Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

Hoteli 100 kufunguliwa mashitaka ya ukiukaji matakwa ya utumiaji Maji

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Bonde la Wami/Ruvu linatarajia kuwafikisha wamiliki hoteli 100 kutokana na kushindwa kulipa Maji ya visima walivyovichimba.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Afisa wa Maji Bonde la Wami/Ruvu Simon Ngonyani amesema watafungulia mashitaka Novemba 21 kutokana na kushindwa kulipa maji wanayoyatumia katika visima walivyovichimba.Amesema wamekuwa wakifanya mazungumzo na mwisho hakuna matokeo ya ulipaji wa visima hivyo na kuamua kwenda mahakamani.Ngonyani amesema wamiliki wa hoteli 100 wamekuwa wakaidi kuhusiana na ulipaji wa ada ya maji wanayoyatumia.

Aidha amesema kuwa kutokana ulipaji huo uko kisheria sehemu yao ya kwenda kulipia.Amesema kuwa hakuna mtu atakayeachwa salama katika matumizi ya maji ambayo yako kisheria labda hiyo sheria haipo na kama ipo lazima watalipa ili fedha hiyo iendelee kutinza vyanzo vya maji.

"Bonde la Wami/Ruvu litaendelea kusimamia vyanzo vya maji kuhakikisha vinalindwa kwa vizazi vilivyopo na vijavyo hivyo hakuna mtu anayeonewa"amesema Ngonyani.Amezitaja baadhi ya Hoteli zitakazofunguliwa mashitaka mahakamani ni Kebbs Hoteli,Lamada Hoteli, Ubungo Plaza, King Gulf, New Land Hoteli, Flex Hoteli, Rungwe Palace,Roland Hoteli,Luch Time,Saneth Hoteli,pamoja na New Laki.

Ngonyani ,Amesema kuwa kampuni 25 wamepewa notisi ya kuchepusha na kutumia maji kinyume cha sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za maji.Alizitaja baadhi kampuni hizo ni GSM Mall, Farm Equip,Man Trac, Sido Regional, Tol Gases, St.Mary's International School, Dar Group Hospital pamoja na Tarmal Industries Ltd..

Hata hivyo kampuni 25 za mafuta zimepewa notisi ya uchepushaji maji na kutumia kinyume cha sheria.Baadhi ya Kampuni hizo ni PetroAfrica ,State Oil,Meck one Industry,Kobil, Victoria,TSN,Oil Com,Puma,JM Energy Maunt Meru, Lake Group(Lake Oil),GTL Group,Mogas, GBP.
Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu  Simon Ngonyani akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na watumiaji wa Maji ambao hawafuati sheria katika ofisi za Maji Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mahiga amwakilisha Rais Magufuli katika Mkutano Maalum Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU

0
0
Mhe. Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alimwakilisha Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano Maalum wa 11 wa Wakuu Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliyofanyika tarehe 17-18 Novemba, 2018 mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano huo, uliitishwa kufuatia maamuzi ya Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi Julai 2018 mjini Nouakchott, Mauritania ambapo Wakuu hao walielekeza uitishwe Mkutano Maalum kujadili kwa kina mabadiliko ya kitaasisi ndani ya Umoja huo. 


Mkutano huo ulijadili na kutolea maamuzi mapendekezo kuhusu Muundo wa Uongozi (Portfolios) za Kamisheni za Umoja wa Afrika; chaguzi za Uongozi wa Kamisheni; Kusitisha ajira za viongozi wa Kamisheni; na Mabadiliko ya kiutawala na fedha ikijumuisha utendaji.Mkutano ulikubaliana kupunguza idadi ya wajumbe wa Kamisheni klutoka 10 hadi 8 ambao ni Mwenyekiti wa Kamisheni, Makama Mwenyekiti na Makamishna 6. Maamuzi hayo yataanza kutekelezwa mwaka 2021 baada ya uongozi wa Kamisheni uliopo sasa kumaliza muda wake. Maamuzi yote yaliyotolewa yalilenga kuboresha utendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika. 


