Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WANUNUZI WA KOROSHO JIJINI DAR ES SALAAM NA KUTOA MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSU BEI YA KOROSHO

$
0
0
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanunuzi wa zao la Korosho katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na kutoa msimamo wa Serikali kuhusu bei ya Korosho kuwa isipungue shilingi 3000 kwa kilo moja.
Wadau na Wanunuzi wa Korosho wakiwa wanasikiliza Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokutana nao na kuzungumza nao jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

INTRODUCING "TUONE VIDEO" BY FRIDA AMANI FT G NAKO

INTRODUCING NEW SONG "UKINIPENDA" FROM TANZANIA FINEST R BYSER ft PASHA

KILUWA GROUP YAWAPOKEA WADAU WAKE WA UWEKEZAJI KUTOKA CHINA,WADHAMIRIA KUWEKEZA KWENYE BIDHAA ZA NGOZI

$
0
0

 Mwenyekiti wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd,Mohamed Kiluwa ( wa nne kulia) pamoja na ujumbe wake wakiwa na wageni wao katika picha ya pamoja kwenye moja ya chumba maalum cha kufikia Wageni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,mara baada ya kuwasili Oktoba 27,2018 jijini Dar kutoka nchini China .Kampuni hiyo yenye ujumbe wa watu wa Watano umekuja nchini kwa mwaliko wa kampuni ya Kiluwa Group Ltd kufanya mazungumzo mbalimbali yakiwemo ya kutafuta fursa za uwekezaji ikiwemo pia kuonana na uongozi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC).
 Mwenyekiti wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd,Mohamed Kiluwa  pamoja akipokea zawadi aliyoletewa na mgeni wake,Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yinengda New Material Technology,Mayi Hong mara  kwenye moja ya chumba maalum cha kufikia Wageni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,mara baada ya kuwasili Oktoba 27,2018 kutoka nchini China.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd,Mohamed Kiluwa  pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yinengda New Material Technology,Mayi Hong wakimsikiliza Meneja wa kampuni ya Kiluwa Group Ndugu Madoweka (ambaye ni mkalimani wa lugha ya Kichina),akifafanua jambo kurahisisha mawasiliano kwa mgeni wao Ndugu Mayi Hong akiwa ameambatana na ujumbe wake wa watu wanne kutoka kwenye kampuni yake ambayo inajishughulisha na uzalishaji/utengenezaji wa bidhaa za ngozi nchini China.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Group,Naima Kiluwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yinengda New Material Technology,Mayi Hong,mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar  Oktoba 27,2018.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Group,Naima Kiluwa pichani kati akiwa ameambatana na Wageni wake mara baada ya kuwapokea jana uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea nchini Chaina,Pichani kulia ni Mkurugenzi Mtendani wa kampuni ya Yinengda New Material Technology,Mayi Hong.kampuni hiyo inajishughulisha na uzalishaji/utengenezaji wa bidhaa za ngozi nchini China.

TAARIFA KUHUSU MAHAFALI YA 12 CHUO KIKUU CHA ARDHI

MWIJAGE: VIWANDA VIDOGO, BIASHARA NDOGO VINA MCHANGO MKUBWA KATIKA UCHUMI, MAENDELEO, USTAWI WA NCHI

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema viwanda vidogo na vya kati vina mchango mkubwa katika uchumi, maendeleo na  ustawi wa nchi yoyote, kwa kuwa vinatoa ajira kwa watu wengi ikilinganishwa na viwanda vikubwa hivyo havipashwi kubezwa kwa namna yoyote.

Mhe. Mwijage ameyasema hayo Oktoba 28, 2018 wakati akihitimisha Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa yaliyofanyika Kitaifa kwa mara ya kwanza katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 23.

“ Najua kuna watu wanapenda kubeza lakini napenda niwaeleze nafasi ya viwanda na biashara ndogo katika uchumi, maendeleo na ustawi ya nchi yoyote, Sisi Tanzania tangu uhuru mpaka leo tuna viwanda 54,000, lakini asilimia 99 ni viwanda vidogo, vidogo sana na vya kati; sisi siyo kilema kwenye viwanda nchi zote zipo hivyo, viwanda vyenye tija  na vinavyoajiri watu wengi ni viwanda vidogo, vidogo sana na vya kati” alisema Mwijage.

