Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109584 articles
Browse latest View live

Taifa linahitaji watakwimu katika kusukuma maendeleo- Dkt. Kijaji

0
0
 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa kufikia uchumi wa kati kufikia 2025 kunategemea kuwepo kwa takwimu rasmi na bora  ambazo ndio zitaonesha maendeleo yaliyofikia kufika mwaka huo. Dkt Ashatu ameyasema hayo katika Mahafali ya Nne ya Chuo cha Takwimu yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es salaam.

 Amesema kuwa wahitimu wa chuo cha takwimu wanajibu wa kufikiria ni kitu gani wanaenda  kuzalisha kwa taifa kuweza kunufaika na utalaam huo kwa maendeleo ya taifa. Dkt. Ashatu amesema kuwa kupungua idadi ya wanaojiunga katika chuo cha takwimu sio tatizo kwani wanaohitajika ni watu wenye ujuzi na ubunifu ambao wataleta mageuzi ya takwimu katika taifa.

Aidha amekiagiza Chuo hicho kufundisha takwimu shirikishi kutokana na kuwepo maswali mwngi yanayotoa changamoto kwa wananchi hivyo ni chuo kiweze kutatua changamoto hizo kupitia takwimu shirikishi. “Bila takwimu hakuna mipango na mipango bila takwimu hakuna maendeleo hivyo wahitimu lazima muonyeshe ujuzi na umahiri wenu katika ofisi mtazoenda kufanya kazi na kuleta mabadiliko  chanya  ya kusaidia taifa”amesema Kijaji.

Amesema kuwa chuo kinawajibu wa kuzalisha watalaam wenye weledi ambao watakidhi soko la ajira kutokana na eneo hilo kuwa muhimu katika maendeleo ya nchi yeyote duniani. Kaimu Mkuu wa Chuo Takwimu Dkt. Frank Mkumbo amesema kuwa safari haikuwa ndogo katika kufikia siku ya leo katika kuwaandaa watalaam ambao wataleta mbadiliko katika sekta ya takwimu.

Amesema kuwa wameanzisha shahada ya takwimu za kilimo kutokana na uhitaji wake mkubwa kwa taifa kupata takwimu rasmi katika sekta hiyo kwa kushirikiana na NBS pamoja na Ofisi ya Rais Tamisemi. Dkt Mkumbo amesema chuo hicho kinapata wanafunzi katika nchi mbalimbali za Afrika  baadhi ya nchi hizo  ni Kenya, Uganda, Rwanda, Botswana, Zimbambwe , Elntrea , Sudani Kasikazi na Sudani Kusini, Ephiopia, Ghana, Msumbiji
 Naibu Waziri Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza katika Mahafali ya Nne ya Chuo cha Takwimu yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri wa Chuo hicho Dkt Albina Chuwa akiazungumza kuhusiana mahitaji ya watalaam watakwimu katika Mahafali ya Nne ya Chuo cha Takwimu  Takwimu yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Dkt Frank Mkumbo akitoa taarifa ya Mahafali ya Nne ya Chuo Takiwimu Takwimu yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri Dkt. Ashatu Kijaji akitunuku wahitimu katika chuo cha Takwimu.



TAZAMA LIVE WASAFI FESTIVAL 2018 KUTOKA MTWARA

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI NA MKEWE MAMA JANETH MAGUFULI WAMESALI IBADA YA MISA TAKATIFU DOMINIKA 34 KATIKA KANISA LA MTAKATIFU PETRO PAROKIA YA OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM.NOVEMBA 25,2018.

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 34 ya mwisho wa mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo ni mwisho wa mwaka ya sherehe ya Kristo Mfalme iliyoongozwa na Padre Projestus Marko Kahitwa . Novemba 25,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa sadaka yake wakati wa Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 34 ya mwisho wa mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo ni mwisho wa mwaka ya sherehe ya Kristo Mfalme iliyoongozwa na Padre Projestus Marko Kahitwa . Novemba 25,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakipeana mkono wa Amani na Masista na waumini walipojumuika na waumini wengine wakati wa Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 34 ya mwisho wa mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo ni mwisho wa mwaka ya sherehe ya Kristo Mfalme iliyoongozwa na Padre Projestus Marko Kahitwa . Novemba 25,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikomunika Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 34 ya mwisho wa mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo ni mwisho wa mwaka ya sherehe ya Kristo Mfalme iliyoongozwa na Padre Projestus Marko Kahitwa . Novemba 25,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoka kanisani mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 34 ya mwisho wa mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo ni mwisho wa mwaka ya sherehe ya Kristo Mfalme iliyoongozwa na Padre Projestus Marko Kahitwa . Novemba 25,2018.PICHA NA IKULU

MHANDISI NYAMHANGA AAGIZA MKANDARASI KURUDI ENEO LA KAZI

0
0

Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga, ameagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kumuandikia barua mkandarasi wa Kampuni ya Impesa di Construzioni anayejenga kituo cha ukaguzi wa pamoja (one stop inspection station) eneo la Manyoni mkoani Singida na Nyakanazi mkoani Kagera kurejea eneo la kazi na kuendelea na ujenzi.

Akizungumza katika kijiji cha Muhalala mkoani Singida wakati wa ukaguzi wa kituo hicho, Katibu Mkuu huyo amesema Serikali tayari imeshashughulikia madai ya mkandarasi huyo, hivyo hana sababu ya kutoendelea na ujenzi wa mradi huo. “Naagiza Mkandarasi huyu arudi eneo lake la kazi na kuanza kazi ya ujenzi wa mradi huu mara moja”, amesema Mhandisi Nyamhanga.

