Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

TPA YAWAASA WAHANDISI WAZALENDO KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI BANDARINI

$
0
0

WAHANDISI wazalendo wametakiwa kujipanga ili kuweza kuchangamkia fursa za uwekezaji katika miradi mbalimbali ya bandari nchini. 

Akizungumza wakati wa warsha iliyoandaliwa na Chama cha Wataalamu Washauri wa Wahandisi ‘Association of Consulting Engineers Tanzania’, (ACET), Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit C.V. Kakoko amesema wakati umefika kuchangamkia fursa zilizopo bandarini. 

Amesema kwamba japo malengo ya TPA kwenye warsha hiyo ni kuwafahamisha uwepo wa miradi mikubwa ya maendeleo hivyo kuchukua nafasi hiyo ili kuendeleza bandari kwa huduma zao kupitia miradi iliyopo na kuwaasa wachangamkie fursa zilizopo. 

“Bandarini kuna fursa ya kazi za ujenzi wa miundombinu katika nyanja zote kama ujenzi wa mitambo, umeme, mafuta, gesi na TEHAMA,” amesema Mhandisi Kakoko. 

Amesisitiza kwamba changamoto kubwa kwa sasa ni pamoja na kutochukua hatua za makusudi za kuchangamkia fursa kwa makampuni ya ujenzi ya ndani, uwezo mdogo wa makampuni ya wahandisi, wataalam wachache wenye weledi pamoja na vikundi vya taaluma kutoshirikiana. 

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akizungumza wakati wa warsha iliyoandaliwa na Chama cha Wataalamu Washauri wa Wahandisi ‘Association of Consulting Engineers Tanzania’, (ACET) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Picha ya pamoja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

JAMII YA WABARBAIGI WAPATA HATI MILIKI ZA KIMILA ZINAZOWASAIDIA KUPATA MAKAZI YA KUDUMU

$
0
0

NA FREDY MGUNDA,IRINGA
JAMII ya Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wameanza kuondokana na mfumo dume baada ya kukubali wanawake kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future unaotekelezwa katika wilaya za mkoa wa Iringa na Mbeya.


Wakizungumza wakati wa kukabidhiwa hati za kimira wanawake wa kibarbaigi walisema kuwa awali walikuwa hawaruhusiwi kumiliki mali yoyote ile bali mali zote zilikuwa zinamilikiwa na wanaume.

“Kwenye kabila letu mila zinawapa sana nafasi wanaume kumiliki mali na vitu vingine na kumfanya wanamke kuwa tegemezi jambo ambalo miaka ya nyuma limerudisha maendeleo nyuma ya wanawake” walisema wanawake hao wa Kibarbaigi

Wanawake hao walisema kuwa baada ya kupata elimu ya upimaji wa ardhi na kuifanya ardhi kuwa na hati miliki imesaidia wanaume wa kabila hilo kuanza kuitambua nafasi ya mwanamke na kumuwezesha mwanamke naye kumiliki mali sawa na wanaume wa kabila la wabarbaigi.

Tunaishukuru serikali na mradi wa LTA kwa elimu waliyoitoa kwa wanaume wa kabila la Barbaigi kwa kukubali wanawake wamiliki ardhi kwa kupewa hati miliki za kimira bila elimu hiyo wanawake sisi tungeendelea kuwa wakina mama wa nyumbani tu.

Naye mwenyekiti wa kabila hilo la wafugaji Shabani Ntasham alisema kuwa kupatikana kwa hati miliki za kimira kumekomesha hamahama ya jamii hiyo pamoja na kumuwezesha mwanamke wa jamii hiyo kumiliki ardhi.


Diwani wa kata ya Idodi Onesmo Mtatifikolo ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa utoaji wa hati hizo katika kijiji cha Kitisi ambapo jamii ya wabarbaigi wanaishi maeneo hayo nao walipewa hati miliki za kimira na kuanza kukomesha hama hama ya kabili hilo la wafugaji.
Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wameanza kuondokana na mfumo dume baada ya kukubali wanawake kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future
JAMII ya Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wakiwa kwenye picha na viongozi mara baada ya kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future
 

CHOO CHA SHULE YA MSINGI SELIAN WILAYANI ARUMERU CHATITIA ,DC MURO AONGOZA UOKOAJI

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

 HALMASHAURI ya Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha imepata changamoto ya kutitia na kuanguka kwa jengo la choo cha Shule ya Msingi ya Seliani iliyopo kijiji cha Olevolosi kata ya kimnyaki wilayani humo.

Ambapo katika tukio hilo Mkuu wa Wilaya wa Arumeru Jerry Muro kwa kushirikiana na viongozi wengine na wananchi wameweza kuokoa mwanafunzi mmoja wa kiume aliepata majeraha na bado wanaendelea na jitahada za kuondoa kifusi kilichochanganyikana na matofali.

Taarifa iliyotolewa Oktoba 26  na Muro ni kwamba choo ambacho  kimezama  kilikuwa na  matundu 20 .Hivyo katika kukabiliana na changamoto iliyotokea Muro ameliamua kuambatana na Katibu Katibu tawala wa mkoa na viongozi wa halmashauri ya Arusha wamefika eneo la tukio.Taarifa ya Muro ni kwamba baada ya kufika walianza kazi ya kuratibu jitihada za uokoaji wakishirkiana na vikosi vya uokoji na zimamoto pamoja na wananchi wa Kata ya kimnyaki.

