Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti 8 wa bodi na Mtendaji Mkuu 1


SAMIA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA YA LAMI YA MKURANGA - KISIJU

$
0
0


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kutengenezea Gypsum Board kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Knauf kilichopo Mwanambaya Mkuranga Bw. Zachopolous Georgions. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
810
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua ujenzi wa barabara Mkuranga – Kisiju inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhimiza shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
13
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya mpango wa kuborsha barabra za Mkuranga kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (katikati) wakati akikagua ujenzi wa barabara Mkuranga – Kisiju inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhimiza shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani kulia pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
19
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya vifungashio vinavyotumika kufungashia vigae vya marumaru (tiles) alipotembelea kiwanda cha Goodwill Ceramic ltd kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Robin Huang. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
20
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ya vigae (tiles) moja alipotembelea kiwanda cha Goodwill Ceramic ltd kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Robin Huang. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MICHUZI TV: Mwanamuziki Peter Msechu ampa sifa hizi Lady Jaydee

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUTOA HUDUMA YA KLINIKI YA MOYO INAYOTEMBEA MKOANI KAGERA

$
0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera wanatarajia kutoa huduma ya kliniki ya Moyo inayotembea (Cardiac Mobile Clinic) katika Mkoa wa Kagera kuanzia tarehe 5 hadi tarehe 11 Novemba, 2018.

Huduma tutakazozitoa ni pamoja na upimaji wa vihatarishi vya Magonjwa ya Moyo, ushauri wa kiafya kuhusiana na Magonjwa ya Moyo, na kutoa rufaa kwa wananchi watakaokutwa na matatizo ya Moyo yanayohitajika kupewa rufaa kuja kwenye Taasisi yetu kwa uchunguzi wa tiba zaidi.

Matibabu ya kliniki ya moyo inayotembea ni matibabu endelevu yanayolenga kuhakikisha kuwa wagonjwa wa Moyo waliopo mikoani wanapata huduma bora ya matibabu ya Moyo na kuwa na elimu inayohusiana na magonjwa ya Moyo.

Wananchi wote wa Mkoa wa Kagera pamoja na mikoa ya jirani tunawakaribisha mfike katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera ili muweze kupata huduma za uchunguzi za matibabu ya Moyo.

MICHUZI TV: JSP Marketing Link Limited yatwaa ushindi wa tatu, tuzo za kampuni bora 100 Tanzania

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHIRIKI KATIKA TAMASHA LA UTAMADUNI WA MTANZANIA KWA JAMII YA WATU WA MKAO WA LINDI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kuuheshimu na kuuendeleza utamaduni ambao ndio urithi wao ili kulifanya Taifa liendelee kuwa hai. Amesema suala la kuuenzi utamadini ni jambo zuri ambalo linatoa fursa kwa watu wengine hususan wa mataifa ya nje kuja kujifunza historia ya Watanzania na maisha yao.

Waziri Mkuu aliyasema yao jana jioni (Ijumaa, Oktoba 26, 2018) alipotembelea shughuli za tamasha la utamadini wa Mtanzania kwa jamii ya watu wa Lindi. Katika tamasha hilo linalofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania waendelee kuupenda utamaduni wao.

“Nimefurahi kuona nyumba zikiwa na zana mbalimbali za kitamaduni ambazo zilikuwa zikitumiwa na wazee wetu pamoja na namba ya utayarishaji wa vyakula vyetu vya asili.”

“Sikutarajia kuona haya ninayoyaona, nawashukuru wote walioshiriki katika kandaa tamasha hili pamoja na uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Kijiji cha Makumbusho.”

Waziri Mkuu alisema tamasha hilo ambalo limewakutanisha Wanalindi kutoka katika wilaya mbalimbali linatoa fursa ya wao kujadili maendeleo ya mkoa wao na Taifa kwa ujumla. Kadhalika, Waziri Mkuu aliwaomba wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenda katika Kijiji cha Makumbusho kwa ajili ya kujifunza historia ya mkoa wa Lindi pamoja na fursa zilizoko.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alisema mkoa umetumia tamasha hilo kutoa ujumbe kwa umma kuhusu vivutio mbalimbali walivyonavyo pamoja na fursa za uwekezaji.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati alipowasili kwenye kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salam kushiriki katika Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania kwa Jamii ya Watu wa Mkoa wa Lindi, Oktoba 26, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati alipowasili kwenye kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salam kushiriki katika Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania kwa Jamii ya Watu wa Mkoa wa Lindi, Oktoba 26, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amekaa katika mazingira ya asili wakati aliposhiriki katika Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania kwa Jamii ya Watu wa Mkoa wa Lindi lililofanyika kwenye kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam, Oktoba 26, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vyakaula vya asili wakati aliposhiriki katika Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania kwa Jamii ya Watu wa Mkoa wa Lindi lililofanyika kwenye kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam, Oktoba 26, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda mti wa asili wakati aliposhiriki katika Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania kwa Jamii ya Watu wa Mkoa wa Lindi lililofanyika kwenye kijiiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam, Oktoba 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WANA-JUNDOKAN ULIMWENGUNI WAFURIKA MJINI NAHA, OKINAWA, JAPAN, KUADHIMISHA MIAKA 65 YA CHAMA HICHO CHA GOJU RYU KARATE-DO

