Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109611 articles
Browse latest View live

KAIMU SHEIKHE WA MKOA MWANZA AELEZA MIKAKATI YA KUBORESHA UCHUMI WA VIONGOZI, WALIMU NA MASHEIKHE

0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

KAIMU Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza Hassan Musa Kabeke amesema moja ya vipaumbele vyake ni kuimarisha uchumi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na elimu ya dini.

Sheikhe Kabeke alitoa kauli hiyo jana kwenye ukumbi wa ofisi za BAKWATA zilizopo Mbugani katika Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri ya mkoa, masheikh wa wilaya na kata mkoani humu.

Alisema miongoni mwa mambo yanayomkera ni hali duni ya maisha na udhalili (unyonge) hivyo ameweka mikakati na mipango ya kuimarisha uchumi wa BAKWATA ili kubadilisha maisha ya walimu wa madrasa, masheikhe na maimamu wa misikiti ambao ni zao la uislamu (kiwanda) na misingi ya dini hiyo ya Kiislamu.

Kaimu Sheikhe huyo wa mkoa alisema madrasa na msikiti ndio eneo dhaifu kutokana na walimu na masheikhe kushindwa kufundisha elimu ya dini na hata ujira wao ni mdogo wanazidiwa na watumishi wa ndani jambo ambalo linamkera na hivyo ameamua kulitafutia tiba.

Sheikhe Kabeke alieleza kuwa ili kuboresha hali za walimu wa madrasa,masheikhe na maimu na waumini wa kiislamu lazima kuwe na vyanzo vya mapato yatakayosaidia Waislamu na haiwezekani kuendelea kuwa na BAKWATA ombaomba.


Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Musa Kabeke akizungumza na wajumbe wa halmashauri ya BAKWATA mkoani Mwanza, masheikhe wa wilaya, Kata na Misikiti ya wilaya zote za Mwanza jana, kwenye ukumbi wa mikutano wa baraza hilo Mbugani katika Wilaya ya Nyamagana jana. Picha na Baltazar Mashaka


Kaimu Katibu Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza, sina Mwagalazi akizungumza na wajumbe wa Halmashauri kuu ya baraza hilo, masheikhe wa wilaya na kata wa wilaya za mkoani humu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya BAKWATA Mkoa wa Mwanza Amran Batenga akizungumza na wajumbe wa halmashauri hiyo, masheikhe wa wilaya na kata za mkoani humu jana kwenye ukumbi wa baraza hilo Mbugani katika Wilaya ya Nyamagana. 


USAILI BONGO STAR SEARCH KUFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO

0
0
BAADA  ya kukamilika kwa Usaili wa Shindano la Bongo Star Search katika mikoa minne ya Tanzania bara ikijumuisha Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam sasa usaili huo utaendelea kupitia mitandao ya kijamii hasa Instagram na Facebook.

Usaili huo wa mtandaoni unatarajiwa kudumu kwa muda wa wiki tatu kuanzia leo Oktoba 25 ambapo mshindi ataingia kambini  kwa mafunzo kutoka kwa walimu na hatua ya mchujo itafuata.

Akizungumza na vyombo vya habari jaji mkuu wa mashindano hayo na Mkurugenzi Mkuu wa Benchmark Rita Poulsen amesema kuwa; “Ni nafasi ya kipekee kabisa kwa watanzania kushiriki na kupata nafasi ya kujiunga na BSS msimu wa 9, kwa sababu kama mlivyoona kwa mwaka huu tumeenda mikoa michache zaidi ni kutokana na sababu ambazo zimekuwa nje ya uwezo wetu, ila kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya BSS tunatoa nafasi ya ushiriki kupitia Mitandao ya kijamii” amesema MadamRita.

Aidha amesema kuwa “Kushiriki ni rahisi sana unachotakiwa kufanya ni kurekodi video ukiwa unaimba, video isiyozidi dakika moja ama sekunde sitini kisha post katika mtandao wa Instagram au facebook kwenye akaunti yako tag akaunti za @startimestz na @bongostarsearch na uambatanishe na hashtag #BSSOnlineAudition ili video yako iweze kutufikia na kufanyiwa usaili na majaji”. Aliongezea Madam Rita.

Hatua ya mchujo inatarajiwa kuanza katikati ya mwezi wa kumi na moja baada ya usaili wa mtandaoni kukamilika. Shindano la BSS msimu wa tisa linaendelea kurushwa na kituo cha StarTimes Swahili katika king’amuzi cha StarTimes kila siku saa tatu Usiku. Chaneli inayorusha mashindano hayo   ipo katika kifurushi nafuu kabisa cha Nyota ambacho kinagharimu Tsh 8000 tu kwa watumiaji wa dikoda za Antenna na Tsh 11,000 kwa watumiaji wa dikoda za Dishi kote nchini.

