Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 258 | 259 | (Page 260) | 261 | 262 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Baadhi  ya wahitimu wa  darasa la saba shule ya Southern Highlands Mafinga mwaka 2013
  mkurugenzi mtendaji  wa shule ya Southern Highlands Mafinga Iringa Bi Mary A. Mungai akiwahakikishia  wazazi ubora wa shule  yake
  mkurugenzi mtendaji  wa shule ya Southern Highlands Mafinga Iringa Bi Mary A. Mungai akimpongeza mmoja kati ya  wahitimu wa  darasa la  saba mwaka 2013.

  Na Francis Godwin Blog

  WAKATI wanafunzi wa darasa la saba kote nchini wakiendelea kusubiri matokeo ya mtihani wa darasa la saba ,uongozi wa shule ya kimataifa ya Southern Highlands Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani hapa umewahakikishia wazazi kuwa wawe na uhakika mkubwa wa watoto wao kufaulu mtihani huo.

  Mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Bi Mary Mungai ambae amepata kuwa afisa elimu wa shule za msingi alitoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya 13 ya darasa la saba shuleni hapo juzi.

  Alisema kuwa toka shule hiyo ilipoanzishwa mwaka 1994 kama Day Care na Pre-school na mwaka 1997 kuanza shule ya msingi imekuwa ikifanya vizuri na hakuna mtoto aliyepata kufeli .

  “Shule yetu mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanza wa darasa la Saba na wanafunzi walikuwa 17, wote walifaulu vizuri na wote walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza” Alisema katika matokeo ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 Southern Highlands School ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani ya Somo la Kiingereza. 

  “ Tulimshukuru Mungu na tunaendelea kumshukuru Yeye. Kwa kuwezesha watoto wetu wa Southern Highlands School, kufaulu vizuri, kwa kishindo” alisema Bi Mungai Hata hivyo alisema kila wanafunzi wote wamekuwa wakifaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na wote kuchaguliwa na kuendelea na masomo ya Sekondari.

  “Ninaamini wanafunzi wote wa darasa la saba 47 waliomaliza mwaka huu 2013, watafaulu na kuchaguliwa kuendelea na sekondari….. Sababu walikuwa wanapenda masomo na nidhamu yao ni nzuri.”

  Kwa upande wake mkurugenzi wa bodi ya shule hiyo Bw Omary Mahinya alisema kuwa katika moja ya vielelezo kuwa shule hiyo ni bora nchini ni wazazi kutoka mikoa karibu yote ya Tanzania kupeleka watoto wao hapo .

  “Wahitimu toka shule yetu wamekuwa wakifanya vizuri katika Sekondari kidato cha IV na kidato cha VI popote walipo kwenda… hii inadhihirisha kuwa Southern Highlands School imewajengea msingi bora wa Elimu ambao ni TUNU ya kujivunia sana. Aidha alisema kuwa lengo la uongozi wa shule hiyo ni kuhakikisha kuwa Southern Highlands School inakuwa mfano bora na kioo kwa jamii inayotuzunguka kwa kuweka mazingira bora ya kuishi

  0 0

  Na Tamimu Adam, Jeshi la Polisi

  Jumla ya watuhumiwa 32 wa unyang'anyi wa kutumia silaha na wahamiaji haramu 6809 wamekamatwa kufuatia operesheni kimbunga ya kuwasaka majambazi, watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na kuwaondoa wahamiaji haramu inayoendelea katika mikoa mitatu Kigoma, Kagera na Geita hapa nchini.

  Akizungumzia operesheni hiyo Naibu kamishina wa Polisi (DCP) Simon Siro alisema kuwa operesheni hiyo ilifanyika na kufanikiwa kuwakamata wahamiaji Hao haramu wakiwemo wanyarwanda 1446, warundi 4229' na waganda 647.

  Wengine ni wakongo 443,wasomali 42, Myemeni1 pamoja na mhindi 1 Alisema kuwa operesheni hiyo pia ilifanikisha kukamata silaha 22 zikiwemo bunduki nne (4 ) za kivita aina ya SMG, gobole 15 ,shot gun moja(1)mark iv moja (1)na risasi za bunduki za kivita SMG na SAR 265 mark iv 20 na risasi za gobole 82 , Pamoja na mitambo miwili (2) ya kutengenezea magobole.

