Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

AZAM vs JKT TANZANIA KESHO UWANJA WA MEJA JENERALI ISAMUHYO MBWENI

$
0
0

BAADA ya kucheza mechi nne nyumbani, Azam  itakuwa ugenini kuvaana na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) utakaofanyika Kesho kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.

Azam  inaenda kucheza na JKT ikiwa na ari kubwa baada ya kushinda mechi tatu mfululizo huku ikivuna pointi 10 kati ya 12 katika mechi nne zilizopita, hadi sasa ikiwa kileleni kwa pointi zake 21 baada ya kucheza mara tisa, ikishinda sita, sare tatu na kutopoteza hata mmoja.

Wapinzani wao JKT Tanzania wanaofundishwa na Bakari Shime, nao hawajapoteza mchezo wowote hadi sasa ikiwa nafasi ya tisa kwenye msimamo na pointi zake 15, ikishinda mechi tatu na kutoka sare sita.

Kocha Msaidizi wa Azam , Juma Mwambusi, ameweka wazi kuwa wamekiandaa vema kikosi chao kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo huku akidai wanawafahamu vilivyo wapinzani wao.

Kuelekea mchezo huo, Azam  inatarajia kumkosa kiungo wake na Nahodha Msaidizi, Frank Domayo ‘Chumvi’, ambaye anasumbuliwa na majeraha ya goti akitarajia kukosekana kwa miezi minne huku pia Nahodha Agrey Moris, akiwa mgonjwa akitarajiwa kutokuwa sehemu ya mechi hiyo.

Kiungo wake mshambuliaji, Tafadzwa Kutinyu, aliyekuwa kwenye majukumu ya timu yake ya Taifa Zimbabwe tayari ameshajiunga na wenzake mazoezini tayari kwa maandalizi ya mchezo huo.

Huo utakuwa ni mchezo wa 19 timu hizo kukutana kwenye ligi hiyo, kwa mara ya kwanza zilikutana Septemba 6, 2008 ukiwa ni msimu wa kwanza tokea Azam FC ipande daraja, ilishuhudiwa JKT Ruvu ikishinda mabao 2-1 huku pia wakipata ushindi kama huo kwenye mechi ya mzunguko wa pili.

Katika mechi 18 zilizopita, Azam FC imeonekana kuwa na wastani mzuri wa kushinda mechi nyingi pamoja na mabao mengi dhidi ya JKT Tanzania, imeshinda mara 10, ikafungwa tatu huku nne zikiisha kwa sare.

Jumla ya mabao 47 yamefungwa katika mechi hizo 18, ukiwa ni wastani wa kufungwa mabao 2.6 kwenye kila mechi, Azam FC imefunga robo tatu kati ya hayo ikiweka nyavuni 33 huku JKT Tanzania yenyewe ikitupia 14 tu.

Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana tokea JKT Tanzania ibadilishe jina kutoka JKT Ruvu Stars hadi jina hilo la sasa na Azam FC nayo kuwa rasmi kampuni msimu huu ikijulikana kama Azam FC Company Limited, pia matajiri hao watacheza kwa mara ya kwanza kwenye uwanja huo mpya wa maafande hao.

Matumizi ya gesi kuzalisha umeme yaokoa Dola za Marekani Bilioni 10.29

$
0
0
Na Teresia Mhagama, Dodoma
Imeelezwa kuwa, matumizi ya gesi asilia katika kuzalisha umeme yameokoa fedha za kigeni kiasi cha Dola za Marekani bilioni 10.29 ambazo zingetumika kununua mafuta nje ya nchi kwa ajili ya kuzalisha umeme kutoka mwaka 2004 hadi Septemba 2018.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Eng. Kapuulya Musomba wakati akiwasilisha taarifa kuhusu mchango wa Gesi asilia katika uzalishaji wa umeme kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

“ Kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2004 hadi Septemba 2018, Gesi asilia kiasi cha futi za ujazo bilioni 381 kilitumika kuzalisha umeme pekee ambapo hadi kufikia mwezi Septemba 2018, mitambo yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa jumla ya megawati 831 kwa siku kutokana na gesi asilia imewekezwa nchini,” alisema Musomba.

