Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

Naibu Mkurugenzi Mkuu UNEP atembelea sekondari ya Jangwani ataka wasichana kujipanga kuwania nafasi za juu

$
0
0

Na Mwandishi wetu
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya amewataka wasichana nchini kujipanga vyema kutafuta maisha kwa kuzingatia fursa ambazo zipo.
Akizungumza baada ya kutembelea shule ya sekondari Jangwani ambayo na yeye alisoma katika miaka ya 1970 Mkurugenzi huyo alisema elimu ni mojawapo ya kitu muhimu katika kufanikisha malengo ya kuwa juu kiuchumi na kimadaraka.
Alisema nafasi za juu zinaweza kupatikana kwa kukazania elimu, kujituma kwa bidii na kujifunza kutoka kwa wengine hasa nchi zilizoendelea.
Alisema wakati yeye anasoma hapakuwepo na nafasi kubwa kwa wasichana lakini kwa sasa nafasi zipo wazi na wakijipanga vyema watakuwa miongoni mwa watu wanaoendesha uchumi na kutegemewa na familia zao.
Alisema kitu muhimu kwa wasichana waliopo sasa ni kujijenga kwa namna ambavyo wataweza kutumika vyema katika sekta zozote huku wakiendeleza uhusiano mzuri na familia zao ambazo ndio msingi wa mafanikio.
Katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya ziara yake hiyo ya kutia hamasa wasichana wa Jangwani alisema mazingira magumu yaliyoelezwa na Mkuu wa shule ya sekondari Jangwani  ataangalia namna ya kusaidia ingawa si moja kwa moja kulingana na nafasi yake.
Katika mazungumzo Mkuu wa shule hiyo yenye wanafunzi 1,470 , mwalimu Bi. Nyaibuli Boke alisema shulehiyo inakabiliwa na changamoto za mabweni kwani lililopo linakidhi mahitaji ya walemavu kwa asilimia 75 huku asilimia zilizobaki ni za wanafunzi wa kawaida.
Aidha alisema wana uhaba wa vitabu vya mchepuo wa Sanaa a na pia zana za walemavu za kujifunzia zikiwa pungufu.
Pamoja na changamoto zilizopo ambazo zilisababisha shule hiyo kushuka ufaulu, mwalimu Boke ambaye amehamishiwa hapo mwaka huu akitoka sekondari ya King’ongo iliyopo manispaa ya Ubungo, alisema wamejipanga kurejesha heshima ya shule hiyo.
Alisema kumekuwa na kamati ya mitihani, kurejesha hamu ya ufaulu na pia kuwa na mazungumzo na wazazi kwa wale wanafunzi ambao wanaonekana hawafanyi vyema kujua matatizo na kusaidia kuyatatua.
Alisema wamekuwa wakishirikisha wazazi kufanikisha kampeni ya kuzingatia kauli mbiu ya divisheni ziro na 4 mwiko.
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya akizungumza na wasichana wa Shule ya Sekondari Jangwani kuwamasisha kufanya vyema kwenye masomo yao alipotembelea shuleni hapo kuwashukuru walimu kwani bila wao asingefika hapo wakati wa ziara yake nchini jana jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa viungo wakimsikiliza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya (hayupo pichani) alipokuwa akiwapa hamasa ya kufanya vyema kwenye masomo yao ikiwemo na kujitambua wakati wa ziara fupi shuleni hapo jana jijini Dar es Salaam.
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya katika picha ya pamoja na wasichana wa Shule ya Sekondari Jangwani mara baada ya kuwahamasisha na kuwatia moyo wakati wa ziara yake fupi shuleni hapo jana jijini Dar es Salaam.
Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Jangwani, Bi. Nyaibuli Boke (wa pili kushoto), Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Ilala, Bi. Eliza Ngonyani (kulia) katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya (wa pili kulia) aliyeambatana na Afisa mwakilishi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa nchini, Bi. Clara Makenya (kushoto) alipofanya ziara fupi ya kutembelea shuleni hapo jana jijini Dar es Salaam.


 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Tigo Yamwaga Zawadi Kibao Kwenye Shindano la Tigo Fiesta 2018 Chemsha Bongo Trivia

$
0
0
 Mshindi wa Shindano la Tigo Fiesta 2018  Chemsha Bongo Trivia , Zam Mohammed Zam wa Mombasa Unguja akipokea shilingi milioni moja kutoka kwa Msimamizi wa Kampuni ya Tigo tawi la Zanzibar, Adolph Mapenzi baada ya kushinda katika promosheni hiyo, makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za Tigo ziliopo Malindi Unguja
Mshindi wa Shindano la Tigo Fiesta 2018 Chemsha Bongo Trivia toka Mkoa wa Tanga, William Alloyce Mganga(katikati) akikabidhiwa zawadi ya simu aina ya Tecno Camon X toka kwa Meneja Mauzo wa Tigo mkoa wa Tanga, Robert Kasulwa(kulia) na kushoto ni Msimamizi wa Duka la Tigo mkoa wa Tanga Hassani Nkua.

WAKANDARASI WAZAWA WAASWA KUACHA UBABAISHAJI WANAPOPEWA KAZI

$
0
0
Na, Vero Ignatus, Karatu
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameiagiza kampuni ya Kiure Engineering Ltd kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa daraja uliogharimu Sh. milioni 250 fedha zilizotolewa na serikali kwaajili ya ujenzi wa daraja hilo eneo la Getamok.

Gambo aliyasema hayo wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa daraja hilo ambalo ni muhimu kwaajili ya wakazi wa maeneo hayo.

Alisema kampuni ya Kiure Engineering Ltd imekuwa kikwazo kikubwa cha kutokamilisha ujenzi wa daraja hilo kwa muda uliopangwa hali iliyopelekea kuongezewa muda wa miezi nane ili wamalize ujenzi huo.

