Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110004 articles
Browse latest View live

KAMISHNA MKUU WA TRA AFUNGUA FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI

$
0
0
Na Veronica Kazimoto -Dar es Salaam

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amefungua fainali za mashindano ya kumi na moja (11) ya vilabu vya kodi katika Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es salaam na Pwani yaliyofanyika leo katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati akiwahutubia wanafunzi na wageni waalikwa, Kichere amesema lengo la mashindano hayo ni kuwafundisha wanafunzi uzalendo na kukuza uelewa wao juu ya masuala mbalimbali ya kodi ili waweze kuelewa umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari. "Haya mashindano yanafanyika kama sehemu ya kujenga uzalendo kwa wanafunzi wetu ili waweze kuelewa umuhimu wa kulipa kodi na hatimaye waweze kulipa kodi kwa hiari maana tunasema samaki mkuje angali mbichi," alisema Kichere.

Ameongeza kwa kusema kuwa, "Sisi Mamlaka ya Mapato Tanzania tunasema kwamba elimu ndio kitu muhimu sana kwasababu watu wakielewa umuhimu wa kulipa kodi, tutakusanya kodi nyingi zaidi ambazo hutumika katika kuboresha huduma mbalimbali za jamii kama vile utoaji wa mikopo ya elimu ya juu, utoaji wa elimu bure, uboreshaji wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa, mabweni, nyumba za walimu na ununuzi wa vifaa vya maabara na kufundishia."

Aidha, Charles Kichere amebainisha kuwa, Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali inafanya mpango wa kuingiza mtaala wa somo la kodi kuanzia Shule za Msingi hadi vyuoni ili kujenga uzalendo wa kulipa kodi kwa hiari nchini. Mamlaka ya Mapato Tanzania ilianzisha vilabu vya kodi mwaka 2008 na mpaka sasa kuna jumla ya vilabu 226 Tanzania Bara vikiwa na jumla ya wanafunzi 27,250 ambao ni wanachama hai wa vilabu hivyo.

Mashindano ya mwaka huu yameshindanisha jumla ya shule 50 kutoka Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ambapo shule 28 zimeingia fainali zikiwa zimegawanyika katika makundi mawili, shule 18 zinashindana katika kujibu maswali wakati shule 10 zinashindana kuwasilisha mada mbalimbali zinazohusu kodi. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akiwahutubia wanafunzi na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa mwaka 2018 wa Shule za Sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani uliofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
Jopo la majaji likifuatilia na kutoa alama kwa makundi ya wanafunzi wanaojibu maswali mbalimbali yanayohusu kodi wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa mwaka 2018 yaliyofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanafunzi wa shule za Sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (hayupo pichani) wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa mwaka 2018 yaliyofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Zanaki Salma Mtanda akiwasilisha mada kuhusu mapato yatokanayo na uwekezaji wa rasilimali wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa mwaka 2018 yaliyofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.


WAZIRI LUGOLA AKUTANA NA WATENDAJI WAKUU WA IDARA ZAKE, AHOJI UTENDAJI KAZI WAO KWA KIPINDI CHA MWEZI AGOSTI HADI OKTOBA, 2018

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Wizara na Taasisi zake katika kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi kwa kipindi cha mwezi Agosti hadi Oktoba, 2018. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwa Waziri Lugola ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati meza kuu) akifuatilia kwa makini taarifa ya Jeshi la Polisi iliyokua inasomwa na Kamishna wa Polisi Jamii, Musa Ali Musa (kulia), kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Polisi nchini, katika kikao kilichokua kinajadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi kwa kipindi cha mwezi Agosti hadi Oktoba, 2018. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu akizungumza katika Kikao cha Watendaji Wakuu wa Taasisi za Wizara hiyo, kilichokuwa kinajadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi wao kwa kipindi cha mwezi Agosti hadi Oktoba, 2018. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Katibu ni Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akifurahi jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu, katika kikao cha Watendaji Wakuu wa Taasisi za Wizara yao (hawapo pichani), kilichokua kinajadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi kwa kipindi cha Mwezi Agosti hadi Oktoba, 2018. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

SERIKALI, ACACIA WASAINI HATI ZA MAKUBALIANO KUTEKELEZA MRADI WA MAJI SHINYANGA NA GEITA

$
0
0
Halmashauri za Wilaya ya Msalala, Shinyanga (Shinyanga)  Nyang'hwale (Geita), Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji) na Wadau wa Maendeleo ambao ni ACACIA Mining PLC (kupitia Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu) wamesaini hati za makubaliano ya kisheria kutekeleza  Mradi wa Pamoja wa Maji ujulikanao kama JOINT WATER PARTNERSHIP PROJECT (JWPP). 
Akizungumza wakati wa kutia saini makubaliano hayo (Legal Agreement) kijiji cha Ilogi halmashauri ya Msalala, Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo amesema katika mradi huo sehemu kubwa ya fedha za mradi zimetolewa na Serikali kupitia wizara ya maji na ACACIA Bulyanhulu Gold Mine Ltd ambapo pia halmashauri hizo tatu zinachangia kiasi cha fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za mradi huo kutoka katika makusanyo yake ya ndani. 

