Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA HABARI - AZAM TV 5/11/2018


HABARI ZA UN KUTOKA NEW YORK, MAREKANI, NOVEMBA 5, 2018

POLISI TANZANIA BINGWA KATIKA TAEKWONDO, KENYA YA PILI, RPC AWAITA OFISINI

$
0
0
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Mashindano ya ya Nane Nane Taekwondo Clubs Championship yamemalizika jana jioni kwa timu ya Polisi Arusha Taekwondo Club kuibuka mshindi baada ya kuzipiku timu zote zilizoshiriki kwa siku mbili katika ukumbi wa Tripple “A” uliopo jijini hapa.
Timu hiyo ambayo inajumuisha wachezaji wa kike na wa kiume pamoja na watoto wadogo wanaoanzia umri wa miaka mitano iliweza kuibuka na ushindi huo baada ya kupata jumla ya medali 27 toka katika makundi yote matatu ambapo watoto wa umri wa miaka 5, 8 na 13 walipata Gold Moja na Silver Mbili, huku askari pekee wa kike Ester Yohana akipata Gold na wanaume wakipata Gold 6, Silver 5 na Bronze 12.
Mashindano hayo ambayo yana umuhimu mkubwa katika kupima uwezo wa kila mchezaji yalishirikisha jumla ya timu kumi ambazo ni Polisi Arusha,Kijenge, Kili, Edmund Rise School,Perfect, Tripple A, Naura zote za Tanzania na Kilifi, Regional  A na Regional B zote toka nchini Kenya.
Katika mashindano hayo timu ya Polisi Arusha ilijinyakulia medali 8 zilikuwa za Gold, 7 za Silver na 12 za Bronze huku nafasi ya pili ilishikwa na timu ya Chuo Kikuu cha Kilifi toka Kenya ambayo ilipata medali 15 ambapo za Gold zilikuwa 4, Silver  5 na Bronze 6 , wakati nafasi ya tatu ilikwenda kwa kwa timu ya Regional.
Mara baada ya kupata taarifa hiyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi ambaye ndio mlezi wa timu hiyo alitikisa kichwa juu na chini kama ishara ya kufurahia ushindi huo na kuialika timu hiyo bingwa ofisini kwake siku ya Jumamosi.
Kufuatia ushindi huo baadhi ya wachezaji wa Kenya Joy Ludoro na Charity Manga wote kwa pamoja walitoa pongezi kwa timu ya Polisi Arusha kwa kushika nafasi ya kwanza na kuahidi katika mashindano yajayo wanaamini watafanya vizuri zaidi na kushika nafasi ya kwanza.
“Mashindano haya yametuongezea hari ya kuongeza juhudi zaidi ili mashindano yajayo tushike nafasi ya kwanza kama walivyofanya Polisi safari hii” Alisema Joy Ludoro mchezaji wa timu ya Kilifi ya nchini Kenya.
Kwa upande wa Charity Manga alisema Arusha ina wachezaji wa kike wachache hivyo alishauri viongozi wanaosimamia mchezo huo watoe hamasa kubwa kwa wanawake hali ambayo hata katika mashindano hayo huo wakose washindani wa uzito wao.
Naye kocha wa timu bingwa ya Polisi Arusha Taekwondo Club, Master Shija Shija alisema abweteki na ushindi alioupata bali atazidi kuongeza mazoezi na mbinu mbalimbali kwa wachezaji wake na kutoa wito kwa watanzania kuwa, wajitokeze kushiriki mchezo huo utakaowawezesha kuimarisha afya zao pamoja na kujilinda wao wenyewe.
 Mchezaji mwenye umri mdogo toka Kenya akiwa ameuangushwa chini baada ya kupigwa teke na mchezaji wa timu ya Taekwondo ya Polisi Arusha katika mchezo wa mashindano ya Nane Nane yaliyofanyika jana katika ukumbi wa Tripple A uliopo jijini hapa na Polisi kuibuka mshindi.
 Wachezaji wa timu ya Polisi Arusha Taekwondo wakimpongeza mmoja wa wachezaji wao mwenye umri mdogo mara baada ya kushinda mchezo wake dhidi ya mpinzani wake toka Kenya katika pambano la Nane Nane Taekwondo Clubs Championship lililofanyika ukumbi wa Tripple A uliopo jijini Arusha. 
Wachezaji wa timu ya Polisi Arusha Taekwondo ambao ni mabingwa wa michuano ya Nane Nane Taekwondo Clubs Championship wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu za Kilifi na Regional toka nchini Kenya mara baada ya mashindano hayo kumalizika jana. (Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha)


