Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

MAJALIWA AWASILIMIA WANANCHI WA MJI MDOGO WA KATORO MKOANI GEITA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Mji Mdogo wa Katoro mkoani Geita, Novemba 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TANZIA .

$
0
0
UONGOZI wa Bodi na Menejimenti ya Baraza la Kilimo Tanzania unasikitika kutangaza kifo cha Mwakilishi wake katika Wilaya ya Wangi’ng’ombe Mkoani Njombe Bw. John Wihallah aliyefariki Dunia katika ajali iliyohusisha Basi alilokuwa amepanda la Rungwe Express lilokuwa likitokea Dar es saalm kuelekea Mkoani Mbeya kwa kugongana na Gari aina ya Coaster katika eneo la Iyovi Mkoani Morogoro.

Bw. John alikuwa akitokea Jijini Dar es Salaam alikokuwa akishiriki Warsha ya Kitaifa ya Wadau wa Kilimo iliyofanyika Nov 26/27 na baadae kushiriki Mkutano Mkuu wa Baraza la Kilimo uliofanyika Nov 28. 

Taarifa za kifo chake zimepokelewa kwa maskkitiko makubwa hasa ikizingatiwa Bw John alikuwa kiunganishi muhimu kati ya wakulima na Baraza la Kilimo Wilayani Wang’ing’ombe Mkoani Njombe,

Uongozi wa Baraza la Kilimo Tanzania utamkumbuka kwa mchango wake mkubwa katika Sekta ya Kilimo lakini pia Baraza limeahidi kufanyia kazi mapendekezo na ushauri wote alioutoa wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kilimo Tanzania ambapo lipata fursa ya kuchangia masuala mbalimbali.

Mwili wa Marehemu John Wihallah unatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Wilaya ya Wang;ing;ombe Mkaoni Njombe Jumapili Dec 02 Mwaka huu.

Bwana alitoa Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.

Imetolewa na Baraza la Kilimo Tanzania,
Dar es salaam.
Nov 30, 201 

Ndugu John Wihallah (enzi za uhai wake) akishiriki mkutano mkuu wa Baraza la Kilimo Tanzania Nov 28, Jijini Dar es Salaam, kabla ya kufikwa na mauti Nov 29 alipokuwa akirejea Mkoani Njombe.

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA SMZ BALOZI SEIF AL I IDD APONGEZA MAFANIKIO YA TASAF.

$
0
0
Na. Estom Sanga- Zanzibar. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd amesema utekelezaji wa shughuli za Maendeleo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kisiwani Zanzibar umekuwa wa mafanikio makubwa na wenye tija katika jitihada za serikali za kupunguza umaskini kwa wananchi.

Balozi Seif Ali Idd ameyasema hayo alipokutana na Wadau wa Maendeleo na Maafisa wa TASAF Ofisini kwake mjini Unguja wakiwa katika ziara ya kutembelea Walengwa wa Mfuko huo ikiwa ni utaratibu wa kukutana na Walengwa kuona namna wanavyonufaika na huduma za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Makamu huyo wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,amesema maeneo yote ambako TASAF kupitia Mpango wake wa Kunusuru Kaya Maskini unatekelezwa, Walengwa wameboresha maisha yao kwa kiwango kikubwa kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi na kujiongezea kipato chao.

Amesema ongezeko la kipato limezifanya Kaya za Walengwa kumudu gharama za kuhudumia Watoto na wengine kuboresha makazi yao ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya kujumuishwa kwenye Mpango huo ulioanzishwa na serikali kwa lengo la kuboresha maisha ya Walengwa nchini kote.

Balozi Seif Ali Idd amesema kutokana na mafanikio yaliyoanza kuonekana kutokana na huduma za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Serikali itaendelea kusimamia kwa karibu mpango huo ili wananchi hususani wanaokabiliwa na kero ya umaskini waweze kuondokana na kero hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga, amesema mafanikio ya utekelezaji wa Mpango huo wa kunusuru Kaya Maskini yamechangiwa kwa kiwango kikubwa na usimamizi wa karibu wa viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali za uongozi kote nchini kote. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar.Balozi Seif Ali Idd (anayetazama kamera) akizungumza na Wadau wa Maendeleo na Maafisa wa TASAF ofisini kwake-mjini Unguja. 
Balozi Seif Ali Idd (aliyevaa Kaunda Suti nyeupe) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga baada ya kikao na wadau wa maendeleo ofisini kwake.

Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ (walioketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Maendeleo na Maafisa wa TASAF ofisini kwake kisiwani Unguja. 


Madaktari Ocean Road timizeni wajibu wenu Dkt.Mpoki

$
0
0
Na.WAMJW, Dar es Salaam 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya amewataka Madaktari wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kutimiza wajibu wao katika kuwahudumia wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kila siku na kumuagiza Mkurugenzi wa Huduma za Uhakiki na Ubora kutoka Wizarani kwake kufuatilia. 

