Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

NSSF YASHIRIKI MAONYESHO YA VIWANDA VIDOGO MKOANI MTWARA

$
0
0
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linashiriki maonyesho ya viwanda vidogo vidogo yanayoendelea mkoani Mtwara kuanzia Novemba 5 hadi 11,2018. Maonyesho hayo yalianzia mkoani Simiyu, na sasa yanaendelea mkoa wa Mtwara na yatamalizikia mkoani Tanga.

Maonesho haya yenye lengo kuu la kuwasidia wajasiriamali kupata masoko ya bidhaa zao, kujifunza kupitia wenzao na kujenga mahusiano baina ya taasisi moja na nyingine, yameshirikisha taasisi takribani 16 za kiserikali na zisizo za kiserikali pamoja wajasiriamali zaidi ya 278 kutoka mkoa wa mtwara na mikoa ya jirani.

NSSF kupitia maonesho hayo imepata fursa ya kuwafikia washiriki Mbalimbali na kutoa elimu kwa ukaribu zaidi juu ya huduma zitolewazo na shirika pamoja na hifadhi ya jamii kwa ujumla.Baada ya kupatiwa elimu wajasiriamali wanapata nafasi ya kusajiliwa na kuwa wanachama wa nssf ili nao waweze kunufaika na mafao yote yatolewayo na shirika hili ambayo ni pamoja na matibabu bure kwao na familia zao.

Meneja wa NSSF mkoa wa Mtwara,Ndugu
Stanley Millanzi  ametoa wito kwa wakazi wa Mtwara, mikoa ya karibu na nchi nzima kwa ujumla kutembelea banda la NSSF katika maonesho hayo ili kupata elimu na kujiandikisha, hususan baada ya Mabadiliko ya sheria yaliyofanyika mwaka 2018, ambapo NSSF ilipewa jukumu la kuwaandikisha na kuwapa hifadhi ya jamii wananchi wote waliopo katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi ikiwemo wajasiriamali. 
 Afisa uhusiano wa NSSF Rehema Urembo akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa viwanda Mhandisi  Stella Manyanya katika banda la NSSF kwenye maonesho ya viwanda vidogo yanayoendelea mkoani Mtwara
 Naibu Waziri wa viwanda Mhandisi  Stella Manyanya akiwa sambamba na Mbunge wa Mtwara Vijijini Mh Hawa Ghasi wakimsikiliza  Afisa uhusiano wa NSSF Rehema Urembo alipokuwa akitoa ufafanuzi wa baadhi ya huduma zitolowezo na Shirika hilo,kwenye maonesho ya viwanda vidogo yanayoendelea mkoani Mtwara

Meneja NSSF na PSSSF  mkoa Mtwara,Ndugu Stanley Millanzi  pamoja na Zaida Mhava wakimsikiliza Naibu Waziri wa viwanda Mhandisi  Stella Manyanya (hayupo pichani) kwenye  Banda la NSSF,wakati wa maonesho ya SIDO yakiendelea mkoani Mtwara


Mbunge Biteko achangia miradi ya maendeo jimboni Bukombe

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo 

Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM), ameunga mkono juhudi za maendeleo za wakazi wa Kata ya Namonge jimboni humo kwa kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na wakazi hao.

Akizunguma kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Shilabela Novemba 03, 2018, Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini alichangia mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Shilabela pamoja na shilingi laki nane kwa ajili ya ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Nyamagwangala.

Biteko alitumia mkutano huo kuwapongeza wananchi wa Jimbo la Bukombe kwa kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ya ya maendeleo na kwamba serikali itaendelea kuwaunga mkono kwani maendeleo ni ushirika baina ya serikali na wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini, akizungumza na wakazi wa Kata ya Namonge kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Shilabela.

MBUNGE WA LIWALE ASEMA HUU SASA NI MUDA WA KUFANYA KAZI,AWASHUKURU WANANCHI

$
0
0
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Dodoma

MBUNGE wa  Lilwale kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)Zuberi Kuchauka amesema huu sasa ni muda wa  kufanya kazi na  kutekeleza Ilani ya Chama hicho kwa kasi  ya Rais Dk.John Magufuli katika jimbo  lake.

Kuchauka amesema hayo Mjini  Dodoma ambapo anashiriki Bunge la  11 ,kikao cha 13 mara baada ya kuapishwa kuwa Mbunge kwa tiketi ya CCM.

"Nawashukuru wananchi wa  Liwale kwa kuendelea kuniamini katika kipindi kingine nikiwa ndani ya CCM.Mnakumbuka nilikuwa upinzani na kisha kujiunga CCM na leo ni mbunge kupitia chama hicho.Nawashukuru wananchi kwa kuendelea kuniamini.

" Niwahaidi wakazi wa  Liwale kuwa sitowaangusha katika miaka miwili iliyobaki.Nitashirikiana nanyi katika kuhakikisha jumbo letu linapata maendeleo kwa kasi,"amesema Kuchauka

Amesema kuwa katika miaka hii miwili ambayo imebaki  atahakikisha anaendeleza pale alipoishia kwani uwanja ni ule ule na kilichobadilika ni timu ambayo amejiunga nayo ambayo ni sahihi kwa kuleta maendeleo ya Jimbo la Liwale.

Amefafanua  yeye ni Mbunge wa  CCM na  Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM chini  ya Rais Dk. Magufuli ambaye msimamo wake ni kusaidia watu maskini na  kuchapa kazi kwa  bidii.

