Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

SERIKALI KUONGEZA MAWASILIANO ENEO LA UWEKEZAJI MKURANGA

$
0
0
NAIBU Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amefanya ziara ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye Wilaya ya Mkuranga iliyopo mkoa wa Pwani na kuahidi wananchi kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaongeza mawasiliano kwenye Wilaya hiyo ambayo ina viwanda vingi vyenye uwekezaji wa aina mbali mbali

Amesema kuwa katika ziara yake amebaini kuwa yapo baadhi ya maeneo ambayo yanahitaji kuongezewa nguvu ili mawasiliano yaweze kufika eneo kubwa zaidi na kupeleka mawasiliano kwenye baadhi ya maeneo ambayo yana ukosefu wa mawasiliano kwenye Wilaya hiyo kwa kuwa mawasiliano ni maendeleo, uchumi na ulinzi na usalama.

Amefafanua kuwa, “kimsingi mawasiliano yapo Mkuranga ila tunatakiwa kuongeza nguvu ili wananchi wapate mawasiliano. Tunahitaji wananchi wa Tanzania wawasiliane,” amesema Nditiye. Ameongeza kuwa minara iliyopo inaweza kuongezwa nguvu, kampuni nyingine zitafunga mawasiliano kwenye minara ya kampuni nyingine zilizopo na kujenga minara kwenye maeneo ambayo hayana mawasiliano kabisa. 

Nditiye amemshukuru Ulega na kuwapongeza wananchi wa Tanzania kwa kuonyesha uhitaji wa mawasiliano na wamegundua mawasiliano ni maendeleo yao, uchumi, ulinzi na usalama. Amesema kuwa karibu asilimia 60 ya eneo la Mkuranga halina mawasiliano na ameyataka makampuni ya simu yaliyojenga minara kwenye Wilaya ya Mkuranga kuongeza nguvu ya mawasiliano kutoka teknolojia ya 2G hadi teknolojia ya 4G. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akifafanua jambo wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye vijiji mbali mbali vya Wilaya ya Mkuranga. (wa kwanza kushoto) Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo hilo,Abdallah Ulega.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kushoto pili ) akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega kuhusu ukosefu wa mawasiliano ya uhakika kwenye eneo hilo. Wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Peter Ulanga.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta,Nditiye akitoa maelekezo namna minala ya mawasiliano itakavyo jengwa katika ya  Wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.

WANANCHI WA MKURANGA WALALAMIKIA KUINGIA KWA MADADA POA

$
0
0
WANANCHI wa Kata Magawa wilayani Mkuranga wamelalamikia kuingia kwa wanawake wanaouza miili yao (Madada poa) kwa kutumia mazao.

Wananchi hao wamesema ujio wa wanawake ni katika kipindi cha mauzo ya msimu wa Korosho na Nazi ndio wanaingia na kuanza kufanya biashara ya ngono.

Wamesema wanawake hao wanachukua debe moja ya kurosho kwa wanaume kwa ajili ya kufanya ngono au kutoa Nazi 10 hadi 15.

Akizungumza na Michuzi Blog Mariam Hamis amesema kuwa ujio wanawake hao imekuwa kero katika ndoa zao.

Amesema kuwa serikali ya wilaya isipowatoa watakwenda wenyewe kupambana nao hata kwa mapanga.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga Juma Abeid amesema kuwa suala hilo kwa Mkuu wa Wilaya.

Abeid amesema amesema ujio wadada hao ni changamoto katika kuambukizana na magonjwa. 
Amesema kila msimu wa korosho wanawake hao wamekuwa wakiweka kambi.Mwenyekiti wa halmashaul ya Wilaya Mkuranga na Diwani wa kata ya Magawa,Juma Abed akizungumza na michuzi blog juu ya changamoto ya uwepo wa dada poa katika kata yake.
Picha na Emmaniel Massaka wa Global ya jamii)
Wakazii wa kata ya Magawa Wilaya ya mkuranga mkoa Pwani wakizungumza na michuzi blog juu ya ambapo wameiomba serikali iwasaidie kuondoa dadapoa abapo huwa napiga gambi kilaunapofika msimu wa wa korosho.

