Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

OPERESHENI KOROSHO YAZIDI KUNUFAISHA WAKULIMA WA MIKOA YA KUSINI

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, Rukia Muwango (wa pili kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Market Watch Co. Ltd anayesimamia wa Ghala la kuhifadhia korosho la Lindi –Nachingwea Farmers Msafiri Zombe (wa pili kushoto) kuhusu hali ya upokeaji na usafirishaji wa korosho katika Ghala hilo wakati wa ziara yake aliyoifanya Ijumaa Novemba 23, 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, Rukia Muwango (mbele) akizungumza na Uongozi wa Umoja wa Akina Mama wanaotoa huduma ya chakula kwa wabebaji na washushaji wa zao la korosho katika Ghala la Lindi-Nachingwea Farmers waliofika mbele yake kwa ajili ya kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili mara baada ya kufanya ziara katika Ghala hilo Ijumaa Novemba 23, 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Rukia Muwango akitazama orodha ya majina ya wabebaji na washushaji aliyopatiwa na Uongozi wa wapokeaji na washushaji wa zao la korosho katika Ghala la kuhifadhia zao la korosho la Lindi-Nachingwea Farmers wa waliofika mbele yake kwa ajili ya kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili mara baada ya kufanya ziara katika Ghala hilo Ijumaa Novemba 23, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, Rukia Muwango akizungumza na watoa huduma ya ushushaji na upakiaji wa shehena ya zao la korosho katika Ghala la Lindi-Nachingwea Farmers waliofika mbele yake kwa ajili ya kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili mara baada ya kufanya ziara katika Ghala hilo Ijumaa Novemba 23, 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, Rukia Muwango akizungumza na Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati alipofanya ziara katika Ghala la kuhifadhia zao la korosho la Lindi-Nachingwea Farmers Ijumaa Novemba 23, 2018 kujionea hali halisi ya zoezi la usafirishaji wa korosho kuelekea katika Maghala Makubwa yaliyopo Mkoani Mtwara.
Katibu Mtendaji Mkuu wa Chama cha Ushirika wa Msingi cha Makanjiro AMCOS kilichopo Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, Rashidi Chihope akionesha nakala ya orodha ya majina ya wanachama wa Chama hicho wakulima wa zao la korosho waliolipwa na Serikali kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) sehemu ya taarifa ya kifedha kutoka Benki ya NMB Ijumaa wiki iliyopita.

WAZIRI WA KILIMO ATANGAZA KIAMA KWA WASAMBAZAJI WA MBEGU FEKI

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Morogoro

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga, 24 Novemba 2018 ametangaza kiama kwa wafanyabiashara wa mbegu nchini wanaouza Mbegu feki zilizopigwa marufuku na serikali.

Amewataka wafanyabiashara wote wa mbegu ambao wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa kuwauzia wakulima mbegu feki zilizopigwa marufuku na serikali kuacha haraka iwezekanavyo kwani serikali itawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kukiuka maagizo ya serikali.

Ametoa agizo hilo akiwa ziarani Mkoani Morogoro ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Taasisi iliyopewa jukumu na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la usajili wa wafanyabiashara wa mbegu (Seed Dealers). “Serikali imepokea malalamiko mengi kwa wananchi kuhusu Ubovu wa mbegu jambo ambalo limepelekea kwa kiasi kikubwa kuwa na mavuno kidogo pasina kukidhi matakwa ya wakulima wetu nchini” Alikaririwa Mhe Hasunga

Waziri huyo pia ameiagiza Taasisi ya udhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) kutimiza majukumu yao kwa kuwabaini wafanyabiashara wanaokiuka maagizo ya serikali pamoja na taratibu na sheria za nchi. “Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu mbegu feki jambo hili serikali haiwezi kukubaliana nalo hivyo TOSCI wanapaswa kusimamia kwa weledi ukaguzi na usajili wa Mbegu bora, pia ni lazima kuwabaini wasambazaji feki wa mbegu ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao” Alisisitiza Mhe Hasunga

Alisema Wizara ya Kilimo imepewa jukumu mahususi la kuhakikisha sekta ya kilimo inaimarika kwa usimamizi madhubuti wa sera, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali hivyo kunapokuwa na kelele za wananchi kuhusu mbegu feki ni dhahiri kuwa Taasisi zenye jukumu hilo hazitekelezi kazi yake kwa weledi.

Mhe Hasunga alieleza kuwa serikali imejipanga kuhakikisha kuwa inaongeza thamani ya mazao yote yanayozalishwa nchini, sambamba na kutafuta masoko mazuri. Vilevile, ameitaja Wizara ya Kilimo kuwa ina wataalamu wengi hivyo unaandaliwa mfumo mzuri wa kuwaunganisha watalaamu hao ili kujadili kwa pamoja namna ambavyo kilimo kinaweza kubadilika kutoka kilimo cha kujikimu na kuwa kilimo cha kibiashara ili kutoa malighafi za kutosha zitakazohuisha serikali ya viwanda.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua Maabara ya
Kutazama kiwango cha Uotaji wa Mbegu wakati wa ziara yake ya kikazi MkoaniMorogoro alipotembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), tarehe 24 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo) .

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga, 24 Novemba 2018 ametangaza kiama kwa wafanyabiashara wa mbegu nchini wanaouza Mbegu feki zilizopigwa marufuku na serikali.

Amewataka wafanyabiashara wote wa mbegu ambao wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa kuwauzia wakulima mbegu feki zilizopigwa marufuku na serikali kuacha haraka iwezekanavyo kwani serikali itawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kukiuka maagizo ya serikali. 


