Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

WAMASAI SIMANJIRO WATAKIWA KUACHA KUWATUMIA WATOTO WA KIKE KAMA BIDHAA

$
0
0
Na Anthony Ishengoma – Manyara

Jamii ya Wamasai nchini imetakiwa kuacha tabia ya kumtumia mtoto wa kike kama bidhaa na kuanza kuwapeleka watoto wakike shuleni badala ya kuwaozesha wakiwa wadogo kama mtaji wa kujipatia ng’ombe.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile aliyasema hayo jana alipofanya ziara ya siku moja Wilayani Simanjiro kwa aijili ya kukagua hospitali lakini pia kuzindua Kituo cha Mtandao wa Kupinga Ukeketaji kilichopo Makao Makuu ya Wilaya ya Simajiro eneo la Orkesumet.

Dkt. Ndugulile aliongeza kuwa ni muhimu kwa Wamasai kuanza kujenga jamii inayoelimika ili kuweza kutokomeza baadhi ya mila zisizofaa kwani jamii ikielimika baadhi ya mila na desturi katika jamii husika upotea zenyewe.

Awali Mkurugezi Mtendaji wa Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji Simanjiro Bw. Francis Selasini alimwambia Dkt. Ndugulile kuwa kituo chake kilimwokoa mtoto wa miaka minane ambaye alikuwa anakaribia kuolewa na mzee wa miaka 72 ambaye tayari alishakubaliana na wazazi wake kumuoa na mtoto huyo kwa sasa amemaliza darasa la saba kwa msaada wa kituo hicho.

Dkt. Ndugulile aliwaambia Wazee wa Kimila kutambua kuwa ni kinyume na matakwa ya serikali na ni dhambi kubwa kuozesha watoto wadodo hususan watoto walio chini ya miaka kumi na nane akiitaka jamii hiyo kubadilika na kuelimisha watoto wa kike kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

Naibu Waziri Ndugulile pia amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mhandisi Zephania Chaula kuwezesha wanawake wa kimasai kiuchumi kwa kuwapatia mikopo ili waweze kuzalisha mali kama hatua ya kupambana na umasikini kwani wanaume wao mara nyingi uhama na mifugo yao na kuacha na mzigo mkubwa wa kutunza familia.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na Laigwenani wa Kimasai Mzee Maika Ngukuu (84) wakizindua Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji cha Shirka la NAFGEM kilichopo Orkesumet Simanjiro mkoani Manyara.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akionesha kufuraishwa kwake na baadhi ya bidhaa za wanawake wajasiliamali wakimasai wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji Orkesumet Simanjiro Mkoani Manyara .
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akipanda mti mara baada ya kuzindua Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji Orkesumet Simanjiro Mkoani Manyara.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akiwa na Wasichana waliokolewa na vitendo vya ukatili wa ukeketaji wanaopatiwa mafunzo ya ujasiliamali na Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji Orkesumet Simanjiro Mkoani Manyara.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW


MOI KUANZA KUZIBUA MISHIPA YA DAMU ILIYOZIBA KWENYE UBONGO

$
0
0
Mkurugenzi wa Ubora na Uhakiki wa Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia Wazee na Watoto Dr. Mohamed Mohamed akifungua kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu.

Mkurugenzi wa ubora na uhakiki wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt Mohamed Mohamed leo tarehe 5/11/2018 amefungua kongamano la tano kimataifa la mafunzo ya madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu katika ukumbi mpya wa Mikutano MOI ambapo mafunzo yanafanyika kwa siku tano, siku mbili za nadharia na siku tatu za mafunzo ya vitendo ambayo itahusisha upasuaji.

Dkt Mohamed amesema kongamano hili la tano limehudhuriwa na zaidi ya madaktari 100 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Ethiopia, Malawi, Namibia na nchi nyingine za Afrika, ulaya, na marekani ambapo mafunzo yatatolewa na Madaktari bingwa 8 wazalendo kutoka MOI na wengine 15 kutoka Marekani na Ulaya.
Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya MOI Prof Charles Mkonyi akizungumza katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amesema mafunzo haya yameratibiwa na Taasisi ya MOI kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Weil Cornel cha New York Marekani ambapo hii ni mara ya tano kufanyika hapa Tanzania (MOI).

“Mafunzo ya mwaka huu yatakuwa ya kipekee zaidi kwani wataalamu wetu watajifunza jinsi ya kufanya upasuaji wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo (Celebral aneurysm) kwa mara ya kwanza hapa nchini ,kabla ya hapo wagonjwa walilazimika kwenda nje ya nchi kwa gharama kubwa ” Alisema Dkt Boniface.

