Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

TCRA YAWATIA KIBANONI WANANE WANAODAIWA KUKIUKA SHERIA ZA MTANDAO KUANZIA JULY -SEPT

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeshawachukulia hatua za kisheria watu nane wanaodaiwa kukiuka sheria za mtandao, ikiwemo kusambaza picha za nusu uchi, video za ngono na kutupia matusi katika kipindi cha Julai -Septemba mwaka huu. 

Aidha jamii imekemea matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na video za ngono kwani kwa kufanya hivyo hawatamuangalia mtu kwa sura ama umaarufu bali sheria itachukua mkondo wake. 

Ofisa mkuu wa mawasiliano kwa umma (TCRA) Semu Mwakyanjala aliwatahadharisha ,watu wasisambaze picha ama video za ngono na kuanzisha tovuti hizo kwani ni kukiuka sheria .

Alieleza kuna faida unapotumia mtandao inarahisisha mawasiliano ,unapunguza gharama ,inaokoa muda ,inatoa elimu na kukuza biashara badala ya kutumia masuala yasiyo na tija.“Kwasasa hatuna masihala, tunashirikiana na jeshi la polisi kubaini wale wanaokaidi kufuata sheria zilizopo “alieleza Mwakyanjala. Aliiomba jamii kutunza vifaa vya kielektronik ili watu waeiibe na kutymia vibaya .

Nae mkuu wa kanda ya Mashariki (TCRA) Lawi Odiero alisema, sheria ya kielektroniki iliyopo inakataza kusambaza ngono na baadhi ya watu wanachukuliwa hatua ya kulipa faini sh. mil tano ama miaka mitatu jela.

Aliwaasa wananchi kwenda kutembelea banda lao kujifunza ili kuelewa sheria zinazowabana ili kuepukana na adhabu. Odiero alieleza wazingatie wasiweke namba za siri kwenye simu ama internet miaka ya kuzaliwa bali watumie maneno mengine kwani sio rahisi kughushi .Akizungumzia ving’amuzi alisema ,serikali kupitia TCRA iliondoa baadhi ya channel kwenye baadhi ya visimbuzi. 

Odiero alifafanua, Azam, Dstv na Zuku huduma wanatoa kwa kulipisha hivyo hawaruhusiwi kubeba channel za ndani. Watumiaji wa internet hadi sasa nchini wapo milioni 22 ,luninga zipo 34 ,vituo vya redio zaidi ya 150 kutoka kituo kimoja kilichokuwepo mwaka 1961.
Mkuu wa kanda ya Mashariki (TCRA) Lawi Odiero akizungumza.kwenye maonyesho hayo 

WAZIRI LUKUVI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU MPYA NA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC)

$
0
0

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimkabidhi ripoti Mapitio ya Muundo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC Dk Sphia Kongela jana jijini Dodoma. 
 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akifurahia jambo wakati alipokutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dk. Maulid Banyani wa kwanza kulia, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC Dk Sophia Kongela wa pili kulia walipokuenda kujitambulisha ofisini kwake Dodoma, wengine kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi Dk Angeline Mabula na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Doroth Mwanyika. 
 
 Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabula akimpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC Dk Sophia Kongela kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kushika nafasi hiyo, alipotembelea ofisi za Wizara ya Ardhi jijini Dodoma. 
 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na Naibu wake Dk Angeline Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi mpya wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC Dk. Sophia Kongela wa pili kulia na Mkurugenzi Mkuu Dk. Maulid Banyani. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Mipango Miji Wizara ya Ardhi Profesa John Lupala wakati akioneshwa ramani ya mji wa Serikali uliopo Dodoma.

MUSOMBA -TPDC KUONGEZA VITUO VYA KUJAZA GESI ASILIA KATIKA MAGARI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli nchini ( TPDC), linatarajia kuongeza vituo 10 hadi 20 kwa Dar es salaam -Mtwara -Lindi, vya kujaza gesi asilia kwenye magari yaliyowekewa mfumo huo ambapo kipo kituo kimoja Ubungo ,kwa miaka kumi sasa ambacho hakikidhi mahitaji. 

Ili kufikia malengo yake ya kuongeza vituo vingi katika maeneo mbalimbali limejipanga kuruhusu na kukubaliana na watu binafsi wenye vituo vya mafuta kuweka gesi kwenye vituo vyao .

Akitembelea maonyesho ya bidhaa za viwandani yanayoendelea viwanja vya sabasaba, Pichandege Kibaha Pwani, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini ( TPDC), Kapuulya Musomba, alisema mwamko wa watumiaji upo vizuri tatizo hakuna vituo mikoani. 

Alieleza mwaka ujao wa fedha wataongeza vituo hivyo na sasa wapo kwenye hatua ya manunuzi. Musomba alisema ,wataanza kuongeza vituo viwili ama vitatu Dar es salaam na kuendelea maeneo mengine, na kusema watatangaza tenda ili wawekezaji na watu binafsi wajitokeze kufanikisha hilo. 

