Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV: WAWEKEZAJI WAZIDI KUMIMINIKA NCHINI, SAFARI HII UTURUKI KUJENGA VIWANDA VYA NGUO...


MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA MKOANI MANYARA NA KUREJEA DODOMA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amemaliza ziara yake ya siku 5 mkoani Manyara. Akizungumza kwenye kikao cha majumuisho ambacho kilihudhuriwa na Viongozi na Watendaji wa mkoa huo Makamu wa Rais aliwapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya na kuainisha maeneo kadhaa ambayo yanatakiwa kutupiwa jicho.

Baadhi ya maeneo hayo ni Mazingira ambapo aliuambia Uongozi huo kupanda miti ya kutosha, kulinda maeneo yanayochimbwa madini kuwa kuwasimamia wachimbaji katika kutunza mazingira pamoja na kutunza vyanzo vya maji. Eneo jingine alilozungumzia Makamu wa Rais ni suala zima la Lishe bora kwa watoto na kuhamasisha wananchi kuwa na Bima ya Afya.

Makamu wa Rais ameutaka Uongozi wa mkoa huo kuliangalia suala la mimba za utotoni ambalo kwa kiasi kikubwa linaupa mkoa sura mbaya ambapo mpaka sasa kwa mujibu wa ripoti zaidi ya watoto 4200 wamepata mimba wakiwa na umri mdogo.

“Njia pekee ya kuwalinda watoto wa Kike ni kuwapeleka shule”alisema Makamu wa Rais. Aidha Makamu wa Rais amehimiza umuhimu wa elimu kwa kushirikisha Mabaraza ya Wazee wa Makabila ili kuzuia mila potufu za ukeketaji. “Si rahisi kumuachisha mila yake lakini tukiwaelewesha na kuwaelimisha vizuri taratibu watatuelewa na kuacha kabisa”

Makamu wa Rais ameuambia Uongozi wa mkoa huo wafuate miongozo ya kazi “Kazi za Serikali zina Miongozo, Sheria na Kanuni tulizojiwekea” Mwisho, Makamu wa Rais aliushukuru uongozi huo na kuahidi kurudi tena kwenye Wilaya ambazo hakufika. Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Manyara amemshukuru Makamu wa Rais kwa kufanya ziara mkoani humo ambapo alisema ziara hiyo imekuwa na Mafunzo, Ushauri na Maelekezo ambayo wataenda kutakeleza kama walivyoambiwa.

Akiwa njia kuelekea Dodoma, Makamu wa Rais alisimama barabarani na kuwasalimia wananchi wa Kondoa waliojitokeza ambapo aliwaeleza azma ya Serikali ya kuendelea kutekeleza ahadi zake kwa wananchi na kuwapongeza kwa kupata barabara nzuri inayotoka Dodoma mpaka Babati.
 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Watendaji wa mkoa wa Manyara wakati wa kikao cha Majumuisho ya ziara yake kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa uliopo Babati mkoani Manyara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Sehemu ya Viongozi na Watendaji wa mkoa wa Manyara wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yako mkoani humo. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti mara baada ya kumaliza kikao cha Majumuisho ya ziara yake na Viongozi pamoja na Watendaji wa mkoa huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Flatei Massay mara baada ya kumaliza kikao cha Majumuisho ya ziara yake na Viongozi pamoja na Watendaji wa mkoa huo

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wakazi wa wilaya ya Kondoa wakati akiwa njiani kurudi Dodoma akitokea mkoani Manyara ambapo alikuwa kwenye ziara ya siku tano ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

RAIS Dk. Shein Azungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Kangi Lugola Ikulu Zanzibar

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe. Kangi Alphaxard Lugola, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar Mhe. Dk. Shein, akiwa na Viongozi wa Wizara hiyo Katibu Mkuu Meja Jenerali.Jocob G.Kingu na Naibu Katibu Mkuu Ndg. Kailima Ramadhan, leo Ikulu Zanzibar Novemba 19/11/2018.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Alphaxard Lugola, alipofika Ikulu Zanzibar na Viongozi wa Wizara hiyo kujitambulisha rasmin kwa Rais wa Zanzibar Dk. Shein leo Ikulu Zanzibar.Novemba 19/11/2018.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola, walipofika Ikulu Zanzibar kuona na Rais wa Zanzibar Dk. Shein, kwa kujitamulisha na kufanya mazungunzo leo Ikulu Zanzibar, novemba 19/11/2018. 
/RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Kangi Lugola, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo 19/11/2018.(Picha na Ikulu )  