$
0
0
Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya Okinawa Goju Ryu Jundokan  Karate kuanzia Novemba 8 hadi 16 mwaka huu itaadhimisha miaka 65 toka ianzishwe sambamba na maadhimisho ya miaka 20 toka kufariki kwa  mwanzilishi wa Jundokan master Eiichi Miyazato aliyefariki Disemba 11, 1999 huko mjini Naha, Okinawa, Japan. Maadhimisho hayo yataudhuriwa na kuwakilisha toka matawi yake yote ya dunia, au mabara yote, ikiwemo pia tawi la Tanzania chini ya mkufunzi wake mwakilishi sensei Fundi Rumadha mwenye Dan nne, au Yondan.
Hii ni moja ya matukio ya kihistoria ya chama cha Jundokan hususani kwa mrithi wa Goju Ryu kama mwalimu msaidizi wa ( Soke ) master Chojun Miyagi mwanzilishi  wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu Karate-Do. Baada ya kifo cha mwanzilishi huyo wa Goju Ryu kufariki Oktoba 8, 1953, hapo ndipo wanafunzi wake walipotawanyika kimakubaliano kuendeleza Sanaa hii ya asilia toka visiwa vya Okinawa na kuunda vyama tofauti kama heshima ya kumuenzi master Miyagi na kueneza mtindo wa  Okinawa Goju Ryu.
Master Miyagi, alikuwa ana wanafunzi wengi mahili waliobobea katika Sanaa ya Karate mtindo wa Okinawa Goju Ryu kama vile: Eiichi Miyazato, aliyeanzisha Jundokan 1957, Meitoku Yagi, aliyeanzisha Meibukan Goju Ryu, Gogen Yamaguchi, mwanzilishi wa Goju Kai, Seikichi Toguchi, mwanzilishi wa Shorei Kan Goju Ryu na Seko Higa, mwanzilishi wa Goju Ryu Kokusai Karate Kobudo.

Baadhi ya wanafunzi wa master Eiichi Miyazato ni: Kiichi Nakamoto sensei, Morio Higaonna sensei, Anichi Miyagi sensei, Teruo Chinen sensei, Chuck Merriman sensei, Kuniyuki Kai sensei, Nantambu Camara Bomani sensei (Mwanzilishi wa Jundokan Tanzania na Ghana), Masaji Taira sensei, Tetsunosuke Yasuda Sensei, Koshin Iha sensei, Teruya Koei sensei, Tetsu Gima sensei, Tsuneo  Kinjo sensei na mamia ya wanafunzi wengi toka ndani na nje ya Japan.
Maadhimisho haya ya kihistoria yatafanyika katika moja ya kumbi mpya maarufu kwa jina la “Okinawa Karate Kaikan Hall”, ukumbi uliojengwa mahususi kwa mahafali ya Karate kama historia ya sehemu palipozaliwa Karate na kufunguliwa na mfalme Akihito na mkewe Michiko mapema mwaka jana. Washiriki wote watakaoshiriki kongamano hilo, watashiriki katika na mafunzo maalum tokea tarehe 8 Novemba hadi 12, na kufuatiwa na mafunzo maalum trehe 13 hadi 16 Novemba hapo Kaikan Hall.
Sensei Fundi ataambatana na wana Karate wengine wa  chama hicho cha Jundokan mjini Taipei, Taiwan akitokea Marekani wiki moja tokea sasa na tayari kwa kongamano hilo 8 Novemba mjini Naha, Okinawa, Japan. Pia vilevile kutakuwa na warsha sambamba na mafunzo mbalimbali ya kujiliinda kufuatiwa na tafrija za kila siku jioni katika Hotel ya Orion mjini Naha kwa washiriki wote wa Jundokan toka pembe zote za dunia ikiwemo mabara yote. Pia vilevile sambamba na yote yaliyotajwa hapo, kutakuwa na heshima maalum kudhuru makaburi ya waanzishilishi hao kupata historia ya makumbusho ya Karate pia.

