Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

TATIZO LA MAJI CHALINZE KUBAKI HISTORIA IFIKAPO 2019-SAMIA

$
0
0


NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE 

SERIKALI imewahakikishia wananchi wa jimbo la Chalinze ,mkoani Pwani kuwa wataondokana na tatizo la maji na kubaki historia ifikapo mwezi april mwakani. 

Tatizo la maji limekuwa likiwapa shida wananchi hao kwa miaka mingi hali iliyokuwa ikiondoa imani na serikali yao. Akizungumza na wakazi wa Chalinze, makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu alisema ,shida ya maji Chalinze imekuwa kubwa ambapo wamekuwa wakikosa huduma hiyo ya maji safi na salama ya uhakika. 

"Faraja inakuja, naimani ifikapo 2019 kero hii itakuwa historia, "alisisitiza. 
Pamoja na hayo, Samia amewataka akinamama wajawazito wakiwa tayari kujifungua wakimbilie hospital ama vituo vya afya badala ya kuendekeza masuala ya kishirikina suala linalosababisha vifo kwa mama na mtoto. 

Aliwaomba ,watumie vituo vya afya kunusuru vifo vya akinamama na watoto. Akizungumzia tatizo la mgogoro wa wakulima na wafugaji aliwaasa waheshimiane. Akitolea ufafanuzi juu ya kudhibiti tatizo hilo, naibu waziri wa mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega alisema, NARCO inaanzisha maeneo ya wafugaji na imetenga heka 100,010 ambapo ng'ombe watahamishia malisho ndani ya Narco.

"Miezi mitatu ng'ombe mmoja atalipiwa sh. 10,000 na ukiisha muda huo unaanza mkataba upya"alielezea.Ulega alifafanua, njia hiyo itapunguza ongezeko la mifugo hiyo.Mkurugenzi mkuu wa DAWASA Cyprian Luhemeja alieleza wanaendelea kufanyia kazi miradi mbalimbali na wanatarajia italeta jibu ndani ya jamii na kuondokana na kero hiyo. 

Awali mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete anasema ,uchelewaji wa hatua za kupata huduma ya maji inaleta sura ya kufanya siasa kwa wananchi ambao bado wanaiamini serikali yao. Ridhiwani aliiomba, serikali kuendelea kusukuma na kuusimamia mradi wa CHALIWASA ili uanze kazi haraka na kuondoa kero hiyo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiteta jambo na ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) na Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi Abdallah Ulega katika ziara ya kukagua shughuli za kimaendeleo Bagamoyo na Chalinze. (Mwamvua Mwinyi

WAZIRI WA MAJI ATEMBELEA HALMASHAURI YA MADABA

$
0
0
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na kukagua miradi ya maji ya Madaba, Lilondo na Maweso.

Miradi hiyo ambayo ujenzi wake unaendelea inalenga kuimarisha huduma ya upatikanaji wa maji kwa maeneo ya vijiji hivyo, mkoani Ruvuma.

Akizungumza na wananchi wa Lilondo, Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amepongeza juhudi za wakazi wa kijiji hicho wa kukabiliana na tatizo la maji kwa kujenga tenki la maji na kuahidi wizara yake itatoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa mabmba na kazi ya ulazaji wa mabomba hayo kwa ajili ya kusambaza maji kwa wananchi.

Amesema wananchi hao ni mfano wa kuigwa na kuwashukuru kwa nia yao njema ya kuinga Serikali mkono katika kuleta maendeleo ya Sekta ya Maji. Akitoa ahadi kwa viongozi wa Halmashauri hiyo kuwa atalipa fedha zilizobaki kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya Lilondo na Maweso ili waweze kumaliza kazi ya ujenzi.

Aidha, Profesa Mbarawa ameanzisha zoezi la upandaji miti katika chanzo cha maji Maweso na kuitaka Serikali ya Kijiji na wananchi wapande miti ya kutosha na zoezi hilo liwe endeevu kwa lengo la kuwa na chanzo cha uhakika cha maji kwa miaka mingi. Mradi wa maji wa mtiririko wa Lilondo umefikia asilimia 65 ya ujenzi, lengo la mradi likwa ni kutoa huduma kwa wakazi 5,919 ifikapo 2024 katika Kijiji cha Lilondo, utagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 1.048.

Huku mradi wa maji wa mtiririko wa Maweso ukiwa umefikia asilimia 65 ya ujenzi, lengo la mradi ni kutoa huduma ya maji kwa wakazi 2,876 ifikapo 2023 katika Kijiji cha Maweso, utagharimu zaidi ya Silingi Milioni 546. Profesa Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku 6 mkoani Ruvuma ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maji.

Mhandisi wa Wilaya ya Madaba, Jonas Maganga akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa kuhusu ujenzi wa chanzo cha Mradi wa Maji wa Maweso, mkoani Ruvuma. 
Afisa Maji wa Bonde la Ziwa Nyasa, Mhandisi Elise Englebert akitoa taarifa kwa Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa kuhusu ujenzi wa ofisi ndogo za Bonde la Ziwa Nyasa na Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini, Songea Mjini. 
Waziri wa Maji, Profesa Mbarawa (aliyevaa kofia) akiwa na viongozi wa Halmashauri ya Madaba akisikiliza taarifa kuhusu Mradi wa Maji wa Lilondo akiwa juu ya tenki la mradi huo uliopo wilayani Madaba, mkoani Ruvuma. 
Waziri wa Maji, Profesa Mbarawa akipita kukagua maendeleo ya ujenzi wa tenki la Mradi wa Maji wa Madaba, mkoani Ruvuma. 
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa tenki la Mradi wa Maji wa Madaba, mkoani Ruvuma. 