Dkt.Mpoki ametoa agizo hilo alipotembelea taasisi hiyo ili kujionea hali ya utoaji huduma pamoja na kusikiliza wagonjwa wanaofika kupata huduma kwenye taasisi hiyo kutokana na kulalamikiwa kwa baadhi madaktari na wauguzi “Taasisi hii ni ya faraja lazima mtengeneza mazingira mazuri yakuwahudumia wagonjwa,kwani ndugu wanafuatilia hali za wagonjwa wao hivyo jamii inapolalamika tusiseme moja kwa moja ni waongo bali tushughulikie malalamiko yao ,kama huna jibu muelekeze kwa mtu ambaye anaweza kumpa jibu ili aweze kupata faraja”.Alisisitiza Dkt.Mpoki. 

Aidha, aliwataka watumishi wa taasisi hiyo kuvaa vitambulisho ambavyo vinaweka wazi utambulisho wao ili ndugu na wagonjwa waweze kuwatambua na kutaja ni nani ambaye hajatimiza wajibu wake ipasavyo.
“watakaoshindwa kwenda nasi tutawapeleka kwingine,hatutaki maumivu yawe sehemu ya uzoefu wa wagonjwa wanaolazwa Ocean Road,nyinyi kazi yenu ni kuwahudumia wagonjwa”. 

Hata hivyo aliwataka madaktari wabobezi (Mabingwa) kutimiza wajibu wao na sio kuwaachia jukumu la kuwahudumia wagonjwa madaktari waliopo mafunzo kwa vitendo”kuanzia sasa tukigundua mgonjwa ameachiwa daktari wa mafunzo kwa vitendo tutawaondoa wasifanye mazoezi hapa lazima tuishi kwa kutii na kufuata miiko ya taaluma zetu”alisema dkt.Mpoki 

Aliagiza kufanyika mikutano ya ndani mara kwa mara ya kufuatilia utendaji kazi wa taasisi na kujibu malalamiko yanayotolewa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na masanduku ya maoni ili kupata mrejesho kutoka kwa wananchi ili kuboresha huduma zinazotolewa kwenye taasisi. 


Kuhusu adha ya umbali wa kufuata huduma kwenye taasisi hiyo Dkt. Mpoki aliwathibitishia wagonjwa na ndugu waliopo hospitalini hapo kuwa Serikali kupitia wizara ya afya iko mbioni kupeleka huduma za saratani kanda ya kusini mara tu itakapokamilika hospitali ya Rufaa ya kanda,pia huduma kama hizo zipo mbioni kupelekwa kwenye hospitali ya rufaa ya Tabora pamoja na hospitali maalum ya Benjamin Mkapa iliyopo jijini Dodoma kwani ni wajibu wao kuhakikisha huduma hizo karibu na wananchi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na wagonjwa kwenye dirisha la dawa lililopo hospitalini hapo ambapo wagonjwa walisema wanapata dawa hizo bila malipo

Dkt.Mpoki akimjulia hali mmoja wa wagonjwa kwenye wodi ya wanaume hospitalini hapo na kuahidi wizara yake ipo mbioni kusogeza huduma za saratani kwenye baadhi za hospitali za rufaa za kanda na mkoa ili kuondoa adha ya kusafiri kwenda ocean road. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akisisitiza wananchi (hawapo pichani) kuandika maoni na kuweka kwenye Kisanduku kuhusiana na huduma zinatolewa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ili uongozi uweze kusoma na kuyafanyia kazi maoni hayo. 
Katibu Mkuu akisikiliza wagonjwa waliofika kupata huduma kwenye hospitali hiyo.Dkt. Mpoki aliutaka Uongozi wa hospitali hiyo kufanyia kazi malalamiko ya ndugu wa wagonjwa kama mrejesho wa utoaji huduma 

Introducing "Mwanadamu" by Pastor Ronald Laulau

$
0
0
Recorded at Nanobeatz Tanzania From Mwanadamu Album It is a Song About Man's Relationship with God

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI MAPINGAMIZI YA SERIKALI KWENYE KESI YA MBOWE ,SASA KUSIKILIZA RUFAA YAO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa Serikali na kukubali kusikiliza rufaa ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini,  Esther Matiko ya kupinga kufutiwa dhamana na Mahakama ya Kisutu.

 Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama kutupilia mbali hoja za pingamizi la Serikali ambazo ziliiomba Mahakama iitupilie mbali rufaa hiyo bila hata kusikilizwa sababu zina mapungufu kisheria.

Mbowe na Matiko wamekata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 23, 2018  kuwafutia dhamana katika kesi ya jinai inayowakabili mahakamani hapo inayosilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri, Kutokana na  maombi ya upande wa mashtaka, kwa madai ya kuwa wamekiuka masharti ya dhamana kwa kutokufika mahakamani tarehe ambazo kesi yao ilipangwa kwa ajili ya usikiljzwaji wa awali (PH).