Pia ameshukuru viongozi wa CCM pamoja na wananchi wote kwa kumuamini na  kurudi kugombea tena katika uchaguzi Mdogo na hatimaye kuibuka na ushindi.
MBUNGE wa  Lilwale kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Zuberi Kuchauka  alipofanya mahojiano mafupi na Michuzi TV jijini Dodoma.

OKOA MTOTO WA KIKE,OKOA JAMII

$
0
0

Katika maeneo mengi ya Tanzania bado kumekuwa na vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia ambapo wasichana wengi wamekuwa wakiolewa katika umri mdogo, wengine wakibakwa na wengine kupata ujauzito huku wakiwa bado wanafunzi. 

Hili ni janga kubwa lakini bado wasanii wengi wamekuwa wakilikaushia, ila kwa ujasiri na kuthubutu, mabinti hawa wameamua KUSEMA na kulizungumzia. Wimbo ambao umezalishwa na Tanzania Bora Initiative na Producer Mocco Genius na video kufanywa na Hascana.  Okoa mtoto wa kike, okoa jamii.


NEWS ALERT: CGP KASIKE AFANYA MABADILIKO MAKUBWA WAKUU WA MAGEREZA MIKOA TANZANIA BARA

$
0
0
Katika kuboresha utendaji kazi ndani ya Jeshi la Magereza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Martin Kasike amefanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi kwa kuwateua Wakuu wa Magereza wa Mikoa Tanzania Bara(RPOs) 19 wapya na saba (7) kuwabakiza katika nyadhifa zao. 
Katika mabadiliko hayo Kamishna Jenerali Kasike ameteuwa na kuthibitisha maafisa sita (6) kuwa Wakuu wa Vyuo vya Magereza na kuwabadilisha maafisa wengine watatu (3) katika vitengo muhimu ndani ya Jeshi hilo. 
Aidha, Kamishna Jenerali Kasike katika mabadiliko hayo kwa mara ya kwanza amewateua Wakuu wa Magereza wa Mikoa katika mikoa ya Katavi, Songwe, Njombe, Simiyu na Geita ambayo ilikuwa haina uongozi wa kimagereza katika ngazi ya mikoa hiyo. 
Katika mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa RPO (DSM) SACP. Hamis Nkubasi ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza kitengo cha Ujenzi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP. Julius Ntambala, SACP. Salum Hussein RPO (Dodoma) amebakia katika kituo chake na aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kiwira SACP. Luhende Makwaia anakwenda kuwa RPO (Mbeya) na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Mathias Mkama na aliyekuwa RPO (Mbeya) SACP. Kijida Mwakingi amehamishiwa Makao Makuu, Kitengo cha TEHAMA. RPO (Shinyanga). 

PRECISION AIR YATOA PUNGUZO LA BEI KUADHIMISHA JUBILEE YA MIAKA 25

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KUELEKEA miaka 25 toka kuanzishwa kwa Shirika la Ndege la Kitanzania  limezindua mfululizo wa nauli zenye punguzo kubwa ambalo litawawezesha wale wote ambao hawajawahi kutumia usafiri wa Ndege kupata fursa ya kufanya hivyo.

Shirika hilo ambalo lilianzishwa mwaka 1993 na Mtanzania  Michael Shirima, ni miongoni mwa mashirika machache barani Africa yaliyoweza kudumu kwenye biashara kwa miaka 25 mfululizo. 

Akizungumzia sherehe hizo Meneja Masoko na Mahusiano Hillary Mremi amesema, Precision Air inajivunia mafanikio waliyoyafikia kama kampuni ya Kitanzania na kwamba sherehe hizo si za Precision Air pekee bali za nchi nzima. 

“ Huu ni ushahidi ya kwamba Watanzania wanauwezo wakuanzisha na kusimamia biashara zao wenyewe kama tunavyoelezwa mara kwa mara na Raisi wetu Mpendwa, Dkt.John Joseph Pombe Magufuli, ya kwamba tunauwezo wa kufanikiwa kwa jambo lolote ikiwa tutajiamini na kufanya kazi kwa bidii. Precision Air ni kampuni ya kitanzania, inayomilikiwa na Watanzania ambayo imepata kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa na Wananchi pamoja na Serekali na kutokana na uungwaji mkono huo leo tunaona matunda yake kwa kusherehekea miaka 25 ya kutoa huduma.” amesema  Mremi

“katika kushereherekea miaka 25 ya kutoa huduma tunazindua mfululizo wa nauli zenye punguzo kubwa ambalo litawawezesha wale wote ambao hawajawahi kutumia usafiri wa Ndege kupata fursa ya kufanya hivyo, na kwa kuanzia tumewapa nafasi ya watu wenye safari kati ya Dar – Kilimanjaro nafasi ya kujaribu huduma zetu kwa nauli ya Sh.50,000 tu ikiwa ni pamoja na kodi zote. Ofa hii inapatika kupitia tovuti yetu pamoja na ofisi zetu za mauzo. Tunapenda kuwataarifu wateja wetu kujiandaa kwani muda wowote ofa hii itahusika katika maeneo wanayo safari.” Mremi amefafanua zaidi.

