Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

KAMPUNI YA KILUWA GROUP YAWATAMBULISHA WADAU WAKE WA UWEKEZAJI WA VIWANDA KWA MKUU WA MKOA WA PWANI

0
0
Mkuu wa mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo akimsikiliza Mwenyekiti wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd,Mohamed Kiluwa alipokuwa akiwatambulisha Wadau wake wa uwekezaji kutoka nchini china,waliofika Oktoba 29,2018  kumtembelea na kujitamulisha ofisini kwake ,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yinengda New Material Technology,Mayi Hong akiwa ameambatana na Wenzake Wane.Kampuni hiyo inajishughulisha na uzalishaji/utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za ngozi nchini China. 
Meneja wa Kampuni ya Kiluwa Group Ndugu Madoweka pichani kulia akifafanua zaidi kwa lugha ya Kichina, kilichokuwa kikizungumzwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo kwa Wawekezaji hao waliofika nchini kwa mwaliko wa Kampuni ya Kiluwa Group,kutafuta fursa za uwekezaji wa viwanda katika bidhaa mbalimbali za ngozi
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yinengda New Material Technology,Mayi Hong akiwa ameambatana na Wenzake Wane (hawapo pichani),akiushukuru uongozi wa Mkoa wa Pwani pamoja na Kampuni ya Kiluwa Group kwa mapokezi mazuri kufuatia ujio wao wa kutafuta fursa za uwekezaji kupitia kampuni yao inajishughulisha na uzalishaji/utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za ngozi nchini China,pichani kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Group Bi.Naima Kiluwa.
Mkuu wa mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na ugeni wake uliomtembelea Ofisini kwake Oktoba 29,2018 na kuzungumza nae mambo kadhaa katika suala zima la uwekezaji katika mkoa wa Pwani,wakiwa na mwenyeji wao Mwenyekiti wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd,Mohamed Kiluwa .
Mkuu wa mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yinengda New Material Technology,Mayi Hong inayojishughulisha na uzalishaji/utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za ngozi nchini China.
Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya utambulisho

Makamu wa Rais atembelea Banda la IPP TOUCHMATE wiki ya maonyesho ya Viwanda Kibaha Inbox x

0
0
Makamu wa Rais atembelea Banda la IPP TOUCHMATE wiki ya maonyesho ya Viwanda Kibaha
Na Mwandishi wetu,
Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan jana amezindua wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’ yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani.
Kabla ya kutoa hotuba yake katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais alitembelea banda la kampuni ya IPP TOUCHMATE na kupata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makapuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi.
Dk. Mengi alimweleza Makamu wa Rais kuhusu ushirikiano wa kampuni hizo mbili wa kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vifaa mbalimbali vya Kielekroniki nchini vitakavyouzwa kwa bei nafuu na kutumika katika utoaji wa elimu, ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu wa tano ya kuboresha  elimu.
Dk. Mengi alimweleza Makamu wa Rais kuwa kampuni ya Touchmate ipo Dubai na ina uzoefu wa miaka 30 wa kutengeneza vifaa vya kielektroniki kama simu za kisasa (smart phones, tablets, kompyuta na vifaa vya nyumbani).
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi akisalimiana na mgeni rasmi Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan alipowasili katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani kwa ajili ya kufungua wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’.
 Mgeni rasmi Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (kulia), alipotembelea banda la IPP TOUCHMATE katika maonyesho ya wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’. Kushoto ni Mwasisi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Touchmate, Bw. Vasant Menghani.
 Mgeni rasmi Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan akikagua vifaa vya kielektroniki kama simu za kisasa (smart phones, tablets, kompyuta na vifaa vya nyumbani) huku akipata maelezo kutoka kwa mwasisi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Touchmate, Bw. Vasant Menghani (kushoto) alipotembelea banda la IPP TOUCHMATE katika maonyesho ya wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’. Kushoto ni Mwasisi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Touchmate, Bw. Vasant Menghani. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa  IPP Touchmate, Bw. Victor Tesha na wa pili kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi.
 Mgeni rasmi Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan akisoma maelezo yaliyomo kwenye moja ya bidhaa za kielektoniki alipotembelea banda la IPP TOUCHMATE katika maonyesho ya wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’. Kushoto ni mwasisi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Touchmate, Bw. Vasant Menghani.
Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la IPP Ltd lililopo katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani  wakiangalia vifaa vya kielektroniki kama simu za kisasa (smart phones, tablets, kompyuta na vifaa vya nyumbani) wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’, yaliyofunguliwa rasmi jana na Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan mkoani humo.
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Nishati, Mh. Subira Mgalu wakati wakisubiri kuwasili kwa mgeni rasmi Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Sabasaba, Kibaha picha ya Ndege, Mkoani Pwani kwa ajili ya kufungua wiki ya maonyesho ya viwanda ambapo taasisi 25 zinashiriki kuonyesha  bidhaa zake huku yakibeba kauli mbiu ya ‘Viwanda Vyetu, Uchumi Wetu’. Katikati ni Mwasisi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Touchmate, Bw. Vasant Menghani

