Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

YANGA YAJIKITA KILELENI BAADA YA USHINDI WA 3-0 DHIDI YA JKT TANZANIA

$
0
0
Na Agness Francis, blogu ya Jamii. 

VIJANA wa Jangwani Yanga SC wameibuka na ushindi baada ya kuwatandika mafande wa JKT mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa leo katika dimba la Taifa Jijini Dar es  Ligi Kuu Tanzania Bara(TPL). 

Yanga anakaa kileleni kwa kufikisha alama 35 wakiwa na  michezo 13 wakishinda mechi kumi na sare mbili, ambapo Azam akiwa chini yao kwa pointi  33 michezo  sawa na Yanga, huku Simba akiwa nafasi ya tatu alama 27. 

Mtanange huo wa aina yake ulioanza majira ya saa kumi jioni na kila upande  walicheza kwa kukamiana na  kutafuta magoli ya ushindi ambapo kwa kipindi hicho cha kwanza na katika  dakika  ya 19 za mapema Yanga anapata bao la ushindi kutoka kwa mchezaji Heritier Makambo kutikisa nyavu za JKT ambapo anafikia rekodi ya mchezaji wa Simba Meddie 8 Kagere kwa kufikisha idadi ya  magoli 7.

Mpira uliendelea kupigwa kila timu ilishambulia lango la Maafande wa JKT wakitafuta goli la kusawazisha na Yanga wakitafuta magoli ya kuongoza mpaka wachezaji wanaenda mapumzikoni matokeo yalibaki kuwa ni 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi zaidi  kwa pande zote JKT walionyesha kufika langoni kwa Yanga ambapo wamelenga mashuti yasio Leta madhara kwa Yanga, na dakika ya  52 mchezaji Mrisho  Ngasa (Anko) ameiandikia klabu yake goli 2.

Mchezo uliendelea kuchezwa kwa kuwakamiana JKT wwalionyesha kushambulia langoni kwa Yanga kutafuta magoli wakati Yanga waliitaji ushindi zaidi wa magoli mengi na kutoka na alama ili kujiweka Katika msimamo wa nafasi nzuri Ligi kuu Tanzania bara (TPL). 

Katika dakika za 78  Ibrahim Ajibu anaiandikia timu yake goli la 3 kwa mkwaju wa Penati iliyosababishwa na mchezaji wa JKT kuunawa mpira, 

Kocha mkuu wa klabu ya  yanga Mwinyi Zakhera amezungumza na waandishi  wa habari ni baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika kati uwanja wa Taifa amesema kuwa "Nimefurahishwa na matokeo wachezaji wangu wamejitahidi licha ya  jana saa nne usiku kupigiwa simu kuwa  tff wamebadilisha ratiba muda wa kuchezwa mechi ambapo ilitakiwa ichezwe saa 12 jioni, na kusema itachezwa sa 10 jioni"

Zahera amesema "lakini haikuwa sawa ilitakiwa watoe taarifa masaa 24 kabla"

Huku kocha mkuu wa JKT Bakari Shime amesema kuwa  "tulipata nafasi nne mpaka tumeshindwa kuzitumia inamana tungezitumia vema tungekuwa na matokeo mazuri, baada ya goli la 2 wachezaji wangu walionyesha kukosa kujiamini, mimi kama kocha nitakaa na wachezaji wangu na kufanyia kazi makosa yetu"

Mchezo ujao Yanga anatarajia kusafiri mkoani Mbeya kumenyana na Prison katika uwanja wa Sokoine Disemba 3.

WAZIRI ANGELA KAIRUKI, AZINDUA KITABU CHA MIAKA 10 CHA SIMULIZI ZA LUKUNDO

$
0
0
Waziri wa Madini Angela Kairuki Akikata Utepe Kuzindua Kitabu Cha Simulizi ya za Lukundo Kilichoandikwa na Mama Fatma Kange,Anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Same Rose Staki Pamoja na Salehe Njaa mume wa Mwaandishi wa kitabu hicho (Kushoto).Uzindui Huo Umefanyika Jijini Dar es salaam.

Aidha Waziri Kairuki Amewataka Watanzania Kupenda vitu vya Nyumbani ili kuwapa Moyo watazania wenzetu katika Kazi nao na Ubunifu wao.Amepongeza Sana Mwandishi wa Kitabu Hiko Bi Fatma Kange ambaye katika Kitabu hicho amegusia Maisha na Malezi ya Kabila la Wapare.
Fatuma A. Kange, amefurahi kuzindua kazi yake kubwa “ KITABU CHA SIMULIZI ZA LUKUNDO” ambachoamekifanyia utafiti na kuelezea mambo mengi ya msingi kwa muda mrefu mno.. imemchukua takribanimiaka 10 kukamlisha kazi yake hiii kuntu! wakati wa ufunguzi Fatuma alisema amekuwa akitumia likizoyake kila mwaka anapokwenda kijijini kwao Makanya,Kimunyu Same kufanya utafiti.

 Anasema alikuwaanaona raha kwenda kwao, kumsalimia babu yake Mzee Juma Kimomwe na bibi yake Kozaina naKorashid ambao kupita likizo hiyo, alijikita kufanya tafiti ndogondo za kitongoji cha kimunyu ambachoamelelewa na kutumia muda huo vizuri kuhifdha habari mbalimbali. maeneo aliyoyataja ni yale yoteambayo yanaizunguka kitongoji cha kimunyu kama yote ya Chome, Mwembe, Hekapombe,Mongoloma,Mnazi, Mzumura, Tae, Makuyuni, Makanya stasheni, Mgwasi na kimunyu.
Uzinduzi ulipata wafadhili wakutosha na kushukuru kwamba kazi aliyoifanya kumbe imekuwa ya faida!kitabu chake kimechambuliwa na maprofesa waliobobea katika kiswahili na kukipa kitabu hicho nguvuya kuthibitishwa na Mhe. mama Samia Suluhu Hassan-Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, ambaye amekipa heshima kubwa ya kukiandikia dibaji. 