MICHUZI TV: MRITHI WA PROFESA MAJI MAREFU AANZA KUUNGURUMA KOROGWE VIJIJINI

MICHUZI TV: SERIKALI YAWATUA MZIGO WANANCHI /MIUNDO MBINU YA AFYA MBEYA

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA NA BALOZI WA NAMIBIA NCHINI

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi akisalimiana na Balozi wa Namibia nchini, Mhe. Theresa Samaria alipofika Wizarani kwa ajili ya kumsalimia na  kuzungumzia kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia kwenye sekta mbalimbali ikiwemo biashara, kilimo, uvuvi na mifugo. Mazungumzo hayo yamefanyika tarehe 19 Novemba, 2018.
Mhe. Balozi Samaria akimweleza Dkt. Kasidi kuhusu fursa mbalimbali za biashara ambazo Tanzania inaweza kuzichangamkia kwenye nchi yake ambayo ina ukame uliokithiri kutokana na kuzungukwa na Majangwa ya Kalahari na Namib. Fursa hizo ni pamoja na biashara ya nyama, matunda, nafaka mbalimbali na korosho.
Katibu Mkuu, Dkt. Kasidi akisoma nyaraka aliyopatiwa na Balozi Samaria ambayo ni mkataba ulioanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia miaka 20 iliyopita. 

Dkt. Kasidi akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi Samaria mara baada ya kumaliza mazungumzo yao

Piacha ya pamoja kati ya Dkt. Kasidi na Balozi Samaria pamoja na  Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa Namibia nchini walioshiriki mazungumzo kati ya viongozi hao 


NDTYK: Diamond platnumz in Toronto, Canada, full Show

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU NOVEMBA 19, 2018


SERIKALI YAJENGA SEKONDARI YA MFANO KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI ARUSHA

$
0
0
Serikali inajenga Shule ya Sekondari Maalum ya mfano kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Chuo cha Ualimu Patandi kilichopo mkoani Arusha yenye uwezo wa kudahili wanafunzi 600 kwa mara moja ikiwa ni mkakati wake wa kuongeza fursa za udahili kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako katika ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kwa Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo amesema Serikali imekarabati miundombinu kwenye shule kongwe ya Moshi Ufundi inayopokea wanafunzi wenye mahitaji maalum.

“Serikali inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali inayolenga kuongeza upatikanaji wa fursa na kuimarisha ubora wa elimu inayotolewa katika ngazi zote kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo tayari serikali imekarabati miundombinu ya shule kongwe ya Moshi Ufundi ambayo inapokea wanafunzi wenye mahitaji maalumu”. Alisisitiza Prof. Ndalichako.