Aliongeza kuwa, zaidi ya asilimia 50 ya umeme unaozalishwa nchini, unatokana na Gesi asilia huku vyanzo vingine vya uzalishaji umeme vikiwa ni maji, nishati jadidifu  na mafuta.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, akitoa taarifa ya utangulizi kwa Kamati hiyo, alisema kuwa kiasi cha gesi kilichopatikana nchini hadi sasa ni futi za ujazo trilioni 57.54 ambapo futi za ujazo trilioni 8.96 zimepangwa kutumika kuzalisha umeme hadi ifikapo mwaka 2046.

Alisema kuwa, Serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme  kwa kutumia  gesi asilia ukiwemo mradi wa upanuzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I kwa kuongeza mitambo itakayozalisha megawati 185 na kufanya kituo hicho ambacho kwa sasa kinazalisha megawati 150, kuweza kuzalisha jumla ya megawati 335.

“ Tunatarajia pia kutekeleza mradi wa Somanga Fungu utakaozalisha umeme wa kiasi cha megawati 330 kwa kutumia Gesi asilia unaotarajiwa kukamilika mwaka 2021 ambapo mahitaji ya Gesi asilia katika mtambo huu yatakuwa takriban futi za ujazo milioni 46 kwa siku,” alisema Dkt. Kalemani.

Vilevile alisema kuwa, Gesi asilia itatumika kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 330 mkoani Mtwara ambapo mradi huo utakamilika mwaka 2021 na matumizi ya gesi asilia katika mtambo huo yatakuwa ni takriban futi za ujazo milioni 42 kwa siku.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (aliyesimama) akitoa taarifa ya utangulizi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu mchango wa Gesi asilia katika uzalishaji wa umeme jijini Dodoma.
 Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakifuatilia kikao baina yao na Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Eng. Kapuulya Musomba akiwasilisha taarifa kuhusu mchango wa Gesi asilia katika uzalishaji wa umeme kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jijini Dodoma.

RAIA WA USWISI AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 34 AMA JELA MIAKA 20

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii

MKURUGENZI wa Fairme NGO, Rene Staheli (62) ambaye pia ni raia wa Uswis leo Oktoba 23, 2018 amehukumiwa kulipa faini ya Sh Sh. Milioni 34 ama kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani baada ya kukiri kosa la kukutwa na vipande vitatu vya meno ya Kiboko.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Rwizile amesema mahakama imemtia hatiani mshtakiwa kufuatia yeye mwenyewe kukiri kosa lake.

Kufuatia kukiri kutenda kosa linalokukabiki na kukubali vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapa,mahakama inakutia hatiani na inakuhukumu kulipa faini ya Sh 34,036,188 na iwapo utashindwa basi utatumikia kifungo cha miaka 20 gerezani", amesema Hakimu Rwizile.

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, wakili wa serikali Mwandamizi, Patrick Mwita aliiomba mahakama kutoa adhabu Kali kwa mshtakiwa huyo kwa kukutwa na maliasili yetu ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.Katika utetezi wake, ameiomba mahakama impe adhabu ndogo kwa kuwa hili ni kosa lake la kwanza, haijaisumbua mahakama ndio maana amekiri kosa lake na pia anafamilia kubwa inayomtegemea huko kwao Uswisi. 

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi, mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Oktoba 16, mwaka huu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere alikamatwa akiwa na nyaraka za Serikali ambazo ni vipande vitatu vya meno ya Kiboko vyenye uzito wa kilogeamu tano na thamani ya USD 1,500 ambazo ni sawa na Sh 3, 403, 618.80 Mali ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa wanyama pori.

Hadi MICHUZI BLOG inaondoka katika mahakama ya Kisutu mshtakiwa alishindwa kulipa faini na amepelekwa gerezani.
Mkurugenzi wa Fairme NGO, Rene Staheli (62) ambaye pia ni raia wa Uswis leo Oktoba 23.2018 akitoka katika Mhakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuhukumiwa kulipa faini ya Sh Sh. Milioni 34 ama kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani baada ya kukiri kosa la kukutwa na vipande vitatu vya meno ya Kiboko.

WAZIRI JAFO AWATWISHA MZIGO MEYA, MKURUGENZI MANISPAA YA ILEMELA

$
0
0
Na Baltazar Mashaka, Mwanza 
HALMASHAURI ya Manipaa ya Ilemela imeagizwa kukusanya na kusimamia mapato ili kusukuma maendeleo kwa maslahi ya wananchi.

