Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live

BENKI KUU YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA UKAGUZI, UDHIBITI WA BIASHARA HARAMU YA FEDHA ZA KIGENI NA UKIUKAJI WA SHERIA KATIKA KUENDESHA BIASHARA YA UBADILISHAJI FEDHA

$
0
0

*Wenye maduka ya kubadilisha fedha waliokiuka sheria kukiona,leseni zao zatakiwa BoT
*Pia kuzuia kuendelea kwa ukiukaji wa sheria na kudhibiti uendeshaji wa biashara ya ubadilishaji fedha

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imesema imefanya oparesheni ya kushtukiza ya kukagua maduka ya ubadilishaji fedha na baadhi ya maduka bubu ambayo hayana leseni lakini yalikuwa yakiendesha biashara hiyo kinyume na sheria.

Operesheni hiyo iliratibiwa na Kitengo cha Ukaguzi cha Benki Kuu katika kutekeleza majukumu yake kisheria na kwamba hiyo ni oparesheni ya tatu kufanyika. 

Akizungumza leo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania amesema uchunguzi wa kina katika miezi sita iliyopita ulibaini kuongezeka kwa biashara za kubadilisha fedha kinyume cha sheria, na kukua kwa biashara haramu ya fedha za kigeni na utakatishaji fedha, hususan kupitia maduka ya kubadilisha fedha.

Amesema BoT kupitia juhudi za Kitengo cha Ukaguzi kuwapata wahusika hazikuzaa matunda katika oparesheni mbili zilizopita. Hiyo ni kwa sababu iligundulika kuwa kuna mtandao mpana na madhubuti wa shughuli hizo na ambao ulilenga kuhakikisha kuwa shughuli za udhibiti hazifanikiwi. Baada ya mashauriano na wataalam na kushirikisha vyombo vya upelelezi na usimamizi ilionekana kuwa ili kufanikisha operesheni hiyo lililokusudiwa ni muhimu wahusika wote wadhibitiwe kwa wakati mmoja na kufanyiwa ukaguzi.

" Hii ilihitaji ushiriki wa maofisa wengi sana kutoka vyombo mbalimbali na kuhakikisha kila mahali ambapo ukaguzi uliendeshwa kuna usalama wa kutosha na Wananchi wanaarifiwa kutoingia sehemu husika kwa wakati huo. Baadhi ya washiriki katika zoezi hilo ni askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania wakiwa katika sare zao bila silaha.

"Hii ni kwa sababu siku oparesheni ilipofanyika askari wengi wa Jeshi la Polisi wapo kwenye kusimamia usalama katika vituo vya mitihani ya kidato cha pili inayoendelea," imeeleza taarifa hiyo ya BoT.Napenda kuwaarifu wananchi kuwa oparesheni hii imeisha salama na bila kuathiri mtu yeyote na tunawashukuru wananchi wa Jiji la Arusha kwa ushirikiano, hasa kwa kuwa watulivu,"amesema.

Amefafanua taratibu zinazoendelea ni za kisheria na kwamba mahojiano na wahusika yanakamilishwa na wale watakaokutwa na tuhuma za ukiukaji sheria watashughulikiwa kufuatana na taratibu za kisheria. Aidha amesema Benki Kuu inachukua hatua zifuatazo kuzuia kuendelea kwa ukiukaji wa sheria na kudhibiti uendeshaji wa biashara ya ubadilishaji fedha. Kwa takribani miezi mitatu sasa benki hiyo imesitisha utoaji wa leseni za biashara ya ubadilishaji fedha. 


KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU

$
0
0

NA LUSUNGU HELELA .

Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewatoa hofu watumishi wa Taasisi zenye jukumu la kulinda na kuhifadhi Wanyamapori na Misitu nchini kuwa hakuna maslahi yao yatakayobadilika baada ya ujio wa Jeshi Usu
 
Naibu Waziri Kanyasu ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana na watumishi hao tangu alipoteuliwa kushika wadhifa wa Naibu Waziri katika Wizara hiyo nyeti kwa uchumi wa nchi. Amesema ziara yake imelenga kuzifahamu Taasisi anazoziongoza ili kujua namna zinavyotenda kazi na changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi. 