  Aidha, aliongeza kuwa katika operesheni hiyo walifanikiwa kukamata mabomu sita(6) ya kurusha kwa mkono pamoja na nyara za Serikali.

  Alibainisha nyara hizo kuwa ni ngazi ya Duma mmoja(1), ngazi mbili za Swala na magogo 86 pamoja na vipande kumi (10) vya nyama vinavyodhaniwa kuwa ni vya nyara za Serikali.

  Kamanda SIro aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa zozote za uhalifu, wahamiaji haramu, na watu wanaowajua kuwa wanamiliki silaha kinyume cha Sheria ili waweze kukamatwa na kuwafikisha katika vyombo vya Sheria.

  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe kuzindua maonyesho ya siku ya Mara yaliyofanyika Mugu wilayani Serengeti Septemba 15, 2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama magugu maji baada ya kufungua maonesho ya siku ya Mara kwenye uwanja wa Sokoine Mjini Mugumu, Septemba 15, 2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Soka ya Wnawake ya Manispa ya Musoma, Mariam Ibrahim baada ya timu yake kunyakuwa ushindi wa kwanza katika shindano ya kuadhimisha siku ya Mara, katika kilele cha maadhimisho ya siku hiyo mjiniMugumu Septemba 15,2013.


  0 0

  Jeshi la  polisi  mkoani Iringa  linamshikilia mwalimu wa  shule ya msingi Makungu wilaya ya  Mufindi Bw Edwin Ambukile kwa  tuhuma  za  kuwasaidia majibu wanafunzi wa  darasa la  saba katika mtihani  wa Taifa  wa kuhitimu elimu ya msingi.

  Kamanda  wa polisi mkoa  wa Iringa Bw Ramadhan Mungi (pichani) amesema  kuwa tukio  hilo limetokea  Septemba 15 mwaka  huu.
  Alisema kuwa mwalimu  huyo ambae ni mwalimu wa masomo ya Sayansi katika  shule  hiyo pia alikuwa ni mwalimu wa masomo ya ziada ( katika  shule  hiyo na  sababu ya  kuwasaidia  wanafunzi majibu ni kutaka  kupata umaarufu kwa wanafunzi  watano aliokuwa akiwafundisha masomo ya  ziada aliopata  kuwaahidi kuwa watafaulu mtihani  huo. 
  Alisema  kuwa  mwalimu  huyo tarehe 11 septemba  alipokea mitihani kutoka kwa msimamizi  na baada ya hapo akafungua bahasha   ya masomo ya  Sayansi na kuanza  kufanya mwenyewe  na majibu kuyatuma kwa Sms kwa  mke  wake .
  Hata  hivyo  siku ya mtihani mmoja kati ya wanafunzi  waliopata majibu hayo alipoingia katika  chumba  cha mtihani alionekana akitetemeka  kupita  kiasi na  hivyo msimamizi wa mitihani alipompekua alimkuta na majibu hayo na kueleza jinsi alivyosaidiwa na mwalimu  huyo .
  Kamanda  wa  polisi alisema  siku ya mtihani  mwalimu Ambukile  alipangiwa kusimamia  shule  ya msingi Igomaa na  sasa amekamatwa na atafikishwa mahakamani  wakati  wowote kuanzia sasa. 

  0 0   Siku za hivi karibuni, ongezeko la huduma za mawasiliano nchini limekuwa kwa kasi sana. Huduma za mawasiliano nchini katika kipindi kifupi zimekuwa sana na kuwafikia Watanzania wengi zaidi. Kutoka laini za simu za mkononi milioni tatu tu mwaka 2000 hadi kufikia laini 28,000,000.


  Watanzania walio wengi hivi sasa wanafaidika kwa huduma za mawasiliano, yakiwemo mawasiliano ya simu za mikononi, utangazaji. Vile vile huduma za ziada kama kutuma na kupokea fedha kwa kutumia mitandao na simu za mkononi zimeongezeka maradufu. Wananchi wengi wanapata huduma za kibenki kwa kutumia simu zao, wanawasiliana kwa kutumia simu zao kupitia sauti, SMS na kadhalika.