Fatuma Kange amejionamwenye bahati kubwa sana.kikubwa katika kitabu hicho, Fatuma ameeleza masuala ya malezi kwa mtizamo wa kipare, dhana zakipare zote zililenga kumjenga mtoto wa kike, hivyo amezungumzia, kuratera, kuja ghwi, kirighi cha ngwina upendo kama ambavyo bibi yake Kozaina alimpa! mapenzi makubwa yaliyotukuka! hakuna kama bibi

kozaina na ndiyo maana ameona ahifadhi kumbukumbu zote alizolelewa na bibi yake katika kitabu hikikikubwa cha SIMULIZI ZA LUKUNDO ambacho kimebeba jina la kozaina.


SERIKALI YA NORWAY YARIDHISHWA NA UKARABATI WA VITUO VYA KUZALISHA UMEME NCHINI

$
0
0

SERIKALI ya Norway imefurahishwa na jitihada zilizofanywa na serikali nchini katika kusimamia fedha walizotoa mwaka 1995 kugharamia miradi ya ukarabati wa vituo vya kuzalisha umeme vilivyopo hapa nchini.

Akizungumza leo baada ya kutembelea kituo cha New Pangani Falls, katika ziara yake ya kukagua miradi wanayoifadhili, Waziri wa Maendeleo nchini Norway Nicolai Astrup, alisema walitoa fedha hizo kwa serikali kutokana na uhusiano uliopo baina ya mataifa hayo ikiwemo usimamizi mzuri uliofanywa na serikali ya awamu ya tano.

 Waziri huyo pia alisema kuwa serikali yake imeongeza mkataba wa kusaidia uwekaji wa nishati ya umeme katika maeneo ya vijiji kutoka mwaka 2020-2021 baada ya kuridhika na usimamizi mzuri uliofanywa katika ukarabati wa vituo hivyo.

“Nipo hapa Pangani Falls, Norway na Tanzania wanahusiano muda mrefu, nimekuja kufuatilia matokeo ya msaada tuliotoa mwaka 1995, kwa vituo vya kuzalisha umeme ‘Hydro Power Plants’,” alisema. 

Baadaye akizungumza na wananchi wa mji wa Bagamoyo wilayani Korogwe Waziri huyo alisema kwamba nishati ya umeme ni muhimu katika maendeleo ya wananchi katika kufanya shughuli zao za kiuchumi na kwamba serikali yao itanedelea kushirikiana na Tanzania kusaidia nishati hiyo.

Serikali ya Norway ilitoa kiasi fedha za Kimarekani dola milioni 126 awamu ya kwanza na kisha awamu ya pili ya ukarabati wa vituo vya kuzalisha umeme vya New pangani Falls, Kidatu, Kihansi, Nyumba ya Mungu na Mtera ukarabati uliomalizika Aprili mwaka huu walitoa jumla ya shilingi bilioni 21.

NAIBU Waziri wa Nishati wa tatu kutoks kushoto akiwa na Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup wakimsikiliza kwa umakini Kaimu Meneja wa Pangani Hydro System Lewis Loiloi akieleza namna ya uzalishaji wao wakati wa kutembelea kituo cha New Pangani Falls, katika ziara yake ya kukagua miradi wanayoifadhili
Kaimu Meneja wa Pangani Hydro System Lewis Loiloi akieleza namna ya uzalishaji wao wakati wa kutembelea kituo cha New Pangani Falls, katika ziara hiyo kukagua miradi wanayoifadhili kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup katikati ni Naibu Waziri wa Nishati Subiri Mgalu 
Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup kushoto akiteta jambo na Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu 

Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup kushoto akisaini kitabu cha wageni kulia ni Naibu Waziri wa Nishati Subiri Mgalu.

MABULA AZITAKA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA NA MAJI PAMOJA NA UMEME KUFIKISHA HUDUMA MJI WA SERIKALI IHUMWA JIJINI DODOMA

$
0
0
Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi imezitaka mamlaka zinazohusika na maji pamoja na umeme kufikisha huduma hizo mapema iwezekanavyo katika mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma ili kurahisisha ujenzi wa ofisi za Wizara kuanza.

Naibu waziri wa wizara hiyo Angelina Mabula ametoa maagizo hayo leo alipotembelea eneo zinapojengwa ofisi za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto katika eneo hilo.

Mabula amesema kuwa kutokana na kasi walinayo Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) ambao ndio wanatekeleza ujenzi huo wanaweza kukwamishwa na changamoto ya maji .

