Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Article 1


TAASISI YA ROOM TO READ YAPUNGUZA KASI ZA MIMBA ZA UTOTONI KUTOKA ASILIMIA 18 %HADI 1%

$
0
0

IMEELEZWA kuwa Mkoa wa Pwani umefanikiwa kutokomeza  mimba za utotoni  na utoro mashuleni kwa watoto wa kike  kutoka asilimia 18 hadi kushuka kiwango hicho na kufikia  asilimia moja.


Yamesema hayo  na  Mkurugenzi Mkazi  kutoka Taasisi ya Room to Read Peter Mwakabwele  aliyezungumza katika maadhimisho  ya siku ya mtoto wa kike duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoka 11  kila mwaka.

Amesema kuwa taasisi hiyo ya  Room to Read ilijikita  katika Mkoa wa  Pwani  na kuweka mikakati ya kusimamia  haki ya kupata elimu kwa watoro wa kike ambao wanaishi katika  mazingira magumu na kuwapa msaada wa kuwapeleka shule na kuwasimamia katika ngazi ya shule za msingi, sekondari na hata wanao  pata nafasi  ya kuendelea katika ngazi za elimu ya juu.

"Room to Read  tumeweza kufanikisha tunapunguza kasi ya ndoa  za utotoni na utoro mashuleni kwa  kwa watoto wa kike  kwa kuhakikisha  karibu na wazazi  wa mabinti gao na kufuatilia maendeleo yao ya masomo na kuwaelewesha wazazi umuhimu wa mtoto wa kike   kupata elimu" alisema Mkurugenzi huyo.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa miaka mingi nyuma Mkoa wa Pwani ulikua ukiongoza kwa ndoa za utotoni na utoro shuleni jamabo ambalo lilichangiwa na mila na desturi za unyago wa kuwaweka ndani mabinti na kuwacheza ngoma wakati wenzao wakiendelea na masomo huku wengine  wakiozeshwa baada ya kuchezwa lakini hivi sasa hali imebadilika  kwani mabinti hao wamekuwa wakiongoza kwa ufaulu kwenye mitihani ya kitaifa.

Amekwenda mbali zaidi  kwa kusema kuwa  Room to read wamekuwa wakitumia mbinu za   hali ya juu kwa kuwaweka karibu na kuwasikiliza ikiwemo kuwafundisha stadi za maisha  ili waweze kujiongoza  kielimu na kuweza kukabiliana na  changamoto   mbalimbali wanazokutana nazo katika maisha ya kila siku na hata familia kwa ujumla.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa  Taasisi hiyo ya Room to Read imekuwa ikitoa  bure sare  zashule ,  kuwalipia ada za shule na bweni  kwa wanaoishi  mbali na shule, pia huwapatia chakula na usafiri wa kwenda  na kurudi shuleni pia wapo ambao wamenunuliwa baiskeli ili kuwarahisishia  kwenda shuleni pia wanao wasimamizi na wagamasishaji ambao huwa nao  kwa muda wote ili kuhakikisha lengo la kumkomboa mtoto wa kike linatimia.

Amesema kuwa tayari  mradi huo wa Room to Read umefanikiwa kuwasomesha  wanafunzi wa kike zaidi ya 3500 ambao tayari wamesha hitimu katika viwango vya  ngazi  mbalimbali vya elimu huku wengine wakiwa nje ya nchi wakijiendeleza na  masomo ya elimu ya  juu.

Hivi sasa wanao wanafunzi wanaowasimamaia 8000 ambao wako katika shule ya msingu huku katika sgule za sekondari wako wanafunzi zaidi ya 2,900.

Aidha amezitaja Wilaya ambazo zinanufaika na mradi huo kuwa ni Kibaha, Bagamoyo na Chalinze pia amesema kuwa katika kipindi cha mwaka huu mradi huo umefanikiwa kutanuka baada ya kuongeza kipengele cha kuwawekea somo la biashara ili wale watakaofeli waweze kujiendeleza kibiashara na kujiajiri ili kuweza kujikimu kimaisha.

Naye Katibu tawala wa Mkoa wa Pwani  Mama Theresia Mbwambo amesema kuwa amewapongeza wadau wa mradi huo  wa Room to Read  kwa kumkumbuka mtoto wa kike na kufanikiwa kumkomboa kielimu.

"Tunatarajia  kwamba hivi sasa watoto wetu wa kike watafanikiwa kusoma vema kama jinsi walivyopanda katika ufaulu kwenye darasa la saba na  mitihani ya kidato cha nne"alisema  Mama mbwambo.

Naye Afisa habari wa Mkoa wa Pwani Alhaji  Maulid Abdul amesema kuwa serikali  ya awamu ya tano ni serikali makini  na kamwe haitovumilia  vitendo vya wazai kuwacheza ngoma watoto wakati wa kipindi cha masomo.

"Hatuzikatai  mila na desturi ni nzuri lakini  ku a  baadhi ya mila inabidi tuziache"alisema 
Mkurugenzi Mkazi  kutoka Taasisi ya Room to Read Peter Mwakabwele akizungumza katika maadhimisho  ya siku ya mtoto wa kike duniani mkoani Pwani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoka 11  kila mwaka. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa mradi  wa Room to Read  Zamaradi  na wa pili kulia ni Afisa elimu mkoa  wa Pwani Alhaj Maulid Abdul nanaliyeketi mwenyw ushungi 
Mrisho Mpoto pamoja na wasanii wengine wakitoa burudani katika maadhimisho  ya siku ya mtoto wa kike duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoka 11  kila mwaka yaliyofanyika mkoani Pwani.

Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua tawi la Tegeta

$
0
0
Na Mwandishi wetu,
Benki ya Biashara ya Mkombozi imezindua rasmi Tawi la Tegeta Jijini Dar es Salaam baada ya tawi hilo kupanda hadhi kutoka kituo cha huduma za fedha na sasa kuwa tawi kamili.

