Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110144 articles
Browse latest View live

Wachimbaji Wadogo watakiwa kuhakikisha leseni kutokuwa chanzo cha migogoro

$
0
0
Na Rhoda James – Bukombe 
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amewataka wachimbaji wadogo nchini kuhakikisha kuwa leseni za uchimbaji Madini zinazotolewa na Wizara kupitia Tume ya Madini ikiwemo mikataba ya ubia wanayongia na Kampuni mbalimbali kutokuwa chanzo cha migogoro nchini.
Naibu Waziri Biteko aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akisuluhisha mgogoro uliokuwepo kati ya Kampuni ya Pamoja Mining Ltd na Mkazi wa Nyarugusu Salum Othman ambaye aliilalamikia kampuni hiyo kwa kukiuka mkataba waliojiwekea kati yao.
Akizungumza katika kikao hicho cha usuluhishi, Naibu Waziri Biteko alisema kuwa, wachimbaji wadogo wanapoingia mikataba na kampuni yoyote ile yenye nia ya kuwa na ubia na Mzawa  ni lazima  wazingatie  na kukubaliana juu ya mikataba wanayoingia  kwa kuwa, pindi  taratibu zinapokiukwa zinaichafua nchi.
 “Mikataba hii mnayoingia mjue ya kuwa nyinyi mnakuwa ni taswira ya nchi sasa mkikiuka mnakuwa mnaichafua nchi yetu, lazima mzingatie makubaliano mnayojiwekea nyie wote, mwekezaji na mzawa,” alisema Biteko.
Aidha, aliainisha baadhi ya masuala ambayo yanatakiwa kuzingatiwa wakati wa kuingia mikataba na wabia  na kueleza kuwa ni pamoja na kuangalia uhai wa leseni zao, kusajili mikataba yao kwenye Tume ya Madini, kuhakikisha kuwa eneo au biashara wanayoingia haina migogoro, wazawa kujua kuwa wanatakiwa kuwa na asilimia angalau zisizopungua 25 na kuhakikisha kuwa kodi zote za serikali zinalipwa kwa wakati.
Vilevile, Naibu Waziri Biteko alimtaka, Othman ambaye ni mlalamikaji kuhusu ukiukwaji wa mkataba kati yake na Kampuni ya Pamoja Mining Ltd kuhakikisha kuwa wanazingatia sheria zote ili pande zote mbili ziweze kufanya kazi  kwa tija na bila kukwepa kodi za serikali. 
Pia, alitumia fursa hiyo kuzitaka Ofisi za Madini kote nchini kuhakikisha kuwa zinaendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo ili matatizo kama hayo yanayojitokeza sasa yasiendele kujitokeza kwani ni wajibu wa Wizara kuhakikisha kuwa migogoro baina ya wachimbaji  na wawekezaji inakwisha.
Naye, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Daniel Mapunda alimshukuru Naibu Waziri Biteko kwa kusuluhisha mgogoro huo ambao umedumu kwa kipindi kirefu nakueleza kuwa, ofisi hiyo itaendelea kuzingatia na kutekeleza maagizo hayo kwa mujibu wa sheria.  
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akisikiliza mgogoro uliokuwepo kati ya Kampuni ya Pamoja Mining Ltd na Mkazi wa Nyarugusu Salum Othman (hawapo pichani) katika Ofisi ya Halmashauri ya Bukombe. Kushoto ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Daniel Mapunda.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa kwanza kulia mbele) akisikiliza mgogoro uliokuwepo kati ya Kampuni ya Pamoja Mining ltd na Mkazi wa Nyarugusu Salum katika Ofisi ya Halmashauri ya Bukombe. Wengine katika picha ni Wafanyakazi kutoka Ofisi ya Madini Geita na  kampuni ya Pamoja Mining Ltd.

UWT PWANI YAMPA SALUTE RAIS .DK MAGUFULI KWA UTEKELEZAJI NA KASI YA MAENDELEO NCHINI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI .

JUMUIYA ya wanawake ya Chama Cha Mapinduzi (UWT) mkoani Pwani, imempa big up ,Rais Dk. John Magufuli kwa kasi yake ya utekelezaji katika sekta mbalimbali, ikiwemo miradi ya REA awamu ya III kwa vijiji 150 na mradi mkubwa wa Rufiji Hydropower utakaozalisha 2,100MW baada ya kukamilika .

Aidha wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutenga bajeti ya bilioni 12.4 kwa ujenzi wa vituo 18 vya afya mkoa mzima na hospital tatu Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini na Kibiti. 

Awali akiishukuru serikali Mbunge wa viti maalum mkoani hapo, Subira Mgalu, wakati wakisheherekea miaka mitatu ya Rais Magufuli akiwa madarakani, sherehe iliyodhuriwa pia na kamati ya utekelezaji ya UWT mkoa. Anasema"Nikianzia sekta nayoisimamia nikiwa naibu waziri wa nishati nampongeza kupitia uongozi wake na maelekezo yake kuwasilisha bajeti ndani ya bunge ,wizara ya nishati imekuwa ikipata ongezeko kila mwaka "

"Wakati akiingia madarakani mh Rais alikuta asilimia 38 ya wanapata huduma za umeme lakini sasa ni asilimia 60 wamepata umeme kupitia miradi iliyokaribu nao, na miradi ya umeme vijijini "alifafanua Subira. Subira alielezea, kuna REA awamu ya tatu ambayo inaendelea ambapo vijiji 7,873 vilikuwa havina umeme lakini kwa kazi inayoendelea mzunguko wa kwanza vijiji 3,559 vinafanyiwa kazi na wakandarasi wapo kazini .