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua shamba la mahindi wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro alipotembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), tarehe 24 Novemba 2018.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) Ndg Patrick Ngwediagi akitoa taarifa ya Taasisi hiyo mbele ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga tarehe 24 Novemba 2018.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua bustani ya nyanya wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro alipotembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), tarehe 24 Novemba 2018. 

MICHUZI TV: Wanaoisema vibaya Dodoma kuhusu mapato WATAPATA TABU SANA: Kunambi

DARAJA LA MTO MARA KUKAMILIKA JANUARI

$
0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Elias John Kwandikwa ameutaka muungano wa Makampuni mawili ya kizalendo ya M/S Gemen Engineering Construction Co. Ltd na Mayanga Constractors Co. Ltd yanayojenga daraja la mto Mara kukamilisha ujenzi huo Januari mwakani.

Amesema Serikali haitawaongezea muda katika kazi hiyo hivyo wahakikishe daraja hilo pamoja na barabara za maingilio zinakamilika kwa wakati na ubora unaostahili. “Hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii na weledi ili Serikali izidi kuwaamini na kuwapa miradi mingi zaidi wakandarasi wazawa na hivyo kukuza ujuzi na uchumi wa nchi”, amesema Mhe. Kwandikwa.

Daraja la mto Mara lenye urefu wa mita 94 ambalo linaunganisha Wilaya za Tarime na Serengeti ujenzi wake unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 8.5 na ni miongoni mwa madaraja mawili makubwa yanayopitiwa na mto Mara unaoanzia katika kijiji cha Masai Mara nchini Kenya kuelekea Ziwa Victoria, daraja jingine ni Kirumi lenye urefu wa mita 223.3 lililojengwa mwaka 1985.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa amekagua kiwanja cha ndege cha Musoma na kusisitiza kuwa Serikali itakijenga kiwanja hicho ili ndege nyingi zaidi ziweze kukitumia na kuhuisha uchumi wa mkoa wa Mara. Amesema ujenzi wake ukikamilika utafungua uchumi wa mji wa Musoma na mkoa wa Mara kwa ujumla kwani utavutia watalii wengi kufika katika vivutio vya mkoa huo ikiwemo hifadhi ya Serengeti.

Naye Mkuu wa mkoa wa Mara Bw, Adam Malima amemhakikishia Naibu Waziri Kwandikwa kuwa kufunguka kwa barabara, madaraja na uwanja wa ndege mkoani humo kutahuisha uchumi wa mkoa huo. Meneja wa kiwanja cha ndege cha musoma bwana Shadrack Chilongani amesema kiwanja cha ndege hicho ambacho kiko daraja la tatu C kina urefu wa mita 1,600 na upana wa mita 30 hivyo uboreshaji wake utakapokamilika utakipandisha daraja na kukiwezesha kuongeza miruko ya ndege na abiria na hivyo kukuza utalii wa mkoa wa Mara.

Sehema ya chini ya daraja la mto Mara lenye urefu wa mita 94, mto Mara unaoanzia katika kijiji cha Masai Mara nchini Kenya maji yake huelekea na kuishia Ziwa Victoria upande wa Tanzania.

Muonekano wa daraja la mto Mara lenye urefu wa mita 94 na barabara ya maungio ambayo ni sehemu ya barabara ya Tarime-Mugumu ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea.


Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw, Adam Malima (wa pili kushoto), akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (wa pili kulia), eneo litakaloongezwa katika upanuzi wa njia ya kurukia ndege katika kiwanja cha ndege Musoma alipokagua kiwanja hicho (kushoto), ni Kaimu Meneja TANROADS Mara Mhandisi Reginald Masawe na (kulia) ni Meneja wa kiwanja cha ndege cha Musoma Bw, Shadrack Chilongani.

WFP Yakubali Kuipa Nguvu Wizara ya Kilimo

$
0
0
Naibu Waziri wa Kilimo nchini Mheshimiwa Innocent Bashungwa amekutana na muwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Michael Dunford na mkuu wa usambazaji wa shirika hilo Riaz Lodhi katika ofisi za wizara hiyo jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kuboresha ushirikiano baina ya Serikali na shirika hilo.  

Katika kikao hicho ndugu Michael Dunford alielezea namna WFP imekuwa ikishirikiana na serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya kilimo kupitia miradi mbalimbali ikiwemo ya kuboresha lishe, kuongeza thamani ya mazao, utafiti na ubunifu katika kilimo na pia katika masoko.

Alimuhakikishia Mheshimiwa Bashungwa kuwa shirika la WFP lina nia ya dhati ya kumkomboa mkulima wa Tanzania ikiwa ni sehemu ya Malengo Endelevu ya Dunia (SDG) ya kutokomeza njaa ulimwengu ni kuishukuru Serikali kwa ushirikiano ambao imekuwa ikilipatia katika kutimiza majukumu yake. 

Nae Naibu Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Innocent Bashungwa amemueleza muwakilishi huyo nia ya Serikali ya kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri ya mazao ndani na nje ya nchi ambapo shirika la WFP limekubali kununua tani laki moja na nusu ya mahindi toka ghala la taifa na kuahidi kununua nyingine. Pia Mheshimiwa Bashungwa alimuhakikishia kuwa serikali itaendelea kurekebisha na kuboresha baadhi ya sheria ili kurahishisha biashara ya mazao nje ya nchi.  


