Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

TCRA YAENDELEA KUWAKUMBUSHA UMMA KUHUSU MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA MITANDAO YA KIJAMII


BENKI YA CRDB YATWAA TUZO MAONYESHO YA VIWANDA MKOANI PWANI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimkabidhi tuzo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela, kwa kuwa wadamini wakuu wa Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani, yaliyofunguliwa rasmi leo Oktoba 29, 2018, katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani. Katikati ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela, akitoa hotuba yake wakati wa Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani, yaliyofunguliwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 29, 2018, katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela, baada ya kutoa hotuba yake wakati wa Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani, yaliyofunguliwa rasmi leo Oktoba 29, 2018, katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani. Benki ya CRDB ni wadhamini wakuu wa Maonyesho hayo. Katikati ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela, wakati wa Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani, yaliyofunguliwa rasmi leo Oktoba 29, 2018, katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (wa tatu kulia) alipokuwa akimueleza machache juu ya huduma wanazotoa, wakati alipotembelea Banda la Benki ya CRDB, kwenye Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani, yaliyofunguliwa rasmi leo Oktoba 29, 2018, katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela.

Italia yaiahidi Afrika Ushirikiano wa kiuchumi

$
0
0

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Italia na Afrika wameazimia kukuza na kuimarisha Ushirikiano katika nyanja mbalimbali, hususan biashara na uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya kweli barani Afrika.

Mawaziri hao walifikia azimio hilo wakati wa mkutano wa pili wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Italia na Afrika uliofanyika Farnesina, Italia tarehe 25 Oktoba 2018 na kuhudhuriwa na Mawaziri wa zaidi ya nchi 40 akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb). 

Mawaziri hao walikutana kwa madhumuni ya kujadili kwa pamoja changamoto zinazohusu usalama, uhuru, amani, demokrasia na namna wadau wa Italia (wenye viwanda, Wafanyabiashara, wanazuoni na taasisi zisizo za kiserikali) watakavyoweza kushiriki katika kukuza uchumi barani Afrika hasa katika sekta ya uwekezaji na biashara. 

IGP SIRRO AKUTANA NA KIKOSI MAALUM KINACHOPAMBANA NA UHALIFU WILAYANI BIHARAMULO

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na askari wa kikosi maalum cha kupambana na matukio ya uhalifu na wahalifu katika eneo la Midaho wilayani Biharamulo mkoani Kagera leo 29/10/2018 wakati akiwa safarini kuelekea wilaya ya Ngara mkoani humo kwa ziara ya kikazi. Picha na Jeshi la Polisi.
Askari wa kikosi maalum kinachopambana na matukio ya uhalifu na wahalifu kama wanavyoonekana Pichani wakitekeleza majukumu yao katika eneo la Midaho wilayani Biharamulo mkoani Kagera leo 29/10/2018. Picha na Jeshi la Polisi.

Results Based Monitoring and Evaluation 2018

MGANGA MKUU SINGIDA APEWA WIKI MBILI KUBORESHA AFYA MAKAZI YA WAZEE

$
0
0
Na ANTHONY ISHENGOMA

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida kuhakikisha wazee wasiojiweza wanaoishi Makao ya Wazee ya Taifa Sukamahela wanapatiwa vyandarua kwa ajili ya kujikinga na Malaria.

Naibu Waziri Ndugulile ametoa agizo hilo alipotembelea makao hayo yaliyoko nje kidogo ya mji mdogo wa Manyoni kujionea hali halisi ya maisha ya Wazee wasiojiweza.

Dkt. Ndugulile ametoa muda wa wiki mbili kwa Mganga Mkuu Mkoa kutekeleza jambo hilo na kutaka mrejesho wa utekelezaji wa agizo hilo.“Hili ni kosa ambalo siwezi kulisamehe tuna vyandarua vingi vya kutosha sioni sababu wazee hawa kulala kwenye vyumba bila vyandarua, nawapa wiki mbili kuhakikisha kila mzee analala kwenye chandarua.,” Aliagiza Dkt.Ndugulile.