Alibainisha kwamba, kulikuwa na mradi wa ujazilizi ambapo vijiji 105 vimepata umeme na wananchi zaidi ya 25,000 kwenye mikoa nane ukiwemo nane wameunganishiwa umeme na mradi unaendelea .Hata hivyo alisema, serikali hiyo imeweza kufanikisha miradi ya maji katika miji ya Bagamoyo, Kibiti ,Utete pamoja na mradi wa maji WAMI -Chalinze ,Ruvu -Chalinze -Msoga, mradi wa maji katika miji ya Kisarawe na Mkuranga. 

GOR MAHIA KAMILI GADO KUVAANA NA EVERTON, UINGEREZA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA NA MATUKIO BUNGENI JIJINI DODOMA LEO

$
0
0
1
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa jimbo la Gairo Mh. Ahmed Shabiby katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma mara baada ya bunge kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana.PICHA NAJOHN BUKUKU-BUNGENI JIJINI DODOMA
2
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha Mh. Amina Mollel.
3
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Mbunge wa jimbo Mufindi Mh. Mahmoud Mgimwa katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma leo.
4
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa jimbola Dodoma mjini na Naibu waziri Ofisi ya waziri mkuu (kazi, Vijana na ajira) Anthony Mavunde na vijana wa UVCCM Dodoma walipotembelea bungeni.

SERIKALI YAFUNGUA FURSA UZALISHAJI WA MIFUKO MBADALA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

SERIKALI  imesema kuwa katika kukabiliana na uhifadhi mazingira ni wakati muafaka kwa wadau  kuwekeza katika uzalishaji wa mifuko mbadala  ambayo haina madhara  katika  utunzaji wa mazingira.
Akizungumza katika kikao kilichohusisha wadau wa mazingira kuhusu fursa za uwekezaji  katika uzalishaji wa mifuko mbadala, Naibu katibu  mkuu  Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Edward Sokoine  amesema kuwa malengo ya kikao hicho ni kujadili mabadiliko katika uhifadhi ya mazingira  pamoja na kujadiliana na wadau juu ya namna bora ya kutokomeza matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kutengeneza mifuko mbadala ya karatasi au nguo
Balozi Sokoine amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wajasiriamali kuwekeza katika uzalishaji wa mifuko ya karatasi na nguo ili kuchangia katika uhifadhi wa mazingira na kuongeza kipato chao na kipato ha taifa kwa ujumla.
Balozi Sokoine  amesema kauli mbiu ya "Mifuko mbadala kwa ustawi wa afya, mazingira na uchumi wetu" itumike katika kuhamasisha namna bora ya utunzaji wa mazingira kwa jamii kwa ujumla.
Balozi Sokoine  amesema kuwa mifuko mbadala iwe na gharama nafuu na amewataka wadau wa mazingira kuendeleza kampeni ya kutokomeza matumizi ya mifuko na plastiki ambayo inachangia katika  uchafuzi wa mazingira.
Kwa upande wake Mhandisi kutoka Wizara ya Viwanda, Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Julius Enock amesema kuwa athari  za mifuko ya plastiki ni kubwa sana na hudumu kwa muda mrefu zaidi.
Amesema kuwa takribani mifuko bilioni 7.8 hadi 10 hutumika  kwa mwaka nchini na mifuko hiyo hudumu ardhini kwa miaka 500 hadi 1000 huku ikiendelea kuathiri mazingira.
 Amesema kuwa mifuko iliyozalishwa 1950 kwa mara ya kwanza bado ipo ardhini  ikiendelea kuathiri mazingira kwa kiasi kikubwa huku akitaja athari nyingine ikiwa ni pamoja na  kuathiri shughuli za kitalii, kuuwa mifugo na viumbe vya baharini hali ambayo hupelekea kuathiri kipato cha mtu mmoja mmoja na Serikali kwa ujumla.
Julius amesema kuwa asilimia 60 hadi 80 ya taka za plastiki huishia baharini na mkakati wa kutokomeza janga hili ni  kwakila mtu kutimiza wajibu wake katika ulinzi wa mazingira .

BENKI YA AMANA,KAMPUNI YA TY SERVICES LTD WASAINI MKATABA KUWEZESHA MADEREVA KUMILIKI MAGARI

$
0
0
 BENKI ya Amana na Kampuni ya TY Services Limited inayoendesha mtandao wa Taxify nchini zimesaini mkataba wa kuwawezesha madereva 50 wa mtandao huo kumiliki magari. Hayo yamesemwa  jijini Dar es Salaam na Meneja Biashara wa Benki ya Amana Dassu Mussa wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusainiana mkataba huo.

Mussa alisema benki hiyo imejipanga kuwezesha jamii ya Kitanzania kuondoka katika wimbi la umaskini hivyo mkataba huo utafungua njia ya kiuchumi.  Alisema benki hiyo inayoendeshwa kwa kuzingatia mfumo wa kiislam hatua hiyo ya kushirikiana na Taxify ni sehemu ya mikakati ya kuwa benki kiongozi katika kutoa hiding za kibunifu. 

"Uwezeshaji huu utakuwa wa vikundi vya madereva 10 ambao watadhaminiana wenyewe na ataweka dhamana isiyopungua asilimia 10 ya thamani ya chombo anachohitaji kuwezeshwa, na dhamana hiyo itatumika hadi kumaliza marejesho,"alisema.
Alisema mkataba huo unamtaka dereva aweke akiba ya Sh. 15,000 kwa wiki ambayo itakuwa dhamana hadi dereva atakapokamilisha rejesho miaka miaka miwili.

