Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

DK. MABODI AFANYA ZIARA KTK MANISPAA YA MAGHARIB 'A' UNGUJA.

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi', amesema CCM inasimamia Sera zake ipasavyo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii na kiuchumi.

Kauli hiyo ameitoa leo katika mwendelezo wa ziara yake kwa siku ya tatu ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM Katika Baraza la Manispaa ya Magharibi 'A' Zanzibar.

Amesema CCM inaamini kwamba suala la maendeleo kwa jamii halina itikadi za kisiasa bali linatakiwa kutekelezwa kwa wananchi wote bila ya ubaguzi, hatua ambayo imefikiwa kwa kiasi kikubwa na mfumo wa ugatuzi wa madaraka katika Serikali za Mitaa.

Ameeleza kwamba fikra na dhana ya zanzibar kuwa 'Singapore' ya Bara la Afrika inaendelea kutekelezwa kwa vitendo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na CCM kupitia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Amesema sifa kuu ya viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi ni uadilifu, hekima, busara, ukweli, utu na uongozi bora katika kutatua kero za wananchi.Kupitia ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu huyo, Dk. Mabodi amewaonya baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani nchini kuacha tabia ya kupotosha umma kwa makusudi juu ya hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa na Serikali katika Sekta ya Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia na kueleza kuwa Sera hiyo ipo katika Ilani ya CCM na inaendelea kutekelezwa kwa kufuata matakwa ya kisheria.

" Kuna baadhi ya watu wanaojiita wanasiasa hapa Zanzibar wao kazi yao kubwa ni kuisubiri Serikali itekeleze jambo lolote la maendeleo, na wao waibuke na kukosoa na kubeza bila ya hoja za msingi ili waweze kupata siku za kuishi kisiasa.
NAIBU katibu Mkuu CCM zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla pamoja na Mkuu wa Mkoa Mjini MAGHARIB Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud wakikagua machine ya wajasiriamali wa kuuza dagaa huko Kihinani Wilaya ya Magharibi 'A' Unguja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

RC MTAKA ATOA WITO KWA WALIMU KUEPUKA VITENDO VINAVYOHARIBU HAIBA NA HESHIMA YA UALIMU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa walimu kuendelea kuwa walezi wa wanafunzi wao na kuepuka vitendo vyovyote vinavyoharibu haiba na heshima ya ualimu, ili waweze kukabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili kwao na wanafunzi wanaowafundisha.

Mtaka ameyasema hayo Novemba 28, 2018 katika mahafali ya 26 ya kidato cha nne shule ya sekondari Mwembeni (ambayo alisoma kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne mwaka 1997-mwaka 2000),  iliyopo Mjini Musoma ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Amesema katika baadhi ya maeneo baadhi ya walimu wamekuwa wakifanya mambo ambayo yanaharibu heshima na haiba ya ualimu jambo ambalo linapelekea wazazi kutowaamini walimu na kuogopa kuwapeleka watoto wao katika shule hizo.

" Naishukuru sana bodi ya shule na walimu wa Mwembeni kwa kuendelea kuhakikisha walimu wetu wanalinda heshima na haiba ya ualimu na wazazi wameendelea kuiamini shule kwa kuleta watoto wao, kwa sababu hakuna matukio yanayohatarisha uwepo wa watoto wao shuleni na masuala la elimu, maadili na nidhamu kwenye shule hii kama Taasisi yameendelea kuimarishwa" alisema.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Mwembeni Mjini Musoma, ambako alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akisalimiana na Mwl.Anselm Mnibhi wa Shule ya Sekondari Mwembeni ambaye pia alimfundisha yeye akiwa mwanafunzi wa shule hiyo mwaka 1997-2000, wakati wa mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo,  iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo alikuwa mgeni rasmi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye kipaza sauti) akiwa na wenzake aliosoma nao katika shule ya sekondari Mwembeni mwaka 1997- mwaka 2000 na baadhi ya walimu waliwafundisha, katika  mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne wa  shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo alikuwa mgeni rasmi.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwembeni mjini Musoma wakitoa burudani ya ngoma ya asili ya kabila la Wakurya, katika  mahafali ya 26 ya ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  alikuwa mgeni rasmi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wenzake aliosoma nao katika shule ya sekondari Mwembeni mwaka 1997- mwaka 2000 na baadhi ya walimu waliowafundisha, katika  mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo alikuwa mgeni rasmi.


 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAFANYAKAZI TISA TPA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MALI,UTAKATISHAJI FEDHA

$
0
0
Na Karama Kenyunko,Blogu ya jamii 

WAFANYAKAZI tisa wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) leo Novemba 
29, 2018 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mahakimu watatu tofauti kujibu tuhuma za wizi wa mali isafirishwayo na utakatishaji wa jumla wa zaidi ya sh. milioni 277.