HUYU NDIYE MWALIMU KASHASHA

Introducing "Umeniacha" by Dj Hunter Ft Stizzo X Mafioso Produced By PAPA

Muhimbili Wahitimisha Huduma ya Matibabu Hospitali ya Rufaa Musoma

$
0
0
Wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) waliokuwa wakitoa huduma ya matibabu kwa njia ya mkoba kwa kushirikiana na watalaam wa Hospitali ya Rufaa ya Musoma mkoani Mara wameitimisha huduma hiyo leo Ijumaa baada ya kuwaona wagonjwa zaidi 1960 na kuwafanyia upasuaji zaidi wagonjwa 146.
Awali wataalam wa Muhimbili walikuwa watoe huduma ya matibabu kwa wananchi wa Mkoa wa Mara pamoja na kuwajengea uwezo watalaam wa Hospitali ya Rufaa ya Musoma kwa muda wa wiki moja, lakini uongozi wa Muhimbili ulilazimika kuongeza siku saba kutokana na wingi wa wagonjwa walijitokeza kutoka Mkoa wa Simiyu, Mwanza na Shinyanga kwa ajili ya kupata huduma za kibingwa.
Wakati akihitimisha huduma hiyo leo  Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt. Joachim Eyembe aliwashukuru wataalam wa Muhimbili kwa kutoa huduma za kibingwa kwa kushirikiana na wataalam wake.
“Tunawapongeza sana kwa mara nyingine kwa ujio wenu, na tutawasiliana na uongozi wa Muhimbili ili tuwaombe mrudi tena Musoma kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Mara. Siwezi kueleza furaha yangu kwa ujio wenu kwani naamini wataalam wangu wamejifunza mengi kutoka kwenu na wananchi wamepata huduma za kibingwahi,” amesema Dkt. Eyembe.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Nje, Dkt. Farbian Besiyegwa wa hospitali hiyo amesema amejifunza mambo mengi kutoka kwa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani, Dkt. Brighton Mushengezi wa Muhimbili.
“Kwa kweli nashukuru kufanya kazi na Dkt. Brighton, amenifundisha mambo mengi, hivi sasa  natamani kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya ndani,” amesema Dkt. Besiyegwa wakati wa kuwaaga wataalam wa Muhimbili.
Akizungumzia changamoto ambazo zimebainishwa na watalaam wa Muhimbili, Dkt. Eyembe kwa niaba ya uongozi wa hospitali hiyo ameahidi kushughulikia changamoto zote ili kuboresha zaidi huduma za afya katika hospitali hiyo.
Mganga mfawidhi ameahidi kutafuta fedha kwa ajili ya kuwapatia mafunzo zaidi wataalam wake pamoja na kuboresha maeneo ya kutolea huduma ili kufikia malengo ya hospitali hiyo ya kuwa moja hospitali kubwa ya rufaa inayotoa huduma bora nchini.
Naye daktari Bingwa wa Macho wa Muhimbili, Dkt. Neema Kanyaro amesema wataalam wenzake walipewa ushirikiano mkubwa na wataalamu wa Hospitali ya Rufaa ya Musoma.
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Musoma mkoani Mara, Dkt. Joachim Eyembe leo akiwaaga wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kumaliza kutoa huduma ya matibabu kwa njia mkoba kwa kushirikiana na wataalamu wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Musoma.
 Baadhi ya wataalamu wa Muhimbili wakiwa kwenye kikao cha kuagana leo na wataalam wa Hospitali ya Rufaa ya Musoma katika ofisi za Mganga Mfawidhi.
 Baadhi ya wataalam wa Hospitali ya Rufaa Musoma wakiwa kwenye kikao hicho leo.
Wataalam wengine wa Hospitali ya Rufaa Musoma wakifuatilia kikao hicho leo.

MCHEKESHAJI KIBOKO MTAANI..

Twanga Pepeta balaa,Full story Miaka 20 na Asha Baraka.

ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA WILAYANI BAHI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mtalaam wa Maabara, Petronila Olomi  (kushoto) wakati alipotembelea Maabara ya Kituo cha Afya cha Bahi mkoani Dodoma, Oktoba 19, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  Selemani Jafo na Wapili kushoto ni Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Kassim  Kolowa. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo orodha ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ambao bado hawajahamia Bahi na wanaishi mjini  Dodoma ili awachukulie hatua. Alikuwa katika kikao na Watumishi wa Halmashuri hiyo, Oktoba 19, 2018. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TRA yawaonya wafanyabishara kariakoo