"Benki itazingatia vigezo mbalimbali katika kutoa uwezeshaji huo ikiwemo dereva kuwa na uzoefu wakutosha,"alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa TY Services, Remmy Eseka alisema ushirikiano huo ni chachu ya kuongeza ajira kwa Watanzania. Eseka alisema mtandao wa Taxify upo katika mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma hiyo ujio wa Amana katika huduma hiyo ni fursa muhimu.

"Tumejipanga kutumia fursa hii ya Amana Benki kuwezesha madereva wa taxify nchini naamini utakuwa mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi,"alisema.

RATIBA YA KUMUAGA MAREHEMU PROF .ISSARIA KIMAMBO

BENKI YA I & M IMETOA ZAWADI NONO KWA WATEJA WAKE 5 KATIKA KUELEKEA MSIMU WA SIKUKUU.

$
0
0
Na Agness Francis,Globu ya Jamii. 

Benki ya I & M imetoa zawadi nono kwa wateja wake katika droo  ya kwanza ya JIDABO na I & M bank chini ya usimazi kutoka bodi ya Taifa  ya michezo ya kubahatisha iliyochezeshwa leo ambapo washindi  watano wamepatikana kutoka sehemu mbali mbali hapa nchini .

Droo hiyo imekuwa ni kwa wateja wao katika kuelekea msimu wa sikukuu ya Christmas na mwaka mpya  2018.

Akizungumza na waandishi wa  habari leo Jijini Dar es  Salaam  Mkuu wa kitengo cha Wateja na reja reja Ndabu Swere I & M benki amesema kuwa  promosheni hiyo iliyoanza mwezi Octaba na kuendelea mpaka Disemba kwa kila mwezi kutaja washindi watano wa droo hiyo.

"Washindi watano waliopatikana Leo ni sehemu ya wshindi 15 ambao watapatikana katika kipindi chote cha miezi  mitatu ya  JIDABO na I &M  ambayo ili kushiriki unapaswa kufungua akaunti  ya  akiba, akaunti ya mshahara au ya mtoto katika tawi lolote la benki yetu"amesema Swere. 

Aidha Swere ameongezea kuwa kwa mteja ambaye tayari  ana akaunti tayari ya benki hiyo anapaswa kuhakikisha kuwa ana akiba ya shilingi 200,000 ikiwa anashiriki akaunti ya biashara au 100,000 ikiwa anamiliki akaunti yingine  zinazohusika katika promosheni hiyo.

Mkuu wa kitengo cha Uendeshaji   I & M Benki Donald Mate amewataja washindi wa promsheni hiyo ambao ni watano baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo ambao ni  Selcom wireless LTD, Jumanne Mchench, Eliakunda Shoo,Sherbanu Osman, Eco dry Cleaners  LTD. 

Meneja Mauzo I & M benki  Norman Vasta  amebainisha kuwa kwa mujibu wa promosheni hiyo washindi hao watano  watapata mara mbili ya akiba zilizopo kwenye akaunti zao.

"kiwango cha juu zaidi  kutolewa kwa mteja kitkuwa shilingi 5,000,000,mfano ikiwa akiba ya mwezi husika ya mteja ni 5,000,000 basi atazawadiwa mara mbili na Kuwa 10,000,000"amesema Vasta.

Swere amemalizia kwa kuwataka watanzania wawe na utanaduni wa kuhifadhi akiba kwenye mabenki na kuchangamkia fursa hiyo ya kufungu akaunti katika Matawi yanayopatikana Mwanza,Kilimanjaro, Arusha pamoja na Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha Reja Reja  Ndabu Swere I & M Benki akitoa wito na kuwataka watanzania wawe na utanaduni wa kuhifadhi akiba kwenye mabenki na kuchangamkia fursa hiyo ya kufungu akaunti katika Matawi yanayopatikana Mwanza,Kilimanjaro, Arusha pamoja na Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji I & M Benki Donald Mate  akiwataja washindi watano wa droo hiyo ya kwanza ya promosheni ya JIDABO na  I & M Benki iliyofanyika leo Jijini Dar es Salam.

Meneja Mauzo I & M Benki Norman  Vasta  akichezesha droo ya promosheni ya JIDABO na I & M Benki iliyofanyika leo katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam na kushoto ni mteja wa Benki hiyo akichagua karatasi ya mmoja ya  mshindi kati ya watano walioshinda  droo ya kwanza ya promosheni hiyo iliyosimamiwa na Chiku Saleh kutoka bodi ya  Taifa ya michezo ya kubahatisha.

OBITUARY: PROF. ISARIA KIMAMBO

$
0
0
The Vice Chancellor, Prof. William A. L. Anangisye, regrets to announce the death of Professor Isaria Kimambo (1931 – 2018) who passed away on 2nd November 2018 at his residence in Makongo Juu, Dar es Salaam.

Prof. Kimambo, born in 1931, was the first Tanzanian Professor of History at the University of Dar es Salaam. He also served in different managerial positions, most importantly as Vice Principal of the then University College, Dar es Salaam from 1969 to 1970 and the first Chief Academic Officer (CACO) of the University of Dar es Salaam from 1970 to 1982 where he significantly contributed to the development of the university generally and particularly in the development of academic programs as well as the appointment of new faculty. 

Prof. Kimambo was a dedicated scholar, educator and leader working particularly in the areas of History and most especially African History. Among his famous publications are “Penetration and Protest in Tanzania: Impact of World Economy on the Pare, 1860–1960”; “East African Expression of Christianity”; and “Custodians of the Land: Ecology and Culture in the History of Tanzania”. 