  Hali kadhalika kumekuwa na ongezeko la matumizi ya intaneti kwa watanzania walio wengi kutoka watumiaji laki tatu miaka mitatu iliyopita hadi watumiaji milioni 7.6 kwa takwimu za hivi karibuni. Wengi wa watumiaji wa intaneti matumizi yao ni katika kujifunza na kujielimisha pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, BBM, LinkedIn na blog mbalimbali zinazotoa habari mbalimbali zikiwemo za kimaendeleo, burudani pamoja na michezo. 

  Matumizi haya ya intaneti yamewanufaisha watanzaia walio wengi kwani ni fursa murua ya kujifunza kupitia mitandao hiyo ya kijamii kwa kupata habari mpya, kujifunza na kuelimishana kuhusu shughuli za maendeleo na kuleta amani miongoni mwa watanzania.
  Hata hivyo pamoja na maendeleo haya, kumekuwepo na baadhi ya watu wachache wanaotumia mawasiliano ya simu, mitandao ya kijamii, redio, TV na mawasiliano mengine kwa lengo la kuvuruga amani, kuchocheo vurugu, kuchonganisha watu, kusababisha ugomvi, kuwaumiza wengine kwa mambo yasiyo na ukweli, kupotosha jamii na hata kuvuruga maendeleo kwa ujumla.
  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezindua kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi mazuri ya mawasiliano na inawatahadharisha wananchi kwamba kutumia mawasiliano vibaya kama ilivyoainishwa katika sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 ni makosa. Katika kampeni hii, Mamlaka inakusudia kuwasihi wananchi kuhakikisha wanatumia mawasiliano vizuri ili kudumisha amani, mshikamano na upendo miongoni mwa watanzania.
  Watumiaji wa simu za mkononi na wananchi wote wanashauriwa kuunga mkono juhudi zinazofanyika ili kufanikisha kampeni hii kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta ya Mawasiliano inaendelea kuchangia uchumi wa Taifa na kuiweka Tanzania katika mazingira mazuri zaidi kijamii, kiuchumi na kisiasa.

  Tunawasihi wananchi na watumiaji wa huduma za mawasiliano kuwa wakipokea ujumbe wowote wa kueneza chuki, unaopelekea kuvuruga amani, uchochezi na kuvuruga amani, toa taarifa kwa vyombo husika, kisha futa ujumbe huo. Usiueneze kwa wengine kwani utakuwa sehemu ya uhalifu.


  IMETOLEWA NA 
  Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA),
  Mawasiliano Towers,
  20 Sam Nujoma Road,
  Dar es salaam

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, leo amewasili nchini akitokea India alikokwenda kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.

  Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, Maalim Seif alipokelewa na viongozi mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdallah Mwinyi Khamis.

  Aidha mapokezi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na viongozi pamoja na wafuasi wa Chama Cha Wananchi CUF, yaliambatana na shamra shamra mbali mbali za burudani.

  Maalim Seif aliondoka nchini tarehe 24 mwezi uliopita kuelekea India kwa ajili ya uchunguzi wa kawaida wa afya yake, utaratibu ambao umekuwa ukifanyika tangu alipofanyiwa upasuaji wa goti miaka mitatu iliyopita.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis pamoja na viongozi wengine, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na viongozi mbali mbali, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisawapungia mkono wananchi waliojitokeza kumpokea, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
  Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Awena Sinani Masoud (kulia), alionesha uso wa bashasha baada ya kuwasili nchini akitokea India. (picha na Salmin Said, OMKR)

  0 0  Aloe Fleur de Jouvence-Flower of Youth
  • The world’s best natural and wrinkles treatment facial
  • Lifting and rejuvenating facial
  • Includes the power of aloe combining with anti-aging ingredients to deliver results you can see, feel and love the skin you are in @ only Tsh 210,000.
  • Call 0718144039/0786766028 for more information

  Aloe Fleur de Jouvence-Flower of Youth is one of the most effective restorative beauty collections ever assembled. It is a collection of six wonderful components – each designed to fill a special part in a complete regimen of facial skin care.

  To create one of the most effective restorative beauty regimes ever assembled, we took pure, stabilized Aloe Vera gel, combined it with nature’s own collagen, and added exceptional moisturizers, emulsifiers and humectants.

  Each product in Aloe Fleur de Jouvence has been developed with great care and attention to the daily needs of your skin. We start with pure, Stabilized Aloe Vera gel, and combine it with nature’s unique cellular substance, Collagen, along with exceptional moisturizers, emulsifiers and humectants. This creates a unique skin care range that helps counteract the threat of time, weather and environmental elements. The preventive and restorative Aloe Fleur de Jouvence program provides a daily skin care regime to help promote the naturally occurring attributes of youth, vigor, freshness and radiance of the skin.