Shirika la Precision ilianzishwa  kama kampuni ya Ndege za kukodi, ikitumia Ndege aina ya Piper Aztec inayobeba abiria watano, Precision Air limeendelea kukua na kuwa moja ya hadithi za mafaniko nchini Tanzania na Afrika Mashariki. Ikiwa na Ndege tisa (9) aina ya ATR Precision Air sasa inafanya safari zake kutokea Dar es Salaam kwenda Arusha,Bukoba,Kilimanjaro, Kahama,Mtwara, Mwanza, Tabora, Zanzibar,Seronera,Nairobi na Entebbe ikitoa huduma ya uhakika ya usafiri wa anga katika maeneo hayo.

Baadhi ya mafanikio ambayo Precision Air imeafanikiwa kuyatima katika kipindi cha miaka ya karibuni ni pamoja na : -

Desemba 2015 – Tuzo ya Tanzania Leadership Awards - Kampuni Bora Upande wa mashirika ya Ndege 
2013 – Tuzo za TASOTA Shirika Bora la Ndege Tanznaia mwaka.
Februari 2012 – Aviation News Portal- Tuzo ya Shirika Bora la Mwaka Afrika- Tuzo ya shaba.
Desemba 2011 – Precision Air,ilikua shirika la kwanza la Ndege kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam.
Februari 2011 - Precision Air, izindua karakana ya kisasa yenye thamani ya Dola milioni 5.
2011 – Tuzo za TASOTA - Shirka Bora la Ndege Tanzania 
2010 – Tuzo za AFRAA –Shirika bora la safari za kikanda.
Oktoba 2009 – TCAA iliipatia Precision Air leseni ya kujihudumia yenyewe. 
2008 – Tuzo ya Mkurugenzi anayeheshimika Tanzania.
2007 – Tuzo ya Shirika linalo heshimika Tanzania.
2006 – Tuzo Za Tasota- Shirika bora la Ndege Tanzania.
Machi 2006 – Precision Air, ilikua shirika la tatu barani Africa kuanza kutumia mfumo wa tiketi za kieltroniki. 
Septemba 2006 – Ilipata cheti cha usalama cha IATA ikiwa ni shirika la kwanza Tanzania na la sita barani Africa. 

TANGAZO KWA UMMA

$
0
0


TAARIFA KUHUSU UTHIBITISHAJI WA NYARAKA


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuukumbusha Ummakwamba wale wote wanaohitaji kupata huduma ya kuthibitisha vyeti na nyaraka mbalimbali wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:


(1)  Huduma hizo zinatolewa katikaOfisi zaWizara Mjini DODOMA jengo la LAPF, Barabara ya Makole Ghorofa la 6.


(2)Malipo ya nyaraka zitakazothibitishwa yatalipwa kwa njia ya benki, akaunti namba 0150275408200 Foreign Collection Account, CRDB Bank kwa kiasi cha Shilingi Elfu Kumi na Tano tu kwa kila nyaraka(@TSHS 15,000/=). Hati ya malipo ya benki iwasilishwe Wizarani ili kuthibitisha malipo hayo.


(3)Mteja mwenye nyaraka yeyote inayohusu masuala ya talaka, ndoa, hali ya ndoa, tangazo la kuzaliwa, cheti cha kuzaliwa, Cheti cha Kifo, cheti cha ndoa anatakiwa kuanzia ofisi za Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Registration, Insolvency, Trusteeship Agency- RITA) Dar es Salaam.


(4)Vyeti vyote vinavyoletwa Wizarani kwa ajili ya kuthibitishwa, havina budi kupelekwa kwanza katika Taasisi za Tanzania zilizotoa vyeti/nyaraka hizo ili vihakikiwe na kuthibitishwa. Aidha, kwa vyeti au nyaraka zilizotolewa na mamlaka za nchi za nje zinatakiwa kupelekwa kwenye Balozi wa nchi amabayo vyeti hivyo vilitolewa kwa ajili ya uhakiki.


(5)Mteja anayeleta nyaraka za ajira (Mkataba wa ajira) anatakiwa kuanzia ofisi za Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (Tanzania Employment Services Agency –TAESA)


(6)Mteja anayeleta nyaraka iliyo katika lugha tofauti na kingereza anatakiwa kufanya Tafisri ya nyaraka hiyo na kuiambatisha na nyaraka halisi iliyofanyiwa tafsiri. Aidha, tafsiri ya nyaraka ifanywe na BAKITA, BAKWATA na taasisi zilizosajiliwa na kutambulika na Serikali.


(7)Kwa yeyote mwenye Power of Attorney na Deed Poll ahakikishe imesajiliwa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi kabla ya kuiwasilisha Wizarani.


(8)Nakala ya nyaraka yeyote inayotakiwa kufanyiwa uhakiki imbatane na nakala halisi ya nyaraka hiyo.


(9)Mteja anatakiwa kuandika barua kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiomba nyaraka hizo zithibitishwe na kueleza matumizi tarajiwa ya nyaraka hizo nje ya nchi. Aidha, Barua ya Katibu Mkuu iambatishwe na nakala (copies) za nyaraka zilizothibitishwa na taasisi husika ambazo zinahitaji kuthibitishwa na Wizara.



WATEJA WOTE WANAOMBWA KUZINGATIA RAI KWAMBA HUDUMA HIZI ZITAKUWA ZINATOLEWA SIKU YA JUMANNE NA ALHAMISI TU, KUANZIA SAA 3.00 ASUBUHI HADI SAA 6:00 MCHANA.


Imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki


Serikali Kuendelea Kufutia Milki Mashamba Yaliyotelekezwa

$
0
0
Na: Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma.

Serikali imeendelea kuchukua hatua za kubatilisha milki za ardhi za mashamba yaliyotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamesema Bungeni leo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula wakati akijibu swali la Mhe. Dustan Kitandula Mbunge wa Mkinga kuhusu kufuta hati za mashamba yaliyotelekezwa.

"Katika kipindi cha Disemba, 2015 mpaka Octoba, 2018 mashamba yenye ukubwa wa ekari 84,240.803 yamebatilishwa katika Halmashauri za Ngorongoro, Arumeru, Moshi, Kinondoni,(Manispaa), Kigamboni(Manispaa), Mvomero, Kilombero, Kilosa, Mvomero, Iringa, Bukoba, Tarime, Kibaha, Serengeti, Busega, Muheza, Lushoto na Mkinga" amefafanua Naibu Waziri Mabula. 

Mabula anasema kuwa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Shamba Na. 278 Mkomazi lenye ukubwa wa ekari 15,442 lililokuwa likimilikiwa na kampuni ya M/S Mkomazi Plantations Limited kwa Hati Namba 4268, 9780 na 9781 milki yake ilithibitishwa tarehe 20 Juni, 2018.

Aidha anafafanua kuwa, baada ya kubatilishwa kwa milki ya shamba hilo, Serikali ya Mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga zipange matumizi mapya ya shamba hilo kwa kuzingatia mahitaji ya ardhi katika eneo hilo kipaumbele kikiwa ni mahitaji ya wananchi na ardhi kwa ajili ya uwekezaji.

Mbali na hayo Mabula amezitaka Halmashauri zote nchini kubaini mashamba yaliyotelekezwa kutuma ilani kwa wamiliki wa mashamba hayo kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi (Sura 113) na kuwasilisha mapendekezo katika Wizara ya Ardhi kwa hatua za kubatilisha milki za mashamba hayo ziweze kufanyika.

WALIOFARIKI AJALI YA MSATA WATAMBULIWA MAJINA YAO -RPC WANKYO

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

WATU sita kati yao akiwemo mtoto mchanga jinsia ya kike ,waliofariki dunia katika ajali ,iliyotokea kijiji cha Msata, barabara kuu ya Segera /Chalinze mkoani Pwani ,wametambuliwa majina yao ili ndugu wakabidhiwe kwa ajili ya mazishi. 

Akitoa taarifa za muendelezo kuhusu ajali hiyo, kamanda wa polisi mkoani Pwani, (ACP) Wankyo Nyigesa alisema hakuna idadi ya vifo iliyoongezeka zaidi ya taarifa iliyotolewa awali. Alitaja miili ya marehemu iliyotambuliwa kuwa ni Ibrahim Kilama (28), Mohammed Amir Shekaoneka (28 mkazi wa Korogwe na Omary Rashid (28) Tanesco Magomeni jijini Dar es salaam. 

Wengine ni Lihatu Yahaya mtoto mchanga miezi mitatu mkazi wa Handeni ,Hassan Zabuni kondakta wa gari namba T. 124 DHW aina ya Toyota coaster na Emmanuel Cosmas (30) mkazi wa Chalinze . Aidha Wankyo alieleza, watu saba waliopata majeraha kwenye maeneo mbalimbali ya mwili yao , kati yao watano wameruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu na wengine wawili bado wapo hospital ya Tumbi Kibaha kwa ajili ya matibabu zaidi. 

“Ajali hiyo ilitokea novemba 5, majira ya saa moja usiku baada ya gari namba T. 124 DHW aina ya Toyota coaster ikitokea Mkata kwenda Mbezi -Dar es salaam ,kuligonga kwa nyuma bila kuchukua tahadhari ,lori namba KBV 746C/ZE2861 FAW iliyokuwa imeegeshwa barabarani kutokana na kuharibika.” Wankyo alitaja chanzo cha ajali, ni uzembe wa dereva wa gari namba T. 124 DHW aina ya Toyota coaster kujaribu kulipita bila tahadhari gari jingine lililokuwa limeegeshwa baada ya kuharibika na wanaendelea kumsaka. 

Kamanda huyo alitoa rai kwa madereva, kutii sheria za usalama barabarani na kudai hawatakuwa na muhali nao wale watakaokiuka sheria ili iwe fundisho kwa wengine.

WODI YA UZAZI KATIKA KITUO CHA AFYA CHALINZE CHAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UFINYU WA JENGO,VITANDA NA WATUMISHI WA AFYA

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE

WODI ya uzazi katika kituo cha afya Chalinze,mkoani Pwani inakabiliwa na baadhi ya changamoto ikiwepo ufinyu wa jengo hali inayosababisha wakati mwingine akinamama wazazi kusongamana na kulazimika kulala wawili katika kitanda kimoja.

Aidha kina tatizo jingine la upungufu wa vitanda na watumishi wa afya hasa madaktari . Akikabidhiwa msaada wa vifaa vya akinamama waliojifungua kutoka kwa kikundi cha Pwani generation queens ,mganga mfawidhi wa kituo hicho Salama Masukuzi alisema kuwepo kwa mlundikano wa wagonjwa kunatokana na upungufu wa majengo ya wodi ya uzazi pamoja na vitanda .

