Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya kwenye maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya halmashauri ya wilaya ya Lushoto.

Amesema lengo ni kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya chenye uwezo wa kutoa huduma mbalimbali muhimu zikiwemo za maabara, upasuaji na mama na mtoto.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano, Oktoba 31, 2018 wakati akizungumza na wakananchi katika kata ya Malindi, baada ya kutembelea jengo la soko mbogamboga la Malindi.

Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga vizuri katika sekta ya afya baada ya bajeti ya kununulia dawa kuongezeka kutoka sh. bilioni 31 kwa mwaka na kufikia bilioni 269.

“Hatutaki tena kusikia mgonjwa anaenda hospitali na kukosa dawa biashara hiyo tumeimaliza, Rais Dkt. John Magufuli ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa dawa.”

Amesema katika wilaya ya Lushoto Serikali imetenga sh. bilioni 1.4 kwa ajili ujenzi na ukarabati wa majengo ya vituo vya afya vya kata za Kangagai. Mnazi na Mlola.

“Halmashauri wekeni mpango thabiti wa kujenga wodi mbili kati yake moja ya wanaume na nyingine ya wanawake, lengo la Serikali ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi.”

Aizungumzia kuhusu mradi wa ujenzi wa soko, Waziri Mkuu amesema mradi huo ni sehemu ya huduma zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kuboresha huduma za jamii nchini.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto  akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga Oktoba 31, 2018. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu, watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela. na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto, Ikupa Harrison Mwasyoge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Ikupa Harrison Mwasyoge wakati alipotembelea ofisi mpya za Halmshauri hiyo baada ya kuzindua jengo la utawala, Oktoba 31, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Soko la Kisasa la mbogamboga na matunda linalojengwa na Serikali katika kijiji cha Malindi wilayani Lushoto, Oktoba 31, 2018. Alikuwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga.  Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa kijiji cha Lukozi wilayani Lushoto wakati alipowasili kijijini hapo akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Oktoba 31, 2018. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Lukozi katika Jimbo la Mlalo wilayani Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga,  Oktoba 31, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SPIKA NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA TUME YA UTUMISHI WA BUNGE NA WATUMISHI WA OFISI YA BUNGE

0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akizungumza na Watumishi wa ofisi ya Bunge katika kikao cha pamoja kati ya Tume ya Utumishi wa Bunge na Watumishi wa ofisi ya Bunge kilichofanyika leo tarehe 31 Oktoba 2018 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Ndg. Alois Makoi
 Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai (aliesimama) akizungumza na Watumishi wa ofisi ya Bunge (hawapo kwenye picha) katika kikao cha pamoja kati ya Tume ya Utumishi wa Bunge na Watumishi wa ofisi ya Bunge kilichofanyika leo tarehe 31 Oktoba 2018 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (Kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Ndg. Alois Makoi (kulia), Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Mussa Zungu (wa pili nyuma) na Mhe. Mary Chatanda (wa pili kulia nyuma)
 Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Ndg. Alois Makoi akizungumza na Watumishi wa ofisi ya Bunge katika kikao cha pamoja kati ya Tume ya Utumishi wa Bunge na Watumishi wa ofisi ya Bunge kilichofanyika leo tarehe 31 Oktoba 2018 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Katikati mbele ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (Kushoto mbele) na Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai (mbele kulia), Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Zungu (wa pili nyuma kushoto), Mbunge wa korogwe Mjini Mhe. Mary Chatanda (wa pili kulia nyuma) na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Fakharia khamis

Watumishi wa ofisi ya Bunge wakifuatilia kikao cha pamoja na Tume ya Utumishi wa Bunge kilichofanyika leo tarehe 31 Oktoba 2018 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

NMB YADHAMINI SHINDANO LA KAMPUNI BORA 100 TANZANIA

0
0

KAMPUNI Bora 100 Tanzania (Top 100 Mid-sized Companies' Survey) ni shindano linaloendeshwa na Mwananchi Communications Limited kwa kushirikiana na KPMG. Shindano hili ambalo hufanyika kila mwaka tangu 2011, huku likiwa na lengo la kuzitambua na kuzizawadia kampuni za kati zinazofanya vizuri, kuchochea maendeleo ya Tanzania kiuchumi.

