Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

RC ZAMBI- LINDI IMEKUSANYA KILO MILIONI 44.6 ZA KOROSHO NA KUWALIPA WAKULIMA TSH. BILIONI 3.9


Dkt.Shein awasili Jijini Nairobi Kuhudhuria Mkutano wa Blue Economy.

0
0
Na.Suzan Kunambi. Nairobi..

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amewasili nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa uchumi endelevu wa bahari(Sustaniable Blue Economy Confrence) utakaoanza kesho katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta Jijini Nairobi Nchini Kenya.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi, Dk.Shein amepokelewa na viongozi mbali mbali wakuu wa Serikali ya Kenya wakiongozwa na balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kanzungu pamoja na Balozi wa Tanzania nchini humo Dk. Pindi Chana.

Katika ziara hiyo, Dk. Shein amefuatana na viongozi mbali mbali wa SMT na SMZ, akiwemo Waziri wa Kilimo Maliasili Mifungo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma,Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe.Dk.Sira Ubwa Mamboya,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais Mazingira na Muungano Mhe January Makamba.

Mkutano huo Mkubwa unaohusu sekta ya uchumi wa bahari ni wa kwanza kufanyika nchini Kenya, ambao utawakutanisha wadau kutoka sekta mbali mbali kutoka nchi zilizoendelea na sinazoendelea kujadili namna bahari,maziwa na mito vinavyoweza kutumika katika kuimarisha uchumi wa nchi na dunia kwa ujumla.

Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya Mhe.Uhuru Kenyatta, ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein atatoa tamko la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Uchumi Endelevu wa Bahari, akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muunhano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Magufuli.

Mkutano huo utajadili maswala mbali mbali ya uchumi endelevu wa bahari na mchango wake katika kutekeleza Agenda ya 2030 ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa.vile vile washiriki wa mkutano huo watajadili hatua za utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika ,mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wa mwaka 2015 wa Paris Ufaransa pamoja na mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari wa mwaka 2017 kwa ajili ya maendeleo endelevu pamoja na usalama na ulinzi baharini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Aliu Mohamed Shein, akimsikiliza Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Balozi Dan Kazungu kulia na kushoto Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dkt. Pindi Chana,baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nchini Kenya.akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli katika Mkutano wa Blue Economy unaotarajiwa kufanyika keshi Jijini Nairobi. katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiutambulisha Ujumbe wake kwa Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mr. Dan Kazungu,wakiwa katika chumba cha VIP baada ya kuwasili leo jioni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika chumba cha VIP katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nchini Kenya akiwa anahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Blue Economy,kulia Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mr. Dan Kazungu na kushoto Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dkt. Pindi Chana. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dkt.Pindi Chana na anayefuata ni Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Balozi Dan Kazungu, alipowasili katika hotelini.Jijini Nairobi. 

MUFTI WA TANZANIA AZINDUA MAANDALIZI YA IJITIMAI YA KIMATAIFA ITAYOFANYIKA T ZANZIBAR

0
0

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Fiy Sabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Alhaji Shekh. Mwalim Hafidhi Jabu akimkaribisha Mufti wa Tanzania Shekh. Abubakari Zubeir Ali katika viwanja Markaz Kidoti Mkoa Kaskazini Unguja.
Mufti wa Tanzania Shekh. Abubakari Zubeir Ali akizindua rasmin maandalizi ya Ijitimai ya kimataifa itayofanyika tarehe 22/02/2019 katika Kijiji cha Kidoti Mkoa Kaskazini Unguja uzinduzi huo umefanyia Msikiti wa Jumuiya ya Fiy Sabilillahi Tabligh Markaz Kidoti.
Mufti wa Tanzania Shekh. Abubakari Zubeir Ali akimsalimia Bii. Mwajuma juma mkaziwa Kidoti alietoa kiwanja kwa ajili ya kujengwa Mskiti huo.Picha na Makame Mshenga.

Mufti wa Tanzania Shekh. Abubakari Zubeir Ali akiwa na mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Vuai Mwinyi Khamis wa kwanza (kulia) na  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Fiy Sabilillahi Tabligh Markaz Alhaji Mwalim Hafidhi Jabu kukagua Mskiti unaotarajiwa kufanyika Ijitimai ya kimataifa huko Kidoti.
Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Vuai Mwinyi Khamis akimkaribisha Mufti wa Tanzania Shekh. Abubakari Zubeir Ali katika uzinduzi wa maandalizi ya Ijitimai ya kimataifa itayofanyika tarehe 22/02/2019 huko kijiji cha Kidoti Mkoa Kaskazini Unguja.

Amber Rutty na Mpenzi wake waendelea kusota rumande,upelelezi wa kesi yao bado haujakamilika

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Wakati Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Ruty na mpenzi wake Said Kitomali wakiendelea kusota rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana, katika kesi inayowakabili ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile upelekezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Amber Ruty na Said wanashtakiwa pamoja na James Charles maarufu kama 'James Delicious' ambaye yeye yupo nje kwa dhamana.kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Amber Rutty alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine, Rwizile kuwa mdhamini wake mmoja amefika mahakamani hapo lakini mwingine bado hajafika.

Hata hivyo, Hakimu Rwizile  amemwambia Amber Rutty kwamba dhamana ipo wazi na shughuli za mahakama zinaisha saa 9 alasiri hivyo wadhamini wake wakikamilika atadhaminiwa.Kesi  hiyo imeahirisha hadi Decemba 10,2018.

Katika kesi hiyo, Amber Ruth,  anadaiwa kufanya mapenzi kinyume na maumbil kosa analodaiwa kulitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, 

Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Ruth kinyume na maumbile.Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya October 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Katika shtaka la nne ambalo ni kusababisha kusambaa kwa picha za ngono linamkabili Amber Ruth na Said Aboubakary ambapo wanadaiwa kati ya 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kweli.Amber  Rutty na mpenzi wake ili waweze kuwa nje kwa dhamana wanatakiwa kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini 2 ambapo kila mtu atasaini bondi ya Shilingi Milioni 15.

