Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109584 articles
Browse latest View live

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK. SHEIN AHUDHURIA MKUTANO WA BLUE ECONOMY KENYA LEO

0
0
 RAIS wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Uchumi Endelevu wa Bahari (Sustainable Blue Economy Conference) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta Jijini Nairobi Nchini Kenya leo 26/11/2018 na kuwashirikisha Marais mbalimbali wa Nchi za Afrika.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa kuhusiana na Uchumi Endelevu wa Bahari (Sustainable Blue Economy Conference ) uliofanyika katika ukumbi wa Kmataifa wa mikutano wa Kenyatta, akiwasilisha Tamko la Serikala ya Jamuhuri ya Muungano, akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli.katika mkutano huo uliofanyika leo 26/11/2018, jijini Nairobi Kenya.
 BAADHI ya Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa Unaozungumzia Uchumi Endelelevu wa Bahari (Sustainable Blue Economy Conference) uliofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Kanyatta Jijini Nairobi Kenya, leo 26/11/2018. Wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia Mkutano huo akitowa Tamko la Serikali ya Jamuhuri ya Muungano, akimuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Monica Juma, alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Kenyatta Jijini Nairobi kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Sustainable Blue Economy).
 BAADHI ya Washiriki kutoka Nchini mbalimbali wakiwasili katika viwanja vya Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Kenyatta Jijini Nairobi kuhudhuria Mkutano wa Uchumi Endelevu wa Bahari.(Picha na Ikulu)

Watanzania wajengewa uwezo wa kupata ajira Umoja wa Mataifa

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhani Mwinyi Muombwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi kutoka Umoja wa Mataifa, Bi. Huda Hanina ambaye yupo nchini kwa ajili ya kutoa Semina ya kuwajengea uwezo Watanzania kuhusu mbinu za kuomba ajira kwenye Umoja wa Mataifa. Balozi Mwinyi alipongeza hatua hiyo kwa kuwa Tanznaia licha ya kuwa ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kuchangia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa duniani, lakini idadi ya Watanzania waliojairiwa katika Sekretarieti ya umoja huo ni ndogo mno. 
Sehemu ya Uongozi wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania pamoja Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Hellen Maduhu wakifuatilia mazungumzo .
Sehemu nyingine ya watumishi wa Serikali wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Balozi Mwinyi na Bi. Hanani 
Mazungumzo yakiendelea. 
Balozi Mwinyi na Bi. Hanani wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi kutoka serikalini na Umoja wa Mataifa. 

TAKUKURU PWANI YAMFIKISHA MAHAKAMANI MTUMISHI DAWASA KWA KOSA LA KUOMBA RUSHWA

0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Pwani, imemfikisha mahakamani Romani Michael Jovin ambae ni  (volunteer surveyor )wa DAWASA kwa kosa la kuomba rushwa ya sh.70,000  na kupokea  ya kiasi cha sh.50,000 .

Mtuhumiwa huyo amejikuta akifikishwa kizimbani baada ya kwenda kinyume na kifungu cha 15(1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba. 11 ya mwaka 2007. Romani Michael ambaye alifunguliwa kesi ya jinai mamba 140 ya mwaka 2018 ni volunteer Surveyor DAWASA Ubungo.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya hakimu mkazi wilaya ya Kibaha  Herieth Mwailolo, mwendesha mashtaka wa TAKUKURU, Prisca Mpeka amedai,   mshitakiwa alitenda kosa la kuomba rushwa ya sh.70,000 na kupokea rushwa ya sh. 50,000 kutoka kwa mtoa taarifa  ili aweze kumsaidia mtoa taarifa kupata mita ya DAWASA.

Alidai  jambo hilo ni kosa kisheria kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa, sheria namba 11 ya mwaka 2007.

Aidha Prisca alidai , mshitakiwa alipokea rushwa ya kiasi cha sh.50,000 kutoka kwa mtoa taarifa, jambo ambalo pia ni kosa kisheria  kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa, namba 11 ya mwaka 2007. 

Mshitakiwa alikana makosa yote mawili na amerudihswa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana
Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 27/11/2018.

Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Pwani, Suzana Raymond anaendelea kuwaasa wananchi wote kufuata taratibu kanuni na sheria za nchi ili kuweza kwenda na kasi ya awamu ya tano chini ya Raisi dk. John Magufuli.

