Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

NECTA YAFUTA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA KWA BAADHI YA SHULE ZA MSINGI NCHINI

$
0
0
*Ni baada ya kubaini kufanya udanganyifu, yatangaza kurudiwa kwa mtihani

Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii
HATIMAYE Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza kuyafuta matokeo ya mitihani ya darasa la saba kwa shule za msingi zote zilizopo ndani ya Halmashauri ya Chemba mkoani Dodoma,  pamoja na baadhi ya shule zilizopo katika halmashauri ya Ubungo, Kinondoni, Kondoa na Mwanza.

Kwa mujibu wa Necta imeamua kufuta matokeo ya shule hizo baada ya kubaini kuvuja kwa mtihani huo katika shule hizo na kwamba hilo ni jambo ambalo ni kinyume na sheria na kanuni za mitihani nchini kwetu.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Taifa (NECTA) Charles Msonde ametangaza uamuzi huo leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuvunjwa kwa kanuni za mitihani baraza hilo limeamua kufuta matokeo ya mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi katika shule  za msingi za halmashauri hizo.

"Hivyo watahiniwa wote watarudia tena mtihani huo Oktoba 8 na 9 mwaka huu kwa halmashauri zote ambazo halmashauri zao uchaguzi umefutwa baada ya kubaini umevuja," amesema Dk.Msonde.

Ametaja shule ambazo zimefutiwa matokeo ya mtihani imo Shule ya Msingi Hazina na New Hazina zilizopo Magomeni wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Pia Shule ya Aniny Nndumi na Fountain of Joy zilizopo Ubungo, Shule ya Msingi Kondoa Integrity  iliyopo Halmashauri ya Kondoa, pamoja na Shule ya Msingi Kisiwani,  Alliance na New Alliance zilizopo Mwanza.

Dk.Msonde amesema pia  baraza hilo limefuta vituo vya mitihani kwa shule nane ambazo zilihusika katika uvujishaji wa mitihani hiyo sambamba na kupendekeza kuondolewa kwenye nafasi za ajira kwa baadhi ya maofisa elimu kata na wilaya waliohusika kwenye udanganyifu huo.

Amefafanua Necta wameidhinisha vituo mbadala vya mtihani vitakavyotumiwa na watahiniwa katika mtihani wa marudio utakaoufanya Ocktoba 8 na 9 wiki ijayo.

" Shule ya Msingi  Hazina na New Hazina wanafunzi wake wa darasa la saba watafanya mtihani huo katika shule ya Msingi Osterbay.

" Shule ya Fountain of Joy na Aniny Nndumi za Ubungo zitafanya mtihani katika shule ya Msingi Mbezi.Shule ya Msingi Kisiwani ya jijini Mwanza wanafunzi wake watafanya mtihani huo kwenye shule ya Msingi Kakebe.

"Shule ya Alliance na New Alliance watahiniwa watafanya mtihani katika shule ya Msingi Mahina na Shule ya Msingi ya Kondoa Integrity wanafunzi watafanya mtihani kwenye shule ya Msingi Bicha, " amefafanua.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU AWEKA WAZI NAMNA ATAKAVYOIENDESHA TAASISI HIYO NYETI YA KUPAMBANA NA WALA RUSHWA NCHINI

$
0
0
Awaaga Rasmi Watumishi na Wananchi 
wa Mkoa wa Kagera Kama Katibu Tawala wa Mkoa

Na Sylvester Raphael
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini Kamishina wa Polisi (CP) Diwani Athumani aongea rasmi na Vyombo vya Habari nchini kwa mara ya kwanza akiwa Mkoani Kagera na kutaja vipaumbele vyake katika kuiongoza TAKUKURU ili iweze kufanya kazi kwa kasi na ufanisi katika mapambano dhidi ya rushwa.

Mkurugenzi Mkuu Diwani Athumani akitaja vipaumbele hivyo Oktoba Mosi, 2018 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwenye hafla fupi ya kuongea na kuwaaga rasmi Watumishi wa Serikali kama Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera alisema kuwa vipaumbele hivyo vimegawanyika katika sehemu kuu mbili ambapo kuna vipaumbele vya muda mfupi na vya muda mrefu ili kuifanya TAKUKURU kutekeleza majukumu yake kulingana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Vipaumbele vya Muda Mfupi; Kwanza ni kuwasimamia watumishi walio chini ya TAKUKURU kuchapa kazi kwa bidii na kuachana na utendaji wa mazoea. Pili, atahakikisha anachukua hatua stahiki na kwa wakati kwa watumishi wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa. Tatu, Kupeleka Kesi zote za masuala ya rushwa  Mahakamani na kufuatilia mienendo ya kesi hizo. Nne, kufuatilia miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa kama inatekelezwa kwa thamani stahiki kulingana na fedha iliyotolewa na Serikali.

