Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110149 articles
Browse latest View live

wachezaji watakaoshiriki miachuano ya Airtel Rising stars nchini Nigeria wakabidhiwa daruga

$
0
0

 Afisa uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde Akikabithi viatu vya kuchezea mpira kwa wachezaji watakaoshiriki miachuano ya Airtel Rising stars nchini Nigeria itakayoanza jumatatu wiki ijayo na kushirikisha nchi 17 barani Afrika, wakipokea vifaa hivyo ni makaptani wa  timu hizo  Athanas Mdam na Stumai  Athumani. wa pili kushoto ni kocha wa timu ya wavulana ya Airtel Rising Stars Abel Mtweve

 Afisa uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde Akikabithi viatu vya kuchezea mpira  kamptaini wa timu ya kike Stumai  Athumani wakati Airtel ilipogawa vifaa kwa timu itakayosafiri kwenda kwenye michuano ya Airtel Rising stars Nchini Nigeria, Michauno hiyo itashirikisha nchi 17 barani Afrika, wakishuhudia ni kikosi cha timu ya Airtel Rising stars Tanzania

 Baadhi ya wachezaji  watakaoshiriki miachuano ya Airtel Rising stars nchini Nigeria wakijaribu viatu mara baada ya kukabithiwa vifaa vya michezo na Airtel kwaajili ya  miachuano ya Airtel Rising stars nchini Nigeria itakayoanza jumatatu wiki ijayo na kushirikisha nchi 17 barani Afrika

Baadhi ya wachezaji  watakaoshiriki miachuano ya Airtel Rising stars nchini Nigeria wakijaribu viatu mara baada ya kukabithiwa vifaa vya michezo na Airtel kwaajili ya  miachuano ya Airtel Rising stars nchini Nigeria itakayoanza jumatatu wiki ijayo na kushirikisha nchi 17 barani Afrika


tamasha la kumuaga rasmi mwanamuziki mkongwe wa msondo ngoma muhidin maalim gurumo laandaliwa

$
0
0
MWANAMUZIKI mkongwe aliyestaafu muziki akiwa na bendi ya Msondo Ngoma, Muhidini Maalim Gurumo, ameandaliwa shoo mbili za kumuaga, moja wapo ikipangwa kufanyika Oktoba 11, ikiwa ni VIP, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. 
Shoo nyingine kwa wapenzi wote itafanyika Novemba Mosi mwaka huu katika Ukumbi wa TCC Sigara Chang’ombe, jijini Dar es Salaam, zote zikiwa na lengo la kumuaga kwa heshima mwanamuziki huyo na kumpa nafasi ya kuyamudu maisha yake baada ya kuachana na muziki. 
 Akizungumza leo na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa shoo hiyo iliyopewa jina la (Gurumo 53), Asha Baraka, alisema kuwa ni heshima kuwa na mwanamuziki kama Gurumo, hivyo wadau wameamua kuandaa shoo hizo za kumtafutia fedha mkali huyo. 
 Alisema wazo hilo limefanyiwa kazi kwa pamoja, akiwa na wadau kadhaa, akiwamo Said Mdoe Katibu wa Kamati hiyo, Richard Sakala mjumbe, Cosmas Chidumule, Waziri Ally, Said Kibiriti na Juma Mbizo, ambaye ndio mratibu wa Kamati hiyo. 
 ”Lengo si kumpa karatasi za kuthamini mchango wake katika tasnia ya muziki wa dansi Tanzania, ila kuhakikisha kuwa anapata mwangaza wa maisha yake baada ya kuachana na muziki. 
 ”Huyu ni mwanamuziki mwenye uwezo wa juu wakati huo, hivyo kwa sasa lazima sisi wadau tuhakikishe anajiweka katika ramani nzuri, ikiwa ni kutambua ataishi vipi nje ya muziki,” alisema. Naye Gurumo aliwaambia waandishi wa habari kuwa ameamua kuachana na muziki kwa sababu umri na afya yake hairuhusu kufanya kazi hiyo, hivyo asitokee mtu wa kupotosha ukweli wake huo. 
 ”Nasikia watu wanasema naachana na muziki Msondo nikiwa na lengo la kurudi tena Sikinde, jambo ambalo si kweli kwa kuwa sioni nitamuimbia nani wakati nimechoka. 
 ”Naomba kwa sasa kuwapa nafasi watu waliojitolea kunisaidia hasa kwa kuunda kamati hii ambayo nitapanda jukwaani kuimba mara ya mwisho, ukizingatia kuwa kazi yangu inahitaji kuagana na mashabiki wangu jukwaani na si mahali pengine,” alisema. 
 Katika hatua nyingine, mwanamuziki Cosmas Chidumule, alisema kuwa licha ya kuwa ameokoka, ila atapanda jukwaani kuimba na mzee Gurumo kama sehemu ya kutambua mchango wake. ”Nimeokoka lakini si sababu ya kunifanya nishindwe kumheshimu mwanamuziki ambaye nina uhakika mchango wake ulinifanya niwe juu katika muziki wa dansi Tanzania,” alisema.
 Kwa mujibu wa Kamati hiyo ambayo Mdoe ndio Katibu wake, taratibu zote zinaendelea ikiwa ni kuandaa nyimbo alizowahi kuimba na kuziweka katika mfumo wa kibiashara, ikiwamo mpango wa kuuza nyimbo zake katika makampuni ya simu za mikononi.
Mwenyekiti wa kamati ya kumuenzi Muhidin Maalim Gurumo, Asha Baraka, akizungumza jambo katika kutambulisha onyesho maalum la Gurumo litakalofanyika Oktoba 11 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. Anayefuata upande wa kushoto wa Asha ni mzee Muhdini Gurumo, Juma Mbizo, na Said Kibiriti.
Asha Baraka na wanakamati katika kutambulisha onyesho maalum la Gurumo litakalofanyika Oktoba 11 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. Anayefuata upande wa kushoto wa Asha ni mzee Muhdini Gurumo, Juma Mbizo, Cosmas Chidumule na Said Kibiriti. Kulia ni Katibu wa kamati Saidi Mdoe
Juma Mbizo, mratibu wa shoo hiyo, akionyesha mfano wa cd itakayouzwa ikiwa ni juhudi za kumuwekea mazingira mazuri mwanamuziki Muhdini Gurumo, baada ya kutangaza kustaafu muziki. Picha zote na Kambi Mbwana