"Gesi asilia ikitumika kwenye magari inaweza kupunguza zaidi ya nusu ya gharama mafuta na kuleta unafuu katika sekta ya usafirishaji nchini,Hata hivyo alitaja mpango mwingine ni kuwafikia wananchi 120,000 ambao watafaidika na raslimali ya gesi lakini wanakwenda kwa awamu kulingana na fedha wanayoipata. 

"Gesi kwa ajili ya majumbani tumeanza Dar es salaam na Mtwara, na kuhusu viwandani tumeshaanza Pwani, Dar es salaam na Mtwara kwa njia ya mabomba "Musomba alielezea,mwaka huu wa fedha kufikia 2019 watapeleka Kibaha kwa mitungi kwa kuwa mabomba hayajafika kwa kujazia Dar es salaam kisha kuwafikishia wananchi. 

Alifafanua kwa wale wa mikoa mingine wameshaanza utafiti wa kina kuona kama watoa bomba Dar es salaam, Kibaha, Bagamoyo, Chalinze, Tanga litembee kwenye mikoa kama nane na kwa kushirikiana na wadau watafikia lengo hilo. Nae Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alisema ,wakati ujenzi wa bandari mpya Bagamoyo ukianza watahitaji gesi kutokana na ujenzi kuambatana na viwanda vingi. 

Ndikilo alibainisha awamu ya kwanza ya ujenzi huo utaendana na ujenzi wa viwanda 190 ambapo awamu ya pili utakuwa na takriban viwanda 1,000 hivyo gesi itahitajika pia. 
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini ( TPDC),  Kapuulya Musomba, (wa kwanza kulia) akieleza jambo. (picha na Mwamvua Mwinyi) 

EALA SWEARS IN NEW EX-OFFICIOMEMBER

$
0
0
East African Legislative Assembly, Arusha, Tanzania: 

The new Deputy Minister for Foreign Affairs and East African Co-operation, United Republic of Tanzania, Hon Dr Damas Ndumbaro, this afternoon took Oath of Allegiance as an Ex-OfficioMember of the Assembly.

Hon Dr Ndumbaro was sworn in by the Clerk to the Assembly at a brief ceremony witnessed by the Speaker and Members of EALA in line with the Rule 5 of the Rules and Procedures of the Assembly. The Rule 5(4) of the Rules of Procedure says in part that: “No Member can sit or participate in the proceedings of the House until the Oath or Affirmation of Allegiance to the Treaty is taken”.

Rule 5(5) specifically states that “when a Member first attends to take his or her seat other than at the first Sitting of a new House, he or she shall be brought to the table by two Members and presented by them to the Speaker who shall then administer the Oath or Affirmation of Allegiance”.

Hon Dr Ndumbaro was ushered in to the House by EALA Members, Hon Simon Mbugua, Hon Pamela Massaay and Hon Dr Ngwaru Maghembe. EALA Speaker, Rt Hon Ngoga Karoli Martin congratulated Hon Dr Ndumbaro upon his swearing in – as he assumes his ex-officio role in the regional August House. 
The Deputy Minister for Foreign Affairs and EAC, United Republic of Tanzania, Hon Dr Damas D. Ndumbaro takes the oath of allegiance to the House, flanked in background by Hon Dr Ngwaru Maghembe and Hon Simon Mbugua (right)


The EALA Speaker, Rt Hon Ngoga Karoli Martin congratulates Dr Damas Ndumbaro, who joins the bench as an ex-officio Member of EALA 
A Section of the House pay attention as EALA proceedings continue 


The Deputy Minister for Foreign Affairs and EAC, United Republic of Tanzania, Hon Dr Damas D. Ndumbaro (left) is led to the House by Hon Dr Ngwaru Maghembe, Hon Pamela Massaay and Hon Simon Mbugua(partially hidden).

MKUTANO WA MAJAJI WAKUU NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA WAFANYIKA MJINI LILONGWE NCHINI MALAWI

$
0
0
Pichani kulia ni Mheshimiwa Jaji Mkuu Prof Ibrahim Hamis Juma akiwa sambamba na Mheshimiwa Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Othman Chande (kushoto) walipokwenda kumtembelea mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi Ben Mashiba nyumbani kwake jana jijini Blantyre,nchini Malawi.
Majaji wakuu nchi za kusini mwa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja,wakati wa Mkutano wao Mjini Lilongwe nchini Malawi

REGIONAL FARMERS FEDERATION MEET EALA SPEAKER, PUSH FOR INCREASED FUNDING FOR SECTOR

$
0
0
East African Legislative Assembly, Arusha, Tanzania: 30thOctober, 2018: Small scale farmers under the aegis of the East and Southern Africa Small Scale Farmers Forum (ESAFF) are set to petition the EAC Heads of State to galvanize for increased financing for agricultural sector in the EAC region to ensure food security, reduce poverty and increase public awareness on the Comprehensive Africa Agriculture Development Programme (CAADP). This morning, officials of the ESAFF paid a courtesy call on Rt Hon Ngoga Karoli Martin, Speaker of EALA, in Arusha and made a plea for the petition, when ready, to be forwarded for the attention of the Summit of EAC Heads of State. 

