Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

VIJANA WAASWA KUEPUKA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO YA KIJAMII

0
0
Na Woinde Shizza,Arusha.

Vijana nchini wametakiwa kuepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ambayo imekua ikitumika kufanya uhalifu wa kimtandao pamoja na kuchangia kuporomoka kwa maadili ya vijana wanaoiga tamaduni za nchi za nje zisizofaa.

Akizungumza katika Kongamano la Maadili liliofanyika Wilaya ya Karatu ,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Arusha Dk. John Pallangyo amesema kuwa vijana wanapaswa kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao pamoja na kuhakikisha kuwa wanalinda maadili ya Tanzania na kuchangia maendeleo kwenye jamii na taifa.

Dk.John alisema kuwa vijana wanatakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa na kujiongezea maarifa sahihi pamoja na kukuza kipato badala ya kutumia katika mambo yasiyofaa.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Karatu Peter Mmasy amesema kuwa jumuiya hiyo ina jukumu la kusimamia malezi,maadili ya jamii na kuwataka Wazazi kutimiza wajibu wao kwa kuwalea vyema vijana.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa mkoa wa Arusha kupitia CCM, Cylius Daniel Mlekwa amesema kuwa licha ya kusisitiza maadili pia vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita rushwa ili kuwa na jamii bora.

Cylius alisema kuwa vijana nchini waunge mkono juhudi za kupambana na rushwa katika kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinalindwa kama anavyofanya Raisi John Magufuli.

Kwa Upande wake Kijana aliyeshiriki katika Kongamano hilo Elitumaini Rweyemamu amesema maadili na nidhamu ni nguzo ya mafanikio kwa vijana hivyo vijana hawana budi kusimamia vyema maadili ya kitanzania ambayo yamegubikwa na utandawazi.

Visit of Ambassador of Finland to the African Court in Arusha today

0
0
Ambassador of Finland to Tanzania Pekka Hukka (centre) today, Tuesday, 23 October 2018, visited the African Court in Arusha to familiarise with its activities. In the picture, Head of the African Court’s Library Dr Fidelis Katonga(r) briefs the Ambassador. Left is Head of African Court’s Legal Division Grace Wakio (Picture by a Correspondent).

UMOJA WA MATAIFA KUADHIMISHA MIAKA 73 TOKEA KUANZISHWA

0
0
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza na Waandishi jana katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere ikiwa ni matayarisho ya kusherehekea miaka 73 ya Siku ya Umoja wa Mataifa ambapo tarehe 24 Oktoba husherehekewa Duniani kote na kwa Tanzania yataadhimishwa jijini Dar es Salaam na Zanzibar, kushoto ni Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na kulia Bw. Deusdedit B. Kaganda Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa. 
Bw. Deusdedit B. Kaganda Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano  wa Kimataifa kulia akimkaribisha Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kushoto kuzungumza na waandishi wa habari katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Mkutano huo ulifanyika kufuatia tarehe 24 Oktoba, Umoja wa Mataifa utaadhimisha Miaka 73 ya tokea kuanzishwa kwake. Katikati Mhe. Dkt. Damas Ndumaro (Mb) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Bw. Alvaro Rodriguez, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania aliyekaa kushoto alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere akilelezea juu ya maendeleo ya Umoja huo na kaulimbiu ya mwaka huu katika kuadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa tarehe 24 Oktoba iliyobeba ujumbe wa "Uwezeshaji Vijana na Ubunifu kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu" 
Baadhi wa waandishi wa Habari walioshiriki katika mkutano wa Waandishi wa Habari katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

WACHIMBAJI WA MADINI WAPEWA ELIMU KUHUSU TAHADHARI YA MIONZI.

0
0
Na Vero Ignatus Arusha.

Zaidi ya wataalamu 20 kutoka katika kampuni mbalimbali za uchimbaji madini nchini wanatarajiwa kuwa mabalozi chanya katika kutoa elimu kuhusu tahadhari na matumizi sahihi ya mionzi kwa wachimbaji pamoja na jamii.

Akizungumza na wataalamu hao mkurugenzi wa tume ya nguvu za mionzi (Atomic) Profesa Lazaro Busagala nchini amesema niwakati muafaka kwa jamii kuwa na elimu,uelewa kuhusu mionzi hususani katika maeneo ya migodi na jamii inayo pakana na migodi ya uchimbaji madini.

Denis Mwalongo ni muwezeshaji wa mafunzo maalumu kwa wataalamu hao amesema kuwa katika migodi mingi nchini wafanyakazi wamekuwa wakiathirika zaidi kwa kufanya kazi zao bila vifaa vya kujikinga kiafya.

Amesisitiza kuwa endapo mionzi ikiingia Zaidi mwilini kwa muda mrefu mtu anaweza kupoteza maisha kwa kuugua hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari kabla ya madhara kutokea katika maeneo ya kazi na jamii inayozunguka migodi ya uchimbaji madini.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema matarajio yao baada ya kupata elimu zaidi juu ya matumizi na tahadhari kwa wafanyakazi na jamii kwa ujumla,ambapo wamesisitiza kuwa watakuwa mabalozi katika kutoa elimu hiyo ilikuokoa maisha ya wananchi na wafanyakazi wengine.

Mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo zaidi wataalamu hao pamoja nakuinusuru jamiii nayo inayopakana na maeneo ya migodi ilikuokoa vizazi vya sasa na vijavyo.

Proff Lazaro Busagala Mkurugenzi Tume ya nguvu za atomic Tanzania akizungumza na washiriki wa mafunzo.Picha na Vero Ignatus 
Denis Mwalongo muwezeshaji wa mafunzo maalumu kwa wataalamu. 
Washiriki wa kiwa katika Mafunzo

TANGAZO LA KUHAMISHA MAKABURI KWA MIKOA YA PWANI NA MOROGORO ILI KUPISHA UJENZI WA RELI YA KISASA

TTCL INAKULETEA MKOA 2 MKOA NDANI YA RUVUMA

Maandalizi ya Rock City Marathon yakamilika.