Vipaumbele vya Muda Mrefu: Kwanza, Kufanya uchunguzi katika mfumo wa mapato ili kuziba mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali. Katika kipaumbele hiki Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Diwani Athumani alitolea mfano wa Wafanybiashara wanaotoa risiti za (EFD) zenye gharama pungufu ya kiwango cha fedha tofauti na thamani halisi ya bidhaa ilyonunuliwa kutoka katika maduka yao.

Kipaumbele cha Pili ni kufuatilia kesi zote za rushwa  zilizopo Mahakani na kuhakikisha kesi hizo zinafika mwisho kwa kutolewa hukumu. Tatu, Kutoa elimu kwa umma kuhusu athari za rushwa na kuelimisha wananchi kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwani madhara yake ni makubwa. Nne, Kuweka mfumo mzuri wa kuhakikisha wananchi wanatoa taarifa za wala rushwa lakini pia kuhakikisha wananchi hao wanalindwa mara baada ya kutoa taarifa za kweli. Tano, ni kuongeza ushirikiano kati ya TAKUKURU na wadau wote katika mapambano dhidi ya wala rushwa nchini.

Mkurugenzi Mkuu mpya wa (TAKUKURU) nchini Kamishina wa Polisi Diwani Athumani alisema kuwa ameweka vipaumbele hivyo katika kutekeleza majukumu yake akiwa Mkurugenzi Mkuu lengo kuu likiwa ni kumsaidia Rais John Pombe Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa nchini. Lakini pia kuhakikisha anashirikiana na wadau wote wapinga rushwa kuhakikisha kaulimbiu ya “Tanzania Bila Rushwa Inawezekana”  inatimia.
 Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Nchini Kamishina wa Polisi Diwani Athumani akiongea na watumishi wa mkoa wa Kagera wakati wa ziara yake pamoja na kuwaaga.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Mstaafu Marco E Gaguti akitoa shukrani zake kwa  Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Nchini Kamishina wa Polisi Diwani Athumani.
 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nesphory  Bwana akitoa neno katika hafla fupi ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuongea watumishi.
Watumishi wakimsikiliza kwa umakini Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Diwani Athumani
 Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Kagera wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU  CP Diwani Athumani.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Mazao ya Chai, Kahawa, Mbogamboga pamoja na Matunda yapewa kipaumbele cha kuongeza thamani

$
0
0
Na Khadija Seif , Globu ya Jamii
SERIKALI  imepata msaada wa sh. Bilioni 265.5  kutoka Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuboresha mnyororo wa thamani wa mazao ya ya Chai, Kahawa, Mbogamboga  pamoja na Matunda.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutiliana saina na umoja wa Ulaya  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James amesema kuwa fedha hizo sio mkopo hivyo zitakwenda katika miradi iliyokusudiwa. Kutokana na vipaumbele vya fedha hizo.
James amesema msaada huo unatokana na miradi iliyofanyika kwa msaada wa umoja wa Ulaya kufanya vizuri na ndo maamna wamekuwa na imani na kutopa fedha kwa mara nyingine.

Amesema lengo  kuu mradi  wa kuboresha kilimo hicho ni  kukuza uchumi , kuimaraisha sekta binafsi na kuongeza ajira , Chakula na Lishe nchini.

Kipaumbele cha kwanza ni kutekeleza sera ya kilimo bora nchini ili kuongeza thamani ya Mazao ya Chai,Mbogamboga na Matunda ikiwa ni katika kuboresha barabara za vijijini katika maeneo ya utakapotekelezwa, uboreshaji wa sera ,sheria ,na mazingira ya biashara katika sektaa husika, kuendeleza mnnyororo thamani katika mazao ya Chai, Kahawa, Mbogamboga na Matunda, pamoja na kuongeza elimu na kuimarisha matumizi ya lishe bora.

Katibu Mkuu ofisi ya  waziri Mkuu sera na uratibu profesa Faustine Kamuzora ametoa shukrani kwa msaada huo wa fedha ambazo zitatumika katika vipaumbele vilivyoanishwa .

Kamuzora amesema wanakilimo wanakumbwa sana na changamoto ya miundombinu ya usafirishaji wa mazao  kwani imekua vigumu kisafirishwa  kwenda sehemu za mbali kutoka na barabara kuwa mbovu hivyo kupelekea mazao ambayo yanashindwa kuhimili hali ya hewa  inamlazimu kupeleka zao ambalo tayari limepoteza uhalisia wake.

