Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

RC TABORA AAGIZA KUPEWA ORODHA YA WATOTO AMBAO BADO NI WATORO

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT, RS TABORA.

VIONGOZI wa kuanzia ngazi za Kata hadi vijiji na Shule zote wametakiwa kuandaa orodha ya watoto ambao bado ni watoro na kuziwasilisha ngazi za juu ili wao na wazazi wao waweze kuchukuliwa hatua kwa kudai amri halali ya Serikali ya kuwataka kuwa madarasani toka mwezi Julai mwaka huu. Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa kikao kazi cha siku moja cha Maofisa Elimu Kata, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi, Wakuu wa Shule za Sekondari kutoka Wilaya ya Sikonge, Uyui na Tabora Manispaa.

Alisema kwa takwimu za hivi karibuni ni watoto 6,206 kati ya 11,004 ambao walikuwa watoro ndio wamerudi darasani kwa ajili ya kuendelea na masomo kama alivyokuwa ameagiza. Mwanri alisema watoto waliorudi ni zaidi ya asilimia 50 na waliobaki wanaofikia 4,998 na kutaka waanze mara moja kutafutwa walipo kwa ajili ya kurudishwa madarasani.

Alisema hakuna sababu ya kufanya mzazi ashindwe kumpeleka shule mtoto wake kwani Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeondoa vikwazo vyote vilivyokuwa vikisababisha ugumu kwa mzazi.

Mwanri alisema Mwalimu , Afisa Elimu Kata na Mtendaji wa Kata akishindwa kuchukua hatua atalizika kuchukuliwa hatua yeye kama kikwazo cha kukwamisha jitihada za Mkoa za kuondoa utoro, ziro na utumishaji watoto katika mashamba ya tumbaku na migodini.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka walimu Mkoani humo kufanyakazi kama chaja ili wasaidie katika unoaji na uibuaji wa vipaji vya wanafunzi kuanzia msingi hadi Sekondari kwa ajili ya maendeleo ya Tabora.

Alisema hatua hiyo itasaidia kurudisha historia ya Mkoa wa Tabora wa kuwa chimbuko la wasomi na viongozi watakaoshika nyadhifa mbalimbali hapa nchini.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alisema kuwa wao ndio wasimamizi wakuu wa elimu katika maeneo yao ni vema wakazingatia kampeni ya Mkoa wa Tabora inayosema Tabora bila sifuri,utoro, utumikishaji watoto mashambani, na mimba za utotoni inawezekana kila mmoja atimize wajibu wake.

Aidha aliwataka kuhakikisha wanaboresha mazingira ya shule kwa kupanda miti na maua ili kuwavutia watoto wapende kujifunza.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua kikao kazi cha siku moja cha Maofisa Elimu Kata, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi, Wakuu wa Shule za Sekondari kutoka Wilaya ya Sikonge, Uyui na Tabora Manispaa leo mjia hapa. Wengini ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu(wa pili kutoka kushoto) , Kaimu Katibu Tawala Msaidizi(Utawala na Utumishi) Aidan Lucas(kulia) na Afisa wa Serikali za Mitaa Shukuru Kazembe(kushoto).
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maelezo mafupi wakati kikao kazi cha siku moja cha Maofisa Elimu Kata, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi, Wakuu wa Shule za Sekondari kutoka Wilaya ya Sikonge, Uyui na Tabora Manispaa leo mjini hapa.
Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Susan Nussu akitoa maelezo mafupi wakati kikao kazi cha siku moja cha Maofisa Elimu Kata, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi, Wakuu wa Shule za Sekondari kutoka Wilaya ya Sikonge, Uyui na Tabora Manispaa leo mjini hapa.