WAZIRI MKUU AMPA SIKU SABA WAZIRI MWIJAGE KUSIMAMIA KIBALI CHA BM MOTORS

$
0
0
Na scolastica Msewa, kibaha
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amempa siku saba Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuhakikisha Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linatoa kibali kwa kampuni ya BM Motors cha kutengeneza na kuunganisha bodi za magari. 
Waziri Mkuu alisema hayo wakati akifunga maonesho ya Wiki ya Viwanda yaliyomalizika mkoa wa Pwani, katika Uwanja wa Sabasaba,Picha ya Ndege,  Kibaha.
Alimtaka Waziri Mwijage, ifikapo Ijumaa wiki ijayo ampe taarifa ya maendeleo ya kampuni hiyo kuhusiana na kibali hicho kutoka TBS.
Alisema wakati mwingine huo ni urasimu, kama ana tatizo ambiwe aboreshe hawezi awe amekaa tangu mwaka jana analalamika hajapata kibali cha kutengeneza mabodi.”
Na kwa nini msimpe hiyo fursa atengeneze bodi halafu mmwambie  arekebishe na mkiwa mmejiridhisha kama ana uwezo wa kutengeneza hayo mabodi na Watanzania waendelee kutengeneza hapa nchini,  badala ya kuagiza nje kwa gharama kubwa haina maana” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Aliongeza kuwa  “ulisema unaogopa kutumbuliwa (Mwijage), sasa sikutumbui nakupa wiki moja nipate taarifa ya mwenendo wa kampuni yetu ya ndani inayotaka kuunganisha mabasi.”
“Kwanza ni kampuni pekee inayotaka kuunganisha magari nchini, apewe fursa atujengee magari ya luxury (ya starehe) hapa Tanzania, alifafanua.
Mapema Waziri Mwijage akisalimia wananchi, alisema kwamba mashirika yaliyo chini ya wizara yake yakifanya kinyume yanahatarisha ajira yake, na yeye hayuko tayari kwa hilo.
Waziri Mkuu, aliutaka uongozi wa mkoa wa Pwani kujipanga kwa kuandaa maonyesho ya viwanda kama hayo kila mwaka, ili wajasiriamali wapate fursa ya kuonyesha bidhaa zao.
Pia aliagiza miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali kutumia bidhaa zinazotengenezwa nchini zikiwemo saruji, nondo na mabomba.
Akizungumzia eneo linalomilikiwa na Shirika la Elimu Kibaha lililopo Kibaha, Pwani, Majaliwa alisema shirika hilo liendelee kutafuta wawekezaji zaidi kwa eneo hilo.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Pwani,  Evarist Ndikilo wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya mkoa  huo,  alisema shirika hilo limepata mwekezaji ambapo limetenga eneo la hekta 38.8  kwa ajili ya ujenzi wa shughuli za kibiashara kama hoteli na maduka makubwa,  na hekta 100 ambazo zimetengwa kwa ajili ya makazi.

MKUU WA MKOA WA TABORA MH. AGGREY MWANRI: SUKUMA NDANI MWANZO MWISHO UBAONI

DUDU BAYA: Kimenirudia Mwenyewe! / MTOTO wangu Mvuta Bangi

TID: Wanatuita ma LEGENDS ili kutupoteza, wawapandishe wasanii wao

MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 6,2018


MSEMAJI MKUU WA SERIKALI : TANZANIA INAFANYA VIZURI KATIKA UKUAJI WA UCHUMI

WASHINDI WA PROMOSHENI YA SHINDA ZAIDI YA SPORT PESA WAZIDI KUJINYAKULIA ZAWADI ZAO

$
0
0
Unaweza kusema watanzania wameamua na kila mtu anapambana kwa nafasi yake kuhakikisha anashinda na timu ya ushindi SportPesa Hii ni kutokana na ubashiri na haya yote ni kujitahidi kushinda bajaj na kufungua ukurasa mpya.