RC MAKONDA APATIA UFUMBUZI KERO SUGU ZA WANANCHI WA BUGURUNI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana amefanya ziara ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa Buguruni ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli.

RC Makonda amesema wananchi tunapaswa kuunga mkono juhudi za serikali za ujenzi wa Reli ya kisasa (standard gauge) ambayo inaenda kulifikisha taifa katika uchumi wa kati na kuitangaza Tanzania katika ramani ya Dunia hivyo amewasihi wananchi waliovunjiwa kuwa wavumilivu.

Aidha RC Makonda ameiomba kampuni hodhi ya rasilimali za reli RAHCO kuangalia uwezekano wa kuwapatia wananchi angalau njia za kupita ili kuwapunguzia mizunguko mirefu.Katika ziara hiyo RC Makonda amemuagia Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa kumuhamisha kituo kingine mkuu wa kituo cha Polisi Buguruni kwakuwa watu anaowaongoza hawamuamini.

Hata hivyo RC Makonda ametoa siku Saba kwa kigogo wa Bodi ya Mikopo kumkabidhi bajaji kijana alietambulika kwa jina la Jafari Raphael aliegongwa na gari na kigogo huyo na kupelekea ulemavu wa kukatwa mguu mmoja pasipo kulipwa fidia yoyote na kumfanya kijana huyo kugeuka kuwa mtu wa kuomba misaada huku kigogo huyo akiendelea kula maisha na familia yake.

Pamoja na hayo RC Makonda amepatia ufumbuzi kero ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili Umoja wa Madereva wa daladala buguruni Chama waliokuwa wamezuiwa kuegesha magari eneo la Buguruni station ambapo RC Makonda amewaagiza madereva hao kurudi katika eneo hilo.

Miongoni mwa kero zilizotolewa na wakazi wa buguruni ni pamoja na tozo kubwa ya uchafu, polisi jamii,ukamataji wa watu, watu kubambikiziwa kesi, migogoro ya mirathi na watu kudhulumiwa ambapo RC Makonda amezipatia majibu kero hizo papo kwa papo kwa kupigia simu kwa walengwa.
 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na Wakazi wa eneo la Buguruni jana,alipofanya ziara ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa eneo hilo ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akisikiliza moja ya swali kutoka kwa mkazi wa Buguruni jana,wakati Makonda alipofanya  ziara ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa Buguruni ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda  na ujumbe wake alipokuwa akiwasili maeneo ya Buguruni jana,katika ziara yake ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa Buguruni ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda  akizungumza na mmoja wakazi wa Buguruni ,katika ziara yake ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa Buguruni ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli. 

TANAPA NA WADAU WA UTALII WAFANYA KAMPENI YA KUTANGAZA VIVUTIO KATIKA JIJI LA MWANZA

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii. 
WADAU wa Utalii kwa kushirikiana na Vyuo Vikuu katika jiji la Mwanza leo wameanza kampeni ya siku tatu ijulikanayo kama “Discover the Treasures of Mwanza” itakayoshirikisha zaidi ya wanafunzi 800 waliojiunga na vyuo vikuu mwaka huu. 

Lengo la kampeni hii inayotarajia kufanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane linatajwa kuwa ni kutoa fursa kwa wanafunzi hao wa elimu ya juu kutambua umuhimu wa kutembelea rasilimali zilizopo nchini na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa utalii wa ndani. 
 Akizungumzia tukio hili mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya tukio hilo ambaye pia ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine(SAUT), Judith Wanda,anasema kampeni hiyo inatarajiwa kuanza leo oktoba 26 hadi 28 mwaka huu.
 
 Wanda amefafanua kuwa kupitia kampeni hiyo wanafunzi hao ambao ni wa mwaka wa kwanza watapata fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusu masuala ya uhifadhi na utalii wa ndani pamoja na namna bora ya kutangaza vivutio vilivyopo nchini. 

 "Vyuo vinaanza udahili hivyo tumelenga wanafunzi wapya wanaojiunga na elimu ya juu na tunatarajia kutumia fursa hiyo kuwafundisha wanafunzi kutembelea vivutio na rasilimali zilizopo nchini kama njia ya kujifunza na tunaamini hawa wataenda kuelimisha jamii umuhimu wa uhifadhi na utalii wa ndani.

 "Kampeni hii ya siku tatu imelenga kukutanisha wanafunzi 800 na kila mwanafunzi atajigharamia kiasi cha Sh 8,800 kwa ajili ya usafiri na shughuli nyingine hifadhini Saanane. Tulishawahi kufanya kampeni ya kwanza na tulikuwa tukihusisha wanafunzi wa maeneo ya Mwanza," 
Kundi la Waandishi wa Habari wakiwa katika boti maalumu kwa ajili ya safari ya kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane .
Eneo hili limo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane ambalo linajulikana kama jiwe la kuruka "Jump Stone" limekuwa ni kuvutio kwa wageni walitembelea hifadhi hiyo kwa ajili ya kuchukua Taswira wakati wakiruka.

