Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110102 articles
Browse latest View live

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AZUIA LIKIZO ZA WATENDAJI WAKUU WA MKOA NA WILAYA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akizungumza na watendaji wa Mkoa na wilaya jana kuhusu maandalizi ya mapokezi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza 2019.Kulia aliyekaa ni Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katika kuhakikisha mkoa wake unawezesha wanafunzi wote watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2019 wanapata nafasi ya kusoma kwenye madarasa ya kutosha,amesitisha likizo zote za watendaji wakuu wa mkoa na wilaya ili wasimamie ujenzi wa madarasa mapya kwenye shule za sekondari.

Mndeme ametoa agizo hilo jana wakati wa kikao chake na viongozi na watendaji wa taasisi za umma na binafsi kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuwataja viongozi ambao hawapaswi kwenda likizo hadi vyumba vipya 142 vikamilike kujengwa.

Ametaja viongozi aliozuia likizo zako kuwa ni Katibu Tawala Mkoa,Wakuu wote wa wilaya,wakurugenzi wa Halmashauri ,Afisa Elimu Mkoa na wale wa wilaya zote pia wahandisi wa ujenzi wa halmashauri.

“Nataka katika halmashauri zote zenye upungufu wa vyumba madarasa hakuna kiongozi kwenda likizo ya mwisho wa mwaka hadi madarasa mapya yakamilike kujengwa ili wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019 waingie darasani ” alisema Mndeme.

Awali akitoa taarifa fupi ya hali ya hali ya miundombinu ya madarasa Katibu Tawala Mkoa Prof Riziki Shemdoe alisema jumla ya wanafunzi wapya 1,556 watahitaji madarasa mapya ya kidato cha kwanza kwenye shule za sekondari .

Aidha mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mndeme amezuia safari za mafunzo za madiwani wote katika halmashauri nane za Ruvuma hadi watoto wote watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza hapo mwakani watakapoingia darasani.

AZAM WAANZA KUJIFUA KUSAKA ALAMA TATU KWA STAND UNITED

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KIKOSI cha Klabu ya  Azam FC, kimeanza rasmi mazoezi yale leo  tayari kuanza safari ya kuzisaka pointi kuelekea mchezo ujao dhidi ya Stand United.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) utafanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex Desemba 4 mwaka huu, ambapo Azam FC iko kwenye mwenendo mzuri baada ya kushinda mechi saba mfululizo za ligi hiyo.

Wachezaji wote wa Azam FC wameripoti mazoezini wakiwa na hali nzuri kabisa isipokuwa kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, ambaye ni mgonjwa.

Beki wa kulia Nickolas Wadada, aliyekuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Uganda, naye amesharejea kundini akiwa ni miongoni mwa wachezaji walioripoti kwenye mazoezi hayo.

Kikosi cha Azam FC kinatarajia kuendelea na mazoezi kwa wiki hii yote, na siku ya Jumamosi wanatajia  kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya vijana ya timu hiyo (Azam U-20) kwa ajili ya kujiweka sawa utakaopigwa asubuhi kwenye Uwanja wa Azam Complex..

Azam FC inayonolewa na Kocha Mholanzi Hans Van De Pluijm akisaidiana na Juma Mwambusi hadi sasa imeshacheza mechi 13 za ligi, ikiwa imesdhinda mara 10 na kutoka sare mara tatu ikijikusanyia jumla ya pointi 33 na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikifuatiwa na Yanga wenye alama 32 tayari kwakicheza michezo 12 wakishinda 10 wakitoka sare mara 2.

Na katika dirisha la Usajili lililofunguliwa Novemba 15, Azam wameshafanikiwa kunasa saini ya Mshamuliaji wa Kimataifa wa Zambia Obrey Chirwa huku ikiwaotoa wachezaj wake Ditram Nchimbi, Mbaraka Yusuf kutolewa kwa mkopo.