WAZIRI MHAGAMA AKUTANA NA WATENDAJI WA OFISI YAKE KUJADILI UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM YA MWAKA 2015-2020

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo kwa Wakuu wa Taasisi, Idara na Vitengo vilivyopo chini ya Ofisi hiyo (hawapo pichani) alipokutana nao kujadili utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 na Maagizo ya Mhe. Rais Dkt.John Magufuli aliyoyatoa katika kikao cha kufungua Bunge la kumi na moja la tarehe 20 Novemba 2015 kilichofanyika Ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma Oktoba 1, 2018 Kulia kwake ni Naibu wake anayeshughulikia wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa na kushoto kwake Mhe.Anthony Mavunde anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Wakuu wa Taasisi, Idara na Vitengo vilivyopo chini ya Ofisi hiyo wakati wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Maagizo ya Mhe. Rais aliyoyatoa katika kikao cha kufungua Bunge, Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akielezea jambo kwa Wakuu wa Taasisi, Idara na Vitengo vya Ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa Kikao kazi hicho.
 Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Peter Kalonga, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, akiwasilisha hoja kwa Wakuu wa Taasisi, Idara na Vitengo vya Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa kujadili utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 na Maagizo ya Mhe. Rais Dkt.John Magufuli aliyoyatoa katika kikao cha kufungua Bunge la Kumi na Moja Novemba 2015.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KIGOMA WANOLEWA UELEWA KUHUSU UALBINO-

$
0
0


Mashirika ya Under The Same Sun, CEFA Tanzania na GNRC Tanzania, yaendelea kuelimisha jamii kuhusiana na ualbino
.Mradi wa HAKI YETU wakutana na Maafisa Maendeleo na ustawi wa jamii .Kigoma na kuzungumza madhara ya kuwatenga watu wenye ualbino
Maafisa Maendeleo ya Jamii, na ustawi wa jamii Kigoma wapigwa msasa uelewa kuhusu Ualbino

Maafisa Maendeleo ya Jamii, na ustawi wa jamii, kutoka manispaa ya kigoma Ujiji leo wamehudhuria mafunzo ya uelewa kuhusu ualbino na elimu ya Amani na maadili iliyotolewa na mradi wa Haki Yetu mkoani Kigoma.

Mradi huo umekua ukiendeshwa tangu Aprili,2018 katika Mikoa ya kigoma na maeneo ya jirani kwa ushirika wa wadau Mbalimbali lengo lao likiwa ni kutoa msaada kwa jamii kuelewa zaidi kuhusu ualbino, kupunguza imani potofu, kuwajengea watu wenye ualbino misingi ya kujiamini ualbino pamoja na kutengeneza jamii shirikishi isiyokuwa na ma waa ya ubaguzi wa aina yoyote kwa watu wenye ualbini 

Katika mradi huu misingi muhimu ambayo imekua ikiwekewa msisitizo ni pamoja na kuzingatia utu, kuwapa nafasi watu wenye ualbino bila kuwabagua, kushirikiana nao kwenye maswala ya elimu na uchumi lengo likiwa ni kujenga Taifa bora 

Mradi wa Haki Yetu unatekelezwa na Mashirika ya Under The Same Sun, CEFA Tanzania na GNRC Tanzania, ukilenga kuelimisha jamii kuhusiana na ualbino.

 Pichani juu na chini ni Maafisa Maendeleo ya Jamii, na ustawi wa jamii, kutoka manispaa ya kigoma Ujiji leo wamehudhuria mafunzo ya uelewa kuhusu ualbino na elimu ya Amani na maadili iliyotolewa na mradi wa Haki Yetu mkoani Kigoma.

Wakiwa katika picha ya pamoja.

JENERALI MSTAAFU MWAMUNYAGE ATEMBELEA MIRADI MBALIMBALI YA MAJI YA DAWASA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange ametembelea miradi mbalimbali na ujenzi wa matanki ya kuhifadhia maji  inayosimamiwa na Mamlaka hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo ya kwanza toka kuteuliwa kwake Mwamunyage ametembelea mradi wa maji wa Bunju, Mabwepande, Salasala, Wazo na Kibamba hadi Kisarawe.

Jenerali Mstaafu ameambatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja na baadhi ya viongozi wa bodi hiyo katika kukagua miradi na  hatua iliyofikia.