Pia wadhamini wawe na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati zenu za kusafiria na msitoke nje ya Dar es Salaam bila ruksa.
Pichani kati Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Ruty akirudishwa rumande huku upelelezi wa kesi yao bado haujakamilika

UPELELEZI KESI YA UCHOCHEZI INAYOMKABILI ZITO KABWE WAKAMILIKA

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi katika kesi ya uchochezi inayomkabili, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe umekamilika.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Mutalemwa Kishenyi ameeleza hayo leo Novemba 26.2018 wakati kesi hiyo ilipokuwa kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi.

Kufuatia kukamilika kwa upelelezi huo maelezo ya awali (PH) dhidi kesi hiyo ya Zitto yatasomwa Desemba 13,2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi

Katika kesi hiyo Zitto anadaiwa Oktoba 28, 2018 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya ofisi ya chama cha ACT Wazalendo, kwa nia ya kuleta chuki kwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la polisi alitoa Maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.

Pia Zitto anadaiwa kutoa Maneno ya uchochezi ambayo yalikuwa na lengo lenye kuleta hofu.

Aidha Zitto anadaiwa Kutoa walaka kwa umma ukiwa na Maneno ya kichochezi kwa nia ya kuleta chuki kwa watanzania dhidi ya polisi.
 Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe  (wa pili kulia) akizungumza jambo na baadhi ya wadau wake/wanachama wa chama chake alipokuwa akitoka nje ya jengo la Mahakama ya Kisutu leo

Elimu zaidi inahitajika mapambano dhidi ya Ukimwi

0
0
Na Mwandishi Wetu
Elimu zaidi na kampeni inahitajika kupunguza kasi ya maambukizi mapya ya Ukimwi nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge wakati akizungumza katika wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani iliyoambatana na matembezi ya hisani na mauzo ya tisheti kwa ajili ya kuchangia mfuko wa mapambano dhidi ya Ukimwi.
Katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri alisema ipo mikoa takwimu za maambukizi mapya zinapanda huku maeneo mengine hali ikibaki kuwa vile vile.
Aliwataka wananchi kubadili tabia hasa kujitokeza kupima kujua afya zao ili kama wameathirika basi waanze kutumia dawa.
Shekimweri alisema juhudi za makusudi zinatakiwa kuhakikisha mapambano dhidi ya maradhi hayo yanaongezeka .
Alisema mkoa wa Dodoma, mathalani kwa sasa maambukizi mapya yamefikia asilimia 5 yakipanda kwa asilia mbili zaidi ya ilivyokuwa miaka 2011/12.
Lakini alisema maeneo kama ya Zanzibar maambukizi yamepungua na kusema ipo haja ya kutafiti na kueneza majibu ya utafiti kwa umma ili uweze kujihami na maambukizi mapya.
Alisema watu kama Zanzibar inaonekana wamefanya vyema kutokana na kuwa na taratibu njema za kuzuia ‘ngono’ zembe ikiwa na pamoja na matumizi mazuri ya nyumba za kulala wageni.
Pamoja na kuhimiza elimu na utafiti kuzuia maambukizi mapya alizungumzia haja ya kushawishi wadau zaidi kuchangia mfuko wa Ukimwi ambapo kilomita 5 za matembezi ya hisani zimechangia sh 14,500.000 kwa mauzo ya fulana na ahadi mbalimbali.
Alisema ipo haja ya kuandaa mkakati mpya wa kuwezesha kutunisha mfuko huo wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi ambao unahitaji zaidi ya shilingi bilioni tatu. Mkakati huo ni pamoja na kufanya harambee na kutengeneza bidhaa za mauzo kwa ajili ya mfuko.
Aliongeza kuwa mtu binafsi, taasisi au makampuni ambao wangependa kushiriki zoezi hili endelevu la kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi (ATF) wanaweza kutuma michango yao kupitia namba za 0684909090.
 Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri (katikati) akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5Km ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani Disemba mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk Leo Zekeng (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk Leonard Maboko (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi ambaye pia ni Mbunge wa Biharamulo, Mhe. Oscar Mukasa (kushoto).
 Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk Leo Zekeng akitoa salamu za Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5Km ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani Disemba mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk Leonard Maboko akizungumza kuhusu maandalizi pamoja na kuhamasisha uchangiaji wa hiyari unaohusisha mtu binafsi, taasisi mbalimbali za serikali, sekta binafsi na makampuni kupitia 0684909090 wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5KM kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
   Baadhi ya wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali za serikali, wananchi pamoja na wanafunzi wa shule za sekondari Dodoma walioshiriki matembezi ya hisani ya 5KM kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba Mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
 Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa NACOPHA wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5KM kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba Mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WATATU WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI

0
0

 Na. VERO IGNATUS, MANYARA

Jeshi la polisi Mkoani Manyara, linawashikilia watu watatu kwa kudaiwa kukutwa na nyara za serikali ikiwemo vipande vitatu vya jino la Tembo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Augostino Senga akizungumza jana alisema watu hao walikamatwa kwenye nyumba ya kulala wageni ya Top In One iliyopo mtaa wa Oysterbay mjini Babati.

Kamanda Senga aliwataja watu hao kuwa ni Anthony Paschal (28) na Juma Ingi wote wakazi wa Endasak wilayani Hanang' na Tluway Gosi mkazi wa Simbay wilayani Hanang'. Alisema mbinu waliyotumia ni kuficha vipande hivyo ndani ya mfuko wa sulphate kisha kuweka chini ya uvungu wa kitanda ili wakaiuze.