 Amesema pamoja na viwanda vidogo na vidogo sana kuwa na tija katika uchumi wa nchi viwanda hivyo pia ni shule na vinaweza kumilikiwa kirahisi huku akisisitiza kuwa lengo la Serikali ni kujenga uchumi jumuishi ambao nji rahisi ya kuufikia ni kupitia uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO), Prof.Sylvester Mpanduji ametoa wito kwa Watanzania kuwa, ili waweze kushiriki katika Ujenzi wa Uchumi waViwanda hawana budi kuanza na viwanda vidogo ambavyo SIDO itakahakikisha vinakuwa endelevu.

Akizungumzia Maonesho ya Viwanda Vidogo Prof. Mpanduji amesema yamesaidia kuwaleta wajasiriamali pamoja kuonesha bidhaa zao na kubadilisha uzoefu katika teknolojia, usindikaji na masuala mengine yanayohusu bidhaa wanazozalisha kupitia viwanda vidogo na vya kati.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji  wa Mkoa huo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage wakati wa Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa  katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani humo,kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018(kulia) Balozi wa Nigeria nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Shahabi Issa Gada.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza na wajasiriamali mara baada ya kutembelea mabanda yao katika Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi,kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza na baadhi ya viongozi wa World Vision na Halmashauri ya Wilaya ya Itilima alipotembelea banda lenye bidhaa za sabuni zinazozalishwa kupitiakiwanda kidogo kilichopo wilayani Itilima, katika Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi, kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
 Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akiwasalimia wananchi wakati wa Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi, kuanzia Oktoba  23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.  

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


NAIBU WAZIRI HASUNGA AFUNGA TAMASHA LA UTAMADUNI WA MTANZANIA

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akizungumza na  Athumani Issa wakati alipotembelea nyumba ya kabila la Wamwela katika kijiji cha Makumbusho wakati wa   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akiwasaidia akina Mama wa kabila la Wamwela  kutwanga nafaka  wakati alipotembelea nyumba ya kabila la Wamwela katika kijiji cha Makumbusho wakati wa   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akipewa kibuyu chenye  pombe na Halima Abdallah ambacho kimekuwa kikitumiwa na kabila hilo kunywea pombe  wakati alipotembelea nyumba ya kabila la Wamwela katika kijiji cha Makumbusho wakati wa   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es Salaam 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akiangalia baadhi ya mabaki ya samaki aina ya nguva aliyekutwa amekufa kando kando mwa bahari ya Hindi mkoani Lindi wakati alipotembelea mabanda  kabla ya   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es Salaam 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga (katikati) akiwa na Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi wakiwa wameongozana na   Wakurugenzi pamoja na Wazee wa kabila la Wamwela wakati kutembelea nyumba ya kabila la Mwela katika kijiji cha Makumbusho  kabla ya kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es salaam 
Baadhi ya vikundi vya ngoma vikitumbuiza wakati wa  kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika kijiji cha Makumbusho    jijini Dar es salaam 
                              ( PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA)   

NAIBU WAZIRI ASEMA IGENI UTARATIBU WA KILA MTOTO KUWA NA MLEZI WAKE KATIKA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT
VITUO vya kulelea na kutunza watoto yatima na wale walioko kwenye mazingira hatarishi nchini vimetakiwa kuiga utaratibu wa Kituo cha Shirika Masista wa Upendo wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora wa kumwekea kila mtoto mdogo mlezi na mwangalazi wake wa karibu wakati wote ili kuwafanya wasijione wapweke.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza kwa ajili ya kuwapa sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake.

Alisema utaratibu unaotumiwa na Kituo hicho wa kumwakea mtoto mlezi na mwangalizi wake wa karibu ambaye siye Sista ni njia nzuri ya kuwasaidia watoto kutojiona kama yatima kwa kuwa wapweke na kuisi yule ndiye mzazi wake.

Aidha Naibu Waziri huyo alilipongeza Shirika hilo kwa malezi na huduma nzuri wanazotoa kwa watoto hao na wazee wasijiweza jambo ambalo limefanya waishi kwa furaha na ushirikiano miongoni mwao.

Alisema kazi inayofanywa na Shirika hilo ni nzuri na kubwa ambayo kimsingi ilikuwa ifanywe na Serikali lakini wao wameamua kwa upendo wao kuwalea na kuwatunza watoto ambao wamepoteza wazazi wao na wazee wasijiweza ambao wametelekezwa na ndugu zao.