U.S. Ambassador Alfonso E. Lenhardt swears in 41 Peace Corps Volunteers for their two years of service in Tanzania.

$
0
0
United States Ambassador Alfonso E. Lenhardt, (6th from right, front row); Guest of Honor Commissioner of Education, Eustela Bhalalusesa, from the Ministry of Education and Vocational Training, (5th from right, front row); Peace Corps Country Director, Elizabeth O’Malley, (8thfrom right, front row); in a group photo with Peace Corps Volunteers and officials from partner agencies. U.S. Ambassador Alfonso E. Lenhardt swore in 41 Peace Corps Volunteers for their two years of service in Tanzania.  The American volunteers who will work in the education field will be stationed in Masasi, Lushoto, Kilwa, Hanang, Rungwe, Same, Ruangwa, Bahi, Kondoa, Newala, Lindi, Mbinga, Rungwe, Iramba, Mufindi , Iringa Rural, Mbeya Urban, Mbeya Rural, Kongwa, Mwanga, Moshi Urban, Hai, Mkinga, Wete, Kati, Singida Urban, Kaskazina A., Kusini Unguja, Monduli and Njombe districts.

Windhoek, mojawapo wa majiji masafi kuliko yote barani afrika

mama salma kikwete aongoza mapokezi ya mbio za mwenge wilayani Lindi

$
0
0
 
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge taifa Juma Ali Simai akimkabidhi Mwenge wa Uhuru  mkimbiza mwenge namba moja katika manispaa ya Lindi Mke wa Rais ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) Mama Salma Kikwete wakati mwenge huo ulipowasili leo katika eneo la Mto Mkavu – Mbanja. Wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Dk. Mohamed Nassor.
 Mkimbiza  Mwenge namba moja katika manispaa ya Lindi Mke wa Rais ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Mchinga Mhe Said Mtanda wakati mwenge huo ulipowasili leo katika eneo la Mto Mkavu – Mbanja. Kiongozi wa Mbio za Mwenge taifa Juma Ali Simai (hayupo pichani) alipongeza Mbunge huyo kutokana na moyo wake wa kujitoa na kushiriki katika mbio za mwenge mkoani Lindi na kuwataka wabunge waige mfano.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Taifa Juma Ali Simai akimkabidhi Mwenyekiti wa klabu ya kupinga  rushwa katika chuo cha Ufundi VETA kilichopo Manispaa ya Lindi Abdallah Makwinya kifurushi chenye nakala  mbalimbali zinazoeleza jinsi ya kupambana na rushwa chuoni hapo. Kushoto ni Mkimbiza  Mwenge namba moja katika manispaa ya Lindi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
 Afisa kutoka Ofisi ya TAKUKURU mkoani Lindi Amos Ndege akielezea umuhimu wa klabu ya kupinga  rushwa  iliyopo katika chuo cha Ufundi VETA jinsi itakavyosaidia kutoa elimu kwa vijana. Wanaomsikiliza kwa makini ni Mkimbiza  Mwenge namba moja katika manispaa ya Lindi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Taifa Juma Ali Simai.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Taifa Juma Ali Simai akifungua  darasa litakalotumiwa na  klabu ya kupinga  rushwa katika chuo cha Ufundi VETA kilichopo Manispaa ya Lindi kwa ajiili ya kutoa elimu kuhusiana na madhara ya rushwa kwa jamii. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Dk. Mohamed Nassor.
 Mama Salma Kikwete akijumuika na viongozi wa Serikali na vyama vya siasa wa manispaa ya Lindi wakijiandaa kuupokea Mwenge wa Uhuru kutoka wilaya  ya Lindi zoezi hilo limeafanyika leo katika eneo la katika eneo la Mto Mkavu – Mbanja. Ukiwa katika Manispaa ya Lindi Mwenge huo utafungua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.5.
Wakimbiza Mwege Taifa, Viongozi wa Serikali wa wilaya ya Lindi na Askari Polisi  wakielekea  kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa viongozi manispaa ya Lindi  zoezi hilo limefanyika leo katika eneo la Mto Mkavu – Mbanja. Picha zote na Lorietha Laurence – Maelezo

Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
Vijana nchini wametakiwa kuwa wawazi, waaminifu na waadilifu kwani huo ndiyo msingi mkubwa wa kupambana na  rushwa ili waweze kuwa viongozi wazuri hapo baadaye.
Rai hio imetolewa leo na Kiongozi wa Mbio za Mwenge taifa Juma Ali Simai wakati akiongea na wanafunzi wa chuo cha ufundi cha Veta likichopo katika  Manispaa ya Lindi mara baada kuzindua klabu ya kupinga  rushwa chuoni hapo.
Alisema kuwa hivi sasa kuna baadhi ya viongozi ambao wanakusanya mapato na kodi za wananchi na kuzitumia vibaya na hivyo kusababisha shughuli za maendelea kutofanyika ikiwa ni pamoja na kutojengwa kwa shule na vituo vya afya na wanaoathirika ni wananchi wote.
Simai alisema, “Vijana ni tegemeo la taifa chukueni  hatua dhidi ya rushwa, kila mtu awajibike kwa kutoa  taarifa na ushahidi ili wahusika wachukuliwe hatua ni lazima mjifunze kutokana na makosa yanayofanyika leo ili nanyi msifikie huko kwani rushwa ni mbaya na adui mkubwa wa maendeleo”
Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge Taifa  alisema mtu ukiwa muadilifu na muaminifu hata  sehemu ya  kazi utaonekana na utapanda kutoka hatua moja kwenda nyingine bila ya kutoa rushwa na kutoa mfano kwa wanafunzi hao mara baada ya kumaliza masomo yao watapata ajira  bila ya kutoa rushwa kwani ni haki yao kuajiriwa au kujiajiri.
 “Kama wananchi watapata  taarifa na haki zao kwa wakati kutoka kwa viongozi wao wataepukana na  mazingira ya rushwa lakini hivi sasa kuna baadhi ya watu wanaona kuwa hawawezi kupata haki zao za msingi hadi watoe rushwa.
Ninawaomba wale wote wenye tabia hii muiache na mtoe taarifa kwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) ili pale mnapoombwa kufanya hivyo kwani rushwa ni adui wa haki na mfahamu kuwa kwa anayetoa na anayepokea wote wanakabiliwa na kosa la jinai”, alisema Simai.
Simai alisema kuwa ni muhimu vijana wakawajibika  na kuwa wawazi katika mambo wanayoyafanya kwa maana ya kwamba wakipata nafasi wawashirikishe na wengine pia wafuate  misingi ya utawala bora katika kupambana na rushwa.
Akisoma taarifa ya klabu ya wapinga rushwa katika chuo hicho Christina Mkolela ambaye ni mwanachama alisema kuwa ili kupambana na rushwa katika halmashauri ya Manispaa ya Lindi waliamua kuanzisha klabu hiyo ikiwa ni moja ya mkakati wa kuelimisha vijana waliopo vyuoni ili kuwajengea uzalendo wa kuchukia rushwa na baadaye kuwa raia wema wasiopenda kupokea wala kutoa rushwa.
Alisema klabu hiyo ilianzishwa mwaka 2013 ikiwa na wanachama 91 kati ya hao wasichana ni 21 na wavulana ni 70 ambao wanashiriki katika kutoa elimu ya kuzuia na kupambaa na rushwa kwa wenzao.
Mkolela alisema, “Klabu hii ni ya kudumu na itaendelea kupokea wanachama ambao ni wanavyuo watakaokuja chuoni hapo kila mwaka na hivyo kuifanya kuwa  endelevu”.
Kabla ya kuwasili chuoni hapo Mwenge huo wa uhuru ulipokelewa kutoka wilaya ya Lindi na  viongozi wa Serikali na vyama vya siasa wa Manispaa ya Lindi akiwemo mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika eneo la Mto Mkavu – Mbanja.
Ukiwa katika Manispaa ya Lindi Mwenge wa uhuru utafungua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.5 kati ya miradi hiyo ni mradi wa maji safi kwa matumizi ya binadamu na mradi wa samaki.
Sherehe za kilele za  mbio za Mwenge wa Uhuru ambazo zitaenda sambamba na kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na maadhimisho ya wiki ya vijana zinatarajia kufanyika tarehe 14/10/2013 katika uwanja wa Samora uliopo Manispaa ya Iringa.