Pia imeelezwa kuwa mshindi wa Usaili wa mtandaoni anatarajiwa kutangazwa tarehe 18 Novemba mwaka huu na atasafirishwa kutoka popote pale nchini hadi Dar es Salaam kujiunga kambini na washiriki wengine 16 ambao tayari wameshapatikana katika Usaili wa mikoa 4 ya Tanzania bara.

Dkt. Ndumbaro akutana kwa mazungumzo na Balozi wa China

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya watu wa China Mhe. Wang Ke, katika mazungumzo hayo yaliyojikita katika kuimarisha mahusiano kwenye sekta mbalimbali zikiwemo Elimu, biashara, kilimo na teknolojia. Pamoja na mambo mengine Dkt. Ndumbaro amemshukuru Mhe. Wang Ke, kwa kuendelea kuliwakilisha Taifa lake vyema hapa nchini. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje jijini Dar es Salaam Tarehe 25 Octoba, 2018 
Maafisa Mambo ya Nje wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Dkt. Ndumbaro na Mhe. Wang Ke 
Sehemu ya maafisa wa Ubalozi wa China wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Dkt. Ndumbaro na Mhe. Wang Ke. 
Balozi Wang Ke akimwelezea Dkt. Ndumbaro zawadi ya sahani yenye mchoro wa maua 
Dkt. Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Wang Ke (wa tatu kutoka kushoto), kulia ni maafisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kushoto ni Maafisa Ubalozi wa China. 

AWAMU YA TANO YA MAZUNGUMZO YA KUSAKA AMANI YA BURUNDI YAANZA LEO

0
0

 Na Ahmed Mahmoud Arusha

Serikali yashindwa kushiriki licha ya juhudi za msulushi, kundi kubwa la viongozi washiriki wakiwemo marais wastaafu, majadala wa mapitio ya kayanza na enteber kutoka na azimio moja

Mchakato wa mazungumzo ya kusaka amani nchini burundi yameanza rasmi leo ambapo Makubaliano ya Kayanza 1 ,2 na ,makubaliano ya Enteber yanaendelea kujadiliwa ili kuweza kupata taarifa moja ambayo msuluhishi ataipeleka kwenye kikao cha wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika mashariki.

Pamoja na jitihada za Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa ambaye ni msimamizi wa msuluhishi wa amani ya Burundi za kuitaka serikali ya nchi hiyo kuja katika meza ya maungumzo hadi sasa hawajtoa majibu yeyote kama waja au la Juhudi hizo zimepelekea wadau wengine katika mazungumzo ya amani kuendelea na mazungumzo hayo ikiwemo kujadiliana kuhusiana na baada ya serikali kutotuma mwakilishi hadi sasa huku wakiwa hawajatoa majibu kama wanakuja au la.

Akifungua mazungumzo hayo mh.Mkapa akiwa anamaanisha kile alichosema kuwa hadi sasa hakupata maelezo sahihi kutoka kwenye serikali ya Burundi kwani hadi muda huu hawajatoa maelekezo yoyote kama watakuja au hawaji katika mazungumzo hayo. Amesema serikali hiyo imekuwa ikitoa maagizo ya kutaka kusijadiliwe baadhi ya vipengele ikiwemo suala la uchaguzi

Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin mkapa akifungua majada wa mazungumzo ya kusaka amani ya nchi ya Burundi kwenye ukumbi wa mikutano wa Ngurdoto Mountain Lodge leo wilayani Arusha 

JAJI MRUMA AKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA MWANZO MAGOMA-KOROGWE

0
0

Na Amina Ahmad, Mahakama Kuu, Tanga

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mhe. Amir Mruma amemuhimiza Mkandarasi SUMA JKT kuharakisha ukamilishaji wa ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Magoma iliyopo Wilayani Korogwe ili ianze kutumika mara moja.

Akiwa katika ziara ya kikazi Wilayani Korogwe; Mhe. Jaji Mruma alipata fursa ya kutembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Mahakama hiyo Oktoba 23 ambapo hata hivyo aliridhishwa na hatua iliyofikiwa.