Rt Hon Ngoga assured the ESAFF officials of the Assembly’s support towards initiatives that leverage agriculture to ensure food security and raise the region’s GDP. He pledged to work closely with the EAC Council of Ministers and the EAC Secretary General to ensure the petition, once done by ESAFF is given attention and channeled appropriately to the EAC Heads of State. Rt Hon Ngoga further said time was ripe for the establishment of an institution dealing specifically with matters of agriculture and food security. The Speaker noted that the Assembly would champion Partner States to set aside public spending for agriculture at 10% as envisaged under the Malabo Declaration. 

Speaking on behalf of the Forum, Mr Alfayo Kurunah, a farmer from Kenya and board Member of ESAFF reiterated his organization was keen to collaborate with EALA in organizing a high-level meeting to deliberate on the status of commitment by Partner States in achieving the commitments under the Malabo Declaration. According to Mr Kurunah, the meeting which is expected to bring together Ministers for Agriculture and Ministers for Finance from the Partner States, as well as legislators from the National Legislatures and EALA would lead to a regional position on the progressive implementation of the Malabo goals reflected to national budgets 

“We hope that this meeting would take place in the coming sitting of EALA in November or December 2018 and that the review will be done during the next agriculture summit in May 2019”, Mr Kurunah said. 

The Malabo declaration of June 2014, hopes to accelerate agricultural growth and transformation. It among other things calls for commitment to ending hunger by 2025 by at least double productivity while focusing on inputs, irrigation and mechanization. 
EALA Speaker admires a memento as Ms Rachel Muyoboke representing ESAFF, Rwanda and Hon Mathias Kasamba, Chair of the EALA Agriculture, Tourism and Natural Resources (ATNR) look on. 
The ESAFF delegation in talks with the EALA Speaker, Rt Hon Ngoga Karoli Martin earlier today. 
Mr Alfayo Kurunah, ESAFF Board Member, Kenya (left) addresses as Hakim Baliraine, ESAFF, Uganda and Richard Kipara from Muungano wa Vikundi vya Wakulima Wadogo (MVIWATA), Tanzania look on. ESAFF Board officials today paid a courtesy call on the EALA Speaker, Rt hon Ngoga Karoli Martin.
EALA Speaker, Rt Hon Ngoga Karoli Martin (centre) in dark suit with representatives of the East Africa Small Scale farmers Forum who paid him a courtesy call this morning in Arusha.


TRAFIKI WAOMBA RUSHWA WASHTAKIWA KWA WAZIRI MKUU

$
0
0
*Waziri Mkuu akabidhi majina hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga kwa hatua

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela orodha ya matrafiki wanaodaiwa kuwaomba rushwa madereva wa noah wilayani Lushoto.

Majina ya trafiki hao wanadaiwa kuomba rushwa kwa madereva wa noah wanaofanya kazi ya kusafirisha abiria ndani ya wilaya hiyo yaliwasilishwa kwa Waziri Mkuu kupitia mabango.

Waziri Mkuu alimkabidhi majina hayo jana jioni (Jumatano, Oktoba 31, 2018) baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Sabasaba, Lushoto mjini.

Baada ya kumkabidhi majina hayo alimuagiza afanye uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazowakabili askari hao na kisha awasilishe taarifa kwake leo Alhamisi Novemba 1, 2018.

Mbali ya wananchi kuwasilisha malalamiko hayo, Pia mbunge wa Lushoto, Shaaban Shekilindi alimuomba Waziri Mkuu awasaidie kutatua kero hiyo inayowakabili wananchi.

Awali, Waziri Mkuu alizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Lushoto katika ukumbi wa chuo cha Mahakama Lushoto ambapo aliwasisitiza wafanye kazi kwa bidii.

Alisema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haina msamaha na mtumishi wa umma asiyetaka kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia weledi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa CCM  Sabasaba uliopo Lushoto, Oktoba 31, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa Lushoto wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa  hadhara kwenye uwanja wa CCM Sabasaba akiwa  katika ziara ya mkoa wa Tanga Oktoba 31, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU SPIKA AKUTANA NA TIMU YA MBEYA CITY FC JIJINI DODOMA

$
0
0
 Naibu Spika wa Bunge Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Wachezaji pamoja na Viongozi wa Timu ya Mbeya City FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara walipotembelea Bungeni kwa ajili Ziara ya Mafunzo hii leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. 
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mbeya James Kasusura akifafanua jambo mbele ya Naibu Spika wa Bunge Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa katika Ziara ya Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Mbeya City FC walipotembelea Bungeni kwa ajili ya Ziara ya Mafunzo hii leo Jijini Dodoma. 
Naibu Spika wa Bunge Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Mbeya City FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara walipotembelea Bungeni kwa ajili ya kufanya Ziara ya Mafunzo hii leo Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)

