Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 259 | 260 | (Page 261) | 262 | 263 | .... | 3284 | newer

  0 0

                                                                     
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima wa Tanzania jijini San FranciscoMh.Ahmed Issa,(wapili kushoto) muda mfupi baada ya kufungua ofisi za ubalozi wa Tanzania jijini San Francisco nchini Marekani leo jioni.Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula na kulia ni mke wa balozi Ahmed Mama Sherry julin Issa.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi ofisi ya ubalozi wa heshima(Honorary Consulate) wa Tanzania jijini San Francisco nchini Marekani leo jioni.Kulia ni Balozi wa heshima wa Tanzania jijini San Francisco Mh.Ahmed Issa na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula na wapili kushoto ni Mke wa Balozi Mama Sherry Julin Issa.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio jijini San Francisco Marekani muda mfupi baadaya kufungua ubalozi wa heshima wa Tanzania na kuzungumza nao leo jioni.
   Rais Dkt.Jakaya MrishoKikwete akizungumza na baadhi ya Watanzania waishio jijini San Francisco Marekani leo jioni.Rais Kikwete yupo nchini Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine atahutubia kikao cha 68 cha Umoja wa Mataifa Jijini New York Marekani(picha na Freddy Maro).

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mbaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Iringa ameagiza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu utendaji wa vituo vya mizani mkoani Iringa. Agizo hilo lilitolewa katika mkutano ambao Waziri huyo wa Ujenzi alikutana na wafanyakazi wa taasisi zinazosimamiwa na Wizara ya Ujenzi mkoani humo.


  Meneja wa Tanroads wa mkoa wa Iringa Injinia Poul Lyakurwa alimtaarifu Waziri Magufuli kuwa kiasi cha Shilingi milioni 31.9 kilikusanywa katika kipindi hicho cha mwezi mmoja.


  Akishitushwa na kiwango hicho Waziri Magufuli  alibainisha kuwa, kiasi hicho kilichosomwa katika taarifa kimetokana na magari 735 yaliyokamatwa kati ya magari 20,700 yaliyopimwa sawa na asiliamia 3.5.

  “Takwimu hizi sizikubali kwani wastani wa magari yanayokamatwa katika nchi nzima unakaribia asiliamia 40 iweje barabara kuu kama hii iwe na kiwango kidogo kiasi hicho cha magari yaliyokutwa na makosa” hapa ni lazima pafanyike uchunguzi” alisisitiza Mheshimiwa Magufuli na kueleza kuwa hali hiyo hawezi kuiruhusu hata kidogo kuendelea.


  Katika hatua nyingine Waziri Magufuli amempongeza Meneja huyo wa Tanroads kwa kufukuza wafanyakazi 18 katika Kituo cha Mizani cha Makambako kwa kutokuwa waaminifu katika kazi zao. Waziri huyo wa Ujenzi aliendelea kubainisha kuwa, takriban asilimia 70 ya wafanyakazi waliokuwa katika vituo mbali mbali vya mizani ya barabara nchi nzima wamebadilishwa baada ya kukamilika kwa zoezi la kutangaza nafasi hizo upya.


  Akisisitiza zaidi, Waziri Magufuli alisema “Wizara ya Ujenzi itaendelea kushirikia na taasisi mbali mmbai zikiwemo PCCB, Jeshi la Polisi, TRA na hata kwa kutumia makondakta na wasaidizi katika magari ya usafirishaji ili kuendelea kubaini mbinu mbali mbali ambazo zinaendelea kutumika katika suala zima la vitendo vya rushwa katika vituo vya mizani hapa nchini”.


  Kwa upande mwingine Wakala wa Majengo Nchini pamoja na Wakala wa Ufundi na Umeme wametakiwa kuwa wabunifu ili waweze kukabiliana kikamilifu na changamoto mbali mbali zinazowakabili.

  0 0


  Baadhi ya raia wa Nigeria wanaodaiwa kutunzwa na  Mwinjilisti mwanamke  mwenye kibali cha kazi hiyo, Blessing  Dangana katika huduma ya Life Changer  Chapel iliyoko Sinza  jijini Dares Salaam, wakitoka  nje ya Mahakama ya  Hakimu Mkazi ya Kisutu mara baada ya kufikishwa mahakamani hapo huku wengine wa kijificha sura zao.Picha zote na Magreth Kinabo- Maelezo
  Mwinjilisti  mwanamke  kutoka nchini Nigeria ambaye ana kibali cha kazi ya uinjilisti  katika huduma ya Life Changer  Chapel  iliyoko Sinza  jijini Dares Salaam, Blessing  Dangana, anayedaiwa kuwatunza raia wa Nigeria watano ambao wanatoa huduma hiyo bila kibali maalum akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu mara baada ya kufikishwa mahakamani hapo leo.

