Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Mhini, Sonia waonyesha cheche zao katika Olimpiki ya Vijana, Argentina

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Muogeleaji anayekuja kwa kasi katika mchezo huo hapa nchini, Dennis Mhini amevunja rekodi ya muda wake katika michezo ya vijana ya Olimpiki inayoendelea Buenos, Argentina katika staili ya backstroke ya mita 50 na freestyle ya mita 100.

Mhini ambaye ameshiriki katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza alimaliza katika nafasi ya tatu kwa upande wa mita 100 freestyle kwa kutumia  sekunde 58.53 na kujizolea pointi 514 wakati kwa upande wa mita 50 backstroke, alitumia muda wa sekunde 29.79 na kupata pointir 525 baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu.

Muogeleaji huyo amoenyesha kuwa ni lulu ya nchi katika mashindano yajayo ya kimataifa ikiwa ya Jumuiya ya Madola, Olimpiki ya wakubwa na mashindano ya dunia ya kuogelea.

Mbali ya Mhini, pia muogeleaji wa kike, Sonia Tumiotto naye aliweza kufanya vizuri pamoja na wote wawili kushindwa kuingia fainali.

“Waogeleaji wetu bado wadogo sana na wamekutana na changamoto nyingi za kiufundi. Makocha wao wamejitahidi sana kuwafikisha katika hatua ya juu, lakini hakuna vifaa vya kisasa kulinganisha na nchi nyingine,”

“Hatuna maswawa ya kisasa ya kuogelea, hali imewafanya waogeleaji kuwahi kuondoka kuelekea kwenye mashindano kwa lengola kufanya mazoezi kwenye mabwawa hayo, sisi ni tofauti sana na wenzetu,” alisema kocha Michael Livingstone.

Livingstone ambaye ameongozana na waogeleaji hao, amesema kuwa Mhini na Sonia wamejitahidi sana na alama walizopata ni ishara tosha kuwa mchezo huo unapata mafanikio.

Kwa upande wa Sonia, muogeleaji huyo aliweza kulinda muda wake katika mita 100 na 200 katika mtindo wa freestyle.

Sonia alimaliza kwa kwanza katika kundi la kwanza (heat 1) kwa upande wa mita 100 kwa kutumia muda wa 1.01.47 na kupata pointi 595 na kushika nafasi ya tatu kwa kutimia muda wa 2.12.05 na kupata pointi  626.

Mwenyekiti wa chama cha kuogelea nchini (TSA), Imani Dominick aliwapongeza waogeleaji hao kwa kuhimarisha muda wao pamoja na kutotwaa medali.

“Najua wadau wengi wa michezo wanataka kuona medali, ni kweli, lakini kwa hali ya mchezo wetu ambao ndiyo kwanza unakua, tunaangalia zaidi kuhimarisha muda na kupata muda wa kufuzu, mpaka sasa hatuna hata bwawa la kuogelea la kisasa, bado tunatafuta bwawa pia,” alisema Dominick.
 Dennis Mhini ‘akichapa maji’ katika mchezo wa kuogelea katika michezo ya vijana ya Olimpiki inayoendelea Buenos, Argentina katika staili ya backstroke ya mita 50 na freestyle ya mita 100
 Sonia akionyesha ufundi wake katika kuogelea katika michezo ya vijana ya Olimpiki inayoendelea Buenos, Argentina.
 Dennis akionyesha umahiri wake katika staili ya backstroke

CCM YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUTELEZA ILANI

$
0
0
Na Tiganya Vincent
HALMASHAURI kuu ya CCM Mkoa wa Tabora imeipongeza Serikali ya Awamu ya tano kutokana na kutekeleza kwa vitendo Ilani yake ya miaka mitano tangu ulipofanyika uchaguzi Mkuu uliopita mwaka 2015 hadi sasa.

Pongezi hizo zimetolewa jana kwenye kikao maalumu cha wajumbe wa Halmashauri hiyo iliyokutana kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kutoka serikali ya Mkoa wa Tabora.

Wajumbe hao walisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dokta John Pombe Magufuli iliahidi miradi mbalimbali kwa wakazi wa Mkoa huo ikiwemo ya maji, afya, barabara na kilimo ambapo utekelezaji wake unaonekana kwa macho.

Waliitaja miradi ambayo utekelezaji wake umeanza na unaendelea kwa kasi mkoani humo kuwa ni wa maji kutoka ziwa Victoria kwa ajili ya wakazi wa Wilaya za Nzega, Tabora na Igunga.

Miradi mingine ni ujenzi wa barabara za kiwango cha lami kuunganisha Mkoa huo na mikoa jirani ambapo ujenzi unaendelea.