Mhe. Waziri aliungana na viongozi wengine waliochangia katika mjadala wa kuboresha utendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kuunga mkono mabadiliko ya kitaasisi katika Umoja huo. Mhe. Waziri alieleza kwamba maamuzi hayo yanalenga kuleta ufanisi kwenye kutekeleza majukumu ya Kamisheni na kuhakikisha Afrika inapata maendeleo inayostahili haswa kwa kuzingatia Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia. Nyuma yake ni Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Bi. Naimi Aziz. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Rais Mpya wa Ethiopia, Mhe. Sahle Work Zewdu katika Ikulu ya nchi hiyo tarehe 18 Novemba 2018. Dkt. Mahiga alikwenda kumpongeza Mhe. Rais kwa kuteuliwa na wote wawili walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Ethiopia. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga. (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Mhe. Dkt Workneh Gebeyehu alipokwenda kumtembelea kwa ajili ya kufahamiana jijini Addis Ababa.

TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI YATAKIWA KUHAKIKI ENEO LINALOFAA KWA KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI.

0
0
Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Omary Mgumba ameitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ishirikiane na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali na wataalam kutoka chuo kikuu cha ardhi kuhakiki eneo lenye ukubwa wa hekta 475,052 liloripotiwa na Tume hiyo kuwa linafaa kwa kilimo cha Umwagiaji nchini. 

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Mgumba ameyasema hayo alipofanya ziara katika ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam ili kuongea na watumishi, ambapo aliwataka wao kama Tume washiriki kwanza kuhakiki eneo hilo na kuweza kutoa taarifa za uhakika. 

“Mnaweza kushirikiana na ofisi za kanda na halmashauri ili kuweza kurahisisha kufanyika kwa kazi hii , kwenye kilimo ni vyema tukaenda na mambo yote matatu, kilimo cha kutegemea maji ya mvua, kiimo cha kutegemea maji ya ardhini na kilimo cha kisasa cha umwagiliaji cha kutumia miundombinu, kilimo ambacho kitatuhakikishia uhakika wa chakula kwani ni kilimo ambacho mkulima analima zaidi ya mara moja kwa mwaka.” Alisema Naibu Waziri. 

Sambamba na hilo, Naibu Waziri ameitaka Tume pia kuwasilisha kwake taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi katika eneo la kilimo cha umwagiliaji kwa kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya awamu ya tano na taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali. 

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Omary Mgumba akizungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, wakionekana baadhi katika picha jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Omary Mgumba akiongea na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Miundombimu ya Umwagiliaji Mhandishi Pascal Shayo, kulia ni katibu wa TUGHE tawi la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Cretus Mbogo
Baadhi ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kikao na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba jijini kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo. 

BENKI YA AMANA WAZINDUA MIKOPO YA VIKUNDI KWA WAJASIRIAMALI WADOGO

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

BENKI ya Amana imeadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kuzindua rasmi mikopo ya vikundi ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kutimiza azma ya kuwafikia na kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini. 

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dr Muslim Masoud amesema kuwa, mikopo hiyo ya vikundi itawawezesha wananchi wa kipato cha chini kujikwamua kiuchumi kama wanavyoendelea kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kuwapa mikopo inayoanzia milioni moja hadi kumi. 

Dr Masoud amesema kuwa, mpaka sasa wameshatoa mkopo wa Bilioni 143 kwa wateja wakubwa , wakati na wadogo na wakisaidia kuwainua kiuchumi wajasiriamali wengi na wafanyabiashara wadogo."Benki ya Amana inatimiza miaka saba na mpaka leo tumetoa mikopo ya Bilioni 143 kwa wateja wote wakiwa wameweza kutimiza azma ya kuwafikia na kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini,"amesema Dr Masoud.

Amesema kwa wajasiriamali wadogo watatakiwa kuwa kwenye vikundi na sio mmoja mmoja nanwakiwa katika vikundi hivyo hawatahutajika kuweka dhamana ya aina yoyote.Kwa upande wa Meneja wa Tawi la Benki ya Amana Barabara ya Nyerere, Aisha Awadh amesema, kwa sasa wanatoa mkopo huo kwa wajasiriamali wadogo wale wasio na ajira rasmi ikiwemo Mama Lishe, wauza bidhaa ndogondogo ila watatakiwa wajiunge kwenye kikundi kimoja ili wapatiwe mkopo huo.