Waziri Ndalichako amesema watu wenye mahitaji maalum wana fursa sawa ya kushiriki katika michezo na kufanya hivyo kunasaidia kuondoa kasoro za kimwili na kiakili na baadhi ya ulemavu unaweza kurekebishwa kwa kushiriki katika michezo na burudani.
picha 1
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wadau wa Elimu pamoja na wanafunzi wenye mahitaji maalum ( Hawapo Pichani) katika ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.
P2
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimpongeza mwanafunzi mwenye mahitaji maalum baada ya kufanya vizuri katika maonyesho ya mavazi katika ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kwa Mkoa wa Kilimanjaro
P3
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi cheti za kutambua mchango wa CCBRT wa udhamini wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports lililoshirikisha wanafunzi wenye mahitaji maalum, ambapo alitoa wito kwa wadau wa Elimu kuendelea kushiriki katika kuboresha Elimu Maalum
P4
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akibadilishana mawazo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Walemavu) katika ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kwa Mkoa wa Kilimanjaro
P5-min
Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwa katika maandamano wakipita mbele ya Mgeni Rasmi Prof. Joyce Ndalichako (Hayupo Pichani) wakati wa ufunguzi wa Bonanza la Kilimanjaro Committee for Sports iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kwa Mkoa wa Kilimanjaro iliyoshirikisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Kilimanjaro zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA NA MWAKILISHI WA HESHIMA WA TANZANIA, PERTH PAMOJA NA BALOZI WA KENYA NCHINI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Konseli wa Heshima wa Tanzania kwenye Jimbo la Perth nchini Australia, Bw. Didier Murcia alipofika kwenye Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 19 Novemba, 2018 kwa lengo la kujitambulisha kwa Mhe. Naibu Waziri pamoja na kumweleza utekelezaji wa majukumu yake katika kuiwakilisha Tanzania, Perth. 
Bw. Murcia akimweleza jambo Mhe. Dkt. Ndumbaro wakati wa mazungumzo yao 
Mazungumzo yakiendelea. Kulia ni Katibu wa Mhe. Naibu Waziri, Bw. Charles Faini.
Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro alikutana kwa mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini, Mhe. Dan Kazungu. Mazungumzo hayo yalifanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 19 Novemba 2018. Pamoja na mambo mengine walizungumzia namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pia Balozi Kazungu alitumia fursa hiyo kumweleza Mhe. Naibu Waziri kuhusu Mkutano wa Kimataifa kuhusu Rasilimali Endelevu za Majini utakalofanyika nchini Kenya kuanzia tarehe 26 hadi 28 Novemba 2018 .

MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 20.2018

MAHAFALI YA PILI YA CHUO CHA MANJANO BEAUTY ACADEMY YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Wahitimu wa Chuo cha Urembo cha Manjano wametunikiwa vyeti katika nyanja ya urembo na vipodozi (Cosmetology). Baadhi ya wahitimu waliofika kwenye mahafali hayo walivikwa taji kama ishara ya mafanikio ya kitaaluma, na kuweka alama kwenye hatua muhimu katika maendeleo yao ya kitaaluma kwenye tasnia ya urembo na vipodozi. Zaidi ya wanafunzi 87 wamehitimu kwa mwaka huu wa 2018 na wataendelea na mafunzo ya utarajali (internship program) kwa kipindi cha miezi 12 katika masalon, kampuni na taasisi mbalimbali zenye kujihusisha na urembo na vipodozi ili kuweza kujijengea ujuzi (skills) na uzoefu (experience) katika kazi zao. Sherehe ilizinduliwa na Mkufunzi kutoka VETA, Mwl. Salehe Omari, akimwakilisha Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam, mama Florence Kapinga. 
Mkuu wa Chuo cha Urembo mama Shekha Nasser akizungumza machache wakati wa mahafali ya pili ya Chuo cha Manjano Beauty Academy. Amewataka wanawake kujiongezea elimu ya matumizi sahihi ya Vipodozi na Urembo ili kuweza kutoa huduma sahihi na yenye ueledi kwa wananchi. Mama Shekha alisema Tanzania kuna upungufu mkubwa wa Wataalamu, hasa walimu wenye sifa za kufundisha elimu ya Urembo na Vipodozi, hivyo aliwashauri wanawake wengi kujiunga na Chuo cha Manjano Beauty Academy ili waendeleze tasnia hii na kuboresha huduma zao kwa wateja. Aidha alitaja changamoto kubwa alizokabiliana nazo wakati anaanzishi Chuo hicho ikiwemo ukosefu wa wataalamu wazawa wa maswala ya Urembo na Vipodozi. Akieleza zaidi alisema sekta ya urembo ina fursa kubwa kwa ajira na inaweza kusaidia kujiongezea kipato na kuondokana na ukosefu wa ajira na umasikini.Mgeni rasmi, uongozi wa Chuo cha Manjano Bauty Academy na Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja.
Mgeni rasmi, Mwl. Salehe Omari, naye pia aliwashukuru wanawake wa Kitanzania waliojiunga kwenye chuo hicho kwa lengo la kupata ujuzi wa maswala ya urembo na vipodozi. Alisema Urembo, Vipodozi na mitindo ni moja kati ya sekta zinazoajiri mamilioni ya wanawake kwa sasa, na kuchangia kwa kiasi kwenye pato la Taifa. Akiendelea zaidi alisema, elimu na mafunzo kwa vitendo (Vocational training) ni elimu na mafunzo ambayo yanayotoa ujuzi na elimu muhimu kwa ajili ya ajira. Elimu ya aina hii ni ambayo humuandaa mtu kufanya kazi katika fani mbalimbali, kama biashara, utengenezaji wa vitu, au kama fundi. 