Agizo hilo lilitolewa na Waziri wa Nchi,  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo wakati akikagua miradi ya ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri hiyo,barabara na hospitali ya Wilaya ya Ilemela.

Alisema kuwa halmashauri hiyo haikufanya vizuri kwenye mapato baada ya kukusanya sh.bilioni 4.6 kati ya bilioni 5.7 ya makisio ya bajeti na hivyo kusababisha ishike nafasi ya mwisho ambapo awali ilikisia kukusanya bilioni 11.7.

Jafo alisema kwenye amebini halmshauri nyingi zimegubikwa na mianya ya upotevu wa fedha za mapato kwa kutumia mashine za Possy ambapo fedha zinazokusanywa kwenye mfumo ni tofauti na baadhi ya watu wanakimbia na fedha huku wengine wakibaki nazo.

 “Agenda ya serikali ni mapato hivyo watumishi badilikeni kiutendaji, maana mapato hayo yanatakiwa kusukuma maendeleo ya wananchi na halmashauri haziwezi kujiendesha bila mapato .Ilemela ni tajiri lakini imefanya vibaya na kuharibu sifa ya Mkuu wa Mkoa, Wilaya na Mkuerugenzi sababu ya uzembe wa watendaji, ni aibu na tafakarini mbadilike,”alisema.

Aliwaagiza Meya  Manispaa hiyo Renatus Mulunga na Mkurugenzi  John Wanga pamoja na kamati ya fedha kusimamia mapato yote kwa umakini kwa sababu wamepewa dhamana hiyo kwa ajili ya Watanzania  wanyonge.
 Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akikagua miradi ya ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.
  Mhandisi Charles Mathias wa kampuni ya Ushauri ya Nimeta Consultancy akimwelekeza jambo Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo wakati akikagua jengo la utawala la Manispaa ya Ilemela.kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.
 Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiangalia ramani ya mradi wa ujenzi wa jengo la kituo cha afya Buzuruga alipoafanya ziara katika Wilaya ya Ilemela.
 Selemani Jafo ambaye ni Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) akizungumza na baadhi ya wananchi na watumishi wa kituo cha afya Buzuruga kabla ya kukagua uboreshaji wa majengo ya kituo hicho.
Mhandisi Peter Marmo anayetekeleza mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya majengo ya kituo cha Afya buzuruga katika Manispaa ya Ilemela akimweleza jambo Waziri wa Ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua miradi inayotekelezwa chini ya wizara hiyo. Picha Zote na Baltazar Mashaka.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Matumizi ya gesi kuzalisha umeme yaokoa Dola za Marekani Bilioni 10.29

$
0
0

Na Teresia Mhagama, Dodoma
IMEELEZWA kuwa, matumizi ya gesi asilia katika kuzalisha umeme yameokoa fedha za kigeni kiasi cha Dola za Marekani bilioni 10.29 ambazo zingetumika kununua mafuta nje ya nchi kwa ajili ya kuzalisha umeme kutoka mwaka 2004 hadi Septemba 2018.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Eng. Kapuulya Musomba wakati akiwasilisha taarifa kuhusu mchango wa Gesi asilia katika uzalishaji wa umeme kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

“ Kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2004 hadi Septemba 2018, Gesi asilia kiasi cha futi za ujazo bilioni 381 kilitumika kuzalisha umeme pekee ambapo hadi kufikia mwezi Septemba 2018, mitambo yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa jumla ya megawati 831 kwa siku kutokana na gesi asilia imewekezwa nchini,” alisema Musomba.

Aliongeza kuwa, zaidi ya asilimia 50 ya umeme unaozalishwa nchini, unatokana na Gesi asilia huku vyanzo vingine vya uzalishaji umeme vikiwa ni maji, nishati jadidifu na mafuta.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, akitoa taarifa ya utangulizi kwa Kamati hiyo, alisema kuwa kiasi cha gesi kilichopatikana nchini hadi sasa ni futi za ujazo trilioni 57.54 ambapo futi za ujazo trilioni 8.96 zimepangwa kutumika kuzalisha umeme hadi ifikapo mwaka 2046.

Alisema kuwa, Serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ukiwemo mradi wa upanuzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I kwa kuongeza mitambo itakayozalisha megawati 185 na kufanya kituo hicho ambacho kwa sasa kinazalisha megawati 150, kuweza kuzalisha jumla ya megawati 335.

