Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

UINGEREZA KUSAIDIA JUHUDI ZA TANZANIA KUONGEZA IDADI YA WATALII KUPITIA ATCL

0
0
Naibu Katibu Mkuu Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki akimkabidhi majarida na vipeperushi vya utalii wa Tanzania (promotional materials) Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza katika masuala ya biashara, Andrew Rosindell .

Na Geofrey Tengeneza

Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza katika masuala ya biashara Mheshimiwa Andrew Rosindell ameahidi kusaidia kufanikisha mpango wa Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) kufanya Safari zake London, Uingereza.

Mheshimiwa Rosindelli alitoa ahadi hiyo jana alipokutana na kuwa na mzungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa WIzara ya Maliasili na Utalii Dkt Aloyce Nzuki katika maonesho ya utalii ya World Travel Market yanayoendelea jijini London Uingereza ambapo alimuomba mwakilishi huyo kusaidia mpango huo ambao alisema utasaidia sana kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania kutoka Uingereza.

Aidha Dkt.Nzuki amemuomba Mheshimiwa Rosindell kuandaa mkutano wa pamoja baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uingereza mapema iwezekanavyo ili kujadiliana namna ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uingereza kwa manufaa ya nchi hizo mbili.

Aidha, Dkt.Nzuki ameweza kukutana na kufanya mazungunzo na Mjumbe maalum ambaye pia ni Mbunge wa nchi hiyo Andrew Rosindell ambaye ni mbunge aliteuliwa na Waziri Mkuu huyo kuwa Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza wa masuala ya Biashara (Trade Envoy) ambaye miongoni mwa kazi zake ni kukuza biashara, uwekezaji na Utalii baina ya Uingereza na Tanzania.
Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza katika masuala ya biashara, Andrew Rosindell akisoma moja ya majarida ya utalii alipotembelea banda la Tanzannia katika maonesho ya World Travel Market jijini London Uingereza.

Katika hatua nyingine Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dkt.Hamisi Kigwangalla amepongeza timu ya Tanzania inayoshiriki maonyesho hayo kwa kazi nzuri ya kuitangaza vyema Tanzania kama eneo bora la utalii Afrika na Duniani kwa ujumla.

Kupitia ukurasa wake Twitter aliandika "hii ni taswira ya leo ya banda letu la maonesho kule jijini London, kwenye World Travel Market (WTM), Uingereza, ambapo slogan yetu ya Tanzania: Unforgettable! imetumika ipasavyo kuuza vivutio vyetu. Nawapongeza sana washiriki wote kutoka Tanzania na wa Kamati yetu ya Destination Branding chini ya uenyekiti wa Ndg. Devotha Mdachi kwa kazi nzuri. Huu ni mwanzo tu” aliandika DKt Kingwangala.

Ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo umeratibiwa na Bodi ya Utalii Tanzania –TTB ambapo timu ya washiriki kutoka Tanzania ikijumuisha waoneshaji kutoka sekta ya umma na binafsi inaongozwa inaongozwa na Naibu Katibu MKuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki.

MAFUNZO YA KUKOMESHA BIASHARA YA USAFIRISHAJI HARAMU YA BINADAMU YAFUNGULIWA RASMI .

0
0
          Na Khadija Seif,Globu ya Jamii.
Mafunzo ya elimu ya kutokomeza biashara haramu ya usafirishaji binadamu yafunguliwa rasmi jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na majaji wa nchini Tanzania pamoja na wawakilishi kutoka nchi ya Afrika Kusini na Marekani.

Mafunzo hayo ya siku tatu yataendeshwa na Wizara ya Mambo kwa majaji wa Nchini Tanzania, na wawakilishi kutoka Afrika Kusini na Marekani.

Jaji Mfawidhi wa  Mahakama Kuu ya Tanzania Beatrice Mutungi ameeleza lengo la mafunzo hayo kupatiwa kwa majaji ili kupunguza kasi na kutokomeza biashara hiyo haramu ya usafirishaji binadamu.

