Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live

KOCHA MATTHEW McCOLLISTER JUSAKA VIPAJI VYA WACHEZAJI WADOGO WA KIKAPU KESHO JMK PARK

0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Rais wa  Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) Phares Magesa amesema kuwa  Kocha wa Kikapu Matthew McCollister ataendesha mafunzo kwa vijana na kusaka vipaji. 

Mafunzo hayo yatakayoendeshwa  7 Novemba yataanza  saa 3 asubuhi  na kutakuwa na ufunguzi wa mafunzo ya vijana ya kikapu, yatakayoendeshwa na Kocha huyo Matthew McCollister ambaye ni Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Marekani.

Mafunzo hayo yatafanyika viwanja vya JMK Youth Park, Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni tarehe 7 na 8, Novemba, 2018.

Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) linaomba vijana wote wanaopenda kushiriki katika mafunzo haya wafike JMK Park ili kufaidika na mafunzo hayo, ambapo pia Kocha huyo atachagua baadhi ya vijana wenye vipaji ambao watapatiwa nafasi ya kufanya mafunzo zaidi nchini Marekani.

Tayari Kocha huyo amefanya mafunzo kama haya Arusha tarehe 3 - 5 Novemba, 2018.

TBF inaishukuru Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya habari, utamaduni, sanaa na Michezo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kituo cha michezo cha JMK Youth Park na wadau wengine kwa kufanikisha mafunzo na ziara hii Kocha Matthew.

TAIFA STARS YAELEKEA SAUZI KUWEKA KAMBI YA SIKU 10

0
0
Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imeondoka leo alfajiri kuelekea nchini Afrika Kusini kuweka Kambi kujiandaa na mchezo wake wa kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon 2019 dhidi ya Lesotho.


Kambi hiyo ya siku 10 itakuwa katika Mji wa Bloemfontein kabla ya kikosi hicho kuelekea mjini Maseru,Lesotho.

Taifa Stars ipo nafasi ya pili katika kundi L ikiwa na alama 5 nyuma ya vinara Uganda wenye alama 10 wakati Cape Verde wapo nafasi ya tatu wakiwa na alama 4 na Lesotho wakiburuza mkia na alama mbili.

Mchezo dhidi ya Lesotho unataraji kuchezwa Novemba 18,2018 mchezo ambao utatoa taswira ya Taifa Stars kufuzu kucheza Afcon mwakani itakayofanyika Cameroon.


Wachezaji walioitwa kujiunga na kikosi hicho kinachodhaminiwa na Bia ya Serengeti ni

Aishi Salum Manula (Simba SC)

Shomari Salum Kapombe (Simba SC)
Ally Abdulikarim Mtoni (Lipuli FC)
Kelvin Patrick Yondani (Young Africans)
Gadiel Michael Kamagi (Young Africans)
Benno David Kakolanya (Young Africans0
Benedict Tinocco Mlekwa (Mtibwa Sugar)
Agrey Morris Ambross (Azam FC)
Mudathir Yahya Abbas (Azam FC)
Yahya Zayd Omari (Azam FC)
Simon Happygod Msuva (Diffa Eljadida – Morocco)
Erasto Edward Nyoni (Simba SC)
Himid Mao Mkami (Petrojet – Egypt)
Abdi Hassan Banda (Baroka FC – South Africa)
Aron Ally Kalambo (Tz Prisons)
Rashid Yusuf Mandawa (BDF – Botswana)
Salum Mashaka Kimenya (Tz Prisons)
Feisal Salum Abdallah (Young Africans)
Abdallah Salu Kheri (Azam FC)
John Raphael Bocco (Simba SC)
Mbwana Samatta (Genk – Belgium)
Abubakar Salum (Azam FC)
Jonas Mkude (Simba SC)
Thomas Ulimwengu (Alhilal – Sudan)
Hassan Ramadhan Kessy (Nkana Ranger – Zambia)
Shaban Idd Chilunda (Tenerife FC – Spain
Shiza Ramadhan Kichuya (Simba SC)

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

TAARIFA YA KINA YA MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA NA MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI YA MWAKA 2019/20

0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akiwasilisha Hotuba ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/2020 bungeni leo jijini Dodoma.

ZIARA YA JUKWAA LA WANAWAKE WILAYA YA MKURANGA YAJA NA FURSA YA MKOPO BILA RIBA

0
0
Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MWENYEKITI wa Jukwaa la wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega ameendelea na ziara yake iliyolenga kuhamasisha kuwainua wanawake kiuchumi kupitia jukwaa hilo.