  Aloe Vera has always been great for the skin. Now, pamper yourself even more with Aloe Fleur de Jouvence!

  The Aloe Fleur de Jouvence Collection includes:
  Aloe Cleanser
  Rehydrating Toner
  Firming Day Lotion
  Recovering Night Creme
  Mask Powder
  Aloe Activator
  Mixing spoon, applicator brush

  For more information Call 0718 14 40 39 / 0786 76 60 28

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mhe.Deodorus Kamala(,mwenye suti) akitoa maelezo kwa Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ambae ameongoza ujumbe wa Wabunge wawili na watumishi nchini Ubelgiji kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa wabunge toka nchi za Afrika,Carribbean na Pacific. Wengine pichani ni Mbunge wa Viti Maalum Dr Mary Mwanjelwa na Katibu wa Msafara huo Bw.Aggrey Nzowa ambae pia ni Mkurugenzi Msaidizi (Huduma za Maktaba) katika Ofisi ya Bunge.
  Mhe Mussa Azzan Zungu (kulia) akifuatilia kwa makini maelezo ya Balozi Kamala. Picha na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.

  0 0
 • 09/17/13--00:02: KIJIWE CHA UGHAIBUNI

 • 0 0

  NA VOA KISWAHILI

  0 0

  Marehemu Adubo Mustafa Omer 
  enzi za uhai wake

  Baada ya uchunguzi wa zaidi ya wiki tatu,Ubalozi wa Tanzania Washington DC umethibitisha kuwa Marehemu Adubo M. Omer hakuwa Raia wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania bali alikuwa Raia wa Sudan.
  Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu Dar Es Salaam ilielezwa kuwa,hakuna kumbukumbu zozote zinazoonyesha kuwa, Marehemu Adubo aliwahi kupewa Uraia wala Pasipoti ya Tanzania.
  Aidha,kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa kutoka kwenye taasisi mbali mbali za Kiserikali zilizopo mjini Dallas Texas, Marehemu Adubo M Omer alizaliwa tarehe 25.04.1956 katika sehemu iitwayo Maridi Abang, iliyopo Sudani ya Kusini.

  Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa marehemu Adubo, alikuwa amepewa hati ya kudumu ya ukaazi Nchini Marekani (Permanent Resident card) ambayo ilikuwa inamaliza muda wake tarehe 8.03.2014.

  Ubalozi ulipotaka kujua, ilikuwaje hadi ofisi ya 'Medical Examiner' ambayo inafanya uchunguzi wa sababu za kifo cha Marehemu Adubo imtambulishe ubalozini marehemu huyo kama Raia wa Tanzania? Msemaji wa ofisi hiyo alieleza kuwa, hii ni kwa mujibu wa maelezo ambayo marehemu mwenyewe aliyatoa kwenye kituo cha Police cha Dallas, alikokuwa amekamatwa na
  kuwekwa ndani kwa siku chache kisha akaachiwa kabla ya kifo chake.

  Inaelekea Marehemu Adubo hakutaka Uraia wake ujulikane kwa sababu ambazo hazikuweza kueleweka. Suala hili, lilileta utata na hisia ambazo zimeuletea Ubalozi usumbufu ambao haukuwa na ulazima wowote.

  Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania washington DC, inapenda kuwashukuru Watanzania wote waliopo Ndani na Nje ya Nchi waliosaidia katika jitihada za kupatikana kwa taarifa sahihi za mtu huyu. vile vile Ubalozi unazishukuru taasisi zote za hapa Marekani ambazo kwa namna moja au nyingine zimetoa ushirikiano wenye tija uluotuwezesha kulitatua suala
  hili.

  Shukurani za pekee, ziwaendee blogs za vijimambo na swahili villa, bila kuwasahau uongozi wa jumuia ya Watanzania waishio Dallas Texas, Bw Franklin Maji, Mchungaji Absalom na Bi aysha Burnett.
                    IMETOLEWA NA OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA
  WASHINGTON DC.