Katika ziara yake Wilayani humo, Mhe. Jaji Mfawidhi alifanikiwa pia kukutana na Kamati za Maendeleo za Kata ya Magoma na Mashewa na kutoa elimu juu ya haki na wajibu wa wananchi katika migogoro ya ardhi, kesi za ubakaji, mimba za utotoni na usimamizi wa Mirathi.

Kwa upande wao; Wajumbe wa Kamati za Maendeleo (WDC) walitoa shukrani zao za dhati kwa Jaji Mfawidhi kwani ilikuwa ni mara yao ya kwanza kukutana na Jaji na kupewa elimu ya kisheria, hali iliyowapelekea kumuomba Jaji Mfawidhi aendelee na utarabu wa kukutana nao mara kwa mara kuwajengea wigo na uelewa mpana wa masuala ya kisheria ili kufanikisha majukumu yao.

Muonekano wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Magoma lililopo katika hatua za mwisho za ujenzi. 
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mhe. Amiri Rajabu Mruma (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Fundi wa Kampuni ya SUMA JKT alipokuwa akikagua ujenzi wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Magoma Wilayani Korogwe. 
Mhe. Jaji Mruma akiendelea na ukaguzi. 
Jaji Mruma akitoa elimu kwa Wajumbe wa Kamati ya maendeleo ya Kata ya Hale Wilayani Korogwe. 


JAMII YA WABARBAIGI WAPATA HATI MILIKI ZA KIMILA ZINAZOWASAIDIA KUPATA MAKAZI YA KUDUMU.

0
0
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

JAMII ya Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wameanza kuondokana na mfumo dume baada ya kukubali wanawake kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future unaotekelezwa katika wilaya za mkoa wa Iringa na Mbeya.

Wakizungumza wakati wa kukabidhiwa hati za kimira wanawake wa kibarbaigi walisema kuwa awali walikuwa hawaruhusiwi kumiliki mali yoyote ile bali mali zote zilikuwa zinamilikiwa na wanaume.

“Kwenye kabila letu mila zinawapa sana nafasi wanaume kumiliki mali na vitu vingine na kumfanya wanamke kuwa tegemezi jambo ambalo miaka ya nyuma limerudisha maendeleo nyuma ya wanawake” walisema wanawake hao wa Kibarbaigi

Wanawake hao walisema kuwa baada ya kupata elimu ya upimaji wa ardhi na kuifanya ardhi kuwa na hati miliki imesaidia wanaume wa kabila hilo kuanza kuitambua nafasi ya mwanamke na kumuwezesha mwanamke naye kumiliki mali sawa na wanaume wa kabila la wabarbaigi.

Tunaishukuru serikali na mradi wa LTA kwa elimu waliyoitoa kwa wanaume wa kabila la Barbaigi kwa kukubali wanawake wamiliki ardhi kwa kupewa hati miliki za kimira bila elimu hiyo wanawake sisi tungeendelea kuwa wakina mama wa nyumbani tu.

Naye mwenyekiti wa kabila hilo la wafugaji Shabani Ntasham alisema kuwa kupatikana kwa hati miliki za kimira kumekomesha hamahama ya jamii hiyo pamoja na kumuwezesha mwanamke wa jamii hiyo kumiliki ardhi.
Diwani wa kata ya Idodi Onesmo Mtatifikolo ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa utoaji wa hati hizo katika kijiji cha Kitisi ambapo jamii ya wabarbaigi wanaishi maeneo hayo nao walipewa hati miliki za kimira na kuanza kukomesha hama hama ya kabili hilo la wafugaji
Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wameanza kuondokana na mfumo dume baada ya kukubali wanawake kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future
JAMII ya Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wakiwa kwenye picha na viongozi mara baada ya kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future.





WATENDAJI WAKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI WAENDELEA NA KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU JIJINI DODOMA

0
0


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (katikati), akimfafanulia jambo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold Kihaule, wakati walipokua wanatoka katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold Kihaule, wakati walipokua wanatoka katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba (kulia) wakifurahia jambo na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Wanja Mtawazo, wakati walipokua wanatoka katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

ASHIRIKA YENYE SIFA KAMA ZA NGOs YATAKIWA KUWA NA CHETI CHA UKUBALIFU

0
0


Serikali imesema Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005 imeweka masharti kwa mashirika yaliyokuwa yamesajiliwa katika Sheria nyingine na yanasifa za kusajiliwa kama Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kuomba Cheti cha Ukubalifu chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Hayo yamesema mapema leo mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha taarifa ya usimamizi wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii.