“Shirika la Nyumba wako serius kweli na kazi hii maana walipewa kazi ya kujenga ofisi za Wizara tatu baada ya siku mbili tu wakaanza kufanyia kazi agizo hilo, ila changamoto inakuwa kwenye huduma ya maji na umeme ambazo hazipo katika eneo hili.
Bw.Frank Mambo,mbunifu majengo kutoka Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) akimuonyesha eneo Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula itakapojengwa ofisi za Wizara hiyo alipotembelea eneo hilo leo jijini Dodoma
Mafundi mbalimbali kutoka Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) wapo kazini katika eneo la ujenzi wa ofisa za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto
Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula akiangalia ramani ya ujenzi wa ofisi ya wizara yake katika ni Frank Mambo,mbunifu majengo kutoka Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) na kulia ni wa msimamizi mradi huo Hasani Bendera 
Bango likionesha mji wa Serikali ambapo eneo hilo zitajengwa ofisi za wizara mbalimbali Ihumwa jijini Dodoma

Serikali Yaandaa Mtaala Utakaotumika Kuwanoa Wanasheria Wapya

$
0
0
Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Chadhamiria Kuwajengea Uwezo waajiriwa wapya Serikalini wa Kada ya Sheria ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt . Laurean Ndumbaro wakati akifungua Kongamano la Wadau lililolenga kupitia na kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa mawakili na wanasheria wa sekta ya umma, Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Mick Kiliba amesema kuwa lengo ni kuwajengeauwezo wanasheria hao ili waweze kujua mifumo ya uendeshaji wa shughuli za Serikali, Uongozi na Utumishi wa Umma.

“Lengo la kuwaandaa waajiriwa wapya wa Kada ya Sheria ni kujenga utumishi uliotukuka na bora katika Kada hii muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu”; Alisisitiza Kiriba.Akifafanua Bw. Kiliba amesema kuwa waraka namba (5) Tano wa mwaka 2011 wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, unaoelekeza kutolewa kwa mafunzo elekezi kwa watumishi wapya katika Utumishi wa Umma.

Aliongeza kuwa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kimekasimiwa madaraka ya kuandaa na kutoa mafunzo ya awali na elekezi kwa waajiriwa wote wa kada ya Sheria katika sekta ya Umma nchini.


Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais; Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mick Kiliba akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro leo Jijini Dodoma wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma.Kongamano hilo limeandaliwa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. 
Mkuu wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Mhe. Jaji Paul Kihwelo (PhD) akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma leo Jijini Dodoma. 
Mkuu wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Mhe. Jaji Paul Kihwelo (PhD) akisisitiza jambo kwa washiriki wa kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma leo Jijini Dodoma. 


KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

DKT. NDUGULILE ASIKITISHWA NA UTENDAJI KAZI SEKTA YA AFYA NA MAENDELEO YA JAMII TANGA

$
0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesikitishwa na utendaji kazi usioridhisha katika Sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii kwa mkoa wa Tanga kutokana na kutokuwa na usimamizi mzuri katika utekelezaji wa majukumu yao

Ameyasema hayo leo Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga alipofanya ziara ya kujionea shughuli zinazosimamiwa na Wizara yake katika Sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii na kukuta baadhi ya maafisa wahusika wakiwemo Waganga Wakuu wa Wilaya na Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Lushoto hawapo katika ziara yake..

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya Wilaya ya Lushoto amesema kuwa watendaji wa Wilaya hiyo hawako makini katika kutekeleza majukumu yao na hakuna usimamizi wa moja kwa moja katika kuhakikisha mambo yanaenda wilayani hapo.

“Nimesikiliza taarifa sijaona masuala ya Maendeleo ya Jamii na pia Afisa Maendeleo ya Jamii hayupo hapa na nimetembeela na Wilaya nyingine Waganga Wakuu wa Wilaya hawakuwepo hii inaonesha hamko makini katika kazi yenu” alisisitiza Dkt. Ndugulile

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na watendaji wa Wilaya ya Lushoto wakati wa ziara yake mkoani Tanga kufuatilia utekelezaji wa utoaji huduma katika Sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akipokea zawadi ya ua kutoka kwa mmoja wa mtoto anayeishi katika makao ya kululelea watoto yatima na wenye shida ya Irente yaliyopo Lushoto mkoani Tanga wakati wa ziara yake mkoani humo. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiwa amembeba mmoja wa mtoto anayeishi katika makao ya kululelea watoto yatima na wenye shida ya Irente yaliyopo Lushoto mkoani Tanga wakati wa ziara yake mkoani humo. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW 

NDITIYE: TAKUKURU FUTUATILIENI UJENZI WA GATI YA BANDARI YA LINDI

$
0
0

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameilekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufuatilia na kuchunguza thamani ya fedha zilizotumika kujenga gati ya bandari ya Lindi ili kuweza kubaini kama gharama iliyotumika inaendana na ujenzi uliofanyika
 
Hayo yameelezwa na Nditiye wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi mkoani humo ambapo amebaini kuwa kasi ya utendaji kazi kwenye gati hilo hairidhishi na kuongeza kuwa kazi ni ya mwaka mmoja ila imechukua miaka mitatu hadi sasa na bado haijakamilika. “Naielekeza TAKUKURU waje wafuatilie thamani ya fedha zilizotumika kujenga gati hili,” amesema Nditiye. 

Nditiye amesema kuwa kwa bahati mbaya miradi ya maendeleo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) inayotekelezwa nje ya bandari ya Dar es Salaam haitekelezwi ipasavyo, tufike mahala tuheshimu fedha za Serikali na za wananchi. “Kwa bahati mbaya TPA hamfiki eneo la mradi wakati wa kuandaa nyaraka na hata ujenzi wa miradi husika inavyoendelea hivyo tunaingia hasara,”amesema Nditiye .

Mhandisi Ujenzi wa Bandari ya Mtwara Twaha Msita wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa gati hiyo kwa Nditiye amesema kuwa Kampuni ya Comfix & Engineering Ltd ilipewa kazi na TPA ya kujenga gati hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Mei mwaka 2015 na kutakiwa kukamilika mwezi Mei mwaka 2016 kuendana na mkataba husika kwa gharama ya shilingi bilioni 3.1 ambapo baada ya muda ilionekana kazi zimeongeza na hivyo kuongezewa fedha hadi kufikia shilingi bilioni 3.5 .



   Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Ujenzi wa Bandari ya Mtwara, Twaha Msita (hayupo pichani) kuhusu kutoridhishwa na ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi wakati wa ziara yake ya kukagua bandari hiyo mkoani humo. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyevaa fulana ya bluu) akikagua ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi unaosuasua wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi huo mkoani Lindi. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa gati ya bandari ya Nyamisati wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi huo Kibiti, Lindi. Meneja Mradi wa TPA Mhandisi Erick Madinda akitoa maelezo.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

WAZIRI LUGOLA AWATAKA MAJAMBAZI WAJISALIMISHE PAMOJA NA SILAHA ZAO, POLISI HAWATALALA MPAKA JAMBAZI WA MWISHO AMETIWA MBARONI

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka majambazi popote walipo nchini kujisalimisha pamoja na silaha zao wakati Polisi wakiendelea na msako mkali mpaka jambazi wa mwisho anatiwa mbaroni. Lugola amesema Jeshi la Polisi lipo imara na litawasaka majambazi hao usiku na mchana popote walipo na litahakikisha nchi inaendelea kuwa salama na wananchi wema wakiendelea kufanya shughuli zao za maendeleo kwa kulijenga Taifa.

Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kasahunga, Kata ya Neluma, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, leo, Lugola amesema usalama wa nchi hauchezewi na mtu yeyote na watu wasijaribu kutikisa kiberiti kwa kulichezea Jeshi la Polisi.
 Lugola amesititiza kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano ambayo inaongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ujambazi hauna nafasi na pia amewataka majambazi hao wafanye kazi nyingine ya kuwaingizia kipato kwa njia halali. 

“Msijaribu kukitikisa kiberiti, Serikali ipo macho muda wote, Jeshi lenu lipo imara, majambazi wanaofanya uvamizi, tutahakikisha tunawasaka popote walipo jambazi mmoja baada ya mwingine, hatutalala wala kupumzika hadi jeshi letu litakapomtia mbaroni jambazi wa mwisho,” alisema Lugola. Kutokana na msako huo, Lugola alisema majambazi hao wajisalimishe wenyewe pamoja na dhana zao kwenye kituo cha polisi wanachoona kipo jirani na wao, vinginevyo hawatasalimika na hawatabaki salama.

“Kama kuna ndugu zetu, watoto wetu, majirani zetu tuwaambie serikali hii ya magufuli nafasi hiyo ya kufanya ujambazi haipo, nimepata taarifa za uhalifu, wizi wa mifugo na uvamizi wa aina mbalimbali, tuone taarifa polisi ili tuweze kuwatia mbaroni majambazi hao kwa wale wote ambao mnahisi wanajihusisha na uhalifu, toeni ushirikiano bila woga ili meneo yetu yazidi kuwa na amani,” alisema Lugola.

Hata hivyo, Lugola alisema ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake ambavyo anavisimamia wapo baadhi ya askari wachache ambao wanajihusiha na vitendo vya rushwa na alishatoa onyo mara nyingi, hivyo atakao wakamata hatawaonea huruma. 
 

“Kuna baadhi ya mazingira ambayo yanachangia rushwa zaidi ndani ya Jeshi la Polisi ikiwemo kutokutolewa kwa dhamana katika siku za mapumziko Jumamosi na Jumapili, baada ya kuona kunamianya ya rushwa nikatangaza nchi nzima vituo vyote vya polisi vitoe dhamana saa 24 na siku 365 na robo, pia kutowekwa mahabusu watuhumiwa ambao wanamakosa madogo madogo,” alisema Lugola.

Lugola anaendelea na ziara jimboni kwake ya kuhamasisha wananchi kuanza maandalizi ya kilimo pamoja na kuendeleza miradi ya maendeleo huku wakiendelea kuheshimu sheria za nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Kasahunga, Kata ya Neluma, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo. Lugola aliwataka wananchi wa Mwibara washirikiane na polisi kuwafichua majambazi, na pia aliwataka majambazi wajisalimishe pamoja na silaha zao katika kituo chochote cha polisi nchini, kwa kuwa polisi usiku na mchana wanawasaka na watahakikisha wanamtia mbaroni jambazi wa mwisho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akiwapelekea zawadi kikundi cha kwaya ya Kijiji cha Kasahunga, Kata ya Neluma, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, wakati waimbaji hjao walipokua wanampokea kwa kijijini hapo. Lugola katika hotuba yake kwa wananchi zaidi ya 100 waliohudhuria mkutano huo, aliwataka wananchi wa Mwibara washirikiane na polisi kuwafichua majambazi, na pia aliwataka majambazi wajisalimishe pamoja na silaha zao katika kituo chochote cha polisi nchini, kwa kuwa polisi usiku na mchana wanawasaka na watahakikisha wanamtia mbaroni jambazi wa mwisho.

PETRONILA SIRINYA AJISHINDIA BAJAJI YA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA

$
0
0
Timu Shinda Zaidi na SportPesa imebahatika kumpata mshindi mwigine mwanamama akiwa ni mwanamke watatu kujishindia Bajaji kutoka jiji la Dar es Salaam, Goba.Katika droo ya 64 Petronila Sirinya ambaye alibashiri na moja kwa moja kuingia kwenye droo ya Shinda Zaidi na SportPesa na kujishindia Bajaji Re kutoka SportPesa.

Mshindi Huyo wa Droo ya 64 alisema alianza kushawishika kucheza na SportPesa baada ya kuona vile watu wengine wanashinda kwenye promosheni ya Shinda zaidi ndipo na yeye kuchukua uamuzi wa kuanza kucheza na timu ya kushinda kuutafuta ushindi wake.