Alieleza ,kwasasa wapo maafisa tabibu wanne ,madaktari wasaidizi wawili na daktari mmoja ambao bado ni wachache kutekeleza majukumu yao ya kutoa huduma bora ya kiafya . “Kituo hiki kinapokea wagonjwa mbalimbali na wengine wakitokea kwenye zahanati 44 zinazozunguka halmashauri ya Chalinze suala ambalo linawawia vigumu kutekeleza wajibu wao ” alifafanua Salama .

Alieleza wamepata manesi wanne kupitia ajira mpya, ameishukuru serikali lakini aliiomba kuwaboreshea zaidi huduma ya afya ili kuwahudumia wananchi. Kwa upande wa akinamama wa Chalinze,akiwemo Demertia Milichadesi pamoja na Mariam Muhoja walisema wanapata shida katika kununua drip,vifaa vya uzazi na kipimo cha kujua wingi wa damu ambacho hutakiwa kwenda nje wakati mjamzito akiwa tayari yupo wodini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

SERIKALI INAENDELEA KUIMARISHA USIKIVU WA TBC NCHI NZIMA:DKT.MWAKYEMBE

$
0
0


Na Shamimu Nyaki –WHUSM.

Katika kuimarisha usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Serikali imeendela kuweka mikakati mizuri ya kuongeza usikivu wa shirika hilo hapa nchini kutegemea na upatikanaji wa fedha.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akijibu swali la mbunge Mhe. Zaynab Matitu Vulli (Viti Maalum) aliyeuliza Ni chanagamoto zipi zinazopelekea TBC kutosikika katika baadhi ya maeneo ya Pwani ambapo Mhe. Waziri alieleza kuwa katika Bajeti ya mwaka 2016/17 maeneo mengi ya nchi yaliongezewa usikivu.

“TBC ina mitambo ya kurushia matangazo  ya redio ya masafa ya FM katika Wilaya ya Kisarawe ambayo hufikisha matangazo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani katika masafa ya  87.8 MHz kwa idhaa ya TBC Taifa, 90.0 MHzkwa idhaa ya TBC FM na 95.3 kwa idhaa ya TBC International”.Alisema Dkt. Mwakyembe.Aidha ameongeza kuwa katika Bajeti ya mwaka 2016/17 TBC ilitekeleza mradi wa upanuzi wa usikivu katika Wilaya tano zilizopo mpakani ambazo ni Wilaya za Longido, Rombo,Tarime,Nyasa na Kibondo.

Vilevile katika Bajeti ya mwaka 2017/18 mradi wa usikivu katika mkoa wa Mtwara na Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga ulitekelezwa ambapo hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu TBC ilikua na vituo thelathini na tatu vya kurushia matangazo katika masafa ya FM kwenye Wilaya 102 kati ya 161 nchi nzima.

Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuhakikisha kuwa TBC inapanua usikivu ambapo kwa mwaka huu wa fedha maeneo ya Unguja na Pemba,Simiyu,Njombe,Songwe,Lindi maeneo ya Nangurukuru  pamoja na Mkoa wa Morogoro maeneo ya Morogoro Vijijini,Bondwa na Mahenge yatafikiwa.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa bungeni Jijini Dodoma.

BODI YA UTALII YAMTAKA MISS TANZANIA QUEEN ELIZABETH KUTANGAZA UTALII WA NCHI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imemkabidhi Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth baadhi ya vielelezo vya utalii ili akavitumie kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii kwa washiriki na watu kutoka mataifa mbalimbali. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Geofrey Tengeneza amesema kuwa Queen Elizabeth jukumu lake kubwa ni kushirikiana na bodi ya utalii katika kutangaza utalii wa ndani kwa maana ya kuvitangaza vivutio  vya utalii kwa watanzania na kuwahimiza kuvitembela vivutio vyetu hivyo.

 Amesema kuwa, mrembo huyu aliteuliwa kuwa Miss Domestic na tafanya kazi ya kutangaza vivutio vyote kwa kushirikiana na TTB na kwa kuzingatia hilo ndiyo maana leo  amefika ofisini kwao kwa ajili ya kuwaaga akielekea kuiwakilisha Tanzania katika shindano la Miss World litakalofanyika nchini China . 

Mrembo wetu anatarajia kusafiri siku ya Ijumaa 9/11/2018 na atakuwa huko kwa mwezi mmoja mpaka siku ya kilele cha shindalo hilo litakalo fanyika tarehe 8/12/2018. 

Tengeneza amesema kwa niaba ya Bodi ya Utalii Tanzania wanapenda kuchukua  fursa hii kumtakia kila la heri na ushindi katika shindano hilo na pamoja ya kwamba yeye pia ni Miss 3 Domestic Tourism lakini kwa kutambua kuwa atakapokuwa huko China atakutana na washiriki wengine kutoka mataifa mbalimbali tumeona ni vema pia tumkabidhi baadhi ya vielelezo vya utalii ili akavitumie kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii kwa washiriki na watu kutoka mataifa mbalimbali. 

"Ni matumaini yetu makubwa kuwa ataifanya kazi hii vizuri na kwa uzalendo mkubwa, lakini tuna imani kubwa kuwa atafanya vizuri sana katika shindano hili na hasa ikizingatiwa kuwa Queen Elizabeth anayo rekodi nzuri sana katika mashindano ya urembo kwani mtakumbuka vizuri kuwa mbali ya kuwa Miss Tanzania anashikilia pia taji la mshindi wa kwanza la Miss World University Kundi la Afrika alilolinyakua huko Cambodia mwaka jana 2017,"amesema Tengeneza.