KAMATI ZA BUNGE ZAFANYA VIKAO JIJINI DODOMA

$
0
0
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusu hali ya migogoro ya ardhi Nchini katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Taarifa hiyo iliwasilishwa na Kamishna wa Ardhi Ndugu Mary Makondo
  Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mheshimiwa Nape Nnauye akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kamati hiyo leo ilipokea na kujadili Taarifa ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusu hali ya migogoro ya ardhi Nchini.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angelina Mabula akifafanua hoja mbalimbali za wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati hiyo iliyokutana katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo ilipokea na kujadili Taarifa ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusu hali ya migogoro ya ardhi Nchini.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma wakiwa katika kikao cha kamati kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo leo walipokea na kujadili taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu Uwekezaji katika Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).
 Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Mheshimiwa Richard Ndasa akichangia jambo katika kikao cha kamati hiyo  kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo leo walipokea na kujadili taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu Uwekezaji katika Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Mheshimiwa Raphael Chegeni akifuatilia jambo katika kikao cha kamati hiyo  kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo leo walipokea na kujadili taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu Uwekezaji katika Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).Pembeni yake ni Katibu wa Kamati hiyo Ndugu Amina.
 Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Mazingira na Utafiti kutoka Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)  Ndugu Joseph Kombe akiwasilisha taarifa Kuhusu uhifadhi wa maeneo lindwa pamoja na jitihada za Serikali za kuyahifadhi maeneo hayo mbele ya kikao cha Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Sadiq Murad.

 PICHA NA OFISI YA BUNGE

JUMUIYA ZA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR (ZPC) NA (PPC) ZATEMBELEA MRADI WA MAENDELEO MJINI FUMBA NYAMANZI

$
0
0
 Mkuu wa Kituo cha huduma za Mradi wa maendeleo ya Mji wa Fumba Franco Gohse akiwaeleza Wanajumuiya na Waandishi wa Habari kutoka Zanzibar na Pemba Press Club namna wanavyotunza mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na baadae.
 Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) na Jumuiya ya Waandishi wa Habari Pemba (PPC) watembelea Mradi wa Maendeleo ya Mji wa Fumba Nyamanzi (FTD) kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira.
 Maneja Mauzo wa FTD Fatma Mussa akitowa maelezo kwa Viongozi wa Jumuiya za Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) na (PPC) hawapo pichani,walipotembelea Mradi huo huko Fumba Nyamanzi, kulia kwake ni Franco Gohse na kushoto Muhsini kotoka Mradi wa Maendeleo ya Mji wa Fumba.
 Viongozi wa Jumuiya za Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) na (PPC) wakimsikiliza Meneja Mauzo wa Kampuni ya CPS inayojenga Mji wa Kisasa wa Fumba Nyamanzi. Viongozi hao walitembelea kujifunza mambo mbali mbali kuhusu Mradi huo.
 Msimamizi wa Bustani kutoka Kampuni ya CPS Muhsin Said akitoa maelezo kwa Wanajumuiya na Waandishi wa Habari kutoka ZPC na PPC kuhusu namna wanavyotunza na kuhifadhi mazingira huko Fumba.
 Mkuu wa Kituo cha huduma za Mradi wa maendeleo ya Mji wa Fumba Franco Gohse akiwaeleza Wanajumuiya na Waandishi wa Habari kutoka Zanzibar na Pemba Press Club namna wanavyotunza mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na baadae.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Washindi wa "SHINDA NA SIM ACCOUNT'' ya CRDB Bank

SERIKALI YAMALIZA MGOGORO WA KIWANDA CHAI MPONDE

$
0
0
*Yaagiza mashine zichunguzwe, mitambo yenye hitilafu ikarabatiwe kazi ianze
SERIKALI imemaliza mgogoro uliodumu kwa miaka mingi kati ya wakulima wa chai wa wilaya za Lushoto na Korogwe na kampuni ya Mponde Tea Estate uliosababisha kufungwa kwa kiwanda cha chai cha Mponde baada ya kuagiza kiwanda hicho kianze kazi.

“Waziri Mwijage na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilomo Prof. Siza Tumbo hakikisheni kazi ya kukagua kiwanda na mitambo inafanyika haraka na kubaini mitambo ipi ni mizima na ipi ina hitilafu ili ukarabati ufanyike na kiwanda kianze kazi mara moja.”

Uamuzi huo wa Serikali umetangazwa leo (Alhamisi, Novemba 1, 2018) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kweminyasa kata ya Mponde, wilayani Lushoto baada ya kutembelea kiwanda hicho .

Waziri Mkuu amesema mwaka 1999 Serikali iliamua kuwapa wakulima wa chai na kiwanda hicho  kwa ajili kuwawezesha kuwa na sehemu ya kuchakata chai yao lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi. Imeamua kukirudisha Serikali baada ya kuwepo migogoro iliyoathiri uzalishaji kiwandani hapo.