Akizungumza kuhusu utendaji wa Jeshi USU, Naibu Waziri Kanyasu amesema kufuatia mabadiliko ya mfumo wa utendaji kutoka katika mfumo wa kiraia na kuwa Jeshi USU kutakuwa na mabadiliko kiutendaji yatakayoendana na taratibu za Jeshi USU lakini utakaoheshimu na kulinda maslahi ya watumishi. 

Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa, uanzishwaji wa Jeshi hilo haukusudii kubadili maslahi ya watumishi hao na endapo maslahi hayo yatabadilika basi yatakuwa na mabadiliko chanya kwao. Naibu Waziri Kanyasu ameongeza kuwa Jeshi USU litaongeza nidhamu uwajibikaji na maadili kwa watumishi wa sekta ya Maliasili na Utalii ili waweze kusimamia ipasavyo uhifadhi endelevu wa maliasili na si vinginevyo. 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (wa pili kushoto) akimsikiliza Mhifadhi ,kuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya enoe la n Ngorongoro, Dkt.Freddy Manongi wakati alipowatembelea jana katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi wa Mamlaka hiyo juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ( kushoto) akipewa maelezo na Dkt. Maurus Msuha (katikati) wakiwa kwenye sehemu ya kuonea wanyamapori (View point) ya Ngorongoro Kreta wakati alipotembelea jana kwa ajili ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ( wa kwanza kushoto) akiwa ameongozana na Menejimenti ya Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro akipewa maelezo wakati alipotembelea jana kabla ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi wa Mamlaka hiyo juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi 
Watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wakati alipowatembelea jana. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa na baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro wakiamungalia Faru mwenye umri wa miaka 65 ambaye ni faru mzee duniani .


Bunge la China lasifu Juhudi za Serikali za Ujenzi wa Miradi

$
0
0


Na Grace Semfuko-MAELEZO.

Bunge la Jamhuri ya Watu wa China limepongeza kasi ya ujenzi wa Miradi inayofanywa na Serikali  ya Tanzania na kwamba ushirikiano uliopo baina ya China na Tanzania utaendelea kuimarishwa ili kuzifanya nchi hizo kuzidi kuwa na maendeleo ya kuichumi

Hayo yamebainishwa na Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang alipotembelea Darala la Nyerere Kigamboni Jijini Dar Es Salaam lililojengwa na Kampuni ya China Railway Jiangchang Engineering CRJE na China Major Bridge Engineering Company  ujenzi ulioanza mwaka 2012 na kukamilika April 2016.

Daraja hilo linalovuka mkondo wa maji wa Kurasini hadi Kigamboni  Jijini Dar Es Salaam lina urefu wa mita 680 na njia sita za kupitishia magari ni daraja kubwa katika nchi za Afrika Mashariki na lilizinduliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli April 19 mwaka 2016 na kupewa jina la Julius Nyerere kwa heshima ya Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Ujenzi wa Daraja la Nyerere ulibuniwa na Serikali lengo likiwa ni kupunguza msongamano wa magari uliokuwepo katika kivuko cha Magogoni Jijini Dar Es Salaam na kurahisisha usafiri lengo ni kuwaondolea watanzania changamoto kwenye sekta ya usafirishaji.Akizungumza katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti huyo wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Cai Defang amesema ni muda muafaka sasa kwa daraja hilo kutumika kama njia za kiuchumi kwa watu wa Tanzania.
 
 Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Mhe. CAI Dafenga akipunga mkono wakati alipotambulishwa  Bungeni mapema leo Jijini Dodoma. Wa pili toka kulia ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Balozi wa China nchini Bi. WANG wa kwanza kulia. Makamu huyo wa Rais ametembelea Bunge la Tanzania akiambatana na Wabunge kumi na tano kwa lengo la kudumisha ushirikiano baina ya pande zote mbili.