Pia Dkt. Ndugulile amewataka watendaji wa Idara ya Afya wa Zahanati ya Sukamahela iliyopo katika eneo la makao ya Wazee hao kuhakikisha wanakuwa na dawa za kutosha hasa zile maalumu kwa ajili magonjwa ya Wazee.Makao ya Wazee Sukamahela pamoja na mambo mengine yanayowakabili na upungufu wa chakula, na wamekili kuchoshwa na ulaji wa aina moja ya mboga hivyo kutoa ombi lao kwa Naibu Waziri kutatua changamoto hiyo.

Naibu Waziri Ndugulile amehaidi kushughulikia suala la ukarabati wa majengo chakavu ya yaliyopo katika Makazi hayo.Kwa nyakati tofauti wazee waishio katika makazi hayo wamelalamikia ukosefu wa umeme katika makazi hayo, dawa za magonjwa ya ukoma na vifaa vidogo vidogo kwa ajili ya usafi na kilimo cha mbogamboga pamoja na miundo mbinu chakavu ya vyoo.Aidha Dkt.Ndugulile amesema serikali inakusudia kufunga baadhi ya vituo na kuvipanga kikanda ili iweze kudumisha huduma kwa wazee wasiojiweza lakini kugeuza makazi yatakayofungwa kuwa nyumba salama kwa ajili kupambana na vitendo vya kikatili.

Naibu Waziri Ndugulile yupo mkoani Singida kufuatilia utekelezaji wa masuala ya Afya, Ustawi na Maendeleo ya Jamii.
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo yaJamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Wazee waishio Makao ya Wazee Sukumahela Wilayani Manyoni wakati wa ziara take inayoendelea Mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo yaJamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Jiko kinapoandaliwa chakula cha Wazee waishio Makao ya Wazee Sukumahela Wilayani Manyoni wakati wa ziara take inayoendelea Mkoani Singida

SACOSS NCHINI ZAASWA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA USHIRIKA KWA WANACHAMA

$
0
0


Na Lucas Mboje, Dodoma

VYAMA vya ushirika nchini vimetakiwa kuendelea kutoa elimu ya ushirika mara kwa mara kwa wanachama wake ili kujenga uelewa wakutosha kuhusu sheria, kanuni na masharti mbalimbali ya ushirika.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa sita wa mwaka wa Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza nchini, Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa ametoa rai hiyo kwa vyama vya ushirika nchini kuendelea kutoa elimu ya ushirika kwani ni muhimu katika uendeshaji wa shughuli za chama.

Amesema kuwa elimu ya ushirika isitolewe tu kwa watendaji na viongozi wa chama bali itolewe kwa wanachama wa ushirika ili wajue uendeshaji wake na kunufaika na huduma zitolewazo na chama. “Vyama vingi vya ushirika hapa nchini vimekufa kwa kukosa elimu ya ushirika, niwaombe sana wasimamizi wa ushirika muendelee kutoa elimu kwa wanachama”. Amesisitiza Kaimu Mrajis Chilewa.

Aidha, Kaimu Mrajis Chilewa amewaasa Magereza SACCOS pamoja na Saccos zote nchini kufanya shughuli zake kwa kufuata sheria ya ushirika pamoja na kuheshimu na kusikiliza maoni ya wanachama kwani wao ndo wenye mali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mbaraka Semwanza akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara ulifanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma. 
Meza Kuu wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. 
Mjumbe wa Mkutano Mkuu akitoa hoja ya kuthibitisha notisi kabla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. 
Mlezi wa Magereza Saccoss ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akitoa neno kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa.  
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi kama inavyoonekana katika picha. 


MTANZANIA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 23 NCHINI UINGEREZA KWA KUMUUA MKEWE

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MTANZANIA Kema Salumu (39) amehukumiwa kifungo cha miaka 23 baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mkewe Leyla Mtumwa (35) wakiwa nyumbani kwao huko Haringey Uingereza mapema April mwaka huu.

