Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Article 2


RELI TV: WAZEE WALIOFANYA KAZI AFRIKA MASHARIKI KUHAKIKIWA MALIPO YA PENSHENI NA TRC

MAONYESHO YA SWAHILI FASHION WEEK KUFANYIKA NOVEMBER 30 HADI DISEMBA 2 MWAKA HUU JIJINI DAR

$
0
0
Katika kuendeleza mafanikio makubwa na ya kipekee kwa msimu wa 11  ya maonyesho  ya jukwaa la mitindo (SWAHILI FASHION WEEK) ambalo ni la kipekee Afrika mashariki, maandalizi yafunguliwa rasmi jijini Dar es salaam.

Mbunifu  wa mitindo nchini Mustafa hassanali amezungumza na wadau, wabunifu pamoja na wanahabari kuwa maonyesho hayo yatafunguliwa rasmi tarehe   30 mwezi huu mpaka tarehe 2 disemba katika  ukumbi wa makumbusho ya taifa posta na amesema kuwa maandalizi ya mwaka huu ni ya kusisimua na kufurahisha sababu kazi za mitindo zipo na ni za hali ya juu .

Hassanali  amesema kwa utiifu wote  lengo la kuendeleza na kuimarisha  nafasi ya mitindo kwa Afrika  linabaki kuwa mbele,kupitia jukwaa hili na mchango mkubwa wa waandishi wa habari tutaendelea kuunga mkono vipaji  vilivyopo katika sekta ya mitindo.


Aidha,amefafanua zaidi licha ya kuunga mkono kuendeleza vipaji bali pia kutengeneza na kukuza soko la kimataifa na ndio sababu kuu ya kuunga mkono kutekeleza juhudi za Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Katika sera ya kuelekea uchumi wa viwanda kupitia bidhaa za nguo zilizotengenezwa Tanzania.

Alikadhalika balozi wa italia nchini Tanzania Robert Mengoni amesema ifike pahala kila mtu aheshimu kazi za Ubunifu wa mitindo kama biashara kutokana na wabunifu kuwekeza na kupata vipato vya kuendesha maisha yao pamoja na familia kupitia Ubunifu huo.      kwa upande wa mwakilishi wa baraza la Sanaa (BASATA) Vivian shalura amepongeza juhudi zinazofanywa na mbunifu huyo mahiri katika mitindo ambae amekua akifata sheria pamoja na vibali huku akiwa amejisajiri kikamilifu.

Shalua amewataka wabunifu chipukizi wajaribu kubuni nguo ambazo hazitawabugudhi au kudharirisha watazamaji,pia amewashauri wabunifu kukuza lugha yetu ya kiswahili kupitia baadhi ya Nguo ambazo majina yake yanatokana na kiswahili chetu kama vile mshono wa mwanamke nyonga.

DC Jokate atembelea pacha waliotenganishwa Muhimbili

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo akiwa na Ester Simon baada ya kumtembelea leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako pacha walifanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha kutokana na kuzaliwa wakiwa wameungana.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akisalimiana na Ester Simon baada ya kumtembelea wodini leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo mara baada ya kuwatembelea watoto pacha leo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na Prof. Museru na Sister Ester Mwambogoja.

WASAFI FESTIVAL 2018 YAZINDULIWA RASMI, DIAMOND AMUALIKA ALI KIBA KUSHIRIKI

MUBASHARA: DKT. ABBAS AONGELEA MIAKA MITATU YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

MAHAKAMA YAUAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUFUATILIA JALADA LA KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOWAKABILI VIGOGO WAWILI WA SERIKALI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeuagiza upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wawili wa uthamini wa madini ya almasi wa serikali kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kulifuatilia jalada la kesi hiyo na Novemba 17, 2018 wake kueleza maendeleo halisi ya upelelezi dhidi ya kesi hiyo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ameeleza hayo Leo Novemba 5, 2018 Kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa serikali, Elizabeth Mkunde kuieleza Mahakama kuwa Kesi hiyo leo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na  upelelezi bado haujakamilika na kwamba DPP ametoa maelekezo ambazo yanafanyiwa Kazi.

