Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

MKAZI WA MBEYA AJISHINDIA NYUMBA NA SH MILIONI 20 ZA BIKO,AKABIDHIWA.


NAIBU WAZIRI WA NISHATI AFANYA ZIARA WILAYANI MUFINDI

$
0
0


 
Akikagua kituo binafsi cha kuzalisha umeme cha Mwenga ambacho kinazalisha megawati 4 na kuunganishwa umeme vijiji 32
IMG_7991-min
Naibu Waziri akicheza na wananchi wa kijiji cha Ikondosi wilayani mufindi
IMG_7958-min
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumzia mikakati ya serikali ya kuwafikishia wananchu umeme wa uhakika na kwa gharama nafuu, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa iringa, Ally Happi

MICHUZI TV: TRENI YA UMEME KUPITA KATIKA MAHANDAKI YA MILIMA YA KILOSA YENYE UREFU WA KM 2.7

MICHUZI TV:UJENZI WA RELI YA SGR KUTOKA MOROGORO MPAKA MAKUTUPORA SINGIDA UNAVYOENDELEA

NAIBU WAZIRI WA KILIMO AWAONYA MAWAKALA MAZAO YA WAKULIMA,MBOLEA

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba ametoa onyo kali kwa madalali wanaowauzia wakulima wa mazao ya chakula,biashara na mbolea kwa bei ya Sh.70,000 badala ya kufuata bei elekezi ya Sh.64,700 kwa mfuko mmoja .

Akiwa Katika ziara mkoani Iringa  ya ukaguzi wa upatikanaji wa mbolea kwenye maghala ya  Serikali na wawekezaji  waliopo mkoani hapa.

Naibu Waziri huyo was Kilimo amewataka madalali hao kuacha mara moja tabia hiyo kwani   Serikali ya Awamu ya Tano chini ya  Rais Dk.John Magufuli haina utani katika kuwasaidia watu maskini na wanyonge.Ameamua kutoa onyo hilo baada ya wananchi wa kijiji cha Ngulwe wilayani Kilolo kutoa malalamiko yao wakati wa kikao kilichowahusisha wakulima ,wadau pamoja na Naibu Waziri hugo.

“ Wananchi nimeskia malalamiko yenu kuhusu bei ya mbolea, nitoe rai kwa wauzaji wa mbolea nchi nzi.a kufahamu atakeyeuza mbolea kwa bei tofauti na elekezi iliyopangwa na Serikali tutamchukulia hatua za kisheria,"amesema Mgumba.Aidha amewatoa hofu wakulima wote nchini kuhusu upatikaji wa mbolea katika  kipindi cha kuelekea msimu wa kilimo na kwamba Serikali imejidhatiti kikamilifu na mbolea ipo ya kutosha.

Imeelezwa wakulima wengi nchini wamekuwa katika  changamoto ya upatikanaji wa mbolea ambapo hapo awali kulikuwa na  Mbolea waagizaji zaidi ya mmoja hali iliyosababisha usumbufu kwa wakulima  na kwa bei ya juu.Kutokana na hiyo Serikali kuingilia  kati kwa kuweka Wakala Maalum wa kuagiza  mbolea kutoka nje ya nchi na kutoa bei elekezi kwa wauzaji.


Naibu Waziri Omari Mgumba akizungumza na Wakulima wa Kijiji cha Ngulwe.
Naibu Waziri Omari Mgumba akipata maelezo mafupi kutoka mmoja wa wauzaji wa Mbolea.
Naibu Waziri Omari Mgumba akikagua Maghara ya kuhifadhia Mbolea mkoani Iringa.

PROFESA MBARAWA YUKO WILAYANI KAKONKO KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA

$
0
0
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa amefanya ziara katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maji kwa lengo la kuhakikisha lengo la Serikali kuwapatia wananchi huduma ya majisafi na salama linatimia.

Akiwa wilayani humo Profesa Mbarawa amejionea changamoto mbalimbali zinazosababisha utekelezaji usioridhisha na kuwataka watendaji wa wilaya hiyo kuchukua hatua sahihi ili kuwezesha miradi hiyo kukamilika, ambapo baadhi yake imeanza mwaka huu na mingine ni ya muda mrefu.

