilia muhadhara huo.


Kituo cha Pamoja cha Ukaguzi Namanga Kuiingizia Tanzania Bil. 58 Mwaka Huu wa Fedha

0
0
Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema kituo kipya cha ukaguzi Namanga kinatarajia kuingizia Tanzania Shilingi Bil. 58 mwaka huu wa fedha, 2018/2019. Rais Magufuli ameyasema hayo leo Namanga, Jijini  Arusha wakati wa ufunguzi wa kituo hicho uliofanyika mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Rais Magufuli amesema, kukamilika kwa kituo hicho kumeongeza mapato kutoka wastani wa shilingi Bil. 3 kwa mwezi hadi shilingi Bil. 4.5 kwa mwezi ambapo kwa mwaka huu wa fedha Serikali ya Tanzania inatarajia kukusanya jumla ya shilingi Bil. 58 kutoka katika kituo hicho.

"Ujenzi wa vituo vya huduma za pamoja mipakani vimerahisha huduma za usafiri na kupunguza gharama za muda.Zamani watu walikuwa wakitumia siku nzima kuvuka mpaka, lakini sasa hivi mtu anatumia dakika 15 tu kuvuka mpaka huo," amesema Rais Magufuli.

Amesema, kituo hicho kitawawezesha wafanyabiashara kuvusha bidhaa zao zaidi ya mara  Kumi kwa mwezi tofauti na ilivyokuwa mwanzo ambapo ilikuwa nadra kwa mfanyabiashara kuvuka mpaka huo hata mara Nne kwa mwezi.

Aidha amesema, kituo hicho kitaimarisha shughuli za biashara na utalii kwa nchi zote mbili kutokana na kurahisishwa kwa huduma ya usafiri pamoja na miundombinu mingine katika kituo hicho.

Kwa upande wake, Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta amesema ni jukumu lao viongozi kuhakikisha wananchi wanafanyabiashara bila kupingwa na waweze kuimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili. Amesema dhumuni la ujenzi wa kituo hicho ni kuwarahisishia wafanyabiashara wadogo na wakubwa kufanya biashara zao kwa urahisi, ili kila mwana jumuiya wa Afrika Mashariki aweze kunufaika na umoja huo.

Aidha amewataka wale wote waliopewa jukumu la kusimamia kituo hicho basi wajue kazi yao sio kumnyanyasa mwananchi bali kumsaidia mwananchi afanye biashara yake. Pia wananchi wajue kuwa wakisaidiwa kufanya biashara hawajaambiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya, kuua wanyama au biashara ya magendo bali wanatakiwa kufanya biashara ya haki ili mtu apate fedha yake ya haki.

Nae, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe Balozi Dkt. Augustine Mahige amesema, kuwa na kituo kimoja cha forodha na uhamiaji kinaboresha soko la pamoja la Afrika Mashariki. Vile vile amesema, baada ya soko la pamoja, Jumuiya ya Afrika Mashariki inajiandaa kuwa na sarafu moja ifikapo 2020.

Kituo cha pamoja Namanga kimejengwa kwa ufadhili wa nchi ya Japani kupitia Shirika la Maendeleo la JICA ambapo kwa upande wa Tazania jumla ya shilingi Bil. 18.6 zimegharamiwa . Aidha Benki ya Maendeleo ya Afrika imefadhili kiasi cha Dola za Marekani 117,000 kwa ajili ya kuweka vifaa vya ofisi kwa upande wa Tanzania na Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wanachi wa Kenya na Tanzania katika eneo la Mpakani Namanga mara baada ya hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania na Kenya.


