Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109941 articles
Browse latest View live

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


TAARIFA YA HABARI SAA MBILI KAMILI USIKU ITV NOVEMBA 01, 2018

MAHAKAMA YAAMBIWA FREEMAN MBOWE MGONJWA, APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU YA MOYO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Freeman Mbowe anayekabiliwa na kesi ya Uchochezi namba 112 ya mwaka huu amesafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini akiwa mahututi kwa ajili ya matibabu ya moyo na shinikizo la damu.

Hayo yameelezwe leo Novemba Mosi mwaka huu na Wakili Peter Kibatala mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali, (PH).

Wakili Kibatala ameieleza Mahakama kuwa alimuhoji mdhamini wa Mbowe, Grays Celestine na akamueleza kuwa Mbowe amesafirishwa jana jioni akiwa mahututi kuelekea Afrika Kusini na nyaraka za usafiri na matibabu zitawasilishwa kwa barua mahakamani.

Kibatala alieleza kuwa Mbowe amekuwa akifika mahakamani mara kadhaa bila kukosa, hivyo adhabu kwamba kueleza anaidharau mahakama kwani hata kitendo cha kumtuma mdhamini wake si jambo la dharau.Kutokana na taarifa hiyo, Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi ameiomba Mahakama itoe amri ya kumkamata mara moja Mbowe ili ajieleze kwani dhamana aliyopewa na mahakama isifutwe kwa kushindwa kuiheshimu.

Baada ya mdhamini huyo kueleza hayo, Hakimu Mashauri alimuuliza kama ana nyaraka ya kuithibitishia mahakama kuwa Mbowe amesafiri nje ya nchi kwa Matibabu lakini mdhamini huyo alidai kuwa hana na kwamba mshtakiwa akirejea atawasilisha nyaraka za safari na Matibabu kwa mahakama na upande wa mashtaka. 

TCRA YATANGAZA KUWACHUKULIA HATUA WAVUNJIFU WA MAADILI KATIKA MITANDAO

$
0
0
Na Khadija Seif,Globu ya jamii

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) imesema haitasita kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote wanaopotosha jamii na vitendo vya uvunjifu wa maadili ya kitanzania kwa kujirekodi na kisha kusambaza picha za video za utupu mtandaoni.

Akizungumza leo Dar es salaam Mkurugenzi wa TCRA Joannes Karungura amesema kutokana na video inayosambaa kwa sasa nchini ikimuhisha msanii wa filamu nchini Wema Sepetu imeamua kumfikisha mahakamani ili asomewe shtaka linalomkabili na kwamba huo ni mwanzo tu kwani wote ambao wanaokiuka maadili mitandaoni watachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha Karungura amebainisha kuwa sheria zitaendelea kufuatwa na kwa yoyote atakayekiuka maadili ya kitanzania kama alivofanya Wema 
Sepetu na wengine ambao kesi zao ziko Kwenye taratibu kufikishwa 
mahakamani basi watatumikia kifungo cha miaka Saba au kutoa faini 
ya Sh.millioni saba.

Ametoa mwito kwa Watanzania kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha jamii yetu inakua na maadili,tabia njema pamoja na desturi nzuri ili kukijenga kikazi cha kesho na vinavokuwa maadili mazuri na hofu ya kutokufanya vitendo viovu.

Pia amewataka watu wenye picha pamoja na video chafu kufuta mara 
moja kwani TCRA wana mikakati mizito kwa watu ambao wanahifadhi 
pamoja na wanaosambaza picha hizo kuwafikisha Kwenye sheria 
ichukue mkondo wake.

DC Katambi atinga Stesheni ya Dodoma, Atishia Kuwatumbua

$
0
0
Charles James

MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi ametishia kuwatumbua watumishi wa Stesheni ya Treni endapo hawatotekeleza maagizo maagizo yake.

DC Katambi ametoa kauli hiyo leo alipofika katika stesheni hiyo baada ya kupigiwa simu na abiria waliokua wamekwama tangu jana kufuatia treni mbili kukutana.

Mkuu huyo wa Wilaya pamoja na kuzungumza na abiria hao ambao aliwaomba kutulia huku akiuagiza uongozi wa Reli kuwatafutia usafiri mwingine wa kuwapeleka jijini Dar es Salaam pia alikagua mazingira ya stesheni hiyo kutokana na kulalamikiwa na wasafiri hao.