$
0
0
Na mwandishi wetu, Dar es salaam
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewaonya wafanyabiashara wa eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, wanaotumia risiti moja iliyotolewa kwenye mashine ya EFD kwa ajili ya kusafirishia mzigo zaidi ya mmoja kutoka eneo la Kariakoo kwenda eneo la Jangwani wanapoenda kupakia mizigo kwa ajili ya kusafirisha mikoani, kwani atakayekamatwa adhabu yake ni faini ya asilimia 200 ya kodi iliyopaswa kulipwa katika mzigo huo.
Onyo hilo limetolewa na Kamishna wa Kodi za Ndani kutoka TRA Bw. Elijah Mwandumbya, alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa eneo la Kariakoo katika utaratibu wake wa kuwafuata wafanyabiashara katika maeneo yao na kuzumgumza nao masuala mbalimbali ya kodi. 
Kamishna Mwandumbya amesema kuwa TRA imethibitisha kwamba, baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia mikokoteni au magari madogo ya kubebea mizigo maarufu kama ‘Kirikuu’, wanatumia risiti moja iliyotolewa kwenye mashine ya EFD muda wa asubuhi ili kupeleka mzigo eneo la Jangwani, na risiti hiyo hiyo inaendelea kutumika kusafirishia mizigo mingine hadi jioni kwa safari zaidi ya mara moja.
“Tumethibitisha hata wengine, risiti ile ile moja imetolewa asubuhi, inapeleka mizigo jangwani kwa kutumia kirikuu kwenda na kurudi mpaka jioni, hii siyo sawa, ni vyema kila mmoja atimize wajibu wake, jambo hili tutalijadili,” amesema Bw. Mwandumbya.
Bw.Mwandumbya, amesema hata kwenye vitabu vitakatifu vinaonesha kwamba mtoza ushuru hapendwi, ila TRA inapenda kujenga mazingira mazuri ya mahusiano kati ya mtoza ushuru na mlipakodi.
Aidha, Kamishna Mwandumbya, amesisitiza wafanyabiashara wa eneo la Kariakoo nan chi nzima, kutoa risiti sahihi za mauzo yao lakini pia kuchukua risiti pale wanapofanya mazunuzi ya bidhaa za jumla na rejareja ili kuepuka usumbufu wowote kutoka kwa maofisa wa TRA wanapokuwa kwenye operesheni.
“Niwaombe wafanyabishara na watanzania wenzangu tudai na tuchukue risiti za EFD kwa kila manunuzi tunayofanya, hii itaisaidia kuongeza mapato ya serikali na kuiwezesha nchi kufikia malengo yake pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuunga mkono juhudi za rais wetu”, amesema Mwandumbya.
Naye mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Mch. Silva Kiondo, amesema imekuwa Faraja kwa Kamishna kukutana na wafanyabiashara wa eneo la kariakoo kwa kuwa wanayo mambo mengi ya kujadiliana ili kuifufua Kariakoo kibiashara.
“Nadhani, sababu kubwa iliyomfanya Kamishna wa Kodi za Ndani kufika hapa ni kutaka kuona Kariakoo inafufuka kibiashara”, amesema.
 Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA Bw. Elijah Mwandumbya akijibu hoja za wafanyabiashara wa eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam alipokutana nao kwa mazungumzo katika mkutano uliofanyika mtaa wa Mchikichi eneo la Kariakoo
 Mfanyabiashara wa Kariakoo Bw. Emmanuel Mwakatungila, akiuliza swali wakati wa mkutano kati Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA na wafanyabishara wa eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam. 
Wafanyabiashara wa eneo la Kariakoo jijini Dar es salaam wakimsikiliza Kamisha wa  Kodi za Ndani Bw. Elijah Mwandumbya alipofanya nao mkutano katika mtaa wa Mchikichi, Kariakoo.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA OKTOBA 19, 2018

Polisi Kishapu yakabidhiwa gari jipya kutoka mgodi wa Mwadui

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiliangalia gari alilokabidhiwa kwa ajili ya Jeshi la Polisi wilayani Kishapu.

Na Robert Hokororo, Kishapu

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga limepokea gari jipya kwa ajili ya matumizi ya shughuli zake kutoka mgodi wa almasi wa Mwadui.

Gari hilo aina ya Nissan Hilux lenye thamani ya sh. milioni 80 limepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack ambaye alikabidhi jeshi hilo.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya gari hilo yaliyofanyika wilayani humo Mhe.Telack aliushukuru mgodi kwa msaada huo. Telack ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa alisema kuwa gari litawezesha shughuli za Polisi kufanyikaa kwa ufanisi.

Aliwaomba wasichoke kuendelea kuisaidia Kishapu pamoja na kushirikiana na Serikali ya wilaya hiyo kwani wao pia ni sehemu ya jamii hiyo.

Aidha alilitaka jeshi hilo kulitumia gari hilo walilokabidhiwa kwa matumzi yaliyokusudiwa ya kulinda wananchi ili waendelee kuwa na imani nalo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akitoa maelekezo na kumkabidhi funguo na kadi ya gari Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) ya Kishapu, Emmanuel Galiyamoshi. Anayeshuhudia kushoto ni Alchelaus Mutalemwa.
Sehemu ya maafisa wa Jeshi la Polisi wilayani Kishapu wakinyakua baada ya kushuhudia makabidhiano ya gari.

Breaking Nyuuuuzzzz.... : Mfanyabiashara Mo Dewji apatikana

$
0
0
*Apatikana baada ya waliomteka kumtupa viwanja vya Gymkhana Dar
*Waliomteka inadaiwa walikuwa wanaongea lafudhi ya South Afrika
*MO mwenyewe awashukuru Watanzania kwa dua zao kwake

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MFANYABIASHARA maarufu Mohammed Dewji 'MO' aliyekuwa ametekwa akiwa katika Hoteli ya Collessium jijini Dar es Salaam hatimaye amepatikana akiwa mzima na mwenye afya njema.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amethibitisha kupatikana kwa MO ambapo anasema yeye amemuona na amezungumza naye akiwa mzima na tayari ameungana na familia yake.

Kamanda Mambosasa akifafanua zaidi leo jijini Dar es Salaam amewaambia Watanzania, MO alitupwa viwanja vya Gymkhana usiku wa kuamkia leo wa Oktoba 20 mwaka huu."Baada  ya kutekwa tarehe Oktoba 11,2018 gari ya watekaji iliendeshwa speed takribani dakika 15 na kuwekwa kwenye chumba akiwa amefunikwa  ili asiwatambue watekaji."