Akizungumza na wanawake akiwa ziarani katika kijiji cha Mwandege bi. Mariamu amesema kuwa lengo la kufanya ziara hiyo kuwafahamisha wanawake kuhusiana majukumu yanayofanywa na jukwaa hilo tangu kuanzishwa kwake.

Amesema kuwa akiwa kama mweyekiti wa Wilaya hiyo atahakikisha fursa za kiuchumi zinawafikia ili waweze kuendeleza shughuli zao za kijasiriamali.Kuhusiana na mikopo kwa wanawake bi. Mariamu amesema kuwa wanachotakiwa kufanya ni kuendeleza miradi yao ili waweze kupata mikopo katika halmashauri zao bila riba.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Mwandege Adolf Kowero amesema kuwa amekuwa akifarijika na juhudi za akina mama hao na kuhusu ahadi ya eneo alilohaidi kwa ajili ya biashara lipo tayari na ramani imeandaliwa ambapo soko kubwa litajengwa kwa ajili ya wanawake na vijana.

Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega akizungumza na wajasiriamali wa kata ya Mwandege ,ambapo amewaomba kufanya kazi kwa waminifu ili waweze kunufaika na kazi zao na kuongeza pato la Taifa.
Diwani wa kata ya Mwandege wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani,Adolf Kowero akizungumza na wajasiriamali wa kata hiyo.
Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya Mkuranga,Mariam Ulega akiwakabidhi viongozi wa kata ya Mwandege laki nne na doti 20 za kanga kwajili ya mtaji wa vikundi mbalimbali vya kata hiyo.
Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya Mkuranga,Mariam Ulega akiwaunga mkono wajasiriamali wa kata ya Mwandege.(Picha na Emmanuel Massaka MMG)
Sehemu ya wajasiriamali wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika kata ya Mwandege wilayani Mkuranga Mkoani wa Pwani.

ALIYOYAZUNGUMZA KATIBU MKUU DKT JINGU WAKATI AKIZUNGUMZA NA WATUMISHI WA WIZARA

Muonekano wa kisanifu wa New Ubungo Intersection

JUKWAA LA WAKULIMA ARUMERU LAPATA NEEMA

0
0

Na. Vero Ignatus, Arumeru. 

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro amejitolea kuwasadia kuandika Maandiko ya kibiashara wananchi wanaotaka kufanya Kilimo na Ufugaji wa Kibiashara ili waweze kukopesheka na Ta asisi za kifedha 

Amesema hatua hiyo imefikia baada ya kubaini kuwepo kwa vikwazo katika maandiko katika hatua za awali kwani Taasisi hizo kabla ya kutoa msaada au mkopo huitaji mchanganuo, andiko la kibiashara kwanza kabla ya kuwawezesha wananchi ambao wanataka kuanza kilimo au ufugaji wa kibiashara.

Wanapoanza safari ya kutimiza ndoto zao za kuwekeza katika sekta hizo, ambapo baada ya kubaini uwepo wa vikwazo hivyo aliamua kujiongeza Kwa kutafuta wadau ambao atashirikiana nao katika kuwasaidia wananchi kuondoa Vikwazo hivyo.

Mhe Muro amesema tayari kampuni Binafsi ya Wawezeshaji wa wakulima (PASS)Private Agricultural Sector Support imekubali kuwaandalia na kugharamia Mpango kazi wa kibiashara zitakazowasaidia Wakulima na Wafugaji katika kupata Mkopo katika Taasisi za Kifedha hali ambayo itawasaidia katika uendelezaji wa Kilimo chenye tija na ufugaji wa kibiashara. 
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akipata maelezo ya bidhaa kutoka kwa mmoja wa mkulima katika maonyesho ya wakulima wilayani hapo. 
DC Muro akizungumza na wakulima katika maonyesho hayo ya kilimo yaliyoanza tarehe 1-3 Novemba 2018 wilayani humo. 
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na wakulima na wananchi wa wilaya hiyo katika maonyesho hayo ya wakulima
Mmoja kati ya mkulima. Wilayani humo akimpatia maeleza ya mbegu ya mahindi kama inavyoonekana katika picha Mkuu wa wilaya Jerry Muro katika maonyesho hayo
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro akiwa katika picha ya pamoja na wakulima katika maonyesho hayo ya wakulima Meru. 



