Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

USIKU WA MIAKA 20 YA TWANGA PEPETA ILIVYOWKUMBUSHA WENGI


STEVE NYERERE ANG'AKA, ASEMA MUZIKI WA DANSI ULIYUMBA WENYEWE KWENYE RAMANI YA MUZIKI.

KAMPUNI YA CRJE YA CHINA YAUNGA MKONO JUHUDI ZA RC MAKONDA KWA KUJENGA OFISI MBILI ZA WALIMU

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda jana amezindua ujenzi wa Ofisi moja Kati ya ofisi mbili za kisasa katika shule ya msingi Vijibweni katika Manispaa ya Kigamboni ikiwa ni ahadi alizoahidiwa na Kampuni ya Ujenzi ya CRJE iliyoguswa na Kampeni ya Makonda ya Ujenzi wa Ofisi 402 za walimu katika jiji la Dar es salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika shule ya msingi Vijibweni ambako ni moja ya shule ambayo ofisi za walimu zitajengwa Makonda amesema kuwa moja kati ya vitu vinavyomnyima usingizi ni kuona walimu wanafanya kazi katika mazingira magumu ikiwemo kufanya kazi chini ya miti na kwenye korido na lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni kuhakikisha thamani walimu inarejea.

Aidha Makonda amesema uwepo wa mazingira bora ya kufanyia kazi kwa walimu Ndio chachu ya kuongezeka kwa ufaulu ambapo amewapongeza walimu na watendaji wa elimu kwa kuifanya Dar es salaam kuongoza kitaifa katika matokeo ya mtihani wa Darasa la Saba.Pia Makonda amesema kuwa ofisi hizo zitakuwa na mahitaji yote muhimu ikiwemo ofisi ya mwalimu mkuu, mwalimu mkuu msaidizi, ukumbi wa mikutano, ofisi ya walimu wote, chumba cha mitihani, chumba cha mhasibu, mapokezi, stoo, Vyoo na Bafu.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri amesema kuwa kama watendaji wataendelea kuunga mkono jitihada za Mh. Rais na Mkuu wa Mkoa katika suala zima la elimu ili kuhakikisha watoto wanapata elimu iliyo bora na walimu wanafanya kazi zao katika mazingira ya kuridhisha.Diwani wa kata ya Vijibweni na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amesema kuwa anashukuru kwa kufanya kazi na viongozi kwa ushirikiano bila kujali itikadi za vyama.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Vijibweni amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa shule hiyo haina ofisi yoyote ya walimu hivyo wamekuwa wakifanyia kazi chini ya miti na kwenye korido ambapo wamemshukuru kwa kuwaletea mfadhili wa kuwajengea ofisi ya kisasa.
RC Makonda akiwa ameongozana na baadhi ya viongozi wa maispaa ya Kigamboni akikagua madarasa ya wanafunzi wa Shule ya msingi ya vijibweni katika uzinduzi wa ujenzi wa ofisi za walimu ikiwa ni muendelezo wa ilani yake kujenga ofisi hizo 402 hapa Jijini Dar es Salaam.
RC Makonda akiwapungia wanafunzi mkono wa kwaheri Mara baada ya zoezi la uzinduzi wa ujenzi wa ofisi kumalizika jana  Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza jana na wageni waaliohudhuria wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa ofisi mbili za kisasa za walimu wa Shule ya msingi ya vijibweni iliyopo katika manispaa ya Halmashauri ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam akitimiza ahadi aliloahidiwa na kampuni ya ujenzi ya CRJE kutoka nchini China iliyoguswa na kampeni ya RC Makonda ya kujenga ofisi 402 za walimu.

Wanafunzi wa Shule ya msingi vijibweni waliohudhuria katika uzinduzi wa ujenzi wa ofisi mbili za walimu za kisasa jana jijini Dar es Salaam.

Asha Baraka atoa TUZO za heshima kwa wadau wa TWANGA PEPETA

Mtanzania Rebeca Gyumi aibuka kidedea tuzo ya haki za binadamu ya UN

0
0
Rebeca Gyumi, mwanaharakati wa haki za wanawake na wasichana nchini Tanzania pamoja na watu wengine wawili na shirika moja la kiraia, wameshinda tuzo ya mwaka huu ya haki za binadamu


Washindi hao wametangazwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Maria Fernanda Espinosa ambaye kupitia ukurasa wake wa Twitter amewapongeza kwa mchango wao wa kusongesha mbele haki za binadamu.