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAS TABORA AAGIZA MZABUNI ALIYESHINDA HUDUMA JAZIA KUHAKIKISHA DAWA ZILIZOPO KWENYE MKATABA ZIPATIKANA WAKATI WOTE

0
0
NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI  Mkoani Tabora imemtaka  mzabuni aliyeshinda na kusaini mkataba wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja kutoa huduma ya dawa na vifaa tiba (JAZIA- Prime Vendor System) kuhakikisha orodha ya dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba vilivyopo kwenye mkataba vinapatikana wakati wote ili kuepuka malalamiko kutoka kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba na Kampuni ya Chacha Magasi Pharmacy Ltd na Serengeti Care  kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo ambazo hazipatikani Bohari Dawa(MSD). 

Katibu Tawala Mkoa alisema afya bora ni kitu muhimu sana ndio maana Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga fedha nyingi kwa ajili ya dawa na vifaa tiba ili kuwawezesha wananchi kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo na kuongeza ndio maana hakuna sababu ya kutokuwepo dawa katika Kituo cha Afya chochote.

Aidha Makungu aliwataka Wakurugenzi Watendaji wote kuhakikisha wanasimamia makubaliano yaliyomo katika mkataba huo ikiwa ni pamoja na kuwahimiza wasimamizi wa vituo vya  kutolea huduma kuagiza dawa kutoka Bohari ya Dawa(MSD) na zile zitakazokosekana MSD ziagizwe kwa Mzabuni aliyeingia na Mkoa huo Mkataba na siyo vinginvyo.

Alisema ni vema waka wanafuatilia ili kuhakikisha Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali wakati wote zinakuwa na  dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba vya kutosha ili wagonjwa wasipate usumbufu.

Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunini Kamba alisema lengo la JAZIA ni kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba katika Vituo vya kutolea huduma, kuboresha uwazi na uwajibikaji kwenye matumizi fedha za umma na kupunguza muda wa kuomba na kupokea dawa na vifaa tiba.
 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maagizo  kwa Mzabuni aliyeshinda kutoa huduma kupitia unajulikana kama Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kuzingatia maelekezo ya mkabata kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo mara baada ya kusaini mkataba huo.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt Gunini Kamba akitoa maelezo mafupi kuhusu uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo.
 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu ( mwenye suti ya bluu) akisaini Mkataba wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Sekiete Yahaya naye akisaini huku wakishuhudiwa na Mkurugenzi wa Chacha Magasi Pharmacy Ltd  Chacha Magasi (wa pili kutoka kushoto)  na Serengeti Care Albinus Mongore(kushoto), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt Gunini Kamba(kulia aliyesimama)
 Baadhi ya Watendaji kutoka Chacha Magasi Pharmacy Ltd na Serengeti Care wakifuatilia maelezo ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora kabla ya kusaini Mkataba wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo. 
 Baadhi ya Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya Mkoani Tabora wakiwa katika hafla fupi ya kusaini mkataba wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo. 
 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu ( mwenye suti ya bluu waliokaa ) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote za Mkoa huo na watendaji wa Chacha Magasi Pharmacy Ltd   na Serengeti Care  mara baada ya kusaini Mkataba wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo.  

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI WA AFYA HAMAD RASHID MOHAMMED AZUNGUMZA NA UJUMBE WA MADAKTARI WA MENO KUTOKA NCHINI UTURUKI

0
0
Miza Kona, Maelezo Zanzibar 
WIZARA ya Afya Zanzibar imepokea ujumbe wa Madaktari 11 kutoka nchini Uturuki kwa ajili ya kutoa huduma ya meno kwa wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba.