Naibu Balozi wa Israel Nchini Mhe. David Eyal Atembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

0
0
Na Genofeva Matemu – JKCI.

Zaidi ya watoto 750 wenye matatizo ya moyo hapa nchini wamefaidika na matibabu ya moyo kutoka kwa wataalam wa Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel tangu mwaka 1999.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Balozi wa Israel hapa nchini mwenye makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. David Eyal alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuangalia kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na madaktari bingwa kutoka SACH kwa kushirikiana na JKCI.

Mhe. Naibu Balozi Eyal alisema watoto hao kutoka Tanzania Bara na Visiwani walifanyiwa uchunguzi na kutibiwa hapa nchini wale ambao walikutwa na matatizo yanayohitaji utaalamu wa hali ya juu walipelekwa nchini Israel kwa ajili ya matibabu zaidi. Gharama za usafiri na matibabu ziligharamiwa na Serikali ya Israel.

“Kujitoa kwa wataalam kutoka Shirika la SACH kuja Tanzania kufanya uchunguzi na matibabu kwa watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo ni ubalozi wa kweli wa kuitangaza nchi ya Israel kwa vitendo, ni matarajio yetu kuwa huduma hii itakuwa endelevu na kuendelea kuokoa maisha ya watoto wetu wengi zaidi”, alisema Mhe. Naibu Balozi Eyal.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David alipotembelea Taasisi hiyo jana (5/11/2018) kwa ajili ya kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. Jumla ya watoto 85 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua. 
Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akiongozana na mkuu wa kitengo cha ufundi na matengeneza cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mhandisi Abella Rwiguza akielekea kuangalia ukarabati wa jengo jipya la watoto la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea Taasisi hiyo jana (5/11/2018) kwa ajili ya kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. 
Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akiangalia kipimo kinachoonyesha jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO Cardiogram) alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwa ajili ya kuangalia kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto(Save a Child Heart – SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. 
Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akiongea na wazazi wa watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. Jumla ya watoto 85 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua

NOT TO BE MISSED EVENT IN CANTON, MICHIGAN, USA KESHO....!

MAANDALIZI YA UJENZI WA BARABARA YA NJIA SITA YA KUTOKA KIMARA HADI KIBAHA YAIVA

0
0
Muonekano wa barabara ya Morogoro eneo la Kimara mwisho Jijini Dar es salaam hivi leo ambapo tayari maandalizi  ya ule mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Ubungo hadi Kibaha Mkoani Pwani yenye urefu wa kilometa 16 umeiva. Ujenzi wa barabara hiyo unaotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka huu utasaidia kukuza uchumi kwa kuongeza kasi ya usafirishaji wa bidhaa katika nchi jirani kupitia bandari ya Dar es Salaam.  Pia inatarajiwa utasaidia kupambana na changamoto ya msongamano wa magari na kuziwezesha barabara zote za Jiji la Dar es Salaam kupitika katika majira yote ya mwaka.  Picha na IKULU