Tawi hilo lilifunguliwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa katika hafla iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali, wafanyakazi na wateja wa Benki ya Biashara ya Mkombozi.

Akizindua tawi hilo jipya, Askofu Nzigilwa alisema benki inaendelea kukua vizuri kama ilivyotarajiwa na kwamba malengo ya Benki ya Biashara ya Mkombozi ni kuwa na matawi nchi nzima ili Watanzania wote waweze kupata huduma za kibenki.

“Nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania wote kuitumia  benki hii. Hii ni benki  inayomilikiwa na Watanzania wenyewe kwani mpaka sasa hakuna pesa yeyote iliyowekwa na mwekezaji yeyote wa nje,” alisema na kuongeza kuwa ufunguzi  wa tawi hilo la Tegeta ni udhihirisho wa dhamira njema ya Benki ya Mkombozi kama mdau muhimu katika uchumi na maendeleo ya sekta ya fedha.

Askofu huyo pia alitoa witokwa Serikali kuendelea kuunga mkono mipango hii ya maendeleo kwani yote hii ipo kwa ajili ya kuwahudumia Watanzania.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya Mkombozi Bw. George Shumbusho alisema kituo cha huduma Tegeta kilifunguliwa  tangu tarehe 23 Julai 2016 na kimepata mafanikio ya kuridhisha katika kipindi hiki kifupi na hata kupata hadhi ya kuwa tawi.
 Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa akijaza fomu ya kuweka fedha wakati wa uzinduzi wa Tawi la Tegeta Jijini Dar es Salaam.
 Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa akikata utepe kuzindua Tawi la Tegeta Jijini Dar es Salaam huku viongozi wa benki hiyo wakishuhudia tukio hilo. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya Mkombozi, Bw . George Shumbusho akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi la Tegeta Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya Mkombozi Profesa Marcelina Chijoriga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi la Tegeta Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya Mkombozi wakifuatilia kwa umakini wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tawi la Tegeta Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WANANCHI WA JIMBO LA LIWALE WAJITOKEZA KWA WINGI KUTIMIZA HAKI YAO YA KIMSINGI YA KUPIGA KURA

$
0
0
Na. Vero Ignatus , Liwale-Lindi

Wananchi wa Liwale na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi asubuhi ya leo katika vituo vya kupigia kura kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge 2018 mkoa wa Lindi.

Kwa mujibu wa Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Liwale Luiza Mlelwa amesema jumla ya wapiga kura waliojiandikisha 55777 na vituo vya kupigia kura 158 wote hawa watapiga kura kumchagua mbunge wao pamoja na diwani kata ya Kibutuka

Balozi Ramadhani Mapuri mjumbe wa Tume ya Taifa ya uchaguzi amesema kuwa ameshuhudia ufunguzi wa vituo, ambapo wapiga kura wamejitokeza kwa wingi na zoezi limeanza kwa wakati hivyo wananchi wasisite kwenda kupiga kura kwani uchaguzi unaendeshwa kwa Amani na Utulivu

Amesema katika vituo vya kupigia kura vya Likongowele Galani pamoja na Kituo cha Ujenzi hali ya uchaguzi ni shwari na wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

Wananchi hao wanapiga kura kuwachagua viongozi wanaowapenda kutoka vyama mbalimbali vya siasa, Abduli Kombo Ngakolwa kutoka chama cha wakulima AAFP, Hamis Mohamed Lihindi kutoka ACT Wazalendo, Kachauka Zuberi Mohamed (CCM) Mtesa Mohamed Rashid (CUF) na Mwajuma Noty Mirambo (UMD).
Balozi Ramadhani Mapuri mjumbe wa Tume ya Taifa ya uchaguzi akiwa katika Kitio cha kupigia kura cha Ujenzi. Picha na Vero Ignatus. 
Pichani ni foleni ya kupiga kura katika kituo cha Likongowele Galani leo asubuhi Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi. Picha na Vero Ignatus. 
Mmoja ya mwananchi kama anavyooneka tayari ameshapiga kura leo asubuhi. Picha na Vero Ignatus. 
Upigani kura ukiendelea kama inavyoonekana Pichani wananchi wakiwa kwenye foleni. Picha na Vero Ignatus
Wananchi wakiwa katika kituo cha kupigia kura Likongowele ghalani katika Jimbo la Liwale Mkoani Lindi leo asubuhi 13 Octoba 2018, Picha na Vero Ignatus. 
Hapa ni kituo cha kupiga kura cha Ujenzi wananchi wakiwa kwenye foleni tayari kwa kupiga kura leo asubuhi. Picha na Vero Ignatus. 

UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA LIWALE NA KATA 37 ZA TANZANIA BARA WAFANYIKA LEO

$
0
0
Wananchi wa jimbo la Liwale wamepongezwa kwa kujitokeza kwa wingi na mapema kwenda kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka, 

 Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Balozi Ramadhani Mapuli akiwa anafuatili uchaguzi mdogo katika Jimbo la Liwale. 
Balozi Mapuli amesema kwamba, ameridhishwa na utaratibu wa upigaji wa kura ikiwa ni pamoja na vituo kufunguliwa kwa wakati na hakuna malalamiko yoyote yaliyojitokeza katika hatua za awali. 

 Amewasihi wakazi wa Jimbo hilo kuendelea kujitokeza kwa wingi na kupiga kura katika hali ya amani na utulivu.
Kwa mujibu wa Mkurugezi wa uchaguziJimbo la Liwale  Luiza Mlelwa amesema  kuwa Jimbo hilo lina wapiga kura  55,777 na Vituo vya kupigia kura 158. 

NSSF yashiriki maonesho ya wiki ya Taifa ya vijana mkoani TANGA

$
0
0
Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii NSSF ni kati ya Tasisisi za serikali iliyoshiriki kwenye maonyesho ya wiki ya Taifa ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Tangamano wilaya ya Tanga mjini Mkoani Tanga ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye mpango wa hiari . 