Naibu Katibu Mkuu kutoka Zanzibar Hamadi Kassim Haji ametoa shukrani kwa kuendeleza  Kutuunga Mkono katika harakati za Maendeleo kwa Msaada wa euro 100.

 Haji amesema kwa upande wa Mji wa Zanzibar wamejikita Kwenye Kilimo cha chai na Mbogamboga na fedha hizi zimefika wakati ambao serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inajipanga kuboresha Maendeleo kwa wakulima wa mazao mbalimbali.

Mkurugenzi wa shirika la EU ameeleza lengo la kusaidia fedha hizi ni kwa lengo la wakulima wadogowadogo japo hakuna ushirika wa wakulima kupitia serikali za mitaa itaweza kufikisha fedha hizo kwa vyama vya wakulima hao.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akitia saini makubaliano na Umoja wa Ulaya katika mradi uboreshaji mnyororo wa thamani katika mazao ya Kahawa, Chai, Mbogamboga  pamoja na Matunda
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akizungumza mara baadaya kutia saini ya msaada uliotololewa na Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuongeza thamani ya mnyororo wa thamani katika mazao Chai, Kahawa, Mbogamboga pamoja na Matunda katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini  Roeland Van De Gier akizungumza katika hafla ya kutiliana saini na serikali ya Tanzania ya utoaji wa fedha katika uboreshaji wa mnyororo wa thamani wa mazao ya Chai, Kahawa, Mbogamboga pamoja na Mtunda.
Picha ya pamoja Makatibu wakuu waliohudhuria utiaji saini, Balozi Umoja wa Ulaya  pamoja na wawakilishi wa Umoja huo.

DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOFANYIWA SUPRISE NA WAFANYAKAZI WA WASAFI TV

Michuzi TV: Aunty Ezekiel afunguka katika red carpet ya Jibebe challenge finals jijini Dar es salaam

MICHUZI TV: BODABODA ZITAKAZOINGIA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM SASA KUKIONA - KAMANDA MAMBOSASA

NTUC MEDIA: Mkoa Wa Tabora unaongoza kwa Mauaji, ndoa za utotoni na Ushirikina Nchini Tanzania - RC Aggrey Mwanri

Rais Magufuli atekeleza ahadi ya kutoa Milioni 20 kwa wavuvi na Mama Janeth Magufuli Milioni 5 za mama ntilie eneo la feri jijini Dar es salaam

$
0
0

Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwa na  Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani   wakielekea sehemu itapojengwa ofisi zao katika utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwaangalia Makamu Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani na kiongozi wa akina Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga wakiweka sahihi katika hati za makabidhiano ya fedha taslimu kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli huku wakishuhudiwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sofia Mjema, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Tulusubisya Kamalama na mshauri wa Rais Masuala ya sheria Bw. Dunstan Kiobya (kushoto)
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi  msaada wa shilingi Milioni 20 kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli alizowaahidi kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Umoja huo Bw. Amiri Amani, Mwenyekiti wa Umoja wa Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam. 
  Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi msaada wa shilingi milioni 5 kutoka kwa mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kwa kiongozi wa Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga alizoahidi kuwasaidia Mama wajasiriamali wanaofanya biashara ndogondogo hasa ya Mamalishe katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam. 
  Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimsikiliza Bw. Amiri Amani, Mwenyekiti wa Umoja wa Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam akishukuru kwa msaada wa shilingi Milioni 20 kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli alizowaahidi kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Umoja huo PICHA NA IKULU
Habari zaidi BOFYA HAPA

MBIO ZA ROTARY DAR MARATHON ZAPIGA HODI

$
0
0
Dar es Salaam. Mwaka huu unaweka alama ya maadhimisho ya miaka 10 ya Mbio za Rotary Dar, tukio la hisani ambalo limekuwa likiweka rekodi kubwa katika usajili kila mwaka.

Kupitia mbio hizo,miradi mbalimbali ya huduma za kijamii imekuwa ikitekelezwa kwa miaka tisa mfululizo iliyopita kupitia fedha ambazo huwa zinachangwa ikiwemo upandaji miti zaidi ya 26,000,utoaji wa huduma ya maji safi ya kunywa shuleni,

Ujenzi wa wodi ya saratani ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kituo cha maendeleo ya ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwaka huu, matembezi ya hisani na mbio za Rotary Dar zinalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa kliniki maalum katika Hospitali ya CCRBT itakayowezesha utoaji huduma na kupunguza gharama zinazotolewa kwa watu wenye ulemavu.