Unesco yataka juhudi zaidi za walimu kuinua elimu

0
0
Na Mwandishi wetu,
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limewataka walimu nchini kuendeleza juhudi wanazozionyesha katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi ili kuendelea kuinua kiwango cha elimu kinachotolewa nchini.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa kitengo cha Elimu kutoka UNESCO, Faith Shayo wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo mbalimbali kwa walimu na wadau iliyofanyika katika ukumbi wa kituo cha ‘America Corner’ uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Tuzo hizo zimeandaliwa maalumu kwa ajili ya kutambua michango mbalimbali ya walimu hao katika ufundishaji na maeneo mengine ambayo kimsingi yanaleta tija katika kukuza maendeleo ya Taifa.
Alisema licha ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo, walimu nchini wamekuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa majukumu yao na kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri katika masomo yao, suala alilowataka kutokufa moyo na badala yake kuongeza bidii.
“Sote tunashuhudia namna ambavyo walimu wanavyojitahidi kutimiza wajibu hao kikamilifu kila siku licha ya changamoto mbalimbali zinazowakabili, nitumie nafasi hii kuwapongeza kwa utekelezaji wa majukumu yenu katika kuinua maendeleo ya Taifa” alisema Faith.
Alisema tuzo hizo zinapaswa kuchukuliwa kama changamoto na walimu hao kwa kufanya vizuri wakati wote wanapotimiza wajibu wao wa kazi, hatua ambayo pamoja na sababu mengine zitawafanya wazidi kupata mafanikio.
Aidha alimpongeza muandaaji wa tuzo hizo Raymond Luanda kwa kubuni wazo hilo lililolenga kutambua mchango wa walimu nchini, suala alilosema kuwa kwa kiasi kikubwa litazidi kuwapa moyo wa kazi walimu hao.
Awali muandaaji wa tuzo hizo Raymond Luanda, alisema ‘How is My Teacher’ ni wazo alilolibuni kwa ajili ya kutambua mchango unaotolewa na walimu wote hapa nchini ikiwa na lengo la kuwahamasisha kuongeza msukumo katika utekelezaji wa majukumu yao ya ufundishaji.
Alisema tuzo hizo ambazo ni mara ya kwanza mwaka huu, zinatarajiwa kuwa endelevu kila mwaka kwa lengo la kuendeleza utamaduni wa kutambua mchango wa walimu hao.
Jumla ya tuzo kumi zilitolewa kwa walimu mbalimbali waliopatikana kupitia mchakato maalumu wa uliowahusisha wanafunzi  kupendekeza walimu wao na baadae kupigiwa kura.
 Mgeni rasmi Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo akizungumza na walimu pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati hafla ya utoaji tuzo na kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mwanzilishi wa tuzo za walimu (HIMT Awards), Bw. Raymond Luanda akizungumzia mchakato uliopitiwa mpaka kuwapa washindi wakati hafla ya utoaji tuzo na kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mwalimu wa Shule ya Sekondari Msimbazi ambaye pia ni Mwalimu wa Elimu maalum wa shule ya walemavu Kimanga Sekondari , Bi. Sylvia Ruambo akielezea furaha yake baada ya kupokea tuzo wakati hafla ya utoaji tuzo na kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo (kushoto) akimkabidhi tuzo mshindi wa kategori ya mtu aliyefanya vyema katika utoaji wa huduma za elimu, Bi. Sylvia Ruambo (katikati) wakati hafla ya kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mwanzilishi wa tuzo za walimu (HIMT Awards), Bw. Raymond Luanda
 Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo akimkabidhi tuzo mshindi wa kategori ya mtu aliyewezesha changamoto kuondolewa katika utoaji wa huduma za elimu kutoka Visiwani Zanzibar, Bw. Ami Vuai (katikati) wakati hafla ya kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu nchini iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mwanzilishi wa tuzo za walimu (HIMT Awards), Bw. Raymond Luanda
 Mgeni rasmi Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo (kushoto) akimkabidhi tuzo mshindi wa kategori ya mtu wa mfano katika utoaji wa huduma za elimu nchini, Bw. John Bosco (katikati) wakati hafla ya kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu nchini iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo kwenye jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mwanzilishi wa tuzo za walimu (HIMT Awards), Bw. Raymond Luanda.
 Mgeni rasmi Mgeni rasmi Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu walioshinda tuzo pamoja na wawakilishi wakati hafla ya kutambua michango inayotolewa katika huduma za elimu nchini iliyoandaliwa na ‘HIMT AWARDS’ na kufanyika kwenye ukumbi wa America Corner uliopo kwenye jengo la Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MADAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA WATOTO KUTOKA SAUDI ARABIA WATUA MUHIMBILI

0
0
Jopo la Madaktari bingwa na wataalamu wa magonjwa ya watoto wamefika katika Hopitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuendesha kambi ya matibabu ya hiyari kwa watoto wadogo na wachanga wanaozaliwa katika Wodi ya Watoto ya Hospitali ya Muhimbili.
Kambi hii ya matibabu itadumu kwa muda wa juma moja kuanzia tarehe 5 Novemba. 2018.
Madaktari hawa wamekuja Tanzania kwa mpango wa matibabu ya hiyari unaoratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Taasisi ya Misaada ya Kijamii ya PELEKS na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kambi tiba kama hii hufanyika mara nne kwa mwaka.
Pamoja na kufanya matibabu ya bure kwa watoto pia madakatari hawa wamekuja na vifaa tiba kadhaa zikiwemo ventilators ambavyo vimetolewa msaada kwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoka King Faisal Specialist Hospital (KFSH) ya Riyadh.
  Madaktari bingwa kutoka Saudi Arabia wakiwa kazini na madaktari wenyeji katika wodi ya watoto kambi hii ya matibabu itadumu kwa muda wa juma moja kuanzia tarehe 5 Novemba  2018.
 Baadhi ya Madaktari Bingwa kutoka Saudi Arabia wakijadiliana na madaktari wenyeji wa Wodi ya watoto.
 Maelekezo na majadiliano yakiendelea.
 Mmoja wa Wataalamu kuto Saudi Arabia akitoa maelezo mafupi kwa watendaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kambi hii ya matibabu itadumu kwa muda wa juma moja kuanzia tarehe 5 Novemba. 2018.

