Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

FIVE HOUSES FOR SALE IN ONE TITLED PLOT.


USHIRIKIANO WA TAASISI ZA DINI NA SERIKALI NI MUHIMU-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ushirikiano mzuri baina ya taasisi mbalimbali za dini nchini na Serikali ni jambo la muhimu katika kuboresha na kuimarisha amani.

Ameyasema hayo Jumatatu, Oktoba 22, 2018 alipowasili jijini Mwanza akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako leo anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali.

Alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, Waziri Mkuu amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiwemo wa Serikali na wa dini mbalimbali.

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua mkakati wa viongozi wa dini wa kuunda kamati za amani nchini ambapo walianzia kwenye ngazi ya mkoa na sasa wamefikia katika kata.

“Viongozi wa dini mnadhamana kubwa katika kulifanya  Taifa liendelee kudumisha amani, utulivu na mshikamano, hivyo ushirikiano wenu na   Serikali ni muhimu.”

Amesema viongozi wa Serikali wakati wote wamekuwa tayari kufanyakazi na viongozi pamoja na taasisi mbalimbali za dini, lengo ni kuimarisha amani na utulivu uliopo nchini.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza inawajibu wa kuhakikisha kwamba maeneo ya mkoa huu yanaendelea kuwa salama.

Pia, Waziri Mkuu amempongeza Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikh Hassan Bin Mussa Kabeke kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo.

“Nakupongeza kaimu sheikh wa mkoa kwa kuteuliwa na ninakutakia kila la heri katika kazi yako na kwamba dhamana yako kubwa ni kuwaunganisha waislamu na waumini wa dini zote.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikh Hasani Bin Mussa Kabeke wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza  Oktoba 22, 2018 akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako kesho anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali.   Sheikh huyo amechaguliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella  (katikati) wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako kesho anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


AWESO AAGIZA WATALAAM WA MAJI NA WAKANDARASI WA MIRADI YA MAJI YA TSAMAS NA DARAKUTA-MINJINGU WAITWE POPOTE WALIPO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameelekeza Watalaam wa maji walioshiriki katika kusimamia ujenzi wa miradi ya maji ya Tsamas na mradi wa maji Darakuta-Minjingu pamoja na Wakandarasi waliopewa kandarasi katika miradi hiyo kufika katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Babati bila kukosa asubuhi ya tarehe 23.10.2018.

Mhe. Aweso (Mb) ambaye yuko mkoani Manyara katika ziara ya kikazi ametoa maelekezo hayo baada ya kubaini kasoro katika utekelezaji wa miradi hiyo ambapo pamoja na Serikali kutoa fedha, bado wananchi hawajapata huduma ya majisafi na salama.

Mradi wa maji wa Darakuta-Minjingu ambao hadi sasa umetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 1.7 ulisanifiwa mwaka 2009 na ulitakiwa kuhudumia vijiji vya Minjingu, Mwada, Ngoley, Olasiti, Masaini, Maramboi na Eluwai. Aidha, mradi wa maji wa Tsamas mkandarasi amelipwa zaidi ya Shilingi milioni 100, hata hivyo mabomba yaliyotumika katika chanzo cha maji yanapasuka hivyo kusababisha ukosefu wa huduma ya majisafi ya uhakika kwa wananchi.

Naibu Waziri Aweso (Mb), pamoja na hayo,  amepongeza utekeleza wa mradi wa maji wa Haraa unaozalisha lita elfu 21 kwa saa kwa kukamilika vizuri, na kuagiza fedha za mradi ziwekwe benki ili kuwezesha kamati ya watumia maji  kuendesha mradi.

Hadi mwezi Septemba 2018 mkoani Manyara, huduma ya upatikanaji maji vijijini ilikua asilimia 52 na Babati mjini asilimia 75.
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiongea katika eneo la mradi wa maji wa Bonga, uliopo kata ya Bonga Babati  mkoani Manyara. Mradi huo utakapokamilika utatoa maji lita elfu 40 kwa saa na kufikisha kiwango cha upatikanaji majisafi na salama katika mji wa Babati kuwa asilimia 95. Aidha, vijiji vya jirani navyo vitapata huduma ya majisafi na salama kupitia mradi huo. Waziri Aweso (Mb) amesema wote watakaostahili fidia kupisha mradi Serikali itawalipa.
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb)-kushoto, akimsikiliza Mbunge wa Babati vijijini Mhe. Jitu Soni –kulia, akimweleza kuhusu hali ya mradi wa maji wa Tsamas. Katikati ni MKuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Elizabeth Kitundu. 
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb)  aliyenyoosha mkono, akitoa maelekezo kuitwa popote walipo kwa Watalaam wa maji waliosimamia miradi ya maji ya Tsamas na mradi wa maji Darakuta –Minjingu, pamoja na Wakandarasi wa miradi hiyo mara moja.  Miradi hiyo imebainika kuwa na kasoro nyingi za kitalaamu, na haitoi maji ingawa Serikali imewalipa Wakandarasi
 Baadhi ya wanakijiji wa Kijiji cha Tsamas mkoani Manyara wakijadili kuhusu maji  katika kikao kifupi katika shamba la migombawakati wa ziara ya kikazi ya  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) haonekani pichani.
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiangalia maji yanayochotwa  katika mto Tsamas kwa matumizi mbalimbali na wananchi. 
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akikagua ubora wa bomba zilizotumika katika mradi wa maji Darakuta-Minjingu. Mradi huo ulisanifiwa mwaka 2009, na umeshatumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.7, hatahivyo wananchi bado hawajapata huduma ya majisafi na salama, hivyo wahusika wote, wakiwamo watalaam wa maji na wakandarasi wa mradi wameelekezwa kufika  katika kikao kitakachofanyika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Babati. 