Aidha, Mhandisi Nyamhanga, ameeleza kuwa jumla ya gharama za mradi wa vituo hivyo ni takribani shilingi bilioni 55, ambayo itahusisha gharama za ujenzi, usimamizi na fidia.Mhandisi Nyamhanga amefafanua kuwa ujenzi wa kituo hicho unaenda sambamba na ujenzi wa kituo kingine eneo la Nyakanazi mkoani Kagera ambapo kituo kingine cha vigwaza mkoani Pwani kimeshakamilika na hivyo kutafanya jumla ya vituo vikuu vitatu vya ukaguzi vyenye umbali wa kilomita 500 kutoka kwa kila kimoja.Amefafanua kuwa lengo la ujenzi wa mizani hizo ni kupunguza vizuizi barabarani na gharama za usafirishaji wa mizigo kupitia barabara ya ukanda wa kati.

Kwa sasa magari ya mizigo husimama takriban katika vituo 31 ambapo kati ya hivyo vituo nane ni vya mizani, vituo 20 ni vya polisi na vituo 3 ni vya ukaguzi wa mapato ambavyo vyote viko kati ya Dar es Salaam hadi mipaka ya Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa umbali wa kilomita 1000.Awali, akitoa taarifa za maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho, Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida Mhandisi Masige Matari, amesema ujenzi wa kituo hicho umefikia asilimia 60 na kazi zinazoendelea kutekelezwa ni kama vile barabara zinazoingia na kutoka kituoni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akikagua moja ya boksi kalvati iliyojengwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, Mkoani Tabora.
Muonekano wa baadhi ya nyumba za watumishi wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Polisi watakaoishi mara baada ya ujenzi wa Kituo cha Ukaguzi wa Pamoja kukamilika katika kijiji cha Muhalala, Wilayani Manyoni, Mkoani Singida.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri Adel alkhateeb, anayesimamia ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami wakati alipoukagua mradi huo, Mkoani Tabora.

Muonekano wa kazi zikiendelea za ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora. Ujenzi wa sehemu ya barabara hiyo utafungua mkoa huo na mikoa ya Katavi na kigoma.



Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Singida Mhandisi Masige Matari, akitoa taarifa ya mradi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja (One Stop Inspection Station), katika kijiji cha Muhalala, wilayani Manyoni, mkoani humo.

Miaka Mitatu ya Mageuzi Katika Sekta ya Afya

UKATILI WA KIJINSIA NI KANSA MPYA NCHINI-DKT NDUGULILE

0
0

Imesemekana kuwa vitendo vya Ukatili wa kijinsia kwa miaka hivi karibuni vimezidi kukithiri na kuathiri wanawake na Watoto nchini nahivyo kufikia hatua ya kufananishwa na ugonjwa wa Kansa. 

Hayo yamebainishwa wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Shirika lisilo la Kiserikali la Kilimanjaro Women Information Exchange Community Organization (KWIECO) na kujionea shughuli za huduma za kisheria zinazotolewa kwa wahanga wa Ukatili wa Kijinsia katika Mkoa wa Kilimanjaro. 

Naibu Waziri Ndugulile amesema vitendo vya Ukatili wa Kijinsia vimekuwa vinaongezeka sana na kwa mwaka 2017 vitendo 41,000 viliripotiwa na kati ya hivyo vitendo 13,000 vilifanywa dhidi ya watoto. “Kwa idadi ya vitendo hivi vya kikatili ingekuwa kwa ujambazi hali ingekuwa mbaya yani ukatili wa kijinsia ndio Kansa mpya nchini” alisisitiza Dkt. Ndugulile 

Dkt. Ndugulile amewataka Wataalam wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii kutoka ofisini na kwenda kwa wananchi kusikikiza kero na kutatua changamoto zao ili kuwapa chachu ya kuboresha maendeleo na ustawi wao. Amesisitiza kuwa Serikali imeamua kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuanzisha Mpango Mkakati wa Taifa wa Kutokomeza vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watotokwa kipindi cha mwaka 2016/2017 hadi 2021/2022 ili kuondokana kabisa na vitendo hivyo dhalili. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wana Shirika la KWIECO lilichopo Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro linaloshughulisha na utoaji wa masaada wa kisheria kwa wahanga waliofanyiwa vitendo vya ukatili wa Kijinsia. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenzwa na wanachama wa Shirika la Floresta Tanzania lililopo Marangu Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya kukagua kazi zinazofanywa na wanawake wajasiriamali mkoani humo 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia mua uliokuzwa vizuri kwa njia za kiasili bila kutumia mbolea za kisasa unaolimwa na wanawake wajasiriamali wa Umoja wa Vicoba Marangu (UVIMA) uliopo Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya kukagua kazi zinazofanywa na wanawake wajasiriamali mkoani humo
Wanakikundi kutoka Shirika la Floresta na kutoka Umoja wa Vicoba Marangu (UVIMA) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo Pichani) wakati akizungumza nao mara baada ya kukagua shughuli wanazofanya .

Biteko Atatua Mgogoro Sugu Madini

0
0
Ni baada ya kruhusu wananchi kijiji cha Mhandu kuendelea na uchimbaji dhahabu 


Na Greyson Mwase, Shinyanga

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameruhusu wananchi wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kuendelea na uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la utafiti wa madini hayo lililokuwa linamilikiwa na Menan Sanga kwa kushirikiana na kampuni ya Lion Town.

Biteko aliyasema hayo leo tarehe 24 Novemba, 2018 katika mkutano wa hadhara ulioshirikisha wananchi wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa huo yenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto za wachimbaji wa madini.

Katika ziara hiyo, Biteko aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, Mbunge wa Jimbo la Msalala, Ezekiel Maige, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Wataalam kutoka Wizara ya Madini pamoja na waandishi wa habari.