Rufaa hiyo ilitarajiwa kusikilizwa jana lakini upande wa Serikali uliwasilisha pingamizi la awali ikitoa sababu tatu za kutaka rufaa hiyo itupwe ikiwemo kuwa rufaa hiyo iko mahamakani isivyo  halali kwani inakiuka vifungu vya sheria.

Akitoa uamuzi leo Novemba 30,2018 Jaji Sam Rumanyika
amekataa sababu ya pingamizi la Serikali kuwa rufaa hiyo iko mahakamani isivyo halali.

Jaji Rumanyika amesema kuwa rufaa hiyo iko mahakamani kihali kwani si lazima  kutaja kifungu cha kisheria kinachoipa mahakama mamlaka ya kusikiliza rufaa hiyo.

Hata hivyo amekubaliana na hoja za Serikali za kupewa mwenendo wa kesi ya msingi wa shauri hilo uliochapishwa  ambao unasomeka vizuri. Pia Jaji Rumanyika amekubaliana na hoja  kuwa sababu mbili za rufaa za kupinga masharti ya dhamana zinakiuka matakwa ya sheria kwa kuwa zimekatiwa rufaa bila kutoa kwanza taarifa ya kusudio la kukata rufaa kupinga masharti hayo ya dhamana yaliyotolewa kati ya mwezi Machi na April.


Hata hivyo imeelezwa kuwa rufaa hiyo itasikilizwa saa nane mchana.  

UNICEF Tanzania encourages role of youth in development

$
0
0
United Nation Children's Fund (UNICEF) Representative Ms. Maniza Zaman 
UNICEF Tanzania has encouraged Tanzania to double her efforts in encouraging her young citizens of today to play an even more significant role as the country works towards realization of its Vision 2025, the global Sustainable Development Goals and Agenda 2063.
Addressing tens of youth during this year’s World Children's Day celebrations on Tuesday in Dar Es Salaam, United Nation Children's Fund (UNICEF) Representative Ms. Maniza Zaman said youth of Tanzania should be encouraged and engaged in realizing of the country’s development objectives.
Ms. Maniza who was addressing over 100 young men and women from different schools and higher learning institutions from all over the country at an event organized at the Bank of Tanzania Conference Facilities said that Tanzania’s children under the age of 18 have their hopes and dreams in life, just like adults and, that these aspirations should not only be encouraged to blossom but also to benefit the country’s development agenda.
The Oxford University educated Ms. Maniza said that if every boy and girl is given a fair chance and the opportunity to be heard in life as well as supported accordingly, then chances are that they will be successful and make significant contribution to the country’s struggle for development.
“Let us encourage them to make the right choices and pursue the paths to make those choices a reality in their lives. This will surely help them achieve their goals in life as well as significantly contributing to the country’s major development goals,” said Ms Maniza.
        During the event five young Tanzanians shared their aspirations, dreams, and narrated their stories on how they chose their path in life, bringing them to some encouraging achievements.
The five included Brigitte Lyimo, Miss Tanzania 2012 and now an activists for the rights of young people with albinism in Tanzania,  an activist for youth rights from Arusha Raphael Dennis and an IT and engineering student at the University of Dar Es Salaam Witness Mtui.
Other were a popular radio presenter and online influencer Millard Ayo as well as Vanessa Innocent, a form two student at Chang’ombe Secondary School in Dar Es Salaam, who received a standing ovation for her articulate presentation on her hopes and aspirations in life, where she told participants that she wants to be a motivational speaker in life.
The aim of these talks was to draw attention to the issues and challenges being faced by children and young people in Tanzania, as well as encouraging them to believe in themselves, knowing that hopes and dreams cultivated at young age in life and driven by self confidence can turn them into successful citizens of their country.
The United Nations Children Fund (UNICEF) was first set up on December 11th in 1946 in New York, and for more than 70 years the Fund has worked to promote children’s survival, protection and development in key life support areas such as health and nutrition, clean and safe water provision and sanitation, basic quality education and protection from violence, exploitation and recently, from HIV/AIDS.
The work of UNICEF which has now operations in more than 170 globally with more than 13,000 staff, 85 percent of which is in filed activities was significantly enhanced by the adoption of the Declaration of the Rights of the Child in 1959 which was followed, twenty nine years ago, in 1989, by the global adoption of the Convention of the Rights of the Child (UNCRC), which then became the most rapidly and widely ratified international human rights treaty in the history of mankind.
The Convention changed the way children are viewed and treated.
They came to be seen as human beings with a distinct set of rights – and not just passive objects in need of care and charity.
Twenty-seven years ago, Tanzania ratified the UNCRC, and. today, the country has much to celebrate – from less children under-five dying, less babies getting HIV, a steady decline in malnutrition over the years, more children accessing schooling to name a few.
        Maniza says that Tanzania’s commitment and efforts in support of children’s rights have to be recognized and appreciated.
"Tanzania’s growing child population (set to double by 2030), socio-economic and cultural diversity, and its regional, gender and social disparities, still pose challenges to the realization of all that is in the Convention on the Rights of the Child" she said.
She added that there are children still dying too
soon, who are not growing up healthy and well
nourished, who don’t manage to go to school and learn, who live in fear and experience all forms of violence, which do not have clean water and proper toilets to use.
Maniza added that there are children whose voices are not heard – never heard, insisting that these children must be the focus of everybody's collective attention – “leave no one behind” as world leaders said when they signed the Sustainable Development Goals.
She insisted that UNICEF has a special role in supporting the Convention.
"Article 45 assigns UNICEF a legal obligation to promote and protect child rights by supporting the work of the Committee on the Rights of the Child. Guided by the provision and principles of the CRC, child rights are at the heart of UNICEF’s work" she said.