WAZIRI MWINYI AKAGUA MIRADI YA BUNGE INAYOTEKELEZWA NA SUMA JKT

$
0
0
Waziri wa ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Hussein Mwinyi ameridhishwa na hatua za utekelezaji wa miradi mitatu ya ujenzi wa Ofisi ya Bunge inayotekelezwa na Shirika la Uzalishaji la Jeshi hilo (SUMA JKT).

Mhe. Mwinyi alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea Ofisi ya Bunge kwa ajili ya kukagua miradi hiyo akiwa ameambatana na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Kanali Rajab Mabele.

“Nimeridhishwa hatua ya utekelezaji wa miradi mitatu inayotekelezwa na SUMA JKT ya ujenzi na ukarabati wa Ofisi ya Bunge, naishukuru Ofisi ya Bunge kwa kuliamini shirika la SUMA kwa ajili ya kutelekeza miradi hii,” alisema.

Kwa upande wake Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai  alilipongeza SUMA JKT kwa kuendelea kutelekeza miradi hiyo kwa ufanisi na kwamba hadi sasa miradi yote inaendelea vizuri.

Alitaja miradi hiyo kuwa ni Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Bunge, ukarabati wa Jengo la Ofisi ya Bunge pamoja na ujenzi wa lift na ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Bunge.

Alisema kwa upande wa ukarabati wa Jengo la Ofisi ya Bunge pamoja na ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Bunge tayari SUMA JKT wameshalipwa asilimia 40 na kazi zinaendelea vizuri.

“SUMA JKT ni shirika ambalo tumekuwa tukifanya nalo kazi na tunaridhika na kazi zao tunatamani wapewe miradi mingi ya Serikali,” alisema. 
Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma. Waziri mwinyi ametembelea Ofisi ya Bunge kukagua miradi mitatu 3 ya ujenzi ya inayotekelezwa na Suma JKT. 

Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi wakimsikiliza Mkuu wa SUMA-JKT – Ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Luteni Kanali Zabron Mahenge akitoa maelezo ya hatua ya utekelezaji mradi wa ukarabati wa Ofisi ya Bunge ulipofikia. Nyuma ya Waziri Mwinyi (mwenye miwani ) ni Mkurugenzi Mtendaji SUMA JKT Kanali Rajab Mabere na anayefuata ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerari Martin Busungu .

Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi wakipata maelezo kutoka kwa  Mkuu wa SUMA-JKT – Ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Luteni Kanali Zabron Mahenge wakati viongozi hao walipotembelea eneo linapojengwa lift katika Jengo la Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma . 

Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi wakimsikiliza Mkuu wa SUMA-JKT – Ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Luteni Kanali Zabron Mahenge akitoa maelezo ya hatua ya utekelezaji mradi wa ukarabati wa Ofisi ya Bunge ulipofikia.

UKOSEFU WA UWAJIBIKAJI NA UWAZI CHANZO CHA MIGOGORO AZAKI

$
0
0
Ukosefu wa uwazi na uwajibikaji katika  shughuli za Asasi za Kiraia Tanzania  unaathiri uwezo wa nchi kutambua kiwango cha michango na misaada inayotolewa na wadau wa maendeleo na matokeo yake katika maendeleo ya  nchi.

Hayo yamesema jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu Wa Asasi za KIrai Tanzania katika hotuba aliyoitoa kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kasimu Majaliwa wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Asasi za Kirai Tanzania.  

Dkt. Jingu aliongeza kuwa ukosefu wa uwazi na uwajibikaji wa baadhi ya AZAKI unatoa fursa ya rasilimali za umma ambazo hutolewa kwao kutumika vibaya na hivyo kuathiri kufikiwa kwa matokeo yanayotarajiwa.

Katibu Mkuu huyo aliendelea kusema kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha malalamiko na manung’uniko kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo wafadhili wao na walengwa wa miradi yao.

“Ukosefu wa uwazi umekuwa chanzo cha migogoro miongoni mwa wanachama wa AZAKI husika.  Pia, kukosekana kwa uwazi na uwajibikaji kumesababisha baadhi ya AZAKI kutumika vibaya kinyume na sheria za nchi na kinyume malengo ya kuanzishwa kwao’’. Aliongeza Dkt Jingu.