KAILIMA AKUTANA NA WASEMAJI NA WAKUU WA TEHAMA WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI

0
0
Naibu  Katibu  Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ramadhani Kailima amekutana na  Wasemaji na Wakuu wa vitengo vya Tehama wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kikao kilichofanyika Dar es Salaam, na kuwataka watendaji hao kuboresha mifumo ya utoaji  taarifa na elimu kwa umma ya Idara zao.  
Katika kikao hicho kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Wakimbizi Wizara ya Mambo ya Ndani, Kailima amewataka watendaji hao kukaa na kutengeneza mfumo wa pamoja utakaoziunganisha Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi ya katika kutoa taarifa na elimu kwa umma hasa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi  wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020. 
Amewataka Wasemaji na Wakuu wa hao wa vitengo vya Tehama kuhakikisha kuwa wanaihabarisha jamii kuhusiana na matukio na shughuli zinazofanywa na Idara zao ili jamii ipate ufahamu wa kutosha kuhusiana na majukumu ya idara hizo.
Wasemaji na Wakuu wa vitengo vya Tehama waliohudhuria kikao hicho ni wa kutoka Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya Uhamiaji. 
 Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima akiongea  na Wasemaji na Wakuu wa vitengo vya Tehama wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza Naibu katibu mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani ya Nchi katika kikao kilichofanyika Dar es Salaam

Wasemaji na Wakuu wa vitengo vya Tehama wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza Naibu katibu mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani ya Nchi (hayupo Pichani) (Picha na Jeshi la Polisi)

NMB YASAIDIA VITANDA 9 KITUO CHA AFYA KIGAMBONI

0
0

BENKI ya NMB imetoa msaada wa vitanda tisa vya wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Kigamboni vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni tano. Vitanda hivyo sita (6) vikiwa vya wagonjwa wa kawaida na vitatu (3) vikiwa maalum kwa ajili ya kujifungulia kwa wajawazito, vimekabidhiwa leo kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija.

Akikabidhi vitanda hivyo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd alisema msaada huo ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa NMB kurejesha faida kidogo kwa jamii. Alisema Benki hiyo, hutenga takribani bilioni moja fedha ambayo hurejesha kwa jamii kwa kusaidia sekta za afya, elimu na masuala mengine yanayoikumba jamii kama maafa na majanga.

Alisema Benki ya NMB inaunga mkono juhudia za Serikali za kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo afya kwa wananchi, ili jamii ambao ni sehemu ya wateja wa benki hiyo wawe na afya njema."..Kama tunavyojua afya ni huduma ya msingi kwa jamii wakiwemo wateja wetu, hivyo tuna kila sababu ya kuisaidia pale tunapopata fursa ya kufanya hivyo," alisema Bw. Badru Idd katika hotuba yake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija akipokea msaada huo aliipongeza Benki ya NMB kwa juhudi zake za kuendelea kusaaidia sekta mbalimbali za huduma za kijamii. Aliziomba taasisi nyingine kuiga mfano wa Benki ya NMB kutoa sehemu ya faida yake kusaidia jamii ili kuchochea maendeleo ya taifa. Alisema Serikali inapambana katika kuhakikisha inaboresha huduma za afya kwa wananchi, lakini haiwezi kufanikiwa kwa kiwango kikubwa bila kushirikiana na wadau wengine kama ilivyofanya NMB kutoa msaada kwenye kituo hicho cha afya.