SSRA Yaondoa Utata Kikokotoo cha Pensheni

SSRA Yaeleza Namna Warithi Watakavyonufaika kwa Kutumia Kikokotoo Kipya

Naibu Waziri aomba wanaotumia ARVs kutoacha

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Dodoma
WATANZANIA wanaotumia dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi wametakiwa kuendelea kutumia pasipo kuacha, ili waweze kuishi maisha yenye afya iliyoimarika hivyo kuendelea kulitumikia taifa. Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde wakati akifungua kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
Alisema kati ya watu wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15 hadi 64 ambao walitoa taarifa kuwa wanatumia dawa za kufubaza VVU, asilimia 87.7 ndio wamefubaza VVU ambapo wanawake ni asilimia 89.2 na wanaume ni asilimia 84. “Napenda kuhamasisha watanzania wote wanaotumia dawa za kufubaza VVU waendelee kuzitumia pasipo kuchoka na kwa kufanya hivyo wataweza kuishi maisha yenye afya iliyoimarika na furaha na hivyo kuendelea kulitumia taifa vyema” alisema Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ni Pima VVU, Jitambue Ishi ambayo inaonesha ushahidi kutokana na matokeo ya utafiti wa viashiria vya UKIMWI wa mwaka 2016/2017 hapa nchini.
Alisema utafiti huo unaonesha kuwa kama nchi bado hatujafanya vizuri katika kutimiza malengo 90 ya kwanza ya kimataifa yaani asilimia 90 ya WAVIU nchini wawe wamepima na kujua hali zao ifikapo mwaka 2020.
Mavunde alisema matokeo yameonesha ni asilimia 52 tu ya WAVIU nchini wanajua hali zao. “Hii ina maana kwenye eneo la kupima kuna vikwazo vingi vinavyowafanya watu hasa wanaume kutojua afya zao, pengine nchi bado hatujapata ufumbuzi bado kwani kutokana na matokeo ya utafiti huo ni asilimia 45 tu ya WAVIU wanaume wanajua hali zao” alisema
Alisema katika kutekeleza tisini ya pili yaani asilimia 90 ya WAVIU wajuao hali zao wawe wameanza dawa za ARV ifikapo mwaka 2020 kama nchi, imepiga hatua japo kwa kusuasua kidogo kwa upande wa wanaume. Alisema utafiti wa mwaka 2016/2017 umeonesha kati ya watu wanaoishi na VVU wenye umri kati ya miaka 15 hadi 64 ambao wanajua hali zao za maambukizi asilimia 90.9 walianzishiwa dawa za kufubaza VVU, wanawake wakiwa asilimia 92.9 na wanaume ni asilimia 86.1. Alisema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika mapambano dhidi ya UKIMWI, inaahidi kutoa ushirikiano. Alisema malengo hayo ni pamoja na kupunguza maambukizi mapya kwa asilimia 85 ifikapo mwaka 2023 kama ilivyobainishwa kwenye mkakati wa nne wa taifa wa kudhibiti UKIMWI nchini na hatimaye kufikia malengo ya sifuri tatu ifikapo mwaka 2030.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na washiriki wa kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akitoa salamu za UNAIDS wakati wa kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
 Wadau mbalimbali wanaoshiriki kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DKT. MABODI AFANYA ZIARA WILAYA YA KUSINI UNGUJA

$
0
0
Na Is-Haka Omar, Zanzibar
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amesema endapo Wabunge na Wawakilishi watashindwa kutumia fedha za maendeleo ya mfuko wa jimbo zinazoingizwa katika Halmashauri za Wilaya, CCM itachukua hatua ya kuidhinisha fedha hizo zitumike kutatua kero sugu zinawakabili wananchi.

Msimamo huo ameutoa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 katika Halmashauri ya Wilaya Kusini Unguja, amesema fedha za mfumo wa maendeleo ya Jimbo ni haki ya wananchi na sio fedha za viongozi wa jimbo. Amesema viongozi hao  wanakabidhiwa fedha hizo kwa ajili ya kusimamia utaratibu wa matumizi yake na sio kuziacha katika akounti za benki bila kutumika hali inayosababisha kutokamilika kwa baadhi ya miradi ya wananchi.