Akitembelea miradi hiyo ya Maji itakayosaidia upatikanaji wa maji wa takribani Lita milioni sita kwenye Kila tanki  kwa siku, Jenerali Mstaafu Mwamunyange amefurahishwa na hatua kubwa iliyofikiwa na Dawasa katika kuhakikisha mkoa wa Dar es Salaam na baadhi ya Maeneo ya Mkoa wa Pwani yanapata maji salama na ya uhakika.

Katika mradi wa Salasala unaosimamiwa na Kampuni ya Jain Irrigation Systme ambao upo katika hatua ya mwisho unatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi Oktoba utakaowezesha kupatikana kwa wateja wapya 40,000.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) Mhandisi Cyprian Luhemeja  (wa pili Kulia) akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Dawasa Jenerali Mstaafu Davis Mwamjnyange (wa kwanza kushoto) wakiwa wanakagua moja ya Tanki la kuhifadhia maji wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya Mamlaka hiyo Leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majinsafi na Maji Taka (Dawasa) Mhandisi Cyprian  Luhemeja  akimuelezea moja ya mradi wa maji kwa  Mwenyekiti wa Bodi ya Dawasa Jenerali Mstaafu Davis Mwamjnyange katika ziara yake iliyofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa wakandarasi wa mradi huo kutoka kampuni ya Jain Irrigation System  wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya Mamlaka hiyo Leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mpango Apokea Ripoti Tathmini ya Utendaji wa PPRA

$
0
0


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akizindua ripoti ya tathmini ya utendaji ya Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa mwaka wa fedha 2017/18 leo jijini Dodoma.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA Balozi Matern Lumbanga. 

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akizungumza wakati alipokuwa akipokea ripoti ya tathmini ya utendaji ya Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa mwaka wa fedha 2017/18 leo jijini Dodoma. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Balozi Matern Lumbanga akiwasilisha ripoti ya tathmini ya utendaji wa PPRA kwa mwaka wa fedha 2017/18, leo jijini Dodoma.Kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi. Ayoub Kisuwi. 
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa ununuzi wa Umma (PPRA) wakifuatilia ripoti ya tathmini ya utendaji wa PPRA kwa mwaka wa fedha 2017/18, leo jijini Dodoma. 
Baadhi ya watendaji kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kikao baina ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango (hayupo pichani) na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) leo jijini Dodoma. 

PREMIER BET YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI 15

$
0
0
Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Premier Bet leo imekabidhi zawadi kwa washindi 15 waliocheza bahati nasibu ya jackpot yenye thamani ya shilingi milioni 79 ambapo washindi hao 15 kila mmoja alifanikiwa kuondoka na kitita cha zaidi ya milioni 5 za kitanzania .

Premier Bet imeendeleza kuhamasisha wateja wake kuendelea kucheza na kuweza kuibuka mshindi wa Jackpot itakayochezwa kila siku ya Jumanne na Jumamosi.

Premier Bet imeendelea kubadilisha maisha ya watanzania wengi kupitia jackpot inayochezeshwa kila jumanne na jumamosi. Washindi hao 15 wametoka katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mtwara, Tabora na Dar Es Salaam.
Meneja Rasilimali watu na Utawala kutoka Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya Premier Bet Amanda Kombe(katikati) akizungumza na waadishi wa habari leo kuhusu droo iliyochezeshwa na kampuni hiyo na kupatikana washindi 15 kwenye droo ya Jackpot ya Premier Bet. Kushoto ni
Mhamasishaji wa Mchezo wa Kubashiri wa Premier Bet Salama Jabir.
Picha na Mohamed Ibrahim, Michuzi Blog.
Mhamasishaji wa Mchezo wa Kubashiri wa Premier Bet Salama Jabir akionesha namna ya kubet wakati walipotangazwa washindi 15 wa Droo ya Jackpot ya Premier Bet. Kulia ni Meneja Rasilimali watu na Utawala kutoka Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya Premier Bet Amanda Kombe.
Washindi wakiwa kwenye picha ya pamoja.

BODI YA BARAZA LA KILIMO TANZANIA LAHITIMISHA ZIARA YAKE YA KUKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA UBIA WA KILIMO TANZANIA.

