Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 2,2018


OLE NASHA AITAKA VETA KUANZISHA KOZI YA UFUNDI WA ZANA ZA KILIMO SONGEA

0
0

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ametoa wiki moja kwa mtaalamu Elekezi wa Kampuni ya Archquants Service Limited  kuhakikisha inawasilisha michoro ya kazi za nje ya Chuo cha ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Namtumbo kilichopo Mkoani Ruvuma ili ujenzi wa chuo hicho uweze kukamilika. 

Mheshimiwa Ole Nasha ametoa agizo hilo wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho ambapo amesema ucheleweshwaji wa michoro hiyo unapelekea kuchelewesha ukamilishaji wa mradi huo. 

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ole Nasha ameitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA kuhakikisha wanaanzisha kozi ya ufundi wa zana za kilimo (Agro mechanics) katika Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo Songea ili kupata vijana wengi watakaosomea fani hiyo. 

Naibu Waziri amesema ukanda wa Nyanda za Juu Kusini unategemea sana kilimo, hivyo kuanzishwa kwa kozi hiyo kutasaidia wananchi wengi kupata uelewa wa kina kile wanachokisoma na baadae kutekeleza kwa vitendo. 

“Serikali inatilia mkazo Elimu ya ufundi na imejielekeza katika kuhakikisha inapanua fursa ya vijana wengi kupata Elimu ya ufundi na ndio maana Serikali ya awamu ya Tano imeamua kuweka Vyuo vya VETA katika kila Wilaya na Mkoa,” alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha 

Naibu Waziri Ole Nasha yuko mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa ajili ya kukagua miradi ya Elimu inayotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayasni na Teknolojia.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo (katikati) na baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,wakielekea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo (katikati) na baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,akikagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akisalimiana na baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,alipowasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.pichani kusho ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo.
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipewa maelezo kuhusina na maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo (wa tatu kulia) na baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,akikagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

DIRA YA KITAA NA KINYOZI MBABE MTAA MZIMAA...

ORODHA YA PILI WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MASOMO YA SHAHADA YA KWANZA KWA MWAKA WA MASOMO 2018/1

BODABODA ZINAZOINGIA KATIKATI YA JIJI LA DAR SASA KUKIONA-KAMANDA MAMBOSASA

0
0
*Ndani ya saa 24 zakamatwa 104, wahusika kufikishwa mahakamani


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limeanza operesheni maalumu ya kukamata bodaboda zote zinazoingia katikati ya Jiji ambapo ndani ya saa 24 wamekamata pikipiki 104. Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa wakati anazungumza na waandishi wa habari kuhusu operesheni ambazo wanazifanya.

Amefafanua Polisi wameanza operesheni ya kukamata waendesha bodaboda ambao wanaingia katikati ya mji wakati wamezuiliwa kuingia huko.
Kamanda Mambosasa amesema baadhi ya bodaboda ambazo zimekamatwa zimetokana na makosa ya kutovaa kofia ngumu kwa wanaoendesha, kupitia njia tofauti na utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria na kupakia mishikaki.
"Ni marufuku bodaboda kuingia katikati ya Mji,hatuwezi kuacha hilo likaendelea kufanyika.Walishakatazwa kuingia katikati ya mji." Mbali ya kuwakamata wanaiongia mjini pia tunaendelea na operesheni ya kukamata bodaboda ambazo zinatumika kutenda matukio ya uhalifu.Pia tutakamata bodaboda ambazo wanaoziendesha wanashindwa kufuata sheria za usalama barabarani.

MAKOSA YA BARABARANI DAR YAIINGIZA ZAIDI YA BIL 2.74/- KWA JESHI LA POLISI DAR,MAMBOSASA ATOA ONYO

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MAKOSA mbalimbali ambayo yanafanywa na wanaoendesha vyombo vya moto barabarani yamesababisha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupata zaidi ya Sh.Bilioni 2.74.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema hayo leo ambapo amefafanua jeshi hilo linaendelea na operesheni ya kuwasaka madereva wa magari na watumiaji wa vyombo vya moto ambao hawazingatii sheria ya usalama barabarani.