  Baadhi ya vijana wanaodai kuwa wanatoka mkoa wa Kigoma  wakiwa wajaza fomu  leo  ambao taarifa zao zinaendelea kuchunguzwa  kama  kweli ni Watanzania wakiwa katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dares Salaam.

  Gari la Idara ya Uhamiaji likiwa limebeba baadhi ya watuhumiwa hao mara baada ya kutoka mahakamani.
   NA MAGRETH KINABO 
  – MAELEZO

  OFISI  ya Uhamiaji mkoa wa Dares Salaam imemfikisha mahakamani Mtanzania anayedaiwa kuwatunza raia watano kutoka   Nigeria  wanaoishi nchini bila kibali halali baada ya kuwapiga na kuwazuia kufanya kazi maofisa wa uhamiaji kwenye ofisi za Serikali.

   Hayo yalisemwa leo na  Ofisa wa Uhamiaji wa Mkoa wa Dares Salaam, Grace  Hokororo wakati akizungumza na mwandishi wa Idara ya Habari –MAELEZO   ofisini kwake ambapo alisema Mtanzania huyo alifikishwa leo(jana) katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu baada ya kutenda kosa hilo jana majira ya saa 1:00 jioni.
   Alimtaja Mtanzania huyo kuwa ni Christopher Kanyala mwenye umri unaokadiriwa kuwa kati miaka 29 hadi 34 mkazi wa Sinza na anadaiwa kuwa aliwaHI kutumikia Jeshi la Polisi nchini, ambapo kesi yake na raia hao watano wa Nigeria itatajwa kesho katika mahakama hiyo.
  Akizungumzia kuhusu suala hilo , Grace aliwataka wananchi   wasipende kuishi na raia ambao ni wageni na hawajaripoti katika ofisi za uhamiaji kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria. Huku akiwataka raia wa kigeni kuripoti katika ofisi hizo mara baada ya kuwasili nchini  ili waweze kufuata  taratibu za kisheria.
  Aidha  alisema  operesheni ya kuwakamata wahamiaji haramu inaendelea vizuri.  Grace alisema kwa upande wa wahamiaji haramu kutoka Malawi walijitokeza kwa hiari mpaka leo mchana idadi yao imefikia 1,863 tangu zoezi hilo lilipoanza.
  Aliongeza kuwa opresheni hiyo imehusisha mataifa 31 ambapo alitaja baadhi yake kuwa ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda,Italia, Singapore Ethiopia,Libya Yemeni,Somalia,Komoro, Ujerumani, Afrika Kusini,Uturuki, Nigeria, Cameroon,Liberia na Bokinafaso., Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo(DRC) na India.

   Alisema jumla ya raia hao wa mataifa mengine waliokamatwa ni 502.

  0 0
 • 09/17/13--11:02: IN LOVING MEMORY
 • In loving memory of our dearest Elder Joseph Shem Onyango who passed away September 17th, 2010. If years could build stairway, and memories a lane, we would walk right up to heaven, to bring you home again. We all miss you so much and the world has lost a truly remarkable individual thank you for touching so many hearts in so many ways.


  God bless.


  0 0
 • 09/17/13--11:59: KINANA AKOMAA NA MAWAZIRI
  • Sasa kuongozana na Mawaziri mguu kwa mguu
  • Asema kazi yake ya kuijenga chama inahitaji watu makini kama mtu hawezi kasi yake awapishe.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikaribishwa kwa kahawa katika kijiji cha  Budalabujiga wilaya ya Itilima mkoani Simiyu ambapo Katibu Mkuu alifanya ziara ya siku moja wilayani hapo.
    Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikaribishwa kwa kahawa katika kijiji cha  Budalabujiga wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Katibu wa Itikadi na Uenezi ameongozana na Katibu Mkuu wa CCM katika ziara ya mkoa wa Simiyu.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akipata maelezo wakati akikagua Bwalo la chakula la shule ya sekondari ya kata ya Kanadi, wilayani Itilima mkoa wa Simiyu.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya kata ya Kanadi baada ya kutembelea bwalo na bweni la shule hiyo ambapo aliwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii na kuahidi kuwapatia sola.
   Katibu Mkuu wa CCM akiwa amembeba mtoto Dhahabu katika kituo cha afya cha Nangale wilaya ya Itimila mkoani Simiyu.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZIDI

  0 0

  Madubi Marcely afisa Mradi wa kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko kwa mazao ya horticulture-Morogoro kutoka iWASH akinena na washiriki wa Warsha hiyo. Kushoto ni Isaac Ndamanhyilu Mtaalamu wa masuala ya kilimo cha mazao ya Horticulture kutoka TAHA na kulia ni George Mhina Afisa kilimo na mifugo wa wilaya ya Mvomero, Morogoro.
  Washiriki wakimsikiliza Ndugu Isaac Ndamanhyilu wakati wa Warsha hiyo.
  Anani Bansimbile Afisa mradi wa kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko kwa mazao ya horticulture-Morogoro kutoka TAHA-Morogoro akichagiza neno wakati wa mjadala kwenye Warsha iliyofanyika ukumbi wa Gwami Executive Hotel, Morogoro.
  Washiriki wa Warsha wakiwa ukimbini
  Bi. Cyrila Mlay, Afisa masoko kutoka TAHA akizungumzia juu umuhimu wa masuala ya uzalishaji wa mazao ya horticulture kwa kuzingatia mahitaji ya Masoko.
  Mandhari ya Mji wa Morogoro eneo la Msamvu ambapo Warsha inafanyika 
  Tanzania Horticultural Association (TAHA) yenye makao makuu yake Arusha na ofisi ndogo Mkoa wa Morogoro leo imefanya Warsha ambayo imelenga Kuwaleta pamoja Wadau wa mazao ya horticulture hasa Wakulima (Wazalishaji) na Wanunuzi (Soko) ili kuainisha changamoto zinazowakabili na hatimaye kuwaunganisha pamoja ili waweze kufanya biashara pamoja.

  0 0

  Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa, akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa duka la huduma kwa wateja la Vodacom lililoko Msimbazi kariakoo jijini Dar es Salaam. Pamoja nae katika picha ni Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh kulia na Mkurugenzi wa Planetell David Hayes. Hilo ni duka la 70 la kampuni hiyo nchini.
  Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh, akimfafanulia jambo Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kuhusu mfumo wa uhifadhi wa taarifa za M-pesa zinazowahusu wateja wakati Meya akiangalia huduma mbalimbali zinazotolewa kwenye duka jipya la Vodacom Msimbazi mara baada ya kulizindua.Wengine pichani ni Meneja wa duka hilo Josephine Swai na Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa Vodacom .
  Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (kulia), akisalimiana na Mkurugenzi wa Pantell David Hayes wakati akiwasili kwa ajili ya ufunguzi wa Duka jipya la Vodacom lililoko Msimbazi kariakoo jijini Dar es Salaam, Wanaoshuhudia wa kwanza kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa kampuni hiyo Upendo Richard, Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh na Meneja uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
  Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mfanyakazi wa wa duka jipya la Vodacom Msimbazi namna huduma zinavyotolewa kwa wateja wa kampuni hiyo. Wa kwanza kulia ni Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh. Meya Silaa alilizundua rasmi duka hilo.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya WaziriMkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. William V. Lukuvi (MB)akipokea maelezo kutoka kwa Meneja Mkuu wa Kituo cha Mpanda Bw. Nahoda Khatib (wakatikati)wakati wa Ziara yake kikazi katika Mkoa wa Katavi iliyoanza jana tarehe 16 Septemba,2013. Kushoto (mwenyetai) ni Bw. C. Sadda Meneja Usafirishaji Kanda ya Tabora.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. William V. Lukuvi (MB) akikagua Soko la Kimatifa la Mahindi la Isunta katika Wilaya ya Nkasi akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea sehemu za Ununuzi na Uhifadhi Mahindi nchini. Katika ziara hiyo Waziri Lukuvi amewaagiza Wakala wa Hifadhi ya Chakula NFRA pamoja na TRL kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kuanza kusafirisha Mahindi mapema kuelekea Shinyaga kabla ya kuanza kwa mvua ili kuweza kupunguza gharama za usafirishaji katika kipindi hicho, alisema hayo tarehe 17 Septemba, 2013. Habari Picha na Afisa Habari Ofis ya Waziri Mkuu

  0 0

  AMRI YA RAIS JK KUHUSU WAHAMIAJI HARAMU !

  Wananchi washirikishwe katika kuwafichua wahamiaji haramu na kuwa ripoti katika vyombo vya dola !