Hii ni tuzo ya 10 ambayo mwaka huu inaendana na miaka 70 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambapo washindi hao watapokea tuzo hizo tarehe 10 mwezi disemba mwaka huu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Taarifa ya ofisi ya Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa imefafanua kazi za washindi hao akitolea mfano Rebeca Gyumi.

Bi. Gyumim muasisi na mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Msichana Initiative nchini Tanzania, kwa miaka 8 amekuwa akihoji uhalali wa ibara ya 13 na 17 ya sheria ya ndoa yam waka 1971 nchini Tanzania ambayo inahurusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 na 15 kwa ridhaa ya wazazi au mahakama.

Taarifa hiyo inasema “Bi. Gyumi alishinda kesi hiyo mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzaina mwaka 2016.” Mshindi mwingine ni Asma Jahangir mwanaharakati mwanasheria wa Pakistani ambaye amefariki dunia mwaka huu.

Marehemu Jahangir kwa miongo mitatu amekuwa akitetea haki za wanawake, wasichana, watoto na makundi madogo ya kidini na maskini nchini mwake ambapo alifungua kituo cha msaada wa sheria. Ingawa hivyo alikuwa akikumbwa na misukosuko lakini alikuwa na uwezo wa kushinda kesi zilizokuwa na utata.

Kwa upande wake, mshindi mwingine Joênia Wapichana au Joênia Batista de Carvalho, mwanaharakati wa haki za watu wa jamii ya asili nchini Brazil, ni mwanamke wa kwanza wa jamii hiyo kuwa mwanasheria. “Baada ya kuwasilisha mbele ya tume ya haki za binadamu ya nchi za Amerika, Bi. Wapichana alikuwa mwanasheria wa kwanza wa jamii ya asili kuingia Mahakama Kuu ya Brazil.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA >>>>>>

SHERIA MPYA YA PSSSF NA SULUHISHO LA “FAO LA KUJITOA

0
0
Kwa kipindi kirefu kumekuwepo na changamoto ya kimtazamo kati ya dhana ya Hifadhi ya Jamii na Fao la kujitoa, Changamoto hii kwa kiasi kikubwa inasababishwa na uelewa mdogo miongoni mwa wanachama na wadau wa sekta ya Hifadhi ya Jamii. Suala hili limepelekea malalamiko mengi huku wengine wakijutia kuchangia kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Ili kulielewa jambo hili kwa mapana yake nianze kwa kuelezea dhana ya Hifadhi ya Jamii kama utaratibu unaowekwa na Jamii kwa lengo la kuwapatia wanajamii kinga dhidi ya majanga ya kiuchumi na kijamii yanayosababisha upungufu au upotevu wa kipato kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ugonjwa, ukosefu wa ajira, ulemavu na uzee. Kuna aina mbili za mifumo ya hifadhi ya jamii ambayo ni mifumo rasmi na mifumo isiyo rasmi. Mifumo rasmi ni ile ambayo inawekwa kwa mujibu utaratibu, kanuni na Sheria zinazotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mifumo isiyo rasmi ni ile ambayo jamii inajiwekea kupitia mila na desturi zake. 

Katika Mfumo rasmi wa Hifadhi ya Jamii umegawanyika katika makundi makubwa mawili ambayo ni Hifadhi ya Jamii kwa utaratibu misaada kwa jamii “Social Assistance Schemes” ambapo misaada na ruzuku hutolewa kwa jamii kuwapatia wananchi huduma za misingi za Hifadhi ya Jamii. Huduma hizo hutolewa kwa malengo mbalimbali kama vile; kugharamia elimu ya msingi, afya, maji, ruzuku, uzee, ulemavu na kukabiliana na majanga yanayotokea kwenye jamii. 

Pili ni Hifadhi ya Jamii katika utaratibu wa bima kwa jamii “social insurance”.  Aina hii ya hifadhi ya jamii ipo katika sehemu mbili ambazo ni sehemu ya kwanza ni Fao la jamii kwa mujibu wa Sheria; Wafanyakazi hupaswa kuchanga na kupata mafao kwa mujibu wa Sheria kama vile Mifuko ya pensheni na Fao la Afya. Sehemu ya pili ni Mfuko wa hiari “Supplementary Schemes”, ambapo Wanachama huchangia kwa hiari.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

MAKAMU WA RAIS AKATAA KUZINDUA STENDI KUU MPYA YA MAILMOJA KIBAHA

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekataa kuzindua stendi kuu mpya ya Mailmoja Kibaha mkoani Pwani, akiwa katika ziara yake mkoani humo. 