Baada ya maelekezo hayo, wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko ameeleza kuwa, inaumiza sana, ni mwaka sasa umepita shtaka moja lakini upelelezi wake bado haujakamilika huku dhamana ya washtakiwa ikiwa imezuiwa na kuhoji kuna makesi yenye mashtaka mengi upelelezi wake umekamilika ndani ya miezi mitatu, hili shtaka moja linatimiza mwaka mmoja  unaenda wa pili sasa.

Amedai, shtaka linalowakabili washtakiwa hao, limejitosheleza na lina kila  kitu toka mwaka Jana lugha ni hiyo hiyo upelelezi haujakamilika.Mheshimiwa, tunaamini kiwa DPP  anapozuia dhamana ya mtu basis huyo mtu atasikilizwa kwa wakati, tunaomba Mahakama iwalazimishe upande Wa mashtaka watueleze msimamo halisi wa upelelezi ili tujue wamekwama wapi na sisi tufuatilie." Alieleza Nkoko.

Baada ya kusikiliza hoja zote, Hakimu Mashauri emeutaka upande wa  mashtaka kulifuatilia jalada hilo la kesi. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 17. Mwaka huu.Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania  (Tansort) Archard Kalugendo na mthamini almasi wa serikali, Edward Rweyemamu ambao ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na Madini,

Kalugendo na Rweyemamu wanasota mahabusu kutokana na DPP kuzuia dhamana zao na Wanakabiliwa na  kesi ya uhujumu uchumi wakidaiwa kuisababishia serikali hasara ya sh 2.4 bilioni.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wanakabilkiwa na ashtaka la kuisababishia serikali hasara ya sh  2,486,397,982.54 ambapo wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, 2017  katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga.

Washtakiwa hao wanadaiwa kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathaminishaji wa almasi wa serikali na waajiriwa wa wizara hiyo waliisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43  ambazo ni sawa na sh 2,486,397,9.

SERIKALI YARIDHISHWA NA HUDUMA ZA PSSSF MKOA WA DODOMA

$
0
0

Na.Alex Sonna wa Fullshangweblog,Dodoma

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Jijini Dodoma,wametakiwa kutilia mkazo ulipaji wa mafao ya wastaafu kwa wakati.

Akitoa maagizo hayo leo jijini hapa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde, alipotembelea ofisi za mfuko huo kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.

Mhe.Mavunde amesema kuwa inatakiwa mlipe kwa wakati mafao kama ilivyo kauli mbiu yenu ya “Tunalipa Kuanzia jana” ili lengo la serikali la kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii, litimie .''Inatakiwa wastaafu wapewe umuhimu wa elimu kabla ya kuwalipa mafao ili waweze kujiandaa vyema kwa kuanzisha miradi na kutunza kumbukumbu za matumizi ya fedha''amesema Mavunde

Aidha Mhe.Mavunde amewaagiza wafanyakazi wote kuhakikisha wanatoa huduma stahiki zenye ubora na kwa wakati ili kuisaidia serikali kusonga mbele katika huduma ya hifadhi ya jamii.“Matarajio ni kwamba mtatoa huduma kwa ufanisi na kwa ubora ili yale matarajio ya serikali yaweze kutimia, awali kulikuwa na malalamiko watu hawapati huduma stahiki lakini naimani hakutakuwa na malalamiko hayo,”amesema Mavunde

Kwa Upande wake, Meneja wa PSSSF Mkoa wa Dodoma, Meshack Bandawe, amesema kuwa ofisi hiyo imeanza kufanya kazi zake Septemba mosi mwaka huu na kuna wanachama wanaochangia ni zaidi ya laki moja.“Tumejipanga kuwahudumia ipasavyo na hadi sasa tumekusanya Sh.Milioni 880 katika mkoa wa Dodoma na tutaendelea kusimamia na kutekeleza majukumu kwa mujibu wa sheria,”amesema Bandawe

Hata hivyo amebainisha kuwa hadi sasa wanachama 2792 wameshapita kupata huduma na wamepokea madai 796 ya wanachama wa mifuko mbalimbali iliyounganishwa kwenye mfuko huo. Bandawe amesema kuwa madai 717 yameshughulikiwa na wanachama wamelipwa mafao yao na mengine 79 yapo kwenye hatua mbalimbali za kufanyiwa kazi katika mkoa wa Dodoma tu.