Jaji Mutungi amesema kuwa waashiriki hao wametoka sehemu mbalimmbali nchini  ambao ni  hakimu mkazi kutoka mikoani kama Arusha,Tanga,Lindi,Mtwara,Iringa na Dar es salaam na kuwapa fursa ya kupata uelewa mkubwa zaidi ili kutoa adhabu na hukumu ambazo zitastahili kwa watuhumiwa wanaojihusisha na biashara hizo haramu.

Mutungi amefafanua kwakina kuwa biashara hizo zinaambatana na uongo ambao unaowafanya walezi au wazazi wa vijana kutoa ruhusa kwa vijana wao  kwa wafanyabiashara hiyo haramu na kutoa ahadi za kuwasomesha wakifika mijini  na wakifika mambo hubadilika na kufanyiwa biashara za usiku za mabaa, na wengine kufanyishwa biashara ya kuuza mwili (uchangudoa)

Alikadhalika Mutungi amewapongeza washiriki wote na anatumaini elimu hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza na kutokomeza biashara haramu ya usafirishaji binadamu.

Hata hivyo serikali inaendelea na mikakati ya kukamatwa maharamia wote wa ndani na nje ya nchi kwani ndio wanaoendelea kuumiza nguvu kazi ya  Taifa.

Mwenyekiti wa Kuzuia na Kupamabana na biashara haramu ya usafirishaji binadamu ADASTUS MAGERE amesema mafunzo hayo yamekuja kipindi hiki kutokana na kushamiri kwa kesi nyingi za mauaji,mimba za utotoni,utekaji.

Magere amewaambia watanzania kuwa licha  ya mimba za utotoni bali pia wasichana pamoja na  wavulana wa umri mdogo wamekua wakihamishwa vijijini kwenda mijini kwa ajili ya kutumiwa Kwenye biashara haramu kama kujihusisha na uchangudoa, uhalifu ikiwemo ujambazi.

Kutokana na biashara hiyo haramu kunawanyima vijana wengi haki zao za msingi kwani wengi wana umri mdogo ambapo wangekua mashuleni na vitendo hivo vinatokea kutokana na umasikini kwa jamii na familia zao kutokumudu gharama za kimaisha na kulazimika vijana wadogo kutafuta maisha sehemu zingine na hata nje ya nchi.

MBUNGE MUNDE TAMBWE AMWAGA CHECHE BUNGENI DODOMA LEO PART ll

MBUNGE MUNDE TAMBWE AMWAGA CHECHE BUNGENI DODOMA LEO PART l

WASEMAVYO MAJAJI WAKUU KATIKA MIAKA 3 YA RAIS MAGUFULI MADARAKANI

WASEMAVYO MARAIS WAASTAAFU KATIKA MIAKA 3 YA RAIS MAGUFULI MADARAKANI

UJENZI WA RELI YA KISASA SGR KURUSHWA LIVE NA TBC,MKURUGENZI KADOGOSA KUUNGURUMA NA WAHANDISI SOGA IJUMAA

MICHUZI TV: MILIONI 18 ZAOKOLEWA MBEYA, ZILIZOPORWA KWA MFANYABIASHARA


MICHUZI TV: ALI KIBA AWAJIBU WASAFI KUHUSU USHIRIKI WA TAMASHA LAO...

VOA SWAHILI: Duniani Leo November 7, 2018

BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO (TADB) YAAHIDI MAKUBWA PANGANI

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mh. Zainab Abdalah ametembelea uongozi wa Benki ya Maendeleo ya kilimo nchini kufanya kikao kilichomkutanisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ndg. Japhet Justine na viongozi waandamizi ambao kwa pamoja wameahidi kuifanya Pangani wilaya ya mfano na ya kimkakati kwenye mipango yao.
..
Kikao hiki kimetoka na maazimio mazito kuelekea mapinduzi ya kilimo Pangani na moja kwa moja Mkurugenzi amekubali kua tayari kujenga kituo kikubwa cha ukusanyaji maziwa Pangani eneo la Madanga.Aidha kikao kimeadhimia kuisaidia sekta ya uvuvi Pangani kuhakikisha inaleta mapinduzi ya uchumi kwa wavuvi.
..
Muhimu zaidi mazungumzo yamefanyika na kuweka misingi itakayowasaidia vijana wa Pangani hasa waliotayari kuungana na kunufaika na mipango ilioazimiwa na uongozi mzima kuahidi hivi karibuni kufika Pangani kuchagiza yaliopangwa na kujionea nini zaidi wanaweza kufanya na Pangani.
..
Mkuu wa Wilaya Pangani amemshukuru Kaimu Mkurugenzi Mtendaji kwa ufanisi wake na utayari aliounesha,kasi uwajibikaji na zaidi alivo tayari kujitoa kwa ajili ya Maendeleo ya nchi yetu.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ndg. Japhet Justine akiungumza na viongozi wa wilaya ya Pangani wakati wa kikao chao cha pamoja kuhusiana ushirikiano
 Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akizungumza katika kikao hicho kulia ni Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George
 Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George kulia akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ndg. Japhet Justine  kushoto akiangana na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
Wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kufanya mazungumzo hayo.