Biteko alisema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini haiwezi kuruhusu mwekezaji kumiliki eneo pasipo kuliendeleza, kutokulipa kodi inayohitajika Serikalini huku wananchi wenye nia ya kuchimba katika eneo husika wakiendelea kuteseka.

Alisema kuwa, Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli imeweka mikakati mbalimbali ya uboreshaji wa Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja marekebisho ya Sheria ya Madini inayotambua madini kama rasilimali za watanzania wote.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga tarehe 24 Novemba, 2018 ikiwa ni sehemu ya ziara yake kwenye mkoa huo yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani ) kwenye mkutano wa hadhara.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia mbele) akiendelea na ziara katika eneo la uchimbaji wa chini ya ardhi kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu uliopo katika eneo la Kakola Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akipata maelezo jinsi shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu zinavyofanyika chini ya ardhi katika eneo la Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na msafara wake pamoja na watendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu kabla ya kushuka chini ya ardhi ili kujionea uchimbaji wa madini unavyofanyika.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati mbele) akiendelea na ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu uliopo katika eneo la Kakola Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.


TAKUKURU PWANI YAFUATILIA MIRADI NANE YA BILIONI 9.8 AMBAYO INATILIWA SHAKA

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 


TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU )mkoani Pwani ,inafuatilia miradi nane yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 9.800.4 kutokana na kuitilia shaka. 

Aidha taasisi hiyo imetaja,idara zinayoongoza kwa malalamiko ya vitendo vya rushwa ,kuwa ni serikali za mitaa kwa malalamiko hasa katika mamlaka za watendaji wa vijij,mitaa na kata, ikifuatiwa na polisi.

Kamanda wa TAKUKURU mkoani Pwani, Suzan Raymond alieleza hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji katika kipindi cha miezi mitatu. Alieleza, miradi tisa ilifuatiliwa katika kipindi cha julai – septemba mwaka huu ,ikiwa ni pamoja na sekta ya kilimo, afya, maji na elimu. 

Susan alisema, kati ya miradi hiyo iliyofuatiliwa, miradi nane inatiliwa shaka na uchunguzi unaendelea ili ikibainika kuna mapungufu hatua zaidi zitachukuliwa. WAKATI HUO HUO katika kipindi hicho ,taasisi hiyo ilipokea malalamiko 79 kati ya hayo malalamiko 35 yanahusiana na vitendo vya rushwa na uchunguzi wake unaendelea.

Suzan alifafanua, idara inayoongoza kwa malalamiko ya vitendo vya rushwa ni serikali za mitaa kwa malalamiko 21, ikifuatiwa na polisi 09, binafsi 08, baraza la ardhi 07, mahakama malalamiko 06, elimu 06, Afya 05, Ardhi 04, Kilimo 03, Ujenzi 02, fedha 02, TASAF 01, NIDA 01, Siasa 01, Uhamiaji 01, mali asili 01 na RITA 01. 

Kwa mujibu wa Suzan , hadi sasa jumla ya kesi 28 zinaendelea kusikilizwa katika mahakama mbalimbali za Pwani. Alielezea katika kipindi cha julai – septemba ,kesi nne zimeamuliwa kati ya hizo tatu zimeshinda na moja mshitakiwa ameachiwa huru. 

Kamanda huyo, ameomba ushirikiano kwa jamii katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa na kuwa tayari kutoa ushahidi kwa mtu mmoja mmoja ama taasisi kwa lengo la kuthibitisha uwepo wa vitendo vya rushwa vinavyotolewa taarifa.

Wananchi na Wadau wa Maendeleo wahamasishwa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF)

0
0

Wananchi na Wadau wa Maendeleo wamehamasishwa kujitokeza kuchangia fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF) ili kujenga uwezo na kuongeza mapambano dhidi ya ugonjwa huo ambapo takribani milioni 15 zimechangishwa katika hafla iliyofanyika leo Jijini Dodoma ikitanguliwa na matembezi ya hisani.

Akizungumza leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge , wakati wa hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amesema kuwa kuna umuhimu Mkubwa wakuchangia mfuko huo ili Taifa liweze kujitegemea katika kuendeleza mapamabano dhidi ya UKIMWI.
” Tuwe wepesi kuchangia mfuko huu kupitia namba 0684909090 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kupambana na UKIMWI hapa nchini”; Alisisitiza Mhe. Shekimweri

Akifafanua amesema kuwa kuna haja ya kuweka mikakati ya pamoja katika mapambano dhidi ya UKWIMWI hapa nchini ikiwemo kuangalia namna bora yakuwaelimisha vijana hasa walio mashuleni kwa kutumia mbinu za kisasa. Aliongeza kuwa, Kwa sasa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI katika mkoa wa Dodoma yameongezeka kutoka asilimia 2.5 hadi asilimia 5 mwaka 2017 hali inayotaka mikakati zaidi ikiwemo udhibiti wa nyumba za kulala wageni na elimu kwa makundi maalum kama wanafunzi wa Shule na Taasisi za elimu zilizopo katika mkoa huo.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Bw. Jabir Shekimweri akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akizungumzia mambo yatakayofanyika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ikiwemo wiki ya maonesho itakayoenda sambamba na kuanzishwa kwa jiji cha vijana ndani ya uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ambapo vijana watajifunza masuala mbalimbali ikiwemo Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Upimaji wa Virusi vya UKIMWI, Ushauri nasaha, upimaji wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama shinikizo la damu na kisukari . 

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI (UNAIDS) hapa nchini Dkt. Leo Zekeng wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya  hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI. 
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI (UNAIDS) hapa nchini Dkt. Leo Zekeng akizungumzia hali ya UKIMWI Duniani ambapo alibainisha kuwa takribani watu milioni 37 wameambukizwa virusi hivyo, hayo yamejiri leo wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI. 
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Bw. Jabir Shekimweri (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wananchi walioshiriki katika wa hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI. 
Kikosi cha Bendi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikiongoza matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI kwa lengo la kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF). 