Dk. Mabodi akikagua miundombinu ya vyoo katika skuli ya Sekondari na Msingi ya Kusini Makunduchi alikuta skuli hiyo ina changamoto ya upungufu wa vyoo huku wanafunzi na walimu wakitumia vyoo chakavu, na kuamua kutoa agizo kwa Halmashauri kuidhinisha kiasi cha shilingi milioni 10 kutoka fedha za maendeleo ya jimbo hilo zilizokaa muda mrefu bila ya kutumiwa. Pia Naibu Katibu Mkuu kupitia Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein aliahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya matengenezo ya haraka ya miundombinu ya vyoo hivyo kuhu akisisitiza viongozi wa Chama na Serikali kuchukua hatua za makusudi kumaliza changamoto za aina hiyo katika skuli mbali mbali za Unguja na Pemba.

Akiwa katika skuli hiyo alitoa wito kwa viongozi wa Chama na Serikali kushuka kwa wananchi hasa wa vijijini kuangalia changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu kwa mujibu wa maelekezo yaliyomo katika Ilani ya CCM. Aidha Dk.Mabodi akiwa katika shamba la kuotesha miti mbali mbali ikiwemo ya Matunda huko katika Kijiji cha Mungoni, alishauri wananchi wanaofanya shughuli hizo kuhakikisha wanaotesha miti inayotoa matunda yenye soko  ikiwemo miti aina ya midimu.

Katika maelezo yake Dk.Mabodi wakati akikagua ukarabati wa Kituo cha Afya Mungoni aliitaka Halmashauri kuharakisha ujenzi huo ili wananchi waendelee kupata huduma bora za Afya. Pamoja na hayo Naibu Katibu Mkuu aliipongeza Halmashauri ya Kusini Unguja kwa kutekeleza vizuri miradi ya ujenzi wa vyoo na madarasa ya kisasa katika Skuli za Mtende na Bwejuu yaliyotekelezwa kupitia mpango wa ugatuzi wa madaraka kupitia Serikali za Mitaa.
 MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja Kassim Mtoro Abu (wa kwanza kushoto) akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa Ilani katika Halmashauri hiyo kwa mwaka 2015/2018, Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Mhe. Hassan Khatib Hassan (wa pili kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi (wa kwanza kulia).
  NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Dk. Abdulla Juma Mabodi akiwa katika ziara ya katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja uliotekelezwa chini ya mpango wa ugatuzi.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Dk. Abdulla Juma Mabodi akikagua maendeleo ya Kikundi cha wanawake cha ujasiriamali cha Furahia kilichopo Kijiji cha Paje ambacho kinanufaika na miradi ya uwezeshaji iliyopo katika mpango wa ugatuzi.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Dk. Abdulla Juma Mabodi akizungumza na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja pamoja na Viongozi wa CCM wa Jimbo, Wilaya na Mkoa wa Kusini Unguja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

HISTORIA YA UTALII ILIYOSAHAULIKA KATI YA TANZANIA NA MSUMBIJI

$
0
0
Tanzania ni nchi iliyoisaidia Nchi ya Msumbiji kupata Uhuru, lakini makazi ya Wapigania uhuru wa Msumbiji yaliyokuwa katika Wilaya Ya Tunduru Mkoani Ruvuma yamekuwa kama yamesahaulika na nchi hizi mbili.

INTRODUCING OFFICIAL VIDEO ASLAY-MARIOO COVER BY MALISAM


MCL DIGITAL EXCLUSIVE: KUTANA NA MTANZANIA WA BOEING ALIYESAIDIA KUITENGENEZA 'DREAMLINER'

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA KITUO CHA AFYA CHA BWANGA WILAYANI CHATO

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Mradi wa Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Bwanga wilayani Chato, Novemba 27, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani  na wapili kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwikwabe Mwita Waitara. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi  Robert Gabriel na wapili kushoto ni  Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj  Said Kalidushi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole  Bibi Jenifer Erasto  aliyelazwa katika wodi ya wazazi  kwenye  Kituo cha Afya cha Bwanga wilayani Chato wakati alipotembelea Kituo hicho na Kuweka Jiwe la Msingi la  Maradi wa Ukarabati wa Kituo, Novemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi baada ya kukagua  na Kuzindua Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Bwanga wilayani Chato, Novemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WARSHA YA WADAU WA KILIMO YABEBA KAULI MBILI YA KILIMO NA MAENDELEO YA VIWANDA TANZANIA