Kuhusu suala la madeni ya watumishi, ameagiza watafutwe na madai yaorodheshwe kwa ajili ya malipo, amewahakikisha wananchi hao kuwa suala la ajira ambazo zilipotea baada ya kiwanda kufungwa zitarudi kwa sababu Serikali inataka kuona kiwanda kikifanya kazi.

“Serikali imeamua kukichukua kiwanda hiki ambacho awali ilikikabidhi wakulima wa chai na kwamba itahakikisha lengo lake la kuboresh kilimo linafanikiwa na  wakulima wanaendelea kulima zao la chai. Hatutaki kusikia masuala ya Utega wala Mponde hapa si mahali pake.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto Novemba 1, 2018.  Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Novemba 1, 2018. Alikuwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto, Novemba 1, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela na wanne kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Bumbuli wilayani Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Novemba 1, 2018. 
 Wananchi wakimpungia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  alipowasili kwenye kijiji cha Mponde wilayani Lushoto kukagua kiwanda cha chai cha Mponde na kuzungumza na wananchi, Novemba 1, 2018.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WANACHAMA MNIPE KURA KWA WINGI NIKAMALIZIE NILIPOISHIA- IDDY KAJUNA

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MGOMBEA wa nafasi ya .Ukurugenzi wa Bodi ya Klabu ya Simba Iddy Kajuna amesema anahitaji kurejea kwenye nafasi kuu ni kutaka kuendeleza pale apoishia.

Kajuna mpaka sasa ni Kaimu Makamu wa rais wa Klabu y Simba ameweka wazi nia yake kurejea katika uongozi wa Klabu hiyo ili kuendelea pale alipoishia.

Akizungumza wakati wa kampeni za Uchaguzi zinazoendelea katiika Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na Morogoro, Kajuna amesema kuwa amekuwa ndani ya uongozi wa Simba kama Makamu wa Rais na amefanya mambo mengi sana na uamuzi wake wa kuwania nafasi ya Ukurugenzi wa bodi ni kumalizia alipoishia.

Amesema kuwa, mawazo yaliyopo katika Klabu ya Simba anahitaji kuyaendeleza na kufikia malengo ya  Kuwa na uwanja wake, kuwa na kituo cha kukuzia soka vijana pamoja na hosteli za timu.

"Nimekuwa makamu wa rais wa Simba kwa muda kidogo na tumefikia katika hatua nzuri ya kuelekea katika mabadiliko, naomba ridhaa ya wanachama nirejee kwenye Uongozi wa klabu ya Simba ili nikamalizie pale nilipoishia,"amesema Kajuna.

"Tumekuwa na mikutani mingi ya usiku na mingine ikimaizika saa nane usiku, yote ikiwa ni katika kuijenga Simba mpya, Simba ya mabadiliko ya kuingia kwneye mfumo wa hisa na tumefanikiwa katika hilo,"amesema

Kajuna amesema kuwa, mbali na hilo ataweka zaidi ukaribu na wanachama zaidi ya huu aliokuwa nao sasa hivi, ataweka maslahi mbele ya Klabu ya Simba pamoja na kuhakikisha Simba wanapata ushindi kwa hali yoyote ile.

Klabu ya Simba inatarajiwa kufanya uchaguzi wake November 04 ukihusisha nafasi ya mwenyekiti wa klabu na wajumbe watano watakaoingia moja kwa moja kwenye bodi ya wakurugenzi.

Kampeni za Uchaguzi zinaendelea kwa wagombea kunadi sera zao pamoja na mikakati walioiweka ili kuifikisha Simba kuwa moja ya timu Afrika ikiwemo kuchukua Klabu Bingwa Afrika.
Mgonbea wa nafasi ya Ukurugenzi wa Bodi ya Klabu ya Simba Iddy Kajuna alipokuwa anachukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB aendelea na ziara ya kujitambulisha rasmi Viongozi na Taasisi mbalimbali za Serikali

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wiki hii ameendelea na ziara yake ya kutembelea Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Serikali ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kujitambulisha rasmi na  kuboresha mahusiano baina ya Benki ya CRDB na taasisi hizo.

Katika mikutano tofauti iliyofanyika siku ya Jumanne, Jumatano na Alhamisi wiki hii, Nsekela alimtembelea Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Venance Mabeyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, Kamishna Diwani Athumani na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Siang’a.

Pamoja na kufanya utambulisho rasmi kwa viongozi hao, Nsekela ambaye aliambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Ally Laay na Maofisa wengine, alitumia pia nafasi hiyo kuwaelezea viongozi hao juu mikakati yake ya kuipeleka mbele zaidi  Benki ya CRDB na kuomba ushirikiano zaidi wa kibiashara kutoka kwa viongozi hao na taasisi wanazoziongoza.

Kwa upande wao viongozi hao waandamizi, pamoja na kumpongeza Nsekela kwa uteuzi huo mkubwa, walimuahidi kumpa ushirikiano na kumhakikishia kuwa wako tayari kuendelea kuwa wadau wakubwa wa Benki ya CRDB katika mikakati yake ya kibiashara.

