Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

KUSIMAMISHWA SOKO LA JUMLA LA FEDHA ZA KIGENI (IFEM) HAKUHUSU HUDUMA ZINGINE-BoT

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imesema soko la jumla la fedha za kigeni kati ya benki za biashara (IFEM) ni muhimu katika soko la fedha za kigeni huku ikifafanua hilo ni soko linaloziwezesha benki za biashara na taasisi za fedha kuuza na kununua (kubadilishana) dola za Kimarekani na Shilingi kati yao. 

Taarifa ya BoT iliyotolewa Novemba 30,2018 na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki imesema kuwa soko hilo husaidia kuamua kiwango 
rasmi cha kubadilisha dola dhidi ya shilingi kwa siku husika. Benki Kuu ya Tanzania pia hushiriki kuuza na kununua fedha za kigeni pale ambapo inalazimu. 

Imesema wakati mwingine huingilia soko ili kuhakikisha hakuna mabadiliko makubwa sana ya kiwango cha kubadilisha fedha.Soko la fedha za kigeni kati ya mabenki (IFEM) lina kanuni na taratibu zake, ambazo zinaeleza kinagaubaga namna washiriki wote wanavyotakiwa kufanya biashara hiyo. 



BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA DK.YOUQING

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BALOZI wa China nchini Dk. Lu Youqing na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Mwambe wamekutana na kufanya kikao cha kazi ambapo wametumia kikao hicho pia kuzungumzia masuala yanayohusu uwekezaji hasa kwa kampuni za kutoka nchini China.

Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za TIC jijini Dar es Salaam ambapo Mwambe ametoa ufafanuzi pia kuhusu sheria ya kutoa vivutio vya uwekezaji hasa vinavyohusu msamaha wa kodi kwa wawekezaji huku akiendelea kutoa ufafanuzi zaidi kuwa kampuni za Kichina ziache kutumia taarifa za madalali na badala yake wafike TIC kupata taarifa mbalimbali za nchi kuhusu uwekezaji.

"Kituo hakipo hapa kukwamisha mwekezaji, tupo kwa ajili ya kusaidia kuanzisha uwekezaji wake nchini kwa kuwa tunatambua umuhimu wa uwekezaji huo kwa nchi,"amesema Mwambe.

Baada ya maelezo hayo Balozi ameridhishwa na amepongeza Serikali kwa kusimamia uwekezaji kwa uwazi na kufuata sheria na China inafurahia jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuboresha mazinga ya biashara na uwekezaji nchini."Mazingira ya biashara na uwekezaji yanaboreshwa na ndiyo sababu kubwa ya makampuni mengi ya China kuendelea kuonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania,"amesema Balozi.
Balozi wa China nchini Tanzania Dk.Lu Youqing (kulia) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Balozi wa China nchini Tanzania Dk.Lu Youqing akifafanua jambo wakati wa kikao chake na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geoffrey Mwambe kilichofanyika kwenye ofisi za Kituo hicho jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geoffrey Mwambe (kushoto) akifafanua jambo kwa Balozi wa China nchini Tanzania Dk.Lu Youqing (kulia) walipokutana jijini Dar es Salaam
Balozi wa China nchini Tanzania Dk.Lu Youqing (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geoffrey Mwambe (wa pili kushoto).

WAHITIMU CHUO CHA USTAWI WA JAMII WASHAURIWA KUTUMIA UJUZI ,UWEZO WALIOUPATA KUSAIDIA JAMII

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya jami
            
TAASISI  ya Ustawi wa Jamii imewatunuku vyeti wahitimu 1,387 katika mahafali ya 42 ya chuo hicho katika ngazi ya astashahada,stashahada, katika fani ya Kazi za jamii kwa Watoto na vijana,Mahusiano kazini na Menejimenti ya sekta ya Umma( Industrial Relations and Public Management).