Alisema baada ya timu ya makachero kwa kushirikiana na maofisa wanyamapori wa shirika la hifadhi ya Taifa ya Tarangire kupata taarifa walifika eneo hilo na kuwakamata watu hao. "Watuhumiwa hao wote wanashikiliwa na polisi na tunaendelea na upelelezi kabla ya kuwafikisha mahakama kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayowakabili," alisema kamanda Senga.

Katika tukio lingine, kamanda Senga alisema watu watatu wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na lita 40 za pombe haramu ya moshi maarufu kama gongo. Alisema watu walikamatwa juzi kwenye kijiji cha Kazamoyo kata ya Kisangaji wilayani Babati wakiwa wamebeba kwenye pikipiki aina ya Skygo yenye namba za usajili MC 970. Aliwataja watu hao kuwa ni Daniel Hewasi (47) mkazi wa Magugu, Hussein Athuman (50) mkazi wa kijiji cha Kazaroho na Idd Hamis (35) mkazi wa kijiji cha Magugu.

Alisema watu hao walikuwa wamebeba pombe hiyo haramu kwenye pikipiki hiyo wakiwa wamehifadhi kwenye madumu mawili ya lita 20 kila moja.Alisema pikipiki hiyo iliyokuwa imebeba pombe hiyo haramu ni mali ya Idd Hamis na lengo lao ilikuwa ni kwenda kuuza ili kujipatia kipato.

Alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kuwafikisha mahakamani wakajibu mashtaka yanaoyowakabili.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Augostino Senga 

WAWEKEZAJI WA LIGANGA MCHUCHUMA WAOMBA KUKAA MEZA MOJA NA SERIKALI

0
0
*Kampuni ya Sichuan Hongda Group ya China yaomba kukaa meza moja na Serikali ili kufikia muafaka wa mradi wa uchimbaji  Liganga  Mchuchuma, ambapo yasubiri  hatima ya mradi huo kutoka Serikalini.

MICHUZI TV:SERIKALI YAAGIZA TCRA KUCHUNGUZA KILA ANAYETUMIA MITANDAO YA KIJAMII

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU BABA ASKOFU EVARISTO CHENGULA WA JIMBO KUU LA MBEYA NOVEMBA 26, 2018

0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akisainib kitabu cha maombolezo mara baada ya kuwasili Makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa kanisa Katoliki Tanzania (TEC) kuaga mwili wa Marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo kuu la Mbeya,Ibada iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Immakulata Makao Makuu ya Baraza hilo Kurasini Jijini Dar es Salaam Novemba 26, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akitoa salamu zake za mwisho kwa mwili wa Marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo kuu la Mbeya,Ibada iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Immakulata Makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam Novemba 26, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akizungumza wakati wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo kuu la Mbeya,Ibada iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Immakulata Makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam Novemba 26, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa,Mama Anna Mkapa pamoja na Maaskofu, Mapadre, Masista na Waumini wenginne wakati ibada ikiendelea ya kuaga mwili wa Marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo kuu la Mbeya, iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Immakulata Makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam Novemba 26, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akipongezwa mara baada ya kutoa salamu za rambirambi na Makamu wa Rais wa baraza la Maaskofu wa Kanisa katoliki Baba Askofu Dkt.Flavian Kasalla wakati wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo kuu la Mbeya,iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Immakulata Makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam Novemba 26, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akipongezwa mara baada ya kutoa salamu za rambirambi na Makamu wa Rais wa baraza la Maaskofu wa Kanisa katoliki Baba Askofu Dkt.Flavian Kasalla wakati wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo kuu la Mbeya,iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Immakulata Makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam Novemba 26, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akipongezwa mara baada ya kutoa salamu za rambirambi na Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam Mhadhama Polycapy Kadinali Pengo wakati wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo kuu la Mbeya,iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Immakulata Makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam Novemba 26, 2018.

PICHA NA IKULU.

MKUTANO WA 12 WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI KUANZA JUMATANO

0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar 
Mkutano wa 12 wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano tarehe 28 Novemba 2018 katika Ukumbi wa Baraza hilo Chukwani. Akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari Ofisini kwake, Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Raya Issa Msellem alisema jumla ya maswali 123 yameratibiwa kwa ajili ya kujibiwa kwenye mkutano huo.

Alisema Miswada mitatu ya sheria iliyowasilishwa na kusomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa mwezi Septemba itasomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa katika mkutano huo. Aliitaja miswada hiyo kuwa ni mswada wa Sheria ya kuweka masharti yanayosimamia Utoaji wa Huduma za msaada wa Kisheria, kurahisisha upatikanaji wa haki na kuweka masharti mengine yanayohusiana na hayo.

Mswada wa Sheria ya kufuta Sheria ya ukuzaji na kulinda vitegau uchumi Zanzibar Nam. 11 ya mwaka 2004 na kutunga sheria ya Mamlaka ya Ukuzaji na kulinda vitega uchumi Zanzibar. Katibu wa Baraza Raya Issa Msellem alitaja mswada mwengine kuwa ni mswada wa Sheria ya kufuta Sheria ya Vyama vya Ushirika Nam. 4 ya mwaka 1986 na kutunga Sheria ya vyama vya Ushirika Zanzibar ya mwaka 2018 ambayo inaweka utaratibu wa uundaji na uendeshaji wa vyama vya Ushirika na mambo mengine yanayohusiana na hayo.