Dkt Boniface amesema gharama za upasuaji huu nje ya nchi ni zaidi ya Tsh milioni 60 na hapa nchini haitazidi Tsh milioni 10 hivyo kuanza kwa huduma hii kutaokoa fedha nyingi za Serikali na tayari Serikali imeshanunua darubini maalum ya kufanyia upasuaji huu mkubwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akitoa neno la ukaribisho katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu.

Aidha, Dkt. Roger Hartl Mkurugenzi wa Kitivo cha upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu kutoka chuo kikuu cha Weill Cornell amesema ni heshma kubwa kufika Tanzania kwa mara nyingine, pia kupata fursa ya kubadilishana uzoefu na madaktari wa Tanzania na nchi nyingine duniani.

“Pamoja na mafunzo ya nadharia tutafanya upasuaji kwa pamoja kwa njia za kisasa, hili ndilo lengo letu hasa la kuja hapa, tunataka wenzetu wa MOI na madaktari walio mafunzoni waweze kutoa huduma hizo kwa weledi mkubwa, tumekuwa tukifanya hivi kwa muda sasa na tunaona wanakwenda vizuri hii inatia faraja sana” alisema Dkt Hartl.

Pia, Dkt. Hartl amesema mafunzo ya mwaka huu yanalenga kuwajengea uwezo washiriki ili waweze kutumia teknoljia ya kisasa ya matibabu ya Ubongo na mgongo na kuwapa mbinu mpya za upasuaji hususani kwa mgonjwa aliyeumia kwenye eneo la mfumo wa fahamu hususani kwenye ubongo , uti wa Mgongo na mishipa ya fahamu iliyoharibika.

Taasisi ya MOI imeendelelea kufanya mageuzi makubwa katika huduma zake kwa lengo la kuhakikisha huduma zote za kibingwa zinapatikana hapa nchini na kuendelea kuokoa maisha ya watanzania na nchi nyingine za Afrika ambazo zinazoleta wagonjwa kutibibiwa MOI.
Kiongozi wa jopo la wakufunzi kutoka chuo kikuu cha Weill Cornel cha marekani Prof Roger Hartl akiwasilisha mada katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo ,Mgongo na Mishipa ya fahamu.
Mkurugenzi wa Ubora na Uhakiki kutoka Wizara ya Afya Dkt Mohamed Mohamed wapili kutoka kushoto aikwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano kutoka mataifa mbalimbali. Wakwanza kushoto ni Profesa Charles Mkonyi mwenyekiti wa bodi ya wadhamini MOI, watatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface na wakwanza kulia ni Kiongozi wa jopo la wakufunzi kutoka marekani Profesa Roger Hartl.

PWANI YATILIANA SAINI MKATABA WA USAMBAZAJI DAWA ,VIFAA TIBA KUPITIA MSHITIRI MMOJA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI 

MKOA wa Pwani,umefikia asilimia 90 ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ,hadi kufikia octoba 2018, hatua ambayo inaelekea kwenda kupunguza kero ya upungufu wa dawa na vifaa hivyo kwenye vituo vya afya.

Hayo yalibainika ,wakati wa kikao cha mkoa cha zoezi la kusaini mkataba wa usambazaji wa dawa ,vifaa tiba na vitendanishi kupitia mfumo wa mshitiri mmoja (prime vendor system),zoezi ambalo limefanywa baina ya katibu tawala wa mkoa Theresia Mbando na mkurugenzi wa Astra Pharmacy Ranjiy Jha.

“Kwa mujibu wa taarifa zinavyotolewa katika mfumo wa kukusanya na kuchambua data za afya (DHIS 2 ),hadi kufikia kipindi hicho wamefikia asilimia hiyo jambo ambalo limenifurahisha” alisema Theresia . Theresia alisema ,kwa hatua waliyofikia mzabuni huyo anatarajiwa atafikisha lengo la upatikanaji wa dawa kwenye vituo na halmashauri za mkoa kwa asilimia 100.

“Wananchi wamekuwa wakilalamikia juu ya upungufu wa dawa na vifaa tiba katika vituo vyetu hivyo ni imani yangu kwa hatua hii ,itakuwa muarobaini wa malalamiko hayo “ Aidha alisema, kumekuwa na wastani wa utimilizaji wa oda kwa kiwango ambacho ni cha kubadilika badilika kutoka bohari ya madawa (MSD). “Kufuatia uwepo wa mshitiri huyu naamini kwa bidhaa ambazo hazijatimia utimilifu kama ziliombwa bohari ya madawa zitajaziwa na mshitiri na hilo ndilo lengo kuu “alifafanua Theresia .

