Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

AMBER RUTY AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE

$
0
0
Na Khadija Seif blogu ya Jamii

MCHEZA  video Rutyfiya Abubakari maarufu kwa jina la Amber Ruty (23), Said Bakari Mtopali (21) (kijana wake AmberRuty) na kijana anayedaiwa kuwa Shoga maarufu, James Charles Mpali a.k.a James Delicious(22) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Washtakiwa hao ambao wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile wamesomewa mashtaka yao leo na Wakili wa Serikali Mwandamizi Nassoro Katuga aliyekuwa akisaidiana na Wakili wa Serikali Nguka Faraji.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili Katuga amedai katika shtaka la kwanza linalomkabili AmberRuty peke yake, kuwa, kabla au Oktoba 25 mwaka huu katika maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa alimruhusu mshtakiwa Mtopali kumuingilia kimwili kinyume na maumbile.

Katika shtaka la pili, mshtakiwa Mtopali anadaiwa kufanya mapenzi kinyume na maumbile na AmberRuty.Aidha, mshtakiwa Delicious anadaiwa kuchapisha na kusambaza video za kingono kupitia kompyuta kosa analodaiwa kulitenda kati au Oktoba 25, 2018 akiwa katika sehemu tofauti za jiji la Dar es Salaam.Anadaiwa, siku hiyo alisambaza video za ngono zisizokuwa na maadili kupitia mtandao wa kijamii  wa WhatsApp

Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruty na Said Abubakary Mtopali ambapo wanadaiwa kati Oktoba 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kwel.Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana

Kabla ya kusomwa kwa masharti ya dhamana Wakili Katuga ameieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika wanasubiri taarifa za Kitaalamu kutoka kwa daktari na statement kutoka kwa mashahidi juu ya picha hizo za ngono za minato. Katika masharti ya dhamana, Mahakama imewataka washtakiwa kuwa kila mmoja kuwa na wadhamini 2 waliotakiqa kusaini bondi ya Sh. Milioni 15.

Pia wadhamini wametakiwa kuwa na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati zeo za kusafiria na pia hawaruhusiwi kutoka nje ya Dar es Salaam bila ruksa.Hata hivyo ni mshtakiwa James Delicious pekee ndiye aliyefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana, huku Amber Ruty na Said Bakary Mtopali wameshindwa kutimiza masharti na kupelekwa gerezani.Kesi hiyo imeahirishwa hadi November 12,2018.
MCHEZA video Rutyfiya Abubakal a.k.a Amber Ruty , Said Bakari (kijana wake AmberRuty)  pamoja na James Charles maarufu kama James Delicious anayedaiwa kuwa shoga wakielekea kwenye moja ya chumba cha Mahakama mara baada ya kufikishwa   Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka yao kwa kupiga picha za utupu na kusimbaza mitandaoni.

AMBER RUTTY NA KIJANA WAKE PAMOJA NA JAMES DELICIOUS WALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI KISUTU

UONGOZI INSTITUTE WAFANYA KONGAMANO LA KUKUZA, KUIMARISHA UONGOZI NA VIONGOZI NCHINI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

TAASISI ya Uongozi nchini (Uongozi Institute) imefanya kongamano lenye mlengo wa kukuza na kuimarisha uongozi na viongozi nchini hasa katika kutekeleza majukumu yao katika sekta wanazohudumia.

Akimwakilisha  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora George Mkuchika wakati  wa uzinduzi wa kongamano hilo  mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Uongozi Prof. Penina Mlama amesema kuwa lengo la kufanya kongamano hilo ni  kubadilishana mawazo kuhusu kukuza na kuimarisha masuala ya uongozi na viongozi nchini hasa katika utendaji.

Ameeleza kuwa mawazo yatakayotolewa katika mjadala huo yatumike katika kuboresha uongozi serikalini na katika sekta binafsi na yaendelezwe ili kuwawezesha viongozi kutenda kazi kwa kuzingatia misingi bora zaidi.Aidha ameeleza  Serikali iliona tatizo katika masuala ya uongozi na ilipofika mwaka 2010 Serikali ilianzisha Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) ili kuwajengea uwezo na kuwaimarisha katika utekelezaji wao wa majukumu.

Mlama amesema kuwa Serikali ya Awamu tano imedhamiria katika kuhakikisha viongozi wanafanya kazi kwa kuzingatia mihimili na maadili kwa ujumla na amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli amesimamia kwa kiasi kikubwa masuala ya uadilifu, nidhamu katika matumizi ya fedha za umma, maadili sehemu za kazi na kupiga vita vitendo vya rushwa na ufisadi.