Akizungumzana leo jijini Dar es Salaam katika mahafali hayo, Katibu Mkuu - Idara Kuu ya Maendeleo ya jamii -Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk.John Jingu amesema wahitimu wote wamekula kiapo kwa ajili ya kulitumikia Taifa na ujuzi waliopatiwa ni rasilimali kwa ajili ya Taifa kwa ujumla.

Dk.Jingu ameeleza fani ya ustawi wa jamii ni nyeti na muhimu katika jamii na wanapaswa kuwa katika sekta mbalimbali kwani wamefundishwa kujiajiri na kuajiri watu kwenye kazi. idha katika nchi zilizoendelea kuna hitajika kuwa na Ofisa Ustawi na chuo kwa sasa kinatakiwa kuweka wigo mpana kwa ajili ya kuendelea kuzalisha wataalam kwa lengo la kusaidia jamii na manufaa ya nchi kwa ujumla.
 Wahitimu wa chuo cha Ustawi wa jamii waliotunukiwa tuzo ya uzamili na Dkt John Jingu wakati wa mahafali hayo leo Jijini Dar es Salaam.


WAZIRI MBARAWA ASIKITISHWA NA UTENDAJI KAZI WA BOHARI KUU YA MAJI ( MAJI CENTRAL STORES)

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii. 

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amesema lengo la serikali ni kuona bohari kuu ya maji inasaidia katika kupunguza gharama za madawa.

Ameyasema hayo baada ya kutembelea bohari kuu ya maji (Maji Central Stores) na kusisitiza uongozi uliopo hauridhishi kutokana na namna wanavyoendesha taasisi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Prof Mbarawa amesema nia ya serikali ni kuona mamlaka zinafaidika na bohari kuu na muda mwingine wanatakiwa kusambaza vifaa vyake kwa mamlaka za maji kote nchini.

Mbarawa amesema, kuna mita zaidi ya 10,000 zimefungiwa tu ndani hawazisambazi kwa mamlaka za maji, kuna miradi mingi imesimama kutokana na kukosa vifaa ila bohari kuu imeviweka na havifanyi kazi yoyote.

Amewaagiza bohari kuu ndani ya wiki mbili wawe wamesambaza mita hizo kwa mamlaka za maji nchini ikiwemo Mkoa wa Lindi ambao wana uhitaji wa mita za maji karibia 3,000 na mikoa mingine pia.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akieleza jambo kwa Boharia Mkuu Crepin Bilamu baada ya kutembelea ghala la vifaa na madawa leo Jijini Dar es Saalla
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akikagua baadhi ya vifaa vilivyopo ndani ya ghala ndani ya bohari kuu ya maji Jijini Dar es Salaam.
Vifaa mbalimbali vilivyopo ndani ya Bohari kuu ya maji ambapo vina  muda mrefu bila kutumika.

TAWLA YAANDAA MJADALA KUJADILI HAKI ZA MTOTO...

BURUNDI YAKWAMISHA MKUTANO 20 WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0

Na. Vero Ignatus, Arusha

Mkutano wa 20 wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika ya mashariki uliokuwa ufanyike leo Mkoani Arusha umeaihirishwa. 

Akitaja sababu za kuahirishwa kwa mkutano huo Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika ya mashariki kutoka Uganda Kirunda Kivejinja amesema nchi ya Burundi imekwamisha mkutano huo kwa kitokutuma muwakilishi 

Waziri wa mambo ya nje ya nchi ya Tanzania Mhe. Augustino Mahiga amesema marais wawili wa Sudan ya Kusini na Rwanda wametuma wawakilishi lakini Rais wa Burudi hakutuma muwakilishi yeyote kwenye vikao vyote

'' Kwenye mikutano kama hii kuna kuwa na maandalizi ya ngazi tatu kwanza ni maafisa wataalam,makatibu wakuu na mwisho ya mawaziri na hatimaye inakuwa mkutano wawakuu lakini Burundi haikuleta wawakilishi kabisa na hawakutoa maelezo hivyo hatujui ninini kiewapata''alisema Mahiga

Hivyo kutokana na sheria za mkataba wa Afrika ya Mashariki kikao cha mawaziri kilishindwa kuchukua maamuzi, kwani hata kikao cha maamuzi lazima kiwe na wawakilishi kutoka nchi zote sita ."Hivyo kikao cha mawaziri hakikutoa maamuzi yeyote, tulijadiliana tu hayo ni kutokana na kilichopo katika mkataba wetu.