Kwa mujibu wa Theresia, baada ya kusaini mkataba huo halmashauri hazitakiwi kutumia wazabuni wengine na badala yake zitatakiwa kununua kwa mzabuni aliyepatikana kisheria kupitia mchakato uliofanywa na OR-TAMISEMI mwaka 2017. Nae mfamasia wa mkoa wa Pwani Elias Mabonesho ,alielezea mfumo huo ulianzia Dodoma kama majaribio na kwasasa uko katika mikoa ya Morogoro ,Shinyanga na sasa Pwani .

Anasema ,mfumo utasimamiwa na ofisi ya katibu tawala wa mkoa kupitia ofisi ya uratibu wa mfumo wa mshitiri mmoja chini ya Mganga mkuu wa mkoa akisaidiwa na mfamasia ambae ndie mratibu huu . Kwa upande wa wakurugenzi na waganga wakuu wa wilaya ,akiwemo mkurugenzi wa Mafia ,Erick Mapunda alisema ,kwa mfumo wa Jazia tatizo la ukosefu wa dawa linakwenda kuwa historia.
Katibu tawala wa mkoa wa Pwani Theresia Mbando (wa pili kulia ) na mkurugenzi wa Astra Pharmacy Ranjiy Jha(wa kwanza kushoto ) wakitia saini mkataba wa usambazaji wa dawa ,vifaa tiba na vitendanishi kwa kupitia mfumo wa mshitiri mmoja (prime vendor system),wa kwanza kulia ni mfamasia wa mkoa Elias Mabonesho


Katibu tawala wa mkoa wa Pwani Theresia Mbando (wa kwanza kulia ) akisaini mkataba wa usambazaji wa dawa ,vifaa tiba na vitendanishi kwa kupitia mfumo wa mshitiri mmoja (prime vendor system)

Baadhi ya wakurugenzi na waganga wakuu wa wilaya ambao wameshiriki katika zoezi la utiaji saini wa mkataba wa usambazaji wa dawa ,vifaa tiba na  vitendanishi kwa kupitia mfumo wa mshitiri mmoja (prime vendor system).(picha na Mwamvua Mwinyi ) 

DAWA YA WAKEKETAJI WATOTO WACHANGA YAJA

$
0
0
Dawa ya wale wanaofanya vitendo vya Ukeketaji kwa watoto wadogo na ukeketaji kwa ujumla nchini inaelekea kupatikana kutokana na kukidhiri kwa vitendo vya ukeketaji vya aina hiyo. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akizundua kituo Maalum cha kuwasaidia wahanga wa vitendo vya ukeketaji cha Shirika la NAFGEM kilichopo  Orkesumeti Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali inaendelea na mapambano dhidi ya vitendo vya ukeketaji kwani inaonekana wahusika wamenzisha mbinu mpya za ukeketaji baada ya watoto kupta elimu juu ya madhara ya ukeketaji na wengi wao kukimbia kufanyiwa vitendo hivyo. Naibu Waziri Ndugulile amezitaja mbinu mpya za ukeketaji ni pamoja na kuwakeketa Watoto wachanga, kutofanya Sherehe wakati wa ukeketaji na kufanya vitendo hivyo nyakati za usiku.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Serikali haipingi mila na desturi zilizopo katika makabila ndani ya Tanzania ila kusiwepo na mila zisizofaa ambazo zinaleta ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa vitendo vya ukeketaji.

"Vitendo hivi havikubaliki katika Tanzania ya awamu hii tuongeze nguvu katika kupambana na vitendo vya ukeketaji" alisisitiza Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile pia amewataka viongozi wa kimila kutoa ushirikiano kwa Serikali na wadau katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na vitendo vya ukeketaji katika maeneo yao.

"Ni aibu kubwa sana kwa kukeketa na kuwaozesha watoto wadogo ambao tunawaharibia ndoto zao" alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro  ameahidi kushirikiana na wadau katika kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya ukeketaji Wilayani humo.

"Nikuahidi Naibu Waziri tutaendelea na mapambano dhidi ya vitendo hivi hatutamuacha mtu salama " Alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Mkurugezi Mtendaji wa Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji Simanjiro Bw. Francis Selasini amesema Shirika lake liekuwa likiwasaidia watoto wa kike wanakimbia vitendo vya ukektaji na kuwapa elimu ya ujasilimari na kuwasomesha wale ambao hawakupayta nafasi ya kusoma na mpaka sasa wamefanikiwa kusomesha mtoto mmoja wa kike ambaye amerudi na kuanza kuwafundisha wenzake.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Simanjiyo Mhandisi Zephania Chaula amesema Serikali yaWilaya imeweka nguvu kubwa katika kupambana na vitendo vya ukeketaji katika Wilaya hiyo na kuweka jitihada za kuondoka na mila zisizofaa zinazo mkandamiza mtoto wa kike.