Kaimu meneja wa mkoa waTanga Bi Aisha Nyemba amesema kuwa katika maonyesho haya wananchi wote wanaotaka kujiunga kwa hiari na kujiwekea akiba wanaweza kufanya hivyo na kwamba NSSF itawatambua na kuweka katika rekodi za wananchama wapya. 

“Ukija hapa katika banda letu utaweza kuandikishwa na kutambulika kwenye rekodi zetu hivyo ni fursa ya pekee kwa wananchama wapya kujiandikisha katika maonyesho haya”alisema bi Aisha. Bi Aisha amesema kuwa tangu maonyesho haya yaanze Oktoba 8 mwaka 2018 wananchi wengi wamejitokeza kujiandikisha na kupata elimu kuhusiana na umuhimu wa mafao ya NSSF na kuvutiwa hasa hasa katika eneo la matibabu bure. 

Wananchi wanaojiandikisha kwenye mpango wa hiari ni wale waliopo kwenye sekta isiyo rasmi kama vile waendesha bodaboda,mama lishe, wajasiriamali na wengine wengi. 

Maonyesho haya ya Taifa ya wiki ya vijana yaatafikia kilele oktoba 14 mwaka huu ambapo yataendana na sherehe za uzimaji wa mwenge kitaifa katika uwanja wa Mkwakwani.
Kaimu meneja wa mkoa NSSF mkoa wa Tanga bi Aisha Nyemba akitoa maelekezo kwa mkazi wa Tanga ,Yahaya Katubu alipofika kwenye banda la NSSF,wakati wa maonesho  wiki ya vijana yanayofanyika katika viwanja vya Tangamano mkoani Tanga
OFisa madai wa shirika la Taifa ya Hifadhi ya Jamii NSSF Athuman Bakari akitoa amelekezo kwa wananchi wa mkoa wa TANGA waliotembelea kwenye maonesho ya wiki ya kitaifa ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Tangamano Tanga
Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF Bi Aisha Sango akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea katika banda la NSSF kwenye maonesho ya wiki ya Kitaifa ya Vijana inayofanyoka katika viwanja vya Tangamano mkoani TANGA
Ofisa mikopo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF Athuman Bakari akitoa maelekezo kwa wananchi waliofika kwenye viwanja vya Tangamano yanapofanyika maonyesho ya wiki ya vijana.

PROFESA MBARAWA AAGIZA DAWASA WAANZE KUVITUMIA VISIMA VYA KIMBIJI MPERA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa ametoa maagizo kwa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka DAWASA kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi kwenye visima vilivyokamilika.

Amesema hayo baada ya kutembelea visima vilivyopo mpiji vinavyojengwa na Kampuni ya Serengeti katika mradi ulioanza 2014 utakaowezesha upatikanaji wa maji katika maeneo mengi ya Jijini Dar es salaam na Pwani.

Akizungumza baada ya kumaliza kuvikagua visima hivyo, Mbarawa amesema kuwa visima vilivyokuwa vimekamilika vianze kujengwa matanki ili wananchi waanze kupata maji Safi na salama.

Mbarawa amesema, "DAWASA msisubiri mkabidhiwe visima vyote kutoka kwa mkandarasi kwa sasa mnatakiwa mjenge matanki kwa ajili ya kuhifadhi maji na kuanza kuwahudumia wananchi,"

“Visima vya Kimbiji vipo tayari na hapa nimetembelea kisima ch M1, 2 na 5 na viwili hapo vimekamilika M1 kikitoa Lita 120,000 kwa saa na M5 Lita 100,000 kwa saa, ni hatua kubwa kwakuwa vimeshakamilika.”

Amesema, visima vya Kimbiji vimeshakamilika na viwili vya Mpiji vipo tayari na amewaagiza DAWASA kuhakikisha wanaanza kuvitumia ambapo awali walitaka kuvunja mkataba na Mkandarsi ila wakaacha suala hilo baada ya kuona watapata hasara ya kumtafuta mkandarasi mpya.

Kaimu Mkurugenzi wa  Miradi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka  DAWASA  Lidya Ndibalema  amesema kuwa watafuata kama maagizo yaWaziri aliyowapa ya kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi kutoka katika vile visima vilivyokuwa vimekamilika.

Amesema kuwa, wamekubaliana na Mkandarsi kuwa kila baada ya wiki mbili atawakabidhi kisima na wataanza kufanya dizaini mpya katika maeneo machache kuhakikisha wanaweka maji katika matankli ili kuwapelekea wananchi.

Mbali na hilo, Lyida amesema kuwa kama wataalamu walivyowaagiza watakuwa makini katika  masuala ya kimazingira na , watafanyia usanifu ili kuona chumvi isije  kuingia kwenye visima hivi.

Mradi huu wa Kimbiji na Mpera umegharimu takribani Bilioni 23 mpaka kukamilika kwake na lengo kuu la Serikali ni kuhakikihsha wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wanapata maji safi na salama na kwa Mkoa wa Dar es Saalaam Serikali imeweza kutumia Trilioni moja katika kipindi cha miaka mitatu kuboresha miundombinu ya maji kutoka Ruvu juu na Ruvu chini.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profesa Makame Mbarawa akilezwa na Meneja wa mradi huo visima vya Mpijo na uwezo wake wa uzalishaji maji kwa saa.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akizungumza baada ya kukagua kukagua kisima cha M1 na M5 vilivyokuwa vimeshakamilika na kuagiza Mamlaka ya Maji Safi na Majo Taka DAWASA kuanza kuwahudumia wananchi wasisubiri mpaka kukabidhiwa visima vyote.

MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI MBARALI YAWANUFAISHA WAKULIMA

$
0
0
Imeelezwa kuwa maboresho ya miundombinu ya skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Igomelo iliyopo wilayani Mbarali Mkoani Mbeya, imewanufaisha kwa namna mbalimbali wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha mbogamboga. 