Prof. Isaria Kimambo started his career as a Primary School Teacher at Lutheran Primary School Natiro. He was awarded a scholarship to pursue his Undergraduate studies and Master’s Degree majoring in Education at Pacific Lutheran University, USA, and later PhD in History at Northwestern University in 1967. He was promoted through the ranks to Professor in 1971. He has been a chairperson and member of different national and international bodies.  

Funeral arrangements are underway at his residence in Makongo Juu, Dar es Salaam. The University community will celebrate Prof. Kimambo’s life and pay last respect on Wednesday 7th November 2018 at Nkrumah Hall from 9:00am to which you’re all invited to attend this important event. He will be laid to rest at his residence in Mbokomu, Moshi, Kilimanjaro on 8th November 2018. 

May his Soul rest in Eternal Peace!

ISSUED BY THE PUBLIC RELATIONS OFFICE
5th November, 2018.

KMC WAMTUPIA VIRAGO ABDULHALIM HUMUD KWA UTOVU WA NIDHAMU

$
0
0
     Kaimu Katibu Msaidizi wa timu ya mpira wa miguu Manispaa ya Kinondoni (KMC) Walter Harrison akizungumza na wadau pamoja na wanahabari jijini Dar es salaam kuhusu kufukuzwa kwa mchezaji wao  Abdulhalim humud

Na Khadija Seif,Globu ya jamii


Uongozi wa Klabu ya Kinondoni municipal council (KMC) umeweka wazi msimamo wao wa kumfukuza rasmi aliyekua mchezaji wao, Abdulhalim Humud. Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam leo, Kaimu Katibu Msaidizi wa timu hiyo, Walter Harrison amesema mchezaji huyo amefukuzwa rasmi kutokana na utovu wa nidhamu kwa viongozi wake pamoja na wachezaji wenzake.

Harrison ameeleza kuwa, vitendo vya Humud vya utovu wa nidhamu vimekua vikijirudia mara kwa mara na kwa uongozi kushindwa kuweza kuvikabili na kulazimika kumfukuza rasmi.

"Vitendo vya utovu wa nidhamu vimekuwa vinajirudia mara kwa mara, kwa viongozi na hata wachezaji wenzake na imepelekea kushindwa kuvumulia na kulazimika kuachana nae rasmi,"amesema Harrison


Alikadhalika Humud alishawahi kuandika barua kwa uongozi wa KMC kuomba kuachwa ili asiendelee kuichezea timu hiyo kwa sasa na hivyo uongozi wakaamua alipe gharama kiasi kutokana na pesa nyingi zilitumika kama vile gharama za matibabu, mshahara pamoja na fedha zilizokua zikitumika wakati yuko kambini.

Aidha , Kaimu Katibu huyo amekumbusha wadau na wanamichezo kuwa tabia hiyo kwa Humud imekua kama ni desturi yake kwani alishawahi kufanya vitendo hivyo kwa baadhi ya timu kongwe hapa nchini.

WATUHUMIWA 14 WA WIZI WA MAGARI, SILAHA AINA SHOTGUN NA BASTOLA WATIWA MBARONI

$
0
0
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, LIBERATUS SABAS-DCP akizungumza na waandishi wa habari akizungumziwa kukamatwa kwa watuhumiwa 15 wa uhalifu wa wizi wa magari, silaha na mlipuko mmoja.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya Short Gun, risasi nne za short gun na mlipuko moja uliotengenezwa kienyeji.


Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, LIBERATUS SABAS-DCP ametos taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, amesema Silaha hiyo ilikamatwa tarehe 25 Oktoba 2018 majira ya saa 21:30 huko maeneo ya Kijichi. Askari wakiwa doria waliitilia mashaka pikipiki iliyokuwa haina namba za usajili ikiendeshwa na kijana mmoja akiwa amewapakia wenzake wawili.

Vijana hao baada ya kutambua kuwa wanafuatiliwa na Polisi walianza kuwafyatulia risasi huku wakikimbia, ndipo askari walipojibu mapigo na kufanikiwa kumjeruhi kijana mmoja na kupelekea kufariki akiwa anapelekwa hospitali.
Kijana huyo alipekuliwa na kukutwa akiwa na silaha aina ya Shotgun iliyokatwa mtutu na kitako ikiwa na risasi nne pamoja na mlipuko mmoja.

Msako mkali unaendelea kuwasaka watuhumiwa wote waliotoroka ikiwa ni pamoja na wahalifu wengine wanaofanya matukio ya kihalifu kwa kutumia silaha za moto ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Katika tukio lingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam huko maeneo ya Kijichi limefanikiwa kukamata silaha ndogo bastola aina ya Star ambayo haikuwa na namba za usajili na risasi nne ndani ya magazine.

Katika tukio hilo lililotokea tarehe 1 Novemba 2018 majira ya saa 22:15 huko maeneo ya Kijichi Mgeninani askari wakiwa doria walitilia mashaka waendesha pikipiki yenye usajili wa namba MC 854 BBY aina ya TVS iliyokuwa ikiendeshwa na mtu mmoja huku akiwa amepakia watu wengine wawili. 

Askari walipowasimamisha watu hao walikataa kutii amri halali na ghafla watu hao walifyatua risasi hewani ndipo Polisi walijibu mapigo na kuwajeruhi majambazi hao ambao walifariki wakiwa wanapatiwa matibabu hospitalini.
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, LIBERATUS SABAS-DCP akionesha silaha zilizokamatwa katika matukio tofauti ya uhalifu.
Watu hao walipekuliwa na kukutwa na silaha hiyo.

Kukamatwa kwa mtandandao wa wizi wa magari

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 14 kwa tuhuma za wizi wa magari.