Naye moja wa msichana aliyekimbia ukeketaji Nagalali Molell amesema avitendo vya Ukeketaji bado vinaendelea ktika maeneo ya vijijini na elimu zaidi inahitajika ili kuweza kuikomboa jamii hiyo kwani watoto wa kike wamekuwa wakikandamizwa kwa kulazimishwa kuolewa kukuketwa na kutopata elimu sawa wa watoto wa kiume.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akiwa na Wasichana waliokolewa na vitendo vya ukatili wa ukeketaji wanaopatiwa mafunzo ya ujasiliamali na Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji Orkesumet Simanjiro Mkoani Manyara.

AGPAHI YATOA MSAADA WA MAGARI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI MWANZA

$
0
0
Asasi ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Health Initiative (AGPAHI) inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia nchini Tanzania imetoa msaada wa magari mawili aina ya Nissan Patrol kwa halmashauri za wilaya za Buchosa na Misungwi mkoani Mwanza kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri hizo.

Magari hayo yenye namba za usajili DFPA 7015 na DFPA 7016 yana thamani ya shilingi milioni 186 yamenunuliwa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) chini ya vituo vya Kudhibiti Magonjwa na Kinga (CDC).

Hafla fupi ya Makabidhiano ya magari, imefanyika leo Jumatatu Novemba 5,2018 wakati wa kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoa wa Mwanza kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella.

Akizungumza wakati wa kukabidhi magari hayo kwa Mkuu huyo wa mkoa, Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa alisema msaada huo wa magari ni kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma za afya hususani za VVU na UKIMWI kwenye vituo vya kutolea huduma.

Dkt. Mwakyusa alisema, AGPAHI imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na halmashauri katika kuboresha huduma za VVU na UKIMWI kwa ajili ya ustawi wa wananchi na taifa kwa ujumla.
Magari yenye namba za usajili DFPA 7015 na DFPA 7016 yenye thamani ya shilingi milioni 186 yaliyonunuliwa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) chini ya vituo vya Kudhibiti Magonjwa na Kinga (CDC).
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella, akikata utepe wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari yaliyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya kuboresha huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri ya wilaya ya Buchosa na Misungwi mkoani Mwanza.
Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Buchosa,Crispin Luanda na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella (wa tatu kulia) wakioneshana magari yaliyotolewa na AGPAHI.
Muonekano wa magari yaliyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya kuboresha huduma VVU na UKIMWI katika halmashauri ya wilaya ya Misungwi na Buchosa.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa, akikabidhi ufunguo wa gari kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella.

SERIKALI YA MAREKANI YAZINDUA MRADI WA KUHIFADHI MAZINGIRA UKANDA WA MAGHARIBI MWA TANZANIA

$
0
0
Dar es Salaam: Novemba 5, 2018, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Inmi Patterson na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa Muungano na Mazingira Ndugu January Makamba wamezindua mradi utakaogharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni 20 ili kuboresha usimamizi katika kuhifadhi mazingira kwenye ukanda wa magharibi mwa Tanzania.

Mradi huu wa uhifadhi wa mazingira unafadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na utatekelezwa kwa ushirikiano wa pamoja na Taasisi ya Jane Goodall (JGI).

Mradi huu mpya utasaidia watu wa Mikoa ya Kigoma na Katavi, pamoja na serikali za mitaa, katika utekelezaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi na utakaonufaisha vijiji 104.

Mradi huu wa Uhifadhi wa Mazingira umeundwa kulinda mazingira wakati pia unasaidia wananchi katika shuhuli za kujikimu kiuchumi na maisha bora kama vile uzalishaji wa kahawa na utalii asili kwa ajili ya watanzania. Taasisi ya Jane Goodall itafanya kazi kwa karibu na jamii ili kuhamasisha mazoea endelevu zaidi ya usimamizi wa ardhi na kukuza elimu ya mazingira, kwa kutumia majukwaa kama vile mradi iliyofanikiwa sana ya Roots na Shoots ya Taasisi ya Jane Goodall.