Hayo yameelezwa jana na Mhandisi wa kanda ya Mbeya wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Elibariki Mwendo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea skimu hiyo.

Mhandisi Mwendo alisema kuwa, Serikali imetumia kiasi cha shilingi Milioni mia mbili hamsini (250Milioni) kukarabati miundombinu ya skimu hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa banio kubwa linalotoa maji katika chanzo cha maji cha mto Mbarali na mifereji inayopeleka maji mashambani.

“katika skimu hii wakulima wanajikita zaidi katika kilimo cha mbogamboga kama vile vitunguu, nyanya, matango, na hata zao la mpunga, ambapo kabla ya marekebisho na maboresho ya miundombinu hii, hali haikuwa nzuri kwani wakulima walikuwa wanajichotea maji kiholela ili kuweza kumwagilia mazao yao, lakini kwa sasa kama mnavyoona, maji yanakwenda moja kwa moja mashambani kwa utaratibu maalum ulivyopangwa ambapo kila mkulima ana zamu yake ya kuingiza maji mashambani tayari kwa kilimo, jambo ambalo limepelekea wakulima hawa kuongeza uzalishaji katika mazao wanayolima na kujiongeza pato la familia.” Alisisitiza Mhandisi Mwendo.

Mmoja wa wakulima wanaojishughulisha na zao la kilimo cha vitunguu katika skimu hiyo Bw. Yohana Mbuna (52) amesema amekuwa akijishughulisha na kilimo katika skimu hiyo kwa takribani miaka ishirini sasa, “ Kabla ya maboresho katika skimu hii hali ilikuwa mbaya kwanza tulikuwa tunalima bila kufuata utaratibu, tulikuwa tunagombania maji na hata mavuno hayakuwa mengi kwa heka moja nilikuwa napata magunia 30 lakini kwa sasa kwa heka moja ninaweza kupata zaidi ya magunia 100 na hii hunisaidia kupata fedha za kusomesa watoto wangu, na ninalima vitunguu kama zao la biashara, pamoja na hilo mazao mengine ya chakula kama mpunga ninalima kwa ajili ya familia yangu.” Alisema Bw. Mbuna.


Katika Picha Mhandisi Elibariki Mwendo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akizungumza kuhusu maboresho yaliyofanywa katika banio (halipo pichani) lililopo katika chanzo cha maji cha mto Mbarali kinachopeleka maji katika skimu ya umwagiliaji ya Igomelo, nyuma pichani ni mto Mbarali.
Bibi Victoria Kinyega akifanya kazi ya kuchambua vitunguu katika skimu ya umwagiliaji wa Igomelo.
Vijana wanaofanya kazi katika shamba la vitunguu kwenye skimu ya Igomelo iliyopo Mbarali Mkoani Mbeya wakijaza vitunguu katika gunia maarufu kwa jina la net, tayari kwenda sokoni kuuzwa.
Kulia Afisa Kilimo Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kanda ya Mbeya, Bw. Mnadi Taribo akimuelezea mgeni aliyetembelea shamba la mpunga katika skimu ya Umwagiliaji Igomelo, kuhusu teknolojia ya kisasa ya kilimo cha mpunga inayotumia kiasi kidogo cha maji, yaani kilimo shadidi.
moja ya ghala la kuifadhia vitunguu linalotumiwa na wakulima katika skimu ya umwagiliaji ya Igomelo.
Miundombinu inayopeleka maji katika mashamba ya mazao ya mbogamboga na mpunga katika skimu ya umwagiliaji ya Igomelo.



NAIBU WAZIRI MASAUNI AWASILI JIJINI ARUSHA KWA ZIARA YA KIKAZI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiweka saini katika daftari la wageni baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), tayari kwa ziara ya kikazi jijini Arusha.Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kilimanjaro,Mrakibu Msaidizi Zauda Mohamed na katikati ni Mkuu wa Kituo cha Polisi KIA,Mrakibu Msaidizi Abel Mgode .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), tayari kuelekea jijini Arusha kwa ziara ya kikazi.Katikati ni Mkuu wa Kituo cha Polisi KIA, Mrakibu Msaidizi Abel Mgode na kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kilimanjaro, Mrakibu Msaidizi Zauda Mohamed.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

TAMASHA KUBWA LA UTALII KUFANYIKA ZANZIBAR, KUPAMBWA NA VIONGOZI WA KITAIFA NA TUZO KABAMBE

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

TAMASHA la kihistoria la utalii linatarajiwa kufanyika visiwani Zanzibar kuanzia Oktoba 17 hadi 19 mwaka huu katika hoteli ya Verde, Mtoni visiwani humo na hiyo ni katika mpango kazi wa kupunguza umaskini na kuendeleza sekta ya utalii visiwani humo.

Akizungumza na vyombo vya habari Waziri wa Habari, utalii na mambo ya kale wa Zanzibar Mh. Mahmoud Kombo amesema kuwa Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuzindua tamasha hilo akiambatana na viongozi wengine wa kitaifa akiwemo aliyekuwa Rais wa Zanzibar Dr. Amani Abeid Karume, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani, Rais mstaafu Jakaya Kikwete na Waziri wa utalii na maliasili kutoka Tanzania bara Dkt. Hamis Kigwangalla.

Mahmod ameeleza kuwa tamasha hilo ni fursa na litawavutia wawekezaji, wamiliki wa hoteli na wamiliki wa kampuni za kitalii wazawa na wageni kwa kutangaza bidhaa zao za kitalii na amesema kuwa shughuli za kitalii zimechangia kwa asilimia kubwa sana katika ukuaji wa uchumi na hiyo ni kutokana na ubora wa huduma zitolewazo katika sekta hiyo.

Aidha amesema kuwa makampuni 150 na waoneshaji wa bidhaa za kitalii zaidi ya 130 kutoka ndani na nje ya nchi wanataraji kushiriki katika tamasha hilo na hiyo ni baada ya kutoa fursa kwa wadau hao kuja kujifunza na kupata semina za utalii wa ndani.