Amesema kwa mujibu wa MO ni kwamba watekaji hao walikuwa wakiongea lugha za Afrika Kusini na hivyo inathibitisha waliomteka hawakuwa Watanzania na kinachoendelea Polisi nao wanaendelea kukamilisha taratibu za kiuchunguzi.

Mambosasa amesema kuwa MO kwa siku zote ambazo alikuwa anashikiliwa na watekaji alikuwa kwenye mazingira magumu lakini wanashukuru amepatikana akiwa salama kwani kwa kipindi chote Jeshi la Polisi lilikuwa likihangaika kuhakikisha anapatikana na kweli amepatikana.

Ameongeza kupitia upelelezi wao walipata taarifa MO ametupwa maeneo ya Gymkhana na hivyo baada ya kupata taarifa hizo yeye pamoja na maofisa wake wa upelelezi wamefika nyumbani kwa mfanyabiashara huyo ambaye ameungana na familia yake.

Hata hivyo Mambosasa alimuomba MO kama hatojali kuzungumza ili Watanzania waweze kumuona na kumsikia ambapo alimpa nafasi ya kusalimia.Kwa upande wake MO amesema kuwa anawashukuru Watanzania wote na katika shukrani hizo ameanza kwa kumshukuru Rais Dk.John Magufuli na kisha akatoa shukrani kwa Jeshi la Polisi kutokana na jitihada zao za kuhakikisha anapatikana.

"Ahsante wote na nawashukuru Watanzania wote ,nipo salama," amesema MO Dewji akiwa nyumbani huku Mambosasa akiwataka Watanzania kuendelea kuwa watulivu.Kwa kukumbusha tu Mo alitekwa Oktoba 10 mwaka huu saa 11 asubuhi baada ya kufika kwenye hoteli ya Collessium kwa ajili ya mazoezi ambapo kabla ya kushuka kwenye gari yake watekaji walimteka na kuondoka naye kwenye gari aina ya Toyota Suff na kisha kwenda kusikojulikana.

Hata hivyo Polisi waliamua kuweka mikakati ya kuhakikisha MO anapatikana.Wakati wakiendelea na upelelezi wao jumla ya watu 27 waliwashikilia kwa mahojiano lakini hadi jana walikuwa wamebaki na watu nane.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro wakati anazungumza jana asubuh na waandishi wa habari alisema jeshi hilo halijalala tangu MO alipotekwa kwani wanaendelea kufuatilia na kukusanya taarifa ambazo zitafanikisha kupatikana kwake.



IGP Sirro pia alionesha picha ya gari ambayo ilihusika katika tukio la kutekwa MO pamoja na risasi mbili ambazo zilikuwa eneo la tukio ambazo nazo walizichukua kwa ajili ya uchunguzi ambapo aliwahakikishia Watanzania jeshi lao la Polisi liko imara na linafanyakazi zake kwa weledi.
Mfanyabiashara Mo Dewji amepatika. Waziri January Makamba amesema kuwa amemuona na kuongea nae kwa kirefu, ni mzima wa afya isipokuwa ana alama za kufungwa kamba mikononi na miguuni. Ameongeza kuwa, majira ya saa nane za usiku, watekaji walimtupa kwenye viwanja vya Gymkhana, Dar.

Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua Tawi la Morogoro

$
0
0
Benki ya Biashara Mkombozi imezindua rasmi Tawi la Morogoro ambalo limepandishwa hadhi kutoka kituo cha huduma za kifedha na sasa kuwa tawi kamili.

Zoezi hili linafanyika wiki moja tu baada ya Benki ya Biashara Mkombozi kuzindua Tawi la Tegeta ambalo pia lilikuwa kituo cha cha huduma za kifedha hapo awali.

 Ufunguzi wa Tawi hilo ulifanywa na Katibu Tawala Wilaya ya Morogoro Bi. Ruth John akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa,  wadau mbalimbali, wafanyakazi, wafanyabiashara na wateja wa Benki ya Biashara Mkombozi.

 Akizindua tawi hilo jipya, mgeni rasmi aliipongeza Benki ya Biashara Mkombozi kwa hatua iliyofikia na kusema uzoefu kutoka nchi nyingine unaonyesha kuwa wafanya biashara wadogo na wale wakati ni wadau muhimu sana katika kukuza uchumi na kuondoa umasikini.

“Hivyo napenda kuwapongeza benki ya Biashara Mkombozi kwa kuamua kuwafikia wadau hawa muhimu ambao baadhi ya taasisi za kifedha zinawatizama kama ni soko hatarishi katika biashara ya kukopesha,” alisema.

Mgeni rasmi pia aliipongeza Benki ya Biashara Mkombozi kwa kutoa huduma za kibenki kwa watanzania wote bila ubaguzi wa rangi, ukabila, dini, dhehebu tofauti na baadhi ya watu wanavyotafsiri kuwa ni benki ya kanisa tu.