Baadhi ya Watalii wa ndani wakiwa katika Lango la kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiw acha Saanane kwa ajili ya kujionea vivutio vya utalii vilivyopo katika Hifadhi hiyo.  




WALENGWA WA TASAF WAFURAHIA MAONESHO YA SIDO MKOANI SIMIYU.

$
0
0

Na Estom Sanga- Simiyu

Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF waliopata fursa ya kushiriki katika maonyesho yaliyoandaliwa na Shirika la Kuhudumia viwanda vidogo vidogo –SIDO yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu wamesema maonyesho hao yamekuwa ya manufaa makubwa kwao na kuishukuru serikali kupitia TASAF kwa kuwawezesha .

Maonyesho hayo yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassimu Majaliwa yanawashirikiwa Wajasiliamali wadogo na wakati ambao wamepata fursa ya kuonyesha bidhaa wanazozalisha na pia kujifunza teknolojia rahisi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa lengo la kutimiza azma ya serikali ya kukuza sekta ya viwanda nchini.

Bidhaa zilizoletwa na Walengwa wa TASAF kwenye maonyesho hayo hutengenezwa kwa njia ya vikundi baada ya kuwezeshwa na Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii kama njia mojawapo ya kuinua kipato cha Walengwa na kupunguza adha ya umaskini. Miongoni mwa bidhaa ambazo Walengwa hao wa TASAF wanaonyesha , ni pamoja na sabuni za vipande na maji, majani ya chai yaliyozalishwa kutokana na mmea wa mchaichai,vyungu,bidhaa za ususi ,nguo aina ya batiki,urembo na mafuta ya kupakaa.

Wakizungumza kwenye banda hilo la TASAF, Walengwa hao wamesema fursa waliyoipata imewawezesha siyo tu kuuza na kupata soko la bidhaa zao, bali pia wameweza kujifunza mbinu za kuendesha shughuli za uzalishaji mali wenye tija jambo ambalo wamesema litainua kipato chao. “tunashukuru sana TASAF kwa kutufungua macho tumeweza kujua namna bora ya kuendesha shughuli zetu za kuzalisha bidhaa na kupata soko “amesema mmoja wa Walengwa ambaye kikundi chake kinajishughulisha na uzalishaji wa mafuta ya kujipakaa na sabuni.

Wakizungumzia changamoto wanayokabiliana nayo katika utekelezaji wa shughuli za uzalishaji wa bidhaa zao, Walengwa hao wametaja tatizo la uduni wa vifungashio vya bidhaa ambayo wamesema ikipatiwa ufunguzi watakuwa wamepiga hatua kubwa kuelekea katika maendeleo ya uhakika. “tazama hivi sasa tunalazimika kuweka sabuni ya maji kwenye chupa za plastiki tunazookoteza baada ya kutumika na kutupwa na watumiaji wengine jambo hilo linapunguza sana ubora wa bidhaa zetu” amelalamika mlengwa huyo wa TASAF.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umekuwa na utaratibu wa kuwashirikisha baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko huo kwenye maonyesho mbalimbali ya Wajasiliamali ili kuwawezesha Walengwa hao kujifunza na kuonyesha bidhaa wanazozalisha kwa lengo la kupata pia soko la bidhaa zao.

Baadhi ya Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF waliopata fursa ya kushiriki katika maonyesho yaliyoandaliwa na Shirika la Kuhudumia viwanda vidogo vidogo –SIDO yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu wamesema maonesho hayo yamekuwa ya manufaa makubwa kwao na kuishukuru serikali kupitia TASAF kwa kuwawezesha .
 Baadhi ya Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF waliopata fursa ya kushiriki katika maonyesho yaliyoandaliwa na Shirika la Kuhudumia viwanda vidogo vidogo –SIDO yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu,wakiwa na baadhi ya bodhaa zao walizozitengeneza,aidha wamesema maonesho hayo yamekuwa ya manufaa makubwa kwao na kuishukuru serikali kupitia TASAF kwa kuwawezesha .

Dkt. Abbasi Kuhutubia Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Habari China

$
0
0


Na Beatrice Lyimo – CHINA.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi ataendelea na ziara yake nchini China ambapo leo Ijumaa mchana atatembelea Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Habari cha China na kutoa mhadhara.

Katika mkutano huo, moja ya masuala anayotarajia kuzungumza na wahadhiri na wanafunzi wa chuo hicho ni kuhusu  diplomasia ya Tanzania na China iliyopelekea kuwa na ushirikiano wa karibu mpaka sasa.

Aidha, Dkt. Abbasi pia atazungumzia wajibu wa wanahabari na namna wanavyotakiwa kuenenda ili kutekeleza wajibu wao katika sekta nzima ya habari na mawasiliano.Mbali na hayo, akiwa msimamizi wa sekta ya habari nchini Tanzania Dkt. Abbas katika mkutano huo  ataeleza  hali ya sekta ya habari Tanzania ilivyo sasa na ijayo kwa maendeleo ya nchi.