 Mahojiano aliyofanyiwa Sensei Fundi na gazeti la Okinawa Times Newspaper nchini Japan 
 Sensei Fundi akiwa na Masensei toka jumuiya za Ulaya Jundokan mjini Warsaw,  Poland

 Sensei Fundi akisimamia mazoezi ya pamoja  katika Dojo la Jundokan la Tanzania shule ya msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam


Sensei Fundi akichambua mbinu za kujilinda kiufanisi katika Dojo la Jundokan la Tanzania shule ya msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam

Mhini aenda kujiunga St Felix Uingereza, aahaidi kuleta medali ya kwanza ya kuogelea Tanzania

$
0
0
Muogeleaji, Dennis Mhini (wa nne kutoka kulia) akiwa na wazazi wake na ndugu na jamaa kabla ya kuondoka kwenda nchini Uingereza kuanza mafunzo ya mchezo wa kuogelea na kusoma katika shule ya St Felix.

Mugogeleaji wa Tanzania kutoka klabu ya  Morogoro, (Mis Piranha) , Dennis Mhini ameondoka jana kwenda Uingereza kuanza mafunzo ya mchezo huo pamoja na masomo katika shule ya St Felix. Dennis aliagwa na familia yake ikiwa pamoja na baba, Hamis Mhini na Mama, Bhoke Mukoji kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Muogeleaji huyo ambaye amepata nafasi ya kusoma na kujifunza mchezo huo kupitia kipahji chake amesema kuwa atahakikisha anatumia fursa hiyo vizuri na kuiletea Tanzania medali ya kwanza kupitia mchezo wa kuogelea.

“Ndoto zangu zimetimia, leo (jana) ndiyo naamini kuwa kupitia kipiaji changu na bidi katika masomo, naenda Uingereza kwa ajili ya nia moja tu, kuongeza ujuzi na

Dennis aliyeiwakilisha Tanzania katika michezo ya  Olimpiki ya Vijana nchini, Argentina amepata nafasi hiyo baada ya kufikiwa viwango vilivyowekwa na shule hiyo chini ya kocha maarufu, Sue Purchase. Kigezo cha kwanza ni ubora wake katika mchezo kuogelea baada ya kufikia muda unaotakiwa na pili uwezo wake wa darasani.

Baba wa mchezaji huyo, Hamis Mhini alisema kuwa mwanaye pamoja na kutoweza kutwaa medali Argentina, alifanikiwa kupunguza muda wake wa kuogelea, jambo ambalo limewavutia sana walimu na kocha maarufu wa mchezo wa kuogelea nchini uingereza, Sue Purchase. Mhini alisema kuwa hatua hiyo ni kubwa katika maendeleo ya mchezo wa kuogelea nchini kwani anaamini kuwa mwanaye ataiva na kuwa muogeleaji bora Tanzania na dunia.

Alisema kuwa Dennis anapenda sana mchezo wa kuogelea na ndiyo maana waliamua kumpa nafasi ya kufanya kile ambacho anakipenda na kufikia kiwango cha kufuzu michezo ya Olimpiki ya Vijana iliyofanika mjini Buenos Aires.

Katika michezo hiyo, Dennis aliweza kushika nafasi ya tatu katika kundi la kwanza kweye staili ya freestyle ya mita 100 kwa kupata muda wa sekunde, 58.53 na pointi 514 na vile vile kumaliza katika nafasi ya tatu kwa upande staili ya backstroke kwa mita 50 kwa kutumia sekunde 29.79 na kupata pointi 525.

Dennis alisema kuwa amefurahi sana kupata nafasi hiyo na kuahidi kufanya mambo makubwa kwa Taifa lake.

MWANZA KUFURIKA NA VIBE KAMA LOTE LA TIGO FIESTA 2018

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Wa Mwanza, Mhe. John Mongella akizungumza na waandishi wa habari leo kufungua rasmi pazia la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote litakalofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mkoani humo. Wengine pichani kushoto ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa,Uthman Madati na Msanii Nikki Wa Pili.
Mkuu wa Hifadhi ya Kisiwa cha Saanane kilichopo mkoani Mwanza, Beatrice Kessy akizungumza na waandishi wa habari na Wasanii watakaopanda jukwaa la Tigo Fiesta kesho jumamosi kuhusu umuhimu wa watalii na watanzania kutembelea kisiwa hicho.
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthman Madati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye mkutano wa uzinduzi wa Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote mkoani Mwanza. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella, Msanii Nikki wa Pili na Meneja wa Masoko Tigo Mkoa wa Mwanza, Kassimu Azziz. 

MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB AUNGANA NA TIMU YA MPIRA WA KIKAPU KATIKA MICHUANO YA MABENKI

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) akielekeza jambo wakati alipokuwa akiwapatia mawaidha wachezaji wa Timu ya Mpira wa Kikapu (Basket Ball) ya Benki hiyo, inayoshiriki michuano ya mabenki (Bankers Basketball League) iliyoanza kutimua vumbi leo katika viwanja vya Gymkana, Ocean Road jijini Dar es salaam. Nsekela alifika uwanjani hapo kuwapa hamasa vijana wake na kuwatakia ushindani uliokuwa mwema katika mchezo huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akiepana mkono na mmoja wa wachezaji wa Timu ya Mpira wa Kikapu (Basket Ball) ya Benki hiyo, inayoshiriki michuano ya mabenki (Bankers Basketball League) iliyoanza kutimua vumbi leo katika viwanja vya Gymkana, Ocean Road jijini Dar es salaam.
 Kikosi cha Timu ya Benki ya CRDB. 
 Mchezaji wa Timu ya Mpira wa Kikapu ya Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (kushoto) akiwa katika harakati za kutoka ngome ya wapinzani wao Benki ya DTB, katika mchezo uliopigwa leo katika viwanja vya Gymkana, Ocean Road jijini Dar es salaam.

MEJA JENERALI KINGU AONGOZA KIKAO CHA KUPITIA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MUUNDO MPYA WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, JIJINI DODOMA LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (kushoto), akizungumza na Wakuu wa Idara na Taasisi pamoja na maafisa mbalimbali wa Wizara hiyo, katika kikao cha kupitia taarifa ya utekelezaji wa muundo mpya wa Wizara hiyo kilichofanyika jijini Dodoma leo. Kushoto kwa Katibu Mkuu, ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima, akifuatiliwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Issa Ng’imba.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhan Kailima akizungumza katika kikao cha kupitia taarifa ya utekelezaji wa muundo mpya wa Wizara hiyo kilichofanyika jijini Dodoma leo. Kikao hicho kilihudhuriwa na Wakuu wa Idara na Taasisi zilizopo ndani ya Wizara hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (katikati), akizungumza na Wakuu wa Idara na Taasisi pamoja na maafisa mbalimbali wa Wizara hiyo, katika kikao cha kupitia taarifa ya utekelezaji wa muundo mpya wa Wizara hiyo kilichofanyika jijini Dodoma leo. Watatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima, na watatu kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Issa Ng’imba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (wapili kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima (kulia), pamoja na Wakuu wa Idara na Taasisi pamoja na maafisa mbalimbali wa Wizara hiyo, wakimsikiliza Mwasilishaji wa taarifa kwa niaba ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ASF Athuman Nassa, alipokua anawasilisha katika kikao cha kupitia taarifa ya utekelezaji wa muundo mpya wa Wizara hiyo kilichofanyika jijini Dodoma leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MAKAMU WA RAIS AWATAKA WANANCHI KULINDA MIUNDO MBINU YA MAJI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akizungumza wakati wa ziara yake ya Mkoa wa Pwani baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa tenki la maji la Kisarawe lenye uwezo wa kuhifadhi Lita Milioni sita kwa siku na kuupongeza uongozi wa DAWASA kwa kazi nzuri wanayofanya Leo Wilaya ya Kisarawe.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu amewataka wananchi wa Kisarawe kulinda miundo mbinu ya maji ili iwapatie maji safi na salama.

Mama Samia ameyasema hayo wakati akitembelea  mradi wa ujenzi wa tenki la maji la Kisarawe  lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita Milioni sita kwa siku.

Akizungumza baada ya kutembelea mradi huo,  Mama Samiaa ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa hatua kubwa wanayoifanya ya kutimiza azma ya mkoa wa Pwani kupata maji safi na salama.

Amesema kuwa, pongezi pia ziende kwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji inayoongozwa na Profesa Makame Mbarawa kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuhakikisha maji yanapatikana kwa uhakika kabisa sio tu Dar es salaam na Pwani bali Tanzania nzima.

Mama Samia amesema kuwa, kumekuwa na miradi kusuasua  ila kwa usimamizi wake wa Waziri wa Maji utaenda vizuri na maji yatapatikana.

"Kuja kwa mradi huu mkubwa wa maji utawapatia vijana ajira katika viwanda baada ya wawekezaji kuja na najua umeme upo na wa gesi unakuja,"amesema Mama Samia.

Kwa upande wa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amesema  mradi huu utagharimu bil 10.04 na fedha zote zitalipwa na DAWASA baada ya kukubaliana kwa mamlaka hizi kujiendesha zenyewe.

Mbarawa amesema kuwa mradi huu utakuwa chini ya kampuni ya Chico na utadumu kwa miezi minane na kufikia Julai 2019 utakuwa umekamilika na pia kutakuwa na ujenzi wa bomba la Km 5 kwenda Vigungu na Km 14 kwenda Viwandani, kujenga tenki litakalohifadhi maji Lita 480 na pampu nne kubwa na wananchi wa Kisarawe kupata maji kwa asilimia 100.