  0 0  0 0

  Timu ya Copa Coca-Cola iliyoshiriki katika michuano ya kimataifa ya Copa Coca-Cola nchini Afrika Kusini wiki iliyopita ikiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu jioni. Timu hiyo ilitolewa katika hatua ya makundi na Zimbabwe kuibuka mabingwa.
  Afisa maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Salum Madadi akiipokea timu ya vijana ya Copa Coca-Cola iliyoshiriki katika michuano ya kimataifa ya Copa Coca-Cola nchini Afrika Kusini wiki iliyopita. Timu hiyo ilitolewa katika hatua ya makundi na Zimbabwe kuibuka mabingwa. Zimbabwe waliibuka mabingwa wa 2013 wa mashindano ya kimataifa ya COPA Coca-Cola kwa kuwafunga Uganda 3-0 katika mchezo wa fainali iliyochezwa High Performance Center, Pretoria, Afrika Kusini.  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akiwasilisha mada ya kwanza juu ya Ukubwa wa Sekta ya Mawasiliano hapa nchini wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
   Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akifafanua jambo wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Sekta ya Washangiaji na Watoa Huduma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Dkt. Raynold Mfungahema akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya Wapiga Picha kutoka Vyombo mbali mbali vya habari wakiendelea na zoezi la kuchukua matukio mbali mbali wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Blogggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.


  0 0

   RPC wa Mkoa wa Morogoro,Faustine Shilogile akisalimiana na Mkurugenzi wa Anatory Pool club,Anatory Makasi alipotembelea ofisini kwake kutambulisha club yake kuwa ndio wanaopeperusha bendela ya mkoa katika fainali za kitaifa ziazotarajiwa kufanyika wiki hii mkoani humo kwa kushirikisha mikoa 17,ikiwakilishwa na vilabu 17.
   RPC, Faustine Shilogile,Mkurugenzi wa Anatory,Anatory Makasi,Uongozi wa TBL Mkoa wa Morogoro na wachezaji wa Club ya Anatory wakiwa kwenye picha ya pamoja.
   Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Anatory Pool Club, Anatory Makasi,Supervisor kutoka Kampuni ya Integrated Communications Limited, Amadeo Thadeo, Meneja mauzo TBL Mkoa wa Morogoro, Jemes Gomila na Wachezaji wa Club ya Anatory wakimsikiliza RPC wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile(hayupo pichani) walipomtembelea ofsini kwake leo kujitambulisha kuwa wao ndio mabingwa wa mkoa watakaopeperusha bendera ya mkoa kwenye fainali za kitaifa zinazofanyika wiki hii mkoani hapo.
   Mkurugenzi wa Anatory Pool Club, Anatory Makasi(wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wake kwenye Clab yake kabla ya kuanza ziara.

  0 0

  Kikosi cha timu ya wavulana kinachoshiriki michuano ya Airtel Rising stars nchi Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuondoka katika uwanja wa Julius Kambarage nyerer kuelekea Nigeria kwenye michuano ya Afrika inayoshirikisha timu kutoka nchi 17 barani Afrika .Wa kwanza kulia ni mwakilishi wa Airtel Bi Lilian Kibiriti
  Kikosi cha timu ya wasichana kinachoshiriki michuano ya Airtel Rising stars nchi Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuondoka katika uwanja wa Julius Kambarage nyerer kuelekea Nigeria kwenye michuano ya Afrika inayoshirikisha timu kutoka nchi 17 barani Afrika. (mwenye shuti) ni kocha wa timu hiyo Rogacian Kaijage.
  Kikosi cha timu ya Airtel Rising stars wakati wa ufunguzi wa michuano ya Airtel Rising Stars ya Afrika inayozinduliwa rasmi jana (jumatatu) Nchini Nigeria na kushirikisha timu kutoka katika nchi 17 barani Afrika.

  Timu zinazoshiriki michauano ya pili ya Afrika ya Airtel rising Stars inayofanyika nchini Nigeria mwaka huu zimewasili ambapo michuano hiyo imeanza rasmi jana katika viwajnja vya Agege. michuano hiyo imeudhuriwa na wachezaji guru wakiwemo Rober Pires mchezaji nyota wa zamani wa kablu ya Arsenal