"Jitihada hizo tulifanikiwa  kumuokoa mwananfunzi mmoja akiwa amejeruhiwa usoni na kukimbizwa katika hospital ya Seliani kwa matibabu zaidi ambapo mpaka sasa vikosi vya uokoaji vinaendelea na jitihada za kufukua kifusi na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 21 ambacho ndio choo pekee kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo," amesema Muro kwenye taarifa yake.

Amesema katika eneo la tukio kwanza walilazimika kurejesha hali ya amani na kutuliza taharuki za wananchi ambao baadhi wana watoto wanaosoma katika shule hiyo na kutoa nafasi kwa vikosi vya ukoaji kuendelea na zoezi la kutafuta wanafunzi wengine kutokana na kutokupatikana kwa taarifa za awali zinazoonesha idadi ya wanafunzi ambao huenda walikuwa kwenye choo hicho.

Hata hivyo kutokana na shule hiyo kuwa na choo kimoja chenye matundu 20 ambacho ndicho kilikuwa pekee kwa shule hiyo ilimlazimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru kuchukua hatua za kuzungumza na uongozi wa Kanisa la KKKT  Usharika wa Seliani na kuomba shule kutumia vyoo vya Kanisani ombi ambalo lilikubaliwa na Mkuu wa Jimbo la Arusha Magharibi Mchungaji Philemon Joseph Mollel aliyeungana na Mkuu wa Wilaya katika shughuli za uokoaji na hivyo kuondoa Mashaka ya kufungwa kwa shule.

Pia kutokana na kadhia hiyo ilimlazimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Muro kuzungumza na wananchi waliojitokeza ambapo katika mazungumzo yake aliwataka wananchi kutulia na kutoa fursa ya kuendelea kwa zoezi la utoaji wa kifusi ili kujirisha na madhara zaidi ambayo huenda yametokea.

Awali baadhi ya wananchi waliungana na Muro katika kuchanga fedha kwa ajili ya kuanza mikakati ya ujenzi wa choo kingine ili kutokwamisha masomo ya wanafunzi kazi ambayo ilifanywa na Mkuu wa Wilaya pamoja na viongozi wa Kanisani na halmashauri na kuitikiwa kwa wingi na wananci wailiotoa Fedha zao.Wakati huo huo Muro alilazimika kumtembelea majeruhi ambae amelazwa katika Hospitali ya Seliani na kumjulia hali huku akiongozana na viongozi mbalimbali.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro akimjulia hali mmoja wa wanafunzi aliyejuruhiwa usoni na kukimbizwa katika hospital ya Seliani kwa matibabu zaidi kufuatia kutitia na kuanguka kwa Jengo la choo cha shule ya Msingi ya Seliani katika kijiji cha Olevolosi kata ya kimnyaki Wilaya ya Arumeru 
vikosi vya uokoaji vikiendelea na jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo.
vikosi vya uokoaji vikiendelea na jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo.
vikosi vya uokoaji vikiendelea na jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo. 
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro akizungumza na wananchi waliojitokeza kushuhutia tukio hilo,ambapo katika mazungumzo yake aliwataka wananchi kutulia na kutoa fursa ya kuendelea kwa zoezi la utoaji wa kifusi ili kujiridhisha na madhara zaidi ambayo huenda yametokea.

KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA>>>>>>>

USIKU WA MASAUTI YA JIDEE KUPAMBWA NA ZAHARA PAMOJA NA JULIANA KANYAMOZE MLIMANI CITY LEO

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
MWANAMZIKI  mkongwe nchini Judith Wambura maarufu kama komando binti machozi lady jdee amewatambulisha rasmi wasanii kutoka nje ambao watatumbuiza usiku wa sauti siku ya leo katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es salaam.

Aidha , jidee ameeleza ujio wa  wasanii wenzake Zahara kutoka Afrika kusini pamoja na Juliana kanyamoze kutoka Uganda kuwa ni kuonyesha hadhira kuwa vipaji bado vinaishi na kukonga mashabiki pia kwani wasanii wakike ni wachache sana na ameona kuwapa fursa hiyo wasanii wakike wapate hamasa na kuendeleza vipaji vyao na kutimiza. 
  
Alikadhalika jidee amekaribisha wasanii wengine kujumuika Kwenye usiku huo na mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Naibu Waziri mwenye dhamana ya habari,sanaa ,utamaduni na michezo Juliana shonza.

 Aidha amewataja wasanii kama Damian soul pamoja na grace matata watakuepo Kwenye usiku huo kama wasanii wa ndani ya nchi na ambao wanavipaji lukuki.  

Msanii wa kike kutoka nchini Uganda Juliana Kanyamoze amefafanua juu ya kuwa na mashabiki wengi kutoka nchini Tanzania huku akiwa na nyimbo ambazo zinawakonga kutokana na kutumia lugha ya kiswahili wakati hawezi kuongea kiswahili fasaha.

Kanyamoze amesema usiku huo atasherehesha na  nyimbo zote alizoimba kwa lugha Kiswahili kwani Zina wapenzi wengi hasa wimbo alioimba na msanii Bushoke wa nchini unaojulikana kama usiende mbali.