$
0
0



Mratibu wa ASDP 2 Mhandisi January Kayumbe akiwasilisha Mada ya fursa ya Sekta binafsi katika utekelezaji wa ASDP 2 katika warsha ya siku mbili ya wadau wa Kilimo iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania, ambapo ameonyesha fursa nyingi zinazopaswa kutumiwa na sekta binafsi katika Mpango huo wa Pili wa Kilimo nchini.
Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya baraza la kilimo Tanzania Bw. Julias Nyabicha na Mh Jitu Soni ambaye ni Mjumbe wa Bodi Mstaafu wakifuatilia kwa karibu uwasilishwaji wa Mada mbalimbali katika Warsha ya wadau wa Kilimo iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania.
Sehemu ya wadau wa Kilimo nchini wanaoshiriki Warsha ya Kitaifa ya wadau wa Kilimo inayofanyika Jijini Dar es Salaam wakifuatilia Warsha hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania yenye kauli mbili ya Kilimo na Maendeleo ya Viwanda Tanzania.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya baraza la kilimo Tanzania Dkt Sinare Yusuph Sinare akiwa na wadau wengine wa kilimo wakifuatilia warsha ya wadau wa kilimo iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania.
Makamo Mwenyeki wa SACAU Bi Doreen Hlatshwayo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko wakifautilia uwasilishwaji wa mada za kilimo kwa wadau wa walioshiriki warsha ya siku mbili ya wadau wa kilimo iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania.

WAZIRI MKUU AAGIZA MRADI WA MAJI CHATO UKAMILIKE KWA WAKATI

$
0
0
*Ni wa Imalabupina/Ichwankima wenye thamani ya sh. bil. 8.28
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Imalabupina/ Ichwankima wilayani Chato ambao una thamani ya sh. bilioni 8.28 na amewaagiza viongozi wa wilaya hiyo wahakikishe unakamilika kwa wakati.
Waziri Mkuu amesemaSerikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi. Ameyasema hayo leo (Jumanne, Novemba 27, 2018) alipozungumza na wananchi kwenye kijiji cha Nyamirembe baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika mradi huo wa maji wakati akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Geita.

Amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha wananchi wote nchini wakiwemo na wa wilaya ya Chato mkoani Geita wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao, hivyo amewataka waendelee kuwa na imaji na Serikali yao. “Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwenye maeneo mbalimbali nchini vikiwemo na vijiji vya wilaya ya Chato ili kuwawezesha wananchi kupata maji.”

Waziri Mkuu ameagiza mradi huo ukamilike kwa wakati kwa kuwa Serikali inahitaji kuona wananchi wakinufaika na huduma hiyo. Mradi huo ulianza kujengwa Mei, 2017 na ulitakiwa ukamilike Mei, 2018 ila kutokana na changamoto mbalimbali unatarajiwa kukamilika Februari 2019. Awali,Mkuu wa wilaya ya Chato Mhandisi, Mtemi Simeon alisema mradi huo unatarajiwa kuhudumia watu takribani 59,609 katika vijiji 11 vilivyopo kwenye kata nne za Nyamirembe, Ichwankima, Kachwamba na Kasenga.

“Vijiji vitakavyonufaika na mradi huu ni Nyamirembe, Kalebezo, Nyambiti, Busalala, Imalabupina, Ichwankima, Kachwamba, Ipandikilo, Idoselo, Igagula na Mwangaza. Tayari vituo 240 vya kuchotea maji vimeshakamilika na matenki nane kati ya tisa yamekamilika pamoja na mabirika 10 ya kunyweshea mifugo.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Viongozi wa Dini wakati alipowasili kwenye eneo la Mradi wa Maji wa Imalabupina - Ichwankima kuweka jiwe la msingi la Mradi huo wilayani Chato, Novemba 27, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Mradi wa Maji wa Imalabupina - Ichwankima wilayani Chato Novemba 27, 2018. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandishi Robert Gabriel. (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu)