Mradi huu utanufaisha jumla ya vijiji kumi na nne (14) kutoka katika Halmashauri za Wilaya tatu ambapo kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga  vijiji viwili ambavyo ni Mwenge na Mahando vitanufaika na mradi huo.

Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akitia saini hati za makubaliano hayo (Legal Agreement) kutekeleza  Mradi wa Pamoja wa Maji ujulikanao kama JOINT WATER PARTNERSHIP PROJECT (JWPP). Wa kwanza kulia ni Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi,Benedict Busunzu. 
 Viongozi wa ACACIA na Serikali wakitia saini hati za makubaliano hayo (Legal Agreement).
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akishiriki kuchimba mtaro katika eneo la Kijiji cha Bushing'we halmashauri ya Msalala ambapo bomba la maji litapita.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

TANZIA: MSANII WA MAIGIZO NCHINI, MASHAKA AMEFARIKI DUNIA

$
0
0
Na.Khadija Seif, Globu ya Jamiii.

Aliyewahi kuwa Msanii wa maigizo wa Kundi la Kaole Ramadhani Ditopile maarufu kama Mashaka amefariki dunia mapema Leo asubuhi katika hospitali ya Amana jijini Dar es salaam.

Aidha marehemu Mashaka aliwahi kuonekana kwenye maigizo akishirikiana na waigizaji kama mama Ambiliki,  Cheni, Kisa ,Zawadi akiwa ameshiriki maigizo kama fukuto,sayari, maisha na mingine mingi.

Akizungumza na  wanahabari msanii mwenzie Zawadi amethibitisha kifo hicho na kwa sasa haijafahamika shughuli za msiba zitafanyika wapi.

Na mpaka sasa familia ya marehemu imekaa Kwenye kikao na watatoa taarifa kamili kuhusu maziko ya marehemu mashaka.

Innallillah wahina illah rajuun.

WAZIRI MKUU ATOA SIKU 25 KWA WATUMISHI CHAMWINO

$
0
0
*Ni wale washio nje ya kituo, wawe wamehamia ifikapo Desemba 15

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaametoa siku 25 kwa watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino wanaoishi nje ya kituo chao cha kazi wawe wamehamia.

Pia amemkabidhi Mkuu wa wilaya hiyo Bibi Vumilia Nyamoga orodha ya watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino ambao wanaishi nje ya kituo cha kazi kwa hatua zaidi. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Oktoba 20, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Chamwino.

“Ifikapo Desemba 15 mwaka huu watumishi wote wawe wamehamia katika kituo chao cha kazi. Sheria ya utumishi inamtaka mtumishi aishi katika maeneo ya kituo cha kazi.” Waziri Mkuu amesema lazima watumishi wote wa umma wafuate sheria, kanuni na taratibu za utumishi na atakayeshindwa kuhamia atakuwa amejiondoa kwenye utumishi.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wakuu wa idara na madiwani watambue vyanzo vyote vya mapato. Amesema baada ya kuvitambua wasimamie utaratibu wa ukusanyaji kwa njia ya kielekroniki ili kuiwezesha halmashauri kupanga miradi na kuitekeleza kupitia fedha za ndani.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge wakati alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chamwino,     Vumilia Nyamoga ordha ya watumishi ambao hawaishi kwenye kituo chao cha kazi cha Chamwino na badala yake wanaishi jijini Dodoma. Alikuwa katika mazungumzo na watumishi wa Halmashauri hiyo kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmshauri ya wilaya Chamwino kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya waziri Mkuu) 
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018. 

MAKAMU WA RAIS AZINDUA USHIRIKA WA MAMLAKA SACCOS ZANZIBAR LEO

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali zote mbili, yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt. Ali Mohamed Shein zinaamini kuwa vyama vya Ushirika ni njia muhimu sana ya kuzalisha ajira hususan kwa wanawake na vijana.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos uliofanyika katika ukumbi wa Abdul Wakiil, Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni, Zanzibar.Ushirika wa Mamlaka Saccos ulianza na wanachama 55 na mpaka sasa wakati wa uzinduzi wake una wanachama 250 pamoja na mambo mengine Ushirika huo umeshatoa mikopo bila riba shilingi milioni 93 kwa wanachama 133.