RAIS DKT MAGUFULI NA UHURU KENYATA KUZINDUA KITUO CHA FORODHA CHA PAMOJA KESHO

$
0
0
Na Vero Ignatus, Arusha
RAIS  Dkt John Magufuli na Rais Uhuru Kenyata  kesho wanatarajia kuzinduwa kituo cha Forodha cha pamoja Namanga One Stop Bonder Point.
Aidha Disemba 2,  mwaka huu Rais John Magufuli ataweka jiwe la Msingi la mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh bilioni 520  katika Jiji la Arusha na baadhi ya maeneo katika wilaya ya Arumeru.


Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambapo alisema kituo hicho cha Forodha kimejengwa kwa ushirikiano wa nchi ya Kenya na Tanzania. Kwa mujibu wa Gambo kituo hicho cha forodha kitakuwa mwarobaini wa kubithibiti vichochoro vya kupitisha magendo zikiwemo nyara za serikali.
Alisema katika kuimarisha ulinzi wa kituo hicho mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Saimon Sirro ametoa mbwa wawili ambao watagundua aina yeyote ya magendo ikiwemo meno ya tembo,madawa ya kulevya na mlipuko.


"Niwasihi wananchi wote kuheshimu sheria za nchi kwa kuepuka kufanya vitendo vya kupitisha magendo kwenye mpaka wa Namanga kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimeimarisha ulinzi na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kuhusu uwekaji msingi mradi huo wa maji Gambo alisema Rais Magufuli ataweka jiwe la Msingi eneo la chanzo cha maji hayo kilichopo wilayani Arumeru.Alisema baada ya kuweka jiwe hilo la Msingi atatembelea ujenzi mradi huo kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha sambamba na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta walipokutana leo kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC)  leo Novemba 30, 2018 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museven kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC) leo Novemba 30,2018

Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika kikao chao cha ndani kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC) leo Novemba 30, 2018.
Picha na IKULU

RAIS WA ZANZIBAR AZUNGUMZA NA UJUMBE WA WASHIRIKA WA MAENDELEO SEKTA YA KILIMO TANZANIA

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Meneja Mkaazi wa Growing Africa’s Agriculture (AGRA) wakati wa mazungumzo na Ujumbe wa Washirika wa Sekta ya Kilimo Tanzania, ukiongozwa na Mwakilishi wa FAO Tanzania na Mwenyekiti wa Washirika wa Maendeleo Sekta ya Kilimo Tanzania  Mr. Fred  Kafeero, ulipofika Ikulu leo 30/11/2018 kwa mazungumzo.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwakilishi  wa FAO Nchini Tanzania na Mwenyekiti wa Washirika wa Maendeleo Sekta ya Kilimo Tanzania Mr. Fred Kafeero, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kungozana na Ujumbe wake.
  Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Washiriki wa Maendeleo Sekta ya Kilimo Tanzania kushoto Mwakilishi wa FAO Nchini Tanzania pia ni Mwenyekiti wa Washiriki wa Maendeleo Sekta ya Kilimo Tanzania Mr, Fred Kafeero akiwa na Mwakilishi wa UNIDO Tanzania,Mauritius na EAC.Mr. Stephen Bainous Kargbo, 30/11/2018.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mwakilishi wa FAO Nchini Tanzania Mr.Fed Kafeero, alipofika Ikulu Zanzibar na Ujumbe wake wa Washirika wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo Tanzania, kwa mazungumzo leo 30/11/2018. 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na mgeni wake Mwakilishi wa FAO Nchini Tanzania pia ni Mwenyekiti wa Washirika wa Maendeleo Sekta ya Kilimo Tanzania Mr. Fed Kafeero, wakitoka katika ukumbi wa mkutano  baada ya kumaliza mazungumzo yao  yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo 30/11/2018.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mwakilishi wa FAO Nchini Tanzania Mr. Fred Kafeero kushoto na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Ujumbe wa Washirika wa Maendeleo Sekta ya Kilimo Tanzania, baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar.30/11/2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Mwakilishi wa FAO Nchini Tanzania Mr. Fred Kafeero, alipofika Ikulu Zanzibar na Ujumbe wake wa Washirika wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo Tanzania, kwa mazungumzo na Rais wa Zanzibar. (Picha na Ikulu) 