"Nimeufurahia ushindi huu sijawahi kushinda kabisa tena mimi ni mama wa nyumbani sikufikiri kama ningeshinda lakini Mungu kanisaidia sasa ntaweza kumudu mahitaji yangu kutoka kukaaa nyumbani mpaka kumiliki bajaji yangu hizi ni baraka kubwa sana kutoka kwenu SportPesa" alisema Petronila.Aidha, Petronila alisema kipato atakachopata kupitia bajaj hiyo kitamsaidia kujiendeleza kielimu zaidi huku pesa nyingine ataziwekea mipango mizuri kumuwezesha mtoto kusoma shule nzuri.
"Najua hata mume wangu atakuwa ameshawishika sasa maana wakati nacheza alikuwa ananiambia shauri yako unapoteza pesa zako lakini baada ya kushinda yeye ndio ananisisitiza niendelee kucheza kweli ushindi una raha yake " alisema Bi. Sirinya.

Upande mwingine aliipongeza SportPesa kwa kutoa huduma bora kwa wateja wake sambamba na kuwajali kwa kuwatumia pesa za ushindi mara baada tu ya mechi kumalizia, huku akiweka wazi mikakati yake ya kuanza kusaka mtonyo wa Jackpot.Kutoka SportPesa, Meneja Uhusiano Bi. Sabrina H. Msuya alisema kampuni yetu inahuduma mbalimbali ambazo mteja akicheza anaweza kujishindia pesa ambazo anapata mara baada ya kuweka ubashiri wake na kupatia kiusahihi, Bajaji , Simu janja pamoja na Jezi orijino za Simba na Yanga

“Wikii hii Jackpot yetu imepanda mpaka shilingi 403,525,820/= ambapo mteja akibashiri kwa usahihi mechi kumi na tatu, na kuzawadiwa bonasi kwa watakao bashiri kwa usahihi kwa usahihi kuanzia mechi kumi hadi kumi na mbili.

Mojabet yatangaza kudhamini fainali za Bongo Star Search

$
0
0
KAMPUNI ya Mojabet inayojishughulisha na mchezo wa kubahatisha kupitia mmoja ya michezo yake ya Boompesa leo imetangaza kudhamini fainali za Bongo Star Search (BSS) ambazo zinatarajiwa kufanyika tarehe 22 Disemba mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wakutangaza kudhamini Bongo Star Search msimu wa 9, Mkurugenzi wa Masoko kutoka kampuni ya Mojabet Diana Chacha alisema kuwa wameona ni muhimu kushirikiana na Bongo Star Search ili kuendelea kuimbua vipaji vipya vya muziki hapa nchini na pia kufanya vijana zaidi waweze kujiajiri kupitia muziki.

Sisi lengo ni kuwafanya Watanzania wengi waweze kujiajiri kupitia zawadi za fedha taslimu ambazo huwa tunawapa washindi wetu. Kwa maana hiyo tumeona ni muhimu kutanua wingu wetu na kuelekeza kwenye muziki kwani huko pia kuna vipaji vyingi lakini kutokana na kutopata nafasi ya kuonekana, tunaamini kuwa ushirikiano wetu na BSS utaweza kutanua wingu na kufikia Watanzania wengi na hasa kupitia vijana kupitia Boompesa, alisema Chacha.

Chacha aliongeza kuwa Boompesa ni mchezo ambao unachezwa kwenye mitandao yote ya simu za mkononi kwa kununua tiketi , na mara mshindi anaposhinda anapewa fedha zake papo hapo kwenye simu yake , na mchezaji anaweza kununua tiketi kuanzia shilingi 100 na kuendelea.

Jaji Mkuu wa shindano ya Bongo Star Search (BSS) Rita Paulsen akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza zawadi na fainali za BSS msimu wa 9 ambapo mshindi atapata zawadi ya fedha taslimu TZS5M pamoja na mkataba wa mwaka mmoja kutoka kwa wadhamini wakuu ambao kampuni ya Mojabet inayojishughulisha na mchezo kupitia Boompesa. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko Mojabet Diacha Chacha.

SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka mikakati mizuri kuhakikisha wananchi hususani wachimbaji wadogo wadogo wananufaika na uwepo wa rasilimali hiyo.

Hivyo, Waziri Mkuu amewashauri wachimbaji wadogo wadogo wajiunge katika vikundi ili Serikali iweze kuwapatia misaada mbalimbali ikiwemo mkopo ili waongeze mitaji.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 29, 2018) alipozungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi jengo la halmashauri ya Mbogwe.Amewahamasisha wachimbaji hao watumie taasisi mbalimbali za kifedha na kukopa fedha na kununua mitambo ya uchimbaji na uchenjuaji kwa lengo la kujiongozea tija.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Geita kwa ziara ya kikazi, amesema wachimbaji wadogo wadogo waendelee kuwa na imani na Serikali yao, kwa kuwa imewapangia mambo mazuri.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kwamba Serikali imedhamilia kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

Amesema katika kumaliza tatizo la maji Serikali imetoa zaidi ya sh. bilioni moja kwa ajili ya uchimbaji visima virefu 11 na visima vifupi 43 katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati ya kumaliza tatizo la maji nchini kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa Hadhara kwenye Kiwanja cha Shule ya Msingi ya Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018.
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Mkutano wa Hadhara kwenye Kiwanja cha Shule ya Msingi ya Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018.
Wananchi wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipoingia kwenye Kiwanja cha Shule ya Misngi ya Masumbwe wilayani Mbogwe kuhutubia Mkutano wa Hadhara, Novemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

BILIONI 4 KULIPWA KILA SIKU KWA WAKULIMA WA KOROSHO-MHE HASUNGA

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara

Serikali imetangaza kuongeza kasi ya malipo ya wakulima wa Korosho ili kufikia kiasi cha shilingi Bilioni nne (4) kila siku kwani kufanya hivyo zoezi la malipo kukamilika haraka.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 29 Novemba 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho Mjini Mtwara ili kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa na serikali za ununuzi wa korosho za wakulima.