$
0
0


Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafasi (TPSF) Bw. Salum Shamte ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) akimuonyesha Mwenyekiti wa Baraza la kilimo Tanzania (ACT) Dkt Sinare Yusuph (katikati) Barua kutoka Benki ya Kilimo inayokataa kuwapatia Mkopo wakulima wa Kijiji cha Minepa Wilayani Ifakara kwa kile walichodai mpaka wakulima hao wawe na hati miliki ya Mashamba hayo kitu kinachotajwa kuwa si sahihi, ambapo wajumbe wa bodi wameazimia kulifanyika kazi suala hilo.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Lonagro inayojihusisha na uuzaji wa zana za Kilimo hifadhi Bw Ray Travas akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kilimo Tanzania waliofika ofisini kwake Mjini Arusha ambapo alisema bado kuna mwitikio mdogo kwa wakulima kutumia zana za kisasa katika kilimo kutokana na uzalishaji wao kuwa mdogo huku pia wakikwamishwa na bei za mazao ambazo zimekuwa chini zaidi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafasi (TPSF) Bw. Salum Shamte ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Kilimo Tanzania (ACT),akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko na wakulima mbalimbali katika moja ya ziara ya wajumbe wa bodi ya ACT kukagua miradi inayosimamiwa na Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP).
Mkurugenzi wa kampuni ya Siza Agro Processing iliyoko Mjini Mufindi inayojishughulisha na kukoboa na kupaki kwa viwango tofauti bidhaa za mchele na unga akiwaonyesha wajumbe wa Bodi bidhaa ya Mchele inayozalishwa na Kiwanda chake, ingawa kwa sasa anasema shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho chenye mashine za kisasa unasuasua.

Dkt. Mwakyembe: BMT waiteni TASWA kujadili Katiba kabla ya Uchaguzi Mkuu

$
0
0
Na Lorietha Laurence –WHUSM,Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  amewataka watendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuitisha kikao na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA)  pamoja na baadhi ya waandishi wa habari hizo kujadili na kupitia katiba ya chama hicho.
Dkt. Mwakyembe ametoa rai hiyo jana Jijini Dar es Salaam alipokutana na baadhi ya Waandishi wa Habari za michezo , alichokiitisha baada ya kupokea barua ya malalamiko  zinazoelezea changamoto mbalimbali zinazowakabili waandishi hao wa michezo.
“ Watendaji wa Baraza la Michezo la Taifa  waiteni viongozi wa TASWA wakiwemo na wawakilishi ambao ni waandishi wa habari za michezo  ili kupitia katiba inayokiongoza chama hicho kabla ya uchaguzi Mkuu” alisema Dkt. Mwakyembe.
Aliongeza kwa kueleza kuwa waandishi wa habari za michezo wana uhuru wa kuunda chama kipya endapo hawaridhishwi na utendaji wa TASWA ingawa kabla ya kufanya maamuzi yoyote, kikao kifanyike kwanza ili kufikia muafaka.
Alizidi kufafanua kuwa  waandishi wa habari za michezo ni muhimili muhimu katika sekta ya habari na maendeleao ya michezo  ndani na nje ya nchi, kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhabarisha jamii  kuhusiana na masuala ya michezo.
Wakati huo huo, Dkt. Mwakyembe alipata nafasi ya kutembelea wasanii wa kikundi cha Nafasi Arts Space kilichopo Mikocheni B Jijini Dar es Salaam, ambapo alifurahishwa na kazi mbalimbali za sanaa zinazofanywa na kikundi hicho.
 Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe (Kushoto) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari za michezo kilichofanyika jana Uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam, kulia ni Afisa Habari wa TFF Cliford Ndimbo.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari za michezo wakimsikiliza Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe (Hayupo katika picha) katika kikao kilichofanyika jana Uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akipata maelekezo kutoka kwa Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Bw. Ramadhani Mabera (kushoto) na kulia ni Mwalimu wa Sanaa za Uchoraji kutoka Zanzibar Bw. Abdulla Omar maarufu kama Dulla Wise.
 Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe (Kushoto) akipokea zawadi ya picha ya kuchora kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Nafasi Arts Space Bibi. Sauda Simba   baaada ya kuzungumza na wasanii hao jana Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUZI TV: KAULI NZITO YA MZEE MWINYI KWA CHAMA CHA SKAUTI