JAFO ARIDHISHWA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA AFYA MPWAYUNGU

0
0


Nteghenjwa Hosseah, Mpwayungu. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameridhishwa na miundombinu ya Afya inayoendelea kujengwa katika kituo cha Afya Mpwayungu kilichopo katika Jimbo la Mtwera Wilayani Chamwino.

Jafo ameonyeshwa kuridhishwa kwake alipokwenda kutembelea kituo hicho na kukagua ujenzi wa miundombinu ya Afya inayoendela ambapo kituo hicho ni miongoni mwa vituo vya Afya Nchini vilivyopokea Fedha Tsh Mil 400 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Maabara, Upasuaji, chumba cha kuhifadhia maiti pamoja na nyumba ya mganga.

“Mmewatendea haki wananchi wa Mpwayungu kituo hiki mimejengwa kwa kiwango kinachostahili nina uhakika na huduma zitakazotolewa hapa ni za uhakika na ile adha waliyokuwa wanapata wananchi ya kutembea umbali mrefu wa kufuata huduma za upasuaji sasa wataweza kuzipata hapa hapa” alisema Jafo.Wakati huo huo Waziri Jafo alimuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino kutafuta Fedha kwa ajili ya kukamilisha vitu vidogo vidogo ambavyo havijakamilika katika majengo mapya yaliyojengwa.

Naye Mbunge wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde amesema anaishukuru Serikali ya awamu ya Tano kwa kuona na kujali shida za wananchi wa Mpwayungu kwa kuwapelekea fedha kwa ajili ya uboreshaji wa Kituo cha Afya.Kituo hiki kinahudumia wananchi wengi sana wa Mpwayungu na maeneo ya jirani hivyo kwa kupata majengo haya mapya yatasaidia katika kutoa huduma ambazo hapo awali zilizkua hazipatikani kutokana na uhaba wa majengo na vifaa amesema Lusinde.

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bi. Asteria Mpota amesema kuwa ujenzi wa miundombinu ya Afya imefikia asilimia 95 na kuwa ameshakamilisha mchakato wa kuleta watumishi wapya watakaongeza nguvu katika utoaji wa huduma za Afya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(katikati) akiwasili katika kituo cha Afya Mpwayungu kilichopo katika Jimbo la Mtera Wilayani Chamwino ambacho ni miongoni mwa Vituo vilivyopokea Tsh Mil. 400 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Afya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(katikati) akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya Mpwayungu wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Chamwino.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(katikati) akizungumza na wananchi wa Mpwayungu(hawapo pichani) wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Chamwino.

ILI UPATE KITAMBULISHO CHA TAIFA LAZIMA UPITIE MCHUJO MKALI, SERIKALI IPO MAKINI KUEPUKA KUTOA KWA WAHAMIAJI HARAMU-WAZIRI LUGOLA

0
0

Na Felix Mwagara, MOHA.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema vitambulisho vya taifa vitatolewa kwa watanzania wenye sifa ambao watapita katika mchujo ili kuepusha kutoa kwa wahamiaji haramu.

Amesema mchujo huo unaofanywa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) upo makini ili kuhakikisha hakuna makosa yatakayofanywa wakati wa utoaji wa vitambulisho, hivyo wananchi wawe na uvumilivu wakati mchujo huo ukiendelea.

Waziri Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara aliyasema hayo leo, wakati alipokua anazungumza na mamia ya wananchi wa jimbo lake katika Kijiji cha Mwisenyi, Kata ya Butimba, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara na kuwataka wapiga kura wake na Watanzania kwa ujumla wawe na subira wakati hatua za utambuzi na usajili zikiendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini.

“Hakuna Mtanzania mwenye sifa atakayekosa kitambulisho cha taifa, lakini lazima muwe na subira wakati zoezi la utambuzi wa watu gani wanaweza kupata vitambulisho hivi, na pia katika utambuzi tunapaswa kuwa makini sana kwasababu tusije tukapenyeza wahamiaji haramu wasiostahili na wao wakaweza kupata vitambulisho na baadaye tukaja kupata shida,” alisema Lugola.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mwisenyi, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo kwa kuwa msimu wa kilimo umeshafika. Na pia aliwataka wananchi hao waondoe hofu ya kutopata vitambulisho vya taifa kwani Watanzania wote wenye sifa watavipata vitambulisho hivyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kamulebya, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo kwa kuwa msimu wa kilimo umeshafika. Na pia aliwataka wananchi hao waondoe hofu ya kutopata vitambulisho vya taifa kwani Watanzania wote wenye sifa watavipata vitambulisho hivyo
Mkazi wa Kijiji cha Kamulebya, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, Mzee Range, akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (hayupo pichani), wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo. Lugola aliwapa nafasi wananchi kutoa kero zao ndani ya Jimbo lake. Pia aliwataka wananchi hao waondoe hofu ya kutopata vitambulisho vya taifa kwani Watanzania wote wenye sifa watavipata vitambulisho hivyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Afisa Tarafa ya Kenkombyo, Rebeca Mdodo alipokua anatoa taarifa ya Tarafa yake kwa Waziri Lugola, kabla ya Mbunge huyo hajaanza kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Bulamba, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara. Lugola ameanza ziara jimboni humo leo akisikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo. Pia aliwataka wananchi hao waondoe hofu ya kutopata vitambulisho vya taifa kwani Watanzania wote wenye sifa watavipata vitambulisho hivyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

21 JELA KWA KUSHINDWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE

0
0
Na Mwandishi wetu Tunduru

MAHAKAMA ya Mwanzo Mbesa wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma,imewahukumu kifungo cha miezi mitatu jela au kulipa faini ya shilingi laki tatu wazazi 21 baada ya kupatikana na kosa la kushindwa kupeleka watoto wao shule.