Katika hatua nyingine wajumbe hao wamezitaka Halmashauri  za wilaya mkoani humo kuhakikisha kiasi cha fedha inachotenga kutokana na mapato ya ndani kwa ajili ya vijana, akinamama, walemavu na ile ya miradi ya Maendeleo zinatumika kama ilivyokusudiwa.
  Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Janath  Kayanda akitoa maelezo ya awali kabla ya ufunguzi wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa huo jana cha kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi akifungua Kikao maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa huo jana cha kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi. 
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ( wa pili kutoka kulia) akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi jana katika Kikao maalumu cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi  CCM Mkoa wa Tabora.
 Baadhi ya Wajumbe wa Hamashauri Kuu ya Cahama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora wakiwa katika kikao maalumu jana kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. 
 Mbunge wa Urambo Margaret Sitta akiomba ufafanuzi jana wakati kikao maalumu jana Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora cha kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele akitoa maoni yake jana wakati kikao maalumu jana cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora cha kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. 
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora-Uyui Saidi Ntahondi akitoa maoni yake jana wakati kikao maalumu jana cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora cha kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Picha na Tiganya Vincent

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WIZARA YA AFYA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA HOSPITALI KUTOKA SHIRIKA LA HHRD

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar 

Msaada wa Dawa na Vifaa Tiba unaotolewa na wafadhili mbali mbali unaweza kupunguza matumizi ya Serikali yaliyopangwa katika bajeti ya mwaka 2018/19 iwapo Wafanyakazi wa Wizara ya Afya watachukua juhudi ya kuilinda na kuitunza misaada hiyo. 

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed alieleza hayo Ofisini kwake Mnazimmoja wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vifaa tiba na vitendea kazi vya Hospitali kutoka Shirika linalotoa misaada ya Kijamii la Marekani la HHRD kupitia Jumuiya ya Muzdalifa ya Zanzibar. 

Alisema Serikali inaendeleza mashirikiano na Mashirika na Taasisi za ndani na nje ya nchi ili kuona huduma za Afya zinaimarika na wananchi wanapata huduma bila usumbufu. Waziri Hamad alilipongeza Shirika la HHRD kwa msaada huo na kulishauri kuangalia uwezekano wa kusaidia zaidi katika maeneo ya mama na mtoto na kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa Hospitali. 

Alikumbusha kuwa pamoja na misaada inayotolewa na wafadhili, Serikali imeweka Bajeti ya kutosha kwa ajili ya dawa na amewataka wafanyakazi wanaosimamia uagiziaji wa dawa kuwa waangalifu kuepuka kununua dawa ambazo zipo kwa wingi katika Hospitali na vituo vya afya. 
Katibu Mkuu Shirika la HHRD la Marekani Ayoub Mohd akimkabidhi hati ya mkabidhiano ya vifaa vilivyotolewa na Shirika hilo katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja, Mjini Zanzibar. 
Meneja Mkaazi wa Shirika la HHRD Ofisi ya Nairobi Musa Ibrahim akieleza kuridhishwa na watendaji wanpopkea misaada wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya Hospitali iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja. 
Katibu Mkuu Shirika la HHRD Ayoub Mohd akizungumza baada ya kumkabidhi Waziri wa Afya msaada wa vifaa vilivyotolewa na Shirika hilo katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar. 
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akitoa shukrani zake kwa Shirika la HHRD kwa msaada waliotoa kwa ajili ya wananchi wa Zanzibar. 
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akimkabidhi mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Haidar Hassan Madoea moja ya baskeli zilizotolewa msaada na Shirika la HHRD .Picha na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar 

DKT TIZEBA AWATAKA WAKULIMA WA PARETO KUJIUNGA NA MFUMO WA USHIRIKA

$
0
0

Na Mathias Canal-WK, Mufindi-Iringa


Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) amewataka wakulima wa Pareto kote nchini kujiunga na mfumo rasmi wa vyama vya msingi vya ushirika.

Dkt Tizeba ametoa Mwito huo Jana tarehe 13 Octoba 2018 wakati akizungumza na wakulima wa Pareto katika kijiji cha Ikanga kilichopo kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa.

Alisema kuwa ushirika ni dhana ya kuleta maendeleo kwa kushirikiana ambapo dhana hiyo imefanikiwa kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita. “Kutokana na changamoto mbalimbali zilizoikumba sekta hii ya ushirika watu wengi wamekosa imani na vyama hivi na baadhi ya vyama vimeshindwa kufanya kazi vizuri hivyo nawahakikishia serikali inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli imerejesha nidhamu kwenye ushirika” Alikaririwa Dkt Tizeba na kuongeza kuwa

Alisema kuwa Ushirika maana yake ni muungano wa watu ambao wanafanya kazi pamoja kwa hiari ili kufanikisha mahitaji yao ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kupitia shughuli ya biashara inayomilikiwa kwa pamoja na kudhibitiwa kidemokrasia. Ushirika unazingatia maadili ya kujisaidia wenyewe, jukumu binafsi, demokrasia, usawa na mshikamano.

Wanachama wa Ushirika wanaamini katika misingi ya uaminifu, uwazi, uwajibikaji kwa jamii na kuwajali wengine. Muundo wa Ushirika kwa ujumla unategemea uimara wa chama cha msingi cha Ushirika, hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha vyama imara vya msingi vinaanzishwa.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa Pareto katika kijiji cha Ikanga kilichopo kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa, Jana tarehe 13 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akikagua shamba la Pareto la mkulima Bahati Mhapa, katika kijiji cha Ikanga Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa, Jana tarehe 13 Octoba 2018. 
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza na wakulima wa Pareto katika kijiji cha Ikanga kilichopo kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa, Jana tarehe 13 Octoba 2018. 
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akikagua kiwanda cha Pareto Mafinga (PCT) kilichopo mamlaka ya Mji wa Mafinga wakati akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa, Jana tarehe 13 Octoba 2018. 