 “Natambua kuwa bado tuna changamoto kubwa ya kuwafikia na kuwashawishi watanzania walio wengi kutumia huduma za fedha za kibenki. Rai yangu kwenu Uongozi na Wafanyakazi wa Benki ya Biashara Mkombozi ni kwamba, mjikite zaidi katika ubunifu ili kuweza kuwavutia kundi hili ambalo linahitaji huduma zenu lakini labda utambuzi bayana bado haujakuwepo,” alisema.

Alitoa wito kwa Benki ya Mkombozi pia ijitahidi kufahamu mahitaji halisi ya soko na hivyo kuboresha huduma zake na bidhaa ili ziendane na mahitaji. “Elimu juu ya fedha kwa wananchi (yaani Financial literacy) ni muhimu sana, naomba pia muweke nguvu zenu katika hili,” alisema.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Ruth John  (wa tatu kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tawi jipya la Morogoro la Benki ya Biashara ya Mkombozi  huku viongozi na wageni waalikwa wakishuhudia tukio hilo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Ruth John akijaza fomu ya kufungua akaunti katika Benki ya Biashara ya Mkombozi baada ya kuzindua tawi jipya la Morogoro. 

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Biashara ya Mkombozi Tawi la Morogoro wakifuatilia matukio ya uzinduzi wa tawi hilo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TACAIDS - MAAMBUKIZI YAPO JUU HASA KWA KUNDI LA WANAWAKE WALIO VIJANA, HIVYO TUPAMBANE NA MAAMBUKIZI MAPYA

$
0
0
Kaimu mkurugenzi idara ya mwitikio wa kitaifa ,kutoka TACAIDS, Audrey Njelekela akizungumza ,wakati akifungua mkutano uliolenga kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi za kiraia na mitandao ya vijana pamoja na zinazojishughulisha kuwahudumia watuamiaji wa dawa za kulevya,uliifanyika Bagamoyo, Pwani .

NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO

TUME ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), imeziasa asasi na mikoa kujiwekea mipango ya kupambana na maambukizo mapya hasa kwenye kundi la vijana wa kike (10-24 )kwani inaonyesha maambukizi yapo juu katika kundi hilo.

Aidha imewataka ,wanaoishi na virusi vya ukimwi kutumia kikamilifu dawa za kufubaza virusi (ARVs), bila kukatisha dozi na wale wasio na maambukizi hayo kupiga vita maambukizi mapya.

Kaimu mkurugenzi idara ya mwitikio wa kitaifa ,kutoka TACAIDS  ,Audrey Njelekela alitoa rai hiyo ,wakati akifungua mkutano uliolenga kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi za kiraia na mitandao ya vijana pamoja na zinazojishughulisha kuwahudumia watuamiaji wa dawa za kulevya,uliifanyika Bagamoyo ,Pwani .

Alisema ,maambukizo mapya yapo  81,000 kwa mwaka,sawa na 6,750 kwa mwezi ambapo asilimia 40 ni maambukizo yaliyopo kwenye kundi la wasichana (10-24) na asilimia  80 ni wanawake wa miaka (15-24 ).
Mkurugenzi wa Sober house Bagamoyo,Karim Banji akizungumza katika mkutano uliolenga kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi za kiraia na mitandao ya vijana pamoja na zinazojishughulisha kuwahudumia watuamiaji wa dawa za kulevya,uliifanyika Bagamoyo, Pwani.

"Tujue mipango tunayofanya tunatafsiri mkakati wa nne
wa kudhibiti ukimwi Tanzania ,na tuna uhakika mikakati yetu ya  ukimwi ya mkoa tulijiwekea vipaombele kwahiyo kulingana na takwimu tulizopewa tunajua ukimwi ulipoegemea "alisema Audrey .
Awali mratibu wa asasi za kiraia kutoka TACAIDS ,Mary Manzawa alisema ,lengo la mkutano huo ni kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi za kiraia na mitandao ya vijana na zinazojishughulisha kuwahudumia watuamiaji wa dawa za kulevya .

Mary alitaja, walioshiriki kuwa ni pamoja na asasi za kiraia ,mitandao ya vyama na asasi zinazojishughulisha kuwahudumia watumiaji wa dawa za kulevya nchini .

Mtoa mada katika mkutano huo ,mratibu wa TACAIDS wa Dar es salaam na Pwani ,Yahaya Mbaga alisema maambukizi yapo juu kwa wanawake zaidi kuliko wanaume.
Alieleza,malengo ya Kitaifa yamelenga kuhakikisha asimilia 90 ya kwanza ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini ambao bado hawajajitambua afya zao wawe wamepima ifikapo mwaka 2020.
"Pia wanaoishi na virusi vya ukimwi ifikapo 2020 wawe wameingia katika kutumia dawa za kufubaza VVU na ifikapo mwaka huo asilimia 90 ya ambao wanatumia dawa hizo wawe na virusi vilivyokuwa tayari vimefubaa". Yahaya alitaja lengo jingine, ni kutimiza 000 na ifikapo 2030 kuondoa maambukizi mapya ya UKIMWI,Unyanyapaa na Vifo.