“ Nimepita kukagua mazingira ya stesheni yetu, nimekutana na mambo mengi ya hovyo ambayo yanaweza kutatulika ili kuondoa kero za abiria wetu ambao kimsingi ni Watanzania wenzetu ambao wanalipa kodi ya Nchi yao kwa kulipa nauli.

“ Stesheni kubwa kama hii haina vyoo vya kutosha na vilivyopo vimeziba kutokana na wingi wa vinyesi, maji hakuna pia kwa sababu stesheni inadaiwa na nimewaagiza kulipa deni wanalodaiwa. Na wasipotekeleza basi wajue nitawatumbua,” amesema DC Katambi.
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi

WALIOMALIZA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI WAHAMASISHWA KUCHANGIA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA CHUO HICO

$
0
0

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini 

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) wanaoishi katika hosteli za nje ya chuo hicho wako kwenye mazingira hatarishi kutokana na baadhi yao kufanyiwa vitendo vya kinyama huku ikidaiwa wengine tayari wamepoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.

Matukio mengine yanayotajwa kuwafika Wanafunzi hao ni pamoja na kuvamiwa na kuporwa mali ,kujeruhiwa kwa kuchomwa visu na kupigwa hasa kwa wanafunzi wa jinsia ya Kike jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limechangia baadhi yao kuathirika kimasomo na hata kupunguza hali ya kuendelea na masomo.

Kutokana na hali hiyo, Wahitimu wa Chuo hicho kuanzia mwaka 1963 wameanza kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa hosteli yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1000 ili kupunguza changamoto zilizopo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Harambee hiyo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira amesema miundombinu ya Chuo kikuu cha Ushirika Moshi haikidhi mahitaji ya sasa na ya baadae kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kwamba kwa kiasi kikubwa inahitaji kuboreshwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akizungumza wakati wa uzinduzi wa Harambee ya kuchangia ujenzi wa miundombinu katika Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) .
 Baadhi ya Watumishi wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira wakati wa uzinduzi ya kuchanga ujenzi wa Miundombinu ikiwemo Hosteli katika chuo hicho. 
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika,Moshi (MoCU) Prof,Faustine Bee akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katik aukumbi wa mikutano wa Ushirika . 
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa Harambee ya kuchangia ujenzi wa miundombinu katika chuo hicho.



ZIARA YA NAIBU WAZIRI DKT FAUSTINE NDUGULILE KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA

DC AJITOSA KUHAMASISHA UHIFADHI WA MAZINGIRA WILAYANI NAMTUMBO

$
0
0
MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo ameamua kufanya ziara katika Kata za Rwinga na Namtumbo kwa ajili ya kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kusikiliza kero za wananchi.

Kizigo amefanya ziara hiyo jana ambapo amepata nafasi ya kuelezwa baadhi ya kero za idara ya maji na mazingira ya mji wa Namtumbo (NAUWASA) kutoza flat rate ya Sh.7,000 kila mwezi kwa wananchi kulipia maji, wakati maji yanatoka mara moja kwa wiki inayosababisha maji kutoka mara nne kwa mwezi.

Taarifa ya ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ambayo imetolewa kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa Mkuu wa idara ya maji alitoa majibu kwamba wanatoza 7000 flat rate kwasababu hakuna mita za maji katika baadhi ya maeneo.Hata hivyo Mkuu wa wilaya ameiagiza idara ya maji iwaandikie EWURA  kuomba kupewa mita za maji haraka ili wananchi walipe kwa haki kutokana na maji wanayoyatumia kwani sio haki kuwalipisha Sh.7000 kwa kuchota maji mara nne tu kwa mwezi tena kwa uchache.

Pia wananchi walitoa malalamiko yao kwa Mkuu wa Wilaya huyo kuwa katika kituo cha afya Namtumbo kuna wakati dawa hawapati na 
wanaambiwa wakanunue kwenye maduka ya dawa. Pia hakuna huduma za haraka kwani watendaji wa kituo cha afya wanachukua muda mrefu kuingiza taarifa kwenye komputa badala ya kuhudumia mgonjwa.

Hivyo Kizigo amemuagiza Mganga Mkuu wa wilaya ahakikishe kabla dawa hazijaisha kabisa awe ameshaagiza zingine ili ziwepo wakati wote. Lakini pia ahakikishe anaagiza dawa zinazotosha kata mbili (Rwinga na Namtumbo) kwani ni dhahiri kituo kinazidiwa na idadi ya wagonjwa kwani kinahudumia kata mbili badala ya moja.