Aidha, mahakama hiyo imetoa hukumu ya kuchapwa viboko vinne kila mmoja watoto 21 ambao ni wanafunzi wa shule ya sekondari Mbesa kwa kosa la kutokwenda shule.

Hukumu hiyo imetolewa jana na hakimu wa mahakama ya Mwanzo Mbesa Kavula Katabu ambapo wazazi wawili kati yao,waliachiwa huru baada ya kulipa faini.Akitoa hukumu hiyo mbele ya mamia ya wananchi wa kijiji cha Mbesa waliofika mahakamani hapo hakimu Katabu alisema,wazazi hao wametiwa hatiani kwa mujibu wa kifungu cha 8(E) na kifungu cha 14 cha sheria ya mtoto ya mwaka 2009.

Kwa upande wa wanafunzi Katabu alisema, wamekutwa na kosa la kukataa kwenda shule na hivyo kuwatia hatiani wanafunzi hao kwa mujibu wa sheria ya Elimu namba 25 cha mwaka 1978 kifungu cha 2 na kifungu kidogo cha 4.

Wakizungumza nje ya mahakama,baadhi ya wananchi wamepongeza uamuzi wa mahakama kwa kutoa hukumu hiyo kwa kuwa itasaidia sana kupunguza tatizo la utoro kwa wanafunzi na wazazi wenye tabia ya kukatisha masomo watoto wao na badala yake wanawafanyisha kazi za nyumbani ikiwemo kuokota korosho mashambani.

Ali Mohamed na Rashid Said walisema, hukumu hiyo imefika kwa wakati muafaka kwani ndiyo msimu wa kuandikisha watoto wenye sifa ya kuanza elimu ya awali,msingi na wale watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza.Kwa upande wake,mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera alisema, operesheni ya kuwasaka wazazi na watoto wasiotaka kwenda shule ni endelevu katika tarafa zote saba katika wilaya hiyo.

Amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanapeleka watoto wao shule kupata elimu ambao ndiyo urithi mkubwa kwa mtoto badala ya kuanza kuwafanyisha kazi za nyumbani ambazo zina changia sana tatizo la umaskini kwa baadhi ya kaya.

WANANCHI WILAYA YA TUNDURU WAMSHUKURU RAIS DKT MAGUFULI KWA KUCHUKUA HATUA ZA KUMKOMBOA MKULIMA

0
0

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme wa pili kulia akiwa ameshika jembe pamoja na baadhi ya wananchi wa kata ya Mindu wilaya ya Tunduru kama ishara ya matumizi ya Ardhi kwa ajili ya kilimo endelevu ya kumkomboa mkulima katika umaskini,Kushoto kwake mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akishiriki maandamano ya Amani na wananchi wa kata ya Mindu wilaya ya Tunduru kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt John Magufuri kutokana na uamuzi wake wa kununua korosho katika msimu wa 2018/2019 kwa bei ya shilingi 3300.
Mkazi wa kijiji cha Mtonya Issa Yasin aliyepiga magoti,aliyeuz tani 4 na kg 200 za korosho na kujipatia kiasi cha shilingi milioni 13.8 akimshukuru Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme kwa niaba ya Rais Dkt John Magufuri kutokana na uamuzi wa serikali ya awamu ya tano kununua zao la korosho katika msimu wa 2018/2019 kwa bei ya 3300.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme kulia,akimpongeza mkazi wa kijiji cha Mtonya ambaye ni mkulima wa korosho Issa Yasin baada ya kujipatia zaidi ya shilingi milioni 13.8 kutokana na kuuza korosho tani 4.200 kwa bei ya shilingi 3,300.Picha na Muhidin Amri

WADAU WAJITOKEZA KUUNGA MKONO KAMPENI YA UZALENDO

0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo  kwa wadau wa Wizara hiyo katika  hafla fupi  ya Uzinduzi wa Uzalendo na Utaifa iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam .
 Kaimu Mkurungezi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa  Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Leah Kihimbi akiongea jambo na wadau wa Wizara hiyo (Hawapo katika picha) katika  hafla fupi ya Uzinduzi wa  Kampeni ya Uzalendo na Utaifa leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mawasiliano na Uhusinao wa Umma kutoka benki ya NBC Bw. William Kallage ambao  ndio Wadhamini Wakuu wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa mwaka  huu inayotarajiwa kufanyika tarehe 8  Disemba  2018 Jijini Dodoma, akieleza jambo kwa wadau wenzake waliofika kuunga mkono uzinduzi wa kampeni hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurungezi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa,  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi(kulia) akimvalisha nembo inayoashiria uzalendo Mkuu wa Mawasiliano na Uhusinao wa Umma kutoka benki ya NBC Bw. William Kallage ambao ndio wadhamini wakuu wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa mwaka  huu inayotarajiwa kufanyika tarehe 8  Disemba  jijini Dodoma.
 Wadau wa Sanaa kutoka katika sekta binafsi taasisi za Serikali wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea  katika  hafla fupi ya uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa leo Jijini Dar es Salaam.

WAZIRI DKT.KIGWANGALLA AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 289 WA CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI-MWEKA

0
0

Na Andrew Chale,Moshi.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla amewataka watumishi walio kwenye Wizara yake hiyo kupitia mafunzo ya Jeshi Usu ili kujiimalisha zaidi katika kutokomeza vitendo vya ujangili wa Maliasili zilizopo sehemu mbalimbali hapa nchini.