INTRODUCIND:MWASITI FEATURING ROMA-FALL IN LOVE (OFFICIAL VIDEO).

JAMII YAASWA KUACHA FIKIRA POTOFU JUU YA UGONJWA WA KIFAFA

$
0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Imani potofu ndiyo inayopelekea kuongezeka wa Ugonjwa wa Kifafa katika maeneo mbali mbali ya nchi ya Tanzania hasa Wilaya ya Mahenge, Morogoro.
 

Hayo ameyasema Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja wakati akiwasilisha ufatifi wake  katika muhadhara uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ili kuweza kutoa mapendekezo yake njia za kuweza kusaidia jamii.

Profesa Matuja amesema Jamii inahitaji kuondokana na imani potofu maana watu wengi wamekuwa wakijua kuwa ugonjwa unasambabishwa na ushirikina.Ameongeza kuwa jamii ni bora kujitokeza kupima mara kwa mara ili kuweza kupatiwa tiba mahususi ili kuweza kuondokana na tatizo hilo.

"Nimefanya utafiti katika wilaya ya Mahenge, Morogoro ila tulichogundua mwanzo ni jamii haikuwa na ueleza zaidi kuhusiana na ugonjwa wa kifafa na hivyo kupelekea watu wengi sana kuugua ugonjwa huo, lakini wengi wao wanafikiria imani potofu hasa haya mambo ya ushirikina," ameongeza Prof Matuja.

Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja akiwasilisha utafiti wake juu ya Ugojwa wa Kifafa katika muhadhara wa Kiprofesa uliofanyika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Profesa Matuja alifanya utafiti wa Ugonjwa wa Kifafa kwa muda wa miaka minne katika Wilaya ya Mahenge, Morogoro. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Mwenyekiti wa Muhadhara huo, Prof. Gadi Kilonzo akifungua majadiliano ya kuulizana maswali juu somo la ugonjwa wa kifafa alilolitoa Profesa William Matuja (kushoto). 
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Ndani wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja akiwasilisha utafiti wake juu ya Ugojwa wa Kifafa katika muhadhara uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Profesa Matuja alifanya utafiti wa Ugonjwa wa Kifafa kwa miaka minne katika Wilaya ya Mahenge, Morogoro. 
Wageni waalikwa wakifuatilia muhadhara huo.



TAWLA YAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI MASUALA MBALIMBALI YA KISHERIA ZINAYOMHUSU WATOTO

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA cha Wanasheria Wanawake(TAWLA) kimewakutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kujadili , kuchambua na kuweka mikakati ya namna ya kuwasaidia watoto  ambao wapo kwenye ukinzani wa kisheria hasa kipindi hiki ambacho mmomonyo wa maadili kwenye jamii umekuwa mkubwa na kusababisha watoto wengi kujikuta wakiingia kwenye ukinzani huo wa kisheria.

Baadhi ya wadau ambao wamekutanishwa na TAWLA ni polisi, maofisa ustawi wa jami, wanasheria wenyewe, mahakimu, masheikh na wachungaji pamoja na wadau wengine wanaojihusisha na masuala ya watoto nchini  Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA)Tike Mwambipile amesema wameamua kukaa pamoja na kisha kutazama nini wafanye katika kuwasaidia watoto walioko kwenye ushindani wa kisheria na kwamba wakati wa najadiliana kwenye hilo watatumia nafasi hiyo kuulizana maswali ya msingi ya kisheria likiwamo la wapi wamekosea.