January Makamba azindua tume ya tehama leo jijiini Dar.

$
0
0
Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba (wa pili toka kushoto mstari wa mbele), wa kwanza wake toka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt. John Mngodo. Wa kwanza kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Mawasiliano Bi. Clarence Ichwekelezwa na anayemfuatia ni Katibu Mkuu Prof. Patrick Makungu. 
 Mgeni rasmi Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba akitoa salamu zake kwa wadau mbalimbali (hawako pichani) waliohudhuria mkutano kabla ya kutoa hotuba yake wakati alipokuwa akizindua rasmi Mkutano wa wadau wa uanzishwaji wa Tume ya TEHAMA uliofanyika leo Peacock Hotels jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Prof. Patrick Makungu na kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt. John Mngodo.  
 Baadhi ya wadau mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi wa Mkutano wa wadau juu ya uanzishwaji wa Tume ya TEHAMA wakifauatilia kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi . Mkutano huo umefanyika leo Peacock Hotels jijini Dar es Salaam. 
 Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba akijibu maswali mbalimbali toka kwa waaandishi wa habari mara alipomaliza kuzindua rasmi Mkutano wa wadau wa uanzishwaji wa Tume ya TEHAMA uliofanyika leo Peacock Hotels jijini Dar es Salaam.


.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.

======= =====  ======
UZINDUZI WA MKUTANO WA UANZISHWAJI WA TUME YA TEHAMA.
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
12/09/2013.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba amezindua rasmi mkutano wa Washikadua juu ya uanzishwaji wa Tume ya TEHAMA leo jijini Dar es Salaam.¨

Mhe. Makamba amesema kuwa TEHAMA kitakuwa chombo kikubwa ambacho kitashirikisha wadau wengi hapa nchini kwa lengo la kuhakikisha kuwa matumizi ya TEHAMA yanasonga mbele na inatoa fursa mbalimbali zenye kuweza kutatua changamoto za kimaisha kwa watanzania.

Mhe. Makamba aliongeza kuwa TEHAMA ndiyo inaleta mabadiliko na kuleta maendeleo makubwa hivyo amesisitiza juu matumizi ya TEHAMA katika ofisi za serikali na sekta binafsi. Aidha, amewashauri wadau wote kuangalia wenzetu nchi zilizoendelea jinsi wafanyavyo ili kuhakikisha kuwa matumizi ya TEHAMA nchini Tanzania yanasonga mbele. “Kama Taifa hakuna sehemu ambapo tunakutana kutafakari juu hali ilivyo katika matumizi ya TEHAMA hapa nchini”. Alisema Mhe. Makamba.

Kwa upande mwingine Mhe. Makamba alisisitiza juu ya wanataaluma wa TEHAMA wawe wanajulikana na amesema kuwa katika uundaji wa Tume hiyo ni vema wataalamu na ufanisi wa kazi zao ujulikane ili kuepukana na kuwa na wataalamu ambao ni Makanjanja. “Hapa nchini Tanzania hatuna uhakika wa wahitimu katika mambo ya TEHAMA hivyo kuna uwepo wa vyuo na tasisi ndogondogo nyingi zilizosambaa ambazo zinajikita kutoa taaluma hiyo, katika masuala ya TEHAMA ni lazima wataalamu wajulikane na kusajiliwa kama ilivyo katika bodi nyingine za serikali hapa nchini”. Alisema Naibu Waziri.

Aidha, Mhe. Makamba alimalizia kwa kuipongeza Serikali kwa kazi kubwa inayofanya kwa upande wa TEHAMA kwani mpaka hivi sasa nchi imefikia mahali pazuri katika mambo ya mawasiliano pia ameshauri juu ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika uundaji wa tume ya TEHAMA. 

MAANDAMANO YA KUPINGA UJANGILI WA TEMBO NCHINI YAFANYIKA JIJINI DAR

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) (watano kutoka kushoto msitari wa mbele) akiwa anandamana pamoja na waandamanaji wanaopinga ujangili wa tembo ‘Tembea kwa ajili ya Tembo’ mara baada ya kuwapokea leo, Ubungo  jijini Dar es Salaam asubuhi. Maandamano hayo yamechukua muda wa siku 19 na waandamanaji wametembea kilomita 650, kutoka Jijini Arusha.