Aidha amesema takribani wastaafu 1027 wanatarajiwa kustaafu katika kipindi cha 2018/19 ambapo mfuko huo umejipanga kutoa elimu ya kujipanga na ustaafu wao ikiwemo kubuni miradi ya kujiimarisha kiuchumi kwa mkoa wa Dodoma peke yake.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde,akizungumza waandishi wa habari (hawapo pichani) alipotembelea ofisi za mfuko huo leo jijini Dodoma kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde,akizungumza na Meneja wa PSSSF Mkoa wa Dodoma, Meshack Bandawe, alipotembelea ofisi za mfuko huo kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSSSF Mkoa wa Dodoma leo alipotembelea ofisi za mfuko huo kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.

Tanzania yazidi kupaa Kiuchumi

$
0
0
Tanzania kati ya nchi 10 zinazokua kiuchumi ni ya Tisa na Nchi za Kusini Tanzania ni ya Nne na Afrika Mashariki ni ya kwanza ukuaji huo wa uchumi ni kutokana na ripoti ya Benki ya Dunia.

Akizungumza na waandishi habari wakati akitoa Salaam za Rais Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari Marketing Dkt. Hassan Abbas amesema kuwa katika miaka mitatu Tanzania imekuwa ikifanya vizuri.

Amesema kuwa katika ukusanyaji mapato umepanda kutoka sh.bilioni 850 mwaka 2015 hadi kufikia sh.Trioni 1.3.Amesema kuna mashirika yameweza kufanya kazi na katika ukusanyaji wa mapato ikiwemo Dawasa , TPA pamoja shirika la Posta.

Dkt. Abbas amesema zaidi ya viwanda 3000 vimesajiliwa na vingine kufanya kazi.Ajira zaidi ya 26000 zimepatikana kutokana na viwanda na kufanya
Kazi ya mahakama ya mafisadi imeanza na kazi mbalimbali zinafanyika .

Upande wa rushwa Tanzania ya pili kwa Afrika Mashariki ya pili katika mapambano ya rushwa.Tanzania imenunua ndege za saba na Nne tayari na Desemba ndege mbili aina ya air bus.

Dkt. Abbas amesema kuwa kuna ujenzi wa reli ya kisasa na iko katika asilimia 35 pamoja na kujenga barabara ya juu ya Tazara huku zingine zikiendelea.Mardi wa stiglers Gorge kuondoa changamoto ya umeme.Amesema serikali imepeleka maendeleo kwa wananchi na sio kuwekea watu fedha mfukoni.
Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari Marketing Dkt. Hassan Abbas alipokuwa akizungumza na Wanahabari leo jijini Dar kuhusu miaka mitatu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli tangu aingie madarakani.

MAHAKAMA YAUAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUFUATILIA JALADA KWA DPP, KESI YA VIGOGO WAWILI WA UTHAMINI WA MADINI YA ALMASI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeuagiza upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wawili wa uthamini wa madini ya almasi wa serikali kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kulifuatilia jalada la kesi hiyo na Novemba 17, 2018 waje kueleza maendeleo halisi ya upelelezi dhidi ya kesi hiyo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ameeleza hayo leo Novemba 5, 2018 Kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa. Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa serikali, Elizabeth Mkunde kuieleza Mahakama kuwa Kesi hiyo leo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika na kwamba DPP ametoa maelekezo ambazo yanafanyiwa Kazi.

Baada ya maelekezo hayo, wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko ameeleza kuwa, inaumiza sana, ni mwaka sasa umepita shtaka moja lakini upelelezi wake bado haujakamilika huku dhamana ya washtakiwa ikiwa imezuiwa na kuhoji kuna makesi yenye mashtaka mengi upelelezi wake umekamilika ndani ya miezi mitatu, hili shtaka moja linatimiza mwaka mmoja  unaenda wa pili sasa.