Makamu wa Rais aliwapongeza wanaushirika huo kwa kusema “Ni wazo zuri sana kama mtalisimamia na kulitekeleza ipasavyo kwa haika mtajikomboa kiuchumi na kubadilisha kwa kiasi kikubwa hali zenu za maisha”Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa Binafsi anaamini sana katika ushirika tena ushirika wa kuweka na kukopa kwani ni moja ya njia sahihi ya kujikomboa kiuchumi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewaomba wananchi wa Zanzibar kupinga kwa nguvu zote masuala ya udhalilishaji na ukatili kwa wanawake na watoto na kuwataka watoe ushirikiano na Serikali katika mapambano dhidi ya udhalilishaji pia aliwahimiza wananchi hao kutunza mazingira kwa faida ya sasa nay a baadae.

Wakati huohuo Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Mhe. Moudline Castico amewataka wanachama wa Saccos hiyo kufanya kazi kwa bidii na si kwa mazoea.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa ameshikilia bango lenye maneno ya uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos kama ishara ya uzinduzi rasmi, kushoto ni Mwenyekiti wa Ushirika Ndugu Mohammed Khamis Ali. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha picha yake aliopewa kama zawadi wakati uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos kama ishara ya uzinduzi rasmi, wengine pichani ni Waziri wa Kazi Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Mhe. Moudline Castico (kulia) kushoto ni Mwenyekiti wa Ushirika Ndugu Mohammed Khamis Ali. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos kwenye ukumbi wa Abdul Wakiil, Baraza la Wawakilishi la Zamani, Kikwajuni, Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos kwenye ukumbi wa Abdul Wakiil, Baraza la Wawakilishi la Zamani, Kikwajuni, Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

SHIRIKA LA GREAT HOPE WATOA TUZO KWA WASHIRIKI WA UWEZO AWARD

$
0
0
 SHIRIKA la Great Hope Foundation leo limetoa tuzo kwa washiriki wa mradi wa UWEZO AWARD katika sherehe zilizofanyika chuo kikuu cha Dar es Salaam leo katika shule za Sekondari za hapa nchini.

 Mradi huu unaendeshwa kwa njia ya mashindano ambapo wanafunzi hushindana kutumia uwezo wao kufanya kazi mbalimbali za kijamii ambazo wao wanachagua kufanya.

UWEZO AWARD ina malengo makuu matano ambayo ni  Kuwatengenezea wanafunzi jukwaa la kujitambua/kufahamu uwezo/vipaji walivyonavyo ( hata vile ambavyo havionekani zaidi darasani.

Kuwapa wanafunzi jukwaa la  kujifunza uongozi  Kuwapa wanafunzi jukwaa la kujifunza kuwajibika na kuwa mstari wa mbele kutatua changamoto zinazoikabili jamii inayowazunguka, Kutambua na kutoa tuzo kwa miradi bunifu iliyofanywa na wanafunzi katika UWEZO AWARD na  Kukuza na kuwajengea wanafunzi ujuzi katika maeneo ambayo wanafunzi wameonesha UWEZO.
Washindi wa kwanza wa tuzo za UWEZO AWARD wakipokea tuzo yao kutoka kwa mgeni rasmi Maida waziri mara baada ya kuibuka kidedea kwa kufanya vizuri zaidi katika mradi huo ulioendeshwa na shirika la Great Hope foundation jijini Dar es Salaam leo. Washiriki hao ambao ni kutoka shule ya sekondari ya Zanaki wamejinyakulia Tofi ya Silva pamoja na safari ya kutembelea mbuga za wanyama hapa nchini.
Washindi wa pili wa tuzo za UWEZO AWARD wakipokea tuzo yao kutoka kwa mgeni rasmi Maida waziri mara baada ya kuibuka kidedea kwa kufanya vizuri zaidi katika mradi huo ulioendeshwa na shirika la Great Hope foundation jijini Dar es Salaam leo.
Washindi wa tatu wa tuzo za UWEZO AWARD wakipokea tuzo yao kutoka kwa mgeni rasmi Maida waziri mara baada ya kuibuka kidedea kwa kufanya vizuri zaidi katika mradi huo ulioendeshwa na shirika la Great Hope foundation jijini Dar es Salaam leo.
  Washindi wa nne wa tuzo za UWEZO AWARD wakipokea tuzo yao kutoka kwa mgeni rasmi Maida waziri mara baada ya kuibuka kidedea kwa kufanya vizuri zaidi katika mradi huo ulioendeshwa na shirika la Great Hope foundation jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wanafunzi wakionyesha umahili wao katika michezo mbalimbali.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya jamii.