Viongozi hao pia walipongeza sana jitahada za Benki ya CRDB katika kusaidia juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, zenye kulenga kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kujenga Tanzania yenye uchumi wa Kati unaoshamirishwa na viwanda.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kulia) pamoja na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, aliyemtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha, tangu alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, Kamishna Diwani Athumani (kulia) akizungumza jambo wakati wa kikao chake na viongozi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (Mwenyekiti), Abdulmajid Nsekela (Mkurugenzi Mtendaji) pamoja na Tully Esther Mwambapa (Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja) ambao walimtembelea kwa lengo la kumtambulisha, Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, Kamishna Diwani Athumani (wa pili kulia) akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Siang’a, akizungumza jambo wakati wa kikao chake na viongozi wa Benki ya CRDB waliomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kumtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kushoto).

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA KONGAMANO LA HALI YA UCHUMI NA SIASA NCHINI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITATU YA UONGOZI WAKE

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alikuwa Mshiriki Maalum, akizungumza na Wageni mbalimbali wakiwemo Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Viongozi wa Kiserikali, Mabalozi kutoka nchi mbalimbali, pamoja na wananchi   waliohudhuria katika Kongamano la Hali ya Uchumi na Siasa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano lililofanyika katika ukumbi wa Nkuruma uliopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 Sehemu ya Watoa Mada wakiwa Wanasikiliza michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa katika Ukumbi wa Nkuruma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wakwanza kushoto ni Profesa Humphrey Moshi, Profesa Kitila Mkumbo, Makamu Mkuu wa Chuo Profesa William Anagisye, Profesa Rwekaza Mukandala, Profesa Martha Qorro pamoja na Profesa Hudson Nkotagu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alikuwa mshiriki Maalum katika Kongamano hilo akiandika baadhi ya Hoja katika Kongamano hilo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alikuwa Mshiriki Maalum akiwa pamoja na washiriki wengine wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Watoa Mada katika Kongamano la Hali ya Uchumi na Siasa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano lililofanyika katika ukumbi wa Nkuruma uliopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Hali ya Uchumi na Siasa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano wakisikiliza kwa makini wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alikuwa mshiriki Maalum alipokuwa akizungumza katika ukumbi wa Nkuruma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliokuwa nje ya Ukumbi wa Nkuruma wakifatilia Kongamano la Hali ya Uchumi na Siasa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa njia ya Luninga wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alikuwa mshiriki Maalum alipokuwa akizungumza katika ukumbi wa Nkuruma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alikuwa mshiriki Maalum katika Kongamano hilo akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Wasichana ya Kisutu mara baada ya kutoka katika Ukumbi wa Nkuruma katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU


KILUWA AFANIKIWA KUWAHAMASISHA WACHINA KUJA NCHINI TANZANIA KUJENGA VIWANDA VITATU MLANDIZI

$
0
0
*Dola za Marekani milioni 100 kutumika katika ujenzi 
*Ahimiza Watanzania kuwa wazalendo kwa nchi yao

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWENYEKITI wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd Mohammed Kiluwa amesema katika kuhakikisha anaunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli za ujenzi wa Tanzania ya viwanda amefanikiwa kuwashawishi wawekezaji kutoka nchini China kuja kujenga viwanda kuwekeza nchini.

Kiluwa amesema kupitia ushawishi wake na kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) wawekezaji hao kutoka China wamekubali kujenga kiwanda cha kuongeza thamani ya bidhaa za ngozi, Kiwanda cha Saa pamoja na Kiwanda cha Simu na kwamba awamu ya kwanza ya uwekezaji huo jumla ya dola za Marekani milioni 100 zitatumika.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu ujio wa wawekezaji hao Kiluwa amesema viwanda hivyo vitajengwa Mlandizi mkoani Pwani na wakati wowote kuanzia sasa baada ya kukamilisha taratibu zote ikiwemo za vibali ujenzi wa viwanda hivyo utaanza mara moja.Pia amesema mbali ya kujengwa kwa viwanda hivyo wawakezaji hao wameonesha nia ya kujenga kiwanda cha kubangua korosho mkoani 

Mtwara na kinachoendelea sasa ni mazungumzo ambayo yanakwenda vizuri na hakuna kitakachoshindikana."Wawekezaji hawa wameonesha nia kujenga kiwanda cha korosho na walikuwa tayari kwenda mkoani Mtwara kuona mazingira." 

Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. John Mathew Mnali akizungumza jambo mbele ya waandishi wa Habari leo jijini Dar kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji wa viwanda,ikiwemo na kuwapokea wageni wa uwekezaji wa viwanda kutoka nchini China na wenyeji wao kutoka kampuni ya Kiluwa Group Ltd.


MWENYEKITI wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd Mohammed Kiluwa (pichani kushoto) akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari leo alipokwenda kuwatambulisha Wadau wake wa Uwekezaji katika masuala ya Viwanda kutoka nchini China,kwa kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),na kueleza mikakati yao mbalimbali waliyonayo kuhusiana na uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania,kulia ni Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. John Mathew Mnali. 