Ujumbe huo una lengo la kutoa huduma ya meno kwa wananchi mbali mbali wa vijijini ili kuweza kupunguza tatizo la meno pamoja na kutoa taaluma ya kujiepusha na madhara ya meno huko katika hospitali ya Kivunge Wilaya yaKaskazini A Unguja

Akizungumza mara baada kuwasili ujumbe huo huko Wizara ya Afya Waziri wa wizara hiyo Hamad Rashid Mohammed amesema ujumbe wa madaktari hao una lengo la kutoa huduma ya meno pamoja na kutoa taaluma hiyo katika chuo kikuu cha SUZA ili kupata wataalamu wa meno hapa nchini

Amesema ujio huo utasaidia kusomesha madaktari wa fani hiyo ili kupata wataalamu wazalendo kwa lengo la  kuondosha upungufu wa madaktari wa  meno.

Aidha amesema madaktari hao watatoa huduma hiyo kuanzia Kivunge, Makunduchi, Tumbatu, Unguja Ukuu, Chake, Wete na Mkoani .   
 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed akizungumza na Ujumbe wa Madaktari wa Meno kutoka Nchini Uturuki huko katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
 Mratibu wa Ujumbe wa Madaktari wa Meno kutoka Nchini Uturuki Dkt. Feroz Jafferji  akitoa shukrani kwa Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed (hayupo pichani) juu ya mapokezi mazuri waliyoyapata.
 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed akizungumza na Waandishi wa habari ( hawapo Pichani) kuhusu ujio wa Ujumbe wa Madaktari wa Meno kutoka Nchini Uturuki huko  Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed akiwa katika  Picha ya pamoja na Ujumbe wa Madaktari wa Meno kutoka Nchini Uturuki huko Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

POLISI, TRA KILIMANJARO WANASA KIWANDA FEKI CHA KUTENGENEZA POMBE KALI

0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini.
JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wamefanikiwa kukamata kiwanda  cha kutengeneza Pombe kali ambacho kimekuwa kikizalisha bidhaa hiyo bila ya usajili.
Moja ya dira za serikali ya awamu ya tano ni kufikia uchumi wa kati kupitia Viwanda ,hata hivyo baadhi ya wafanyabiahara watafsiri Dira hii tofauti kwa kuamua kuanzisha Viwanda bila ya kufuata matakwa ya Sheria na taratibu za nchi.

Hali hii imejidhihirisha mkoani Kilimanjaro katika mji mdogo wa Himo baada ya Polisi,TRA na TFDA kubaini uwepo wa kiwanda bandia kinachozalisha Pombe kali .
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamisi Issah amesema jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na idara nyingine za serikali kuhakikisha kodi ya serikali inapatikana pamoja na kuhakiki ubora wa bidhaa kwa ajili ya afya ya watumiaji.
Zoezi la kubaini uwepo wa viwanda bandia katka mkoa wa Kilimanjaro ambapo katika siku za karibuni viwanda vilivyogundulika ni vile vinavyotengeneza Pombe za kienyeji na Pombe kali ,baadhi  vikiwa katika wilaya ya Rombo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Hamisi Issah akitizama baadhi ya chupa ambazo zimendaliwa kwa ajili ya kujaza kimiminika cha Pombe kali.
Sehemu ya Mitambo iliyopo ndani ya kiwanda hicho kilichopo katika wilaya ya Himo ambacho kinaaminika kuhusika katika kutengeneza Pombe kali bila ya kufuata taratibu.
Anayedaiwa kuwa mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho akitoa maelezo kwa kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Hamisi Issah pamoja na Meneja Msaidizi wa TRA Kilimanjaro anayeshughulikia masuala ya forodha ,Godfrey Kitundu ndani ya kiwanda hicho.

MAHAKAMA KUTAJA TAREHE YA KUSOMEWA HUKUMU KWA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TBC

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imesema Novemba 16, 2018 itataja tarehe ya kusomwa kwa hukumu ya kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili aliyekuwa  Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando.

Hatua hiyo imefikiwa leo Oktoba 30, 2018 baada ya mshtakiwa Mhando kupitia wakili wake Martin Matunda kuitaarifu mahakama kuwa wamefunga ushahidi dhidi ya kesi hiyo ambayo mshtakiwa Mhando amejitetea mwenyewe.

Aidha mahakama imewataka pande zote mbili, upande wa serikali na ule wa utetezi kuwasilisha hoja za majumuisho ya mwisho ya kesi hiyo Novemba 15, 2018.