Washtakiwa waliofikishwa Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile wametajwa kuwa ni Naushad Mohamed, Alfred Mhina, ,Joseph Mrema, Justine Mosha, Anuary Shampoo Pius Nyeregeti,ambapo imedaiwa na mwendesha mashtaka mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi kuwa, kati ya Agosti 30 na Sepemba 9 mwaka huu, washtakiwa walikula njama ya kuiba Mali iliyokuwa ikisafirishwa.

Imedaiwa katika shtaka la pili kuwa, Septemba 8 mwaka 2018 katika eneo la Geti namba tano la TPA lililopo wilayani Temeke, mshtakiwa Nyeregeti, alijitambulisha kama Nassoro Mohamed kwa Gaspa Swai ambaye ni Ofisa wa TRA huku akijua kuwa si kweli.

Katika shtaka la tatu, watuhumiwa hao waliiba kontena lenye nguo zenye thamani ya sh. 177,608,761 mali ya Nkonde Bright ambayo iliyokuwa ikisafirishwa kutoka Dar es Salaam kwenda Lusaka Zambia.Aidha washtakiwa hao wanadaiwa kujihusisha katika muamala uliohusiana na wizi wa nguo hizo huku wakijua mali hiyo ni zao la kosa la utangulizi la mali isafirishwayo.

Mbele ya Hakimu, Maira Kasonde imedaiwa na Wakili wa Serikali Eric Shija kuwa Septemba 18, 2018 washtakiwa Anuary Shapoo, Pius Nyeregeti, Athanas Nsenye, Yusuph Mkuja, na Ismail Hajji walikula njama ya kuiba mali iliyokuwa ikisafirishwa.Katika shtaka la pili imedaiwa washtakiwa waliiba contena lililokuwa na magunia 520 ya mahindi yenye thamani ya sh. 31,698,411 Mali ya Brian Mwacha ambayo ilikuwa ikisafirishwa kutoka Dar kwenda Zambia.

Pia washtakiwa hao wanadaiwa kubadilisha magunia hayo na na fedha kwa kuyauza huku wakijua kuwa kosa hilo ni zao la kosa la utangulizi la wizi wa mali isafirishwayo kwa dhumuni la kupotezea uhalisia wa mali.
WAFANYAKAZI tisa wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) leo Novemba 
29, 2018 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mahakimu watatu tofauti kujibu tuhuma za wizi wa mali isafirishwayo na utakatishaji wa jumla wa zaidi ya sh. milioni 277.

Miaka Mitatu ya Rais John Magufuli-Bei ya Dawa yapungua kwa asilimia 40

Miaka Mitatu ya Rais John Magufuli-Hali ya Upatikanaji wa dawa yaimarika na kufikia asilimia 92

SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka mikakati mizuri kuhakikisha wananchi hususani wachimbaji wadogo wadogo wananufaika na uwepo wa rasilimali hiyo.

Hivyo, Waziri Mkuu amewashauri wachimbaji wadogo wadogo wajiunge katika vikundi ili Serikali iweze kuwapatia misaada mbalimbali ikiwemo mkopo ili waongeze mitaji. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 29, 2018) alipozungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi jengo la halmashauri ya Mbogwe. 

Amewahamasisha wachimbaji hao watumie taasisi mbalimbali za kifedha na kukopa fedha na kununua mitambo ya uchimbaji na uchenjuaji kwa lengo la kujiongozea tija. Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Geita kwa ziara ya kikazi, amesema wachimbaji wadogo wadogo waendelee kuwa na imani na Serikali yao, kwa kuwa imewapangia mambo mazuri.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kwamba Serikali imedhamilia kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama. Amesema katika kumaliza tatizo la maji Serikali imetoa zaidi ya sh. bilioni moja kwa ajili ya  uchimbaji visima virefu 11 na visima vifupi 43 katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati ya kumaliza tatizo la maji nchini kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani. Waziri Mkuu amesema kampeni hiyo inalenga kuhakikisha wananchi katika maeneo yote wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilembela wilayani Mbogwe akiwa katika ziara ya mkoa wa Geita, Novemba 29, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua jengo la Maabara ya Kituo cha Afya cha Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wazazi waliolazwa kwenye Kituo cha Afya cha Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bibi Frola Samwel aliyelazwa katika Kituo cha Afya  cha Masumbwe wilayani Mbogwe akimuuguza mwanae  Mathias Paschal wakati alipofungua jengo la Maabara ya Kituo hicho, Novemba 19, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bibi Flora Samwel aliyelazwa katika Kituo cha Afya  cha Masumbwe wilayani Mbogwe akimuuguza mwanae  Mathias Paschal wakati alipofungua jengo la Maabara ya Kituo hicho, Novemba 19, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAJAMBAZI SITA SUGU WAUAWA DAR KWA KUPIGWA RISASI

$
0
0
*Wakutwa na mabomu ya kutupa kwa mkono, risasi 217,wamo Waburundi 
*Mambosasa ataja matukio ya kutisha yaliyofanywa na majambazi hayo

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limesema leo Novemba 29 mwaka huu maeneo ya Ubungo UFI jijini Dar es Salaam kupitia kikosi kazi maalum cha kupambana na ujambazi kimefanikiwa kuwaua majambazi sita.