KUMBU KUMBU YA BABA WA TAIFA

RAIS MAGUFULI ASHIRIKI IBADA MAALUMU KUMUOMBEA BABA WA TAIFA, AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakiungana na waumini wengine katika Ibada Maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakitoa sadaka walipoungana na waumini wengine katika Ibada Maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Rosari baada ya kuhudhuria Ibada Maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakiwa na Mama Maria Nyerere na mwanae Makongoro Nyerere walipomtembelea nyumbani kwao Msasani jijini Dar es salaam baada ya kungana na waumini katika Misa Maalumu kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018
   
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mjane wa Baba Taifa, Mama Maria Nyerere, aliyemtembelea nyumbani kwake Msasani baada ya kutoka katika Ibada Maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakiwa na Mama Maria Nyerere walipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam baada yakuhudhuria Misa Maalumu kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakisindikizwa na Mama Maria Nyerere pamoja na mwanae Makongoro Nyerere na wajukuu wake walipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam baada yakuhudhuria Misa Maalumu kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018.

UWEKEZAJI KATIKA ELIMU SULUHISHO LA CHANGAMOTO ZA KIUCHUMI AFRIKA

$
0
0
Na. WFM, Bali Indonesia

Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania zinatakiwa kuwekeza kwa kiasi kikubwa kwenye maarifa na elimu ili kuendana na soko la ushindani linaloendelea kwa kasi Duniani

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni mwakilishi wa Tanzania katika Bodi ya Magavana wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Dkt. Philip Isdor Mpango, wakati wa mikutano ya WB na IMF mjini Bali Indonesia.

Dkt. Mpango alisema kuwa, katika mikutano hiyo ya Kimataifa yapo mambo ambayo Tanzania inatakiwa kuyafanyia kazi wakati huu ambao inapiga hatua kuelekea katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda ambapo elimu inayotolewa inatakiwa kujikita katika kukuza maarifa na ujuzi .

“Wakati suala la teknolojia likiangaziwa katika bara la Afrika ni vema kuangalia pia namna ya kukabiliana na changamoto zinazotokana na teknolojia hiyo kwa kuwa katika maeneo mengi ajira za watu zimepungua kutokana na mashine kuchukua nafasi za watu”, alisema Dkt. Mpango.

Alisema mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa imekua na umuhimu mkubwa kwa kuwa wadau wamebadilishana mawazo ambayo yamelenga kukabiliana na changamoto za kiuchumi ambazo zimeendelea kutokea Duniani ikiwa ni pamoja na baadhi ya nchi kuwa juu kiuchumi na nyingine kuendelea kuporomoka kwa kasi. 

Katika mikutano hiyo Tanzania imetajwa kuwa uchumi wake unaendelea kuimarika ambapo kwa sasa unakua kwa takribani asilimia sita hivyo kuwa mfano wa kuigwa barani Afrika na Dunia kwa ujumla.Wajumbe wa mikutano hiyo wametakiwa pia kukabiliana na suala la mabadiliko ya tabia nchi katika nchi zao kwa kuwa yanaathari kubwa katika uchumi hasa katika Sekta ya afya kutokana na kuongezeka kwa magonjwa lakini pia mafuriko na ukame.

Naye Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuka, alisema kuwa suala la amani duniani limejadiliwa kwa kina katika mikutano hiyo kwa kuwa ni chachu ya maendeleo si tu ya kiuchumi lakini pia ya kijamii.Mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa inaendelea Mjini Bali Indonesia, ambapo imewakutanisha Mawaziri, Magavana na wadau wa masuala ya Fedha na Uchumi kutoka nchini mbalimbali duniani.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Benki ya Dunia (WB,) anayewakilisha Afrika (Africa group 1 constituency), Bi. Anne Kabagambe, wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayoelendelea mjini Bali Indonesia, kushoto kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
Wajumbe wa Benki ya Dunia (WB) kundi la Afrika (Africa group 1 constituency), wakiwa katika Mkutano Mjini Bali Indonesia.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wa pili kulia, akijadili jambo na Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoelendelea mjini Bali Indonesia.
Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Ushauri wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Dunia- WB kwa nchi za Afrika (Africa group 1 constituency) Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisoma ujumbe wa nchi hizo, wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoelendelea mjini Bali Indonesia (kushoto ) ni  na Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Bali Indonesia)

HATIMAYE JIMBO LA LIWALE LAPATA MUWAKILISHI BUNGENI

$
0
0
Na. Vero Ignatus, Liwale - Lindi

Hatimaye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Liwale umemalizika kwa huku mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Zuberi Kuchauka akiibuka mshindi wa kiti cha ubunge

Msimamizi uchaguzi Jimboni hapo Luiza Mlelwa amesema waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 55777 na waliojitokeza kupiga kura walikuwa 40706 kura halali zilikuwa 40,301 kura zilizokataliwa ni 405 

Akimtangaza mshindi wa kiti cha ubunge (6:30usiku ) Jimbo la Liwale msimamizi wa uchaguzi amesema kuwa Zuberi ameshinda kwa kura 34, 582 sawa na asilimia 85.81.Mara baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha Ubunge Zuberi Mchauka amesema ameyapokea matokeo kwa furaha na ameahidi kushirikiana na wananchi wa Jimbo la Liwale kutatua changamoto mbalimbali zilizopo

Aidha Mchauka amesema kuwa changamoto nyingi zilizopo katika Jimbo la Liwaleni pamoja na miundombinu ya barabara, maji, Elimu, mawasiliano na Afya ambapo ameahidi wananchi kuwa atashughulikia changamoto hizo. 

