Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

KINANA AITEMBELEA FAMILIA ILIYOUNGULIWA NA NYUMBA SHINYANGA MJINI

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa pole Nassoro Rashid Tinde mmiliki wa duka la vipuri vya magari Tinde Store lililotekea kwa moto jana usiku,Shinyanga.
 Katibu Mokuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia jinsi moto ulivyoteketeza  Duka la Tinde Store  lililopo mtaa wa Nkurumah ,Shinyanga mjini kushoto ni mmiliki wa duka hilo Rashid Nassoro.
 Seif Ally akionyesha namna duka lilivyoteketea.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapa pole majirani waliomsaidia Ndugu Nassoro Rashid kuzima moto uliounguza Duka la Vipuri vya magari pamoja na nyumba.


maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka jijini dar es salaam kama inavyoonekana leo septemba 14, 2013

MTEMVU AKABIDHI MSAADA WA MAGODORO 30 HOSPITALI YA TEMEKE

$
0
0
 Mbunge wa temeke  Abbas Mtemvu akikabidhi kwa Lucy Sozigwa ambae ni katibu wa hospitali ya temeke  moja ya magodoro 30 yaliotolewa na kikundi cha akina mama wa  Neema Woman's Power (NWP).
 Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akisalimiana na Mgeni Otto  katibu wa kikundi cha Neema Woman's Power(NWP) mara alipowasili katika hospitali ya Temeke.
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akisalimiana na Moshi Ndungu ,mjumbe halmashauri tawi la Azimio.

Mbunge wa Temeke  Abbas Mtemvu akikabidhiwa magodoro 30 na Maryam Dedes ambae ni mwenyekiti wa kikundi cha Neema Woman's Power (NWP)

Naibu Waziri wa Fedha,Mhe. Saada Mkuya afungua mkutano wa kikao kazi kwa wafanyakazi wa Wizara ya Fedha,Mjini Bagamoyo leo

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha ,Mhe. Saada Salum Mkuya akifungua mkutano wa kikao kazi unaofanyika hapa mjini Bagamoyo kwa muda wa siku mbili. Kikao kazi hicho kitakuwa na jukumu kubwa la kujadili ripoti ya kutathmini utendaji kazi wa mfumo wa usimamizi wa fedha za umma ambayo imeshakamilika( PEFA Report). Lengo kubwa la kikao hicho ni kutafuta ufumbuzi wa matatizo ambayo yamebainishwa katika ripoti hiyo. Kikao hicho kitawashirikisha washirika wa maendeleo pamoja Wizara ya fedha yenyewe.
Janne Rajpar mwenyekiti mwenza kwa upande wa wahisani katika kusimamia matumizi ya fedha za umma kutoka ujerumani.
Juma Salumu Maguru Mkurugenzi Msadizi idara ya Mipango Wizara ya fedha akitoa utangulizi kwa washiriki wa kikao hicho, hawapo kwenye picha.

Kutoka kushoto ni Bi Ingiahedi Mduma ,ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano serikalini, wakatikati ni Bi. Hannah Mwakalinga kutoka PPRA ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za kiushirikiano na wakushoto kwake ni Bw. Malima Nkilijiwando ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Mipango kutoka Kwa Mkaguzi mkuu wa Mahesabu, wakisikiliza kwa makini mada na maoni yaliyokuwa yakitolewa katika mkutano huo.
Wa kwanza kushoto ni Bw. Sebastian Ndandala ambaye ni Kaimu msimamizi wa mradi wa maboresho ya fedha za umma( PFMRP) kwa upande wa serikali na anayefuata ni Bi. Paddy Siyanga Knudsen ambaye ni msimamizi kwa upande wa Washirika wa maendeleo,wakisikiliza kwa makini mada na maoni yaliyokuwa yakitolewa katika kikao hicho.
Naibu Waziri wa Fedha ,Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Serikali ya Tanzania pamoja na Washirika wa maendeleo kutoka nchi Wahisani.

Ujenzi wa Barabara ya Kutoka Manyoni,Itigi mpaka Tabora waendelea

$
0
0
 Ujenzi wa Barabara ya Kutoka Manyoni,Itigi mpaka Tabora unaonekana kwenda kwa kasi nzuri kama inavyoonekana pichani.Barabara hiyo ina Urefu wa Kilometa 254 na iwapo itakamilika mapeka kama ilivyopangwa,itakuwa imerahisisha sana safari kwa watumiaji wa njia hiyo wakaokuwa wanakwenda Mkoani Tabora na maeneo mengine.
 Moja ya Katapila likiendelea na kazi ya Ujenzi katika Barabara hiyo.
 Mafundi wakiweka moja ya Madaraja katika barabara hiyo.
 Kifusi kikimwagwa.
 Sehemu ya Mkeka huo iliyokamilika,japo bado magari hayajaanza kuruhusiwa kutumia.