Katika kikao hicho pia kilihudhuriwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba na Elimpa Kiranga (Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Chakula.
Naibu Waziri wa Kilimo Ndugu Innocent Bashungwa akijadiliana na wawakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Michael Dunford na Riaz Lodhi katika ofisi za Wizara ya Kilimo jijini Dar es Salaam

Kutoka kulia: Riaz Lodhi (Mkuu wa Kitengo cha Mnyororo wa thamani WFP), Michael Dunford (Muwakilishi wa Shirika la WFP), Naibu Waziri Kilimo Mheshimiwa Innocent Bashungwa, Bi Vumilia Zikankuba na Elimpa Kiranga katika picha ya pamoja baada ya kikao 

WANANCHI WANAOISHI KANDO YA MITO WAACHE KUHARIBU VYANZO VYA MAJI- MHANDISI KALOBELO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WANANCHI wanaoishi karibu na vyanzo vya maji wameswa  na serilali  kuvilinda na kuvitunza kwa kuacha kufanya shughuli za kijamii. kwenye maeneo hayo.


Hayo yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanule Kalobelo wakati wa ziara yake katika mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Juu.Akizungumza baada ya kukamilisha ziara yake kwenye mtambo wa Ruvu Juu, Mhandisi Kalobelo amesema wananchi wanatakiwa kuvitunza vyanzo vya maji ili maji yaendelee kuwepo kwa matumizi ya kila siku.

Amesema, chanzo kikuu cha maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni mto Ruvu, kukiwa na Ruvu juu na Ruvu chini na wananchi wanazidi kuongezeka karibia na mto huo."Wananchi wanazidi kuongezeka kwenye maeneo ya vyanzo vya maji ikiwemo Mto Ruvu ambao ndio chanzo kikuu cha maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam, na katikka sheria za mazingira inawataka wananchi wakae mita 60 kutoka kwenye mto,"amesema Mhandisi Kalobelo.

Ameeleza kuwa, wananchi wanaoishi kando ya maeneo hayo wanatakiwa kuacha kupanda miti inayonyonya maji au kutumia maji mengi bali wanatakiwa kupanda miti inayovutia maji kuwepo kwenye  vyanzo hivyo.

Mbali na hilo, Mhandisi amesema shughuli za kijamii ikiwemo kilimo na ufugaji vinaweza kusababisha kuharibu vyanzo vya maji na kusababisha kukosekana kwa maji ambapo kwa sasa maji yapo kwenye wastani unaowatosheleza wananchi wa Dar es Salaam kwa asilimia kubwa.

Aidha, katika ziara hito, Naibu Katibu Mkuu aliambatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja na Mkurugenzi wa Usafu na Mazingira wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Mjumbe wa bodi ya DAWASA Mhandisi Nadhifa Kemikimba.Mhandisi Kalobelo ametemebelea maeneo mbalimbali ya miradi ya ujenzi wa matenki na upanuzi wa mtambo utakaofanikisha kupatikana kwa maji kwenye maeneo yalioyokuwa hayapo kwenye mtandao hapo awali.

Amewapongeza DAWASA  kwa jitihada wanazozionyesha kwa kuhakikisha wananchi wanapata maji na ametoa rai kwa wananchi wajiunge kwenye mradi huu ili wapate maji safi na salama.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanule Kalobelo  akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa ameambata na Mkurugenzi wa Usafi na Mazingira wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Mjumbe wa bodi ya DAWASA Mhandisi Nadhifa Kemikimba.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanule Kalobelo  akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa pili kulia)  wakati alipotembelea Chanzo cha uzalishaji maji cha Ruvu Juu katika ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya DAWASA.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanule Kalobelo  akielezea jambo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja  na Mkurugenzi wa Usafi na Mazingira wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Mjumbe wa bodi ya DAWASA Mhandisi Nadhifa Kemikimba.

DK. SHEIN ZIARANI KENYA

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, wakati akielekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Salum Maulid Salum katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume, wakati akielekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na wakuu wa Vikosi vya ulinzi na usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume, wakati akielekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume, wakati akielekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.(PICHA NA HAROUB HUSSEIN

WACHORAJI JENGO LA ABIRIA MWANZA AIRPORT WAHARAKISHWA

$
0
0

WACHORAJI wa jengo jipya la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, wametakiwa kuharakisha ili serikali itangaze zabuni ujenzi uanze haraka.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema jana mkoani hapa alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kiwanja hicho ambayo ipo kwenye maboresho makubwa.

Mhe. Kamwelwe amesema kukamilika kwa michoro hiyo ya jengo la kisasa kutasaidia serikali kupitia wasimamizi wa ujenzi huo Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kutangaza zabuni na kupatikana kwa mkandarasi atakayejenga jengo hilo. “Kiwanja cha ndege kinashughuli nyingi na jengo la abiria ni kityu muhimu sana, hivyo ninaharakisha hao wachoraji wajitahidi kufanya haraka ili kukamilisha michoro hiyo,” amesisitiza Mhe. Waziri.