Amesema kuwa zoezi hilo litaenda sambamba na kuongezwa kwa wataalamu kwa ajili ya kuongeza nguvu ya malipo huku akisisitiza kuwa wataalamu wengine tayari wamekuwa na uzoefu wa namna ya kuhakiki na namna ya kulipa tangu kuanza kwa zoezi hilo.

Mhe Hasunga alisema kuwa mikoa inayolima korosho ni mingi nchini hivyo wakati tathmini sambamba na malipo zikiendelea timu ya wataalamu wengine itaundwa kwa ajili ya kuanza kufanya tathmini katika mkoa wa Pwani na mikoa mingine inayolima korosho nchini.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na waandishi wa habari tarehe 29 Novemba 2018 katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho Mjini Mtwara ili kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa na serikali za ununuzi wa korosho za wakulima. (Picha Zote Na Mathias Canl, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na waandishi wa habari tarehe 29 Novemba 2018 katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho Mjini Mtwara ili kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa na serikali za ununuzi wa korosho za wakulima.

SPIKA WA BARAZA LA SENETI LA BURUNDI AMTEMBELEA SPIKA NDUGAI

$
0
0
pic 1-min
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na Spika wa Baraza la Seneti la Burundi Mhe. Reverien Ndikuriyo (katikati) alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Burundi nchini Mhe. Prefere Ndayishimiye.
PIC 2-min
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimueleza jambo Spika wa Baraza la Seneti la Burundi Mhe. Reverien Ndikuriyo alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mahiga akutana na Viongozi kutoka Norway, Denmark, Venezuela na China

$
0
0
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga wa pili kutoka kushoto ukiwa katika mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam leo. Viongozi hao walijadili namna ya kukuza na kuimarisha ushirikiano hususan wa kibiashara ikiwemo mchakato wa kampuni ya Equinor wa kuzalisha gesi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kusafirisha nje ya nchi. 
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup wa pili kutoka kulia akisisitiza jambo. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga wa pili kutoka kushoto akiongea wakati wa mkutano wake na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup. Wengine katika picha kutoka kulia ni Katibu wa Mhe. Waziri, Bw. Magabilo Murobi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Jestas Nyamanga na Afisa Dawati, Bi. Tunsume Mwangolombe
Balozi Zhui Yuxiao, Mwakilishi kutoka China anayesimamia masuala ya Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga. Mwingine ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga katikati akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Yuri Pimentel Moura hayupo pichani. Wengine ni Katibu wa Mhe. Waziri, Bw. Magabilo Murobi na Afisa Dawati, Bi. Lillian Kimaro. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Yuri Pimentel Moura katikati akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga. Mhe. Naibu Waziri pamoja na mambo mengine ameleta ujumbe kuwa Venezuela inataka kufungua ofisi ya ubalozi nchini jambo ambalo Mhe. Mahiga amelikaribisha kwa mikono miwili na kueleza kuwa endapo Venezuela itafungua ubalozi itakuwa nchi ya nne kutoka Latin Amerika kuwa na ofisi ya Ubalozi Tanzania. 
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga wa pili kutoka kushoto ukiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu anayesimamia Maendeleo na Ushirikiano kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark, Bi. Trine Rask Thygesen. Katibu Mkuu alikuja kupata ufafanuzi kuhusu masuala ya haki za binadamu na kuihakikishia Tanzania kuwa haijasitisha msaada wake kwa Tanzania.
Katibu Mkuu anayesimamia Maendeleo na Ushirikiano kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark, Bi. Trine Rask Thygesen wa kwanza kulia akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahig.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU: TUTABORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WOTE WA UMMA

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuboresha maslahi ya watumishi wote wa umma wakiwemo wa kada ya afya kupitia Bodi ya Mishahara na Motisha baada ya kukamilisha uhakiki wa taarifa za kiutumishi.

Amesema kukamilika kwa uhakiki huo wa taarifa za kiutumishi kwa watumishi wa umma kutaiwezesha Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kupanga upya mishahara na motisha kwa watumishi.

Waziri Mkuu alitoa taarifa hiyo jana jioni (Alhamisi, Novemba 29, 2018) alipozungumza na watumishi wa Kituo cha Afya cha Ushirombo wilayani Bukombe baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi mradi wa uboreshaji miundombinu wa kituo hicho uliogharimu sh. milioni 500.

Alisema Serikali inaendelea kushughulikia maslahi ya watumishi, hivyo aliwataka waendelee kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote. “Tunataka mwananchi akifika kwenye maeneo ya kutolea huduma apokelewe, asikilizwe na ahudumiwe.”

Kadhalika, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe kwa kutekeleza kwa vitendo agizo la Serikali la kujenga Zahanati katika kila kijiji kwa kuwa wilaya hiyo imebakisha vijiji 2 kati ya 52 kumalizia ujenzi huo.