Amesisitiza kuwa lazima wakandarasi wazawa wakajithamini pale wanapoomba kazi za ujenzi wa aina mbalimbali za miradi ya maendeleo na kama hawana uwezo huo wa kufanya kazi ni vyema wakaacha kuepusha kuingia matatani kwani serikali inapotoa fedha kwaajili ya jambo fulani ni lazima likamilike kwa wakati.

"Tunawapa hadi Oktoba 23 mwaka huu daraja hili liwe limeshakamilika, na ikifika saa kumi jioni Mkuu wa Wilaya hii atakuja na OCD kuangalia kama mmekamilisha kinyume na hapo tutatumia nguvu za ziada kusukuma jambo hili''alisema Gambo.

Pia niwaonye nyinyi wakandarasi wazawa mjitathimini maana mnaomba kazi halafu mnaleta ubabaishaji wa mara kwa mara na hamkamilishi kazi zenu kwa wakati, kama hamuwezi kazi acheni " alisema Gambo.

Naye Msimamizi wa Mradi huo kutoka kampuni ya Kiure Engineering Ltd, Said Idd alikiri ni kweli wamechelewesha kukabidhi daraja hilo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mvua kubwa kunyesha mwezi Machi mwaka huu pia walipokuwa wakichimba udongo walikumbana na chemchem kubwa ya maji hali iliyopelekea kuchelewa kutekeleza ujenzi wa daraja hilo.

Alisema kwa sasa daraja hilo limekamilika kwa asilimia 90 na kazi iliyobaki hivi sasa ni kusambaza mawe na kuweka kingo za maji ikiwemo kurekebisha kasoro mbalimbali kwaajili ya kukabidhi kwa DC wa Karatu Bi. Theresia Mahongo.

Naye DC, Mahongo alisema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa daraja hilo na mara kwa mara alikuwa anaenda eneo hilo kuangalia ujenzi wake na kusisitiza kuwa ni vyema sasa wakandarasi wakapima uwezo wa kazi wanazotaka kuzifanya kwani uzembe wa mkandarasi huyo umepelekea kukatwa fedha zake za mradi huo baada ya kuzembea kazini.
Daraja la Kijiji cha Getamok linalosuasua kukamilika kwake kutokana na changamoto mbalimbali.

ISSA NAMPEPECHE NA HASHIMU CHISOLA WAPIMA UZITO KUZIPIGA OCTOBAR 20

$
0
0
Na Mwandishi wetu
BONDIA Issa Nampepeche na Hashimu Chisola wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa raundi kumi utakaofanyika jumamosi ya Octobar 20 katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala akizungumza wakati wa upimaji mratibu Ibrahimu Kamwe 'BigRaght' 

amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya kukata na shoka kwani wamejipanga kuinua mchezo wa masumbwi katika kitongoji cha mwananyamala na viunga vyake

mbali na pambano hili siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka kati ya Shabani Madilu atakaezipiga na Selemani Bangaiza na bondia machachari anaekuja kwa kasi ya ali ya juu Hamisi Maya atazipiga na Zumba Kukwe kutoka Kibaha Mkoa wa Pwani mpambano mwingine utawakutanisha Mbena Rajabu atakae oneshana umwamba na Fredy Masinde na Josephe Mbowe atazikunja na Mwinyi Mzengela 

aliongeza kwa kusema BigRight Sports and Arts Promotion imejizatiti kuinua vipaji vya mabondia chipkizi na kuwaendeleza wale walio katika chati ya juu kwa kuwandalia mapambano mbalimbali yakiwemo ya ubingwa wa taifa na yale ya ubingwa wa kimataifa

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua mpaka kujua kitu kamili katika mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchini kama vile Glove gumshirt clip bandeji bukta protecter na vifaa vingine.

MAONI YA MDAU: Tuiasaidie Polisi kukabiliana na watekaji watu

$
0
0
Na Evance Ng’ingo 

HIVI karibuni mfanyabiashara mkubwa nchini na Afrika nzima kwa ujumla, Mohamed Dewji, Moo alitekwa na watu wasiojulikana ambao hadi sasa jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka. Habari za kutekwa kwa Moo zimetangazwa kwenye vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi ambapo kwa namna moja au nyingine limetia dosari taswira ya nchi hii inayosifika kwa amani duniani.

Tukio hilo limewashtua watu wengi ndani na nje ya nchi huku akiombewa apatikane akiwa salama, lakini pia kuna watu ambao wanatumia tukio hilo kama mwanya wa kuikosoa serikali kwa madai ya kuwa imeshindwa kumpata mfanyabiashara huyo hadi sasa. Wapo ambao wanalibeza jeshi la Polisi kuwa limeshindwa kumsaka na kumpata mfanyabiashara huyo huku wengine wakidai kuwa limeshindwa kukabiliana na matukio ya utekwaji watu nchini.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Jeshi hilo hivi karibuni linaonesha kuwa mwaka juzi, walitekwa watu tisa ambapo watano walipatikana wakiwa hai na wanne hawajulikani walipo hadi sasa huku watuhumiwa sita wamekamatwa na kufikishwa mahakamani na mmoja aliuliwa na wananchi.

Mwaka 2017 walitekwa watu 27 ambapo 22 walipatikana wakiwa hai, wawili wamekufa huku watatu hadi sasa hawajapatikana watatu wamefariki huku watu 11 wamefikishwa mahakamani. Kwa mwaka huu Januari hadi Oktoba watu 21 walitekwa na Jeshi limewaokoa 17 huku wanne hawajapatikana hadi sasa na watuhumiwa 10 wamefikishwa mahakamani.
Kwa takwimu hizi zinaashilia kuwa jeshi hilo linaweza kukabiliana na matukio ya utekwaji nchini licha ya changamoto za kiteknolojia zinazolikabili. Binafsi ningependa kuwasihi wanasiasa na watu wengine mbalimbali kuwa na imani na jeshi hilo katika kumsaka na kumpata mfanyabiashara huyo tajiri.

Tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara mkubwa wa kiwango cha Mo ni la kwanza kutokea nchini hasa ikizingatiwa kuwa takwimu za waliotekwa hakuna mfanyabiashara wa kiwango cha Mo hivyo ni tukio linalohitaji umakini zaidi. Utekwaji wa aina hii unahitaji nguvu ya ziada katika kuukabili na kuwa jeshi la Polisi peke yake haliwezi kufanikisha bila ya kuwapo kwa ushirikiano thabiti wa wananchi.

Ushirikiano huo wa wananchi sio tu kuishia kusaidia kupatikana kwa Mo lakini pia ni pamoja na kushiriki katika kuwafichua watu wenye tabia za utekaji kwa ujumla. Jamii ikishiriki kikamilifu ni wazi kuwa matukio kadhaa ya utekwaji hayataendelea kuwapo nchini hasa ikizingatiwa kuwa tangia mwaka juzi kumekuwa na matukio ya aina hiyo.

Lakini pia ni lazima kwa hoteli na maeneo makubwa ambayo hutembelewa na watalii nchini kuhakikisha kuwa yanalindwa na walinzi kutokea kwenye kampuni zenye uzoefu na uwezo mkubwa wa ulinzi.

Pia ufungwaji wa kamera za kurekodia matukio ni muhimu zaidi katika kuwafichua kwa urahisi watekaji na wahalifu wengine kwa ujumla. Watanzania, wanasiasa, viongozi wa dini, wasomi na jamii nzima kwa ujumla tushirikiane kukemea matukio ya utekwaji wa watu ili kunusuru haiba ya nchi yetu.

RC Wangabo ataka “work plan” ujenzi wa VETA wenye thamani ya Bil.10.7

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametaka kupewa mpango kazi wa ujenzi unaoendelea wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) cha Mkoa, kinachojengwa katika mtaa wa Kaswepepe, kata ya Sumbawanga asilia, Wilayani Sumbawanga ili kufuatilia kwa ukaribu na kuweza kukosoa pale mkandarasi atakapokwenda kinyume na alichokiandaa.

Amesema kuwa kwa kufanya hivyo, itasaidia kukosoa maendeleo ya ujenzi mapema kabla mambo hayajaharibika na si kulalamika baada ya kukamilika kwa ujenzi na kulaumu ubadhirifu uliojitokeza wakati fursa ya kufuatilia ilikuwepo.

“Ningependa nipatiwe “Work plan” mpango kazi ambao mnao, hatua kwa hatua ili na mimi nikikaa kule najua mwezi lazima mko hatua Fulani, nikiona inafaa ntakuja kukagua, mwenyekiti wa ulinzi na usalama Wilaya nae apewe mpango kazi, Mstahiki Meya nae apewe ili tufuatilie kwa pamoja ili kama kuna mapungufu tuambiane mapema, tusingoje kuviziana kwamba hili limeharibika,” Alisisitiza.

Ameongeza kuwa kwenda vibaya kwa mambo na kufika mwisho itashindikana kurudisha nyuma na matokeo yake ni kumfunga mhusika aliyesababisha uharibifu wakati fedha za serikali zimekwishapotea na huku wananchi bado wanahitaji maendeleo. Ameyasema hayo alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa chuo hicho.

Kwa upande wake akisoma taarifa ya ujenzi Mkadiriaji majengo wa ujenzi huo Faraji Selemani alisema kuwa ujenzi huo utagharimu shilingi bilioni 10.7 hadi kukamilika kwake ambapo kutakuwa na majengo tisa yatakayohusisha fani mbalimbali pamoja na jengo la utawala.
Ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (mbele kulia) akitoa akitaka ufafanuzi juu ya uwakilishi wa majengo kwa mashimo yaliyochimbwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akitoa akitaka ufafanuzi juu ya uwakilishi wa majengo kwa mashimo yaliyochimbwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiangalia ubora wa matofali yatakayotumika katika ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) ambapo Mkandarasi alisema kuwa anatumia mfuko mmoja wa saruji kutoa matofali 20.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

IGP SIMON SIRRO AVUNJA UKIMYA KUTEKWA KWA MO

$
0
0
*Asema kuna gari wanaishikilia inayodhaniwa kuhusika katika kutekwa kwake
*Watu nane waendelea kushikiliwa, azungumzia umuhimu wa CCTV Kamera

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JESHI la Polisi nchini limesema wakati uchunguzi ukiendelea kuhusu kutekwa kwa Mfanyabiashara, Mohamed Dewji 'MO' wamefanikiwa  kuitambua gari inayodhaniwa kuhusika kwenye tukio hilo.

Pia limesema watu nane wanashikiliwa kutokana na tukio hilo ambapo wanaendelea kuhojiwa. Awali Jeshi hilo lilikuwa linawashikilia watu 27 lakini baada ya upelelezi limebaki na hao nane.Akizungumza leo na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema Polisi wanaendelea na upepelezi wa tukio la kutekwa kwa Mfanyabiashara huyo.

Kuhusu gari ambayo inasadikiwa kutumika kwenye tukio hilo IGP Sirro amesema kamera za CCTV zimewasaidia  kutambua gari iliyotumika kumteka Mo Dewji.Ametaja namba za usajili wa  gari hiyo ni AGX 404 MC ambapo amewaeleza waandishi wa habari limetoka nchi jirani na tayari wameshapata taarifa za mtu mwenye umiliki wa gari hilo.