Pamoja na mapungufu hayo Dkt. Jingu amezisifu Asasi hizo za Kiraia kuwa zinatoa mchango mkubwa katika kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali za umma na kuleta uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa mali za umma.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ,Dkt John Jingu akikata utepe kufungua maonesho ya Wiki ya Asasi za Kiraia Tanzania AZAKI yanayofanyika  jijini Dodoma kwa siku tano kuanzia Oktoba 22-26, 2018.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ,Dkt John Jingu akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Asasi za Kiraia Tanzania AZAKI inayoendelea leo jijini Dodoma Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu Profesa Faustine Kamuzora na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usajili na Uratibu Wa NGOs Bw. Leornard Baraka .
 Kaimu Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali wa  Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ,Bw. Leornad Baraka akijibu hoja za wadau Wiki ya Asasi za Kiraia Tanzania AZAKI yanayofanyika  jijini Dodoma kwa siku tano kuanzia Oktoba 22-26, 2018 kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ,Dkt John Jingu.
 Baadhi ya wadau wa Mkutano wa Asasi za kiraia wakifuatilia kwa makini yanayojili katika Mkutano Mkuu wa Asasi za Kiraia Tanzania AZAKI unaofanyika  jijini Dodoma kwa siku tano kuanzia Oktoba 22-26, 2018. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Ujerumani Yampongeza Rais Magufuli Kupambana na Rushwa

$
0
0
Na Judith Mhina - MAELEZO

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt Detlef Waechter amempongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kufanikiwa kupambana na rushwa nchinI Tanzania na kupata mafanikio makubwa ndani ya kipindi kifupi.

Hayo amesema Balozi Waechter alipofanya mahojiano na Idara ya Habari-MAELEZO mapema jana katika hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro Dar-es-salaam Kempinski katika barabara ya Sokoine Jijini Dar-es –salaam.

Akielezea jinsi rushwa ilivyoota mizizi sehemu nyingi ikiwemo Ujerumani amesema “Tatizo la rushwa sio la Tanzania peke yake, hata kule Ujerumani lipo japo si kwa kiasi kikubwa kila mara Serikali inapaswa kujiangalia na kuhakikisha inapambana na “mfumo wa rushwa mahala popote Ili wananchi wawe na imani na serikali yao.

Kwa dhati kabisa nampongeza Rais Magufuli kwani hali ilikuwa sio nzuri kulingana na ripoti tuliyoisikia wakati wa Mkutano wa 38 wa Bara la Afrika wa Kuthibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya miezi mawili iliyopita. Uwepo wa rushwa Tanzania ilikuwa ni eneo linalotumiwa katika kupitisha dawa za kulevya lakini hivi sasa suala hili limepungua kwa kiasi kikubwa kutokanana juhudi za Rais Magufuli”, alieleza Balozi Waechter.

Akielezea ubaya wa rushwa, Balozi Waechter amesema kuwa matatizo ya rushwa yanarejesha nyuma maendeleo kwa kuwa watu hawapati huduma wanazostahili kwa kuwa tu kuna wengine wanatumia rushwa na kwamba uwepo wa rushwa unaondoa uaminifu kutoka Taifa moja kwenda linguine.

Anasema maeneo ambayo hayana utulivu na amani mara nyingi husababishwa na kushamiri kwa rushwa na kwamba na Serikali ambazo hazisimamii vema huduma kwa wananchi wake.

“Raia kutoka nchi za Afrika wanakwenda Ulaya sio kwa kupenda bali ni kwa sababu wamekosa utulivu na amani katika nchi zao,  kinachopatikana nchini kwao ni kwa ajili ya wajanja wachache wanaoweza kutoa rushwa na kuhodhi utajiri wa nchi badala ya kuhudumia wananchinwote”, ameeleza Balozi Waechter.

Pia Balozi Waechter ameelezea kufurahishwa na Tanzania kuona umuhimu wa viwanda katika kujenga uchumi wa nchi ya Tanzania kwani haiwezekani nchi ikazalisha malighafi halafu itegemee nchi nyingine inunue kwa ajili ya kutengenza bidhaa halafu ziuzwe tena kwa nchi iliyotoa malighafi.

“Nadhani ni uamuzi wa busara kabisa Tanzania imefanya kuelekea katika nchi ya uchumi wa viwanda”, aliongeza.

Ameeleza kuwa nchi zote zilizoendelea kama Ujerumani zimefika zimepata maendeleo baada ya kufanya mageuzi ya hali ya juu katika suala zima la viwanda na tekinolojia. Amesema Ujerumani ipo tayari kushirikiana na Tanzania pale ambapo itahitajika katika kuendeleza juhudi za kufanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda,

Akielezea suala zima la nchi zote mbili kujifunza kutoka kwa mwenzake, Balozi huyo amesema kuwa Ujerumani inajifunza kitu kikubwa sana hapa Tanzania ambacho chimbuko lake ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere suala zima la Amani na Utulivu ambao anasema yeye binafsi hajawahi kuona sehemu yeyote ambayo aliweza kuishi.

Tanzania na Ujerumani zimekuwa na uhusiano mzuri na kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kimaendeleo.