Naye Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Kigamboni, Dk. Julius Nyakazilibe alisema msaada wa NMB umefika wakati muafaka kwani kwa sasa kituo kinapanua huduma zake ikiwemo kuongeza majengo hivyo vitasaidia kuziba mapengo yanayojitokeza.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (wa pili kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitanda vya wagonjwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija (wa pili kushoto) vilivyotolewa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni viongozi wa NMB. 
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija akimshukuru meneja wa NMB Tawi la Kigamboni mara baada ya kupokea msaada huo wa vitanda. 
Sehemu ya vitanda vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa Kituo cha Afya cha Kigamboni jijini Dar es Salaam. Vitanda hivyo sita (6) vikiwa vya wagonjwa wa kawaida na vitatu (3) vikiwa maalum kwa ajili ya kujifungulia wajawazito vinathamani ya shilingi milioni tano. 
Sehemu ya viongozi wa Kituo cha Afya cha Kigamboni cha jijini Dar es Salaam wakifurahiaa sehemu ya msaada pamoja na viongozi wa NMB waaliokabidhi msaada huo. Vitanda hivyo sita (6) vikiwa vya wagonjwa wa kawaida na vitatu (3) vikiwa maalum kwa ajili ya kujifungulia wajawazito vinathamani ya shilingi milioni tano

WATAALAM WANAWAJIBU WA KUINGIZA UTAALAM KATIKA UCHUMI WA VIWANDA

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
CHUO Kikuu Mzumbe kimesema watalaam katika sekta mbalimbali wanawajibu kuingiza uwezo wao katika uchumi wa viwanda ili kuendana na malengo ya serikali.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi wakati wa kikao cha maafisa rasilimali watu kilichofanyika Chuoni hapo, amesema watalaam katika kada mbalimbali wanahitaji kutambua na kufungua fursa katika sekta ya viwanda katika kuhakikisha nchi inafikia malengo.

Amesema kuwa Chuo kimekuwa kikiendesha Program katika kada zinazozalishwa katika chuo ili kuhakikisha watalaam wanapeleka ujuzi wao ambao utasaidia taifa kuvuka mipango yake ya kufika kwenye uchumi wa viwanda vya ndani.

Profesa Ngowi amesema kuwa maafisa Rasilimali watu wanawajibu wa kuhakikisha kila anayefanya kazi katika viwanda anapanda kutokana na taratibu zilizowekwa ili kukidhi mahitaji ya wafanyakazi.

Kwa upande wa Mratibu wa Program hiyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam Dkt Faisal Issa amesema kuwa maafisa Rasilimali watu ni watu muhimu katika mapinduzi ya uchumi wa viwanda na usimamizi wa maslahi ya wafanyakazi kwa kufuata misingi iliyowekwa.

Issa amesema kuwa wafanyakazi wanatakiwa kupanda cheo ikiwa ni pamoja na kusimamia masilahi yao katika kuhakikisha viwanda hivyo vinazalisha na kufikia malengo.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi akizungumza katika kikao cha maafisa Rasilimali watu kilichofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Program za  kujengea uwezo wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe  Mhadhiri Dkt Faisal Issa akizungumza  kuhusiana na kikao hicho kwa maafisa rasilimali watu kilichofanyika Chuo Kikuu Mzumbe jijini Dar es Salaam.
 Mwendeshaji wa Mdahalo wa Maafisa Rasilamali Watu Carl Bosser akitoa maalezo kuhusiana na mdahalo kwa maafisa kilichofanyika Chuo Kikuu Mzumbe jijini Dar es Salaam.
 Meza kuu wakijibu maawali ya wadau mbalimbali
Picha ya Pamoja maafisa wa Rasilamali Watu na Watendaji wa Chuo Kikuu Mzumbe

WAHITIMU MAJENGO SEC. 2000 WASAIDIA YATIMA, DAR, MWANZA NA KILIMANJARO

0
0
Mmoja wa wakilishi wa Kundi la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro, Eng. Willbard Gandu (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada wa wanafunzi hao katika kituo yatima cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wakilishi wa Kundi la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro, Injinia Eng. Maeda (kulia) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo yatima cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam sehemu ya msaada uliotolewa na wanafunzi hao.
Mmoja wa viongozi wa kundi hilo la wanafunzi waliohitimu Sekondari ya Majengo, Joachim Mushi (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha watoto yatima ‘Green Pastures’, Mchungaji Douglas Kiseu sehemu ya msaada uliotolewa na kundi lao.
Mmoja wa wakilishi wa Kundi la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro, Bw. Oswald (kulia) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo yatima cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam sehemu ya msaada uliotolewa na wanafunzi hao.
Mmoja wa viongozi wa Kundi la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya Majengo, Bi. Grace Minja (kulia) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo yatima cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam sehemu ya msaada uliotolewa na wanafunzi hao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BALOZI MPYA WA KUWAIT NCHINI AJITAMBULISHA KWA MAKAMU WA RAIS LEO JIJINI DODOMA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi mpya wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohammed Faleh ALSEHAIJAN aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais Kilimani jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi mpya wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohammed Faleh ALSEHAIJAN aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais Kilimani jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohammed Faleh ALSEHAIJAN aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais Kilimani jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi mpya wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohammed Faleh ALSEHAIJAN aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais Kilimani jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