Watuhumiwa hao wamekamatwa sehemu mbalimbali hapa jijini Dar es Salaam na mikoa mingine wakiwa na magari 7, Bajaji moja na pikipiki moja ya wizi vyote vimeibwa maeno mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam.

Watuhumiwa hao ni Luckman Ramadhani (36 , Ignasi Faustine (35), Ally Shaweji (30), Stephen Mwanzalima (43), Emmanuel Mabula (42), Dismas Mfoyi (32), Nyamuhanga Matiko (29), Freeman Paul (35), Ayubu Makame (41), Erasto Nyamboneke (35), Seleman Saidi (42), Dickson Mbembaji (32), Ally Rashidi (35) na Robert Nassoro (46)

Magari yaliyokamatwa ni T 162 BLW Toyota land Cruiser MALI YA UWT-TANZANIA, STL 6434 Toyota Land Cruise MALI YA WIZARA YA AFYA, T 855 DLE Toyota Harrier, T 199 DEU Toyota Noah, T 249 DLL Toyota IST, T 255 AJG Rav4 gari hii ILIIBIWA udsm IKIWA na namba T 271 DFF, T 556 DJQ Toyota Allion ,  MC 854 BYY pikipiki aina ya  TVS Honda , MC 639 BYA Bajaji

Aidha kuna magari zaidi ya manne ambayo yamekamatwa mikoani, na yako njiani yanaletwa hapa jijini Dar es salaam kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi.

Watuhumiwa wanahojiwa na watafikishwa mahamani kwa hatua zaidi. Jeshi la polisi linaendelea na msako mkali dhidi ya wezi wa magari na watuhumiwa wengine.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, LIBERATUS SABAS-DCP  akionesha moja ya gari lililoibiwa mali ya Wizara ya Afya na kukamatwa Mikumi Mkoani Morogoro.

DIASPORA CANADA (ZACADIA )YAKABIDHI WHEEL CHAIR IDARA YA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR

$
0
0
 KAIMU Mkurugenzi Idara ya Diaspora Zanzibar Ndg Hassan Khatib Hassan,akimkabidhi msaada wa wheel chair Mkurugenzi wa Idara ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Bi. Abeda Abdalla Rashid, vivilivotolewa na Wazanzibar wanaoishi Nchini Canada wa Jumuiya ya Diaspora ya ZACADIA, kushoto Menaja wa Diaspora ya ZACADIA, Bi. Firdaus Rashid Rabia,hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Idara hiyo migombani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 MKURUGENZI wa Idara ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Bi. Abeda Rashid Abdallah, akimkabidhi Wheel Chair,Ndg Abubakar Abdulatif  mlezi wa Mtoto mwenye Ulemavu Saleh Mustafa Mussa, baada ya kukabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Zanzibar,Ndg. Hassan Khatib Hassan, katika viwanja vya Idara hiyo Migombani Zanzibar Wheel Chair hizo zimetolewa na Wazanzibar wanaoishi Nchini Canada, wa Taasisi ya ZACADIA Diaspora.
MKURUGENZI wa Idara ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Bi.Abeda Rashid Abdallah, akimuendesha Mtoto mwenye Ulemavu Saleh Mustafa Mussa,baada ya kumkabidhi Wheek Chair, zilizotolewa na Diaspora Wazanzibari wanaoishi Nchini Canada wa Jumuiya ya ZACADIA, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Idara hiyo Migombani Zanzibar.(Picha na Ikulu)

TADB ‘yatupa’ jembe la mkono kwa kuwakopesha matrekta wakulima wa pamba

$
0
0
Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) imetoa matrekta 24 yenye thamani ya zaidi ya TZS 1.5 bilioni kwa Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Masoko (AMCOS) 24 vinavyolima zao la pamba katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kuongeza tija na uzalishajji wa zao hilo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema kuwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo inalenga katika kuwawezesha wakulima wa zao la pamba nchini ili waweze kuongeza tija na uzalishaji kama inavyobainishwa katika Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba nchini, Bw. Marco Mtunga amesema kuwa kupitia mkopo wa viua dudu uliotolewa msimu uliopita na TADB, ambapo uliwanufaisha zaidi ya wakulima laki sita wa zao la pamba ambapo uliwezesha kuongeza uzalishaji kufikia tani 221,600 ikiwa ni ongezeko la asilimia 67 ikilinganishwa na tani 133,000 zilizozalishwa msimu wa 2017/18.

Bw. Mtunga ametoa wito kwa taasisi nyingine kushirikiana ili kuweza kuongeza tija katika uzalishaji wa pamba hapa nchini.

Wakizungumza wakati wa makabdihiano hayo, baadhi ya wakulima walionufaika na matrekta hayo, waliishukuru serikali kupitia benki ya maendeleo ya kilimo kwa kuweza kuwakopesha matrekta hayo hali itakayochagiza tija na uzalishaji wa zao la pamba nchini.
 Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba (aliyevaa tai) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) wakikata utepe wakati wa kukabidhi matrekta 24 yaliyotolewa kwa vyama vya Ushirika vya Msingi na Masoko (AMCOS) za mikoa ya Kanda ya Ziwa. Matrekta hayo yenye thamani ya zaidi ya TZS 1.5 bilioni yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) akikabidhi ufunguo wa trekta kwa mmoja kati ya viongozi 24 wa vyama vya Ushirika vya Msingi na Masoko (AMCOS) za mikoa ya Kanda ya Ziwa waliokopeshwa matrekta yenye thamani ya zaidi ya TZS 1.5 bilioni yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Wanaoshuhudia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine na baadhi ya viongozi wa AMCOS hizo.
 Pichani ni matrekta yenye thamani ya zaidi ya TZS 1.5 bilioni yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo kama mkopo kwa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Masoko (AMCOS) 24 zinazolima pamba Kanda ya Ziwa. Mkopo huu umewezesha AMCOS hizo ‘kutupa‘ majembe ya mkono katika kilimo.