Amefafanua katika operesheni hiyo wamefanikiwa kukamata magari madogo,maroli, pikipiki na daladala ambapo wahusika wametozwa faini ambapo zaidi ya Sh.Bilioni 2.74 zimepatikana.

Pia amesema kuwa ni vema madereva kuhakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani huku akionya tabia ya baadhi ya madereva wanaondesha magari huku wakichati muda wote.

Amesema ni vema wakaacha tabia ya kuendelea kutumia simu kwani madhara yake ni makubwa na ni sawa na kukitafuta kifo.

Pia Kamanda Mambosasa amewawataka watu ambao wametozwa faini za barabani kulipa kwa wakati kwani kuna tabia ya kulimbikiza deni na wataendelea kuwasaka wadaiwa wote na iwapo watashindwa gari litachukuliwa na kuwekwa Polisi.

WAZIRI MWAKYEMBE AAGIZA UCHAGUZI CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO USIMAMISHWE,ATAKA KATIBA IPITIWE UPYA

0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amekutana na kufanya mazungumzo na  waandishi wa habari za michezo ambapo wametumia muda mwingi kujadili mwenendo wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA).

Akizungumza na Waandishi hao, Dkt. Mwakyembe ameliagiza Baraza la Michezo nchini (BMT) kusimamisha Uchaguzi wa TASWA unaotarajiwa kufanyika Novemba ya mwaka huu.

Dkt. Mwakyembe ameiagiza BMT kuita uongozi wa TASWA na Uongozi wa Vijana ambao hawana Uanachama wa Chama hicho kukaa pamoja kujadiliana changamoto zinazokikabili Chama hicho.

"Uchaguzi wa TASWA usimamishwe na mkae pamoja mzungumze kuhusu Katiba ya Chama hicho ili baadae mpate uongozi ulio imara kwa maslahi ya waandishi wa habari za michezo nchini", amesema Dkt. Mwakyembe.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwakyembe amesema Wizara yake iko katika mikakati yakuboresha mazingira, ikiwa kuhakikisha kila .wandishi anakuwa na Bima itakayomlinda katika mslahi yake.

Pia kuunda Baraza la Habari (Media Council), Chombo cha Idhibati, Kamati ya Malalamiko itakayokuwa na Mamlaka ya Mahakama pamoja na Mfuko wa Wanahabari kwa ajili ya Mafunzo kwa Wanahabari.

Kwa kukumbusha TASWA iliundwa mwaka 1977 chini ya Sheria za Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