WAZIRI MKUU MAJALIWA MGENI RASMI JUKWAA LA BIASHARA NA UWEKEZAJI MKOANI TABORA

$
0
0
Na Tiganya Vincent

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji na Maonesho ya wajasiliamali mkoani Tabora.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa sala na dua maalumu ya kuliombea Jukwaa hilo iliyofanyika katika sanamu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Alisema Jukwaa hilo linatarajiwa kufunguliwa tarehe 21 Novemba mwaka huu na Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa na kufuatiliwa na uwaslishaji wa mada mbalimbali.

Mwanri alisema wakati wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kutakuwepo na mada mbalimbali za kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizipo katika Halmashauri nane ya Mkoa wa Tabora zitawasilishwa na wadau mbalimbali.

Alisema kila Halmashauri mkoani humo imechagua maeneo muhimu ya uwekezaji ambayo itatumia fursa kuwatangazia wadau kwa ajili ya kuwavutia watu au Kampuni ambazo zinataka kuwekeza.

Mwanri aliwakaribisha wananchi wa mkoa huo na Watanzania wote kwa ujumla kuja kushiriki maonesho na Jukwaa hilo chini ya kauli mbiu ya wekeza Tabora kwa Mapinduzi ya Uchumi wa Kati.

Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa Jukwaa hilo pia litahudhuriwa na viongozi mbalimbali na Mawaziri.

Jukwaa la Biashara na Uwekezaji limeandaliwa na Ofisi ya Mkoa wa Tabora na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa lengo la kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana mkoani humo.

RAIS DK.SHEIN AJUMUIKA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLA KATIKA SHEREHE ZA MAULIDI YA KUZALIWA MTUME (S.A.W) VIWANJA VYA MAISARA SULEIMAN ZANZIBAR

$
0
0




RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi, alipowasili katika viwanja vya Maisara Suleiman, katika hafla ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W ), Maisara Zanzibar.jana usiku 19-11-2018.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa jukwaa kuu wakiwa wamesimama wakati ikisomwa Qaswida ya Kumtakia Rehema Mtume (S.AW) kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya Maulid yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Zanzibar jana usiku.19-11-2018.

NAIBU Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Hassan Othman Ngwali, akizungumza na kutowa maelezo ya hafla hiyo ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Zanzibar jana usiku,19-11-2018.

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa na Wake wa Viongozi na Wananchi akihudhuria Maulid Matukufu ya kuazaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Zanzibar jana usiku.19-11-2018.

WAUMINI wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakihudhuria hafla ya Maulid Matukufu ya Kuzaliwa Mtume Muhammad(S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya mpira vya Maisara Suleiman Zanzibar usiku tarehe 19-11-2018.

MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi akiongoza dua ya ufunguzi wa Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika viwanja vya mpira Maisara Suleiman Zanzibar, kulia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Alhajj Ali Mohamed Shein na kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.

/WANAFUNZI wa Madrassa Nouru’l Iman kutoka Karakana Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, wakisoma Qaswida wakati wa hafla ya Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika Kitaifakatika viwanja vya Maisara Suleiman Zanzibar jana usiku 19-11-2018

NDITIYE AITAKA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA KUSITISHA MPANGO WAKE WA KURASIMISHA BANDARI BUBU ZA DAR ES SALAAM

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kusitisha mpango wake wa kurasimisha bandari bubu zilizopo mkoa wa Dar es Salaam

Hayo yameelezwa na Nditiye wakati wa ziara yake Wilayani Bagamoyo ya kukagua bandari bubu zilizopo ambapo amebaini uwepo wa bandari bubu zaidi ya kumi na tisa zinazosafirisha bidhaa kwenye eneo la mwambao wa bahari lililopo wilayani Bagamoyo. 

Amesema kuwa uwepo wa bandari bubu hizo ni kipenyo cha baadhi ya wafanyabiashara kukwepa kulipa kodi kwa kutumia bandari rasmi na hivyo kupunguza mapato ya Serikali na kuihujumu nchi kwa kufifisha jitihada za Serikali za kufikia uchumi wa kati na azma yake ya ujenzi wa viwanda, utoaji wa huduma za afya, elimu, maji, umeme na ujenzi wa miudombinu ya sehemu mbali mbali nchini