 Na pia amewaomba mashabiki wakae mkao wa kula kwani kazi yake mpya ataitambulisha hivi karibuni ambayo ni miondoko ya injili.

Mwanamziki mkongwe nchini Judith Wambura akizungumza na wanahabari wakati wa kutambulisha wasanii ambao watapamba usiku wa masauti Mlimani city katika akiwa zuhura kutoka nchi ya afrika kusini ,wa mwisho kushoto ni msanii Juliana kanyamoze kutoka uganda.
 Msanii wa kike kutoka nchini Uganda Juliana Kanyamoze akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

CHOO CHA SHULE YA MSINGI SELIANI CHATITIA, WANAFUNZI WAHOFIWA KUZAMA

$
0
0
 Wakazi wa Jiji la Arusha wameingiwa na hofu kubwa baada ya choo cha shule ya msingi Seliani kutitia na kujeruhi mwanafunzi mmoja huku wengine wakihofiwa kufukiwa. Mkuu wa wilaya ya Arumeru iliyopo mkoani humo, Jerry Murro amewaomba wananchi kuwa watulivu, wakati wa ufukuaji wa vifusi vilivyoporomoka katika choo hicho ili waweze kuona kama kuna wanafunzi wengine wamefukiwa ama la, ingawa inadaiwa kuwa walikuwa zaidi ya mmoja ndani ya choo hicho. Pichani ni jitihada za uokoaji zikiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru iliyopo mkoani humo, Jerry Murro akizungumza na wananchi wa eneo hilo walofika eneo la tukio.

JAJI MSTAAFU AWAASA WADAU WA MAHAKAMA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI

$
0
0
Na Karama Kenyunko,Globu ya Jamii

JAJI mstaaafu Mahakama Kuu ya Tanzania, Aloycisious Mujulizi amewaasa wadau wa mahakama na wasomi waliopo kwenye tasnia ya sheria kuacha kutumia lugha ya Kingereza pale wanapofanya shughuli zao hasa wakati wa kuandika ushahidi na hukumu badala yake watumie lugha ya kiswahili kwa kuwa inajylikana na watanzania walio wengi.

Jaji Mujuluzi ameyasema hayo leo Oktoba 26.1018 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kuwaaga kitaaaluma majaji saba  wa mahakama kuu waliostaafu wamestaafu. Amesema hakuna haja kwa mahakama kutumia lugha ya kingereza kama lugha rasmi ya kunukuu kumbukumbu za mahakama na kuongeza, jambo hilo likiachwa liendelee wananchi wataendelea kuamini kuwa vyombo vya utoaji haki zinakula rushwa wakati si kweli. 

Amesema, kama lugha ya kiingereza ikiachwa iendelee basi wala rushwa watatumia kivuli hicho kuhararisha mambo yao hivyo ili kuondokana na uwepo wa ukalimani mahakamani jaji au Hakimu aandike kwa kiswahili ushahidi wote unaotolewa mahakamani hata hukumu pia lakini anavyopokea neno la kishwahili na kuandika kwa kingereza.

"Lugha ya kiswahili imefanywa kuwa ya taifa lakini pia anaamini lugha nyingine za kienyeji zinapaswa kuendelezwa katika vyuo mbalimbali nchini na kuandikwa kwenye vitabu ili iwasaidie majaji wanaopelekwa mkoani kuweza kusoma vitabu hivyo". Amesema.Ameongeza, kitu kingine kinachowafanya baadhi ya watu kutoiamini mahakama ni pale ushahidi unaotolewa kukutwa umeandikwa tofauti jambo linalochangiwa na majaji kutokuwa na utaalamu wa kuandika kwa ufupi na wingi wa kazi. 

Wote tunafahamu kuwa ukiwa unaandika uwezi kuwa wakati huo huo unamuangalia kwa umakini usoni shahidi anayetoa ushahidi mbele yako  kwahiyo mimi naona hakuna haja ya kutumia kingereza ni vema tuondokana Kabisa.

Naye Jaji Kiongozi Mahakama kuu ya Tanzania,  Dk. Eliezer Feleshi amesema anatambua kuwa yapo maeneo ambayo yanahitaji maboresho hasa mifumo ya kuwezesha usikilizwaji wa kesi.Amesema mahakama inaendelea na kazi yake ya kufanya maboresho na kwamba ni safari ya muda mrefu ambayo bado wanaendelea nayo kwa kuchukua hatua mbalimbali. Ukiwemo na mpango mkakati wa kumrahisishia jaji au hakimu kuandika hukumu, 

Aidha amesema kupitia kwa majaji wastaafu wamejifunza mambo mengi hasa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii kwa kufuata misingi ya haki na utawala bora. 
 Jaji kiongozi Elieza Fereshi watatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya majaji mara baada ya hafla fupi ya kuwaaga kitaaaluma majaji saba  wa mahakama kuu waliostaafu wamestaafu. 
Jaji kiongozi Elieza Fereshi watatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya majaji mara baada ya hafla fupi ya kuwaaga kitaaaluma majaji saba  wa mahakama kuu waliostaafu iliyofanyika leo jijini Dar Es Salaam katika ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu.
Jaji kiongozi Elieza Fereshi akimkabidhi ua jaji mstaaafu Mahakama Kuu ya Tanzania, Aloycisious Mujulizi mara baada ya hafra ya kuwaaga kitaaluma iliyofanyika leo jijini Dar Es Salaam katika ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu.