Dkt. Ndumbalo aliongeza kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikano kwa kadiri itakavyowezekana kwa Shirika hilo na mengine ambayo yanatunza watoto walioko katika mazingira hatarishi na wazee wasiojiweza ili nao wajione kuwa ni Watanzania sawa na wengine.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro akisalimia wazee  leomara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza  kwa ajili ya kuwapa  sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro akimsalimia Mzee Lucas Simon(kushoto)  leo mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza  kwa ajili ya kuwapa  sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake.
 Kaimu Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa Wamisionari wa Upendo wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Sisita Emmanuella MC (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro(katikati) leo mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza  kwa ajili ya kuwapa  sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro akikabidhi maziwa na sukari kwa Masisita mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza  kwa ajili ya kuwapa  sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ leo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Airtel Tanzania yatoa msaada kwa kituo cha yatima Morogoro

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia kitengo chake cha huduma kwa wateja imetoa msaada wa vitu mbali mbali kwa kituo cha yatima cha Mgolole Orphanage Center, Morogoro.

Msaada huo ni pamoja na vitanda, neti, magodoro, deep freezer, chupa za chai, hot pot, sukari, sahani, sabuni, nepi, pampers na toy za watoto vyote vikiwa na thamani ya TZS 18 milioni.

Kutoa kwa msaada huo ni muendeleo wa kampuni ya Airtel Tanzania kupitia programu ya Airtel Tunakujali ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo kukubali kutoa sehemu ya mshahara wao ili kusaidi huduma za kijamii na hasa kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Akiongea mara baada ya kutoa msaada huo kwa kituo hicho cha Mgolole cha Morogoro, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adriana Lyamba alisema muda mrefu wafanya kazi wa Airtel kupitia Airtel tunakujali imekuwa ikitembelea na kusaidia vituo mbali mbali vya yatima ikiwa ni pamoja na kuwapa misaada mbali mbali.

Leo ni siku yenye furaha sana kwetu zote kwani mayatima ni sehemu ya Jamii yetu na ni muhimu kuwapa upendo pamoja na kuwafariji. Hiki ambacho tumekuja kutoa leo hapa  ni kidogo lakini nina uhakika kitagusa mioyo yenu lakini zaidi ni kujua tuko pamoja nanyi na tunawajali sana, alisema Lyamba.

Naomba kutoa pongezi za dhati kwa wafanyakazi wenzangu wa Airtel kwa kukubali kutoa sehemu ya kipato chao na leo tumeweza kufika hapa. Lakini zaidi napongeza uongozi wa kampuni yetu kwa kukubali na kuridhia programu yetu hii hapa ya Airtel Tunakujali ambayo imekuwa ikituleta karibu na Jamii inayotuzunguka, alisema Lyamba.

Tunayo furaha kuweza kuwafikia watoto hawa ambao wako kwenye kituo hiki na dhamira yetu ni kuendelea kugusa maisha ya watoto wanaoishi kwenye mazingira mangumu na kuwafanya wajisikia kuwa sehemu ya familia ya Airtel, aliongeza Lyamba.

Kwa upande wake, Makamu Mama Mkuu wa kituo cha Mgolole Sista Valeria Mnyanzaga alisema ni furaha kwa kampuni kubwa ya Airtel kuguzwa na maisha ya watoto wanaoishi kwenye kituo hiki na hatimaye kuja kutoa msaada na kutuunga mkono.
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adriana Lyamba (kulia) akikabidhi msaada kwa Makamu Mama Mkuu wa kituo cha yatima cha Mgolole, Morogoro. Airtel Tanzania kupitia mradi wake wa Airtel Tunakujali walitembelea kituo hicho pamoja na kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye dhamani ya TZS 18 milioni mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adriana Lyamba (kulia) akikabidhi msaada wa dogoro kwa Makamu Mama Mkuu wa kituo cha yatima cha Mgolole, Morogoro. Airtel Tanzania kupitia mradi wake wa Airtel Tunakujali walitembelea kituo hicho pamoja na kutoa msaada wa vitu mbali mbali vyenye dhamani ya TZS 18 milioni mwishoni mwa wiki. Kati kati ni Meneja wa Kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Tanzania Deogratius Hugo. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

HELIKTOPA NA MAJONZI YA THE BLUES NDANI YA OKTOBA

$
0
0
Oktoba 22, 1996, makamu mwenyekiti wa Chelsea, Mathew Harding alifariki dunia kwenye ajali ya helikopta, wakati akitoka kuangalia mechi ya Bolton Wanderers dhidi ya Chelsea.

Oktoba 27, 2018, mmiliki na mwenyekiti wa Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha, amefariki dunia kwenye ajali ya helikopta, wakati akitoka kuangalia mechi ya Leicester City na West Ham.