UONGOZI WA BENKI YA CRDB WAMTEMBELEA KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James (kulia) akizungumza na Viongozi wa Benki ya CRDB waliofika ofisini kwake leo, kwa lengo la kumtambulisha Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto). Ujumbe wa Benki ya CRDB uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay (kushoto), Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Esther Kitoka pamoja na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao chao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James (kushoto) walipomtembela ofisini kwake, jijini Dar es salaam leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James (wa pili kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akijadiliana jambo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Esther Kitoka wakati wa kikao chao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James.
Picha ya pamoja.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo kwa kila Mkuu wa Mkoa aifanye afya ya uzazi na mtoto kuwa ajenda ya kudumu katika vikao vya ushauri vya Mkoa (RCC).

Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” ya Kuongeza kasi ya Uwajibikaji Kupunguza Vifo Vitokanavyo na Uzazi na Watoto Wachanga.

“Ili kuhakikisha suala la kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto katika nchi yetu linapewa kipaumbele cha juu katika shughuli za Serikali za kila siku” alisema Makamu wa Rais

Tafiti zilizofanyika mwaka 2015/2016 zinaonyesha kuwa, kiwango cha vifo vitokanavyo na uzazi ni 556 kwa kila vizazi hai 100,000 ambayo ni sawa na vifo 11,000 kila mwaka ambayo ni sawa na wanawake 30 hufariki kila siku, kutokana na matatizo yatokanayo na uzazi na kwa uapnde wa watoto wachanga ni 25 kwa kila vizazi hai 1000 .

Makamu wa Rais amesema jamii ina jukumu zito la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kwa kuhakikisha kuwa inajiwekea mpango mahsusi wa rufaa wakati wa dharura na utambuzi wa dalili hatarishi kwa mama na mtoto mchanga.

“Nitoe rai kwa wananchi, wanawake na wanaume na vijana kujitokeza kuchangia damu mara kwa mara kwa kuwa wakifanya hivi wanaokoa maisha ya mama mjamzito na watoto.” Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 80 ya damu salama inatumika kwa wakina mama wajawazito na watoto alisema Makamu wa Rais.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya "Jiongeze Tuwavushe Salama" jijini Dodoma.wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Jiongeze Tuwavushe Salama" jijini Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha taarifa inavyoonyesha hali halisi ilivyo sasa katika masuala yanayohusu uzazi salama wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Jiongeze Tuwavushe Salama" jijini Dodoma.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Jiongeze Tuwavushe Salama" ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
 Sehemu ya Wageni kutoka Taasisi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kampeni ya "Jiongeze Tuwavushe Salama" ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUZI TV:JESHI LA POLISI LAMSHIKILIA DAKTARI KWA TUHUMA ZA WIZI WA GARI MALI YA WIZARA YA AFYA

SIMIYU YAZINDUA MFUMO WA MSHITIRI MMOJA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA , JAZIA

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  amezindua rasmi mfumo wa ununuzi wa dawa na vifaa tiba kupitia kwa mshitiri mmoja wa mkoa ujulikanao kama JAZIA, uliobuniwa kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, vifaa vya maabara na uchunguzi katika vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali ngazi ya Mkoa na Halmashauri.

Akizindua mfumo huo Novemba 05, 2018  Sagini amesema mfumo wa JAZIA si mbadala wa Bohari ya Dawa (MSD) bali unalenga kuziba upungufu wa dawa, vifaa tiba, vifaa vya maabara na uchunguzi katika Bohari ya Dawa (MSD).

“JAZIA ni mfumo uliobuniwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na wataalam washauri ili kuweza kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, vifaa vya maabara na uchunguzi katika vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali ngazi ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, JAZIA si mbadala wa MSD bali ni msaidizi wa MSD inapokuwa haina bidhaa husika.” alisema.

Aidha, Sagini alibainisha kuwa mfumo huu utasaidia kupunguza gharama na bei ya upatikanaji wa dawa kwani bei za dawa na vifaa tiba zitalingana na bei ya soko na sio matakwa binafsi ya wazabuni.

Aliongeza kuwa mfumo huo utapunguza urasimu uliokuwepo wa namna ya kununua dawa nje ya MSD na hivyo kusaidia dawa kupatikana kwa muda mfupi huku akiwataka Waganga wafawidhi wa vituo vyote vya kutolea huduma za afya kuagiza dawa na vifaa tiba mapema wanapoona vinapungua kabla ya kusubiri vifaa hivyo na dawa kuisha kabisa.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (katikati) akisaini mkataba wa mshitiri mmoja wa Mkoa katika dawa na Vifaa Tiba(JAZIA), Novemba 05, 2018  katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi, waliosimama kushuhudia ni Baadhi ya Wenyeviti wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu.
 Mkurugenzi wa Operesheni kutoka Kampuni ya Total Health Lab ya jijini Dar es salaam ,  Crispin Mtete na Mkurugenzi wa Mufuruki Traders Company Ltd ya jijini Mwanza, Khalifa Mufuruki wakisaii mkataba kama wazabuni walioungana kama mshitiri mmoja wa mkoa wa Simiyu katika kutoa huduma za dawa na vifaa tiba , Novemba 05, 2018 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.
 Mkurugenzi wa Mufuruki Traders Company Ltd ya jijini Mwanza, Khalifa Mufuruki akizungumza jambo katika uzinduzi rasmi wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa  tiba “ JAZIA” uliofanyika Novemba 05, 2018 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, ASF. James John akichangia hoja katika uzinduzi rasmi wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa  tiba “ JAZIA” uliofanyika Novemba 05, 2018 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.
 Viongozi mbalimbali wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa  tiba “ JAZIA” uliofanyika Novemba 05, 2018 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KILIO CHA BARABARA PANGANI HISTORIA MPYA IMEANDIKWA-JUMAA AWESO

$
0
0
 Anaandika Mh.Jumaa Hamidu Aweso .