Katika kutekeleza miradi mbalimbali ya DAWASA imetengwa akaunti maalumu ambapo asilimia 30 ya mapato inawekwa kwenye akaunti hiyo kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema kuwa ana imani na DAWASA mpya na maji yatakuja Mkoa wa Pwani na uwepo wa mradi huu hali ya upatikanaji wa maji itabadilika. 

Amesema kuwa Serikali ya mkoa itatoa msaada kwa kandarasi ili maji yafike ikiwemo kutoa vibali mbalimbali kwa ajili ya kupitisha mabomba ya maji na kuna maeneo ya uwekezaji ikiwemo ujenzi wa viwanda ulikua unasuasua kwani walikuwa wakihitaji maji ila kwa sasa watakuja baada ya maji kufika Kisarawe.

Naye Waziri wa TAMISEMI na Mbunge wa Kisarawe Seleman Jafo ameshukuru kwa mradi wa maji kufika Wilaya ya Kisarawe na kupitia mradi huu wana kisarawe watakuwa wamenufaika kwa asilimia kumi.

Ameyataja maeneo ya Mzenga na Mwanalumango kuwa na shida kubwa ya maji na watu wa Kisarawe wanaishukuru sana serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kufanikisba mradi huu kwani ni mara ya kwanza toka kupata kwa uhuru.

Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Selemani Jafo akizungumzia mradi wa ujenzi wa Tenki la maji la Kisarawe lenye uwezo wa Kuhifadhi maji Lita Miliono sita kwa siku kuwa utawanufaisha Wananchi wa Kisarawe na kupata maji safi na salama kwa uhakika zaidi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akimuelezea Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu mradi wa ujenzi wa tenki la maji linalojengwa Kisarawe wakati wa ziara yake Leo.
 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Mbarawa akielezea jambo kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu wakati wa ziara yake ya Mkoa wa Pwani na kutembelea mradi wa ujenzi wa tenki la  maji la Kisarawe lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni sita kwa siku.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Samia Suluhu katika Wilaya ya Kisarawe leo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian  Luhemeja wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu alipotembelea mradi wa ujenzi wa tenki la Maji lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milioni sita kwa siku.


IGP SIRRO AKAGUA UJENZI WA NYUMBA ZA KISASA ZA KUISHI ASKARI NA FAMILIA ZAO MKOANI GEITA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Mhe Hamim Gwiyama (aliyesimama) akitoa neno mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, wakati alipofanya ziara ya kikazi katika wilaya hiyo iliyopo mkoani Geita leo 26/10/2018 kwa lengo la kukagua utendaji kazi wa Jeshi la Polisi na utolewaji wa huduma za kipolisi kwa wananchi, wengine ni wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akitoka kukagua nyumba  za makazi ya askari zitakazokuwa na uwezo wa kuchukua familia saba za askari wa jeshi hilo zilizopo wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, zinazojengwa na Watumishi House. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akitoka kukagua ujenzi wa nyumba zinazojengwa kwa ushirikiano wa wafayabiashara na wananchi wa Geita Mjini mkoani Geita leo 26/10/2018 ambapo jumla ya nyumba 20 zitakazokuwa na uwezo wa kuchukua familia 40 za askari Polisi zilizopo katika eneo la Magugu. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akimsikiliza kamanda wa Polisi mkoa wa Geita SACP Mponjoli Mwabulambo, wakati akimuonyesha moja kati ya eneo litakalotumika kujenga Ofisi za Makao makuu ya Polisi mkoani humo katika eneo la Magugu.

PROF.KAMUZORA: JAMII INAPASWA KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI ZINAZOWAKANDAMIZA WANAWAKE NA WATOTO NCHINI

$
0
0
NA MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera na Uratibu Prof.Faustin Kamuzora ameiasa jamii kutokomeza mila na desturi potofu zinazokwamisha maendeleo ya wanawake na watoto sambamba na kuwapatia fursa ya kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Wito huo ameutoa Oktoba 26, 2018 wakati akifungua mkutano wa Kamati Elekezi ya Taifa ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto uliohusisha Wizara 11 pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya wanawake na watoto nchini walipokutana mkoani Morogoro kujadili na kupitia Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.

“Jamii inapaswa kuwa mstari wa mbele katika kupinga mila na desturi potofu zinazokandamiza makundi haya na badala yake kutumia muda mwingi katika kuzalisha mali na kujishughulisha katika masuala ya maendeleo ili kuondokana na umasikini na kujiletea maendeleo”.alisema Kamuzora

Aidha Kamuzora aliongezea kuwa, jamii inapaswa kuendelea kusaidia jitihada za Serikali katika kutokomeza mila na desturi potofu kwa kuunga mkono mipango mikakati iliyopo na kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya masuala ya Haki na Usawa katika jamii.