Benki ya NMB ni miongoni mwa wadhamini wa shindano hili, huku ikijikita katika kusaidia eneo la SME, kipengele ambacho ni muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kuchochea makampuni hayo kufanya vizuri zaidi. NMB ni kichocheo muhimu cha SME pia, lazima ijenge mazingira mazuri ili kuleta maendeleo zaidi. Utafiti huu kwa makampuni ni muhimu kwa sababu unatoa jukwaa la SMEs, kampuni ambazo wengi ni wateja wetu, kupata mafanikio katika maendeleo ya kiuchumi na taifa kwa ujumla.

Makampuni ambayo yanaingia katika ushindani ni yale ambayo mauzo yao yanaanzia shilingi 1 za kitanzania hadi bilioni 20, na kumbukumbu zake za kifedha kukaguliwa kwa miaka 3 iliyopita, na pia isiwe kwenye orodha ya soko la hisa wala kuwa kampuni ya benki / bima / SACCOS / Sheria / Uhasibu au kampuni ya ukaguzi mahesabu.

Makampuni za Juu 100 zilizopitishwa kati za makampuni yote yaliyoshiriki yatazingatiwa katika ukuzaji kimapato.Mbali na NMB, wengine wa kampuni bora Bora ya mwaka 2018/2019 ni pamoja na Soko La Hisa la Dar es Salaam na Azam Media na Hoteli ya Hyatt Regency.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akizungumza kwenye hafla ya kutunuku kampuni Bora ya mwaka 2018/2019 (Top 100 Mid-sized Companies' Survey).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akisalimiana na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kwenye hafla hiyo.
Meza kuu katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kulia) katika mazungumzo na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harison Mwakyembe (katikati) kwenye hafla hiyo. 

USHOGA NI KESI YA JINAI NCHINI - RC MAKONDA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KAMPUNI YA AIRTEL AFRICA KUUZA HISA KWENYE SOKO LA KIMATAIFA.

NEWZ ALERT: WAFANYAKAZI WATANO WA NEMC WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI SAINI YA WAZIRI JANUARI MAKAMBA

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

WAFANYAKAZI watano wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi likiwamo la kughushi saini ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais -Muungano na Mazingira Januari Makamba katika vyeti vya tathmini ya uharibifu wa mazingira.

Wakili wa Serikali Faraja Nguka amewasomea washtakiwa makosa yao leo Oktoba 31, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando.Wakili Nguka amedai washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, mawili ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuisababishia Serikali hasara ya Sh 160 milioni.

Aidha Mahakama imetoa hati ya kukamatwa kwa mshtakiwa Magori Wambura (38) mkazi wa Bombambili kwa sababu wakati washtakiwa hao wakisomewa mashtaka hayo yanayowakabili mshtakiwa huyo ambae ni Ofisa mazingira wa Nemc, hakuwepo mahakani.Wakili Nguka amewataja washtakiwa hao kuwa ni Ofisa wa Mazingira NEMC Deusdith Katwale, Msewe, Luciana Lawi, Edna Lutanjuka, Ofisia Mwaruka na Lilian Laizer.Imedaiwa kati ya Septemba 27, 2016 na April I mwaka huu wa 2018 washtakiwa walikula njama ya kutenda kosa la kughushi.

Katika shtaka la pili washtakiwa hao wanadaiwa, Oktoba 17,2017 kwa udanganyifu walighushi cheti cha tathmini ya uharibifu wa mazingira chenye namba ya usajili EC/EIA/3366 wakijaribu kuonesha kuwa cheti hicho ni halali na kwamba kimetolewa na NEMC wakati wakijua si kweli.Pia washtakiwa hao wanadaiwa kughushi saini ya Januari Makamba ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais -Muungano na Mazingira katika cheti cha tathmini ya uharibifu wa Mazingira chenye usajili namba EC/ EIA/3366 wakijaribu kuonesha kuwa cheti hicho ni halali na kwamba kimetolewa na NEMC wakati wakati wakijua si kweli.

WAFANYAKAZI watano wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)  wakiwa wamefishwa katika chumba cha  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi likiwamo la kughushi saini ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais -Muungano na Mazingira Januari Makamba katika vyeti vya tathmini ya uharibifu wa mazingira.