Hatahivyo, amesema ameridhishwa na mradi wa ujenzi wa jengo la mizigo ambalo lipo mita chache kutoka eneo la abiria, ambapo ndege za mizigo zimejengewa maegesho yake rasmi tofauti na awali zilikuwa zikishusha upande wa ndege za abiria. Halikadhalika ametembelea jengo la kisasa la kuongozea ndege, ambalo nalo limekamilika kwa asilimia 90 na kuridhishwa na utendaji wa Mhandisi Mkazi, Godfrey Asulumenye wa Kampuni ya Unetec ya Dubai, pamoja na eneo linapojengwa rada. 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe jana  akipata maelezo ya ujenzi wa Jengo la mizigo la Kiwanja cha Ndege cha Mwanza kutoka kwa Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Unetec ya Dubai, Geofrey Asulumenye (aliyenyoosha mkono. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Prof. Ninatubu Lema. 
Baadhi ya vyumba katika jengo la mizigo la Kiwanja cha Ndege cha Mwanza ambalo linaendelea kujengwa, jana Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alitembelea na kuridhika na maendeleo ya ujenzi.
Mhandisi Simon Makoye (mwenye kofia ngumu), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati), mchoro wa eneo linapojengwa rada, jana alipotembelea na kukagua maendeleo ya miradi inayoendelea kwenye Kiwanja cha Ndege cha Mwanza. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akimsikiliza 
Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Unetec ya Dubai, Geofrey Asulumenye (kushoto) wakatii akimpa maelezo mbalimbali ya ujenzi wa Jengo la kuongozea ndege la Kiwanja cha Ndege cha Mwanza wakati alipofanya ziara jana. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) YA Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Prof. Ninatubu Lema (kulia), akiongozana na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Mwanza, Mhandisi Marwa Rubilya wakiambatana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe aliyetembelea kukagua maendeleo ya miradi kwenye kiwanja cha Ndege cha Mwanza. PICHA ZOTE KWA HISANI YA TAA .


MIAKA MITATU YA MAPINDUZI YA KIFIKRA KATIKA SEKTA YA MADINI

MAJALIWA AZINDUA KAMPENI YA SIKU 16 YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA JIJINI DODOMA

$
0
0



*Ni dhiri ya wanawake na watoto katika jamii kwa silimia 50 ifikapo 2022

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeandaa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwa lengo la kupunguza kiwango cha ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.

Amesema mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000); Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Jinsia (2005); Sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008); Sheria ya Makosa ya Kujamiiana – SOSPA (1998).

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Novemba 25, 2018) wakati akizindua Kampeni ya siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsiakatika Uwanja vya Jamhuri jijini Dodoma. Amesema katika kukabialia na ukatili wa kijinsia Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imekuwa ikichukua hatua mbalimbaliza kuzuia na kutokomeza ukatili.

Waziri Mkuu amesema utekelezaji wa mpango huo utachangia katika utekelezaji wa mipango na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa kuhusu usawa wa kijinsia, uwezeshaji wanawake na wasichana pamoja na haki na ustawi wa mtoto.

Kadhalika Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaagiza Wakuu wa Mikoa wote wahakikishe wanasimamia uanzishwaji wa Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto za ngazi za Mikoa, Halmashauri, Kata na Vijiji kama inavyoelekezwa katika Mwongozo wa uratibu wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.

“Vilevile, nawaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuanzisha Programu za Kijamii za kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Halmashauri husika zitakazozingatia hali halisi na kuzitengea bajeti programu hizo kama inavyoelekezwa kwenye Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Kampeni ya Siku 16 ya Kupinga Ukatili  wa Kijinsia kwenye  Uwanja  wa Jamhuri jijini Dodoma, Novemba  25, 2018.
PMO_8646-min
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozindua kampeni ya Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Novemba 25, 2018.
PMO_8638-min
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wapili kulia), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto)  na   Mratibu wa Kitaifa wa Shirika la  Wanawake Katika Sheria  na Maendeleo Barani Afrika ( WILDAF), Anna Kulaya  wakati alipowasili kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kuzindua Kampeni ya Siku  16 ya Kupinga Ukatili  wa Kijinsia, Novemba 25, 2018.
PMO_8829-min
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya  pamoja na  baadhi ya viongozi wa kitaifa na kimataifa walkishiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia ulifanywa na Waziri Mkuu kwenye Uanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Novemba 25, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri mkuu.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>


iStore Tanzania yazindua simu mpya hapa nchini

$
0
0
DUKA la istore nchini Tanzania imezindua simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max inayoanza kutumika nchini kuanzia sasa. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mtaalamu wa Bidhaa za simu za Apple, Salum Abdalla amesema kila nchi yenye bidhaa hiyo ina muda wake wa kuzindua simu mpya na kwa Novemba 23 imekuwa ni muda wa nchi ya Tanzania kuzindua simu ya iPhone Xs na iPhone Xs max.

Amesema wamezindua simu hiyo baada ya kukamilisha taratibu zote ikiwemo kuwasiliana na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) ili kuitambulisha kwao na kuiruhusu kutumia mitandao ya hapa nchini.


 Abdalla amesema kila nchi ina taratibu zake na kwa Tanzania lazima wafike TCRA na iStore Tanzania imefanya jambo hilo na kwa hiyo sasa hivi iPhone Xs na iPhone Xs max rasmi zinaweza kutumika nchini.