Chelsea na Leicester City, zote hutumia rangi ya bluu na walipokezana ubingwa wa EPL, 2015, 2016 na 2017.

SRIVADDHANAPRABHA WA LEICESTER CITY.

Mwaka 2010, Vichai Srivaddhanaprabha aliinunua Leicester City ikiwa daraja la kwanza na kuwekeza pesa ya kutosha iliyoisaidia klabu hiyo kupanda ligi kuu 2014/15 na kutwaa ubingwa 2015/16.

Katika orodha wamiliki wa vilabu wenye mapenzi ya dhati navyo, Srivaddhanaprabha anakaa kwenye nafasi za juu kabisa akiwa na rekodi ya kuhudhuria asilimia kubwa sana ya mechi za Leicester City.

HARDING WA CHELSEA.
Mwaka 1993, mwenyekiti wa Chelsea, Ken Bates, alitoa wito kwa matajiri kuwekeza klabuni hapo ili kuokoa jahazi lilikuwa likielekea kuzama.

Harding, kama shabiki wa Chelsea tangu utotoni, akajitokeza na kuwekeza pauni ml. 26 zilizoiokoa The Blues na kuanza kujenga msingi mpya wa mafanikio ya sasa.

Kifo chake kilikuja miezi saba kabla ya Chelsea kutwaa taji kubwa la kwanza baada ya miaka 27, waliposhinda Kombe la FA.

Harding pia alitoa pesa zake kujenga moja ya majukwaa ya Stamford Bridge lenye uweso wa kuchukua watu 10,884. Kwa heshima yake, jukwaa hilo sasa linaitwa Mathew Harding Stand, kukiwa na kaulimbiu ya One Of Our Own.

KAMATI YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YAKUTANA NA WIZARA YA UTUMISHI

$
0
0
 Kamati ya Bunge ya Utawala  na Serikali za Mitaa ikiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo imekutana na  Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais, Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Mwanne Nchemba akisisitiza jambo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kamati hiyo imekutana na  Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais , Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika akitolea ufafanuzi hoja za wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati Kamati hiyo ilipokutana na Wizara yake  kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais , Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma.

Wasichana 600 kunufaika na kampeni ya kujiweka salama wakati wa hedhi ya taasisi ya Her Africa

$
0
0
Katika dhamira yake ya kuhakikisha Watoto wa kike wanapata elimu kuhusu umuhimu wa usafi katika kipindi vya hedhi, taasisi ya Her Africa imezindua kampeni ya kitaifa inayojulikana kama “Hedhi yangu, Furaha yangu” katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike ambayo huadhimishwa tarehe 11, Oktoba kila mwaka kama ilivyopangwa na Umoja wa Mataifa (UN).

Kupitia kampeni hii mifuko maalum itatolewa kwa wasichana ambao ndani yake kukiwa na mahitaji muhimu katika kipindi cha hedhi kama vile, paketi za pedi za kutumia mara moja na za kutumia zaidi ya mara moja, vitambaa laini vya kujisafishia, chupi na khanga mpya, sabuni ya kuogea pamoja na ya kufulia na dawa ya Dettol. Vifaa vinavyopatikana katika kifurushi hiki vimetolewa na wadau mbalimbali katika jamii kama msaada kutokana na jitihada kubwa zilizofanywa kupitia mitandao ya kijamii na taasisi ya Her Africa kufanya  uhamasishaji wa kulielezea tatizo na kutafuta kuungwa mkono kulipatia ufumbuzi.

Meneja Miradi wa Her Africa, Salha Kibwana amesema “Wanawake wengi na wasichana katika jamii zetu hupata changamoto kubwa katika kipindi cha mzunguko wao wa mwezi wa siku za hedhi, kutokana na kutoweza kumudu kununua pedi za kutumia, ukosefu wa elimu kuhusiana na hali hiyo, imani za mila ambazo zinawafanya wengi kuamini kuwa suala la hedhi halipaswi kuongelewa, ukosefu wa mazingira rafiki ya kujihifadhi mtu anapokuwa kwenye hali hiyo kama vile vyoo na maji safi ya kutumia. Changamoto hizo zote zinasababisha watumie vifaa vya kuwasitiri visivyofaa ambavyo vinaweza kuwasababishia kupata maradhi.”

Naye Zena Tenga, kutoka taasisi hiyo ya Her Africa, aliongeza kusema “Kampeni yetu hii imelenga kutoa elimu ya ufahamu kuhusiana na umuhimu wa usafi katika kipindi cha hedhi, kuwezesha kufahamu mzunguko wa siku za hedhi kwa mwezi kwa ajili ya kujiandaa, kujua dalili za kuingia kwenye siku za hedhi na mengineyo mengi.”