Kabla ya kufungwa kwa kesi, akihojiwa na wakili wa upande wa mashtaka kutoka Takukuru Leornad Swai, Mhando amedai kuwa mchakato mzima wa kuingia ubia wa kuhamisha TBC kutoka mfumo wa analogia kwenda Digitali ( Star times) ulifanywa na bodi ya TBC.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, Mhandi amesema hakuna kitu alichofanya bila ridhaa ya bodi, kwani bodi ndiyo iliniagiza nifanye mchakato wa awali na ulipokamilika niliwasilisha kwao mwaka 2009 na mpaka naondoka TBC hakuna mtu aliyezungumzia suala hilo la mkataba siyo Serikali wala bodi hiyo.

Alipoulizwa juu ya tofauti za mkataba aliongia na Chanel 2 na ule wa Startimes Mhando amedai, yeye aliandikishiana mkataba wa makubaliano na Chanel 2 kwa sababu walitaka kuhakikishiwa kama wangeitwa na bodi ya TBC ambao aliusaini yeye peke yake hukumkataba halisi waliingia na Star times ambao alisaini yeye Mhando na Mwanasheria.
"Mkataba wa Startimes ndiyo mkataba halisi ambao tuliandikishiana baada ya bodi kurudhia". Amedai Mhando.
Amesema kutokana na sheria na taratibu za manunuzi mkataba halali lazima usainiwe na watu wawili ambao ni Mkurugenzi na Mwanasheria na pia lazima uwena muhuri wa shirika.

 Mkataba wa makubaliano ya awali baina  ya TBC  na kampuni ya Channel 2 group ya Dubai niliusaini mimi kama Tido kwa kuwa walikuwa wanataka kuthibitishiwa.

Miongoni mwa  mashahidi  wa upande wa mashtaka ambao wametoa ushahidi  katika kesi hiyo ni  Afisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, Mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana huku kwa upande wa utetezi, mashtakiwa Mhando amejitetea Mwenyewe.

Katika kesi hiyo Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh. Milioni 887.1

IGP SIRRO AKUTANA NA IGP WA RWANDA

0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda DCG Dan Munyuza, leo 30/10/2018 walipokutana katika eneo la Kirehe karibu na mpaka unaotenganisha nchi hizo mbili Tanzania na Rwanda ambapo baadae watafanya kikao cha Ujirani mwema kitakachojadili masuala mbalimbali ya kiusalama baina ya nchi hizo mbili. Picha na Jeshi la Polisi Tanzania.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kushoto) akiwa amefuatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda DCG Dan Munyuza, leo 30/10/2018 wakivuka mpaka unaotenganisha nchi hizo mbili Tanzania na Rwanda na kuingia eneo la Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera kwa ajili ya kikao cha ujirani mwema kitakachojadili masuala mbalimbali ya kiusalama baina ya nchi hizo mbili. Picha na Jeshi la Polisi Tanzania.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda DCG Dan Munyuza, wakati wa kikao cha ujirani mwema kinachofanyika Rusumo wilayani Ngara mpakani mwa Tanzania na Rwanda leo 30/10/2018. Picha na Jeshi la Polisi Tanzania.
Kikao kikiendelea

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA HICHO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha amati Kuu ya CCM katika ofisi ndogo za chama hicho mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo Okotoba 30, 2018.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu Mwenyekiti wake (Bara) Ndg. Philip Mangula na Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally, baada ya kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM katika ofisi ndogo za chama hicho mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo Okotoba 30, 2018.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM katika ofisi ndogo za chama hicho mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo Okotoba 30, 2018. Katikati yao ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai

PICHA NA IKULU

KAMATI ZA BUNGE ZAENDELEA NA VIKAO VYAO JIJINI DODOMA

0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Selemani Moshi Kakoso akifafanua jambo mbele ya Kamati hiyo ilipokutana na Shirika la Reli nchini TRC hii leo Jijini Dodoma na kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ujenzi wa Reli ya mpya ya Kiwango cha Kimataifa (SGR).
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati hiyo Selemani Moshi Kakoso ilyokutana na Shirika la Reli nchini TRC hii leo Jijini Dodoma na kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ujenzi wa Reli ya mpya ya Kiwango cha Kimataifa (SGR).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Injinia Isack Aloyce Kamwelwe akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipokutana na Shirika la Reli nchini TRC hii leo Jijini Dodoma na kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ujenzi wa Reli ya mpya ya Kiwango cha Kimataifa (SGR).
 Mwenyekiti wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mussa Azan Zungu akifuatilia uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018  iliyowasilishwa na Meja Jenerali A. Bahati mbele ya Kamati Bungeni Jijini Dodoma
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hussein Alli Mwinyi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Florens Turuka  wakiwa mbele ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wizara hiyo ilipoenda kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018  pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019.
 Wajumbe wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama  na Watendaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  wakifatilia uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018  iliyowasilishwa na Meja Jenerali A. Bahati mbele ya Kamati Bungeni Jijini Dodoma