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC),Geofrey Mwambe akisalimia na Mkurugenzi wa kampuni ya Kiluwa Group,Naima Mohamed Kiluwa,walipokwenda kwenye ofisi za kituo hicho kuwatambulisha wadau wao wa uwekezaji katika mambo ya Uwekezaji wa Viwanda,anaeshuhudia pichani kati Mwenyekiti wa Kampuni ya Kiluwa Group,Mohamed Kiluwa (pichani kati) na kuwasilisha mikakati yao mbalimbali ya uwekezaji wa viwanda.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC),Geofrey Mwambe akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yinengda New Material Techonology Mayi Hong alipokuwa akifafanua jambo kuhusiana na mambo ya uwekezaji wa viwanda hapa nchini Tanzania,maara aada kuzungumza na waandishi wa habara katika ofisi za kituo hicho .
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yinengda New Material Techonology Mayi Hong akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC),Geofrey Mwambe walipowasili leo kwenda kutambulishwa na Mdau wake Mkubwa kwenye mambo ya Uwekezaji wa Viwanda,Mwenyekiti wa Kampuni ya Kiluwa Group,Mohamed Kiluwa (pichani kati) na kuwasilisha mikakati yao mbalimbali ya uwekezaji wa viwanda. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA  HAPA>>>

RAIS MAGUFULI ASEMA SERIKALI YAKE INAYO FEDHA ZA KUTOSHA

$
0
0
*Aamua kugusia alivyobana mianya ya upotevu wa fedha 
*Aeleza namna Serikali inavyotekeleza miradi bila wafadhili

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amewahakikishia Watanzania kuwa hivi sasa Serikali yake inayo fedha za kutosha ambayo inaweza kuiendesha nchi kwa miezi sita kwa kununua bidhaa bila tatizo lolote huku akieleza kuwa fedha zilizopo ndio maana wakati mwingine zinasababisha kiburi 
ambacho wakubwa hawapendi.

Dk.Magufuli amesema hayo leo kwenye Kongamano la uchumi lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo pamoja na kuelezea mambo mbalimbali ambayo yamefanywa na Serikali ya Awamu ya Tano amezungumzia namna ambavyo wamefanikiwa kudhibiti upotevu wa fedha.

"Tuna pesa za kufanya mambo yetu na unapokuwa na pesa wakati mwingine unakuwa na jeuri ambayo hata hivyo haipendwi na wakubwa.Ukweli ni kwamba tumeziba mirija ya kuvujisha fedha na ndio maana hata makusanyo yameongezeka,"amesema.Amefafanua katika jitihada za kuziba upotevu wa fedha Serikali yake iliamua kuweka mkakati wa kuondoa watumishi hewa ambapo kwa mwezi Serikali ilikuwa inalipa Sh.bilioni 423 kwa mwaka kwa watu ambao hawapo."Kwa mwezi tulikuwa tunalipa mshahara wa Sh.bilioni 777 na bada ya uhakiki mishara inayolipwa kwa mwezi ni Sh.bilioni 251 kwa mwezi,"amesema Rais Magufuli.

WEMA SEPETU KORTINI KWA TUHUMA ZA KUWEKA PICHA ZA NGONO MTANDAONI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.

MUIGIZAJI maarufu wa filamu Tanzania Wema Sepetu amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Novemba Mosi, 2018, akikabiliwa na shtaka moja la kuchapisha picha za ngono mtandaoni.

Wema ambaye pia ni Miss Tanzania mwaka 2006, anashtakiwa chini ya kifungu cha sheria namba 14(1)(b) na( 2) (b) cha makosa ya mtandao.Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono amedai mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde kuwa  Oktoba 15, 2018, katika maeneo tofauti tofauti jijini Wema kupitia 
ukurasa wake wa Instagram alichapisha picha za ya video za ngono ( Phonograph).

Hata hivyo, Wema ambaye alitinga kizimbani saa saba kasorobo mchana amekana kutenda kosa hilo.Wakili anayemtetea Wema, Simwanza Rubeni ameiomba Mahakama kumpatia mteja wake dhamana kwa kuwa shtaka linalomkabili mshtakiwa Wema 
linadhaminika.

Pia ameiomba Mahakama kumpatia mteja wake huyo masharti nafuu 
ya dhamana.Hata Wakili Kombakono alipinga na kuiomba mahakama kumpatia mshtakiwa huyo masharti magumu ya dhamana kwani kitendo alichofanya kijamii na kimaadili linapingana kabisa na maadili ya Tanzania, amedai mshtakiwa Wema pia anafollowers wengi sana kwenye ukurasa wake wakiwemo watoto wadogo ambao wanakuwa wanafuatilia kile anachofanya.

"Tunaomba mahakama ikiwezekana iweke masharti magumu kwake ili iwe fundisho kwa wale ambao wangependa kuiga,"amesema Wakili.Hata hivyo Wema yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.Mahakama imemtaka Wema mwenyewe kisaini bondi ya sh. Milioni 10 na kuwa na mdhamini mmoja ambaye atakayesaini bondi ya kiasi hicho cha fedha.