“ Tunatarajia pia kutekeleza mradi wa Somanga Fungu utakaozalisha umeme wa kiasi cha megawati 330 kwa kutumia Gesi asilia unaotarajiwa kukamilika mwaka 2021 ambapo mahitaji ya Gesi asilia katika mtambo huu yatakuwa takriban futi za ujazo milioni 46 kwa siku,” alisema Dkt. Kalemani.

Vilevile alisema kuwa, Gesi asilia itatumika kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 300 mkoani Mtwara ambapo mradi huo utakamilika mwaka 2021 na matumizi ya gesi asilia katika mtambo huo yatakuwa ni takriban futi za ujazo milioni 42 kwa siku.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (aliyesimama) akitoa taarifa ya utangulizi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu mchango wa Gesi asilia katika uzalishaji wa umeme jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Eng. Kapuulya Musomba akiwasilisha taarifa kuhusu mchango wa Gesi asilia katika uzalishaji wa umeme kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jijini Dodoma.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakifuatilia kikao baina yao na Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jijini Dodoma.

TEMBO WAHARIBU MAZAO YA WAKULIMA SEGWA HUKO FUKAYOSI

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, FUKAYOSI 
BAADHI ya wakulima kitongoji cha Segwa, kata ya Fukayosi Bagamoyo mkoani Pwani, kinakabiliwa na tatizo la uvamizi wa tembo ambao wameharibu mazao yao kwenye hekari kumi na kuvunja nyumba mbili. 

Akielezea kero hiyo wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dk.Shukuru Kawambwa, katika kata ya Fukayoso, mwenyekiti wa kijiji cha Mwavi,Shabani Mkumbi alisema ,tembo wamekuwa wakitokea hifadhi ya Taifa Saadani na kuvuka mto WAMI na kuingia katika maeneo ya watu kwenye vijiji vya Fukayosi  na Mwavi . 

"Mazao yaliyoharibiwa ni muhogo 
,matikiti,nyanya Maji ,nyanya chungu,maboga , hoho, mananasi, migomba na miwa ." alisema.
 
Mkazi wa Segwa Hassan Kalahuka alisema ,kutokana na tatizo hilo wameamua kuunda kamati ambayo itafuatilia suala la fidia kupitia ofisi ya wilaya kwani wao wamekwama. 

Mmoja wa aliyeathiriwa shamba lake na tembo hao ,Ramadhani Mfaume alielezea ,mbali ya kuharibiwa mazao yake pia gunia zake kumi zimeharibiwa. 

Alibainisha tangu apate hasara hiyo agost 21 mwaka huu hajalipwa kifuta jasho hadi sasa hivyo amemuomba mbunge Kawambwa kuwasaidia. 

Akipokea kero hiyo kubwa, Dk .Kawambwa alisema amepokea taarifa hiyo na ataangalia namna ya kuzungumza na TANAPA, wilaya na wizara husika kuona namna watakavyosaidiwa. 

Akiwa katika kitongoji hicho alifikishiwa bado kuna kero ya ukosefu wa maji safi na salama, wanatumia maji ya visima vya asili ambapo mvua zikikatika wanapata shida zaidi. 

Dk.Kawambwa aliwaambia serikali inaendelea kutatua tatizo la maji kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa CHALIWASA, ili hali kupunguza makali ya kero hiyo. 

SERIKALI YAAINISHA DAWA MUHIMU ZINAZOPATIKANA MSD

$
0
0
WAMJW, BUNGENI DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeainisha dawa aina 135 kama dawa muhimu na za kipaumbele cha wizara kwa lengo la kuhakikisha kuwa zinapatikana nyakati zote katika bohari zote za kanda za MSD.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Janii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa ya utendaji ya Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) aliyowasilisha katika kamati ya kudumu ya Bunge huduma na maendeleo ya jamii jijini Dodoma.

Waziri Ummy alisema tathimini ya upatikanaji wa dawa hizo ni wa hadi mwezi Julai 2018 ambapo ni sawa na asilimia 93 hivyo Wizara yake imeitaka MSD kuongeza idadi ya dawa muhimu 177 na kufikia dawa za kipaumbele 312 ambapo upatikanaji wa dawa hizo ni asilimia 73 kufikia robo mwaka ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019.