NAIBU WAZIRI HASUNGA AHAMASISHA UTALII WA NDANI MASHULENI

0
0
NA LUSUNGU HELELA- SONGWE
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga  ameanza ziara ya  kimkakati ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa wanafunzi wa  shule za sekondari nchini lengo likiwa ni  kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao kwa wanafunzi hao. 
Mhe. Hasunga amesema sekta ya utalii inaweza kuongeza pato lake maradufu iwapo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari  wataanza kujua umuhimu juu ya utalii wa ndani bado angali wakiwa wadogo.
Katika ziara hiyo aliyoianza mkoani Songwe wilayani Mbozi, Naibu Waziri Mhe. Hasunga ameweza kutembelea shule za Sekondari tatu ikiwemo Shule ya Kilimampimbi, Vwawa pamoja na  Ilolo ambapo amezungumza na wanafunzi pamoja na walimu   kuhusu umuhimu wa utalii wa ndani.
Amefafanua kuwa Wanafunzi ni mabalozi wakubwa wa mabadiliko, wanapopata elimu juu ya  utalii wa ndani wataweza kuifikisha kwa wazazi, walezi pamoja na jamii kwa ujumla.
Katika ziara hiyo, Mhe. Hasunga  ametoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliokuwa wakijibu maswali kuhusiana na vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Amesema sekta ya utalii inachangia  asilimia 17.5 ya pato la taifa na inaweza ikawa asilimia 30 kama kutajengeka utamaduni kwa jamii  wakiwa bado  wanafunzi   kuhusu umuhimu wa kutenga muda pamoja na pesa kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
‘’Nchi yetu imejaliwa kuwa na vivutio vingi lakini imekuwa haifanyi vizuri ukilinganisha na nchi kama Misri aambao wao hawana vivutio vingi kama tulivyonavyo sisi, Wenzetu wana magofu pekee lakini wametuacha mbali’’ amesema Mhe. Hasunga.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kilimampimbi iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe  akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini  kwa lengo la  kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao. 
 Baadhi ya wanafunzi wa Vwawa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Vwawa iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe  akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa  lengo la  kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (katikati)  akizungumza na walimu wa  shule ya sekondari ya Vwawa  iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe mara baada ya kumaliza   kuzungumza na  wanafunzi wa shuke hiyo  kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa lengo la  kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilolo  iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe  akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa  lengo la  kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akiwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbozi, Bi. Hossana Mshule wakati w akielekea kukagua baadhi ya majengo yaliyojengwa kwa mfuko wa jimbo la Vwawa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAHAKAMA YAGOMA KUFUTA KESI YA TUHUMA ZA UTAKATISHAJI FEDHA INAYOMKABILI AVEVA,NYANGE

0
0
Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema haiwezi kifuta kesi ya utakatishaji wa fedha inayomkabili Rais wa Klabu ya Simba Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange maarufu Kaburu sababu kesi hiyo imeishafikia hatua ya usikilizwaji wa awali.

Badala yake Mahakama kwa mara nyingine, imetoa amri na kuwapa siku 14 upande wa mashtaka kutekeleza amri iliyoitoa ya kuwataka aidha wafute mashtaka dhidi ya Zacharia Hanspoppe na mfanyabiashara, Franklin Lauwo au wabadilishe hati ya mashtaka kwa kuwaondoa washtakiwa hao ili kesi isikilizwe.

Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, kutokana na ombi la mawakili wa washtakiwa hao wakiongozwa na Nehemia Nkoko kuiomba mahakama ifute kesi hiyo kwa sababu upande wa mashtaka wameshindwa kuiendesha.

Akisoma uamuzi huo hakimu Simba amesema amepitia hoja za pande zote mbili na ameona kuwa, huu si muda muafaka wa kufuta kesi hiyo kwa sababu tayari ilikuwa katika hatua ya (PH) na pia ilishatoa amri ambayo bado haijatekelezwa.Hakimu Simba amesema upande wa mashtaka wanatakiwa watekeleze amri iliyotolewa Mei 12 mwaka ,2018, kwa hiyo haiwezi kufuta kesi hiyo, kwa sababu itafuta hadi amri ambayo tayari ilishaitoa na haijatekelezeka.

"Si muda mwafaka wa kufuta kesi hii, natoa siku 14 kuanzia kesho kwa upande wa mashtaka kufanya mabadiliko na kama hawatafanya hivyo, Mahakama inaweza kuamua vingine itakavyoona inafaa, " amesema Hakimu Simba.Aidha Hakimu Simba ametaka amri hiyo itekelezeke kwa sababu hawajulikani ni lini Hansoppe na Lauwo watakamatwa  wakati Aveva na Kaburu wapo mahabusu.