HOSPITALI YA MACHO YATOA HUDUMA YA KUPIMA MACHO LEO

$
0
0
 Daktari wa macho wa Hospitali ya Macho ya Kimataifa (The International Eye Hospital), Dk. Mahija Matola akimfanyia uchunguzi wa macho, Stanslaus Shanyeli wakati wa huduma ya upimaji wa macho bure ilisyoendeshwa kwa ushirikiano na Hospitali ya Heameda Medical Clinic ya Bunju B Dar es Salaam. Huduma hiyo ya bure ya siku mbili inatarajiwa kukamilika leo.
 Daktari wa macho wa Hospitali ya Macho ya Kimataifa (The International Eye Hospital), Dk. Mahija Matola akimfanyia uchunguzi wa macho mkazi wa Bunju B, Regina Mwakasungula wakati wa huduma ya upimaji wa macho bure ilisyoendeshwa kwa ushirikiano na Hospitali ya Heameda Medical Clinic ya Bunju B Dar es Salaam. Huduma hiyo ya bure ya siku mbili inatarajiwa kukamilika leo.
 Daktari wa macho wa Hospitali ya Macho ya Kimataifa (The International Eye Hospital), Dk. Mahija Matola akimfanyia uchunguzi wa macho mkazi wa Bunju B, Rehema Kasapale wakati wa huduma ya upimaji wa macho bure ilisyoendeshwa kwa ushirikiano na Hospitali ya Heameda Medical Clinic ya Bunju B Dar es Salaam. Huduma hiyo ya bure ya siku mbili inatarajiwa kukamilika leo.


Daktari wa macho wa Hospitali ya Macho ya Kimataifa (The International Eye Hospital), Dk. Mahija Matola akimfanyia uchunguzi wa macho mkazi wa Keko,Leornard Lawrence wakati wa huduma ya upimaji wa macho bure ilisyoendeshwa kwa ushirikiano na Hospitali ya Heameda Medical Clinic ya Bunju B Dar es Salaam. Huduma hiyo ya bure ya siku mbili inatarajiwa kukamilika leo.
 (Na Mpiga Picha Wetu)


Tanzania, DRC Zaanza Mazungumzo Ujenzi wa Kinu/Kiwanda cha Kuchenjua Colbat

$
0
0


Asteria Muhozya na Rhoda James, GEITA.

 Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Madini imeanza kufanya mazungumzo na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili iweze kujenga Kiwanda cha Kuchenjua madini ya Colbat nchini.
 Hayo yalibainishwa Oktoba 19, mkoani Geita  na Waziri wa Madini wa Tanzania Angellah Kairuki wakati wa kuhitimisha ziara ya siku Nne ya  Waziri wa Madini wa Kongo (DRC), Martin Kabwelulu aliyoifanya nchini kwa mwaliko wa Waziri Kairuki.

Kairuki alisema kuwa, nchi ya Kongo ndiyo mzalishaji mkubwa wa madini ya Colbat duniani ambapo asilimia 70 ya madini hayo duniani yanazalishwa nchini humo.Aliongeza kuwa, kwa sasa nchi hiyo inayo changamoto ya kusafirisha madini hayo yakiwa ghafi ikiwemo ukosefu wa umeme wa kutosheleza kwa ajili ya ujenzi wa viwanda hivyo.

“Tumekubaliana kuendelea na mazungumzo  na Kongo ili shughuli za uchenjuaji na uyeyushaji wa madini hayo ufanyike nchini  kwa kuwa tumeshaanza kuwekeza kwenye Vinu/viwanda  vya Kuchenjua na kuyeyusha madini mbalimbali. Hivyo, tunataka wayasafirishe makinikia ya Colbat hapa na tuyachenjue hapa,” alisisitiza Kairuki.

Akizungumzia matumizi ya madini hayo, Kairuki alisema kuwa, madini ya Colbat yanatumika kutengeneza betri na vihifadhi nishati (capacitor) ambazo zinahitajika sana hususan, kwenye magari yanayotumia umeme.bali na makubaliano ya ujenzi wa kiwanda hicho, pia Waziri Kairuki alisema kuwa nchi hizo zimekubaliana masuala kadhaa ikiwemo kuendelea kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa sekta ya Madini ili kuweza kunufaisha wananchi hasa wale wanaozunguka maeneo ya migodi.
 