Profesa Mbarawa ametembelea miradi ya Kakonko Mjini, Muhange, Kiga, Gwanumpu na Nagwijima kwa lengo la kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa miradi hiyo. Akizungumza na watendaji wa Wilaya ya Kakonko, Profesa Mbarawa amewataka watendaji hao kuhakikisha wanachukua hatua, ikiwemo kuvunja mikataba ya wakandarasi wanaoonekana kukosa uwezo wa kutekeleza miradi hiyo kwa kufuata taratibu za kisheria na kutafuta wakandarasi wanaoweza kufanya kazi nzuri.

Profesa Mbarawa amesema anataka kuona miradi yote wilayani Kakonko inakamilika kwa wakati ikiwa ni sehemu ya kutekeleza lengo la Serikali kutoa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi kwa kuwa fedha za kutimiza lengo hilo zipo, hivyo haoni sababu ya kutokukamilika kwa miradi ya maji.

Huku akitaka kuwe na mawasiliano mazuri kila baada ya miezi miwili kati ya watendaji, wabunge na viongozi wa Serikali kuhusu maendeleo ya miradi kwa kila hatua ya utekelezaji. Wakati huo, Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mhandisi Christopher Chiza amesema utendaji wa wataalamu umekuwa kikwazo kikubwa kwa Serikali, kutokana na kutokufuatwa kwa taratibu sahihi za manunuzi na usimamizi mbovu wa miradi ya maji.

Mhandisi Chiza amewaasa watendaji wa Serikali wenye dhamana ya usimamizi wa miradi ya maji kutumia taaluma zao vizuri ili kupata matokeo chanya kwenye miradi ya maji.

Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiwa na Mhandisi wa Wilaya ya Kakonko (kushoto), Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mhandisi Christopher Chiza (kulia) pamoja na na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala kwenye Mradi wa Maji wa Gwanumpu katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma. 
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wakazi wa Kijiji cha Muhange wakati alipofanya ziara kwa lengo la kujua hali ya upatikanaji wa maji katika kijiji hicho. 
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (mwenye kofia) akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mhandisi Christopher Chiza wakiwa pamoja na na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala kwenye Mradi wa Maji wa Nyagwijima katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma. 
Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mhandisi Christopher Chiza akimuongoza Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa wakitoka kwenye Chanzo cha Maji cha Mugembezi kinachotumika kwa ajili ya Mradi wa Maji wa Muhange wilayani Kakonko, mkoani Kigoma. 
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiwa na akina mama kijijini Kiga mara baada ya kujionea mradi wa Kiga na kuzungumza na Jumuiya ya Watumiaji Maji wa Mradi wa Maji wa Kiga katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma. 

TRC YAENDELEA KUTOA MAFUNZO MAALUM KWA WAHANDISI WA KITANZANIA

WAZIRI WA KILIMO AFUNGUA WARSHA YA KITAIFA YA WADAU WA KILIMO

$
0
0
Waziri wa kilimo Mh Japhet Hasunga akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Kitaifa ya wadau wa Kilimo iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania ambapo amewataka wakulima kulima Kilimo chenye tija.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya baraza la kilimo Tanzania Dkt Sinare Yusuph Sinare akizungumza wakati muda mfupi kabla ya kumakribisha waziri waziri wa Mh Japhet Hasunga kufungua warsha ya kitaifa ya wadau wa kilimo, ambapo Dkt Sinare alisema ili sera ya viwanda ifanikiwe ni muhimu kilimo kikaunganishwa na viwanda.
Mwenyekiti wa TPSF Bw Salum Shamte ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Kilimo, Bi Jacqueline Mkindi Makamo Mwenyeki wa Bodi, na Mwenyekiti Dkt Sinare Yusuph Sinare wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Kitaifa ya wadau wa Kilimo, iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya kitaifa ya Kilimo iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania wakifuatilia kwa umakini uwasilishwaji wa mada mbalimbali wakati wa warsha ya siku mbili inayofanyika Dar es Salaam. 
M/kiti wa bodi ya wakurugenzi wa baraza la kilimo, bi Jacqueline Mkindi akiteta jambo na mwenyeki wa bodi dkt sinare yusuph wakati wa warsha ya kitaifa ya wadau wa kilimo iliyoandaliwa na baraza la kilimo Tanzania, anayefutia ni Waziri wa Kilimo Mh Japhet Hasunga.
Sehemu ya washiriki wa warsha ya kitaifa ya wadau wa kilimo wakifuatilia mjadala kuhusu sera za kilimo, warsha hiyo ya siku mbili iliyoanza leo jijini dare s salaam imeandaliwa na abraza la kilimo Tanzania.