MASHIRIKA YA UMMA YAPEWA MWEZI MMOJA KUSAINI MIKATABA YA UTENDAJI KAZI

0
0
Na Mwandishi Wetu,
SERIKALI kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imetoa kipindi cha mwezi mmoja kwa mashirika na taasisi za umma zisizokamilika taratibu za kuwekeana saini ya mikataba ya utendaji kazi kwa mwaka 2018/19 kufanya hivyo haraka iwezekanavyo.
Akizungumza katika halfla ya utiliaji saini wa mikataba ya utendaji kazi kwa Taasisi na Mashrika ya Umma 80 kwa mwaka 2018/19 leo Jumanne (Oktoba 2, 2018) Jijini Dar es Salaam, Msajili wa Hazina Athuman Mbuttuka alisema mikataba hiyo ya kazi ni utekelezaji wa sharia na Serikali itaendelea kusimamia  Taasisi na Mashirika yao ili yaweze kufikia malengo yaliyowekwa.
Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2017/18, Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina iliwekana saini na taasisi na mashirika ya umma 105 na kutaka taasisi zingine zilizobaki kukamilisha taratibu hizp kabla ya Serikali haijaanza kuzichulia hatua kwa mujibu wa Sheria.
Akifafanua zaidi alisema Ofisi yake imesajili jumla ya Taasisi na Mashirika ya Umma 185 kati ya makampuni, mashirika, wakala na taasisi 233 zilizopo nchini ambazo  baadhi yake zimeunganishwa na Serikali kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa umma.
Mbuttuka alisema mikataba hiyo imelenga katika kuhakikisha kuwa Serikali na mashirika yanawekeana na ili kuwa na na mwelekeo unaowiana katika kuongeza ufanisi katika maeneo makuu manne ikiwemo Utawala Bora, rasilimali fedha, mikataba ya huduma kwa wateja na uzingatiaji wa kanuni, sharia na taratibu.
 “Tumewekeana mikataba na Wenyeviti wa Bodi katika mashirika na taasisi za Umma katika kuhakikisha kuwa yanaongeza tija na ufanisi katika kuleta matokeo chanya katika maeneo ya kazi pia kuwaweka kwa karibu zaidi Menejimenti na Bodi kufahamu wajibu na majukumu yao katika taasisi hizo” alisema Mbutuka.
Aidha alisema katika mikataba hiyo, Serikali iliweka mkazo katika maeneo hayo manne kwa kutambua kuwa ni sehemu muhimu zilizohitajika kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha utoaji huduma na kufanya mashirika na taasisi za umma kuweza kujiendesha vyema na kuleta tija kwa Serikali na Umma kwa ujumla.
“Katika hili eneo la rasilimali watu tumeangalia ni mafunzo, muundo na motisha kwa watumishi zinawezesha watumishi kutekeleza vyema majukumu yao lakini pia eneo la usimamizi wa fedha tumeangalia ni kwa namna gani tutaweza kupunguza gharama zisizo za lazima katika taasisi na mashirika haya” alisema Mbuttuka.
 Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi akisaini Mkataba wa utendaji kazi kwa mwaka 2018/2019 mbele ya Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka kati ya Taasisi hiyo na Serikali wakati wa hafla ya utiaji saini ya mikataba baina ya Taasisi na na Serikali Mashirika ya Umma  zoezi leo  jumanne Oktaba 2,2018. Kulia ni Kamshina wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijan Mssanzya.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Nchini (TTCL), Mhandisi Omary Nundu akisaini Mkataba wa utendaji kazi kwa mwaka 2018/2019 mbele ya Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka kati ya Taasisi hiyo na Serikali wakati wa hafla ya utiaji saini ya mikataba baina ya Taasisi na na Serikali Mashirika ya Umma  zoezi leo  jumanne Oktaba 2,2018.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu Anne Makinda akikadhi nakala ya mkataba wa utendaji kazi kwa mwaka 2018/19 mbele ya Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka kati ya Taasisi na Mashirika ya Umma wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba baina ya Taasisi hizo  na Serikali iliyofanyika leo jumanne Oktoba 2, 2018. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Kilimo Tanzania (TADB), Bi. Rosebud Kurwijila wakati wa hafla utiaji saini baina ya Taasisi na Mashirika ya Umma na Serikali kwa mwaka 2018 iliyofanyika leo Jumanne Oktoba 2, 2018.
 Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka (katikati) akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Prof. Ninatubu Lema  wa wakati ya saini baina hafla ya utiaji Taasisi na Mashirika ya Umma na Serikali kwa mwaka 2018/2019, Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, hafla iliyofanyika  leo Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BENKI YA KILIMO YAOMBWA KUSAIDIA ZAO LA CHAI WILAYANI LUSHOTO

0
0
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeombwa kusaidia uzalishaji wa zao la chai wilayani Lushoto mkoani Tanga ili kuchagiza shughuli za kiuchumi na kunyanyua kipato cha wakulima wadogo wadogo wilayani humo humo.