MAOFISA SITA WIZARA YA ARDHI WASIMAMISHWA KAZI

Washiriki Master Tanzania kutambulishwa Forty Forty Tabata leo

$
0
0
WASHIRIKI wa Shindano la Master Tanzania 2018/19, wanatarajiwa kutambulishwa leo Forty Forty Club, iliyopo Tabata Bima, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mratibu wa shindano hilo, Michael Maurus, alisema kuwa utambulisho huo ni sehemu ya maandalizi ya shoo ‘bab kubwa’ ya mchujo itakayofanyika wikiendi ya pili ya mwezi huu katika ukumbi utakaotangazwa.

Alisema kuwa jumla ya washiriki 30 watakuwapo Forty Forty leo ambapo watapata nafasi ya kujitambulisha mbele ya wadau wa sanaa ya uanamitindo na burudani kwa ujumla.“Tunaushukuru uongozi wa Forty Forty kwa kutupa nafasi hii, wadau wa burudani waje kwa wingi kuwaona vijana wanatashati watakaoshiriki shindano letu ambalo fainali zake zitafanyika Februari mwakani kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam,” alisema Maurus.

Maurus alisema kabla ya fainali za shindano hilo, kutakuwa na hatua ya robo na nusu fainali ambapo lengo lao ni kuwa na washiriki wa awali 50.

“Lengo letu ni kuwa na washiriki 50 na kesho (leo) ni siku ya mwisho kwa vijana wanaopenda kushiriki mashindano hayo kujiandikisha, baada ya hapo watalazimika kulipia fomu. Hivyo kwa wanaopenda kushiriki, waje pale Forty Forty kuanzia saa 2:00 usiku wachukue fomu, wazijaze na kuzirejesha hapo hapo,” alisisitiza Maurus.
Baadhi ya washiriki Master Tanzania 2018

WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA BALOZI AMINA SALUM ALI AZUNGUMZA NA WAANDISHI ZANZIBAR

$
0
0
Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Balozi Amina Salum Ali akizungumza na Waandhishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali kuhusiana na Maadhimisho ya kutimia miaka 50 toka kuundwa kwa Shirika la ZSTC 1968 mkutano uliofanyika katika ukumbi wa ZSTC Migombani mjini Zanzibar.
 Muandishi wa Habari wa Bahari FM Tabia Makame akiuliza maswali katika mkutano na Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali kuhusiana na Maadhimisho ya kutimia miaka 50 toka kuundwa kwa Shirika la ZSTC 1968 mkutano uliofanyika katika ukumbi wa ZSTC Migombani mjini Zanzibar.
 Mwandishi wa Habari wa ITV Farouk Kariym akiuliza maswali katika mkutano na Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali kuhusiana na Maadhimisho ya kutimia miaka 50 toka kuundwa kwa Shirika la ZSTC 1968 mkutano uliofanyika katika ukumbi wa ZSTC Migombani mjini Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Gulio la TCRA kuelimisha umma juu ya matumizi bora ya huduma za mawasiliano lafana

$
0
0
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imesema kuwa wananchi wanatakiwa kutumia Mawasiliano kwa maendeleo. Hayo ameyasema Mkuu wa Kitengo cha Watumiaji wa Mawasiliano wa TCRA Thadayo Ringo wakati wa Gulio lililofanyika kata Ilembo mkoani Mbeya amesema kuwa mawasiliano yameleta fursa kwa wananchi hivyo watumie katika kujiletea maendeleo.

Amesema kuwa katika uchumi wa viwanda hivyo watumie katika kutangaza biashara au bidhaa wanazozalisha viwandani. "TCRA itaendelea kutoa elimu katika kuhakikisha kila mwananchi anatumia mawasiliano katika kujiletea uchumi na sio kutumia kwa matumizi yasiyo na faida"amesema
Aidha amesema kuwa katika Gulio katika sehemu mbalimbali wameambata na watoa huduma za mawasiliano, pamoja na Jeshi la Polisi ili kutoa elimu kwa wananchi hao.

 Wananchi wa Kata ya Ilembo wakiwa kwenye banda la TCRA baada ya kuwasogezea huduma za za utoaji huduma ya mawasiliano  wakati wa Gulio la TCRA la kuelimisha umma juu ya matumizi bora ya huduma za mawasiliano.

JUHUDI ZA HKMU ZAPONGEZWA, WASHAURIWA KUONGEZA IDADI YA WADAHILIWA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
KONGAMANO la kwanza la kitaaluma la Chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki limefanyika leo kwa kuwakutanisha wataalamu na baadhi ya wanafunzi waliosoma katika chuo hicho.