Pia IGP Sirro ametoa rai kwa Watanzania wenye uwezo wa kuwa na silaha na wenye uwezo wa kifedha ni vizuri wakawa na silaha zao kwa ajili ya kujilinda na ni vema hata wasaidizi wao nao wakawa na silaha.

Alipoulizwa kuhusu Mo kuwa hai au laa, IGP amejibu kwamba hana jibu la swali hilo kwa sasa na kuhusu malengo ya watekaji amefafanua watakapopatikana waliohusika wataeleza lengo lao. Ameonya watu wanaotaka kuchafua taswira ya nchi  kwa kufanya tukio hilo na wakipatikana watakiona cha moto.

Kuhusu Jeshi la Polisi kuendelea kuaminika IGP Sirro amewaomba watanzania kuendelea kuwaamini kwani linafanya kazi kubwa na wamefanikiwa kuifanya nchi kuendelea kuwa salama huku akifafanua huko nyuma kulikuwa na matukio mengi lakini Polisi wamedhibiti matukio ya hayo.

"Jeshi la Polisi limefanikiwa kudhibiti matukio mengi ya uhalifu nchini kwetu bila kuomba msaada kutoka nchi nyingine. Kwanini hilo tukio la kutekwa Mo tuombe msaada wa mataifa mengine. Tunao uwezo mkubwa na tumesomea hivyo hatuna mashaka na kazi tunayoifanya na hatuna sababu ya kuomba msaada," amesema IGP Sirro.Amefafanua sababu za kumtaka mtu kuja kusaidia Tanzania kwa ajili ya uchunguzi ni kwa ajili ya nini wakati Jeshi la Polisi liko imara na wamesomea mambo ya upelezi na wanaoweledi wa kutosha.

Kuhusu familia ya Mohammed Dewji amesema kwamba wamekuwa wakiwasiliana na familia hiyo ambayo inalishukuru Jeshi la Polisi kutokana na jitihada zinazofanyika kuhakikisha Mo anapatikana."Ni siku ya tisa leo Jeshi la Polisi halilali kwa ajili ya kumtafuta MO. Kama familia ya MO itakuwa haina imani na Polisi hilo litabaki kuwa la kwao lakini ukweli wanatushukuru sana kwa kazi tunayoifanya," amesema.

Hata hivyo amesema kwa sasa kuna tatizo kwamba kila mtu anataka kuwa mpelelezi na kama kazi hiyo waliipenda wangeanda chuo cha polisi kusomea.
Amesema Jeshi la Polisi linapokea mawazo mazuri yenye kufanikisha kupatikana kwa MO lakini si mawazo yenye mlengo wa kupotosha ambayo kwao hawana nafasi .

Wakati huo huo amesema kumekuwa na kasumba siku hizi hata Mtoto akipotea Kanisani utasikia wanasema ametekwa au  mtu kapotea nyumbani kwake utasikia katekwa lakini ukweli  kuna mazingira ya aina yake.

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WAWILI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Japan hapa nchini Shinichi Goto Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto mara baada ya kupokea Hati zake za Utambuliso Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto mara baada ya kupokea Hati zake za Utambuliso Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto mara baada ya kupokea Hati zake za Utambuliso Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Georgia hapa nchini Zurab Dvalishivili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mteule wa Georgia hapa nchini Zurab Dvalishivili  mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Georgia hapa nchini Zurab Dvalishivili  mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Georgia hapa nchini Zurab Dvalishivili  mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Georgia hapa nchini Zurab Dvalishivili  mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WAWILI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Japan hapa nchini Shinichi Goto Ikulu jijini Dar es Salaam.
3-Japan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto mara baada ya kupokea Hati zake za Utambuliso Ikulu jijini Dar es Salaam.
4-Japan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto mara baada ya kupokea Hati zake za Utambuliso Ikulu jijini Dar es Salaam.
5-Geogia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Georgia hapa nchini Zurab Dvalishivili Ikulu jijini Dar es Salaam.
7-Georgia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mteule wa Georgia hapa nchini Zurab Dvalishivili  mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.. PICHA NA IKULU

RAIS MAGUFULI KUTANA NA TAIFA STARS, AWAPATIA MILIONI 50

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametoa kiasi cha Milioni 50 kwa timu ya Taifa ya Tanzania.

Fedha hizo ni  kwa ajili ya safari ya mchezo wa marudiano baina ya Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' dhidi ya Lesotho utakaochezwa Novemba 16.

Akiwa anazungumza na wachezaji na viongozi katika hafla ya chakula cha Mchana Ikulu Jijini Dar es Salaam, Dkt Magufuli amesema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya safari na sio kwa wasindikizaji.

“Nawapa Millioni 50 kwa ajili ya safari ya Lesotho, fedha hizi zitumike kwa ajili ya wanaotakiwa kusafiri tu, sio mambo ya wachezaji 15, viongozi wasindikazaji 30. Haya mambo yafikie mwisho.” amesema Dkt Magufuli.

Mbali na hilo amewataka wachezaji kujituma na kuacha mambo ya kihuni, "Wachezaji wasipoacha uhuni watakuwa wanafunga magoli mengine ila ya uwanjani watashindwa"

Taifa Stars  katika mchezo uliopita dhidi ya Cape Verde walifanikiwa kuondoka na ushindi wa goli 2-0 mechi iliyopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa na kufikisha jumla ya alama 5 akishika nafasi ya pili nyuma ya Uganda.

NHIF YATUMIA MAAFALI YA SHULE YA MSINGI KANA CENTRAL ENGLISH MEDIUM KUTOA ELIMU YA TOTO AFYA KADI

$
0
0
MFUKO wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umewapa mbinu bora za wazazi na walezi kuwapa zawadi muhimu watoto wao katika maisha yao ni kuwaingiza kwenye mpango wa Toto Afya kadi ili waweze kunufaika na huduma za matibabu.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga Ally Mwakababu wakati akizungumza na wanafunzi na walezi kwenye mahafali ya nane ya darasa la Saba katika shule ya Kana Central English Medium Primary School.