Matembezi hayo ya kupinga ujangili yameandaliwa Bw. Patric Patel, Mkurugenzi, African Wildlife Trust (wanne kutoka kulia msitari wa mbele) yakiwa na lengo la kuelimisha wananchi na Ulimwengu mzima kwa ujumla juu ya madhara ya ujangili. Matembezi yamehusisha raia wa nchi mbalimbali duniani.



Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) ambaye ndiye mgeni rasmi katika kilele cha matembezi hayo ametoa wito kwa wananchi wote waendelee kushirikiana na serikali kupiga vita ujangili kwa kuwafichua majangili popote wanapowaona; na taasisi zote za umma zishirikiane kupambana na ujangili ili kuutokomeza kabisa.

Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexander Songorwa (aliyeshika karatasi nyeupe mstari wa mbele) akiwa ameungana na msafara wa waandamanaji eneo la Ubungo kutembea nao hadi viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo atapokea risala kutoka kwa waandamanaji. 

Article 11


mafunzo ya Uhusiano wa Kimataifa kwenye chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar yaandaliwa

$
0
0

Mkuu wa Chuo cha Dilpomasia Jijini Dar es salaam Balozi Dr. Mohammed Maundi yeye na ujumbe wake akibadilishana mawazo  na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi juu ya mfumo wa kuanzisha mafunzo ya Uhusiano wa Kimataifa kwenye chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar.Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Utumishi wa Umma Zanzibar Nd. Yakout Hassan Yakout.
Mkuu wa Chuo cha Dilpomasia Jijini Dar es salaam Balozi Dr. Mohammed Maundi akiongea.

Uongozi wa Chuo cha Diplomasia Cha Jijini Dar es salaam umepongezwa kwa hatua zake ulizoanza kuzichukuza katika harakati za  kusaidia Taaluma ya masuala ya Uhusiano wa Kimataifa katika Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar.Makamu wa Pili wa Rais wa
 Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Balozi Seif alitoa pongezi hizo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati akizunguma na Uongozi wa Chuo cha Diplomasia ukiongozwa na Mkuu wa chuo hicho Balozi Dr. Mohammed Maundi uliofika Zanzibar kwa hatua za awali za namna ya kuanza mpango huo.
Balozi Seif ambae aliwahi kutoa ombi hilo wakati akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya Tano ya chuo cha Utawala wa umma Machi 30 mwaka huu huko Tunguu alisema taamula hiyo inaweza kusaidia wanafunzi hao wakati wanapoamua kuendelea na mafunzo yao katika ngazi za Kimataifa.
Alifahamisha kwamba Dunia hivi sasa ina mfumo wa mazingira ya kutegemeana hivyo ni vyema kwa watumishi wa umma pamoja na wana jamii wakaanza utaratibu wa kujipatia taaluma inayofanana na mazingira hayo ya Ushirikiano wa Kimataifa.
“ Nimefurahi na kushukuru kuona kwamba lile wazo langu nililolitoa kwenye mahafali ya chuo cha utawama wa Umma Zanzibar Mapema mwaka huu limeanza kutoa matumaini mazuri ambayo kwa kweli  yananipa moyo mkubwa “. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kuwa taaluma hiyo ikienea zaidi miongoni mwa jamii italenga kukomaza   mfumo wa uhusiano wa Kidiplomasia hapa Nchini.
Naye Mkuu  wa Chuo cha Diplomasia cha  Mjini Dar es salaam Balozi Dr. Mohammed Maundi  alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Uongozi wa chuo hicho unajiandaa kuleta  wataalamu Zanzibar ili kuangalia na kuona hatua za pamoja za kuchukuliwa katika muelekeo wa pamoja na chuo cha Utumishi wa Umma wa kuanzisha mitaala ya mafunzo ya Diplomasia.
Balozi Maundi alisema ipo haja ya kubadilishana mihula ya wanafunzi kati ya vyuo hivyo ili kuongeza ushirikiano kati ya wana taaluma wa Chuo cha Diplomasia Dar es salaam na wale waChuo cha Utawala wa Umma hapa Zanzibar.
“ Tunaweza kuanzisha mafunzo ya pamoja miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vyote viwili. Hii itasaidia pande zote husika kwa vile uwezo wa walimu wetu unaweza kutumiwa na pande zote mbili “. Alifafanua Balozi Maundi.
Alisema chuo cha Diplomasia hivi sasa kiko katika mchakato wa kuanzisha kiwango cha Digirii ya kwanza kufuatia ongezeko kubwa la wanafunzi wanaoomba kujiunga na chuo hicho ambao wengi wao wanatokea Visiwani Zanzibar.
Mkuu huyo wa Chuo cha Diplomasia anayehusika zaidi na fani ya usuluhishi katika migogoro ya rasimlali asilia Balozi Maundi alimshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa wazo lake lenye mustakabali wa kuwajengea uwezo zaidi wa kitaaluma wanafunzi wa Zanzibar.