DC Makete aagiza kuchapwa bakola kwa wanaovaa nguo zinazoacha maungo wazi

0
0
Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe Veronika Kesi ametoa amri ya kupewa adhabu  ya kuchapwa viboko kwa vijana au mtu yeyote atakaye onekana kuvaa mavazi yasiyo na staha katika jamii ya wakazi wa Makete.
  
Mkuu wa wilaya ametoa agizo hilo alipo kuwa katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi wa kata za Iniho na Kipagalo ambapo amesema mavazi hayo sio maadili ya wakazi wa wilaya yake  pamoja na Tanzania kwa Ujumla.

Bila kueleza idadi gani ya viboko itolewe kwa vijana wakiume wanaovaa suruali mlegezo (chini ya makalio) au wasichana kuvaa mavazi yanayobana au yanayoonesha maumbile yao au mavazi yanayochora miili yao wachapwe viboko tangu kutolewa kwa amri hiyo wakati akizungumza na wakazi wa kata hizo.

''Nataka kuona vijana suruali zenu zinashuka kutokana na wallet kuwa nzito umefanya shughuli zako huko walleti imejaa hela ndio ina inashusha sio kushusha tu ni viboko nasisitiza ni viboko wakati sheria za adhabu zingine zikiendelea kutungwa huko kwenye kata''

Amesema kuwa kuanzia sasa viboko vianze kuchapwa kwa kila mtu atakaye vaa hivyo na kumtaka mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Makete  Godfrey Gogadi kushirikiana na serikali za vijiji kutunga sheria itakayomhukumu na kupewa adhabu kwa watu wa aina hiyo.

''huu ni utamaduni wa wapi?? sie wabantu hatuna utamaduni huo naagiza mkimkamata chapa viboko tu,watoto wetu hao!''

Kwa upande wake wake Mwanasheria bw Godfrey Gogadi amesema ameshaanza kuwasiliana na viongozi wa serikali ili kuanza kutunga sheria ndogondogo za kusimamia agizo hilo.

''Tumeanza kukusanya maoni ya Wadau kwa watendaji ili kutunga sheria hizo ndogodndogo kama mkuu alivyosema ila wakati hilo likiendelea viboko viendelee maana anavyo vaa chini ya makalio anakwambia anataka viboko hivyo nikupiga Tu''

Aidha Mkuu huyo wa wilaya akiendelea kusikiliza kero za wananchi amesistiza kuwalea watoto katika maadili na kuwalinda dhidi ya ukatili ikiwemo ubakaji na mimba za utotoni.

ALIKIBA AKUBALI KUSHIRIKI WASAFI FESTIVAL, MOFAYA KUDHAMINI TAMASHA HILO

0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


Msanii wa muziki wa Bonofleva Ali Kiba amemjibu msanii mwenzake Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz'  kuptia ukurasa wake wa Instagrama kuwa amekubali mualiko wa kwenda kushiriki katika tamasha la Wasafi Festival.


Katika ujumbe wake Ali Kiba amesema kuwa, ameshurukuru kwa kupata mualiko wao ila hataweza kushiriki kutoakana na kuwa na majukumu mengine ya kuzindua kinywaji chake ch Mofaya Energy.

Mbali na hilo Kiba amemuomba Diamond kudhamini tamasha hilo ili kusongesha gurudumu la muziki wa Tanzania.

"Pia ndugu zangu #Wasafi tumepata salamu zenu, nashukuru kwa mualiko wenu, ila kwa bahati mbaya sitoweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi zingine. Hata hivyo tusingependa kuwaacha hivi hivi, tupo tayari kuwapa support ya kudhamini tamasha lenu kupitia #MofayaEnergyDrink ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Africa . Management #RockstarAfrica yangu tutaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya hili jambo kubwa "
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live




Latest Images