Habari za UN KUTOKA NEW YORK, MAREKANI, Novemba 7 2018

Arsenal mikononi mwa Sporting CP usiku wa EUROPA

0
0
Katika mechi ya nne ya hatua ya makundi kwenye ligi ya EUROPA Alhamisi hii timu ya Arsenal itakuwa nyumbani katika dimba la Emirates dhidi ya Sporting CP ya Ureno. Katika mchezo wao wa mzunguko wa kwanza Arsenal waliibuka na ushindi wa bao 1 ambao uliwawezesha kuwa vinara na kuongoza kundi E.
Arsenal wamekuwa katika kiwango bora na wanacheza kandanda safi tangu wampate kocha Unai Emery ambaye amebadilisha aina ya uchezeji wake. Mchezo huo utachezwa Alhamisi tar 8 Novemba, majira ya saa 5:00 Usiku saa za Afrika Mashariki na utarushwa moja kwa moja kupitia chaneli ya ST World Football katika king’amuzi cha StarTimes.
Katika Usiku huo wa EUROPA mechi nyingine zitakazochezwa ni pamoja na ule wa Chelsea ambao watakuwa ugenini dhidi ya BATE Borisov (saa 2:55 Usiku), Fenerbahce vs Anderlecht (saa 12:50 jioni), Lazio vs Olympique Marseille (saa 2:55 Usiku), Celtic vs RB Leipzig (saa 5:00 Usiku) na Real Betis vs AC Milan (saa 5:00 Usiku), yote kupitia chaneli za michezo za StarTimes.
Michuano ya EUROPA inaonyeshwa kupitia king’amuzi cha StarTimes pekee na kwa wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi cha MAMBO kwa Tsh 14,000 kwa upande wa Antenna na wale wanaotumia dish watalipia Tsh 21,000 tu, kupata uhondo huu.
Mbali na ligi ya EUROPA StarTimes wanaonyesha ligi ya Bundesliga pamoja ile ya Ufaransa, maarufu kama Ligue 1. Katika Bundesliga wikiendi hii kuna mchezo mkubwa ambao unafahamika kama Der Klassiker unaokutanisha miamba miwili, wazee njano na nyeusi Borussia Dortmund watawakaribisha Bayern Munich katika dimba la Signal Iduna Park saa 2:30 Usiku jumamosi hii.
Dortmund ndio vinara wa ligi hiyo baada ya kuanza vizuri msimu huu wakiwa hawajapoteza mchezo wowote hadi sasa. Bayern ambao wamesuasua sana msimu watakuwa na kibarua kigumu kuidhibiti safu ya ushambuliaji ya Dortmund ambayo in amagoli kila kona.

MKUU WA WILAYA YA CHUNYA AAHIDI KUPAMBANA NA WAFUGAJI WANAOHALIBU VYANZO VYA MAJI

0
0
Na David Nyembe, Chunya 

MKUU wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Maryprisca Mahundi, amewapa wiki tatu wafugaji wa Kijiji cha Igundu katika Kata ya Sangambi wilayani humo kuhamisha mifugo yao na kuipeleka katika Kijiji cha Paris ambacho kimetengwa kwa ajili ya wafugaji.

Ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano wa Hadhara uliofanyika kijijini hapo ambapo alisema lengo la kuondoa mifugo hiyo ni kumaliza mgogoro kati ya wakulima wa kijiji hicho na wafugaji pamoja na kuokoa chanzo cha maji ambacho wakazi wa eneo hilo wanakitegemea. Alimuagiza Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Joseph Nangale, kusimamia na kuhakikisha mifugo hiyo inahamishwa huku akimtaka kutumia nguvu iliyotumika kuwazuia wakulima kufanya shughuli zao karibu na chanzo cha maji.

Mahundi alisema amechoshwa na migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijji hicho cha Igundu na kwamba agizo lake hilo ni la mwisho na kwamba atakaporudi tena kwenye kijiji hicho na kukuta inaendelea hakutakuwa na majadiliano tena na kwamba wasije wakamlaumu.

“Mkae chini mjadiliane na mkubaliane idadi ya mifugo ambayo kila mfugaji wa kijiji hiki atatakiwa kubaki nayo hapa, nimewapa siku 10 viongozi wenu waniletee taarifa ya majidiriano hayo, lakini nimewashauri kila mfugaji abaki na mifugo 10,” alisema Mahundi.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Meryprisca Mahundi (katikati) akimkisikiliza kwa makini Afisa Mtendaji Kata ya Sangambi kijiji cha Igundu  Joseph Nangale ,kuhusiana na namna ambavyo wafugaji wamefanya uhalibifu wa vyanzo vya maji katika kjiji hicho.Picha David Nyembe . 
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh Meryprisca Mahundi (Katikati)akiteta jambo na viongozi wa vijiji vinavyo zunguka kata ya Sangambi ambako kumefanyika uhalibifu wa vyanzo vya maji kutokana na baadhi ya wafugaji wa vijiji hivyo kunywesha mifugo yao sanjali na kupitisha mifugo katika maeneo ya vyazno hivyo. 
Wananchi wa kijiji cha Igundu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chunya Merryprisca Mahundi (hayupo pichani) mara baada ya kukamilisha ziara ya  kutembelea maeneo ya vyanzo vya maji ambako kumefanyika uhalibifu mkubwa kutokana na baadhi ya wafugaji kupitisha mifugo yao .


TANZANIA KUSHIRIKI MAONESHO YA CIIE YATAKAYOFANYIKA SHANGHAI NCHINI CHINA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KATIKA  kuendeleza mkakati wa kutangaza utalii wa Tanzania nchini China, Bodi ya Utalii Nchini (TTB) kwa kushirikiana na wadau wa Utalii wa Tanzania pamoja na Sekta ya Madini inashiriki onesho kubwa la biashara yaliyoandaliwa na Serikali ya China.

Maonesho hayo makubwa  yajulikanayo kama China International Impact Expo (CIIE) yatafanyika katika jiji la Shanghai kuanzia  5-10 Novemba, 2018 na  Kupitia maonesho haya, sekta ya madini itaudhihirishia ulimwengu kuwa Madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania tu. 

Akielezea safari hiyo ya nchini China, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii  Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema kuwa safari hiyo ya nchini China imeandaliwa na bodi ya utalii kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini China na Shirika la Ndege la Tanzania ATCL, wameandaa ziara ya utangazaji nchini China ambapo pamoja na kushiriki maonyesho ya CIIE watafanya ziara ya utangazaji katika miji mbalimbali.

Amesema miji hiyo ni Shanghai (12 Novemba, 2018), Guangzhou (14 Novemba, 2018), Hong Kong (16 Novemba, 2018), Chengdu (19 Novemba, 2018) na Beijing (20 Novemba, 2018). Misafara hii itatuwezesha kukutana na wafanyabiashara wa utalii wakubwa katika miji hiyo na wawekezaji wakubwa katika sekta ya utalii pamoja na vyombo vya habari mbalimbali vya China. 

  Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)  Jaji Mstaafu Thomas akizungumzia safari ya China na ushiriki wao wa Maonesho  makubwa  yajulikanayo kama China International Impact Expo (CIIE) yatafanyika katika jiji la Shanghai kuanzia  5-10 Novemba, 2018, Kushoto ni  Mihayo    Meneja Masoko na Usambazaji Edward Mkwabi.