Kwa upande wa mnyane huyo Queen Elizabeth amesema kuwa ana uhakika taji la Miss World kwa mwaka huu linakuja nchini Tanzania kikubwa ni watanzania kumuombea na kumuunga mkono pindi atakapokuwa nchini China kwenye kipindi cha mwezi mmoja.

Queen Elizabeth amesema kuwa, vielelezo vya utalii alivyopewa atavitumia vizuri ikiwemo kutangaza lugha adhimu ya Kiswahili.

Tofauti na mashindano yaliyopita ya Miss Tanzania, mwaka huu washindi watanowalipewa hadhi na majukumu mengine ya kiutalii. Mshindi wa kwanza ambaye ndiye Miss Tanzania Bi Queen Elizabeth Mkune alipewa hadhi ya kuwa Miss Domestic Tourism na tafanya kazi hiyo chini ya uratibu wa TTB, mshindi mwnginemiongoni mwa hao watano amepewa hadhi ya kuwa Miss Ruaha National Park natafanya kazi chini ya uratibu wa TANAPA, mshindi mwingine alipewa hadhi ya kuwaMiss Ngorongoro, mwingine Miss Selous na mwingine Miss Nature and ecology.

 Kwa ujumla hawa wote watakuwa na majukumu ya kuyatangaza hayo maeneowaliyopewa. Kwa upande wa Bi Queen Elizabeth jukumu lake kubwa ni kushirikianana sisi katika kutangaza utalii wa ndani kwa maana ya kuvitangaza vivutio vyetu vyautalii kwa watanzania na kuwahimiza kuvitembela vivutio vyetu hivyo. Kazi hiii kamanilivyosema ataifanya kwa kushirikiana na sisi.
 Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Geofrey Tengeneza akimvalisha shuka la kimasai kwa  Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth kama moja ya vielelezo vya utalii ili akavitumie kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii kwa washiriki na watu kutoka mataifa mbalimbali.

WAZIRI LUGOLA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA JIJINI DODOMA LEO

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke na kumuakikishia ushirikiano zaidi kati ya Wizara yake na Ubalozi huo nchini.
Mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Lugola, jijini Dodoma leo ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa ushirikiano kati ya Wizara na ofisi ya Balozi huyo nchini.
Waziri Lugola alimuakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini. 
“Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola.
Hata hivyo, Balozi Sara alimpongeza Waziri Lugola kwa kuteuliwa na Rais John Magufuli kuiongoza Wizara hiyo na pia alimuakikishia ushirikiano zaidi kati ya Uingereza na Tanzania.
“Hongera sana mheshimiwa Waziri kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani na pia nimefurahi kuja katika ofisini yako kufanya mazungumzo nawe,” alisema Balozi Sara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Lugola, jijini Dodoma leo.
Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke (kushoto) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Lugola, jijini Dodoma leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimkaribisha ofisini kwake jijini Dodoma, Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke kwa ajili ya mazungumzo ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi ya Mzinga na Mkuu wa Chuo cha NIT

KINASA wamekuja na wimbo unaoelimisha jamii juu ya matumizi ya madawa ya Kulevya

$
0
0
Ni mara chache sana kwa vijana kuamua kuandika wimbo unaolenga kuelimisha jamii, mara nyingi sana tumekuwa tukisikia nyimbo za mapenzi au ku-bang na kujirusha lakini kwa namna ya kipekee kabisa kikundi cha Muziki cha Kiswahili na Sanaa (KINASA) wamekuja na wimbo unaoelimisha juu ya matumizi ya madawa ya Kulevya. 

Wimbo huo unaofahamika kama Narudi nyumbani ambao ndani yake umekuwa ukielezea kuwa mwathirika wa madawa sio muhalifu, anahitaji kusaidiwa na sio kutengwa, anahitaji kuheshimika na kuthaminika. Wimbo huo ulioandaliwa na Tanzania Bora Initiative chini za mzalishaji mahiri anyefanya vizuri kwenye game ya muziki (Mocco Geneius) na video kufanya na Adam Juma ambaye ni miongoni mwa ma-director wakubwa sana nchini Tanzania. 


Tembelea Katika link https://www.youtube.com/watch?v=5B7ru4V_mpQ kuona kile ambacho vijana wa kitanzania wanaweza kufanya kwa ajili na Vijana wenzao na nchi yao. Enjoy.