Amefafanua sheria inasema kesi ya mtoto isikilizwe ndani ya siku mmoja na hiyo ni changamoto kwani ni ngumu kutumia siku moja kusikiliza kesi ambapo utahitaji pia mashahidi na mambo mengine ya kisheria na hivyo wadau hao wataangalia nini kifanyike angalau kutoa nafasi ya kutosha ya kusikiliza kesi za watoto kwenye makosa ya haki jinai.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Tike Mwambipile akizungumza na Michuzi TV pamoja na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam wakati wa semina maalum iliyoandaliwa na chama hicho kujadili haki za Watoto wenye matatizo ambao wanahitaji msaada wa kisheria.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Tike Mwambipile akisoma moja ya Kitabu kinachohusu masuala ya kisheria wakati wa semina ya kujadili namna ya kumsaidia mtoto ambaye ameingia kwenye ukinzani wa kisheria.Semina hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Wakili Barnabas Kaniki akizungumzia mjadala ulioandaliwa na Chama hicho, uliokuwa unajadili haki za watoto wenye matatizo ambao wanahitaji masaada wakisheria.
Baadhi ya washiriki wa mjadala huo wakiwa kwenye semina maalum iliyoandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake(TAWLA) walipokutaa leo jijini Dar es Salaam.

PROF MBARAWA ATEMBELEA OFISI YA DAWASA BUNJU

$
0
0
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa ameambatana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea ofisi za DAWASA Bunju Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akipewa taarifa na mfanyakazi wa DAWASA kitengo cha kuunganisha wateja wapya, Chini akieleza jambo kwa muhudumu huyo kuhusiana na utaratibi wa kuunganisha wateja wapya.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji akizungumza na kuwasikiliza wananchi waliokwenda kupata huduma kwenye ofisi za DAWASA Bunju Jijini Dar es Salaam.

MBOWE, MATIKO WARUDISHWA TENA MAHABUSU SEGEREA

$
0
0
*Ni baada ya Mahakama Kuu kusimamisha usikilizwaji wa rufaa yao

Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam  leo Novemba 30, 2018  imesimamisha usikilizwaji wa rufaa ya  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko kwa muda usiojulikana kupisha rufaa iliyofunguliwa na upande wa Serikali dhidi ya uamuzi wa Jaji Sam Rumanyika iliyoyatoa leo asubuhi itakaposikilizwa  na kutolewa maamuzi.

 Jaji Sam Rumanyika ametoa uamuzi huo baada ya upande wa mashtaka katika kesi hiyo kukata rufaa Mahakama ya Rufani ikipinga uamuzi uliotolewa na Mahakama  Kuu  mapema leo asubuhi wa kukubali kuendelea na usikilizwaji wa rufaa ya  Mbowe na Matiko baada ya kutupilia mbali mapingamizi yao ya awali.

Katika uamuzi wake Jaji Rumanyika amekubaliana na hoja za Serikali kuwa uamuzi mdogo ambao hauwezi kumaliza shauri hauwezi kukatiwa rufaa na wadaa wengine isipokuwa DPP tu na kuongeza kuwa, ni DPP pekee ndiye anapewa mamlaka ya kukata rufaa kwa uamuzi mdogo 
chini ya kifungu cha 6 cha Sheria ya Mamlaka ya Rufaa.

Aidha Jaji Rumanyika amesema kuhusu taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufani, amesema hilo liko wazi kwamba kunapokuwepo na taarifa hiyo mahakama ya chini haiwezi kuendelea na shauri."Hivyo mwenendo wa shauri hili unasimama hadi rufaa iliyokatwa Mahakama ya Rufani itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi", amesema Jaji Rumanyika.