Alieleza kuwa Katika Mkutano huo taarifa ya Serikali kuhusu hoja ya Mjumbe Jaku Hashim Ayoub ya kutoa Azimio la kuitaka Serikali kuja na Mkakati unaotekelezeka kwa kutatua changamoto zinazowakabili wakulima wa zao la mwani itatolewa. Hoja nyengine ni ya Mjumbe kuhusu wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka viti maalum vya wanawake kufaidika na fedha za Mfuko wa Maendeleo wa Jimbo na hoja ya Mjumbe kuhusu kuimarisha tathmini na ufuatiliaji wa miradi Zanzibar zitawasilishwa. 
 Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Raya Issa Msellem akitoa taarifa  kwa Waandishi wa Habari kuhusu kuanza Mkutano wa 12 wa Baraza la Tisa la Wawakilishi (kulia) Mkuu wa Idara ya shughuli za Baraza Mussa kombo na Mkuu wa Idara ya Utawala Amour Mohd.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (hayupo pichani) alipokuwa akitoa taarifa ya kuanza Mkutano wa 12 wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Ofisini kwake Chukwani. Picha na Ramadhani Ali – Maelezo.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

Waziri Kamwelwe aomba subira kwa TBA, Aridhishwa ujenzi wa Ihungo Boys

0
0
Na Mwandishi Wetu, Bukoba
WAKATI Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe ameomba taasisi za serikali, Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wizara, ambazo zimeipa kazi Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA), kuwa na subira kwa kuwa inaupungufu wa wafanyakazi, lakini ameridhishwa na ujenzi wa shule ya sekondari ya Wavulana ya Ihungo ya mkoani Kagera iliyojengwa na taasisi hiyo.
Akifafanua Mhe. Kamwelwe amesema TBA wanakumbwa na changamoto kubwa ya upungufu wa wafanyakazi, ambapo kwa Tanzania nzima wanawafanyakazi 300 pekee, ambao wanajitoa kwa kufanya kazi kwa bidii, ambapo idadi kamili inayotakiwa ni wafanyakazi 1700.
Hatahivyo, ameipongeza TBA kwa kufanya kazi nzuri za ujenzi mbalimbali za majengo ya serikali kwa kutumia thamani halisi ya fedha tofauti na wakandarasi binafsi wamekuwa na gharama kubwa.
“Utendaji wa TBA bado unaleta mashaka nchi nzima na nimefanya nao kikao nikabaini wapo wafanyakazi 300 pekee na wanatakiwa angalau 1000 ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, hivyo nashauri pamoja na kusikia malalamiko kila upande kutoka kwa Wakuu wa Wilaya, Mikoa, Bungeni na Watendaji wengine wa serikali, ninayafanyia kazi likiwemo la uhaba wa wafanyakazi,” amesema Mhe. Kamwelwe.
Baadhi ya kazi za ujenzi wanazofanya na walizofanya TBA ni pamoja na ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mkoani Dodoma; ujenzi wa hospital ya Mkoa wa Simiyu na Ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma mikoa mbalimbali. Akizungumzia ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Katika hatua nyingine, Mhe. Kamwelwe ameipongeza TBA kwa ujenzi wa shule ya kisasa ya sekondari ya wanaume ya Ihungo iliyoathirika na tetemeko la ardhi lililotokea Kagera 2016.
“Nawapongeza sana kwa kujenga shule nzuri tena kwa gharama nafuu ya Bil. 10.4, ukiangalia wengine walitaka kujenga kwa Bil. 36, hivyo TBA wameokoa fedha nyingi sana za Watanzania na kiwango chao cha kazi ni kizuri,” amesema Mhe. Kamwelwe. Naye Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Kagera, Mhandisi Herico Bahati amesema ujenzi wa shule hiyo ulianza Oktoba 5, 2016, ambapo kuna majengo matatu ya ghorofa ya madarasa yenye vyumba 24, ofisi 12 za walimu, jengo la vyoo 80, mabweni matatu yenye vyumba 96, nyumba 30 za walimu, upanuzi wa bwalo la chakula na wamechimba kisima cha maji.
Shule hiyo inawanafunzi 600, ambapo sasa pia imeongezewa wanafunzi 751 wa shule ya Sekondari ya Bukoba waliohamishiwa hapo kwa muda baada ya shule yao kuezuliwa paa na upepo mkali uliotokea Oktoba 2018.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba, ambaye pia anakaimu wilaya ya Bukoba Mjini, Mhandisi Richard Ruyangu ameishukuru serikali kwa kuijenga tena shule hiyo na sasa wanafunzi wanaendelea na masomo.
“Tunaishukuru serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa kutujengea tena shule nzuri na tunaimani kwa mazingira haya watoto watasoma kwa bidii, na hata walimu hali kadhalika watafundisha kwa moyo tumeona wamejengewa nyumba nzuri na za kisasa tena zipo maeneo ya karibu na shule itakuwa hawatoki mbali kuja kufundisha,” amesema Mhandisi Ruyangu.
Kiranja mkuu wa shule hiyo, Bw. Athuman Mohamed kwa niaba ya wanafunzi wenzake, ameishukuru serikali kwa kuwajengea tena shule yao na wameahidi kusoma kwa bidi ili kufanya vizuri katika masomo yao.
 Waziri Mkuu wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe  (mwenye suti ya bluu) akiwaeleza jambo wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo ya Kagera, alipofanya ziara hivi karibuni. Kulia (mwenye suti ya udongo ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Bw. Philip Boniventura.
  Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA) mkoa wa Kagera, Mhandisi Herico Bahati (mwenye shati la batiki) akimpa maelezo mbalimbali Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kushoto) kuhusiana na ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo, waliyoijenga baada ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016. Mbele ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Philip Boniventura.
Waziri Mkuu wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (mwenye suti ya bluu) akimsikiliza Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA) mkoa wa Kagera, Mhandisi Herico Bahati (mwenye shati la batiki) akimpa maelezo mbalimbali ndani ya moja ya vyumba 96 vya mabweni ya shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo, waliyoijenga baada ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016.

FCS YAJITOLEA KUCHANGIA DAMU HOSPITALI YA MUHIMBILI, KITENGO CHA MOI

0
0
Taasisi inayojihusisha na kutoa ruzuku kwa asasi za kiraia hapa nchini ya Foundation for Civil Society mapema jana imeendesha zoezi maalum la kujitolea damu kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa mbalimbali wenye uhitaji wa damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha MOI.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana katika zoezi hilo la uchangiaji wa damu Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga amesema kuwa, wao wameamua kuchangia damu kwa wagonjwa ikiwa ni kama njia moja wapo ya kurudisha kitu kwa jamii.