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI, SKAUTI MKUU WA TANZANIA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea saluti toka kwa Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza muda mfupi baada ya kumuapisha kuwa Skauti Mkuu wa Chama Cha Skauti Tanzania. Aliyeketi ni Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe aliyemuapisha kuwa Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Hafla hii imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya kuongea machache kwenye hafla ya kuwaapisha Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na Skauti Mkuu wa Tanzania Ndg. Mwantumu bakari Mahiza Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiongea machache kwenye hafla ya kuwaapisha Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na Skauti Mkuu wa Tanzania Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2018.
\
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Skauti Mkuu wa Tanzania Ndg. Mwantumu bakari Mahiza Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe kuwa Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi Rais wa Chama cha Skauti na Waziri wa Elimu, sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Technolojia Dr. leonard Akwilapo,  Skauti Mkuu Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza, Mama Anna Abdallah, Mwenyekiti wa Chama cha Skauti nchini Mhe. Abdulkadir Shah na makamishna wa Skauti na Girl Guide  kwenye hafla ya kuwaapisha Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na Skauti Mkuu wa Tanzania Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro, Katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi na Skauti Mkuu Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama  baada ya kuwaapisha Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na Skauti Mkuu wa Tanzania Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 20 Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2018. Picha na IKULU

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS MAGUFULI ATOA UJUMBE KWA SKAUTI MKUU WA TANZANIA, MWANTUMU MAHIZA

RC MAKONDA AKUTANA NA WATENDAJI TPSF, WAWEKA MIKAKATI MADHUBUTI YA KUWASAIDIA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea ofisi za Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania TPSF na kufanya mazungumzo ya kutafuta namna bora ya kuweka mazingira bora ya kibiashara ilikuondoa kero zinazowakabili wawekezaji na wafanyabiashara jijini humo. 

Miongoni mwa mambo waliyoridhia kushirikiana ni pamoja na utoaji wa elimu ya biashara, usimamizi wa fedha pamoja na namna bora ya kutumia fursa ya 10% za mkopo zinazotolewa na serikali kwaajili ya vijana, Wanawake na walemavu ili fedha hizo ziwe na tija.

Aidha RC Makonda amezungumza ushiriki wa TPSF katika ziara ya Rais Dkt. John Magufuli jijini Dar es salaam ambayo tunaamini itakuwa fursa kubwa kwa sekta zote ikiwemo Biashara, uchumi, afya, elimu, miundombinu na maji ambapo amewahimiza kuitumia vizuri ziara hiyo ili kufikia ndoto ya Dar es salaam kuwa jiji la kibiashara.

Pamoja na hayo RC Makonda ameelezea mpango wa kuweka kitengo cha uwekezaji (one stop center) itakayohusisha watendaji kutoka taasisi za TIC, TRA, TBS, BRELA, Uhamiaji na wadau wote wanaohusika na biashara ilikuondokana na ukiritimba uliokuwa ukipelekea mianya ya rushwa kwa wawekezaji na mwisho wa siku wawekezaji kukata tamaa ya kuwekeza Dar es salaam.

Kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania TPSF Bwana Godfrey Simbeye amemuahidi ushirikiano wa kutosha kwa RC Makonda katika masuala mbalimbali yanayolenga kuliboresha jiji la Dar es salaam. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea ofisi za Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania TPSF na kufanya mazungumzo ya kutafuta namna bora ya kuweka mazingira bora ya kibiashara ili kuondoa kero Mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania TPSF Bwana Godfrey Simbeye
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akisalimiana na Mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania TPSF Bwana Godfrey Simbeye alipowasili leo na kutembelea ofisi za Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania TPSF na kufanya mazungumzo ya kutafuta namna bora ya kuweka mazingira bora ya kibiashara ili kuondoa kero

SERIKALI YAWAPA WAKULIMA MIKOPO YA SH. BIL. 56.45-MAJALIWA

$
0
0

*Asema zaidi ya wakulima wadogo 527,000 katika Mikoa 13 wamenufaika 

WAZIRIMKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa mikopo yenye thamani ya sh. bilioni 56.45 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kilimo katika mikoa 13 hapa nchini.