Katika kuadhimisha miaka saba toka kuanzishwa kwa benki hiyo, wameweka ofa mbalimbali kwa wateja wao kupitia Wiki ya huduma kwa wateja kwa kupata punguzo maalumu la bei ya Viwanja vinavyotolewa kwa njia ya mkopo na benki hiyo, kwa kushirikiana na kampuni ya Property International Ltd ikiwemo na kuwaonesha viwanja mahali vilipo kwa kuwapeleka eneo husika.

Pia, katika kuwajali wateja wao wamezindua rasmi kampeni ya maalumu ya nufaika na akiba yako kwa wateja watakaowekwa kiasi kisichopungua milioni tano (5,000,000) kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu mfululizo watapata nafasi ya kushinda pikipiki aina ya TVS.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Amana, Dr Muslim Masoud akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja pamoja na ofa mbalimbali walizojipanga kuzitoa kwa wateja wao katika kuadhimisha miaka saba toka kuanzishwa kwa benki hiyo.
Meneja wa Tawi la Benki ya Amana Barabara ya Nyerere, Aisha Awadh akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa mkopo wa vikundi kwa wajasiriamali wadogo utakaokuwa unatolewa kwneye tawi la benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Amana, Dr Muslim Masoud akimsikiliza mteja wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja uliofanyika Tawi la Benki ya Amana Barabara ya Nyerere.

DUCE YAENDESHA SEMINA MASUALA YA KIJINSIA NA RUSHWA YA NGONO KWA WANAFUNZI MWAKA WA KWANZA

0
0

Dk. Neema Gedion Mogha Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Elimu DUCE Chang'ombe jijinin Dar es salaam na Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Viumbe Hai (Baiolojia) akifumgua semina ya Klabu za Jinsia (DUCE Gender Club) za wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho iliyofanyika chuoni hapo mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo mada mbalimbali zilitolewa katika kuwajengea uwezo wanafunzi hao katika masuala ya kijinsia ili kujiepusha kufanya mambo mbalimbali yanayoweza kupelekea rushwa ya ngono.

Ikiwa ni pamoja na wanafunzi wanawake kujitoa bila woga katika masuala ya uongozi, katika picha kulia ni Bi. Upendo Mlungusye Msaidizi Mshauri wa Wanafunzi DUCE na kutoka kushoto ni Dorothea Fumpuni Mhadhiri na Mlezi wa klabu za Jinsia DUCE na Dk. Ikupa Moses Mratibu wa Kitengo cha Jinsia DUCE.
Dk. Neema Gedion Mogha Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Elimu DUCE Chang'ombe jijinin Dar es salaam na Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Viumbe Hai (Baiolojia) akifafanua jambo wakati akifumgua semina ya Klabu za Jinsia (DUCE Gender Club) za wanafunziwa chuo hicho mwishoni mwa wiki iliyopita kulia ni Bi. Upendo Mlungusye Msaidizi Mshauri wa Wanafunzi DUCE na kushoto ni Dk. Ikupa Moses Mratibu wa Kitengo cha Jinsia DUCE.
Dk. Ikupa Moses Mratibu wa Kitengo cha Jinsia DUCE akimkaribisha Dk. Neema Gedion Mogha Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Elimu DUCE Chang'ombe jijinin Dar es salaam na Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Viumbe Hai (Baiolojia) ili kufungua semina hiyo kutoka kulia ni Mhadhiri wa Chuo hicho Dk. Perpetua John Urio na Bi. Upendo Mlungusye Msaidizi Mshauri wa Mshauri wa Wanafunzi DUCE.

Dk. Ikupa Moses Mratibu wa Kitengo cha Jinsia DUCE akizungumza katika semina hiyo.
Baadhi ya wanafunzi na wanachama wa klabu za jinsia Chuo Kikuu cha Elimu DUCE wakiwa katika semina hiyo.