Kwa upande wake  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja amesema kuwa kongamano hilo ni la kubadilishana mawazo kuhusiana na ukuzaji na uimarishaji wa uongozi na viongozi nchini na washiriki wametoka katika sekta mbalimbali ikiwemo Serikalini, Bungeni, Jeshini, vyama vya siasa na dini.Semboja amesema kuwa kongamano hilo ni la kupanga mikakati na sio kutathimini mifumo iliyopita na ya sasa. Na ameeleza kuwa watatathimini mifumo ili kujenga matokeo bora hapo baadaye.

Amesema kuwa historia inaonesha kuwa viongozi wanaofanya vizuri wanajengwa kutokana na mazingira ambayo watakuja kuongoza na wao kama taasisi watahakikisha wanasimamia majukumu hayo kikamilifu kwa kuandaa mijadala na makongamano mbalimbali yanayolenga kukuza na kuimarisha masuala ya uongozi na viongozi nchini.
 Aliyekuwa Spika wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda (kushoto) na aliyekuwa Waziri wa fedha Zakia Meghji wakifuatilia mjadala huo uliokuwa ukiongozwa  prof. Issa Shivji.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja akihutubia wakati wa kongamano hilo ambapo ameeleza kuwa Taasisi hiyo itaendelea kuandaa mijadala na mada mbalimbali katika kukuza na kuimarisha uongozi na viongozi nchini.
 Mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Uongozi Prof. Penina Mlama akisoma hotuba wakati wa uzinduzi wa kongamano lililokuwa na mlengo wa kukuza na kuimarisha uongozi na viongozi nchini lililofanyika leo jijini Dar es salaam.
Aliyekuwa Spika wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda (kushoto) na aliyekuwa Waziri wa fedha Zakia Meghji wakifuatilia mjadala huo uliokuwa ukiongozwa  prof. Issa Shivji.

KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA KIKAPU MAREKANI MATHEW McCOLLISTER ATUA KUSAKA VIPAJI NA KUFANYA SCOUTING KWA VIJANA CHINI YA MIAKA 20.

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa kikapu nchini (TBF) linapenda kuutaarifu umma kuwa kutakuwa Mafunzo kwa ajili ya kusaka Vipaji na Kuendeleza Vipaji kwa vijana wanaoshiki Mchezo wa Mpira wa kikapu hapa Nchini Tanzania.

Kocha wa Timu ya Taifa wa Mpira wa Kikapu Matthew McCollister pamoja na Msaidizi wake Kocha Steven Michael Priestley wataingua Nchini leo tarehe 2/11/2018 kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro toka Marekani.

Kocha huyo anakuja kwa mara ya pili nchini Tanzania, kwa mara ya kwanza akija na baadhi ya wachezaji nguli wa zamani wa mchezo huo wa kikapu na kutoa mafunzo kwa vijana mbalimbali.

Mafunzo yatakuwa kwa Vijana wote wenye umri kuanzia miaka 10 hadi 20, Mafunzo yamegawanyika sehemu mbili kama inavyo elekeza hapa chini
a) Arusha Kuanzia tarehe 3- 5 November 2018 Viwanja vya Soweto na Sheikh Amri Abedi b) Dsm Kuanzia tarehe 7-8 November Viwanja vya JMK Pack kidongo Chekundu.
c) Muda wa Mafunzo ni kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 na Baadaye saa 9 hadi saa
11 jioni.

Shirikisho linapenda kuwakaribisha Vijana wote pamoja na mikoa jirani ili tuweze kupata fursa ya mafunzo kupitia Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa, katika Maeneo niliyo eleza hapo juu.Pia Shirikisho linapenda Kuwa karibisha Wazazi wote ili waweze kuwapa Moyo vijana wetu wakati wa mafunzo haya endelevu ili kuwajengea uwezo vijana wetu wawe wachezaji wazuri kwa Taifa letu.

Pia Shirikisho linawaomba wadau wote kutoa ushirikiano katika Mafunzo haya kwa Vijana wetu katika kuhakikisha mchezo wa mpira wa kikapu unarejesha heshima yake kitaifa na kimataifa.

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo Ijumaa tarehe 2 Novemba  2018 Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU



TFF YAMTANGAZA MWAMUZI JONESIA RUKYAA KUCHAGULIWA KUCHEZESHA FAINALI ZA AFCON YA WANAWAKE

$
0
0
Na Agness Francis, Glogu ya jamii

UONGOZI wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF ) umemtangaza kuchaguliwa kwa mwamuzi Jonesia Rukyaa kuchezesha Fainali za Afrika za Wanawake zitakazofanyika nchini Ghana.

Rukya ambaye ni muauzi kutoka mkoani Kagera ambaye amekuwa akiminiwa sana katika umakini wa kazi yake na hasa katika kuchezesha mechi za Ligi kuu Tanzania bara.