Pia Mahakama imempiga marufuku mshtakiwa Wema kutochapisha picha yoyote ya ngono katika ukurasa wake wa Instagram au kuchapisha maneno yoyote yenye viashiria vya ngono.Kesi hiyo  imeahirishwa hadi Novemba 20.2018 Kwa mujibu wa upande wa 
mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

MISS TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA KUIWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA DUNIA

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amemkabidhi bendera ya taifa Miss Tanzania (2018) Queen Elizabeth Makune  atayewakilisha taifa katika mashindano ya urembo ya dunia "Miss World" yatayofanyika nchini China.

Akizungumza na vyombo vya habari Mwakyembe amesema kuwa mlimbwende huyo analiwakilisha taifa na amemtaka akawe balozi bora hasa katika kuitangaza lugha adhimu ya Kiswahili pamoja na maadili ya kiafrika.

Aidha Mwakyembe amemshukuru na kumpongeza mkurugenzi wa "The Look" na mwandaaji wa mashindano hayo Basila Mwanukuzi kwa kurudisha heshima ya mashindano hayo na ametenda haki katika katika tasnia hiyo ya ulimwende.Vilevile amewashukuru wadhamini wa mashindano hayo na kusema kuwa wao kama Wizara kwa kushirikiana na waandaaji wa mashindano hayo watahakikisha kuwa tasnia hiyo inaendelea kusimama imara, na kwa washindi na washiriki wa mashindano hayo watachukuliwa na shirika la ndege nchini ili wawe mabalozi wa kulitangaza taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi na muandaaji wa mashindano hayo Basila Mwanukuzi amesema kuwa tarehe 8 mwezi huu mrembo huyo ataondoka nchini  kuelekea  China ambako mashindano hayo yatafanyika na amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili Tanzania ing'are katika mashindano hayo.Mlimbwende anayewakilisha nchi katika mashindano hayo ambaye ni miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth Makune amesema kuwa anakwenda China kuwakilisha nchi na amejiandaa vya kutosha na amehaidi kuleta ushindi nyumbani.

Queen Elizabeth ameeleza kuwa atakuwa balozi katika kuitangaza lugha ya Kiswahili akiwa huko pamoja na utamaduni na maadili ya Kitanzania.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akikabidhi Bendera ya Taifa kwa Mshindi wa Miss Tanzania 2018,Queen Elizabeth Makune ambaye anataraji kwenda nchini Uchina katika Mashindano ya Urembo ya Dunia kuiwakilisha Tanzania katika Masuala ya Urimbwende
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza na Waandishi wa habari kabla ya kukabidhi Bendera kwa Miss Tanzania 2018 , Queen Elizabeth Makune
 Miss Tanzania 2018 , Queen Elizabeth Makune akiongea na Waandishi wa Habari na kutoa Tumaini kwa Watanzania kuwa atatwaa taji la Urembo la Dunia
 Mkurugenzi wa Shindano la New Miss Tanzania , Basila Mwanukuzi akizungumza na Waandishi juu ya Safri ya Miss Tanzania Uchina na Fursa walizopata Warembo walioshiriki shindano hilo Mwaka huu.
Afisa Uhusiano wa Baraza la Sanaa nchini, (BASATA), Agness Kimwanga akizungumza jambo kwa niaba ya katibu Mkuu wa BASATA wakati wa makabidhiano ya Bendera kwa Miss Tanzania 2018

STAA WA ZAMANI WA ARSENAL ROBERT PIRES AWASILI NCHINI KWA MUALIKO WA BARCLAYS

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MCHEZAJI maarufu wa zamani wa Timu ya Arsenal ya Uingereza Robert 
Pires amewasili nchini Tanzania leo Novemba 1,2018 kwa mwaliko maalum wa Benki ya Barclays kwa lengo la kushiriki uzinduzi wa Kampeni ya benki hiyo inayoitwa Superfans.

Pires akiwa nchini kwenye kampeni hiyo ambayo itampa nafasi mteja mwenye akaunti ya biashara au anayetumia kadi kufanya manunuzi mara nyingi kipindi cha kampeni fursa ya kujishindia bahati nasibu ya safari ya Uingereza kushuhudia mechi moja mubashara ya ligi Kuu ya Uingereza.

Akizungumza leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya Pires kutua nchini, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania Aron Luhanga amesema ujio wa mchezaji huo ni maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni hiyo na atakuwa nchini kwa siku tatu.

"Gwiji wa zamani wa timu ya Arsenal Robert Pires amekuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuzindua kampeni ya wateja iitwayo Superfans inayomwezesha mteja anayemiliki akaunti ya biashara au anayetumia kadi ya Barclays kufanya manunuzi mara nyingi kuzawadiwa safari ya Uingereza kushuhudia mechi mubashara ya Ligi Kuu ya Uingereza,"amesema.

Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images