0
0

Maandalizi ya mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Octoba 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza yamekamilika huku zaidi ya washiriki elfu tano (5,000) kutoka ndani na nje ya nchi wakitarajiwa kushiriki katika mbio hizo.

Tayari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt Philis Misheck Nyimbi wamekwisha thibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo ambazo pia zitahusisha ushiriki wa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali, wabunge na washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Mwanza jana, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi alisema kamati yake imejiandaa kupokea washiriki zaidi ya 5,000 wa mbio hizo kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wakimbiaji wa kimataifa.

“Tunatarajia kuwa na mbio zenye mafanikio makubwa mwaka huu. Maandalizi kwa kiasi kikubwa yamekwisha kamilika na kinaochoendelea kwa sasa ni usajili wa washiriki kutoka ndani na nje ya nchi na tunatarajia kufunga zoezi hilo siku ya Jumamosi Oktoba 27,’’ alibainisha.

Akizungumzia kuhusu zawadi, Ngowi alisema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh.mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi kumi nao pia wakiibuka na medali na pesa taslimu.

Kwa upande wa mbio za Kilomita 21, Ngowi alisema, pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 3/- kila mmoja, sh. Mil 1/- kwa washindi wa pili na sh. 750,000/- kwa washindi wa tatu huku pia washindi wanne hadi wa kumi wakiibuka na zawadi za pesa taslimu na medali kila mmoja.

Mwanariadha Alphonce Simbu akionyesha tabasamu baada ya kukabidhiwa fedha taslimu ikiwa ni zawadi baada ya kuibuka mshindi kwanza katika mbio za km 21 katika mashindano ya Rock City Marathon mwaka 2013.

PROFESA MBARAWA AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI MBINGA

0
0

WAZIRI wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amezindua mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma ya maji mjini Mbinga akiwa katika ziara yake kikazi mkoani Ruvuma.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Profesa Mbarawa amesema mradi huo ni hatua ya Serikali kufikia lengo la kufikia asilimia 90 kwa miji mikuu ya wilaya itakapofika mwaka 2020, na imepanga kutumia Silingi Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji kwa miji mingine 25 Tanzania Bara na Visiwani.


Amesema mradi huo utabadilisha kwa kiasi kikubwa maisha ya wananchi wa Mbinga sio tu kwa kutoa huduma ya majisafi na majitaka kwa wananchi.  Pia, ni muhimu kwa shughuli za kila siku za kiuchumi zinazofanyika katika mji huo.


Vilevile, Profesa Mbarawa ameipongeza Mamlaka ya Maji ya Songea Mjini (SOUWASA) kwa kazi nzuri ya kusimamia mradi huo mpaka umekamilika.

Mradi huu upo chini ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya mji wa Mbinga (MBIUWASA) ulianza kujengwa Mei, 2017 chini ya mkandarasi Almasi General Supplies Ltd ya Songea na kuanza kutoa huduma ya maji kwa mji wa Mbinga Februari, 2018 umegharimu   Shilingi Bilioni 1.029.


Naye Meneja wa MBIUWASA, Patrick Ndunguru amesema kukamilika kwa mradi kumeleta ongezeko la uzalishaji wa maji kutoa wastani wa lita 700,000 wakati wa kiangazi na lita 1,600,000 wakati wa masika, ikichangia kuongeza mapato kutoka Shilingi Milioni 18 hadi Milioni 25 kwa mamlaka hiyo.


Wizara ya Maji kwa kutumia Kampuni ya Don Consult ilisanifu mradi huu kwa lengo la kumaliza tatizo la maji katika mji wa Mbinga, pamoja na mfumo wa uondoaji salama wa majitaka.
  Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa  akizindua mradi mkubwa wa maji wa uboreshaji wa huduma ya maji mjini Mbinga uliogharimu Sh. Bilioni 1.029 akiwa na DC Mbinga, Cosmas Nshenye.
  Sehemu ya mradi wa maji wa uboreshaji wa huduma ya maji mjini Mbinga.
 Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akifungua maji katika mradi wa maji Kagugu, wilayani Mbinga katika mkoa wa Ruvuma kuashiria kukamilika kwake.
  Sehemu ya watu waliohudhuria hafla ya kusheherekea kukamilika kwa mradi wa maji wa Kagugu, wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma.

AMANI NA UTULIVU ULIOJENGWA NA NYERERE NI FUNZO KWETU UJERUMANI - BALOZI DKT DETLEF WAECHTER

0
0
Na Judith Mhina-MAELEZO
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt Detlef Waechter, amesema hajawahi kuona amani anayoiona hapa Tanzania.

Amesema maneno hayo wakati wa mahojiano maalum na Idara ya Habari MAELEZO mapema wiki hii katika Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro Dar-es-salaam Kempinski katika barabara ya Sokoine Jijini Dar-es –salaam.

Mheshimiwa Balozi Waechter amesema “Hayati, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni kiongozi ambaye hatasahaulika kwa kuwa amani aliyojenga Tanzania ni ya pekee haipatikani mahali popote duniani”. 

Kwa kutambua hilo Balozi amesema kuwa Ujerumani imeona umuhimu wa Baba wa Taifa la Tanzania kama mfano wa kuigwa duniani kwa kujenga amani na usalama wa binadamu. Ambapo watu wa dini tofauti, makabila tofauti na asili tofauti wanakaa pamoja na kushirikiana kujenga nchi. Huu ni urithi na funzo kubwa kwetu ambapo Julius Nyerere ametuachia.

Kutokana na amani na usalama wa binadamu alioujenga, Serikali ya Shirikisho ya Ujerumani imejifunza jambo kubwa sana kutoka kwa Mwalimu Nyerere na kuona ni busara kufadhili jengo la Makao Makuu la Umoja wa Afrika pale Adiss Ababa Ethiopia. Linaloitwa The Julius Nyerere Peace and Security Building.

“Jengo lile ni kielelezo tosha kuwa vizazi na vizazi vitakavyofika pale Addiss Ababa Ethiopia watatambua uwepo wa Mwalimu Nyerere duniani na pia, anakumbukwa kwa Amani na Utulivu alioujenga akiwa hapa duniani na kamwe hatasahaulika” Amesisitiza Balozi Waechter.