 Waziri wa Madini Angellah Kairuki na mgeni wake Waziri wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) Martin Kabwelulu (wa pili kushoto) wakimsikiliza Mtaalam Mwelezi  Martin Sezinga Akiwaonesha mashine mbalimbali zinazotumiwa katika hatua mbalimbali za uzalishaji na uchenjuaji wa madini ya dhahabu katika mgodi wa mfano wa Lwamgasa.
PICHA 2- BUSOLWA
Waziri wa Madini Angellah Kairuki (kushoto) na Waziri wa  Madini wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Martin Kabwelulu wakiteta jambo baada ya kutembelea mgodi wa Busolwa Mining Ltd unaomilikiwa na Mtanzania, mkoani Geita
PICHA 3 KONGO TANZANIA
Meneja wa Mgodi wa Busolwa Mining Ltd, Flex Adoph akimweleza jambo Waziri wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Martin Kabwelulu (katikati) wakati alipotembelea katika mgodi huo kujifunza namna mmiliki wa mgodi huo alivyotoka katika uchimbaji mdogo hadi kuwa mchimbaji wa Kati lakini pia kujifunza namna mgodi huo unavyofanya shughuli zake za uchenjuaji na uzalishaji wa madini ya dhahabu. Anayeshuhudia ni Waziri wa Madini Angellah Kairuki.
PICHA 5 B
Waziri wa Madini wa  Angellah Kairuki na Mgeni wake Waziri wa Madini wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Martin Kabwelulu (Wa tatu kushoto) wakiangalia madini ya Dhahabu yanayozalishwa na kuchenjuliwa katika Mgodi wa Nsangano Gold Mine mkoani Geita walipoutembelea mgodi huo.

IGP SIRRO AELEZA HATUA KWA HATUA NAMNA MO DEWJI ALIVYOPATIKANA...INASIKITISHA

$
0
0
*Atangaza ms4ako mkali kuwasaka watekaji,agusia walivyotaka kuchoma gari kupoteza ushahidi 
*Silaha ya kivita,bastola zakutwa ndani ya gari ya watekaji ,atoa onyo kali


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JESHI la Polisi nchini limesema baada ya mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji 'MO' kupatikana, kwa sasa linaendelea na uchunguzi na msako mkali kuwakamata watekaji.

Akizungumza mchana huu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro amewaambia Watanzania leo kupitia vyombo vya habari kuwa MO yupo salama na kwa sasa wao ndio uchunguzi kama umeanza upya kubaini watekaji na lazima wapatikane aidha wakiwa hai au wamekufa.

 Amesema wametoa taarifa za tukio hilo kwa nchi jirani,hivyo waliohusika na utekaji huo wajue hawana pa kukimbilia kwani kokote watakaoenda watapatikana tu.

Pia amesema watekaji hao baada ya kumtupa mfanyabiashara huyo katika viwanja vya Gymkhana barabara ya ya Ghana jirani na Ubalozi wa Denmark walitaka kulichoma moto gari waliyoitumia yenye namba za usajili T 314 AXX lakini kwenye vioo vya pembeni kukiwa na namba za usajili AGX 404 MC yenye rangi ya blue nyeusi na ufito wa rangi ya shaba kwa chini kwa lengo la kupoteza ushahidi lakini hawakufanikiwa.

"Jeshi la Polisi linaendelea na msako kuhakikisha waliokuwa wamemteka mfanyabiashara huyo wanapatikana," amesema IGP Sirro na kusisitiza Jeshi la Polisi litahakikisha linafanikiwa kuwapa wahusika wa tukio hilo.

NAMNA MO ALIVYOPATIKANA 

IGP Sirro amesema kutokana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu Alhamisi ya Oktoba 10 mwaka huu ,anaufahamisha umma kuwa MO amepatikana akiwa mzima wa afya usiku wa kuamkia Oktoba 20 baada ya kutekelezwa na watekaji eneo hilo la Gymkhana.

Amesema taarifa za awali zinaeleza kuwa baada ya kutekwa mfanyabiashara huyo alifungiwa kwenye nyumba ambayo bado haijajulikana na kufungwa miguu na mikono huku wakimziba macho.