WAZIRI LUGOLA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA JIJINI DODOMA LEO

0
0
Na Felix Mwagara, MOHA 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke na kumuakikishia ushirikiano zaidi kati ya Wizara yake na Ubalozi huo nchini. Mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Lugola, jijini Dodoma leo ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa ushirikiano kati ya Wizara na ofisi ya Balozi huyo nchini. 

Waziri Lugola alimuakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini. “Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola. 


Hata hivyo, Balozi Sara alimpongeza Waziri Lugola kwa kuteuliwa na Rais John Magufuli kuiongoza Wizara hiyo na pia alimuakikishia ushirikiano zaidi kati ya Uingereza na Tanzania. “Hongera sana mheshimiwa Waziri kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani na pia nimefurahi kuja katika ofisini yako kufanya mazungumzo nawe,” alisema Balozi Sara.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya  Waziri Lugola, jijini Dodoma leo.

Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke (kushoto) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo  yalifanyika katika ofisi ya Waziri Lugola, jijini Dodoma leo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimkaribisha ofisini kwake jijini Dodoma, Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke kwa ajili ya mazungumzo ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MATUKIO YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA BUNGENI LEO JIJINI DODOMA

0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Jenista Mhagama, Bungeni jijini Dodoma Novemba 7, 2018.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mbunge wa viti maalum Salma Kikwete, Bungeni jijini Dodoma. Novemba 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mbunge wa Malindi Ally Saleh, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Novemba 7, 2018

HESLB YAKUTANA NA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA WA CHUO CHA DUCE

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) imekutana na wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) kwa ajili ya kutoa elimu kuhusiana na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Akizungumza na wanafunzi hao katika chuo hicho Meneja wa Upangaji Mikopo wa Bodi hiyo Julitha Miyedu amesema kuwa taratibu za kuomba mikopo ziko wazi na jinsi ya kuupata mkopo huo kutokana na vigezo na masharti vilivyoanishwa.Amesema kuwa Bodi ya Mikopo iko kwa ajili ya wanafunzi katika kuhakikisha kila mwenye vigezo vya mikopo anapata kwa wakati ili kuwezesha wanafunzi wasifikirie suala fedha katika kufanya mahitaji.

Miyedu elimu wanayoitoa kuhusiana na mikopo ni endelevu katika kuhakikisha kila mwanafunzi anapata uelewa wa bodi inavyochakata mikopo kwa wanafunzi.“Hatutamuacha mtu kwenye suala linalohusiana na utoaji mikopo nia ya bodi ni kuona kila mtu anapata mkopo kutokana vigezo vilivyoanishwa katika kuijenga nchi yetu na kupata watalaam mbalimbali”amesema Miyedu.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo Veneranda Malima amesema kuwa wanafunzi wanatakiwa kusoma vitu katika mitandao na vipeperushi vya bodi kwa kupata taarifa kufika ofisi za bodi kwa vitu vikubwa.Amesema kuwa bodi imeweka mfumo wa Kielekroniki katika kurahisisha malipo ya mikopo kwa wanafunzi kupitia kwa maafisa wa mikopo wa chuo.

Malima amesema kuwa Bodi itaendelea kutoa taarifa katika utaratibu uliozoeleka hivyo wanafunzi wajiepushe na kupata taarifa katika sehemu zisizo rasmi.
 Meneja wa Upangaji Mikopo wa Bodi hiyo Julitha Miyedu akizungumza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) kuhusiana na ujio bodi katika utoaji wa mikopo ya elimu juu , iliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mawasiliano Mwandamizi  wa Bodi ya  Mikopo ya Wanafunzi  wa Elimu ya Juu Veneranda Malima akizungumza na wanfunzi wa mwaka wa kwanza wa DUCE.
 Afisa Mikopo wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE)   Salmon Daud akitoa maelezo kwa wanafunzi wa chuo hicho kuhusiana na utaratibu wa kupata mikopo ni mara baada ya kujiridhisha na taarifa.
 Baadhi ya Wanafunzi wa mwaka wa kwanza 

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAWAALIKA WADAU WA MASUALA YA FEDHA KUTOA MAONI KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA WA MWAKA 2018

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images