Akifungua kongamano hilo Katibu mkuu wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amepongeza juhudi zinazofanya na taasisi hiyo katika kuboresha sekta ya afya na anafurahi kuona wanafunzi bora wanatoka katika chuo hicho ambacho aliwahi kufundisha wakifanya kazi ndani na nje ya nchi.

Amesema kuwa taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake imekuwa ikifanya vizuri na mchango wao katika sekta ya afya unaonekana na wao kama Wizara wapo bega kwa bega katika kuhakikisha wanaimarisha vyema sekta ya afya nchini.

Dkt. Mpoki amewataka wahitimu na wanafunzi kujiunga katika taasisi mbalimbali za afya na ameshauri kuwa kongomano hilo liwe endelevu katika kuimarisha  na kufikia malengo waliyojiwekea ambayo yataonesha uimara na ubora wa taasisi hiyo.

Aidha amesema kuwa taasisi hiyo lazima ijijenge ili kuweza kuendelea kudahili wanafunzi wengi bora na hilo litafanikiwa kama wahitimu watafanya kazi zenye thamani za kutangaza taasisi hiyo.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza katika kongamano la kwanza la kitaaluma katika chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki ambapo amewapongeza kwa kutoa mchango katika sekta ya afya na kuwataka kuongeza idadi ya wadahiliwa katika chuo hicho.
 Rais wa kongamano la kitaaluma chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hurbet Kairuki Dkt. Leonard Malasa akizungumza na hadhara wakati wa kongamano hilo ambapo amesema kuwa wanashirikishana ujuzi na kushirikiana ili kuweza kukuza hadhi na thamani ya chuo hicho.
Naibu Makamu Mkuu (taaluma) wa chuo  kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki Dkt. Moshi Ntabaye  akizungumza wakati wa kongamano la kwanza la kitaaluma kufanyika chuoni hapo ambapo amesema kuwa wamejizatiti katika kuhakikisha wanashiriki vyema katika kuimarisha  sekta ya afya nchini.
 Katibu Mkuu Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akikabidhi zawadi kwa Michael Kalimba mmoja ya kati wanafunzi waliofanya vizuri kwa mwaka 2018, kulia ni makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa. Charles Mgone na kushoto ni Rais wa kongamano hilo Dkt. Leonard Malisa.(Picha na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

ASILIMIA 85 YA WANAWAKE MKOANI MARA WANAJIFUNGUA KATIKA VITUO VYA AFYA.

$
0
0
Na WAMJW - MARA.

Asilimia 85 ya Wanawake Mkoani Mara wanajifungua kwenye vituo vya Afya, hali iliyosaidia kupunguza idadi kubwa ya vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu wakati alipotembelea Hospitali ya Mkoa wa Mara kukagua hali ya utoaji Huduma.

"Mko Asilimia 85, kitaifa tupo Asilimia 51, kwahiyo niwapongeze kwa hilo, lengo letu ilikuwa ifikapo 2020 tunataka angalau Asilimia 80 ya wanawake wajawazito wajifungulie kwenye vituo vya Afya" Alisema Waziri Ummy.

Pia Waziri Ummy ameitaka Mikoa mingine nchini kuiga jitihada zinazofanywa na mkoa wa Mara za kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kuhakikisha wanawake wajawazito wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

"Sitaielewa mikoa mingine kwa kushindwa kuhamasisha na kuweka Mazingira mazuri kwa wanawake kwenda kujifungulia katika vituo vya kutoa huduma za Afya" alisema Waziri Ummy

Hata hivyo Waziri Ummy Mwalimu amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara kuhamasisha jamii hususan wanawake katika maeneo mbali mbali kuhudhuria kliniki angalau Mara 4 katika kipindi cha ujauzito.

"Wanawake ambao wanahudhuria Kliniki angalau mara 4 ni Asilimia 45 hivyo hamjafanya vizuri kwasababu kitaifa ni Asilimia 51, mjenge tabia ya kuwahamasisha wanawake kuhudhuria kliniki angalau Mara 4, kama watoa huduma za Afya wanavyotushauri" alisema Waziri Ummy.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akihoji juu ya gharama za huduma za Afya zinazotolewa katika Hospitali ya Mkoa wa Mara, pindi alipofanya ziara ya kukagua ubora wa huduma na miundombinu katika Hospitali hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisikiliza maoni ya mmoja kati ya wagonjwa waliofika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akitoa maoni juu ya namba za mawasiliano zilizopo kwenye ubao mdogo wa matangazo katika Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Mara, pindi alipofanya ziara ya kukagua ubora wa huduma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisikiliza maoni ya mmoja kati ya wagonjwa waliofika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.