Nditiye ameielekeza TPA iache mara moja mpango huo wa kurasimisha bandari bubu zilizopo Mbweni na Temeke kwa kuwa Dar es Salaam ipo bandari na itumike hiyo kwa shughuli za usafirishaji wa bidhaa na abiria. “TPA wafute mara moja mpango wao wa kurasimisha bandari bubu za Mbweni, Temeke kuwa bandari rasmi wakati kuna bandari ya Dar es Salaam,” amesema Nditiye. Pia, ameongeza kuwa fedha zilizotengwa na TPA kwa ajili ya mpango huo lipewe jeshi la bandari ili waweze kununua vifaa kwa ajili ya kufanya doria ya kuimarisha ulinzi kwenye mwambao wa bandari

Amefafanua kuwa yapo majahazi yanayofanya shughuli za usafirishaji ufukweni mwa bahari ya Hindi kwenye mwambao upatao kilomita 300 kwenye eneo la Bagamoyo ambapo majahazi yanashusha mizigo kinyemela. “Nimeshuhudia taratibu za nchi zikikiukwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Bagamoyo inapata changamoto ila inawadhibiti kwa namna moja au nyingine japo yapo majahazi yanayoshusha bidhaa na kuficha kwenye misitu iliyopo ndani ya bahari,” amesema Nditiye.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) akipata maelezo kuhusu bandari bubu kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa (mwenye koti nyekundu) wakati wa ziara yake ya kukagua bandari bubu hizo wilayani humo. Anayesikiliza ni Msimamizi wa Bandari ya Bagamoyo, Witharo J. Witharo 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Bandari ya Bagamoyo, Witharo J. Witharo (wa kwanza kulia) kuhusu kudhibiti bandari bubu zilizopo wilayani Bagamoyo wakati wa ziara yake kwenye bandari hizo 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa maelekezo kwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Bagamoyo kuhusu kudhibiti bandari bubu zilizopo wilayani humo wakati wa ziara yake ya kukagua bandari hizo 

WAKALA WA MAJENGO TANZANIA YATAKIWA KUMALIZA KWA WAKATI UJENZI KITUO CHA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA

$
0
0

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imetakiwa kukamilisha kwa wakati mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa cha Kanda ya Ziwa uliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Wito huo, umetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko wakati wa ziara ya kikazi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

Bi. Mwaluko ameitaka Wakala hiyo kuhakikisha inakamilisha ujenzi kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kukusanya, kuchambua, kutunza na kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali kutoka katika Taasisi za Umma zilizopo kanda ya Ziwa kwa lengo la kulinda urithi andishi na historia ya Taifa letu.

Bi. Mwaluko ameielekeza Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kuzungumza na Wakala wa Majengo Tanzania na kukubaliana tarehe rasmi ambayo jengo litakuwa limekamilika ili taarifa hiyo itolewe kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyopanga kutembelea kituo hicho hivi karibuni kwa lengo la kujiridhisha na ujenzi uliofanyika.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akitazama ramani ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza wakati wa ziara ya kikazi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho. 
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akitoa maelekezo ya kuboresha ujenzi wa Kituo cha kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakati wa ziara ya kikazi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho. 
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza na Wataalam wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Kanda ya Ziwa wakati wa ziara ya kikazi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho. 

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MASHINDANO YA SHIMMUTA JIJINI DODOMA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa Mashirika na Taasisi kutenga fedha kwa ajili ya michezo.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi wa Mashindano ya SHIMMUTA uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. “Kwa Wakuu wa Taasisi, kwa kuwa kalenda za michezo hii inajulikana ni vyema mkahakikisha bajeti zinapangwa mapema” alisema Makamu wa Rais.

Akiwa Mlezi wa SHIMMUTA Makamu wa Rais amesema angependelea kuiona SHIMMUTA ya 2019 ikiwa sawa na ya miaka ya 60 ambapo timu zaidi ya 60 zilishiriki. Makamu wa Rais ametoa rai kwa Taasisi, Mashirika na Makampuni kuwajibika kikamilifu kuhakikisha mashindano haya yanakuwa endelevu ikiwa pamoja na kupata mbinu mbadala za kupata washirika zaidi wa kugharamia michezo hii.