Zaidi ya hayo, kama sehemu ya ruzuku hii, Taasisi ya Jane Goodall itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuunda mifumo imara zaidi katika kuhifadhi na kulinda sokwe walioko ndani na nje ya maeneo tengefu.

UKARABATI KIVUKO CHA MV. CHATO WAKAMILIKA

$
0
0
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akijadiliana jambo na Meneja wa kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza Major Songoro mara baada ya kukagua kivuko cha MV. Chato ambacho ukarabati wake umemalizika, kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba tani 75 sawa na abiria 200,na magari 6 kinatoa huduma Wilaya ya Chato, maeneo ya Ikumba Itale, Izumacheli, Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita .

 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle wa pili kulia akisisitiza jambo kwa Meneja wa kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Boatyard Major Songoro wa pili kushoto mara baada ya kukagua kivuko cha MV. Chato ambacho ukarabati wake umemalizika, tukio lililofanyika katika yadi ya Songoro iliyopo Ilemela mjini Mwanza. Kivuko hicho cha tani 75 kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 na kinatoa huduma katika Wilaya ya Chato, maeneo ya Ikumba Itale, Izumacheli, Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita. Kushoto ni Mkurugenzi Huduma za Ufundi (WUUM) Mhandisi Lazaro Vazuri na kulia ni Meneja wa TEMESA mkoa wa Mwanza Mhandisi Hassan Karonda.

 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (aliyevaa suti) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua kivuko cha MV. Chato ambacho ukarabati wake umemalizika, tukio lililofanyika katika yadi ya Songoro mjini Ilemela Mwanza. Kivuko hicho cha tani 75 kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 na kinatoa huduma katika Wilaya ya Chato, maeneo ya Ikumba Itale, Izumacheli, Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita.

 Muonekano wa kivuko cha MV. Chato mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake. Kivuko hicho cha tani 75 kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 kinatarajiwa kurudishwa katika kituo chake kuendelea na kazi ya kuvusha abiria maeneo ya Ikumba Itale, Izumacherl, Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita.


Kivuko cha MV. Chato kikielea majini baada ya kukamilika kwa ukarabati wake ambao. Kivuko hicho cha tani 75 kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 kinatarajiwa kurudishwa katika kituo chake  Wilayani Chato Mkoani Geita kuendelea na kazi ya kuvusha abiria.

PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA)



MICHUZI TV: SPIKA NDUGAI AZUNGUMZIA MUSWADA WA SHERIA, BUNGE KUANZA KESHO


GOOD NEWS KWA WAZEE WALIOFANYA KAZI AFRIKA MASHARIKI KUHAKIKIWA MALIPO YA PENSHENI NA TRC

ALI KIBA ATAJWA KUSHIRIKI TAMASHA LA WASAFI

REVOCATUS KUULI AFUNGIWA MAISHA KUTOKUJIHUSISHA NA SOKA

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) imemfungia kifungo cha maisha cha kutojihusisha na Soka aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati cha Uchaguzi wa Shirikisho hilo Wakili Revocatus Kuuli. 

Hukumu hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hamidu Mbwezeleni ambaye amezitaja sababu kubwa za kufungiwa kwa Kuuli kuwa ni kwenda kinyume na misingi ya Katiba ya TFF kwa kusambaza barua alizotumiwa na Katibu wa Shirikisho hilo Wilfred Kidao. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya TFF, Mbwezeleni amesema kuwa Kuuli amefungiwa kufuatia sakata la uchaguzi Simba ambapo alihojiwa kwanini ameamua kuuzuia mchakato wake kipindi unaanza na kupewa siku tatu kwa ajili ya kutoa majibu. 

Wakili hiyo alipewa siku hizo na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Wilfred Kidao lakini hakuweza kujibu chochote na kisha baadaye kuja na majibu ya dhihaka na lugha kali kwa Kidao. Hata hivyo, Kuuli kabla hajafungiwa ilielezwa kuwa angetangaza kuachia nafasi hiyo ndani ya TFF akielezwa kukerwa kuingiliwa kwenye majukumu yake ya kazi. 

Licha ya kuuzia mchakato wa uchaguzi Simba, klabu hiyo iliendelea nao kama kawaida ambapo jana rasmi imefanikisha kufanya uchaguzi wake na kuwapata viongozi wapya. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF)  Hamidu Mbwezeleni akifafanua hukumu ya kifungo cha maisha cha kutojihusisha na Soka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati cha Uchaguzi wa Shirikisho hilo Wakili Revocatus Kuuli. 

MICHUZI TV: Pinda ashindwa kujizuia kuhusu Mvinyo wa Dodoma.

CDF YATOA ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE NA WATOTO KUPITIA MICHEZO.