Kampeni hii imeungwa mkono kwa kiasi kikubwa na jamii, kampuni ya AIM Group Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kuhakikisha inashiriki kukabili changamoto za hedhi kwa kutoa msaada wa pedi 144 na kugharamia mifuko maalum 14 yenye vifaa vya hedhi ambayo ilitolewa kama msaada kwenye kituo cha Watoto yatima cha Hiari.

“Tumejitoa kusaidia kukabili changamoto hii kwa kuwa wanawake wengi na wasichana katika jamii wanapata shida wakati wa kipindi cha mzunguko wa siku zao za hedhi kwa mwezi, kutokana na kutoweza kumudu gharama za vifaa vya kuwasitiri, ukosefu wa elimu hiyo na imani potofu kuwa suala la hedhi ni mwiko kuongelewa hadharani. Wakati umefika sasa wa kuunganisha nguvu na kuunga mkono watu binafsi na taasisi ambazo zimejitoa kupambana kuondoa changamoto hizo.”alisema Ritha Tarimo kutoka kampuni ya AIM Group.
 Moja ya mwanzilishi wa mradi wa " Her Africa" akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka shule ya primary St Joseph kuhusu elimu hedhi kabla ya kutoka msaada wa mifuko maalum kwa wasichana hao yenye vitu muhimu vya kutumia wakatika wa kipindi cha hedhi.
Wanafunzi  kutoka shule ya msingi ya St Joseph wakionesha mifuko maalum waliyopokea kutoka kwa "Her Africa" yenye vitu muhimu vya kutumia wakatika wa kipindi cha hedhi. Her Africa imeanzisha kampeni ya "Hedhi yangu, Furaha Yangu" ambayo inatarajia kuwafikishia wasichana 600 mifuko hiyo maalum yenye vifaa vya hedhi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SWEDEN YASAINI MAKUBALIANO MAPYA NA SHIRIKA LA FEMINA, YATOA BILIONI 4.5 KUENDELEZA MPANGO MKAKATI 2018/20

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
UBALOZI  wa Sweden nchini umesaini makubaliano na shirika la Femina Hip ikiwa ni msaada wa kutekeleza mpango mkakati wa Femina Hip kwa mwaka 2018/2019. Katika makubaliano hayo  jumla ya shilingi bilioni 4.5 zimetolewa kwa shirika hilo ili kuendelea kukuza elimu ya afya ya uzazi, haki, uwezeshaji kiuchumi na uraia kwa vijana nchini. Makubaliano hayo yametiwa saini na Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Ulf Kallstig na mwanzilishi na Mkurugenzi mtendaji wa Femina Hip Dkt. Minou Fuglesang katika ofisi za ubalozi wa Sweden leo jijini Dar es salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa makubaliano hayo Ulf Kallstig amesema kuwa mchango wa Sweden utaboresha mipango ya Femina Hip inayolenga kuwawezesha vijana kutoka kona zote nchini hasa katika kuwajengea juhudi za kuwawezesha, kuboresha maisha ya vijana nchini na kuwajengea tabia ya uwajibikaji.

Aidha amesema kuwa, "Vijana wana jukumu muhimu katika kuiendesha Tanzania kuelekea taifa la uchumi wa kati wa viwanda na ni muhimu kwetu kuzishirikisha sauti za vijana katika mijadala ya kimaendeleo inayolenga kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu yanafanikiwa pamoja na ari ya ushirikishwaji na ustawi wa Tanzania" ameeleza Ulf.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Femina Hip Dkt. Minou Fuglesang amesema kuwa, " Femina Hip inashukuru kwa ushirikiano na ubalozi wa Sweden, tutaendelea kuchangia kazi zinazofanywa na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba katika kizazi hiki cha vijana hususani wasichana wanalindwa na kusaidiwa kuwa raia wema wenye kuwajibika ipasavyo" ameeleza Dkt. Minou.

Dkt. Minou amesema kuwa, asasi za kiraia ni chombo muhimu na zina nafasi ya kipekee katika kuwapa sauti wananchi na kwa Femina kwa miaka mingi imekuwa chombo kinachoaminiwa kwa kuimarisha kitengo cha uhamasishaji na ushirikiano kwenye mitandao ya shule za sekondari na mashirika ya ndani katika kufikisha ujuzi muhimu vijana kila kona nchini.