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI MAKTABA MPYA YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke kuashiria ufunguzi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2100 kwa wakati mmoja. Wengine katika picha wanaoshuhudia ni Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea mfano wa funguo kutoka kwa Balozi wa China hapa nchini Wang Ke kuashiria ufunguzi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2100 kwa wakati mmoja huku viongozi wengine wakipiga makofi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika hafla hiyo ya ufunguzi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Vitabu kutoka kwa Balozi wa China hapa nchini Wang Ke kabla ya ufunguzi wa Maktaba hiyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma moja ya kitabu kilichomo katika Maktaba hiyo mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla hajaifungua rasmi huku Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akitazama.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akirudisha kitabu hicho kwenye shelfu la vitabu mara baada ya kukisoma huku Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akiangalia. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia moja ya kompyuta zinazohifadhi vitabu (onlinebooks) ambazo wanafunzi watakuwa wakijisomea pamoja na kupata huduma ya mtandao internet.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Msataafu Edward Lowassa mara baada ya kuwasili katika eneo la Maktaba mpya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WALIOVAMIA ARDHI YA BAKWATA MWANZA WATAKIWA KUONDOKA KWA HIARI

$
0
0
Na Baltazar Mashaka, Mwanza
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza linakusudia kujenga hospitali itakayowahudumia waumini wa dini hiyo na jamii. Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Sheikh Hassan Musa Kabeke alisema jana wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na waumini wa dini hiyo baada ya kufanya usafi kwenye Msikiti wa Nyegezi Kijiweni katika Wilaya ya Nyamagana.

Alisema baadhi ya wananchi wamevamia na kujenga kwenye maeneo yanayomilikiwana taasisi hiyo ya dini likiwemo eneo la msikiti wa Nyegezi Kijiweni wanalotaka kujenga kituo cha afya na baadaye hospitali na hivyo wote waliovamia maeneo yake waondoke wenyewe. Sheikh Kabeke alifafanua kuwa wamebaini maeneo ya BAKWATA mkoani Mwanza likiwemo eneo la msikiti wa Nyegezi ambao ulichomwa moto na watu wasiojulikana, yamevamiwa na kuwataka walioingia na kufanya ujenzi wajitathmini na wachukue uamuzi sahihi kwa maslahi ya Waislamu na jamii ya Watanzania.

Alisema waliojenga kwenye ardhi ya maeneo ya baraza hilo la Waislamu ni vema wakaondoka wenyewe badala ya viongozi wa kiroho kuingia kwenye mgogoro na misuguano isiyo ya lazima na waumini wake ama jamii inayowazunguka.Kaimu sheikh huyo wa mkoa alisema; “ Katika utaratibu wa BAKWATA wa kukagua na kuhakiki mali zake wamebaini baadhi ya maeneo yao yamevamiwa na kujengwa nyumba za kudumu.Waliovamia waje tukae mezani kwa mazungumzo ili wapishe kwa hiari badala ya kuingia kwenye migogoro na marumbano.”
 Katibu wa BAKWATA Kata ya Nyegezi akifafanua jambo kwa Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Sheikh Hassan Musa Kabeke wakati wakikagua mipaka ya eneo la taasisi hiyo Nyegezi Kijiweni. 
 Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Sheikh Hassan Musa Kabeke akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wakiwemo waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kumaliza kufanya usafi kwenye Msikiti wa Nyegezi Kijiweni katika Wilaya ya Nyamagana. Wa pili kutoka kulia ni Kaimu Katibu wa BAKWATA mkoani humu, Sina Mohamed Mwagalazi.
 Ustadhi Khatibu Imani akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) kuhusu uvamizi wa ardhi ya BAKWATA ulipojengwa Msikiti wa Nyegezi Kijiweni. Picha zote na Baltazar Mashaka

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TIMESFMTZ: Aslay atajwa kuwa msanii bora Afrika - Taarifa kutoka Nigeria