Mmoja wa washiriki katika mkutano huo ,mkurugenzi wa Bagamoyo Sober House ,Karim Banji aliiongeza TACAIDS kwa kushirikisha asasi zinazojishughulisha kuwahudumia watumiaji wa dawa za kulevya.

Hali ya maambukizi ya ukimwi Tanzania kwasasa ni asilimia 4.7 kutoka asilimia 5.1 ,hali inapungua lakini jamii iendelee kupambana na maambukizi mapya ,na Tanzania bila ukimwi inawezekana".

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA KAMATI YA CPPCC YA CHINA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Mashauriano ya Kisiasa ya China (CPPCC), Bw. Lou Jiwei alipofika ofisini kwake Dodoma tarehe 19 Oktoba, 2018 kwa lengo la kumsalimia na kumpongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo. Mkurugenzi huyo anaongoza ujumbe wa watu wanne wa Kamati hiyo ambao wapo nchini kwa mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai. 
Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Mashauriano ya Kisiasa ya China (CPPCC) Bw. Lou Jiwei akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) walipokutana katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Jengo la LAPF jijini Dodoma kwa mazungumzo. Mkurugenzi huyo ni mgeni wa kwanza kutoka nchi za nje kumtembelea katika ofisi yake ya Dodoma. 
Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Mashauriano ya Kisiasa ya China (CPPCC) Bw. Lou Jiwei akimkabidhi zawadi ya kitabu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) ikiwa ni kumbukumbu ya kukutana naye jijini Dodoma.

DKT. MWAKYEMBE AIPONGEZA NIT PROGRAMU YA UFADHILI WA MASOMO KWA MISS TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akizungumza na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zacharia Mganilwa wakati wa mazungumzo baina yao leo Ijumaa Jijini Dar es Salaam kuhusiana na mikakati mbalimbali ya Chuo hicho kwa ajili ya kuboresha tasnia ya mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amekipongeza Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa kuandaa programu ya ufadhili wa masomo ya uhudumu wa ndege kwa washindi wawili wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania. Akizungumza jana Ijumaa (Oktoba 19, 2018) Jijini Dar es Salaam na Viongozi wa Chuo hicho, Dkt. Mwakyembe alisema Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano na kuunga mkono juhudi za NIT, na kuahidi kufanya mawasiliano taasisi mbalimbali za ikiwemo Shirika la Ndege Nchini (ATCL) ili kuchangamkia fursa hiyo.

Dkt. Mwakyembe alisema programu ya mafunzo hayo, yatasaidia kuongeza tija na thamani ya mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania kwani kwa sasa yatapitia katika mchujo wa kuwapata washindi waliojengeka katika mmaarifa na weledi wa kitaaluma.

“Sasa hatutakuwa na sababu ya kuhangaika kutafuta wahudumu wa ndege, NIT mmekuja na programu inayounga mkono mageuzi makubwa katika Shirika letu la ndege la ATCL na hivyo sehemu pekee ya kupata wahudumu wa ndege zetu ni kupitia mchakato wa mashindano ya Miss Tanzania” alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha Dkt. Mwakyembe alisema Serikali itaendelea kuhamasisha  taasisi mbalimbali za Serikali ili kuhakikisha kuwa mkakati huo wa programu ya mafunzo ya NIT  yanaungwa mkono tija katika kuchagiza mageuzi ya kimkakati katika sekta ya Uchukuzi yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Akifafanua zaidi, Dkt. Mwakyembe alisema malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kuanzia mwakani mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania yanaanza kuzalisha mabalozi wa lugha ya Kiswahili, ikiwa ni kielelezo cha utambulisho wa Mtanzania katika eneo lolote duniani.

“Kati ya lugha 6000 duniani, Kiswahili ni miongoni mwa lugha 10 zinazozungumzwa na watu wengi zaidi na kwa mujibu wa Utafiti ya Umoja wa Afrika, ifikapo mwaka 2063 lugha ya Kiswahili itakuwa lugha ya utambulisho wa mtu mweusi, hivyo hatuna budi kujivunia lugha yetu adhimu ya kiswahili” alisema Dkt. Mwakyembe.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha NIT, Prof. Zacharia Mganilwa alisema Taasisi yake imeamua kufanya mageuzi ya kimkakati katika mitaala ya Chuo hicho ili kwenda sambamba na Mageuzi ya Sekta ya Uchukuzi yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Aliongeza kuwa katika mwaka wa masomo 2018/19, Chuo hicho kimeanza kutoa mafunzo ya programu ya uhudumu wa ndege yenye jumla ya wanafunzi wa 24, ambapo inafundishwa kwa kipindi cha miezi mitatu.

TUMEKAMATA SILAHA NNE IKIWEMO YA KIVITA NDANI YA GARI LILILOTUMIKA KUMTEKA MO-IGP SIRRO

$
0
0
Na Said Mwishehe

MKUU wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro amesema wamekata silaha nne ikiwemo ya kivita ambayo inarisasi 19.