Dkt. Abbasi na ujumbe wake wa Maafisa Habari na Uhusiano Serikalini wapo mjini Beijing kwa ziara iliyolenga kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano.
 Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Ujumbe wake wakipewa  maelezo ya kiutendaji wa kazi za kila siku zinazofanywa na Shirika la Habari la CCTV na CGTN kutoka kwa mmoja wa viongozi wa juu wa Shirika hilo mapema Jana jijini Beijing, China.
IMG-20181026-WA0015 IMG-20181026-WA0014 IMG-20181026-WA0017
Picha mbalimbali za ziara ya Msemaji Mkuu wa Serikali  Dkt. Hassan Abbasi na Ujumbe wake alipotembelea vyombo vya habari vya CCTV na CGTN na China Redio Kimataifa Beijing China.

Ufungaji wa flow meters katika bandari zote nchini kukamilika hivi karibuni.

$
0
0
Na Zuena Msuya, Dodoma

Serikali imesema kuwa taratibu za ufungaji wa flow meter katika bandari zote nchini ziko katika hatua za mwisho baada ya taratibu zote kukamilika.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, jijini Dodoma wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini,iliyokuwa ikijadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari Kuu, Maghala ya kuhifadhi mafuta, pamoja na Flow Meters.

Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Danstan Kitandula, ambaye alihoji mambo kadhaa kubwa likiwa ni hatua gani zimefikiwa katika zoezi za ufungaji flow Meter katika bandari kuu nchini ili kudhibiti upotevu wa mafuta na kuongeza mapato ya serikali.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alieleza kuwa tayari hatua mbalimbali zimekwisha kuchukuliwa ili kukamilisha zoezi hilo, baada ya Mawaziri wa wizara tano, zinazoshirikiana katika sekta hiyo kukutana pamoja na kuweka ratatibu za kuimarisha na kudhibiti upotevu wa mafuta na mapato ya serikali.

Dkt. Kalemani alieleza wazi kuwa, kwa sasa Flow Meters zipo kwenye mchakato wa Manunuzi, ambapo zoezi hilo linakwenda haraka na muda si mrefu litakamika na kulitolea taarifa.“ Zoezi la kununua Flow Meter linaendelea vizuri na kwa kasi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, ndiyo ilipewa jukumu la kusimamia zoezi hilo, kwa kuwa sekta hii inahusisha Wizara tano, ikiwemo Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda na Wizara ya Nishati yenyewe:, ufungaji wa flow meter hizo utafanyika katika bandari zote nchini ikiwemo Dar es salaam, Tanga pamoja na Mtwara”, alisisitiza Dkt. Kalemani.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( aliyesimama) akifafanua jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, iliyokuwa ikijadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari Kuu, Maghala ya kuhifadhi mafuta, pamoja na Flow Meters. kilichofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya watendaji wa wizara na taasisi zilizochini yake wakiwa katika wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kilichofanyika jijini Dodoma na iliyokuwa ikijadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari Kuu, Maghala ya kuhifadhi mafuta, pamoja na Flow Meters.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali wa Uwagizaji Mafuta kwa Pamoja( PBPA), Mhandisi Erasto Simon (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari Kuu, Maghala ya kuhifadhi mafuta, pamoja na Flow Meters.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Danstan Kitandula,( katikati) akitoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara ya Nishati, wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini,iliyokuwa ikijadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari Kuu, Maghala ya kuhifadhi mafuta, pamoja na Flow Meters. 

BENKI YAJINASUA KWENYE HASARA,YATANGAZA KUPATA FAIDA

$
0
0
YAJIVUNIA FAIDA YA BIL 1.4/- ROBO YA TATU 2018

BENKI ya Biashara ya DCB imefanya juhudi za makusudi kuhakikisha inatoka kwenye hasara iliyopata mwaka 2017 ya Sh.bilioni 1.6 na kurudi kwenye faida na kwamba baadhi ya hatua zilizochukuliwa ni kuboresha mfumo wa endeshaji biashara ambapo gharama za uendeshaji zimeshuka na huduma mpya za kidigitali zimeanzishwa ambapo zimevutia wateja wengi zaidi kufungua account na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama zitokanazo na amana za wateja.

Hayo yameelezwa na Benki ya DCB jijini Dar es Salaam wakati ikitangaza kufanikiwa kupata faida ya Sh. bilioni 1.4 katika kipindi kinachoishia Septemba mwaka 2018 huku ikiipiku hasara ya Sh.bilioni 1.6 iliyopatikana kipindi kama hicho mwaka 2017 ambayo inawakilisha ongezeko la asilimia 187.Faida hiyo ni kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka 2018.

Taarifa ya DCB inaeleza kuwa moja ya huduma za kidigitali ambazo benki imezindua ni akaunti ya kidijiti (DCB Digital Account), DCB Kibubu Digital Account na DCB FDR Digital account.Hivyo akaunti hizo zinamuwezesha mteja wao kufungua akaunti na kufanya miamala yote ya kibenki, kutunza fedha na kuwekeza kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Kuhusu kukua kwa faida ,benki hiyo imesema kukua huko kwa faida umechagizwa na ukuaji wa mikopo ghafi ya wateja kutoka Sh. bilioni 89.3 Septemba mwaka 2017 kufikia Sh. bilioni 91.3 mwezi Septemba, 2018. Ukuaji huo umechagizwa na utoaji wa mikopo ambapo mikopo ya jumla ya Sh.bilioni 50 imetolewa hadi kufikia Septemba mwaka 2018.

