Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 02.11.2018


TAARIFA YA HABARI SAA MBILI USIKU YA ITV NOVEMBA 02, 2018

MICHUZI TV: RC MBEYA AWATAKA WATENDAJI KUWA WABUNIFU UKUSANYAJI WA MAPATO

MICHUZI TV: HALI ZA MAJERUHI WALIOPATA AJALI YA TRENI JIJINI DAR ES SALAAM

VOA SWAHILI: Duniani Leo November 2nd, 2018

MICHUZI TV: KAULI YA YANGA KUHUSU UCHAGUZI WA KLABU HIYO

MICHUZI TV: ZITTO ASOMEWA MASHTAKA MATATU YA UCHOCHEZI, APATA DHAMANA...

MICHUZI TV: FAHAMU: Utamu wa muziki wa "Disco" na ulikotokea, Dj John Dillinga afunguka


BancABC yaja na ofa kwa wateja wa akaunti za amana.

0
0
· Wateja wanaoufungua akaunti za amana kupata riba hadi asilimia 14 papo hapo.

BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara na ambao imeorodhesha kwenye soko la hisa la London, imepiga hatua nyingine kwenye soko baada ya kutangaza ofa kabambe kwa wateja wakati huu wa kuelekea msimu wa Krismasi na sikukuu za mwisho wa mwaka.

Ofa hiyo ni maalum kwa wateja wote wanaofungua akaunti za amana ambapo Watapata riba ya hadi asilimia 14 papo hapo, Ofa hiyo imeanza leo na wateja wote watanza kufaidika nayo kuanzia leo Novemba mosi mpaka Disemba 31 mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza hatua ya benki hiyo kutoa ofa hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja binafsi BancABC Joyce Malai alisema kuwa benki yake imeamua kutoa ofa hadi asilimia 14 ya papo kwa papo kwa wateja wote ambao wanafungua akaunti za amana.

Hata hivyo, Malai alisema wateja watakuwa na uhuru wa kuchangua kuchukua riba papo hapo au kwa kila mwezi au mwishoni mwa amana. Vile vile, mteja atakuwa na uwezo wa kuchukua mkopo wa hadi asilimia 80 ya amana yake, Malai aliongeza. Hii ni ofa bora kwenye soko kwa sasa na hivyo tutoa wito kwa wateja wetu na hata wale wasiokuwa na akaunti kwetu kutumia fursa ya ofa hii ya msimu huu wa sikukuu kwa manufaa yao,” alisema alisema Malai.


Mkuu wa Kitengo cha Wateja binafsi BancABC Joyce Malai (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa benki hiyo Barton Mwasamengo wakionyesha bango baada ya benki hiyo kutangaza kutoa ofa maalum kwa wateja wote wanaofungua akaunti za amana ambapo Watapata riba ya asilimia 14 papo na inaanza leo Novemba mosi mpaka Disemba 31 mwaka huu.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja binafsi BancABC Joyce Malai (kushoto) kutangaza hatua ya benki hiyo kutoa ofa maalum kwa wateja wote wanaofungua akaunti za amana ambapo Watapata riba ya asilimia 14 papo na inaanza leo Novemba mosi mpaka Disemba 31 mwaka huu. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa benki hiyo Barton Mwasamengo.


KATIBU WA BUNGE AKUTANA NA MKURUGENZI WA TBC

0
0

Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji (TBC)Dkt. Ayoub Rioba wakati Mkurugenzi huyo alipomtembelea na kufanya nae mazungumzo Ofisini kwake Jijini Dodoma.

KAMATI YA BAJETI YAKUTANA NA WIZARA YA FEDHA

0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mheshimiwa George Simbachawene akielezea jambo mbele ya Kamati hiyo ilipokuwa ikijadili Taarifa za Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/2020 na Mwongozo wa maandalizi ya Mpango wa Bajeti kwa mwaka wa Fedha 2019/20 – 2021/22 katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
Waumbe wa Kamati ya Bajeti wakijadili Taarifa za Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/2020 na Mwongozo wa maandalizi ya Mpango wa Bajeti kwa mwaka wa Fedha 2019/20 – 2021/22 kataika Kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.

MAAGIZO MATANO YA NAIBU WAZIRI NDUGULILE KWA KAMISHNA WA USTAWI WA JAMII

DKT FAUSTINE NDUGULILE AZINDUA KAMATI YA ULINZI NA WATOTO MKOANI MANYARA

USIKOSEE KUTAZAMA JUMAMOSI HII NA JUMATATU MIAKA MITATU YA JPM TBC NA MKURUGENZI MKUU TRC

DC MURO AIBUA UFISADI WAKUTISHA KANISANI,VIGOGO KUBURUZWA


DKT.TULIA ATOA RAI KWA MIKOA NA WILAYA NCHINI KUIGA MKOA WA PWANI KWA KASI YA UWEKEZAJI

0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

NAIBU Spika wa Bunge ,Dkt .Tulia Ackson amewataka wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuiga mfano wa mkoa wa Pwani ,kuvutia wawekezaji pamoja na kutenga maeneo ya uwekezaji ili kwenda na kasi ya ujenzi wa viwanda .