Akielezea utofauti wa simu ya
iPhone Xs naiPhone Xs max, amesema ni simu zenye uwezo mkubwa sana tofauti na simu zingine.
Mkurugenzi wa iStore Tanzania, Vipul Shah akizungumza na wanafamilia wa iStore Tanzania waliofika kwenye uzinduzi wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max uliofanyika katika dula la iStore Tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi na wateja wa iStore Tanzania wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa Simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max uliofanyika katika duka la iStore Tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa iStore Tanzania, Pareshi Gohil akitoa ufafanuzi kuhusu laptop kwa mmoja wa wateja waliofika kwenye uzinduzi  wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max ,duka la iStore tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa iStore Tanzania, Shamim Goliama(kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu simu mpya ya iPhone Xs na iphone Xs max kwa baadhi ya wateja waliofika kwenye tukio hilo la uzinduzi uliofanyika katika duka la iStore tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa iStore Tanzania, Vipul Shah(kushoto) akizungumza na mmoja wa wateja waliofika katika duka la iStore tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max.
Afisa masoko na Mtaalamu wa Bidhaa wa iStore Tanzania, Salum Abdalla akizungumza na wandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max ilinayoanza kutumika hapa nchini
Baadhi ya wateja wakiangalia bidhaa za iStore wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max uliofanyika katika duka la iStore Tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UJENZI WA JENGO LA ABIRIA MKOANI TABORA KUANZA KUJENGWA HIVI KARIBUNI

$
0
0
Imeelezwa kuwa ujenzi wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Tabora ambao utaweza kuchukua abiria 500 kwa wakati mmoja utaanza hivi karibuni ili kuufanya uwanja huo kuwa na hadhi ya kupokea ndege kubwa nyingi.

Hayo yamesemwa mkoani humo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, mara baada ya kukagua uboreshaji wa uwanja huo kwa awamu ya pili, ambapo pamoja mambo mengine amesema kuwa tayari mkataba umeshasianiwa kati ya Mkandarasi na Wakala wa Barabara (TANROADS) na fidia kwa wananchi zimeshalipwa.

“Jengo hili lililopo ni dogo ambalo linauwezo wa kubeba abiria 60 tu kwa wakati mmoja hivyo Serikali imeamua kuongeza ukubwa wa jengo hili ili liweze kuwa na hadhi ya kupokea abiria wengi kwa wakati mmoja”, amesema Katibu Mkuu huyo.Amefafanua kuwa ujenzi wa jengo hilo unagharamiwa na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 29.

Ameongeza kuwa ujenzi wa jengo hilo mkoani humo utaenda sambamba na utekelezaji wa uboreshaji wa viwanja vya ndege vingine vitatu kwa kiwango cha lami ambavyo ni Kigoma, Sumbawanga na Shinyanga.Mhandisi Nyamhanga amesisitiza juu ya lengo la uboreshaji wa viwanja vya ndege hapa nchini ambayo ni azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kupitia usafiri wa Anga.

“Serikali inanunua ndege zenye ukubwa wa aina tofauti tofauti hivyo ni lazima ziende sanjari na uboreshaji wa miundombinu mbalimbali ya viwanja vya ndege hapa nchini”, amesisitiza Mhandisi Nyamhanga.Mapema Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Tabora, Godfrey Kaaya, alitoa taarifa kwa Katibu Mkuu huyo ya mradi wa upanuzi na uboreshaji wa kiwanja hicho kwa awamu ya pili uliohusisha upanuzi wa ujenzi wa maegesho ya ndege kwa kiwango cha lami, barabara unganishi za kutua ndege ndogo, ujenzi wa mitambo ya kuongozea ndege, taa za kuongozea ndege, jengo la kuchukulia umeme na jeneta kubwa.

Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Nyamhanga, yupo katika ziara ya kikazi mkoani Tabora ikiwa ni lengo la kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na sekta yake hususani barabara, madaraja na kiwanja cha ndege.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi Damian Ndabalinze, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, wakati alipokagua Kiwanja cha Ndege cha Tabora, mkoani humo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akifafanua jambo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi Damian Ndabalinze (katikati) na Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Tabora, Geofrey Kaaya (kushoto), mara baada ya kukagua kiwanja hicho, mkoani humo.
Muonekano wa jengo la sasa la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Tabora ambapo linaweza hudumia abiria 60 kwa wakati mmoja. Serikali iko katika hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa jengo jipya litakalokuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 500 kwa wakati mmoja.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 26,2018

WAJASIRIAMALI MARANGU WAMKANA AFISA MAENDELEO YA JAMII

$
0
0

Na Mwandishi Wetu Marangu Moshi 

Umoja wa Vicoba Marangu (UVIMA) wamemueleza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile kuwa ndani mwaka mzima hawajawahi kumwona Afisa Maendeleo ya Jamii wa mkoa wala Wilaya kuja kuwatembelea katika vikundi vyao.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo katika Shirika la Froresta linalojihusisha na utunzaji wa mazingira na Umoja wa Vicoba Marangu katika kujionea shughuli za uwezeshaji wananchi hasa wanawake kiuchumi. Naibu Waziri Ndugulile amewaagiza Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kilimanjaro na Wilaya ya Moshi Vijijini kuhakikisha wanawatembelea wajasiriamali na kuweka wazi vigezo vya uanzishaji vikundi na utoaji wa mikopo katika vikundi hivyo.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa ili kuwezesha kiuchumi hasa wanawake mamlaka husika zinatakiwa kutimiza wajibu katika kulifanikisha hilo. Aidha Dkt. Ndugulile ameziagiza Mamlaka za SIDO, TFDA, na TBS kutoa elimu kwa wajasiriamali ili kuwawezesha katika kupata elimu juu ya uanzishaji wa biashara na kutengeneza wa bidhaa bora. “Natoa agizo kwa kila ziara yangu wawepo SIDO, TFDA, na TBS waongozane na mimi ili kutatua changamoto na kero za wananchi kwa kila napoenda” alisisitiza Dkt. Ndugulile

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Floresta Mchungaji Winford Mosha amemshukuru Naibu Waziri kuwatembelea na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza majukumu ya kuwawezesha kiuchumi wananchi hasa wanawake. Ameongeza kuwa uazishwaji wa vikundi na umoja wa Vicoba umewasaidia wanawake wengi kujipatia kipato kinachowawezesha kutekelza majukumu yao katika familiana jamii.