  Katika kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete kuwataka wahamiaji wote haramu waondoke nchini,kuna haja kubwa ya wananchi kushirikiana vyombo vya dola katika kuwafichua wahamiaji hao haramu ,kwa kuwashirikisha wananchi kazi ya kusafisha maovu na uvunjwaji wa amani unasababishwa na wahamiaji hao itafanikiwa kwa kasi kubwa.

  Kama vyombo vya dola vitawashirikisha wananchi na viongozi wa mashina katika serikali za mitaa zoezi hili litafanikiwa kwa haraka sana.

  Mkuu wa nchi ambaye ndiye amri jeshi mkuu mwenye majukumu makubwa nchini Rais Dkt.JK kuanzia mwezi Julai 2013 alitoa agizo la siku 14 kwa wahamiaji wote haramu kuondoka nchini au kujisalimisha kwa vyombo vya dola,lakini hadi sasa wahamiaji walioondoka ni wachache na wengi wao bado wanajifaragua mitaani huku vyombo vya dola vikiwatazama.

  Kwanini ? agizo hili la Rais JK lisiliwashirikishe wananchi,madiwani,wakuu wa mikoa na wilaya,wenyeviti wa serikali za mitaa . kazi ifanyike kwa haraka. Mungu Ibariki Tanzania Mungu mbariki Rais JK

  0 0

  BILA STEPS INAWEZEKANA

  Kwa muda mrefu nimekuwa nikiulizwa sababu ya kuamua kusambaza filamu zangu mwenyewe badala ya kuzipeleka kwa wasambazaji ambao nilikuwa nikifanya nao kazi kwa muda mrefu, yaani kampuni ya Steps Entertainment. 

  Najua maswali yamekuwa mengi kwa kuwa kuna watayarishaji wengi wa filamu nchini wanaohangaika usiku na mchana ili kupata mkataba wa kufanya kazi chini ya kampuni hiyo kwa kuwa Steps Entertainment ndiyo kampuni ya usambazaji inayolipa vizuri zaidi kuliko makampuni mengine yote kwa sasa. 

  Leo nimeamua kuongea walau kidogo …….

  “Kwanza nikiri kuwa maneno ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, mhesimiwa Dr. Jakaya Kikwete aliyotamka siku aliyoiita Ikulu kamati ya mazishi ya marehemu Steven Kanumba ndiyo yamekuwa yakinisukuma sana hadi kufikia uamuzi huu mzito.

  Kati ya waliounda kamati hiyo iliyoitwa Ikulu, mimi nilikuwa katibu, Mwenyekiti alikuwa Gabriel Mtitu au maarufu kama Mtitu Game, pia kulikuwa na wajumbe wengine kama Ruge Mutahaba, Asha Baraka, Jacob Steven ‘JB’ na Mzee Chilo. Baada ya kuongea mengi kuhusiana na msiba wa Kanumba na mazishi yake, mheshimiwa rais aliuliza ‘Hivi marehemu Kanumba kaacha filamu ngapi?”

  Kwa aibu tulimjibu mheshimiwa rais kuwa marehemu Kanumba hajaacha hata filamu moja, zote ni za msambazaji wake na hata mbili ambazo zilikuwa hazijatoka yaani ‘Ndoa yangu’ na ‘Love & Power’ tayari zilikuwa ni za msambazaji kutokana na aina ya mkataba tunayoingia na msambazaji.

  Mheshimiwa Rais alisikitika sana, akatuambia kuwa yeye hawezi kutumia nguvu kutukataza kuuza mali zetu lakini angependa kuona kuwa tunamiliki wenyewe filamu zetu na tutakapoona tumekwama tumwambie. Aliongeza kuwa kuuza haki zetu ni kama kuuza utu wetu. Maneno ya mheshimiwa Rais yalinichoma sana.

  Mimi ni msanii wa kwanza kufanya kazi na kampuni hiyo kama mtayarishaji wa filamu na filamu yao ya kwanza kuisambaza ilikuwa ni ‘Jeraha la Ndoa’ ambayo niliitengeneza mimi. Na kwa kuthibitisha hilo, mwaka huu kampuni hiyo ya Steps ilitoa tuzo ya heshima kwa kampuni yangu ya 5 Effects Movies Ltd kwa ajili hiyo.