ADA ZA SHULE NA BODABODA KUTOLEWA KWA MARA YA KWANZA KUPITIA MWALIMU COMMERCIAL BANK

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MWALIMU Commercial Bank imefanya droo yake ya kwanza ya kampeni ya "Weka Akiba na Ushinde"  iliyoanza rasmi Septemba 10 mwaka huu na itaendelea mpaka Novemba 30 mwaka huu, na hiyo ikiwa na moja ya mikakati ilinayofanywa na benki hiyo hasa katika kutoa hamasa kwa wateja wao katika kujiwekea akiba.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi Mkuu wa  Mwalimu Commercial Bank (MCB,) Ronald Manongi  amesema kuwa mteja akijiwekea akiba katika akaunti yake kuanzia shilingi 30,000 na kuendelea wakati wote wa kampeni hiyo  basi atapata tiketi moja ya kuingia katika droo inafanyika kila mwezi.

"Mteja anapoweka akiba zaidi hupata nafasi zaidi na kupata tiketi nyingi zaidi na kujiweka katika nafasi ya ushindi zaidi katika droo kubwa na zawadi zitakazotolewa ni pamoja na  ada za shule na bodaboda." ameeleza Manongi.

Aidha Manongi amesema kuwa Mwalimu Commercial Bank imeanzisha akaunti ya tukutane Januari ambayo inamuwezesha mteja kujiwekea akiba kidogo kidogo ili aweze kumudu majukumu ya mwezi Januari, aidha benki hiyo ina akaunti ya nastaafu vipi ambayo huwaanda vijana kwa kuweka akiba  itakayowasaidia baada ya kustaafu na kwa wateja wanaotumia akaunti hizo wataingia kwenye droo na kujiweka katika nafasi ya kushinda ada yenye thamani ya shilingi 500,000 na bodaboda.

Pia amewaasa wananchi kuwa na utamaduni wa  kujiwekea akiba mara kwa mara kwa ajili ya matumizi ya baadae na wao wapo kwa ajili ya kuwasaidia hivyo wasisite kutembelea ofisi zao ili waweze kujipatia huduma hizo.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha biashara na masoko Valence Luteganya amesema kuwa uzinduzi wa kampeni hiyo unalenga katika kutoa bidhaa na huduma zinazolenga maslahi ya watanzania wote.

"Mwaka huu utakuwa mwaka wa neema kwa wateja wetu na tunakaribisha watanzania wote kuja kufungua akaunti ili waweze kujiwekea akiba zao na kujiweka katika nafasi za kujishindia zawadi kemkem" amesema  Luteganya.

Hii ni droo ya kwanza kufanywa na Mwalimu Commercial Bank (MCB) na imelenga kuwanufaisha wateja kwa zawadi zikiwemo bodaboda na ada za shule kupitia kampeni hiyo ya Weka akiba na ushinde na katika droo iliyofanyika leo Tatu Lyimo amejishindia ada ya shule ya shilingi 500,000 na Godian Madinda amejishindia ada ya shule kiasi cha shilingi 500,000 na bodaboda.
Mkurugenzi Mkuu wa Mwalimu Commercial Benki (MCB),Ronald Manongi akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuchezesha droo ya kwanza ya kampeni ya kuweka akiba na kushinda bodaboda na ada za shule, jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkuu wa kitengo cha biashara na masoko,Valence Luteganya.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE DKT. KIKWETE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara alipowasili leo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2018.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2018.  PICHA NA IKULU


Legal Services Facility yashiriki kuadhimisha wiki ya Asasi za Kiraia Dodoma

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt John Jingu ambaye pia ni mgeni rasmi katika ufunguzi wa wiki ya Azaki ya kiraia akipata maelezo juu  kutoka kwa Meneja Biashara na Mawasiliano wa Legal Service Facilty (LSF), Jane Matinde alipotembelea banda la maondesho kuona kazi mbalimbali zinazofanywa na watoa huduma wa msaada wa kisheria chini ya ufadhili wa LSF.
 Meneja Biashara na Mawasiliano wa Legal Service Facilty (LSF), Jane Matinde akimshukuru Raisi wa Foundation for Civil Society, Dr Tenga wakati alipotembele banda la Legal Services Facility (LSF) wakati wa ufunguzi wa wiki ya Azaki Tanzania. akishuhudia, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt John Jingu
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt John Jingu ambaye pia ni mgeni rasmi katika ufunguzi wa wiki ya Azaki ya kiraia akisalimiana na moja ya watoa huduma za msaada wa kisheria (paralegal) wa mkoa wa Dodoma bwana Aggrey Masaga Wakati alipotembelea banda la maondesho kuona kazi mbalimbali zinazofanywa na watoa huduma wa msaada wa kisheria chini ya ufadhili wa LSF. Akishuhudia ni Meneja Biashara na Mawasiliano wa Legal Service Facilty (LSF), Jane Matinde.

WAKAZI WA MUHEZA WAITIKIA WITO KWA KUJENGA VYOO BORA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Muheza Tanga
MSANII wa Muziki wa Kughani , Mrisho Mpoto alimaharufu kama Mjomba amesema kuwa kampeni ya Nyumba ni Choo inayoendelea katika Wilaya ya Muheza imeweza kuja na Matokeo mazuri ya awali kwa wakazi wa eneo hilo kuweka mahadhimio ya kujenga vyoo bora.