Balozi Waechter amesema kuwa kwa muda nilioishi hapa Tanzania, tangu 2016 ninashangazwa kuambiwa watanzania ambao walio wengi ni Wakristu na Waislamu wanaoishi pamoja na kushirikiana kwa upendo na mambo yanaendelea kama kawaida. 

Ameongeza kwa kusema kuwa, Watanzania walio wengi hawajui hili la kuwaweka watu wenye asili tofauti, dini tofauti mahala pamoja ni vigumu sana na haliwezekani katika nchi nyingine. Nimeambiwa hapa Tanzania watu wanaoishi mchanganyiko wa makabila tofauti, dini tofauti na Itikadi tofauti kwa kweli alichokifanya Nyerere kitabakia kama kumbukumbu ya dunia na ni lazima dunia iige mfano huu.

Balozi Waechter amesema kuwa imani za dini hapa duniani zinaleta mgongano mkubwa katika jamii nyingi. Huwezi kuwaweka wakaishi katika eneo moja na ni lazima kila mara kuwa na tahadhari ili kuepuka mgongano wa aina yeyote ile.

Mara nyingi pale Ujerumani tumekuwa tukishuhudia migongano ya mara kwa mara kwa Wakimbizi walioingia Ujerumani kutokana na tofauti za kimazingira walikotoka na imani zao za dini. Hii ni changamoto kwetu, lakini nina hakika sisi Ujerumani tutajifunza mengi hapa Tanzania kutokana na amani na utulivu mlionao.

Lakini kwa Baba wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Nyerere kwake sio shida kabisa amekaa na Wakimbizi bila shida Taifa lina watu wa imani tofauti kweli sio tatizo wanashirikiana na kutekeleza mambo ya taifa na ya kila siku kwa pamoja kama vile ni watu wa kundi moja hakika hii ni ajabu. Ameshangaa Balozi Waechter

Ujerumani inamtambua Mwalimu Julius Nyerere kuwa ni kiongozi muhimu sana katika Bara la Afrika, pamoja na Rais wa kwanza wa Weusi waliowengi Afrika ya Kusini Hayati Rais Nelson Mandela. Hii imepelekea serikali ya Ujerumani kuona umuhimu wa Amani na Usalama na kufadhili kwa kutoa fedha za walipa kodi wa Ujerumani ambao wamefanikisha ujenzi wa Makao Makuu ya Umoja wa Afrika. 

Nyerere ni Baba wa Amani na Usalama Barani Afrika na dunia kwa ujumla, kwa kulitambua hilo Ujerumani imeona iko haja ya kuunga mkono juhudi za Umoja wa Afrika ya kuhakikisha Afrika inakuwa na Amani na Usalama, ili kuweza kuwaweka raia wake ndani ya Bara husika badala ya kukimbilia Ulaya ambapo wanatumia njia ambazo sio salama kwa uhai wa binadamu.

Pia, serikali ya Shirikisho la Ujerumani umejitahidi kufanya jitihada ya kutembelea nchi za Afrika Magharibi ambazo zinaweza kusaidia kupunguza wimbi la Wakimbizi kwenda Ulaya kwa kujaribu kushirikiana nao ili wajenge uchumi Imara. Tunafahamu sio kwamba Wakimbizi hawapendi kukaa kwao ila hali halisi ya amani na usalama inapokosekana, rushwa inaposhamiri hivyo kubaki katika nchi zao ni kuhatarisha maisha yao. 

Wito wangu kwa Watanzania wasisahau mambo muhimu ambayo Nyerere amewaaasa kuhusu Amani na Usalama. Nchi nyingi zinatamani mlichonacho Tanzania lakini najua kazi aliyoifanya Mwalimu Nyerere haikuwa ndogo ni kubwa na kama kweli mnamheshimu, itunzeni Amani yenu na Utulivu ili mumuenzi kwa vitendo. Amesisitiza Balozi Waechter.

Sisi Ujerumani hatuchoki kusema ukweli kuhusu Amani na Utulivu wa Tanzania tunawaasa mataifa mengine kwa kuwaambia kuwa waangalie mfano wa Tanzania ni nchi ambayo imetambua Amani na Utulivu utaleta mambo mengine yote. Nadhani hakuna faida ya kuwa na maendeleo ambayo watu wako hayawafaidishi kutokana na kukosa amani. Sasa unatafuta maendeleo kwa ajili ya nani? Aliuliza Balozi Waechter.

Eneo hili la Amani na Utulivu mnaweza kulitangaza sana na kuwaambia watu mbalimbali duniani waje waone mfano kwa kutembelea maeneo mnayoishi kuangalia nyumba zenu za ibada unakuta msikiti, makanisa ndani ya jamii na kila mmoja anaabudu kwa muda wake, angalia mikusanyiko ya sherehe za kijamii hazibagui na Mtanzania yupo huru kuishi mahala popote ndani ya nchi yenu.

Hivyo Watanzania msikate tamaa katika suala zima la uchumi kwa kuwa mmepata uongozi wenye nia ya kulipelekea Taifa lenu mahali pazuri tumieni fursa mliyoipata kujenga nchi yenu kwa manufaa ya Taifa lenu na dunia kwa ujumla.

Balozi Waechter, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa ushirikiano mzuri unaoendelea kati ya Tanzania na Ujerumani na ameahidi kutumia ushirikiano huo kwa manufaa ya nchi zote mbili.

MAKAMU WA RAIS KUANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI PWANI

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan.

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi  Mkoani Pwani  leo oktoba 24 ambapo atatembelea miradi mikubwa ya kitaifa ikiwemo ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo.

Hayo yamesemwa mjini Kibaha na Mkuu wa Mkoa  wa Pwani,  Mhandisi Evarist Ndikilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari .

Ndikilo amesema ,makamu wa Rais akiwa mkoani humo  atakagua miradi  mbalimbali   ya maendeleo katika Wilaya  nne za mkoa huo na ataanzia ziara kwa kukagua miradi ya maendeleo ya Wilayani Bagamoyo.

"Miradi hiyo ni pamoja na kutembelea   mradi mkubwa wa  Bandari mpya ya Mbegani wilayani Bagamoyo  yenye ubia  na nchi tatu za Tanzania,Oman na China," alisema Ndikilo.

Amesema kuwa baada  ya kukagua miradi wilayani Bagamoyo atakwenda  Halmashauri ya wilaya ya Chalinze  ambako atakagua miradi ya maendeleo.

 "Baada ya hapo atakwenda , Wilaya ya Kisarawe, Mkuranga na atahitimisha ziara hiyo wilaya ya Kibaha"

Aidha mradi mwingine wa kitaifa ni atakaotembelea ni ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge (SGR) kwenye karakana kubwa iliyoko Soga wilayani Kibaha.

"Mbali ya kutembelea miradi hiyo mikubwa pia atatembelea miradi mingine ikiwemo ya miradi ya  afya,  maji na elimu,"alisema Ndikilo.

Ndikilo alisema kuwa akiwa wilayani Kibaha Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonyesho ya wiki ya viwanda itakayozinduliwa Oktoba 29 katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo  katika eneo la Picha ya Ndege.

Makamu wa Rais atakapoanza ziara hiyo  atapokea taarifa kutoka  Halmashauri zote  za mkoa huo pia atapata nafasi ya kuzungumza na  Wakurugenzi wa Halmashauri hizo.

WATALAAM WA MAJI ENDESHENI VIKAO KAZI KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIRADI-AWESO

0
0
Watalaam wa maji nchini wametakiwa kuendesha vikao kazi mara kwa mara ili kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama kwa wakati, pia wahandisi wa maji wa mikoa kuhakikisha wanapitia miradi ya maji kabla ya utekelezaji wake. 

 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema hayo wilayani Hanang’ wakati akikagua miradi ya maji na kusisitiza watalaam wa maji kukutana katika vikao ni fursa ya kubadilisha uzoefu katika usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maji, pia kujifunza zaidi ili kuleta ufanisi katika kazi.
Mhe. Aweso amesema haiwezekani mtaalam wa maji anakaa ofisini na kupokea ripoti za mradi bila kujiridhisha kwa kutembelea mradi, na kuwashirikisha watalaam wenzake anapoona baadhi ya maeneo kazi haiendi kama inavyotakiwa.  

Mhe. Aweso katika ziara hiyo ameweka jiwe la msingi la mradi wa maji Katesh ambao ukikamilika utakua na uwezo wa kuhudumia zaidi ya wakazi 40,000, na utakua na uwezo wa kutoa huduma kwa zaidi ya miaka 20. 

Mhe. Aweso wakati wa hafla hiyo amewaelekeza watalaam wote wa mabonde ya maji nchini kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa kwa kuwashirikisha wananchi ili kuhakikisha rasilimalimaji inatumika kwa matumizi endelevu kwa maendeleo ya wananchi wote.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na; mradi wa maji Lambo, mradi wa maji Endasaboghechan, mradi wa maji Endagaw, mradi wa maji Waranga na mradi wa maji Gehandu.

 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb), watatu kutoka kushoto, akikata utepe tayari kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa  Katesh utakaohudumia zaidi ya wakazi 40,000 na kutarajiwa kuhudumia wakazi wa Katesh  kwa zaidi ya miaka 20.
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Katesh. Anayeshuhuda ni mkuu wa wilaya ya Hanang’ Mhe. Joseph Mkirikiti 
 Naibu Waziri wa Maji akisikiliza maelezo ya mradi wa maji wa Endasaboghechan ulifanikishwa kwa ushirikiano na Kampuni ya Bia ya Serengeti. Mradi huo unatumia nishati ya jua.
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb)  akiongea na wakazi wanaotarajia kunufaika na mradi wa maji wa Endagaw-Gedangu ambapo Mhe Aweso amewahakikishia wananchi kuwa Mkandarasi wa mradi atalipwa kiasi cha shilingi milioni 184 akamilishe mradi na huduma ya maji ipatikane mara moja.
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akisaidia kuchota maji katika eneo la Waranga. Hata hivyo, Mradi wa maji wa Waranga unatarajia kukamilika siku za usoni hivyo kuondoa adha ya wananchi kuchota maji katika mashimo.

KUSOMA ZAIDO BOFYA HAPA

THE DESK &CHAIR YATOA VIFAA TIBA VYA WALEMAVU WA MACHO

0
0
Na Baltazar Mashaka, Mwanza.

SERIKALI mkoani Mwanza imepokea msaada wa vifaa tiba na upasuaji kwa walemavu wa macho vilivyotolewa na The Desk & Chair Foundation (TD & CF) Tawi la Tanzania.

Vifaa hivyo vitakavyotumika kwenye kambi ya upasuaji wa mtoto wa jicho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Fimbo Nyeupe yanayofanyika kitaifa jijini humu, vilipokelewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk. Philis Nyimbi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.

Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa The Desk & Cir Foundation Sibtain Meghjee alisema wanaunga mkono juhudi za serikali za kuhudumia jamii kwa kuwa taasisi hiyo inatambua watu wenye ulemavu wana changamoto nyingi zikiwemo kushindwa  kumudu gharama za matibabu.

“Taasisi hii inafanya shughuli za kusaidia jamii (walemavu,wagonjwa na masuala ya elimu),kulingana na mahitaji.Kwa changamoto za walemavu wa macho ni kushindwa kumudu gharama za tiba sababu ya ugumu wa kipato hivyo serikali iangalie jinsi ya kuwasidia wapate Bima ya Afya,”alisema Meghjee.

Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo Mongela alisema maadhimisho ya ya Fimbo Nyeupe ni kielelezo kuwa walemavu wana mchango mkubwa na ndiyo maana TEHAMA inawaelekeza kwenye Uchumi wa Viwanda kama ilivyo kauli mbiu.