Mbali na kuua majambazi hayo wamekamata silaha moja aina ya AK 47, risasi 11, kitambulisho chenye namba OP 0216239 kwa jina la Theophili Manirakiza mkazi wa Rukana Rugombo nchini Burundi na kitambulisho cha kazi kinachotumiwa na kikundi cha CNDD-FDD chenye jina hilo la Theopili Manirakiza katika majibizano ya risasi.

Kamanda Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewaambia waandishi wa habari kuwa majambazi hao wameuawa baada ya mtego uliowekwa na askari kutokana na taarifa za watuhumiwa watatu waliokuwa wamekamatwa.

Amewataja watuhumiwa hao ni Willy Irakozes maarufu kwa jina la mandoo ambaye ni wa Burundi, Jean Mugisha raia wa Burudi na Mtanzania Omary Nassoro ambaye ni Mtanzania na kwamba walikuwa na bunduki tatu aina ya AK47 na magazine 8, risasi 217 na mabomu ya kutupa kwa mkono 8.
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kuwaua watu sita wanaosadikika kuwa Majambazi katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo huku miongoni mwa wahalifu hao akitambulika kuwa ni raia wa kutoka nchini Burundi akiwa na kitambulisho cha Chama cha CNDD-FDD.Pichani ni kamanda wa polisi wa kanda hiyo SACP LAZARO MAMBOSASA akizungumza na wanahabari.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI WA UNESCO KANDA YA AFRIKA PAMOJA NA MWAKILISHI WA TANZANIA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika Bi. Ann Therese NDONG-JATTA pamoja na Mwakilishi Mpya wa UNESCO nchini Tanzania Bw. Tirsa A.S Dos Santos ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika Bi. Ann Therese NDONG-JATTA (kushoto) na Mwakilishi Mpya wa UNESCO nchini Tanzania Bw. Tirsa A.S Dos Santos (kulia) ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA BALOZI WA ITALIA NA BALOZI WA FALME ZA KIARABU NCHINI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kumkaribisha  Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WAZIRI LUGOLA AWATAKA MAJAMBAZI WAJISALIMISHE PAMOJA NA SILAHA ZAO, POLISI HAWATALALA MPAKA JAMBAZI WA MWISHO AMETIWA MBARONI

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Mara.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka majambazi popote walipo nchini kujisalimisha pamoja na silaha zao wakati Polisi wakiendelea na msako mkali mpaka jambazi wa mwisho anatiwa mbaroni. Lugola amesema Jeshi la Polisi lipo imara na litawasaka majambazi hao usiku na mchana popote walipo na litahakikisha nchi inaendelea kuwa salama na wananchi wema wakiendelea kufanya shughuli zao za maendeleo kwa kulijenga Taifa.  

Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kasahunga, Kata ya Neluma, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, leo, Lugola amesema usalama wa nchi hauchezewi na mtu yeyote na watu wasijaribu kutikisa kiberiti kwa kulichezea Jeshi la Polisi. Lugola amesititiza kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano ambayo inaongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ujambazi hauna nafasi na pia amewataka majambazi hao wafanye kazi nyingine ya kuwaingizia kipato kwa njia halali.

“Msijaribu kukitikisa kiberiti, Serikali ipo macho muda wote, Jeshi lenu lipo imara, majambazi wanaofanya uvamizi, tutahakikisha tunawasaka popote walipo jambazi mmoja baada ya mwingine, hatutalala wala kupumzika hadi jeshi letu litakapomtia mbaroni jambazi wa mwisho,” alisema Lugola. 
Kutokana na msako huo, Lugola alisema majambazi hao wajisalimishe wenyewe pamoja na dhana zao kwenye kituo cha polisi wanachoona kipo jirani na wao, vinginevyo hawatasalimika na hawatabaki salama.

“Kama kuna ndugu zetu, watoto wetu, majirani zetu tuwaambie serikali hii ya magufuli nafasi hiyo ya kufanya ujambazi haipo, nimepata taarifa za uhalifu, wizi wa mifugo na uvamizi wa aina mbalimbali, tuone taarifa polisi ili tuweze kuwatia mbaroni majambazi hao kwa wale wote ambao mnahisi wanajihusisha na uhalifu, toeni ushirikiano bila woga ili meneo yetu yazidi kuwa na amani,” alisema Lugola. 

Hata hivyo, Lugola alisema ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake ambavyo anavisimamia wapo baadhi ya askari wachache ambao wanajihusiha na vitendo vya rushwa na alishatoa onyo mara nyingi, hivyo atakao wakamata hatawaonea huruma. “Kuna baadhi ya mazingira ambayo yanachangia rushwa zaidi ndani ya Jeshi la Polisi ikiwemo kutokutolewa kwa dhamana katika siku za mapumziko Jumamosi na Jumapili, baada ya kuona kunamianya ya rushwa nikatangaza nchi nzima vituo vyote vya polisi vitoe dhamana saa 24 na siku 365 na robo, pia kutowekwa mahabusu watuhumiwa ambao wanamakosa madogo madogo,” alisema Lugola.