LIGI KUU VODACOM: KAGERA SUGAR NA AZAM NGOMA DROO 1-1

$
0
0
Waamuzi na timu makepteni wakijuzana kuhusu uelekeo wa kila timu
Timu ya Kagera Sugar ndiyo iliyotangulia kupata bao kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kupitia mchezaji Themi Felix Buhaja aliyefunga bao la kichwa baada ya kupigwa kona katika dakika ya 25 ya kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili dakika ya 55 Khamis Mcha ‘Vialli’ aliisawazishia  Azam FC bao na kufanya mpira kuisha kwa matokeo hayo hayo mpaka dakika 90 za mchezo. Kwa picha zaid na mdau Faustine Ruta 

Article 17

mh. lowassa alipozungumza na Machifu Mkoani Tabora


taswira maridhawa: TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD, DAR ES SALAAM

Ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya Mzee Fundi Konde ya 'Ajali' haichuji. Na hii ndiyo original yenyewe...ya mwaka 1950

Msanii wa Bongofleva Niki wa Pili akizungumza kwenye semina ya kamata fursa twendzetu Morogoro leo.

KILI MUSIC TOUR YAFUNIKA JIJINI DAR USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB,JIJINI DAR

$
0
0


JideJaydee na Mr Blue wakiimba "Wangu" katika Tamasha la Kili Music Tour lililofanyika Usiku wa Kuamkia leo Katika Viwanja Vya Leaders.


Si mwingine ni Roma Mkatoliki akiendeleza makamuzi katika Kili Music Tour Usiku wa Kuamkia leo katika Viwanja Vya Leaders ambapo Kili Music Tour ndio imehitimishwa jijini Dar Usiku wa Kuamkia leo


Recho katika jukwaa la Kili Music Tour Usiku wa Kuamkia leo katika Viwanja vya leaders akitoa burudani kwa wakazi wa Jiji la Dar na Vitongoji Vyake wakati wa Tamasha hilo lililofanyika katika Viwanja Vya leaders usiku wa kuamkia leo.

Article 11

$
0
0
SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD

AIR CARGO TO DAR NOW £3.80
INCLUSIVE CLEARANCE
STILL THE CHEAPEST AND SIMPLY THE BEST!
WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
KUCHUKUA MZIGO WAKO DAR ES SALAAM 
MPIGIE AGENT WETU DAR; TORNADO LUKOSI TEL; 0713607116
MZIGO UNANDOKA KILA IJUMAA

ONCE YOU PAY HERE IN UK YOU DONT PAY ANYTHING IN TANZANIA
UKIISHA LIPA UK UNAKWENDA KUCHUKUA ILALA DAR BILA KULIPA TENA

FLIGHTS EVERY WEEK

KWA WALE WANAOTAKA KUNUNUA VITU UK TUTUMIE EMAIL AU TUPIGIE
MINIMUM WEIGHT IS 40K HANDLING/ADMIN FEE £20
KABLA HUJATULETEA MZIGO HAKIKISHA UMEANDAA ORODHA YA VITU UNAVYOTAKA TUKUSAFIRISHIE NA NI LAZIMA TUUFUNGUE MZIGO NA KUHAKIKISHA UNACHOSAFIRISHA . KAMA HAUNA PACKING LIST HATUTASAFIRISHA MZIGO.
USITEGEMEE KUSAFIRISHA MBUZI HALAFU UPOKEE NG'OMBE!

40' CONTAINER TO DAR/MOMBASA NOW £1,800
SALOON CARS TO DAR 750
4X4 VEHICLES 850
OUR AGENT IN DAR; TORNADO TEL; +255 713607116

Tupigie kwa namba hizo hapo chini au  tutumie email tafadhali

HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477

TANZANIA YALITAKA GAZETI LA MALAWI NEWS KUOMBA RADHI KWA UPOTOSHAJI

$
0
0
Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene akitoa ufanunuzi kwa waandishi wa habari jana mjini Dar es salaam juu ya taarifa zilizochapishwa na gazeti la Malawi News kuwa Wamalawi waishio nchini Tanzania wanaogopa kutoka nje kutokana na ubaguzi wanaofanyiwa na Watanzania taarifa ambazo sio kweli.
Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene akiwaonyesha waandishi wa habari jana mjini Dar es salaam kichwa cha habari cha gazeti la “Malawi News” kinachosemeka “MALAWIANS FACE XENOPHOBIA IN TZ” ambacho kilichapishwa na gazeti hilo kuhusu madai ya kubaguliwa raia hao wa kutoka Malawi jambo ambalo sio kweli.

Na Benedict Liwenga-MAELEZO_Dar es salaam

SERIKALI ya Tanzania imekanusha taarifa zilizochapishwa na gazeti la nchini Malawi lijulikanalo kama “Malawi News” kuwa Wamalawi waishio nchini Tanzania wamekuwa wakiogopa kutoka nje kutokana na ubaguzi wanaofanyiwa na Watanzania.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene amesema kuwa taarifa hizo ni za kupotosha umma na kuleta chuki dhidi ya Tanzania na nchi jirani na hazina ukweli wowote ule.

Bw. Mwambene ameongeza kuwa hakuna raia yeyote wa kutoka Malawi aliyebakwa wala kunyanyaswa kwa namna moja ama nyingine.