“Hali ya upatikanaji dawa muhimu umeimarika kuanzia mwaka 2016/2017 na kufikia asilimia 93 nchi nzima katika mwaka 2017/2018 na hivyo kuweza kufanikiwa katika maeneo mengi na kufikisha dawa moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma za afya nchi nzima”.Alisema Waziri Ummy Mwalimu. Aidha, Waziri Ummy alisema MSD imeweza kusambaza dawa moja kwa moja hadi vituo vya kutolea huduma za afya vinavyofikia 5,432 nchi nzima kwa kutumia magari 215 na hivyo kusambaza dawa zenye thamani za shilingi bilionini 600 kwa mwaka kupitia mfumo wa ugavi ulio enea nchi nzima.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifafanua hali ya upatikanaji wa dawa nchini kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini hawapo pichani wakati wa kikao cha kamati ya hiyo kinachoendelea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , katikati aliyekaa ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile. 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akichangia mada wakati wa kikao cha kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini kinachoendelea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , wa kwanza kulia aliyekaa ni Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu. 
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Bw. Peter Serukamba akitoa mwongozo kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini wakati wa kikao cha kamati ya hiyo kinachoendelea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,wa kwanza kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

WAZIRI MKUU AITAKA SIDO KUBUNI TEKNOLOJIA RAFIKI

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO)lijielekezekatika kubuni teknolojia na mitambo rafiki inayolenga kutatua changamoto za wajasiriamali kulingana na mazingira yao. 

Amesema Serikali inaendelea kuimarisha shughuli za SIDO lakini bado kuna  changamoto za wajasiriamali wadogo ambazo lazima zishughulikiwe kwa kasi kubwa ili kufungamanisha shughuli za SIDO na uchumi wa Viwanda

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Oktoba 23, 2018) wakati akifungua Maonesho ya SIDO kitaifa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nyakabindi vilivyoko wilayani Bariadi mkoani Simiyu na kuhudhuriwa na wajasiriamali 500.Amesema ili kufikia uchumi wa kati inambidi kila Mtanzania mahali alipo afanye kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu. “Tusipoteze wakati kwa kufanya mambo yasiyo na tija. Tuzingatie falsafa ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa Kazi Tu.”

“Mfano kwa hapa Bariadi, tunatarajia SIDO watuletee teknolojia na mitambo inayoweza kurahisisha ukamuaji wa mafuta yanayotokana na mbegu za alizeti na pamba, kwa Dodoma taknolojia na mitambo kwa ajili ya kuchakata zabibu.”

“Kigoma pelekeni teknolojia na mitambo kwa ajili ya kuchakata mbegu za michikichi na kwenye maeneo yanayolimwa korosho teknolojia na mitambo  ya kubangua korosho na maeneo kama Ilula ambayo yanazalisha nyanya kwa wingi wapate teknolojia na mitambo ya kusindika na kuhifadhi nyanya na mbogamboga.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chaki zilizotengenezwa wilayani Maswa katika maonesho ya Shirika la Kuhudumia  Viwanda Vidogo (SIDO) kwenye  uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea jembe la asili kutoka mhunzi,  Mashaka Daniel wa  Bukoba katika Maonesho ya Shirika la Kuhudumia  Viwanda Vidogo (SIDO)  aliyoyafungua kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa  Ufundi wa Shirika la Kuhudumia  Viwanda Vidogo (SIDO), Prosper Godfrey (kulia)  kuhusu majiko makubwa yanayotengenezwa na SIDO wakati alipofungua Maonesho ya SIDO kwenye uwanja wa Nyakabindi  mkoani Simiyu Oktoba  23, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simyu, Anthony Mtaka na watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi  Stella Manyanya.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Maonesho ya Shirika la  Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Badhi ya wananchi wa  mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua Maonesho ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO)  kwenye uwanja wa Nyakabindi.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) kitanzania ili wakue na kuwa wawekezaji wakubwa. Pia kuwawekea mazingira wezeshi ya kufanya shughuli zao.”
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Ujerumani Yampongeza Rais Magufuli kwa Kupambana na Rushwa – Balozi Waechter

$
0
0

Na Judith Mhina – MAELEZO

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt Detlef Waechter amempongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kufanikiwa kupambana na rushwa nchin Tanzania na kupata mafanikio makubwa ndani ya kipindi kifupi.

Hayo amesema Balozi Waechter alipofanya mahojiano na Idara ya Habari MAELEZO mapema jana katika hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro Dar-es-salaam Kempinski katika barabara ya Sokoine Jijini Dar-es –salaam.