Mkurugenzi wa habari wa Femina Amabilis Batamula amesema kuwa, wakielekea miaka 20 ya Femina wanaishukuru sana serikali ya Tanzania na Sweden kwa kuwaunga mkono na  hadi sasa wanawafikia watu Milioni 15 kwa mwaka na kuna  zaidi ya klabu 2340 za Fema kwa  katika shule za sekondari kote nchini.

Aidha Batamula ameishukuru serikali kwa kuruhusu na kutambua mchango wa asasi za kiraia  ikiwepo Femina katika kuwajenga vijana katika ujenzi wa taifa.

Pia amesema kuwa katika wiki ya vijana iliyohitimishwa kitaifa Mkoani Tanga, mgeni rasmi Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alipendekeza uwepo wa Klabu za Fema katika shule zote za serikali na binafsi nchini na wao wanasubiri mwitiko kutoka kwa vijana katika shule mbalimbali nchini.

Mwisho ameushukuru ubalozi wa Sweden kwa kuwa marafiki wazuri kwa Serikali na Femina na kwa msaada walioupata leo utawasaidia sana vijana.
Mkurugenzi mtendaji wa Femina Hip Dkt. Minou Fuglesang akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam ambapo ametoa shukurani kwa ubalozi wa  Sweden kwa  kuonyesha ushirikiano ambao utaiwezesha shirika la Femina kuendekeza juhudi za kuwawezesha kuboresha Maisha ya  vijana wa Tanzania na kuwajengea tabia ya uwajibikaji.
  Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden Ulf Kallstig pamoja na Mkurugenzi mtendaji  wa Femina Hip Dkt.Minou Fuglesang leo Jijini Dar es Salaam katika ubalozi wa  Sweden wakisaini mkataba wa makubaliano Mapya ya shilingi bilioni 4.5 za Kitanzania na shirika la Femina Kwa kipindi cha mwaka 2018-2020 ili kuboresha  mipango ya shirika hilo.
Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden Ulf Kallstig wakikabidhiana mkataba huo na Mkurugenzi mtendaji wa Femina  Dkt Minou Fuglesang pamoja na  Mkurugenzi  wa  habari wa shirika hilo Amabili  Batamula baada ya zoezi la utiaji saini kumalizika leo Jijini Dar es Salaam katika ubalozi wa Sweden.

TADB, YARA kuendelea kuchagiza tija katika uzalishaji wa kilimo

$
0
0
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imekubaliana na Kampuni YARA Tanzania kuendelea kuchagiza tija katika uzalishaji katika mazao ya kimkakati ya kilimo hapa nchini.

Dhamira hiyo ya kuwasaidia wakulima imewekwa wazi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine na Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno kilichofanyika katika Ofisi za YARA jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho, Bw. Justine amesema kuwa Benki ya Kilimo imejidhatiti kuwasaidia wakulima wadogo wadogo nchini kwa kuchagiza uzalishaji ili kuongeza kipato kwa wakulima hao.

“Tumedhamiria kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka  kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kuongeza kipato kwa wakulima wadogo nchini,” alisema.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno alisema kuwa uhakika wa mbolea bora na viuatilifu vya uhakika ni muhimu katika kuongeza tija na uzalishaji hali itakayochochea kuongeza kipato cha mkulima nchini.

Aliongeza kuwa matumizi ya pembejeo bora ni msingi katika mapinduzi ya kilimo kama inavochagizwa na TADB.

“Matumizi bora ya pembejeo yanasaidia kuongeza tija katika kilimo hivyo kuleta uhakika wa mavuno kwa wakulima wadogo wadogo” alisema.
 Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno (kushoto) akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) wakati walipokutana kuzungumzia mikakati ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo nchini. Wengine pichani ni maofisa kutoka TADB na YARA Tanzania.
 Meneja wa Utafiti wa Udongo wa YARA Tanzania, Bw. Peter Assey (kulia) akitoa maelekezo ya namna wanavyofanya utafiti wa udongo ili kubaini mbolea sahihi kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo hapa nchini. Wanaomsikiliza ni Meneja wa Wakulima Wadogo kutoka TADB, Bw. Joseph Mabula (kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (katikati) na Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno (wapili kulia)
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine na timu yake wakiangalia namna mbolea inavyofungwa tayari kwenda sokoni.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akizungumza wakati wa ukaguzi wa shughuli za uzalishaji wa mbolea unaofanywa na Kampuni ya YARA Tanzania. Pichani ni Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno (kushoto), Meneja wa Wakulima Wadogo kutoka TADB, Bw. Joseph Mabula (wapili kushoto) na Meneja wa Utafiti wa Udongo wa YARA Tanzania, Bw. Peter Assey (kulia).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (wa pili kushoto) akisikilza maelezo kuhusu aina ya mbolea zinazozalishwa na Kampuni ya YARA Tanzania. Anayetoa maelezo hayo ni Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Bw. William Ngeno (kushoto). Wengine pichani ni Meneja wa Wakulima Wadogo kutoka TADB, Bw. Joseph Mabula (wapili kulia) na Meneja wa Utafiti wa Udongo wa YARA Tanzania, Bw. Peter Assey (kulia).