Amesema mikopo hiyo imetolewa katika kipindi cha kuanzia Agosti 2015 hadi  Septemba 2018, kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Oktoba 3, 2018) kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) mjini Mororogo.

Mikopo hiyo imewanufaisha wakulima wadogo zaidi ya 527,000 waliopo kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya kahawa, karafuu, mahindi, mbogamboga na mazao mengine.Amesema Serikali inatekeleza mipango mbalimbali kwa lengo la kutatua kero zinazowakabili na kuwawezesha wakulima wadogo kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo. 

Amesema Juni 14, mwaka huu Rais Dkt. John Magufuli, alizindua Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo hapa nchini (ASDP II) yenye lengo la kuboresha sekta ya kilimo.Waziri Mkuu amesema ASDP II inalenga kuhakikisha sekta ya kilimo inapewa kipaumbele stahiki ili iweze kuleta tija kwa wakulima wenyewe na Taifa kwa ujumla.

“Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha sekta ya kilimo ikiwemo kutoa mikopo kwa wakulima wadogo; kuondoa baadhi ya tozo zenye kufifisha uzalishaji.” Pia kuweka mipango mizuri ya matumizi bora ya ardhi na kutafuta masoko pamoja na kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo ili kumuongezea tija mkulima.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Oktoba 3, 2018.
Baadhi ya washiriki wa Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima (MVIWATA) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Oktoba 3, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Uswiss nchini, Florence Tinguely Mattli katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima (MVIWATA) kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro, Octoba 3, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa uyoga, Maria Shindika wa Mvomero (kulia) kabla ya kuhutubia katika Maadhidhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima (MVIWATA) yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Oktoba 3, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu unga na bidhaa mbalimbali zinaotokana na zao la soya kutoka kwa Julie Bwire wa Mvomero (kushoto) kabla ya kuhutubia katika Maadhimisho ya miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Oktoba 3, 2018. 



DKT. ABBASI AHIMIZA VIONGOZI WA MKOA WA SIMIYU KUTANGAZA NA KUTETEA MAGEUZI YANAYOFANYWA NA SERIKALI

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, akitoa mada ya umuhimu wa mawasiliano ya kimkakati mbele ya viongozi mbalimbali wa mkoa wa Simiyu. Kwenye wasilisho lake amesisitiza kutangaza na kutetea mageuzi yanayofanywa na Serikali ya amamu ya tano.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mheshimiwa Anthony Mtaka pamoja na viongozi wengine wa mkoa huo waliohudhuria kikao cha uwasilishaji wa mada iliyohusu umuhimu wa mawasiliano ya kimkakati katika kutangaza ahadi za serikali.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji wa Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mheshimiwa Anthony Mtaka (katikati) na Katibu Tawala wa mkoa huo Jumanne Sagini.

WANACHAMA NA WAFANYAKAZI NCHINI WATAKIWA KUPITIA UPYA  SHERIA YA MIFUKO YA PENSHENI

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii.
Chama cha waajiri nchini ATE wamefanya Mkutano wa pamoja kwa kukutana na wanachama na wafanyakazi  kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa kuungana kwa mifuko ya jamii nchini na kuunda PSSSF.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha waajiri ATE  Dr Aggrey Mlimuka amesema sheria mpya ya waajiri iliyotolewa Agosti Mosi mwaka huu imebainisha taratibu zote za kujiunga na mifuko hiyo.

Amesema kuwa, kwa upande wa waajiri wanatakiwa kuhakikisha waajiriwa wao wanajiunga na mifuko hiyo ya kijamii NSSF,GEPF na Mfuko wa Taifa wa bima ya  afya NHIF ili kupata haki na wajibu .