Kwa mujibu wa TFF mwamuzi huyo amechaguliwa katika orodha ya Waamuzi wa katikati kuchezesha michezo ya fainali za Afrika za wanawake zitakofanyika nchini Ghana. Ambapo jumla ya Waamuzi 13 waliochaguliwa ni wa kati Kati na wasaidizi ni 12.

Hivyo TFF imesema fainali hizo pia zitatumika kupata timu zitakazowakilisha Afrika kwenye Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake zitakazofanyika mwakani nchini Ufaransa.

Ambapo Washindi watatu wa juu ndio watakaofuzu kushiriki Kombe la Dunia..

Watendaji Wakuu na Wenyeviti wa Bodi Waaswa Kuzingatia Sheria Kanuni na Taratibu

$
0
0
Na: Frank Mvungi- MAELEZO

Msajili wa Hazina Bw. Athumani Selemani Mbuttuka amewata Watendaji wakuu , Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi za Taasisi na mashirika ya umma kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na miongozo inayotolewa na Serikali .

Akizungumza katika Semina ya kuwajengea uwezo Viongozi hao, Bw. Athumani amesem,a kuwa lengo la Serikali ni kuona dhamira ya kuazishwa kwa Taasisi na Mashirika ya Umma inafikiwa kwa wakati.

“Kwa mujibu wa vifungu Na.10 (2) (e) na 10 (5) vya Sheria ya Msajili wa Hazina ina mamlaka ya Kusimamia Bodi za Taasisi na Mashirika ya Umma hivyo, tuna wajibu wa kuhakikisha kuwa Bodi na Viongozi wote wanaelewa majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu”; Alisisitiza Mbutuka.

Akifafanua amesema kuwa Bodi na Watendaji wakuu wanapaswa kuwa makini, wabunifu na kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati ili kuhakikisha kuwa Taasisi zinajiwekea mikakati ya kupunguza gharama za uendeshaji zinazotokana na matumizi yasiyo ya lazima hususani safari za Bodi na viongozi zisizokuwa na manufaa kwa Taasisi husika.

Alibainisha kuwa Taasisi zinapaswa kuwa na mikakati madhubuti ya kukusanya mapato ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, sambamba na kuhakikisha kuwa matumizi yote yanafanyika kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali ya Serikali.

Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbuttuka akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina kwa Watendaji Wakuu, Wenyeviti na wajumbe wa Bodi kuhusu usimamizi wa Taasisi na mashirika ya Umma ili kuyawezesha kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Bw. Edwin Rutageruka akizungumza wakati wa semina kwa Watendaji Wakuu, Wenyeviti na wajumbe wa Bodi kuhusu usimamizi wa Taasisi na mashirika ya Umma ili kuyawezesha kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake, Semina hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina. 
Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbuttuka (katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya watendaji wakuu wa mashirika ya umma walioshiriki katika semina kwa Watendaji hao, Wenyeviti na wajumbe wa Bodi kuhusu usimamizi wa Taasisi na mashirika ya Umma ili kuyawezesha kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake. 


WAGONJWA 23 WAPATIWA HUDUMA YA TIBA YA RADIOLOJIA MUHIMBILI

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Taasisi ya Tiba Mifupa (MOI), Chuo Kikuu cha Yale na Emory nchini Marekani wameendesha kambi maalum ya kutoa huduma za kibingwa kupitia tiba Radiolojia ambapo wagonjwa 23 wamenufaika na tiba hiyo.

Tiba hiyo inahusisha utaalam wa kutumia vifaa vya Radiolojia kama X-Ray, MRI, CT-Scan na Ultra- Sound kutibu moja kwa moja ugonjwa au kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Radiolojia MNH, Dkt. Flora Lwakatare amesema huduma hiyo ya kibingwa ilianza kwa mara ya kwanza nchini Novemba mwaka jana ambapo kabla ya uanzishwaji wake wagonjwa waliokuwa wanahitaji huduma hizi walikuwa wakienda nje ya nchi.