"Idadi ya wateja imeongezeka kutoka 144,445 Desemba mwaka 2017, kufikia wateja 157,366 Septemba mwaka 2018. Mapato halisi ya benki yatokanayo na riba yameimarika katika robo ya tatu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita hali ambayo imechagizwa na mkazo wa benki katika kuongeza amana za gharama nafuu kupitia bidhaa za amana za kidijiti, usimamizi wa mizania wenye ufanisi na usimamizi wa gharama za uendeshaji wa benki. Uwiano wa mikopo ghafi na jumla ya amana za benki umeongezeka kwa asilimia 3.1 ikilinganishwa na robo ya pili ya mwaka huu.

BEI YA NYAMA KATIKA MACHINJIO YA VINGUNGUTI

$
0
0

 Wafanyabiashara nyama katika  Machinjio ya Vingunguti apima nyama  kabla ya kuuzwa kwa wafanya biashara mbalimbali waliofika katika ambapo kilomoja ya nyama ya Ng`ombe ni shilingi 4500,6000.
Wafanyabiashara nyama katika  Machinjio ya Vingunguti akiinda  nyama  kabla ya kuuzwa kwa wafanya biashara mbalimbali waliofika katika ambapo kilomoja ya nyama ya Ng`ombe ni shilingi 5000,7000.picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
afanyabiashara wa nyama katika machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam wakisubili wateja wanaotoka sehemu mbalimbali ambapo kilomoja ya maini ya ng`ombe ni shilingi 6000, 7000.
Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

WAJASIRIAMALI WAWEZESHWA KIUCHUMI

$
0
0
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa jimbo la Mkuranga abdallah Ulega ametoa  sh.milioni mbili m kwa vikundi vya ujasiriamali 11 vya kata ya Kimanzimchana wilayani Mkuranga mkoani Pwani ikiwa ni  lengo la kukuza mitaji yao na kuwainua kiuchumi wajasiriamali hao.

Akizungumza kwa niaba ya mbunge huyo, Katibu wa Mbunge wa jimbo la Mkuranga Kisatu Omary  amevitaja baadhi ya vikundi vilivyopewa fedha hizo kuwa ni Tupendane Group,Mshikmano pamoja na mazingira group.
Aidha  Kisatu amesema ulega ametoa fedha hizo kwa lengo la kuinua mitaji yao, na kuwaomba kuzitumia kwenye malengo yaliyokusudiwa.

"Serikali inawapenda wananchi wake na ipotayari kuwasaidia mkiwa kwenye vikundi hivyo kwahiyo dumisheni vikundi vyenu mpate kukopesheka.

"Serikali inatoa fedha kwa ajili ya wajisiriamali ambayo ni asilimia kumi kupitia  Halmashauri lakini ni lazima muwe kwenye vikundi tena vyenye sifa"amesema Kisatu.

Aidha Kisatu ameomba wajasiriamali hao kutumia hela hiyo kwa kukuza mitaji yao na sio kwenda kwa matumizi yao binafsi ili iweze kuleta tija na taifa kwa ujumla.
 Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkuranga, Mariam Ulega akinunu miti kwa wajasiriamali wa kata ya Kimanzi chana Wilaya Mkuranga mkoa wa Pwani, ambapo kila kikundi kilipokea  shilingi laki mbili kwajili ya kukuza mitaji yao.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
 Katibu wa Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Kisatu Omary akikabidhi zaidi ya sh.milioni mbili kwa vikudi vya wajasiriamali 11 vya kata ya Kimanzi chana Wilaya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Picha ya pamoja.

AFISA TARAFA ITISO ATANGAZA KIAMA KWA WAVAMIZI WA MAENEO YA MALISHO

$
0
0
AFISA Tarafa wa Itiso  Remidius Emmanuel ametangaza vita kwa watu wote waliovamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Malisho  katika Tarafa hiyo iliyopo wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma..

Remidius amesema hayo mapema wiki hii  katika mkutano maalumu wa kujibu kero mbalimbali katika  kijiji cha Gwandi na kuhusisha  Wafugaji kutoka kata ya Zajilwa. 

Akisoma taarifa mbele ya Afisa Tarafa, Katibu wa Chama Cha Wafugaji Wilaya ya Chamwino Bw. Reginaldo Lubeleje alitaja baadhi ya  Changamoto wanazokumbana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa  malisho,njia za mifugo, upungufu wa Majosho ya Mifugo, Mahusiano madogo kwa baadhi ya  Viongozi wachache wa  Serikali na Chama cha Wafugaji.

Imeelezwa kuwa baadhi ya maeneo katika Tarafa ya Itiso  yalitengwa kabisa kwa ajili ya Wafugaji lakini yamevamiwa na Wakulima wakubwa na baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na Mbuga ya Yobo, Uliuli,Dongo, Jelesa, Mazuguni na Haneti  hizi mbuga zilitengwa kwa ajili ya malisho ila maeneo hayo yamevamiwa na wakulima wakubwa.

Akieleza mafanikio yao katibu wa chama cha wafugaji Iti amesema kuwa;  chama hicho kimefanikiwa kuwaunganisha Wafugaji  wote bila kujali Ukabila, dini na Itikadi ya mtu, mbali na kuweza kutatua baadhi ya matatizo yao wenyewe  wamefanikiwa pia  kushiriki katika vikao mbalimbali vilivyo husisha Makundi ya Wafugaji aidha wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamoga kwa kuendelea kuwashirikisha katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya Wilaya ya Chamwino.