Waziri Dkt. Kigwangalla amesema hayo Novemba 24, 2018 wakati wa kuwatunuku vyeti wahitimu 289 katika kozi mbalimbali ikiwemo Shahada, Stashahada na Astashada kwenye Usimamizi wa Wanyamapori na Utalii kwenye Mahafali ya 54 ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori- Mweka, Wilayani Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Akielezea suala la kupata mafunzo kwa watumishi hao, amesema suala hilo la uhifadhi ni la kudumu hivyo ni vyema watumishi hao kujiandaa katika ulinzi wa Maliasili za Taifa.Dkt Kigwangalla amesema mifumo wanayotengeneza ikiwemo Jeshi Usu lazima ifanye kazi imara na iwe madhubuti ili kusaidia kulinda Malisili zilizopo kwani hali ya uvamizi wa wananchi na waalifu wa Maliasili za taifa ni kubwa.

“Kama Serikali tuna nia na dhamira ya dhati ya kulinda na uhifadhi Maliasili tulizonazo ambazo ni urithi sio tu kwa watoto wetu hapa Tanzania, lakini ni urithi wa vizazi na vizazi vya Dunia yote” amesema Dkt. Kigwangalla.Aidha, Waziri Dkt. Kigwangalla ametoa wiki mbili kuanzia Novemba 24, kwa taasisi nne zilizo chini ya Wizara hiyo Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kila kutoa Shilingi Milioni 100 ilikuchangia ujenzi wa jengo la Utawala na mafunzo chuoni hapo ili kuanza mara moja ujenzi wa jengo hilo jipya.

Waziri wa Maliasi na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akimtunuku cheti Mhitimu wa Shahada ya Usimamizi wa Wanyamapori, katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka katika mahafali ya 54 yaliyofanyika jana Novemba 24, 2018 chuoni hapo katika wilaya ya Moshi mkoani Kiliamanjaro. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho. Jumla ya wahitimu 289, wa kozi mbalimbali walitunukiwa vyeti.
Waziri akicheza muziki wa Kwaito na wahitimu
Waziri akizungumza katika mahafali hayo

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi na Maliasili Nape Nnauye akizungumza katika tukio hilo.
Waziri wa Maliasi na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akipokea zawadi ya picha ya kuchorwa aliyochorwa na mwanafunzi wa chuo hicho (kushoto) anayemkabidhi. Wakati wa tukio la kukabidhi zawadi katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka katika mahafali ya 54 yaliyofanyika jana Novemba 24, 2018 chuoni hapo katika wilaya ya Moshi mkoani Kiliamanjaro.


WATANZANIA HAWABABAISHWI NA WANASIASA WENYE MAWAZO DUNI-SHAKA

0
0

Na Ripota Wetu, Morogoro

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa morogoro, Shaka Hamdu Shaka amesema Watanzania hawana shauku wala ndoto ya kufanya mabadiliko ya utawala kwa kuwategemea wanasiasa wenye mtazamo na mawazo duni.

Amesema katika kipindi hiki ambacho Serikali ya CCM ikijibadili kimfumo na kisera kukidhi matakwa ya wananchi na wakati ni vigumu vyama vya upinzani kushika dola.

Shaka alitoa kauli hiyo wakati aliposhiriki mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari Morogoro Open School, Mkoani hapa. “Tofauti ya kati ya viongozi CCM na wa vyama vingine, viongozi wa Serikali ya CCM hujikuta katika kujadili hoja na utekelezaji wa mipango na si kuishi kwa nadharia isiyo na tija.

Aliongeza: “Serikali ya CCM itabaki kuamini katika siasa ya ujamaa na kujitegemea. Tangu zama za sera za uchumi hodhi na ujio wa soko huria na utandawazi, CCM imekataa kushikilia ukale bali hufanya mabadiliko ya kisera,”alisema

Alisema anayefikiria siasa ya ujamaa na kujitegemea imekufa hawana uelewa kwani serikali inaposomesha wanafunzi bure, kutoa huduma bora za afya ni katika utekelezaji wa msingi ya ujamaa. Katibu huyo wa CCM mkoa, alisema wanasiasa hawapaswi kukosoa kwa pupa na jazba badala yake wawe na vipimo vya uhalisia wa madai yao kwani wananchi ni werevu, wanajua kutofautisha yaliyokuwepo na ufanisi wa mabadiliko yanayooneka.

Shaka aliwahimiza wanafunzi kuendelea kujenga matumaini kwa sera za CCM kwani ndicho chama chenye uwezo wa kufanyakazi kwa uhodari katika kuleta maendeleo. “Nawawatia shime wanafunzi mjipe jukumu la kusoma kwa bidii. Wale waliohitimu watambue wana jukumu la kujiandaa mwa kutumia fursa zinazotolewa na serikali pia mshiriki ushindanikwenye soko la ajira” alisema Shaka

HALMASHAURI NA MIJI ILIYOFANYA VIBAYA KATIKA MASHINDANO YA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA ZATAKIWA KUJITATHMINI

0
0

NA WAMJW-DODOMA

Halmashauri za Miji, Majiji, Wilaya, Vitongoji na Vijiji zilizofanya vibaya katika mashindano ya afya na usafi wa mazingira zimetakiwa kujitathmini na kuhakikisha zinaweka mikakati madhubuti ya utunzaji wa mazingira.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kilele cha wiki ya usafi wa mazingira ulioenda sambamba na mkutano uliojumuisha Maafisa Afya nchini na Wadau mbalimbali wa maendeleo kilichofanyika jijini Dodoma.

Waziri Ummy alisema hayo wakati akitaja washindi waliofanya vizuri katika Halmashauri za Miji, Majiji, Wilaya, Vitongoji na Vijiji viliyofanya vizuri katika mashindano ya afya na usafi wa mazingira ambayo Wizara imekuwa ikitekeleza tangu mwaka 1988.