Waziri Ummy Mwalimu amesema kimsingi Cheti cha Ukubalifu kinatolewa ili kuyaweka Mashirika yote Yasiyo ya Kiserikali chini ya usimamizi mmoja ili kuondokana na changamoto za awali ambapo mashirika hayo yalikuwa yakiratibiwa chini ya Sheria na Mamlaka zaidi ya moja.

Waziri Ummy aliwaambia wajumbe wa Kamati hiyo kuwa kutokana na kutungwa kwa Sera na Sheria hii kwa mara ya kwanza Tafsiri ya “Shirika Lisilo la Kiserikali” ilipatikana rasmi akiongeza kuwa Tafsiri hii inayotofautisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Asasi nyingine za kiraia kama vile Jumuia za kijamii zinazosajili Wizara ya Mambo ya Ndani, Makampuni yanayosajiliwa BRELA na Bodi za wadhamini zinazosajiliwa na RITA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akitoa taarifa kuhusu usimamizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma kushoto ni Niabu wake Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akitoa maelezo kuhusu usimamizi wa uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kusaidia makundi maalum nchini wakati Wizara ilipokuwa ikiwasilisha taarifa kuhusu usimamizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo jijini Dodoma kushoto ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba akitoa maoni yake kwa Viongozi na Watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto walipowasilisha taarifa ya usimamizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mbele ya Kamati yake jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo jijini Dodoma kuhusu Marekebisho ya Kanuni za Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na itakavyosaidia kuweka uwazi na uwajibikaji kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile. 


LADY JAYDEE AFUNGUKA HAYA NA MICHUZI TV KUHUSU USIKU WA VOCAL

Shirika la Reli Lawapa Nafasi Wasanii Kushoot Video zao Bure kwenye Treni ili kutangaza Maendeleo

Habari za UN KUTOKA NEW YORK, MAREKANI, OKTOBA 25, 2018

ZOEZI LA KUWARUDISHA WAKIMBIZI NCHINI KWAO NI LA HIARI-WAZIRI MKUU

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 25.10.2018

Wabunge nchini Ethiopia wamchagua Sahle-Work Zewde kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini humo

0
0
Bi Sahle-Work ni mwanadiplomasia mwenye uzoefu ambaye sasa amekuwa kiongozi wa kipekee mkuu mwanamke barani Afrika. 
 Kuchaguliwa kwake katika wadhifa huo kunajiri wiki moja baada waziri mkuu Abiy Ahmed kuliteua baraza la mawaziri ambapo nyadhifa nusu katika baraza hilo zimewaangukia wanawake. 
Katika hotuba yake ya kukubali wadhifa huo, rais Sahle-Work amezungumza kuhusu umuhimu wa kudumisha amani, vyombo vya habari nchini humo vinaeleza. 
 Amechaguliwa baada ya kujiuzulu ghafla kwa kiongozi aliyekuwepo Mulatu Teshome.Mkuu wa wafanyakazi katika ofisi ya waziri mkuu, Fitsum Arega, alituma ujumbe katika mtandao wa twitter kwamba uteuzi huo wa "kiongozi mkuu mwanamke haidhihirishi viwango vya miaka ijayo, lakini pia inafanya kuwa jambo la kawaida kwa wanawake kuwa waamuzi wakuu katika maisha ya umma". Chanzo BBC

BEI YA NYAMA KATIKA MACHINJIO YA VINGUNGUTI

0
0
Wafanyabiashara wa nyama katika  Machinjio ya Vingunguti wakianda  nyama  kabla ya kuuzwa kwa wafanyabiashara mbalimbali waliofika machinyioni hapo, ambapo kilomoja ya nyama ya Ng`ombe huuzwa kati ya shilingi 5,000 mpaka 7,000.picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
wafanyabiashara wa nyama katika machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam wakisubili wateja wanaotoka sehemu mbalimbali.