Ombi hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. January Lugangika wakati akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine alipotembelea Ofisini kwake.

Bw. Lugangika alisema kuwa Serikali imejipambanua katika kukufua viwanda hasa vyenye kusaidia wakulima wadogo wadogo kupitia ununuzi wa malighafi akilitaja zao la chai kuwa ni la kipaumbele katika kuchagiza juhudi hizo za Serikali.

“Benki ya Kilimo ikisaidia kufufua viwanda vyetu vya chai itawanufaisha wakulima wetu wanaolima chai hivyo kuweza kunyanyua kipato cha wakulima wilayani kwetu,” alisema.

Aliongeza kuwa wilaya ya Lushoto imejaliwa kuwa na eneo kubwa la uzalishaji zao la chai hivyo kuongeza tija katika kuendeleza zao hilo.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine alisema TADB ipo tayari kuchagiza uzalishaji wa mazao ya kimkakati yenye masoko ya uhakika ikiwemo zao la chai na yenye kulenga kunyanyua hali za maisha ya wakulima wadogo wadogo nchini.

Aliongeza kuwa TADB ipo tayari kusaidia juhudi za wilaya ya Lushoto katika kuwasaidi wakulima walio kwenye vikundi vya ushirika au skimu za uzalishaji wa mazao ya kilimo wilayani humo.
 Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Bw. January Lugangika (wapili kushoto) akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ulipomtembelea Ofisini kwake wilayani Lushoto kkuzungumzia fursa za uwekezaji katika kilimo. Wanaomsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kushoto), wengine ni Afisa Biashara Mwandamizi wa TADB, Eunice Mbando (kulia) na Afisa Ushirika wa Wilaya hiyo, Bw. Tito Kayugyuma (wapili kulia).
 Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Bw. January Lugangika akihimiza jambo wakati wa kikao.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine akifafanua jambo wakati akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Bw. January Lugangika (hayupo pichani).
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akiwa katika mazungumzo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Lushoto, Bw. Nicodemas Tambo (katikati). Anayesikiliza ni Afisa Ushirika wa Wilaya hiyo, Bw. Tito Kayugyuma (kushoto).
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Lushoto, Bw. Nicodemas Tambo akizungumza wakati wa kikao hicho alitumia fursa hiyo kuiiomba Benki ya Kilimo kuwaelimisha wakulima wa wilaya hiyo juu ya uwepo fursa za mikopo ya gharama nafuu kutoka TADB.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Lushoto, Bw. Nicodemas Tambo (kushoto) akiagana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA YASAINI MKATABA WA UTENDAJI KAZI NA TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA

BENKI YA KILIMO YAOMBWA KUSAIDIA ZAO LA CHAI WILAYANI LUSHOTO

0
0


Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeombwa kusaidia uzalishaji wa zao la chai wilayani Lushoto mkoani Tanga ili kuchagiza shughuli za kiuchumi na kunyanyua kipato cha wakulima wadogo wadogo wilayani humo humo.

Ombi hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. January Lugangika wakati akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine alipotembelea Ofisini kwake.

Bw. Lugangika alisema kuwa Serikali imejipambanua katika kukufua viwanda hasa vyenye kusaidia wakulima wadogo wadogo kupitia ununuzi wa malighafi akilitaja zao la chai kuwa ni la kipaumbele katika kuchagiza juhudi hizo za Serikali.“Benki ya Kilimo ikisaidia kufufua viwanda vyetu vya chai itawanufaisha wakulima wetu wanaolima chai hivyo kuweza kunyanyua kipato cha wakulima wilayani kwetu,” alisema.