DAWASA Yawahakikishia Wakazi wa Dar es Salaam na Pwani Huduma Bora ya Maji

$
0
0
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) imedhamiria kuendelea kuimarisha huduma zake katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano hasa katika ujenzi wa Viwanda kwa kuhakikisha kuwa huduma hiyo inafika maeneo ya Viwanda na kwa wananchi kwa kiwango kinachotakiwa.

Akizungumza katika kipindi cha mizani kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Afisa  Mtendaji mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa maeneo yote yanafikiwa na huduma ya maji safi na salama yakiwemo ya Viwanda na maeneo ya pembezoni  mwa Jiji la Dar es Salaam ambapo tayari hatua zimechukuliwa katika kutekeleza azma hiyo.

 “Tumejipanga kuhakikisha kuwa  hata wananchi wasio na uwezo  wanafikiwa na huduma ya maji kwa njia ya mkopo ambapo tunawaunganishia maji na wanalipia kidogo kidogo hivyo mwananchi hatakuwa na sababu ya kukosa maji na hii ndiyo dhamira ya Serikali yetu;” Alisisitiza  Mhandisi Luhemeja.

Aliongeza kuwa Mamlaka hiyo pia ina miradi yakupeleka maji katika maeneo rasmi ya viwanda katika mkoa wa Pwani ambapo kuna miradi katika Wilaya za Kisarawe, Kibaha,Bagamoyo na Mkuranga ili kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Akifafanua Mhandisi Luhemeja amesema kuwa tayari  maeneo ya pembezoni yakiwemo Kiwalani, Ukonga, Salasala na Mbagala yameanza kunufaika na mpango wa kuhakikisha kuwa wananchi ambao hawajafikiwa na huduma hiyo wanafikiwa ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi na uzalishaji.

Akitolea mafano wa hatua zinazochukuliwa katika  kuimarisha huduma ya maji katika Wilaya ya Kigamboni Mhandisi Luhemeja amesema kisima cha Gezaulole kimeshafungwa pampu na mtandao  wa mabomba utawekwa ili maji yatakayozalishwa yasambazwe katika eneo hilo ikiwa ni hatua mojawapo yakuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama

“ Upanuzi wa mfumo wa usambazaji maji kati ya Changanyikeni hadi Bagamoyo kwa ufadhili wa Benki ya Dunia unaendelea kwa kuongeza mtandao wa kusambaza maji ambao  utachangia kuondoa changamoto ya upotevu wa maji “,Alisisitiza Luhemeja.

Akizungumzia suala la watu binafsi kumiliki visima na kuuza maji Luhemeja amesema kuwa Mamalaka yake inachukua hatua madhubuti kuhakikisha kuwa maji hayo ni salama kwa matumizi ya wananchi  na si vinginevyo.

“Maji yanayosambazwa kwa wananchi lazima yakizi vigezo, DAWASA itapima maji hayo na kama hayakidhi vigezo basi visima husika vitafungwa ambapo kwa sasa tutasajili upya visima vyote vya watu binafsi wanaofanya biashara ya kuuza maji;’’Alisisitiza Luhemeja.
Kwa upande wa majitaka Mhandisi  Luhemeja amesema kuwa huduma hiyo inapanuliwa kwa kununua magari 20 ya kunyonya maji taka hali itakayopanua wigo wa huduma hiyo kwa wananchi na pia mifumo 9 ya majitaka imeanza kukarabatiwa ili kuweza kupokea na kutibu majitaka.

 Mamlaka hiyo imebuni mikakati mbalimbali ya kuimarisha utendaji  wake na huduma zake kwanza kwa kuanzisha kituo cha huduma kwa wateja, kuweka mikakati ya makusudi kuhakikisha kuwa wananchi wa pembezoni wanafikiwa na huduma ya maji, kuimarisha miundombinu, kuzuia uvujaaji wa maji, kuongeza mapato na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza maji kupitia katika Kampeni maalum itakayoendeshwa katika shule za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ili kujenga utamaduni wa kulinda na kutunza maji na miundombinu.