Alisema vifaa hivyo vitahudumia wilaya saba za Mkoa wa Mwanza  na hivyo serikali imejipanga wananchi watakaojitokeza hawatakosa huduma kwenye maadhimisho hayo na kambi ya uchunguzi wa macho, watakaobainika watatibiwa kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou Toure.
 Mwenyekiti wa The Desk Chair Foundation Sibatain Meghjee akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba vya macho na upasuaji kwa serikali ya Mkoa wa Mwanza. Kushoto wa kwanza ni Katibu Tawala Msaidizi Seif Rashid, wa pili ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagan Dk. Philis Nyimbi.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Silas Wambura akizungumza kuhusu ubora wa vifaa hivyo kabla ya kukabidhiwa.
  Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk. Philis Nyimbi,akipokea vifaa tiba na upasuaji pamoja na fimbo nyeupe kutoka kwa Mwenyekiti wa Desk & Chair Foundation Sibtain Meghjee (kulia) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela.
 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk. Philis Nyimbi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akizungumza baada ya kupokea msaada wa fimbo nyeupe, vifaa tiba vya macho na upasuaji vilivyotolewa an The Desk & Chair Foundation.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MTAWALA WA RAS AL KHAIMA SHAIKH SAUD BIN SAQR AL QASIMI AONDOKA ZANZIABR NA KUREJEA MYUMBANI

0
0
 Mtawala wa Ras al khaima Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi akipeana mikono na Viongozi mbalimbali alipokua  akiondoka Zanzibar na kurejea nyumbani.
 Mtawala wa Ras al khaima Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi akipita katika zulia kuelekea kwenye ndege tayari kwa kuiondoka Zanzibar na Kurejea nyumbani.
 Mtawala wa Ras al khaima Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi(Gavu)alipokua akiondoka Zanzibar na kurejea nyumbani.
Mtawala wa Ras al khaima Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi akipunga mkono ikiwa ni ishara ya kuaga wakati akipanda ndege na kuondoka Zanzibar na kurejea nyumbani.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

MMILIKI NA MWANZILISHI WA TIMU YA TUKUYU STARS (BANYAMBALA),RAMNECK PATEL (KAKA) KUZIKWA LEO

0
0
Mwili wa aliyekuwa Mmiliki na Mwanzilishi wa Timu ya Tukuyu Stars (Banyambala) Ramneck Patel(Kaka) aliyefariki octobar 18 nyumbani kwake alipokuwa akiendelea na matibabu baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospital ya Kanda ya Rufaa ya Mbeya alikokuwa akipatiwa matibabu, umewasili nyumbani kwake majira ya saa 4 asubuhi kwa ajili ya taratibu za mazishi.

 Taarifa za ndugu wa marehemu kuhusu taratibu za mazishi zinasema, Mwili wa marehemu Baada ya kufanyiwa Ibada Nyumbani kwake leo Oktoba 24,2018, utapelekwa viwanja vya Sokoine -kwa wananchi ndugu jamaa na kuaga na baadaye kusindikizwa katika nyumba yake ya milele Makaburi ya sabasaba jijini Mbeya, ambapo kwa mujibu wa dhehebu la Baniani mwili huo utachomwa kama sehemu ya taratibu za mazishi. 

 Klabu hiyo ilianzishwa mwaka 1980 na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu wakati huo ikiitwa daraja la kwanza bara mwaka 1985 -86 na baada ya mwaka mmoja ikashuka daraja. 
 Mwili wa aliyekuwa Mmiliki na Mwanzilishi wa Timu ya Tukuyu Stars (Banyambala) Ramneck Patel(Kaka) ukiandaliwa mapema leo nyumbani kwake kwa ajili ya sala na baadae   kwa ajili ya taratibu za mazishi.
 Gari iliyobeba mwili wa aliyekuwa Mmiliki na Mwanzilishi wa Timu ya Tukuyu Stars (Banyambala) Ramneck Patel(Kaka) ukiwasili yumbani kwake kwa ajili ya sala na baadae   kwa taratibu za mazishi.
 Kikosi cha Timu ya Tukuyu Stars wakati huo alipokuwa akiisimamia,na yeye akiwemo pichani kulia enzi za uhai wake.
 Mwili wa aliyekuwa Mmiliki na Mwanzilishi wa Timu ya Tukuyu Stars (Banyambala) Ramneck Patel(Kaka) enzi za uhai wake.

RC Wangabo aagiza kushughulikia udumavu kuongeza ufaulu

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaagiza wakurugenzi kushirikiana na madiwani kuhakikisha suala la kupunguza udumavu katika mkoa wa Rukwa linakuwa ni ajenda ya kudumu katika vikao vya mabaraza ya madiwani pamoja na mikutano ya hadhara katika kuwaeleimisha wananchi juu ya athari ya udumavu.

Amesema kuwa suala la udumavu lisisahaulike pindi tunapoangalia ufaulu wa watoto wetu mashuleni, na kuwa mstari wa mbele kutoa ahadi za kuhakikisha watoto wanaongeza ufaulu huku udumavu ukiwa bado haujashughulikiwa.

“Tuone kwamba kama huna hali mbaya ya matokeo ya kielimu yanachangiwa pia na udumavu kwasababu udumavu umekuwa wa muda mrefu na kama tunaukubali upo, sasa kwanini usikubaliane pia na matokeo yanayotokea, tuweke jitihada kubwa sana kuondoa udumavu ili watoto wetu waongeze ufaulu,” Alisisitiza.

Ameongeza kuwa kama si hivyo basi itabidi takwimu udumavu ziangaliwe upya, ama kama kwenye elimu kuna kupasi sana basi kuna wizi wa mitihani ama kuna wageni wengi sana wanaotoka nje kuja kusoma Kwetu.

Mwanzoni mwa mweze wa nane Mh. Wangabo aliingia mkataba wa utendaji kazi na kusimamia shughuli za lishe baina ya Ofisi yake pamoja na wakuu wa wilaya ambapo ni utekelezaji wa maagizo ya Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mikoa juu ya kupunguza utapiamlo ambao kitaifa ni asilimia 34.