UJUMBE KUTOKA TFDA

BREAKING NEWZZZZZZ: MDOGO WAKE ROSTAM AZIZ AFIKISHWA KORTINI AKIKABILIWA NA MASHITAKA 75 LIKIWEMO LA UTAKATISHAJI FEDHA

0
0
*Yamo ya kutakatisha fedha, kukutwa na nyara za Serikali

Na  Karama Kenyunko,Globu ya jamii

MDOGO wake mfanyabishara maarufu nchini Rostam Aziz, anayetambulika kwa jina la Akram Azizi leo Oktoba 31, 2018 amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka 75 yakiwemo ya mashtaka 71 ya kukutwa na silaha za aina mbali mbali pamoja na kutakatisha fedha za Marekani dola 9018.

Mshtakiwa huyo anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 82/2018 pia anakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na nyara za Serikali zenye thamani ya Sh. milioni 108, risasi 6496 pamoja na kosa la kukutwa na nyama ya Nyati kilogramu 65 yenye thamani ya Sh.milioni 4.35 bila kuwa na kibali.

Ambapo anadiwa kulitenda kosa hilo Oktoba 30,2018  katika eneo la Oysterbay Kinondoni Dar es Salaam.

Mshtakiwa amesomewa mashtaka yake na jopo la mawakili wawili wa Serikali likiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi aliyekuwa akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi Paul Kadushi mbele ya Hakimu Mkazi Augustine Rwizile.

Akisoma hati ya mashtaka hayo leo mahakamani hapo Wakili Kadushi amedai katika shtaka la utakatishaji mshtakiwa anadaiwa kati ya Juni 2018 na Oktoba 30, 2018 katika eneo la Oyesterbay, mtuhumiwa alijipatia jumla ya dola za Marekani 9018 huku akijua  fedha ni zao la kosa tangulizi la kujihusisha na biashara haramu ya nyara za Serikali pamoja na kukutwa na silaha bila kibali.

Katika mashtaka ya kukutwa na risasi, mshtakiwa anadaiwa kuwa Oktoba 30 mwaka 2018 (Jana) huko Oyesterbay, alikutwa na risasi 4092 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mrajisi wa kibali cha silaha.
Pia imedaiwa Oktoba 31, 2018 (leo) huko huko Oyesterbay mshtakiwa alikutwa na risasi 2404 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mrajisi wa silaha.

Baada ya kusomewa makosa hayo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa sababu Mahakama hiyo  haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa upande wa mshtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na hivyo mshtakiwa amerudishwa rumande.Kesi imeahirishwa hadi November 11,2018.
MDOGO wake mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz, anayetambulika kwa jina la Akram Aziz leo Oktoba 31, 2018 amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka 75, yakiwemo mashtaka 71 ya kukutwa na silaha za aina mbalimbali pamoja na kutakatisha fedha zaidi ya Dola za Marekani 6494.
 MDOGO wake mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz, anayetambulika kwa jina la Akram Aziz leo Oktoba 31, 2018 akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka 75, yakiwemo mashtaka 71 ya kukutwa na silaha za aina mbalimbali pamoja na kutakatisha fedha zaidi ya Dola za Marekani 6494.


TAKUKURU MKOANI ARUSHA YAOKOA ZAIDI YA MILIONI 11

0
0

 Na. Vero Ignatus, Arusha

Imeelezwa kuwa Taasisi ya kupambana na Rushwa mkoa wa Arusha imepokea jumla ya malalamiko 108 kwa njia mbalimbali ikiwa ni jitihada za kupambana na rushwa mkoani hapo.

Akitoa ripoti ya miezi mitatu ya kiutendaji Naibu mkuu wa Takukuru mkoa wa Arusha Frida Wikesi amesema taarifa hizo zimehusu halmashauri mbalimbali katika mkoa, idara ya ardhi, Nida, afya, kilimo, elimu, serikali za vijiji na mahakama

Amesema jumla ya majalada 23 ya uchunguzi yalifunguliwa na yanaendelea kuchunguzwa ambapo chunguzi hizo zipo katika hatua mbalimbali, haswa zilizo katika muelekeo wa makosa ya rushwa. Aidha amesema sheria ya kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 inashauri, ushauri yakinifu kutolewa kwa watoa taarifa kwa malalamiko yanayoonekana kutokuangukia kwenye sheria hiyo.