Mahakama imeeleza kuwa chanzo cha tukio hilo ni Salumu kuwa na wivu wa kimapenzi kwa mkewe mara baada ya kutoka na rafiki zake usiku.

Imeelezwa kuwa mapema Machi 30 Salumu aliandaa mpango kabla ya kwenda jikoni na kuchukua kisu na kumjeruhi Leyla kwa kumchoma kisu mara 49 katika maeneo ya kichwa, shingo, mwili na mikono huku kijana wao wa miaka 12 akishuhudia na kupiga kelele akimzuia baba yake.

Aidha imeelezwa kuwa awali alikana kufanya mauaji hayo kwa kusema kuwa alikuwa anajilinda na baadaye Septemba akakiri kufanya mauaji hayo.

Salum Kema amekuwa akiishi Uingereza kwa miezi sita tangu waoane na Leyla  na baadaye kumuua papo hapo kwa kisu.

DKT.KIGWANGALLA AFANYIWA TAMBIKO NA WAZEE WA MILA WA LUSU

$
0
0
*Sasa naanza safari mpya*

WAZIRI wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbao la Nzega Vijijini la Mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangalla amewashukuru viongozi mbalimbali wa dini Nchini kwa dua na maombi yao kwa kipindi chote alichopata ajali hadi sasa kupona na kurejea tena na majukumu yake.

Akizungumza katika mkutano wake wa pili uliofanyika katika Kata ya Lusu Tarafa ya Nyasa iliyopo kwenye jimbo lake hilo la Nzega Vijijini, jana Oktoba 28, 2018,  Dkt. Kigwangalla amewashukuru viongozi hao wa dini pamoja na Wazee wa Mila kwani wao wamekuwa chachu kwenye kupona kwake tokea alipolazwa Hospitali kwa zaidi ya miezi miwili kwa kuuguza majeraha ya mwili wake kutokana na ajali ya gari aliyopata Agosti 4, mwaka huu.

Amesema viongozi wa hao wa dini pamoja na  Wananchi kila mmoja kwa nafasi yake walikuwa ni wa kipekee na dua zao zimeweza kusaidia  na kwa sasa amerejea kutoa shukrani na kupokea dua zao hizo kwani kwa sasa ameanza kufanya kazi.

“Kwa sasa nimeanza kurudi kwenye majukumu yangu kama kawaida. Kwa hivyo nikaona kabla ya kuanza kuonekana nikiruka huku na kule kwenye majukumu ya kiwizara, nikasema hapana nirudi kwanza nyumbani nipate dua za wazazi wangu, dua za wazee na viongozi wa dini.
Kwa tukio lile kwa sisi tunaoamini,  ni mkono wa Mungu ulikuwa mahala pale” amesema Dkt. Kigwangalla.
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbao la Nzega Vijijini la Mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa na Mkewe Dkt. Bayoum Kigwnagalla wakisindikizwa na Wazee wa mila wa Lusu wakati alipowasili kutoa shukrani na dua kwa wananchi wa jimbo lake hilo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbao la Nzega Vijijini la Mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa na Mbunge wa jimbo la Manonga, Seif Gulamali wakifuatilia kwa makini wakati wa tukio la kutoa shukrani na dua maalum iliyoandaliwa kwa wananchi wa jimbo lake hilo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbao la Nzega Vijijini la Mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifanyiwa tambiko la kichifu na Watemi wakiongoza na Chifu Ng’wana Ng’washi wa Wasukuma wakati wa kutoa dua na shukrani.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbao la Nzega Vijijini la Mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipokewa na Wananchi wa Jimbo hilo wakati alipowasili kwenye Kata ya Lusu wakati wa kutoa dua na shukrani.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Vituo vya Luninga vya ITV, STAR TV na EATV kuondolewa kwenye King’amuzi cha StarTimes