Lugola anaendelea na ziara jimboni kwake ya kuhamasisha wananchi kuanza maandalizi ya kilimo pamoja na kuendeleza miradi ya maendeleo huku wakiendelea kuheshimu sheria za nchi.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Kasahunga, Kata ya Neluma, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo. Lugola aliwataka wananchi wa Mwibara washirikiane na polisi kuwafichua majambazi, na pia aliwataka majambazi wajisalimishe pamoja na silaha zao katika kituo chochote cha polisi nchini, kwa kuwa polisi usiku na mchana wanawasaka na watahakikisha wanamtia mbaroni jambazi wa mwisho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akiwapelekea zawadi kikundi cha kwaya ya Kijiji cha Kasahunga, Kata ya Neluma, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, wakati waimbaji hjao walipokua wanampokea kwa kijijini hapo. Lugola katika hotuba yake kwa wananchi zaidi ya 100 waliohudhuria mkutano huo, aliwataka wananchi wa Mwibara washirikiane na polisi kuwafichua majambazi, na pia aliwataka majambazi wajisalimishe pamoja na silaha zao katika kituo chochote cha polisi nchini, kwa kuwa polisi usiku na mchana wanawasaka na watahakikisha wanamtia mbaroni jambazi wa mwisho.

MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB AKUTANA NA NAIBU WAZIRI SHONZA, ATEMBELEA NHC

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati akizungumzia mikakati mbalimbali ya kibenki pamoja na ushirikiano wa kibiashara kati ya Benki hiyo na Serikali, kikao kilichofanyika kwenye makao makuu ya Benki ya CRDB, Azikiwe jijini Dar es salaam hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akisaini kitabu cha wageni wakati alipomtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, ofisini kwake, Azikiwe jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani alipomtemebela ofisini kwake, jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia), akifurahi jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani (katikati) wakati kikao chao kilichofanyika leo, jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dorah Ngaliga (kulia), Mkurugenzi wa Utawala wa Benki hiyo, Beatus Segeja (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Muendelezaji Biashara wa NHC, William Genya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza jambo katika kikao kilichokutanisha uongozi wa Benki hiyo na Shirika la Nyumba nchini (NHC), kilichofanyika kwenye makao makuu ya NHC, jijini Dar es salaam leo. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani pamoja na Manaibu Wakurugenzi Wakuu wa Benki ya CRDB, Dorah Ngaliga (kulia) na Esther Kitoka.

NDITIYE: TAKUKURU FUTUATILIENI UJENZI WA GATI YA BANDARI YA LINDI

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameilekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufuatilia na kuchunguza thamani ya fedha zilizotumika kujenga gati ya bandari ya Lindi ili kuweza kubaini kama gharama iliyotumika inaendana na ujenzi uliofanyika
Hayo yameelezwa na Nditiye wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi mkoani humo ambapo amebaini kuwa kasi ya utendaji kazi kwenye gati hilo hairidhishi na kuongeza kuwa kazi ni ya mwaka mmoja ila imechukua miaka mitatu hadi sasa na bado haijakamilika. “Naielekeza TAKUKURU waje wafuatilie thamani ya fedha zilizotumika kujenga gati hili,” amesema Nditiye. 
Nditiye amesema kuwa kwa bahati mbaya miradi ya maendeleo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) inayotekelezwa nje ya bandari ya Dar es Salaam haitekelezwi ipasavyo, tufike mahala tuheshimu fedha za Serikali na za wananchi. “Kwa bahati mbaya TPA hamfiki eneo la mradi wakati wa kuandaa nyaraka na hata ujenzi wa miradi husika inavyoendelea hivyo tunaingia hasara,”amesema Nditiye
Mhandisi Ujenzi wa Bandari ya Mtwara Twaha Msita wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa gati hiyo kwa Nditiye amesema kuwa Kampuni ya Comfix & Engineering Ltd ilipewa kazi na TPA ya kujenga gati hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Mei mwaka 2015 na kutakiwa kukamilika mwezi Mei mwaka 2016 kuendana na mkataba husika kwa gharama ya shilingi bilioni 3.1 ambapo baada ya muda ilionekana kazi zimeongeza na hivyo kuongezewa fedha hadi kufikia shilingi bilioni 3.5 
Nditiye amesema kuwa tayari mkandarasi amelipwa shilingi bilioni 2.448 na kazi hiyo ilisimama kwa kipindi cha mwaka mzima mwaka 2017 na kuanza tena ambapo hadi sasa haijakamilika na imechukua kipindi cha miaka mitatu tofauti na mkataba wa awali ambapo ilitakiwa ijengwe kwa kipindi cha mwaka mmoja. “Serikali hatuwezi kuvumilia jambo hili kwa kuwa tunawatesa wananchi kwa kukosa huduma na kutumia vibaya fedha za Serikali,” amesema Nditiye
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Ujenzi wa Bandari ya Mtwara, Twaha Msita (hayupo pichani) kuhusu kutoridhishwa na ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi wakati wa ziara yake ya kukagua bandari hiyo mkoani humo. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyevaa fulana ya bluu) akikagua ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi unaosuasua  wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi huo mkoani Lindi. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa gati ya bandari ya Nyamisati wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi huo Kibiti, Lindi. Meneja Mradi wa TPA Mhandisi Erick Madinda akitoa maelezo