'' Malalamiko mengi yanayowasilishwa yanahusiana na rushwa, aidha kwa kipindi tajwa jumla ya makosa mapya mawili (02)yamefikishwa mahakamani '' alisema.Hata hivyo amesema kuwa ofisi ya takukuru mkoa wa Arusha wamefanya dhibiti moja la rushwa, na kuendesha zoezi la ufuatiliaji wa kuziba mianya ya rushwa.

'' Hadi kufikia mwezi septemba 2018 jumla ya mashauri 18 yaliendelea kusikilizwa mahakamani ambayo yalikuwa katika hatua mbalimbali za mahakama"alisema Wikesi.Katika kipindi tajwa TAKUKURU iliweza kuokoa jumla ya fedha kiasi cha 11,345,000 ambazo zililipwa kwa watumishi waliokua wakishughulikia maonyesho ya 88 kanda ya kaskazini mwaka 2017(10,055,00) fedha zilizokuwa za ujenzi wa mahabara sekondari ya Ilkiding'a Arumeru sh 1,290,000 ambazo zilirejeshwa serikalini. 

TANZANIA MWENYEJI WA MAZOEZI YA KIJESHI YA PAMOJA YA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

0
0
Na Khadija seif, Globu ya jamii

NCHI ya Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mazoezi ya kijeshi ya pamoja kwa nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki ambayo yatafanyika kuanzia Novemba 5 mpaka 21 mwaka huu mkoani Tanga.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mafunzo na Operesheni ya kivita jeshini wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Meja Jenerali Alfred Kapinga ametaja baadhi ya nchi ambazo zitashiriki ni Burundi, Rwanda,Kenya,Uganda na Tanzania ambaye ndiye mwenyeji wa mafunzo hayo ambayo yatafanyika 

wilayani Muheza mkoani Tanga. Mafunzo hayo yatafafahamika kwa jina la Ushirikiano Imara 2018.Pia amesema kwenye mafunzo hayo pamoja ni mambo mengine yatalenga kujenga uwezo wa kukabiliana na uhalifu pamoja na majanga huku akieleza namna ambavyo yatasaidia kubadilishana uzoefu wa kiutendaji, kuimarisha uhusiano baina ya nchi, majeshi ya Afrika Mashariki pamoja na taasisi zingine za kiraia ambazo 
zitashiriki zoezi hilo. 

Ameongeza katika kipindi hicho cha mafunzo kutakuwa na kazi za kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali  zikiwemo ujenzi wa madarasa, ofisi za walimu pamoja na vyoo katika Shule ya Msingi ya Machemba iliyopo wilayani Muheza mkoani Tanga, pia kutakuwa na utoaji wa huduma za tiba kwa wananchi katika eneo la zoezi.
Mkuu wa Mafunzo na Operesheni ya kivita jeshini wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Meja Jenerali Alfred Kapinga , akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Mazoezi ya Pamoja ya kijeshi yatakayofanyika Mkoani Tanga mwaka huu
Mkuu wa Mafunzo na Operesheni ya kivita jeshini wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Meja Jenerali Alfred Kapinga akiwa na Waandishi wa Habari

MHANDISI NDIKILO APONGEZA JITIHADA ZA TIC KATIKA KUKUZA,KUVUTIA UWEKEZAJI NCHINI

0
0
Na Ripota Wetu,Kibaha

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ametembelea banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) katika Maonesho ya wiki ya

Viwanda Mkoa wa Pwani ambapo ameipongeza TIC kwa jitihada zake katika kukuza na kuvutia uwekezaji nchini na namna inavyowahudumia wawekezaji kupitia huduma za mahala pamoja zinazotolewa na taasisi mbalimbali zilizopo ndani ya ofis za kituo hicho.

Akizungumza leo akiwa kwenye banda la TIC, Mhandisi Ndikilo amesisitiza ni ukweli kwamba Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa inayopokea wawekezaji wengi na hivyo nguvu ya

kuwahudumia lazima iimarishwe. Aidha ameshauri TIC kuhakikisha inapata taarifa zote muhimu zinazohusiana na uwekezaji ndani ya mkoa wa Pwani kwa kuwasilian na ofisi za Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani kwani kwa kufanya hivyo kutarahisisha uratibu na huduma kwa wawekezaji nchini.