Akitembelea maonyesho ya bidhaa za viwandani ,Pichandege Kibaha Mkoani Pwani ,Dkt.Tulia alisema mkoa wa huo una viwanda vikubwa 109 ambavyo ni vingi kwenye mkoa mmoja .Alieleza ,mikoa mingine ardhi zimefinywa bado hawajaona fursa hii, hivyo watenge maeneo na kuweka mipango mkakati ili kuwarahisishia wawekezaji kupata maeneo .

"Nimepita kwenye mabanda mengi ya wenye viwanda kwenye maonyesho haya ,wameonyesha nia ya kukuza viwanda vyao kwa maana ya kwamba kwenda kwenye kanda mbalimbali ,wanataka kuendeleza zoezi hili sehemu nyingine ""Tunaweza kujiiuliza kwanini viwanda vinaenda Pwani lakini kumbe wamesharahisisha kwa kutenga maeneo mengi na kujiwekea mipango na kuboresha miundombinu " alifafanua Dkt.Tulia .

Aidha ,alisema wataishauri serikali namna ya kufanya navyo kazi viwanda vya nguzo za umeme za zege kwani matumizi ya kusogeza huduma ya umeme bado ni makubwa hivyo zikitumika itasaidia tofauti na nguzo za miti ambazo zinagusa suala la athari za kimazingira .
 NAIBU Spika wa Bunge ,Dkt .Tulia Ackson ,alipotembelea maonyesho ya bidhaa za viwandani ,Pichandege Kibaha Mkoani Pwani (picha na Mwamvua Mwinyi)
 Banda la kampuni inayojishughulisha na uingizaji wa dawa za kutibu maji nchini (Junaco), (wa katikati)ni ofisa uendeshaji wa kampuni hiyo ,Edwin Magere.(picha na Mwamvua Mwinyi)


TFDA YATOA SOMO LA KUDHIBITI SUMUKUVU KWA WASINDIKAJI WA UNGA MCHANGANYIKO NA SIAGI YA KARANGA

0
0
Na: James Ndege Arusha 

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) inaendesha kampeni ya kuhamasisha wasindikaji wa unga mchanganyiko wa mahindi na nafaka nyingine maarufu kama unga wa lishe pia siagi ya karanga ili kudhibiti sumu kuvu. 

“Sumukuvu (Aflatoxin) hutokana na aina ya ukungu (fangasi) unaoota zaidi kwenye mazao ya mahindi na karanga na huweza kutokea katika mazao haya wakati yakiwa shambani, kuvunwa , kusafirishwa au kuhifadhiwa endapo wahusika hawatazingatia ushauri wa wataalam. 

Kabla ya kusindika, ikitokea wasindikaji hawajachambua mazao hayo na kuondoa mabovu na kuyateketeza ili yasiliwe na binadamu au wanyama, bidhaa hizo zitakuwa na kiwango kikubwa cha sumukuvu na hivyo kuathiri afya ya watumiaji kwa kuwa atakayekula kiwango kidogo kidogo cha sumu hiyo anaweza kupata madhara baada ya muda mrefu kama vile saratani ya ini, upungufu wa kinga na udumavu. 

Vile vile atakayekula kiasi kikubwa cha sumu hiyo kwa muda mfupi, huweza kupata madhara makubwa ya kiafya ya kuharibika ini hata kusabisha kifo, hivyo ni muhimu wasindikaji wetu mzingatie ushauri wa TFDA katika kusindika bidhaa zenu ili kulinda afya ya jamii lakini pia kupata masoko ya ndani na nje ya nchi” alisema Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa TFDA Makao Makuu, Bi. Immaculata Justine wakati wa maelezo ya awali ya ufunguzi wa mafunzo ya Wajasiriamali wapatao 70 wa Mkoa wa Arusha. 

Mgeni Rasmi katika mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo katika hotuba yake ya ufunguzi alisema “Ubora na Usalama wa vyakula vinavyosindikwa na Wasindikaji nchini ni jambo la msingi kwa afya za Wananchi. Vyakula ni bidhaa muhimu na nyeti kwa usalama wa jamii na kamwe Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli haitakubali vyakula visivyo na ubora viingie katika soko la Tanzania”. 

“Vyakula duni visivyo na ubora vikiingia katika mzunguko wa soko vitaleta madhara makubwa kwa afya za watumiaji lakini pia vitakosa soko la ndani na nje ya nchi hivyo kudumaza ukuaji wa sekta ya viwanda nchini. Mafunzo haya ya udhibiti wa sumu kuvu yatawasaidia wasindikaji wetu kuweza kuzalisha bidhaa za chakula salama na bora kwa mujibu wa vigezo vya kisheria”. 