“Hakuna mwananchi yoyote kutoka Malawi aliyebakwa , wala hakuna raia yoyote wa Malawi aliyepo hapa nchini anayeogopa kutoka nje kwa sababu ya ubaguzi wowote ” amesisitiza Mkurugenzi huyo.

Amesema kuwa licha Tanzania kuwakamata wahamiaji haramu 1030 kutoka Malawi, Serikali ya Tanzania iliwapa fomu ili kama walikuwa wanahitaji kuishi nchini wahalalishe uwepo wao hapa Tanzania kwa wale wote walionyesha nia ya kuendelea kuwepo hapa nchini .

Aidha wahamiaji wote haramu 1030 kutoka Malawi waliachiwa huru na wanaendelea kukamilisha taratibu za kuhalalisha uwepo nchini.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa mpaka sasa kati wahamiaji haramu 1030 hakuna aliyewekwa ndani ama kushikiliwa na vyombo vya dola kwa kosa la kuwepo kinyume.

Kufuatia taarifa hizo ,Mkurugenzi huyo amelitaka gazeti hilo kusahihisha taarifa hiyo na kuiomba radhi Tanzania kwa upotoshaji huo na kuongeza kuwa kauli hiyo ni sawa na matusi kwa Tanzania.

Aidha amesema kuwa hadi hivi sasa zaidi ya wahamiaji haramu 24,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokarisia ya Kongo (DRC) , Rwanda, Burundi , Uganda na Zambia wamerejeshwa makwao kwa kosa la kuishi Tanzania bila vibali.

KAMATA FURSA TWENDZETU KWA VIJANA IMEFANYIKA MKOANI MOROGORO LEO.

$
0
0
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mwansiti Almasi,akifafanua namna anavyonufaika na huduma za NSSF,mara tu walipojiunga kupitia kundi lao la Lekadutigite,ndani ya semina ya fursa twendzetu iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi.
 Mbunifu wa mavazi kutoka mkoani Morogoro,ambaye pia ni mjasiliamali aliyejitambulisha kwa jina la Diana Magessa akionesha mbele ya washiriki wa semina ya Fursa kwa Vijana (hawapo pichani) baadhi nguo zake alizozidizaini kwa ubunifu wake.

Meneja huduma wa Wajasiliamali-Zantel akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Morogoro waliojitokeza kwenye semina ya Kamata fursa twendzetu,kuhusiana na fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya kampuni hiyo,Semina hiyo iliofanyika ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi iliwakutanisha wadau mbalimbali.Semina ya kamata fursa twendzetu inaratabiwa na Clouds Media Group,ambapo kwa sasa imekwishafanyika ndani ya mikoa zaidi ya nane,ikiwemo Kigoma,Singida,Tabora,Dodoma,Mtwara,Mbeya,Morogoro pamoja na Iringa.
 Mkali wa kughani Mashairi,Mrisho Mpoto akizungumza na wakazi wa Morogoro waliojitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya fursa twendzetu ndani ya ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi.
 Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji, Ruge Mutahaba akifunga semina ya kamata Fursa twendzetu kwa vijana, iliyofanyika mapema leo mkoani Morogoro.

LOWASSA AFUNGUA JENGO LA MADARASA YA SHULE YA AWALI YA KANISA LA AICT MJINI KAHAMA LEO,ACHANGISHA ZAIDI YA MILIONI 200 ZA UJENZI

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe na kufungua pazia katika jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya Ufunguzi rasmi wa Jengo la Madarasa ya Shule ya awali ya Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini.ambapo baadae aliendesha Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa hilo ambapo zaidi ya shilingi Milioni 212 zilipatikana zikiwemo na ahadi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipanda Mti katika eneo la Kanisa hilo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono waumini wa Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini,wakati alipokuwa akiwasili kwenye kanisa hilo kwa ajili ya kuendesha Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Shule ya Msingi wa ya Kanisa hilo.

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOA MPYA SIMIYU, LEO YUKO MEATU

$
0
0

sikiliza fursa uzipatazo mara baada ya kujiunga na NSSF

TAARIFA TOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO

MAMA SALMA KIKWETE AONGEA NA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MSIMBU,KISARAWE

$
0
0
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Kisarawe hivi karibuni wakati alipowasili katika Shule ya Sekondari Msimbu iliyopo wilaya hiyo mkoani Pwani ili kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi.Fatuma Kimario .
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Msimbu iliyopo wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani wakati alipowatembelea hivi karibuni. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya kisarawe Fatuma Kimario,na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri Adam Ng’imba anayefuatiwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Zipporah Simwanza.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) akizungumza hivi karibuni na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Msimbu iliyopo wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani juu ya umuhimu wa elimu na athari za mimba za utotoni wakati alipowatembelea wanafunzi hao.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi.Fatuma Kimario akisisitiza jambo wakati Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipotembelea Shule ya Sekondari Msimbu na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo ambapo aliwaasa wapende shule na kuepukana na mambo mabaya kama vile mafataki na uvutaji bangi ili waweze kufikia malengo waliojiwekea,kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) anayefuatia ni Mwenyekiti wa Halmashauri Adam Ng’imba na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Kisarawe Bi.Tatu Kano.Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images