Akielezea jinsi rushwa ilivyoota mizizi sehemu nyingi ikiwemo Ujerumani amesema “Tatizo la rushwa sio la Tanzania peke yake, hata pale Ujerumani lipo japo si kwa kiasi kikubwa, bali kila mara serikali inapaswa kujiangalia na kuhakikisha inapambana na mfumo wa rushwa mahala popote. Ili raia wako wawe na imani na serikali yako”

Kwa dhati kabisa nampongeza Rais Magufuli kwani hali ilikuwa sio nzuri kulingana na ripoti tuliyoisikia wakati wa Mkutano wa 38 wa Bara la Afrika wa Kuthibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya miezi mawili iliyopita. Uwepo wa rushwa Tanzania ilikuwa ni eneo linalotumiwa katika kupitisha madawa hayo ambapo sasa suala hili limepungua kwa kiasi kikubwa kutokanana juhudi za Rais Magufuli.

Akielezea ubaya wa rushwa Balozi Waechter amesema kuwa matatizo ya rushwa yanarejesha nyuma maendeleo kwa kuwa watu hawapati huduma wanazostahili kwa kuwa tu kuna wengine wanatumia rushwa. Halikadhalika uwepo wa rushwa unaondoa uaminifu kutoka Taifa moja kwenda linguine au nchi moja kwenda nyingine.

Ukiangalia maeneo ambayo hayana utulivu na amani, inatokana na kushamiri kwa rushwa na kuwa na serikali ambazo hazisimamii vema huduma kwa wananchi wake. Hili ni tatizo kubwa lililokumba nchi za kiafrika ambazo raia wake kila siku wanatafuta njia ya kuelekea Ulaya.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

WAKULIMA SKIMU YA UYOLE WAOMBA KUTEMBELEWA NA WAKALA WA VIPIMO

$
0
0
Wakulima, katika skimu ndogo ya kilimo cha mbogamboga ya Iganjo Iliyopo Iliyopo Uyole nje kidogo ya jiji la Mbeya, wameomba wataalam kutoka wakala wa vipimo kuwatembelea ili kuweza kusaidia tatizo la vipimo halisi vya mazao yao ambavyo vinafanywa katika hali ya udanganyifu na kuwasababishia hasara. 

Hayo yemeelezwa na Mwenyekiti wa chama cha Wamwagiliaji Iganjo Bw. John Soda alipokuwa akizungumza katika eneo hilo mbapo alisema kuwa suala la kuzidisha ujazo unaotakiwa (lumbesa) bado ni tatizo jambo ambalo linawasababishia wao kama wakulima kuuza mazao yao kwa bei ya hasara.

Bwana Soda alisema kuwa kumekuwa na tatizo la upimaji wa mazao katika magunia ambapo magunia yanayokaguliwa yanakuwa na vipimo halisi lakini magunia yanayokwenda sokoni yanakuwa hayana uhalisia. Tunawaomba wakala wa vipimo waweze kuja kututembelea na kusimamia kwa ukaribu swala hili la udanganyifu katika vipimo, jambo ambalo kwa kiasi fulani limekuwa likitusababishia hasara sisi wakulima wa mboga mboga hasa katika zao la viazi, vitunguu na karoti, Pamoja na hilo naiomba serikali iweke utaratibu wa kuuza mazao na kutoa bei elekezi.” Alisema Bwana Soda.

Kwa Upande wake Bwana Solomon Soda Mkulima katika skimu hiyo aliishukuru Serikali kwa ukarabati na ujenzi wa miundombinu katika skimu hiyo na kuiomba iendelee kuwasaidia waweze kupata pembejeo kwa bei ya ruzuku, na kumalizia kuboresha miundombinu katika sehemu iliyobakia.

Katika picha ni Miundombinu mfereji wa maji unaopeleka maji katika skimu ya umwagiliaji Iganjo Uyole mkoani Mbeya, pembeni yake ni shamba la mahindi yanayomwagiliwa kwa kutumia maji yanayopita katika mfereji huo. 

Bwana John Soda mkulima katika skimu ya Iganjo Uyole Mkoani Mbeya akizungumza kuhusu ukarabati uliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika skimu hiyo, inayoonekana kwa nyuma ni sehemu ya miundombinu hiyo.