$
0
0
Na Agness Francis, blogu ya Jamii. 


Taasisi inayopinga ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake CDF ikishirikiana na ISDI wamefanya bonanza kwa ajili ya kuhamasisha na kutoa elimu ya utokomezaji wa ukatili.

Boanza hilo lilofanyika katika  kata ya Kitunda halmashauri ya Ilala imehusha michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu na kuhamasisha wanaume wawe mstari wa mbele kupinga ukatili wa kijinsia.


Akizungumza na waandishi wa habari Mgeni rasmi wakati wa bonanza hilo, Afisa Ustawi wa Jamii Ilala Joyce Maketa  amesema Kuwa kwa kuwakutanisha vijana katika bonanza hilo linasaidia kufikisha ujumbe kwa jamii nzima katika kuhakijisha janga la ukatili wa kijinsia  linapingwa vikali hapa nchini. 


"Katika Kata ya Kitunda yapo mambo mbalimbali yanayohusisha ukatili wa kijinsia hususani kwa watoto na kumpelekea kupoteza haki zake, na sana yanakuwa kwenye upande wa  kulawitiwa na ukeketaji, hivyo basi uwepo wa bonanza hilo litasaidia ongezeko la wigo la watu kupata ujumbe huo na ukatili wa kijinsia katika manispaa ya Ilala"amesema Maketa. 

Aidha Afisa Uhamasishaji wa wanaume jukwaa la utu wa mtoto CDF, Kiswigo Mwang'onda amesema Kuwa lengo la kuwepo kwa bonanza hilo na kushirikisha michezo ni kusaidia ukatili huo unatokomezwa kwa kuwa wanaume ndio vyanzo vya ukatili huo,kwa kuhakikisha mtoto anapata haki Zote zinazostahili kama elimu na mali.

"Baadhi ya wanawake wengine hapa nchini hufanya vitu ili waonekane bora kwa wanaume zao Kama suala la ukeketaji, ikiwa pia wanaume ndio sehemu ya matatizo hayo,kupitia michezo mwanaume atapata elimu ili kutatua tatizo hili na kuwa suluhisho la kudumu"amesema Mwang'onda. 

Hata hivyo Nahodha wa timu ya Kitunda, Miraji Suleiman amesema kuwa bonanza hilo Kwa ajili ya kupinga unyanyasaji,ukeketaji,ulawiti pamoja na mimba za utotoni litasaidia kutoa ujumbe kwa Jamii nzima ya wakazi wa kitunda.



"Taasisi kama hizi zikiwa nyingi na kuhamasisha upingaji wa ukatili kwa kutumia michezo kuna watoto pia watajifunza siku nyingine watakuwa wajumbe wazuri kuhusiana na ukatili kijinsia itasaidia jamii mbali mbali kupata elimu hiyo"amesema Nahodha Suleiman.

Afisa uhamasishaji wanaume na utu wa mtoto kutoka Taasisi ya  CDF Kiswigo Mwang'onda akizungumzia  lengo la kufanya bonanza hilo katika viwanja vya Shule ya Msingi Kitunda Jijini Dar es Salaam na kuhusisha vijana na kusaidia kutoa elimu Kwa wanaume juu ya utokomezaji wa ukatili kwa watoto na kinamama
Afisa Ustawi wa Jamii  Halmashauli ya Wilaya ya Ilala ambaye ni  Mgeni rasmi katika bonanza  kuhamasisha na kutoa elimu ya utokomezaji wa ukatili Joyce Maketa akisalimina na wachezaji wa mpira kabla ya kuanza kwa mechi katika Viwanja vya Shule  ya Msingi Kitunda Jijini Dar es Salaam.
Afisa Ustawi wa Jamii  Halmashauli ya Wilaya ya Ilala Joyce Maketa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa mpira pamoja na wafanyakazi wa  Taasisi za CDF na ISDI katika bonanza la kuhamasisha utokomezaji wa ukatili wa watoto na wanawake katika viwanja vya Shule ya Msingi Kitunda Jijini Dar es Salaam.

TAMASHA LA WASAFI FESTIVAL KUZINDULIWA RASMI NOVEMBA 24 MTWARA

$
0
0
Na Khadija Seif,Globu ya Jamii 

Msanii wa Bongofleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platinumz ametangaza ramsi kuanza kwa tamasha la Wasafi Festival Novemba 24 mwaka huu. 

Tamasha hlo linalotarajiwa kufanyika kwenye mikoa mbalimbali nchini litaanzia Mkoani Mtwara ikiwa ni mara ya kwanza toka kuanza kwa Tv na Redio.