Akielezea kuhusu huduma zilizitolewa katika kambi hiyo amesema ni utoaji wa sampuli kutoka kwenye vivimbe katika sehemu mbalimbali za mwili ambazo si rahisi kufikiwa bila upasuaji mkubwa, kuzibua mirija ya nyongo, kuweka mirija kwenye figo ambazo mirija ya mkojo imeziba na unyonyaji wa vivimbe vyenye maji au usaha.‘‘Kambi hii imehusisha wakufunzi ambao ni madaktari bingwa, mafundi sanifu Radiolojia, wauguzi Radiolojia kutoka vyuo vikuu vya Yale na Emory. Pia, watalaam kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa na CCBRT nao wananufaika na mafunzo hayo.’’
Mkuu wa Idara ya Radiolojia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Flora Lwakatare akizungumza na waandishi wa habari juu ya wataalam kuzibua njia ya nyongo ya mgonjwa kupitia huduma ya kibingwa ya tiba radiolojia kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Chuo Kikuu cha Yale na Emory nchini Marekani. Kutoka Kushoto ni daktari bingwa wa upasuaji wa Muhimbili, Dkt Godfrey Mchele na mtaalam wa tiba ya radiolojia, Profesa Frank Minja kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani.
Baadhi ya wataalam wa tiba hiyo pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Dkt. Flora Lwakatare.
Wataalam wa radiolojia wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) pamoja na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Yale na Emory nchini Marekani wakishirikiana kuzibua njia ya nyongo ya mgonjwa kupitia huduma ya kibingwa ya tiba radiolojia.
Mtaalam wa tiba radiolojia, Profesa Frank Minja kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jinsi wataalam wa Muhimbili, MUHAS na MOI walivyofanya maandalizi ya kufanikisha huduma ya tiba radiolojia. Kushoto ni Dkt. Lwakatare na kulia ni mtaalam wa huduma za radiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Emory nchini Marekani.


RC MAKONDA AKABIDHI MABASI 4 KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, NI YALE YALIYOKUWA "UKWECHE".

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhi Mabasi 4 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na Jeshi la Magereza kwaajili ya kuongezea ufanisi katika utendaji wa Kazi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Mabasi 4 aliyoyakabidhi RC Makonda Leo ni Kati ya Mabasi 11 yaliyokuwa yamekufa (ukweche) ambapo baada ya RC Makonda kuyaona na kubaini uhaba wa magari kwa vyombo vya ulinzi na usalama aliwatafuta wafadhili wa Kampuni ya Dar Coach Ltd waliojitolea kuyarejeshea uhai magari hayo na hatimae leo yanatembea Barabarani yakiwa mazima.

RC Makonda amesema ukarabati wa mabasi hayo ulihusisha Kubadilisha Bodi, kupaka Rangi, kubadili Viti, kuweka Mfumo wa kuchaji simu, AC, TV, Taa,Madirisha, Matairi pamoja na kuongeza na kupunguza idadi ya viti.

Aidha RC Makonda amesema mkakati wa kuendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa vyombo vya ulinzi na usalama utaendelea ikiwa ni pamoja na kugusa maisha ya mtumishi mmojammoja kwa kuwapatia mikopo ya viwanja vya bei nafuu. Hata hivyo RC Makonda ameshukuru Kampuni ya Dar Coach Tanzania Ltd kwa uzalendo walioonyeaha kukarabati magari hayo pasipo kutumia pesa ya serikali.

Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Luteni Jenerali Yacoub Mohamed amempongeza RC Makonda kwa ubunifu wa kufufua magari yaliyokuwa yamekufa ambapo ameeleza kuwa yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaongezea ufanisi katika kazi kwa kupunguza changamoto ya usafiri.

Mabasi 4 yaliyokabidhiwa leo ni Ashok Leyland 01, Iveco 2 na Toyota Coaster moja huku magari mengine 7 yakiwa hatua ya mwisho kukamilika.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akisalimiana na baadhi ya Maofisa wa jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),wakati alipokwenda leo kukabidhi Mabasi 4 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na Jeshi la Magereza kwa ajili ya kuongezea ufanisi katika utendaji wa Kazi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
 Baadhi ya magari yaliyokabidhi wa kwa JWTZ na Jeshi la Magereza
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiagana na mmoja wa Maoisa wa JWTZ,mara baada ya kukabidhi Mabasi 4 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na Jeshi la Magereza kwaajili ya kuongezea ufanisi katika utendaji wa Kazi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
 Picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano hayo
 

MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI KIGOMA

$
0
0

Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

KUFUATIA operesheni ya kutokomeza uvuvi haramu ndani ya Ziwa Tanganyika inayoendelea Waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina ameteketeza zana mbalimbali za uvuvi haramu zenye zaidi ya shilingi bilioni tatu zilizokuwa zikitumika katika ziwa Tanganyika.

Akiongea na wananchi baada ya zoezi la kuteketeza zana hizo haramuza uvuvi katika eneo la Businde nje kidogo ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Mpina amewataka wananchi kushirikiana na serekali kwa kuwafichua wahalifu wanaotumia zana haramu ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupigwa faini na kwenda jela.