Kwanini watanzania wameamua kuipa jina la timu ya ushindi SportPesa kikubwa ni namna ambavyo timu hii imeonyesha kuwajali maana kwenye promosheni ya Shinda zaidi Na SportPesa wanatoa bajaj mia na mtanzania mmoja anaondoka na bajaj yake kila siku hii ndio maana halisi ya timu ya ushindi yani hawakubali ubashiri wako ukuache hivihivi.

Na kama kawaida SportPesa imeendelea kutoa bajaj kwa washindi wa promosheni ya shinda zaidi huku kwa wakati huu Mussa Mathias Kutoka Hapa Jijini Dar es salaam ndiye anayekabidhiwa bajaj baada ya kushinda. Huyu ni mshindi wa droo ya 34 ambaye alitusimulia ni kwa vipi alianza kucheza na timu ya ushindi mpaka kufanikiwa kushinda bajaj na hatimaye kuanza mwanzo mpya katika Maisha.

Mathias alisema watu wa huduma kwa wateja kutoka SportPesa ndio walimsababisha kujiunga na kuanza kucheza na hii ilitokea siku ambayo walikuwa wanapita mtaani kutoa elimu kuhusu timu ya ushindi ndipo na yeye alishawishika na kuanza kucheza.

"kwenye maisha kuna mambo mengi sana mimi ni dereva bajaj nimepitia mambo mengi nilikuwa natamani siku moja kumiliki bajaj yangu mpya ila sikufahamu ni wapi pangekamilisha ndoto yangu hii, ndio maana nilivyosikia na nyie mnatoa bajaj nilijitajidi kucheza sana kweli mungu sio dhalimu na mimi nimebahatika kushinda kweli hata siamini ila ama hakika sportpesa mmekwamua maisha yangu nawashukuru sana " alisema Mathias.
Pichani kuli ni Mshindi MUSSA MARTIAS wa Dar es Salaam akikabidhiwa funguo ya Bajaj yake aliyojishindia


 

BARAZA LA KILIMO TANZANIA LAENDELEA NA UJENZI NA UKARABATI WA MAGHALA MKOANI KATAVI.

$
0
0
ZAIDI ya wakulima 57,000 Mkoani Katavi wanatarajiwa kunufaika na mafunzo yatakayowasaidia kuongeza uzalishaji katika mazao yao, namna bora ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na kujengewa uwezo wa namna ya upatikanaji wa masoko kwa mazao wanayolima.

Aidha pia imeelezwa kuwa ili kuendelea kuinua kiwango cha uzalishaji kwa wakulima mkoani humo zaidi ya maghala 18 ya kuhifadhia mazao yanatarajiwa kujengwa hasa katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao,

Hayo yalielezwa na Afisa Biashara kutoka Baraza la Kilimo Tanzania Bw Alinanuswe Ambalile Mkoani Katavi na kusema kazi kubwa katika Mkoa huo imekwisha kufanyika hasa katika kuwajengea uwezo wakulima wadogo ili kuongeza thamani mazao yao.

Bw Ambalile alisema kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2018/19 Baraza la Kilimo Tanzania kwa kushirikiana na Mradi wa TIJA TANZANIA wanatarajia kujenga mashamba darasa zaidi 42 kwa mazao ya Mahindi, Mpunga na Maharage,lengo ikiwa ni kuendelea kumjengea uwezo mkulima.