Amedai, shtaka linalowakabili washtakiwa hao, limejitosheleza na lina kila  kitu toka mwaka Jana lugha ni hiyo hiyo upelelezi haujakamilika.

Mheshimiwa, tunaamini kiwa DPP  anapozuia dhamana ya mtu basis huyo mtu atasikilizwa kwa wakati, tunaomba Mahakama iwalazimishe upande Wa mashtaka watueleze msimamo halisi wa upelelezi ili tujue wamekwama wapi na sisi tufuatilie." Alieleza Nkoko.

Baada ya kusikiliza hoja zote, Hakimu Mashauri emeutaka upande wa  mashtaka kulifuatilia jalada hilo la kesi. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 17. Mwaka huu.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania  (Tansort) Archard Kalugendo na mthamini almasi wa serikali, Edward Rweyemamu ambao ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na Madini,

Kalugendo na Rweyemamu wanasota mahabusu kutokana na DPP kuzuia dhamana zao na Wanakabiliwa na  kesi ya uhujumu uchumi wakidaiwa kuisababishia serikali hasara ya sh 2.4 bilioni.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wanakabilkiwa na ashtaka la kuisababishia serikali hasara ya sh  2,486,397,982.54 ambapo wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, 2017  katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga.

Washtakiwa hao wanadaiwa kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathaminishaji wa almasi wa serikali na waajiriwa wa wizara hiyo waliisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43  ambazo ni sawa na sh 2,486,397,9.

NAIBU KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AKUTANA NA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, JIJINI DAR

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Ramadhani Kailima akizungumza na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Phaustine Kasike alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo Novemba 5, 2018 jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Phaustine Kasike akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Ramadhani Kailima leo Novemba 5, 2018 alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza(Picha na Jeshi la Magereza).

Wafugaji wa nyuki Iringa kunufaika na kampuni ya Ruaha farm

$
0
0
KAMPUNI  ya  uchakataji  wa  asili  ya Ruaha farm  mkoani Iringa kupitia asali yake Ruaha  Honey  imeanza  kuwaokoa  kiuchumi  wafugaji wa  nyuki  mkoani Iringa kwa kutoa  mizinga na  kuwaunganisha na  soko la asali .

"kampuni  ya Ruaha Farm  imekuja  kivingine  baada ya  kufunga mashine  za  kisasa  za  kuchakata  asali  yenye  ubora pasipo  kutumia vifaa vya  kienyeji kama moshi  na vingine "
 Mkurugenzi  mtendaji wa kampuni ya Ruaha  Honey  Fuad Abri  alisema  kuwa  kampuni yake  imeendelea  kuunga mkono jitihada za  serikali  ya  awamu ya  tano  chini ya   Rais Dkt  John Magufuli ya Tanzania  ya  viwanda.

 Alisema ubora wa  asali  ya kampuni ya Ruaha Honey  ni tofauti na  asali   nyingine  zinazouzwa  mitaani kwani  sifa  kubwa ya  asali  ya Ruaha honey ni asali halisi toka katika vijiji vinavyozunga hifadhi ya Ruaha national park. Asali ya ruaha honey ni Asali bora inayozingatia usafi wa vyombo, usafi wa uchakatishaji pamoja na ufugaji wa nyuki kwa njia salama na rafiki kwa nyuki.

 Alisema  Ruaha honey ni asali ya kampuni ya ruaha farm pamoja na wafugaji wa nyuki wa vijiji vinavozunguka hifadhi ya ruaha. 

 Kampuni ya Ruaha honey inashirikiana na  wafuga nyuki wa Iringa kwa kuwawezesha kupata mizinga ya kisasa na kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara ya ufugaji  sahihi wa nyuki ili kulinda ubora wa mazao ya nyuki yanayopatikana kama asali na nta.