Kuhusiana na hali ya utalii visiwani humo Mahmoud ameeleza kuwa kwa mwaka 2017 zaidi ya watalii milioni moja waliingia nchini na watalii laki nne walitembelea Zanzibar na kwa mwaka huu wamevuka malengo kwa  kufikia watalii laki tano na hiyo ni kwa kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi chini ya uongozi wa Rais Dkt. Ali Mohamed Shein.

Kuhusiana na mchango wa utalii katika uchumi wa taifa Mahmoud amesema kuwa asilimia 27 ya uchumi wa Zanzibar unachangiwa na shughuli za kitalii huku asilimia 80 ya uchumi wa hutokana na fedha za kigeni.

Pia ameeleza kuwa tamasha hilo litakuwa na maonesho, semina na kutolewa kwa tuzo takribani 21 kwa sekta za utalii zitakazotolewa Oktoba 20.

Mwisho amewataka wananchi wote wa bara na visiwani pamoja na wageni kutoka maeneo yote mbalimbali kuhudhuria tamasha hilo la aina yake na sio kwa utalii pekee bali kuona utamaduni, ukarimu na malikale zipatikanazo Zanzibar na kwa wawekezaji na wafanyabiashara watumie fursa hiyo katika kutangaza bidhaa zao.

Kwa upande wake Katibu wa kamisheni ya utalii Zanzibar Dkt. Abdallah Mohamed amesema kuwa tamasha hilo la  ni kwa wote katika kuonesha na kudumisha mila na tamaduni zetu.

Kuhusu usalama amesema kuwa hali ni shwari kabisa katika maeneo yote hasa bandari, viwanja vya ndege na fukwe zote hivyo wananchi na watalii wawe huru katika kufurahia tamasha hilo la kipekee.

TUTAJUA SABABU YA KUTEKWA KWA MO DEWJI AKIPATIKANA, NA TANZANIA NI NCHI SALAMA - LUGOLA.

$
0
0
*Waziri wa Mambo ya Ndani asema tukio 
la MO si kigezo cha kuingiwa hofu kuwekeza nchini 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

SERIKALI imewahakikishia Watanzania na dunia kwa ujumla kwamba Tanzania ni nchi usalama ya kuwekeza na tukio la kutekwa kwa mfanyabiasbafa Mohammed Dewji lisiwape hofu. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amesema si sawa kutumia tukio la kutekwa kwa MO kama kigezo cha kuifanya Tanzania kuonekana si mahala na kuwahakikishi nchi iko salama na kufafanua hakuna nchi iliyosalama zaidi ya Tanzania. 

"Mimi niwahakikishie Watanzania na dunia kwa ujumla kwamba nchi yetu iko salama na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara kwetu ni geni na limetushutukiza.Hata hivyo nitoe rai nchi ya Tanzania ni salama na wawekezaji wake kuwekeza tu,tuko salama sana," amesema Waziri Lugola. 

Ametoa kauli hiyo baada ya waandishi wa habari kutaka kufahamu iwapo tukio la kutekwa kwa MO Dewji linaweza kusababisha kuwatia hofu wawekezaji na kutumia nafasi hiyo kuhakikisha nchi iko salama kwa uwekezaji. 

Waziri Lugola amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli imeampa kuhakikisha nchi iko salama na kusisitiza vyombo vya ulinzi na usalama viko imara."Wapi ambako wawekezaji watakwenda kukawa salama zaidi ya Tanzania.Watakuja tu na sababi nchi yetu tukio salama sana na inafaa kwa wawekezaji kuja kuwekeza.Wasiwe na hofu," amesema Lugola.

AONYA, ATAKA MITANDAO ITUMIKE 

Waziri Lugola amewataka wananchi kutumia mitandao ya kijamii kwa uangalifu kwani kinyume na hapo wataitumia kuleta uchochezi, hofu na udanganyifu.“Wananchi wawe makini na kwani umakini utasaidia kuondoa mkanganyiko.Taarifa zozote za matukio ya uhalifu zitatolewa na Jeshi la Polisi,”amesema . 

Ametoa onyo kwamba asitokee mtu yoyote anayetaka kutumia matukio yanayojitokeza kama mtaji wa kisiasa au kujipatia umaarufu. 

Asitokee mtu yoyote ambaye atatumia matukio hayo kuaminisha mataifa mengine kwamba nchi haiko salama. Akitokea mtu wa aina hiyo ajue atakamatwa na atachukuliwa hatua,”amesema.
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani ),alipokuwa akizungumza nao leo mchana katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya ndani kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo tukio la utekwaji wa Mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji,ambapo pia amewaonya watu kutotumia mitandano ya kijamii kupotosha kwa kuiaminisha Dunia kuwa Tanzania si mahali salama pa kuwekeza,kwani atakabainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola akizungumzia usawa ambao Jeshi la polisi na vyombo vingine vya dola katika kushughulikia matukio yoyote yanayotokea na kwamba Watanzania wote wana haki sawa hakuna cha tajiri au masikini kwani kuna dhana imeanza kujengeka kuwa matajiri wanapopatwa na tatizo wanaangaliwa zaidi 
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola alipokuwa akizungumza nao leo mchana katika ofisi ndogo za Wizara ya Mamo ya ndani kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo tukio la utekwaji wa Mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji.
Waziri Kangi Lugola akijibu baadhi ya maswali.