Akijibu kero hizo Afisa Tarafa Remidius Emmanuel amesema kuwa, uwezekano wa kuibuka  kwa migogoro ya Wakulima na Wafugaji  wakati mwingine hutokana na uzembe wa baadhi ya viongozi wanaoshindwa kutimiza wajibu wao.

Amesema kuwa; "Sasa unakuta kiongozi anafahamu kabisa kwamba haya maeneo yametengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo, alafu anaona yanavamiwa alafu yeye amenyamaza tuu, na ninazo taarifa kuna baadhi ya viongozi wa  Serikali za Vijiji ambao wameshiriki kuuza maeneo hayo, Wajiandae kuyarejesha kabisa na zoezi hili litafanyika Tarafa nzima.Kwa hiyo kama kuna watu wamejimilikisha maeneo hayo wambieni wayarejeshe  haraka.Watatueleza nani aliwauzia na ni kwa utaratibu upi? na katika hili sitorudi nyuma, ni jukumu letu viongozi kutatua migogoro na sio kuwa sehemu ya Migogoro" Amesem Remidius.

Hata hivyo amewaeleza kuwa licha ya juhudi za Serikali katika kutatua kero ya  Majosho ya mifugo lakini amewataka Wafugaji kupokea ushauri kutoka kwa  wataalamu wa Mifugo  ili kuepuka Magonjwa mbalimbali yanayoweza kuipata mifugo yao.

Aidha amesema kuwa, "Ni kweli ipo Changamoto ya Majosho kwa ajili ya Mifugo yetu, lakini baadhi ya  Serikali za Vijiji na Kata  wamefanikiwa kutatua kero hii kwa kuwatumia Mawakala na Makundi ya wafugaji  lakini nasisitiza ili kufanikisha taratibu hizo nimewaelekeza kushirikisha Wataalamu wetu wa Halmashauri, lakini ninazo taarifa pia baadhi yetu  sisi Wafugaji bado hatuna muamko wa kupeleka Mifugo yetu katika Majosho yaliyopo, niombe uongozi wa Chama cha Wafugaji kuhimiza umuhimu wa kutekeleza ushauri wa Kitaalamu ili Mifugo yetu isishambuliwe na magonjwa" Amesema Remidius.
 Afisa Tarafa wa Itiso Remidius Emmanuel akizungumza na Wafugaji katika mkutano maalumu wa kujibu kero mbalimbali kijiji cha Gwandi na kuhusisha Wafugaji kutoka kata ya Zajilwa.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji kanda ya kati, Neema Ally akizungumza na wafugaji  wakati wa mkutano huo uliofanuka katika kijiji cha Gwandi kata ya Zajilwa.
Baadhi ya wafugaji wakiwasilisha kero zao mbele ya Afisa Tarafa

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

INTRODUCING "CHAMPION" BY Shilole Ft Chid Beenz

Dkt. Abbasi Kuhutubia Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Habari China

$
0
0
Na Beatrice Lyimo - CHINA
MKURUGENZI wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi ataendelea na ziara yake nchini China ambapo leo Ijumaa mchana atatembelea Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Habari cha China na kutoa mhadhara.

Katika mkutano huo, moja ya masuala anayotarajia kuzungumza na wahadhiri na wanafunzi wa chuo hicho ni kuhusu  diplomasia ya Tanzania na China iliyopelekea kuwa na ushirikiano wa karibu mpaka sasa.

Aidha, Dkt. Abbasi pia atazungumzia wajibu wa wanahabari na namna wanavyotakiwa kuenenda ili kutekeleza wajibu wao katika sekta nzima ya habari na mawasiliano.

Mbali na hayo, akiwa msimamizi wa sekta ya habari nchini Tanzania Dkt. Abbas katika mkutano huo  ataeleza  hali ya sekta ya habari Tanzania ilivyo sasa na ijayo kwa maendeleo ya nchi.

Dkt. Abbasi na ujumbe wake wa Maafisa Habari na Uhusiano Serikalini wapo mjini Beijing kwa ziara iliyolenga kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano.
 Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Ujumbe wake wakipewa  maelezo ya kiutendaji wa kazi za kila siku zinazofanywa na Shirika la Habari la CCTV na CGTN kutoka kwa mmoja wa viongozi wa juu wa Shirika hilo mapema Jana jijini Beijing, China.


Picha mbalimbali za ziara ya Msemaji Mkuu wa Serikali  Dkt. Hassan Abbasi na Ujumbe wake alipotembelea vyombo vya habari vya CCTV na CGTN na China Redio Kimataifa Beijing China.

Makamu wa Rais afanya ziara Chalinze

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema atamuagiza Waziri wa Kazi kufanya ziara kwenye Viwanda mkoani Pwani kusikiliza kero za wafanyakazi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akihutubia wakazi wa Chalinze kwenye uwanja wa Chalinze Polisi ikiwa siku ya pili ya ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.

“Nimesikia nong’ono kuna tatizo la maslahi ya wafanyakazi wanaofanya kazi viwandani sasa hivi lakini nataka niwaahidi kwamba hili nitakwenda zungumza na Waziri wa Kazi afanye ziara ya kupita viwandani ili asikie malalamiko ya wafanyakazi katika viwanda vile” alisema Makamu wa Rais.