Kaulimbiu ya mwaka huu inasema ‘ufanisi katika utendaji kazi hutegemea afya bora ya wafanyakazi, tuhumize michezo sehemu za kazi’ Timu 21 zinashiriki SHIMMUTA ya mwaka huu na michezo yote itachezwa kwenye viwanja vya michezo vya chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Kwa upande mwingine Naibu Waziri wa Michezo, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Julliana Shonza amesema Wizara yake inatambua uwepo wa mashindano hayo na kutoa pongezi kwa kamati iliyoanda michezo hiyo mwaka huu. Wakati huo huo Mwenyekiti wa SHIMMUTA Dkt. Hamis Mkanachi amesema michezo hiyo ilianzishwa mwaka 1967 ikiwa na lengo la kuhimiza michezo sehemu za kazi na kuwaweka Watendaji, Taasisi na Mashirika na kudumisha mahusiano na kutangaza shughuli za Taasisi zao.

Katika ufunguzi wa leo timu ya mpira wa miguu TPDC na Geita Goldmine walifungua dimba wakati kwa upande wa mpira wa pete (netball) timu ya Chuo Kikuu Dodoma na Geita Goldmine zilifungua dimba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipungia mkono maandamano ya washiriki wa mashindano ya SHIMMUTA wakati yakiingia katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. 
Timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa sherehe za uzinduzi wa mashindano ya SHIMMUTA jijini Dodoma. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa mashindano ya michezo ya SHIMMUTA jijini Dodoma. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasalimia wachezaji wa timu ya mpira wa pete (Netball) ya Geita Gold Mine wakati wa uzinduzi wa mashindano ya SHIMMUTA kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasalimia wachezaji wa timu ya mpira wa pete (Netball) ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakati wa uzinduzi wa mashindano ya SHIMMUTA kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

BREAKING NEWZZZZZ....RAIS DKT. MAGUFULI AAHIRISHA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA UHURU

$
0
0

*Aagiza fedha zilizotengwa zikatumike 
katika kujengea hospitali Dodoma
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha maadhimisho ya siku ya Uhuru, Disemba 9, 2018 na fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha shamrashamra hizo ameelekeza zitumike kujenga hospitali mkoani Dodoma ambayo itaitwa Uhuru Hospitali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Novemba 20, 2018 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais Dkt. Magufuli ameagiza kiasi cha shilingi milioni 995.182 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha sherehe hizo zitumike kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mkoani Dodoma. 
Waziri Mkuu ametoa taarifa hiyo wakati alipokutana na viongozi waandamizi wa mkoa wa Lindi pamoja na wilaya zake katika kikao cha maandalizi ya shughuli za kuzima Mwenge kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano kwenye ofisi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Amesema hospitali hiyo itakayojengwa katika eneo la kati ya barabara ya kwenda Hombolo na Chamwino  kwenye barabara ya kwenda Dar es Salaam itakuwa inawahudumia wakazi wa mkoa wa Dodoma pamoja na wananchi wengine watakaokuwa  mkoani humo.
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya waandae matukio watakayoyatekeleza katika maeneo yao yatakayoashiria maadhimisho ya siku ya Uhuru. “Wanaweza kutumia siku hiyo kwa kufanya usafi maeneo ya wazi au kwenye hospitali.” 
Kufuatia maagizo hayo, Waziri Mkuu amewataka wananchi katika maeneo yote nchini wajiandae kufanya shughuli mbalimbali za kijamii zitakazopangwa na wakuu wao wa mikoa na wilaya kufanyika katika maeneo yao.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, NOVEMBA 20, 2018.

Madaktari Bingwa MNH Waendelea kutoa Tiba Ligula

$
0
0
Wataalam wa afya wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na wataalam wa afya wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mtwara, Ligula wanaendelea kutoa huduma mbalimbali za afya kwa wananchi wa mkoa huo ikiwemo huduma za kibingwa ambazo awali hazikuwahi kufanyika hospitalini hapo.