“Mashindano hayo huanza katika ngazi ya Kitongoji na kuhitimishwa kwa kupata washindi wa kitaifa. Kila mwaka tumekuwa tukiboresha mashindano haya ambapo kwa mwaka huu tumeongeza makundi manne kutoka sita ya awali. Makundi yalioongezeka ni; Hospitali za Rufaa za Binafsi, Shule za Msingi za Vijijini, Shule za Sekondari za Bweni za Serikali, na Shule za Sekondari za Bweni za Binafsi”. Alisema Waziri Ummy.

Aidha, waziri huyo alitaja makundi ya washindi waliofanya vizuri na makundi ya Halmashauri, Majiji na Mikoa iliyofanya vibaya.

Katika kundi la Halmashauri za Manispaa na Majiji lilihusisha Manispaa 25, ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ilikua kinara kwa asilimia 92.7, ikifuatiwa na mshindi wa pili Halmashauri ya Jiji la Arusha asilimia 90.5 na mshindi wa tatu ikiwa ni Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwa asilimia 89.7.

Kundi la pili lilikua la Halmashauri za Miji ambapo lilihusisha Halmashauri za miji 22 nchini. Mshindi wa kwanza ni Halmasahuri ya mji wa Njombe asilimia 93.4, Halmashauri ya Mji wa Kahama ikishika nafasi ya pili kwa asilimia 75.0 na Halmashauri ya Mji wa Tunduma ikiwa nafasi ya tatu kwa asilimia 73.5.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa kilele cha wiki ya usafi wa mazingira ulioenda sambamba na mkutano uliojumuisha Maafisa Afya nchini na Wadau mbalimbali wa maendeleo kilichofanyika jijini Dodoma.Waziri Ummy amezitaka Halmashauri za Miji, Majiji, Wilaya, Vitongoji na Vijiji zilizofanya vibaya katika mashindano ya afya na usafi wa mazingira kujitathmini na kuhakikisha zinaweka mikakati madhubuti ya utunzaji wa mazingira.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALLU AMEZINDUA HUDUMA YA UMEME WA BEI NAFUU REA JARIBU MPAKANI MKOANI PWANI

0
0
Na  Linda Shebby,  Pwani
NAIBU Waziri wa Nishati Subira Mgallu  amezindua  huduma ya usambazaji wa umeme wa vijijini  REA katika nyumba 22 za awali   katika  kijiji cha Jaribu Magharibi  kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya  Kibiti Mkoani Pwani ambapo mpango huo umejipanga kuhakikisha  inapeleka huduma  ya umeme huo wa bei rahisi katika vijiji 7,873 vilivyopo nchini kote.

Alisema kuwa, huduma hiyo  ya usambazaji wa umeme Vijijini chini ya REA kwasasa umefikia  hatua ya mzunguko wa pili ambapo mpaka sasa tayari Vijiji 235 tayari  vimepata umeme na huku mzunguko wa tatu utaanza Machi mwakani.

Mgallu alisema kuwa huduma hiyo  ya umeme  wa Vijijini inatolewa kwa gharama ya Sh. 27,000 tu kwa kaya moja  na kwamba Serikali imeweka kiwango hicho ili kuhakikisha kila Mtanzania anayeishi maeneo ya Vijijini ananufaika na huduma hiyo .

“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli imejipanga na imeelekeza nguvu zake  katika kuhakikisha mnafikiwa na huduma ya umeme popote mlipo ndiyo maana imeweka gharama nafuu ili kusudi kila mwananchi anayeishi Kijijini aweze kumudu gharama na kupata huduma  hii ya umeme,”alisema Mgallu.

Alisema kuwa kupatikana  kwa huduma hiyo  ya umeme Vijijini inachochea maendeleo ambapo aliwaomba wananchi wanaofikiwa na huduma hiyo kuitumia kikamilifu katika kufanya shughuli zao za uzalishaji kupitia biashara zitakazoweza kuwaongezea kipato.

Hatahivyo,Mgallu aliziomba kaya ambazo bado hazijalipia ni vyema zikachangamkia fursa hiyo ili waweze kunufaika na huduma hiyo kwa haraka kwakuwa Serikali imekusudia kupeleka umeme huo kwa kila aina ya nyumba  zote iwe ya udongo ama  iliyojengwa kisasa zote ziwe na umeme  bila ya ubaguzi.

“Serikali itapeleka umeme huu kwa kila nyumba iwe ya Tembe,Udongo au Matofali, hatutobagua nyumba ila cha msingi ni kuhakikisha unaweka miundombinu ya waya vizuri(Wiring) na unalipia kiasi cha Sh .27,000 tu za kuunganishiwa kwahiyo nawaomba mtumie fursa hii kikamilifu,”alisema

Kwa upande wake Mhandisi Mkuu wa Shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Pwani Selemani Mgwira,alisema kuwa Mkoa wa Pwani mpaka sasa unajumla ya Vijiji 150 na kwamba jitihada za kusambaza umeme huo bado zinaendelea kama ambavyo Serikali imeweka mipango yake.

Kuhusu Halmashauri ya Kibiti Mgwira alisema kuwa Kibiti inajumla ya Vijiji 19 ambapo kati yake Vijiji vinne tayari vimepata huduma hiyoya  umeme wa bei nafuu( REA) na kwamba  watahakikisha wanapeleka huduma hiyo katika vijiji vingine  na kwamba  watahakikisha kila anayehitaji umeme huo anapata huduma haraka.
 Naibu  Waziri wa Nishati Subira Mgallu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Jaribu Magharibi kilichopo katika Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani kuhusiana na  usambazaji wa umeme wa vijijini REA huku akiwataka wachangamkie  fursa  hiyo ili kila nyumba  iwake taa za umeme na kuachana na  matumizi ya vibatari na mishumaa kwani matumizi hayo yanahatarisha usalama wa mali na  maisha yao.
Naibu Waziri wa Nishati  Subira Mgallu akibonyeza swichi ya umeme kwenye  nguzo akiashiria kuwasha umeme  wa REA  katika kijiji cha Jaribu Mpakani kilichopo katika Halmashauri  ya Kibiti Mkoani Pwani.