Hivyo aliwausia wahitimu kuitumia vizuri elimu na ujuzi walioupata kwenye Chuo cha Manjano. Alielezea pia kwa kusema elimu ya ufundi na ujuzi ni muhimu katika kuleta usawa kwenye jamii kwani ni moja ya kitovu cha kuleta maendeleo na kuendana na kasi ya Awamu ya Tano ya Uchumi wa Viwanda. Elimu ya ufundi, stadi za kazi au wa kazi za mikono ni mojawapo ya vipaumbele vya UNESCO. Kwani elimu hii inasaidia kuendeleza elimu ya ubora na usawa na fursa za kujifunza kwa wakati wote ule haijalishi umri wako, “wewe ni mwanafunzi wa kudumu alisema.”
Tunawatakia wasomi wetu wote kila la kheri katika kazi zao. Mkuu wa Chuo cha Urembo Mama Shekha Nasser akizungumza.
Shekha ni mmiliki wa kampuni ya Shear Illusions na mnamo mwaka 2015, kupitia bidhaa za LuvTouch Manjano alianzisha chuo cha Manjano Beauty Academy kwa lengo la kutoa elimu na ujuzi wa kuwawezesha wasichana na wanawake kujiajiri na kujiongezea kipato kupitia tasnia ya Urembo na Vipodozi.

WAZIRI MKUU AZINDUA MSIKITI NA KUSISITIZA UTUMIKE VIZURI

$
0
0

*Awataka waumini wautumie kwa kufanya ibada na kuhamasisha amani

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua msikiti wa Nandagala na amewataka waumini wa dini ya Kiislamu katika Kata ya Nandagala wilayani Ruangwa wautumie vizuri msikiti huo kwa kufanya ibada na kuhamasisha amani na si vinginevyo.

“Msikiti huu ninauzindua leo (jana) naomba tuutunze vizuri na tuutumie kwa kufanya ibada na si ibada za kiuanaharakati. Watakaokuja msikitini na kufanya mambo ya hovyo Mwenyezi Mungu atawalaani.”Waziri Mkuu alizindua msikiti huo jana jioni (Jumatatu, Novemba 19, 2018), ambapo alitumia fursa hiyo kuwasisitiza waumini wa dini ya Kiislamu kuhakikisha muda wa kufanya swala unapofika waende msikitini hapo kufanya ibada.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwataka waumini hao waanzishe madrasa na kuwafundisha watoto quran lengo likiwa ni kuwafundisha misingi ya dini na kuwaandaa vizuri na kuwawezesha kukua kiimani ili waje kuwa waja wema.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alimshukuru Mzee Suleiman na familia yake kwa uamuzi wao wa kujitolea kujenga msikiti huo ambao utawawezesha waumini katika kijiji cha Nandagala kufanya ibada zao. “Namshukuru na Mzee Mamboleo na mkewe kwa kutoa eneo lao bure ili litumike kujengea msikiti.”

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Msikiti wa Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika dua iliyoongozwa na Sheikh Hilal Shaweji, maarufu Sheikh Kipozeo (watatu kulia) wakati alipozindua Msikiti wa Nandagala wilayani Ruangwa Novemba 19, 2018. Wapili kulia ni Mfadhili ambaye kwa pamoja na familia yake alijenga Msikiti huo, Mzee Suleyum Mohammed Ahmed. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuzindua Msikiti wa Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Taarifa za Utafiti wa Madini Zitolewe kwa Wananchi- Biteko

$
0
0

Na Greyson Mwase, Singida

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameuagiza Mgodi wa Dhahabu wa Shanta uliopo katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida kuhakikisha unatoa taarifa za tafiti zake zilizofanyika katika maeneo mbalimbali ili wachimbaji wadogo waweze kuzitumia katika kubaini madini yaliyopo na kuanza kuchimba kwa kufuata sheria na kanuni za madini.