MKULIMA AJISHINDIA KITITA CHA MIL. 10 KUTOKA CRDB SIM ACCOUNT

0
0
Meneja Uendeshaji wa CRDB Microfinance, Raymond Urassa (kulia) akizungumsa na waandhi wa habari wakati wa kuendesha droo kubwa ya mwezi katika kampeni ya Shinda na SimAccount iliyofanyika Oktoba 25, 2018 Mikocheni jijini Dar es salaam. Jumla ya wateja 924 wameweza kujishindia viwango mbalimbali vya fedha, wakiongizwa na Stanford Mdolo kutoka Isaka Mkoani Shinyanga aliyejishindia kitita cha Milioni 10 katika droo hiyo, Wengine ni Godfrey Nzoha kutoka Nzovwe, Mbeya (Milioni 5) pamoja na Jacob Lucas kutoka Mkuranga, Pwani (Milioni 1) . ambapo asilimia kubwa ya washindi hao ni wakulima. Kushoto ni Meneja Masoko wa CRDB Microfinance, Ariel Mkony
Meneja Masoko wa CRDB Microfinance, Ariel Mkony kabla ya kufanyika kwa droo kubwa ya mwezi katika kampeni ya Shinda na SimAccount iliyofanyika Oktoba 25, 2018 Mikocheni jijini Dar es salaam. Katikati ni Meneja Uendeshaji wa CRDB Microfinance, Raymond Urassa na kulia ni Balozi wa Kampeni hiyo, Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Zuwena Mohamed (Shilolole).

WAZIRI LUKUVI AAGIZA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA USHIRIKA KUTOONDOLEWA ENEO LA LAMBO ESTATE NA KUPATIWA EKARI MBILI KILA MMOJA

0
0
Na Munir Shemweta, WANMM Kilimanjaro

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekata mzizi wa fitna ambapo ameagiza waliokuwa wafanyakazi wa chama cha ushirika katika eneo la Lambo Estate Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro kutoondolewa katika eneo hilo na kila mmoja kupatiwa ekari mbili kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kimaisha. Uamuzi  huo wa Lukuvi wa kutoa ekari mbili kwa wananchi hao 78 unafanya kutolewa kwa jumla ya ekari 156  kati ya ekari 1600 . Uamuzi huo unafuatia mgogoro wa muda mrefu baina ya waliokuwa wafanyakazi wa ushirika na uongozi .Mgogoro huo umeibuka baada ya wafanyakazi hao kutakiwa kuondoka katika makazi yaliyopo kwenye eneo la shamba  kutokana na utumishi wao kukoma.

Waziri Lukuvi alitoa maamuzi hayo leo katika wilaya Hai  ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kutembelea wilaya za Hai, Moshi na Same kushughulikia migogoro ya ardhi katika wilaya hizo mkoa wa Kilimanjaro. Mhe Lukuvi ameshangazwa na ushirika wa watu wachache kutaifisha ardhi na kuamuru watu waliokuwepo muda mrefu katika eneo la lambo estate kuondoka na kusema kuwa safari hii serikali itawanyoosha wale wote wanaofanya ujanja wa kuwaonea wanyonge.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Manufacturing Co Ltd cha eneo la Viwanda la Weruweru wilaya ya Hai Andreano Nyaluke wakati wa ziara ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika mkoa wa Klimanjaro.

"Sijawahi kuona ushirika wa namna hii ambapo wenye rasilimali hawanufaiki na ardhi iliyopo katika  kijiji chao halafu ardhi hiyo inakodishwa kwa wanachama wa ushirika wanaotoka  vijiji vingine"*  alisema Waziri Lukuvi.

Huku akishangiliwa na wananchi wakati akitoa maamuzi hayo, Mhe. Lukuvi alisema  amekwenda katika eneo hilo la Lambo Estate kushughulikia mgogoro wa ardhi. Suala la ushirika litashughulikiwa na waziri mwenye dhamana na vyama vya  ushirika ambae ataamua iwapo ushirika huo unafaa. Waziri Lukuvi alisisitiza kuwa, serikali haiwezi kuwaondoa wazee  walioishi kwa muda mrefu. Waziri wa Ardhi ametoa maagizo kwa wananchi watakaopewa ekari mbili kuwa maeneo watakayopatiwa ni kwa ajili ya kufanyia shughuli zao na hawaruhusiwi kuuza na kwa yeyote atakayeamua kuondoka eneo hilo basi eneo hilo litabaki kuwa la serikali.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akipata maelezo ya mashine iliyotengenezwa katika Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Manufacturing Co Ltd cha eneo la Viwanda la Weruweru wilaya ya Hai kutoka kwa meneja wa kiwanda hicho Andreano Nyaluke wakati wa ziara ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika mkoa wa Klimanjaro.

Kufuatia maelekezo hayo Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai kuanza mara moja zoezi la kuwagawia  wananchi ekari hizo kama ilivyoagizwa na  mhe Lukuvi.