Alisema serekali haitomuonea mtu yoyote huruma ambayeatakamatwa anafanya uvuvi haramu au kuwa na zana za uvuvi haramu awe kiongozi au raia wa kawaida sheria lazima ichukue mkondo wake.''Sisi lengo letu ni kuona samaki wanaongezeka katika ziwa Tanganyika,na watu wavue kwa kufuata sheria ili Taiafa lipate mapato na watu wapate ajira"alisema

Alisema oparesheni inayofanyika katika ziwa Tanganyika ni oparesheni ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo itaendelea katika maeneo yote ya ziwa Tanganyika lengo likiwa ni kuondoa uvuvi haramu na mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia samaki wachanga na utoroshwaji wa samaki na mazao yake kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.

Alisema takwimu zinaonyesha utoroshwaji wa samaki na dagaa kwenda nje katika ZIwa Tanganyika ilikuwa ni mkubwa kwenda nje ya nchi bila kulipa chochote na wageni nao kutoka nchi za jirani wanakuja kwenye maji yetu wanavua na kuondoka.
 Waziri wa Mifugo na Uvivu Luhaga Mpina akiteketeza nyavu 352 haramu za uvuvi katika eneo la Businde nje kidogo ya Manispaa ya Kigoma Ujiji zilizokamatwa kwenye oparesheni maalum ya kuzuia uvuvi haramu ndani ya ziwa Tanganyika.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiongea na wavuvi pamoja na wafanyabiashara wa mazao ya dagaa na samaki katika mwalo wa Kibirizi kabla ya kuteketeza zana haramu za Uvuvi zilizopatikana kufuatia oparesheni ya kuzuia uvuvi haramu inayoendelea katika Ziwa Tanganyika.

HALI ZA MAJERUHI WALIOPATA AJALI YA TRENI JIJINI DAR ES SALAAM

MASHIBA- UPATIKANAJI WA ARDHI NA BAADHI YA VIBALI NI TATIZO KWA BAADHI YA WAWEKEZAJI

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA

MENEJA wa kanda ya Mashariki wa kituo cha uwekezaji Tanzania TIC Venance Mashiba , asema lipo tatizo kwa baadhi ya wawekezaji hasa katika upatikanaji wa ardhi na baadhi ya vibali vinavyochukua muda mrefu kwenye upatikanaji wake .

Alisema hayo wakati akizungumzia changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao ,wakati wa maonyesho ya bidhaa za viwandani yanayoendelea Pichandege Kibaha ,mkoani Pwani .

Mashiba alieleza ,huduma za uwekezaji ni mtambuka ambapo zinatolewa na taasisi mbalimbali ambazo taratibu zake zikigongana inasababisha changamoto ya ucheleweshaji wa huduma kwa wawekezaji."Tatizo kubwa lipo kwenye ardhi kwani ardhi zote zipo chini ya halmashauri ,mwekezaji lazima apeleke wazo lake halmashauri na akipatiwa ardhi ndipo aje kwetu kuandikisha mradi wake "

"Sasa mradi wake utakubaliwa endapo atapata ardhi na taratibu za upatikanaji wa ardhi ni nyingi na ni ndefu"alifafanua Mashiba .Mashiba alisema ,kutokana na hilo kituo hicho , kimeimarisha huduma zake kwa kuongeza taasisi 11 za serikali ambazo zinatoa huduma mbalimbali, vibali na leseni ili mwekezaji apate huduma mahala pamoja na sio kuzunguka .

Alisema, ikitokea mwekezaji ana changamoto zinazohusuana na huduma zinazotolewa kwenye hizo taasisi basi wakuu wa taasisi hizo hukutana na kuamua kuzitatua .Nae mkuu wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo aliipongeza TIC kwa jitihada zake katika kukuza na kuvutia uwekezaji nchini na namna inavyohudumia wawekezaji kupitia huduma za mahala pamoja zinazotolewa na taasisi mbalimbali zilizopo ndani ya ofisi za kituo hicho .

Alielezea kwamba ,Mkoa huo ni miongoni mwa mikoa inayopokea wawekezaji na hivyo nguvu ya kuwahudumia iimarishwe. Ndikilo aliitaka TIC kuhakikisha inapata taarifa zinazohusiana na uwekezaji Mkoani humo kwa kuwasiliana na halmashauri za mkoa ."Kwa kufanya hivyo kutarahisisha uratibu na huduma kwa wawekezaji wa Mkoa na Taifa kijumla " alisema Ndikilo.

Alisisitiza ni vyema wakawa na taarifa za maeneo ya uwekezaji yaliyotengwa pamoja na ,takwimu za miradi ya uwekezaji.Katika kuhakikisha mkoa wa Pwani unaendelea kuvutia wawekezaji Ndikilo alisema atawasilisha TIC maeneo ambayo tayari yametengwa kwa ajili hiyo ili yatafutiwe wawekezaji.
Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto )akizungumza wakati alipotembelea banda la maonyesho ya ,kituo cha uwekezaji Tanzania( TIC )katika maonyesho ya bidhaa za viwandani Pichandege ,Kibaha Pwani.(picha na Mwamvua Mwinyi)

NIMEFARIJIKA NA MAENDELEO YA VIWANDA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema amefarijika na maendeleo ya ujenzi wa viwanda kwenye mkoa wa Tanga kwa sababu vitasaidia katika ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira.