Kalogeresi atoa vigezo vya kuwapata wagombea 2020

0
0
Na Ripota Wetu, Morogoro

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kimesema kupatikana kwa wagombea wa udiwani na ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kutatokana na kuthibitika kwa vigezo vya ushiriki wao katika shughuli za maendeleo ya chama hicho.

Pia, kimesema hadhi wanaoyopata ama wabunge ambao baadhi yao huteuliwa na kuwa mawaziri au manaibu waziri huku madiwani wakiwa wenyeviti wa halmashauri na mameya ni kutokana na heshima ya CCM kukubalika kwa wananchi.

Hayo yalielezwa jana Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Karogelesi alipokuwa akifunga mafunzo ya siasa, itikadi na maadili kwa vijana wa chama hicho huko Kilosa mkoani Morogoro.Kalogelesi alisema chama ndicho kinachowapa tiketi wanachama wake kugombea ubunge na udiwani hivyo wanapochaguliwa hawapaswi kujiweka mbali na shughuli za ujenzi wa CCM.

Alisema hakuna mwanafunzi anayeweza kujivunia kufanikiwa kwake kielimu ikiwa hawezi kutambua au kuheshimu mchango mkubwa uliotolewa na walimu wake ama katika masomo ya awali au shule ya msingi."Ili tuwapitishe wagombea wetu kwenye udiwani au ubunge mwaka 2020, tutampima kila mgombea kutokana na ushiriki wake katika kazi za chama bila kumtazama usoni. Sifa ya msingi na ya awali nje ya uanachama wake ni kujihusisha kwa kwake na maendeleo ya CCM," alisema Karogelesi.

Mwenyekiti huyo alisema chama cha siasa kitakachokosa kujijenga, kuimarika na kukubalika hakitapata madiwani na wabunge hivyo hata rais atashindwa kuteua mawaziri na manaibu wake pia kwenye majiji na halmashauri hakutakuwa na wenyeviti au mameya wa CCM.

Aliwataka wabunge wa kuchaguguliwa, madiwani na wale wa viti maalumu kutambua kuwa kufika kwao walipo sasa kumetokana na nguvu ya chama na sio uwezo wao binafsi.Kalogeresi aliwataka wanachama wa CCM na jumuiya zake kutambua kuwa wana wajibu na ulazmia wa kuishi kwa kuheshimu misingi ya chama kikatiba, kinidhamu na kimaadili ili kila kiongozi haiba yake iwe ni kioo kinachoakisi mema kwa chama na jamii. 

Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa alimuagiza Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka, kuwaandikia barua ya ukumbusho wabunge na madiwani wote juu ya ushiriki na wajibu wao ndani ya chama na kwenye jamii.Pia, makatibu wote wa CCM na jumuiya zake mkoani aliwataka kutoa maelekezo na kuwataka wanachama wao kujiweka mbali na vitendo vya udalali wa kisiasa na rushwa.

MKOA WA TABORA WAAINISHA MAENEO NANE YA UWEKEZAJI

0
0

Mkoa wa Tabora umeanisha maeneo ya vipaumbe vya uwekezaji katika kila Halmashauri nane za Mkoa huo ambayo yatajengwa viwanda vikubwa na uanzishaji wa ranchi kwa ajili ya ufugaji wa ng’ombe.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa majumuisho ya kikao cha Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani humo. Alisema kwa upande wa Wilaya ya Urambo wamepewa jukumu la kutenga eneo la ujenzi wa Kiwanda cha Kusindika Tumbaku, Halmashauri ya Kaliua wapewa jukumu la kujenga kiwanda cha mazao ya misitu.

Mwanri alisema Sikonge wenye wanatakiwa kuandaa eneo kwa ajili ya kujenga kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki ikiwemo asali na nta kwa ajili ya kuongeza ubora wake ili yaweze kupata soko kubwa ndani na nje ya Nchi .Alisema Halmashauri ya Mji wa Nzega imepewa jukumu la kuwa na eneo kwa ajili ya machijio ya nyama na Kiwanda cha kuchakata nyama ya ng’ombe na Halmashauri ya Wilaya ya Nzega inapewa jukumu la kuandaa na kuanzisha Rachi kwa ajili ya kunenepesha ng’ombe ili kuwezesha kuwa na nyama nzuri itakayopata soko ndani na nje ya Nchi.

Mwanri alisema Igunga wamepewa jukumu la kuimarisha kilimo kikubwa cha pamba kwa ajili ya viwanda Tabora na Manonga na kuongeza maeneo ya miradi ya umwagiliaji mpunga, ujenzi wa viwanda vya kukoboa mpunga ambavyo vitasaidia kuuweka katika madaraja. Alisema Uyui watahusika zaidi kutenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti na mazao mengine.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa Manispaa ya Tabora wanatakiwa kutenga eneo kwa ajili ya ukanda maalumu wa uwekezaji ambapo vitajengwa viwanda kama vile wa EPZA Ubungo Jijini Dar es salaam. Alisema Mkoa umefikia uamuzi huo ili kutogawanya nguvu na kufanya baadhi ya viwanda kushindwa kufanya kazi vizuri kwa sababu ya uchache wa malighafi kutokana na kuwepo kwa mrudikano wa viwanda vya aina moja katika eneo moja.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa ufafanuzi hivi karibuni wakati wa majumuisho ya kikao cha Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani humo.
 
Viewing all 109584 articles
Browse latest View live




Latest Images