Kuhusu matumizi ya kompyuta amemuagiza Mganga Mkuu wa wilaya ahakikishe mafunzo kwa vitendo yanatolewa na kufanyika ili kuongeza kasi ya watumishi kuhudumia watu kwa kutumia kompyuta kwani bado hawajazizoea katika kufanya kazi zao. Pia wakati huohuo kama kuna 
mgonjwa amezidiwa waweke kipaumbele katika kumhudumia hata 
kama hawajamaliza kuingiza taarifa kwenye kompyuta.
MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo akizungumza na Wakazi wa Kata za Rwinga na Namtumbo,alipofanya ziara yake  kwa ajili ya kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kusikiliza kero za wananchi.Kizigo amefanya ziara hiyo jana ambapo amepata nafasi ya kuelezwa baadhi ya kero za idara ya maji na mazingira ya mji wa Namtumbo (NAUWASA) kutoza flat rate ya Sh.7,000 kila mwezi kwa wananchi kulipia maji, wakati maji yanatoka mara moja kwa wiki inayosababisha maji kutoka mara nne kwa mwezi.
 Wananchi wakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo . 

SERIKALI YATOA BILIONI 21 UJENZI MIUNDOMBINU MTWARA

$
0
0
Na Evaristy Masuha – Mtwara 

Serikali kupitia mradi wa uendelezaji miji Mkakati (Tanzania Strategic Cities Project) imetoa bilioni 21.7 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimblai ya maendeleo katika Manispaa ya Mtwara mikindani. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara 4 za mitaa kwa kiwango cha lami, Ujenzi wa maeneo matatu ya kupumzikia (Recreation Center), mfereji mkubwa wa kuondoa maji ya mvua, ujenzi wa soko la kisasa pamoja na kituo cha daladala eneo la Mikindani. 

Akizungumza leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda amesema fedha hizo zimetolewa kwa mkopo na Benki ya dunia na kwamba ujenzi wa miradi hiyo yote inatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2019. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutaufanya mji wa mtwara kuwa na muonekano mzuri na kwamba hiyo ndiyo hatua nzuri kuifanya Manispaa kuwa na sifa ya kuwa Jiji. “Naamini baada ya kukamilika miradi hii Mtwara itakuwa sehemu nyingine na pengine inaweza kupata sifa ya kuelekea kuwa jiji”. Amewataka vijana waliopata nafasi ya kuajiliwa katika ujenzi wa miundombinu hiyo kuwa waamifu ili kujijengea imani kwa waajiri. 

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa (mwenye shati Jeupe) akikagua ujenzi wa mfereji wa maji kutoka Skoya, Nabwaba, Shakuru hadi Mtepwezi.
Mfereji wa kuondoa maji kutoka Skoya, Nabwada Shakuru hadi Mtepwezi

Ujenzi wa soko la Chuno 

 

CCM NYAMAGANA YAWATIMUA MAKATIBU WAWILI KWA UDHALILISHAJI

$
0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana kimewavua uongozi Makatibu wa Siasa na Uenezi wa kata za Buhongwa na Mkolani wilayani humo kwa tuhuma na makosa ya kukidhalilisha na kukichafua kwenye jamii.

Pia kimelaani matukio hayo yaliyofanywa na viongozi hao wasio na hofu ya Mungu,katiba na sheria za nchi ambao wanakiangusha CCM kwa kufanya vitendo viovu na mambo ya ovyo yanayodhalilisha.

Akitoa tamko la kuwavua nyadhifa za uongozi makatibu hao wa Uenezi kwenye mkutano wa dharura wa Kamati ya Siasa ya Wilaya mbele ya vyombo vya habari Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Salum Kalli alisema viongozi wa namna hiyo hawatavulimiwa kwa sababu wanafedhehesha chama.

“CCM inalaani vikali mambo yaliyofanywa na viongozi hao kwenye jamii na hatua hii itakuwa fundisho kwa viongozi wenye tabia kama hizo,maana si utamaduni na maadili ya CCM kwani inawataka wawe waadilifu na waaminifu kwenye nafasi zao.Hivyo tutafuatilia tabia, mienendo na maadili ya kila kiongozi wa CCM aliyepo madarakani,”alisema.

Kalli alieleza kuwa Kamati ya Siasa ya Wilaya imechukua hatua hiyo na kutoa tamko hilo Watanzania wajue ili viongozi wenye tabia chafu zisizofaa kwenye jamii waache kwa kuwa CCM haitawavumilia.