Aidha Mkurugenzi huyo aliendelea kusisitiza umuhimu wa wananchi kuchangia damu nakuwataka wajitokeze kwa wingi katika zoezi hilo hasa vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa.

“Tumekuja hapa kuchangia damu kwa kuwa ni hospitali ya Taifa na ni sehemu yenye uhitaji mkubwa sana wa damu. Tunawaomba watanzania wengine wajitokeze kuchangia ili kuwaokoa watanzania wenzetu lakini pia kuunga mkono jitihada za shirika la damu salama ambalo kila kukicha wanaelezea umuhimu wa wananchi kuchangia damu ili kunusuru maisha ya wananchi wenzetu ” Alisema Kiwanga

Ameongeza kuwa mbali na kujitoa kwao katika zoezi la kuchangia damu lakini pia wamejipanga kwenda kuwasaidia wasichana wanaoishi katika mazingira magumu wa kituo cha New Hope for Girls kilichopo Kimara jijini Dar es salaam Tarehe 27/11 mwaka huu katika siku ya Jumanne ya kutoa.
Mmoja wa wachangiaji wa damu katika Kampeni hiyo iliyoendeshwa na Taasisi ya Foundation for Civil Society, Gloria Wangeleja(Mwenye nguo ya Rangi Nyekundu) akitoa damu mapema jana katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

KWA upande wake Mkuu wa Kitengo cha Maabara Moi Dokta Mbuta Jakckson alisema kuwa licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na makundi ikiwamo wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali, vikundi vya dini lakini bado changamoto hiyo haikuweza kumalizika na kusema kuwa kwa mahitaji ya kaiwada ya damu kwa siku ni unit 70 lakini zinazopatikana ni unit 40 mpaka 50 peke yake.

Amesema hospitali ina wataalamu wa kutosha wa kukusanya damu, watu hawana haja ya kutia shaka na uwezo wa taasisi hiyo katika kukamilisha zoezi hilo. “Tumekuwa tukienda hata nje ya kituo hiki, kwa mfano tulikwenda temeke katika msikiti mmoja hivi jina nimelisahau, lakini pia tulifika kwenye makampuni mbalimbali kuchukua damu. Tunachohitaji ni utayari wa raia, tuko tayari wakati wote kufika mlipo ili tuchukue damu itakayowasaidia wagonjwa” alisema.

Aliendelea kusisitiza kuwa hapo mwanzo wagonjwa walikuwa wakichangiwa damu kutoka kwa ndugu na jamaa zao, lakini kwa sasa hali imebadilika na wanaochangiwa na ndugu zao ni wachache sana ukilinganisha na wasio na watu wa kuwachangia, hali inayosababisha kuchelewa kwa huduma kutokana na kutokuwepo na damu katika benki hiyo.
Wachangiaji wakiendelea kujitolea damu.

Naye Shabani Mwin’juma Shekihenda, Mlemavu wa macho ambaye alijitokeza katika zoezi hilo la uchangiaji damu, ameshindwa kutimiza azma yake hiyo baada ya kupimwa na kugundulika kuwa damu yake ni ndogo na asingeweza kuhimili kama angetolewa.

Akizungumzia tukio hilo, Mwin’juma anasema amesononeshwa sana na kushindwa kuchangia damu kwani aliamini chupa ya damu yake ndogo ingeweza kunusuru maisha ya kiumbe mwingine.

Amesema Licha ya ulemavu wake lakini anauwezo wa kutembea sehemu yoyote ile, hivyo haina maana kuwa hana wajibu wa kusaidia wengine, ameguswa na tukio hilo na kuamua kutoka nyumbani kwakwe Buza kwa lengo la kutoa damu.

VIONGOZI NCHI MARAFIKI WAENDELEA KUTEMBELEA TANZANIA WAKIONGOZWA NA WAZIRI WA MAENDELEO YA KIMATAIFA WA NORWAY

0
0

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup atafanya ziara ya kikazi nchini kuanzia tarehe 27 hadi 30 Novemba 2018.

Wakati wa ziara yake nchini, Waziri huyo anatarajiwa kufanya mazungumzo na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ratiba ya Waziri huyo itahusisha pia mikutano na viongozi wengine wa Serikali wakiwemo Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango na Bw. Charles Kichere, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Mikutano hiyo itajadili namna ya kukuza uhusiano kati ya Tanzania na Norway hususani kwenye maeneo ya ukusanyaji wa mapato, mazingira, nishati na kilimo.

Mheshimiwa Waziri Astrup pia atatembelea Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme inayofadhiliwa na Serikali ya Norway ikiwemo iliyoanzishwa kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na mtambo wa kuzalisha umeme wa maji uliojengwa na Norway, Sweden na Finland kwenye miaka ya 1990 na kukarabatiwa hivi karibuni na Serikali ya Norway. Kwenye ziara mkoani Tanga, Waziri huyo ataambatana na Mhe. Subira Mgalu (Mb), Naibu Waziri wa Nishati.

Vilevile, Waziri huyo pamoja na Mhe. Omary Mgumba (Mb), Naibu Waziri wa Kilimo watatembelea maghala na mtambo wa kuhifadhi mbolea uliopo karibu na Bandari ya Dar es Salaam, unaomilikiwa na kampuni ya Yara kutoka Norway ambapo Waziri kutoka Norway atasaini makubaliano na uongozi wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ambapo Norway itasaidia Programu inayoitwa Farm to Market Alliance (FtMA) iliyo chini ya WFP.