Alisema wakati wa ukuaji wa watoto wamekuwa wakikumbana na magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kupelekea kukwamisha ndoto zao lakini wanapokuwa wameandikishwa kwenye mpango wa Toto Afya Kadi wanaweza kupata matibabu kwenye vituo mbalimbali vya Afya.

“Nimekuja hapa kwa lengo kuu moja kuhamaisha umuhimu wa wazazi na walezi kuwapa zawadi ya Bima watoto wao kupitia mpango wa Toto Afya Kadi kwani hakuna anayweza kuelezea gharama za matibabu wakati mtoto wake anayweza kuungua”Alisema.

Hata hivyo alisema kwamba wazazi wanapowaingiza watoto wao kwenye mpango huo unawapa uhakika wa matibabu na wanaweza kuwa na kumbukumbu nzuri ya maisha yao . 
 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza wakati wa mahafali ya 8 ya Darasa la Saba katika Shule ya Kana Eglish Medium Central  School ya Jijini Tanga ambapo alitumia nafasi hiyo kuhamasisha mpango wa Toto Afya Kadi kwa watoto na wazazi.
 Afisa Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Nico Kasebwa kushoto akisisitiza jambo kwa mmoja wa wananchi wa Jiji la Tanga aliyefika kwenye banda lao kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo uli kuweza kunufaika na huduma za matibabu wakati wanapougua kushoto ni Afisa Uanachama NHIF Jesca Nyau
 Afisa Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Nico Kasebwa akimuonyesha kitu kwenye kipeperushi chenye maelezo ya Mpango wa Toto Afya Kadi mkazi wa Jiji la Tanga Daudi Mbisco mara baada ya kutembelea banda lao
 Sehemu ya wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.

DKT TIZEBA AWATAKA WAKULIMA WA NYANYA IRINGA KUCHANGAMKIA FURSA YA UZALISHAJI SOKO LIPO

$
0
0

Na Mathias Canal-WK, Mseke-Iringa

Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), amewataka wakulima wa nyanya Mkoani Iringa kuchangamkia fursa ya kuongeza uzalishaji wa nyanya ili kuakisi uhitaji wa viwanda vya nyanya ikiwa ni pamoja na kiwanda cha Darsh chenye uwezo wa kusindika Tani 250 za nyanya kwa siku.

Waziri Tizeba ametoa mwito huo jana Octoba 18, 2018 wakati akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Kiwanda hicho kinafanya shughuli za ukusanyaji wa nyanya kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa na mikoa ya jirani na kufanya usindikaji wa nyanya ambapo hupeleka kiwanda cha Arusha kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na nyanya ambazo huuzwa ndani na nje ya nchi.

Waziri Tizeba, aliwataka wakulima hao kujiunga kuanzisha kikundi cha ushirika ili kuwa na urahisi wa mikopo ili kuwezesha uwezo wa uwekezaji kupitia kilimo cha umwagiliaji kitakachoongeza tija katika kipato chao na jamii kwa ujumla.“Wakulima wa nyanya hapa Igwachanya na hata katika maeneo mengi nchini wanalima kwa kutegemea mvua na uzalishaji huwa mdogo na usiokidhi mahitaji ya soko hivyo nawasihi kuongeza uzalishaji wa nyanya kwani soko la uhakika lipo” Alikaririwa Dkt Tizeba

Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), (katikati) akikagua mtambo wa kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela (Kulia) wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018. Mwingine Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Darsh Ndg Bhadresh Pandit. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakifatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), alipotembelea na kukagua kiwanda cha Darsh jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), (katikati) akikagua mitambo ya kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela (Kulia) wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
aziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), akikagua mitambo ya kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018.



DK.MABODI AMUOMBEA KURA MGOMBEA WA CCM JANG’OMBE

$
0
0

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR. 

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amewatahadharisha wanachama wa chama hicho, kuwa makini kwa kuepuka propaganda na njama chafu zinazofanywa na viongozi wakuu wa CUF waliotengeneza migogoro bandia ili waweze kupata huruma ya wananchi kuingia madarakani. 

Tahadhari hiyo aliitoa wakati akimnadi mgombea wa nafasi ya Uwakilishi kwa tiketi ya CCM Ramadhan Hamza Chande katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang’ombe huko katika Uwanja wa Kwaalinatu. Alisema CUF wametengeneza mgogoro bandia wenye lengo la kuiyumbisha CCM mwaka 2020 mbinu dhaifu ambazo hazitoweza kufanikiwa mbele ya CCM ya sasa iliyokuwa imara na inayokwenda sambamba na ulimwengu wa siasa za Kisayansi. 

Dk. Mabodi alisema ushahidi pekee wa kuonyesha kuwa viongozi wa CUF hawana uadui kwa upande wa Zanzibar na Tanzania bara ni pale waliposhirikiana kumnadi mgombea wa Chama hicho katika kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Liwale ambao mgombea wa CCM ameibuka mshindi. Akimnadi na kumuombea kura Mgombea wa CCM katika Uchaguzi wa mdogo wa Jimbo la Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande, Dk. Mabodi aliwasihi Wana-CCM na wananchi wa Jimbo hilo kumchagua mgombe huyo ili aendeleze mambo mema yaliyoasisiwa na viongozi wa waliopita wa nafasi hiyo. Alisema CCM imempitisha Ramadhan ikiamini kuwa ana uwezo na anafaa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa kasi kubwa. 