Alifafanua kuwa Katibu wa Siasa na Uenezi wa Kata ya Buhongwa Hassani Bushagama, anadaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha tatu wa shule moja ambayo haikutajwa ambapo alitoroka na kutokomea tangu Julai mwaka huu.
Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Salum Kallia akisoma tamko la kuwavua uongozi makatibu wa Siasa na Uenezi wa kata za Buhongwa na Mkolani, Hassani Bushagama na Zephelin Maiko Shibugulu, mbele ya wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu wilayani Nyamagana jana.
Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Salum Kallia akisoma tamko la kuwavua uongozi makatibu wa Siasa na Uenezi wa kata za Buhongwa na Mkolani, Hassani Bushagama na Zephelin Maiko Shibugulu, mbele ya wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu wilayani Nyamagana jana.waliokaa mbele kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Zebedayo Athuman, Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire na wa kwanza kulia ni Katibu wa Siasa na Uenezi Musptapha Banigwa
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athuman akifungua kikao kazi cha kamati ya siasa ya wilaya hiyo jana, kushoto ni Katibu wa Chama wilayani humo Salum Kalli na kutoka kulia wa kwanza ni Katibu wa Siasa na Uenezi Mustapha Banigwa na Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athuman akifungua kikao kazi cha kamati ya siasa ya wilaya hiyo jana, kushoto ni Katibu wa Chama wilayani humo Salum Kalli na kutoka kulia wa kwanza ni Katibu wa Siasa na Uenezi Mustapha Banigwa na Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire. Picha na Baltazar Mashaka.

LUGOLA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA VITUO VYA POLISI TABATA,BUGURUNI NA KUTOA MAAGIZO YA DHAMANA KUTOLEWE SAA 24

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amefanya ziara ya kushtukiza kituo cha Polisi Tabata na Buguruni vya jijini Dar es Salaam ili kujua kama maagizo yake aliyoyatoa katika vituo mbalimbali kama yameanza kufanyiwa kazi.

Waziri Lugola alianza ziara yake saa 2:45 asubuhi kwa kuibukia katika kituo cha Tabata na moja kwa moja alianza kuulizia mahudhurio ya wafanyakazi wote wa kituo hicho na kujua nani yupo kazini na nani hayupo na kwanini hajafika ofisini hapo kwa muda huo wa asubuhi.

Wakati alipokua kituoni hapo, pia Lugola alikichukua kitabu cha taarifa za watuhumiwa wote waliopo mahabusu na baadaye kuelekea katika mahabusu hiyo akiwahoji watuhumiwa kwa kuwaita kwa majina kujua makosa yao yaliyoyafanya wawepo kituoni hapo.

Lugola baada ya kumaliza katika kituo hicho, saa 5:27 alielekea kimyakimya katika kituo cha Polisi cha Buguruni, na aliwahoji watuhumiwa waliopo mahabusu katika kituo hicho na kujua makosa mbalimbali yanayowakabili huku polisi wapepelezi wa tuhuma zao wakiwepo katika tukio hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiingia Kituo cha Polisi Tabata, jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha polisi hicho kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi nchini. Pia Lugola alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha polisi Buguruni jijini humo leo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiwaita majina watuhumiwa (hawapo pichani) waliopo katika mahabusu ya Kituo cha Polisi cha Tabata, jijini Dar es Salaam, leo, ili kujua aina ya makosa waliotuhumiwa pamoja na kujua muda waliokaa katika kituo hicho endapo imefika zaidi ya saa 24 bila kupewa dhamana. Pia Lugola alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha polisi Buguruni jijini humo leo. Lengo la ziara hiyo ni kuboresha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi nchini
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuhoji Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Tabata, jijini Dar es Salaam, Bakari Gothi (watatu kushoto) kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi katika kituo chake, mara baada ya Waziri huyo kufanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo. Pia Lugola alifanya ziara kama hiyo katika Kituo cha Polisi Buguruni jijini humo. Lugola anafanya ziara ya kushtukiza katika vituo mbalimbali nchini kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akionyeshwa taarifa za watuhumiwa waliopo mahabusu ya Kituo cha Polisi cha Buguruni, jijini Dar es Salaam, leo, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo hicho kwa lengo la kufuatilia utendaji kazi. Pia Lugola katika siku hiyo hiyo alifanya ziara ya aina hiyo katika kituo cha polisi Tabata, jijini humo. Kulia ni Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi Buguruni, Adam Maro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni, mara baada ya Waziri huyo kumaliza ziara yake ya kushtukiza katika Kituo cha Polisi cha Tabata na Buguruni jijini Dar es Salaam, leo. Lugola alisema lengo la ziara hiyo ni kuboresha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi nchini. Kushoto ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Buguruni, Adam Maro. 
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

MAWAKALA WA NMB WAPEWA SEMINA KUONGEZA UFANISI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA

$
0
0
BENKI ya NMB imetoa semina kwa mawakala wake wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuboresha huduma na ufanisi kwa wateja wa NMB wanaojipatia huduma za kibenki kwa mawakala hao.