Hatua hiyo ameifikia kutokana na kupata wasiwasi wa utekelezaji wa mradi kuwa na baadhi ya mapungufu ambapo amedai baada ya kufanya uchunguzi wiki mbili ama tatu zijazo atakwenda kuuzindua. Akizungumza katika stand hiyo, Samia alieleza, kuna minong’ono wameisikia kuhusu mradi huo hivyo ni jukumu lake kuibeba na atakapo jiridhisha atarudi kwa mara nyingine . 

Hata hivyo, alisema atakutana na mkuu wa wilaya, mkurugenzi na mkuu wa mkoa kuzungumzia suala hilo. “Msishtuke kwa hili ni kawaida kwa kuchukua hatua za aina hii ili kujiridhisha kwa maslahi ya halmashauri, mkoa na watumiaji kijumla “Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni sikivu na kusikia malalamiko ya wananchi, tumepata malalamiko kidogo kuhusu stand hii, serikali ni ya uwazi na ukweli hivyo sitofungua stendi “alisisitiza Samia. 

Samia alimpongeza mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha, Jennifer Omolo na mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama na wahusika waliohusika kufanikisha mradi huo. Nae waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa -TAMISEMI ,Selemani Jafo alisema yeye kama waziri wapo wataalamu wanaohakiki lakini ameridhishwa na kazi hiyo . 

“Kwani kila kazi ina changamoto za kibinadamu, hasi na chanya, lakini wamejitahidi “alisema Jafo. Jafo alieleza, mradi huo umepata msaada wa mkopo nafuu kutoka bank ya Dunia ambao wamepata fedha za kimarekani dollar milioni 255 .# Alielezea , wanagusa miji 18 na wanachokifanya wanagusa stendi tisa, barabara za miji kwa kiwango cha lami na madaraja makubwa ya kisasa. 

Wakitoa kero ya stand hiyo, madereva pikipiki walidai eneo lililotengwa kwa ajili yao halina sehemu ya kujikinga hivyo kusababisha usumbufu wakati wa mvua na jua. Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha, Jennifer Omolo alisema katika stendi ndogo ya awali walikuwa wakikusanya ushuru sh. 950.000 kwa siku ambapo sasa wanakusanya sh. milioni 1.6 .Alisema mradi huo umegharimu sh. bilioni 2.9 na walishamlipa mkandarasi bilioni 2.7 ,stendi hiyo itakuwa na mabanda kumi ya kukatia tiketi, mawakala 40 ,eneo la tax, na wafanyabiashara ndogondogo wanaojiingizia kipato kwa kuuza biashara zao wapo 100 . 

Samia akiwa katika ziara yake Kibaha vijijini na mjini pia alipata fursa ya kutembelea mradi wa reli ya kisasa ya standard gauge kujionea namna unavyoendelea.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji Mhandisi Farid M. Abdallah wakati akikagua shughuli za ujanzi wa Reli ya Kisasa “Standard Gauge” katika kijiji cha Soga wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua stendi mpya ya mabasi Kibaha . Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais 

WAZIRI LUKUVI ALITAKA SHIRIKA LA NYUMBA NHC KUWA MFANO KATIKA KUSIMAMIA NA KUTUNZA NYUMBA ZAKE

0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuwa mfano katika, kuhifadhi, kutunza na kujenga nyumba bora za gharama nafuu kwa ajili ya kuziuza au kuzipangisha kwa wananchi wakiwemo watumishi wa umma.

Aidha, amelitaka shirika la NHC kuwa mfano kwa taasisi nyingine zinazojishughulisha na ujenzi kwa kujenga nyumba bora na wakati huo kuwapangisha wananchi kwa malipo ya kodi ya mwezi mmoja mmoja badala ya utaratibu uliozoeleka wa kupangisha kwa malipo ya kipindi cha miezi sita au mwaka mzima na kuepuka kutumia ‘vishoka’ wakati wa kupangisha nyumba zake.