INTRODUCING "INSTAGRAM" BY BORN KILLER

SSRA Yaeleza Namna Warithi Watakavyonufaika kwa Kutumia Kikokotoo Kipya

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN, AZUNGUMZA NA RAIS WA SEYCHELLES JIJINI NAIROBI

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na ujumbe wake akizungumza na Rais wa Seychelles.Danny Faure,hayuko picha kushoto Balozi wa Tanzania Nchini Kenya.Dkt. Pindi Chana na kulia Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe Rashid Juma, Waziri wa Ujuenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Dkt. Sira Ubwa Mwaboya na Mshauri wa Rais Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa Uchumi na Fedha Mhe. Balozi Mohammed Ramia, wakifuatilia mkutano huo
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Rais wa Nchi ya Seychelles Mhe. Danny Faure, wakati wa mazungumzo yao yaliofanyika katika Hoteli ya Inter Continental Jijini Nairobo Nchini Kenya, wakihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Endelevu wa Bahari (Blue Economy)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kulia akizungumza na Rais wa Seychelles Mhe.Danny Faure, katika ukumbi wa Hoteli ya InterContinental Nairobi Kenya. 
Picha na IKULU

NSSF YASHIRIKI MAONESHO YA VIWANDA VIDOGO (SIDO) KANDA YA KASKAZINI, MKOANI TANGA

$
0
0
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeungana na wafanya biashara wadogo na wadau wengine katika kushiriki maonesho ya viwanda vidogo yanayofanyika kuanzia  Novemba 22 , 2018 na kufunguliwa rasmi  Novemba 23 , 2018 na Naibu Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyaya katika viwanja vya Tangamano mkoani Tanga.

Lengo la maonesho hayo ni kusaidia wajasiriamali wadogo kupata masoko ya bidhaa zao, kuweza kujifunza kupitia wajasiriamali na wafanya biashara wengine waliofikia malengo yao pia kujenga mahusiano baina ya taasisi mbali mbali ambazo ni wadau na washirika wa maendeleo.

Kwa upande wa NSSF maonesho hayo yamekuwa ni moja ya fursa kubwa ya kuweza kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa Hifadhi ya Jamii na kutoa huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko kwa wanachama wake na jamii kwa ujumla kwa ukaribu zaidi. Pia imekuwa ni fursa kwa NSSF kuwafikia washiriki wa maonyesho hayo na kuwajuza kwa namna gani wanaweza kunufaika na huduma za hifadhi ya jamii hususani walio katika ajira binafsi kupitia mfumo wa uchangiaji wa Hiari.

Meneja wa Mkoa wa Tanga Elinami Massaoe ametoa wito kwa wakazi wote wa Tanga kutembelea maonyesho hayo na kufika katika banda la NSSF ili kuweza kupata elimu ya kujiwekea akiba itakayo wanufaisha kwa maisha yao ya sasa na ya baadae, pia kuwatoa hofu wanachama kuhusu michango yao na wadau wa mfuko ya hifadhi ya jamii kuhusu muelekeo wa mfuko hususani baada ya kuongonishwa kwa mifuko ya Pensheni na kuwa na mifuko miwili; PSSSF na NSSF.

Meneja pia amesisitiza wajiri walio wadaiwa sugu wa NSSF kwa kusema, “Wajiri wote waliojiunga na NSSF wajitahidi kuleta michango ya wanachama kwa wakati ili wasi wakoseshe haki zao za msingi wanachama wa Mfuko wa hifadhi ya jamii, sambamba na hilo hatua mbalimbali zimeshaanza kuchukuliwa kwa wajiri wote walio wadaiwa sugu ikiwemo kuwafakisha mahamakani ili kupata amana za wanachama wetu.
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akipata maelezo mafupi kutoka kwa Afisa Uhusiano na Masoko Bi Ummy-kulthum Mnjeja, kuhusu Mafao na huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii alipotembelea Banda la NSSF Siku ya ufunguzi wa maonyesho ya SIDO Kanda ya Kaskazini viwanja vya Tangamano Mkoani Tanga kuanzia Novemba 23/2018.
  Afisa Mwandamizi Idara ya Elimu na  Uhusiano NSSF, Bi Amina Mmbaga akiwa anamkaribisha Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Tanga Ndg. Martin Shigella alipotembelea Banda  la Nssf katika kilele cha maonesho ya SIDO,Mkoani Tanga.
  Meneja Mkoa wa Tanga  Elinami Massaoe akiwa anazungumza na waandishi wa Habari waliofika katika Banda la Nssf  na kuelezwa maendeleo ya NSSF Mkoani Tanga.

DAWASCO YAWAKUMBUSHA WATEJA WAKE KULIPIA BILI ZA MAJI

Viewing all 110102 articles
Browse latest View live




Latest Images