Akizungumza na wadau pamoja na wanahabari Leo Jijini Dar es salaam, Diamond amesema kuwa tamasha la Wasafi Festival lina lengo la kutoa burudani nchini na nje ya nchi ili kutangaza mziki wa kitanzania zaidi na kufundisha jamii jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii vizuri. 

Diamond amesema kuwa, licha ya kutangaza mziki huo kwenye mikoa ambayo itapata kushuhudia burudani hiyo ni wataanzia tarehe 24 mwezi huu kwenye mkoa wa Mtwara katika viwanja vya Nangwanda na ikifatiwa na mkoa wa Iringa,Morogoro , Zanzibar na mikoa mingine na pamoja na nchi ya Kenya. 

Amefafanua zaidi katika kila Mkoa utakaotembelewa pia watapata fursa kwa kukarabati shule , Wanafunzi kupatiwa sare za shule, madaftari na kupatiwa madawati huku kwa wakina mama wasiopungua 200 kupewa mitaji ya kibiashara ili kujikwamua kiuchumi . 

Sambamba na hilo wasichana wasiopungua 20 watapewa mafunzo ya urembo wa uso pamoja na vifaa vya kupambia. Meneja wa msanii Daimond Platinum Hamis Tale maarufu kama Babu Tale amewaambia wazi kwa sasa radio ya wasafi iko hewani kupitia masafa ya 88.9 ambayo ipo kwa ajili ya kutoa fursa kwa ambao vipaji vyao havijapata nafasi ya kuvuma. 

Tale ametoa rai kwa mashirika ,wadau na wanamuziki ambao wangependa kushiriki katika tamasha hilo nafasi zipo wazi wanakaribishwa.

Msanii wa Bongofleva Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akizungumza na waandishi wa habari wakati wakutambulisha rasmi tamasha la Wasafi Festival Nov 24 mwaka huu Mkoani Mtwara.

TFF YATANGAZA UCHAGUZI WA YANGA KUFANYIKA JANUARI 13 2019

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF imetangaza kuanza mchakato wa uchaguzi maalum wa kujaza nafasi ambazo zilizo wazi ndani ya klabunya Yanga ikiwemo ile ya Mwenyekiti.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ally Mchungahela amesema zoezi la kuchukua fomu kwa wagombea litaanza Novemba 8 hadi 13 2018 na wanachama wote watatakiwa kuhakiki majina yao kwenye matawi.

Aidha ameeleza kuwa uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Januari 13 2019. TFF wamemua kutangaza rasmi kuanza mchakato huo mara baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuwataka wausimamie wakieleza kuwa kamati ya Yanga haijitoshelezi.

BMT waliitaka TFF itimize majukumu hayo katika kikao na wanahabari kilichofanyika siku chache zilizopita.BMT iliiwataka Yanga kuitisha uchaguzi wake kwa ajili ya kujaza nafasi za viongozi waliojizuru huku ikiwemo ya Manji aliyeiandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya Mwenyekiti wa Klau hiyo

Taarifa ya BMT kwa vyombo vya Habari ilisema kwamba, Yanga imebaki na Wajumbe wanne kati ya 13 waliochaguliwa katika uchaguzi wa Juni 12, mwaka 2016 Dar es Salaam.Viongozi waliojiuzulu ndani ya klabu hiyo ni Mwenyekiti Yusuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga, na wajumbe Hashimu Abdallah, Salum Nkemi, Omary Said, Ayoub Nyenzi na huku waliobaki ni wajumbe Thobias Lingalangala, Samwel Lukumay, Siza Lyimo na Hussein Nyika. 
Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya TFF , Ally Mchungahela akizungumza na waandishi kuhusiana na uchaguzi wa klabu ya Yanga.

MTEGO WA DC MURO,POLISI WAFANIKISHA KUWANASA 'WATIAJI MIMBA' MABINTI WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ARUMERU

$
0
0
Na Imma Msumba Arumeru, 

MKUU wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Jerru Muro kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wilayani humo limewakamata watuhumiwa watatu ambao wameshiriki kumtoa mimba mwanafunzi wa kidato cha nne kwa kutumia dawa za miti shamba suala ambalo linachochea mimba kwa wanafunzi na kuzorotesha elimu yao.