Baadhi ya tarifa alizosisitiza TIC iwe nazo ni pamoja na maeneo ya uwekezaji yaliyotyengwa, takwimu za miradi ya uwekezaji. Katika kuhakikisha kwamba Mkoa wa Pwani unaendelea kuvutia uwekezaji Mkuu wa Mkoa atawasilisha TIC maeneo ambayo tayari yametengwa kwa ajili ya uwekezaji ili yaweze kutafutiwa wawekezaji.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika banda la TIC kwenye maonesho ya Wiki ya Viwanda Mkoa wa Pwani yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo Picha ya Ndege wilayani Kibaha mkoani Pwani, Meneja wa Kanda ya Mashariki Venance Mashiba .Amesema kuwa katika kuharakisha utatuzi wa changamoto zinazowakabili wawekezaji, Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kimeunda Kamati Maalum ya kiaifa inayojumuisha Wakuu wa Taasisi za Serikali ambazo ni wadau katika kuhudumia uwekezaji. 
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Kanda ya Pwani Venance Mashiba leo kwenye Maonesho ya viwanda mkoani humo.

 Baadhi ya wadau wa masuala ya viwanda wakiwa kwenye banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) wakipata maelezo leo baada ya kutembelea maonesho ya viwanda mkoani Pwani
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akisaini kitabu cha wageni leo baada ya kufika kwenye banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC). Anayeshuhudia ni Meneja wa TIC Kanda ya Mashariki Venance Mashiba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

MSAFARA WA WAZIRI LUGOLA WANUSURIKA KUGONGWA NA BASI LILILOKUA MWENDOKASI LIKIOVATEKI KATIKA KONA GAIRO, DEREVA AKAMATWA

0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Gairo. 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amenusirika kupata ajali wilayani Gairo, Mkoani Morogoro baada ya basi la Hekima za Mungu kuovateki katika kona wakati gari la waziri huyo likiwa eneo sahihi. 

Tukio hilo lilitokea saa 6:04 mchana wakati Waziri huyo alipokua anatokea Mjini Dodoma kuelekea Jijini Dar es Salaam, katika eneo la nje kidogo ya Mji wa Gairo, basi hilo likiwa mwendokasi likiovateki katika kona, ndipo dereva wa gari la Waziri Lugola alipunguza spidi ili kuiepuka ajali hiyo. 

Hata hivyo Basi hilo lilipopita, Waziri huyo aliekeza gari hilo lifuate kwa nyuma mpaka walikamate, hata hivyo Basi hilo lilikamatwa na dereva wa basi hilo kukaguliwa kama alikua na sifa ya kua dereva. Bara baada ya kumkagua dereva huyo, Waziri Lugola alizungumza na abiria wa basi hilo lenye namba za usajili T140 AZZ ambalo lilikua linatoka Dar es Salaam kuelekea Mjini Kahama mkoani Shinyanga. 

“Kwanini mnashindwa kukemea hii tabia ya huyu dereva, mnataka awaue?, alitaka kusababisha ajali mbaya sana hapa, nanyi mmekaa kimya, mnafanya makosa kutokuripoti hii tabia mbaya kabisa,” alisema Lugola. Aliongeza kua, yeye ni Waziri ambaye anakemea mwendokasi na kiuwataka madereva nchini waendeshe kwa umakini, lakini dereva huyo anashindwa kufuata sheria za usalama barabarani, hivyo anapaswa kuchukuliwa hatua na iwe fundisho kwa madereva wenye tabia kama hiyo. 

Licha ya Dereva wa Basi hilo, Isaac Vian alikiri kosa hilo na kuomba msamaha lakini Waziri Lugola aliekeza akamatwe lakini atakapofika mwisho wa safari.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Dereva wa Basi la Hekima za Mungu, Isaac Vian, alipomkimbilia Waziri huyo huku akimuomba msamaha mara baada ya kusimamishwa kutokana na kuendesha kwa mwendo kasi pamoja na kuovateki katika kona katika eneo nje kidogo na mji wa Gairo Mkoani Morogoro. Dereva wa Basi hilo lenye namba za usajili T140 AZZ lililokua linatoka jijini Dar es Salaam kuelekea Kahama Mkoani Shinyanga alielekezwa akaripoti kituo cha polisi mkoani Dodoma ili aweze kufunguliwa mashtaka. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akiangalia namba za usajili T140 AZZ la Basi la abiria la Hekima za Mungu lililokua linatoka Jijini Dar es Salaam kuelekea Kahama ambalo Waziri alilisimamisha kutokana na kosa la mwendokasi pamoja na kuovateki katika kona nje kidogo wa Mji wa Gairo Mkoani Morogoro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na abiria wa basi la Hekima za Mungu baada ya Dereva wa Basi hilo, Issac Vian kuendesha kwa mwendokasi na kuovateki katika kona kali ambapo angeweza kusababisha ajali kwa kugongana na gari la Waziri Lugola, uso kwa uso Kijijini, nje kidogo na Mji wa Gairo. 

BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO KUHAMASISHA UZALISHAJI WA MAZIWA

0
0

Katika kuhakikisha tasnia ya maziwa inawanufaisha wazalishaji wadogo wadogo wa maziwa nchini Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) ipo kwenye mikakati ya kuanzisha Jukwaa la Ushirikiano wa Tasnia ya Maziwa.

Akizungumza na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine alisema Benki ya Maendeleo ya Kilimo imejipanga kuhakikisha uzalishaji wa maziwa unaongezeka nchini ili kutoa fursa kwa wazalishaji wadogo kuweza kuchangia ukuaji wa tasnia hiyo.

Bw. Justine alisema kuwa shughuli za usindikaji wa maziwa zipo chini ya kiwango kwa viwanda vyote vinavyosindika maziwa nchini kutokana na uzalishaji duni wa maziwa hali inayorudisha nyuma ukuaji wa tasnia hiyo. “Fursa za kimasoko na uendelezaji wa tasnia ya maziwa ni kubwa hivyo tumejipanga kuhakikisha tunachagiza tasnia hii ili kuongeza uzalishaji na kuwaongezea kipato wazalishaji hasa wale wadogo wadogo,” alisema.

Aliongeza kuwa TADB imejipanga kuwakutanisha wadau wa tasnia ya maziwa ili kujadili kwa kina mipango ya muda mfupi, wa kati na mrefu ili kuja na mpango mkakati wa kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini. Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Kampuni ya NARCO, Prof. Philemon Wambura alisema NARCO imejipanga kuwezesha wazalishaji wa wadogo kote nchini kwa kuwapatia huduma za ugani ili waweze kuongeza uzalishaji wa maziwa.

Prof. Wambura aliongeza kuwa mchango wa Benki ya Kilimo katika kuhakikisha tasnia ya maziwa inachangia shughuli za uzalishaji ni jambo la kuungwa mkono. “Mchango huu wa TADB utasaidia kuongeza uzalishaji hali itakayowaongezea kipato wazalishaji wadogo nchini na hivyo kutasaidia kuwaongezea kipato wafugaji wetu,” alisema.

Kwa mujibu wa twakwimu za Bodi ya Maziwa Tanzania, tasnia ya maziwa inachangia asilimia 3.9 ya GDP huku ikikadiriwa kuwa na ng’ombe wa maziwa zaidi ya milioni 1.1 kati ya jumla ya ng’ombe milioni 30.5.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akimkaribisha Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Prof. Philemon Wambura (kushoto) alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akizungumza na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Prof. Philemon Wambura (kushoto) wakihimiza jambo wakati wa kikao cha kujadili nafasi ya taasisi zao katika kuchagiza uzalishaji wa tasnia ya maziwa nchini. 

SERIKALI YAANDAA MPANGO MKAKATI KUWANOA WASAIDIZI WA KISHERIA NCHINI

0
0
SERIKALI imeandaa mpango mkakati wa kutoa mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria ikiwa ni njia ya kuboresha huduma za msaada wa kisheria kwa watanzania maskini wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ya kisheria nchini.

Mpango wa mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria nchini unatarajiwa kuanza mapema Novemba mwaka huu na walengwa wakuu ni wasaidizi wote wa kisheria ambao wanaotoa huduma za msaada wa
kisheria katika maeneo mbalimbali nchi nzima.

Katika sehemu ya maandalizi ya mafunzo hayo, Serikali kupitia ofisi ya Msajili wa Watoa Huduma za Kisheria –Wizara ya Katika na Sheria, imeendesha mafunzo yaliyolenga kupika wataalum (wawezeshaji) wapatao 40 kutoka mashirika mbalimbali ya huduma za kisheria) watakaoendesha mafunzo hayo maalamu kwa wasaidizi wa kisheria.