$
0
0
Kampuni ya Star Media (T) Limited (MUX) ambayo ina jukumu la kisheria la kurusha matangazo ya televisheni zenye leseni ya kurusha matangazo bure nchini, chini ya Sheria, na vile vile Chaneli hizo zenye leseni za kurusha maudhui yao (CSP0 zina wajibu KISHERIA wa kusaini mikataba ya kurushwa na MUX yaani (SLA) ili kuweza kurushwa katika ving’amuzi vyao katika mfumo wa (FTA au wa kulipia kutokana na aina ya leseni) yaani ili watumiaji waweze kupokea matangazo yao kupitia ving’amuzi.

Kutokana na hilo, StarTimes imekua ikifanya juhudi mbali mbali kuhakikisha kwamba inaingia mikataba na chaneli hizo ili ziweze kurushwa kwa mujbu wa sheria, la sivyo inakua kinyume cha sheria kurusha chaneli bila kuwa na makubaliano (SLA) na chaneli iliyoko kwenye king’amuzi.

“Hivyo basi, ni kwa muda mrefu sasa tumekua tukirusha baadhi ya chaneli bila kuwa na makubaliano hayo hivyo tumefanya  juhudi za makusudi kuhakikisha tunakubaliana  na kuingia mikataba na chaneli hizo kwa mujibu wa Sheria za Nchi. 

Kwa juhudi hizo kwa ushirikiano na mamlaka husika, tumefanikiwa kuingia mikataba na baadhi chaneli  Chaneli ila kwa baadhi ya chaneli  imeonakena kuwa ngumu hata baada ya Mamlaka husika kuingilia kati, sababu kuu ikiwa ni maslahi ya kibiashara.

Hivyo basi kutokana na kushindikana kufikia muafaka wa makubaliano hayo, Star Media tumefikia uamuzi wa kuondoa chaneli  za ITV, STAR TV na EATV kutokana na sababu ya kutokuwa na Mikataba (SLA) kwa kuwa ni kinyume na Sheria kubeba chaneli hizo bila kuwa na mikataba au makubaliano.” Bw Wang Xiaobo, CEO StarTimes.

“Hivyo basi tunapenda kutoa taarifa kwa wateja wetu na umma kwa ujumla kwamba, kutokana na sababu tajwa tutasitisha matangazo ya chaneli tajwa hadi pale tutakapokuwa na makubaliano rasmi kwa mujibu wa sheria. 

Hivyo basi chaneli hizo zitaondolewa mara moja kutoka kwenye ving’amuzi vyetu.” Aliongeza Bw Wang.

UJENZI WA RELI YA SGR , WAFIKIA ASILIMIA 32, MAKAMU WA RAIS ALIPONGEZA SHIRIKA LA RELI

Habari za UN Kutoka New York. Marekani, OKTOBA 29, 2018

TTGA WATAMBUA MCHANGO WA WAONGOZA WATALII WALIOOKOA MTOTO WA FARU

$
0
0

Na. Vero Ignatus Arusha

Chama cha Waongoza Watalii Tanzania(TTGA) kimetoa vyeti kwa Madereva 12 waongoza watalii waliofanikiwa kumuokoa mtoto wa Faru asiuwawe na Simba katika Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa Ngoro ngoro na Hifadhi ya Taifa Serengeti.
 

Akizungumza katika hafla hiyo mwenyekiti wa TTGA Khalifa Msangi amesema kuwa waongoza watalii wa Tanzania wapo vizuri sana kwa kuwa ndio sekta inayoongoza katika kuingiza fedha za kigeni hapa nchini na kuchangia pato la Taifa (GDP).

Msangi amesema Waongoza watalii wana mchango mkubwa wa kuiletea taifa maendeleo kwa kuwa wakifanya kazi kwa Uzalendo,na kujituma basi ni wazi kuwa wanapelekea Idadi ya watalii nchini.