Profesa Mbarawa apigia chapuo matumizi ya Mkongo Wa Mawasiliano Kwa Maendeleo Ya Kiuchumi, kijamii

$
0
0
Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini zimeshauriwa kutumia Mkongo wa mawasiliano ili kuchochea shughuli za maendeleo ya kijamii na uchumi. Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa aliawambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kuziunganisha nchi hizo na mkongo wa mawasliano. 
“Mkutano wetu leo umeshirikisha wajumbe kutoka nchi nane zikiwemo za Kenya, Rwanda, Angola, Sudan, Uganda na Burundi,” lengo likiwa ni kupanua wigo wa matumizi ya mawasiliano kupitia mkongo huo. 
Alisema Tanzania tayari inapata mawasiliano kupitia mkongo wa taifa na ile ya kimataifa inayopita chini ya bahari ikiwemo ya Ezecom na Celcom kwa mawasiliano ya kimataifa. Alifafanua kwamba mafanikio hayo yamewezesha pia nchi kama Burundi, Rwanda, Zambia, Malawi na Uganda kunganishwa na mkongo wa Tanzania. 
Pia Tanzania ipo mbioni kuziunganisha nchi nyingine kama Sudan Kusini na Msumbiji kupata huduma hiyo hiyo muhimu kimaendeleo. Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Dkt. Kamugisha Kazaura alisema mkongo umesaidia nchi kuhama kutoka katika mfumo wa Analojia kwenda katika matangazo ya Dijitali. 
“Tunatarajia pia nchi nzima itapata matangazo yake kwa mfumo huu wa dijitali baada ya kuzima analojia katika maeneo yaliyobaki,”alisema. 
Alisisitiza kwamba matumizi ya mkongo wa mawasiliano ni rahisi na huduma hiyo kupatikana kwa bei nafuu. Mkongo ni muhimili wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambapo kwa sasa TTLC imeshinda tenda ya kutoa huduma ya internet kwa serikali ya Tanzania na Rwanda kwa miaka 10. Pia nchi imeweza kupata wateja waliounganishwa na mkongo wa mawasiliano wa Tanzania. 
Waziri wa Sayansi na Mawasiliano wa Sudan, Dkt. EIsa Bashari Mohmed Hamid alisema mkutano huo umetoa changamoto kubwa kwa nchi yake kujiunga na mkongo wa Tanzania. “Tuna mawasiliano ya karibu na nchi ya Tanzania katika kufanikisha jambo hili,” na hii ni huduma muhimu kwa maendeleo kwa vile ni rahisi na inapatikana kwa bei ya chini.
 Alisisitiza kuwa mawasiliano yakiwa ya uhakika husaidia wananchi kupata maendeleo. Mkutano huo ulishirikisha nchi nane na uliandaliwa na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL).
Waziri wa Mawasliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa matumizi ya Mkongo wa Mawasiliano katika kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini, kushoto ni Waziri wa Sayansi na Mawasiliano wa Sudan, Dkt. Eisa Bashari Mohmed Hamid wa Sudan na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA, Profesa John Nkoma, mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe kutoka nchi nane.
Waziri wa Mawasliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akichangia mada  wakati wa mkutano wa matumizi ya Mkongo wa Mawasiliano katika kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini,wapili kushoto ni Waziri wa Sayansi na Mawasiliano wa Sudan, Dkt. Eisa Bashari Mohmed Hamid wa Sudan, Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano nchini (TTCL), Dkt. Kamugisha Kazaura na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA, Profesa John Nkoma, mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe kutoka nchi nane.

KINANA AHITIMISHA ZIARA YAKE KISHAPU KWA MAFANIKIO MAKUBWA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi waliofika kumpokea kwenye wilaya ya Kishapu katika eneo la Maganzo ambapo Katibu Mkuu alikuwa na ziara katika wilaya ya Kishapu.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi moja ya madarasa katika shule ya Sekondari Mwigumbi.
Moja ya Nyumba mpya iliyojengwa kwa ajili ya makazi ya Walimu wa Shule ya Sekondari Mwigumbi, wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ambayo ilizinduliwa leo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitumia usafiri wa baiskeli kufika kijiji cha  Mwigumbi ambapo kulikuwa na shughuli za kuzindua mradi wa maji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kuzindua mradi wa maji wa kata ya Mondo,kijiji cha Mwigumbi wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga.
 Mbunge wa Kishapu Suleiman Masoud Mchambi akishiriki kucheza ngoma ya kiasili wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliofanyiaka kata ya Mondo kijiji cha Mwigumbi.
 Tanki la maji litakalowasaidia wakazi zaidi ya 4000 katika kijiji cha Mwigumbi ,pichani wakazi wa kijiji hicho wakiwa wamekusanyika kushuhudia uzinduzi rasmi wa tanki hilo.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mwigumbi mara tu baada ya kuzindua mradi wa maji utakaosaidia zaidi ya watu 4000.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Ndugu Azah Hilal Hamad akiwahutubia wakazi wa kata ya Mondo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mwigumbi.
 Mbunge wa Kishapu Ndugu Suleiman Masoud Mchambiakihutubia wakazi wa kata ya Mondo na kuelezea namna gani jimbo lake limekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiingia kwenye viwanja vya Mabela kwa staili ya aina yake tayari kuhutubia wakazi wa Wilaya ya Kishapu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza  Balozi wa China hapa nchini ndugu Lu Youqinq wakati wa mkutano wahadhara uliofanyika katika viwanja vya Mabela, kushoto kwake ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