Aliongeza kuwa wilaya ya Lushoto imejaliwa kuwa na eneo kubwa la uzalishaji zao la chai hivyo kuongeza tija katika kuendeleza zao hilo.Akizungumza wakati wa kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine alisema TADB ipo tayari kuchagiza uzalishaji wa mazao ya kimkakati yenye masoko ya uhakika ikiwemo zao la chai na yenye kulenga kunyanyua hali za maisha ya wakulima wadogo wadogo nchini.
 Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Bw. January Lugangika (wapili kushoto) akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ulipomtembelea Ofisini kwake wilayani Lushoto kuzungumzia fursa za uwekezaji katika kilimo. Wanaomsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kushoto), wengine ni Afisa Biashara Mwandamizi wa TADB, Eunice Mbando (kulia) na Afisa Ushirika wa Wilaya hiyo, Bw. Tito Kayugyuma (wapili kulia).
IMG_7031
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Bw. January Lugangika akihimiza jambo wakati wa kikao.
IMG_7032
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine akifafanua jambo wakati akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Bw. January Lugangika (hayupo pichani).
IMG_7033
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akiwa katika mazungumzo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Lushoto, Bw. Nicodemas Tambo (katikati). Anayesikiliza ni Afisa Ushirika wa Wilaya hiyo, Bw. Tito Kayugyuma (kushoto).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

MKURUGENZI MTENDAJI TIC AITA WAWEKEZAJI JNIA-TBIII

0
0



Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bw. Geoffrey Mwambe (aliyenyoosha mkono ukutani), wakati akipata ufafanuzi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (katikati) na Mkurugenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII).
DSC_2314
Mafundi (kulia juu ya mashine) wakiwa wanaendelea na ujenzi wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, wakati wa ziara ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela na wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bw.Geoffrey Mwambe pamoja na msafara wao, leo walipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi huo.
DSC_2318
Mhandisi Barton Komba wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) anayesimamia mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), akielekeza jambo wakati wa ziara ya Wakurugenzi kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bw. Geoffrey Mwambe (wapili kushoto) na wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (watatu kulia) leo walipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya mradi huo.
 DSC_2343
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bw. Geoffrey Mwambe (alinyoosha mikono) leo akijaribu kueleza kwa vitendo katika ziara yake aliyoambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (watatu kushoto) walipotembelea ujenzi wa mradi unaoendelea wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, tayari ujenzi umefikia asilimia 82.

MDAHALO KUELEKEA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE ULIOFANYIKA KATIKA TASISI YA MAENDELEO YA JAMII


Dawa ya asili ya 4A9 yapata usajili rasmi

0
0

Hatimaye baraza la tiba asili na tiba mbadala Tanzania limeisajili na kuitambua rasm dawa ya 4 A 9 kwa lengo la kumpa fursa mtafiti T.R. Msigwa kuitangaza dawa hiyo kwa manufaa ya watanzania na Afrika kwa ujumla ambapo zaidi ya vijana 400 wanatarajiwa kupata ajira nchini. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mtafiti TR Msigwa amesema kitendo cha Baraza hilo kuisajili dawa hiyo kwa namba TZ 17TM 0007 ni faraja kubwa kwa watanzania kwani licha ya kusaidia watanzania kiafya lakini pia itakuwa ni fursa pekee ya kutoa ajira kwa vijana nchini. 
 Amesema mpango wake sasa ni kuhakikisha anatoa ajira kwa Watanzania ambapo atakuwa na mwakilishi mmoja kila wilaya kwa nchi nzima ya Tanzania kitendo ambacho kitasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana hao kuisambaza na kuitangaza dawa hiyo
Amesema dawa hiyo ya 4A9 ambayo inaimarisha kinga ya mwili na kusaidia kutibu kisukari, shinikizo la damu na maradhi mengine nyemelez, baada ya kusajiliwa atahakikisha inasambazwa kila wilaya kwa nchi nzima ya Tanzania na nje ya Tanzaia. 