 Ruaha honey pia inawapatia soko la asali wafugaji wa nyuki kwa lengo la kuinua kiuchumi kaya maskini kupitia ufugaji wa nyuki alisema  Abri. Kuwa  asali ya Ruaha ni asali halisi inayotokana na uoto asili wa miti ya Acacia, mibuyu na miti pori na maua pori hivyo  ni asali  bora   zaidi .

 Alisema  kupitia kampuni  ya Ruaha farm inafugia nyuki katika shamba lake liliopo Tungamalenga ambayo ni hifadhi ya nyuki ya kwanza binafsi Tanzania na Afrika mashariki

Lengo ni kuinua ufugaji wa nyuki wa nyanda za juu kusini  pia  kuendeleza  ufugaji wa nyuki  kisasa  kama  sehemu ya  kuwa na  viwanda  bora  vya mazao  yatokanayo na  nyuki .

 Hifadhi  ya nyuki ya Ruaha ni eneo linafanyika    utafiti mbali mbali wa nyuki pamoja na mazao yake, pia ni shamba darasa kwa wafuga nyuki wengine wanaozunguka eneo hilo.

SPIKA NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI KILICHOFANYIKA LEO TAREHE 5 NOVEMBA 2018 KATIKA OFISI YA BUNGE JIJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai aongoza kikao cha kamati ya Uongozi kilicholenga kujadili na kupokea Shughuli za Mkutano wa kumi na Tatu wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano, Pia Kupokea hati ya dharura ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha wa Mwaka 2018 (The Microfinance Bill, 2018); kilichofanyika leo tarehe 5 Novemba 2018 katika ukumbi wa Spika Jijini Dodoma. Ikiwa ni Maandalizi ya kuanza kwa Vikao vya Bunge vinavyotegemea kuanzia kesho Novemba 6, 2018 Jijini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati ya Uongozi kilicholenga kujadili na kupokea Shughuli za Mkutano wa kumi na Tatu wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano, Pia Kupokea hati ya dharura ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha wa Mwaka 2018 (The Microfinance Bill, 2018); kilichofanyika leo tarehe 5 Novemba 2018 katika ukumbi wa Spika Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya uongozi kuanzia kushoto ni Mbunge wa Bukoba Vijijini, Mhe. Jason Rweikiza, Mbunge wa kibakwe, Mhe. George Simbachawene na Mbunge wa Jimbo la Chemba, Mhe. Juma Nkamia wakiwa katika kikao cha kujadili na kupokea Shughuli za Mkutano wa kumi na Tatu wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano, Pia Kupokea hati ya dharura ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha wa Mwaka 2018 (The Microfinance Bill, 2018); kilichofanyika leo tarehe 5 Novemba 2018 katika ukumbi wa Spika Jijini Dodoma.

KUMBUKUMBU YA KUAPISHWA KWA RAIS WA AWAMU YA TANO DKT JOHN MAGUFULI MIAKA MITATU ILIYOPITA

MKURUGENZI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) AKUTANA NA WAFANYAKAZI WA SHIRIKA HILO LEO

$
0
0
Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa  Felix Maagi akimpokea Mkurugenzi Mkuu mpya Dk. Maulid Banyani katika ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa asubuhi ya leo ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufika katika shirika hilo akiwa Mkurugenzi Mkuu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Dk. Maulid Banyani akisisitiza jambo kwa Menejimenti ya Shirika.
  Mkurugenzi Mkuu Dk. Maulid Banyani akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA

TANGA KUWA MWENYEJI WA MAZOEZI YA MAFUNZO YA USHIRIKIANO IMARA 2018 YA KIJESHI YA VIKOSI VYA MAJESHI YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Mkoa wa Tanga unatarajiwa kuwa mwenyeji mazoezi ya mafunzo ya Ushirikiano Imara 2018 ya kijeshi ya vikosi vya Majeshi ya Nchi za Afrika ya Mashariki Kuanzia Novemba 9 hadi 21 mwaka huu. 

Akizungumza na waandishi wa habari hapo Mkuu wa Mafunzo na Oparesheni (JWTZ) Meja Jenerali Alfred Fabian Kapinga alisema kuwa mafunzo hayo yatalenga katika kujenga uwezo wa kukabiliana na uharibifu pamoja na majanga. 