Waziri Mkuu alisema kwa sasa wananchi wa Ushirombo hawana sababu ya kusafiri umbali mrefu hadi Geita mjini au wilayani Kahama kwa ajili ya kufuata huduma za afya kwa kuwa huduma zote zitakuwa zikipatikana kituoni hapo.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   akiweka Jiwe la Msingi la Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Ushirombo wilayani Bukombe, Novemba 29, 2018. Kulia ni Mbunge wa Bukombe na Naibu waziri wa Madini, Doto Biteko na wapili kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. 
 Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akikagua ukarabati wa Kituo cha Afya cha ushirombo wilayani Bukombe, Novemba 29, 2018. 
 Wanakwaya wa Ushirombo wakiimba wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia Mkutano wa hadhara kwenye Stendi ya Ushirombo, Novemba 29, 2018.
Bibi Mageni Simon akiwa mwenye furaha baada  ya kujifungua katika mazigira safi na salama ya  hospitali ya wilaya ya Geita ya Nzera iliyokaguliwa na kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Novemba 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Beki wa Ivory Coast afanyiwa vipimo vya afya ya moyo tayari kusajiliwa timu ya simba

$
0
0
Fundi Sanifu wa Moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Saada Salum akimwekea kifaa cha kupima kiwango cha afya ya moyo ili kuhimili mchezo awapo uwanjani beki wa Ivory Coast Coulibaly Zana Oumar kabla ya kusajiriwa na klabu ya Simba jana katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George Longopa akiangalia mapigo ya moyo na umeme wa moyo unavyofanya kazi katika mashine ya Trade Mill alipokua akimpima beki wa Ivory Coast Coulibaly Zana Oumar vipimo vya afya ya moyo kabla ya kusajiriwa na klabu ya Simba jana katika Taasisi hiyo.
Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George Longopa akimfanyia beki wa Ivory Coast Coulibaly Zana Oumar kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO Cardiogram) alipowasili katika taasisi hiyo kufanyiwa vipimo vya afya ya moyo kabla ya kusajiriwa na klabu ya Simba jana Jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George Longopa katika picha ya pamoja na beki wa Ivory Coast Coulibaly Zana Oumar baada ya kuwasili katika taasisi hiyo akiwa na daktari wa timu ya Simba Yassin Gembe kufanyiwa vipimo vya afya ya moyo kabla ya kusajiliwa na klabu hiyo kupitia dirisha dogo jana Jijini Dar es Salaam. Picha na: Genofeva Matemu - JKCI.

Serikali ya Misri yawasilisha andiko la kwanza la nia ya kuwekeza nchini

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Misri hapa nchini Bibi. Nevine El-Saeed pamoja na kupokea andiko la awali la nia ya serikali ya Misri kutaka kuwekeza nchini katika sekta ya mifugo.

Kaimu Balozi wa Misri ambaye ameambatana na Mkuu wa Idara ya Uchumi katika ubalozi huo Bw. Mohamed Ibrahim katika ofisi ndogo za wizara ya mifugo na uvuvi zilizopo jijini Dar es Salaam, amesema serikali ya nchi hiyo inahitaji kuwekeza ili kufungua fursa mbalimbali ambazo zitapatikana kupitia uwekezaji huo.

Akizungumza na maafisa hao pamoja na wajumbe waliohudhuria kikao hicho, Katibu Mkuu Ole Gabriel amesema nchi ya Tanzania ina mifugo mingi na kwamba ikitumika vizuri kupitia uwekezaji, ambapo nia ya serikali ya awamu ya tano imejikita zaidi kupitia kufufua na kuanzishwa kwa viwanda vipya kutaongeza fursa nyingi zaidi zikiwemo za ajira.

Aidha, amesema nia yake ni kuhakikisha anasimamia nia ya serikali ya Misri kufanikisha uwekezaji huo ambao anasema wizara yake itahakikisha inaweka mazingira yatakayofanya uwekezaji huo uwe endelevu na kuleta tija kwa nchi zote mbili.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na wakuu wa idara zilizo chini ya ofisi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wawakilishi kutoka Dawati la Sekta Binafsi, Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Kituo cha Kuendeleza kilimo Nyanda za juu Kusini (SAGCOT) na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa maelezo kwa Kaimu Balozi wa Misri nchini Bibi. Nevine El-Saeed na Mkuu wa Idara ya Uchumi katika ubalozi huo Bw. Mohamed Ibrahim katika ofisi ndogo za wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel  Kaimu Balozi wa Misri nchini Bibi. Nevine El-Saeed na Mkuu wa Idara ya Uchumi katika ubalozi huo Bw. Mohamed Ibrahim, wakati akiongoza kikao cha namna bora ya uwekezaji wa serikali ya Misri katika sekta ya mifugo nchini (wajumbe wa mkutano huo hawapo pichani).
 Wajumbe wa kikao kuhusu nia ya serikali ya Misri kuwekeza katika sekta ya mifugo nchini wakifuatilia mazungumzo ya kikao hicho. Wajumbe hao wanatoka idara zilizo chini ya Wizara ya Mifyugo na Uvuvi, Dawati la Sekta Binafsi, Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT) na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea andiko la awali la nia ya serikali ya Misri kuwekeza nchini katika sekta ya mifugo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Uchumi katika ubalozi wa Misri hapa nchini Bw. Mohamed Ibrahim.

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATENGA MAMILIONI KUWEZESHA UFUGAJI NYUKI KISASA

$
0
0
Na Lusungu Helela-Geita
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) imetenga kiasi cha Sh700milioni kwa ajili ya kuwawezesha wananchi  kufuga  nyuki kwa njia ya kisasa kwa mikoa nane. Kauli hiyo imetolewa Mbogwe katika mkoa wa Geita na Naibu Waziri wa Maliasili na Utaii, Mhe,Constanine Kanyasu  wakati  akizungumza na wananchi  kwenye mkutano wa hadhara mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.