WAZIRI MKUU AZINDUZIA WA MKAKATI NA MPANGO KAZI WA KUJUMUISHA MASUALA YA JINSIA NDANI YA BUNGE

$
0
0
 Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akikata utepe katika hafla ya uzinduzi wa Mkakati na Mpango Kazi wa Kujumuisha Masuala ya Jinsia Ndani ya Bunge iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Shughuli hiyo imeshudiwa na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika, Mhe. Tulia Ackson,  Katibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai na mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Ndugu Godfrey Mulisa.
 Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai kitabu cha Mkakati na Mpango Kazi wa Kujumuisha Masuala ya Jinsia Ndani ya Bunge mara baada ya kuzindua Mkakati huo leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Anayefuata ni Naibu Spika, Mhe. Tulia Ackson na Katibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai, wa kwanza kushoto ni mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Ndugu Godfrey Mulisa.
 Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai wakifurahia uzinduzi wa Mkakati na Mpango Kazi wa Kujumuisha Masuala ya Jinsia Ndani ya Bunge uliofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Wengine ni Naibu Spika, Mhe. Tulia Ackson, Katibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai na wa kwanza kushoto ni mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Ndugu Godfrey Mulisa.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya uzinduzi wa Mkakati na Mpango Kazi wa Kujumuisha Masuala ya Jinsia Ndani ya Bunge uliofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma wengine ni Naibu Spika, Mhe. Tulia Ackson, Katibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai, mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Ndugu Godfrey Mulisa (wa kwanza kushoto), wengine nyuma ni watendaji mbalimbali wa Mradi wa kulijengea Bunge Uwezo (LSP).
 PICHA NA OFISI YA BUNGE

MAHAKAMA KUU TANGA YAJIPANGA KUSIKILIZA NA KUMALIZA MASHAURI KWA WAKATI

$
0
0
Na Amina Ahmad, Mahakama Kuu-Tanga
Mahakama Kuu Kanda ya Tanga imefanya kikao cha kusukuma mashauri (Case flow Management Meeting) na kujadili mikakati mbalimbali ikiwemo namna bora ya kuzuia mashauri kuwa mrundikano na kuondoa vikwazo visivyo vya lazima ili kurahisisha uendeshwaji wa mashauri.
Akiongoza Kikao hicho Novemba 05, Mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Tanga, Mhe. Amiri Mruma aliwataka Wadau kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha lengo lililopo mbele yao.
“Wito wangu kwa Wahe. Majaji na Mahakimu wa Kanda hii ni kufanya vikao vya awali na Wadau (Pre – session meeting) ili kuweza kujadili masuala mbalimbali hususani changamoto za Mashahidi ili kurahisisha uendeshwaji wa mashauri pindi vikao vya Mahakama (Session) vitakapokuwa vinaendelea,” alieleza Mhe. Mruma.
Akisoma taarifa katika kikao hicho, Katibu wa kikao ambaye pia ni Naibu Msajili Mahakama Kuu, Kanda ya Tanga, Mhe. Francis Kabwe alisema, tangu kuanza mwaka 2018 Mahakama Kuu Kanda hiyo imefanikiwa kufanya vikao vitatu (3) vya kesi za mauaji (criminal sessions) ambapo jumla ya mashauri 20 ya usikilizwaji wa awali (PH) yalipangwa kusikilizwa. 
Mhe. Kabwe alisema kati ya mashauri hayo, jumla ya mashauri 12 yaliisha na mashauri 8 yalitolewa maelekezo ya kupangwa katika vikao vijavyo ambapo kati ya mashauri 8, mashauri 6 pia yalimalizika. 
Kwa upande wa mashauri ya mrundikano, Mhe. Kabwe alisema, Mahakama Kuu Tanga ina mashauri 21 yenye umri kati ya miezi 13 – 24 yakiwemo mashauri ya Mahakama ya kazi. 
“Mashauri hayo 21yamewekewa mkakati madhubuti wa kuyaondoa ili kuzuia mrundikano (Back stopping) ambapo tayari kikao kimoja kimeshaanza kusikiliza mashauri hayo mbele ya Mhe. Jaji Mruma na kutarajiwa kumaliza Novemba, 15, 2018,” alisema Mhe. Kabwe.
Aidha; Mhe. Kabwe aliwaeleza wajumbe kuwa kikao kingine kitafanyika kuanzia Novemba 12 hadi Novemba 15, 2018 mbele ya Mhe. Jaji Edson Mkasimongwa. 
Wajumbe waliohudhuria ni kutoka Ofisi ya mwanasheria wa Serikali, Mawakili wa kujitegemea, Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CMA na Taasisi ya kutoa msaada wa kisheria (TAWLA).
 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Tanga, Mhe. Amiri Mruma (aliyesimama) akizungumza na Wadau waliohudhuria katika kikao cha kusukuma mashauri.
 Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Francis Kabwe akiwasilisha taarifa  katika kikao hicho. Katikati ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mhe. Amir Msumi, wa pili kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tanga, Bw. Ahmed Ng’eni, wa kwanza kulia ni Kaimu Mwenyekiti chama cha Mawakili wa kujitegemea (TLS – TANGA CHAPTER), Bi. Linda Lugano na Kushoto niKaimu Mwanasheria wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Tanga, Mhe. Shose Naimani. 
Pichani ni baadhi ya Wadau waliohudhuria kwenye kikao.

MKUU WA MKOA WA KAGERA AMTEMBELEA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti aliyemtembelea na kuzungumza naye maswala yakiwemo ya kibiashara kwa mkoa wa Kagera, kilichofanyika jana jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es salaam kwa mazungumzo.

wafanyakazi watatu wa Kampuni ya Jiangxi Internatiol wahukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 2 jela ama kulipa faini ya Milioni 9.3

$
0
0
 Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kutumikia kifungo cha miaka 2 jela ama kulipa faini ya Milioni 9.3 wafanyakazi watatu wa Kampuni ya Jiangxi Internatiol (T) Investment Ltd baada ya kukiri makosa ya kushindwa kuchukua tathmini ya uaribifu wa mazingira.