Alisema kuwa dhumuni la zoezi hilo la kikanda ni kubadilishana uzoefu wa kiutendaji ikiwemo kuimarisha mahusiano baina ya nchi, majeshi ya Afrika Mashariki pamoja na taasisi nyingine. “Kutokana na Oparesheni Matumbawe iliyofanyika mwaka jana kuleta matokeo bora tumeona na awamu hii kuutumia mkoa wa Tanga kwa ajili ya mazoezi hayo ya vikosi “alisema Meja Jenerali Kapinga. 

Alisema kuwa mafunzo hayo ambayo yatakuwa ya awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itakuwa ni mafunzo ya ndani yameanza leo mjini hapa wakati awamu ya pili itahusisha mafunzo ya nje yatakayoanza Novemba 9 mwaka huu.Aliongeza kuwa pamoja na mafunzo hayo majeshi hayo yataweza kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kwa jamii ya wanatanga kama vile ujenzi wa ofisi ya walimu,na vyoo katika shule ya msingi Machemba iliyoko wilayani Muheza. 

Pia alisema kuwa kutakuwa na utoaji wa huduma bure za tiba katika eneo la zoezi kwa wananchi kwa magonjwa mbali hivyo kutumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa Tanga kujitokeza kwa wingi ili waweze kupatiwa matibabu. Nae Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela alisema kuwa vikosi vya majeshi ya nchi za Burundi,Kenya,Uganda na Rwanda tayari vimeshawasili mkoani humo kwa ajili ya maandalizi ya mafunzo hayo. 

Alisema kuwa kwa mwaka huu idadi ya wanajeshi 1500 wanatarajia kushiriki katika mafunzo hayo ,kwa kupeana ujuzi na kubadilishana mbinu mbalimbali za kijeshi. “Mazoezi hayo ni fursa nzuri kwa mkoa wetu nah ii inaonyesha ni namna gani mkoa ulivyo katika hali ya usalama ,utulivu na amani ndio maana kwa mara ya pili mafunzo yanaletwa Tanga.
MKUU wa Mafunzo na Operesheni Jeshini(JWTZ) Meja Jenerali Alfed Fabian Kapinga kushoto akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu kufanyika mafunzo ya Kijeshi mkoani Tanga yanayo julikiana kama “Ushirikiano Imara 2018” ambayo yatahusisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mkoa huo kuwa mwenyeji wa mafunzo ya kijeshi kwa nchi za Afrika Mashariki yatakayoitwa “Ushirikiano Imara 018”yatakayohusisha askari 1500 kutoka nchi tano kushoto ni Mkuu wa Mafunzo na Operesheni(JWTZ) Meja Jenerali Alfed Fabian Kapinga
 Mkuu wa Mafunzo na Operesheni Jeshini(JWTZ) Meja Jenerali Alfed Fabian Kapinga kushoto akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella mara baada ya mkutano na waandishi wa habari.

MOI KUANZA KUZIBUA MISHIPA YA DAMU ILIYOZIBA KWENYE UBONGO

$
0
0
 Mkurugenzi wa Ubora na Uhakiki wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Mohamed Mohamed akifungua kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu katika ukumbi wa Hospitali ya MOI jijini Dar es salaam leo.

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya MOI Prof Charles Mkonyi akizungumza katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akitoa neno la ukaribisho katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu.

Kiongozi wa jopo la wakufunzi kutoka chuo kikuu cha Weill Cornel cha marekani Prof Roger Hartl akiwasilisha mada katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo ,Mgongo na Mishipa ya fahamu



Mkurugenzi wa Ubora na Uhakiki kutoka Wizara ya Afya Dkt Mohamed Mohamed (wa pili) kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa  kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu kutoka mataifa mbalimbali duniani. Wa kwanza kushoto ni Profesa Charles Mkonyi mwenyekiti wa bodi ya wadhamini MOI, watatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface na wa kwanza kulia ni Kiongozi wa jopo la wakufunzi kutoka marekani Profesa Roger Hartl.