Abdul Kombo Ngakolwa mgombea wa chama cha (AAFP) chama cha wakulima amesema ameridhishwa na ushindi alioupata mgombea wa(CCM) na amempongeza, kwa ushindi huo '' Mara zote mtu unaposhindana lazima mmoja ashinde, asiyekubali kushindwa siyo mshindani'' alisema Abdul

Mwajuma Notey mgombea kutoka (UMD) amewapongeza wanaliwale kwa kufanya maamuzi yao na amesema anayaheshimu, amempongeza mbunge mteule kwa ushindi huo ."Nakupongeza sana kwa ushindi ila namkumbusha tu awakumbuke wapiga kura wako wote waliomchagua na wasiomchagua wote ni wapigakura wako" 

Mchakato wa kumtafuta mbunge wa Jimbo la Liwale ulianza mwezi mmoja uliopita ambapo waliotangaza nia ya kuwania kiti hicho ni wagombea kutoka vyama vifuatavyo AAFP kura 18 sawa 0.2% (UMD 109 sawa 0.49% ACT 285 sawa 0.79%CUF 5207 sawa na 12. 92%.
Msimamizi wa uchaguzi mdogo Jimbo la Liwale Luiza Mlelwa akimkabishi chetu mbunge mteuliwa wa Jimbo la Liwale Zuberi Kichauka. Picha na Vero Ignatus
Wa pili kutoka kulia ni Msimamizi wa Uchaguzi mdogo Jimbo la Liwale Luiza Mlelwa akiniandaa kumtangaza mshindi wa kigi cha ubunge Jimboni hapo. 
Mbunge Mteule wa Jimbo la Liwale akionyesha cheti alichokabidhiwa na msimamizi wa uchaguzi mara baada ya kutangazwa rasmi. Picha na Vero Ignatus

KAMPUNI YA DAGE YAWANOA VIZURI WAHITIMU 200,BALOZI WA MAREKANI NCHINI ATOA UJUMBE

$
0
0
 Na Khadija Seif,Globu ya jamii

Balozi wa USAID nchini Marekani Inmi Petterson amepongeza juhudi za wazazi ambao wamewaruhusu watoto wao kujiunga na kupata mafunzo ya ujasiriamali na kuhitimu.

Ambapo amewasisitiza wahitimu hao kuwa mustakabali wa maisha yako ni  juhudi zako binafsi na  si Serikali, hivyo basi waione fursa na kuifanyia kazi kwani tayari wameshapata mafunzo ya kutosha.

Petterson ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema hayo jijini Dar es Salaam na kwamba changamoto zipo na ni sehemu ya maisha na kujiamini ndio silaha tosha katika kukabiliana na maisha ili kujijengea maendeleo kwa ajili ya maslahi yako binafsi na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam John Mbwana  amewatangazia rasmi wahitimu hao kuwa Serikali inashirikiana mao bega kwa bega na tayari wametoa vipaumbele vya mikopo ambayo itawasaidia kufungua miradi yao wenyewe.Aidha, ameeleza wimbi kubwa linalowakuta wasichana wenye umri mdogo katika wilaya hiyo na kupelekea wingi wa vijana ambao hawana ajira nakua tegemezi kwa wazazi wao.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Kampuni ya Dage Genoveva Kiliba ambayo inashughulika na kutoa mafunzo kwa vijana kwa ajili ya ujasiriamali imetoa vyeti kwa wasichana  200 jijini Dar es salaam ambao wamehitimu katika nyanja mbalimbali.Kiliba amepongeza ushirikiano ulionyeshwa baina ya wahitimu hao pamoja na familia zao ambazo zilikubali kuingia Kwenye mafunzo hayo na kuiona fursa ya kutimiza ndoto zao .

Na amesema wengi wa wasichana hao walishapoteza malengo na muelekeo wa maisha  kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata mimba wakiwa mashuleni,wazazi kukosa fedha za kuendelea na masomo pamoja na vifo vya walezi au wazazi.Hivyo basi mafunzo waliyopatiwa ikiwemo elimu ya kujitambua,stadi za maisha,namna ya kufanya biashara zao itawasaidia kuendesha biashara zao kwa uweledi.

Aidha, mwalimu Makene ambae amehusika kwenye kutoa mafunzo amepongeza wasichana wote ambao wamethubutu na wameweza kunyanyuka upya na kuzikimbilia fursa hizo .

NAIBU WAZIRI OLE NASHA AWATAKA WAHITIMU FEZA KUEPUKA VITENDO VIOVU

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amewataka wahitimu wa darasa la saba katika shule ya Msingi Feza kuepuka vitendo viovu ambavyo vinaweza kukatisha ndoto zao katika maisha. 