WASHIRIKI WA MBIO ZA MOROGORO MARATHONI 2018 KUJINYAKULIA MEDALI MBILIMBILI

0
0
 Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii  .
WAANDAAJI wa Mashindano ya Mbio za Morogoro Marathon 2018 wametangaza kutoa zawadi ya Medali mbili kwa kila mshiriki wa tukio hilo ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa tukio  kubwa la kimichezo katika mkoa wa Morogoro. Waandaaji hao ambao ni taasisi ya Itetet  Sports Agency imetangaza zawadi hiyo jana mbele ya waandishi wa habari wakati wa kuzungumzia maandalizi ya Mbio hizo zitakazofanyika kesho alfajiri katika uwanja wa Jamhuri mjini humo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Itete Sports Agency ,Antipas Mgungusi alisema mbali na zawadi hizo kwa washiriki pia zipi zawadi kwa washindi wa mbio za Kilometa 21 kwa upande wa wanaume na wanawake ambapo mshindi wa kwanza atapata pesa taslimu kiasi cha sh 400,000 . “Tuna mbio za Kilometa 21 pamoja na kilometa tano,lakini uwanjani kutakuwa na mbio za kushirikisha watoto kwa maana ya mita 100 na mita 200 ,kwa kilometa 21 mbali na pesa taslimu mshindi pia atapata king’amuzi cha DSTV kutoka kwa wadhamini kampuni ya Multchoice “alisema Mgungusi.
Alisema Mshindi wa pili atapata kiasi cha sh 250,000 pamoja na king’amuzi cha DSTV,mshindi wa tatu akiambulia kitita cha Sh 150,000 pamoja na king’amuzi cha DSTV huku wale watakaoshiriki mbio za Km tano mshindi wa kwanza atapata sh 100,000 pamoja na King’amuzi cha DSTV kwa jinsia zote mbili. “Mshindi wa pili kwa kilometa 5 tutatoa kiasi cha sh 50,000 pamoja na T shirt ,mshindi wa tatu atapata cheti pamoja na t shirt nah ii ni kwa wanawake na wanaume watakao shiriki lakini zawadi kubwa zaidi itakuwa ni udhamini kwa washindi watatu wa kilometa 21 na tani kwa wanaume watapata udhamini wa kushiriki mashindano yajayo hapo mwakani”alisema Mgungusi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Itete Sports Agency ,Antipas Mgungusi ambao ndio waandaaji wa Mbio za Morogoro Marathon akizungumza na  wanahabari kuhusu tukio hilo litakalofanyika kesho katika uwanja wa Jamhuri ,kushoto kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga,Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Morogoro ,Grace Njau na kulia ni Fuhad Hussein ,Meneja wa DSTV mkoa wa Morogoro ambao ndio wadhamini
Meneja wa DSTV mkoa wa Morogoro, Fuhad Hussein akizungumza juu ya zawadi za Ving'amuzi zitakazo tolewa kwa washindi wa mbio za Km 21 na Km 5.
Mkurugenzi wa Mbio, Robert Kaliyahe akitoa ufafanuzi wa njia zitakazo tumiwa na wakimbiaji siku ya Kesho.
Medali zilizoandaliwa kwa ajili ya washiriki wa mbio hizo ambazo zitatolewa Mbili kwa kila mshiriki .

UJENZI WA KAMPASI BOKO KUONGEZA IDADI YA KOZI HKMU

0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
CHUO Kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki cha jijini Dar es Salaam, kipo mbioni kujenga kampasi mpya katika eneo la Boko, mradi ambao utaanza mapema mwakani baada ya kukamilika kwa hatua za mwisho za kupata mkopo kutoka katika taasisi ya Norweigian Gurantee Export Credits (GIEK.)

Akizungumza wakati wa mahafali ya 16 katika ngazi mbalimbali za uuguzi na udaktari yaliyofanyika leo Desemba Mosi ,2018 katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam Makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa  Charles Mgone amesema kuwa ujenzi wa Kampasi hiyo mpya utaongeza idadi ya wadahiliwa pamoja na kuongeza idadi ya kozi zitakazotolewa. Aidha amesema kuwa  kwa mwaka huu jumla ya wanafunzi 230 wamehitimu na kutunukiwa shahada mbalimbali na kati ya hao wanaume 104 na wanawake 126 ambao wametunukiwa astashahada, stashahada na shahada.