TANZIA: Advocate Martin Depores Matunda afariki dunia

$
0
0
Ndugu yetu Martin amefariki ghafla Leo asubuhi nyumbani kwake Sinza jijini Dar es salaam.
Mipango ya mazishi ni ni kwamba mwili umepangwa kuagwa siku ya Jumatano saa saba mchana nyumbani kwake Sinza, jirani na kanisa Katoliki lililo jirani na Lion Hotel. Baada ya kuagwa mwili utasafirishwa siku hiyo0 hiyo kwenda kwenda Bukoba kwa mazishi ambayo yamepangwa kufanyika siku ya Ijumaa.

DKT ABBASI AAINISHA MAFANIKIO YA SERIKALI AWAMU YA TANO KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITATU MADARAKANI (2015-2018)

$
0
0

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akionesha nakala ya Jarida la Nchi Yetu Tanzania linalotolewa na Ofisi yake, ambalo limeainisha mafanikio mbalimbali ya kijamii na kiuchumi yaliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitatu madarakani (2015-2018). Mkutano huo umefanyika leo Jumatatu Novemba, 2018.
6.
Baadhi ya waandishi wa vyombo vya habari nchini wakifuatilia Mkutano baina yao na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati alipotoa taarifa kuhusu Mafanikio ya kijamii na kiuchumi yaliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitatu madarakani (2015-2018). Mkutano huo umefanyika leo Jumatatu Novemba 5, 2018.
1.
  1. Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari nchini kuhusu Mafanikio ya kijamii na kiuchumi yaliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitatu madarakani (2015-2018). Mkutano huo umefanyika leo Jumatatu Novemba 5, 2018.
2.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari nchini kuhusu Mafanikio ya kijamii na kiuchumi yaliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitatu madarakani (2015-2018). Mkutano huo umefanyika leo Jumatatu Novemba 5, 2018.
3.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari nchini kuhusu Mafanikio ya kijamii na kiuchumi yaliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitatu madarakani (2015-2018). Mkutano huo umefanyika leo Jumatatu Novemba 5, 2018.
 

WAFANYABIASHARA TUMIENI MAKAMPUNI YALIYOSAJILIWA NA TIRA KUAGIZA BIDHAA-TIRA

$
0
0
Na. Vero Ignatus, Manyara.

Kamishna wa Bima Tanzania Dkt.Abdallah Saqware Baghayo amewataka wafanyabiashara hapa nchini wanaoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kwa kutumia njia ya magari,ndege,meli ikatiwe Bima kutoka katika makampuni yaliyosajiliwa na mamlaka hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Madarasa Mawili Ofisi Pamoja na Vyoo katika shule ya msingi Gedamar iliyopo Wilayani Babati Mkoani Manyara,Baghayo amesema ni kosa kwa mfanyabiashara kisheria kwa mfanyabiashara kunua bidhaa ambayo haijasajiliwa na mamlaka hiyo.

Amesema ni tegemeo la serikali kuwa makampuni yaliyopewa leseni yatapata biashara ya uagizaji wa bidhaa huku akiwataka wananchi kutambua umuhimu wa bima na kufuata sheria.Dkt.Baghayo amesema mabadiliko ya sheria hiyo yalisainiwa na raisi Dkt.John Pombe Magufuli ili kuweza kutekelezwa na kuzuia wafanyabiashara kutumia bima kupitia makampuni yasiyo sajiliwa.

Kwa Upande wake Mkuu wa Kitengo cha fedha kutoka Jubilee Life Insuarence Helena Mzena alisema kuwa kampuni hiyo inatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake, hivyo kuamua kurudisha faida kwa jamii kwa kuangalia changamoto mbali mbali zilizopo katika shule ya msingi hapa nchini.

Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini Dkt. Abdallah Saqware Baghayo akizungumza na waalimu, viongozi wa kijiji cha Gedamar
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima ya Jubilee. Dipankar Acharya Mkuu wa Kitengo cha fedha kutoka Jubilee Life Insuarence Helena Mzena akizungumza katika hafla hiyo.

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images