Ole Nasha ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam katika mahafali ya 15 ya darasa la saba ya shule hiyo na kuwataka vijana hao kutambua kuwa kuhitimu katika hatua hiyo ndio mwanzo wa safari ndefu waliyonayo katika Elimu na kuwa nidhamu pekee ndio msingi wa mafanikio.

“Jamii yetu kwa sasa inakabiliwa na mmomonyoko wa maadili vitendo viovu kama vile vijana kujishirikisha katika masuala ya ngono, ulevi, matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii jihadharini navyo sana katika maisha yenu, mkijiingiza tu mtaharibu ndoto zenu mlizojiwekea na matokeo yake mtashindwa kushiriki katika jitihada za kuijenga nchi yenu,” alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha

Alisema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Sekta binasfi katika maendeleo ya Elimu nchini kwa kuwaandaa vijana kimaadili na kitaaluma ili kufikia dira ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 inayolenga kuwa na mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitizamo chanya ili kuweza kuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akihutubia wakati wa mahafali ya kumaliza Elimu ya Msingi Feza yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam. Amewataka wahitimu kuwa na nidhamu, bidii na kutanguliza uzalendo katika yale watakayokuwa wakifanya ili kuweza kufikia malengo yao.
Baadhi ya Wahitimu wa Darasa la Saba katika shule ya Msingi Feza wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Mh William Ole Nasha wakati wa mahafali yao yaliyofanyika jana Oktoba 13,108 jijini Dar es salaam. 1. 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akigawa cheti kwa mmoja wa wanafunzi aliyehitimu darasa la saba mwaka huu katika shule ya Msingi Feza wakati wa mahafali yao yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 13, 2018.

TFS YAWAKARIBISHA WATANZANIA KUTEMBELEA MISITU KUONA UMUHIMU WA IKOLOJIA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umetoa wito kwa watanzania kutmbelea Maeneo yaliyohifadhiwa hili kuweza kujionea namna Ekolojia na uhifadhi katika misitu hiyo ilivyo na faida kwa viumbe hai na Wanadamu.

akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema  jana Afisa Misitu Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu nchini(TFS),Arijanso Mlog  katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Tanzania(SITE) Yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam amesema kuwa watu wanpaswa kutemblea misitu hili waweze kujionea na kujifunza umuhimu wa ikolojia katika hifadhi.

"Ni vyema watu wakaja wakatembelea hifadhi ya misitu ya Amani waweze kujionea namna Misitu iliyopakana na makazi ya watu na maporoko ya maji yasikauka muda wote na kujionea maua ambayo yanaamika katika imani kuwa ndio yalitumika wakati wa kristo na watu uyafata kutoka maeneo ya mbali"amesema Mlog.

Kwa upande wakeMeneja Masoko na Uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Nchini, Mariam Kobelo amewataka wadau mbalimbali kwa sasa kutembelea banda lao lililopo katika   Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Tanzania(SITE) Yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam kujionea huduma zitolewazo na TFS na kujua wapi wanaweza kutmebelea kwa ajili ya mapumziko yao.

Mariamu amesema kuwa Misitu inayohifadhiwa na TFS ina mambomengi sana ambayo watu wanweza kupata  ikiwa na sehemu ya kufanyia tafiti, Mapumziko kwa wana ndoa pia wanaweza kwenda kutembelea na familia zao kwa ajili ya kuwafundisha watoto umuhimu wa uhifadhi.
 Afisa Misitu Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu nchini(TFS),Arijanso Mlog akizungumza na Waandishi wa habari katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Tanzania(SITE) Yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
 Meneja Masoko na Uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Nchini, Mariam Kobelo akieleza huduma za kitalii zilizopo ndani ya Hifadhi za Misitu zilizo chini ya TFS
 Afisa Misitu Mwandamizi , Anna Lawuo Akizungumza na Waandishi wa habari  kuhusu umuhimu wa mazao yatokanayo na misitu nchini
 Wafanyakazi wa Huduma za Misitu nchini TFS, Wakiwaonesha wadau Mazao Mbalimbali yatokanayo na misitu ambayo ni mazuri kwa ajili ya kuimarisha afya ya Mwanadamu.
Sehemu ya Mabanda ya Maonesho yakiwa yanaonekana kwa juu katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

NSSF yatakiwa kutoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Watanzania wote

$
0
0

Serikali imelitaka Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii NSSF kutoa elimu zaidi kwa wananchi kuhusiana na faida za kujiunga katika hifadhi za jamii nchini. 

Hayo yameswemwa na Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Sera,Bunge,Ajira ,Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Jenister Mhagama kwenye wiki ya Taifa ya maonesho ya wiki ya vijana yanayofanyika katika viwanja vya Tangamano mkoani Tanga ambapo amesema kuwa bado watanzania wengi hawana elimu ya kutosha kuhusiana na kujiwekea akiba ya uzeeni na faida zake hivyo NSSF inaoaswa kuhakikisha inatoe elimu hii. 