Sirro amesema hayo muda huu wakati anaendelea kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio la kupatikana kwa Mfanyabiashara Mohammed Dewji 'MO'. Ametaja silaha hizo ni AK 47, bastola tatu na risasi 16 ambazo zilikuwa ndani ya gari iliyohusika kumteka MO.

Ameongeza kwamba hata hivyo watekaji hao walijaribu kuichoma moto gari hiyo kwa lengo la kupoteza ushahidi lakini ikashindikana .

IGP Sirro amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini watekaji hao na kwamba kokote walioko watatafutwa na hatimaye wapatikane wakiwa hai au wamekufa .

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi...endelea kufuatilia Michuzi Blog
KUU wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika viwanja vya Gymkana

Serikali Yawekeza Sh. Bilioni 45 Kwenye Miradi ya Maji Mtwara

$
0
0


Serikali imewekeza takribani kiasi cha Shilingi Bilioni 45 kwenye miradi ya maji mkoani Mtwara kwa lengo la kufikisha huduma ya maji mkoani humo kwa asilimia 100.

Akizungumza akiwa ziarani katika Wilaya ya Masasi, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi inataka ifikapo mwaka 2020 upatikanaji wa huduma ya maji nchini uwe kwa kiwango cha asilimia 95 mijini, asilimia 90 kwenye miji mikuu ya wilaya na asilimia 85 vijijini.

Profesa Mbarawa amesema ili kufikia lengo hilo mpaka sasa Serikali imetenga Shilingi Bilioni 45 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji 37 kwenye mkoa wa Mtwara pekee, ambapo mpaka sasa imeshalipa kiasi cha Shilingi Bilioni 25 na Shilingi Bilioni 20 iliyobaki italipwa kwa kadiri hati za malipo zitakapokuwa zinafika wizarani.

Amezungumza hayo mara baada ya kukagua miradi ya maji ya Makong’onda, Chipingo-Mkaliwata na kutembelea chanzo cha maji kinachotumiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA).

Profesa Mbarawa amesema kwa sasa mkoa wa Mtawara una jumla ya miradi 37 inayotekelezwa na 4 kati ya hiyo imekamilika, mingine ikiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji na kuahidi itakamilika kwa wakati ili kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji kwa wakazi wa mkoa huo.
 Ujenzi wa mradi wa maji wa Chipingo-Mkaliwata, wilayani Masasi katika mkoa wa Mtwara ukiendelea.
1
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akitoa msisitizo kwa Jumanne Mackenzie, mkandarasi kutoka Kampuni ya Singilimo Enterprises Ltd akamilishe mradi wa maji wa Makong’onda, uliopo katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara. 
3
Mkurugenzi Mtendaji wa MANAWASA, Mhandisi Nuntufye David akiwa na Waziri wa Maji,  Makame Mbarawa kwenye chanzo cha maji cha Mbwinji.
4
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akitoka kukagua chanzo cha maji cha Kisimani Newala kilichopo katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.
5
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akikagua maendeProfesaleo ya ujenzi wa mradi wa maji wa Chipingo-Mkaliwata, wilayani Masasi katika mkoa wa Mtwara.

DKT NDUGULILE AWAAGIZA WATENDAJI WIZARA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MAKAZI YA WAZEE FUNGAFUNGA.

$
0
0
Serikali imetaka  wazazi,walimu wakuu,watendaji wa kata na vijiji pamoja wale wote watakaousika na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto au kumpa mimba mwanafunzi kuwajibiswa kwa kusababisha watoto wa kike kushindwa kumaliza masomo yao na kusababisha wasichana walio mashuleni kushindwa kutimiza ndoto zao.                                                                                                           
Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile alipofanya ziara Mkoani Morogoro kupata taarifa ya Mkoa huo kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa masuala Afya na Maendeleo ya Jamii Mkoani humo.

Akizungumzia hali hiyo Naibu Waziri Ndugulile alisema kiwango cha matukio haya ni kikubwa mno na kuagiza Mkoa huo kuanzisha Madawati ya Ulinzi na Usalama ya Wanawake na Watoto pamoja na vituo vya mkono kwa mkono (One Stop Centres) akisistiza kuwa haya ni maagizo ya serikali kama sehemu muhimu ya kupambana na vitendo vya ukatili nchini. 

“Vituo hivi kwa nchi nzima ni kumi kwa hiyo akikisheni mnaanzisha Vituo hivi katika Mkoa wa Morogoro kwa kuwa ili ni agizo la serikali katika kuakikisha tunatokomeza vitendo vya ukatili”. Aliongeza Dkt.Ndugulile.