  Nasikitika kukiri kuwa filamu zote ambazo nilizitengeneza kisha zikasambazwa na kampuni ya Steps, siyo zangu tena. Kampuni hiyo imekuwa ikinunua haki zote za filamu wanazopelekewa kwa ajili ya kuzisambaza kwa hiyo baada tu ya kusaini mkataba wao unakuwa huwezi kufaidika tena na chochote kutokana na mauzo au faida nyingine zinazotokana na filamu yako. 

  Kwa aina ya mikataba ambayo wasanii na watayarishaji tunaingia na kampuni ya Steps Entertainment, sisi tumekuwa ni wasimamizi tu wafilamu za zao, yaani ni kama manyapara kwenye mashamba ya mkonge wakati kwa ukoloni. Ni waajiriwa tusio na mafao ya uzeeni.

  Kwa taarifa tu ni kwamba filamu zote mnazoziona mitaani zikisambazwa na kampuni siyo za hayo makampuni yanayotajwa kutengeneza filamu hizo bali ni filamu za Steps Entertainment. Ndiyo maana hata ukienda kwenye Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) utakuta wasanii wakubwa hawamiliki kabisa filamu lakini kampuni ya Steps inamiliki filamu zaidi ya 400.

  Kifupi ni kuwa hadithi ni zetu, sehemu za kuigizia ni zetu, tunaigiza sisi, tunarekodi na kuhariri sisi lakini filamu ni za Steps Entertainment na ndiyo maana hata kampuni ya marehemu Steven Kanumba ‘Kanumba the Great’ imesambaratika baada ya kifo chake na mama yake akikabiliana na ugumu wa maisha lakini filamu za Kanumba bado zinatesa kwenye soko la filamu ndani na nje ya nchi.

  Nawashangaa watu wanaomshutumu mama mzazi wa Kanumba kuwa amemaliza mali za mwanae na sasa anaishi kwa kufadhiliwa na Lulu, wangejua kilicho nyuma ya pazia wangemuonea huruma badala ya kumshutumu. Wakati Steps wanakiri kuwa filamu iliyowahi kuuza sana katika historia ya kampuni yao ni ‘Ndoa yangu’ ya Kanumba, hawasemi kuwa familia yake imenufaika vipi zaidi ya kupewa tuzo.

  Pamoja na kununua haki zote za filamu, kampuni ya Steps hawatoi malipo ya filamu wanazozinunua kwa muda muafaka hivyo kutufanya tuendelee kuwa mafukara siku hadi siku. Hii ni sababu ya pili ya mimi kujitoa Steps, sitaki familia yangu ije kudhalilika baada ya kifo changu.

  Fikiria unapeleka filamu yako Steps, mnaingia mkataba wa kuuziana, lakini hawakulipi mpaka wakati watakapoamua kuiingiza sokoni hivyo hata wakikaa mwaka bila kuiingiza utakaa mwaka mzima unasuburi pesa. Hivi kweli mwaka huo utakuwa unakula nini kama umeamua kuifanya sanaa kuwa kazi yako?

  Cha kuchekesha hata wanapoamua kuiingiza sokoni hawakulipi mpaka baada ya wiki mbili au tatu baada ya filamu yako kuwa imeingia sokoni, utasema hapo wamekulipa au umejilipa mwenyewe baada ya kuwa imenunuliwa?

  Mfano mwingine hai ni wa marehemu Said Juma Kilowoko (Sajuki) ambaye ni miongoni mwa wasanii maarufu na watayarishaji wa filamu. Marehemu Sajuki alilazimika kuzunguka na wasanii wenziye mikoani akiwa anamuwa taabani ili tu aweze kupata fedha za matibabu jambo ambalo naamini lilimzidishia matatizo ya kiafya.

  Na kutokana na kuuza haki zetu zote ilibidi mkewe Sajuki, Wastara atengeneze ‘Mr & Mrs Sajuki’ ili aweze kupata fedha za kujikimu na kurekebisha mambo mbalimbali yaliyovurugika wakati akimuuguza mumewe. Kama tungekuwa hatulazimiki kuuza haki zetu zote, familia hiyo ingeweza japo kupeleka filamu zake kwenye vituo vya runinga barani Afrika ambako ni chanzo kingine cha mapato kwa msanii.

  Baada ya kutafakari kwa kina niliamua kulipia leseni ya usambazaji wa filamu kupitia kampuni yangu ya 5 Effects Movies Ltd ili niwe nasambaza filamu zangu nikitegemewa kupata sapoti kubwa kutoka kwa wasanii wenzangu hasa mastaa wakubwa lakini imekuwa kinyume chake. Kwa sasa naonekana adui mbele ya wenzangu.