Kwa upande wake mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu alisema kuwa utapiamlo unasababisha udumavu wa akili na mwili na ubongo wa mtoto unaendelea kukua tangu ujauzito mpaka anapofikisha miaka mitano.

“Wananchi wengi hawana uelewa wa kutosha juu ya masuala ya lishe bora na athari za utapiamlo.  Pamoja na kuwa Mkoa unazalisha vyakula vya aina mbalimbali tena kwa wingi, lakini wananchi wengi bado wanatumia aina moja au aina za vyakula vilivyozoeleka kwa muda mrefu bila kuchanganya na aina nyingine za vyakula ili kufikia mahitaji halisi ya virutubishi.” Alisema.

Mkoa wa Rukwa una kiwango cha utapiamlo cha asilimia 56.3 wakati kitaifa ni asilimia nne, na kitaifa mkoa wa rukwa umeshika nafasi ya 19 mwak huu tofauti na mwaka jana ulikuwa wa 15 kitaifa katika matokeo ya darasa la saba. 

MAHAKIMU MBULU, WAKUMBUSHWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIKAMILIFU

0
0
Na Catherine Francis, Mahakama Kuu - Arusha

Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu- Kanda ya Arusha, Mhe. Mosses Mzuna, amewakumbusha Mahakimu kutekeleza wajibu wao ipasavyo ili kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mwananchi na kwa wakati.

Akiwa ziarani Mahakama ya Wilaya Mbulu, Mhe. Jaji Mzuna aliwakumbusha Mahakimu wilayani humo kuwa wanapaswa kutoa adhabu kwa kuzingatia ukubwa wa kosa lenyewe na si kwa kuhamasishwa na hisia juu ya kesi husika. “Wajibu wa kila Hakimu ni kuhakikisha haki inatendeka na kupitia mwenendo wa shauri na maamuzi yaliyotolewa kabla hawajaruhusu jalada kwenda kwenye ngazi nyingine za Mahakama,” alisistiza Mhe. Mzuna.

Aidha; Mhe. Jaji Mfawidhi alisisitiza juu ya umuhimu wa taarifa za mashauri kufikia wadaawa kwa wakati unaostahili ambapo mwenendo wa shauri pamoja na nakala ya hukumu vinatakiwa viwafikie wadaawa kwa wakati. Mhe. Mzuna alisema endapo taarifa hizi zitawafikia Wadaawa mapema zinawawezesha kufanya hatua nyingine kama watakuwa hawajaridhishwa na maamuzi ya Mahakama hiyo.

Katika kusititiza hilo Mheshimiwa Jaji Mzuna alifanya ukaguzi mdogo wa majalada ya mashauri yaliyokamilika ili kuweza kugundua ni kwa jinsi gani Mahakimu wamekuwa wakitekeleza wajibu wao.

Ukaguzi huo ulihusisha majalada ya Mahakama ya Wilaya Mbulu na majalada ya Mahakama ya mwanzo Endagikot. Pia aliwapa maelekezo na mapendekezo pale alipogundua kuna changamoto katika kutekeleza wajibu wao.

Katika ziara hiyo, Mhe. Jaji Mfawidhi alikutana pia na Wazee wa Baraza wa Wilaya ya Mbulu ili kuweza kuwafahamu na kujua changamoto wanazokabiliana nazo ambazo zinakwamisha ufanisi wa kazi zao.
Jaji Mzuna akikagua majalada ya Mahakama ya mwanzo ya Endagikot wilayani Mbulu.

Europa League Mubashara ndani ya StarTimes

0
0
Katika mzunguko wa tatu wa ligi ya UEFA Europa, StarTimes kupitia chaneli ya World Football watakuwa wakiuonyesha mchezo wa Sporting CP dhidi ya Arsenal Mubashara majira ya Saa nne Usiku siku ya Alhamisi.
UEFA Europa League inafahamika kwa kuwa na ushindani wa hali ya juu lakini kuwa na matokeo yasiyotabirika kiurahisi. Mchezo wa Sporting CP na Arsenal unatarajiwa mkali sana hasa ukizingatia kiwango cha Arsenal kwa sasa, lakini pia kiwango kizuri cha miamba kutoka Ureno ambao wana faida ya kuchezea uwanja wao wa nyumbani wa Jose Alvalade.
Michezo mingine itakayopigwa usiku wa kesho na kuonyeshwa kupitia StarTimes ni RB Leipzig vs Celtic FC, Anderlecht vs Fenerbahce, AC Milan vs Real Betis, Olympic Marseille vs Lazio, pia Chelsea watakuwa nyumbani dhidi ya FC BATE Borisov. 
Kivutio kingine ni timu anayochezea Mtanzania Mbwana Ally Samatta, Genk ambayo itacheza ugenini dhidi ya Besiktas ya Uturuki. Mbwana Samatta amekuwa na kiwango kizuri sana akiichezea klabu yake lakini pia timu ya taifa ya Taifa Stars, wengi watapenda kumuona akiendeleza kiwango chake katika Usiku wa Europa dhidi ya Besiktas na sehemu pekee unapoweza kumuangalia ni kupitia king’amuzi cha StarTimes.
Mbali na ligi ya Europa, wikiendi hii ligi ya Ujerumani itaendelea kwa mechi kali kati ya RB Leipzig na Schalke 04 itakayochezwa saa 11:30 jioni siku ya Jumapili katika dimba la Red Bull Arena na Utarushwa LIVE na chaneli ya World Football ndani ya StarTimes tena kwa lugha ya Kiswahili.
Huko Ufaransa katika Ligue 1 kutakuwa na mchezo mwingine wa kukata na shoka ambapo mabingwa Paris Saint Germain watakuwa wageni wa Olympique Marseille katika uwanja wa Orange Velodrome. Mara ya mwisho walikutana mwezi wa pili ambapo Marseille walifungwa mabao 3-0. Marseille watamkosa mshambuliaji wao Florian Thauvan ambaye anauguza majeraha. Mchezo huo pia utaonyeshwa moja kwa moja kupitia World Football saa 5 Usiku siku ya Jumapili.
Burudani yote hii ya Soka inapatikana katika kifurushi cha MAMBO kwa watumiaji wa Antenna kwa Tsh 14,000 tu na kwa watumiaji wa Dish ni Tsh 21,000 kwa kifurushi cha SMART.