VODACOM FOUNDATION NA DORIS MOLLEL FOUNDATION WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA KUSAIDIA WATOTO NJITI HOSPITALI YA NYARUGUSU, KIGOMA

$
0
0
 Katibu  Tawala  wa wilaya ya Kasulu aliyemuwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo mkoani Kigoma, Titus Mguha (wa tatu kushoto) akipeana mkono na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu (kushoto) wakati wa kupokea sehemu ya msaada wa vifaa tiba maalumu kwa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) vilivyotolewa na Taasisi ya Vodacom kwa kushirikiana na Taasisi Doris Mollel kwa wadi ya Hospitali inayohudumia kambi wakimbizi ya Nyarugusu, Kasulu mkoani Kigoma hivi karibuni. Wa pili kushoto ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel na katikati ni Afisa Msimamizi wa Kambi hiyo, Francis Chokola.
Katibu  Tawala  wa wilaya ya Kasulu aliyemuwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo mkoani Kigoma, Titus Mguha (wa tatu kulia) akizungumza wakati akitoa shukrani kwa Taasisi za Vodacom Tanzania na Taasisi Doris Mollel kwa msaada walioutoa kwenye hospitali hiyo.
Katibu  Tawala  wa wilaya ya Kasulu aliyemuwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo mkoani Kigoma, Titus Mguh, akiwa ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu na Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel wakimjulia hali mama aliyejifungua mtoto Njiti katika Hospitali inayohudumia kambi wakimbizi ya Nyarugusu, Kasulu mkoani Kigoma hivi karibuni, ambapo pia walimzawadia khanga kama sehemu ya faraja kwake.

Tanzania na China zasaini makubaliano ya sh Bil. 22.4 kujenga Chuo cha VETA Kagera

$
0
0
 Serikali za Tanzania na China zimetia saini makubaliano ya ujenzi wa Chuo cha Mkoa wa Kagera utakaogharimu Shilingi za Kitanzania bilioni 22.4 zikiwa ni ufadhili kutoka serikali ya China.

Makubaliano hayo yametiwa saini leo tarehe 26 Novemba 2018 na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Taknolojia Dkt. Leonard Akwilapo aliyeiwakilisha Serikali ya Tanzania na Yuan Lin, Mwakilishi Mkuu wa Uhusiano wa China na Tanzania katika masuala ya Kiuchumi na Kibiashara aliyeiwakilisha Serikali ya Watu wa China. 

Hafla ya kutia saini makubaliano hayo ilifanyika katika ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na wawakilishi mbalimbali wa pande zote mbili, ambapo kwa upande wa Tanzania miongoni mwa waliohudhuria na kushuhudia utiaji saini huo ni pamoja na Mkurugenzi wa  Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET), Dkt. Noel Mbonde; Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Peter Maduki; Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt. Pancras Bujulu na Mkurugenzi Msaidizi wa TVET, Enock Kayani.

Akizungumza wakati wa kutia saini makubaliano hayo, Dkt. Akwilapo alisema ujenzi huo unatarajiwa kuanza mara moja na  utachukua takribani miezi 18 kukamilika na kwamba unaongeza mchango katika kuandaa nguvukazi kwa ajili ya Uchumi wa Viwanda nchini. 

Alisema, baada ya kukamilika chuo hicho kitakuwa ana uwezo wa kudahili wanafunzi 400 katika kozi za muda mrefu na zaidi ya 1000 kozi za muda mfupi huku kikiwa na nafasi za bweni 200 kwa wanafunzi wa kiume na 120 kwa wanafunzi wa kike. 