“Baraza la kilimo Tanzania linafahamu msimu wa kilimo umekaribia na tayari tumekwisha kukarabati maghala 7 ya kuhifadhia mazao pia tumekwisha kuwajengea uwezo wakulima ili mazao wanayozalisha yaendane na mahitaji ya soko na tunaamini kupitia mabadiliko haya tunayoyafanya katika kuweka mashamba darasa hayo 42 wakulima watakuwa na uwezo mzuri zaidi wakulima kilimo chenye tija” alisema Bw Ambalile.
Muonekano wa Ghala la kuhifadhia mazao linalojengwa na Baraza la Kilimo Tanzania chini ya udhamini wa AGRA katika Kijiji cha Mnyagala Mkoani Katavi likiwa katika hatua za mwisho za kukamilika kwake ambapo baada ya kukamilika litakuwa na uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani 660. 
Mafundi wakiendelea na hatua za uwekaji Kenki katika ghala hilo ambalo litawasaidia wakulima wa kijiji hiki cha Mnyagala ambao ni wakulima wakubwa wa Mpunga mkaoni Katavi kuwa na uwezo wa kuhifadhi mazao yao, ghala hili linatajwa kuwa la kisasa la kipekee katika kijiji hicho.
Mafundi wakiendelea na hatua za mwisho za ukarabati wa Ghala la kuhifadhia mazao la kampuni ya Nondo Investiment iliyoko Mkoani Katavi, Ukarabati ambao unaratibiwa na Baraza la Kilimo Tanzania chini ya udhamini wa AGRA ambapo baada ya ukarabati huo kukamilika ghala hilo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 10000.
Muonekano wan je wa ghala hilo baada ya kufanyiwa marekebisho kwa kuongeza urefu wa ghala hilo ambapo awali lilikuwa na uwezo wa kubeba tani 7000 pekee lakini baada ya kukamilika kwake litakuwa na uwezo wa kubeba tani 10000, ukarabati wote huo unafanywa na Baraza la Kilimo Tanzania chini ya udhamini wa AGRA.
Mafundi wakiwa katika hatua za mwisho za uwekaji wa kenki katika ghala jipya linalojengwa na Baraza la Kilimo Tanzania katika Kata ya Mishamo Mkoani Katavi ambapo baada ya kukamilika kwa ghala hilo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani 660 za mazao.

KUMEKUCHA NAMTUMBO MARATHON, MAMIA WAJITOKEZA KUJIANDIKISHA

$
0
0
Wanariadha kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi wamejitokeza kwa wingi kushiriki Namtumbo Marathon inayotarajiwa kutimua vumbi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma ambapo maelfu ya wakazi wa wilaya hiyo na vitongoji vyake wamekuwa wakizitazamia mbio hizo kuanza wakati wowote ili nao wapate fursa mbalimbali za kushiriki katika mbio hizo.

Akizungumzia usajili unaoendelea katika hospitali ya wilaya ya Namtumbo, Dokta Chihoma amesema watu wengi wameitikia wito na wamejitokeza kwa wingi wao kujiandikisha tayari kwaajili ya kushriki mbio hizo ambazo zilianzishwa rasmi mwaka 2017 kwa malengo mengi lakini kubwa likiwa ni kuchangisha fedha kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo ambayo imefanikia kuanza kwa kiasi kikubwa. 

Aidha Chihoma ameongeza kuwa nafasi bado zipo wazi kwaajili washiriki watakaojitokeza kujiandika kwaajili ya bio hizo. 

Kwa upande wao wadhamini wa na waandaaji wa mbio hizo Mantra Tanzania au Uranium one wamesema kila kitu kipo sawasawa na kuwataka watanzania na wageni kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo ambazo zinalenga kuleta maendeleo ya kiafya katika eneo la Namtumbo na vitongoji vyake. 

Mwakilishi wa Mantra Tanzania Bi. Khadija Pallangyo Kawawa amaesema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba watanzania watafurahia mbio za mwaka huu kutokana na jinsi zilivyopata hamasa kubwa katika maeneo mbalimbali “Nawaomba sana watanzania wajitokeze kwa wingi waje washiriki nasi katika kufanikisha awamu ya pili ya Namtumbo Marathon” 

KUTOKA BUNGENI : MKUTANO WA KUMI NA TATU KIKAO CHA KWANZA

President Abdel El Sisi Welcomes Zuriel Oduwole To Egypt, Talks Development & Gender Issues

$
0
0
As one of the Arab worlds most influential leaders and a great ally of the United states - receiving over $1Billion in strategic aid annually, President Abdel Fattah El Sisi has welcomed Global Speaker, Girl Education Advocate and Film Maker Zuriel Oduwole to the North African country.