Naye mmoja wa wajasiriliamali Bi. Mary Mtei amesema kuwa wanamekuwa akikutana na changamoto mbalimbali katika kufikia malengo ikiweo unyanyasaji kwa wanawake ikiwa ni moja ya Ukatili wa Kijinsia unaowakandamiza wanawake. Naibu Waziri Ndugulile yupo mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku tatu kufuatilia shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akizungumza na wajasirimali kutoka Umoja wa Vicoba Marangu (UVIMA) na Shirika la Floresta wakati wa ziara yake kukagua shughuli zinazofanywa na vikundi hivyo mkoani Kilimanjaro. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akiangalia mkungu wa ndizi unaolimwana wajasirimali kutoka Umoja wa Vicoba Marangu (UVIMA) na Shirika la Floresta wakati wa  ziara yake kukagua shughuli zinazofanywa na vikundi hivyo mkoani Kilimanjaro. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW 

CHINA DASHENG BANK LIMITED YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM, KUSAIDIA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0
NA K-VIS BLOG

BENKI mpya ya China Dasheng Bank Limited, inaanza kutoa huduma leo Jumatatu Novemba 26, 2018, jijini Dar es Salaam, ikiwa na mtaji wa kuanzia wa dola za kimarekani milioni 40 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 92, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo Bw. Yu Jiaqin amesema.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa benki hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Bw. Yu Jiaqin amesema benki hiyo ni benki ya kibiashara inayomilikiwa na makampuni sita ya serikali ya China yakishirikiana na makampuni binafsi kutoka mji wa Shanghai na Jiangsu.

Benki hii inalenga kutoa huduma kwa makampuni makubwa ya kichina yanayofanya miradi mbalimbali hapa nchini, lakini pia watanzania wanaofanya biashara na China ikizingatia makundi yote ya watu wenye kipato cha chini, cha kati na cha juu, alisema Bw. Jiaqin.

“Tutatoa huduma za bidhaa zote za kawaida za kibenki kama vile akaunti za akiba, akaunti za kudumu na za muda maalum, mikopo ya muda mfupi na muda mrefu na mikopo hii itatolewa kwa shilingi za kitanzania pamoja na fedha za kigeni.” Alibainisha Mwenyekiti huyo wa bodi.

Aidha Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bi Nunu Saghaf alishukuru Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kutoa leseni ya kufanya biashara kwa benki yake na kuahidi kuisaidia serikali ya Tanzania katika kufikia malengo yake ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.
Balozi wa China nchini Tanzania Mhe.Wang Ke, (katikati), akiungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, (wapili kushoto), Mwenyekiti wa Banki mpya ya China Dasheng Bank Limited, Yu Jiaqin, (wapili kulia), Afisa mwandamizi kutoka Banki Kuu ya Tanzania, Sadaat Mussa (wakwanza kulia) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka China, Zhujin Feng, baada ya kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki hiyo imeanza kutoa huduma leo Jumatatu Novemba 26, 2018 ikiwa na mtaji wa kuanzia wa dola za kimarekani milioni 40 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 92, Mwenyekiti wa benki hiyo amesema.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, akitoa hotuba yake.
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke akitoa hotuba yake.
Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa China Dasheng Banki Limited, Bi. Nunu Saghaf (watatu kushoto mstari wa mbele akiwa na wageni mbalimbali kwenye hafla hiyo ya uzinduzi.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.


BARAZA LA WAHITIMU WA CHUO KIKUU ARDHI WAFANYA MATEMBEZI YA HISANI KWA AJILI YA HARAMBEE

$
0
0
Jumuiya ya wahitimu ya Chuo Kikuu Ardhi (Adhi University Convocation) jana imefanya matembezi ya hisani yenye lengo la kuwaita wanajumuiya wote wa chuo hicho (ALUMN) ili kukumbuka nyumbani (waliposoma) hivyo kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo za chuo. Maandamano yaliongozwa na Rais wa baraza la wahitimu la Chuo hicho, Haruna Masebu pamoja na Naibu makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala, Profesa Robert Kiunsi.  

Mbali na matembezi hayo kulikuwa na mazoezi ya ya pamoja na michezo mbalimbali kiwemo Aerobic, Soka na mbio.Miongoni mwa washiriki walikuwepo pia sehemu ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ALUMNI wakiongozwa Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Maulid Bajani.Pia alikuwepo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Dkt. Moses Kusiluka ambaye ni mdau mkubwa wa chuo hicho.Wengine ni UCLAS Veteraniambao walicheza soka na wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi na kuibuka kidedea. 
Sehemu ya wadau (ALUMN) na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) pamoja na wadau wao Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakifanya matembezi katika Barabara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Novemba 24, 2018 kwa ajili ya shughuli za chuo jijini humo. Chuo hicho kinatarajiwa kuwa na Kongamano la wahitimu (CONVOCATION) Ijumaa ya Novemba 30, 2018. (Imeandaliwa na Robert Okanda) .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

PANGANI JOGGING CLUB YAZINDULIWA KWA KISHINDO

$
0
0
 Zaidi ya watu mia tano wamejitokeza katika uzinduzi wa PANGANI JOGGING CLUB uliyofanyika asubuhi ya Jumamosi ya tarehe 24/11/2018 katika uwanja wa Bomani Pangani mjini. Uzinduzi huo umepambwa na mazoezi ya pamoja, yaliyoendeshwa na club ya mazoezi kutokea jijini Tanga, Power and Sports ambayo yalinogesha na kuongeza hamasa kwa umati mkubwa ulihudhuria uzinduzi huo wa kihistoria. 