Lukuvi aliyasema hayo jana alipolitembelea Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika mkoa wa Kilimanjaro wakati wa mwisho wa ziara yake ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika wilaya za Hai, Moshi na Same mkoani Kilimanjaro.

Alisema, Shirika la Nyumba la nyumba NHC lazima liwe na mkakati mzuri wa ukarabati nyumba zake na kubainisha kuwa haiwezekani Shirika kubwa kama hilo kuwa na nyumba nyingi katika maeneo ya vitovu vya miji huku nyingi ya nyumba hizo zikiwa zimechoka na kusisitiza kuwa hataki kusikia NHC inakuwa na nyumba za aina hiyo.

Amelitaka Shirika kujipanga vizuri na kuhakikisha linashirikiana vizuri na ofisi za Mikoa na Halmashauri kwa lengo la kujenga nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya watumishi na wakati huo kutangaza shughuli zake kwa kuwa NHC ina Kampuni yake ya ujenzi iliyosheheni wataalamu wa fani mbalimbali sambamba na kuwa na uwezo wa kujenga majengo mbalimbali kama vile Shule, Hospitali, Vituo vya Afya na Vyuo.


SWEDY MKWABI AZINDUA KAMPENI ZA UENYEKITI WA KLABU YA SIMBA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. 

 MGOMBEA wa nafasi ya uenyekiti wa Klabu ya Simba Swedy Mkwabi ameweka wazi mikakati yake iwapo atapewa ridhaa na wananchama wa Klabu hiyo kuiongoza kwa kipindi kijacho. 

 Mkwabi amezindua kampeni zake leo Jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na wanachama wa klabu ya Simba kutoka matawi mbalimbali.  Akizungumza wakati wa kuzindua kampeni zake, Mkwambi amesema kuwa atahakikisha anasimamia vizuri mfumo wa mabadiliko wa uendeshaji wa klabu ya Simba kulingana na katiba mpya ya toleo la mwaka 2018 kama ilivyopitishwa na wanachama. 

 Mkwabi amesema, suala lingine ni kuona klabu ya Simba inakuwa na vyanzo vya mapato endelevu na vya uhakika ikiwemo na kufanya vizuri katika mashindano ya kitaifa  a kimataifa ili litawezekana kwa kusimamia kwa weledi na kuheshimu taaluma ya walimu na benchi la ufundi.  "Katika kuhakikisha maslahi ya wanachama wa Simba yanalindwa vizuri kwa kushirikiana na muwekezaji mkuu wa Simba ni kuondoa makundi ya wanachama na kutengeneza umoja wenye nguvu na kufuata, kuheshimu katiba ya Simba,"amesema Mkwabi.

 Ameweka wazi mkakati mwingine ni kuwa na ushirkiano wa karibu kati ya uongozi wa makao makuu na uongozi wa matawi, Wilaya na Mkoa ili kuleta ufanisi na umoja ndani ya Klabu ya Simba, Kuhakikisha mila na desturi na utamaduni wa klabu hiyo inadumishwa na kuendelezwa.  Mkwabi amezindua kampeni yake leo na kuanzia Oktoba 29 atakutana na viongozi wengine wa matawi wa Wilaya ya Temeke ili kunadi sera zake na amesema kuwa akipewa nafasi ya kuwa mwenyekiti atatumia uzoefu wake wa uongozi wa mpira wa miguu na kushirikiana na viongozi wenzake pamoja na mwekezaji ya klabu hiyo ili kutengeneza dira ya maendeleo ya michezo.

 "Nitahakikisha Simba inakuwa klabu bora sio tu Tanzania bali Afrika kwa ujumla, nitahakikisha tunakuwa na miundo mbinu ya michezo kama viwanja vya michezo, hostel, shule ya michezo kwa vijana na soka la wanawake," amesema Mkwabi.

Katika uongozi wake, Mkwabi ni Mwenyekiti wa Mpira wa Miguu wilaya ya Tanga kuanzia 2013 hadi sasa hivi ila amewahi kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji  wa klabu ya Simba kuanzia mwaka 2010 hadi 2014 na mwenyekiti wa kamati ya mashindano mwaka 2012 hadi 2014 na iwapo atachaguliwa atakuwa moja kwa moja anapata nafasi ya kuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya Simba. 

Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Klabu ya Simba SwedyMkwabi akielezea mikakati yake ndani ya Simba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi wa klabu hiyo.