Akizungumza katika semina hiyo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd alisema semina hizo ni mwendelezo wa mafunzo kwa mawakala wa NMB nchi nzima ili kuboresha huduma, kukuza biashara zao na kuleta ufanisi katika kumuhudumia mteja.

Alisema NMB ndio benki pekee yenye idadi kubwa ya mawakala zaidi ya 6,000 ambao hutoa huduma nchi nzima huku ikiwa na matawi 228 na mashine za ATM zaidi 800 lengo likiwa kusogeza huduma kwa wateja wake.Mafunzo haya yanaenda sambamba na kuwapongeza mawakala waliofanya vizuri kwa mwaka huu katika kazi zao, ili kuleta chachu kwa wengine kufanya vizuri zaidi.

Akiwasilisha mada za mafunzo kwa mawakala, Meneja Mwandamizi NMB Wakala, Tito Mangesho alisema mikakati ya NMB ni kuongeza idadi ya wateja huku ikitumia njia rahisi na salama ya kuwahudumia watanzania. Alisema malengo mengine ni pamoja na kuongeza unafuu wa gharama zake na uharaka wa kuwahudumia wateja, kupunguza msongamano na kuboresha kamisheni kwa mawakala wake.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (kulia) akimkabidhi cheti pamoja na zawaadi wakala bora kwa mwaka 2018 Kandaa yaa Dar es Salaam kwenye semina kwa mawakala wake wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Meza kuu kwenye semina kwa mawakala wa Benki ya NMB wa jijini Dar es Salaam ikipiga picha ya pamoja na mawakala bora kwa mwaka 2018 wa Benki hiyo kwa kanda ya Dar es Salaam.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd akizungumza na mawakala wa NMB kwenye semina kwa mawakala wa Benki hiyo wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Sehemu ya mawakala wa NMB waliohudhuria semina hiyo wakionesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa.

KUTAKUWA NA MECHI KALI KATI YA WASANII WA BONGOFLAVA V/S LIFE CLUB FC

FAHAMU: Utamu wa muziki wa "Disco" na ulikotokea, Dj John Dillinga afunguka

NEWZ ALERT:TRENI inayotoa huduma za usafiri kati ya Stesheni ya Dar es Salaam na Pugu Stesheni yapata ajali.

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

TRENI inayotoa huduma za usafiri kati ya Stesheni ya Dar es Salaam na Pugu Stesheni imepata ajali leo Novemba 2,2018 eneo  la Karakata baada ya behewa mbili kuanguka.

Kwa mujibu baadhi ya abiria waliokuwa kwenye treni hiyo wamesema ajali hiyo imetokea leo kwenye saa moja kasoro asubuhi ambapo baada ya kufika eneo hilo mabehewa mawili yalipinduka.

Mmoja wa abiria hao aliyejitambulisha kwa  jina la Juma Jebe amesema yeye alikuwa behewa la nne kutoka mabahewa yaliyoanguka na kwamba baada ya tukio hilo kuna baadhi ya abiria walionekana kuzimia kutokana na hofu. Hata hivyo amesema anashukuru kwani hakushuhudia mtu yoyote kuumia. 

Michuzi Blog itaendelea kukujuza kilichosababisha kuanguka kwa mabehewa hayo baada ya mamlaka husika kuzungumzia

MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 2,2018

SHEREHE ZA UHURU WA TANZANIA NA KENYA KUFANYIKA KATIKA JIJI LA LUTON NCHINI UINGEREZA

$
0
0

Jumuiya Kuu ya Watanzania nchini Uingereza inapenda kuwatangazia Watanzania wote na wana Africa Mashariki wanaoishi nchini Uingereza (UNITED KINGDOM) na IRELAND kuwa Sherehe za Uhuru Mwaka huu zitafanyika katika mji wa Luton siku ya Jumamosi tarehe 08/Desemba/ 2018 kuanzia saa mbili Usiku mpaka majogoo

Ifikapo saa sita usiku tutakuwa na tukio maalum litalofanywa na Mgeni rasmi pamoja wasanii maarufu wanaotegemewa kuwepo siku hiyo kukaribisha usiku wa tarehe 09/Desemba,  siku ya tuliyopata Uhuru 

Kutakuwa na kila aina ya vinywaji, nyama choma, chapatti’s, supu na mahanjumati ya kumwaga! 