JK AKUTANA NA MCHEZAJI SAMUEL ETOO JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi yenye jina la Mchezaji huyo ambaye pia ni Balozi wa Bia ya Castle Lager, Samuel Etoo, aliyemtembelea leo ofisini kwake, Masaki jijini Dar es salaam.
 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon na vilabu vya Barcelona, Chelsie na Intermilan ambaye sasa anakipiga katika Klabu ya FC Qatar, Samuel Etoo, aliyemtembelea leo ofisini kwake, Masaki jijini Dar es salaam.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipeana mkono na Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon na vilabu vya Barcelona, Chelsie na Intermilan ambaye sasa anakipiga katika Klabu ya FC Qatar, Samuel Etoo, aliyemtembelea leo ofisini kwake, Masaki jijini Dar es salaam. 
 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon na vilabu vya Barcelona, Chelsie na Intermilan ambaye sasa anakipiga katika Klabu ya FC Qatar, Samuel Etoo (kulia kwake)  na Balozi wa Bia ya Castle Lager hapa nchini, Ivo Mapunda (kushoto kwake), pamoja na ukumbe walioambayana nao.  
 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiagana na Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon na vilabu vya Barcelona, Chelsie na Intermilan ambaye sasa anakipiga katika Klabu ya FC Qatar, Samuel Etoo, aliyemtembelea leo ofisini kwake, Masaki jijini Dar es salaam. 
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Msanii Dokii kwa Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon na vilabu vya Barcelona, Chelsie na Intermilan ambaye sasa anakipiga katika Klabu ya FC Qatar, Samuel Etoo, aliyemtembelea leo ofisini kwake, Masaki jijini Dar es salaam. 

MDHAMINI WA CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA NA RAIS MSTAAFU ALHAJ ALI HASSAN MWINYI AKUTANA NA SKAUTI MKUU

$
0
0
 Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Skauti Mkuu Mhe. Mwantumu Mahiza ambaye amemtembelea nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es salaam kumwamkia na kujitambulisha leo Jumamosi Oktoba 13, 2018
 Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akimsikiliza Skauti Mkuu Mhe. Mwantumu Mahiza akimtambulisha wajumbe alioongozana nao nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam kumwamkia na kujitambulisha.
 Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akimsikiliza Skauti Mkuu Mhe. Mwantumu Mahiza akimtambulisha wajumbe alioongozana nao nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam kumwamkia na kujitambulisha.
 Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akipokea zawadi ya kigoda maalumu cha kuwekea Kurani Tukufu kutoka kwa  Skauti Mkuu Mhe. Mwantumu Mahiza ambaye amemtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam kumwamkia na kujitambulisha akiwa ujumbe wake. Wengine kutoka kushoto ni Kamishna Mkuu wa chama hicho Mhe. Abdulkarim Shah, Mjumbe wa Bodi ya Skauti Kennedy Ndosi, Kamishna Mtendaji wa chama hicho Eline Kitaly na Mjumbe wa Bodi ya Skauti Omar Ilyas.  
Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na   Skauti Mkuu Mhe. Mwantumu Mahiza ambaye amemtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam kumwamkia na kujitambulisha akiwa ujumbe wake. Wengine  ni Kamishna Mkuu wa chama hicho Mhe. Abdulkarim Shah, Mjumbe wa Bodi ya Skauti Kennedy Ndosi, Kamishna Mtendaji wa chama hicho Eline Kitaly na Mjumbe wa Bodi ya Skauti Omar Ilyas.  

WATU 20 MIKONONI KWA POLISI TUKIO LA KUTEKWA MO DEWJI...WAZIRI LUGOLA AELEZA KINACHOENDELEA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WaZIRI wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amesema Jeshi la Polisi hadi sasa linawashikilia watu 20 kwa ajili ya kuwahoji na kuchukua ushahidi utakaowezesha kupatikana kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na vyombo vya habari kuhusu matukio mbalimbali yakiwamo ya utekaji watu.

Waziri Lugola amesema kwamba Jeshi la Polisi nchini wanaendelea  kumtafuta Mo Dewji na kuwasaka walimtoka.
"Watu 20 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuhojiwa na kutoa taarifa ambazo zitasaidia kupata ushahidi ambao utasaidia kumpata Mo Dewji," amesema Waziri Lugola.
Pia amesema pamoja na kushikiliwa kwa watu hao kwa ajili ya ushahidi wa kufanikisha kupatikana kwa Mo na kwamba watakaohojiwa na ikibainika wanastahili kuachiwa basi iwe hivyo ndani ya saa 24.
"Nimetoa maagizo kwa Polisi kuhakikisha walioshikiliwa wanahojiwa na ndani ya saa 24  kama hakuna sababu ya kuendelea kushikiliwa waachiwe," amesema.
Alipoulizwa sababu za kutekwa kwa Mo,Waziri Lugola amejibu kuwa kwa sasa hawajui sababu za kutekwa kwa mfanyabiashara huyo na kwamba atakapopatikana basi sababu zitajulikana pamoja ba waliomteka nao watatoa sababu.Alipoulizwa ni hatua gani zinafanyika kuzuia matukio hayo yasitokee amejibu Polisi wamekuwa wamejipanga lakini changamoto mojawapo ni kukabiliana na matukio hayo ambayo mengine ni mapya.

"Jeshi la Polisi wataendelea kukabiliana na matukio ya uhalifu ambayo mengine ni mapya na tutatumia matukio hayo kujifunza ili yasitokee tena," amesema.Hata hivyo Lugola amesema kwamba zipo Sababu nyingi za jumla ambazo zinasababisha kutokea matukio ya watu kutekwa na miongoni mwa sababu ni mambo ya kisiasa,kulipiza kisasi na masuala ya mapenzi.

"Kikubwa tunaomba mtuamini ,tunaendelea kukabiliana na kila aina ya tukio lolote ambalo litatokea tutalifanyia kazi," amesema Waziri Lugola.
Wakati huo huo amesema kuwa thamani ya Watanzania wote ni sawa na inapotokea mmoja wetu amepatwa na tatizo basi Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama vitashughulikia kwa uzito sawa.

Amesema kwamba tukio la kutekwa kwa MO linashughulikiwa kama ambavyo yanashughulikiwa matukio mengine na kuomba vyombo vya habari kitenda haki kwa kuacha upendeleo kwa kuandika habari kwa usawa.