“Ndugu zangu ,nina furaha sana huenda zaidi ya siku zote ukitoa siku niliopata ridhaa ya kuaminiwa na wana Pangani kua Mbunge wao.

Asanteni sana, Kitu kinachoifanya siku hii ya leo kua ya kipekee sana ni BARABARA yetu ya PANGANI kupewa kibali rasmi cha matengenezo toka kwa Mh.Raisi wetu Mpendwa Dk.John Pombe Magufuli na hapa nimefika ofisini kwa Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu Dodoma kujionea na kushukuru. 

Ndugu zangu kila kilio kina mwenye ,;machozi ya furaha yamenitoka nilipopewa habari hizi,nimekumbuka mbali sana tulivyoumia, tulivyoteseka pamoja na kwa miaka mingi sana kusubiri hili. 

Hisia zimenipeleka mbali nilivokosa amani toka nilipopata ridhaa ya kua Mbunge namna nimekosa usingizi kila nikiwaza kulimaliza na kufanikisha hili,nilifikia hatua kila nikisimama Bungeni nasemea barabara tu,nilipiga mpaka MAGOTI kwa Waziri Mbalawa alipofika Pangani,nimeenda ofisi zote hamna sehemu sijafika kuisemea barabara hii,nimetembelea Media mbalimbali.,nimemuomba sana Mungu kila nifapo Dua.! 

 Leo ni siku ya kihistoria ninaomba kuwajulisha rasmi kua tunaenda kupata barabara ya kiwango cha lami na zoezi hili litaanza muda si mrefu. Tumesema sana,tumepaza sauti kila kona,tumezungumza na kila aliehusika na sasa faraja kubwa hii hapa Mbele yetu.! .

 Nichukue nafasi hii kuwashukuru sana wana Pangani kwa uvumilivu wenu kipindi chote nilipowaambia naipambania barabara hii,na niwaombe tuendelee kua na subira mpaka mchakato unapoanza,nawashukuru sana kwa Dua zenu na nawaomba uzidi kuniombea nina mengi ya kufanya kwa ajili yenu. 

 Aidha nimshukuru Mkuu Wa Wilaya Pangani Mh.Zainab,Mkuu wa Mkoa Mh Shigela alielibeba hili kutusaidia na zaidi Waziri wa Uchukuzi,Miundombinu na Mawasiliano MhKamwele kwa kazi kubwa waliofanya kunipa sapoti katika hili pasina kumsahau mtangulizi wake Mh.Mbalawa. 

 Mwisho nikiri nimeupokea utendaji wa Mh.Raisi wetu wa Miaka mitatu kwa moyo wa furaha sana na Mungu ampe nguvu na Afya na maisha marefu tokana na hiki kilio cha muda mrefu kinachokwenda kufutika ikiwa ni kama Pangani tulikua pangoni sasa tunaenda kupaa angani.

WANACHAMA WA YANGA WAKATAA KUSIMAMIWA UCHAGUZI WAO NA TFF, WASEMA WANAYO KAMATI YAO

$
0
0
*Wawaoma BMT, TFF kuheshimu maamuzi ya mkutano mkuu wa Yanga wa kumtambua Yusuf Manji kama Mwenyekiti wao.

*kuhusu uchaguzi, Mwenyekiti wa Matawi aitwa kamati ya maadili kesho

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

WANACHAMA wa Klabu ya Yanga kwa pamoja wameazimia kuweka msimamo wao wa kutotaka uchaguzi wao kusimamiwa na kamati ya uchaguzi ya TFF na Yusuf Manji bado ni Mwenyekiti wao wanamtambua.

Baraza la Michezo (BMT) wiki iliyopita walitoa tamko la kuwataka TFF washirikiane na Yanga kuhakikisha wanafanya uchaguzi mkuu wa kujaza nafasi zilizokuwa wazi baada ya vionozi wake kijiuzulu na pia kujaza nafasi ya Mwenyekiti Yusuf Manji.Hayo yamefikiwa kwa kauli moja baada ya viongozi wa matawi kukutana na kujadiliana baada ya Shitrikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kutangaza mchakato wa uchaguzi wa Yanga na kutaja tarehe ya kufanyika uchaguzi huo.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mkutano wao wa ndani, Mwenyekiti wa Matawi Bakili Makele amesema kuwa wao kama Yanga hawajakataa kufanya uchaguzi ila hawakubaliani na maamuzi ya TFF ya kusimamia mchakato mzima.Makele amesema kwa pamoja wameazimia kutokubali kusimamiwa mchakato wa uchaguzi na TFF kwa kuwa akidi ya kamati ya uchaguzi wa Yanga imetimia na TFF hawajafuata maagizo ya Baraza la Michezo (BMT) la kukutana pamoja ili kujadili uchaguzi huo.