  Kupitia kampuni yangu ya 5 Effects Movies Ltd, niliingiza sokoni filamu ya ‘Omega the Confusion’, na ndani ya masaa matano ya kwanza nilifanikiwa kurudisha gharama zangu zote na kupata faida kidogo. Toka hapo hadi sasa inaendelea kukimbia sokoni hivyo natengeneza faida tu na bado filamu ni yangu, naweza kuifanyia chochote kama kuipeleka kwenye runinga za kimataifa n.k

  Nimalizie kwa kuweka wazi kuwa sina ugomvi wowote na kampuni ya Steps, mmiliki wake wala mtumishi yeyote wa kampuni hiyo. Pia sina chuki na yeyote kati ya wanaoendelea kufanya kazi chini ya kampuni hiyo. Kikubwa ni kuwa haya ni maisha na kila mmoja ana mtazamo wake katika kuyakabili na kujiletea mafanikio”.

  “WOGA WAKO NDIO UMASKINI WAKO”
  ‘TEAM NYATI’

  0 0

   Mmoja wa Waanzilishi wa Mtandao wa Kijamii wa Jamii Forums,Mike Mushi akiwasilisha Mada juu ya namna ya Uendeshaji wa Mitandao ya Kijamii na namna Mtandao wao wa Jamii Forums unavyoendeshwa wakati wa Warsha ya Siku mbili kwa Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii (Bloggers) hapa nchini uliomalizika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Sinza B jijini Dar es Salaam.
  Mmiliki Mwenza kwa Mtandao wa Kijamii wa Jamii Forums,Maxcence Mello akifafanua jambo juu ya namna ya Uendeshaji wa Mitandao ya Kijamii na namna Mtandao wao wa Jamii Forums unavyoendeshwa wakati wa Warsha ya Siku mbili kwa Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii (Bloggers) hapa nchini iliyomalizika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Sinza B jijini Dar es Salaam.
  Mhadhili wa Maswala ya Habari kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Ndg. Doto Kuhenga akiwasilisha Mada yake ya kuhusu Mwenendo na Utaalam unaopaswa kufuatwa na Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii pindi wafikishapo habari kwa jamii,wakati wa Warsha ya Siku mbili kwa Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii (Bloggers) hapa nchini iliyomalizika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Sinza B jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa Viwango na Kanuni za Uandishi wa Habari kutoka Baraza la Habari Tanzania,Mama Pili Mtambalike akiwasilisha mada yake wakati wa Warsha ya Siku mbili kwa Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii (Bloggers) hapa nchini iliyomalizika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Sinza B jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA), Prof. John Nkoma akizungumza jambo wakati wa kufunga Warsha ya Siku mbili kwa Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii (Bloggers) hapa nchini iliyomalizika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Sinza B jijini Dar es Salaam.
  Mmiliki wa Mtandao wa Bongo Celebrity,Jeff Msangi akitoa shukrani kwa niaba ya Waendezaji wa Mitandao ya Kijamii waliokuwepo kwenye Warsha ya Siku mbili kwa Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii (Bloggers) hapa nchini uliomalizika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Sinza B jijini Dar es Salaam.
  Meneja Mahusiano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Inocent Mungy akieleza jambo wakati wa Warsha hiyo.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Tech Wark,Liz Wachura akitoa Mada yake kwenye Warsha ya Siku mbili kwa Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii (Bloggers) hapa nchini uliomalizika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Sinza B jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Kikosi cha Tanzania
  mchezaji wa timu ya Ghana, Michael Owusu akimkabili mchezaji wa timu ya Tanznia wakati timu hizo zilipochuana vikali katika michuano ya Afrika ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja a Onika Lagos Nigeria
  Mchezaji kiungo wa timu ya Tanania George Emmanuel akikabiliwa na mchezaji wa timu ya Ghana wakati nchi hizo zilipopambana vikali katika mechi za michuano ya Afrika ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja a Onika Lagos Nigeria Ghana ilishinda 2 - 1.

  Jumanne September 17 2013.. Tanzania imeanza vibaya mashindano ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars baada ya leo kukubali kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Ghana. Mechi ya wasichana inatarajiwa kupigwa baadae leo ambapo watakutana na Sierra-Leone.

  Mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yanafanyika kwa mara ya pili, kwa mara ya kwanza yalifanyika nchini Nairobi na Niger kuibuka mabingwa , lengo la mashindano haya ni kuzalisha vipaji vingi vya timu za taifa barani Afrika. Katika mechi ya leo , Tanzania ilikua ya kwanza kupata goli katika dakika ya 26 kupitia kwa mshambuliaji hatari Athanas Mdam baada ya kuwapiga chenga mabeki wa Ghana.