Mbio za Rotary Dar ni juhudi za pamoja baina ya klabu nane za Rotary jijini Dar es Salaam ambazo zimekuwa zikiungwa mkono kwa ufadhili mkubwa wa Benki M na Pepsi.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mwenyekiti wa Bodi wa Mbio za Rotary Dar, Bi. Sharmila Bhatt amesema, "Tunaamini ushirikiano wa kimkakati tuliokuwa nao na Benki M ulikuwa na mafanikio makubwa jambo lilopelekea muelekeo mzuri na kutoa motisha kwa wafadhili wengine katika ambao wanatuunga mkono mwaka huu," alieleza na kuongeza kuwa, "mwaka huu Pepsi nao wameongeza hatua nyingine zaidi kwa ajili ya kutangaza michezo Tanzania kwa kutoa ufadhili wa jumla kwa Mtanzania mwanaume na mwanamke atakayefanya vizuri katika mbio za kilomita 42.2, ambapo watapelekwa kushiriki mbio za Beirut Marathon nchini Lebanon.

Msanii wa kike anayetamba zaidi nchini, Vanessa Mdee al-maarufu Vee-Money ambaye pia ni Balozi wa wa Mbio za Rotary Dar kwa mwaka huu akizungumza leo (Oktoba 02, 2018) jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kutangaza rasmi maandalizi ya mbio za Rotary Dar zitakazofanyika Oktoba 14 mwaka huu (Siku ya Mwalimu Nyerere). Vanessa atashiriki mbio za Rotary Dar kwa mwaka huu lakini pia atatumia ushawishi alionao kuwahamasisha watu wengi zaidi kushiriki. Pamoja nae ni Mwenyekiti wa Bodi wa Mbio za Rotary Dar, Bi. Sharmila Bhatt (kulia) na Mkurugenzi Uendeshaji wa CCBRT, Brenda Msangi (kushoto).
Mkurugenzi Uendeshaji wa CCBRT, Brenda Msangi (kushoto) akionyesha kipeperushi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo (Oktoba 02, 2018) jijini Dar es Salaam kuelezea baadhi ya huduma maalumu zinazotolewa na hospitalini hapo wakati wa hafla ya kutangaza rasmi maandalizi ya mbio za Rotary Dar zitakazofanyika Oktoba 14 mwaka huu (Siku ya Mwalimu Nyerere). Pamoja nae ni Msanii Vanessa Mdee al-maarufu Vee-Money (katikati) ambaye pia ni Balozi wa wa Mbio za Rotary Dar kwa mwaka huu na Mwenyekiti wa Bodi wa Mbio za Rotary Dar, Bi. Sharmila Bhatt (kulia).
Mwenyekiti wa Bodi wa Mbio za Rotary Dar, Bi. Sharmila Bhatt (kulia) akizungumza leo (Oktoba 02, 2018) jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kutangaza rasmi maandalizi ya mbio za Rotary Dar zitakazofanyika Oktoba 14 mwaka huu (Siku ya Mwalimu Nyerere). Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio za Rotary Dar, Catherinerose Barretto, Mkurugenzi Uendeshaji wa CCBRT, Brenda Msangi na Msanii Vanessa Mdee al-maarufu Vee-Money ambaye pia ni Balozi wa wa Mbio za Rotary Dar kwa mwaka huu.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 02.10.2018

Color Of Music Exhibition! and Fun October @ NAFASI ART SPACE, DAR ES SALAAM

$
0
0

After an intensive two day workshop of 3D drawing, perspective drawing, then painting, Our Artist in Residence Dullah Wise is ending his visit with a beautiful Exhibition namely-Color of Music. Come explore his beautiful work and have a chance to ask questions and have an exchange with Dullah. 
More infomation on Dullah: https://www.dullahwise.com/
Do not plan to miss this.

INTRODUCING TANZANIA YETU NI NCHI YENYE FURAHA NA PETER MSECHU

TCCIA YAWEKA MIPANGO MKAKATI WA KUTATUA MATATIZO YA WAFANYABIASHARA

$
0
0
CHAMA cha wafanyabiashara, viwanda na kilimo nchini TCCIA ,imeweka mipango mikakati katika kutekeleza maazimio yaliyotolewa na serikali kufuatia tathimini kwamishi ya miaka mitano ambapo imelenga kuboresha shughuli mbalimbali za biashara,viwanda na kilimo.

Kimeweka utaratibu wa kuwawezesha wakulima wa korosho kwa kuwapatia nyenzo bora kwa kuwa zao hilo limechukua nafasi kubwa miongoni mwa mazao ya biashara katika kuliongezea pato Taifa kwa takribani miaka mitatu mfululizo.Maazimio hayo yalitolewa jana jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa bodi ya wakurugenzi wa TCCIA uliowashirikisha wadau kutoka ngazi ya kata wilaya mkoa na taifa katika kujadili masuala mbalimbali yanayowakwamisha wafanyabiashara .