Moja ya huduma za kibingwa zilizofanyika leo ni kuchukua sampuli ya uvimbe uliokua ndani ya ini kwa kutumia sindano wakiongozwa na mashine ya Utra sound. ‘’Mgonjwa huyu tumemfanyia kipimo cha sindano (FNAC) kwa kuongozwa na mashine ya Utra sound lengo ni kufanya uchunguzi zaidi ili mgonjwa aweze kupata tiba sahihi’’. Amesema Dkt. Mosha.

Maeneo mengine ambayo watalam wametoa huduma ni pamoja na magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya kike na uzazi, meno, macho, watoto, magonjwa ya koo, pua na masikio, maabara pamoja na magonjwa ya ndani.

Utoaji wa huduma hizo unaenda sambamba na kuwajengea uwezo watalaam wa Hospitali ya Ligula ili kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. 

Daktari Bingwa wa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ya binadamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Innocent Mosha (kushoto) kwa kushirikiana na mtaalam wa Radiolojia Dkt. Maria Mtolera wakichukua sampuli ya uvimbe uliokua ndani ya ini kwa kutumia sindano wakiongozwa na mashine ya Utra sound. 
Daktari Bingwa kutoka Muhimbili Judith Mwende akifanya upasuaji wa mtoto wa jicho leo katika Hospitali ya Ligula. 
Wataalam wa afya wa MNH kwa kushirikiana na watalaam wa afya wa Hospitali ya Ligula wakimfanyia upasuaji mgonjwa mwenye matatizo ya magonjwa ya kike na uzazi. 
Daktari Bingwa wa upasuaji wa pua, koo na masikio kutoka Muhimbili Willybroad Massawe (kulia) akimuhudumia mgonjwa mwenye tatizo la sikio. 
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara ambao wamejitokeza leo kwa ajili ya kupata huduma za afya, ushauri na matibabu mbalimbali. 

LOWASSA MGENI RASMI UZINDUZI WA ALBAMU YA MARIAM KILYENYI

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ya mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi, utakaofanyika Disemba 2, 2018 katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT)-Sinza Mapambano, jijini Dar es Salaam.

Mbali na Lowassa, waimbaji watakaosindikiza uzinduzi wa albamu hiyo inayoitwa ‘Hakimu wa Haki’ ni Bahati Bukuku, Dk Tumaini Msowoya, Tumaini Njole, Tumaini Mbembela,  Madamu Ruth ,Iren Mwamfupe, Bony Mwaitege, Margie Muliri, Juvenalista Mabuma  Edson Mwasabwite.

Akizungumza na Mwananchi, Mariam alisema amemualika Lowassa kwa sababu ndiyo aliyeanza kuibu kipaji chake, alipompa nafasi ya kuimba siku ya sherehe yake ya kuzaliwa.“Lowassa ni baba yangu, aliibua kipaji change ndio maana nikatamani awe mgeni rasmi na amekubali, namshukuru sana Mungu kwa sababu hii,” alisema.

Alitaja nyimbo zilizo kwenye albamu yake kuwa ni Hakimu wa Haki, Pam Pam tukuza, Natafuta Mshauri, Chereko leo, Nasikia Kuitwa, Agano Langu, Ushindi Lazima na Mapambazuko.“Nasikia kuitwa ndio wimbo ambao niliimba wakati nikianza mbele ya baba Lowassa, kwa hiyo ilipofika hatua ya kuandaa albamu yangu niliuweka na huo kwa sababu ndio ulionifungulia njia,” alisema.

Akizungumzia changamoto alizokutana nazo kwenye muziki huo, Mariam alisema ni gharama kubwa ya uandaaji wa muziki pamoja na kusambaza kazi hiyo.“Naimba muziki kwa sababu nasikia kuitwa kwa ajili ya kazi hiyo, kusema kweli gharama za uandaaji wa kazi nzuri ni kubwa hata hivyo namshukuru Mungu kwa sababu nimeshakamilisha hatua ya kwanza,” alisisitiza.Mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi ambaye atazindua albamu yake skiku ya tarehe 2 mwezi wa 12 mwaka huu.