MBIO ZA NAMTUMBO SELOUS MARATHON ZAZINDULIWA JIJINI DAR,KUFANYIKA NOVEMBA 10, 2018 NAMTUMBO MKOANI RUVUMA

$
0
0
Kwa mara nyingine tena zile mbio ambazo zimekuwa zikisubiriwa kwa hamu na shauku kubwa na wakazi wa mkoa wa Ruvuma na vitongoji vyake hususan wilaya ya Namtumbo maarufu kama Namtumbo Selous Marathon zimewadia ambapo tarehe rasmi ya kufanyika kwa mbio hizo imetangazwa kuwa tarehe10 Novemba2018. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa mbio hizo jijini Dar EsSalaam, Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh. Sophia Kizigo amesema kuwa mbio hizo zilizoanza rasmi mwaka jana chini ya udhamini wa kampuni ya madini ya Uranium one na kampuni ya Nyuklia ya Rosatom ya Urusi zinalenga kukusanya kuchangisha fedha na vifaa vya ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo ambapo ujenzi wa baadhi ya majengo umekwisha anza tangu mwaka jana na kwamba unatarajiwa kuendelea tena mwaka huu. 

Nina kila sababu ya kuwashukuru sana wadhamini wa mbio hizi wenzetu Uranium One na Rosatom kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakijitolea kuhakikisha kuwa mbio hizi sio zinafanyika lakini pia malengo yake kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana pia tunawashukuru wadau mbalimbali wakiwemo chama cha riadha, wafanyakazi na uongozi wote wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo na wananchi wa Namtumbo kwa ujumla kwa michango mbalimbali. 

Naomba pia ni shukuru makampuni na wale wote waliokwisha kuchangia ujenzi wa hospitali hii ya Namtumbo. Makampuni hayo ni MMI, FB Attorney, Namis Corporate, Tanesco, BOT, ITV/Radio One, Halotel, Tulia Trust, wabunge wa mkoa wa Ruvuma, Ma DC na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. 

Kwa upande wake kampuni Uranium One na mwakilishi wa Rosato amesema kuwa mbio hizo pamoja kulenga kuboresha miundombinu ya afya katika wilaya ya Namtumbo, mbio hizo pia zinaleta umoja na mshikamano mzuri baina ya serikali sekta binafsi na wananchi kwa ujumla huku ikihamasisha afya kwa njia ya mazoezi. 

Nao waratibu wa mbio hizo wamewataka watanzania wanaopenda michezo wajitokeze kwa wingi kushiriki katika mbio hizo za KM 21, KM 10, KM 5, na KM 2.5 ambapo walitaja njia nzuri ya kujisajili kuwa ni kutuma ujumbe kwenda runselous2018@gmail.com ambapo kuanzia miaka 16 na kuendelea watashiriki KM 21 na KM 10 lakini KM5 na 2.5 zitawahusu wazee na watoto 

Mbio hizo zinatarajiwa kudhuriawa na wakimbiaji kutoka mataifa mbalimbali kama Marekani, Japan na Urusi ambako wafanya kazi wa kampuni ya Uranium nao watakuja kushiriki mbio hizo. 

Kujisajili: kupitia ofisi ya mganga mkuu wa wilaya ya Namtumbo na barua pepe runselous2018@gmail.com

Mahala: Mbio zote zitaanzia na kuishia Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo 
Muda: Mbio zitaanza saa 12 asubuhi 


“PAMOJA TUNAWEZA” 

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh. Sophia Mfaume Kizigo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Namtumbo Selous Marathon zitakazofanyika Namtumbo,Mkoani Ruvuma Novemba 10 mwaka huu.Kulia ni mwakili kutoka Mantra(Uranium One) Tanzania Mrs Khadija Pallangyo, na kushoto ni katibu wa afya wilaya ya Namtumbo.
Mwakilishi kutoka Chama cha Riadha Tanzania RT Iddi Muhunzi (kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Namtumbo Selous Marathon zitakazofanyika Namtumbo mkoani  Ruvuma Novemba 10 mwaka huu. Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Namtumbo na kulia ni mwakili kutoka Mantra(Uranium One) Tanzania Mrs Khadija Pallangyo.
Mwakilishi kutoka Chama cha Riadha Tanzania RT Ombeni Zavala akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Namtumbo Selous Marathon zitakazofanyika Namtumbo mkoani  Ruvuma Novemba 10 mwaka huu.

JESHI LA POLISI LATOA RAI KWA WAZAZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO

$
0
0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa rai kwa wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao wadogo ikiwa ni pamoja na kuwawekea uangalizi mzuri kwa muda wote ili kuepuka madhara yanayoweza kuwapa watoto hao pindi wanapokuwa wenyewe.

Kwa kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na matukio ya watoto kuanzia umri wa miaka 03 hadi 12 kufariki kutokana na kutumbukia katika visima vya maji, katika mabwawa ya maji au katika mito pindi wanapovuka kuelekea Shuleni.

Kuelekea msimu wa mvua ambazo kwa baadhi ya maeneo tayari zimeanza kunyesha na kuleta madhara kwa binadamu. Yapo mambo ya kuepuka hasa matumizi ya vifaa vya umeme kama vile redio, tv na simu za mkononi wakati mvua kubwa zinazoambatana na radi zikinyesha.