Ratiba ya Waziri huyo itahusisha pia hafla itakayojumuisha watanzania waliowahi kusoma na kufanya kazi nchini Norway. Akiwa ni mmoja wa viongozi waliosoma nchini Norway, Mhe. Job Y. Ndugai (Mb), Spika wa Bunge la Tanzania atakuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo inayotegemewa kuhusisha washiriki wapatao 400.

Viongozi wengine wanaotarajiwa kufanya ziara nchini kati ya tarehe 27 na 30 Novemba 2018 ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Gorge Arreaza tarehe 29 Novemba 2018, Katibu Mkuu anayesimamia maendeleo na ushirikiano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Dernmark, Bw. Trine Rask tarehe 28 hadi 30 Novemba 2018 na Mkurugenzi anayesimamia nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Uswisi, Balozi Anne Lugon- Moulin tarehe 27 hadi 29 Novemba 2018. Ziara hizi zinalenga kuongeza wigo wa ushirikiano baina ya Tanzania na nchi hizo rafiki.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Tarehe 26 Novemba 2018

CDF YAADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

0
0
Na Agness Francis, Blogu Jamii 
SHIRIKA  la Utu wa Mtoto (CDF) kwa kushirikiana na Taasisi ya Ustawi wa jamii kupitia klabu yao ya Social work imeandaa mjadala katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani. 

Mjadala huo uliowakutanisha  Wahadhiri, washauri wa Vyuo, Viongozi wa serikali ya wanafunzi, wanafunzi wa vyuo pamoja na wawakilishi wa asasi za kiraia ambapo walijadili mada inayohusu ukatili wa kingono katika Taasisi za elimu ya juu. Tafiti za hivi karibuni zinaonyesha  kuwa wanafunzi wa kike walio katika vyuo vya elimu ya juu wako katika hatari ya kufanyiwa ukatili wa kingono.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la jukwaa la Utu wa Mtoto CDF,   Lenista Derugabo akizungumza na vyombo vya habari amesema kuwa lengo la kuandaa mjadala wa kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na  masuala ya ukatili wa kingono vyuoni ni kutaka kutokomeza janga hilo linalowakumba watoto wakike hasa walio katika Elimu ya   juu na kuona jinsi gani matokeo hayo yanapotea. 

"Tumeona ni vyema kuandaa mjadala huu kwa wanafunzi wa kike ambapo wako vyuoni kwa kuwa ndio watu wanaongoza kwa kufanyiwa ukatili wa kijinsia  hasa wakiwa masomoni kwa kulazimika kutoa rushwa ya ngono ili kupata alama nzuri katika masomo"amesema Derugabo. Mwanafunzi wa Chuo kikuu Bagamoyo Yudagaspa Mmari ameeleza kuwa  vitendo hivyo vya ukatili wa kingono vinaendelea vyuoni na kwa baadhi ya wanafunzi wanapofanyiwa ukatili huo  hukaa kimya. 

"Unakuta sio wote uelewa unafanana ikitokea labda maksi hazimridhishi mwanafunzi na lengo ni ufaulu vizuri, na hana uwezo wa kumpa pesa mwalimu basi kinachofata ni kutoa rushwa ya ngono." Ameeleza Yudagaspa. Mwanasheria Naemi Silayo amewataka wanafunzi kuvunja ukimya na kuwa na ujasiri wa kuzungumza yanapotokea mambo Kama hayo. 

"Siku hizi kuna utandawazi tumia basi hata simu kurekodi mazungumzo ili uwe na uhakika wa kutosha, vile vile tunaomba Serikali kupitia wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia  iliyo chini ya Profesa Joyce Ndalichako kuweza kuunda chombo huru ambacho hakitatetea walimu wa vyuoni, kwasababu wakati mwingine wanapendeleana ikitokea mwanafunzi amezungunza ukweli"amesema Mwanasheria Silayo. 

Aidha mwanachuo Mmari ametoa wito kuwa  wanafunzi wanapokwenda masomoni wazingatie masomo ili wafaulu vizuri na kuepukana na kutoa rushwa ya ngono, na walimu wawe kama walezi na  wazazi kwao.
 Mwanasheria Naemi Silayo akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu mbali mbali hapa nchini kuwataka wavunje ukimya kuwa na ujasiri wa kuzungumza pindi wanapokumbana na janga la ukatili wa kingono wanaofanyiwa na walimu wao, wakati wa kuhadhimisha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani Jijini Dar es Salaam.
Wahadhili, washauri  Vyuo vikuu pamoja na  wawakilishi  wa Asasi za kiraia wakijadili mada inayohusu ukatili wa kingono katika Taasisi za elimu ya juu, katika ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya usiku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
  Wanafunzi  mbali mbali wa Elimu ya juu  waliohudhiria katika mjadala wa kuhadhimisha siku 16 ya za kupinga ukatili wa kijinsi duniani, katika ukumbi  Chuo cha Ustawi wa Jamii Jijini Dar es Salaam.

“KASI YA UMEME MIJINI NA VIJIJINI NI ILE ILE’’- WAZIRI KALEMANI

0
0
NA YASINI SILAYO, GEITA

Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Medard Matogolo Kalemani akiwa Mkoani Geita, jana Novemba 25 amesema kuwa, kasi ya utekelezaji wa jukumu la kusambaza na kuunganisha wananchi na huduma ya umeme kwa maeneo ya Mijini na Vijijini kote Nchini ni ile ile ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha kuwa huduma ya Nishati ya umeme inatumika kuchochea na kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na huduma za kijamii Nchi nzima. 

Sisi Kama Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na Wakala wa Usambazaji Nishati ya Umeme Vijijini (REA) tumeendelea kusimamia na kutekeleza jukumu la kusambaza na kufikisha huduma za umeme kila pembe ya Nchi ikiwa ni Mijini na Vijijini” Alisema Waziri Kalemani. 