Kwa upande wake, Yuan Lin alisema kuwa ujenzi wa Chuo hicho ni sehemu ya uendelezaji mahusiano mema kati ya China na Tanzania na kwamba unaonesha uhalisia wa China kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Tanzania kuelekea katika uchumi wa viwanda. 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt Pancras Bujulu licha ya kuishukuru serikali ya China kwa msaada huo, alisema kuwa VETA kwa kushirikiana na serikali mkoani Kagera tayari wameshaweka miundombinu muhimu kwa ajili ya kuwezesha shughuli za ujenzi wa chuo hicho kuanza mara moja.

Aliitaja miundombinu iliyoandaliwa kuwa ni pamoja na kuboresha barabara iendayo kwenye eneo la ujenzi wa chuo kwa kuichonga na kuitengeneza kwa kiwango cha changarawe; kuvuta umeme hadi kwenye eneo la ujenzi na kutengeneza chanzo cha muda cha maji kwa ajili ya shughuli za ujenzi. 

Aliongeza kuwa wakati chuo hicho kikitarajiwa kuanza kujengwa, tayari walimu 20 kutoka VETA wamekwenda nchini China kujifunza namna ya uendeshaji wa vyuo vya ufundi stadi ikiwa ni sehemu mojawapo ya kuimarisha mahusiano katika uendeshaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi. 
Alisema, VETA inaendelea kuongeza juhudi za ujenzi na upanuzi wa vyuo na nia ni kuhakikisha kila mkoa una chuo cha elimu na mafunzo ya ufundi stadi chenye hadhi ya Kimkoa.

AZAM WAANZA KUJIFUA KUSAKA ALAMA TATU KWA STAND UNITED

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KIKOSI cha Klabu ya Azam FC, kimeanza rasmi mazoezi yale leo tayari kuanza safari ya kuzisaka pointi kuelekea mchezo ujao dhidi ya Stand United. Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) utafanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex Desemba 4 mwaka huu, ambapo Azam FC iko kwenye mwenendo mzuri baada ya kushinda mechi saba mfululizo za ligi hiyo.

Wachezaji wote wa Azam FC wameripoti mazoezini wakiwa na hali nzuri kabisa isipokuwa kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, ambaye ni mgonjwa. Beki wa kulia Nickolas Wadada, aliyekuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Uganda, naye amesharejea kundini akiwa ni miongoni mwa wachezaji walioripoti kwenye mazoezi hayo.

Kikosi cha Azam FC kinatarajia kuendelea na mazoezi kwa wiki hii yote, na siku ya Jumamosi wanatajia kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya vijana ya timu hiyo (Azam U-20) kwa ajili ya kujiweka sawa utakaopigwa asubuhi kwenye Uwanja wa Azam Complex. Azam FC inayonolewa na Kocha Mholanzi Hans Van De Pluijm akisaidiana na Juma Mwambusi hadi sasa imeshacheza mechi 13 za ligi, ikiwa imesdhinda mara 10 na kutoka sare mara tatu ikijikusanyia jumla ya pointi 33 na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikifuatiwa na Yanga wenye alama 32 tayari kwakicheza michezo 12 wakishinda 10 wakitoka sare mara 2.

Na katika dirisha la Usajili lililofunguliwa Novemba 15, Azam wameshafanikiwa kunasa saini ya Mshamuliaji wa Kimataifa wa Zambia Obrey Chirwa huku ikiwaotoa wachezaj wake Ditram Nchimbi, Mbaraka Yusuf kutolewa kwa mkopo

MHANDISI NYAMHANGA: HAKUNA SABABU ZA KUCHELEWESHA MRADI

$
0
0
Serikali imewataka Makandarasi wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda yenye urefu wa KM 359 inayounganisha Mkoa wa Tabora na Katavi kupitia daraja la Koga, kufanya kazi kwa bidii ili kukamilisha mradi huo kabla ya muda uliopangwa.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph nyamhanga, wakati wa ziara yake katika mikoa hiyo ambapo amesema fedha za mradi huo zipo hivyo hakuna sababu ya kuuchelewesha. "Fedha za ujenzi wa mradi huu zipo hivyo fanyeni kazi usiku na mchana ili kukamilisha mapema barabara hii kwani hakuna vikwazo vyovyote na mvua isiwe sababu ya kusimamisha kazi za ujenzi", amesema Mhandisi Nyamhanga.