Akizungumza leo wilayani hapa, Muro amesema kuwa wamebaini tukio hilo baada ya kuweka mtego ambao umefanikisha kuwabaini watuhumiwa hao pamoja na mtia mimba ambao wamefikishwa polisi na kisha mahakamani

Akielezea jinsi alivyopewa ujauzito na mchakato wa kutaka kutolewa, mwanafunzi Aikaeli Pallangyo amesema ni kweli alipata ujauzito kwa kurubuniwa na kijana wanaeishi nae jirani nyumbani ambae alikuwa akimrubuni kwa kumpatia fedha

Kwa upande wao watuhumiwa wa sakata hilo akiwamo kijana aliyempa mimba binti,pamoja na mama mzazi wa Aikaeli na mwanamke ambae ni ndugu wa Kijana aliempa mimba ambae anatajwa kuhusika na kumtoa ujauzito binti wametoa sababu mbalimbali ambazo hata hivyo zimeonekana kukinzana zenyewe kwa zenyewe kutokana na mama wa binti kukiri kuwafahamu watuhumiwa wenzake na kuelezea tukio la mchezo mzima ulivyokuwa 

Akidhibitisha taarifa za binti huyo kuwa mjamzito na kutoa ujauzito, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Meru Dkt. Cosmas kilasara amesema vipimo vya awali vilionyesha binti kuwa mjamzito na vipimo walivyofanya tena vimeonyesha binti sio mjamzito tena.

Ambapo amesema hata hivyo binti huyo ameendelea kupata dalili zote za kuwa na ujauzito ikiwemo ya maziwa kutoka. Kutokana na tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amevigiza vyombo vya usalama kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote ambao wamehusika katika tukio hilo.Pia amelitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha wanawakamata na wanawafikisha mahakamani watu wote waliohusika katika kuwapa ujauzito wanafunzi 57 kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita. 

SHIRIKA LA WWF LAFANYA ZIARA KUFUATILIA MAENDELEO YA UTEKELEZAJI MRADI WA SECAD WILAYANI NAMTUMBO

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la  World Wide Fund for Nature (WWF) limefanya ziara katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi ujulikanao SECAD program ( Selous Eco-system Conservation and Development program).

 SECAD ni mradi ambao kwa jumla utatekelezwa kwa miaka mitano ikiwa ni awamu ya kwanza na ya pili ambapo umejikita kuhakikisha wanaongeza uhifadhi wa mazingira kwa maana ya kwenye hifadhi ya Selous pamoja na ushoroba (corridor) unaounganisha pori la akiba la Selous na hifadhi ya Niassa ipatikanayo nchini Msumbiji

Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo jana kwamba ugeni wa shirika hili uliofika wilayani kwake ulitembelea na kujionea maendeleo ya mradi  na kutembelea jumuiya ya uhifadhi ya Mbarang'andu ambapo walipata taarifa ya mradi na kujionea mafanikio, mipango na changamoto kwa sasa. 

Mkuu wa Wilaya huyo ameueleza ugeni wa shirika hilo kuwa moja ya mafanikio ni mradi wa ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kurina asali ambao unaosimamiwa na jumuiya hiyo pamoja na mpango wa ujenzi wa kiwanda cha kuongezea thamani asali pamoja na mabwawa ya samaki.

Kuhusu changamoto amesema moja ya changamoto ya mradi ni  wananchi kuvamia maeneo ya hifadhi na kufanya shughuli za kibinadamu kama kilimo na ufugaji

Pia walitembelea Chuo cha Likuyu ambacho kinatumika kufundisha VGS (village scouts) wanaotumika kulinda hifadhi hizo. 
 Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo akipewa maelezo kuhusiana na maendeleo ya mradi wa wa SECAD program ( Selous Eco-system Conservation and Development program) wakati SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la  World Wide Fund for Nature (WWF) likifanya zaira wilayani yumo kufuatilia mradi huo  
 Eneo la mradi wa ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kurina asali
 Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo akiwa sambamba na Wadau wa  SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la  World Wide Fund for Nature (WWF) wakionesha chupa ya asali ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya mradi wa ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kurina asali ,ambao unasimamiwa na jumuiya hiyo pamoja na mpango wa ujenzi wa kiwanda cha kuongezea thamani asali pamoja na mabwawa ya samaki. 
 Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo akikaribishwa mara baada ya kuwapokea wageni kutoka SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la  World Wide Fund for Nature (WWF) llilofanya ziara katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi ujulikanao SECAD program ( Selous Eco-system Conservation and Development program).

HABARI KUTOKA UMOJA WA MATAIFA

ALIYOYAZUNGUMZA NAIBU WAZIRI DKT NDUGULILE WAKATI ALIPOKUTANA NA WAZEE WA KIMILA WILAYA YA SIMANJIRO

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 05.11.2018

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images