TAA NA KIKOSI CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI WAJADILI USALAMA WA USAFIRI WA ANGA

0
0

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imedhamiria kuleta mageuzi Makuu katika usalama wa usafiri wa Anga katika Kitengo cha Zimamoto na Uokoaji katika Viwanja 58 vilivyo chini yake vilivyo katika Mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara.

Katika kutimiza hilo TAA leo imefanya Kikao kazi kikiongozwa na Kusimamiwa na Kamishna Jenerali wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Afande Thobias Adengenye pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Lawrence Thobias na kuhudhuriwa na Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa
Vituo vya Zimamoto na Uokoaji Viwanja vya ndege Bara.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho muhimu, Afande Kamishna Andengenye amebainisha kwamba lengo kuu la kikao kazi hicho ni kuzitambua changamoto za kiutendaji lakini pia kuboresha na kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo.

“Lengo kuu ni kuzitambua changamoto zilizopo, lakini pia kuzipatia ufumbuzi changamoto hizi hii yote itaboresha mazingira ya kazi lakini pia kuimarisha na kuendeleza mahusiano yaliyopo baina ya Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji” alisema Afande Andengenye.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Afande Thobias Andengenye akizungumza na Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vituo vya Zimamoto na Uokoaji Viwanja vya ndege Bara katika kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Banana Ukonga Jijini Dar es Salaam.
 Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vituo vya Zimamoto na Uokoaji Viwanja vya ndege Bara Wakifuatilia Mada katika kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Lawrence Thobias (tatu kulia waliokaa), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Afande Thobias Andengenye (katikati) na  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu KADGO Mhandisi Martin Kanyamagoha wakiwa katika picha ya pamoja na Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vituo vya Zimamoto na Uokoaji Viwanja vya ndege Bara, waliohudhuria katika kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Lawrence Thobias (Mwenye suti ya Kijivu) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Afande Thobias Andengenye mara baada ya kuwasili katika jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) kwa ajili ya kikao Kazi na Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vituo vya Zimamoto na Uokoaji Viwanja vya ndege Bara.

DJ MKONGWE ZAIDI DUNIANI

0
0
SUMIKO Iwamura mwanamke(83) kutoka nchini China ndiye Dj mzee zaidi duniani ambaye hadi sasa anafanya shughuli hiyo.

Sumiko Iwamura maarufu kama Dj Sumirock alizaliwa Januari 23, 1934 na alikuwa na ndoto za kuwa mtu maarufu duniani kote lakini baada ya baba yake kufungua mgahawa alienda kusaidia hapo mara baada ya kumaliza shule.Dj. Sumirock alienda shule na kujifunza fani hiyo akiwa na miaka 77 na kuanza kufanya kazi hiyo mara mbili kwa mwezi huku akiendelea na kazi ya kuuza mgahawa.

Akiwa na ndoto za kusafiri duniani kote Dj. Sumirock amesafiri katika nchi mbalimbali zikiwemo Paris na Newzealand huku akieleza kupendezwa za muziki wa Jazz na Rock.

Alipoulizwa na jarida la Guiness World Report kuhusiana na fani hiyo alieleza kuwa, "Ninafikiri nilizaliwa na kipaji hiki na huwa sifanyi mazoezi kwa ajili ya afya ila ninapopiga muziki naona nafanya kitu cha tofauti, nahisi nna nguvu" ameeleza Dj. Sumirock.

Kuhusiana na vijana wanaopambana kutimiza ndoto zao Dj. Sumirock alinukuliwa akisema kuwa, "Nafasi zipo kila siku, wasikate tamaa na daima wasisite kujaribu kitu" alieleza.Dj. Sumirock ana ndoto za kusafiri duniani kote kwa kazi yake ya kupiga muziki.
Dj. Sumirock akifanya mambo yake

MICHUZI TV: WAJIKI KUADHIMISHA SIKU 16 KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA DUNIANI

MICHUZI TV KAULI YA HAJI MANARA KUHUSU UCHAGUZI WA YANGA SC..