PICHA NA OFISI YA BUNGE

Rukwa wajipanga kutumia Mkaa mbadala kuokoa mazingira

0
0
Mkoa wa Rukwa umejipanga kupambana na uharibifu wa mazingira kwa kuhakikisha wanatumia rasilimali za makaa ya mawe yanayopatikana katika kijiji cha Nkomolo tu, Wilayani Nkasi kuwa mkaa mbadala na kuanza kutumika majumbani.

Mkakati huo ulioanza kwa mafunzo ya siku mbili yaliyoendeshwa na mtaalamu wa makaa hayo kutoka katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Bi. Halima Mpita ukiwakutanisha makatibu tawala wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, madiwani, wataalamu wa mazingira kutoka katika halmashauri, mashirika yasiyo ya kiserikali yanayoshughulikia mazingira pamoja na wazee maarufu.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya nishati mbadala inayotokana na makaa ya mawe mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachima Wangabo amesema kuwa tunafanya kila liwekanalo kuokoa kile kilichopo na kuhakikisha kwamba mazingira hayaendelei kuharibiwa kwa namna yoyote hasa masuala ya kukata miti kwaajili ya kuni na mkaa.

“Makaa ya mawe yapo kilomita 45 toka hapa tulipo (sumbawanga mjini), yale makaa yam awe tunaweza kuyatumia kama mkaa mbadala kwa matumizi ya majumbani, na hili ndio lengo la mafunzo ya leo, mtaalamu wetu atatueleza kule Songwe wanafanyaje, kile wanachofanya kule watatumegea hapa uzoefu wao, na sisi tutaona na kujipanga tufanye nini na haya makaa yam awe tuliyonayo,” Alisema.

Ameongeza kuwa endapo mafanikio yatapatikana na kuanza kutumia makaa ya mawe majumbani, kiwango kikubwa cha uvunaji wa miti kitaokolewa na kutahadharisha kuwa mpango huo ukifanikiwa gharama za kununua bidhaa hiyo isiwakatishe tamaa wanunuzi ili wasirudi tena kukata miti na hatimae kutofikia lengo.

Kwa upande wake Bi. Mpita alisifu muitikio wa wadau wa mazingira wa mkoa wa Rukwa na kusema kuwa endapo nguvu hiyo itafikisha elimu kwa wananchi basi mkoa wa Rukwa utakuwa wa kuigwa na kuongeza kuwa atashirikiana bega kwa bega ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana kwa faida ya kizazi hiki na kijacho.

Akieleza faida za mkaa unaozalishwa na makaa yam awe alisema, “Haya makaa ni suluhisho la kudumu juu ya matumizi mbadala la mkaa wa miti kwa kuwa miamba ya makaa ya mawe ni ya asili na inaweza kuvunwa zaidi ya miaka 500. Pia unaweza kuwaka kwa saa 3 hadi 4  mfululizo na hautoboi wala kuchafua sufuria, ni mkombozi wa ajira maana uanzishaji wa kiwanda chake ni rahisi na majivu yake hustawisha mimea,” Alisisitiza.

Ili kuuwasha Mkaa wa makaa ya mawe unahitaji jiko la mkaa lililotengenezwa kwa udongo, utawasha vijiti viwili maalum vya kuwashia moto utaweka vipande 4 hadi 5 acha viwake pamoja kwa dakika 3, ongeza mkaa na uache uko kwa dakia 15 hadi makaa ubadilike na kuwa rangi nyekundu kuanzia chini. Vipande 34 vya mkaa vinatosha kumaliza mapishi ambapo mkaa huo huwaka kwa masaa 3 hadi 4.
 Bi. Halima Mpita (Kulia) akitoa ufafanuzi juu ya matumizi ya mkaa wa makaa ya mawe kwa wadau mabalimbali waliohudhuria katika semina ya mafunzo hayo ya nishati mbadala inayotokana na makaa ya mawe mkuu wa mkoa wa Rukwa 
Mkaa wa mawe unavyowaka. 