Mrisho Mpoto amesema kuwa wakati wanafika katika Wilaya hiyo walijua itakuwa ni ngumu lakini cha ajabu wakati wanatoa somo la kwanza tu wakazi hao wamehazimia kujengwa vyoo kabla ya kukamilika kwa mradi.

"wakazi wa Muheza wamehazimia kujenga vyoo bora kwa kukubali kauli mbiu yetu kuwa nyumba ni choo hivyo kwasasa wanamiminika uwanjani kwa ajili ya kujifunza namna ya kujenga kuta nne za Choo Bora" amesema Mrisho .

Mpoto  amemaliza kwa kuwataka watanzania kuweka kipaumbele katika ujenzi wa vyoo bora ambavyo vitachangia kupunguza magonjwa ya kuambukiza yatokanayo na uchafu kama kuhara na kipindupindu
 Msanii wa Muziki wa Kughani, Mrisho Mpoto akitumbuiz akatika kampeni ya Nyumba ni Choo Katika Wilaya ya Wizara ya Afya Wilaya Muheza mkoani Tanga ambapo watu wameweza kuitikia wito wa kampeni hiyo na kujiwekea mahazimio ya kujenga vyoo bora kabla ya kukamilika kwa kampeni hiyo
 Wakazi wa Wilaya ya Muheza wakifatilia kampeni ya Nyumba ni Choo inayoendeshwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Mjomba Bendi
 Wacheza Sarakakasi wa kundi la Mjomba Theatre  wakionyesha mchezo wa Sarakasi wa kuhamasisha ujenzi wa Vyoo bora kwa kauli ya Nyumba ni Choo kwa wakazi wa Muheza.
Burudani ikiendelea

MKURUGENZI MTENDAJI WA MIGODI YA PANGEA,NORTH MARA, BULYANHULU KIZIMBANI KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
MKURUGENZI mtendaji  migodi wa Pangea, North Mara na Bulyanhulu, ASA Mbulaja Mwaipopo, leo Novemba 23.2018 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka tisa likiwemo la kutakatisha zaidi ya USD milioni Tisa.

Mshtakiwa Mwaipopo ambaye pia ni mhandisi wa madini amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu  Mkazi  Mfawidhi,  Kevin Mhina na Jopo la mawakili watatu waliokuwa wakiongozwa na wakili  wa  serikali  Mkuu,  Faraja  Nchimbi  akisaidiana na Wakili wa serikali Mwandamizi,  Mutalemwa Kishenyi na Jackilline Nyantori. 

Mbali na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo yako manne, Mwaipopo pia anashtakiwa na shtaka moja la kula njama, shtaka moja la kuongoza kutendeka kwa uhalifu, shtaka moja la kughushi, mashtaka mawili ya kukwepa kodi.

Mshtakiwa Mwaipopo anatarajiwa kuunganishwa na washtakiwa wenzake ambao ni Rais wa zamani wa migodi hiyo,  Deogratias Mwanyika na Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo ambao mwisho mwa wiki iliyopita  (Oktoba 17.2018) walisomewa mashtaka 39, yakiwemo hayo Tisa aliyosomewa Mwaipopo leo, yakiwemo pia ya utakatishaji na kukwepa kodi zaidi ya USD milioni 112.

Mbali na Mwanyika, Lugendo na Mwaipopo washtakiwa wengine ni kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu

Akisoma hati ya mashtaka dhidi ya Mwaipopo wakili Nchimbi amedai, washtakiwa hao pamoja na watu wengine ambao bado hawajakamatwa, walitenda makosa hayo kati ya Aprili 11.2008 na June 30.2007 katika sehemu tofauti za jiji la dar es Salaam, Kahama Mkoani Shinyanga, Tarime Mara, Biharamulo Kagera maeneo ambayo yapo katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo katika mji wa Johannesburg, Afrika Kusini, Toronto Canada na nchini  Uingereza.

Imedaiwa katika kipindi hicho na mahali hapo Mwaipopo na wenzake, pamoja na watu wengine ambao bado hawajakamatwa walikula njama ya ya kutenda makosa ya kughushi na ukwepaji wa Kodi.

Pia mshtakiwa anadaiwa kutoa msaada katika kusimamia mkakati wa kihalifu kwa nia ya kupata faida.

 Aidha mshtakiwa Mwaipopo na wenzake,wadaiwa kati ya Mei 16.2008 na Desemba 31,2008 huko Kahama na Biaramulo, walitoa tamko la uongo kwa kamishna Generali wa  TRA kwa nia ya kukwepa kodi kulipa USD 9,309,600 ambayo ilikuwa ni kodi iliyopaswa kulipwa kwa TRA.

Katika shtaka la kughushi washtakiwa hao wakiwa na nia ya ulaghai waligushi mkataba wa mkopo wakitaka kuonyesha kwamba Aprili 30.2014 Kampuni ya Pangea limited ilikubali kukopa USD 90,000,000 ikiwa na riba Kutoka benki ya kimataifa ya barrick huku wakijua kuwa siyo kweli.