Amb.Kagasheki touts envoys as Tanzania vies for a seat to the World Heritage Committee.

$
0
0
The Minister for Natural Resources and Tourism Hon Ambassador Khamis Kagasheki hosted a luncheon for Members of the Diplomatic Corps with the purpose of presenting Tanzania’s intention to vie for a seat to the World Heritage Committee. 
 The election for a seat to the World Heritage Committee is scheduled to take place during the General Assembly of State Parties to the World Heritage Convention to be held from 19 – 21 November, 2013 in Paris. 
Addressing the delegates, Minister Kagasheki said that Tanzania has demonstrated a high level of commitment to conservation of its natural resources and has dedicated more than 42,000sq.kms of its land to conservation. 
It is worth mentioning that Tanzania is one of the African Countries with most sites inscribed on the World Heritage List. Furthermore, the Minister said that Tanzania’s candidature is supported and was endorsed by the African Union Summit in Addis Ababa in May, 2013. 
Hon Kagasheki therefore reached out an appeal to Members of the Diplomatic Corp and their countries to not only support and vote for Tanzania’s candidature but also requested them to seek support of other European, Arab and South American Regions. 
The Representative of the Members of the Diplomatic Corp, Dr Ishaya Samaila Majambu who is also the Nigerian High Commissioner to Tanzania expressed their gratitude for the kind gesture given them by the Ministry. Dr Ishaya assured the Minister that the delegates will convey Tanzania’s request to their respective countries and that they are sure the request will be well accepted. He concluded by wishing Tanzania a successful candidature.
 The Minister for Natural Resources and Tourism Hon Khamsi Kagasheki giving his remarks during the luncheon.
Hon Khamsi Kagasheki bidding farewell to Members of the Diplomatic Corp after the luncheon.
 The Minister for Natural Resources and Tourism Hon Khamsi Kagasheki having talks with the Representative of the Members of the Diplomatic Corp, Dr Ishaya Samaila Majambu who is also the Nigerian High Commissioner to Tanzania.

TASWIRAZZ MBALI MBALI ZA KUZAMA KWA JUA JIONI YA LEO ENEO LA GAIRO MKOANI MOROGORO

Article 5

Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje akutana na Watanzia nchini Zambia

$
0
0
Leo tarehe 12 Septemba 2013, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewatembelea wajasiliamali, Raia wa Tanzania wanaoishi na kufanya shughuli zao nchini Zambia katika maeneo ya viwanja vya COMESA. Katika zaira hiyo iliyofana, Mhe. Naibu Waziri aliambatana na Mhe. Grace Mujuma, Balozi wa Tanzania nchini Zambia pamoja na maofisa wengine wa Wizara ya Mambo ya Nje.

Baada ya kutembelea mabanda mbalimbali na kukagua shughuli zinazofanywa na Watanzania hao, Mhe. Naibu Waziri alipata fursa ya kubadilishana nao mawazo. Watanzania hao walielezea furaha yao kwa kutembelewa na kiongozi wa Serikali ya Tanzania na kubainisha kufarijika kwao kwa namna Serikali yao inavyowajali. 

Waliomba juhudi zifanyike kupanua barabara katika eneo la Tunduma ili kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo. Aidha, waliomba mashauriano yafanyike ili kituo cha mpaka cha Tunduma/Nakonde kifanye kazi kwa masaa 24. Walisema hatua hiyo itasaidia kuondoa msongamano, kuongeza kasi ya biashara, kupunguza vitendo vya jinai na kuiongezea mapato Serikali.

Naye Mhe. Naibu Waziri aliwapongeza Watanzania hao kwa kuamua kufanya shughuli zinazoweza kuwapatia kipato cha halali na kujenga taifa lao. Aliwataka wahakikishe kwamba wote wanaishi kisheria na kufuata taratibu zilizowekwa na mamlaka za Zambia ili kuepusha usumbufu kwao na kwa Serikali. Aidha, aliwataka wasijihusishe na vitendo vyovyote vya jinai ili kuepusha kuchafua sifa nzuri za taifa la Tanzania.