Ameongeza uchunguzi wa awali umebaini kuwa watekaji hao walitumia gari aina ya Toyota Surf yenye namba za usajili T 314 AXX lakini kwenye vioo vya pembeni ilikuwa na namba AGX 404 MC yenye rangi ya blue nyeusi.

 ATOA PONGEZI KWA SERIKALI, MO ,WANANCHI

Wakati huo huo IGO Sirro ametoa pongezi kwa Serikali,vyombo vya ulinzi na usalama, familia ya Mohamed Dewji ,waandishi wa habari na wananchi wote kwa ushirikiano mkubwa walioutoa katika kipindi chote ambacho mfanyabiashara huyo alikuwa ametekwa kwa jitihada walizofanya hadi kufanikiwa kumpata.

"Ninawaomba muendelee kushirikiana nasi kwa kutupatia taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa watuhumiwa wote wa tukio hili ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.Bahati nzuri watuhumiwa wamelitelekeza gari walilotumia kutekeleza azma yao mita chache kutoka eneo alipotelekezwa mfanyabiashara huyo.

" Ukaguzi wa kina wa gari hilo umefanyika na umewezesha kupatikana kwa bunduki aina ya AK 47 moja na risasi zake 16 ,bastola aina ya Glock 19 ikiwa na risasi 13, bastola aina ya P.Bereta ikiwa na risasi 3 na Gas Pistol 4.5 mm.Nitaendelea kuwapa taarifa kadri maendeleo ya upelelezi yatakavyokuwa yakipatikana,"amesema Sirro.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kutika viwanja vya Gymkhana,jijini Dar kuhusiana na tukio la kupatikana Mfanyabiashara Mohammed Dewji a.k.a MO

MICHUZI TV: ZANAKI SEKONDARI YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA UWEZO AWARD

MICHUZI TV: MRISHO MPOTO AZUNGUMZA UMUHIMU WA CHOO NA FAIDA ZA PAPAI KATIKA SEMINA YA FURSA 2018 TANGA

MICHUZI PRODUCTION: Rose's Send Off Party - Highlights

MICHUZI TV: WAZIRI UMMY AWATAKA WATANZANIA KUZALISHA BISKUTI HILI APIGE MARUFUKU UAGIZWAJI WA BIDHAA HIYO NJE

MICHUZI TV: MWASELELA AZUNGUMZIA FURSA ZA KIPATO ZINAZOPATIKANA KATIKA ELIMU MKOANI TANGA


NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: MUHOGO WA JANG'OMBE BY BI KIDUDE & CULTURE MUSICAL CLUB OF ZANZIBAR

$
0
0



Arab melodies from Zanzibar with the queen of Taarab, the 93 year old Bi Kidude Founded in 1958, the Culture Musical Club is Zanzibar’s premier taarab club. The orchestra performs widely at concerts in Zanzibar town, but also frequently travels overland with a fold-up stage and an electricity generator to bring its music to the rural areas as well. The club has released hundreds of songs on the local market and since 1988 they have had six releases on the international market.
The orchestra has had highly successful tours all over Europe in 1996, 1998, 2000, 2002, 2004, 2005 and 2007; in September 2006 they toured the US to high acclaim, in July 2007 the club performed in Japan. A North American tour is planned for the 2008-2009 season. Besides taarab, many club members are also active in kidumbak groups, smaller ensembles that play a more down-home dance-focused music. Both types of music are played on stage, contrasting the serene sound of orchestral taarab to the festive and sexually charged dance that is kidumbak. On its tours the club regularly features invited guest singers. The summer 2009 will include the legendary 93 year old Bi Kidude, the veteran diva of Zanzibar, who is now in her mid-90s but is still famous for breaking taboos, both in her sexually-explicit lyrics and her bravery for daring to sing with her face uncovered. Rajab Suleiman, qanun, kidumbak Ali Hassan, oud, violin, cherewa Kesi Juma, violin Makame Faki, vocals, violin Taimour Rukuni, accordion, mkwasa Mahmoud Juma, bass, cherewa Amour Haji, dumbak, sanduku Foum Faki, bongos, kidumbak Rukia Ramadhani, vocals, chorus Fatma Juma, chorus, dance, rika Bi Kidude, vocals Mgeni Khamis, chorus, danceBi Kidude (Fatuma binti Baraka), singer, born around 1910; died 17 April 2013 (RiP)

MHAGAMA AAGIZA NEEC KUFANYA TATHIMINI YA UHALISIA WA WANUFAIKA WA MIKOPO INAYOTOLEWA NA TAASISI ZA KIFEDHA

$
0
0
Na Emanuel Madafa, Globu ya Jamii Mbeya 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu anayeshughulikia Sera,Bunge, Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ameliagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kufanya tathamini ya wananchi walionufaika na mikopo iliyotolewa kwenye Taasisi za kifedha ili kubaini idadi halisi ya wananchi hao.