 Hata hivyo wa mshtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. Na kesi itatajwa tena ktoba 31, mwaka huu ambao Mshtakiwa Mwaipopo ataunganishwa na wenzake


Mkurugenzi mtendaji  migodi wa Pangea, North Mara na Bulyanhulu, ASA Mbulaja Mwaipopo,leo Novemba 23.2018 akiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashtaka tisa likiwemo la kutakatisha zaidi ya USD milioni Tisa.

BREAKING NEWZZZZZ: NECTA YATANGAZA MATOKEO YA DARASA LA SABA

MAWAKALA WA NMB KANDA 7 WANUFAIKA NA MAFUNZO YA KIBENKI KUBORESHA BIASHARA ZAO

$
0
0
BENKI ya NMB imetoa mafunzo ya kibenki kwa mawakala wake kutoka Kanda saba nchini ili kuboresha huduma kwa wateja na kukuza biashara zao. Mafunzo hayo yaliotolewa kwa mawakala wa NMB, ambao wanasaidia kutoa huduma za kibenki kwa wateja, yametolewa kwenye Kanda 7, ambazo ni pamoja Nachingwea, Newala, Tandahimba, Mbeya, Dodoma, Morogoro, Arusha, Tabora na Mwanza.

Benki ya NMB iliamua kuwajengea uwezo mawakala wake ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja pindi wanapowahudumia. Katika mafunzo hayo, mawakala walipata elimu kutoka kwa wataalam wa masuala ya kibenki pamoja na timu ya mtandao wa kanda husika. Miongoni mwa mafunzo hayo ni pamoja na uelewa juu ya huduma na bidhaa mbalimbali za benki,

Pamoja na hayo, NMB ilitoa motisha na kutambua michango ya mawakala waliofanya vizuri katika kutoa huduma hizo. Baadhi walipata zawadi mbalimbali na vyeti maalum kwa wakala aliyefanya vizuri kwa kila Kanda. Ujuzi huo utaendelea kutolewa kwa maeneo yaliosalia. Benki ya NMB kwa sasa ina zaidi ya mawakala 6000 nchi nzima.
Meneja wa NMB kanda ya ziwa - Abraham Augustino, akizungumza na mawakala wa benki hiyo kwenye kongamano la mawakala lililofanyika Jijini Mwanza jana. NMB inaendesha semina ya mawakala zaidi ya 6,000 ili kuwajengea uwezo na kutambua mchango wao katika kutoa huduma za kibenki nchini. 
Mmoja wa wakala akitunukiwa cheti baada ya kufanya vizuri katika biashara yake. 
NMB inaendesha semina ya mawakala zaidi ya 6,000 ili kuwajengea uwezo na kutambua mchango wao katika kutoa huduma za kibenki nchini. Baadhi ya mawakala wakiwa katika kongamano la mafunzo. 
Wakala wa NMB kutoka wilayani Chato Mkoani Geita - Suleiman Rweikondo, akionesha cheti cha mshindi wa wakala bora namba moja kwa kanda ya ziwa wakati wa kongamano la mawakala liliofanyika jijini Mwanza jana.NMB inaendesha semina ya mawakala zaidi ya 6,000 ili kutambua mchango wao katika kutoa huduma za kibenki nchini. 

MMILIKI WA MABASI YA PRINCES MURO AFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii.
MFANYABIASHARA na mmiliki wa mabasi ya Princes Muro, Majid Abdallah maarufu kama Kimaro (51) leo Oktoba 23.2018  amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la wizi na utakatishaji wa mafuta.

Mwendesha Mashtaka wakili wa serikali, Esther Martin amedai mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde kuwa mshtakiwa ametenda makosa hayo kati ya Januari 2015 na Januari 2018 katika maeneo tofauti ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Katika shtaka la wizi imedaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa aliiba Lita 15950.3 za Mafuta aina ya Diesel na Lita 10925.22 za Mafuta aina ya Petrol mali ya mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Katika shtaka la utakatishaji, imedaiwa, siku hiyo katika sehemu tofauti tofauti za jiji la Dar es Salaam,mshtakiwa alitakatisha Lita hizo za Mafuta  kwa kuyauza  na kuyabadilisha kwa fedha huku akijua kuwa mafuta hayo ni zao la kosa la wizi naa alifanya hivyo kwa lengo la kupoteza uhalisia wa mafuta.

Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo Kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikilizwa kesi za uhujumu uchumi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 5, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.
Mfanyabiashara na mmiliki wa mabasi ya Princes Muro, Majid Abdallah maarufu kama Kimaro (51) akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bara baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili pamoja na shtaka la wizi na utakatishaji wa mafuta.

DKT MAFUMIKO AWAASA WADAU WA KEMIKALI KUSIMAMIA USALAMA WA KEMIKALI

$
0
0
MKEMIA Mkuu wa Serikali, Dkt Fidelice Mafumiko leo amefungua semina ya wadau wa uhifadhi, udhibiti na usimamizi wa kemikali hatarishi hapa nchini.


Akizungumza na wadau hao jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa semina hiyo inatawakumbusha na kuwajenge uwezo wadau wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini katika kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2003.Pia amewaasa kutunza na kusimamia kwa usalama kemikali hatarishi ambazo zinaweza kuleta madhara kwa binadamu na mazingira ndani ya bandari. 