“Tujitathimini na kuona namna bora ya kuondokana na mila na desturi zote zinazomkandamiza wanamke na mtoto ili kuendelea kusimamia zile zinazoiwezesha jamii kuwa na usawa na haki katika makundi yote bila kuwa na ubaguzi”
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (Kulia) akifungua kikao cha Kamati elekezi ya Taifa ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto kwa ajili ya kujadili Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kilichofanyika Mkoani Morogoro Oktoba 26, 2018 kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. John Jingu.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt.Laurean Ndumbaro akizungumza wakati wa kikao cha Kamati elekezi ya Taifa ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto kwa ajili ya kujadili Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kilichofanyika Mkoani Morogoro Oktoba 26, 2018 kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Amoni Mpanju.
 Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Afya (Maendeleo ya jamii) Bw.Mwambene Atupele akichangia jambo wakati wa kiako hicho.
 Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) kutoka Wizara ya Viwanda Bi.Zaytun Bagholleh akifafanua jambo wakati wa kikao kazi hicho.
 Mjumbe kutoka UNICEF Bi.Maud Droogleever akichangia jambo kuhusu ushirikishwaji wa Taasisi zisizokuwa za Kiserikali katika mapambano dhidi ya Utatili wa wanawake na watoto wakati wa kikao kazi hicho.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inathamini uwepo wa sekta binafsi nchini na kwamba inaendelea kushirikiana nayo katika kuboresha maendeleo ya Taifa.

Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Oktoba 27, 2018) wakati alipokutana na bodi mpya ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania kwenye makazi wa Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ampongeza Mwenyekiti wa taasisi hiyo Bw. Salum Shamte na wajumbe wa bodi hiyo kwa kuchaguliwa kuingoza taasisi hiyo. Bodi hiyo mpya ilikwenda kujitambulisha.

“Serikali inadhamira ya dhati ya kushirikiana na taasisi hii kwa sababu ndio muwezeshaji wa kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025,” amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa taasisi hiyo Bw. Shamte amesema sekta binafsi inatambua juhudi za Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara nchini Tanzania.

“Sisi tupo tayari kushirikiana na Serikali kwa kuwabana wafanyabiashara ambao wanaenda kinyume na maadili na sheria, ila tunaomba Serikali ishirikiane nasi katika utekelezaji wake.”

Pia, Bw. Shamte ameiomba Serikali iendelee kutoa vivutio kwa biashara zinazoanza ili kuhamasisha uwekezaji kwa kuwa baadhi yake zimeonesha gharama kubwa za uzalishaji.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Bodi Mpya ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dsr es salaam Oktoba 27, 2018.  Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Faustin Kamuzora na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Salum Shamte. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi Mpya ya Taasisi  ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) baada ya mazungumzo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es salaam, Oktoba 27, 2018. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Faustin  Kamuzora  na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Salum Shamte.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Salum Shamte  baada ya kukutana na wajumbe wa Bodi hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI KISARAWE

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wananchi mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za lami Kisarawe mjini, Makamu wa Rais yupo wilayani Kisarawe ikiwa sehemu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Kisarawe ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  TAMISEMI Mhe. Selemeni Jafo mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi wa tenki la maji litakalokuwa na uwezo wa kubeba lita milioni 6 katika eneo la Mnarani Kisarawe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Rock City Marathon kufanyika kesho

$
0
0
Mbio za Rock City Marathon msimu wa tisa zinatarajiwa kufanyika kesho jijini Mwanza. Maandalizi ya mbio hizo zinazotarajiwa kuanzia kwenye Daraja la Furahisha na kuishia kwenye viwanja vya Rock City Mall jijini humo yamekamilika huku zaidi ya washiriki elfu tano (3,000) kutoka ndani na nje ya nchi wakitarajiwa kushiriki katika mbio hizo.

Tayari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt Philis Misheck Nyimbi wamekwisha thibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo ambazo pia zitahusisha ushiriki wa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali, wabunge na washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi alisema kamati yake imejiandaa kupokea washiriki zaidi ya 3,000 wa mbio hizo kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wakimbiaji wa kimataifa.

“Tunatarajia kuwa na mbio zenye mafanikio makubwa mwaka huu. Maandalizi kwa kiasi kikubwa yamekwisha kamilika na kinaochoendelea kwa sasa ni usajili wa washiriki kutoka ndani na nje ya nchi na tunatarajia kufunga zoezi hilo siku ya Jumamosi Oktoba 27,’’ alibainisha.