Ametoa kauli hiyo hii leo (Oktoba 20, 2018) wakati akifungua maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya kijamii yaliyofanyika katika viwanja vya Nzovwe Mbeya ambapo yalijumuisha wajasiliamali kutoka Wilaya 15 za Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.Amesema Lengo la kufanya tathimini hiyo ni kupata uhalisia wa wanufaika wa mikopo hiyo ili kuenenda sambamba na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imekusudia kuifanya Tanzania kuwa Nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo Mwaka 2025.

Aliongezea kuwa, tathimini hiyo itasaidia kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi dhidi ya Serikali yao hususani wenye mtizamo hasi kuwa serikali haijafanya jambo lolote kuwawezesha kiuchumi.“Tathimini hii itasaidia kuwa na utaratibu mzuri wa kutunza takwimu sahihi zinazoonesha uhalisia wa wanufaika pia italeta chachu kwa kuhakikisha maonesho haya yanafanyika kwa mzunguko na kutoa fursa kwa wananchi wengi hasa maeneo ya vijijini kufahamu mifuko na programu za uwezeshaji nchini”.Alisitiza Mhagama

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’i Issa aeleza kuwa ofisi yake itaendela kutekeleza kwa vitendo eneo la uwezeshaji wananchi kiuchumi na kuyachukua maagizo ya waziri ili kuhakikisha malengo yaliyoainishwa yanafikiwa.Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Albert Chalamila alipongeza juhudi zinazofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha wananchi wote wanawezeshwa kiuchumi na kujikwamua katika hali za umasikini na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo.

“Lazima tuendelee kuunga mkono jitihada za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa vitendo na kuhakikisha changamoyo ya ajira kwa vijana inakomeshwa na kuwa na Taifa lenye maendeleo na wananchi wake”.Alisema Chalamila.Aidha, kaulimbiu ya maonesho ya Mwaka huu inasema “Vikundi vya Kifedha, Programu na Mifuko ya Uwezeshaji ni Chachu ya Maendeleo ya Viwanda”.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisalimia wananchi walioshiriki katika maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya kijamii (hawapo pichani) yaliyofanyika Oktoba 20, 2018. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Programu ya malengo endelevu ya kuongeza ajira kwa vijana uliozinduliwa wakti wa maonesho hayo. 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’i Issa akihutubia wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya kijamii yaliyofanyika katika viwanja vya Nzovwe Mbeya Oktoba 20, 2018
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipokea maelezo ya nyaraka zilizoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kutoka kwa Mkurugenzi wa mifuko ya Uwezeshaji (NEEC), Bw.Edwin Chrisant wakati wa maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya kijamii yaliyofanyika katika viwanja vya Nzovwe Mbeya Oktoba 20, 2018 
Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa maonesho hayo. 

“SERIKALI KUCHUKUA HATUA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZINAZOVIKABILI VYAMA VYA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO” -DKT TIZEBA

$
0
0
Na Mathias Canal, WK-Iringa

Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania imeendelea kuchukua hatua stahiki katika kukabiliana na changamoto zinazovikabili vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba vinaleta tija kwa jamii.

Hatua zilizochukuliwa na serikali ni pamoja na kuchukua hatua za kiutawala na kidola kwa baadhi ya viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo waliojihusisha na wizi na ubadhirifu wa fedha katika vyama hivi, mfano; Alayabe SACCOS cha Karatu Mkoani Arusha, Mbinga Teachers SACCOS Mkoani Ruvuma na Ulanga Teachers SACCOS Mkoani Morogoro ambako baadhi ya viongozi na watendaji wamefikishwa mahakamani kwa vitendo vya ubadhirifu.

Vilevile, Kutengeneza mikakati ya kuhakikisha kwamba vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo haviendelei kutengeneza madeni yasiyokuwa na tija kwa jamii na kusaidia kuweka mikakati ya kupunguza madeni ambayo tayari yapo katika vyama vyetu vya ushirika wa Akiba na Mikopo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza umuhimu wa SACCOS nchini wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani hafla iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Sehemu ya wanachama wa vikundi vya akiba na mikopo wakifatilia hotuba ya Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani hafla iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Willium Vangimembe Lukuvi (Mb) mara baada ya kuwasili kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani hafla iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018.