 Ametaja baadhi ya   wilaya katika mkoa wa Geita zitakazonufaika na mradi huo kuwa ni wilaya ya Ushirombo pamoja na Mbogwe. Kufuatia hali hiyo, Mhe. Kanyasu  amezitaka wilaya hizo kujiepusha na ukataji miti ovyo kwa  vile nyuki ni rafiki wa mazingira  badala yake zijikite zaidi  katika kupanda miti.

Akizungumzia kuhusu fungu hilo, Mhe, Kanyasu amewataka wakazi wa wilaya hizo wajiunge  katika vikundi  ikiwa ni moja ya vigezo vitakavyozingatiwa katika utoaji wa pesa hizo  kwa ajili ya ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa. Aidha,Naibu Waziri huyo amesema  wafugaji hao wataokakuwa wamejiunga katika vikundi hivyo watapatiwa elimu ya ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa pamoja na kuwezeshwa pesa zitakazotumika kwa ajili ya kununulia  mizinga ya kisasa itakayosaidia kuzalisha mazao ya nyuki yatakayokidhi soko la kimataifa,

Ameongeza kuwa baadhi ya pesa hizo zitatumika katika kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyowasaidia wafugaji hao  kuchakata na kufungasha mazao ya asali yenye viwango bora duniani. Katika hatua nyingine, Mhe. Kanyasu amewahakikishia wananchi hao kuwa tayari Wizara imepata soko la uhakika la  asali watakayoizalisha.

Ameongeza kuwa licha ya nchi ya  Tanzania kusifika katika uzalishaji  wa asali kwa wingi,,Wafugaji walio wengi wamekuwa wakifuga nyuki kimazoea Kufuatia hali hiyo amesema Wizara imedhamiria kuleta mapinduzi katika uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa kuwawezesha wananchi kufuga kisasa hali itakayosaidia wananchi kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kuhifadhi misitu.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utaii, Mhe,Constanine Kanyasu  wakati  akizungumza na wananchi  kwenye mkutano wa hadhara mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.kuhusu mkakati wa Wizara wa kuhakikisha wananchi wanapatiwa mafunzo pamoja na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kufuga nyuki kwa njia ya kisasa kwenye mkutano uliofanyika  Mbogwe katika mkoa wa Geita. (Picha na Lusungu Helela-MNRT)
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa uliofanyika  Mbogwe katika mkoa wa Geita wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utaii, Mhe,Constanine Kanyasu  wakati  akizungumza kuhusu Sh 700 milioni zitakavyowanufaisha katika ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa. (Picha na Lusungu Helela-MNRT

WAZIRI MKUU AAGIZA ALIYEKUWA MHASIBU MBOGWE ASIMAMISHWE KAZI

$
0
0
*Ni kutokana na tuhuma za kuhusika na ubadhilifu wa sh. milioni 19 za CHF

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amsimamishe kazi aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Mbogwe, Adam Nyoni kwa tuhuma za ubadhilifu wa sh. milioni 19.4 za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF). Kadhalika Waziri Mkuu ameagiza Mhasibu huyo ambaye awali alikuwa wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe na sasa amehamishiwa halmashauri ya wilaya ya Nyag’hwale arudishwe Mbogwe na asimamishwe kazi huku shauri lake likifikishwa katika vyombo vya sheria.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Alhamisi, Novemba 29, 2018) alipozungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Masumbwe wilayani Mbogwe akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Geita. Waziri Mkuu aliwataka watumishi wote wa umma wawajibike katika kufanya kazi kwa bidii na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano haitowavumilia watumishi ambao ni wezi, wabadhilifu, wavivu  na haitosita kuwachukulia hatua.

“Serikali hii haitamuhamisha wala kumuundia tume mtumishi atakayetafuna fedha za umma, ukiharibu tunamalizana hapo hapo. Naagiza mtumishi huyo aliyehamishiwa Nyang’hwale arudishwe hapa kwa kuwa kabla ya kuhamishwa kulikuwa na upotevu wa sh. milioni 19.4.” Alisema watumishi wa umma wanapaswa wawatumikie wananchi bila ya ubaguzi wowote pamoja na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. “Lazima mtambue kwamba msimamo wa Serikali ni kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi wa kidini, kiitikadi na kipato.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi kwenda katika ngoma za usiku za chagulaga na kuwachukulia hatua wanaume wote wanaowachagua wanafunzi wa kike kwa kuwa wanawaharibia maisha. Alisema lazima wananchi washirikiane na Serikali katika kuwalinda wanafunzi wa kike ili wasipate ujauzito na kukatisha masomo yao kwa sababu kitendo cha kupata ujauzito kinawafanya wakatishe masomo yao jambo ambalo linakwamisha kufikia lengo lao kielimu.

Kadhalika, Waziri Mkuu alipiga marufuku kwa wanafunzi hao wa kike kuhudhuria kwenye ngoma hiyo ya usiku na badala yake watumie muda mwingi kujishughulisha na masuala ya masomo ili waweze kutimiza ndoto zao. “Wanafunzi wa kike msikubali kushawishika." Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi wa wilayani Mbogwe kuhakikisha watoto wenye umri wa kuanzia miaka minne kuwapeleka shule ili waanze darasa la awali na kwamba hawatakiwi kutoa mchango kwa kuwa Elimumsingi inatolewa bure nchini.

Hata hivyo, Waziri Mkuu aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwekwa kutekeleza kwa vitendo agizo la Serikali la kujenga Zahanati katika kila kijiji kwa kuwa wilaya hiyo inaendelea na shughuli za ujenzi wa Zahanati katika vijiji 82 kati ya vijiji 86.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images