WADAU WA SEKTA YA AFYA KUENDELEA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA NCHINI

0
0

NA WAJMW-DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea kuboresha huduma afya nchini kwa kukarabati vituo vya afya vipatavyo 350 ili  utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto hususani  huduma za dharura wakati wa kujifungua.
Hayo yamesemwa leo na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ya afya wa kujadilia njia zitakazowezesha kufikia malengo na vipaumbele vya kisera vya mwaka 2019/2020 uliofanyika mapema  jijini Dodoma.
“Sekta ya afya tunaona inaendelea kupiga hatua kubwa sana katika maeneo mbalimbali ikiwemo suala la kuimarisha miundombinu ambapo vituo vya Afya takribani 350 vimekarabatiwa kwa  kuongeza miundombinu kwa ajili ya kutoa huduma za afya za dharura ikiwemo huduma za kumtoa mtoto tumboni”.
Waziri Ummy amesema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo duniani inahakikisha sekta ya afya inapata mafanikio kwa kuboresha huduma nchini ikiwemo na kufikia asilimia zaidi ya 90 ya dawa zinapatikana katika sehemu zote za kutoa huduma.
Aidha, Waziri Ummy amesema mkutano huo ulikua na lengo la kukubaliana kutekeleza vipaumbele nane (8) ambavyo serikali pamoja na wadau wa maendeleo itahakikisha vinatekelezwa ipasavyo katika mwaka 2019/2020.
Maeneo hayo ni pamoja na Kuimarisha huduma za afya ya uzazi ,mama na mtoto ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, kwa kuweka miundombinu ya huduma za uzazi wa dharura na watoto wachanga kwani kwa takribani hivi sasa watoto wachanga wapatao elfu tisini hufariki ndani ya siku ishirini na nane (28) za mwanzo. Kuongeza huduma za uzazi salama sambamba na uzazi wa mpango, kupunguza maambukizi ya UKIMWI kutoka mama kwenda kwa mtoto.
Eneo la pili linahusu Afya za wasichana na wavulana walio katika umri wa kubalehe ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kuepuka ngono katika umri mdogo na mimba zisizotarajiwa.
Alitaja eneo jingine  ni kuongeza nguvu kazi katika sekata ya afya ikiwa ni pamoja na kuajiri watumishi wa afya katika ngazi zote, kuongeza ujuzi kwa kutoa nafasi za kusomesha watumishi ili kukidhi vigezo vilivyoweka na shirika la afya duniani (WHO).
Kipaumbele cha Nne, ni kuimarisha ubora wa huduma za afya utakaoenda sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya sehemu za kutolea huduma za afya za serikali pamoja na kuongeza rasilimali fedha kwa ajili ya kutatua changamoto za afya kwa kuongeza  ya bajeti ya afya   kutoka kutoka Bilioni 31 hadi Bilioni 270 mwaka 2018/2019.
Naye Naibu katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia afya dkt.Zainabu Chaula amesema kwamba wao kama sehemu ya utekelezaji wamejipanga kutekeleza maboresho ya afya ngazi ya msingi kuanzia vijijini hadi Taifa kupitia sera ya afya hivyo wamejipanga kuongeza kutoa elimu ya afya kwa umma kuanzia zahanati  kwa kupanga mipango endelevu ili iende sambamba kuanzia ngazi husika kwa kutumia kamati za afya kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.  
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali wa maendeleo na wakurugenzi wa wizara (Hawapo Pichani) wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ya afya wa kujadilia njia zitakazowezesha kufikia malengo na vipaumbele vya kisera vya mwaka 2019/2020 uliofanyika jijini Dodoma.
 Wakurugenzi mbalimbali kutoka wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakimsikiliza Waziri wa wizara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu (Hayupo Pichani) katika mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ya afya wa kujadilia njia zitakazowezesha kufikia malengo na vipaumbele vya kisera vya mwaka 2019/2020 uliofanyika jijini Dodoma
 Wadau mabalimbali wa maendeleo wakifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokua yanaendelea katika mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ya afya wa kujadilia njia zitakazowezesha kufikia malengo na vipaumbele vya kisera vya mwaka 2019/2020 uliofanyika jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (Katikati) akisaini makubaliano ya malengo na vipaumbele vya kisera vya mwaka 2019/2020. Kushoto ni Naibu Katibu mkuu anayeshughulikia ya Afya TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula na Kulia ni Mwakilishi wa wadau wa maendeleo.

VIDEO: Meshack Salum Nasogea( official Gospel video)

Amber Rutty na Mpenzi wake waendelea kusota rumande,upelelezi wa kesi yao bado haujakamilika

0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Wakati Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Ruty na mpenzi wake Said Kitomali wakiendelea kusota rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana, katika kesi inayowakabili ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile upelekezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Amber Ruty na Said wanashtakiwa pamoja na James Charles maarufu kama 'James Delicious' ambaye yeye yupo nje kwa dhamana.kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Amber Rutty alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine, Rwizile kuwa mdhamini wake mmoja amefika mahakamani hapo lakini mwingine bado hajafika.