“Mgombea huyo ni mbunifu, mchapakazi na mwenye uzalendo wa kweli nakuombeni wananchi wa Jang’ombe mfanye maamuzi sahihi ya kumpa kura nyingi za ndio aweze kuwatumikia kwa uadilifu. 
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saadalla ‘Mabodi’ (kulia), akimnadi na kumuombea kura mgombea wa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande(kushoto) katika kampeni za CCM Uchaguzi wa Jang’ombe zilizofanyika Uwanja wa Kwaalinatu.
BAADHI ya Wana –CCM walioudhuria katika Mkutano huo wa kampeni uliofanyika Kwaalinatu.
Mgombea uwakilishi wa CCM Jimbo la Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande akiomba kura kupitia mkutano huo wa kampeni uliofanyika uwanja wa Kwaalinatu.
MKE wa Rais mstaafu wa awamu ya nne ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akimuombea kura Mgombea wa tiketi ya CCM Uchaguzi wa Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande. 

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU IMEMWONDOLEA MASHTAKA MFANYABIASHARA LAUWO

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuondolea mashtaka mfanyabiashara Peter Lauwo aliyetakiwa kuunganishwa katika kesi ya utakatishaji fedha  pamoja na viongozi wa Simba na mfanyabiashara Hans Pope kwa sababu hayupo.

Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi la kumuondoa mshtakiwa Lauo chini ya kifungu cha 91 (1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Aliwasilisha ombi hilo, Wakili wa serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro ameieleza mahakama kuwa, Laou aliahidi kuwa angejisalimisha Takukuru Jana ili leo aletewe hapa mahakamani lakini hajatokea. 

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amekubaliana na ombi na mashtaka dhidi ya lauo yameondolewa nchini ya kifungu cha 91 (1) cha sheria mwenendo wa sheria ya makosa ya jinai.

 Baada ya kuondolewa na Laou, upande wa mashtaka unewasomea maelezo ya awali (PH)  Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva, Makamu wake, Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu na mfanyabiashara Hans Pope.

 Akisoma PH, Kimaro amedai, Machi 12.2016 klabu ya Simba ililipwa USD 319,212 na Timu ya Etoile ya Tunisia kama Malipo ya mchezaji Emmanuel Okwi ambazo ziliwekwa kwenye benki ya CRDB tawi la Azikiwe account ambayo mtia saini wake alikuwa ni Aveva na Kaburu.

Amedai kuwa, Machi 3.2016 kiasi cha USD 300,000 zilihamishwa kwenda kwenye akaunti binafsi ya mshtakiwa Aveva iliyoko katika benki ya Barclays iliyopo mtaa wa Ohio ambayo Aveva ndio mtia saini baada ya kisainiwa na yeye Aveva pamoja na Kaburu.

Kimaro ameendelea ameendelea kudai kuwa, uhamishwaji wa fedha hizo haukuwa na Baraka na ya kamati tendaji ya klabu ya Simba sababu fedha hizo zinadaiwa kuwa zilikopwa na klabu ya Simba.

Imedaiwa, fedha hizo zilianza kuamishwa kidogo kidogo, mwanzo Aveva alihamisha USD 62,183 kwenda kwa kampuni ya Ninah... Kama malipo ya kununua nyasi bandia kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa klabu ya Simba uliopo Bunju Kinondoni. Na kwamba USF zililipwa kwa Lauo kwa ajili ya kujenga uwanja huo huku wakijua kuwa kampuni ya Laou haijasajiliwa na bodi ya wakandarasi.

Hata hivyo, washtakiwa Aveva na Kaburu walikubali anuani zao tu na kukan tuhuma zinazoqakabili huku Hanspope akikubali anuani yake na kusema kuwa, ni kweli alifanya mchakato manunuzi ya nyasi bandia.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wote wanashtakiwa na makosa kumi yakiwemo ya Kughushi,kuwasilisha nyaraka za uongo kula njama, matumizi mabaya ya madaraka, utakatishaji na kuwa kuwasilisha nyaraka za kughushi na kuendesha biashara bila 
 sheria.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 31, mwaka huu, kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.
Mfanyabiashara Hans Pope akitoka nje ya mahakama ya hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili pamoja na viongozi wa Simba.
viongozi wa Simba wakitoka katika mahakama ya hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashtaka anayowakabili.

MAREKANI YAISHAURI TANZANIA KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu jamii
KAIMU Balozi wa Marekani hapa nchini Dk. Imni Patterson, ameishauri Tanzania njia muhimu za kifikia uchumi wa kati na wa viwanda.

Ushauri huo ameutoa leo jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Geoffrey Mwambe wakati wa mazungumzo yao ambayo yalihusu kujadili namna ya kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.

Pia Kaimu Balozi huyo ameihakikishia Serikali ya Tanzania kwamba itatoa kila aina ya ushirikiano ili kufanikisha Tanzania ya viwanda.

"Ubalozi wa Marekani,nchi ya Marekani na Wamarekani wote waliopo nchini Tanzania wapo tayari kusaidiana na serikali katika kuhakikisha nchi ya viwanda inafanikiwa," amesema.

Dk.Imni ameshauri 
kwa Serikali ya Tanzania kuwa ili ifanikiwe kwenye uchumi wa viwanda ni vema ikaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kufanikisha uwekezaji na amefurahishwa na mazungumzo ambayo ya Serikali ya Tanzania inayoyafanya kati yake na sekta binafsi.

"Hakuna nchi ambayo inaweza kufikia nchi ya viwanda bila kushirikisha sekta binafsi pamoja na wawekezaji wa ndani na nje.Hivyo ni vema sekta binafsi zikapewa fursa katika uwekezaji ili kufikia Serikali ya Viwanda ambayo sisi tunaiunga mkono," amesema.

Kuhusu mazungumzo yao amesema yamejikita katika kukuza biashara ,uwekezaji na kukuza uchumi na kwamba kutokana na mazingira mazuri yaliyopo ni imani yao Tanzania itafikia malengo ya kuwa nchi ya viwanda.