Mhandisi Nyamhanga, amewataka wasimamizi wa mradi wakishirikiana na Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), wa mikoa hiyo kusimamia mradi huo kwa ukamilifu na kwa ubora uliopangwa bila kuongeza gharama. "Hakikisheni mradi huu unasimamiwa kwa ubora uliopangwa na mdhibiti gharama za mradi hata ikiwezekana ipatikane akiba ya fedha ambayo itatumika kwa miradi mingine ya barabara hapa nchini", amesisitiza Katibu Mkuu huyo.

Ameeleza umuhimu wa kukamilika kwa barabara hiyo kuwa utakuza uchumi wa wananchi na kuongezeka kwa shughuli za kibiashara kwakuwa ni miongoni mwa mikoa yenye uzalishaji mwingi wa bidhaa mbalimbali za kilimo, ufugaji wa nyuki, madini na utalii. Kuhusu uharibifu wa miundombinu ya barabara hapa nchini, Mhandisi Nyamhanga, ametoa wito kwa wananchi wa mikoa hiyo kuilinda miundombinu hiyo kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekamatwa.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akikagua kingo za daraja la kasisi katika barabara ya Tabora-Sikonge yenye urefu wa KM 30 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.
 Mkandarasi wa kampuni ya  M/S Jiangxi Geo-Engineering, Li Jinaru, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, wakati alipokagua mitambo ya kuchanganya lami katika kambi ya mkandarasi huyo anayejenga barabara ya Usesula-Komanga yenye urefu wa KM 108 kwa kiwango cha lami, Mkoani Tabora.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya LEA International Bw. Sanjeev Gupta (wa tatu kushoto) anayesimamia ujenzi wa barabara ya Usesula-Komanga yenye urefu wa KM 108, kwa kiwango cha lami, wakati akikagua hatua za ujenzi wa barabara hiyo, mkoani Tabora.
 Muonekano wa sehemu ya barabara ya Tabora-Sikonge yenye urefu wa KM 30, iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MSANII AMBER RUTTY NA MPENZI WAKE WAACHIWA KWA DHAMANA BAADA YA KUTIMIZA MASHARTI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
Baada ya kusota rumande kwa takribani siku 25, hatimaye leo Novemba 27, 2018 msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Rutty' na mpenzi wake Said Bakary wamefanikiwa kupata dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama.

Amber Rutty amedhaminiwa na  Salma Omary Bungo (46), na
Asha Mohammed (46) huku anayedaiwa kuwa mpenzi wake akidhaminiwa na mchungaji Daud Mashimo pamoja na Francis Chacha. Mahakama iliwataka kila mmoja kuwa na wadhamini 2,  ambapo kila mmoja  amesaini bondi ya Shilingi Milioni 15 wakitakiwa kuwa na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati zao za kusafiria. Aidha mahakama imewaamuru wasitoke nje ya Dar es Salaam bila ruksa.

Amber Rutty na Said Bakary walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu November 2, 2018 wakikabiliwa na kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile. Mbali na Amber Rutty na Said Bakary ambao walishindwa kudhaminiwa kwa mara tatu mfululizo mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni James Charles maarufu kama 'James Delicious' ambaye yeye alishadhaminiwa.

Wawili hao wameachiwa kwa dhamana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine Rwizire baada ya kutimiza masharti ya dhamana. Katika kesi ya  kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile linamkabili Amber Ruth, ambapo anadaiwa amelitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile ambapo alisema si kweli.

Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, linalomkabili James Delicious imedaiwa Oktoba 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Katika kosa la kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Rutty na Said Aboubakary wanadaiwa Oktoba 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp.
Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Rutty' akiwa anatoka katika maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutimiza masharti ya dhamana 

NAIBU WAZIRI MGALU AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA UMEME VIJIJINI WILAYANI MUFINDI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akikata utepe kuashiria uwashaji wa umeme katika kijiji cha Ikongosi wilayani Mufindi.

Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu amewaasa wananchi wa Mfindi kutunza miundombinu ya umeme ili  kujipatia maendeleo.Mgalu ameyasema hayo wakati alipofanya ziara  ya  utekelezaji wa miradi ya upelekezaji umeme vijijini wilalyani Mufindi.

Amesema kuwa serikali ya awamu ya awamu ya Tano nia kuhakikisha wananchi wote wanatumia umeme kwani matumizi ya vibali yamepitwa na wakati katika ukelekea uchumi wa viwanda.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha taa kweye ofisi ya kijiji katika kijiji cha wilayani Mufindi
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiangalia eneo la uzalishaji umeme wa kampuni ya Mwenga katika mto Mwenga wilayani Mufindi

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWASILI CHATO KUANZA ZIARA YA MKOA WA GEITA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita,  Mhandisi Robert Gabriel wakati alipowasili kwenye Kiwanja  cha Ndege cha Chato kuanza ziara ya kazi mkoani Geita, Novemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj  Said Kalidushi wakati alipowasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Chato kuanza ziara ya kazi mkoani Geita, Novemba 27, 2018.  Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani wakati alipowasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Chato kuanza ziara ya Kazi Mkoani Geita, Novemba 27, 2018. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani wakati alipowasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Chato kuanza ziara ya mkoa wa Geita Novemba 27, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi waliojitokeza kumlaki wakati alipowasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Chato kuanza ziara ya Kazi mkoani Geita, Novemba 27, 2018.  Wapili kushoto ni Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani, kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI,  George Mwita Waitara na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel.  
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mtoto, Naomi Nkingwa ambaye alishirkiana na wanakwaya wa Kikundi cha Mwagazege cha Chato kumwimbia wakati alipowasili kwenye Kiwanja cha ndege cha Chato kuanza ziara ya kazi Mkoani Geita, Novemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WIZARA YASIMAMISHA WATUMISHI 11 WA TFS

Diamond akabidhi rasmi kadi za bima ya Resolution kwa wakazi wa Tandale

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Resolution Insurance, Maryann Mugo akikabidhi kadi za bima ya afya kwa wakazi wa Tandale kwa dada wa msanii Diamond Platinum, Diamond aliahidi kuwapatia wakazi 1000 huduma hiyo ya bima.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nasib Abdul, Diamond Platinum ameshakamilisha ahadi yake ya kuwapatia kadi ya huduma ya bima ya afya wananchi wa Tandale.

Diamond aliwahi kutoa ahadi hiyo wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa ya kuwa angewapatia kadi hizo wananchi 1000 wa eneo hilo ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwao.

Wakazi hao wamepewa msaada huo wa bima ya afya kupitia kampuni ya bima ya Resolution Insurance ambapo Mkurugenzi Mtendaji wake Maryann Mugo alibainisha kuwa huduma hiyo ni kwa ajili ya watu wanne kwenye familia.

Alisema,”sisi tunapenda kuwahudumia wananchi kujipatia huduma nzuri za afya na kwa kile alichokifanya msanii Diamond kuwasaidia wakazi hawa huduma ya bima basi ni fahari kubwa kwetu”.

Kwa upande wake msanii Diamond aliyewakilishwa na dada yake Esma kwenye makabidhiano hayo aliwataka wananchi wa Tandale kutumia vema huduma za bima hiyo na kujiwekea akiba ya fedha ili mwisho wa siku huduma hiyo ya mwaka mmoja ikiisha waweze kujihudumia kama kawaida.

STARTIMES YAZINDUA CHANELI YA 'StarTimes ON', BONGO STAR SEARCH KUNUFAIKA

$
0
0
Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes wamezindua chapa mpya kwa bidhaa yao ya OTT (Application), itakayokuwa ikijulikana kwa jina la StarTimes ON. Bidhaa hiyo inakuwa ya kwanza kabisa barani Africa kutoa huduma ya maudhui mtandaoni kwa teknolojia ya kisasa zaidi ili kuongeza burudani na utazamaji mzuri zaidi.