Mbali na Power and Sport, club nyingine zilizoshiriki katika uzinduzi huo ni pamoja na TK Jogging club kutokea jijini Tanga, na EFM jogging club kutokea jijini Dar es salaam ambayo baadae ilicheza mchezo wa soka wa kirafiki dhidi ya wakazi wa Pangani. 

 Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa PANGANI JOGGING CLUB alikuwa ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Na Mbunge wa Pangani Mh. Jumaa Awesso ambaye mbali na kushiriki mazoezi na wananchi wake, pia amekubali kuwa mlezi wa club hiyo,Pia katika kutambua umuhimu wa michezo na Mazoezi Mh Aweso alitoa zawadi ya mipira kwa klabu za soka wilayani Pangani .

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kiserikali, waheshimiwa madiwani, wakuu wa idara halmashauri ya Pangani pamoja na wadau mbali mbali kutoka sekta binafsi PANGANI JOGGING CLUB imezinduliwa ikiwa na lengo la kuhamasisha mazoezi kwa ajili ya kuboresha afya, kwa mustakabali wa maendeleo ya Pangani, sambamba na kuhamasisha ushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, kukuza mahusiano ya watu na kubadilishana mawazo, pamoja na kusukuma ajenda mbalimbali za kimaendeleo za serikali. 

 Afisa Tarafa wa Pangani mjini na Mwenyekiti wa club hiyo Bi. Zuhura Rashid, sambamba na katibu wake Bwana Midraj Msusa, wamemesema kuwa, club hiyo itakuwa endelevu, na itasaidia kwa kiasi kikubwa wanapangani katika mustakabali wa kupambana na afya zao. 
 Mbunge wa PANGANI na naibu waziri wa maji na umwagiliaji Mh jumaa awesso akikata utepe ikiwa kama ishara ya uzinduzi wa PANGANI JOGGING CLUB
 Mbunge wa PANGANI na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Awesso (Wa tatu toka kushoto) akiwa na Kamati na wajumbe wa awali wa PANGANI JOGGING CLUB wakiwa katika picha ya pamoja 
Mbunge wa PANGANI na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Awesso (Mbele) akiwa katika mazoezi na Wana-PANGANI JOGGING CLUB mara baada ya kumaliza uzinduzi.
Maulidi Kitenge wa Efm sambamba na afisa tawala wa Pangani ndugu Gibson George wakati wa uzinduzi wa PANGANI JOGGING CLUB walipokuwa wakikimbia katika mji huo wa kihistoria.

Serikali yaukataa mpango wa ufungaji mgodi wa Buzwagi

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo
Serikali imeitaka kampuni ya Acacia kuandaa na kuwasilisha haraka mpango mpya wa urejeshaji mazingira katika hali yake ya kawaida baada ya kusitisha shughuli za uchimbaji dhahabu katika mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama ifikapo mwaka 2020.


Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko aliyasema hayo jana alipofanya ziara katika mgodi huo kukagua shughuli zinazoendelea mgodi hapo.


Mapema mwaka huu, Wizara ya Madini iliukataa mpango uliokuwa umeandaliwa na kampuni hiyo ukikadiriwa kutumia dola milioni 18 kwa kuwa haukujumuisha kufukiwa baadhi ya mashimo mgodini hapo (tazama picha), bali yabaki wazi hadi yatakapojaa maji katika kipindi cha miaka 100 ijayo. 
Naibu Waziri Doto Biteko (katikati), akifafanua jambo wakati akikagua shughuli mbalimbali katika mgodi wa Buzwagi.
Naibu Waziri Doto Biteko akielekea kukagua sehemu ambapo mchanga wenye madini (makinikia) umehifadhiwa ndani ya mgodi wa Buzwagi.
Tazama Video hapa chini

POLISI IPO IMARA KUPAMBANA NA UHALIFU WA AINA YOYOTE NCHINI, USALAMA WA WANANCHI SERIKALI YA AWAMU YA TANO ‘HAUBIPIWI’-WAZIRI LUGOLA

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema Jeshi la Polisi lipo imara kupambana na uhalifu wa aina yoyote utakaojitokeza nchini hivyo wahalifu wasithubutu kulichezea, wala ‘kulibipu’.

Lugola pia amewataka wananchi kuendelea kuwapa taarifa za uhalifu Polisi ili ziweze kufanyiwa kazi haraka kwa kuwa Serikali ya Rais Dk. John Magufuli si ya kuchezewa na imejipanga kikamilifu kwa kuwalinda wananchi wake.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Ragati, Kata ya Kasuguti, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, Lugola alisema Jeshi la Polisi lipo imara na litaendelea kuwalinda wananchi pamoja na mali zao, ila Polisi ili waweze kufanya kazi zao kwa umakini zaidi, wananchi wanapaswa kuwasaidia katika kufichua uhalifu katika maeneo yao wanayoishi.

Lugola aliyazungumza hayo baada ya wananchi wa Kijiji hicho kumlalamikia kuwa kuna kundi la vijana ambalo linaongozwa mwananchi mmoja kijijini hapo wanahatarisha amani na kuwafanya kuishi kwa wasiwasi na kushindwa kufanya shughuli zao za maendeleo.