“Nawasihi msikilize kwa makini mafunzo haya ili utakapoanza kwenda kwenye ukaguzi uende kutekeleza matakwa ya Sheria na kanuni zake na sio kwa hiari yako. Kuna vifungu vya sheria ambavyo vinakuhusu kama mkaguzi na utatakiwa kuwajibika pale utakapoenda kinyume chake. Sheria inaainisha wajibu na majukumu ya mkaguzi na pia mkaguliwa, hivyo mnapaswa kuwa makini na kuelewa majukumu na wajibu wenu". amesema Dkt. Mafumiko
Mkemia Mkuu wa Serikali,Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kuufungua semina ya mafunzo ya wa wadau mbalimbali wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na udhibiti wa kemikali, Daniel Ndiyo akizungumza wakati wa kuufungua semina ya mafunzo ya wa wadau mbalimbali wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini.
Baadhi wadau wakiwa katika mafunzo ya wa wadau mbalimbali wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini. 
Mkemia Mkuu wa Serikali, Fidelice Mafumiko akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua semina ya wadau wa uhifadhi usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya jamii.

KAMATI ZA BUNGE ZAFANYA VIKAO JIJINI DODOMA

$
0
0
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo. Wajumbe hao wakiongoozwa na Mwenyekiti Mhe. Naghenjwa Kaboyoka wamekutana na Mwenyekiti wa Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari  (TPA). 
 Viongozi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati Kamati hiyo ilipokutana nao katika kikao kilichofanyika Jijini Dodoma Leo. Wa kwanza ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ndugu Deusdedit Kakoko na Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Profesa Ignas Rubaratuka.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)  Mhe. Abdallah Chikota akizungumza katika kikao cha Kamati  hiyo kililchofanyika Jijini Dodoma leo ambapo walikutana na Halmashauri ya Kilwa.pembeni ni Katibu wa Kamati Ndugu Victor Mhagama.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo. Wajumbe hao wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mhe. Abdallah Chikota wamekutana na Halamshauri ya Wilaya ya Kilwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa Ndugu Renatus Mchau akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakati Halmashauri hiyo ilipokutana na Kamati hiyo katika kikao kilichofanyika leo Jijini Dodoma.

Safari ya kufikisha asali ya Tanzania kimataifa yaiva

$
0
0

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ipo kwenye mazungumzo na Kampuni ya Follow the Honey Tanzania inayojishughulisha na uzalishaji wa asali nchini ili kuchagiza uzalishaji wa asali nchini na kukidhi soko la kimataifa.

Nia hiyo imewekwa wazi wakati wa kikao cha pamoja kati ya uongozi wa kampuni hiyo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB.

Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema kuwa Benki ya Kilimo ipo tayri kushirikiana na wadau mbalimbali wenye lengo la kuwawezesha wafugaji wadogo wadogo wa nyuki ili waweze kufuga kisasa nyuki ili waweze kuongeza tija katika uzalishaji wa asali ili waweze kufikia mahitaji ya soko.

Bw. Justine aliongeza kuwa TADB inatoa mikopo na kusaidia uwekezaji kwa ajili ya uongezaji wa thamani wa ufugaji wa nyuki

“Lengo la benki ni kuwaongezea uwezo wafugaji wadogo wadogo wa nyuki ili waweze kujiongeza kipato,” aliongeza.

Kwa upande Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania, Bw. Kaizirege Camara alisema kuwa kampuni yake imejipanga kusaidia wafugaji wa asali nchini kufikia soko la kimataifa kwa kuwasaidia kuzalisha kisasa asali zao.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine  (wapili kulia) akizungumza na ugeni kutoka na Kampuni ya Follow the Honey Tanzania inayojishughulisha na uzalishaji wa asali nchini kuhusu utayari wa TADB katika kuchagiza uzalishaji wa asali kwa ajili ya kukidhi soko la ndani na nje ya nchi. Wanaomsikiliza ni Mwanzilishi na Afisa Mbunifu Mkuu wa kampuni hiyo, Bibi Mary Canning (kushoto) na Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Kaizirege Camara  (wapili kushoto). Wengine ni Meneja wa Biashara wa TADB, Bw. Dickson Pangamawe (kulia) na Afisa Masoko wa Follow the Honey Tanzania, Bi. Sarah Kibambaza (katikati).
 Mwanzilishi na Afisa Mbunifu Mkuu wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania, Bibi Mary Canning (kushoto) akieleza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine  (kulia). Bibi Canning aliongozana na Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania,  Bw. Kaizirege Camara  (wapili kushoto) na Afisa Masoko wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania, Bi. Sarah Kibambaza (wapili kulia).
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine  (katikati) akifurahi jambo na Mwanzilishi na Afisa Mbunifu Mkuu wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania, Bibi Mary Canning (kulia) wakati wa maongezi yao.
Uongozi wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine  (katikati) mara baada ya mazungumzo yao kuhusu uzalishaji wa asali nchini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KINDA WA KIKAPU JESCA KUELEKEA SENEGAL KWA MAJARIBIO YA NBA ACADEMY

$
0
0
NAODHA wa timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu chini ya Miaka 18 Jesca Ngisaise anatarajia kusafiri kesho alfajiri  kuelekea Senegal kwenye majaribio.