SERIKALI INAFANYA MAPITIO YA LESENI ZA UCHIMBAJI-MAJALIWA

$
0
0
*Zitakazobainika kutofanya kazi kwa muda mrefu itazichukua 

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali inafanya mapitio ya leseni zote za uchimbaji wa madini na zile ambazo zitabainika kuwa hazijafanya kazi kwa muda mrefu zitachukuliwa na kisha maeneo hayo hayo yatagawiwa kwa wachimbaji wadogo. Amesema Wizara ya madini imeimarishwa  na sasa inatengeneza fursa kwa ajili ya wachimbaji wadogo ili waweze kunufaika na rasilimali hiyo muhimu inayopatikana katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na Mji Mdogo wa Katoro.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Novemba 30, 2018) wakati akizungumza na wananchi katika Mji Mdogo wa Katoro uliopo kwenye Halmashauri ya wilaya ya Geita, akiwa kwenye siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Geita.

Waziri Mkuu amewaambia wananchi hao ambao wengi wao ni wachimbaji wadogo kuwa waendelee kuwa na imani na Serikali yao ambayo imedhamiria kuhakikisha wachimbaji hao wanafanya shughuli zao bila ya kubugudhiwa.“Jipangeni kwa kufanya kazi maeneo yapo na Serikali itawapa. Nawashauri mjiunge katika vikundi vitakavyosajiriwa na kutambilika kisheria ili muende kwenye mabenki mbalimbali na kukopa fedha za kununulia mitambo ya kisasa itakayowawezesha kuchimba kwa kutumia teknolojia ya kisasa.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Geita ihakikishe kila kijiji kinakuwa na kisima cha maji ili kuwapunguzia wananchi kutumia muda mwingi kwa kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta maji katika maeneo yasiyojulikana. Kuhusu changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama inayowakabili wanachi kwenye Mji Mdogo wa Katoro, Waziri Mkuu amewataka waendelee kuwa na subira kwani Serikali imepanga kuwafikishia maji kutoka ziwa Victoria. 

Waziri Mkuu amesemaSerikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao. Waziri Mkuu amesema mbali na kuimarisha huduma za maji  kwenye Mji Mdogo wa Katoro, pia Serikali imedhamiria kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya na kikuwezesha Kituo cha Afya cha Katoro kiweze kuwa na maabara, chumba cha upasuaji, wodi ya mama na mtoto, chumba cha kujifungulia, wodi za wanawake na wanaume.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema Serikali imeendelea kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini wakiwemo na wa Mji Mdogo wa Katoro ili waendelee kufanya shughuli zao bila ya usumbufu wa aina yoyote. Amesema katika kuhakikisha wachimbaji hao wafanya shughuli za uchimbaji kwa weledi, Serikali imeamua kujenga vituo vya mfano vyenye lengo la kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo kuhusu namba bora ya uchimbaji kwa kutumia teknolojia ya kisasa

Amesema Mji Mdogo wa Katoro ni miongoni mwa maeneo ambayo Serikali imejenga kituo hicho katika eneo la Lwamgasa. Pia amesema wachimbaji wadogo kwa sasa wanaendelea na shughuli zao katika maeneo mbalimbali kwa uhuru na Amani yakiwemo ya Bingwa, Musasa, Nyamalimbe, Nyarugusu, Lwamgasa. Naibu Waziri huyo ametaja maeneo mengine nchini ambayo Serikali inaendelea na miradi ya ujenzi wa vituo hivyo kuwa ni pamoja na Lindi, Chunya, Mpanda, Tanga na   Buhemba mkoani Mara.

Naye, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewahakikishia wakazi wa Mji mdogo wa Katoro na Buselesele kuwa maeneo yao yote ambayo hajaunganishiwa umeme wasiwe na wasiwasi umeme utawaka kabla ya sikukuu ya X-Mass. Amesema mkandarasi tayari ameshafika kwenye maeneo hayo na kuanza  kazi. Dkt. Kalemani amesemaSerikali maeneo hayo yatasambaziwa umeme kupitia Mradi wa Nishati Vijijini (REA) na wananchi hawatowajibika kulipia gharama za nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme kwani tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.

“Rais wetu Dkt. John Magufuli anataka kuona nyumba ya kila Mtanzania inapata umeme tena kwa gharama nafuu na ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.” Awali, Mbunge wa Busanda, Lolencia Bukwimba alimuomba Waziri Mkuu awasaidie kuwatatulia changamoto mbalimbali zinazowakabili zikiwemo za huduma za afya kwa kuwa kituo chilichopo hakitoshelezi mahitaji kwani watu wengi. Ameomba Serikali iwajengee hospitali na kuimarisha huduma za mama na mtoto kwa kuwa kwa mwezi wanazaliwa watoto 700.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE KUTOKA GIRL GUIDES ASSOCIATION