“Polisi wapo kwa ajili yenu hivyo kuweni huru muda wowote kutoa taarifa za kiuhalifu katika maeneo yenu, hivyo kutokana na viashiria hivyo vya uvunjifu wa amani katika Kata hii namuagiza mkuu wa polisi wilaya (OCD) kuwasaka, kuwakamata wale wote ambao wanahatarisha amani katika Kata hii ya Kasuguti,” alisema Lugola. Lugola aliongeza kuwa, yeye ni Mbunge wa Jimbo hilo na pia ni Waziri ambaye anasimamia usalama wa wananchi na mali zao, hivyo hatakubali wananchi waishi kwa wasiwasi katika maeneo yao na nchi kwa ujumla, na pia Serikali ya Magufuli haichezewi, haijaribiwi na wala haibipiwi na mtu yeyote.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia), akimsindikiza kumpeleka ndani ya gari Mkazi wa Kitongoji cha Songambele, Kata ya Kasuguti, Jimbo la Mwibara mwenye umri wa miaka 100, Mzee Mtatiro Silla, mara baada ya Waziri huyo kumaliza mkutano wake wa hadhara akizungumza na wananchi wa Kata hiyo, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo. Lugola aliwataka wananchi jimboni kwake watoe polisi taarifa za uhalifu nchini na pia Serikali ya Awamu ya tano ipo imara haichezewi na mtu yeyote. Pia Lugola aliwataka wananchi jimboni kwake waanze maandalizi ya kilimo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Mkazi wa Kitongoji cha Songambele, Kata ya Kasuguti, Jimbo la Mwibara, mwenye umri wa miaka 80, Mzee Nyamuhanga Mtatiro Silla, wakati mzee huyo alipokua anamuuliza swali Waziri Lugola katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji hicho, leo. Wapili kushoto meza kuu ni Mzee mwenye umri wa miaka 100, Mtatiro Silla ambaye ni baba mzazi wa anayezungumza, na mtoto wake wa tatu katika kuzaliwa. Baba na mwana wote walihudhuria mkutano huo wa Waziri Lugola. Lugola aliwataka wananchi jimboni kwake watoe polisi taarifa za uhalifu nchini na pia Serikali ya Awamu ya tano ipo imara haichezewi na mtu yeyote. Pia Lugola aliwataka wananchi jimboni kwake waanze maandalizi ya kilimo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kasuguti, Kata ya Kasuguti, Jimbo la Mwibara, Mkoani Mara, akiwataka wananchi jimboni kwake watoe taarifa za uhalifu Polisi na iliwawe na amani na waendelee kufanya shughuli zao za kilimo, pia alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya tano ipo imara haichezewi na mtu yeyote.


WAZEE WASTAAFU 2000 MKOANI TANGA WANUFAIKA NA MIKOPO KUTOKA BENKI YA POSTA.

$
0
0
WAZEE Wastaafu 2000 mkoani Tanga wamenufaika na mikopo kutoka Benki ya Posta (TPB) wenye thamani ya sh.bilioni 6.7 kupitia pensheni zao ambao umeweza kuwasaidia kukidhi mahitaji yao na kuwakwamua kimaendeleo wao na jamii zao. 

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa vya ofisi kwa ajili ya Chama cha Muungano wa Wanajeshi wastaafu mkoa wa Tanga (MUWAWATA) zenye thamani ya milioni 1.5. 

Vifaa vya ofisi ambavyo vilikabidhiwa ni viti sita, meza moja na feni mbili ambavyo vitawawezesha wazee hao kuweza kutekeleza majukumu yao ya kila siku ya kiofisi hali itakayowasaidia kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa ambapo mikopo hiyo bado inaendelea. 

Alisema kwamba huo ni mwanzo hivyo wataendelea kushirikiana na wazee wote nchini wa taasisi mbalimbali ili kuweza kuwasaidia kukidhi mahitaji yao hivyo kuwataka wastaafu kuchangamkia fursa hiyo ikiwemo kuwapa elimu namna ya kutumia fedha husika. “Lakini niwaambie kwamba sisi TPB tunawaambiwa wazee wastaafu nchi nzima tunawajali kwa kutoa mikopo na huduma za kibenki wao wamekuwa wa kwanza kuweza kutoa mikopo kwao kabla ya hapo wastaafu walikuwa wanaonekana kama ni kada ambayo haikopesheni tulianza kutoa mikopo kwa wastaafu kupitia pensheni zao “Alisema. 
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses kushoto akimkabidhi vifaa vya ofisi Mwenyekiti wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu mkoani Tanga (MUWAWATA) Stepheni Mponji vifaa vya ofisi kwa ajili ya Chama cha Muungano wa Wanajeshi wastaafu mkoa wa Tanga (MUWAWATA) venye thamani ya milioni 1.5
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses kushoto akimkabidhi feni kwa ajili ofisi Mwenyekiti wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu mkoani Tanga (MUWAWATA) Stepheni Mponji vifaa vya ofisi kwa ajili ya Chama cha Muungano wa Wanajeshi wastaafu mkoa wa Tanga (MUWAWATA) juzi ambapo benkio hiyo ilitoa vifaa venye thamani ya milioni 1.5.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses kushoto akimkabidhi meza kwa ajili ya matumizi ya ofisi Mwenyekiti wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu mkoani Tanga (MUWAWATA) Stepheni Mponji juzi ambapo benki hiyo ilitoa vifaa venye thamani ya milioni 1.5

Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>