Washtakiwa Mbowe na Matiko ambaye  wamekata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana katika kesi uchochezi inayowakabili wao na wenzao sab Novemba 23,2018 na Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina kuongoza vikao vya ‘Operesheni Sangara III, 2018’ Jumamosi

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina ataongoza vikao vya kufanya tathmini ya kitaifa ya‘Operesheni Sangara III, 2018’  tarehe 01.12.2018 Mkoani Kigoma, ambayo inaendeshwa katika Maziwa ya Victoria, Tanganyika na Bwawa la Nyumba ya Mungu.
Aidha, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ataongoza katika Kanda ya Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza na Katibu Mkuu Uvuvi Dkt. Rashid Tamatama ataongoza katika Kanda ya Nyumba ya Mungu, Mkoani Kilimanjaro.
 Imetolewa na Edward Kondela
                       Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Dkt. kigwangalla na Dkt. Ndumbaro wafanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) akitoa neno la ufunguzi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Maiasili na Utalii, Mhe. Dkt. Khamis Kigwangalla kuongea na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo. Viongozi hao walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kuelezea mikakati inayochukuliw na Serikali ya awamu ya tano ya kuvutia utalii nchini. Mikakati hiyo imeanza kuzaa matunda ambapo wnanchi wa Urusi wameichagua Tanzania kuwa eneo bora zaidi kwa utalii duniani na kutoa Tuzo maalum kwa serikali. Aidha, Mikakati iliyofanywa nchini China hivi karibuni imewezesha kuingiwa kwa Mkataba wa kuleta watalii elf 10 kutoka Shangai mwaka 2019. Kushoto ni Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Yuri popov.
Dkt. Kigwangalla akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo pichani ambapo alitumia fursa hiyo kuwaeleza namna Watalii wanavyoongezeka kuja nchini kwa wingi.  Alisema sekta ya utalii ndiyo inayoongoza kuingizia Taifa hili fedha za kigeni ambapo kitakwimu sekta hiyo inachangia asilimia 25 ya fedha zote za kigeni. Aidha. alitoa pongezi zake za dhati kwa balozi zetu zilizopo nje ya nchi kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuwa zimekuwa zikifanya jitihada kubwa katika kutangaza Vivutio vilivyopo nchini Tanzania  ambapo kutokana na juhudi hizo Tanzania inapokea watalii wapatao Milioni 1.3 na malengo waongezeke zaidi kila mwaka. 
Balozi wa Urusi naye akizungumza na Waandishi wa Habari
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya naAmerika Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Jestas Nyamanga (kushoto) pamoja na Naibu Balozi wa Urusi wakiwasikiliza kwa makini Mawaziri pamoja na Balozi wa Urusi wakizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea




Muhimbili yasisitiza wataalam kufanya tafiti za afya

$
0
0
Wataalam wa afya wameshauriwa kuendelea kufanya tafiti mbalimbali zitakazosaidia kuleta mabadiliko katika utoaji wa huduma za afya nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru wakati akifunga kongamano la pili la kisayansi la Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Prof. Museru ameeleza kuwa kuna umuhimu wa kuendelea kufanya tatifi kwani zitawezesha hospitali kutibu wagonjwa kutokana na rasimali zilizopo na kwamba tafiti pekee ndio itafanikisha wataalam kuendelea kutoa huduma bora zaidi.
Amefafanua kuwa tafiti zinasaidia kutatua matatizo yaliyopo sehemu za kazi hivyo ameahidi kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili itaendelea kuwawezesha watalaam wake katika kufanya tafiti ambazo zitaleta tija katika utoaji wa huduma.
Pia, Profesa Museru ametumia fursa hiyo kuwatunuku vyeti pamoja na fedha Madaktari Bingwa wawili wa Muhimbili ambao wamefanya tafiti ambazo zitaleta mabadiliko katika kuhudumia wagonjwa.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya dharura, Dkt. Juma Mfinanga amefanya utafiti wa kuangalia ubora wa magari ya kubebea wagonjwa pamoja na changamoto zake.
Utafiti huo utasaidia kubaini tatizo lililopo katika kusafirisha wagonjwa kuanzia eneo la tukio mpaka hospitalini pamoja na huduma za dharura zinazotolewa kabla ya mgonjwa kufika hospitalini.
Vilevile utafiti huo utawezesha kutoa muongozo jinsi ya kuhudumia wagonjwa wa dharura kuanzia eneo la tukio mpaka hospitalini na kupunguza vifo vinavyotokea nje ya hospitali.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani, ubongo na mishipa ya fahamu, Dkt. Kigocha Okeng’o, yeye amefanya utafiti ulioangalia viashiria vya kupona haraka kwa mtu aliyepata ugonjwa wa kiharusi.
Katika kongamano hilo la siku mbili, mada mbalimbali zimewasilishwa ikiwemo tiba kwa mama ambaye anatoka damu nyingi baada ya mimba kuharibika, mama kushindwa kuzuia haja ndogo baada ya kufanyiwa upasuaji, matumizi ya rekodi za wagonjwa kwa ajili ya tafiti, upanuzi wa huduma za magonjwa ya dharura nchini, afya ya akili na magonjwa ya kisukari.
Zaidi ya wataalam wa afya 200 wameshiriki katika kongamano hilo ambalo limebaba kauli mbiu inayosema “utoaji wa huduma bora za afya Tanzania hususani huduma ya afya ya mama na uzazi.’’
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza katika kongamano la pili la kisayansi kuhusu wataalam wa afya kutoa huduma bora kwa mama na mtoto. Prof. Museru amefunga kongamano hilo leo ambalo lilianza jana.
 Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Prof. Museru kwenye kongamano hilo.
 Prof. Museru akimtunuku cheti Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga baada ya kufanya utafiti kuhusu ubora wa magari ya kubeba wagonjwa lengo likiwa ni kuboresha huduma hiyo nchini. Katikati ni Kaimu Mkurungenzi wa Huduma za Uuguzi, Bi. Zuhura Mawona. 
 Kutoka kushoto ni Dkt. Juma Mfinanga ambaye ameandika utafiti kuhusu ubora wa magari ya kubeba wagonjwa, Mkuu wa Kitengo cha Utafiti Muhimbili, Dkt. Faraja Chiwanga na kulia ni Dkt. Kigocha Okeng’o wa Muhimbili ambaye amefanya utafiti ulioangalia viashiria vya kupona haraka kwa mtu aliyepata ugonjwa kiharusi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru akiwa katika picha ya pamoja na watoa mada na waandaji wa kongamano hilo.

BABA AUA WATOTO WAKE WATATU AKIWEMO WA MIEZI 10 KWA UGOMVI BAINA YAKE NA MKEWE

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
JESHI la polisi mkoani hapa limethibitisha kutokea kwa vifo vya watoto watatu akiwemo wa miezi kumi ,waliouawa kwa kunyweshwa sumu na baba yao mzazi. Chanzo cha kutenda kitendo hicho cha kikatili kinadaiwa ni kutokana na ugomvi mkubwa kati ya wazazi wa watoto hao. 
Kamanda wa polisi mkoani humo ACP
Wankyo Nyigesa (pichani, mbele)  alieleza tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana huko maeneo ya Kibindu ,Chalinze . Aliwataja watoto hao kuwa ni pamoja na Shaila Salehe miaka sita ,Nurdin Salehe (4)na Sabrat Salehe mwenye miezi kumi waliouawa kwa kunyweshwa sumu ambayo ni dawa ya kuulia magugu iitwayo Twiga Amine na baba yao mzazi Salehe Masokola (22),mkazi wa kijiji cha Kunwe, Mvomero mkoa wa Morogoro . 
Kamanda  Wankyo alibainisha,baba wa watoto hao alikuwa na mgogoro na mkewe ambae ndiye mama wa watoto .
"Mtuhumiwa alipowafuata watoto kutoka kwa mama mkwe wake kwa madai kwamba anakwenda kucheza nao na angewarudisha baadae " alifafanua Wankyo. Alielezea,mtuhumiwa aliwapakia marehemu kwenye baiskeli kutoka Kunke hadi kitongoji cha Ditele, Kibindu, ambapo aliwanywesha dawa hiyo kwa kuwachanganyia na juisi hivyo kupelekea vifo vya watoto hao. Kamanda huyo alisema katika eneo la tukio kumeokotwa chupa mbili za juisi zilizotumika ,chupa ya dawa na matapishi ambavyo vilichukuliwa kwa uchunguzi zaidi. 
 "Mara baada ya tukio mtuhumiwa alikunywa sumu kwa lengo la kutaka kujiua lakini aliokolewa na watu kisha kukimbizwa katika hospital ya mission Bwagala wilaya ya Mvomero kwa matibabu" Wankyo aliweka bayana. Mpaka sasa hali yake sio nzuri kwani yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi akiwa chini ya uangalizi wa polisi . 