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Miaka Mitatu ya Rais John Magufuli-MSD yachaguliwa kuwa mnunuzi mkuu wa dawa ukanda wa SADC

MEJA JENERALI JACOB AZITAKA IDARA YA HUDUMA ZA UANGALIZI, JESHI LA POLISI NA MAGEREZA KUSHIRIKIANA ILI KUONDOA MSONGAMANO WA WAFUNGWA MAGEREZANI

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Morogoro
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu, amewataka watendaji wa Idara ya Huduma za Uangalizi , Jeshi la Polisi na  Magereza kushirikiana kwa pamoja ili kupunguza msongamano wa wafungwa Magerezani. Meja Jenerali Kingu ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Maafisa Wafawithi wa Mikoa waliokutana katika Ukumbi wa Magadu Officers Mess mjini Morogoro, kwa lengo la kutathmini utendaji kazi wao zikiwemo mafanikio pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.

Meja Jenerali Kingu amesema kuwa, Idara ya Huduma za Uangalizi zamani ilikuwa ikiitwa Huduma kwa jamii ambayo ndio inayohusika na utoaji wa adhabu mbadala wa vifungo Magerezani, imeanzishwa ili kuhakikisha kuwa wafungwa wenye makosa madogo yasiyo hatarishi kwa jamii na taifa, wanatumikia adhabu zao kwenye jamii nje ya magereza. “ Kwa  kufanya hivyo kungesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano  Magerezani hivyo kuipunguzia  Serikali  gharama za kuwahifadhi  wafungwa  Magerezani”. Amesema Meja Jenerali Jacob Kingu.

Meja Jenerali Kingu amewataka watendaji hao wa Idara ya Huduma za Uangalizi kubainisha changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao ili ziweze kutatuliwa kwa haraka, jambo litakalosaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi hivyo kupunguza msongamano wa wafungwa Magerezani. Akizungumzia suala la nidhamu kazini, Katibu Mkuu huyo amesema hatosita kumchukulia hatua mtumishi yeyote yule atakayebainika  kwenda kinyume  na maadili ya utumishi wa Umma na sheria za nchi.

Katibu Mkuu huyo amemuagiza Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ungalizi Aloyce Musika kupeleka watendaji katika mikoa mitatu  Lindi, Katavi na Ruvuma ili wakazi wa mikoa hiyo waweze pia kupata huduma zinazotolewa na Idara hiyo, kwani kwa sasa Idara hiyo ina watendaji wawakilishi katika Mikoa 23 hapa Tanzania.
 Mwisho. 
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu  wa kwanza kushoto akitoa maelekezo kwa baadhi ya Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati wa Mkutano wa Maafisa Wafawithi wa Mikoa kilichofanyika Magadu Officers Mess Mjini Morogoro leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu  aliyevaa suti nyeusi akifurahia jambo na baadhi ya Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati wa Mkutano wa Maafisa Wafawithi wa Mikoa kilichofanyika Magadu Officers Mess Mjini Morogoro leo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu wa tatu kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mkutano wa Maafisa Wafawithi wa Mikoa kilichofanyika Magadu Officers Mess Mjini Morogoro wa pili kutoka kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ungalizi Bw. Aloyce Musika.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Chuo cha ustawi wa jamii wawajengea uwezo wa wanafunzi kuelekea mapinduzi ya viwanda

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Eventius Mugyabuso amesema kwa kuelekea mapinduzi ya Viwanda ni fursa ya wasomi kuchangamkia katika fursa ya ajira. Mugyabuso ameyasema hayo leo wakati wa warsha ya kujadili nafasi ya Viwanda kwa wasomi katika kuleta matokeo ya chanya ikiwemo na wao kuwa sehemu ya watu wenye viwanda hivyo.