Aliongeza kuwa hivi sasa Wizara kupitia TANESCO na REA wanaendelea kutekeleza miradi ya usambazaji umeme Vijijini, lakini umeme huo unasambazwa kwa kasi ile ile maeneo ya mijini ikiwemo mitaa yenye makazi mapya na ile ya zamani ambayo ilikuwa bado hayajafikiwa na huduma za Umeme kupitia TANESCO yenye jukumu la kusambaza huduma hiyo katika maeneo ya Mijini. 

Alibainisha pia katika kuimarisha zaidi mpango wa usambazaji umeme vijijini serikali imeanza maandalizi ya kutenga fedha maalumu zitakazotumika kuchochea kasi ya usambazaji umeme maeneo ya mijini. 
Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Medard Kalemani, kulia akiongea na Wananchi pamoja na kutoa maelekezo kwa viongozi wa TANESCO na REA katika eneo la Bulengahasi lililopo Kata ya Katoro Mkoani Geita baada ya kukagua na kujionea maendeleo ya shuguli za usambazaji umeme eneo hilo. Kushoto kwake ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Geita Mhandisi Joaquim Ruweta.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiendelea na kazi ya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya kusambazia umeme katika kijiji cha mapinduzi kilichopo kata ya buseresere Wilayani Chato Mkoani Geita. Kushoto ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Geita Mhandisi Joaquim Ruweta na Kulia ni Diwani wa Kata ya Buseresere Bw. Godfrey Fulko.

BUNGE SPORTS CLUB YAAHIDI USHINDI MICHUANO YA EALA

0
0

Na  Mwandishi wetu, Dodoma
TIMU ya Bunge Sport Club imetamba kuvunja mazoea ya timu hiyo kushika nafasi ya pili na kurejea naushindi wa jumla katika michuano ya mashindano ya michezo ya Wabunge  wa Afrika Mashariki yanayotarajiwa kuanza Desemba mosi mwaka huu Jijini Bujumbura nchini Burundi. Tambo hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti na makocha na nahodha wa timu hiyo wakati timu hiyo ikiendelea na mazoezi makali  katika viwanja vya  Jamhuri na CBE Jijini Dodoma.

Mwandishi wetu amefika katika uwanja wa Jamhuri na uwanja wa CBE  asubuhi na kushuhudia timu hiyo ikiendelea na mazoezi makali ambapo kwa upande wa Soka ilikuwa chini ya Kocha Msaidizi ambaye ni Mbunge wa Wawi, Mheshimiwa Ahmed Juma Ngwali. Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kocha Msaidizi wa Timu ya Soka Mheshimiwa Ngwali ameahidi timu yake kuvunja mazoea ya kushika nafasi ya pili na kuahidi kurejea na ushindi.

“Naahidi matokeo mazuri, najua timu nyingi zimejiandaa kwa sababu haya ni mashindano makubwa, mara nyingi imezoeleka timu za Kenya au Uganda ndio zinashika nafasi ya kwanza, mara hii tunaenda kuvunja huo utaratibu lazima sisi tuchukue nafasi ya kwanza” alisema Mheshimiwa Ngwali  Mheshimiwa Ngwali amesema timu hiyo imejifua vya kutosha na wamejitahidi kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika michuano iliyopita.

Kwa upande wa timu ya Mpira wa Wavu inayojifua katika Viwanja vya Chuo cha Biashara CBE Kocha Salum, timu zote za Wanawake na Wanaume wameahidi kufanya vizuri katika michuano hiyo.
 Nahodha wa timu ya Mpira wa Wavu ya Wanaume Mheshimiwa Aeshi Hilary amesema wachezaji wa mpira wa wavu wako vizuri na amewaahidi wabunge na watanzania kwa ujumla kuwa wanaenda kuchukua Ushindi.

Naye Nahodha wa Timu ya Mpira wa Wavu ya Wanawake Mheshimiwa Jesca Kishoa amesema wachezaji wamejipanga kisawaswa kuhakikisha wanarejea nchini wakiwa na ushindi.  Katika mchezo wa Netiboli, Kocha wa timu Netiboli, Eleonora Mongi alisema maandalizi yanaendelea vizuri kwa mchezo huo na wanauhakika wa kutetea ubingwa wa mashindano hayo kutokana na maandalizi ya kueleweka waliyoyafanya.

Timu ya Bunge Sports Club imeweka kambi ya zaidi ya wiki tatu pamoja na kucheza michezo kirafiki ili kuangalia mapungufu ya timu kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Wachezaji wa mpira wa Wavu wa Bunge, (Wanaume) Mhe. Aeshi Hillary Mhe. Seif Gulamali na Mhe. David Silinde wakifanya mazoezi Uwanja wa Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma leo tayari kwa kushiriki michuano ya Mabunge ya Afrika Mashariki Bujumbura Burundi mapema mwezi ujao.
Mchezaji wa mpira wa Wavu wa Bunge, (Wanawake) Mhe. Rita Kabati akipiga mpira wakati wa mazoezi katika Uwanja wa Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma leo tayari kwa kushiriki michuano ya Mabunge ya Afrika Mashariki Bujumbura Burundi mapema mwezi ujao. Kushoto ni Mhe. Faida Bakari.
Mchezaji wa mpira wa Wavu wa Bunge, (Wanawake) Mhe. Neema Mgaya akipiga mpira wakati wa mazoezi katika Uwanja wa Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma leo tayari kwa kushiriki michuano ya Mabunge ya Afrika Mashariki Bujumbura Burundi mapema mwezi ujao. Kushoto ni Mheshimiwa Rita Kabati. PICHA NA OFISI YA BUNGE.