Katika Picha ni banio linaloruhusu maji toka chanzo cha maji cha mto Nkwanana kupeleka katika skimu ya umwagiliaji ya iganjo iliyopo Uyole mkoani Mbeya.

Fumanizi Bongo vs Nigeria.

Invitation to attend "a night with Mzungu Kichaa" at HYATT KILIMANJARO HOTELI IN DAR Level 8

$
0
0
What: "A night with Mzungu Kichaa"
When: Thursday 25th of October 18.30 - 21.30
Where: Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro - Level8 rooftop
Why: Because it will be epic

MWILI WA ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA MAGOMENI MHE DKT.JULIAN BUJUGO AAGWA LEO

$
0
0
Akiongoza shughuli hiyo ya kuaga mwili wa aliekua Diwani Kata ya Magomeni Manispaa ya Kinondoni Dkt.Julian Bujugo  iliyohudhuriwa pia na viongozi wa vyama na Serkali,  Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni  Mh.Benjamini Sitta amesema,  Kinondoni imepoteza mpiganaji, mpenda haki, mtetezi wa wanyonge,  na mzalendo. 
"Bujugo alikuwa mzalendo, alikuwa ni mtu aliyependa kuona mambo yanakwenda, wanyonge wanapata haki, hata siku ambayo usiku wake mauti inamkuta, Mh Bujugo alikuja ofisini kwangu mchana kwa swala la walemavu wa magomeni kuhusiana na ada ya usajili wa kikundi wanayotozwa", alisema  Meya Sitta.

Shughuli hii ya kuuaga mwili wa marehemu Julian Rushaigo Bujugo imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron Kagurumjuli, wakuu wa idara na vitengo, wananchi wa kata ya Magomeni, pamoja na viongozi wa vyama na serikali, akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bi.Kate Kamba, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Ndg. Harold Maruma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda, pamoja na Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni.

Bwana ametoa, bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amen.

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda
akiongoza waombolezaji  kuaga mwili wa aliekua Diwani Kata ya Magomeni Manispaa ya Kinondoni  Dkt.Julian Bujugo leo katika viwanja nya Manispaa hiyo  jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililobeba mwili wa aliekua  Diwani Kata ya Magomeni Manispaa ya Kinondoni Dkt.Julian Bujugo leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
 Meya  wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akitoa heshima ya mwisho mbele ya jeneza lililobeba mwili wa alikua Diwani wa Kata ya Magomeni Manispaa ya Kinondoni Dkt. Julian Bujugo  katika viwanja vya manispaa hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Madiwani  walioshiriki kuaga mwili wa aliekua Diwani Kata ya Magomeni Manispaa ya Kinondoni  Dkt. Julian Bujugo.
 Sehemu ya waombolezaji walioshiriki kuaga mwili wa aliekua Diwani Kata ya Magomeni Manispaa ya Kinondoni  Dkt. Julian Bujugo.
 Sehemu ya waombolezaji walioshiriki kuaga mwili wa aliekua Diwani Kata ya Magomeni Manispaa ya Kinondoni  Dkt. Julian Bujugo.
 Sehemu ya waombolezaji walioshiriki kuaga mwili wa aliekua Diwani Kata ya Magomeni Manispaa ya Kinondoni  Dkt. Julian Bujugo.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
Sehemu ya waombolezaji walioshiriki kuaga mwili wa aliekua Diwani Kata ya Magomeni Manispaa ya Kinondoni  Dkt. Julian Bujugo.

WIKI YA MAONYESHO YA VIWANDA MKOA WA PWANI KUANZA OKTOBA 29, BENKI YA CRDB WADHAMINI WAKUU

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Evarist Ndikiro (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza siku ya kuanza kwa Maonesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani ambayo yatafunguliwa rasmi tarehe 29 Oktoba 2018 na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, katika viwanja vya Saba Saba mjini Kibaha. Benki ya CRDB ni Mdhamini Mkuu wa Maonyesho hayo. Wengine pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (wa pili kulia), Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Theresia Mmbando (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto) pamoja na Meneja wa Benki ya CRDB, Rosemary Nchimbi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikiro akimuonyosha kitu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto) wakati walipotembelea katika viwanja vya Saba Saba mjini Kibaha ambavyo vitatumika kwa Maonesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani kuanzia tarehe 29 Oktoba 2018. Benki ya CRDB ni Mdhamini Mkuu wa Maonyesho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikiro (wa pili kushoto) akielekeza jambo kwa mafundi wa JKT wanaoendelea na ujenzi katika viwanja vya Saba Saba mjini Kibaha ambavyo vitatumika kwa Maonesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani kuanzia tarehe 29 Oktoba 2018.
Eneo la uwanja utakaotumika kwa Maonesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani, likiwa katika hatua za maandalizi.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 23.10.2018