Nembo ya Red Cross haitumiki kwa matumizi binafsi

0
0
 Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
Tanzania Red Cross imezindua kampeni ya mafunzo ya kutambua matumizi  nembo za Red Cross kutokana na baadhi ya watu au Taasisi kutumia nembo hiyo wakati hawana mamlaka ya kutumia nembo hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo Katibu Mkuu wa Tanzania Red Cross Julius Kejo amesema kuwa uzinduzi wa kampeni hiyo ni kuwajuza wananchi kuhusiana na nembo hiyo juu inavyotumika na Red Cross na hakuna mtu yeyote anayeruhusiw kutu,ia nembo.

Kejo amesema kuwa nembo ya Red Cross kwa nchini wanaweza wakawa wanatumia bila kujua kuwa hawana mamlaka ya kutumia nembo hiyo ni kwa ajili ya kulinda masilahi ya nembo hiyo isijekatumika katika masuala ya uhalifu na kuondoa maana ya Red Cross.

Kejo amesema  kampeni hizi zitatoa mafunzo jinsi ya matumizi kwa ujumla duniani kote hivyo basi ni jukumu la kila mtu kuilinda nembo hiyo 

Katibu Mkuu huyo amewaasa  wanahabari kufikisha ujumbe kwa watu,taasisi pamoja na mashirika binafsi ambao wamekua wakitumika biaadhi ya nembo hizo kuwa si sheria kutumia nembo hizo.

Kejo amesema Red Cross kazi ya Red Cross  ni kukabiliana maafa, kuelimisha jamii kuhusu kujikinga na majanga  mbalimbali ili kupunguza madhara ya majanga hayo pamoja na  kuunganisha wanafamalia na ndugu waliopotezana wakati wa majanga au matatizo mengine ya kijamii.
 Katibu Mkuu wa Red Cross Tanzania Julius Kejo akizungumza na waandishi wa habari wakati akizindua kampeni kuelimisha kuhusiana na nembo ya Red Cross uzinduzi huo umefanyika  jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Malengo wa Kamati ya Red Cross Kimataifa Andrea Heath akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mchango wa Red Cross katika majanga mbalimbali.
 Mwakilishi wa Red Cross kutoka nchini Hispania Monica Cardena akizungumzia kuhusiana na kazi za Red Cross.
Nembo za Red Cross ambazo ndizo zinazotumika 

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA MASHIRIKA YA KIMATAIFA KUFANYIKA JIJINI ARUSHA NOVEMBA 03

0
0
Na Ahmed Mahmoud 
Wananchi wa jiji la Arusha wametakiwa kuchangamkia fursa zinazotolewa na mashirika ya kimataifa yanayofanyakazi ndani ya jiji hilo lengo likiwa ni kuangalia fursa zinazotokana na mashirika hayo kukuza vipato vyao na uchumi wa jiji hilo.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha  Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro amebainisha kuwa Maonyesho hayo Pili ya mashirikia ya kimataifa yanayojulikana kwa jina la (Internation Organization Arusha open day)yanatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi ya tarehe 3 mwezi novemba katika viwanja vya lakilaki nje kidogo ya jiji la Arusha.

Amesema kuwa wananchi watatakiwa kuwa na vitambulisho kuweza kushiriki maonyesho hayo ambayo ni mara ya pili yanafanyika na mgeni rasmi atakuwa Waziri wa mambo ya nje kikanda na Afrika mashariki Balozi Agastine Mahiga na usafiri utakuwepo maeneo yote ya jiji hili na kiingilio ni bure

Amesema kuwa maonyesho hayo ambayo yanafanyika katika majiji matatu tu ya Durban New York na Arusha mwakani kitaifa yatafanyika jijini Dar es salaam na hivyo kutoa fursa kwa taasisi mbali mbali za kimataifa ambazo zipo hapa nchini kuweza kushirikiana na wananchi katika kuonyesha shughuli wanazozifanya hapa nchini lengo likiwa ni wananchi kujua shughuli wanzozifanya na fursa gani wanaweza kushirikiana.