WAZIRI MKUU AFUNGA TAMASHA LA URITHI FESTIVAL

$
0
0
*Atoa miezi miwili Wizara ya Habari ikamilishe mchakato wa vazi la Taifa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa muda wa miezi miwili na nusu kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezoiwe imekamilisha mchakato wa Tanzania kuwa na vazi la Taifa.

Amesema Watanzania bado hawajaunganishwa kwa kuwa na vazi la Taifa, ambalo mchakato wake  umeendeshwa kwa miaka mingi na wizara hiyo bila ya kujulikana wamefikia wapi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Oktoba 13, 2018) wakati akifunga tamasha za Urithi Festival, lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini  Arusha.

“Ifikapo Desemba 30,2018 tuwe tumeanza kupata sura ya vazi la Taifa ili wadau walijadili na waamue ni vazi gani la Mtanzania ambalo litawakilisha Taifa kama nchi nyingine walivyomudu kuwa na vazi la Taifa.”

Aliongeza kuwa ili kufikia azma  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezoiandae tamasha maalumu kwa ajili ya kuonesha aina tofauti za nguo ili kupata vazi la Taifa.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwaagiza waandaaji wa tamasha la Uridhi Festival wahakikishe kuanzia  mwakani kuwe na uratibu wa pamoja baina ya Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara ili tamasha lifunguliwe upande mmoja na kufungwa upande mwingine wa Muungano.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi waliyohudhuria wakati wa kufunga Tamasha la Urithi, lililofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Oktoba 13, 2018.
 Naibu Waziri Maliasili na Utalii Josephat Hasunga, akizungumza na wananchi waliyohudhuria kwenye Tamasha la Urithi, lililofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Oktoba 13, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea maandamano, katika Tamasha la Urithi, lililofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Oktoba 13, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akitembelea banda la Maliasili na Utalii katika Tamasha la Urithi, lililofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Oktoba 13, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Marry, akiangalia bidhaa ya asili katika banda la wajasiriamali katika Tamasha la Urithi, lililofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Oktoba 13, 2018, kutoka kushoto ni Bibi Eliamulika Ayo, Naibu Waziri Maliasili na Utalii Josephat Hasunga.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea zawadi ya ngoma na kikombe kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Wasanii Arusha Fred Thomas, wakati akikagua mabanda kwenye Tamasha la Urithi, lililofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Oktoba 13, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Marry, wakiangalia bidhaa ya bidhaa iliyobuniwa na mwanadada Glory Silayo (kushoto), katika Tamasha la Urithi, lililofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Oktoba 13, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

COSTANTINE MAGAVILA NA UJIO WA KITABU CHA UBISHI KOMAA NA MAISHA

WAZIRI DKT.KIGWANGALLA, PROF. KABUDI WAUNGURUMA LONDON

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, London 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mawaziri wake Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na Wazirri wa Katika na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi wameweza kuhutubia mkutano mkubwa na wa Kimataifa juu ya upigaji vita biashara haramu ya nyara, uliokuwa wa siku mbili Oktoba 11 na 12, 2018, Jijini London, Uingereza.

Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla na Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi wamuwakilisha Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo wa Kimataifa na kuandaliwa na Serikali ya Uingereza chini ya Uenyekiti wa Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William.

Mwaka huu mkutano huo ni wa Nne wa Ngazi ya juu kuhusu Biashara haramu ya nyara ambao huku ukiwakutanisha viongozi wakuu wa nchi, mawaziri na wataalam kutoka zaidi ya nchi 60 Duniani pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali, wasomi na wafanyabiashara.

Mkutano huo una lengo la kuimarisha jitahada zinazofanywa na Serikali mbalimbali duniani katika kupambana na kuzuia biashara haramu ya nyara.Mawaziri hao wa Tanzania kwa nyakati tofauti wameweza kusoma hotuba zao zenye malengo ya na jitihada za Serikali ya Tanzania katika uhifadhi wa Maliasili na kupambana na biashara haramu ya nyara hususani katika hifadhi zake za taifa na maeneo yote ya mapori ya hakiba sambamba na shoroba zilizopo.

Imeelezwa kuwa, Tanzania ni moja ya nchi ambayo imetenga asilimia 32.5% ya eneo lake kwa ajili ya uhifadhi na inasifika kwa uwingi wa bayoanuai. Jitiada za kuzuia ujangili zimepelekea kupungua kwa ujangili kwa asilimia 50 na hii imejidhihirisha kwa kuongezeka kwa Tembo kutoka 43330 mwaka 2014 hadi kufikia tembo 59830 mwaka 2015. Kwa zaidi ya Asilimia 60 

Wakati akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Mkutano huo Prince William wa Uingereza alisifu jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika uhifadhi na upambanaji wa Biashara haramu ya nyara.Prince William alipongeza jitihada alizozishuhudia wakati wa ziara yake nchini Tanzania zikiwemo kutoka Elimu ya uhifadhi kwa wanafunzi pamoja na vyuo vizuri vya Elimu ya uhifadhi kikiwemo Chuo cha Elimu ya Uhifadhi wa Wanyamapori Mweka.

Madhumuni ya mkutano huo ni kujenga ushirikiano baina ya nchi, taasisi binafsi na za kiserikali, NGOs na Wanataaluma, pia unalengo la kubadilishana uzoefu na mbinu za kupunguza mahitaji ya soko la nyara kwa nia ya kulifunga soko hilo duniani.
Waziri Dkt. Kigwangalla na Waziri Prof. Kabudi wakiwa katika mkutano huo. 
Waziri Dkt. Kigwangalla na Waziri Prof. Kabudi wakiwa wakibadilishana mawazo na wadau wa masuala ya wanyama kwenye muda wa mijadala wakati wa mkutano huo 
Waziri Dkt. Kigwangalla akizungumza katika mkutano 

UWEKEZAJI KATIKA ELIMU SULUHISHO LA CHANGAMOTO ZA KIUCHUMI AFRIKA

$
0
0
Na. WFM, Bali Indonesia

Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania zinatakiwa kuwekeza kwa kiasi kikubwa kwenye maarifa na elimu ili kuendana na soko la ushindani linaloendelea kwa kasi Duniani

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni mwakilishi wa Tanzania katika Bodi ya Magavana wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Dkt. Philip Isdor Mpango, wakati wa mikutano ya WB na IMF mjini Bali Indonesia.Dkt. Mpango alisema kuwa, katika mikutano hiyo ya Kimataifa yapo mambo ambayo Tanzania inatakiwa kuyafanyia kazi wakati huu ambao inapiga hatua kuelekea katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda ambapo elimu inayotolewa inatakiwa kujikita katika kukuza maarifa na ujuzi .