MWAKILISHI MTEULE WA JANG’OMBE AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI

0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR

MWAKILISHI mteule wa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Jang’ombe Ndugu Ramadhan Hamza Chande leo amekabidhiwa rasmi Cheti cha udhibitisho wa ushindi wa nafasi ya Uwakilishi wa Jimbo hilo.

Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Wilaya ya Mjini iliyopo Maisara na kuudhuriwa na Viongozi na Wanatendaji wandamizi Tume hiyo na CCM.Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Cheti hicho Mwakilishi mteule huyo Ramadhan Hamza ameahidi kufanya kazi kwa uadilifu na kwa kufuata miongozo na taratibu zote za kisheria kwa maslahi ya wananchi wote wa Jimbo hilo. 

Amewashukuru wananchi na wanachama wa CCM wa Jimbo hilo kwa kumpatia ridhaa yangu kuongoza Jimbo hilo kupitia utaratibu halali wa kidemokrasia. “Nitawatumikia kwa uadilifu wananchi wote wa Jang’ombe bila ya ubaguzi wowote kwani naamini bila yenu nyinyi kuridhia kunipa nafasi hii nisingeweza kushinda katika mchakato huu wa kisiasa uliokuwa na ushindani mkubwa.Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020 tayari nishakabidhiwa muda wowote nitaanza kutekeleza mpango kazi wangu kwa lengo la kutekeleza ahadi nilizoahidi katika kampeni.”,ameeleza Chande.

Kwa upande wake aliyekuwa Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Jang’ombe ambaye pia ni Afisa wa ZEC Wilaya ya Mjini Bi.Mwanapili Khamis Mohamed amemsisitiza kiongozi huyo kufanya kazi zake kwa majibu wa taratibu na kanuni za kisheria ili kutimiza matakwa ya wananchi waliomchagua. 

Mwakilishi huyo aliyeshinda nafasi hiyo jana kwa kura 6,581 sawa na asilimia 90.5 katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang’ombe uliofanyika kwa amani bila ya kujitokeza matukio ya uvunjifu wa sheria za Uchaguzi na nchi kwa ujumla.
AFISA wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Wilaya ya Mjini Mwanapili Khamis Mohamed (kulia) akimkabidhi Cheti cha udhibitisho wa Ushindi wa nafasi ya Uwakilishi Mwakilishi mteule wa Jimbo la Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande (kushoto) , aliyekuwa Wakala wa Mgombea wa CCM katika Uchaguzi huo Rajab Uweje Yakoub (wa pili kushoto).
ALIYEKUWA Wakala wa Mgombea Uwakilishi wa CCM Ndugu Rajab Uweje Yakoub (wa pili kushoto) akisaini Cheti cha udhibitisho wa ushindi wa Uwakilishi cha Mwakilishi mteule wa CCM Jimbo la Jang’ombe.
MWAKILISHI mteule wa Jimbo la Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande akionyesha Cheti cha udhibitisho wa ushindi wa Uwakilishi kupitia Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo uliofanyika Jana.

SHONZA: SERIKALI ITAENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WASANII KUKUZA SOKO LA TASNIA YA SANAA

0
0
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO-Bagamoyo

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema Serikali itaendelea kuwajengea uwezo, umahiri na ubunifu wasanii wa Tanzania kupitia Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi (TASIP) ili kukuza soko la tasnia hiyo katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Akifunga Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani jana (Jumamosi Oktoba 27, 2018), Shonza alisema malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa tasnia ya sanaa nchini inapiga hatua kubwa zaidi na kuwafanya wasanii kunufaika na kazi zao.

Aliongeza kwa kuzingatia kuwa Wizara yake inasimamia na kutekeleza sera ya sanaa nchini, Serikali itahakikisha kuwa kuipitia mradi wa TASIP unawafikia na kuwatambua wasanii wote nchini na kuwawezesha kuwa na utambulisho rasmi utawaozesha kupata mitaji na mikopo ya kuendesha shughuli zao.