Jesca amekuwa zao zuri la vijana katika mchezo wa kikapu nchini akionekana kufanya vizuri pale anapokuwa anapewa nafasi na kama atafanikiwa kufanya vizuri kwenye majaribio hayo atapata nafasi ya kujiunga na NBA ACADEMY. 

 Kama Jesca atafanikwia kujiunga na NBA Academy atakuwa amepiga hatua moja kubwa sana kuelekea kucheza kwenye WNBA nchini Marekani. 

Jescar mwenye umri wa  miaka 17 na amekua akifanya vizuri katika timu ya Taifa pia aliweza kuchagulia katika timu ya All Stars kwenye mafunzo maalumu ya BWB yaliyofanyika kule Africa kusini mwezi wa nane. Tunamtakia kila la heri aendelee kutuwakilisha vyema. 


Hapa nyumbani Jescar anacheza katika timu ya Ukonga Academy na katika ligi ya mkoa wa Dar es salaam iliyomalizika hivi karibuni alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi hiyo.
Naodha wa timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu chini ya Miaka 18 Jesca Ngisaise.

DIWANI KATA YA MAJI CHUMVI TABATA APONGEZWA KWA JUHUDI ZA KUSIMAMIA MAENDELEO

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii

AFISA Mahusiano Halmashauri Wilaya ya Ilala Tabu Shaibu amepongeza juhudi za Diwani wa kata ya Kisukulu kwa kukarabati miundo mbinu bila ya kusubiri serikali.

Tabu ametoa pongezi hizo baada ya diwani huyo kutekeleza kazi za kurekebisha  baadhi ya barabara ambapo pengine zingesubiri mpaka serikali ifanye marekebisho hayo ila ameweza kukusanya vijana na kutengeneza barabara hiyo.Barabara hiyo imekuwa ni njia kubwa ya watu kutoka maeneo ya Gongo la mboto,Bonyokwa,Tabata pamoja na Ubungo.

Tabu  ameeleza kuwa serikali inaendelea na utaratibu ambao ulishapangwa kwa kila sehemu korofi za barabara kurekebishwa kwa awamu na mpaka sasa kuna greda mbili ambapo moja liko Kwenye ukarabati na hivyo kwa barabara hiyo kuendelea kusubiri kwa muda.Amewaomba wananchi waendelee kushirikiana kikamilifu na diwani huyo katika kuboresha maendeleo ya kata hiyo kwani biashara zinazofanywa na wakazi nyingne huhitaji Miundombinu ambayo itawezesha biashara kuwafikia wateja kwa haraka zaidi muhimili mkuu ukiwa ni Barabara.


Diwani wa Kata ya Maji Chumvi Tabata,  Joseph Sayenda ameshirikiana na Wananchi wa kata hiyo katika kuboresha Miundombinu ya awali ya barabara ambayo kwa miaka mingi imekua tatizo kwa Wakazi hao.
Sayenda amesema wananchi wa kata ya maji chumvi waliiona adha hiyo kwa muda mrefu na kuona fursa ya kushirikiana kukarabati barabara hiyo huku wakiendelea kusubiri serikali kutatua tatizo hilo.

Amefafanua kuwa Katika kuunga mkono rai ya serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli Katika kuendeleza Tanzania ya viwanda nchini ambapo katika barabara Hiyo kuna kiwanda cha mashine ya kusaga nafaka ambapo wakazi hutumia kwa ajili ya shughuli za kila siku.

Wananchi wa kata ya  Maji Chumvi Tabata wakifanya ukaraati wa barabara inayounganisha maeneo ya Gongo la mboto,Bonyokwa,Tabata pamoja na Ubungo.

DCP LIBERATUS SABAS AZUNGUMZA NA WANAVIJIJI MKOA WA MTWARA, AKAGUA VIPENYO WANAVYOTUMIA WAHALIFU KUKIMBILIA NCHINI MSUMBIJI.

$
0
0
 Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas akitoa Elimu kwa wanakijiji wa Chikong’o, Wilayani Tandahimba, Mkoa wa Mtwara juu ya kukabiliana na wageni wanaoingia maeneo hayo wakitokea sehemu mbalimbali za Nchi na Nchi jirani ya Msumbiji hiyo itasaidia kupunguza uhalifu katika maeneo na makazi yao.
 Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas akitoa Elimu kwa wanakijiji cha Mkaha Wilaya ya Tandahimba Mkoa wa Mtwara, juu ya kukabiliana na wageni wanaoingia maeneo hayo wakitokea sehemu mbalimbali za Nchi na Nchi jirani ya Msumbiji hiyo itasaidia kupunguza uhalifu katika maeneo na makazi wanayoishi.
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas akiwa katika kijiji cha Chikong’o wilayani Tandahimba mkoani Mtwara akikagua moja ya vipenyo wanavyotumia wahalifu kuvuka kutoka nchini Tanzania kwenda Nchini Msumbiji moja ya vipenyo hivyo ni Mto Ruvuma. (Picha na Jeshi la Polisi)
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images