WAZIRI MKUU AWAPONGEZA WANANCHI KWA UJENZI WA SHULE

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewapongeza wakazi wa kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa kwa kujenga shule ya msingi kwenye kijiji cha Kilimahewa. “Uamuzi wa kujenga shule ya msingi ni sahihi kwa kuwa huwapunguzia watoto kutembea umbali mrefu na pia utarahisisha mazingira ya kusomea kwa watoto wetu.” 

Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo leo (Jumanne, Novemba 20, 2018) alipotembelea eneo la ujenzi wa shule ya msingi Lugalo na kuwataka waendelee na moyo huo. Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli inataka kila mtoto aliyefikia umri wa kwenda shule aanzishwe shule na asome. Kadhalika, Waziri Mkuu ametaka wananchi hao waweke pembeni itikadi zao za kisiasa na badala yake washirikiane kujenga miradi ya maendeleo kwenye eneo lao. 

Nae, Mtendaji wa Kijiji cha Kilimahewa, Majuto Ungulu amesema ujenzi wa shule hiyo uliibuliwa na wakazi wa kijiji hicho, ambacho hakina shule ya msingi. Majuto amesema watoto wa kijiji hicho wanalazimika kutembea umbali wa kilomita mbili hadi shule la msingi Ruangwa, hivyo ujenzi huo utawawezesha kusoma karibu. Amesema kwa sasa wameanzia na ujenzi wa vyumba vinane vya madarasa, matundu 18 ya vyoo na ofisi mbili za walimu ambapo jumla yake ni sh. milioni 399.8. 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ruangwa, Novemba 20, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Ngandirwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ruangwa, Novemba 20, 2018.

Baadhi ya wanawake waliojitokeza kushiriki katika ujenzi wa Shule ya Msingi katika kijiji cha Kilimahewa wilayani Ruangwa wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye eneo la ujenzi wa shule hiyo kukagua ujenzi na kushiriki katika ujenzi huo, Novemba 20, 2010

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Shule ya Msingi ya kwenye kijiji cha Kilimahewa unaofanywa na wananchi wa Kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa, Novemba 20, 2018. 

BUNGE LA CHINA LAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA KASI YA UJENZI WA MIRADI

$
0
0
Na Grace Semfuko-MAELEZO

Bunge la Jamhuri ya Watu wa China limepongeza kasi ya ujenzi wa Miradi inayofanywa na Serikali  ya Tanzania na kwamba ushirikiano uliopo baina ya China na Tanzania utaendelea kuimarishwa ili kuzifanya nchi hizo kuzidi kuwa na maendeleo ya kuichumi.



Hayo yamebainishwa na Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang alipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni Jijini Dar Es Salaam lililojengwa na Kampuni ya China Railway Jiangchang Engineering CRJE na China Major Bridge Engineering Company  ujenzi ulioanza mwaka 2012 na kukamilika April 2016.

Daraja hilo linalovuka mkondo wa maji wa Kurasini hadi Kigamboni  Jijini Dar Es Salaam lina urefu wa mita 680 na njia sita za kupitishia magari ni daraja kubwa katika nchi za Afrika Mashariki na lilizinduliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli April 19 mwaka 2016 na kupewa jina la Julius Nyerere kwa heshima ya Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Hayati  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Ujenzi wa Daraja la Nyerere ulibuniwa na Serikali lengo likiwa ni kupunguza msongamano wa magari uliokuwepo katika kivuko cha Magogoni Jijini Dar Es Salaam na kurahisisha usafiri lengo ni kuwaondolea watanzania changamoto kwenye sekta ya usafirishaji.

Akizungumza katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti huyo wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Cai Defang amesema ni muda muafaka sasa kwa daraja hilo kutumika kama njia za kiuchumi kwa watu wa Tanzania.

“Nimefurahishwa na ujenzi wa Daraja hili uliojengwa na Kampuni ya CRJE ya wachina,wamefanya kazi nzuri, kwa Tanzania daraja hili ni fursa za kiuchumi kwani litarahisisha usafirishaji na kuepukana na vikwazo vilivyokuwepo awali kabla ya dara hili” alisema Cai Defang Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China.



Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi ya jamii la NSSF Bw. William Erio amesema kukamilika kwa daraja hilo kumekuwa na manufaa makubwa kwa Serikali kwani limekuwa likiingizia Serikali mapato yatokanayo na kuvusha magari fedha ambazo zimekuwa zikienda kufanya shughuli zinazoinufaisha jamii ya kitanzania.