Amesema kuwa Chuo cha Ustawi wa Jamii kina nafasi kubwa katika kuelekea Sekta ya viwanda kutokana na elimu wanayoitoa. Nae Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu Elia Kasile amesema kuwa maarifa  wanayopata katika Chuo cha Ustawi ni nafasi tosha katika kuingia katika Sekta ya viwanda. Amesema kuwa wahitimu na wanafunzi wanatakiwa kujiamini katika kitu wanachokifanya. Kasile amesema hakuna kitu kichoweza kushindikana.
 Mhadhiri msaidizi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Prisca Kimario  akizungumza  kuhusiana nafasi ya Viwanda kwa wanataaluma wakati wa warsha ya kujadili sekta ya viwanda kwa wanafunzi na wahitimu wa chuo cha ustawi wa jamii iliyofanyika katika ukumbi wa maktaba wa chuo hicho ,jijini Dar es Salaam leo.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu (THTU) Elia Kasile akitoa mada kwa wanafunzi na wahitimu wa chuo cha ustawi wa jamii kuhusiana na taaluma wanayoipata kwenda kuchagiza katika sekta ya viwanda wakati warsha ya wahitimu na wafunzi wa chuo hicho uliofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam
 Kaimu Makamu wa Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa  Jamii, Eventius  Mugyabuso akizungumza wakati akifungua warsha kwa wanafunzi na wahitimu wa Chuo cha Ustawi wa  jamii  kuhusiana na  elimu wanayipata kuitumia katika sekta ya viwanda iliyofanyika chuuoni hapo leo.
Wanaotarajia kuhitimu Chuo cha Ustawi wa Jamii na wanafunzi wakiwa katika warsha ya kujadili nafasi ya Sekta ya Viwanda kwa wasomi.

BENKI YA NMB YATOA MAFUNZO KWA MAWAKALA WAKE SHINYANGA

$
0
0
Benki ya NMB imeendesha mafunzo kwa Mawakala NMB mkoa wa Shinyanga kwa ajili kuwajengea uwezo wa kiutendaji wafahamu mbinu za kudhibiti fedha haramu pamoja na mbinu za kukuza biashara zao kwa kuongeza wateja.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Alhamis Novemba 29,2018 katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga ambapo mgeni alikuwa Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,Melusori alisema mafunzo hayo yana lengo la kuwawezesha mawakala kukuza kipato chao lakini pia namna ya kudhibiti fedha chafu/haramu ‘Money laundering’.

“Lengo jingine ni kuwasilisha na kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili mawakala hawa,kuwapongeza/kutambua mchango wa mawakala wanaofanya kazi vizuri na kuwaeleza kuhusu maboresho yanayofanywa na NMB”,alisema Melusori.

Hata hivyo aliwataka mawakala wa NMB kufanya kazi kwa umakini na kuzingatia maadili katika utendaji kazi wao na kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria halali za fedha.“Asilimia ya watanzania wanaotumia benki ipo chini ya asilimia 20 kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni hivyo shirikiane na benki kuhakikisha kuwa watanzania ambao hawajaanza kutumia huduma ya benki kwani benki ni sehemu salama zaidi”,aliongeza.
Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Mawakala wa Benki ya NMB mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Novemba 29,2018 katika ukumbi wa Empire Hotel mjini Shinyanga. Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi zawadi ya cheti na fedha taslimu 100,000/- bi Juliana Shilatu aliyetangazwa kuwa Wakala bora wa NMB mkoa wa Shinyanga. Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi Saha Dachi and Company shilingi 75,000 mshindi wa nafasi ya pili ya wakala bora wa NMB. Picha ya pamoja baada ya mafunzo kumalizika. 


Dkt. Ndumbaro atembelea Chuo cha Diplomasia

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Dkt. Bernard Archiula mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika chuo hicho. Mhe. Naibu Waziri aliweza kutembelea maeneo mbalimbali ya chuoni hapo pamoja na kufanya mkutano na Uongozi wa chuo na Wakufunzi. 

Katika mkutano huo, uongozi wa chuo pamoja na Wakufunzi walitumia fursa hiyo kumwelezea Dkt. Ndumbaro changamoto wanazokabiliana nazo chuoni hapo ikiwa ni pamoja na ufinyu wa majengo kulingana na mahitaji ya chuo na uchache na uchakavu wa miundombinu ya kufundishia.

Aidha, Mhe. Naibu Waziri alitumia ziara hiyo kujua mikakati mbalimbali waliyojiwekea chuoni hapo ikiwa ni pamoja na dhamira ya kujenga majengo mapya ambayo ramani ya mchoro wa majengo hayo iliwasilishwa kwa Mhe. Naibu Waziri.

Kwa Upande wa Dkt. Ndumbaro alitumia fursa hiyo kuupongeza Uongozi pamoja na Wakufunzi wa chuo cha Diplomasia kwa kufanya kazi kwa bidii pamoja na changamoto wanazokumbana nazo. Aidha, alitoa rai kwa Uongozi wa Chuo pamoja na Wakufunzi wawe wabunifu zaidi. 
Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Dkt. Archiula akimwelezea jambo Dkt. Ndumbaro huku Naibu Mkurugenzi wa Masomo Prof. Kitojo Wetengere akisikiliza kwa makini. 
Mkutano ukiendelea 
Dkt. Ndumbaro akionyeshwa na kuelezewa ramani yenye mchoro wa majengo ya kisasa yatakayo jengwa katika eneo la Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam .

KAIRUKI KUWAKUTANISHA WAHITIMU WALIOSOMA CHUONI HAPO KUPITIA KONGAMANO LA KITAALUMA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WATAALAMU wa afya ambao wamesoma katika Chuo kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU) wametoa mtazamo wao katika sekta ya afya huku wakijizatiti kupanua wigo wao katika kuimarisha sekta hiyo.