Akizungumzia kuhusu zawadi, Ngowi alisema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh.mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi kumi nao pia wakiibuka na medali na pesa taslimu.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio  za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (katikati) akionesha mbele ya waandishi wa habari baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika kesho jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Mratibu Mtaalamu wa mbio za Rock City Marathon Bw John Bayo (kulia) na  Mwakilishi wa Kampuni ya Ulinzi ya KK Security ambao ni moja wa wadau wa usalama katika mbio hizo, Bw Andrew Maiga ndio
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio  za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (katikati) akionesha mbele ya waandishi wa habari baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika kesho jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Mratibu Mtaalamu wa mbio za Rock City Marathon Bw John Bayo (kulia) na  Mwakilishi wa Kampuni ya Ulinzi ya KK Security ambao ni moja wa wadau wa usalama katika mbio hizo, Bw Andrew Maiga ndio
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio  za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (katikati) akionesha baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika kesho jijini Mwanza.
 Mratibu Mtaalamu wa mbio za Rock City Marathon Bw John Bayo akizungumza kuhusu maandalizi ya mbio hizo.

Marais Kenyatta, Akufo-Addo watoa somo kwa vijana Afrika

$
0
0
Na Ripota Wetu-Lagos, Nigeria

MARAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya na Nana Akufo-Addo wa Ghana wamewataka vijana Bara la Afrika kuwa wabunifu na kumchangamkia fursa za kiuchumi ili kuiweza kusaidia nchini zao.

Kauli hizo wametoa hivi karibuni jijini Lagos nchini Nigeria kwenye jukwaa la nne la kila mwaka lililoandaliwa na Taasisi ya Tony maarufu Tony Elumelu Foundation (TEF), Entrepeneurship Forum.

Rais Uhuru Kenyatta, aliwahimiza vijana kutoka bara la Afrika kutumia ubunifu wao ili kuleta mabadiliko.“Viongozi vijana wabunifu kutoka Afrika wanapigana na mabadiliko yenye nia njema kwa kutumia teknolojia. Kuwa bora iwezekanavyo kwa familia, jamii, taifa yako lakini muhimu wewe mwenyewe,” amesema 

Rais Uhuru alisisitiza ushauri wake kwa vijana kufanya kazi ili kuwa bora kwa taaluma ambayo wamechagua.Tukio hilo ni fursa pekee ya kukusanya vipaji vya biashara kwa vijana, kujenga mitandao yenye nguvu na kupeleka ujumbe kwa watunga sera kwamba sekta binafsi iliyo mahiri na inawajibika inauwezo wa kuleta mabadiliko ya kiuchumi.

Baada ya kupata mafunzo ya miezi tisa, ushauri na ufadhili, jumla ya vijana 4,470 walifaidika na programu hiyo iliyoshuhudia zaidi ya vijana laki tatu wakituma maombi. Mwasisi wa jukwaa hilo, Tony Elumelu, alisisitiza kuendelea kujitolea kuhakikisha maendeleo ya uchumi Afrika kwa kusaidia mafunzo ya kizazi kipya cha wajasiriamali ambao mafanikio yao yanaweza yakabadili bara hili ikwemo kutengeneza ajira. 

“Ujasiriamali ni muhimu kufungua maendeleo ya uchumi katika bara letu. Naamini kwa dhati mafanikio yanaweza yakaleta demokrasia na kama tunaweza kubadili tamaa na kuwa fursa, hiki kizazi cha ajabu kinaweza kufanikiwa kwa kila jambo,” alisema Tony Elumelu.Naye Rais wa Ghana, Nana Akudo-Addo, aliwasisitizia wawakilishi wa sekta ya umma kuhimiza, kusaidia na kuiga kazi inayofanywa na Taasisi ya Tony Elumelu.“Hakuna kinachobadilika au kujiendeleza kivyake. Watu lazima waamke, waonge, wajadili na kubadilisha mada,” alisema Rais Nana Akufo-Addo.

Tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo, imeweza kuwasaidia wajasiriamali Waafrika kutoka pembe zote za Bara la Afrika na washindi katika mashindano mbalimbali katika jukwaa la mwaka huu walipata ufadhili wa dola za Marekani 5000 (takribani Shilingi milioni 11.4 kila mmoja). 
Mwasisi wa jukwaa hilo, Tony Elumelu (kushoto), akiwa na Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, kwenye jukwaa la TEF wakichambua kuhusu hali uchumi na umuhimu wa vijana Afrika kuwa wabunifu jijini Lagos, Nigeria
Mwasisi wa jukwaa hilo, Tony Elumelu (kushoto), akiwa na Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, wakiwa na kijana mshiriki wa kongamano kutoka nchini Ghana baada ya kijana huyu kutaka ufafanuzi kwa Rais wake wa namna vijana wanavyopewa kipaumbele katika ujenzi wa uchumi wa nchi hiyo.
Mwasisi wa jukwaa hilo, Tony Elumelu, akiwa na Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, wakiwa watendaji wa Taasisi wa Tony Emelu Foundation wakati wa uzinduzi wa tovuti ya taasisi hiyo jijini Lagos, Nigeria
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika wakiwa kwenye majadiliano wa maofisa Uhusiano wa Benki za UBA, jijini Lagos
Mshiriki wa kutoka Tanzania, Kinshaga akionesha bidhaa kwa washiriki wa jukwaa la TEF jijini Lagos, Nigeria 