“Tunashukuru Serikali kuendelea kubuni miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambayo inasaidia jamii kwa asilimia mia moja,mfano daraja hili ni moja ya vyanzo vya kiuchumi kwani fedha za makusanyo hapa zinasaidia kuongeza kasi ya kuhudumia jamii kupitia ujenzi wa miradi mingine” alisema William Erio wakati akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China alipotembelea kwenye mradi huo wa daraja.
 Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang na watendaji wa (NSSF) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na uongozi unaosimamia huduma za daraja la Nyerere baada ya kukagua daraja hilo leo jijini Dar Es Salaam.
 Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang (wa katika)  akiwa ameambatana na  viongozi mbalimbali wa wakitembelea daraja la Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Emmanuel Massaka MMG)
 Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi ya jamii la (NSSF) Bw. William Erio leo alipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Muonekano wa Daraja kwa sasa
Picha ya pamoja

BoT INA KIWANGO KIKUBWA CHA FEDHA ZA KIGENI KWA KULIPA MADENI KWA MIEZI MITANO IJAYO

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

BENKI kuu ya Tanzania, (BoT), imesema ina kiwango kikubwa cha fedha za kigeni kinachoweza kutosheleza kulipa madeni ya serikali na kutoa huduma zingine katika kipindi cha miezi mitano ijayo.

Hayo yameelezwa na Gavana wa Benki kuu Profesa Frolence Luoga ,alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari mjini Arusha akitoa ufafanuzi kuhusu oporesheni iliyoendeshwa Juzi na benki hiyo dhidi ya maduka ya kubadilisha fedha jijini Arusha.

Gavana,amesema zoezi hilo liliratibiwa na kitengo cha ukaguzi cha benki kuu katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria na ni zoezi la tatu kufanyika nchini.Uchunguzi wa kina katika kipindi cha miezi sita iliyopita ulibaini kuongezeka kwa biashara ya kubadilisha fedha kinyume cha sheria na kukua kwa biashara haramu ya fedha za kigeni na utakatishaji wa fedha hususani kupitia maduka ya kubadilisha fedha.

Jambo ambalo ni hatari kwa uchumi wan chi.

Juhudi za benki hiyo kuwapata wahusika hazikuzaa matunda katika oporesheni mbili zilizopita kwa sababu iligundulika kulikuwepo na mtandao mpana na madhuhuti wa shughuli hizo ambao ulilenga kukwamisha shughuli za udhibiti .‘’Baada ya mashauriano na wataalamu na kushirikiana na vyombo vya upelelezi na usimamizi ilionekana kuwa ili kufanikisha zoezi lililokusudiwa ni muhimu wahusika wote kudhibitiwa kwa wakati mmoja na kufanyiwa ukaguzi jambo lilihitaji ushiriki wa maofisa kutoka vyombo vya dola’’.Alisema gavana .

Amesema zoezi hilo limeshirikisha askari wa jeshi la wananchi na jeshi la polisi na kuzuia watu wasiingie ndani ya maduka hayo kufanya miamala ya kifedha na zoezi hilo limemalizika salama bila kuathiri mtu yeyote.Gavana,amesema katika kipindi cha miezi mitatu ,Benki kuu imesitisha utoaji wa leseni za biashara ya ubadilishaji fedha na maombi yote mapya yamesitishwa na hayatapokelewa.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 20.22.1028


VOA SWAHILI: Duniani Leo November 20, 2018

Michuzi TV: WCB, TEAM KIBA BADO WAPO KWENYE MAZUNGUMZO YA MWISHO WASAFI FESTIVAL

MICHUZI TV: WAZIRI MKUU AZINDUA MSIKITI RUANGWA NA KUSISITIZA UTUMIKE VIZURI

ITV: TAARIFA YA HABARI SAA MBILI KAMILI USIKU NOVEMBA 20,2018

HABARI - AZAM TV NOVEMBA 20, 2018

Viewing all 110129 articles
Browse latest View live




Latest Images