  Timu ya Zambia ilikuwa yakwanza kutua siku ya Ijumaa ikifatiwa na timu ya Ghana iliyotua muda mchache baadaye siku hiyo. timu ya mabigwa watetezi kutoka Niger ilitua katika uwanja wa ndege wa Murtala Mohammed International siku ya jumamosi mchana pamoja na timu kutoka Congo Brazzaville

  kikosi cha timu ya Tanzania kiliwasili siku ya jumapaili chini ya kocha Abel Mtweve na timu nyingine zinategemea kuwasili kabla ya michuano hiyo kuanza siku ya jumatatu

  michuano ya Airtel Rising stars ni michuano ya kipekee ya nchi za Afrika yenye lengo la kuvumbua na kukuza vipaji huku ikiwezesha nchi za Afrika kupata wachezaji wa timu za taifa

  kwa kupitia mashindano haya Airtel inatoa nafasi kwa vijana hawa kutimiza ndoto zao, na kuonyesha uwezo wao kwa zaidi ya mamilioni ya watu alisema mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria bwana Segun Ogunsanya

  aliongeza "wachezaji wengi wameshiriki michuano mikubwa kama hii kwa mara ya kwanza na wanafurahia kupata nafasi ya kushindana na wachezaji nyota wengine toka katika nchi mbalimbali. kwa wiki nzima tunaamini wachezaji hawa watabaki na kumbukumbu ya mpira ambayo wataifurahia katika maisha yao siku zote"

  michuano ya Airtel Rising stars itafanyika nchini lagos Nigeria kuanzia tarehe 16 hadi 22 septemba 2013. wachezaji nyota waliochaguliwa watashiriki katika clinic itakayosimamiwa na makocha wa Manchester united inayotegemea kufanyiaka mwaka kesho April 2014 nchini Lubumbashi (Democratic Republic of Congo).

  0 0

   AFISA Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Dorris Malulu mwenye miwani akikabidhi hundi yenye thamani ya sh. Mil. 13 kwa Daktari wa Upasuaji katika hospitali ya  Tumbi Kibaha, Pwani,hiyo Dkt. Petter Datan, katikati ni Mkuu wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani mkoani Pwani Nassoro Sisiwaya katikati ni mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo. 
  Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro dk Godfrey Mtey kushoto akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Afisa Uhusiano wa kampuni ya bia ya TBL, Doris Malulu yenye thamani ya sh14.6 milioni ili kuweza kutumika wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ikihusisha madereva wa nagari kupima afya katika mizani ya Mikese mkoa wa Morogoro, katikati ni Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Boniface Mbao.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (pichani) ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Iringa ameagiza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu utendaji wa vituo vya mizani mkoani Iringa. Agizo hilo lilitolewa katika mkutano ambao Waziri huyo wa Ujenzi alikutana na wafanyakazi wa taasisi zinazosimamiwa na Wizara ya Ujenzi mkoani humo.

  Wakati akisomewa taarifa za utekelezaji wa majukumu ya kila taasisi mkoani humo ndipo lilipojitokeza suala la tozo iliyokusanywa kwa magari yaliyokamatwa yakiwa yamezidisha uzito kwa kipindi cha mwezi mmoja wa Julai mwaka huu wa 2013 katika kituo cha mizani cha Wenda kilichop kati ya Iringa na Ifunda katika barabara kuu ya TANZAM.
  Meneja wa Tanroads wa mkoa wa Iringa Injinia Poul Lyakurwa alimtaarifu Waziri Magufuli kuwa kiasi cha Shilingi milioni 31.9 kilikusanywa katika kipindi hicho cha mwezi mmoja.
  Akishitushwa na kiwango hicho Waziri Magufuli  alibainisha kuwa, kiasi hicho kilichosomwa katika taarifa kimetokana na magari 735 yaliyokamatwa kati ya magari 20,700 yaliyopimwa sawa na asiliamia 3.5. “Takwimu hizi sizikubali kwani wastani wa magari yanayokamatwa katika nchi nzima unakaribia asiliamia 40 iweje barabara kuu kama hii iwe na kiwango kidogo kiasi hicho cha magari yaliyokutwa na makosa” hapa ni lazima pafanyike uchunguzi” alisisitiza Mheshimiwa Magufuli na kueleza kuwa hali hiyo hawezi kuiruhusu hata kidogo kuendelea.