WAZIRI MKUU AZINDUA VIZA NA VIBALI VYA UKAAZI VYA KIELEKTRONIKI

0
0
*Yawataka watakaopewa kufanya shughuli zilizoelekezwa kwenye vibali vyao.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezindua huduma za viza na vibali vya ukaazi vya kielektroniki na amewataka watu wote watakaopewa vibali hivyo kutii sheria kwa kufanya shughuli ambazo wameelekezwa kwa mujibu wa vibali vyao na si vinginevyo.

Amesema utoaji wa huduma hizo ni miongoni mwa jitihada za Serikali katika kuvutia uwekezaji, hususan katika sekta ya viwanda kwani hatua hiyo itarahisisha upatikanaji wa vibali hivyo kwa raia wa kigeni na kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Novemba 26, 2028) wakati akizindua huduma za viza na vibali vya ukaazi vya kielektroniki katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kwamba hatua hiyo itasaidia kuondoa urasimu na ucheleweshwaji wa huduma pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi.

Amesema Idara ya Uhamiaji inatarajia kuanza kutoa huduma tajwa kwa raia wa kigeni muda wowote kuanzia sasa na kwa kupitia huduma hiyo, raia wa kigeni wataweza kuomba vibali hivyo kwa njia ya kielektroniki wakati wowote na mahali popote walipo.

Waziri Mkuu amesema watakaopewa vibali wanatakiwa kufanya shughuli zao kwa mujibu wa vibali vyao kwa sababu kufanya shughuli tofauti na ilivyoainishwa kwenye kibali ni kosa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Uhamiaji. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizindua Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 26, 2018.  Kulia ni  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni na wapili kulia ni Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Dkt. Anna Makalala.  


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Nchini, Dkt. Anna Makalala wakati alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam  Kuzindua  Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki , Novemba 26, 2018.  Katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  Nchini (TAKUKURU)  Kamishaina wa Polisi, Diwani Athumani baada ya Kuzindua Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 26, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mstaafu, Augustino Ramadhani baada ya Kuzindua Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 26, 2018. 

 Baadhi  ya Washiriki wa Uzinduzi wa  Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza kabla ya uzinduzi huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam , Novemba 26, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Mshindi wa nyumba na sh Milioni 20 Mbeya akabidhiwa fedha zake

0
0
Mshindi wa pili wa nyumba na sh Milioni 20 wa bahati nasibu ya Biko, Alex Nyoka, amekabidhiwa fedha zake jana mkoani Mbeya, ikiwa ni siku moja baada ya kuibuka kidedea kutoka kwenye droo ya 158 ya Biko, iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki.

Makabidhiano hayo yamefanyika jana Lujewa, Mbalari mkoani Mbeya na kuongozwa na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, huku mshindi huyo akizungumzia mkakati wake wa kujikwamua kimaisha baada ya kuibuka mshindi wa Biko.mechelewa kuamini kama ni kweli anaweza kuwa mshindi wa fedha nyingi na nyumba kutoka kwenye bahati nasibu pendwa ya Biko nchini Tanzania.

"Bado siamini kama ni kweli nimeshinda bahati nasibu ya Biko, ingawa nimeshika fedha hizi kwa sababu nilikuwa natamani nishinde ingawa najua waliokuwa wanataka ushindi huu sipo peke yangu.

"Kwakweli namshukuru Mungu kwa zawadi hii kubwa, huku nikiwataka Watanzania wengine wacheze Biko ili washinde kwa sababu sijawahi kuona bahati nasibu inayochezeshwa kwa uwazi na hata fedha zinaingizwa bank moja kwa moja, hivyo hakuna dalili ya unganyifu," Alisema.
 Mshindi wa nyumba na sh Milioni 20 wa Biko, Alex Nyoka, mkazi wa Mbalari mkoani Mbeya, akiwa na furaha tele baada ya kukabidhiwa fedha zake jana mkoani Mbeya.
Mshindi wa nyumba na sh Milioni 20 wa Biko, Alex Nyoka, mkazi wa Mbalari mkoani Mbeya, akiwa na furaha tele baada ya kukabidhiwa fedha zake jana mkoani Mbeya. Kulia kwake ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage.

SPIKA NA MAMEYA WA MANISPAA ZA JIJI LA DAR ES SALAAM WAIPIGA JEKI DCB KWA KUNUNUA HISA

0
0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndungai ( wa pili kushoto) akipokea nyaraka za ununuzi wa hisa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa, baada ya kununua hisa za benki hizo ofisini kwake Jijini Dodoma hivi karibuni, huku Meneja wa Tawi la DCB la Dodoma Joseph Njile (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Rahma Ngassa (kulia) wakishuhudia. Alijefichika kidogo ni Mkurugenzi wa Mikopo Isidory Msaki.
Mheshimiwa Spika, Job Ndugai (kushoto), akisalimiana na Ofisa Mauzo wa DCB tawi la Dodoma, Nuru Ashraf wakati akiwakarbisha yeye, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa (wa pili kushoto, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Rahma Ngassa na Mkurugenzi wa Mikopo, Isidory Msaki, ofisi kwake mjini Dodoma hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto), akifurahi pamoja na mameya wa manispaa za Jiji la Dar Salaam baada ya kila mmoja kujitokeza kununua hisa za benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kutoka kushoto kwake ni; Mstahiki Meya Ilala Charles Kuyeko, Mstahikli Meya wa Kigamboni Mbadi Hoja, Maya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita , Mstahiki Meya wa Ubungo Boniface Jacob na Mstahiki Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta. Kulia ni Mkurugenzi wa Mikopo wa DCB, Isidory Msaki. Hisa moja inuzwa kwa bei pungozo ya shs 265.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni, Mabadi Hoija akijaza fomu kwa ajili ya kununua hisa. Kushoto ni mfanyakazi wa DCB Brino Londo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Godfrey Ndalahwa (kushoto) akimshukuru Mstahiki Meya wa Ubungo Jacob Boniface baada ya kununua hisa za benki hiyo. Kulia ni mfanyakazi wa DCB Catherine Ngassa.
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images