Hata hivyo, Hakimu Rwizile  amemwambia Amber Rutty kwamba dhamana ipo wazi na shughuli za mahakama zinaisha saa 9 alasiri hivyo wadhamini wake wakikamilika atadhaminiwa.Kesi  hiyo imeahirisha hadi Decemba 10,2018.

Katika kesi hiyo, Amber Ruth,  anadaiwa kufanya mapenzi kinyume na maumbil kosa analodaiwa kulitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, 

Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Ruth kinyume na maumbile.Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya October 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Katika shtaka la nne ambalo ni kusababisha kusambaa kwa picha za ngono linamkabili Amber Ruth na Said Aboubakary ambapo wanadaiwa kati ya 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kweli.Amber  Rutty na mpenzi wake ili waweze kuwa nje kwa dhamana wanatakiwa kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini 2 ambapo kila mtu atasaini bondi ya Shilingi Milioni 15.

Pia wadhamini wawe na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati zenu za kusafiria na msitoke nje ya Dar es Salaam bila ruksa.
Pichani kati Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Ruty akirudishwa rumande huku upelelezi wa kesi yao bado haujakamilika

Your support is needed at the Dhow Countries Music Academy in Zanzibar

0
0
Change Lives in Zanzibar through Music
We are raising funds
Help us reach the target of
$9,000
By December 31, 2018
We want to give 30 young people with talent a chance to grow through music education at Dhow Countries Music Academy, the only music school in Zanzibar.
Please Support us....
https://www.globalgiving.org/donate/52009/dhow-countries-music-academy/

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chamilla akagua madhala ya mbolea ya DSM jijini Dar es salaam

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chamilla (Kushoto) akimisikiliza   Afisa Mkuu wa fedha wa GSM Tanzania,Benson Mahenya(kulia) alipokuwa akimfafanulia jambo kuhusiana na  ubora wa mbolea za Kampuni hiyo,Wakati alipofanya ziara ya kikazi katika maghala ya kuhifadhia mbolea za kilimo  za kampuni hiyo yaliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu na Afisa Mkuu wa Biashara,Remmy Nindi
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya , Albert Chamilla (Kulia) akimisikiliza   Afisa Mkuu wa Biashara wa GSM Tanzania,Remmy Nindi (kushoto)alipokuwa akimfafanulia jambo  juu ya uhifadhi wa mbolea za Kampuni hiyo, wakati wa ziara ya kikazi katika maghala ya kuhifadhia mbole za kilimo  yaliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. Katikati Afisa Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo,Benson Mahenya.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chamilla (Kulia) akikagua mbolea ya kukuzia mimea ya aina ya DAP katika maghala ya kuhifadhia mbolea za kilimo za GSM Tanzania,Yaliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hizo mwishoni mwa wiki,Kushoto ni  Afisa Mkuu wa biashara wa kampuni hiyo,Remmy Nindi na Afisa Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo,Benson Mahenya
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chamilla (Kulia) akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufanya  ziara ya kikazi katika maghala ya kuhifadhia mbolea za kilimo za GSM Tanzania yaliliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.  Kutoka kushoto ni Afisa Mkuu wa Biashara wa GSM Tanzania,Remmy Nindi na Afisa Mkuu wa fedha wa GSM Tanzania, Benson Mahenya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chamilla akiagwa baada ya kufanya ziara ya kikazi katika maghala ya kuhifadhia mbolea za kilimo  za kampuni hiyo yaliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

TAARIFA YA HABARI YA ITV SAA MBILI USIKU NOVEMBA 26, 2018

TFS YAWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI 11 KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO

0
0

Serikali kupitia Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imewasimamisha kutekeleza majukumu yao watumishi 11 wa TFS walioonekana kutenda makosa mbalimbali. Kati yao watatu wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya uhujumu uchumi sambamba na watu wengine wawili.

Aidha, Serikali imezuia biashara ya mti wa Mkurungu kwa matumizi ya ndani au kusafirishwa nje ya nchi hadi hapo itakapotolewa taarifa nyingine.

Kusimamishwa kwa watumishi hao kunafuatia kubainika kwa uwepo wa magogo yaliyovunwa kinyume cha sheria na kutelekezwa katika maeneo mbalimbali kwenye vijiji na msituni kufuatia

va na Kikosi kazi cha kuzuia ujangili kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na kubaini baadhi ya watumishi kuonekana kushiriki katika uhalifu huo.