RAIS WA ZANZIBAR AHAKIKISHIWAUSHIRIKIANO NA MTAWALA WA RAS AL KHAIMAN

0
0
MTAWALA wa Ras al Khaimah Shaikh Saud Bin Saqr Al Qasimi amemuhakikishia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kuwa serikali yake itatoa ushirikiano katika kufanikisha shughuli ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia kupitia Mkataba uliosainiwa hapo jana.

Shaikh Saud Bin Saqr Al Qasimi aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na mwenyeji wake RaisDk. Shein katika ukumbi wa Ikulu mjini Zanzibar, ambapo katika mazungumzo hayo Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd alihudhuria pamoja na viongozi wa Ras al Khaimah na wa Zanzibar.

Katika maelezo yake, Shaikh Al Qasimi alisifu juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Kampuni ya RAK GAS ya Ras al Khaimah katika kutekeleza mipango iliyopo ya utafutaji wa nishati hiyo.

Katika mazungumzo hayo, Mtawala huyo alieleza kuvutiwa kwake na mipango inayoendelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sekta ya mafuta na gesi hasa kwa maamuzi yaliyofikiwa ya kutaka kujenga bandari maalum ya mafuta na gesi katika eneo la Mangapwani.

Aidha, Mtawala huyo alisema kwamba Serikali ya Ras al Khaimah itatekeleza ahadi iliyoitoa mwezi Januari mwaka huu wakati Rais Dk. Shein alipotembelea nchi hiyo ya kushirikiana na Zanzibar kinyenzo na kitaalamu katika kujitayarisha kuingia katika uchumi wa mafuta na gesi asilia.

Shaikh Saud Bin Saqr Al Qasimi ambaye hapo jana aliungana na Rais Dk. Shein katika viwanja vya Ikulu mjni Zanzibar kushuhudia utiaji saini Mkataba wa Mgawanyo wa Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia, alisema kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa kuzingatia kwamba nchi kadhaa duniani zinapata changamoto kwa kushindwa kujitayarisha vizuri katika kuipokea sekta hiyo.

Kadhalika kiongozi huyo alisifu juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuendeleza sekta ya utalii na kuahidi kwamba Serikali yake itaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika ili Zanzibar iweze kufikia malengo yake iliyojiwekea katika kuendeleza sekta hiyo.

Kiongozi huyo alimuhakikishia Rais Dk. Shein kwamba Ras al Khaimah inatumia uzoefu wake ulionao kwa kushirikiana na Zanzibar katika kuendeleza na kuimarisha sekta ya utalii nchini.

Kuhusu sekta ya elimu, Kiongozi huyo aliipongeza Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar chini yauongozi wa Rais Dk. Shein kwa juhudi inazoendelea kuzichukua katika kuendeleza sekta ya elimu ili kuweza kukidhi mahitaji ya wataalamu wanaohitajika nchini katika sekta mbali mbali pamoja na kuweza kwenda sambamba na mahitaji ya karne ya 21.

Kiongozi huyo alieleza kuwa ili kuhakikisha Zanzibar inafikia azma ya kuwa na wataalamu wa kutosha aliahidi kwamba pande zote mbili zitashirikiana kuimarisha sekta ya elimu kwa nchi hiyo kutoa nafasi za masomo kwa wananchi wa Zanzibar pamoja na kubadilishana wanafunzi baina ya pande mbili hizo.  
Alieleza kwamba wananachi wan chi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wanahistoria kubwa inayoonesha kuwa wamekuwa na ushirikiano wa kidugu na ndugu zao wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba ziara hiyo itazidi kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo.

Alisema kwamba ziara yake hiyo inatoa fursa nzuri ya kuharakisha utekelezaji wa mambo mbali mbali yaliyokubaliwa katika ziara aliyoifanya Rais Dk. Shein mwezi Januari mwaka huu katika nchi za Falme za Kiarabu.

Nae Dk. Shein kwa upande wake alitumia fursa hiyo kwa kueleza juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na Serikali katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ili kuimarisha ustawi wa wananchi.

Rais Dk. Shein alieleza kuwa mafanikio yanayoendelea kupatikana katika sekta ya utalii ambayo ni muhimili mkuu wa uchumi wa Zanzibar hivi sasa na kueleza azma na mikakati iliyowekwa ili kuongeza idadi ya watalii ifikapo mwaka 2020.

Aidha, Rais Dk. Shein alieleza mipango ya Zanzibar ya kujenga bandari maalum ya kusafirisha mafuta na gesi asilia kwa azma ya kurahisisha usafiri wa nishati hiyo ili kuondoa changamoto zilizopo hivi sasa za usafirishaji wa bidhaa pamoja na kujitayarisha na mipango ya hapo baadae.

Rais Dk. Shein alitoa shukurani kwa Mtawala huyo kwa kukubali kushirikiana na Zanzibar katika juhudi zake za kuimarisha sekta ya elimu, kwa kukubali kutoa nafasi maalum za masomo kwa wanafunzi wa Zanzibar katika nyanja mbali mbali zinazofundishwa katika vyuo vya Ras al Khaimah.

Alitoa shukurani maalum kwa Serikali ya nchi hiyo kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika juhudi zake za kukuza uchumi na kuimarisha utoaji huduma mbali mbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kusaidia kuimarisha sekta ya maji safi na salama hapa Zanzibar.

Alieleza haja kwa Ras al Khaimah kushirikiana na Zanzibar katika kuimarisha sekta ya utalii hasa ikizingatiwa kuwa nchi hiyo tayari imeshapata mafanikio makubwa katika sekta hiyo huku akieleza umhimu wa pande mbili hizo kushirikiana katika sekta ya usafri wa anga hatua ambayo itasaidia shughuli za utalii, biashara na shughuli nyenginezo za kijamii.




Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein amemueleza kiongozi huyo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejidhatiti kuyatekeleza makubaliano yote yaliyokubaliwa katika ziara zote zilizofanyika nchini humo pamoja na yale yote yaliyokuwemo katika Mkataba wa Mgawanyo wa Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia.

Shaikh Saud Bin Saqr Al Qasimi ameondoka nchini leo kurejea Ras al Khaimah ambapo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume aliagwa kwa heshima zote za Kitaifa pamoja na kuagwa na viongozi mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa  Haji Ussi Gavu.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822  

E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

TANZANIA HAKUNA UBANAJI WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI-MAJALIWA

0
0
*Asisitiza kwa  atakayeenda kinyume na sheria, Serikali itamuwajibisha

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kwamba nchini Tanzania hakuna ubanaji wa uhuru wa vyombo vya habari wala taasisi zisizo za kiserikali.

Amesema jambo hilo linadhihirishwa na uwepo wa jumla ya vituo vya redio 152, ambavyo kati yake ni vituo vitatu tu ndivyo vinavyomilikiwa na Serikali.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Oktoba 24, 2018) katika maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

“Tunapenda kuwahakikishia kuwa, Serikali ya Tanzania inaongozwa na katiba na sheria za nchi ambazo zinatoa uhuru wa kujieleza na kupata habari,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesisitiza kwamba mwananchi yeyote atakayeenda kinyume na sheria, Serikali itamuwajibisha kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Amesema Serikali imeridhia mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na ule wa haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni. 

Sambamba na kusimamia haki hizo, Serikali imeendelea kutekeleza wajibu wake katika kuiwezesha jamii kuishi salama kwa amani na utulivu kwa kuzingatia sheria za nchi.

Amesema kukuza, kuimarisha na kulinda haki za binadamu ni wajibu wa Serikali na kwa kuzingatia umuhimu huo mwaka 1984 iliingiza sheria ya haki za binadamu katika katiba.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua gwaride katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Oktoba 24, 2108. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia upandishwaji wa bendera ya Umoja wa Mataifa katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Oktoba 24, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na watumishi  wa Mashirika ya  Umoja wa Mataifa nchini, katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Oktoba 24, 2018. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali hapa Tanzania  katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Oktoba 24, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na  Mratibu Mkaazi wa Mashirika ya  Umoja wa Mataifa  na Mwakilishi wa  Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,  Bw. Alvaro Rodrigues katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Oktoba 24, 2018. Kushoto ni Meya wa jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TUME YAONYA WATAKAOHARIBU UCHAGUZI

0
0
Na Margareth Chambiri
TUME ya Taifa ya Uchaguzi imewaonya Wasimamizi wa Uchaguzi ambao ama kwa kujua au kwa makusudi wataharibu au kukiuka taratibu za Uchaguzi kutokana na kutofuata sheria na taratibu za Uchaguzi.

Onyo hilo limetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk wakati akifungua mafunzo kwa Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi jijini Dodoma.

Mheshimiwa Mbarouk ambaye amewataka Wasimamizi hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea amesema Sheria ya Taifa ya Uchaguzi na ile ya Serikali za Mitaa zinaunda kosa la jinai na kutoa masharti ya adhabu kwa Afisa yeyote wa Uchaguzi ambaye atasababisha kuharibu uchaguzi.

Makamu Mwenyekiti huyo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  amesema madhara ya kutozingatiwa kwa taratibu za Uchaguzi ni kusababisha kesi nyingi za Uchaguzi na kuitumbukiza Serikali katika gharama ambazo zingeweza kutumika katika shughuli nyingine za maendeleo.

Amewataka Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kuyaelewa vyema maeneo wanayofanyia kazi na kujiamini ambapo pia amewakumbusha jukumu walilo nalo la kuimarisha imani ya wananchi na wadau wengine wa Uchaguzi kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt Athumani Kihamia amewataka washiriki wa mafunzo hayo kutoa ushirikiano kwa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mdogo ikiwa ni pamoja na kuvishirikisha katika kila hatua muhimu wakati wa mchakato wa Uchaguzi.

Dkt. Kihamia amesema Watendaji wote wa Tume wanapaswa kuwapo katika maeneo yao ya kazi wakati wote hususan kipindi cha Uteuzi, kufungua ofisi hadi muda wa kisheria na Vyama vyote ambavyo vimefuata taratibu vipewe fomu za Uteuzi na Wagombea wao wateuliwe kama wamekidhi vigezo.

Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi ameongeza kusema kuwa kutozingatiwa kwa mambo hayo husababisha kuharibu imani ya Wadau na kusababisha malalamiko ya kutoridhishwa na mchakato wa Uchaguzi na hatimaye mashauri ya Uchaguzi kufikishwa mahakamani.

Kadhalika Dkt Kihamia amewataka Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi hao wa Uchaguzi kutojihusisha na migogoro ya ndani ya Vyama na iwapo Vyama vitakuwa na malalamiko vielekezwe kuwasilisha malalamiko yao kwenye Kamati za Maadili na si mahali pengine popote.

Kwa mujibu wa Dkt. Kihamia chaguzi zote duniani ni kielelezo cha demokrasia na kwamba Uchaguzi huru na wa haki hutokana na Wasimamizi wa Uchaguzi wanaozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia Uchaguzi husika.

Jumla ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi 210 kutoka katika Majimbo manne ya Serengeti, Simanjiro, Ukerewe na Babati Mjini pamoja na Kata 47 zinazotarajiwa kufanya Uchaguzi Mdogo Desemba 3, mwaka huu wanashiriki katika mafunzo hayo yatakayodumu kwa siku tatu jijini Dodoma. 
Mkuu wa Idara ya Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Irene Kadushi, akifafanua jambo wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi. 
Mkuu wa Idara ya Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Emmanuel Kawishe akifafanua hoja katika mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi.
Afisa Uchaguzi Meshack Mgovano, akieleza jambo kwenye mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi.
Picha zote na NEC.
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live




Latest Images