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais alisisitiza ahadi ya kuondoa tatizo la maji kwa wananchi wa Chalinze ipo pale pale kwani Serikali ya awamu ya tano imeweka jitihada kubwa kuhakikisha inaondoa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi, pia alitoa rai kwa vijana kujifunza ufundi na kuongeza elimu ili wawe na sifa za kuajirika, pia alihimiza wananchi wa Chalinze kujiandikisha kwenye mfuko wa Bima ya Afya.

Aidha, Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete alimueleza Makamu wa Rais kuwa Halmashauri ya Chalinze inafanya kwa vitendo kutafsiri ahadi ya Mheshimiwa Rais pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 ambapo amesema Chalinze imefungua milango kwa wawekezaji wa aina zote.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili Lugoba ambapo Makamu wa Rais alikagua ujenzi wa kituo cha Afya Lugoba ikiwa siku ya pili ya ziara yake ya siku zita mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara ambao Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi kwenye uwanja wa Polisi Chalinze. 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akihutubia wakati wa mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Polisi Chalinze ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa Mgeni Rasmi, katika mkutano huo Naibu Waziri aliwahakikishia wananchi hao kuwa Wizara yake imekuja na mpango kabambe ambao utasaidia kuondoa migogoro kati ya wafugaji na wakulima.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Chalinze waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Polisi Chalinze ikiwa sehemu ya ziara yake ya kugagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Pwani. 

TATIZO LA MAJI CHALINZE KUBAKI HISTORIA IFIKAPO 2019-SAMIA

$
0
0
NA Mwamvua Mwinyi, Chalinze
SERIKALI imewahakikishia wananchi wa jimbo la Chalinze ,mkoani Pwani kuwa wataondokana na tatizo la maji na kubaki historia ifikapo mwezi april mwakani. 

Tatizo la maji limekuwa likiwapa shida wananchi hao kwa miaka mingi hali iliyokuwa ikiondoa imani na serikali yao. 

Akizungumza na wakazi wa Chalinze, makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu alisema ,shida ya maji Chalinze imekuwa kubwa ambapo wamekuwa wakikosa huduma hiyo ya maji safi na salama ya uhakika. 

"Faraja inakuja, naimani ifikapo 2019 kero hii itakuwa historia, "alisisitiza. 

Pamoja na hayo, Samia amewataka akinamama wajawazito wakiwa tayari kujifungua wakimbilie hospital ama vituo vya afya badala ya kuendekeza masuala ya kishirikina suala linalosababisha vifo kwa mama na mtoto. 

Aliwaomba ,watumie vituo vya afya kunusuru vifo vya akinamama na watoto. 

Akizungumzia tatizo la mgogoro wa wakulima na wafugaji aliwaasa waheshimiane. 

Akitolea ufafanuzi juu ya kudhibiti tatizo hilo, naibu waziri wa mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega alisema, NARCO inaanzisha maeneo ya wafugaji na imetenga heka 100,010 ambapo ng'ombe watahamishia malisho ndani ya Narco.

"Miezi mitatu ng'ombe mmoja atalipiwa sh. 10,000 na ukiisha muda huo unaanza mkataba upya"alielezea.

Ulega alifafanua, njia hiyo itapunguza ongezeko la mifugo hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa DAWASA Cyprian Luhemeja alieleza wanaendelea kufanyia kazi miradi mbalimbali na wanatarajia italeta jibu ndani ya jamii na kuondokana na kero hiyo. 

Awali mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete anasema ,uchelewaji wa hatua za kupata huduma ya maji inaleta sura ya kufanya siasa kwa wananchi ambao bado wanaiamini serikali yao. 

Ridhiwani aliiomba, serikali kuendelea kusukuma na kuusimamia mradi wa CHALIWASA ili uanze kazi haraka na kuondoa kero hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiteta jambo na ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) na Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi Abdallah Ulega katika ziara ya kukagua shughuli za kimaendeleo Bagamoyo na Chalinze. 

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUSHTAKIWA WATUMISHIWA MAKAMPUNI YA MIGODI YA DHAHABU NA KAMPUNI ZAO NCHINI

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA WAKUU WA MIKOA YA LINDI, MTWARA, PWANI NA RUVUMA NA VIONGOZI WA BODI YA KORSHO KUJADILI BEI YA KOROSHO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakuu wa Mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Ruvuma ambao mikoa yao imeanza kuuza korosho, Wenyeviti wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Watendaji Wakuu wa Bodi ya Korosho kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Oktoba 26, 2018. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba.
Washirki wa Mkutano ulioitishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa uliowajumuisha Wakuu wa Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani ambao mikoa yao imeanza kuuza korosho, Wenyeviti wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Watendaji Wakuu wa Bodi ya Korosho wakimsikiliza Waziri Mkuu wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Oktoba 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BODI YA FILAMU YAMFUNGIA WEMA SEPETU KUTOJIHUSISHA NA FILAMU KWA MUDA USIOJULIKANA

$
0
0
*Wema amefungiwa kufuatia kuachia video chafu zinazosambaa mitandaoni kwa sasa

Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
Bodi ya filamu ya nchini imemfungia muiguzaji wa kike Wema Abraham Sepetu anaejulikana kama Tzsweetheart kutokana na kusambaa kwa video pamoja na picha chafu Kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fisso ameeleza kuwa wasanii ni kioo cha jamii ambao wapo kwa ajili ya kuihabarisha ,kuiasa,kuionya jamii yale yanaoendelea katika jamii.