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 30.11.2018

MICHUZI TV: POLISI YAUA MAJAMBAZI SUGU JIJINI DAR ES SALAAM

Habari za UN Novemba 30, 2018

MICHUZI TV: MAFUNZO YA UONGOZI NA MAADILI YATAJWA KUPATA VIONGOZI WENYE MAADILI NA WAZALENDO

MKUU WA MKOA WA MBEYA AKABIDHI MAGARI MAWILI NA PIKIPIKI NNE KWA JESHI LA POLISI MBEYA.

$
0
0
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amefanya ziara ya kikazi tarehe 30.11.2018 kwa kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwake.
Katika ziara hiyo, Mhe.Chalamila alikabidhi magari mawili aina ya Probox kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya ili yatumike katika kuimarisha doria katika barabara kuu ili kupunguza ajali na kupambana na uhalifu.
Aidha Mhe.Chalamila alikabidhi pikipiki nne aina ya FEKON zilizotolewa na mdau wa Jeshi la Polisi kwa askari Polisi walioonyesha uaminifu katika kazi kwa kukamata fedha zaidi ya Tshs.Milioni 17 zilizokuwa zimeibwa dukani kwa mfanyabiashara mmoja huko Wilayani Chunya.
Sambamba hilo, Mhe.Mkuu wa Mkoa amekagua kambi ya Polisi Mbeya na kuahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha unafanyika ujenzi wa nyumba za kisasa za kuishi askari ili kuongeza morali ya kiutendaji kwa askari wa Jeshi la Polisi.
Mhe.Mkuu wa Mkoa alikamilisha ziara yake ya kikazi kwa kuzungumza na askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na kusisitiza uadilifu, nidhamu na uaminifu. Aidha amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kudhibiti ajali za barabarani hasa madereva wa Pikipiki @ bodaboda ambao hawataki kutii sheria za usalama barabarani.
Pia Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alitumia ziara hii kutoa tamko kwa wakazi wa Mbeya kuwa siku ya tarehe 09.12.2018 [uhuru wa Tanganyika] watumishi wote wa umma watashiriki kazi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa majengo ya umma, kufyetua tofali, kuchota maji kwa ajili ya ujenzi na kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yote ya Mkoa wa Mbeya.

 Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akiwasili kuanza  ziara ya kikazi
  Pikipiki nne aina ya FEKON zilizotolewa na mdau wa Jeshi la Polisi kwa askari Polisi walioonyesha uaminifu katika kazi kwa kukamata fedha zaidi ya Tshs.Milioni 17 zilizokuwa zimeibwa dukani kwa mfanyabiashara mmoja huko Wilayani Chunya.
  Magari mawili aina ya Probox kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya ili yatumike katika kuimarisha doria katika barabara kuu ili kupunguza ajali na kupambana na uhalifu.
 Mhe.Chalamila akikabidhi magari mawili aina ya Probox kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
Mhe.Mkuu wa Mkoa akikagua kambi ya Polisi Mbeya na kuahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha unafanyika ujenzi wa nyumba za kisasa za kuishi askari
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images