Naibu Waziri Biteko alitoa agizo hilo leo tarehe 19 Novemba 2018 kwenye mkutano wa hadhara na wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika tarafa ya Mang’onyi wilayani Ikungi mkoani Singida kama sehemu ya ziara yake katika mkoa huo yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wachimbaji wa madini

Aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imeweka mazingira bora ya uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na kuwapatia taarifa mbalimbali za utafiti zilizofanywa na Wakala wa Utafiti na Jiolojia Tanzania (GST) na kampuni za utafiti wa madini lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa uchimbaji wao unakuwa wa uhakika na sio wa kubahatisha.

Akielezea maboresho mengine yaliyofanywa katika sekta ya madini, Biteko alisema Serikali imeboresha Sheria ya Madini inayotambua madini kama mali ya watanzania yanayosimamiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.Aliendelea kusema kuwa, Serikali imeweka mkakati wa kurasimisha wachimbaji wadogo wa madini wasio rasmi na kuwapatia leseni za madini ili uchimbaji wao ulete tija kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Meneja Mkuu wa kampuni inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya jasi ya General Business and Equipment Supply Limited iliyopo katika eneo la Bumbua wilayani Itigi mkoani Singida, Yusuph Kibira (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) mara alipofanya ziara katika eneo la mgodi huo.
Sehemu ya wachimbaji wadogo wa madini wakiwasilisha kero mbalimbali mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika tarafa ya Mang’onyi iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida.
Kutoka kulia, Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu walisikiliza kero mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wachimbaji wadogo kutoka katika tarafa ya Mang’onyi iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida kwenye mkutano wa hadhara. (hawapo pichani).
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu akifafanua jambo kwenye mkutano wa hadhara wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika tarafa ya Mang’onyi iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akielezea mikakati ya Wizara ya Madini katika kuboresha shughuli za uchimbaji mdogo wa madini kwenye mkutano wa hadhara wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika tarafa ya Mang’onyi iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida.

PONGEZI ZA WAKULIMA WA KOROSHO WA KIJIJI CHA MTONYA B, WILAYANI TUNDURU KWA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI


MICHUZI TV: RC MTWARA AZUNGUMZIA MAFANIKIO YA MTWARA KATIKA MIAKA MITATU YA MAGUFULI

MICHUZI TV: WASANII WATAKAO SHIRIKI WASAFI FESTIVAL WAANZA KUINGIA MTWARA

TIMES FM: LADY JAYDEE - WANAFANYA CHOCHOTE WAZUNGUMZIWE / SIWEZI KUFUNGIWA NA BASATA

WAZIRI MKUU MAJALIWA MGENI RASMI JUKWAA LA BIASHARA NA UWEKEZAJI MKOANI TABORA

$
0
0
Na Tiganya Vincent

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji na Maonesho ya wajasiliamali mkoani Tabora.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa sala na dua maalumu ya kuliombea Jukwaa hilo iliyofanyika katika sanamu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Alisema Jukwaa hilo linatarajiwa kufunguliwa tarehe 21 Novemba mwaka huu na Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa na kufuatiliwa na uwaslishaji wa mada mbalimbali.

Mwanri alisema wakati wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kutakuwepo na mada mbalimbali za kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizipo katika Halmashauri nane ya Mkoa wa Tabora zitawasilishwa na wadau mbalimbali.

Alisema kila Halmashauri mkoani humo imechagua maeneo muhimu ya uwekezaji ambayo itatumia fursa kuwatangazia wadau kwa ajili ya kuwavutia watu au Kampuni ambazo zinataka kuwekeza.

Mwanri aliwakaribisha wananchi wa mkoa huo na Watanzania wote kwa ujumla kuja kushiriki maonesho na Jukwaa hilo chini ya kauli mbiu ya wekeza Tabora kwa Mapinduzi ya Uchumi wa Kati.

Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa Jukwaa hilo pia litahudhuriwa na viongozi mbalimbali na Mawaziri.
Jukwaa la Biashara na Uwekezaji limeandaliwa na Ofisi ya Mkoa wa Tabora na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa lengo la kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana mkoani humo.

Introducing "Boyfriend wa Dar es Salaam" by Lady Jaydee

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live


Latest Images