Mafunzo ya kupika wawezeshaji yamefanyika Dodoma na yaliandaliwa na Law School of Tanzania (LST) kwa kushirikiana na Tanzania Law Society (TLS) na kufadhiliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF)—taasisi inayofadhiliwa miradi/shughuli mbalimbali ya wasaidizi wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumzia mafunzo hayo Mratibu wa Mafunzo ya Wawezeshaji Suleiman Pingoni amesema mafunzo hayo yanalenga kupika wataalam mahiri wakaoendesha mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria, yanayotajiriwa kuanza rasmi mapema Mwezi Novemba, na kumalizika kabla ya Disemba 31, Mwaka huu.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo Maalum ya Wawezeshaji watakaotoa mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria ili waweze kupata usajiri rasmi na wa kisheria wa kutoa huduma za kisheria kwa wananchi. Mafunzo hayo yameandaliwa na Law School of Tanzania (LST) na kufadhiliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF) yaliofanyika Dodoma jana. 

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YAPEWA SIKU 14 ZAIDI KUWASILISHA TAARIFA ZA MIRADI NA MATUMIZI YA FEDHA ZA MWAKA 2016 NA 2017

0
0
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa siku kumi nne zaidi (14) kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuhakikisha yanawasilisha taarifa za miradi na za fedha za mwaka 2016 na 2017 zilizokaguliwa kwa Msajili wa Mashirika hayo kabla ya kufutiwa usajili wao. 

Tamko hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa agizo la Serikali lililotolewa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Ufafanuzi ulitolewa kuwa, “Siku ya tarehe 28 Septemba, 2018, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alikutana na wawakilishi wa vyombo vya habari na kutoa maagizo yakuyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuwasilisha taalifa zao kwa Mashirika hayo ikiwa ni pamoja na taarifa za miradi na taarifa za fedha zilizo kaguliwa kwa mwaka 2017 na 2018”, alibainisha DKT. Jingu.

Dkt Jingu amefafanua kuwa, maagizo hayo yalipaswa kutekelezwa ndani ya siku thelathini (30) kuanzia tarehe 28.9.2018 ya agizo lilipotolewa na Serikali. Hata hivyo imeelezwa kuwa mwitikio wa utekelezaji umekuwa wa kuridhisha kutokana na ukweli kuwa Mashirika mengi yamezingatia maelekezo ya Serikali.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto( Idara kuu ya Maendeleo ya jamii) Dkt. John Jingu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu nyongeza ya siku 14 zaidi zilizotolewa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuhakikisha yanawasilisha taarifa za miradi na za fedha za mwaka 2016 na 2017 kwa Msajili wa Mashirika hayo kabla ya kufutiwa usajili wao. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW 
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya jamii) wakifuatilia tamko la Katibu Mkuu Dkt. John Jingu la kuongeza siku 14 zaidi kwa Mashirika ya Yasiyo ya Kiserikali kuhakikisha yanawasilisha taarifa za miradi na za fedha zilizokaguliwa za mwaka 2016 na 2017 kwa Msajili wa Mashirika hayo kabla ya kufutiwa usajili wao. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW. 
Katibu Mkuu wa Braza la NGOs nchini Bw. Ismail A. Suleiman akieleza kuridhishwa kwake na kanuni mpya za NGOs (2018) ambazo zimezingatia matakwa ya kanuni za maadili katika kuboresha utendaji wa NGOs wakati wa kikao cha Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii kilichoeleza kuongeza siku 14 zaidi kwa Mashirika hayo kuwasilisha taarifa za miradi na fedha kwa Msajili wa NGOs. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW. 


KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MIKAKATI YA KUTOKOMEZA MDUDU MBUNG’O DHIDI YA MIFUGO

0
0
NA: VERO IGNATUS-ARUSHA.

Jumla ya nchi 10 duniani zimekutana jiji Arusha kwa lengo la kujifunza mbinu za kisasa na matumizi ya tecknolojia,katika kudhibiti magonjwa ya mifugo yanayo ambukizwa na mdudu mbung’o katika maeneo ya wafugaji na hifadhini.

Katika mazungumzo na wanahabari Mtaalam wa magonjwa ya mifugo Dkt Imna Malele amesema kuwa mdudu mbung’o amekuwa changamoto kubwa kwa wafugaji wengi na baadhi ya maeneo ya hifadhi hivyo ni wakati muafaka kutumia mbinu za kisasa katika kuangamiza mdudu huyo ambae amekuwa changamoto katika maeneo ya wafugaji na hifadhini.