Makamu wa rais TCCIA upande wa kilimoa bw. Joseph Kaungwa alisema kuwa kumejitokeza vikwazo vingi ambavyo vimechangia kukwamisha shughuli za kibashara viwanda na kilimo visisonge mbele vikiwemo kodi na tozo mbali mbali.Pia alisema kutowapa nyenzo bora pamoja na pembejeo uwezeshi na masoko ya uakika yenye kukidhi matakwa ya bidhaa zizalishwazo na wakulima ambazo kimsngi uwapatia wakati mgumu kipindi cha kuandaa mashamba na kipindi cha mavuno.

Kwa upande wake makamu wa rais TCCIA katika masuala ya biashara bwa. Julias kaijage alisema kuwa chama hicho kimeweko mifumo ya uendesheji ambayo ni bodi katika kujadili maazimio mbalimbali na kuwezesha wafanyabiashara kujipatia manufaa .

“Wakati nchi ikielekea kwenye uchumu wa kati tunawataka wafanyabiashara kuachana na masuala ya uchuuzi ambayo hayana nafasi katika kuwaletea maendelo, ‘alisema Kaijage.Nae mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mtwara Bw.Swallah Saidi alisema wamewafundisha wakulima namna ya kuifadhi korosho ili ziweze kupata bei nzuri katika soko la kimataifa ambapo itawapatia wakulima kipato cha kutosha.

“Tumezalisha zaidi ya tani laki tatu kwa lengo la kuongeza uzalishaji na kuitangaza korosdho katika masoko ya nnje ambapo kurosho ya Tanzania imekuwa bora zaidi katika nchi zinazolima zao hili afrika.
Kulia ni Kaimu Rais wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na Killimo (TCCIA) Octavian Mshiu akichangia baadhi ya maazimio yaliyotolewa na wanacha katika mkutano wa bodi ya wakurugenzi TCCIA jijini Dar es Salaam jana . Picha na Nicolas Gilliard.
Washiriki wakiwa katika mkutano wa bodi ya wakurugenzi TCCIA jijini Dar es Salaam jana . Picha na Nicolas Gilliard.
Baadhi washiriki wakiwa katika pica ya pamoja mara baada ya kuamaliza mkutano wa bodi ya wakurugenzi TCCIA jijini Dar es Salaam jana . Picha na Nicolas Gilliard.

UEFA EUROPA league kuendelea tena Alhamis hii ndani ya Startimes

$
0
0
UEFA EUROPA league itarejea tena usiku wa tarehe 4 ya mwezi Oktoba siku ya Alhamisi kama ilivyo kawaida ya ligi hiyo. Kivutio kikubwa kwa msimu huu kikiwa ni timu kubwa kutoka ligi ya Uingereza (PL) Chelsea na Arsenal ambazo zina mashabiki na wapenzi lukuki katika bara la Afrika na hasa nchini Tanzania.

Kwa wiki hii Arsenal itakuwa ugenini dhidi ya Qarabag FK katika dimba la Baku Olympic Stadium, Arsenal wataingia uwanjani bila kiungo wao Muarmenia Henrikh Mkhitaryan ambaye hataweza kuingia nchin Azerbaijan kutokana na uhasama baina ya nchi hizo mbili. Pia timu hiyo imeshinda mechi zao tano zilizopita katika mashindano yote na wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo.

Kwa upande wa Chelsea wao watakuwa nyumbani katika dimba la Stamford Bridge maarufu kama darajani wakiwakaribisha MOL Videoton ya Hungary. Chelsea wamepata matokeo ya kuridhisha tangu kuanza kwa msimu mpya, Eden Hazard anatarajiwa kuendeleza wimbi lake la upachikaji mabao kwa msimu kwani amekuwa na kiwango bora kabisa akiamua matokeo ya mechi kadhaa na za muhimu kwa timu yake.

Mechi kubwa inatarajiwa kuwa ile ya AC Milan dhidi ya Olympiacos katika dimba la Giuseppe Meazza, AC Milan bado hawajawa na makali yao ya zamani lakini wanaonesha kiwango kizuri katika ligi ya Italia, pia watakuwa bila mshambuliaji wao Gonzalo Higuain ambaye anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja. Mchezo huu utarushwa moja kwa moja kwa lugha ya Kiswahili kupitia king’amuzi cha StarTimes pekee.