Kwa Mkoa wa Mbeya mvua zilizonyesha maeneo ya Kyela na Mbalizi zimesababisha vifo vya watu watatu ambao walifariki dunia kwa kupigwa radi huku mmoja kati yao alipigwa na radi wakati akisikiliza radio.

Pia tunatoa angalizo kwa watu wanaofanya shughuli za uchimbaji madini katika migodi, kuchukua tahadhari za kiusalama ili kuepuka ajali katika maeneo hayo hasa za kuangukiwa vifusi vya udongo hususani msimu wa mvua. Tunapaswa kuchukua tahadhari kwa kufukia mashimo yasiyokuwa na dhahabu kwani ni hatari kwa watoto na watu wazima pindi wanapojaa maji.

Ni wito wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuzingatia ulinzi wa mtoto, malezi bora kwa mtoto na pia kuwasaidia watoto hasa kuwavusha katika maeneo yenye mito au maji mengi ili kuepuka madhara yanayoweza kuwapata. Pia ni kipindi cha kufukia mashimo, madimbwi yenye maji kwa ni hatari hasa kuelekea msimu wa mvua.

Imetolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.

MIKAKATI YA DAWASA KATIKA KUWAPATIA HUDUMA YA MAJI MKOA WA PWANI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Tenki maji Bagamoyo ni moja ya mifumo ya matenki matano yaliyojengwa chini ya mradi wa uboreshaji wa mfumo wa usambazaji maji. Mradi huu unaotekelezwa kwa ushirikiano na Serikali ya India kwa thamani ya jumla ya dola za Marekani milioni 39.


Mkandarasi anayejenga huu mradi ni Jain Invngetic ya India akishirikiana na subcontracts Shanxi ya nchini China na mshauri ni WAPCOS kutoka India. Mradi pia umehusisha ujenzi wa vituo vinne vya kusukuma pampu za maji, ujenzi wa matanki, ufungaji wa pampu na transfoma katika vituo hivyo pamoja na ulazaji wa mabomba ili kupeleka maji katika matenki hayo.

Aidha mradi pia umehusisha ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji katika maeneo ya Salasala, Wazo, Bunju na ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji kati ya maeneo yaMbezi na Kiluvya na kwa upande wa Bagamoyo bomba maalum la kupeleka maji katika eneo la viwanda EPZA pamoja na bandari mpya limelazwa. Chini ya mradi huu, jumla ya mabomba ya kipenyo cha kati ya milimita 63 na 400 kwa urefu wa jumla ya kilometa423.899 yamelazwa, mwisho wa mkataba huu ni tarehe 31/10/2018.


 Tunaamini kwa kufanya hivi wametoa mchango stahiki katika kuwezesha eneo letu la huduma hususani Bagamoyo kutekeleza wajibu wake wa kulifikisha Taifa katika uchumi wa kati.


Tenki la Bagamoyo pamoja na matenki mengine matatu yaliyopo Mabwepande, Wazo na Salasala yana uwezo wa kuhifadhi lita milioni sita za maji kila moja na tenki la Changanyikeni lina uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni tano. Matenki yote yaliyopo Dar es salaam yamegawanywa katika sehemu mbili zenye ujazo sawa ili kuwezesha usafi, matengenezo ama ukarabati kufanyika katika sehemu moja na kuruhusu sehemu ya pili kuendelea kutumika na hivyo kutokuathiri huduma kwa wananchi.

Tenki hili la Bagamoyo, tofauti na matenki mengine chini ya mradi huu, limegawanywa katika sehemu nne na halina kituo cha kusukuma maji. Hii ni kwa sababu maji yake yanatoka hapa jirani katika toleo la bomba kuu kutoka Ruvu Chini ambao ndiyo mtambo wa maji mkubwa kuliko yote nchini wenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 270 kwa siku.

Pampu zake zina uwezo wa kusukuma lita 3,125 kwa sekunde na kurusha maji mita 75 kwenda juu. Hivyo basi maji yanaweza kufika katika tenki hili liliopo jirani bila tatizo. Bagamoyo ni mji ambao upo katika uwanda wa tambarare hivyo tenki hili lipo katika eneo lililo na muinuko mkubwa kuliko maeneo mengine mjini hapa Bagamoyo; hivyo litawezesha maji kufika katika maeneo yote yanayolengwa kwa msukumo (pressure) wa viwango vinavyotakiwa.

DAWASA imekuwa ikishirikisha wadau mbalimbali katika kutekeleza miradi yake, ikiwa ni pamoja na viongozi wa wananchi. Katika moja ya ziara za ukaguzi wa ujenzi wa mradi huu, Mheshimiwa Mbunge wa Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa aliomba tenki dogo la zamani lililopo katika ofisi za Mkuu wa Wilaya liunganishwe na Mfumo huu ili liweze kuhudumia wananchi waliopo jirani na tenki hili; na kuruhusu tenki hili kuhudumia wakazi waliopo mbali ikiwemo na maeneo ya kibiashara na mahoteli ya kitalii kwa ajili ya maendeleo ya mji wa Bagamoyo na Taifa kwa ujumla. DAWASA ni Mamlaka sikivu na yenye kupenda kuwatumikia Wananchi, hivyo napenda kutoa taarifa rasmi kuwa Mkandarasi alielekezwa kufanya kazi hii, hivyo atakamilisha kati ya 31/10/2018, baada ya kusafisha tenki (disinfection) wakati tukisubiri Mkandarasi wa kujenga distribution/mtandao apatikane chini ya mradi wa World Bank.