Aidha amesema Chama hicho kimeamua kuwapa Vyeti kama Ishara ya kutambua mchango uliofanywa na Madereva hao kwa kutambua kuwa mnyama faru ni mnyama Adimu na yupo mbioni kutoweka duniani.

“Kwanza tuwapongeze Madereva hawa kwa kazi kubwa ya Kizalendo walioifanya na madereva hawa wanastahili pongezi kwanza kwa kuhataraisha maisha yao na Wageni, ili tu kuweza kuokoa mtoto huyo wa faru ambaye mama yake alishamua kukimbia kutokana na kundi la samba,wamesfanya jambo la kizalendo sana”alisema Msangi.

Juma Rajabu Sumbi ni miongoni mwa wale waliookoa mtoto wa Faru mwaka jana Moru,Ni Freelencer kwa sasa anawafanya nyingi za Tawisa. simba. Anafanya kampuni ya Kiboslope, akipokea cheti kutoka kwa Mwenuekiti wa Bodi ya TTGA Christopher Nzela. 
 Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Utalii Nchini (TTGA) Khalifa Msangi. 

Pichani anaonekana Simba akimshambulia mtoto wa Faru,juzi ngorongoro, guides waliweza kumuokoa, TTGA wametambua mchango wao mkubwa wamefanya matukio yote mawili kuwapongeza guides na kuwapa vyeti. Picha kwa hisani ya TTGA.

Pichani anaonekana mtoto wa Faru aliyekuwa amezama kwenye matope serengeti Moru mwaka jana 2017 akaokolewa baada ya kuonwa na guides, wakawaita Rengers. Picha kwa hisani ya TTGA.



HATUWEZI KUENDELEA KUAGIZA SUKARI WAKATI TUNA UWEZO WA KUFANIKISHA UZALISHAJI-DKT TIZEBA

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Dodoma

Serikali imeipa changamoto Bodi ya sukari nchini kutekeleza majukumu yake kwa weledi ikiwa ni pamoja na kusisitiza kuhuisha uzalishaji wa sukari kwa wingi ili kuondokana na uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.

KaMpuni mbalimbali za uzalishaji wa sukari nchini zimeitikia wito wa Serikali wa kuongeza uzalishaji wa sukari ili nchi iweze kujitegemea kwa bidhaa hiyo pendwa kwa matumizi ya nyumbani na viwandani na ziada jambo litalopelekea Bodi ya sukari kusimamia majukumu yake ipasavyo ili kuondokana na uagizaji wa sukari nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa leo jumatatu tarehe 29 Octoba 2018 na Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma.

Waziri Tizeba amemtaka Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari nchini Bi Mwamini Juma Malemi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof Kenneth Michael Kitundu Bengesi Kudhibiti sukari inayoingia nchini pasina utaratibu huku akiwataka kusimamia kwa weledi ufanisi katika uongezaji wa uzalishaji wa sukari nchini.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Oktoba 29, 2018.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof Kenneth Michael Kitundu Bengesi akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu tarehe 29 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu tarehe 29 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akimkabidhi muongozo wa utendaji kazi Mwenyekiti wa Bodi ya sukari Tanzania Bi Mwamini Juma Malemi kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu  Octoba 29,2018.

KAIMU BALOZI WA MAREKANI ATEMBELEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA SERIKALI YA MAREKANI

$
0
0
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dk. Inmi Patterson akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga alipokwenda kumsalimia hapo jana. Dk. Patterson yupo mkoani Kigoma kutembelea miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Rashid Mchata. (Picha: Ubalozi wa Marekani).

Fourth Round Selection of Applicant's Selected to Join Ardhi University into various Academic Undergraduate Degree Programmes

Rais Magufuli amteua Prof. Humphrey Mushi kuwa Mwenyekiti wa FCC

ZIARA YA NAIBU WAZIRI DKT. FAUSTINE NDUGULILE KATIKA MAKAO YA WAZEE YA SUKAMAHELA MANYONI SINGIDA

MAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 30,2018

Results Based Monitoring and Evaluation 2018

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images