“Nawataka NSSF muhakikishe elimu hii mnaitoa ipasavyo na iwafikie watanzania wote nchini ,mwende vijijini huko muelekeze wananchi nao wapate uelewa wa hifadhi za jamii na faida zake”alisema Waziri Muhagama. Mhagama amesema kuwa NSSF ndio inajukumu sasa la kuandikisha wananchi walio kwenye sekta isiyo rasmi hivyo wahakikishe wanawafikia wananchi wengi waliopo kwenye sekta hiyo na hasa wa vijijini na kuwapatia uelewa na waweze kujiunga na kufaika na mafao yote ya NSSF. 

Kwa upande wake kaimu meneja wa NSSF mkoa wa TANGA ,Aisha Nyemba mpaka sasa wameendelea kutoa elimu kwa wananchi kujiandikisha katika mpango wa hiari ambao utawawezesha kufaidika na mafao mbali mbali ikiwemo mafao ya matibabu. Kwa mujibu wa Nyemba mpaka sasa NSSF imeandikisha vikundi vya wajasiriamali idadi ya 47 katika mpango wa hiari na wanachangia michango yao kila mwezi ambapo pia juhudi zinaendelea kuhakikisha wanafikia vikundi vingi vya wajasiriamali katika mkoa wa Tanga. 

Maonyesho haya ya Taifa ya wiki ya vijana yamefikia kilele chake oktoba 14 mwaka huu ambapo yataendana na sherehe za uzimaji wa mwenge kitaifa katika uwanja wa Mkwakwani na kuenzi miaka 19 ya kifo cha Rais wa kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 
 Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Sera,Bunge,Ajira ,Vijana na Watu Wenye  Ulemavu) Mhe. Jenister Mhagama, akipata maelezo namna ya kujiunga na uchangiaji wa hiari katika Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa maonesho ya Wiki ya Taifa ya Vijana yanayofanyika katika Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga 
Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Sera,Bunge,Ajira ,Vijana na Watu Wenye  Ulemavu) Mhe. Jenister Mhagama na Naibu Waziri Mhe. Anthony Mavunde, wakipata maelezo namna ya kujiunga na uchangiaji wa hiari katika Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa maonesho ya Wiki ya Taifa ya Vijana yanayofanyika katika Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga .

WATOTO 18 WAMETEKWA NCHINI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU-WAZIRI KANGI LUGOLA

$
0
0
*Aweka hadharani idadi ya walipatikana wakiwa hai,na waliofariki dunia

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WATOTO 18 kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi mwaka huu wa 2018 wametekwa na kati yao 15 walipatilana wakiwa hai.Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola wakati anazungumza na waandishi wa habari.

Lugola amesema matukio ya kuteka watoto ambayo yameripotiwa katika kipindi cha mwaka 2016 hadi mwaka huu ni watoto 18, miongoni mwao walikuwa wa kiume sita na wa kike 12.

"Watoto 15 walipatikana wakiwa hai ,watoto wawili walipatikana wakiwa wamefariki na mtoto mmoja bado hajapatikana.Niwakumbushe wananchi kutoa taarifa za uhalifu wa utekaji mara tukio linapotokea ili Jeshi la Polisi lichukue hatua stahiki kwa wakati na kunusuru uhai wa wahusika," amesema Waziri Lugola.

UTEKWAJI WATU WAZIMA NDANI YA MIAKA MITATU

Wakati huo huo amesema juhudi za Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama nchini zimefanikisha kuwapata watu watano wakiwa hai kati ya watu tisa waliokuwa wametekwa mwaka 2016.Amesema watu wanne hakupatikana na katika kipindi hicho watuhumiwa sita walikamatwa na watu watano walifikishwa mahakamani na mmoja aliuawa na wananchi.

Pia amesema mwaka 2017 walitekwa watu 27 ambapo Polisi walifanikiwa kuwapata watu 22 wakiwa hai na watu wawili walipatikana wakiwa wamekufa na watu watatu hawajapatikana.Watuhumiwa 11 walifikishwa mahakamani na watatu walifariki.

Waziri Lugola amesema katika kipindi cha Oktoba 11 mwaka 2018 watu 21 walitekwa ambapo kati yao 17 walipatikana wakiwa hai na wanne hawajapatikana hadi sasa.Watuhumiwa 10 walikamatwa na kufikishwa mahakamani.

Pamoja na matukio hayo Lugola amesema anawahakikishia wananchi kwamba nchi yetu ni salama na waendelee na shughuli zao za kiuchumi na kijamii bila hofu."Jeshi la Polisi linaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kubaini na kuzuia matukio ya uhalifu ukiwemo uhalifu wa utekaji watu.Ni kutokana na juhudi hizo ndio maana wamefanikiwa kuwapata baadhi ya waliotekwa wakiwa hai,"amesema.

SSRA yatoa elimu ya Hifadhi ya Jamii katika maonesho ya Wiki ya Vijana Taifa, Jijini Tanga

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela (kulia)  akipata maelezo kuhusu Hifadhi ya Jamii kutoka kwa Maafisa wa SSRA, wakati wa Maonesho ya Wiki Vijana Taifa yaliyofanyika katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
Meneja wa Huduma za Sheria SSRA Bw, Kitangu Ugula wa kwanza kushoto akitoa Elimu ya Umuhimu wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi waliotembelea banda la SSRA kwenye Maonesho ya Wiki ya Vijana Taifa Jijini Tanga. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Tafiti, Tathimini na Sera wa SSRA Bw. Joseph Mutashubilwa.
Watumishi wa SSRA wakishiriki zoezi la kufanya usafi katika kituo cha kulelea wazee cha Duga Tanga, katika Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Taifa Jijini Tanga.
Maafisa kutoka SSRA wakito elimu ya Hifahi ya Jamii kwa viongozi wa Baraza la Vijana la Taifa Zanzibar walipotembelea banda la Mamlaka wakati wa Maonesho ya Wiki ya Vijana Taifa yanayofanyika katika Viwanja vya Tangamano Mkoani Tanga.
Watumishi wa SSRA wakishiriki zoezi la kufanya usafi katika kituo cha kulelea wazee cha Duga Tanga, katika Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Taifa Jijini Tanga.