Tenki hili la Bagamoyo linatarajiwa kuhudumia wakazi wa mji wote wa Bagamoyo navitongoji vyote vinavyozunguka mji pamoja na vitongoji vya Bongwa, Nianjema, Magomeni, Mangesani, Mianzini, Tandika, Mahotelini, Majani mapana, Majengo, Kidongo chekundu, Kisingani, Saigoni, Mantep, Mji Mpya, Kisutu, Kimala Ng’ombe, Block Pukuni, Sanzale, Polisi, Magambani, Kaole, Chumvi, Makarani, Hospitali, Chunguuni, Msalabani na maeneo ya Shule ya sekondari na chuo kikuu kishiriki_Marian.

Mradi wa Maji wa EPZ tayari bomba la kipenyo cha 400mm limelazwa umbali wa Km 5
la kipenyo cha 400mm limelazwa kwa ajili ya maeneo ya viwanda, Mkandarasi ilitakiwa kukabishi kabla ya tarehe 31/10/2018.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akimuonyesha Makamu ww Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu tenki la maji la mradi wa maji wa Bagamoyo unaotekelezwa na Mamlaka hiyo chini ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakati alipotembelea ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milion sita kwa siku.

RC MAKONDA AMUAGIZA AMBER RUTTY KUFIKA KITUO CHA POLISI LEO KABLA YA SAA 12 JIONI

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemuagiza mwanadada Amber Rutty anayejihusisha na masuala ya muziki wa bongo fleva nchini kufika katika kituo chochote cha Polisi hapa jijini leo  kabla ya saa 12 Jioni.

Rc Makonda kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka picha ya mwanadada huyo na kuandika haya :

"Wakati TCRA wakijipanga kuchukua hatua, mimi namtaka mwenye picha hii kufika kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu na eneo lake kabla ya saa 12 jioni. Na ukifika waambie umeitwa na RC Makonda watakupatia ujumbe wako" ameandika  Makonda.

Hii inakuja baada kwa kosa la matumizi mabaya ya mtandao  linalomkabili kwa kusambaza Video ya  yenye maudhui ya kingono
na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuleta sintofahamu kubwa kwa Wanajaamii.

BREAKING NEWZZZZ: MKURUGENZI MTENDAJI WA PRIDE RASHID MALIMA ASAKWA NA TAKUKURU, UKWEPAJI KODI SOKO LA KARIAKOO WABAINIKA

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) imetoa ripoti ya matukio  ambayo ni mkakati wa kitaifa dhidi ya rushwa na mpango wa utekelezaji wa awamu ya tatu  unaoratibiwa na kitengo cha uratibu wa utawala bora ofisi ya Rais Ikulu katika kupiga vita vitendo vya rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Brigedia Jenerali John Mbungo amesema kuwa aliyekuwa mkurugenzi  mtendaji wa taasisi ya PRIDE  inayojihusisha na utoaji wa mikopo kwa wananchi hasa akina mama ili kuwainua kiuchumi Rashid Malima (60) anatafutwa kwa tuhuma za kughushi nyaraka na ubadhilifu wa fedha za umma.
Amesema kuwa taasisi hiyo iliundwa kwa lengo la kusaidia wananchi wenye kipato kidogo na ilipata mtaji wake wa kwanza wenye thamani ya dola za kimarekani 4,000  kutoka Norway  kupitia NORAD.
Mbungo ameeleza kuwa katika vipindi mbalimbali kati ya mwaka 2015/2017 Malima na wenzake walifanya ubadhilifu wa fedha za kampuni ya PRIDE za kiasi cha shilingi Bilioni moja na milioni nane  na kuandaa malipo hewa kwa watoa huduma mbalimbali yakiwemo Arusha Art, Antelop Safaries, Essence international na paperwork na pia waliandaa malipo ya salary advance ambayo hayakufuata taratibu na baadaye fedha hizo zote walizichukua na kuzitumia kwa matumizi yao binafsi.
Aidha amesema kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kutoroka nchini punde tu uchunguzi wa tuhuma hizo ulipoanzishwa mwaka 2018 na taarifa zilizopo ni kwamba alitoroka kupitia eneo la Namanga, na inasemekana kuwa yupo nchini Marekani hivyo amewaomba watanzania nchini na wale wanaoishi Marekani kutoa taarifa za mtuhumiwa huyo ili sheria ifuate mkondo wake.
Naibu Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kutafutwa kwa watuhumiwa waliokimbia baada ya kutenda makosa ya rushwa, wizi na ubadhilifu wa fedha za umma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