Amesema kuwa kwa Astashahada ya uuguzi wapo wahitimu 11, stashahada ya uuguzi wahitimu 21, shahada ya udaktari wa binadamu wahitimu 153, shahada ya uuguzi wahitimu 32, shahada ya uzalimili  ya ustawi wa jamii wahitimu 3, shahada ya uzamili wa sayansi ya afya ya jamii wahitimu 2, shahada ya uzamili ya magonjwa na afya za watoto wahitimu 5 na shahada ya uzamili ya Magonjwa ya akina mama wahitimu 3. Mgone amesema kuwa  na kwa mwaka huu wa masomo 2018/2019 wamedahili wanafunzi wapya 293 na chuo kimeendelea kufadhili masomo kwa walimu ngazi ya uzamili na uzamivu na hadi sasa wana walimu 4 wanaosomea shahada ya uzamivu na 3 shahada ya uzamili katika fani mbalimbali.
 Mwenyekiti wa baraza la chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki, John Ulanga akizungumza wakati wa mahafali ya 16 katika ngazi mbali mbali za uuguzi na udaktari yaliyofanyika leo Desemba Mosi, 2018 katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki Profesa Charles Mgone, akizungumza wakati wa kuhudhurisha na kutunuku wahitimu 230 waliohitimu mwaka huu ambapo ameeleza kuwa wana mpango wa kujenga kampasi mpya itakayoongeza idadi ya wanafunzi na kozi zitakazotolewa wakati wa mahafali ya 16 katika ngazi mbali mbali za uuguzi na udaktari yaliyofanyika leo Desemba Mosi, 2018 katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam. (Picha na Bakari Madjeshi, Blogu ya jamii)
 Mkuu wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki Dkt. Salim Mohamed Salim (kulia) akiteta jambo na Makamu mkuu wa hicho hicho Profesa Charles Mgone wakati wa mahafali ya 16 katika ngazi mbalimbali za uuguzi na udaktari yaliyofanyika leo Desemba Mosi, 2018 katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wahitimu waliotunukiwa astashahada, stashahada, shahada za awali na shahada za uzamili kutoka chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki wakati wa mahafali ya 16 katika ngazi mbalimbali za uuguzi na udaktari yaliyofanyika leo Desemba Mosi, 2018 katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MRADI WA MAJITAKA MWANZA WAIBUKA KINARA

0
0
Mradi wa Majitaka unaotekelezwa kwenye maeneo ya miinuko Jijini Mwanza unaofahamika kama "Simplified Sewerage" umekuwa miongoni mwa miradi miwili bora zaidi kuwahi kutekelezwa Barani Afrika chini ya ufadhili wa African Infrastructure Trust Fund (EU-AITF). Hayo yameelezwa mwishoni mwa Mwezi Novemba, 2018 wakati wa Mkutano wa kujadili miradi inayofadhiliwa na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) kupitia mfuko huo wa EU-AITF.

Katika mkutano huo ilielezwa kwamba tangu mfuko huo uanzishwe mnamo mwaka 2007 ni miradi miwili pekee ambayo imefuzu na kuwa miradi bora zaidi kuwahi kutekelezwa ambayo ni Mradi wa Majitaka wa Simplified Sewerage wa Jijini Mwanza, nchini Tanzania na mwingine ni mradi wa Nishati ya Umeme wa Benin & Togo.

Akizungumzia mradi wa Majitaka wa Jijini Mwanza, Mshauri wa masuala ya Kiufundi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Raoul Pedrazzani alielezea hali ilivyokuwa hapo awali kabla ya kujengwa kwa mradi mpya wa majitaka kwenye maeneo ya milimani jijini humo. Pedrazzani alisema kuwa kijiografia maeneo mengi ya Jiji la Mwanza ni milima/miinuko na kabla ya mradi huo wa majitaka wakaazi wa maeneo ya milimani hawakuwa na mfumo mzuri wa uondoaji wa majitaka hali ambayo iliwasababishia adha mbalimbali ikiwemo uchafuzi wa mazingira na maradhi.
 Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akikagua ubunifu uliotumika katika ujenzi wa mradi wa majitaka, Mabatini mtaa wa Unguja wilaya ya Nyamagana. Mradi huo umejengwa kwenye maeneo ya miinuko na umesaidia kuondosha uchavuzi wa mazingira na magonjwa ikiwamo Kipindupindu.
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga (mbele) akiwaongoza wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Maji Mjini Moshi (MUWSA) eneo la Mabatini Jijini Mwanza walipotembelea kujifunza mfumo wa majitaka Oktoba, 2018. Ni mradi wa kipekee kuwahi kutekelezwa nchini.
 Moja ya eneo lililonufaika na mfumo wa majitaka ujulikanao kama ‘Simplified Sewerage’. Pichani ni Mtaa wa Unguja, Kata ya Mabatini Jijini Mwanza ambao ni miongoni mwa maeneo yaliyonufaika na mradi wa majitaka wa simplified sewerage kupitia ufadhili wa African Infrastructure Trust Fund (EU-AITF).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS WA ZANZIBAR AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWACHAGUA HIVI KARIBUNI