Kufuatia uchunguzi uliofanywa, gari moja lilikamatwa likiwa na mbao (slippers) 382 za mti wa Mkurungu na kuzuiliwa kwa uchunguzi ambapo watuhumiwa wawili walikamatwa. Aidha, mbao 825 zilikamatwa zikisafirishwa kwa treni katika stesheni ya Usule, Shinyanga na watuhumiwa 6 ambao ni watumishi wa shirika la reli kukamatwa kwa mahojiano.

Ili kudhibiti tatizo hili, uongozi wa Kikosi cha Taifa cha kuzuia Ujangili (NTAP), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ulikutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Tabora (KUU) na kufikia maamuzi yafuatayo:

ITUMIENI FURSA YA MSAADA WA KISHERIA KUTAMBUA HAKI ZENU- PROF. KABUDI

0
0

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amewataka wananchi kutumia fursa ya huduma za msaada wa kisheria ambayo inatolewa nchini ili kutambua haki zao na kuzipata kwa wakati.

Amesema wananchi wakiitumia huduma ya msaada wa kisheria itawawezesha kutambua haki zao na kuzipata kwa wakati , kufahamu sheria mbalimbali ikiwa ni pamoja na utaratibu unaotumiwa na Mahakama na hivyo kusaidia harakati za kupunguza msongamano Mahakamani.

 “Wananchi niwaombe mtumie fursa ya msaada wa kisheria ambayo Serikali imeridhia itolewe kwa wananchi wenye uhitaji, hii itasaidia kutambua haki zenu, kufahamu sheria na utaratibu unaotumika na Mahakama na hivyo kusaidia kupunguza msongamano Mahakamani” alisema Prof. Kabudi.

Prof. Kabudi amesema hayo mjini Morogoro alipokuwa akizindua maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria nchini ambayo inafanyika katika mikoa ya Morogoro, Singida, Tabora, Kagera na Kigoma kuanzia tarehe 26 Novemba hadi tarehe 30 Novemba ,2018. 

Amesema Wizara itaendela kutenga wiki moja kila mwaka kwa ajili ya kutoa msaada wa kisheria nchini ili kuhakikisha wananchi wengi wanafikiwa na huduma za msaada wa kisheia na hivyo kutimiza lengo la kutungwa kwa Sheria Na. 1 ya Msaada wa Kisheria ya Mwaka 2017.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akimpa mkono msanii Afande Sele baada ya kumaliza kutumbuza katika hafla ya ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria nchini uliofanyika mkoani Morogoro 
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiangalia kitabu katika moja ya mabanda yaliyohudhuria uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria mkoani Morogoro , Prof. Kabudi alitembelea mabanda hayo baada ya kuzidua maadhimisho hayo mjini Morogoro 
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza katika banda la Mahakama ambalo linashiriki maadhimisho ya wiki ya Msaada wa kisheria nchini ambayo ufunguzi wake kitaifa ulifanyika mkoani Morogoro uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria mkoani Morogoro 
Wananchi waliofika kupata huduma ya msaada wa kisheria wakati wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria nchini katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe wakati wa uzinduzi wa wiki hiyo mjini Morogoro. 
Wanasheria wa kujitegemea mkoani Morogoro katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe wakati wa uzinduzi wa maadhimisho y awiki ya msaada wa kisheria nchini uliofanyika mkoani Morogoro . 



TUMEKUSUDIA KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA KWENYE SEKTA YA KILIMO-MHE HASUNGA

0
0


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Serikali imedhamiria kufanya mageuzi makubwa katika Sekta ya Kilimo ambapo Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara za Sekta ya Kilimo (ASLMs) na wadau wa kilimo inatekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (Agricultural Sector Development Programme Phase Two-ASDPII).

Katika utekelezaji wa ASDP II serikali imelenga kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo (mazao, mifugo na uvuvi) ili kuongeza uzalishaji na tija, kufanya kilimo kiwe cha kibiashara na kuongeza pato la wakulima wadogo kwa ajili ya kuboresha maisha na usalama wa chakula na lishe.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 26 Novemba 2018 wakati akifungua warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania inayofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam.