Akisoma taarifa ya Mkoa huo kwa Naibu Waziri Ndugulile, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Frank Jacob alisema kuwa mkoa wa Morogoro una jumla ya matukio 2,555 ya mimba za utotoni akiyataja matukio 1,160 kuripotiwa kutoka Dawati la Polisi mengineyo 895 kulipotiwa katika vituo vya Afya, mashuleni na jamii.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na viongozi wa mkoa wa Morogoro na baadhi ya watumishi wa Mkoa huo hawako pichani kuhusu madhumni ya kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo pia kupokea taarifa ya masuala ya Afya na Maendeleo ya Jamii ya Mkoa jana huo.
2
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akitoa ufafanuzi wa hali ya maendeleo sekta Afya na Maendeleo ya Jamii ya Mkoa wa Morogoro kwa  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kabla ya Waziri huyo kuanza ziara ya siku tatu Mkoani humo .
3
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Frank Jackob akitoa taarifa ya Mkoa wa Morogoro kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotombelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kupata taarifa ya Mkoa huo kabla ya kuanza ziara yake ya siku tatu  Mkoani humo.
4
Baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Morogoro wakifuatilia kwa makini maelezo na maagizo ya Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kabla ya kuanza ziara ya siku tatu Mkoani humo.
Picha Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

MKUU WA WILAYA NAMTUMBO SOPHIA KIZIGO AHAMASISHA VIJANA KUPIMA UKIMWI ILI KUJITAMBUA MAPEMA

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WANANCHI wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wameelezwa kuwa wana kila sababu za kuhakikisha wanakuwa na afya bora na salama, kwani afya ni muhimu na afya ni mtaji mkubwa katika maisha ya binadamu.

Pia wamehimizwa kupima afya zao kwa lengo la kutambua iwapo wamepatwa na maambukizi ya UKIMWI au laa, kwani kwa atakaepatwa na ugonjwa huo ataanza kutumia dawa ya ARV  na hivyo ataishi maisha marefu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo wakati akizungumza na wananchi kuhusu kampeni inayoendelea ya  kupambana  na UKIMWI na kujenga jamii yenye uelewa na furaha.Kizigo amesema mbele ya wananchi kuwa Serikali ilianzisha kampeni ya Furaha Yangu iliyozinduliwa kitaifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kwa Mkoa wa Ruvuma ilizinduliwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Agosti  31 mwaka huu 2018

"Wilaya ya Namtumbo tumeendelea na kampeni hii ikiwa na lengo kuu la kuongeza kiwango cha upimaji wa VVU hasa kwa wanaume na wananchi kwa ujumla. Hadi juzi Oktoba 18 mwaka huu wa 2018 Wilaya ya Namtumbo walipima wanaume 873 na 16 walipatikana na VVU ambao kati yao 13 wameshaanza dozi (ARVs)," amesema.

Ameongeza kuwa Wilaya ya Namtumbo wameendeleza jitihada hizo kwa kuanzisha ligi ya mpira wa miguu iitwayo Laigwanani Supwr Cup ambapo Laigwanani ni neno la kimasai linalomaanisha Kijana na lengo ikiwa ni kuhamasisha vijana kujitokeza kupima, kujitambua afya zao na watakaokutwa na VVU kuanza dozi mapema.Mkuu huyo wa Wilaya amewaambia wananchi hao kwa watakaobainika kuwa na virusi vya UKIMWI dawa zipo na wataishi miaka mingi na kwamba anajua vijana wanaogopa kupima kwa kuhofia njia ambazo wamezipitia.

Amewashauri wananchi kujitokeza na kupima afya na watambue afya ni mtaji muhimu katika maisha na ndio maana wilaya ya Namtumbo imeona umuhimu wa kampeni hiyo ya kuhamasisha kupima UKIMWI ikaendelea na lengo ni kihakikisha afya za wananchi zinakuwa salama.Pia amewashauri kwa wale ambao hawapo ndani ya ndoa wawe waache kujihusisha na ngono zembe na wasubiri hadi watakapoingia kwenye ndoa au wawe na wakishindwa basi wawe na mpenzi mmoja na wawe wanatimia mpira ili kujikinga na maambukizi.

Kizigo ameongeza ni vema vijana wakatambua wao ni Taifa la leo na kesho na hivyo kujilinda kwa kuwa na afya njema ni jambo la msingi kwani wakiwa na afya njema watakuwa na fursa ya kujituma kwa ajili ya maendeleo yao ,wilaya,mkoa na taifa kwa ujumla.
 Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akisalimiana na mmoja wa Marefa watakaokuwa wakichezesha Ligi hiyo ya mpira miguu iitwayo LAIGWANANI SUPER CUP, Lengo ikiwa ni kuhamasisha vijana kujitokeza kupima, kujitambua afya zao na watakaobainika kuwa na maambuziki ya VVU wataanza dozi mapema.

 Pichani Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akisalimiana na baadhi wachezaji wa timu walioshiriki  ligi ya mpira wa miguu iitwayo LAIGWANANI SUPER CUP, Lengo la kuanzishwa kwa Ligi hiyo ni kuhamasisha vijana kujitokeza kupima, kujitambua afya zao na watakaobainika kuwa na maambuziki ya VVU wataanza dozi mapema.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akikabidhiwa taarifa kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo,kabla ya kuanza kwa mchezo wa Ligi ya mpira wa Miguu iitwayo LAIGWANANI SUPER CUP.

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images