WAZIRI JAFO AKABIDHI RASMI MASHINE MAALUMU ZA KUTIBU MAGONJWA MBALI MBALI HOSPITALI YA KISARAWE

0
0

VICTOR MASANGU, KISARAWE

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amekemea vitendo vya upokeaji wa rushwa vinavyofanywa na baadhi ya wauguzi,wataalamu wa afya na madaktari kuwataka kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wahakikishe wanatoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa kwa kuzingatia misingi ya weledi ya kazi yao bila kuwa na ubaguzi wowote.

Jafo alitoa kaul hiyo wakati akizungumza na wataalamu wa afya, pamoja na wananchi wakati wa sherehe za kukabidhi mashine maalumu kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa ya aina mbali mbali katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambapo viongozi wa serikali madiwani pamoja na viongozi wa dini waliweza kushiriki katika zoezi hilo.

Aidha Waziri Jafo alibainisha kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaboresha sekta ya afya kuanzia ngazi za maeneo ya vijijini kwa kuongeza ujenzi mpya wa zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali lengo ikiwa ni kuwaondolea adha wananchi katika suala zima la upatikanaji wa huduma ya matibabu kwa urahisi zaidi.

“Napenda kuchukua fura hii kuwambia ndugu zangu wananchi wa Kisarawe kwa kweli Rais wetu anafanya kazi kubwa sana ya kuhakikisha analeta maendeleo katika sekta mbali mbali hapa nchini na kwa sisi watu wa kisarawe tumepata bahati kubwa sana, kwa hiyo nipende kuwaambia tutaendelea kuboresha huduma ya afya katika zahanati zetu, vituo vya afya pamoja na ujenzi wa Hospitali nyingine mpya,”alisema Jafo.

Waziri wa chi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kulia Selemani Jafo akikata utepe wakati wa sherehe ya kukabidhi mashine kwa ajili ya kutibu magonjwa mbali mbali katika hospitali ya Kisarawe, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo 
Mganga mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kulia Jonathan Budenu akifafanua jambo kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa  (TAMISEMI) Seleman Jafo mara baada ya kukabidhi mashine hizo katika hospitali ya Wilaya.  
Waziri wan chi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kulia wakiwa na baadhi ya viongozi wengine wa serikali wa kati kati ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo na kushoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kisarawe Musa Gama katika halfa hiyo ya makabishiano ya mashine za kutibu magonjwa mbali mbali. 

WAZIRI WA FEDHA AHIMIZA TRA KUTENGENEZA WALIPA KODI NCHINI

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ameitaka Mamlaka ya mapato nchini ( TRA) kuwa na mpango wa kuwatengeneza walipakodi na sio kutegemea walipakodi waliozoeleka pekee kwa kuwa wananchi wana utayari wa kulipa kodi ila hawafikiwi na mamlaka hiyo.

Akihutubia na kutunuku vyeti kwa wanafunzi 360 wa ngazi za vyeti, stashahada na shahada  katika mahafali ya kumi na moja ya chuo cha kodi  jijini Dar es Salaam Dkt. Kijaji amesema kuwa maendeleo endelevu yatafikiwa kwa kuangalia na kuwafuata walipa kodi na sio kukaa maofisini, na ameitaka mamlaka hiyo kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi hasa za majengo na kusema kuwa wananchi wapo tayari kulipa kodi hizo ila hawafikiwi na wataalamu kutoka katika mamlaka hizo.

Aidha amesema kuwa kupitia bodi ya mikopo wataendelea kuangalia uwezekano wa kuongeza fedha za mikopo ili kuwawezesha wanafunzi wengi wakiwemo wanaosomea masuala ya taaluma ya kodi kupata fedha za kulipia masomo yao.

Pia Kijaji amewataka wahitimu  hao kutumia vizuri kofia walizopewa na chuo hicho na kuwa mabalozi wazuri wa chuo cha kodi na kuisaidia Serikali kutoa elimu na kukusanya kodi ili kuweza kufikia azma ya Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Dkt. John Magufuli ya kufikia uchumi wa kati.

Kwa upande wake Kamshina mkuu wa mamlaka ya mapato nchini Charles Kichere amewapongeza wahitimu hao na kuwataka kutumia vyeti vyao vizuri katika kuleta maendeleo ya taifa.