Mafunzo hayo yameshirikisha pia Watalam kutoka SIDO Makao Makuu, Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) Makao Makuu, Halmashauri na Mkoa katika Idara za Afya, Lishe, Kilimo na mifugo ili yaweze kuwa endelevu. Ndani ya wiki mbili sasa, mafunzo kama haya yamefanyika katika mikoa ya Dodoma na Morogoro na mikakati inaendelea katika maeneo yaliyosalia.
Mgeni Rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo (aliyekaa katikati) akiwa na viongozi wengine, kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula kutoka TFDA Makao Makuu, Immaculata Justine (wa nne); Kaimu Meneja wa TFDA Kanda ya Kaskazini, Bw. Ben Mcheza (wa pili); Mwenyekiti wa mafunzo hayo Bw. Mathias Msemo (wa kwanza) na Katibu wa Mafunzo husika Bi. Agata Tuheri wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Serikali walioshiriki katika tukio hilo.
Mgeni Rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wasindikaji wa Manispaa ya Arusha. 
Mgeni Rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wasindikaji wa Halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Arusha.
Mtaalam wa TFDA, Bw. Kaiza Kilango akiwasilisha mojawapo ya mada ya udhibiti wa sumu kuvu.

DC MURO AKABIDHIWA MIFUKO 75 YA SARUJI NA MIL. 5 KWA AJILI YA UJENZI WA VYOO

0
0
Na, Imma Msumba Arumeru

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh. Jerry Muro Amepokea misaada ya saruji mifuko 75, shilingi milioni 5 pamoja na vyoo 20 vya kisasa kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya Shule ya Msingi Seliani kilichotitia wiki iliyopita.

Akizungumza mara baada ya kupokea misaada hiyo Dc Muro amesema kuwa misaada hiyo itasaidia kufanikisha ujenzi wa vyoo hivyo kwa muda mfupi, Pia amewashukuru sana wadau wa kampuni ya Usafiri ya Dar Lux kwa msaada wa Milioni Tano ( 5 ).

kwa upande wake Ndg. Nangu amesema wamejitolea Saruji hiyo kwa ajili ya vyoo vya kisasa kabisa yenye thamani ya sh.milioni Moja na Laki moja na ishirini na tano kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Dc Muro baada ya kupata Taarifa za janga la kutitia kwa choo hicho.

“Tunatambua changamoto wanazopata wanafunzi hasa kwa mtoto wa kike kutokana na maumbile yake, hivyo ujenzi wa vyoo hivi utasaidia kuwafanya wanafunzi hao kufurahia mazingira yatakayokuwamo wakiwa shuleni,” alisema Nangu.

Alisema wanafahamu matatizo wanayoyapata watoto wa kike wakiwa shuleni hasa wanapofkia hatua ya kuvunja ungo, kutokana na mabadiliko yanayoanza kutokea na wanapokuwa kwenye tarehe zao ambapo wengine hulazimika kutokwenda shule kutokana na mabadiliko yao ya kimwili, hivyo kwa kushirikiana na Dc Muro wanaamini ujenzi wa vyoo hivyo utawaondolea mabinti wasiwasi.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro Akikabidhiwa mifuko ya Saruji kutoka kwa mdau wa maendeleo Ndg. Ramadhani Nangu mwakilishi wa Bwana Manglan anayeishi nchini Marekani kwa ajili ya ujenzi wa choo cha shule ya Seliani kilicho titia wiki iliyopita.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro,sambamba na Katibu Tawala wa Arumeru Mwl. James Michembe pamoja na Mkurugenzi Halmashauri ya Arusha wakipokea msaada wa Fedha Tsh. Milioni Tano kutoka kwa Ndg. Joel Nathaniel Sasali ambaye ni Operesheni Meneja wa Kampuni ya Usafirishaji ya Dar Lux akiwa ameambatana na baadhi ya watumishi wa kampuni hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Akipokea Vyoo Ishirini kutoka kwa Mdau wa maendeleo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa choo cha wananfuzni wa shule ya msingi Seliani kilichotitia .
Mwakilishi wa Chama cha Mapinduzi akikabidhi mchango wa ujenzi wa choo kilichotitia kwa Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro.

Shirika la SBFIC kuwajengea uwezo watanzania kuhusu huduma za kifedha

0
0



Na George Binagi-GB Pazzo

Shirika la “Savings Banks Foundation for International Coorperation- SBFIC” lenye makao yake makuu nchini Ujerumani, limefungua rasmi ofisi yake nchini Tanzania lengo likiwa ni kufikisha karibu huduma zake  kwa watanzania.