Anuani ya Ukumbi

Lewsey Farm Learning Centre Executive Hall
92 Tomlinson Avenue
Luton
LU4 0QQ

Tiketi zinapatikana kupitia akaunti maalum ya Jumuiya kwa ajili ya kuadhimisha miaka 57 ya Uhuru

Kiingilio ni £20pp, Meza moja yenye kuchukua watu nane mpaka kumi ni £200, ili kujipatia tiketi yako deposit £20 kwa mtu mmoja au £200 kwa meza kisha Tuma ujumbe kwenda anuani Pepe tzukdiaspora@gmail.com

Akaunti maalum ya Jumuiya

Jina la Akaunti- UHURU
Bank - LLOYDS
Sortcode - 30 99 08
Akaunti No. 23619960

Burudani na sound system nzito itaporomoshwa na DJ DOUBLE T, DJ CHAMBI NA DJ ANDREW 

Hii si ya kukosa kwani kutakuwa na suprises za kumwaga, 

UHURU DAY TUKUTANE LUTON

Imetolewa na Jumuiya Kuu ya Watanzania UK

TZUK DIASPORA

08 DECEMBER 2018.

UMOJA NI NGUVU NA PAMOJA TUNAWEZA

BREAKING NEWZZZZ:AMBAR RUTY, JAMES DELICIOUS WAFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUSAMBAZA PICHA ZA UTUPU MITANDAONI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MCHEZA video Rutyfiya Abubakal a.k.a Amber Ruty , Said Bakari (kijana wake AmberRuty) na kijana  James Charles maarufu kama James Delicious anayedaiwa kuwa shoga wamefikishwa  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka yao kwa kupiga picha za utupu na kusimbaza mitandaoni.

Washitakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo ..endelea kufuatilia Michuzi Blog kupata habari kamili.

 MCHEZA video Rutyfiya Abubakal a.k.a Amber Ruty , Said Bakari (kijana wake AmberRuty) (hayupo pichani) wakiwa kwenye moja ya chumba cha Mahakama mara baada ya kufikishwa   Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka yao kwa kupiga picha za utupu na kusimbaza mitandaoni.
Mshtakiwa AmberRuty wa kwanza kulia anayedaiwa kupiga naye Picha kinyume na maumbile, Said Mtopali pamoja ma James Charles maarufu kama James Delicious wakiwa nje ya chumba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakisubiri kusomewa mashtaka yao.
MCHEZA video Rutyfiya Abubakal a.k.a Amber Ruty , Said Bakari (kijana wake AmberRuty)  pamoja na James Charles maarufu kama James Delicious anayedaiwa kuwa shoga wakielekea kwenye moja ya chumba cha Mahakama mara baada ya kufikishwa   Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka yao kwa kupiga picha za utupu na kusimbaza mitandaoni.
 MCHEZA video Rutyfiya Abubakal a.k.a Amber Ruty , Said Bakari (kijana wake AmberRuty)  wakifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka yao kwa kupiga picha za utupu na kusimbaza mitandaoni.

MKUU WA MKOA WA TABORA AMTEMBELEA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanry (wa pili kushoto) akifurahi jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, walipokutana kwa mazungumzo kwenye Makao Makuu ya Benki ya CRDB, Azikiwe jijini Dar es salaam leo. Wengine pichani ni kutoka kulia, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Martha Geleka, Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Wilaya ya Nzega, Philemon Magesa pamoja na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanry (wa tatu kushoto) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela pamoja na ujumbe wake, walipokutana kwa mazungumzo kwenye Makao Makuu ya Benki ya CRDB, Azikiwe jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akimueleza jambo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanry walipokutana kwa mazungumzo kwenye Makao Makuu ya Benki ya CRDB, Azikiwe jijini Dar es salaam.
picha ya pamoja.

NEWS ALERT: MBUNGE ZITTO KABWE APANDISHWA KIZIMBANI LEO

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kushikiliwa katika kituo cha Polisi kwa siku kadhaa.
 Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, akiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa mashtaka yake yanayomkabili. Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi.
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, akiteta jambo na wakili wake Steven Mwakibolwa, kabla ya kwanza kusomewa kwa kesi hiyo katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Viewing all 109941 articles
Browse latest View live




Latest Images