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Wajumbe kutoka Tanzania Girl Guides Association ambapo pamoja na mambo mengine alitambulishwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Bi. Anna Maembe na Wajumbe wengine wa Bodi hiyo kwenye ofisi ya Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akifanya mazungumzo na Wajumbe kutoka Tanzania Girl Guides Association kwenye ofisi ya Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Tanzania Girl Guides Association kwenye ofisi ya Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI MKUTANO MKUU WA 20 WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI ARUSHA.NOVEMBA 30, 2018

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC) Novemba 30, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museven kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC) Novemba 30, 2018.
Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika kikao chao cha ndani kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC) Novemba 30, 2018.
PICHA NA IKULU

WASSIRA ATUMIA MAHAFALI CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KUTOA UJUMBE KWA WASOMI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Blogu ya jamii

CHUO cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam  kimefanya mahafali yake ya 13 ya chuo hicho ambapo jumla ya wahitimu 1578 wamehitimu ngazi mbalimbali za mafunzo huku 
Mwenyekiti wa Bodi chuoni hapo Steven Wassira akishauri somo la maadili na uzalendo liwe la lazima kwa wanafunzi wote.

Mahafali ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere yamefanyika leo Novemba 30 mwaka 2018 ambapo pamoja na mambo mengine wahitimu ambao wamefanya vizuri kwenye masomo wamepewa zawadi na vyeti vya kuwatambua.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakaluka , wahadhiri wa chuo hicho, wahitimu, wanafunzi na wageni waalikwa Wassira ambaye ndiyo alikuwa mgeni rasmi amesema elimu ndio kila kitu kwenye maisha ya mwanadamu amapo pamoja na faida nyingine nyingi faida nyingine ya elimu ni kurahisisha utendaji kazi wa majukumu ya mhusika.

"Elimu ni mfano wa shamba ambalo unapanda mbegu bora na unavuna mazao bora.Hivyo nitumie nafasi hii kuwapongeza wote waliohitimu mafunzo yao chuoni hapa kwa ngazi mbalimbali.Hata hivyo niwakumbushe Watanzania elimu haina mwisho, hivyo ninyi mliomaliza ni vema mkaendelea na hatua nyingine za kielimu kwa maslahi yenu na Taifa kwa ujumla.
 Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakaluka akizungumza kwenye mahafali ya 13 ya chuo hicho yaliyofanyika leo chuoni hapo
 Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Steven Wassira ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 13 ya Chuo hicho ageni rasmi (kulia) akiwa na Mkuu wa Chuo Profesa Shadrack Mwakaluka wakipitia kwa umakini majina ya wahitimu.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya chuo hicho pamoja na viongozi wengine wa chuo wakiwa pamoja na wahitimu waliofanya vizuri kwenye masomo(waliosimama nyuma).
 Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye picha wakati wa mahafali ya 13 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika leo chuoni hapo.


RC MAKONDA KUPAMBA SHEREHE ZA MIAKA 18 YA MAGIC FM

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, anatarajiwa kuzipamba sherehe za kutimiza miaka 18 tangu kuanzishwa kwa kituo cha Redio cha Magic FM kesho.

Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa vipindi na maudhui Orest Kawau amesema sherehe hizo zitafanyika katika viwanja vya shule ya Tandale hivyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi.

Pia amesema zawadi mbalimbali zitagawiwa kwa wasikilizaji wa kituo hicho cha Magic FM na kwa watakaowahi watajipatia zawadi maalum."Tumeamua kuadhimisha miaka 18 ya Magic FM ili kurudisha fadhila kwa wasikilizaji wetu ambao wametuunga mkono kwa kipindi chote tangu tulipoanza mpaka sasa. Tunawaomba watanzania waendelee kutuamini na tunaahidi kuwapa ladha inayostahili kwa wakati wote" Alisema Kawau.

Kwa upande wake Balozi wa Kampuni ya bahati nasibu ya Daka Pesa ambao ni wadhamini wakuu wa hafla hiyo Salum Salehe amesema kampuni imeamua kudhamini ili kuungana na kituo hicho hasa katika kutoa elimu juu ya huduma wanazotoa kupitia mchezo wao wa Daka Pesa ambapo mteja anaweza kucheza kwa kiwango cha kuanzia 500 na kujishindia zaidi ya milioni 1.
Mkuu wa vipindi na Maudhui kutoka redio Magic Fm, Orest Kawau akizungumza kuhusiana na maadhimisho miaka 18 tangu kuanzishwa kwa kituo cha Redio cha Magic FM kesho yatakayofanyika kesho.
Balozi wa Daka Pesa, Salum Saleh (kulia) akizungumza jambo kuelekea maadhimisho ya miaka 18 tangu kuanzishwa kwa kituo cha Redio cha Magic FM kesho.
Balozi wa Daka Pesa ambao ndio wadhamini wa sherehe hizo, Salum Saleh (kulia) akionysha bango la kampuni yao.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images