Aliyasema hayo jana jioni (Alhamisi, Novemba 1, 2018) alipotembelea kiwanda cha saruji cha Rhino na kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh, vyote vya jijini Tanga.Waziri Mkuu ambaye jana alihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tanga, aliwapongeza wawekezaji wa viwanda hivyo kwa kuunga mkono mkakati wa Serikali. 

Alisema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kukuza uchumi kutoka wa chini hadi wa kati ifikapo 2025 kwa kupitia sekta ya viwanda.Akizungumzia kuhusu kiwanda cha Rhino, Waziri Mkuu alisema kiwanda hicho na vingine vya saruji nchini vitasadia kupunguza gharama ya saruji nchini na kurahisisha ujenzi.

“Serikali inaamini kwamba uwepo wa viwanda mbalimbali nchini si tu utawezesha ukuaji wa uchumi wa Taifa, pia utasaidia katika kumaliza changamoto ya ajira hususani kwa vijana.”Akiwa katika kiwanda cha Tanga Fresh, Waziri Mkuu aliwataka wafugaji mkoani Tanga wabadili mfumo wa ufugaji na wafuge kwa kutumia njia za kisasa ili waongeze uzalishaji.

“Wafugaji lazima wakubali kubadilika watumie fursa ya uwepo wa kiwanda hiki kwa kufuga kisasa ili wapate maziwa mengi kwa sababu wana uhakika wa kuyauza kiwandani hapa”.Kadhalika, Waziri Mkuu aliwataka wananchi walioajiriwa kiwandani hapo wafanye kazi kwa bidii, uaminifu na wawe waadilifu na wasijihusishe na vitendo vya wizi kwa kuwa havina tija.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, NOVEMBA 2, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu uzalishaji wa saruji  kutoka kwa Bw. Pradeep Punlana  (katikati) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha saruji cha  Rhino kilichopo eneo la Maweni jijini Tanga  wakati alipotembelea kiwanda hicho  Novemba 1, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu uzalishaji wa saruji  kutoka kwa Bw. Pradeep Punlana  (katikati) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha saruji cha  Rhino kilichopo eneo la Maweni jijini Tanga  wakati alipotembelea kiwanda hicho  Novemba 1, 2018


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama usindikaji wa maziwa wakati alipotembelea kwanda cha Maziwa cha Tanga Fresh cha jijini Tanga, Novemba 1, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, watatu kushoto ni Meneja Ufundi wa kiwanda hicho, Adam Gamba na wanne kukhoto ni Meneja Mkuu wa kiwanda, Michael Karata. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Soni wilayani  Lushoto akiwa katika ziara ya mkoa wa Tanga, Novemba 1, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE ASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA NCHI ZA MWAMBAO WA BAHARI YA HINDI

$
0
0


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya nchi za mwambao wa Bahari ya Hindi unaofanyika Durban, Afrika Kusini leo tarehe 2 Novemba, 2018. 

Mkutano huu umetanguliwa na Kikao cha 20 cha Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi tarehe 31 Oktoba hadi tarehe 01 Novemba, 2018 ambapo ujumbe huo uliongozwa na Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Jumuiya ya nchi za mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) ilianzishwa mwaka 1997 awali, ikijulikana kama Indian Ocean Rim Association for Regional Cooperation IORA-AC kabla ya kubadilishwa kuwa IORA mwaka 2013. Jumuiya hii inaundwa na nchi wanachama 21 ambazo ni Afrika Kusini, Australia, Bangladesh, Comoro, India, Indonesia, Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kenya, Malaysia, Madagascar, Mauritius, Msumbiji, Shelisheli, Singapore, Somalia, Sri Lanka, Sultani ya Oman, Thailand, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Yemen. Tanzania ni moja kati ya nchi waanzilishi wa Jumuiya hii.

Katika muundo wake, IORA pia ina washirika wa mazungumzo (Dialogue Partners) saba (7) ambao ni Jamhuri ya Watu wa China, Japan, Marekani, Misri, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ambao hushiriki katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Jumuiya.