Awali Katibu wa jumuiya ya wanaushirika Edward Chedi alimueleza Mhe Waziri Lukuvi kuwa mgogoro wa eneo hilo ulianza mara baada ya shamba hilo kutaifishwa na ajira za walikuwa wafanyakazi wa ushirika kukoma mwaka 2001 na kuwepo mfululizo wa kesi uliofikia ngazi ya Mahakama Kuu na kuagizwa waliokuwa wafanyakazi kulipwa mafao na kukabidhiwa vyeti vya kutambuliwa pamoja na ekari hamsini za kujikimu kwa kipindi  watakachokaa hapo kabla ya kuondolewa.
Baadhi ya nyumba za wananchi waliokuwa wafanyakazi wa Ushirika katika eneo la Lambo Estates wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro ambao Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi aliamuru wasiondoke eneo hilo na kuwapatia kila mmoja ekari mbili kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao ikiwa ni utatuzi wa mgogoro wa muda mrefu.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 26, 2018

TAASISI YA USTAWI WA JAMII KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI AWAMU YA TATU

ARUMERU WAAZIMIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

0
0
Na Imma Msumba

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Cornel Muro anakusudia kupeleka Ombi Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kufuta Hati za baadhi ya Mashamba makubwa ya ardhi ambayo wamiliki wake wamebainika kuwa chanzo cha kuvuruga Amani na Usalama Kutokana na kuwepo Kwa migogoro ya muda mrefu ambayo baadhi imegharimu maisha ya wananchi pamoja na uharibifu wa Mali.

Dc Muro Ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara ya utatuzi wa mgogoro wa Ardhi katika kata ya Selasi Sing’isi ambayo ina migogoro mikubwa ya Ardhi baina ya wananchi waliovamia Mashamba ya Wizara ya Kilimo pamoja na Mashamba ya wawekezaji ambayo yamesababisha madhara makubwa ya kuuwawa Kwa wananchi wawili uku mali zikiharibiwa vibaya pamoja kukosekana Kwa Amani Kwa muda wa zaidi ya miaka 5 .

Mhe. Muro ambae alilazimika kutembea Kwa miguu katika Kata nzima ameshangazwa kuona wananchi wengi wenye Uwezo wa kulima wakishindwa kulima Kutokana na baadhi ya wawekezaji na wamiliki wa maeneo hayo kushindwa kuyaendeleza hatua iliyosababisha wananchi kuamua kuvamia Mashamba hayo na kulima kienyeji hatua ambayo imeibua Migogoro mikubwa ya ardhi, ambapo amesisitiza Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Wawekezaji wanawekeza Kwa nia ya dhati na sio kuhodhi Mashamba makubwa ambayo wameshindwa kuyaendeleza na hatimae kutoa mwanya Kwa wananchi kuvamia na kisha kuibua migogoro.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara baada ya kukagua maeneo hayo katika viwanja vya chama cha Ushirika Sing’isi Mhe. Muro amesema katika hatua za awali ametumia Busara ya kumtaka Ndugu Aloyce Kimaro mmiliki wa Hotel ya Nakara kutokanyaga Eneo la Madira Sing’isi alilokuwa akitaka kubadilisha matumizi ya Ardhi, hatua iliyosababisha Kuibuka Kwa vurugu kubw,Vifo pamoja na uharibifu wa Mali katika Eneo hilo.

Hapo awali Ndugu Kimaro alipewa Eneo hilo na Wizara ya Kilimo Kwa ajili ya uwekezaji wa hotel Kubwa Kwa ajili ya Mkutano wa kimataifa,ambapo taarifa zinaonesha kuwepo na viashiria vya uvunjifu wa Amani endapo Ndugu Kimaro atarejea katika Eneo hilo kwani taarifa za awali zinaonyesha kuwepo Kwa utata wa njia alizotumia kumilikishwa Shamba hilo na kuviagiza vyombo vya ulinzi na Usalama kuendelea kulichunguza jambo hilo Kwa umakini mkubwa
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mh.Jerry muro akihutubia wananchi wa Kata ya singisi
 Dc Muro akiwa na ujumbe wake akiwa katika ziara ya utatuzi wa mgogoro wa Ardhi katika kata ya Selasi Sing’isi ambayo ina migogoro mikubwa ya Ardhi baina ya wananchi waliovamia Mashamba ya Wizara ya Kilimo pamoja na Mashamba ya wawekezaji ambayo yamesababisha madhara makubwa ya kuuwawa Kwa wananchi wawili huku mali zikiharibiwa vibaya pamoja kukosekana Kwa Amani Kwa muda wa zaidi ya miaka 5 .
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akifafanuliwa jambo na  Afisa Mtendaji kata wa Singisi.

 
Viewing all 109611 articles
Browse latest View live




Latest Images