Wataalamu hao watakutana katika kongamano la kwanza la kitaaluma ambalo litafanyika kesho Novemba, 30 katika viwanja vya chuo kabla ya kufanyika kwa mahafali ya 16 yatakayofanyika mapema jumamosi wiki hii.

Akizungumza na waandishi wa habari Makamu mkuu wa chuo Profesa. Charles Mgone amesema kuwa kongamano hilo  litazinduliwa na katibu mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya ambapo wataalamu hao watajadili kuhusu  magonjwa yasiyoambukiza pamoja na UKIMWI. Aidha amesema kuwa kongamano hilo litawakutanisha wasomi waliosoma katika chuo hicho, wafanyakazi na wageni mbalimbali.

Kwa upande wake Naibu makamu mkuu wa chuo taaluma Profesa. Moshi Ntabaye amesema kuwa kuna vyuo vya afya 7 nchini na chuo chao kinachangia katika ufundishaji wa wataalamu wanaotakiwa kwenye sekta ya afya na kuhakikisha wanakuwa bora zaidi.

Aidha amesema kuwa wana mpango wa kujenga kampasi mpya katika eneo la Boko jijini Dar es salaam ili kuweza kuongeza uwezo wa kudahili wanafunzi wengi zaidi hasa madaktari na manesi ili kuweza kuimarisha sekta hiyo na wamewaomba wadau mbalimbali wa sekta afya kujitokeza kusaidia katika kufanikisha ujenzi wa kampasi hiyo ili kuweza kuimarisha sekta ya afya nchini.

Kwa upande wake Rais wa kongamano hilo Dkt. Leonard Malasa amesema kuwa kongamano hilo ni sehemu ya kusherekea zaidi ya miaka 20 ya hospitali hiyo huku wataalamu mbalimbali walisoma katika chuo hicho ambao wameanzisha taasisi mbalimbali za afya watatoa neno la kuwahamasisha wanafuzi chuoni hapo na hatimaye   zawadi kutolewa kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwa mwaka 2018.
 Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki  profesa Charles Mgone katikati akizungumza na waandishi wa Habari wakati wakitambulisha kuwepo kwa kongamano la kwanza la kitaaluma la chuo hicho litakalifanyika kesho katika ukumbi wa chuo hicho jijini Dar ea Salaam. Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarijiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee jinsia na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya. Kushoto kwake ni Ras wa Kongamano la kwanza la kitaaluma la Chuo cha Kairuki, Dr Leornad Malasa na kulia ni Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Bernad Mutalemwa.
 Naibu Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki Dr, Moshi Ntabaye wa kwanza Kushoto akizungumza na waandishi wa Habari hawapo pichani wakati wakitambulisha kuwepo kwa kongamano la kwanza la kitaaluma la chuo hicho litakalifanyika kesho katika ukumbi wa chuo hicho jijini Dar ea Salaam. Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarijiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee jinsia na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya. Kulia kwake  Rais wa Kongamano la kwanza la kitaaluma la Chuo cha Kairuki, Dr Leornad Malasa akifuatiwa na profesa Charles Mgone na wa mwisho ni Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Bernad Mutalemwa.
Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki  Benard Mutalemwa (kulia) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wakitambulisha kuwepo kwa kongamano la kwanza la kitaaluma la chuo hicho litakalifanyika kesho katika ukumbi wa chuo hicho jijini Dar ea Salaam. Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarijiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee jinsia na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya. Kushoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Kairuki profesa Charles Mgone, (Picha na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii).

TAASISI YA MIFUPA (MOI) YATAKIWA KUWASILIANA NA WATEJA KWA NJIA YA SIMU

$
0
0
Na.WAMJW,Dar es Salaam

Taasisi ya mifupa (MOI) imetakiwa kuanzia leo kuwasiliana na wateja wao kwa njia ya simu pale panapotokea mabadiliko ya watoa huduma kutokuwepo mahali pa kazi ilikuepusha usumbufu wa kukaa hospitalini muda mrefu.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati alipofanya ziara katika taasisi hiyo na kukuta wagonjwa wakisubiri kwa muda mrefu kupata matibabu pamoja na vipimo.Dkt. Mpoki alisema alichokiona kwenye taasisi hiyo ni mawasiliano ambayo inasababisha wagonjwa wengi kutokupata taarifa za kutokuwepo kwa madaktari wao hivyo kufanya wagonjwa kusubiri kwa muda mrefu.

“kuanzia leo taasisi hii itawasiliana nanyi kila inapotokea changamoto inayofanya mabadiliko ya mida yenu na madaktari, mtapigiwa simu sasa wewe utafanya maamuzi yakuja au kusubiri hadi muda ulioambiwa ili uonane na daktari wako muda utakaombiwa”. Alisema Dkt. Mpoki.Aidha, aliwataka madaktari na wauguzi wawe wanawajulisha wagonjwa mapema wao kwa wale wenye simu kwani kwenye kila jarida la mgonjwa huwa wanaandika namba za simu za wateja wao.