Having met and sat down one-on-one with 28 world leaders previously, he is the first Arab leader to welcome her to his country. Breaking all protocols in her dress code, head gear and shoes for the meetings, the event produced by Zuriel and her youthful 'All-Girl-Crew" all aged below 18, was taped for broadcast on National Television for all Egyptians to see, underlying the importance the President places on the growing influence of this simple, unassuming but seriously mission focused 16 year old girl.

Zuriel also wants to tell the story of the successes of educated young women to the Arab world, while highlighting the continued challenges and progress still needed to bring equity with the men across the region
 President Abdel Fattah El Sisi welcomes Global Speaker, Girl Education Advocate and Film Maker Zuriel Oduwole at the Presidential Palace in Cairo
  President Abdel Fattah El Sisi converses with Global Speaker, Girl Education Advocate and Film Maker Zuriel Oduwole at the Presidential Palace in Cairo
  President Abdel Fattah El Sisi thanks Global Speaker, Girl Education Advocate and Film Maker Zuriel Oduwole at the Presidential Palace in Cairo
 President Abdel Fattah El Sisi sees off Global Speaker, Girl Education Advocate and Film Maker Zuriel Oduwole at the Presidential Palace in Cairo

WATU SITA AKIWEMO MTOTO MCHANGA WAFA, SABA WAJERUHIWA KATIKA AJALI MSATA MKOANI PWANI

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
Watu sita akiwemo mtoto mchanga wa jinsia ya kike wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa katika ajali iliyotokea kijiji cha Msata, barabara kuu ya Segera/Chalinze mkoani Pwani. Akithibitisha, kamanda wa polisi mkoani Pwani Naibu Kamishna wa Polisi ACP Wankyo Nyigesa alisema kwamba ajali hiyo imetokea Novemba 5, 2018 majira ya saa moja usiku baada ya gari namba T. 124 DHW aina ya Toyota coaster ikitokea Mkata kwenda Mbezi -Dar es salaam kuligonga kwa nyuma lori namba KBV 746C/ZE2861 FAW iliyokuwa imeegeshwa barabarani kutokana na kuharibika. 
Amesema dereva wa Toyota coaster iliyosababisha ajali ambae hajafahamika jina lake alikimbia baada ya kutokea ajali. 
ACP Wankyo alieleza kuwa waliopoteza maisha ni wanaume watano wenye umri kati ya miaka 30-40 ambao majina yao bado kufahamika Alisema ,watu saba walipata majeraha kwenye maeneo mbalimbali ya mwili yao . 
"Waliopata majeraha ni pamoja na wanaume wanne na wanawake watatu ambao wote wamepelekwa zahanati ya jeshi Kihangaiko -RTS na kituo cha afya Lugoba kwa matibabu zaidi "alisema Wankyo, akiongesza kuwa  miili ya marehemu imehifadhiwa hospital ya wilaya ya Bagamoyo kwa uchunguzi wa daktari. 
 Alitaja chanzo cha ajali, ni uzembe wa dereva wa gari namba T. 124 DHW aina ya Toyota coaster kujaribu kulipita bila tahadhari gari jingine lililokuwa limeegeshwa baada ya kuharibika na wanaendelea kumsaka. 
Kamanda huyo alitoa rai kwa madereva kutii sheria za usalama barabarani na kuacha tabia za kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi ili kuepukana na ajali zembe. Wankyo aliwapa salamu madereva hao, kuwa hawatakuwa na muhali nao kwani watakamatwa na kuwachukulia hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine. 
Kwa upande wao mashuhuda wa ajali hiyo akiwemo mwenyekiti wa kitongoji cha Pugini, kijiji cha Msata Siasa James alisema hii ni ajali mbaya ambayo haijawahi kutokea eneo hilo. 
 "Tulisikia mshindo, na kuona tukimbilie eneo la tukio ndipo tulipokuta gari ya abiria imelivaa lori kwa nyuma na kisha kukatika upande wa kondakta "alieleza. 
 Nae Stephen Hinjo alieleza kwamba, gari ya abiria walikutana nayo ambapo ilipita hata dakika mbili hazijapita walisikia kishindo na kutahamaki waliona limekwenda kujikita nyuma ya lori lililokuwa limepaki pembeni mwa barabara. 
 "Kufika eneo la tukio tulikuta abiria upande wa kondakta umebanwa huku vichwa viwili vikiwa vinaning'inia chini, wengine wamekatika mikono na shingo, ni ajali haijawahi tokea, "kikubwa tulichokifanya ni kuopoa miili na polisi walifika eneo la tukio "alifafanua Hinjo.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani Naibu Kamishna wa Polisi ACP Wankyo Nyigesa na wasaidizi wake wakiwa eneo la ajali
Kamanda wa polisi mkoani Pwani Naibu Kamishna wa Polisi ACP Wankyo Nyigesa na wasaidizi wake wakiwa eneo la ajali