Washtakiwa hao ni Injinia Xia Yanan (26), Chen Jinchuan (31) raia wa China  na Mtala Habibu (29) fundi umeme raia wa Tanzania.

Hukumu hiyo imetolewa leo Novemba 7.2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali Nassoro Katuga kuwasomea washtakiwa makosa yao na kukiri.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Shaidi amesema kutokana na washtakiwa kukiri makosa yao anawahukumu kila mmoja kulipa faini ya Shilingi Milioni Tatu na laki moja kwa makosa yote mawili ama kwenda kutumikia kifungo cha miaka miaka 2 gerezani.


Amesema katika kosa la kwanza la kushindwa kuchukua tathmini ya uaribifu wa mazingira,  anawahukumiwa washtakiwa kila mmpja kulipa faini ya Shilingi Milioni 3 ama kwenda jela miaka miwili.


Pia kosa la pili la kutotii amri halali ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), wamehukumiwa kulipa faini ya Shilingi Laki Moja ama jela miaka 2 kila mmoja.


Washtakiwa hao wamefanikiwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kuachiwa huru.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka kosa la kushindwa kuchukua tathmini ya Uaribifu wa mazingira, wamelitenda kati ya January na August 28,2018 maeneo ya Regent Estate Kinondoni ambapo waliendeleza ujenzi bila kuchukua tahadhari ya mazingira kutoka NEMC.

Pia katika kosa la kutotii amri (NEMC), wamelitenda  August 25,2018 maeneo ya Regent Estate Kinondoni Dar es Salaam, ambapo walishindwa kutii amri halali kupitia barua ya NEMC ya kusimamisha ujenzi.


UBA Benki kuwajengea nyumba watoto pacha waliotenganishwa Muhimbili

$
0
0
Mama wa Watoto pacha waliotenganishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo wamekabidhiwa hundi ya shilingi milioni 16 na elfu 80 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ili kuwawezesha watoto hao kuishi katika makazi bora. Msaada huo umetolewa na United Bank for Africa (UBA), ambapo pia watoto hao wamepatiwa bima ya afya ya miaka kumi pamoja na kuwafungulia akaunti yenye akiba ya shilingi milioni mbili.

Akikabidhi msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo amesema mafanikio ya kutenganishwa kwa watoto hao yametokana na maboresho makubwa ya utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

‘’Nawapongeza Muhimbili kwa upasuaji huu wa kihistoria, utoaji wa huduma hapa Muhimbili umeboreshwa sana hata malalamiko yamepungua ili juhudi hizi zisiende bure naahidi Serikali ya Kisarawe tutaendelea kuwafutilia watoto hawa na kuhakikisha yaliyoahidiwa yanatimizwa.’’Amesisitiza mkuu huyo wa wilaya.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema Muhimbili imetumia takribani shilingi milioni 34 kuwahudumia watoto hao katika kuhakikisha upasuaji huo wa ubingwa wa juu unafanyika kwa mafanikio makubwa.

 ‘’Watoto hawa tuliwapokea mwezi wa saba mwaka huu, kama hospitalli tuliona tuangalie namna ya kuwasaidia mara watakaporuhusiwa, hivyo wataalam wetu wa ustawi wa jamii walienda kuona mazingira wanayoishi na kushuhudia mazingira hayo si rafiki hasa kwa watoto hawa ambao wamefanyiwa upasuaji mkubwa’’. Amesema Prof. Museru.

‘’Suala hili tuliamua tulipe kipaumbe ili juhudi zetu za kuwatenganisha zisipotee bure, juhudi zilifanywa tukatafuta misaada kwa wadau mbalimbali  tunamshukuru sana Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kwa juhudi zake hatimaye suala hili leo limefanikiwa’’. Amesema Prof. Museru.

Pia, Prof. Museru amesema MNH iatendelea kuwapatia matibabu bure watoto hao mpaka pale watakapofikia umri wa kujitegemea katika Maisha yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA Bwan. Usman Isiaka ameeleza kuwa waliona mazingira wanaoshi wazazi wa watoto hao yanachangamoto hivyo wakaamua kuwasaidia ili wapate makazi bora.

‘’UBA benki itashiriki kwenye ujenzi, itasimamia na kuhakikisha ujenzi wa nyumba hiyo mpaka unakamilika. Natoa wito kwa wadau wengine pamoja na watu binafsi kuendelea kuwachangia watoto hawa kwani wanaendelea kukua na watahitaji kwenda shule’’. Amesema Mkurugenzi huyo wa benki ya UBA.

Upasuaji wa kuwatenganisha watoto walioungana ulifanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa mara ya kwanza mwaka 1994.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kabla ya kumkabidhi Ester Simon na mumewe, Michael Mkono hundi ya Tshs. 16,080,000 leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru, Mkurugenzi Mtendaji wa UBA, Usman Imam Isiaka na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa benki hiyo, Dominick Timothy.
Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza kwenye mkutano huo leo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo.
Michael Mkono ambaye ni mume wa Ester Simon akiwa kwenye mkutano huo leo kabla ya kukabidhiwa hundi hiyo.
Ester Simon akiwashukuru wataalam wa Muhimbili kwa kumpatia matibabu ya kibingwa pamoja na uongozi wa UBA benki kwa kumkabidhi hundi ya fedha za ujenzi wa nyumba ya kisasa.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images