Hafla ya uzinduzi wa ofisi hiyo ilifanyika Novemba Mosi 2018 katika eneo la Bwiru Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, yalipo makao makuu ya shirika hilo hapa nchini huku makao makuu ya Afrika Mashariki yakiwa Kigali nchini Rwanda.

Mkurugenzi wa shirika hilo hapa nchini, Stephen Noel Safe alisema limejikita kuwajengea uwezo wananchi pamoja na watoa huduma za kifedha kutekeleza miradi endelevu ili kutambua umuhimu na matumizi sahihi ya mikopo pamoja na kujiwekea akiba hususani kwa taasisi ndogondogo ikiwemo Vicoba.

Mgeni rasmi, Mtendaji Mkuu shirika la SBFIC, Dkt. Christoph Gogler kutoka nchini Ujerumani alisema huduma za shirika hilo zimewafikia wanufaika zaidi ya 2000 kwa njia mbalimbali ikiwemo mafunzo lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kuendeleza miradi yao kupitia huduma za kifedha ikiwemo mikopo na kujiwekea akiba.


Mkurugenzi wa shirika la SBFIC hapa nchini, Stephen Noel Safe akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mtendaji Mkuu shirika la SBFIC, Dkt. Christoph Gogler akizungumza kwenye hafla hiyo.
Steven Revelian amnaye ni Mtendaji Mkuu mradi wa KARUDECA kutoka mkoani Kagera akiwasilisha salamu zake kwenye hafla hiyo.

PROF MKUMBO AONGOZA ZOEZI LA KUHAKIKI MITA ZA MAJI KWA WATEJA WA DAWASA

0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo ameendesha zoezi la kusoma na kuhakiki mita za maji kwa wateja wakubwa na wadogo. 

Zoezi hilo liloandaliwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani (DAWASA) ni la siku moja lenye lengo la kuwezesha mamlaka kuwa na taarifa za wateja na kuhakiki usalama na ubora wa mita. 

Usomaji na uhakiki wa mita hizo za wateja utakuwa ni kwa Mkoa wote wa Dar es salaam, Pwani ikiwemo Kibaha na Bagamoyo na litaendeshwa na wafanyakazi wa DAWASA.Profesa Mkumbo amesema kuwa, zoezi hilo litamsaidia Mteja kufahamu kiasi cha maji anachotumia pia itapunguza upotevu wa maji na kupelekea hasara mamlaka.

Mbali na hilo, amesema kuwa zoezi hili litasaidia Mamlaka kupata njia za kudhibiti upotevu wa maji kama Waziri alivyowaagiza kuhakikisha wanapunguza na kushiriki kwake ni katika kuunga mkono jitihada za DAWASA .Mkumbo amewapongeza DAWASA kwa kuweka mita nzuri na zingine zikiwa mpya kabisa na zinafanya kazi vizuri na hata wateja aliokutana nao wameonesha kupendezwa na huduma za mamlaka hiyo katika utoaji wa maji safi na salama. 

Meneja wa DAWASA Ubungo Mponjoli Damson amesema kuwa zoezi hili limekuwa na tija kubwa sana na kwa mwenendo huu wanaweza kubaini wateja wanaotumia maji kwa wingi na hata wale wanaoiba maji na wameweza pia kuona mivujo na kuweza kuiziba. Kwa upande wa Tanesco mhandisi Laura Hyera amesema kuwa DAWASA wanafanya jambo zuri sana kuja kusoma mita hizi mara kwa mara, inasaidia kumpa mteja au mtumiaji wa maji kujua kiasi anachokitumia. 

Hyera amesema anawapongeza sana kwa hatua hiyo itajenga uaminifu kwa wateja wa DAWASA kulipa maji kwa wakati na kuzuia wizi wa maji. Profesa Mkumbo ametembelea wateja wakubwa akiwemo Tanesco na kusoma mita mbili zilizopo pale na kuhakiki ubora wake, wateja wadogo wa eneo la Changanyikeni na kufurahishwa na utendaji kazi wa DAWASA.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo akijaza fomu ya maji baada ya kusoma mita ya mteja wakati wa zoezi la kusoma na kuhakiki mita za maji kwa wateja wakubwa na wadogo akiwa ameambatana naMeneja wa DAWASA Ubungo Mponjoli Damson leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo akijaza fomu ya maji baada ya kusoma mita ya mteja wakati wa zoezi la kusoma na kuhakiki mita za maji kwa wateja wakubwa na wadogo akiwa ameambatana naMeneja wa DAWASA Ubungo Mponjoli Damson leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo akisoma mita ya mteja wakati wa zoezi la kusoma na kuhakiki mita za maji kwa wateja wakubwa na wadogo akiwa ameambatana naMeneja wa DAWASA Ubungo Mponjoli Damson leo Jijini Dar es Salaam. 
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images