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA KATIKA 'ROTARY DAR MARATHON' LEO

$
0
0
Sehemu ya Umati wa washiriki wa mbio mbali mbali katika 'Rotary Dar Marathon' wakiwa tayari kushuhudia washiriki wa mbio ndefu za kilometa 42.2 (42.2KM Marathon) walipokuwa wakianza mbio hizo mapema leo asubuhi katika makutano ya barabara ya Kenyatta na Toure Drive, Masaki jijini Dar es salaam. Mbio hizo zilizohudhuliwa na watu mbali mbali zilikuwa ni zenye mvuto wa aina yake huku wakimbiaji wakionekana kuchuana vikali, huku kila mshiriki alionyesha uwepo wake wa hali ya juu pamoja na kuchelewa kwa takribaki saa mbili za kuanza kwa mbio hizo.
Washiriki wa mbio ndefu za kilometa 42.2 (42.2KM Marathon) wakianza kutimua mbio hizo mapema leo asubuhi katika makutano ya barabara ya Kenyatta na Toure Drive, Masaki jijini Dar es salaam.


NSSF WAUNGANA NA WATANZANIA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

MASAUNI ASEMA SERIKALI ITAFUNGA CCTV CAMERA KATIKA MIJI NA MAJIJI

$
0
0

 Na Ahmed Mahmoud
Serikali imesema ipo mbioni kufunga kamera maalum (CCTV camera) kwenye miji na majiji mbalimbali nchini ili kudhibiti masuala ya uhalifu ikiwemo suala la utekaji unaofanywa na watu wasiojulikana.

Aidha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuph Masauni amewaonya wanasiasa uchwara wanaotumia matatizo yanayotokea nchini kuacha mara moja tabia za kuisema serikali, taasisi na mashirika na wakiendelea watachukuliwa hatua. Masauni aliyasema hayo mapema leo Jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Murriet jijini Arusha katika ziara yake ya kukagua vituo vya Polisi ikiwemo kujua kama watuhumiwa wanapewa dhamana kwa saa 24 au la na masuala muhimu ya usalama.

Alisema kamera hizo zitafungwa kwaajili ya kubaini wale watekaji na watu wasiojulikana na kusisitiza kuwa ole wao wanasiasa wanaotumia matukio yanayotokea kwaajili ya kujipatia umaarufu wa kisiasa nchini. Alisema suala la ulinzi ni lazima lidhibitiwe haswa maeneo ya mipakani ili kudhibiti wale watu wenye nia ovu ndio maana hivi sasa mkakati wa serikali ni kufunga vifaa vya teknolojia ya kisasa zaidi.

“Hivi sasa serikali inamkakati wa kufunga kamera maalum kwaajili ya kudhibiti matukio ya kihalifu yanatokea katika miji na majiji na natoa onyo kwa wanasiasa kuacha kutumia suala la utekaji wa Mohamed Dewji kama mtaji wao waache vyombo vya dola zifanye kazi yake “ Pia alimwagiza Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha,Almachius Mchunguzi kuhakikisha anatatua changamoto za kihalifu ikiwemo kutoa dhamana kwa washitakiwa kwa makosa yanatistahili dhamana ndani ya saa 24 na kulipobgeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupunguza uhalifu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuph Masauni

NAIBU KATIBU MKUU KAILIMA AKABIDHIWA NYUMBA NA TANROAD KWA AJILI POLISI SIMIYU

$
0
0


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhan Kailima (katikati) akikata utepe kuashiria kupokea nyumba za makazi ya Polisi zilizojengwa na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mjini Bariadi Mkoani Simiyu. Katika hotuba yake mara baada ya kuzipokea nyumba hizo, Kailima aliishukuru Tanroads na kuwataka wananchi mkoani humo kuendelea kutoa taarifa za uhalifu katika maeneo yao ili kuimarisha ulinzi na usalama. Wapili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga, na kushoto ni Meneja wa Tanroad mkoa huo, Albert Kent.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhan Kailima akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya nyumba za makazi ya Polisi zilizojengwa na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mjini Bariadi Mkoani Simiyu. Kailima aliishukuru Tanroads kwa ujenzi wa nyumba hizo na pia aliwataka wananchi mkoani humo kuendelea kutoa taarifa za uhalifu katika maeneo yao ili kuimarisha ulinzi na usalama zaidi. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga.
Sehemu ya nyumba za makazi ya Polisi Jeshi la Polisi mkoani Simiyu zilizojengwa na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS). Nyumba hizo zilipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhan Kailima (hayupo pichani) katika hafla ya mapokezi iliyofanyika mjini Bariadi mkoani humo. Kailima aliishukuru Tanroads kwa ujenzi wa nyumba hizo na pia aliwataka wananchi mkoani humo kuendelea kutoa taarifa za uhalifu katika maeneo yao ili kuimarisha ulinzi na usalama zaidi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MAZINGIRA BORA YA MIRADI KUIPATIA MIKOPO SEKTA BINAFSI TOKAKA KATIKA MASHIRIKA YA KIMATAIFA

$
0
0



Na. WFM, Bali Indonesia.