VOA SWAHILI: Duniani Leo October 23, 2018

UTIAJI SAINI MKATABA WA MGAWANYO WA UZALISHAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA (PSA) ZANZIBAR

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Mtawala wa Ras Al Khaimah Shaikh   Saud bin Saqr  Al  Qasimi wakati alipofanya ziara ya kuitembela Zanzibar mara alipofika katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar  kushuhudia utiaji wa saini mkataba wa mgawanyo wa uzalishaji wa mafuta na Gesi asilia(PSA) baina ya Serikali ya Mapinduzi na Rakgas
Mkurugenzi mtendaji wa  Kampuni ya Rakgas L.L.C ya Ras Al Khaimah Bw.Kamal Mohamed Ataya(kulia) Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Makazi Mhe.Salama Aboud Talib (katikati) Mkurugenzi Katika Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta Zanzibar (ZPDC)Nd,Mwanamkaa Abdulrahman Mohamed wakitia saini mkataba wa mgawanyo wa uzalishaji wa mafuta na Gesi asilia(PSA) baina ya Serikali ya Mapinduzi na Rakgas sherehe iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar leo. Picha na IKULU

TAARIFA YA HABARI YA ITV SAA MBILI USIKU OKTOBA 23, 2018

UKAGUZI WA MIRADI YA BUNGE INAYOTEKELEZWA NA SUMA JKT

$
0
0
Waziri wa ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Hussein Mwinyi ameridhishwa na hatua za utekelezaji wa miradi mitatu ya ujenzi wa Ofisi ya Bunge inayotekelezwa na Shirika la Uzalishaji la Jeshi hilo (SUMA JKT).

Mhe. Mwinyi alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea Ofisi ya Bunge kwa ajili ya kukagua miradi hiyo akiwa ameambatana na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Kanali Rajab Mabele.

“Nimeridhishwa hatua ya utekelezaji wa miradi mitatu inayotekelezwa na SUMA JKT ya ujenzi na ukarabati wa Ofisi ya Bunge, naishukuru Ofisi ya Bunge kwa kuliamini shirika la SUMA kwa ajili ya kutelekeza miradi hii,” alisema.Kwa upande wake Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai alilipongeza SUMA JKT kwa kuendelea kutelekeza miradi hiyo kwa ufanisi na kwamba hadi sasa miradi yote inaendelea vizuri.

Alitaja miradi hiyo kuwa ni Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Bunge, ukarabati wa Jengo la Ofisi ya Bunge pamoja na ujenzi wa lift na ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Bunge.Alisema kwa upande wa ukarabati wa Jengo la Ofisi ya Bunge pamoja na ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Bunge tayari SUMA JKT wameshalipwa asilimia 40 na kazi zinaendelea vizuri.

“SUMA JKT ni shirika ambalo tumekuwa tukifanya nalo kazi na tunaridhika na kazi zao tunatamani wapewe miradi mingi ya Serikali,” alisema

Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma. Waziri mwinyi ametembelea Ofisi ya Bunge kukagua miradi mitatu 3 ya ujenzi ya inayotekelezwa na Suma JKT. 
Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi wakimsikiliza Mkuu wa SUMA-JKT – Ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Luteni Kanali Zabron Mahenge akitoa maelezo ya hatua ya utekelezaji mradi wa ukarabati wa Ofisi ya Bunge ulipofikia. Nyuma ya Waziri Mwinyi (mwenye miwani ) ni Mkurugenzi Mtendaji SUMA JKT Kanali Rajab Mabere na anayefuata ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerari Martin Busungu .

Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi wakipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa SUMA-JKT – Ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Luteni Kanali Zabron Mahenge wakati viongozi hao walipotembelea eneo linapojengwa lift katika Jengo la Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma . 
Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi wakimsikiliza Mkuu wa SUMA-JKT – Ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Luteni Kanali Zabron Mahenge akitoa maelezo ya hatua ya utekelezaji mradi wa ukarabati wa Ofisi ya Bunge ulipofikia.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 24,2018

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images