Kwa upande wake Mwambe amesema TIC jukumu lao ni kukutanisha sekta mbalimbali za Serikali na binafsi ambapo mabalozi wa Tanzania waliopo nchi mbalimbali wanahakikisha wanashiriki kikamilifu kuvutia wawekezaji.

Amefafanua hivyo ubalozi wa Marekani nchini kupitia Kaimu Balozi wake wamekuwa na wajibu wa kuhamasisha uwekezaji baina ya nchi hizo mbili.

"Ni jukumu lake kuhamasisha wawekezaji wa Marekani kuja Tanzania kuwekeza.Tunafahamu juhudi za Serikali ya Marekani katika kuisaidia Tanzania kwa kuhakikisha inajiimarisha kiuchumi," amesema.

Amesema jitihada za Kaimu Balozi zimesaidia kufanikisha kwa ujio wa kundi la wafanyabiashara wa Florida kuja nchini kwa ajili ya kuangalia mazingira ya uwekezaji na kwamba watakuja siku za karibuni.

" Tumezungumzia maeneo mbalimbali ambayo tunaweza kushirikiana ili kutimiza malengo ya Serikali ya kutekeleza uwekezaji nchini. Kama nchi tunataka kuendelea,lazima tutafute njia sahihi za kuendeleza mifumo ya uwekezaji.

"Tunataka kujenga nchi,hivyo tuna jukumu kubwa la kujenga sekta binafsi na tukiwa na private sekta tutakwenda vizuri kama Taifa.Sisi TIC tutahakikisha sekta binafsi inaimarika na maamuzi ya Serikali ni kuijenga sekta binafsi na mjumbe wa bodi yangu ni mtu mmoja kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Bw.Godfrey Simbeye," amefafanua.

Ameongeza Serikali yenye rushwa huwa haikusanyi kodi na huo ni msemo maarufu wa Mwalimu Nyerere, hivyo jukumu lililopo ni kuhakikisha rasilimali zilizopo zinatunufaisha wote."TIC tunataka kutengeneza umoja na mazingira yanayokubalika kwenye uwekezaji zaidi". 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geoffrey Mwambi(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya kufanya mazungumzoa Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Dk.Imni Patterson.

ULEGA AENDELEA NA ZIARA MKURANGA, AHIMIZA AMANI NA WAFUGAJI KUJISAJILI

$
0
0
Na Emmanuel Massaka, Blogu ya jamii
MBUNGE wa Mkuranga na Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega ameendelea na ziara ya kukagua na kuhamasisha miradi ya mandeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi.

Akizungumza na wananchi wa Nganje ulega amesema kuwa maisha ni ya kutegemeana baina ya wavuvi na wakulima hasa katika kujenga uchumi wa nchi.

Aidha amesema kuwa lazima wanakijiji lazima watambulike katika vijiji wanavyoishi na kuishi kama familia na kuheshimu kamati za masuluhisho kwa kuwa hakuna sababu za kuishi kwa kuhitilafiana.

Aidha Ulega amesema kuwa suala la amani na kuishi kwa amani,na ameagiza kata ya Magawa kwa mwezi mmoja kuwatambua wasiotambulika katika vijiji vyao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Juma Abeid amesema kuwa halmashauri wametenga kiasi kama cha shilingi milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo.

Aidha kuhusu bima ya afya amewashauri wananchi kutumia fursa iliyopo katika kuhakikisha suala la afya linapewa kipaumbele kwa kuwa sasa limerahisishwa kwao.

Chama cha Mapinduzi alichangia kwaajili ya kuboreha miundombinu mbalimbali 3,400,000/=Alichangia 6,900,000/_ kwanjli ya maendeo ya  Kata Mdonga ,Magawa , Beta, Lukanga

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb) wa Mkuranga,Abdallah Ulega akimkabidhi Mwenyekiti wa halmashauri na Diwani kata ya Magawa, Juma Abed vitanda viwili  vya kujifungulia.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,(Mb)wa Mkuranga,Abdallah Ulega  akimkabidhi Mwenyekiti wa halmashaul ya Mkuranga,Juma Abed mabati kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya  kata ya Magawa Wilaya Mkuranga mkoa wa Pwani.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na (Mb) wa Mkuranga, Abdallah Ulega  akiwa kwakushiriki na Mwenyekiti Halmashaul wakikabidhi vijana wa kata ya Magawa mipila kumi kwaajili ya mazoezi.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globa ya jamii)