Mazingira bora yakutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Sekta Binafsi kutaiwezesha sekta hiyo kupata fedha katika Mashirika ya Kimataifa ambayo yametenga bajeti kwa ajili ya kuimarisha sekta hiyo.
Hayo yameelezwa mjini Bali Indonesia na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, baada ya kumalizika kwa  mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) iliyowakutanisha Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu wa nchi mbalimbali.

Dkt. Mpango alisema kuwa, yapo Mashirika ambayo yapotayari kutoa fedha iwapo kuna uhakika wakurudishwa kwa fedha hizo kama zitatolewa kwa mfumo wa  mikopo, hivyo ni vizuri mazingira ya utekelezaji miradi ya Sekta Binafsi yakaboreshwa ili kuwe na urahisi wa upatikanaji wa fedha hizo.
Alisema kuwa, nchi za Afrika ikiwemo Tanzania zinahitaji pia fedha za kuwekeza kwenye miundombinu ya kiteknolojia ili kuweza kuchochea ukuaji wa uchumi.

“Kama nchi inatakiwa kuhakikisha  inaongeza mapato ya ndani ya kodi  na yasiyo ya kodi kwa kuwa jambo hilo ni moja ya kigezo chakuweza kupata fedha zaidi kutoka Mashirika ya Kimataifa”, alieleza Dkt. Mpango.
Naye Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Yamungu Kayandabila, alisema kuwa katika mikutano ya mwaka ya WB na IMF, imesisitiza kuondoa vikwazo vya kibiashara kati ya nchi na nchi  kwa kuwa biashara imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza pato na uchumi wa nchi unategemea mahusiano mazuri kati ya taifa moja na lingine.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwa katika Mkutano na  Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Christine Lagarde (hayupo pichani), mjini Bali Indonesia.
2
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kushoto) akiwa na Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi mbalimbali wakati wa Mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Christine Lagarde (hayupo pichani), mjini Bali Indonesia ambapo suala la mwenendo wa uchumi wa Afrika uliangaziwa.
3
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Christine Lagarde, akizitaka nchi za Afrika kuboresha uchumi,  wakati wa mkutano kati yake na Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi mbalimbali mjini Bali, Indonesia.4
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Christine Lagarde (kushoto) akifurahia jambo wakati wa mkutano kati yake na Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi mbalimbali mjini Bali, Indonesia, wakati wa kumalizika kwa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa.
5
Viongozi wa Shirika la Fedha la Kimataifa wakiwa wamesimama  kwa muda mfupi kukumbuka maafa yaliyotokea kipindi kama hiki mwaka uliopita nchini Somalia, wakati wa  mikutano ya Benki ya Dunia (WB)  na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Bali Indonesia.
6
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Christine Lagarde, Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu wa nchi mbalimbali  wakiwa katika Mkutano mjini Bali, Indonesia .(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango mjinin Bali Indonesia).

MATUKIO KATIKA PICHA SPIKA NDUGAI AKIWA KATIKA MISA MAALUMU YA KITAIFA YA KUMUOMBEA HAYATI BABA WA TAIFA LEO JIJINI TANGA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na waumini (hawapo kwenye picha) wa kanisa kuu la Mtakatifu Antoni wa Padua Jimbo katoliki la Tanga katika Misa Maalumu ya kitaifa ya kumuombea Hayati Baba wa Taifa iliyofanyika leo tarehe 14 Octoba, 2018 Jijini Tanga.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati)akiwa katika picha pamoja na wakimbiza mwenge wa uhuru katika tukio lililofanyika leo tarehe 14 Octoba, 2018 katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga, katika kuzima mwenge kitaifa
Waumini wa kanisa kuu la Mtakatifu Antoni wa Padua Jimbo katoliki la Tanga wakiwa katika Misa Maalumu ya kitaifa ya kumuombea Hayati Baba wa Taifa iliyofanyika leo tarehe 14 Octoba, 2018 Jijini Tanga.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiagana na Askofu Mkuu wa kanisa kuu la Mtakatifu Antoni wa Padua Jimbo katoliki la Tanga, Anthony Banzi baada ya kumalizika kwa Misa Maalumu ya kitaifa ya kumuombea Hayati Baba wa Taifa iliyofanyika leo tarehe 14 Octoba, 2018 Jijini Tanga.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (watatu kushoto) aongoza viongozi Mbali mbali wa kitaifa katika Misa Maalumu ya kitaifa ya kumuombea Hayati Baba wa Taifa iliyofanyika leo tarehe 14 Octoba, 2018 katika kanisa kuu la Mtakatifu Antoni wa Padua Jimbo katoliki la Tanga Jijini Tanga.(PICHA NA OFISI YA BUNGE
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images