Michezo mingine ni RB Leipzig dhidi ya Celtic FC, Bayer Leverkusen dhidi ya AEK Larnaca FC, Fenerbahce dhidi ya FC Spartak Trnava, Anderlecht dhidi ya GNK Dinamo Zagreb, michzo yote hii itarushwa moja kwa moja katika chaneli za michezo kwenye king’amuzi cha StarTimes.

Mbali na mechi za EUROPA burudani ya aina yake itakuwa Wikendi hii katika jiji la Paris ambapo vinara wa Ligue 1, Paris Saint German watakuwa nyumbani dhidi ya mahasimu wao Olympic Lyon. PSG wana kikosi bora chenye wachezaji wenye majina na uwezo mkubwa lakini Lyon kikosi chao kinaundwa na Vijana wenye vipaji na uwezo vile vile, itakumbukwa msimu uliopita Lyon waliilaza PSG mabao 3-2 katika dimba hilo hilo. Macho yetu yataelekea Paris wikiendi hii huku mchezo ukiwa mubashara kupitia StarTimes ambao watarusha mechi zote za ligi hiyo.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA AKILI CHA MIYUJI DODOMA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia watoto wenye ulemavu wa akili wakati alipotembelea Kituo cha watoto hao, cha Miyuji Cheshire House cha jijini Dodoma, Septemba 2, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipotembelea Kituo cha Watoto Wenye Ulemavu wa Akili cha Miyuji Cheshire House cha jijini Dodoma, Oktoba 2, 2018. Wapili kushoto ni Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde, watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge, kulia ni mwakilishi wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Dodoma, Padri, Onesmo Wisi na wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo hicho, Peter Mavunde. (Picha na Ofisi a Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhi zawadi ya keki kwa watoto wa Kituo cha Watoto Wenye Ulemavu wa Akili cha Miyuji Cheshire House jijini Dodoma, Septemba 2, 2018. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo hicho, Peter Mavunde na wapili kushoto ni mwakilishi wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Dodoma, Padri, Onesmo Wisi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la zabibu la Kituo cha Watoto Wenye Ulemavu wa Akili cha Miyuji Cheshire House kilichopo Miyuji jijini Dodoma, Oktoba, 2, 2018. Watatu kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge, wapili kulia ni Mwakilishi wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Dodoma, Padri Onesmo Wisi na wanne kushoto ni Mwalimu wa Kituo hicho, Josephine Baharia.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde wakati alipowasili kwenye Kituo cha Watoto Wenye Ulemavu wa Akili cha Miyuji Cheshire House cha jijini Dodoma, Oktoba 2, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Uongozi NHIF watembelea Wadau Mbeya

$
0
0
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dkt. Doroth Gwajima akiangalia mtoto ambaye amezaliwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya Kitengo cha Wazazi Meta. Baadhi ya wajumbe wa Bodi na Maofisa wa NHIF walitembelea hospitali hiyo kuangalia huduma za wanazopata wanachama wake.

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umetembelea Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya na baadhi ya Vituo mkoani humo kwa lengo la kuangalia huduma wanazopata wanachama wake.

Katika ziara hiyo, ujumbe wa NHIF ulikutana na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Kitengo cha Wazazi Meta na Hospitali ya Uyole ambapo pamoja na mambo mengine walijadili juu ya huduma zinazotolewa kwa wanachama wa Mfuko.

Akiongoza ziara hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Bwana Tryphon Rutazamba alisema kuwa mbali na kujadili huduma lakini pia wamepata fursa ya kukagua mradi wa Jengo la Wodi ya Daraja la Kwanza inayojengwa pamoja na uzalishaji wa Maji tiba katika hospitali ya Rufaa Mbeya kwa fedha za Mkopo wa NHIF.

“Tumepita na kuangalia maeneo ambayo wanachama wetu wanapata huduma, tumeona pia wanachama na kuzungumza nao ambao wamekiri kupata huduma nzuri hivyo tunawapongeza hawa watoa huduma kwa jitihada kubwa za uboreshaji wa huduma ambazo wanazifanya,” alisems Bw. Rutazamba.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dkt. Fred Mbwanji aliushukuru Mfuko kwa kuboresha huduma zake lakini pia kwa fursa ya mikopo nafuu ambayo imewawezesha kuboresha kwa kiwango cha juu huduma za matibabu hospitalini hapo.

“Tunajenga Wodi ya Daraja la Kwanza kwa fedha ambazo ni mkopo nafuu kabisa kutoka NHIF, lakini pia tuna mradi wa kuzalisha Maji Tiba ambao ni mkopo pia kutoka kwenye Mfuko hivyo unaweza ukaona ni kwa namna gani NHIF imekuwa ni nguzo kubwa katika uimarishaji na uboreshaji wa huduma,” alisema Dkt. Mbwanji.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi Tryphon Rutazamba akimsalimia Mama na mtoto ambao ni wanachama wa Mfuko waliokuwa wamelazwa katika Hosptali ya Wazazi Meta, Mbeya.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Uyole Mbeya Dkt. Sijabaja akitoa maelezo kwa huduma anazotoa katika hospitali hiyo. 

Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu NIDA

ACACIA kukusanya milioni 340 kuboresha elimu nchini

$
0
0
Kampuni ya uchimbaji wa madini Tanzania – Acacia inatarajia kukusanya zaidi ya Sh milioni 340 kwa kupitia mashindano ya mbio za baiskeli kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa elimu kwa jamii zinazozunguka migodi yetu katika kanda ya ziwa. 

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo nchini, Asa Mwaipopo, Meneja Uboreshaji tija kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini nchini Tanzania – ACACIA, Janeth Ruben alisema mashindano hayo wameyapatia jina la ‘Acacia Imara Pamoja Cycle Challenge’ na yanaenda sambamba na mpango wa kampuni wa kujenga jamii endelevu. 

Alisema mpango huo unaofahamika kwa jina la ‘CanEducate’,unatoa kipaumbele katika kuhakikisha jamii zetu – hasa watoto wa kike - wanapata elimu bora kama njia moja wapo ya kujikwamua na umaskini na kufanikisha dhamira ya serikali ya kuinua uchumi na hali za maisha ya watanzania kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Maendeleo 2025. 

“Fedha hizo zitasaidia wanafunzi wanaotoka katika familia maskini na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia sare na vifaa vingine vya shule ikiwemo vitabu na vifaa mbalimbali. “Pia zitaelekezwa katika kusaidia wanafunzi wa kidato cha tano na sita wanaotoka kwenye maeneo yanayozunguka migodi yetu kwa kuwalipia ada za mitihani, gharama za malazi na usafiri. Wanafunzi wengi wa ngazi hii husafiri umbali mrefu kufika shule zinazotoa elimu kwa ngazi hiyo ya ‘A Level’.” Alisema. 

Ali hasa sasa mpango huo wa CanEducate ulioanza mwaka 2011, umetumia kiasi cha Sh milioni 494 kwa kuwadhamini wanafunzi 3936, na kuziwezesha kwa njia mbalimbali shule zaidi ya tisa. 

Meneja Uboreshaji tija kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini nchini Tanzania – ACACIA, Janeth Ruben (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu wa mashindano ya mbio za baiskeli zinazojulikana kwa jina la ‘Imara Pamoja Cycle Challenge’. Kulia ni Mshauri Mkuu wa Kitengo cha Jamii endelevu – ACACIA, Siama Paul na kushoto ni Rais wa Chama cha Baiskeli Tanzania, Godfrey Mhagama.
Meneja Uboreshaji tija kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini nchini Tanzania – ACACIA, Janeth Ruben (katikati), kulia kwake ni Mshauri Mkuu wa Kitengo cha Jamii endelevu – ACACIA, Siama Paul na kushoto ni Rais wa Chama cha Baiskeli Tanzania, Godfrey Mhagama wakiwa na baadhi ya wanufaika wa mpango wa uwezeshaji wanafunzi wasio na uwezo wa kumudu gharama za elimu ‘CanEducate’. Kampuni hiyo inatarajia kuzindua mbio za baiskeli zinazojulikana kwa jina la ACACIA Imara pamoja kwa lengo la kukusanya fedha za kuboresha sekta ya elimu nchini.
Meneja Uboreshaji tija kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini nchini Tanzania – ACACIA, Janeth Ruben (katikati), kulia kwake ni Mshauri Mkuu wa Kitengo cha Jamii endelevu – ACACIA, Siama Paul, wakimsikiliza mmoja wa wanufaika wa mpango wa kuwawezesha wanafunzi wasio na uwezo wa kumuda gharama za elimu – CanEducate, Jeremiah Nambali ambaye ambehitimu Shahada ya uhandisi wa madini katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kuwezeshwa na mpango huo unaoratibiwa na Kampuni ya ACACIA kwa kushirikiana na taasisi ya CanEducate. 

WANANCHI NAMBINDA WAMUOMBA MGOMBEA UBUNGE CCM KUTATUA KERO YA MKUNGA

$
0
0
Wakazi wa kijiji cha Nambinda Halmashauri ya wilaya ya Liwale Mkoani Lindi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mkunga katika zahanati ya eneo hilo hali ambayo inapelekea kina mama kutafuta wakunga wa jadi ili kupata huduma hiyo.