Uzinduzi huo wa StarTimes ON umekuja baada ya App ya awali (StarTimes App) kufanyiwa maboresho makubwa na kuwa StarTimes ON. StarTimes ON imekuja na Luninga Mubashara, VOD (Video on Demand) pamoja na video fupi ambazo zitakuwa na maudhui mbali mbali kuanzia Habari, michezo, tamthiliya, muziki, burudani, makala, vipindi vya watoto pamoja vipindi vya dini.

“StarTimes ON inamsaidia mtumiaji kuokoa hadi asilimia 40 ya data (bando) wakati anapotumia, tofauti na matumizi ya kawaida ya kuangalia video mtandaoni. Naweza kusema StarTimes ON ni mapinduzi katika upatikanaji wa maudhui mtandaoni.” Mussa Shaaban Lindo, StarTimes ON App Operator.

“Kwa sasa, kuna zaidi ya chaneli 150 ambazo zinapatikana kwa ligha zaidi ya 10 kwenye StarTimes ON huku chaneli 140 kati ya hizo zikiwa ni chaneli  za buree. Miongoni mwa chaneli hizo ni ST Swahili ambayo kwa sasa ina vipindi Bomba kabisa kama shindano la Bongo Star Search ambalo linaendelea na kuna video kibao za waashiriki wote unaweza kuziangalia muda wowote mahali popote ili mradi tu uwe na intaneti inayofanya kazi”. Bw David Malisa, Meneja Masoko wa Kampuni ya StarTimes.

Pia StarTimes ON ina chaneli zaidi ya 40 za StarTimes, huku watumiaji wakiwa na uwezo wa kuona maudhui mapya kila siku.Pamoja na hayo yote, kupitia StarTimes ON watumiaji wanaweza kuwapigia kura washiriki wawapendao katika shindano la Bongo Star Search, wanaweza kutazama Show mbali mbali za washiriki wa BSS na kuwatumia maua majaji wa BSS, StarTimes ON ni App ya kwanza Tanzania yenye aina hiii ya utumiaji.

Kupitia StarTimes ON watumiaji wanaweza kutazama michezo mbalimbali kama vile Ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga, Ligi ya Ufaransa (Ligue 1), ligi ya UEFA EUROPA inayoendelea Alhamisi wiki hii. Kwa sasa Mechi za Bundesliga na Ligue 1 zinaonekana moja kwa moja pia kutazama marudio ya mechi hizo muda wowote na sehemu yoyote.

BENKI YA CRDB YAMTAMBULISHA MKURUGENZI MTENDAJI WAKE NCHINI BURUNDI

$
0
0
 Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay aliyemtembelea Ikulu ya Bujubura, kwa lengo la kumtambulisha Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela (kulia). Rais Nkurunziza alipongeza uteuzi wa Mkurugenzi huyo na kumtakia mafanikio zaidi katika kazi yake na kumuomba kuongeza matawi ya Benki hiyo nchini Burundi ili watu wawe na utamaduni wa kuhifadhi fedha zao benki na sio kuzihifadhi ndani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza jambo wakati alipomtembelea Naibu Katibu Mkuu wa Chama tawala cha CNDD-FDD nchini Burundi, Balozi Joseph Ntakirutimana (kulia) ikiwa ni semu ya ziara yake ya kujitambulisha tangu ateuliwe kushika nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay 
Naibu Katibu Mkuu wa Chama tawala cha CNDD-FDD nchini Burundi, Balozi Joseph Ntakirutimana (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela katika viwanja vya makao makuu ya chama hicho, jijini Bujumbura, Burundi. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Burundi, Bruce Mwile.
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dkt. Edmund Kitokezi akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliyemtembelea Ubalozini, jijini Bujumbura nchini Burundi.
Gavana wa Benki Kuu ya Burundi, Jean Ciza (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay aliyemtembelea ofisini kwake Bujubura, kwa lengo la kumtambulisha Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela (kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati) akifurahi jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Burundi, Jean Ciza (kulia) pamoja na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Burundi, Melchior Wagara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akieleza jambo kwa Mmoja wa Wateja wakubwa wa Benki ya CRDB nchini Burundi na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Interpetrol, Tariq Bashir.

MICHUZI TV: MCHUNGAJI ADHAMINI KESI YA AMBER RUTTY NA MPENZI WAKE

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images