  Ghana walifanya shambulizi la hatari na kupata goli la kusawazisha katika dakika ya 30 kupitia kwa Prince Agyeman baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Tanzania na kuachia shuti kali lilimzidi mlinda mlango wa Tanzania.

  Juhudi za Tanzania kupata goli la pili hazikuzaa matunda , dakika ya 45 kipindi cha kwanza Ghana waliongeza bao la kuongoza na lililodumu mpaka kipyenga cha mwisho kupitia kwa Godfrey Nyarko baada ushirikiano mzuri wa washambuliaji wa Ghana.

  Timu ya wavulana ambayo ipo kwenye kundi D pamoja na Ghana , Zambia , Sierra-Leone itacheza mechi ya pili dhidi ya Zambia jumatano sembemba 18 , watamaliza na Sierra –Leone katika mchezo wa mwisho wa makundi.

  Timu ya wasichana , baada ya kucheza na Sierra –Leone watakutana na Uganda jumatano , Septemba 18 kabla ya kukutana na Malawi siku ya Alhamisi , September 19. Mashindano yanaingia hatua ya mtoano ijumaa na fainali itapigwa jumapili , Septemba 22.

  0 0

  Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na Mshauri wa Rais wa Bunge la Ulaya Bwana Alexandre Stutzman (kulia) na Bwana Marc Jutten (kushoto) Mshauri wa Sera za Nje wa Rais wa Bunge la Ulaya. Balozi Kamala amekutana na Bwana Stutzman leo Ofisini kwake Brussels kushauriana naye kuhusu masuala mbalimbali ya majukumu ya Bunge la Ulaya.

  0 0

  The writer Leila Sheikh (in black) is a Senior Journalist; producer of documentaries and Social Justice Defender.


  By Leila Sheikh  1.     After her second baby was born Eileen was advised by her doctor to undergo Voluntary Counselling and Testing for HIV (VCT).  She did and was found to be HIV positive.  When she gave the results of the test to her husband, he hit her and hurt her badly and she was taken to hospital for treatment where they refused to treat her without a Police Form (PF3).

   At the Police Station she showed them the results of her HIV test and the two Police Officers told her “You are lucky he did not kill you”.

   By then E was contemplating suicide.  It was her sister’s friend who knew a woman who knew an activist for PLHIV (People Living with HIV/AIDS) Rights, who arranged a meeting between E and the activist.


  0 0

  Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Bw. Koenraad Adam akizindua programu ya utawala bora na ujasiriamali kupitia tafiti, elimu na teknolojia iliyofanyika Chuo Kikuu Mzumbe jana. Wengine ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Taaluma, prof. Josephat Itika na baadhi ya washiriki katika hafla hiyo.
  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Taaluma, Prof. Josephat Itika (katikati) akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa programu za utawala bora na ujasiriamali kupitia tafiti, elimu na teknolojia iliyofanyika chuoni hapo jana. Wengine katika picha ni Prof. Auleria Kamuzora (wa kwanza kushoto), Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Morogoro, Bw.Noel Kazimoto (wa pili kushoto) na Balozi wa Ubelgiji Nchini, Bw. Koenraad Adam.
  Balozi wa Ubelgiji nchini, Bw. Koenraad Adam akisisitiza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa programu za utawala bora na ujasiriamali kupitia tafiti, elimu na teknolojia Chuo Kikuu Mzumbe jana. Wengine ni Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Morogoro, Bw. Noel Kazimoto (kushoto), Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Taaluma, Prof Josephat Itika na Prof. Auleria Kamuzora (kulia).

  0 0

  Na Hassan Silayo na Fatma Salum , MAELEZO

  Tanzania inatarajia kuwa mmoja wa wazalishaji wakubwa wa chuma barani Afrika kwa kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka pindi uzalishaji wa madini hayo utakapoanza mwaka 2018/19 katika eneo la Liganga wilayani Ludewa.

  Hayo yamebainishwa na Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Abel Ngapemba wakati akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo.

  Alisema mradi huo wa uzalishaji chuma utakaotekelezwa chini ya kampuni ya Tanzania China Mineral Resources Limited (TCIMRL), ambayo ni kampuni ya ubia kati ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na Shirika la Sichuan Hongda Group (SHG) ya China utaenda sambamba na uzalishaji wa madini ya Titanium na Vanadium.