Alisema Utekelezaji wa lengo hilo ni kuhakikisha kuwa Taifa linaendelea kujitosheleza kwa chakula; kuimarisha uchumi; kuwa kichocheo cha kukua kwa viwanda; na kuongeza ajira ambapo ili kufikia malengo hayo; Utekelezaji wa ASDP II utazingatia mnyororo wa thamani wa mazao ya kipaumbele ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Mhe Hasunga alisema kuwa Serikali itaendelea kuboresha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima na wafugaji na kwa bei nafuu.


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza umuhimu wa sekta binafsi nchini wakati akifungua warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam tarehe 26 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo) 
Sehemu ya Wadau wa Kilimo na Mifugo nchini wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akifungua warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam tarehe 26 Novemba 2018. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua bidhaa zilizoongezwa thamani ndani ya nchi wakati wa hafla ya warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam tarehe 26 Novemba 2018. Kulia ni Maryam Issa mtendaji wa Kampuni ya NatureRipe. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati akifungua warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam tarehe 26 Novemba 2018.

Waziri Kamwelwe aomba subira kwa TBA

0
0

Aridhishwa ujenzi wa Ihungo Boys

WAKATI Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe ameomba taasisi za serikali, Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wizara, ambazo zimeipa kazi Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA), kuwa na subira kwa kuwa inaupungufu wa wafanyakazi, lakini ameridhishwa na ujenzi wa shule ya sekondari ya Wavulana ya Ihungo ya mkoani Kagera iliyojengwa na taasisi hiyo.

Akifafanua Mhe. Kamwelwe amesema TBA wanakumbwa na changamoto kubwa ya upungufu wa wafanyakazi, ambapo kwa Tanzania nzima wanawafanyakazi 300 pekee, ambao wanajitoa kwa kufanya kazi kwa bidii, ambapo idadi kamili inayotakiwa ni wafanyakazi 1700.

Hatahivyo, ameipongeza TBA kwa kufanya kazi nzuri za ujenzi mbalimbali za majengo ya serikali kwa kutumia thamani halisi ya fedha tofauti na wakandarasi binafsi wamekuwa na gharama kubwa.

“Utendaji wa TBA bado unaleta mashaka nchi nzima na nimefanya nao kikao nikabaini wapo wafanyakazi 300 pekee na wanatakiwa angalau 1000 ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, hivyo nashauri pamoja na kusikia malalamiko kila upande kutoka kwa Wakuu wa Wilaya, Mikoa, Bungeni na Watendaji wengine wa serikali, ninayafanyia kazi likiwemo la uhaba wa wafanyakazi,” amesema Mhe. Kamwelwe.


Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA) mkoa wa Kagera, Mhandisi Herico Bahati (mwenye shati la batiki) akimpa maelezo mbalimbali Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kushoto) kuhusiana na ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo, waliyoijenga baada ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016. Mbele ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Philip Boniventura. 
Waziri Mkuu wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (mwenye suti ya bluu) akimsikiliza Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA) mkoa wa Kagera, Mhandisi Herico Bahati (mwenye shati la batiki) akimpa maelezo mbalimbali ndani ya moja ya vyumba 96 vya mabweni ya shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo, waliyoijenga baada ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016. 
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Wavulana ya Ihungo na wa shule ya sekondari Bukoba, wakinawa mikono katika mabomba ya kisasa, ambayo yamejengwa na Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA) baada ya shule hiyo kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016. 


KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 27,2018

WAZIRI MHAGAMA ATEMBELEA KIWANDA CHA MATAIRI CHA GENERAL TYRE ARUSHA

0
0


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiangalia moja ya tairi lilipo katika kiwanda cha Matairi cha General Tyre Arusha wakati wa ukaguzi wa Miradi yenye hisa NSSF tarehe 26 Novemba, 2018.  
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiangalia malighafi zinazotumika kutengeneza matairi na zilizohifadhiwa katika chumba maalumu katika kiwanda hicho.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja na Watendaji kutoka NSSF na baadhi ya viongozi wa kiwanda cha Matairi cha General Tyre wakiangalia hali ya miundombimu katika kiwanda hicho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiuliza jambo kwa Mkurugenzi wa Uwekezaji NSSF Bw.Gabriel Silayo (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara yake katika moja ya mradi wenye hisa za shirika hilo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (katikati) akiwa katika ziara yake katika kiwanda cha matairi cha General Tyre Arusha.wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji NSSF Bw.Gabriel Silayo. 
Viewing all 109584 articles
Browse latest View live




Latest Images