Wakizungumza na michuzi Blog wakati wa Kampeni za uchaguzi mdogo wa marudio ya nafasi ya ubunge katika jimbo la liwale wakazi wa kijiji hicho wamemuomba mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Zuberi Kuchauka kushirikiana na serikali kupata ufumbuzi wa changamoto hizo baada ya kupata ridhaa ya kuwatumikia wakazi hao.

Wakimnadi mgombea huyo katika kampeni za uchaguzi huo baadhi ya wabunge wa chama cha mapinduzi CCM kutoka Tanzania bara na visiwani wamesema watahakikisha serikali inashirikiana na Kuchauka kutatua changamoto hizo baada ya wakazi hao kumpa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo.

Kwa upande wake mgombea huyo ZUBERI KUCHAUKA amesema akipata ridhaa ya kuwatumikia wananchi hao atahakikisha anaondoa changamoto hizo huku mjumbe wa halmashauri kuu mkoa wa lindi Abbasi Matulilo amewahakikishia usalama wananchi watao itokeza kupiga kura siku ya uchaguzi huo.

Uchaguzi huo mdogo wa nafasi ya ubunge katika jimbo la liwale mkoani lindi unatarajia kufanyika 0ctoba 13,mwaka huu baada ya mbunge wa jimbo hilo kuhama chama cha wananchi CUF na kuhami Chama cha Mapinduzi.
Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Liwale Faith Mitambo,akiwa jukwaani kumnadi mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Zuberi Kuchauka katika kampeni za marudio ya uchaguzi mdogo wa nafasi ya ubunge jimbo la liwale mkoani lindi iliyofanyika katika kata ya Nambinda jimboni humo.
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Lindi wakiwa na mgombea ubunge kupitia chama hicho zuberi kuchauka wakiwa katika kata ya Nambinda jimbo la Liwale katika kampeni za kumnadi mgombea huyo.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Singida kupitia Chama cha mapinduzi CCM Martha Moses akiwa katika kampeni za kumnadi mgombea ubunge jimbo la Liwale mkoani lindi kupitia chama hicho Zuberi Kuchauka katika kampeni za marudio ya uchaguzi mdogo katika kata ya Nambinda jimboni humo.

Mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM jimbo la Liwale Zuberi Kuchauka akipeana mikono na Mbunge mstaafu wa jimbo hilo Faith Mitambo katika kampeni za marudio ya uchaguzi wa nafasi hiyo katika kata ya Nambinda jimboni humo

Baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wakitumbuhiza na band ya TOT katika kampeni za kumnadi mgombea ubunge jimbo la Liwale mkoani Lindi kupitia chama hicho zuberi kuchauka katika kata ya Nambinda jimboni humo

WAHAMIAJI HARAMU 298 WAKAMATWA MKOANI TANGA

$
0
0
WAHAMIAJI haramu 298 wamekamatwa mkoani Tanga kutoka nchi mbalimbali ambao waliingia nchini kinyume cha kisheria na hivyo kujikuta mikononi mwa vyombo vya dola.

Hayo yalisemwa na Afisa Uhamiaji Mkoani Tanga Ali Dady wakati akizungumza na mtandao huo ofisini kwake kuhusu wahamiaji haramu waliokamatwa kwa kipindi cha kuanza Januari hadi Agosti mwaka huu.

Alisema mwezi January walikamatwa wahamiaji haramu 49 ambao walikuwa wametoka kwenye nchi mbalimbali ikiwemo Somalia,Kenya,Tanzania na China huku kwa mwezi February wakimatawa 77 kutoka nchi za Somalia,Ethiopia, Burundi,Uganda,Kenya na Paskistani.

Afisa Uhamiaji huyo alisema katika mwezi Machi na Aprili idadi yao uingiaji wa wahamiaji hao ulishuka ambapo Machi walikamatwa 18 na Aprili walikamatwa 26 huku mwezi Mei wimbi la ukamataji wao liliongezeka.

“Kwa mwezi Mei walikamatwa wahamiaji haramu 94 kutoka kwenye nchi za Ethiopia, Congo, China na Somalia huku mwezi June na Julai wakikamatwa wahamiaji 12 “Alisema.

Hata hivyo alieleza kwamba katika mwezi Agosti mwaka huu walimatwa wahamiaji haramu 22 kutoka nchi za Ethiopia,Kenya,Somalia na Tanzania ambao wamekuwa mawakala wa wahamiaji hao.

Alisema idadi ya wahamiaji kuingia mkoani Tanga imekuwa ikipungua kila wakati kutokana na kuwepo kwa ufuatiliaji sambamba na kuwekwa vizuizi kwenye maeneo mbalimbali.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images