"sisi kama Yanga hatujakataa kufanya uchaguzi ila BMT walitoa maelekezo kwa TFF kuwa wakae pamoja na sisi ili kuanz amchakato wa uchaguzi, ila tunashangaa wao wanaamua kuunda kamati yao ya Uchaguzi na kutangaza wanachama waanze kuchukua fomu kitu ambacho hatukubaliani nacho pia Yanga haiwezi kusimamiwa uchaguzi na TFF kwakuwa kamati yetu ya uchaguzi imetimia,"amesema Makele.

"Wanachama kwa pamoja tumefikia azimio la kusema kuwa nafasi ya Mwenyekiti haitajazwa kwani bado tunamtambua Yusuf Manji kama Mwenyekiti wetu na mkutano mkuu wa Yanga ndio wenye maamuzi ya kila kitu na wote tulikubaliana kuwa bado ni mwenyekiti wetu na nafasi zitakazojazwa ni tano tu moja ya makamu mwenyekiti na wajumbe wanne waliojiuzulu wote,"


Mbali na hilo, Mwenyekiti huyo wa matawi ameitwa na kamati ya maadili ya TFF kwenda kujieleza baada ya kutumiwa barua leo mchana ya kutakiwa kwenda na mashahidi wake akituhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukataa kufanyika kwa uchaguzi huo, kufanya mkutano wa hadhara kinyume na utaratibu.

Makele ameeleza kuwa, yeye kesho ataenda kusikiliza aliloitiwa katika kamati ya maadili ila anachokifahamu hajavunja sheria yoyote kwani Mkutano aliofanya ulikuwa ni wa viongozi wa matawi ikiwa ni kujadiliana mambo mbalimbali ya kimaendeleo.Baadhi ya wanachama wa Yanga wameonekana kukerwa na maamuzi ya TFF ya kutaka kusimamia uchaguzi wao na kusema kuwa hawako tayari kuona suala hilo linafanyika na kwa upande wao hawajakataa uchaguzi ila hawatataka wasimamiwe na TFF kwani kamati yao ya Uchaguzi ipo na inafanya kazi kutokana na kutimia kwa akidi ya wajumbe.

Kwa pamoja wameungana na mwenyekiti wao kuitikia wito la kuitwa kwake TFF na kumpa moyo kuwa hili nalo litapita na wataungana nae kuelekea huko ili kutoa ushahidi wao.

njia pekee ya kulipa wema kwa wananchi ni viongozi wake kufanya kazi kwa bidii na ubunifu-ccm

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) ndugu Humphrey Polepole amesema njia pekee ya CCM kulipa wema kwa wananchi ni viongozi wake kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ili kuleta maendeleo endelevu nchini. 

Amesema wananchi wamekiamini Chama na kukipa ridhaa ya kuongoza Serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutokana na usimamizi na utekelezaji mzuri wa Sera zake kwa jamii. Rai hiyo aliitoa leo (jana) katika hafla ya kukabidhi mipira ya kusambazia maji safi na salama kwa wananchi wa Jimbo la Tunguu huko katika ukumbi wa T.C uliopo Dunga Wilaya ya Kati Unguja. 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi mipira hiyo kwa uongozi wa Jimbo la Tunguu kwa niaba ya wananchi, Ndugu Polepole amesifu juhudi za kuwatumikia wananchi zinazofanywa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo.Polepole aliwataja viongozi hao ambao ni Mbunge wa Jimbo hilo Khalifa Salum Said na Mwakilishi wa Jimbo hilo Simai Mohamed Said kuwa wametoa mipira hiyo kwa lengo la kumaliza changamoto ya ukosefu wa huduma za maji. 

Ndugu Polepole alisema Viongozi wa Chama na Serikali hasa Wabunge, Wawakilishi na Madiwani nchini wanatakiwa kuendeleza utamaduni wa kufanya kazi na kuwapelekea wananchi maendeleo na sio ahadi za uongo.Katibu huyo wa NEC,Polepole alifafanua kuwa maisha ya mwanadamu yeyote yanahitaji maji hivyo Kitendo cha kuwapelekea wananchi huduma hiyo ni kuharakisha maendeleo ya jimbo kwani wananchi watafanya shughuli za kujiingizia kipato kwa utulivu.

Kupitia hafla hiyo, kiongozi huyo aliwataka viongozi wa majimbo mengine Zanzibar kuiga mfano huo wa kutatua kero za wananchi ili ifikapo mwaka 2020 CCM iwe imetekeleza ahadi zote zilizotolewa katika Uchaguzi Mkuu wa Dola uliopita. Katika maelezo yake Polepole,alitangaza rasmi kuwa kiongozi yeyote atakayeshindwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 asitarajie kupewa tena nafasi ya uongozi kupitia Chama Cha Mapinduzi kwani anakuwa haitoshi kiutendaji. 
KATIBU wa NEC, Idara ya Itkadi na Uenezi CCM Humprey Polepole akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM mara baada ya kukabidhi miundombinu hiyo ya kusambazia maji safi na salama katika vijiji vya Jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
KATIBU wa NEC, Idara ya Itkadi na Uenezi CCM Humprey Polepole akimkabidhi mipira ya kusambazia maji safi na salama Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Nd. Simai Mohamed Said kwa niaba ya wananchi wa Jimbo hilo.
KATIBU wa NEC, Idara ya Itkadi na Uenezi CCM Humprey Polepole akifukia mipira ya maji safi na Salama katika Kijiji cha Bungi Jimbo la Tunguu.
BAADHI ya wanachama na viongozi wa CCM wakimsikiliza nasaha za Katibu huyo Polepole mara baada ya kukabidhi mipira ya kusambaza maji iliyonunuliwa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu kwa ajili ya kutatua kero za wananchi.

Viewing all 110144 articles
Browse latest View live




Latest Images