Mhe. Naibu Waziri yupo nchini Zambia akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa kimataifa kuhusu Mkataba unaolenga Kutokomeza matumizi ya Mabomu ya kusambaa (Convention on Cluster Munitions). Kabla ya kutembelea wajasiri-amali, Mhe. Najbu Waziri alikutana na kuzungumza na Watanzania wa rika na kada mbalimbali wanaoishi nchini Zambia, mazungumzo ambayo yalifanyika katika Ubalozi wa Tanzania, Lusaka.
Mhe. Naibu waziri akikagua shughuli za wajasiriamali Watanzania katika soko la Comesa. Wa kulia kutoka alipo Naibu Waziri ni Mhe. Grace Mujuma, Balozi wa Tanzania nchini Zambia na wa kulia ni Bw. Mboweto, Raia wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko la Comesa.

Kitabu cha FALLING IN LOVE sasa kinapatikana mtandaoni

kifoleni cha mchana eneo la Kiluvya

$
0
0
Kamera ya Globu ya Jamii,Mchana wa leo iliinasa taswira hii ya Foleni kali katika eneo la Kiluvya,Mkoani Pwani.

ankal akiwa shopping jijini Windhoek, namibia

$
0
0
Ankal akipatana bei ya urembo wa kitamatuni na kinamama wajasiriamali wa kabila la Wahimba katika mtaa wa Independence jijini Windhoek. Kabila hili ambalo linaendelea kudumisha mila na utamaduni wa Mwafrika huishi Kusini mwa Namibia katika mkoa wa Kunene (zamani Kaokoland) na pia hupatikana upande wa pili wa mto Kunene nchini Angola. Lugha inayotembea hapo ni Kiingereza na ishara, ni watu wacheshi na hodari sana kwa biashara. Miili yao imepakwa mafuta ya kondoo na udongo mwekundu ili kujikinga na jua.

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya Maquis du zaire ya 'Kiongo' ilikuwa balaa enzi hizo. Hapa MC Anko J Nyaisanga anakutambulishwa kwa mwagwiji kama vile Vumbi Kahanga Dekula, Kasaloo Kyanga, Kanku Kelly, Mafumu Bilali Bombenga, Adios, Audax na wengineo katika Chekechaaaaa....Asante sana Pablo Machine kwa kumbukumbu hii moto

Mapacha Watatu Band FC, Mashujaa Band FC hakuna mbabe

$
0
0
 Kikosi cha Mapacha Watatu Band FC
Kikosi cha Mashujaa Band FC
MECHI iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa kati ya Mapacha Watatu FC na Mashujaa Band FC  imeisha vizuri huku timu zote mbili zikifungana bao 1-1, katika mchezo uliochezwa jana katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo uliondaliwa na kundi la Bongo Dansi linalopatikana kataika mtandao wa kijamii wa facebook kwa nia ya kuletaa ushirikiano na undugu kwa wanamuziki.
Ilikuwa ni mechi ya kukata na shoka iliyoacha simulizi kubwa kwa  wote walioishuhudia. Hadi Mapumziko, Mapacha Watatu walikuwa mbele kwa kwa bao lililofungwa na Hija Ugando dakika ya 19.
Mfungaji alifunga kufuatia kazi kubwa iliyofanywa na Hamis Dacota aliyeichambua ngome ya Mashujaa kabla ya kutoa pande kwa mchezaji mwalikwa Mathew Kiongozi ambaye naye bila hiyana alimsogezea Hajji aliyeujaza mpira wavuni.
Wachezaji wa Mapacha wakiongozwa na Jose Mara, Khalid Chokoraa, Kasongo, Dacota , Dulla Ngoma na wengineo, waliendelea kulisakama lango la Mashujaa kwa muda wote wa kipindi cha kwanza.
Lakini Upepo ulibadilika kipindi cha pili ambapo Chaz Baba, Abdul Tall, Jado FFU na wengineo walianza kuumiliki mpira na na kuwafunika Mapacha Watatu.
Zikiwa zimesalia dakika 3 mpira kumalizika, Mashujaa walisawazisha kwa bao lililofungwa na Hamis Tanya, ikiwa ni hatua nzuri ya maendeleo ya kundi hilo la Bongo Dansi, lililoanzishwa na kuongozwa na wadau wa muziki, akiwamo Said Mdoe, Mathew Kawogo ama Mathew Kiongozi, Engi Muro Mwanamachame, William Kaijage na Abdulfareed Hussein, Deo Mutta Mwanatanga na Khamis Dacota.
Viewing all 110149 articles
Browse latest View live




Latest Images