MWANAMUZIKI KING KIKII ATETA NA MAOFISA WA POLISI CHUO CHA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Dotto Mwaibale
MWANAMUZIKI Mkongwe hapa nchini Kikumbi Mwanza Mpango 'King Kiki' ameliomba jeshi la polisi kuendelea kusimamia sheria ya haki miliki za wanamuzi ili kazi zao zisiishie kwa maharamia.
Ombi hilo alilitoa mwishoni mwa wiki wakati viongozi wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), ukitoa mada kwa maofisa wa Jeshi la Polisi  waliopo katika mafunzo Chuo cha Polisi cha Kurasini jijini Dar es Salaam kuhusu haki za wanamuziki hapa nchini.
"Ninyi wenzetu jeshi la polisi ndio tunaowategemea katika kusimamia sheria hii tunaamini mtatusaidia kazi zetu zisiibwe na maharamia" alisema King Kiki.
Akizungumza na katika mafunzo hayo Rais wa TAMUFO, Dkt. Donald Kisanga alisema lengo la mafunzo hayo ya siku moja kwa maofisa hao ni kuwajengea  uelewa wa ulinzi wa kazi za muziki ikiwepo  kudhibiti na kuwakamata maharamia wa kazi muziki hapa nchini.
Katibu Mkuu wa TAMUFO Stellah alisema umoja huo ulishatoa mapendekezo kupitia waraka maalumu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Harisson Mwakyembe ili mtu yeyote atakayebainika akihujumu kazi za wasanii ashitakiwe kwa makosa ya jinai.
Alisema TAMUFO pia inaandaa mapendekezo ya kupeleka serikalini ya kuweka dawati la jinsia katika vituo mbalimbali vya polisi hapa nchini ambayo yatakuwa yakishughulikia wizi wa kazi za wanamuziki.
.
 Mwanamuziki Mkongwe nchini Kikumbi Mwanza Mpango 'King Kiki' akizungumza na maofisa  wa Jeshi la Polisi  waliopo katika mafunzo Chuo cha Polisi cha Kurasini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuhusu haki za wanamuziki hapa nchini ambapo ameliomba jeshi la polisi kuendelea kusimamia sheria ya haki miliki za wanamuzi ili kazi zao zisiishie kwa maharamia. Mada katika mkutano huo zilitolewa na viongozi wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO)
 Maofisa wa polisi wa chuo hicho wakisikiliza mada.
 Katibu wa TAMUFO Stellah Joel Diana akizungumza na maofisa hao.
 Rais wa TAMUFO Dkt. Donald Kisanga akizungumza na makamanda hao. 