  “Mradi huo ukikamilika tutaweza kuzalisha tani milioni 219 za chuma ambazo zitadumu kwa zaidi ya miaka 70, na madini mengine yatakayotokana na mgodi huo ni Titanium tani 175,400 kwa mwaka na Vanadium tani 5,000 kwa mwaka”. Alisema Ngapemba.

  Aidha Ngapemba alisema kuwa uzalishaji huo utaiwezesha Tanzania kushika nafasi ya nne ikizifuatia nchi za Afrika Kusini inayozalisha bidhaa za chuma tani milioni 8.5 kwa mwaka, Misri tani milioni 8.0 na Libya tani milioni 2.0 kwa mwaka.

  Mradi huu ni moja ya miradi miwili iliyopo katika mkataba kati ya NDC na SHG uliotiwa saini Septemba 21, 2011 ya uanzishwaji wa mgodi wa makaa ya mawe na ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa megawati 600 katika eneo la Mchuchuma.

   Miradi  mingine ni pamoja na ujenzi wa  msongo wa umeme wa kilovoti 220 kati ya Mchumchuma na Liganga, na uanzishwaji wa mgodi wa chuma pamoja na  ujenzi wa kiwanda cha kuchenjua chuma , kiwanda cha kuzalisha bidhaa za chuma na ujenzi wa barabara kati ya Mchuchuma na Liganga.

  Chuma kinachozalishwa duniani ni takribani tani bilioni 1.55 kwa mwaka, mzalishaji mkubwa ikiwa ni China inayotoa tani milioni 711 kwa mwaka ambayo ni sawa na asilimia 46 ya chuma chote kinachozalishwa duniani.
  Miradi hii itakayogharimu Dola za Kimarekani bilioni 3 inatarajiwa kuliingizia Taifa mapato ya Dola bilioni 1.7 kwa mwaka itakapoanza uzalishaji wake.  

  0 0

   Rais Dkt Jakaya Kiwete  akiingia Ritz Calton Hotel wakati alipowasili Washington, DC kwa kuendelea na ziara yake ya nchini Marekani aliyoanzia kwenye miji ya San Francisco na Vallejo, California.
   Rais Dkt Jakaya Kiwete akisalimiana na Mwambata mpya wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Kanali Adolph Mutta ambaye anachukua nafasi ya Brigedia Jenarali Emamanuel Maganga ambaye amemaliza muda wake.
   Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Afisa Ubalozi Emmanuel Swere kwenye hotel ya Ritz Calton wakati alipowasili Washington, DC.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Leo Siku ya kuzaliwa mwanamuziki Kamanda Ras Makunja,kiongozi wa Ngoma Africa band a.k.a FFU yenye maskani kule Ujerumani.
  Siku kama ya leo 19.September wazazi wawili Bi.Moza Hassan Mpili (Mama) na Mumewe marehemu Bw.Jumanne Saleh Makunja(Baba) walijaaliwa kupata mtoto wao Ebrahim Jumanne Makunja a.k.a Kamanda Ras Makunja wa FFU.
  Tunamtakia kila la heri Kamanda Ras Makunja katika siku yake ya kuzaliwa. Happy Birthday To You Kamanda Ras Makunja
  Pata burudani at   www.ngoma-africa.com 

  0 0

   Nshoma Hostel ni Hostel mpya Kabisa na ya kisasa iliyofunguliwa hivi karibuni huko Gongo la Mboto,Jijini Dar es Salaam katika barabara ya Kuelekea Moshi Bar.ni Hostel yenye uwezo mkubwa wa kuchukua wanafunzi wengi kwa wakati mmoja.Hostel hii ipo karibu kabisa na Chuo Kikuu cha Kiataifa cha Kampala kilichopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

  Kwa wale wahitaji wa Hostel
  Mawasiliano ni haya hapa chini
  +255 717 140 095 au +255 769 074 201 
  Pia wanaweza kuwasiliana na Mkurugenzi Mkuu wa Hostel hiyo kwa namba hizi
  +255 754 595 901 au +255 784 495 901

  Nyote mnakaribishwa.

   Sehemu ya Upande wa Hostel hiyo.
   Sehemu ya Mapokezi.
   Muonekano wa Baadhi ya Vyumba vya Hostel hiyo,vyote vikiwa ni self Contain. 


  0 0
 • 09/18/13--23:05: Article 14


older | 1 | .... | 259 | 260 | (Page 261) | 262 | 263 | .... | 3284 | newer