Katika uongozi, Afrika Kusini ndie Mwenyekiti wa sasa wa IORA akisaidiana na Umoja wa Falme za Kiarabu kama Makamu Mwenyekiti. Hivyo, Mheshimiwa Lindiwe Sisulu (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Kusini aliongoza mkutano huu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiwa kwenye Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya nchi za mwambao wa Bahari ya Hindi (IORA) unaofanyika Durban, Afrika Kusini kuanzia tarehe 2 Novemba, 2018. Mhe. Dkt. Ndumbaro anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo ambao pamoja na mambo mengine nchi hizo zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika kutekeleza miradi ya maendeleo iliyo chini ya maeneo tisa vipaumbele kwa IORA ambayo ni usalama na ulinzi wa bahari; biashara na uwekezaji; usafiri wa bahari; uvuvi; menejimenti ya udhibiti wa majanga; taaluma, sayansi na teknolojia; utalii na utamaduni; uchumi bahari; na uwezeshaji wanawake. Mwingine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi
Mkutano ukiendelea
Picha ya pamoja ya Mawaziri

MSAJI WA HAZINA AWAFUNDA WENYEVITI WAPYA


MAONYESHO YA SWAHILI FASHION WEEK KUFANYIKA NOVEMBER 30 HADI DISEMBA

$
0
0
Katika kuendeleza mafanikio makubwa na ya kipekee kwa msimu wa 11  ya maonyesho  ya jukwaa la mitindo (SWAHILI FASHION WEEK) ambalo ni la kipekee Afrika mashariki maandalizi yafunguliwa rasmi jijini Dar es salaam.

Mbunifu  wa mitindo nchini Mustafa hassanali akizungumza na wadau, wabunifu pamoja na wanahabari amefungua rasmi maandalizi ya wiki ya mitando amesema kuwa maandalizi ya mwaka huu ni ya kusisimua na kufurahisha sababu kazi za mitindo ziko hali ya juu .

Hassanali  amesema kwa utiifu wote  lengo la kuendeleza na kuimarisha  nafasi ya mitindo kwa Afrika  linabaki kuwa mbele,kupitia jukwaa hili na mchango mkubwa wa waandishi wa habari tutaendelea kuunga mkono vipaji  vilivyopo katika sekta ya mitindo.

Aidha,amefafanua zaidi licha ya kuunga mkono kuendeleza vipaji bali pia kutengeneza na kukuza soko la kimataifa na ndio sababu kuu ya kuunga mkono kutekeleza juhudi za Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Katika sera ya kuelekea uchumi wa viwanda kupitia bidhaa za nguo zilizotengenezwa Tanzania.

Alikadhalika balozi wa italia nchini Tanzania ROBERT MENGONI amesema ifike pahala kila mtu aheshimu kazi za Ubunifu wa mitindo kama biashara kutokana na wabunifu kuwekeza na kupata vipato vya kuendesha maisha yao pamoja na familia kupitia Ubunifu huo.      kwa upande wa mwakilishi wa baraza la Sanaa (BASATA) Vivian shalura amepongeza juhudi zinazofanywa na mbunifu huyo mahiri katika mitindo ambae amekua akifata sheria pamoja na vibali huku akiwa amejisajiri kikamilifu.

Shalua amewataka wabunifu chipukizi wajaribu kubuni nguo ambazo hazitawabugudhi au kudharirisha watazamaji,pia amewashauri wabunifu kukuza lugha yetu ya kiswahili kupitia baadhi ya Nguo ambazo majina yake yanatokana na kiswahili chetu kama vile mshono wa mwanamke nyonga.
Mbunifu wa mitindo nchini  Mustafa hassanali akizungumza akifungua maandalizi ya wiki ya mitindo Balozi wa italia nchini Robert mengoni akiwa mwakilishi kutoka baraza la Sanaa (BASATA) Vivian sharula

KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA KIKAPU MAREKANI MATHEW McCOLLISTER ATUA KUSAKA VIPAJI NA KUFANYA SCOUTING KWA VIJANA CHINI YA MIAKA 20

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa kikapu nchini (TBF) linapenda kuutaarifu umma kuwa kutakuwa Mafunzo kwa ajili ya kusaka Vipaji na Kuendeleza Vipaji kwa vijana wanaoshiki Mchezo wa Mpira wa kikapu hapa Nchini Tanzania.

Kocha wa Timu ya Taifa wa Mpira wa Kikapu Matthew McCollister pamoja na Msaidizi wake Kocha Steven Michael Priestley wataingua Nchini leo tarehe 2/11/2018 kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro toka Marekani.

Kocha huyo anakuja kwa mara ya pili nchini Tanzania, kwa mara ya kwanza akija na baadhi ya wachezaji nguli wa zamani wa mchezo huo wa kikapu na kutoa mafunzo kwa vijana mbalimbali.