NGULI WA RIWAYA MOHAMED S. MOHAMED NA ADAM SHAFI KUPAMBA KONGAMANO LA KISWAHILI ZANZIBAR

$
0
0

 Njoo umwone, umsikilize, uongee naye, umshike mkono na upige picha naye mwandishi maarufu wa riwaya za Kiswahili ikiwemo Nyota ya Rehema na Kiu: Mohamed Suleiman Mohamed katika Kongamano la Pili la Kimataifa la  Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA), mjini Zanzibar  Desemba  12 na 13 mwaka huu.
 Riwaya ya kwanza ya mwanariwaya Adam Shafi ilikuwa KULI lakini siku ya Kongamano atakizindua kitabu Kuona Mtoto  wa Mama. Fika umwone, umshike mkono,muongee na kupiga picha naye.Bahati ilioje! Ni  Desemba  12 na 13 mwaka huu.

Article 4

STARTIMES NA SOS CHILDREN’S VILLAGES ZAINGIA UBIA WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA VIJANA KWENYE AJIRA

$
0
0
KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd na SOS Children’s Villages Tanzania wameingia  makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi, lengo likiwa ni kuwapatia fursa  mbalimbali hasa kiteknolojia ili kuendana na malengo ya milenia yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa.

Katika mkataba huo StarTimes itasaidia programu mbalimbali za SOS Children’s Village katika Mikoa zaidi ya saba ikiwemo Unguja, Pemba, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Iringa na Mufindi na program hizo zitalenga hasa kwenye kupanua nafasi za kujifunza na kukuza uzoefu miongoni mwa Vijana wa SOS Children’s Village. 

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makubaliano hayo mwanasheria mkuu wa Star Media (T) Ltd Justine Ndege amesema  kuwa kwa vijana waliopo, kazi yao ya kwanza sio kuwa na uhuru. Kwao jambo la msingi kwanza ni kuishi tofauti ya maisha huru yenye heshima na maisha yenye misukosuko na mahangaiko ndicho wanacholenga kukabiliana nacho.

Ndege amesema kuwa, Ushirikiano baina ya kampuni Startimes na  SOS Village utapiga hatua katika kuwapeleka Vijana katika soko la ajira na kuwapatia namna au njia za kujitengenezea kesho yenye uimara na uhakika zaidi katika jamii zao.


Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa SOS Childre’s Village Dvid Mulongo amesema kuwa moja ya mambo ambao StarTimes itafanya ni kuwapatia nafasi vijana kutoka SOS Villages Tanzania bara na Zanzibar kujifunza kwa vitendo kazi mbalimbali zilizopo kwenye kampuni yao, ushauri, mafunzo ya kiufundi kuhusu namna ambavyo StarTimes inafanya kazi hasa katika Idara ya Masoko na kuhusu bidhaa zake ili kukuza uelewa wa kazi na ajira kwa Vijana.


Mwanasheria Mkuu Star Media (T) Ltd, Justine Ndege(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa kuingia makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SOS Children's Village, David Mulongo
 Mwanasheria Mkuu Star Media (T) Ltd, Justine Ndege(kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa SOS Children's Village, David Mulongo(kushoto)  wakisaini  makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa ofisi za SOS Children’s Villages Tanzania jijini Dar es Salaam.
 Mwanasheria Mkuu Star Media (T) Ltd, Justine Ndege(kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa SOS Children's Village, David Mulongo(kushoto)  wakipeana mikono mara baada ya kumaliza kuingia  makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa ofisi za SOS Children’s Villages Tanzania jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja  

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AWAPONGEZA WABUNGE WALIO KULA KIAPO BUNGENI LEO

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa mkono wa pongezi Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara baada ya kula kuapo Bungeni jijini Dodoma leo Novemba 06, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa mkono wa pongezi Mbunge wa Korogwe Mjini baada ya kula kuapo Bungeni jijini Dodoma leo Novemba 06, 2018.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa mkono wa pongezi Mbunge wa Liwale, Mohamed Kuchauka baada ya kula kiapo Bungeni jijini Dodoma leo Novemba 06, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akijadiliana jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde  wakati wa picha ya pamoja katika Viwanja vya Bunge na  Viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa  Dodoma leo Novemba 06, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images