Fisso amesema kutokana na msanii huyo Wema Sepetu kutumia Sanaa yake kukiuka maadili ,desturi na tamaduni za  kitanzania  imeamuru kumsimamisha kutojihusisha na Sanaa yoyote Ile kwa muda usiojulikana kutokana na video pamoja na picha chafu zilizosambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha Wema Sepetu amepewa adhabu hiyo kutokana na kupotosha jamii kwa ujumla na bodi umejidhihirisha kumfungia na itaendelea kumfatilia mienendo yake kwa sasa mpaka atakapojirekebisha.

Mtendaji huyo amefafanua kuwa kama bodi wamepokea msamaha ambao aliomba kwa wadau, mashabiki na tasnia nzima ya filamu ikijumuisha na bodi ya filamu kupitia waandishi na kuita baadhi ya vyombo vya habari na kukiri kosa lake inaonyesha ni wazi atajirekebisha na makosa yake kutokana na kulidhalilisha taifa kwa ujumla.

Tusiime yazidi kung’ara kitaifa darasa la saba

$
0
0
SHULE ya Msingi Tusiime imeendelea kufanya vizuri kitaaluma baada ya kufanikiwa kuwa ya 13 kitaifa kati ya shule 10,090 na kuwa ya pili kwa Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa na wanafunzi wengi kuliko shule zote.

Shule hiyo pia imefanikiwa kuwa ya kwanza kwa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kati ya shule 90 na kutoa wanafunzi bora wawili kati ya wasichana 10 bora kitaifa na mvulana mmoja kwenye 10 bora kitaifa wavulana.

Wasichana wawili wa shule hiyo waliongia 10 bora ni Hamisa Kasele aliyeshika nafasi ya nne na Kareen Gabriel  aliyeshika nafasi ya tano kitaifa.
Shule hiyo imekuwa ya 13 kitaifa ikiwa na jumla ya wanafunzi 243 ambapo 239 wamepata wastani wa alama A.Shule nyingi zilizoingia 10 bora zilikuwa na wastani wa wanafunzi 70,60, 65 kwa mujibu wa matokeo hayo yaliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani NECTA hivyo Tusiime kuwa shule yenye wanafunzi wengi zaidi.

Baadhi ya wazazi waliozungumza na gazeti hili kuhusu matokeo hayo ya Tusiime walisema wamefurahishwa na matokeo ya shule hiyo ya darasa la saba mwaka huu hasa kwa wanafunzi wote 239 kupata wastani wa alama A.
Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Msingi Tusiime, Maxon Binomtonzi akiwapa matokeo ya darasa la saba wanafunzi wa shule hiyo ambayo  ilikuwa na watahiniwa 243 imefanikiwa kuwa ya 13 kitaifa kati ya shule 10,090 nchini na kuwa ya pili Mkoa wa Dar es Salaam na ya kwanza Wilaya ya Ilala.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

WADAU WANAUNGA MKONO SERIKALI KATIKA KUONGEZA UELEWA WA UWEKEZAJI KUPITIA MASOKO YA MITAJI-DKT MPANGO

$
0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango amesema wadau wamekuwa na mwamko katika sekta ya fedha ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kutekeleza mikakati mbalimbali ya kisera kwa lengo la kuongeza uwelewa na kukuza uwekezaji kupitia masoko ya mitaji. 

Mpango ameyasema hayo wakati wa kutoa zawadi kwa washindi wa shindano kuhusu Masoko na Mitaji kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu pamoja na kutunuku vyeti kwa wahitimu wa kozi ya watendaji katika masoko ya Mitaji wanaokidhi viwango vya kimataifa iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

Amesema kuwa masoko na mitaji kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha hususani masoko ya mitaji na uchumi kwa ujumla hapa nchini. 

Dkt. Mpango ameiagiza Mamlaka yay a Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kuendelea kuandaa shindano hilo katika kuwajengea vijana wa kitanzania kujiamini na kuweza kuwa wabobezi katika eneo hilo. 

Amesema shindano hilo kushirikisha wanafunzi zaidi ya 15000 sio kazi ndogo lakini ina manufaa kwa vijana wa kitanzania. 

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Masoko na Dhamana Nicodemus Mkama amesema kuwa washindi 12 kwa uwiano wa wasichana sita na wavulana sita waliopata alama za juu wamepata fedha sh.milioni 1.8 kwa kila mmoja na kupata safari mafunzo nchini Mauritius kujifunza mamlaka ya usimamizi wa Masoko ya Motaji ya nchi hiyo, Soko la Hisa Mauritius na kampuni tano kubwa za utoaji wa huduma katika masoko ya mitaji. 

Mkama amesema CMSA inaendelea kufanya jitihada za kuongeza idadi wataalam wa masoko na mitaji yenye lengo la kuanzisha na kuendeleza masoko ya mitaji , yenye ufanisi , uwazi na yenye kutoa haki sawa kwa washiriki wote.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango akitoa zawadi kwa washindi wa shindano. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Masoko na Dhamana Nicodemus Mkama akitoa maelezo ya shindano hilo lililoratibiwa na Mamlaka hiyo kwa ajili ya kuwapata vijana mahiri wa masoko ya mitaji katika hafla ya utoaji zawadi uliofanyika jijini Dar es es Salaam. 
 Sehemu ya washiriki wa wanafunzi katika shiondano.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images