Matukio Katika Picha Tamasha la Wajasiriamali wanawake Jijini Dodoma

$
0
0


Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile akisisitiza kuhusu hatua iliyochukuliwa na Serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo kupata alama ya ubora wa bidhaa wanazozalisha ili kuchochea ujenzi wa uchumi wa Viwanda ambapo Serikali inalipa gharama hizo kwa wajasiriamali wadogo, hayo ilikuwa wakati wa Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi.
Afisa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati Bw. Sileja Lushibika akieleza hatua zinazopaswa kufuatwa na mjasirimali ili kupata alama ya ubora kwa mmoja wa wananchi waliofika katika Banda la Shirika hilo wakati wa Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi.
Afisa Elimu, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bw. Paulus Oluochi akizungumzia umuhimu wa kuzingatia vipimo kwa wajasirimali wakati wa kufungasha na kuzalisha bidhaa mbalimbali ili kuchochea dhana ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda,hiyo ilikuwa wakati wa Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi.  
Sehemu ya mabanda ya wajasiriamali wanaoshiriki Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi kama yanavyoonekana katika picha. Picha zote na Frank Mvungi MAELEZO, Dodoma

WAZAZI WAHIMIZA KUUNGA MKONO ELIMU YA KUJITEGEMEA KWA WATOTO WAO

$
0
0
Na Tiganya Vincent
MKUU  wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla amewataka wazazi Mkoani Tabora kutowazuia watoto wao kushiriki katika shughuli mbalimbali za elimu ya kujtegemea kama vile ufugaji na utunzaji wa mifugo ya shughuli na kulima mashamba ya shule yao ili ziweze kuwajengea ujuzi utakaowasaidia baadaye.

Alisema elimu ya kujitegemea inamwezesha mwanafunzi hata kabla au baada ya kumaliza elimu yake ya Msingi kuwa na ujuzi wa kufanya shughuli mbalimbali kitalaamu ikiwemo  kuachana kilimo au ufugaji wa kizamani ambacho hakina tija.

Makalla alitoa kauli hiyowilayani Uyui mkoani Tabora wakati wa ziara ya viongozi wa Mkoa wa Katavi  kujifunza juu ya uendeshaji wa Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP –Tanzania ambao wanatarajia kuanza kuutekeleza katika eneo lao.

Alisema elimu ya kujitegemea itawasaidia watoto kutoa ujuzi walioupata shuleni na kuupeleka ujuzi huo kwa wazazi wao na hivyo kuwa na uzalishaji wa mifugo na mazao ya kilimo kwa tija.

“Mtoto akielimishwa juu ya upandaji kwa kuzingatia vipimo na mistari tangu shule atasaidia kuambukiza elimu hiyo kwa wazazi wake na hivyo kuwa na uzalishaji wa bidhaa nyingi kwa matumizi yao na viwanda vyetu” alisema.

Makalla alisema wazazi wakiona watoto wao wanafundishwa elimu ya kujitegemea kama vile ufugaji , kilimo cha kisasa, wasione kama ni adhabu bali ni faida kubwa wanayopatiwa watoto wao na jamii kwa ujumla.

Aidha Mkuu huyo wa Katavi na ujumbe wake umefurahishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kuinua elimu na kuongeza kipato katika shule mbalimbali mkoani Tabora chini ya Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP –Tanzania.

Alisema kwa kutumia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP –Tanzania Halmashauri kama ile ya Wilaya ya Tabora -Uyui imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Msingi ILolangulu kwa kiasi cha shilingi milioni 35.
 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla (mwenye miwani) akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Uyui mara baada ya kutembelea mradi wa ufugaji kuku  chini ya Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP wakati walipotembelea Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kujifunza.
 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla (mwenye miwani) akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui)  Said Ntahondi (kulia) wakiwa kwenye  moja wa madarasa wakati alipoongoza ujumbe kutoka Mkoa wake kuja Tabora kujifunza utekelezaji wa Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP.
 Afisa Taaluma Mkoa wa Tabora (RAO) Silvano Sichone akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP kwa ujumbe wa Mkoa wa Katavi  walipofika Mkoani humo kwa ajili ya kujifunza mafanikio yaliyotokana na mpango huo.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla miwani) alizungumza na walimu wa Shule ya Msingi Majengo(hawapo katika picha) wakati alipotembelea Mkoa wa Tabora kujifunza jinsi ya utekelezaji wa   Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP. Picha na Tiganya Vincent

KUSOMA ZAIDI BOFYA  HAPA
Viewing all 110004 articles
Browse latest View live




Latest Images