0
0


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ndg. Salum Kassim Ali, hafla hiyo imefanyika leo 1-12-2018 Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
IMG_0814
VIONGOZI walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hivi karibuni wa  kwanza Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi  Zanzibar Ndg. Thabit Idarous  Faina, Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi  wa Umma  Zanzibar Bi. Asma Hamid Jidawi na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg. Salum Kassim Ali, wakipitia Hati zao za kiapo kabla ya kuaza kwa hafla hiyo iliofanyika leo 1-12-2018 Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
IMG_0819
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi  Seif Ali Iddi, akisalimiana na Mkurugenzi Mpya wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar kabla ya kuapisha  Ndg. Thabit Idarous Faina, alipowasili katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar kuhudhuria hafla hiyo ya kuapishwa leo Ikulu 1-12-2018.(Picha na Ikulu)
IMG_0829
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisaini hati ya kiapo ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ndg. Salum Kassim Ali, baada ya kumuapisha hafla hiyo imefanyika leo 1-12-2018 Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
IMG_0839_1
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Katibu  Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma  Zanzibar Bi.Asma Hamid Jidawi, hafla hiyo imefanyika leo  1-12-2018 Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)


MICHUZI TV:Ukimwi wazidi kuwa tishio mkoani Morogoro (Siku ya ukimwi Duniani)

MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI ZINACHANGIA MAAMBUKIZI YA VVU

0
0
Jamii imetakiwa kupiga vita mila potofu, mimba na ndoa za utotoni kwani zinachangia uwepo wa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa vijana na watoto mkoani Shinyanga.

Rai hiyo imetolewa leo Jumamosi Desemba 1,2018 na Afisa Mradi wa Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana wa Shirika la Agape AIDS Control Program la Mjini Shinyanga Lucy Maganga wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani ambapo katika wilaya ya Shinyanga yamefanyika katika kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko.Maganga alisema ili kutokomeza Maambukizi ya VVU ni lazima jamii ipewe elimu ya afya uzazi na madhara ya mila potofu, mimba na ndoa za utotoni kwani vinachangia maambukizi ya VVU na Ukimwi hasa kwa vijana na watoto.

Alisema katika kuhakikisha maambukizi ya VVU kwa watoto yanatokomezwa mkoani Shinyanga,shirika la Agape limekuwa likitoa elimu ya afya uzazi kupitia mradi wake wa wa Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana katika wilaya ya Shinyanga.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akikabidhi sare za shule zilizotolewa na shirika la Agape kwa ajili ya watoto yatima/wanaoishi katika mazingira wanaosoma katika shule ya msingi Pandagichiza wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Mgeni rasmi Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani wilaya ya Shinyanga ambayo yamefanyika katika kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Wanafunzi na wananchi wa Pandagichiza wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1,2018.

GEORGE W. BUSH "41" AFARIKI DUNIA

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
ALIYEKUWA Rais wa 41 wa Marekani, George Herbert Walker Bush amefariki dunia akiwa na miaka 94, familia yake imethibitisha. Bush aliyefahamika kama "the 41" ili kumtofautisha na mwanaye George W. Bush Rais wa 43 wa Marekani.

Familia ya Bush imetangaza kifo cha baba yao kupitia msemaji wa familia Jim MCGrath, ujumbe huo ulieleza kuwa, "Jeb, Neil, Marvin, Dor and I are saddened to announce that after 94 remarkable years, our dad has died" George Bush alieleza kwa niaba ya famila na kunukuliwa na jarida la Sunday News nchini humo.