“Mwaka jana nilizindua mradi huu wa TASIP na mwaka huu tumeanza kushuhudia mafanikio makubwa kupitia program hii, kwa kuwa wapo baadhi ya wasanii waliotambuliwa na kusajiliwa na wameanza kupata mikopo kutoka mabenki hatua inayowezesha kupata kutatua baadhi ya changamoto katika kuendesha shughuli zao” alisema Shonza.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mjasiriamali wa sanaa za uchongaji, Ras Jeshi Beku alipotembelea banda la Msanii huyo wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia), akitazama kikoi kilitengenezwa na Msajiriamali Esther Mwita alipotembelea banda la Msanii huyo wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. 
Naibu Waziri wa Habari, Utanmaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akitazama moja shati lilitengtenezwa na Mjasiriamali Monica Matemba alipotembelea banda la Mjasiriamali huyo wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akitazama chungu kilitengenezwa na mmoja wa Wajasiariamali alipotembelea banda la Mjasiriamali huyo wakati wa kufunga tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Jumamosi Oktoba 27, 2018, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. 

SERIKALI HAITAMWONEA HURUMA MTU YEYOTE ATAKAYEKAMATWA AKIJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU-NAIBU WAZIRI ULEGA

0
0
 Serikali imepiga marufuku uvuvi haramu na kuteketeza  nyavu aina ya makokoro 35 , makila 6 na nyavu za zenia 25 zilizokuwa zikitumiwa na wavuvi haramu katika bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kagongo kata Lang’ata leo,Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi  Abdalah Ulega  amesema serikali haitamwonea huruma mtu yeyote atakayekamatwa akijihusisha na uvuvi haramu kwani serikali  imekua ikipoteza kiasi kikubwa cha mapato kutokana na uvuvi huo.

“Hatuna utani na mtu asiye na huruma na rasilimali za nchi hii, Tanzania ndio nchi yenye  sehemukubwa  yenye maji kuliko sehemu nyingine lakini bado tunaagiza samaki kutoka nchini china, tumeagiza sato., perege hadi kibua wa kichina, tusipotokomeza leo bwawa litakuwa historia kwa vizazi vijavyo” amesema Ulega

Kwa  upande wake mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira  alisema uwepo wa bwawa hilo umekuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika eneo hilo na sasa ni wakati wa wananchi kuwa walinzi kwa kila mmoja ili kutokomeza uvuvi haramu.“Hebu leo amueni kabisa kwamba  biashara ya samaki ndio mfumo wa maisha yenu, Ninyi mkifanya hivyo sisi hatutahitaji kufunga hili bwawa , wakati wote tutahitaji kuongeza kizazi cha samaki na kuleta wataalamu kupima kiwango cha samaki tulichonacho” alisema Mghwira

 Kwa upande wake Dismas Gondwe mkazi wa kijiji cha kigongo kata ya Lang’ata amesema  uvuvi haramu katika bwawa hilo unatokana na kukosekana kwa utaratibu maalumu unaowaelekeza  wavuvi kuendesha  shughuli zao katika bwawa hilo.

Gondwe ameiomba serikali kuwawezesha  wavuvi wa bwawa la Nyumba ya Mungu zana  harali ambazo serikali inazitambua.

Naibi Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi wa kijiji cha Kagongo kata ya Lang`ata mkoa wa Kilimanjaro kuhusu serikali kutokumuonea huruma mtu yoyote ambaye atajihusisha na shughuli za uvuvi  haramu.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG Kilimanjaro)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira.
 Naibi Waziri Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,  Abdallah Ulega (wakwanza kulia) kwa kushirikiana na  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira na  Mkuu wa wilaya ya Mwanga Aarron Mbogho wakiteketeza zana haramu zilizokua zikitumika katika uvuvi haramu kwenye bwawa la Nyumba ya Mungu.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG Kilimanjaro)
 Sehemu ya wavuvi wa kijiji cha Kagongo kata ya Lang`ata mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega.
Zana haramu zilizokua zikitumika katika uvuvi haramu zikiteketezwa

LUGOLA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KITUO KIKUU CHA POLISI DODOMA, AFUATILIA MAAGIZO YAKE DHAMANA ZITOLEWE SAA 24, KUBAMBIKIZIWA WANANCHI KESI NA BODABODA KUONDOLEWA VITUONI

0
0
 Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akiwahoji maswali askari polisi wa zamu wa kituo cha Polisi cha Kati, jijini Dodoma, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo, kwa lengo la kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa nchini kuhusu dhamana zitolewe saa 24, kukomesha tabia ya wananchi kubambikizwa kesi pamoja na pikpiki zilizopo katika vituo mbalimbali nchini ziondolewe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  

 Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wa pili kushoto) akimuuliza maswali Kamanda wa Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Nuru Selemani (kushoto)  kuhusu uwepo wa pikpiki kituoni hapo wakati alishatoa agizo pikipiki zote zilizopo katika vituo vya polisi nchini ziondolewe. Lugola alifanya ya kushtukiza katika Kituo cha Polisi cha Kati, jijini Dodoma, kwa lengo la kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa nchini kuhusu dhamana zitolewe saa 24, kukomesha tabia ya wananchi kubambikizwa kesi pamoja na pikpiki zilizopo katika vituo mbalimbali nchini ziondolewe. Watatu kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Gilles Muroto. 


Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya Kituo cha Polisi cha Kati, jijini Dodoma leo, kwa lengo la kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa nchini kuhusu dhamana zitolewe saa 24, kukomesha tabia ya wananchi kubambikizwa kesi pamoja na pikpiki zilizopo katika vituo mbalimbali nchini ziondolewe. Kushoto ni Gilles Muroto. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 


MASHA NA MBUNGE CHEGENI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUFANYA VURUGU KWA MWEKEZAJI WA MATUNDA MKOANI MBEYA

0
0
ALIEYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lauwrence Masha pamoja na Mbunge wa Jimbo la Busega Raphael Chegeni na vijana wengine 10 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wakituhumiwa kufanya vurugu kwenye nyumba ya mwekezaji wa matunda ya Parachichi Peter Cruise na kutoa vyombo vyake nje kinyume cha taratibu. 
Watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya kosa hilo Oktoba  27,2018  majira ya saa tatu asubuhi kwenye makazi ya mwekezaji yaliyopo katika eneo la Rungwe Mission na kuharibu mali hali iliyozua mabishano makali kabla jeshi la polisi kufika eneo la tukio na kuwakamata watuhumiwa ambao watafikishwa mahakama mara baada ya uchunguzi kukamilika. 
Masha na wenzake wanadaiwa kufika nyumbani kwa mwekezaji huyo kwa kuvunja mlango wa nyumba na kisha kutoa vyombo nje kwa nguvu .
 Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ulrich Matei amekiri kukamatwa kwa watu hao na kueleza kuwa hana taarifa za ujio wao licha ya kudai wanakwenda kutekeleza amri ya mahakama inayowapa uhalali wa kunmwondoa mwekezaji huyo kwenye makazi.

MICHUZI TV: MANINJA walipovamia jukwaa la TWANGA PEPETA


MICHUZI TV: Asha Baraka afunguka kuhusu Nyoshi El Saadat

MICHUZI TV: TWANGA PEPETA hawataki tena Kuliamsha DUDE, Wapasua anga..

MICHUZI TV: Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza aongelea Twanga Pepeta

BREAKING NYUUUUZZZZ: MASHA, CHEGENI NA VIJANA WENGINE 10 WATIWA MBARONI JIJINI MBEYA LEO

0
0
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Laurence Masha pamoja  na Mbunge wa  Jimbo la Busega Raphael Chegeni na vijana wengine 10 wanashikiliwa  na Jeshi  la Polisi wilaya ya Rungwe  mkoani Mbeya wakituhumiwa kufanya vurugu kwenye nyumba ya mwekezaji wa matunda ya Parachichi Peter Cruise na kutoa vyombo vyake nje kinyume cha taratibu.

 Watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya kosa hilo Oktoba 27 majira ya saa tatu asubuhi kwenye makazi ya mwekezaji yaliyopo katika eneo la Rungwe Mission na kuharibu mali hali iliyozua mabishano makali kabla jeshi la polisi kufika eneo la tukio na kuwakamata watuhumiwa ambao watafikishwa mahakama mara baada ya uchunguzi kukamilika. 

Masha na wenzake wanadaiwa kufika nyumbani kwa mwekezaji huyo kwa kuvunja mlango wa nyumba na kisha kutoa vyombo nje kwa nguvu/

 Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ulrich Matei amethibitisha kukamatwa kwa watu hao japo kuwa amesema kuwa hana taarifa za ujio wao licha ya (watuhumiwa hao) kudai wanakwenda kutekeleza amri ya mahakama inayowapa uhalali wa kunmwondoa mwekezaji huyo kwenye makazi

Fourth Round Selection of Applicant's Selected to Join Ardhi University into various Academic Undergraduate Degree Programmes

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images