 TR  Msigwa amesema dawa hiyo baada ya kupata mafanikio makubwa nje ya Tanzania,kwa kupata usajili huo kutasaidia kupata mafaniko zaidi nchini Tanzania, na kuwataka watanzania kumuunga mkono katika juhudi zake za kuhakikisha 4A9 inatambulika na kuisaidia jamii. 

TR Msigwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwatia moyo watanzania katika kuanzisha viwanda ambapo licha ya kuwa na kiwanda kidogo ambacho kinazalisha dawa hiyo ya 4A9 
Amesema kwa sasa ameshanunua eneo la heka mbili wilayani Kibaha mkoa wa Pwanni kwa lengo la kujenga kiwanda kikubwa kitakacho zalisha dawa hiyo na kuongeza ufanisi zaidi.  

 TR Msigwa amesema baada ya kupata usajili huo Oktoba 20 mwaka huu anatarajia kuanza safari ya kuitambulisha dawa hiyo ya 4A9 nchini nzima akianzia Makambako mkoani Iringa,mbeya mtwara, Lindi, Pemba na uguja

KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA DHIDI YA ALIYEKUWA MHASIBU TAKUKURU YAKWAMA

0
0
Na Karama Kenyunko, 
Globu ya Jamii

KESI  ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizolingana na kipato chake halali, inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru, Godfrey Gugai na wenzake wanne, imeshindwa kuendelea kusikilizwa  sababu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina hela ya kuwaleta mashahidi.

Wakili wa Serikali, Pius Hila akisaidiana na wakili kutoka Takukuru, Vitalis Peter ameeleza hayo, leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba,  kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

Wakili Hilla amedai walishaita mashihidi  kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam lakini wameshindwa kufika kwa kuwa Mtendaji wa Mahakama hakuwa na fungu la  fedha, kwa  ajili ya kuwalipa.Ameendela kueleza kwa sasa wamepata  kibali kutoka kwa  Mtendaji wa Mahakama ambacho kinawaelezea kuwa malipo yatasubiri fedha zitakapoingia lakini mashahidi wameshindwa kuja kwa  gharama zao wenyewe.

"Mheshimiwa hakimu kutokana na hali hiyo, tunaomba terehe fupi kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa kesi hii," ameeleza Hilla.Kutokana na maelezo hayo, Wakili wa Utetezi Alex Mgongolwa aliwasilisha maombi mawili mahakamani hapo.

,"Mheshimwa, tunaomba jitihada za kuwapata mashahidi hao waliopo nje ya mkoa wa Dar rs Salaam ziendelee na pia  ni rai yetu kwa  mahakama upande wa mashtaka walete mashahidi ambao hawahitaji kuombewa kibali na hawatoki nje ya mkoa wa Dar es salaam ili Kesi hii iweze kuendelea," amedai Wakili Mgongolwa.

SERIKALI YANUNUA MASHINE ZA MIONZI ZENYE THAMANI YA BILIONI 1.74

0
0
Na WAMJW, Dar es Salaam

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imenunua mashine za Mionzi (digital X-ray) zipatazo kumi zenye thamani ya shilingi bilioni 1.74.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akipokea mashine hizo kwenye Bohari ya Dawa(MSD)  jijini hapa.

Waziri Ummy amesema kuwa Serikaki inaendelea kutoa kipaumbele katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwa ni lengo  la kuhakikisha huduma za afya zinawafikia watanzainia wote karibu na maeneo wanayoishi.

"Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania yataletwa na wananchi wenye afya na wenye uwezo wa kuzalisha mali,hivyo tunaboresha na kuimarisha huduma za tiba na uchunguzi wa magonjwa katika hospitali zetu kuwa na vifaa vya kisasa zaidi na kuondokana na utaratibu wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi".Alisema,Waziri Ummy Mwalimu.