  Katika hatua nyingine Waziri Magufuli amempongeza Meneja huyo wa Tanroads kwa kufukuza wafanyakazi 18 katika Kituo cha Mizani cha Makambako kwa kutokuwa waaminifu katika kazi zao. Waziri huyo wa Ujenzi aliendelea kubainisha kuwa, takriban asilimia 70 ya wafanyakazi waliokuwa katika vituo mbali mbali vya mizani ya barabara nchi nzima wamebadilishwa baada ya kukamilika kwa zoezi la kutangaza nafasi hizo upya.
  Akisisitiza zaidi, Waziri Magufuli alisema “Wizara ya Ujenzi itaendelea kushirikia na taasisi mbali mmbai zikiwemo PCCB, Jeshi la Polisi, TRA na hata kwa kutumia makondakta na wasaidizi katika magari ya usafirishaji ili kuendelea kubaini mbinu mbali mbali ambazo zinaendelea kutumika katika suala zima la vitendo vya rushwa katika vituo vya mizani hapa nchini”.
  Kwa upande mwingine Wakala wa Majengo Nchini pamoja na Wakala wa Ufundi na Umeme wametakiwa kuwa wabunifu ili waweze kukabiliana kikamilifu na changamoto mbali mbali zinazowakabili.

  0 0

  Fundo 2

  Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata akiwaelekeza wanafunzi wa shule ya Msingi Maskul Fundo, Jimbo la Gando kisiwani Pemba jinsi ya kutumia taa za nishati Jua walipotembelea shule hiyo katika moja ya kampeni zake za kugawa taa za nishati mbadala kwa shule za msingi nchini.
  Fundo 3
  Mkurugenzi wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann akiangalia jinsi mwanafunzi anavyoweza kuwasha taa ya nishati ya Umeme Jua jana visiwani katika jimbo la Gando.
  Fundo 1
  Wanafunzi wa shule ya Msingi Maskul Fundo, Jimbo la Gando kisiwani Pemba wakiwa wamepozi kwenye picha ya pamoja wakati wa hafla ya kukabidhiwa taa za nishati ya Umeme Jua zilizotolewa na Hoteli ya DoubleTree.  Ni muendelezo wa kampeni ya nishati ya mbadala
  .Lengo ni kusaidia wananchi kuelewa matumizi ya Umeme Jua ambao ni rafiki wa mazingira
  .Ni programu ya miaka miwili mashuleni

  Na Damas Makangale, Moblog
  Hoteli ya Double Tree by Hilton ya jijini Dar es Salaam imeendelea na kampeni zake kabambe ya matumizi ya nishati ya jua kwa kugawa taa 200 kwenye shule ya Msingi Maskul Fundo, Jimbo la Gando kisiwani Pemba, Moblog linaripoti.

  Akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ya kugawa taa hizo jana, Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Ndugu Said Ali Mbarouk ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Gando, amesema kwamba msaada huo wa Double Tree kwa shule hiyo ni kielelezo tosha kwamba sekta binafsi zina mchango mkubwa katika sekta ya elimu hapa nchini.

  “Napenda kuchukua fursa hii adhimu kuwashukuru uongozi na wafanyakazi wote wa Double Tree kwa msaada wao mkubwa kwa shule yetu ya hapa Gando ambapo watoto wetu watasoma katika mazingira rafiki yatayowawezesha kufaulu mitihani yao,’ alisema Mbarouk.

  Waziri Mbarouk amesema kwamba kutokana na mabadiliko ya tabia nchi Serikali, wananchi na wadau wote wa maendeleo hawawezi kuendelea kutegemea umeme wa vyanzo vya maji na badala yake umeme wa jua ambao ni nishati mbadala ni ufumbuzi wa tatizo la nishati nchini.

  Amesema mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi hasa kwenye nishati ni muhimu kwa sababu ni nishati ndio injini ya Uchumi wa taifa lolote lile hapa duniani kwa sasa. ‘lakini kampeni hizi zitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi kutambua na kuelewa nishati mbadala na umuhimu wake katika maisha ya kila siku ikiwemo mazingira,” alisisitiza Hoteli ya DoubleTree ilizindua rasmi kampeni ya matumizi ya nishati ya jua ambayo itadumu kwa muda wa miaka miwili katika shule za msingi nchi nzima miezi kadhaa iliyopita.

  DoubleTree itakuwa ikigawa taa 200 za mezani zenye kutumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa shule tofauti kila mwezi, lengo likiwa nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira kwa kupitia mafunzo katika madarasa yao.

older | 1 | .... | 258 | 259 | (Page 260) | 261 | 262 | .... | 3284 | newer