“Wakati suala la teknolojia likiangaziwa katika bara la Afrika ni vema kuangalia pia namna ya kukabiliana na changamoto zinazotokana na teknolojia hiyo kwa kuwa katika maeneo mengi ajira za watu zimepungua kutokana na mashine kuchukua nafasi za watu”, alisema Dkt. Mpango.

Alisema mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa imekua na umuhimu mkubwa kwa kuwa wadau wamebadilishana mawazo ambayo yamelenga kukabiliana na changamoto za kiuchumi ambazo zimeendelea kutokea Duniani ikiwa ni pamoja na baadhi ya nchi kuwa juu kiuchumi na nyingine kuendelea kuporomoka kwa kasi. 

Katika mikutano hiyo Tanzania imetajwa kuwa uchumi wake unaendelea kuimarika ambapo kwa sasa unakua kwa takribani asilimia sita hivyo kuwa mfano wa kuigwa barani Afrika na Dunia kwa ujumla.Wajumbe wa mikutano hiyo wametakiwa pia kukabiliana na suala la mabadiliko ya tabia nchi katika nchi zao kwa kuwa yanaathari kubwa katika uchumi hasa katika Sekta ya afya kutokana na kuongezeka kwa magonjwa lakini pia mafuriko na ukame.

Naye Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuka, alisema kuwa suala la amani duniani limejadiliwa kwa kina katika mikutano hiyo kwa kuwa ni chachu ya maendeleo si tu ya kiuchumi lakini pia ya kijamii.Mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa inaendelea Mjini Bali Indonesia, ambapo imewakutanisha Mawaziri, Magavana na wadau wa masuala ya Fedha na Uchumi kutoka nchini mbalimbali duniani.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
Mjini Bali Indonesia

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Benki ya Dunia (WB,) anayewakilisha Afrika (Africa group 1 constituency), Bi. Anne Kabagambe, wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayoelendelea mjini Bali Indonesia, kushoto kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
Wajumbe wa Benki ya Dunia (WB) kundi la Afrika (Africa group 1 constituency), wakiwa katika Mkutano Mjini Bali Indonesia.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wa pili kulia, akijadili jambo na Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoelendelea mjini Bali Indonesia.
Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Ushauri wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Dunia- WB kwa nchi za Afrika (Africa group 1 constituency) Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisoma ujumbe wa nchi hizo, wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoelendelea mjini Bali Indonesia (kushoto ) ni na Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Bali Indonesia)

WAFUGAJI WA KUKU WAASWA KUFUATILIA MASUALA YA UFUGAJI

$
0
0
WAJASILIAMALI,wafugaji wa kuku na wadau wa nyama hapa nchini wameaswa kufatilia masuala ya ufugaji kwa kuwa ufugaji unafursa nyingi hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa  ukuzaji biashara wa mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania (TanTrade) Boniface Michael wakazi akizungumza na MICHUZIBLOG jijini Dar es salaam leo.

 Amesema kuwa maonyesho hayo  nikwaajili ya kukuza biashara na kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini katika masoko ya ndani, kikandana kimataifa.

Michael amesema kuwa maonyesho hayo yanayofanyika jijini Dar es Salaam yapo kwaajili ya kuwaunganisha wazalishaji wa ndani ya nchi na masoko ya kimataifa pamoja na ya kikanda.

Amesema kuwa TanTrade wanakuza biashara za watengenezaji wa bidhaa mbalimbali kwa kuonyesha kupitia maonyesho ya kikanda.
Amema kuwa maonyesho hayo yaliyoanza Oktoba 12 na 13 jijini Dar es Salaam lametoa fursa kwa jamii kujipatia elimu ya ufugaji wa kuku bila gharama yeyote.
Kaimu Mkurugenzi wa  ukuzaji biashara wa mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania (TanTrade) Boniface Michael  akizungumza na MICHUZI BLOG mara baada ya kutemelea maonyesho ya kuku yaliyofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wananchi wakijipatia elimu kutoka kwa wafugaji wa kuku na wadau wa nyama hapa nchini katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.

 Wananchi wakipata maelezo jinsi ya ufugaji kuku kwa kisasa zaidi hapa nchini katika maonesho ya kuku yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Banda la vyakula vya kuku katika viwanja vya maonyesho sabasaba jijini Dar es Salaaam.
Picha na Avila Kakingo globu ya Jamii

WAKURUGENZI WA BODI YA TPA WAKAGUA GATI YA BANDARI YA KASSANGA

$
0
0
Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Bw Ajuaye Msese, kulia akimuonyesha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA, Prof Ignatus Rubaratuka moja ya mashine za kupakua na kupakia mizigo melini wakati  Wakurugenzi wa Bodi hiyo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Deusdedit Kakoko walipokuwa wakikagua gati ya Bandari ya Kassanga iliyopo Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, Prof Ignatus Rubaratuka akiangalia jinsi gati ya Bandari ya Kassanga iliyopo Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa ilivyojengwa.
Wakurugenzi wa bodi ya TPA wakibadilishana mawazo na meneja wa bandari za Ziwa Tanganyika wakati wakikagua gati ya Bandari ya Kassanga iliyopo Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images