Kifo cha Bush kimetokea baada ya miezi kadhaa tangu ampoteze mkewe Bi. Barbara Bush aliyefariki April, 17 mwaka huu. George Herbet Walker Bush atakumbukwa sana kwa mchango wake kwenye vita baridi ya 1988-1992 na aliangushwa kwenye uchaguzi mkali na Bill Clinton mwaka 1992, Bush alipoteza mvuto katika siasa kutokana na sera za nje zilizompelekea kuhudumumu kwa muhula mmoja pekee.

Kinachowavuta wengi ni kuwa Rais pekee aliyedumu kwenye ndoa na mkewe bi. Barbara kwa miaka 73, waliyotimiza mwaka 2017.

MGANGA MKUU HALMASHAURI YA NZEGA ATUHUMIWA KUKIUKA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

0
0
Na Editha Shija-Tabora

Mganga mkuu (DMO) wa halmashauri ya wilaya ya nzega mkoani Tabora Dk,Edward Sengo anatuhumiwa kutumia Lugha za kuudhi na kutotoa ushirikiano kwa viongozi na watendaji wa kata ,hali inayoelezwa kusababisha kuwa inadhoofisha huduma za Afya wilayani humo

Tuhuma hizo zilitolewa Jana na diwani wa kata ya Nkiniziwa Angelina Simon Kisasembe katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ya halmashauri hiyo

Aidha diwani huyo alisema,Mganga huyo amekuwa akikwamisha jitahada na utoaji wa huduma bora za Afya katika kata hiyo kutokana na kauli zake zisizokuwa na mantiki nzuri katika jamii.

Aliongeza kwa kusema kuwa DMO ni kiongozi wa mfano mzuri katika kitengo cha huduma za Afya katika wilaya hiyo kwani anapaswa kushirikiana vizuri na madiwani na watendaji wa kata zote

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Said Shemahonge alipotakiwa kulitolea ufafanuzi jambo hilo alisema kuwa hana taarifa yoyote ile ya malalamiko yanayoelekezwa kwa mtumishi huyo ila aliahidi kulifanyia kazi na atatoa taarifa kwa kikao kijacho cha baraza.
Baadhi ya Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho cha Balaza la Madiwani.

WASHIRIKI MBIO ZA MOROGORO MARATHONI 2018 KUJINYAKULIA MEDALI MBILI MBILI .

0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii .

WAANDAAJI wa Mashindano ya Mbio za Morogoro Marathon 2018 wametangaza kutoa zawadi ya Medali mbili kwa kila mshiriki wa tukio hilo ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa tukio kubwa la kimichezo katika mkoa wa Morogoro.

Waandaaji hao ambao ni taasisi ya Itetet Sports Agency imetangaza zawadi hiyo jana mbele ya waandishi wa habari wakati wa kuzungumzia maandalizi ya Mbio hizo zitakazofanyika kesho alfajiri katika uwanja wa Jamhuri mjini humo

Afisa Mtendaji Mkuu wa Itete Sports Agency ,Antipas Mgungusi alisema mbali na zawadi hizo kwa washiriki pia zipi zawadi kwa washindi wa mbio za Kilometa 21 kwa upande wa wanaume na wanawake ambapo mshindi wa kwanza atapata pesa taslimu kiasi cha sh 400,000 .

“Tuna mbio za Kilometa 21 pamoja na kilometa tano,lakini uwanjani kutakuwa na mbio za kushirikisha watoto kwa maana ya mita 100 na mita 200 ,kwa kilometa 21 mbali na pesa taslimu mshindi pia atapata king’amuzi cha DSTV kutoka kwa wadhamini kampuni ya Multchoice “alisema Mgungusi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Itete Sports Agency ,Antipas Mgungusi ambao ndio waandaaji wa Mbio za Morogoro Marathon akizungumza na wanahabari kuhusu tukio hilo litakalo fanyika kesho katika uwanja wa Jamhuri ,kushoto kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga,Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Morogoro ,Grace Njau na kulia ni Fuhad Hussein ,Meneja wa DSTV mkoa wa Morogoro ambao ndio wadhamini 
Medali zilizoandaliwa kwa ajili ya washiriki wa mbio hizo ambazo zitatolewa Mbili kwa kila mshiriki .
Meneja wa DSTV mkoa wa Morogoro ,Fuhad Hussein akizungumza juu ya zawadi za Ving'amuzi zitakazo tolewa kwa washindi wa mbio za Km 21 na Km 5.

Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images