Kaimu Katibu  wa Mamlaka ya udhibiti wa mifuko ya jamii SSRA Joseph Mutashubilwa  ameeleza  lengo la kutoa elimu hiyo ni kuhakikisha kila mfanyakazi anajiunga na mifuko hiyo ya NHIF,PSPF,GEPF na kupitia upya sheria iliyoanza kutumika rasmi mwaka huu mwezi Agosti ambayo Ina mamlaka ya kusimamia mifuko ya jamii.

Aidha , Mutashubilwa amesema fursa waliyopata waajiriwa katika elimu hiyo wataweza kusambaza kwa waajiri wao ili kuhakikisha wanapata haki zao bila changamoto yoyote japo kumekuwepo kwa tatizo la waajiri hao kupangiwa sehemu za kupata huduma za kiafya na kulazimika kwenda mbali na maeneo ambayo wanayoishi.

Ametoa fursa kwa wanachama hao kuwasilisha malalamiko yao katika ofisi zao zilizopo Dar es salaam, Dodoma au kutuma barua pepe.

Katika hafla hiyo  Mwanachama  wa ATE  ambae ni Meneja rasilimali watu kutoka kampuni ya PSSI  Hollyness Mongi ametoa ufafanuzi kwa mifuko hiyo kuungana na kuwa chini ya SSRA.

 Mongi ameshukuru Mkutano  wanachama walikua Kwenye sintofahamu kutokana na Mabadiliko ya utaratibu wa mifuko hiyo kuungana na kupelekea wafanyakazi wapya kutojua taarifa sahihi ya kujiunga na mifuko hiyo upya.
 Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha Waajiri nchini ATE Dr. Aggrey Mlimuka akizungumzana na wadau pamoja na waajiri katika hafla fupi ya kutambulisha sheria mpya ya Mifuko ya pensheni jijini Dar es Salaam
Kaimu Katibu wa Mamlaka ya udhibiti wa Mifuko ya pensheni nchini (SSRA) Joseph Mutashubilwa akizungumzana na wadau kuhusu kuungana kwa mifuko ya jamii nchini na kuunda PSSSF.
 Meneja rasilimali watu kutoka kampuni ya PSSI Hollyness Mongi   akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sheria mpya kwa Waajiri pamoja na waajiriwa kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama na wafanyakazi  kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa kuungana kwa mifuko ya jamii nchini na kuunda PSSSF.

UCHAGUZI NAIBU MEYA ILALA WAGEUKA ‘UWANJA WA VITA’

$
0
0
*Madiwani watwangana masumbwi hadharani mbele ya Polisi 
*Ni baada ya Kumbilamoto wa CCM kutangaza mshindi 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

UCHAGUZI wa Naibu Meya wa Manispaa Ilala jijini Dar es Salaam umeingia dosari baada ya kugeuka kuwa uwanja wa masumbwi au uwanja wa vita kutokana na baadhi ya madiwani kuamua kurushiana makonde.

Madiwani wa Manispaa ya Ilala leo walikuwa kwenye uchaguzi wa Naibu Meya baada ya aliyekuwa katika nafasi hiyo Omary Kumbilamoto kujiuzulu na kisha kujiunga CCM.

Kumbilamoto kabla ya kujiunga CCM alikuwa diwani wa CUF Kata ya Vingunguti.Hata hivyo baada ya kujiuzulu na kujiunga CCM Kumbilamoto ameshinda tena udiwani wa kata hiyo na leo amechaguliwa Naibu Meya baada ya kushinda kwa kupata kura 27 huku mpinzani wake kura 25.

Dalili za uchaguzi huo kuingia vurugu zilianza kuonekana mapema tu kutokana na kurushiana maneno kwa pande mbili ambazo zilizokuwa zinashiriki uchaguzi huo.Hata hivyo wakati wa kuhesabu hapo ndipo joto la vurugu liliposhika kasi.

Diwani wa Kata Madizini Senga kupitia Chadema aliyekuwa chumba cha kuhesabu aliamua kutoka chumba cha kuhesabu kura na kisha kupaza sauti akidai  msimamizi wa uchaguzi anaharibu uchaguzi huo.Kauli hiyo ilisababisha Polisi waliokuwa eneo hilo kuingia chumba cha kuhesabia kura kwa ajili ya kulinda usalama.