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA BAHI, AZINDUA DARAJA LA CHIPANGA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo orodha ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ambao bado hawajahamia Bahi na wananishi mjini  Dodoma licha ya serikali kuwataka wahame, ili awachukulie hatua. Alikuwa katika kikao na Watumishi wa Halmashuri hiyo, Oktoba 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa  wilaya hiyo, Oktoba 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka  katika moja kati ya nyumba sita za walimu alizozikagua katika Shule ya Sekondari ya Mpalanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2019. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi  Athumani. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwasalimia wananchi baada ya kukagua ujenzi wa nyumba sita za walimu katika shule ya Sekondari ya Mpalanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2018.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua  daraja la Chipanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Bilinith Mahenge, Wanne kushoto ni Mbunge wa Bahi,   Omary Badwel na wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Athumani. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua daraja la Chipanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo na wapili kushoto ni Mbunge wa Bahi,   Omary Badwel. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Bahi, Kassim Kolowa  (kushoto) kuhusu vifaa vilivyopo kwenye chumba cha upasuaji cha Kituo hicho  wakati alipokitembelea, Oktoba 19, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Athumani. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Bibi Subi Mchome, ambaye ni mmoja wa wazazi waliojifungua salama katika wodi ya wazazi ya Kituo cha Afya cha Bahi  mkoani Dodoma, Oktoba 19, 2018. Wapili kushoto ni Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Kassim Kolowa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mtalaam wa Maabara, Petronila Olomi  (kushoto) wakati alipotembealea Maabara ya Kituo cha Afya cha Bahi mkoani Dodoma, Oktoba 19, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , Selemani Jafo na Wapili kushoto ni Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Kassim  Kolowa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wagonjwa wa nje wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Bahi mkoani Dodoma, Oktoba 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI PAMOJA NA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ambao walifika Ikulu jijini Dar es Salaam pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Miguu la Tanzania TFF, BMT pamoja na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Jezi ya Timu ya Taifa kutoka kwa Nahodha wa Timu hiyo Erasto Nyoni Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Nahodha wa Timu hiyo Erasto Nyoni mara baada ya kumkabidhi Jezi ya Timu ya Taifa.
 Beki wa Timu ya Taifa Shomari Kapombe akijitambulisha mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwakabidhi Shilingi milioni 50, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na viongozi wa TFF ili zitumuke katika maandalizi ya mechi inayokuja ya kuwania kufuzi AFCON nchini Cameroon. Wengine katika picha ni Rais wa TFF Wallace Karia, Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa Erasto Nyoni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo mara baada ya kukabidhi Shilingi milioni 50 kwa TFF kwa ajili ya Maandalizi ya  Timu ya Taifa Ikulu jijini Dar es Salaam. P
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Tanzania Taifa Stars mara baada ya kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha mstari wa Mbele ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe watatu kutoka kushoto, Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga watatu kutoka kulia akifatiwa na Leodgar Tenga Mwenyekiti wa BMT, kocha wa timu ya Taifa Emanuel Amunike Pamoja na Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao. Wengine ni Rais wa TFF Wallace Karia akiwa pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa Erasto Nyoni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Nahodha wa Timu ya Taifa Erasto Nyoni mara baada ya kupiga picha ya pamoja na Timu ya Taifa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kipa wa Timu ya Taifa Aishi Manula mara baada ya kupiga picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Beki kisiki wa Taifa ya Tanzania Kelvin Yondani mara baada ya kupiga picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU

MAHAKAMA IMEWAASA MAJAJI NCHINI KUZINGATIA SHERIA ZILIZOPO KULINGANA NA MAZINGIRA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii
MAHAKAMA imewaasa Majaji nchini kuzingatia sheria  zilizopo kulingana na mazingira ya Taifa na Jamii kwa ujumla katika mchakato mzima wa kutoa maamuzi ili kimuweza kutenda haki na usawa.

Wito huo umetolewa na majaji wastaafu wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, jaji Rugazia, John Mjemmas na Agathon Nchimbi wakati wa hafla fupi ya kuwaaga kitaaluma iliyofanyika mapema leo Oktoba 19.2018  katika ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Jaji Nchimbi amewakumbusha majaji na mahakimu kuhakikisha kuwa  wanakuwa waaminifu wakati wanatimiza majukumu yao kama maofisa wa mahakama ili mwisho wa Siku kila mmoja aweze kuona haki imetendeka.

Amesema, kwa kuwa mahakama ni chombo cha kutoa haki basi ni muhimu kuzingatia sheria zilizopo kulingana na mazingira ya taifa na Jamii katika mchakato mzima wa kutoa haki, Maamuzi yawe ya haki na usawa siyo tu hivyo  bali yaonekane kuwa ya haki na usawa" Amesema Jaji Nchimbi.

Aidha amewaasa  majaji wa mahakama kuzingatia matakwa ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwataka wajielekeze katika kutenda haki, kwa mujibu wa viapo walivyoapa bila ya kuwa na uoga, upendeleo wala chuki.

Jaji Kiongozi Eliezer Feleshi, wa katikati,  wa pili kushoto ni Jaji mstaafu Agathon Nchimbi, wa pili kulia ni Jaji Gad Mjemmas, wa kwanza kulia ni Jaji wa mahakama kuu divesheni ya Arshi, jaji, Crensensia Makuru na kwa kwanza kushoto ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu divisheni ya ardhi, Rehema Kerefu wakiwa katika Picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa hafla hiyo
 Jaji kiongozi, Eliezer Feleshi wa katikati waliokaa akiwa katika Picha ya pamoja na majaji wastaafu wa Mahakama Kuu kitengo cha ardhi, na Watumishi wengine wa Mahakama Kuu mara baada ya hafla ya kuwaaga kitaaluma iliyofanyika leo katika ukumbi wa wazi  wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
 Jaji Kiongozi Eliezer Feleshi, wa katikati waliokaa, akiwa katika Picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa Habari walioshiriki katika hafla ya kuwaaga kitaaluma majaji waliostaafu,  wa pili kushoto ni Jaji mstaafu Agathon Nchimbi, wa pili kulia ni Jaji Gad Mjemmas, wa kwanza kulia ni Jaji wa mahakama kuu divesheni ya Arshi, jaji, Crensensia Makuru na kwa kwanza kushoto ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu divisheni ya ardhi, Rehema Kerefu. 
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.

NAIBU SPIKA DKT. TULIA ACKSON ATEMBELEA BENKI YA CRDB NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MTENDAJI, ABDULMAJJID NSEKELA

$
0
0

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson leo ametembelea Benki ya CRDB na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, AbdulMajid Mussa Nsekela. 

Dkt. Tulia alisema dhumuni la Mkutano huo ni kumpongeza, Nsekela kwa uteuzi wake wa kuwa Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Benki ya CRDB na kufanya mazungumzo juu ya masuala mbalimbali ya kiuchumi na maendeleo.
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki wa Benki ya CRDB, AbdulMajid Mussa Nsekela, walipokuwa wakizungumza ofisini kwake, Azikiwe jijini Dar es salaam.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akifurahi jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki wa Benki ya CRDB, AbdulMajid Mussa Nsekela wakati alipokuwa akisaini kitabu cha wageni.
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images