Mafunzo yatakuwa kwa Vijana wote wenye umri kuanzia miaka 10 hadi 20, Mafunzo yamegawanyika sehemu mbili kama inavyo elekeza hapa chini
a) Arusha Kuanzia tarehe 3- 5 November 2018 Viwanja vya Soweto na Sheikh Amri Abedi
b) Dsm Kuanzia tarehe 7-8 November Viwanja vya JMK Pack kidongo Chekundu.
c) Muda wa Mafunzo ni kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 na Baadaye saa 9 hadi saa
11 jioni.

Shirikisho linapenda kuwakaribisha Vijana wote pamoja na mikoa jirani ili tuweze kupata fursa ya mafunzo kupitia Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa, katika Maeneo niliyo eleza hapo juu.
Pia Shirikisho linapenda Kuwa karibisha Wazazi wote ili waweze kuwapa Moyo vijana wetu wakati wa mafunzo haya endelevu ili kuwajengea uwezo vijana wetu wawe wachezaji wazuri kwa Taifa letu.

Pia Shirikisho linawaomba wadau wote kutoa ushirikiano katika Mafunzo haya kwa Vijana wetu katika kuhakikisha mchezo wa mpira wa kikapu unarejesha heshima yake kitaifa na kimataifa.

TAARIFA YA IDARA YA UHAMIAJI KWA WAGENI WOTE WANAOISHI NCHINI

MTANZANIA JONESIA RUKYAA KUCHEZESHA FAINALI ZA AFCON YA WANAWAKE

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya Jamii. 

Uongozi wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) umemtangaza Mtanzania Pekee ambaye ni mwamuzi  Jonesia Rukyaa kuwa amechaguliwa kuchezesha Fainali za Afrika za Wanawake zitakazofanyika nchini Ghana.

Rukya  ni muauzi kutoka Mkoani Kagera ambaye amekuwa akiminiwa Sana katika umakini wa kazi yake na hasa katika kuchezesha mechi za Ligi kuu Tanzania bara.

Muamuzi huyo amechaguliwa katika orodha ya Waamuzi wa katikati kuchezesha michezo ya fainali za Afrika za wanawake zitakofanyika nchini Ghana. 


Ambapo jumla ya Waamuzi 13 waliochaguliwa  ni wa kati Kati na wasaidizi ni 12.

TFF imesema Fainali hizo pia zitatumika kupata timu zitakazowakilisha Afrika kwenye Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake zitakazofanyika mwakani nchini Ufaransa.

Ambapo Washindi Watatu wa juu ndio watakaofuzu kushiriki  Kombe la Dunia.

MAONYESHO YA SWAHILI FASHION WEEK KUANZA NOVEMBER 30

$
0
0
Katika kuendeleza mafanikio makubwa na ya kipekee kwa msimu wa 11  ya maonyesho  ya jukwaa la mitindo (SWAHILI FASHION WEEK) ambalo ni la kipekee Afrika Mashariki maandalizi yafunguliwa rasmi jijini Dar es salaam.

Mbunifu  wa mitindo nchini, Mustafa Hassanali akizungumza na wadau, wabunifu pamoja na wanahabari amefungua rasmi maandalizi ya wiki ya mitando amesema kuwa maandalizi ya mwaka huu ni ya kusisimua na kufurahisha sababu kazi za mitindo ziko hali ya juu.
Hassanali  amesema kwa utiifu wote  lengo la kuendeleza na kuimarisha  nafasi ya mitindo kwa Afrika  linabaki kuwa mbele,kupitia jukwaa hili na mchango mkubwa wa waandishi wa habari tutaendelea kuunga mkono vipaji  vilivyopo katika sekta ya mitindo.
Aidha,amefafanua zaidi licha ya kuunga mkono kuendeleza vipaji bali pia kutengeneza na kukuza soko la kimataifa na ndio sababu kuu ya kuunga mkono kutekeleza juhudi za Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Katika sera ya kuelekea uchumi wa viwanda kupitia bidhaa za nguo zilizotengenezwa Tanzania.
Alikadhalika balozi wa italia nchini Tanzania Robert Mengoni amesema ifike pahala kila mtu aheshimu kazi za Ubunifu wa mitindo kama biashara kutokana na wabunifu kuwekeza na kupata vipato vya kuendesha maisha yao pamoja na familia kupitia Ubunifu huo.      kwa upande wa mwakilishi wa baraza la Sanaa (BASATA) Vivian shalura amepongeza juhudi zinazofanywa na mbunifu huyo mahiri katika mitindo ambae amekua akifata sheria pamoja na vibali huku akiwa amejisajiri kikamilifu.
Shalua amewataka wabunifu chipukizi wajaribu kubuni nguo ambazo hazitawabugudhi au kudharirisha watazamaji,pia amewashauri wabunifu kukuza lugha yetu ya kiswahili kupitia baadhi ya Nguo ambazo majina yake yanatokana na kiswahili chetu kama vile mshono wa mwanamke nyonga.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images