DAWASA imekuwa ikiimarisha utendaji wake ili kuendana na azma ya Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wanafikiwa na huduma ya maji safi na salama katika maeneo yao na kwa wakati.

Tanzania na China yasherekea miaka 50 katika sekta ya afya

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Balozi wa China Wang Ke pamoja na viongozi mbalimbali wakikata kike katika maadhimisho ya miaka 50 kati ya Tanzania na China katika Sekta ya Afya iliyofanyika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya miaka ya 50 ushirikiano katika sekta ya afya kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya miaka ya 50 ushirikiano katika sekta ya afya kuhusiana na China kujihusiha katika masuala ya afya pamoja na ujenzi wa Hospitali uliofanyika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga akizungumza  katika sherehe za maadhimisho ya miaka ya 50 ushirikiano katika sekta ya afya na ushirikiano kati ya Tanzania  na China katika masualaya kidiplomasia , sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi akizungumza kuhusiana na mchango wa China katika Taasisi hiyo katika maadhimisho ya miaka 50 kati ya Tanzania na China katika Sekta ya Afya yaliyofanyika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikabidhi zawadi Balozi wa China nchini  Tanzania Wang Ke ikiwa Serikali ya Tanzania kutambua mchango wa China  katika hafla ya sherehe zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikabidhi zawadi Naibu Gavana wa Jimbo la Shadong Yuan Lini  ikiwa Serikali ya Tanzania kutambua mchango wa China  katika hafla ya sherehe zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja kati ya Mawaziri pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmad Salim. Picha na Chalila Kibuda

HAJI MANARA ATEULIWA KUWA BALOZI WA ASAS

Makamu wa Rais afungua maonyesho ya wiki ya Viwanda mkoani Pwani

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Masanja Kadogosamara baada ya kutembelea banda la kampuni inayotengeneza reli mpya ya kisasa ya YAPI MERKEZ wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya wiki ya Viwanda mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji  wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela Tuzo ya Udhamini Mkuu wa maonyesho ya Viwanda mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji  wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela cheti ya Udhamini Mkuu wa maonyesho ya Viwanda mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi maalum ya kumpongeza kwa kufanya ziara yenye mafanikio mkoani Pwani toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) mara baada ya ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya Viwanda mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi na wadhamini wa maonyesho ya Wiki ya Viwanda mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Mwakyembe Aagiza Wamiliki na Wahariri wa gazeti la Tanzanite Kujieleza

$
0
0
Na mwandishi wetu, Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), amesema habari iliyochapishwa na gazeti la kila siku la Tanzanite la leo Jumatatu tarehe 29 Oktoba, 2018 lenye habari zenye tuhuma za kisiasa dhidi ya Viongozi kadhaa, haziakisi msimamo wa Serikali na ameagiza mmiliki na Bodi ya uhariri ya gazeti hilo waitwe mara moja Idara ya Habari (MAELEZO) kujieleza kuhusu msingi wa habari hiyo.

Dkt. Mwakyembe ametoa ufafanuzi huo leo mchana, mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuelezea kushtushwa kwake na mwenendo wa gazeti hilo kuchapisha habari zinazoibua tuhuma za kisiasa dhidi ya baadhi ya Viongozi nchini, wakiwemo Wabunge na kusababisha taharuki kubwa katika jamii.

Gazeti la Tanzanite linatolewa na kampuni ya CZ Information and Media Consultant LTD ya Dar es Salaam na leo katika toleo lake Na. 254 limeandika katika ukurasa wake wa mbele  habari yenye kichwa kinachosomeka “Vigogo 14 hatari kwa nchi watajwa” ambayo inawataja viongozi kadhaa wa kisiasa na wafanyabiashara.

Mwakilishi wa UN WOMEN awasilisha Hati za Utambulisho

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga amepokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN WOMEN) Bi. Hodan Addou. Baada ya kupokea Hati hizo Dkt. Mahiga alitumia fursa hiyo kumkaribisha nchini na kumuhakikishia kumpatia Ushirikiano wa kutosha kwa kipindi chote cha utendaji kazi wake hapa nchini. 
Dkt. Mahiga akizungumza na Bi. Addou 
Bi. Addou akimwelezea jambo Dkt. Mahiga 
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images