Amesema kuwa maonyesho hayo ambayo mwaka jana yalikuwa ya majaribio hivyo kuwataka wananchi wengi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maonyesho hayo ikiwa ni sehemu ya kukutana na kuweza kujua mashirika hayo yanafanya nini na yapo eneo gani kuweza kujua fursa walizonazo.  
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Kalist Lazaro akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani ofisini kwake jijini Arusha wakati akitoa maelezo ya maonyesho ya kimataifa yatakayofanyika jumamosi ya Tarehe tatu mwaka huu picha na Mahamoud Ahmad Arusha

ROCK CITY MARATHON 2018 ILIVYONOGA: Watanzania, Wakenya wang’ara Rock City Marathon

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella  (katikati) akikabidhi zawadi ya cheti,medali na pesa taslimu kiasi cha sh mil. 4 kwa mwanariadha Mourice Masima Kutoka Kenya  aliemaliza katika nafasi ya kwanza kwenye mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza mwishoni  mwa wiki baada ya kutumia  muda wa saa 2:19:14.
 Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta ya TIPER, Bw Emmanuel Kondi akikabidhi  zawadi ya cheti,medali na pesa taslimu kiasi cha sh mil. 4 kwa mshindi wa kwanza mbio za km 42 kwa wanawake mwanariadha Naomi Jepngetich kutoka Kenya  aliyetumia muda wa saa 02:44:19 kukamilisha mbio hizo. Kulia  ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella. TIPER ni moja ya wadhamini wakubwa wa mbio hizo.
 Mwakilishi kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bi. Flora Ndutta akikabidhi  zawadi ya cheti,medali na pesa taslimu kiasi cha sh mil. 3 kwa mshindi wa kwanza mbio za km 21 mwanariadha Failuna Matanga kutoka Tanzania.
 Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MWAA) Bw Silas Lucas (kulia) akikabidhi zawadi  kwa mshindi wa kwanza mbio za KM 21 Emmanuel Giniki kutoka Tanzania alietumia saa 1:04:09 akifuatiwa na Mkenya Daniel Kayioki alietumia muda wa saa 1:04:47.
 Baadhi ya washiriki wa mbio za km 5 wakimalizia mbio hizo zilizohitimishwa kwenye viunga vya jengo la Rock City Marathon.

RAIS DKT SHEIN AZINDUA KLINIKI YA MENO KIVUNGE KASKAZI UNGUJA.2

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi  wa kliniki ya Meno ambayo katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja,kliniki hiyo inaendeshwa kwa usimamizi wa Taasisi ya HIPZ kutoka Nchini Uingereza ambayo inatoa huduma za Afya katika Hospitali hiyo pamoja na Makunduchi Hospital Mkoa wa Kusini Unguja(kulia) Waziri wa Afya Mhe.Hamad Rashid Mohamed[Picha na Ikulu.] 30/10/2018.

Faida za Sim Account kwa wateja wa Benki ya CRDB


Rais Dk. Shein Atembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja leo

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimskiliza Kaimu Mkurugenzi Tiba Dr. Fadhil Abdallah, akitowa maelezo ya Ujenzi wa Jengo Jipya la Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati alipotembelea Mradi huo wa ujenzi wake katika eneo la Hospitali ya Kivunge Zanzibar, kulia Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed na kushoto Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe Vuai Mwinyi.

Jengo Jipya la Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja likiwa katika Ujenzi wake katika eneo la hospitali hiyo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Eng. wa Kampuni ya World Class Engineering Contractars Ndg. Joshua Christopher Nyari, akitowa maelezo ya michoro ya ujenzi wa Hospitali hiyo inayojengwa katika maeneo ya Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Daktari Dhamani wa Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja Dr. Tamim Hamad Said, akitowa maelezo ya michoro ya jengo jipya la Hospitali ya Kivunge kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, wakati alipotembelea Mradi huo wa Ujenzi wa Hospitali hiyo katika eneo la Hospitali ya Kivunge.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisisitiza jambo wakati akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar, wakati alipotembelea Mradi wa Jengo la Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja. kulia Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed na kushoto Daktari Dhamana wa Hospitali ya Kivunge Dr. Tamim Hamad Said na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Abdallah.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja, kushoto Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed, wakitembelea Mradi huo wa ujenzi wa jengo hilo katika viwanja vya Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja.   
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed akitowa maelezo ya Mradi huo wa ujenzi wa jengo la Hospital ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea Mradi huo, akiwa katika ziara yake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akielekezwa  na kuonesha moja ya sehemu ya jengo hilo na Kaimu Mkurugenzi Tiba Wizara ya Afya Zanzibar na Dr. Fadhil Abdallah wakati akitembelea Mradi huo wa Ujenzi wa Hospitali Mpya ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja.wakati wa ziara yake Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu)  