Hata hivyo Dkt. Mpoki alisema hii ni kutokana na mkakati wa Serikali wakutatua changamoto za wananchi wanaofika kupata matibabu kwenye taasisi zake na hivyo kuboresha huduma kwa wahitaji kadri ya uwezo unavyopatikana.

Katibu Mkuu huyo alifanya ziara katika taasisi hiyo kwa kutembelea idara ya Mionzi, wagonjwa wa nje pamoja na kuongea na wagonjwa waliofika kupata matibabu katika hospitali hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiangalia mashine ya mionzi ya CT SCAN katika Taasisi ya mifupa (MOI) wakati alipoitembea ili kujionea hali ya utoaji wa huduma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Ubora wa Huduma kutoka Wizara ya Afya Dkt. Mohamed Mohamed na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya mifupa (MOI) Dkt. Samuel Swai kuhusiana na kuboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wakati alipoitembelea Taasisi hiyo Leo Jijini Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na wananchi waliofika kupata huduma za uchunguzi na matibabu katika Taasisi ya mifupa (MOI) wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo kujionea hali ya utoaji huduma.

BENKI YA KCB TANZANIA YANDAA SEMINA ‘BIASHARA CLUB’ KWA WAFANYA BIASHARA WADOGO NA WAKATI (SME).

$
0
0
BENKI ya KCB nchini yaendesha kongamano la Biashara Club kwa mara ya pili mwaka 2018 jijini Mwanza,baada ya kongamano la kwanza likiwa na wafanyabiashara zaidi ya 200 jijini Dar es Salaam mapema mwaka huu.

Zaidi ya kutoa elimu ya usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara na sheria za kodi, KCB Biashara Club pia inawawezesha wafanyabiashara kupanua wigo wa biashara zao kwa kuwakutanisha na wafanyabiashara wa nje na ndani ya nchi.

Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2017, KCB Biashara Club imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kukuza biashara katika sekta ya SME kwa kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati (SME) pamoja na kuwaonyesha mbinu za kukuza mitaji ya shughuli zao za kibiashara.

Semina hiyo iliyofanyika katika jijini Mwanza ilikusanya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja tofauti, wakiwa na changamoto mbali mbali za kibiashara zikiwemo rasilimali, ushindani, uelewa finyu katika maswala ya kodi na nyinginezo. Nia kubwa ya KCB ikiwa ni kutaka kuwafundisha wafanyabiashara njia bora ya kukabiliana na changamoto zinazowakumba.

Akiongea katika warsha hiyo, Meneja wa Tawi Benki ya KCB Mwanza, Emmanuel Mzava aliwashukuru wafanyabiashara na wajisiriamali kwa Kujitokeza kwa wingi kuja kupata mbinu muhimu zitakazowasaidia katika kukabiliana na changamoto za kibiashara.

“Mtegemee semina kama hizi kwa siku za mbeleni kwani Mwanza ni jiji linaloonyesha kushamiri kibiashara” aliongezea Mzava.NayeSwetbert Thomas ambaye ni mtaalamu wa mswala ya kodi aliyealikwa na KCB kwa ajili ya kutoa mafunzo katika warsha hiyo aliwahimiza wafanyabiashara hao kuhusu muuhimu wa kuelewa mifumo ya kodi hapa nchini na ni kwa namna gani unagusa biashara zao.

Mbali na kufaidika na ujuzi wa mambo kupitia semina na safai mbalimbali zinazoandaliwa na kitengo cha “Biashara Club”, wanachama pia watafaidika kwa kujenga uhusiano wa kibiashara baina yao ambao utapelekea wao kuongeza si ujuzi wa kibiashara tu, bali pia kupanua wigo wa biashara zao. KCB Bank inatambua umuhimu wa wafanya biashara wadogo na wakati katika kukuza uchumi wa nchi lakini pia inatambua kwamba uchumi hautakuwa kama wafanya biashara hao hawatakuwa na nyenzo sahihi za kibiashara.
Mkuu wa Kitengo cha wafanyabishara wadogo na wa kati Abdul Juma akizungumza na wafanyabiashara wa jiji la Mwanza katika hafla ya Biashara Club Workshop iliyofanyika Gold Crest Hotel tarihe 29.11.2018. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 200 ilikuwa na lento la kutoa mafunzo katika maswala ya usimamizi wa fedha,uendeshaji wa biashara na sheria zinazohusu kodi.
Meneja wa Mauzo ya Kibiashara wa Benki ya KCB Lightness May kijibu maswali kutoka kwa wafanyabiashara wa jiji la Mwanza katika hafla ya Biashara Club Workshop iliyofanyika Gold Crest Hotel tarehe 29.11.2018 jijini Mwanza. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 200 ilikuwa na lengo la kutoa mafunzo katika maswala ya usimamizi wa fedha,uendeshaji wa biashara na sheria zinazohusu kodi.
Wafanyabiashara wakiwa wanaendelea kufuatilia semina.
Wafanyakazi wa Benki ya KCB wakiwa katika picha ya pamona wakati wa utambulisho.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images