AMBASSADOR SLAA PRESENT LETTER OF CREDENCE TO THE PRESIDENT OF FINLAND

$
0
0
On 25th October 2018, Ambassador Dr. Willibrod Slaa presented his Letter of Credence to the President of the Republic of Finland H.E Sauli Niinistö in Helsinki Finland. The Ceremony, included the presentation of letter of Recall for other departing Ambassadors and letter of credence by new Ambassadors accredited to Finland. 
The Credential Ceremony at The Presidential Palace: Arrival of Departing and New Ambassadors Accredited to Finland  
The Credential Ceremony at The Presidential Palace: Arrival of Departing and New Ambassadors Accredited to Finland  
Ambassador Slaa presenting Letter of Credence to H.E Sauli Niinistö, President of the Republic of Finland
Ambassador Slaa after presenting Letter of Credence to H.E Sauli Niinistö, President of the Republic of Finland
Ambassador Slaa was Accompanied By Ms. Prosister Swai, Administrative Attache of the Embassy of Tanzania in Stockholm.
All Photos: Courtesy of Juhani Kandell and Matti Porre - Office of the President of the Republic of Finland

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 26.10.2018

UTALII WA NDANI WASHAMIRI KISIWA CHA SAANANE, MWANZA

$
0
0
Na Mandia Zephania, Mwanza
Watanzania wametakiwa kutambua umuhimu wa utalii wa ndani kwa kujenga desturi ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuongeza uelewa wa maswala mbalimbali pamoja na kujionea vivutio mbalmbali katika hifadhi hizo.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi hiyo BEATRICE KESSY amesema hifadhi hiyo imelenga kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi hiyo kutoka elfu kumi kwa mwaka hadi kufikia elfu kumi na tatu kwa mwaka kupitia kampeni ya GUDUA HAZINA ZA UTALII MWANZA inayohamasisha wanafunzi kutembelea hifadhi hiyo.

Hifadhi ya taifa ya saa nane ni hifadhi pekee iliyopo katikati ya jiji la Mwanza ikiwa ni hifadhi pekee iliyopo katikati ya jiji yenye vivutio mbalimbali ikiwemo wanyama  na manthari ya kuvutia.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi hiyo BEATRICE KESSY amesema kuanzishwa kwa kampeni ya GUDUA HAZINA ZA UTALII MWANZA, imejikita kuhamasisha utalii wa ndani pamoja na kuongeza idadi ya watalii katika hifadhi hiyo.

GLORIA MWIHAMBO msimamizi wa bodi ya utalii kanda ya ziwa (TTB),amesema ukilinganisha na miaka iliyopita watanzania wamepata muamko wa  kutembelea hifadhi mbalimbali nchini.
Watalii kutoka hao kutoka vyuo mbalimbali vya mkoa wa Mwanza wamesema imekuwa fursa kwa wao kuongeza uelewa katika masomo yao pamoja na kufurahi vivutio mbalimbali katika hifadhi hiyo.

Hifadhi hiyo iliyopo chini ya Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) limeanzisha kampeni hiyo itakayodumu kwa siku tatu ambapo pamoja na kutembelea hifadhi hiyo wanafunzi hao watashiriki michezo mbalimbali pamoja na kutoa zawadi kwa mwanafunzi  atakaye  tangaza hifadhi hiyo vyema kupitia mitandao ya kijamii.
MWISHO




Muhimbili yawatunuku vyeti Makatibu Muhtasi nchini

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imehitimisha leo mafunzo ya elimu ya jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa ukimwi kwa makatibu muhtasi kutoka mikoa mbalimbali nchini na kuwatunuku vyeti vya ushiriki.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Muhimbili kwa kushirikiana na Chama cha Makatibu Muktasi Tanzania (TAPSEA) yaliyodumu kwa muda wa siku tatu ambapo wametarajiwa kuisambaza elimu hiyo kwa watu wengine ili wafahamu namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.
Akizungumza kabla ya kuwatunuku vyeti makatibu muktasi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru amesema wameweza kutekeleza moja ya azma ya hospitali ya na sera ya serikali ya kutoa elimu ili makatibu muktasi waweze kujikinga na ugonjwa huo.
“Naomba elimu hii iwe endelevu na mkawe mabalozi wazuri katika kuonyesha manufaa ya mlichojifunza hata kwa wale ambao mtawakuta katika maeneo yetu ya kazi na jamii kwa ujumla,” amesema Prof. Museru.
Alitumia nafasi hiyo pia kuwaeleza kuwa hospitali inajipanga kuandaa mafunzo mengine ambayo yatazungumzia mada mbalimbali kulingana na jinsi makatibu muktasi watakavyopendekeza ili kuwasaidia katika maeneo yao ya kazi pamoja na katika maisha yao kila siku.
Aidha Prof. Museru ametoa rai kwa jamii kuwa wazi pindi mtu anapogundulika kuwa ameathirika na ugonjwa wa ukimwi na kuanza kuchukua hatua za haraka ili kuweza kupata matibabu kwa wakati ili kujikinga na kuwakinga wengine.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akimkabidhi cheti Katibu Muhtasi wa Mamlaka ya Bandari Zanzibar, Bi. Zainabu Abdallah baada ya mkurugenzi huyo kuhitimisha mafunzo ya siku tatu jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa ukimwi.  
 Mmoja wa makatibu muhtasi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro, Bi. Farida Mfaume akipokea cheti cha ushiriki baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo leo.
 Katibu Muhtasi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Neema Makuluni akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Museru.
 Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo leo ambayo yamefanyika kwa siku tatu kwenye hospitali hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru akiwa katika picha ya pamoja na washiriki baada ya kufunga mafunzo hayo leo.