Kichere amesema kuwa  mamlaka hiyo inahakikisha elimu ya kodi inasambaa nchi nzima  kwa wadau  na taasisi kuhusiana na ulipaji wa kodi kwa hiari.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha kodi Profesa Isaya Jairo amesema kuwa zaidi ya watumishi 4449 wa mamlaka ya mapato nchini ndani ya miaka mitano wamepata elimu kuhusiana na masuala ya kodi na forodha na amesema kuwa udahili wa wanafunzi katika chuo hicho umekuwa ukiongezeka kila mwaka na hiyo ni kutokana na upekee na ubora wa elimu inayotolewa chuoni hapo.

Jairo amesema kuwa chuo hicho kinashirikiana na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi  hasa zile zinazojihusisha na masuala ya forodha katika kuhakikisha wanaboresha sekta hiyo kila mwaka.

NEWS ALERT: Magazeti Yasiyohuishwa Kufutwa, Yamo Jamhuri, Jamvi la Habari, Uhuru

0
0

Serikali kupitia Idara ya Habari-MAELEZO imetoa siku saba (7) kuanzia leo tarehe 19 Novemba,2018  kwa wamiliki wa machapisho/majarida ambayo muda wa leseni zao  umekwisha kuhuisha leseni zao.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Bw. Patrick Kipangula kwa niaba ya Mkurugenzi Idara ya Habari-MAELEZO inasema kuwa,  kuendelea kuchapisha na kusambaza machapisho ambayo muda wa leseni iliyoyolewa umekwisha ni kosa kisheria na Idara haitasita kuchukua hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufuta chapisho au jarida katika orodha ya machapisho yaliyopo.
Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa, ili kupata majina ya machapisho ambayo muda wa leseni zao umekwisha tembelea tovuti ya Idara ya Habari - MAELEZOwww.maelezo.go.tz sehemu ya chini kipengele cha "NIfanyeje" au kwa ufafanuzi zaidi wasiliana nao kwa namba zifuatazo 0622 664606 na 0717 312417.
Katika kutimiza utekelezaji wa matakwa ya Kifungu 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari na 12ya 2016 kikisomwa pamoja na kanuni zake 8(3)(4) na 12 ya Kanuni za Sheria za Huduma za Habari 2017 Tangazo la Serikali Na.18 la tarehe 3/2/2017 Idara ya Habari-MAELEZO inaendelea na zoezi la kuhuisha leseni za machapisho na majarida ambayo muda wake umefikia ukomo tangu kutolewa kwa leseni hizo.


RC MTWARA- TUTAKAGUA SHAMBA HADI SHAMBA KUJIRIDHISHA NA MALIPO YA WAKULIMA WA KOROSHO

Michuzi TV: MBUNGE WA KASULU VIJIJINI AZUNGUMZIA HARAKATI ZA MAENDELEO JIMBONI

MICHUZI TV: VIGOGO WAHUSISHWA KUCHOCHEA MIGOGORO YA ARDHI MBARALI

MICHUZI TV: BANK YA CRDB YAZIDI KUIBUA WASHINDI WA "SHINDA NA SIMU ACCOUNT"

Wapigie Kura Rau eco & Cultural Tourism

MICHUZI TV: RAIS DKT MAGUFULI AMEFANYA MAMBO MAKUBWA KWA MUDA MFUPI - MBUNGE KINGU

MICHUZI TV: MIAKA MITATU YA MAGUFULI TUMEISHUHUDIA KWA VITENDO NA SI MANENO - MBUNGE MABULA


Yapi Merkezi Tanzania Standard Gauge Railway Line From Dar Es Salaam to Morogoro Project OCTOBER2018

MICHUZI TV: ATE YAFANYA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA WANAWAKE KATIKA UONGOZI WA MWAKA 2018

MICHUZI TV: JWTZ WAKO KAMILI KATIKA ZOEZI LA UKUSANYAJI KOROSHO, WAKUKLIMA ZAIDI YA 2000 WAPATA MALIPO

GOOD NEWS -HIZI HAPA KILOMITA 30 ZILIZO TANDIKWA RELI UJENZI WAFIKIA ASILIMIA 35

Habari za UN Kutoka New York, Marekani, Novemba 19, 2018

Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images