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWASILI TANGA KWA ZIARA YA KAZI

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Tanga kuanza ziara  ya kazi mkoani humo, Oktoba 30, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Tanga kuanza  ziara ya  kazi mkoani humo Oktoba 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DC CHONGOLO ASITISHA UCHIMBAJI WA KOKOTO KWA MUDA BOKO,JIJINI DAR

0
0

Mkuu wa Wliaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amekiri kuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi kwenye Wilaya hiyo, ambapo amesema migogoro hiyo inaibuka kutokana na kutengenezwa na watu.

DC Chongolo ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea eneo la Uchimbaji Kokoto katika eneo la Boko jijini Dar es Salaam, eneo lililokumbwa na migogoro baina ya Wawekezaji na Wachimbaji hao.

Akizunguma na Globu ya Jamii na Michuzi TV, Mhe. Chongolo amesitisha shughuli za uchimbaji kokoto katika eneo hilo mpaka watakapokaa kwa pamoja Novemba Mosi 2018, kati ya Wachimbaji wa Kokoto,wamiliki wa eneo na Serikali ili kusuluhisha mgogoro huo ikiwa sambamba na kuangalia namna ya kuendelea au kuacha shughuli hizo.

Chongolo amesema katika maeneo hayo ya uchimbaji watahakikisha yanakuwa na Leseni ya Manispaa, Leseni ya Madini, Cheti cha TRA, Mazingira, Mikataba kwa Waajiriwa, Malipo ya ushuru wa Madini kwa Manispaa na usajili katika uzalishaji Madini. "Kwenye haya maeneo ya uchimbaji Kokoto wanachimba kiholela, uharibufu ni mkubwa sana, magari yanapita juu chini wamechimba mashimo, mvua ikinyesha wanakimbilia wanajificha kwenye haya mashimo, ikileta madhara kwa watu malalamiko yote yanakuja kwa Serikali’’, amesema DC Chongolo.

Kwa upande wake mmoja wa Wawekezaji katika eneo la Boko, Mwakilishi wa Kampuni ya Usafirishaji na Uchimbaji wa Kokoto ya Al-Hushoom Evestment, Badi Lema amedai wao ni wamiliki halali wa eneo hilo, amesema kuna Watu wamevamia eneo hilo hivyo waliiomba Serikali ifike kwenye eneo hilo kujionea uvamizi huo.

Badi amesema licha ya kulinda eneo hilo, Wavamizi hao wameendelea kuingia kwenye eneo hilo kwa ajili ya kufanya shughuli za uchimbaji wa kokoto. Hata hivyo moja ya Wananchi wanaofanya shughuli hizo za Uchimbaji amedai kuwa eneo hilo wamepewa na Wazo, wamedai eneo hilo walipewa kama Wananchi wa Boko. Pia baadhi ya Wachimbaji hao wamedai kuwa ruhusa ya Uchimbaji Kokoto katika eneo hilo la Boko wamepewa na Serikali ya Mtaa.
Baadhi ya Wachimbaji wa Kokoto wakiendelea na shughuli zao katika eneo linalodaiwa kuvamiwa na watu hao,ikiwemo uvunjwaji wa sheria za utunzaji mazingira,na utaraibu wa kuchimba kokoto hizo

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akizungumza mbele ya Wachimbaji Kokoto katika eneo la Boko,ambalo linadaiwa kuvamiwa na wananchi huku wakiendeleza shughuli za uchimbaji bila kufuata utaratibu/sheria.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Chongolo akiwa na watalaamu wake wakiondoka kwenye eneo hilo la wachimbaji Kokoto eneo la Boko,mara baada ya kujionea hali halisi na kuamuru uchimbaji kokoto katika eneo hilo usitishwe mara moja,mpaka hapo watakapokutana siku ya Alhamisi na kuamua nini kifanyike.

Mmoja wa wachimbaji Kokoto katika eneo hilo akieleza jambo kwa mkuu wa Wilaya Mh.Daniel Chongolo (hayupo pichani),aliyefika kujionea hali halisi ya eneo hilo.

DIRA YA KITAA MPAMBANAJI NA MTAFUTAJI

MAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 31,2018

Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images