Amesema kwa nchi ya Tanzania tatizo la kuwepo kwa magojwa yatokanayo na mdudu mbung’o bado ni kubwa,na limekuwa likipunguza nguvu kazi katika uzalishaji kupitia mazao yatokanayo na mifugo suala ambalo humnyima amani mfugaji endapo mifugo itaathirika na magojwa yatokanayo na mbung’o.

Mara baada ya kufungua mafunzo hayo maalum kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa tume ya nguvu za atomic nchini Prof Lazaro Busagala, Dkt. Firmi Banzi ambae pia ni mtaalamu wa masuala ya teknolojia na masuala ya nguvu za nyuklia akatumia fursa hiyo kueleza matumizi ya teknolojia ya nyuklia nchini katika kupambana na mbung’o bila ya kuharibu mazingira ambapo amesema njia hiyo imekuwa na manufaa makubwa katika nchi mbalimbali duniani.

Nao baadhi ya washiriki akiwemo Deusdedit Malulu wakaeleza matarajio yao katika masuala ya utafiti dhidi ya kuangamiza mdudu aina ya mbung’o kwa mazingira salama ya utalii ambapo wamesema njia hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa katika jamii za wafugaji na maeneo ya hifadhini.

Mdudu mbung’o hueneza uonjwa wa malale ambao ni hatari kwa maisha ya binadamu ambapo pia njia ya matumizi ya nyuklia imetajwa kuwa ni miongoni mwa njia salama katika mapambano dhidi ya mbung’o ambapo njia hiyo imekuwa mkombozi zaidi katika visiwa vya zanzibar na maeneo mbalimbali nchini.
Pichani, Mdudu mbung’o
Firmi Banzi Mtaalamu wa masuala ya Nyuklia.Mdudu mbung’o
Dkt. Imna malele-mtaalamu wa magonjwa ya mifugo akizungumza na wanahabari baada ya ufunguzi wa mafunzo

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA 1,2018

TTCL YATOA UFAFANUZI KUHUSU KUPUNGUZA WAFANYAKAZI

DC MURO ASHIRIKI UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI YA LOSIKO PAMOJA NA WANANCHI KIJIJI CHA LOSIKITO

0
0


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro jana ameungana na wananchi wa kijiji cha LOSIKITO kata ya Mwandeti Halmashauri ya Arusha katika ujenzi wa shule Mpya ya sekondari ya losiko ambayo inajengwa Kwa nguvu za wananchi.
 
Dc Muro ameamua kuungana na wananchi katika kuhakikisha shule hiyo inaanza kutumika Mwaka 2019 Kwa lengo la kupunguza uhaba wa shule na vyumba vya madarasa Kutokana na ongezeko Kubwa la wananchi waliofaulu Elimu ya Msingi ambao wanapaswa kuingia Kidato Cha kwanza Mwaka 2019.Dc Muro anaendelea na ziara yake katika kata ya mwandeti iliyo halmashauri ya Wilaya ya ARUSHA
2
Dc Muro akiungana na Wananchi kushiriki ujenzi kuhakikisha shule hiyo inaanza kutumika Mwaka 2019 Kwa lengo la kupunguza uhaba wa shule na vyumba vya madarasa Kutokana na ongezeko Kubwa la wananchi waliofaulu Elimu ya Msingi ambao wanapaswa kuingia Kidato Cha kwanza Mwaka 2019.
index
Dc Muro akishiriki ujenzi wa shule  mpya ya sekondari ya Losiko katika kijiji ch Losiko,wilayani Arumeru,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara yake iliyoanza jana katika kata ya mwandeti,katika halmashauri ya Wilaya ya Arusha ambapo Mkuu huyo wa Wilaya anatarajiwa kutembelea Kata zote 53 za Wilaya ya Arumeru.
1
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro akifafanua jambo mbele ya baadhi wa viongozi aliombatana nao alipokwenda kuungana na wananchi wa kijiji cha LOSIKITO kata ya Mwandeti Halmashauri ya Arusha katika ujenzi wa shule Mpya ya sekondari ya losiko ambayo inajengwa Kwa nguvu za wananchi.
3
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live




Latest Images