Alisema mashine hizo zitapelekwa kwenye hospitali za rufaa za mikoa 10 ambazo X-ray za zamani zimekwisha muda wake na zimekua zikiharibika mara kwa mara.Alizitaja hospitali hizo ni Amana, Bukoba, Katavi,Morogoro,Njombe,Ruvuma,Simiyu na Singida pamoja na hospitali  za Wilaya ya Magu na Nzega.

Aidha,Waziri Ummy alisema katika bajeti ya mwaka 2018/2019, Wizara yake imepanga kununua mashine za mionzi nyingine zipatazo ishirini na nne(24) zenye thamani ya shilingi bilioni 4.1 ambazo zitapelekwa kwenye hospitali za rufaa za Mikoa na Wilaya ambazo hazina au zina X-ray za kizamani au chakavu.

Akizungumza kwa niaba ya Waganga Wakuu wa hospitali   zinazopelekwa mashine hizo,Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Amana Dkt.Mashack Shimwela alisema ujio wa mashine hizo za kisasa zitasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa uchunguzi  za mionzi pia utunzaji wa mazingira tofauti na aina zilizokuwa zikitumika mwanzo

Aidha,alisema mashine hizo zina ubora wa picha  pia ina mifumo ya Tehama ambayo ni rahisi kusomwa hata nje ya hospitali husika endapo hakuna msoma picha . 
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu akionesha baadhi ya mashine za mionzi  10 zilizonunuliwa na Serikali zenye thamani ya shilingi bilioni 1.7 na kusambazwa kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa,pichani kushoto ni Mwakilishi wa kampuni ya Phillips Bi.Monica Joseph 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu akipewa maelezo mafupi kutoka kwa Muwakilishi wa Kampuni ya Philips Bi. Monica Joseph mara baada ya kukabidhi baadhi ya mashine za mionzi  10 zilizonunuliwa na Serikali zenye thamani ya shilingi bilioni 1.74 na kusambazwa kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa
 Waziri Ummy akiongea na vyombo vya habari wakati wa kupokea mashine hizo za mionzi (digital X-ray) ambazo zitaboresha huduma za afya nchini hususani za uchunguzi wa mionzi
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Dkt.Mashack Shimwela akiongea na waandishi wa habari baada ya kupokea mashine hizo Picha zote na Wizara ya Afya

WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUHARIBU FEDHA ZA BENKI KUU YA TANZANIA

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

VIJANA 7 wa umri wa miaka 21 hadi 24, leo wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kosa la kuharibu Noti za Benki Kuu ya Tanzania (B.O.T) za Shilingi 70,000 kwa kuzikanyaga.

Mwendesha mashtaka Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Vicent Kaduma (24), Rogers Swale (23 ), Doreen Mwenisongole (22) ni mwanafunzi, Kelvin Mngeyekwa 23, Eia Chengula 24 mfanyabiashara, Said Sadiq 21 na Ramadhan Seleman 23.

Akisoma hati ya mashtaka, chini ya kifungu cha 332 A cha kanuni ya adhabu, mbele ya Hakimu Mkazi Wanjah Hamza wakili Kombakono amedai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na kosa moja la kuharibu noti za BoT.

Imedaiwa, Septemba 16 mwaka 2018 washtakiwa hao wakiwa jijini Dar es Salaam, pasipokuwa na mamlaka waliharibu noti za Sh.70,000 ambazo noti moja ilikuwa na thamani ya Sh. 10,000.Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hata hivyo, washtakiwa hao wako nje kwa dhamana baada ya mahakama kupatiwa masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini 2 waaminifu waliosaini bondi ya Shilingi Milioni 2 kila mmoja.  Kesi imeahirishwa hadi Novemba 11 mwaka 2018.
Pichani juu na chini ni baadhi ya watuhumiwa wakipandishwa kwenye kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kosa la kuharibu Noti za Benki Kuu ya Tanzania (B.O.T) za Shilingi 70,000 kwa kuzikanyaga.

MICHUZI TV: WEMA SEPETU AZUNGUMZIA UJIO WA DAY AFTER DEATH (D.A.D)

Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images