Dkt. Ndumbaro awa Mgeni Rasmi maadhimisho ya Siku ya Mfalme wa Ubelgiji

$
0
0
Kampuni 32 kutoka Ubelgiji zilizowekeza Tanzania ni chache ukilinganisha na uwingi wa fursa za uwekezaji zilizopo nchini ambazo kwa kiasi kikubwa bado hazijatumika kikamilifu.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Mfalme wa Ubelgiji iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi jijini Dar Es Salaam tarehe 16 Oktoba 2018.

“Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji katika sekta mbalimbali kama vile; kilimo, ujenzi wa miundombinu, nishati, madini, teknolojia ya habari na mwasiliano, afya, viwanda vya uzalishaji, mafuta na gesi ambazo hazijatumika ipasavyo. Hivyo, Ubelgiji na Tanzania zikijizatiti zinaweza zikafanya biashara na kufanya uwekezaji mkubwa na wenye manufaa kwa pande zote mbili), Dkt. Ndumbaro alisema.

Alielezea matumaini yake kuwa ujio wa Makampuni makubwa ya Ubelgiji zaidi ya 40 ambayo yamekuwa na mazungumzo yenye tija na Makampuni ya Tanzania na sekta nyingine zinazohusika na uwekezaji kwa siku tatu zilizopita, utaleta ongezeko la uwekezaji na kuimarika kwa kiwango cha biashara kati ya Ubelgiji na Tanzania.

Kwa upande wa biashara kati ya Tanzania na Ubelgiji, Mhe. Naibu Waziri ameridhishwa na urari wa biashara uliopo, ingawa alisisitiza umuhimu wa kuimarisha zaidi. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016, biashara kati ya Ubelgiji na Tanzania imefikia kiwango cha Dola milioni 332 huku Tanzania ikiuza bidhaa zenye thamani ya Dola milioni 208 nchini Ubelgiji.

Dkt. Ndumbaro alihitimisha hotuba yake kwa kuishukuru Ubelgiji kwa kuendelea kuwa mshirika mkubwa wa jitihada za Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuwaletea Watanzania maendeleo. Alitoa mfano wa programu mbalimbali za maendeleo nchini zinazoghramiwa na Serikali ya Ubelgiji kwa kiasi cha Euro milioni 20.

Program hizo zinajumuisha upatikanaji wa maji safi vijijini na uendelezaji endelevu wa sekta ya kilimo katika mkoa wa Kigoma. Utekelezaji wa miradi hiyo imesaidia kuboresha usimamizi mzuri wa vyanzo vya maji, usimamizi wa rasilimali na mnyoro wa thamani katika kilimo, hususan kwa wakulima wadogo.

Kwa upande wake, Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania Mhe. Peter van Acker alisema kuwa Ubelgiji itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano za kubadalisha maisha ya watu masiikini. Alisema jitihada hizo pamoja na mambo mengine, zitaeendelea kuunga mkono juhudi za Tanzania za kuleta utulivu wa kisiasa katika eneo la maziwa makuu ikiwemo usuluhishi wa mgogoro wa Burundi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar Es Salaam, Tanzania
27 Oktoba 2018

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damasi Ndumbaro (Mb.) akihutubia kwenye hafla ya maadhimisho ya siku ya Mfalme wa Ubelgiji yaliyofanyika katika makazi ya Balozi wa Ubelgiji jijini Dar Es Salaam jana. Maadhimisho hayo yamehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya.

Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Mhe. Peter van Acker akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Mfalme wa Ubelgiji yaliyofanyika katika makazi yake jana.

Wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba zilizokuwa zikitolewa

Dkt. Ndumbaro akiendelea kuhutubia.

Dkt. Ndumbaro akigonganisha glasi na Balozi Peter van Acker kwa kuwatakia afya njema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Joseph Magufuli na Mfalme wa Ubelgiji

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb.) wa kwanza kulia akizungumza na Meneja wa mauzo wa Kimataifa wa kampuni ya Cardolite kutoka Ubelgiji Bw. Hans Carleer pamoja na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Mohamed Kamal (wa kwanza kushoto).

BASATA YATOA NENO MIAKA 20 YA TWANGA PEPETA

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images