Hata hivyo wakati wanatoka chumba cha kuhesabia kura ndipo baadhi ya madiwani walianza kurushiana ngumu.Sababu za kurushiana ngumi inatokana na madiwani wa upinzani wakidai mgombea wao ameshinda kiti cha Naibu Meya lakini wanashangaa anatangaza diwani wa CCM ambaye ni Kumbilamoto.Hata hivyo Polisi walifanikiwa kutuliza vurugu hizo na hasa kudhibiti masumbwi yaliyokuwa yanarushwa kutoka kwa diwani wa upinzani kurusha makonde kwa diwani wa CCM.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi huo na baada ya kuhesabiwa kura hizo alimtangaza Kumbilamoto kushinda nafasi ya Naibu Meya wa Manispaa hiyo.Hata hivyo madiwani wa upinzani wameonesha kutofurahishwa na matokeo ya uchaguzi huo wakidai kuna hujuma kwani wanaamini wameshinda uchaguzi huo.

Kwa kukumbusha uchaguzi wa Naibu Meya uliopita nao uligubikwa na vurugu baada ya baadhi ya madiwani walitwangana makonde ukumbini.Hata hivyo Kumbilamoto alishinda uchaguzi huo.
Baadhi ya polisi wakiwa ndani ya ukumi kutuliza vurugu zilizokuwa zimezuka wakati wa uchaguzi
Baada ya vurugu kuibuka askari waliingilia kati kuhakikisha amani inatawala kwenye uchaguzi huo.

JALADA KESI TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MSTAAFU WA TAZAMA LIPO KWA DPP

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia (Tazama), Samwel Nyakirang'ani na wenzake 11, umeileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Jalada la keai hiyo lipo kwa (DPP), kwa ajili ya kulichambua na kulitolea maamuzi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita, ameeeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.Mwita alidai jalada lipo kwa DPP kwa ajili ya kulichambuliwa na kulitolea maamuzi kwa kuangalia washtakiwa gani washtakiwe na washtakiwa gani waachiwe huru na pia itatoa maamuzi kama Mahakama ya Kisutu itapata mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo au itahamishiwa Mahakama ya mafisadi.

Ameongeza wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha uchambuzi, hivyo wanaomba mahakama yako ipange tarehe nyingine, kwa ajili ya kutajwa.Baada ya kusikiliza hoja hizo, wakili wa utetezi, Alex Balomi ameutaka upande wa mashtaka kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa kesi hiyo ili DPP aweze kutoa maamuzi haraka kwa sababu wateja wake wanaendelea kusota mahabusu.

Hakimu Simba ameutaka upande wa mashtaka kuharakisha zoezi la uchambuzi ili haki iweze kupatikana." Upande wa mashtaka mfuatilie kwa DPP kujua anamaliza lini kulipitia faili hili maamuzi yaweze kufanyika na haki iweze kupatikana" alisema Hakimu Simba.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 17, 2018. Mshtakiwa Nyakirang’anyi na wenzake katika kesi hiyo wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta mali ya (TPA), Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Nyangi Mataro, mwalimu wa shule ya msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni. Mfanyabaishara, Farijia Ahmed, mkazi wa Soko Maziwa Kigamboni, Malaki Mathias, mkazi wa Magogoni, Kristomsi Angelus, mkazi wa Soko Maziwa, Fundi Ujenzi Pamfili Nkoronko, mkazi wa Tungi Kasirati na Henry Fredrick, mkazi wa Tungi Kigamboni.

Wengine ni Audai Ismail ambaye ni mkazi wa Kibaha, Chibony Emmanuel, Roman Abdon, Amina Shaban na Zubery Ally.Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta, kinyume cha sheria ya Uhujumu uchumi.

Waziri Mpango Aipongeza Bodi ya Wakurugenzi PPRA kwa Utendaji Kazi

RALLY ROUND AFRICA 2018

CCTV CAMERA KUFUNGWA ENEO LA MAFIATI JIJINI MBEYA KUDHIBITI WAVUNJA SHERIA

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images