TRA YAWABANA WANAOKWEPA KUTOA NA KUDAI RISITI ZA EFD.

MATUKIO KATIKA PICHA SPIKA NDUGAI AKIFUNGA MAONYESHO YA ASASI ZA KIRAIA 2018 YALIYOFANYIKA JIJINI DODOMA

$
0
0


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto)akimkabidhi tuzo ya Mshindi wa kwanza Mwenyekiti wa taasisi ya uhamasishaji uwazi na uwajibikaji katika raslimali za madini, mafuta na gesi asilia Bw. Ludovick Utoh alieipokea kwa niaba ya Haki Ardhi katika maonyesho ya wiki yaAsasi za Kiraia 2018 yenyekaulimbiu “Tanzania ya Viwanda: Watu, Sera na Utekelezaji” katika tukio lililofanyika leo tarehe 26 Octoba, 2018 katika ukumbi wa African Dream Jijini Dodoma. Katikati ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mhe. Fatma Toufiq

Spikawa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wasabakushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mbali mbali kutoka Asasi za kiraia baada ya kufunga maonyesha ya Asasi za kiraia 2018 yenye kauli mbiu “Tanzania ya Viwanda: Watu, Sera na Utekelezaji” yaliyofanyika leo tarehe 26 Octoba, 2018 katika ukumbi wa African Dream Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na washiriki mbali mbali kutoka Asasi za kirai (hawapo kwenye picha) wakati akifunga maonyesho ya Asasi za Kiraia 2018 yenye kauli mbiu“Tanzania yaViwanda: Watu, Sera na Utekelezaji” yaliyofanyika leo tarehe 26 Octoba, 2018 katika ukumbi wa African Dream Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto mbele) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS), Bw. Francis Kiwanga (wa pili kulia) wakielekea katika ukumbi wa African Dream kwa ajili ya kufunga maonyesho ya Asasi za Kiraia 2018 yenye kauli mbiu “Tanzania ya Viwanda: Watu, Sera na Utekelezaji” yaliyofanyika leo tarehe 26 Octoba, 2018 Jijini Dodoma

Washiriki Mbali mbali kutoka Asasi za kiraia wakiwa katika ufungaji wa maonyesho ya Asasi za Kiraia 2018 yenye kauli mbiu “Tanzania ya Viwanda: Watu, Sera na Utekelezaji” yaliyofanyika leo tarehe 26 Octoba, 2018 katika ukumbi wa African Dream Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS), Bw. Francis Kiwanga wakati alipowasili katika ufungaji wa maonyesho ya Asasi za Kiraia 2018 yenye kauli mbiu “Tanzania yaViwanda: Watu, Sera na Utekelezaji” yaliyofanyika leo tarehe 26 Octoba, 2018 katika ukumbi wa African Dream Jijini Dodoma.(PICHA NA OFISI YA BUNGE

DIRA YA KITAA NA MIKASA YA MUUZA MAJENEZA..

LUKUVI AAGIZA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA USHIRIKA KUTOONDOLEWA ENEO LA LAMBO ESTATE NA KUPATIWA EKARI MBILI KILA MMOJA

$
0
0

HAI, KILIMANJARO- 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekata mzizi wa fitna ambapo ameagiza waliokuwa wafanyakazi wa chama cha ushirika katika eneo la Lambo Estate Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro kutoondolewa katika eneo hilo na kila mmoja kupatiwa ekari mbili kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kimaisha. 

Uamuzi huo wa Lukuvi wa kutoa ekari mbili kwa wananchi 78 unafanya kutolewa kwa jumla ya ekari 156 kati ya ekari 1600 na unatokana na mgogoro wa muda mrefu baina ya waliokuwa wafanyakazi wa ushirika na uongozi .Mgogoro uliibuka baada ya wafanyakazi hao kutakiwa kuondoka katika makazi yaliyopo kwenye eneo la shamba kutokana na utumishi wao kukoma. 

Waziri Lukuvi alitoa maamuzi hayo katika wilaya Hai ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kutembelea wilaya za Hai, Moshi na Same kushughulikia migogoro ya ardhi katika wilaya hizo mkoa wa Kilimanjaro. Mhe Lukuvi ameshangazwa na ushirika wa watu wachache kutaifisha ardhi na kuamuru watu waliokuwepo muda mrefu katika eneo la lambo estate kuondoka na kusema kuwa safari hii serikali itawanyoosha wale wote wanaofanya ujanja wa kuwaonea wanyonge.

 *”Sijawahi kuona ushirika wa namna hii ambapo wenye rasilimali hawanufaiki na ardhi iliyopo katika kijiji chao halafu ardhi hiyo inakodishwa kwa wanachama wa ushirika wanaotoka vijiji vingine”* alisema Waziri Lukuvi. 

Huku akishangiliwa na wananchi wakati akitoa maamuzi hayo, Mhe. Lukuvi alisema amekwenda katika eneo hilo la Lambo Estate kushughulikia mgogoro wa ardhi. Suala la ushirika litashughulikiwa na waziri mwenye dhamana na vyama vya ushirika ambae ataamua iwapo ushirika huo unafaa. Waziri Lukuvi alisisitiza kuwa, serikali haiwezi kuwaondoa wazee walioishi kwa muda mrefu. 

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images